Simiyu: Watu 14 wafariki dunia kwenye ajali katika msafara wa Mkuu wa Mkoa Mwanza

Simiyu: Watu 14 wafariki dunia kwenye ajali katika msafara wa Mkuu wa Mkoa Mwanza

Duh Apumzike kwa amani maisha haya sijui anajidillsikiaje huko alipo
Afanye sherehe msibani, na hicho kibali alichokikalia akitumie yeye kuhama.
Na nasikia amekalia vibali vya watumishi wengine wa hiyo halmashauri.
Yani mtu kakamilisha michakato yote, tamisemi wamempa go ahead hama na kibali wamekituma halmashauri, Mkurugenzi anagoma kusaini na kumpa afunge taarifa ahame.
Inauma.
 
Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali ya gari iliyosababisha vifo vya Maafisa Habari, Waandishi wa Habari wa Mwanza na Wananchi. Natoa pole kwa Familia za Marehemu, Waandishi wa Habari wote, ndugu, jamaa na marafiki. Mungu aziweke mahali pema roho za marehemu wote, Amina.
Nape Moses Nnauye

https://t.co/GR9jXA1l4I
 
Moja wa waandishi waliofariki ni huyu Johari Shani wa Uhuru.
IMG-20220111-WA0011.jpg
 
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza alikuwa na ziara Mkoa wa Simiyu?
Umeniwahi kuuliza swali hilo, nakushukuru.

Mkuu wa Mkoa mmoja hawezi kupeperusha bendera yake kwenye mkoa mwingine itifaki inakataza, vivyo hivyo kwa Ma-DC.

Mkoa wa Mwanza umetenganishwa na mkoa wa Mara na mkoa wa Simiyu ambao uko katikati ya Mwanza na Mara, sasa RC wa Mwanza alikuwa anaenda Mara au?

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel naye amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema yuko njiani kuelekea eneo la tukio.
Taarifa imesema RC wa Mwanza msafara huo ulikuwa ni wake, sasa nakunukuu "yuko njiani kuelekea eneo la tukio" tuamini lipi kwamba alikuwa kwenye msafara huo au hakuwemo? Kama msafara haukuwa wa kwake kwanini basi kwenye tukio asiende RC wa Simiyu ambaye tukio limetukia kwenye eneo lake?

Hawajali hata barabara ya mwendokasi wanakatiza tu bila kujali kisa wamechukua silaha
Sijawahi kusikia Askari ameshitakiwa kwa kuvunja sheria za usalama barabarani japo tunawaona kila mara wakizivunja hadharani (Mlinda sheria anayetangulia kuvunja sheria), kama hamuamini basi katafuteni kwenye rekodi za Mahakama kama mtapata shauri kama hilo tangu nchi kuwa huru. Zipo scenario ambazo sheria za usalama barabarani zinaweza kuvunjwa e.g. Ambulance, Zimamoto, Misafara ya viongozi wa kitaifa na kimataifa, maandamano yanayopita barabarani yenye kibali halali.
Ajabu waandishi wa habari wanabebwa kama magunia na kupewa vibahasha vya posho ya mboga ilimradi tu wakaripoti habari kumpaisha mwanasiasa.. waandishi wa habari mjitathmini...kutwa kikimbilia kwenda kuripoti matukio ya wanasiasa na huku mtaani matukio ya wananchi, kero na maoni kuhusu serikali yao yamejaa ila hamuendi..
Wanasiasa hawapendi kuona au kusoma kero (hawapendi ziripotiwe) wanapenda kuona au kusoma habari zenye matokeo chanya tu ya kazi zao.

“In politics if you want anything said, ask a man. If you want anything done, ask a woman.”
 
Afanye sherehe msibani, na hicho kibali alichokikalia akitumie yeye kuhama.
Na nasikia amekalia vibali vya watumishi wengine wa hiyo halmashauri.
Yani mtu kakamilisha michakato yote, tamisemi wamempa go ahead hama na kibali wamekituma halmashauri, Mkurugenzi anagoma kusaini na kumpa afunge taarifa ahame.
Inauma.
Inawezekana kulikuwa na mvutano kati marehemu na Mkurugenzi na hivyo kuamua kutomshirikisha kuhusu kutaka kuhama. Mkurugenzi kuona hajashirikishwa akaamua kutompa ushirikiano marehemu na hivyo kuhisi kama ilikuwa ni insubordination kwa Mkurugenzi which is not the case!!

R.I.P kijana!
 
Afanye sherehe msibani, na hicho kibali alichokikalia akitumie yeye kuhama.
Na nasikia amekalia vibali vya watumishi wengine wa hiyo halmashauri.
Yani mtu kakamilisha michakato yote, tamisemi wamempa go ahead hama na kibali wamekituma halmashauri, Mkurugenzi anagoma kusaini na kumpa afunge taarifa ahame.
Inauma.
Sema inawezekana nyuma ya pazia wanaambiwa wasitoe uhamisho izi maswala ya serikali kuna mengi sana
 
Hivi huko upolisini na serikalini hakuna hata mtu mmoja wa kuweza kuwakanya wakuu wa misafara ya viongozi kwenda mwendo wa wastani?
Hao wakuu kwenye misafara nao wanadhani wanaokufa kwenye ajali Ni watu wadogo tu?
Kama ndivyo Basi sawa....
 
Kuwa Mwafrika ni tatizo, hivi kuna haja gani mkuu wa mkoa kutembea na wanahabari wengi kiasi hichi?
Hao 6 ndio waliofariki, je waliopona na waliofariki jumla ya waandishi wa habari walikuwa wangapi?
Halafuwangeandika Nini?
Badala ya kuandika investigative stories waandishi wa Sasa wanasubiri waitwe na viongozi walishwe story.
 
Back
Top Bottom