Simba tuendelee kuwaombea Njaa Etoile du sahel wako nafasi ya tatu ligi yao

Simba tuendelee kuwaombea Njaa Etoile du sahel wako nafasi ya tatu ligi yao

sidhani kama lile kosa la jwaneng litajirudia, baad aya ile mechi pascal wawa kuchanwa makavu na Gomez wakati alipofukuzwa unaona kabisa wawa alianza kukaza, ile game angecheza Inonga labda hata ule mpira wa kurusha angeweza kuruka...somo viongozi walishalipata team itakaa vizuri mkuu hiiligi iishe tu usajili utangazwe...Etoile nakuhakikishia hamalizi top 2....
Walicheza Wawa na Inonga Ila Inonga kipindi Cha pili alikata moto
 
Kama msimu huu unaoisha tulianzia round ya kwanza tukiwa ranked number 15 kwa ubora afrika na kupata bahati ya timu 5 zilizokuwa juu yetu kuvurunda kwenye domestic leagues zao tukapata nafasi ya kuanzia round ya kwanza why not mwaka huu?

Tuko nafasi ya 14 kwa ubora barani afrika lakini katika teams zilizoko juu yetu uhakika tatu kwenye ligi haziwezi kucheza champions league,team hizo ni Orlando pirates ambao ingawa wana viporo vitatu nafasi mbili z ajuu zishachukuliwa na mamelodi na ajax cape town....pyramids wao wako juu yetu pia lakini kuna kigingi cha ahly na zamalek..huko moroko ,berkane ana kigingi cha wydad na Raja

Sasa shughuli inabaki hapo Tunisia Etoile du sahel anaweza sabisha tukaanzia round ya awali na WAJINGAWAJINGA cha kufurahisha ni kwamba na yeye ana struggle yuko nafasi ya tatu kwenye ligi ndogo ya teams za juu wanaita championship round maana wana system kama ya ubelgiji ligi ikiisha kuna top teams zinagombea ubingwa na bottom ones wana fight relegation

TUENDELEE KUOMBEA SANA HAWA JAMAA WAMALIZE WA TATU AU WA NNE hapo njia nyeupeee kuanzia round ya kwanza na kundi la elites siyo VILAZA

View attachment 2234057View attachment 2234063
Baada ya kuingia nusu fainali nadhani Es setif wameipita simba sc,habari nzuri ni kwamba hawana dalili ya kucheza champions league mwakani hali yao ni tete kwenye ligi ya ndani
 
Baada ya kuingia nusu fainali nadhani Es setif wameipita simba sc,habari nzuri ni kwamba hawana dalili ya kucheza champions league mwakani hali yao ni tete kwenye ligi ya ndani
setif kaingia nusu fainali gani?
 
Egpyt ... Al ahly na zamaleki (1&2)
Morocco... ( waydad&raja) 3&4
Mamelod , petro atletico na horoya... tayar mabingwa ( 5,6&7)
Mazembe wanaongoza Congo na Esperance anaongoza tunis ( 8&9) .

Berkane ,pyramid wapo top 10 wataenda shirikisho.

Simba tupo nafasi ya 14.
Sasa apo tunamuombea njaa no 11 etoile du sahel asifuzu nafasi mbili za juu kwenye ligi Yao au azidiwe na CS sfaxien au club African

Otherwise tutaanzia preliminary .
NB:
5 year ranking
Simba no 14.......... Point 28
Namungo no 56....... Point 2
Yanga no 75 .........point 0.5
 
Simba inacho takiwa iongeze kiwango Cha ushirikina maana katika eneo Ilo ata CAF inawatambua kwamba ni magwiji.
 
Hapo suala siyo bingwa mtetezi, suala ni yupo namba ngapi kwenye rank ya CAF
Waona anza makundi ni zile timu ambazo hazipo kwenye top ten ya Africa hata kama kaongoza ligi nyumbani kwake
Ila kama yupo kwenye top 10 ya CAF, atanzia makundi hata kama yupo run up wa ligi ya nyumbani kwao
Simba anaomba Eto du Sahel wasiwe nafasi ya pili kwenye ligi yao hivyo Sahel automatically atakuwa amejiondoa kwenye top 10 ya CAF na nafas yake kuchukuliwa na Simba hivyo simba kuanza kwenye makundi ingawa ni namba mbili na Tanga kuanza round ya kwanza licha ya kuongoza ligi ya Tanzania
Hakuna sheria ya kuanzia makundi. Top ten zitaazia raundi ya pili. Ili kufikia kucheza hatua ya makundi kuna hatua ya awali na hatua ya pili, timu kumi bora zina skip hatua moja.
 
Baada ya kuingia nusu fainali nadhani Es setif wameipita simba sc,habari nzuri ni kwamba hawana dalili ya kucheza champions league mwakani hali yao ni tete kwenye ligi ya ndani
Setif wana point 43 kazidiwa michezo minne na anayeshika nafasi ya pili ambaye Kabyille wenye point 57 huku michezo mitatu wakibakiza Kabyille kumaliza ligi
 
Setif wana point 43 kazidiwa michezo minne na anayeshika nafasi ya pili ambaye Kabyille wenye point 57 huku michezo mitatu wakibakiza Kabyille kumaliza ligi
mkuu umeangalia table ya overall, angalia table ya champions utaona ES setif wana point 7 (saizi itakua 10 kama wameshinda leo)
 
kwa hiyo libya ambayo ligi yao iko ranked number 12 nyuma ya Tanzania team yao ya Ahl tripoli inayoshika nafasi ya 24 inaanzia round ya kwanza siyo? ndiyo logic yako hiyo na akili zako zimeishia hapo kabisaaaaa??????

Nigeria nayo itatoa team round ya kwanza siyo???lahaula
Sibaishani na Wavaa Shanga aseee.
Nimeeleza wazi huo utaratibu hauna maana, hizo ranks za nini kwa klabu katika kuanzia hatua ya pili??
Wangetumua mfumo wa Ligi 12 6 bora au 10 bora zitoe timu 2 basi.

Huu ujinga wa kwamba time imepewa rank namba kadhaa ikashiriki kuanzia hatua ya pili ndio kitu ambacho kibadilishwe au ww Bi Fatma umeelewaje.??
 
Hii mkuu sio rahisi kufanyika. Ni lazima waangalie club ranking. Form Vs Class!Form is temporary, class is permanent. Wakisema wanachukua tu bingwa ndo aanzie round ya pili pengine bingwa alitokana na changamoto za mashindano(mfano mzuri mabingwa waliopatikana kipindi cha corona baada ya ligi kuahirishwa).

Kwa hiyo ni lazima CAF Champions league iwe na timu zinazoweza kutoa ushindani na walau ziwe zimethibitisha hilo kupitia cumulative points ambazo klabu imekuwa ikizipata kupitia CAFCCL na CAFCC. Na ili kufanikisha hili wanachukua timu zilizofuzu katika ligi za ndani na kulinganisha rankings kwa klabu za nchi tofauti.
UEFA wanaangalia huo UJINGA??
AMERIKA YA KUSINI mashindano yao pia huangaliwa hiv??
 
Egpyt ... Al ahly na zamaleki (1&2)
Morocco... ( waydad&raja) 3&4
Mamelod , petro atletico na horoya... tayar mabingwa ( 5,6&7)
Mazembe wanaongoza Congo na Esperance anaongoza tunis ( 8&9) .

Berkane ,pyramid wapo top 10 wataenda shirikisho.

Simba tupo nafasi ya 14.
Sasa apo tunamuombea njaa no 11 etoile du sahel asifuzu nafasi mbili za juu kwenye ligi Yao au azidiwe na CS sfaxien au club African

Otherwise tutaanzia preliminary .
NB:
5 year ranking
Simba no 14.......... Point 28
Namungo no 56....... Point 2
Yanga no 75 .........point 0.5
Ukiwa bingwa wa SHIRIKISHO huendi KLABU BINGWA AFRIKA??
 
mkuu umeangalia table ya overall, angalia table ya champions utaona ES setif wana point 7 (saizi itakua 10 kama wameshinda leo)
Source zote zinaonesha hivyo mkuu, na leo wamefungwa goli tatu hivyo wameporomoshwa hadi nafasi ya 10 wana vipolo vinne.
 
Sibaishani na Wavaa Shanga aseee.
Nimeeleza wazi huo utaratibu hauna maana, hizo ranks za nini kwa klabu katika kuanzia hatua ya pili??
Wangetumua mfumo wa Ligi 12 6 bora au 10 bora zitoe timu 2 basi.

Huu ujinga wa kwamba time imepewa rank namba kadhaa ikashiriki kuanzia hatua ya pili ndio kitu ambacho kibadilishwe au ww Bi Fatma umeelewaje.??
Hilo tusi la wavaa shanga ndilo unalolijua au kuna lingine mr DUNDERHEAD? ila ni furaha sana kuwa na wajinga hapa jukwaani maana inasababisha sisi ma genius tumshukuru Mungu kwa kutujalia akili nyingi
SASA NIKUULIZE SWALI MR UTOWPINYO: WAKATI SIMBA INACHEZA ROUND YA KWANZA MSIMU HUU LIGI YA TANZANIA ILIKUWA TOP TEN KWA UBORA???UNAJUA HATA KWANZA NI TEAMS 10 NDIZO ZINAANZA ROUND YA KWANZA?
HOJA YAKO YA LIGI BORA NI DHAIFU SANA KWA SABABU CAF INAHESABU LIGI BORA HADI NAMBA 12 NA NDIZO ZINAZOPEWA SLOTS YA TEAMS 4....KWA AKILI YAKO YA KIUTOPOLO UNADHANI ELITES TEAMS NI 12?
FICHA UJINGA WAKO KINABO WEEE
 
Source zote zinaonesha hivyo mkuu, na leo wamefungwa goli tatu hivyo wameporomoshwa hadi nafasi ya 10 wana vipolo vinne.
Setif? ila shida kubwa ni Etoile du sahel mkuu....sababu wao ,simba na setif ndiyo wanaweza ku grab hiyo nafasi moja iliyobaki ..Horoya na Petro atletico washapenya kiulaiini
 
Back
Top Bottom