Simba yamtimua kocha Roberto Oliveira Goncalves Do Carmo (Robetinho)

Huu sasa ndio ujinga wa soka la Bongo. Kocha anafukuzwa kazi kwa kufungwa na mtani.
Mazuri yote yake hayana maana kama asipoweza kumfunga mtani wa timu.
Soka letu linakwama namna hii.
Ndio siasa za mpira
 
Wamuombe msamaha Mgunda kwa kumuharibia wakati wake, bora mngemuacha na Coastal yake kuliko kumfanya kama karai la zege. Simba wakifanya mchezo, mechi zao zinazokuja watasulubiwa na kuwatoa kabisa kwenye mashindano yoyote wanayoshiriki.
Kocha siyo tatizo, tatizo jinsi timu inavyoendeshwa.
Huyo Mgunda mnavyomlilia utazani ana kitu kipya,akipewa mkataba mtarudi hapa kumtukana.
 
Kwa tafsiri nyingine ni kwamba Yanga yamfukuzisha Kocha Objective na kusababisha kocha Kishingo au Profesa Nabi kurudi Tanzania
Nabi hawezi kuja kufundisha timu yenye wachezaji wabovu kama hawa, labda mpate ushauri wake msajili kwa msimu ujao aje na bench lote.la ufundi, sioni dirisha dogo uwezo wa kupata mchezaji mwenye kiwango
 
yaan kocha amefungwa mechi 1 TU katika ligi toka aje nchini lakn anatimuliwa bila hata haya

Kocha wa yanga NASREDIN NAB aliomba siku 90 za kurekebisha mapungufu ya kikos chake akavumiliwa lakn sisi kocha hajapewa hata nafas hyo

Wachezaji wetu wengi n mizigo kutokana na umri Kama kapombe na shabalala bocco saidoo na chama

Kuna tetes Kuna kiongoz alofosi MANULA aanze kwenye Derby bila kujua fitness ya mchezaji lakn lawama anapewa kocha

Hii timua timua ya makocha kila mwaka haitatufikisha popote kwan ngumu kwa kocha kuimplement falsafa zake kwa MDA mchache hivyo

Tatizo la Simba siyo kocha n Zaid ya kocha had uongoz unahusika

Kocha ndio jipu kubwa. Baadae vunja kikoso.
 
Klabu ya Simba imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza Roberto Oliveira Goncalves Do Carmo (Robetinho).

Vilevile tumefikia makubaliano ya kusitisha mkataba wa kocha wa viungo Corneille Hategekimana.

Uongozi wa Klabu ya Simba unawashukuru Makocha hawa kwa mchango wao ndani ya klabu yetu na inawatakia kila la heri katika majukumu yao mapya.

Katika kipindi cha mpito kikosi chetu kitakuwa chini ya Kocha Daniel Cadena akisaidiwa na Seleman Matola.

Tayari mchakato wa kutafuta makocha wapya umeanza na unatarajiwa kukamilika hivi punde.

Kweli Simba hamnazo. Mnamfukuza kocha wakati Mangungu bado yupo pale Msimbazi. Hakuna rangi mtaacha kuona za 5G
 
Klabu ya Simba imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza Roberto Oliveira Goncalves Do Carmo (Robetinho).

Vilevile tumefikia makubaliano ya kusitisha mkataba wa kocha wa viungo Corneille Hategekimana.

Uongozi wa Klabu ya Simba unawashukuru Makocha hawa kwa mchango wao ndani ya klabu yetu na inawatakia kila la heri katika majukumu yao mapya.

Katika kipindi cha mpito kikosi chetu kitakuwa chini ya Kocha Daniel Cadena akisaidiwa na Seleman Matola.

Tayari mchakato wa kutafuta makocha wapya umeanza na unatarajiwa kukamilika hivi punde.

Magoli pekee yanayouma ni ya Yanga
 
Jamaa alikua ana plan nzuri
Kilichomuangusha beki za pembeni
Na watu wachache mbele pale
 
Klabu ya Simba imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza Roberto Oliveira Goncalves Do Carmo (Robetinho).

Vilevile tumefikia makubaliano ya kusitisha mkataba wa kocha wa viungo Corneille Hategekimana.

Uongozi wa Klabu ya Simba unawashukuru Makocha hawa kwa mchango wao ndani ya klabu yetu na inawatakia kila la heri katika majukumu yao mapya.

Katika kipindi cha mpito kikosi chetu kitakuwa chini ya Kocha Daniel Cadena akisaidiwa na Seleman Matola.

Tayari mchakato wa kutafuta makocha wapya umeanza na unatarajiwa kukamilika hivi punde.

Mgunda yupo wapi?wampe timu
 
Kwenye migogoro na ubovu wa timu kufanya vibaya na kufukuza makocha Matola yupo na bado anapewa awe caretaker, huu ujinga Yanga tulishatoka huko.
 
Back
Top Bottom