Kunahaja ya Simba kujiandaa na msimu ujao. Tunaweza kubisha sana lakini huo ndio ukweli. Nashauri uongozi wa Simba kufanya yafuatayo.
1. Kutafuta kocha mwenye kiwango sio ilimradi kocha tu wakati mnamalengo ya kufika nusu final CAF champions league. Tuache ubahili
2. Dirisha dogo la usajili ndio liwe dirisha la usajili kwa ajili ya kuenda kutusaidia msimu ujao ili wapate muda mrefu wa kuzoeana coz mwisho wa msimu huwa tunasajili kwa mihemko.
3. Nikiri tu wachezaji wa kimaraifa tuliosajili ni wakawaida sana. Jmn mnauza wachezaji wa bilioni zaidi ya nne unarudi kuokoteza wachezaji wa million miatatu miatatu. Nendeni mkang'oe mchezaji mwenye akili kwenye timu kubwa angalao wawili tu kuliko kusaji wachezaji nane wote patupu.
4. Acheni kusajili wachezaji wapya wengi ndani ya dirisha Moja. Hebu tujiulize tulikua tunaisema Yanga sana kuwa inasajili wachezaji wengi ndani ya dirisha Moja lakini hebu tujiulize Simba imesajili wachezaji wangapi msimu huu? Sio chini ya wachezaji wapya 8. Nilitegemea replacement mbili ku cover nafasi ya Chama na Miquison na wengine wawili watatu kurekebisha kikosi lakini yaliyotokea hayatofautiani na mipango ya utopolo.
4. Achaneni na wahasishaji wa kijinga mliowapa nafasi. Mashabiki wa Simba walishahamasika kitambo sana. Matokeo ya uwanjani ndio hamasa ya washabiki. Kuweni professional kuakisi malengo ya kufika nusu final mnayoitaja taja midomoni mwenu.