Voicer! Voicer!
Nimekuita mara 2 Kwa sababu Mimi ni miongoni mwa wafuatiliaji wa maandiko ya Kisiasa na kimaono humu JF na nimekuwa nikisoma maandiko yako mengi kuhusu upinzani na michango yako katika hoja zinazopongeza Wapinzani. Nilichokigundua ni kwamba unajua umuhimu wa upinzani ila huwa unajitoa ufahamu labda Kwa maslahi binafsi maana watu wengi maslahi binafsi hutangulia Kila kitu. Kuwa kwako CCM hakupaswi kukugeuza kuwa na roho ya kuunga mkono maumivu Kwa Wenye haki hata kama hawako upande wako. Nimachokiona kwako na wenzio mliokuwa wapiga Debe wa Sera za Magufuli na kuendeleza uhasama na kundi la Samia ndo maana unadhani waliopiga kelele Kwa matendo ya Magufuli Leo hawapigi kelele Kwa kiwango kilekile Kwa Samia. Wewe Hilo linakuumiza Sana lakini hukumbuki na wewe Una nafasi hiyo ya kupiga kelele kupinga dhuluma na uonezi.
Huyu kijana wa Bariadi kweli kaonewa, lakini watu wamepiga kelele tena wengine Kwa verified IDs kama alivyofanya Wakili Jebra Kambole. Kama maoni ya kusema "Hata Samia hili limemshinda" ni kumkashifu basi kumbe Samia ana uwezo wa Kimungu wa kutoshandwa chochote.
Ni wajibu wako wewe kama mwananchi bila kujali itikadi yako kukemea uovu na kuhimiza haki. Lakini wenzetu mmegeuza sitahiki ya haki iwe upande wenu tu, Kwa walio kinyume chenu kimtazamo haki Yao ni Mateso, Badilikeni Sasa au msubiri wakati uwabadilishe.
Mkuu umesema ya Moyoni mwako,mimi siwezi kuyabadilisha aslani.
Mimi sio mwana CCM wa aina hiyo unayoifikiria.
Bali mwana CCM ambaye nimesimama kupinga uchotwaji wa mali na jasho la walipakodi wa nchi hii.
Nilimpigia salute Magufuli kwa sababu,mdie mwana CCM pekee aliyeupata uraisi kupitia CCM,lakini hakuwaonea aibu wana CCM wenzake.
Pale lilipokuja suala la mali za umma.tuliona kwa mara ya kwanza,mtu aliyeweza kutuaminisha kwamba CCM inaweza isiwe ile ile.
Samia amerudishwa na kundi lake ni uelekeo wa kule tulikokuwa tunaelekea kupaacha.
Huenda Magufuli aliwaumiza kundi kubwa la watu nchi hii,kutokana na baadhi ya maamuzi yake.
Lakini Kwa asilimia kubwa,lengo lake ilokuwa ni kuhakikisha,keki ya taifa inawanufaisha watanzania wote.
Na sio tabaka dogo la wahafidhina ndani ya CCM pamoja na washirika wao kimgumo toka sekta zingine binafsi na hata baadhi ya vyama vya upinzani nchini.
Walau Magufuli alikuwa na vision ya kumuonyesha mtanzania mahali alipotaka taifa hili lielekee.
Tofauti na Samia ambaye pamoja na kusambaza pesa na Miradi lukuki nchi nzima.
Lakini ukimuuliza anapotakackuifikisha nchi hii na kuiacha ndani ya utawala wake.
Hapaeleweki.
Unafungua nchi,lakini wanaonufaika ni hao wanaokula posho za safari,kila siku wakipishana angani huku yeye Samia akiwa kinara.
Unafungua nchi huku wakenya wakikomba vyakula hadi mashambani na kutuachia janga la upandaji bei holela nchini.
Unafungua nchi kwa wawekezaji uchwara wa viwanda uchwara vya wachina.
Wanaotukaanga kwa mafuta yetu yenyewe.
Unafungua nchi,ili Makamba aingize wateja wa 20% Kwenye sekta nyeti za nishati ya gesi na umeme keanza.
Tunsongea tunayoyaona na sio ya kufikirika .
Wewe unayekaa ukimuwaza Magufuli saa zote,
Lazima kuna mahali alikunyanganya tonge mdomoni.
Magufuli hakuwa adui wa commonwananchi bali alikuwa adui wa "state captures" na "state cartels"