Simiyu: Watu 14 wafariki dunia kwenye ajali katika msafara wa Mkuu wa Mkoa Mwanza

Simiyu: Watu 14 wafariki dunia kwenye ajali katika msafara wa Mkuu wa Mkoa Mwanza

Watu 14 wamefariki dunia baada ya gari ya waandishi wa habari iliyokuwa kwenye msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (RC), Robert Gabriel kugongana na gari ya abiria Hiace katika eneo la Nyamikoma wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.

Mkuu wa Wilaya ya Busega (DC), Gabriel Zakaria amethibitisha kutokea vifo hivyo.

--
Rais Samia atoa salamu za Rambirambi

''View attachment 2076839

====


Watu 14 wamefariki dunia baada ya gari la waandishi wa habari iliyokuwa kwenye msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (RC), Robert Gabriel kugongana na gari ya abiria Hiace katika eneo la Nyamikoma wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu akiwa eneo la tukio, Mkuu wa Wilaya ya Busega (DC), Gabriel Zakaria amethibitisha kutokea vifo hivyo.

Amesema kati ya vifo hivyo kuna vifo vya waandishi wa habari wanne na dereva wa waandishi na watu wengine sita walifariki papo hapo

“Ni kweli ajali hiyo imetokea, watu 11 wamefariki kwenye eneo la tukio wakiwemo waandishi wa habari 4 na dereva na wengine sita waliokuwa kweneye gari lingine” amesema Zakaria na kuongeza

“Dakika chache majeruhi waliopelekwa kwenye kituo cha afya cha Nasa watatu walifariki, wakiwemo wale waandishi wa habari waliokuwa kwenye msafara”

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyo, Blasius Chatanda yupo katika hospitali ambako majeruhi walikopelekwa akiahidi kuwa atatoa taarifa baadaye.

Chanzo: Mwananchi

======

UPDATES;

=====

Waandishi waliofariki kwenye ajali ya gari ni

1. Husna Mlanzi wa ITV

2. Vanny Charles wa Icon. TV

3. Johari Shani wa Uhuru Digital

4. Antony Chuwa wa Habari leo Digital

5. Abel Ngapemba Afisa habari Mwanza

6. Steven Msengi Afisa Habari Ukerewe

7. Paul Silanga Dereva wao

Miili yao imehifadhiwa katika Kituo cha Afya Nassa wilayani Busega mkoani Simiyu.

Kila Serikali inakujaga na yake... Naona Mama ameingia kama Mkapa.. Hata sijui haya ni maagano gani!?
Hata mwezi nafikiri wamefika 40...
 
Magari ua viongozi na misafara yao ndiyo yanayoongoza kwa kuendeshwa ovyo, ja kuvunja sheria za usalama barabarani.
 
Speed kali kupindukia ndio msafara unakuwa msafara? Hivi hao wengine si wangetangulia, mpaka muongozane kiasi hicho? Sio ya kutengeneza?

Tume iundwe (ikiongozwa na Spika mjiuzulu) kuchnguza ajali hiyo.
 
Ajabu waandishi wa habari wanabebwa kama magunia na kupewa vibahasha vya posho ya mboga ilimradi tu wakaripoti habari kumpaisha mwanasiasa.. waandishi wa habari mjitathmini...kutwa kikimbilia kwenda kuripoti matukio ya wanasiasa na huku mtaani matukio ya wananchi, kero na maoni kuhusu serikali yao yamejaa ila hamuendi..

Uko sahihi, je ndio chanzo cha hii ajali ya leo?
 
Huu utaratibu wa magari yaliyoko kwenye msafara wa viongozi kuendeshwa kama yanaendeshwa na vichaa ufikia mahali ufe.

Hakuna wanapowahi zaidi ya kaburini tu halafu utasikia "ni mpango wa Mungu".

Stupid fools.

Maafisa wa Marekani wakati wakitathimini hali na usalama wa rais wa Baraka Obama alipokuja Tanzania, wali konklud kuwa barabara zetu ni mbovu na hatarishi sana kwa usalama wa rais wao, hivyo katika msafar wake aendeshwe kwa mwendo mdogo from ubungo tanesco to airport.

nashangaa usalama wetu wanapo ruhusu kukimbizwa kwa viongozi wetu kwa mwendo wa mashindano ya magari, as if kuna imejensi huko waendapo given ubovu wa barabara.

Nakuunga mkono mkuu..
 
Sema inawezekana nyuma ya pazia wanaambiwa wasitoe uhamisho izi maswala ya serikali kuna mengi sana
Wanaambiwa na Nani wakati katibu mkuu kashasaini kibali mtu ahame, na wakati huo halmashauri nyingine watu wanapewa vibali....ni kutoheshimu mamlaka na roho mbaya tu ya huyo mkurugenzi, haya mwenzie kafariki sasa, hiko kibali akafungie vitumbua, au akibandike ukutani iwe ukumbusho.
 
Kuwa Mwafrika ni tatizo, hivi kuna haja gani mkuu wa mkoa kutembea na wanahabari wengi kiasi hichi?
Hao 6 ndio waliofariki, je waliopona na waliofariki jumla ya waandishi wa habari walikuwa wangapi?
Dah.... RC wa Mwanza ndani ya Simiyu...ziara ya kikazi..... Kama bi Mkubwa anashinda ndani ya ndege....Basi wengine Ni kina Nani hasa hata wasipende padiemu? 🤣🤣🤣🤣🤭
 
Kutokana na uwongona unafiki wa serikali hii ya kusema walioachwa ni kwasbsb ya kuwania urais ,, mwenyezi mungu kwa kukataa unafiki, leo ajali ya msafara wa mkuu wa mkoa umesababisha maafa ya watu 18 na majruhi wengi na waliathirika zaidi wakiwa ni waadishi wa habari. Bila kutubu dhambi zetu basi mwaka huu ukame utakuwa mkali na amamfa yatatuandama, kazi kwenu
 
Dah.... RC wa Mwanza ndani ya Simiyu...ziara ya kikazi..... Kama bi Mkubwa anashinda ndani ya ndege....Basi wengine Ni kina Nani hasa hata wasipende padiemu? 🤣🤣🤣🤣🤭
Walikuwa wanaelekea Ukerewe, kufika Ukerewe kuna njia mbili, moja ya Meli pale Mwanza, na nyingine kupitia Bunda ambako wangepanda kivuko.
Hao walipita hiyo ya Bunda ambayo unapitia Wilaya ya mkoa wa Simiyu.
Mama anahusikaje hapo?
 
Nina rafiki zangu kibao kwenye tasnia hiyo waliopo Mwanza. Natamani nifahamu majina ya waathirika, lakini nimeshindwa kuwapigia simu mmoja mmoja! Natamani niwatambue kwa njia nyingine!
Aliyepata majina, naomba atupatie!
Waandishi waliofariki kwenye ajali ya gari ni

1. Husna Mlanzi wa ITV

2. Vanny Charles wa Icon. TV

3. Johari Shani wa Uhuru Digital

4. Antony Chuwa wa Habari leo Digital

5. Abel Ngapemba Afisa habari Mwanza

6. Steven Msengi Afisa Habari Ukerewe

7. Paul Silanga Dereva wao

Miili yao imehifadhiwa katika Kituo cha Afya Nassa wilayani Busega mkoani Simiyu.
 
Back
Top Bottom