Simba yasaini mkataba wa miaka mitano na M-Bet kama Mdhamini Mkuu

Inasemekana pesa ni bilioni 10 kwa kipindi cha miaka 5 hivo kila mwaka simba itakunja bilioni 2
 
Wewe ni miongoni mwa mapooza wengi mliojaa hapa nchini! Taarifa rasmi ya club imetoka kuwa timu imeingia mkataba na Kampuni ya M-Bet,kwa muda wa miaka mitano...
Kwanini sasa huyu aliyeleta thread hakumalizia kila kitu mpaka hizo figure? Wewe hizo figure umezitoa kwenye chanzo kipi?
 
Wewe ni miongoni mwa mapooza wengi mliojaa hapa nchini! Taarifa rasmi ya club imetoka kuwa timu imeingia mkataba na Kampuni ya M-Bet,kwa muda wa miaka mitano...
Acha kubwabwaja mkuu leta source ya hii taarifa yako coz taarifa ya Leo iliyotoka wala haina hizo figure ulizotaja
 
Mkataba ni wa miaka mingapi, na una thamani ya kiasi gani cha fedha?

Au ndiyo kusema mashabiki hawatakiwi kufahamu kama ilivyo kwa zile bilioni 20?
 
Mkataba ni wa miaka mingapi, na una thamani ya kiasi gani cha fedha?

Au ndiyo kusema mashabiki hawatakiwi kufahamu kama ilivyo kwa zile bilioni 20?
Uliza na ww mkuu coz tukiuliza wengine tunaoneka vichaaa
 
Bora hata sportpesa kwenye jezi inakaa vizuri..sio Mbet..jezi ya Simba zitakuwa kituko
Ni kawaida tu hata Man U kila walipokuwa wanabadili wadhamin mfano (CHEVLOLET- Teamviewer) watu walikuwa na mtazamo kama wako.

Chelsea nao wakati wanahama kwa SAMSANG watu walijua jersey zitakua hovyo.
 
Nyinyi subirini muda wenu ufike muanze kuuliza zilpowekwa bila nyinyi kuonyesha mlipoweka zenu, hiyo ndo kazi yenu kubwa.

Hela za Simba Sc zitakuwa ni za kufoji ila zenu zitakuwa ni halali, ni kawaida kabisa.
 
Huo ni mtego kwa watani waapoendelea kufanya negotiation za mkataba mpya na Sportpesa.
Ni sahihi ila kuna mwana Simba mmoja humu ndani change formula anadai eti kuwa Simba imeanika kila kitu, Nawakati sio kweli. Lakini kuna maswali najiuliza kupitia hili;

Je wamesaini mkataba kisha wameacha sehemu ya figure? Au wamesaini mkataba uliokuwa na figure ila wamekubaliana kuhaririwa endapo Yanga watapewa pesa nyingi na Sportpesa basi figure itabidi ibadilishwe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…