Simba yatwaa Ngao ya Jamii kwa Penati 3-1 dhidi ya Yanga, Ally Salim awa shujaa wa mchezo

Simba yatwaa Ngao ya Jamii kwa Penati 3-1 dhidi ya Yanga, Ally Salim awa shujaa wa mchezo

Kipindi cha kwanza Simba imecheza sana mipira mirefu ambayo 85% ilikuwa inapotea na kuchukuliwa na wapinzani.

Formation ya kocha sio rafiki, Bocco mechi imemshinda anafanya tuwe 9 uwanjani.

Yanga imemiliki mpira imepiga pasi nyingi na imefika mara nyingi golini kwetu na kutengeneza presha.

Kazi kubwa kaifanya Chemalon huyu ndio man of the match kwa kipindi hiki cha kwanza, mzigo wote upo mabegani mwake.

Simba haikabi mipira na haina kasi, mipira michache sana ambayo Simba imefanikiwa kuichukua kutoka kwenye miguu ya mpinzani. Mostly ilikuwa ni mipira ambayo mpinzani alikuwa amekosa target na kujikuta amepiga uelekeo wetu.

Kocha atulize akili aje na mbinu mpya, ila kama ndio atachelewa kufanya sub basi sioni namna ambayo tutaweza kutoboa mechi hii.
 
IMG_9631.jpg


Kazi Nzuri Ya Mkono, Mwamuzi Msaidizi
 
Back
Top Bottom