Kwenye nchi za wenzetu zinazoheshimu uwajibikaji, this is an embarrassment kwa mzazi!, mwana unleavyo ndivyo akuavyo, Mhe. Simbachawene anawajibika kwa tortuous liability ya malezi ya kijana wake iitwayo vicarious liability ya malezi mabovu ya wazazi, hivyo Baba anapaswa kuwajibika kwa embarrassment iliyosababishwa na makosa ya kijana wake, mzazi anawajibika kwa kosa la mtoto, mume anawajibika kwa kosa la mke, boss anawajibika kwa kosa la mtumishi wake, hata Ali Hassan Mwinyi alipowajibika ile 1976 akiwa Waziri wa mambo ya ndani kwa vifo vya wale mahabusu wawili, Masaga Makhula Mazengenuka na Isaack Ng'wana Ng'hohoboko, Mwinyi did nothing!, mahabusu hao walikufa kufuatia mahojiano na polisi eneo la Kigoto, na waliokolewa na RSO wa Mwanza, na vifo vyao vikamponza Mzee wa watu aliyewaokoa!. Aliyejiuzulu ni Mwinyi na hakuwa na kosa lolote.
UK, US, Canada, Australia na Newsland, Baba, mama, mke na mtoto wa politicians ukifanya kosa lolote la embarrassment and put the public office into disrepute, mfano kukutwa na Wanawake wa barabarani, ukiacha mke, mtoto wako akifanya kituko, you immediately leave the public office!.
P.
Mkuu
Pascal Mayalla
With all due respect, kuna upotoshaji katika bandiko lako.
Awali ya yote nieleze kauli ya Waziri Simbachawene ikifuatiwa na rebuttal
1. Kwa utamaduni wetu wa kijinga Tanzania, inapotokea waziri akikiri kosa kufanywa na mtoto wake, ni jambo la kumpongeza hata kama tunajua yatamalizwa tu. Haitokei , amejitahidi sana kwa std zetu
Pili, Waziri kafanya kosa kutamka kijana wake ashughulikiwe, amechukua 'ownership'' ya tatizo
Waziri alipaswa kusema, ni kijana wake na sheria ichukue mkondo ni mtu anayejitegemea.
2. tortuous liability ina limitation ndiyo maana ya kuwa na umri. Mzazi anakoma kuchukua responsibility katika umri fulani kutegemea nchi. Kwa Tanzania ni miaka 18.
Wazazi hawastakiwi kwa dereva wa miaka 20 aliyelewa na kuua watu. Kwanini Simbachawene abebe dhamana milele?
3. kosa alilofanya kijana halihusiani na uzembe wa waziri hakutumia gari au kifaa cha kazi za waziri.
PM Boris Johnson wa UK alishtakiwa kwa kukiuka sheria za lockdown alizoweka kama kiongozi.
Laiti ile 'party' ingefanywa na mkewe bila Johnson kuhudhuria , metropolitan Police wasingemhoji Boris bali mkewe na Bunge lingemtaka Boris ajisafishe ''ethical Issue''
4. Vicarious liability inatokea sana kwenye kazi, ima boss au msimamizi au agent anachukua dhamana ya waajiriwa. Katika familia tunazungumzia tortious liability zaidi kuliko vicarious liability.
Ulipotuhumiwa kulidhalilisha Bunge, Marhum mzee Mayalla habebi chochote kati ya liability hizo mbili.
5. Mzee mwinyi alijiuzulu kuchukua responsibility za walio chini yake.
Ilikuwa ni lazima alikuwa Waziri wa serikali ya Nyerere. Serikali ilikiri kosa, kamaasingejiuzulu Nyerere angepaswa.
Dhana ya kujiuzulu ni kumkinga boss na dhahma ima kwa uzembe wa moja kwa moja au kupitia wa chini yako kwa kuonyesha kukiri kosa au kujutia.
Nimalizie, Waziri alichukua dhamana ya jina lake lililotumiwa na mtoto wake anayejitegemea.
Kijana wake anajitegemea na anawajibika kwa makosa yake.
Tortious liability imefika kikomo, sheria ichukue mkondo wake kwa Raia aliyetenda kosa si mtoto wa Waziri.
Akishtakiwa kama mtoto wa waziri tayari kuna ku 'compromise ' mfumo wa kutoa haki.
Waziri hapaswi kujiuzulu kwa hili!
JokaKuu Tindo