Huna nidhamu wewe. Duniani uliona wapi timu inayopata mafanikio kiuendelevu bila kutetereka? Lazima ujue kuna kupanda na kushuka.
Wakati ukiwa na mafanikio timu zinatumia muda kusoma mbinu zako, wakishafanikiwa ndio hapo unashuhudia mtetereko wa timu.
Hii ni kawaida katika soka. Acha matusi, unaowatukana si wajinga, watajipanga na kuja kivingine. Ukiona huwezi kuvumilia una machaguo mawili. La kwanza; saga chupa unywe. La pili, anzisha timu yako halafu usiuze wachezaji ili uwe na mafanikio unayoyaota.
Halafu acheni ujinga wa kulalamikia wacheza waliouzwa. Wewe ulitaka afanyeje? Akae nao mpaka wadode? Au akae nao kisha mikataba yao iishe halafu waondoke bure? Kama hujui kuwa soka ni biashara na inafanywaje acha kuwa shabiki, kalime matikiti huko.