SIMIYU: Levinus Kidanabi Jela miaka saba na faini mil 15 kwa kumkashifu Rais Samia

Kwani viongozi wenyewe wa sisiemu wanasemaje? Afungwe mwana sisiemu lawama ziwaendee kina Lissu. Mataga ni nani aliewaloga?
 
Wafuasi wa Magufuli hata wafungwe hata wauawe sitasikitika, waovu sana
Kama walikuwa wakishangilia Lissu kupigwa risasi ya nini kuwatetea, hawa ni wanyama
 
Mbowe alipowekwa gerezani kwa miezi kadhaa kwa kesi feki ya ugaidi, na nyie mkijua kabisa ni kesi feki mlifanya nini? Si mlikuwa mkishangilia? Nyang'au nyie
 
Mbona watu wamejitokeza kumtetea tena mpaka Chadema wanataka kumkatia rufaa au wamchangie atoke jela.

NB
Huyo jamaa tulisoma nae Kampala maarufu kwa jina la Nyanda wakati tupo pale alitingisha chuo kizima kwa misimamo na hoja zake alikua amung'unyi maneno hata kidogo..mara ya mwisho nilikutana nae 2020 aliniambia ameingia kwenye siasa mzima mzima ila hapendezwi na jinsi watanzania wanavyopotezwa kwenye nchi yao hakua mnafki huyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sidhani kama Public Figures nao wanahitaji Fake I'ID's...ila kwa Tanzania lolote linawezekana mkuu!
Viongozi wengi Tanzania ni wa janjanja Kama sisi humu tulivyo!!
 
Wapinzani unajua siwaelewi wamechuna chuu kwenye mambo mengi makubwa. Hii inaelezea ni kwa namna gani hawa wanaojinasibu kuwa ni wapinzani wasipopewa kitu kidogo wanakuwa mbogo ila wakipewa wanakuwa wapole kama paka msafi.

Kimsingi upinzani unahitaji overhauling.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umesema ya Moyoni mwako,mimi siwezi kuyabadilisha aslani.

Mimi sio mwana CCM wa aina hiyo unayoifikiria.
Bali mwana CCM ambaye nimesimama kupinga uchotwaji wa mali na jasho la walipakodi wa nchi hii.

Nilimpigia salute Magufuli kwa sababu,mdie mwana CCM pekee aliyeupata uraisi kupitia CCM,lakini hakuwaonea aibu wana CCM wenzake.
Pale lilipokuja suala la mali za umma.tuliona kwa mara ya kwanza,mtu aliyeweza kutuaminisha kwamba CCM inaweza isiwe ile ile.

Samia amerudishwa na kundi lake ni uelekeo wa kule tulikokuwa tunaelekea kupaacha.

Huenda Magufuli aliwaumiza kundi kubwa la watu nchi hii,kutokana na baadhi ya maamuzi yake.

Lakini Kwa asilimia kubwa,lengo lake ilokuwa ni kuhakikisha,keki ya taifa inawanufaisha watanzania wote.
Na sio tabaka dogo la wahafidhina ndani ya CCM pamoja na washirika wao kimgumo toka sekta zingine binafsi na hata baadhi ya vyama vya upinzani nchini.

Walau Magufuli alikuwa na vision ya kumuonyesha mtanzania mahali alipotaka taifa hili lielekee.

Tofauti na Samia ambaye pamoja na kusambaza pesa na Miradi lukuki nchi nzima.
Lakini ukimuuliza anapotakackuifikisha nchi hii na kuiacha ndani ya utawala wake.
Hapaeleweki.

Unafungua nchi,lakini wanaonufaika ni hao wanaokula posho za safari,kila siku wakipishana angani huku yeye Samia akiwa kinara.

Unafungua nchi huku wakenya wakikomba vyakula hadi mashambani na kutuachia janga la upandaji bei holela nchini.

Unafungua nchi kwa wawekezaji uchwara wa viwanda uchwara vya wachina.
Wanaotukaanga kwa mafuta yetu yenyewe.

Unafungua nchi,ili Makamba aingize wateja wa 20% Kwenye sekta nyeti za nishati ya gesi na umeme keanza.

Tunsongea tunayoyaona na sio ya kufikirika .

Wewe unayekaa ukimuwaza Magufuli saa zote,
Lazima kuna mahali alikunyanganya tonge mdomoni.
Magufuli hakuwa adui wa commonwananchi bali alikuwa adui wa "state captures" na "state cartels"
 
Wafuasi wa Magufuli hata wafungwe hata wauawe sitasikitika, waovu sana
Kama walikuwa wakishangilia Lissu kupigwa risasi ya nini kuwatetea, hawa ni wanyama
Muda utaongea tu,na soon wote mtaongea lugha moja.
Kuna wengi sana wamekufa zaidi ya huyo Lissu unayemsema wewe.

Dk Ulimboka wakati anachomolewa meno ilikuwz kipindi cha nani?

Yule Mwangosi alipigwa Bomu kipindi cha nani?

Watu waliokufa kwenye mikutano Arusha ilikuwa kipindi cha nani?

Sio kipindi cha huyuhuyu aliyeshikilia rimoti saa hii?
 
Well said
 
Good
 
Mimi nikiona mwana CCM kijana kapata majanga kama hayo huwa nafurahi sana sijui nikoje.
[emoji35][emoji35]
 
Wana CCM wana IQ kubwa hawawezi,kamwe hawawezi kumtusi Rais mama yetu mpendwa.Hilo litakuwa jambazi la kile chama kisichojitambua na hilo shati lililovaa ni la wizi kutoka ofisi za chama tawala.
Kama ni akili kubwa mbona Ndugai aliropokaropoka juzi kati hadi akapigwa pini na Mazaa mwenyewe?!
 
Watu wakweli wasiotumiwa na watu wanahitajika sana nchi hii. Waanzishe tu mchango, wengi watachangia.
 
Mkuu hivi mnapoongea haya mambo mnakuwaga na ushahidi wowote au ni story za Vijiweni tu??
 
Kwani viongozi wenyewe wa sisiemu wanasemaje? Afungwe mwana sisiemu lawama ziwaendee kina Lissu. Mataga ni nani aliewaloga?
Tena mwanaccm wa Bariadi huko, ngome ya sukuma gang! Imagine. Wavune walichopanda awamu ya 5. Ingekuwa kafungwa jela mwanaccm Kanda ya Mashariki au Kusini au Nyanda za Juu Kusini tungeuliza kunani?
 
Mkuu hivi mnapoongea haya mambo mnakuwaga na ushahidi wowote au ni story za Vijiweni tu??
Inawezekana wewe usiyajuwe kwa kiwango kile kile ambacho mimi ninakijua.
Inategemeana na upande gani umekulia.

Kama ni huko Mikocheni ni wazi huwezi kuyajua ya kule uswahilini Manzese.

Sababu unapita ukiwa umefunga vioo vyote juu,na A/C ikifanya kazi ndani kukuliwaza.

Na kama wewe ni sehemu ya wanaofaidi :keki"ya Taifa,pia huwezi kuwajua wale wanaokula "Makande" ya Taifa.

Unahitaji ushahidi gani kujua ni nani alikuwa rais wa nchi hii katika kipindi husika,wakati historia iko wazi,na matukio pia yako wazi,ni lini na wapi yalitokea?

Hizi kauli "una ushahidi" huwa ni common kwa kila mhal8fu.
 
Wanaongea mpaka mate yajae ndoo.

Ila kwakua sasa wanalamba asali wacha waendelee.

Asali ikisitishwa utawasikia tu.
 
Wanaongea mpaka mate yajae ndoo.

Ila kwakua sasa wanalamba asali wacha waendelee.

Asali ikisitishwa utawasikia tu.
Ni kweli.....ila muda ni shahidi pekee aliebaki kwetu watazamaji!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…