Simiyu: Watu 14 wafariki dunia kwenye ajali katika msafara wa Mkuu wa Mkoa Mwanza

Mwendo Kasi ni tatizo
 
Huu utaratibu wa magari yaliyoko kwenye msafara wa viongozi kuendeshwa kama yanaendeshwa na vichaa ufikia mahali ufe.

Hakuna wanapowahi zaidi ya kaburini tu halafu utasikia "ni mpango wa Mungu".

Stupid fools.
Ni kweli wakati mwingine madereva wa serikali hujiona wana haki tofauti katika matumizi ya barabara. Na hapo utasikia wametolea kafara.
 
Waandishi wa habari tafuteni habari sio kufuatana na misafara ya wanasiasa matapeli
 
Mimi ninashauri hawa madereva wa serikali wanunuliwe gari za kawaida kama za kwetu watu wa chini. Hizi gari zenye uwezo mkubwa zinawapa viburi na kujiamnini kukimbia mwendokasi wenye matokeo kama haya. Inatakiwa wapewe gari kama kirikuu (suzuki carry) ili tuone kama wataendelea na mwendokasi, wameonywa lakini hawasikii.
 
Si kwa ubaya ila gari la mwanzo limeandikwa Kazi iendelee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…