Watu 14 wamefariki dunia baada ya gari ya waandishi wa habari iliyokuwa kwenye msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (RC), Robert Gabriel kugongana na gari ya abiria Hiace katika eneo la Nyamikoma wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Busega (DC), Gabriel Zakaria amethibitisha kutokea vifo hivyo.
--
Rais Samia atoa salamu za Rambirambi
''
View attachment 2076839
====
Watu 14 wamefariki dunia baada ya gari la waandishi wa habari iliyokuwa kwenye msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (RC), Robert Gabriel kugongana na gari ya abiria Hiace katika eneo la Nyamikoma wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.
Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu akiwa eneo la tukio, Mkuu wa Wilaya ya Busega (DC), Gabriel Zakaria amethibitisha kutokea vifo hivyo.
Amesema kati ya vifo hivyo kuna vifo vya waandishi wa habari wanne na dereva wa waandishi na watu wengine sita walifariki papo hapo
“Ni kweli ajali hiyo imetokea, watu 11 wamefariki kwenye eneo la tukio wakiwemo waandishi wa habari 4 na dereva na wengine sita waliokuwa kweneye gari lingine” amesema Zakaria na kuongeza
“Dakika chache majeruhi waliopelekwa kwenye kituo cha afya cha Nasa watatu walifariki, wakiwemo wale waandishi wa habari waliokuwa kwenye msafara”
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyo, Blasius Chatanda yupo katika hospitali ambako majeruhi walikopelekwa akiahidi kuwa atatoa taarifa baadaye.
Chanzo: Mwananchi
======
UPDATES;
=====
Waandishi waliofariki kwenye ajali ya gari ni
1. Husna Mlanzi wa ITV
2. Vanny Charles wa Icon. TV
3. Johari Shani wa Uhuru Digital
4. Antony Chuwa wa Habari leo Digital
5. Abel Ngapemba Afisa habari Mwanza
6. Steven Msengi Afisa Habari Ukerewe
7. Paul Silanga Dereva wao
Miili yao imehifadhiwa katika Kituo cha Afya Nassa wilayani Busega mkoani Simiyu.