Simba SC yatoa taarifa rasmi, yataka kupewa ushindi kwa Yanga SC kususia kuingiza timu uwanjani

Simba SC yatoa taarifa rasmi, yataka kupewa ushindi kwa Yanga SC kususia kuingiza timu uwanjani

Simba Kama wanatii maagizo na maelekezo ya TFF iweje tena wapinge maelekezo ya kuahirishwa mechi mpaka itakapopangiwa tarehe nyingine? Simba waache uoga na kutaka pointi za mezani ili kukwepa kipigo!
Maagizo ya serikali ni mechi kupigwa saa 1.00 usiku. Maagizo haya yakabadilishwa na bodi ya ligi iliyoamua kuahirisha mchezo. Tunategemea serikali iichukulie hatua TFf kwa kutokutekeleza maagizo ya mechi kupigwa saa 1.00 usiku badala yake wakaahirisha!
 
Mmetuabisha viongozi wetu narudi tena mmetuabisha mnadhani kwamba mnawakomoa Yanga? Acheni u snitch nchi nzima inataka kujua nani alietoa amri saa saba mchana mechi ihaiirishwe hadi saa moja wakati pre match meeting imefanyika saa nne?

Au toka atekwe Mo Dewji wote mnatetemeka tu? Yanga wamesimama kiume tunataka kujua TFF walipokea maagizo kwa nani na kwa nini?
 
M
Usiwapambe sana Yanga hata wao wamefanya hivyo sababu wana visasi vyao na TFF, wameona hii mechi ndio ya kulipiza kisasi, mbona mechi za biashara na azam muda ulibadilishwa na wakacheza.
wechi ya azam taarifa ilitolewa mapema kwamba kuna mashindao ya kurani ikaeleweka kuhusu biashara sikumbuki,suala kubwa jana sababu ni nini ?tunataka kujua wamepeleka mbele kwa ajili gani mbona hawasemi
 
CEO aliandika huko jamii ya T

IMG-20210509-WA0134.jpg
 
Mimi ni Simba lakini kwa hili Simba wanataka tu kuwatoa Wahusika hatiani.

Yanga wapo sahihi, shikamaneni mpambane na Wanaoharibu soka achaneni na usnichi usio na maana.
 
Huu mchezo yanga ameupanga vyema ukapangika,sasa Simba analazimishwa kuucheza nje ya uwanja.

Yanga wanajua ni nani alitoa maelekezo yackuongeza muda,wanajua ni kwa nini maelekezo hayo yalitolewa,baadae TFF na bodi ya ligi wakaingia kichwa kichwa katika mchezo wasioujua,yanga wakafunga goli kwa kutumia kanuni,na leongo lao likawa limetimia.Kuikimbia Simba.

Nashauri Simba waende kwa akili sana
 
Back
Top Bottom