Simtetei Dr. Nawanda, ila binti anaweza kuwa ni tatizo?

Ndunguru J, alitengua kifungo Cha rape kwa Said Seleman kwenye rufaa thus akabakiwa na miaka 7 ya abduction.
 
Mkuu Pascal Mayalla salam,
Wewe ni miongoni mwa great thinkers wachache waliobaki humu JF ila nasikitika sana kusoma huu mtazamo wako kwa mambo kadhaa:
1. Ufahamu wa kawaida tu unataka mhanga yoyote wa masuala ya unyanyasaji wa kingono alindiwe utambulisho wake. Hata jeshi letu la Polisi kwenye taarifa yake kuhusu hii kesi imehifadhi jina la mhusika. Hii nguvu kubwa ya kumuanika mhanga identity yake inaleta mashaka ya nia ya yoyote anayefanya hivyo. Kwa nini tusijikite kwenye actual facts (alleged?). Mtu akilalamka amebakwa kinachoangaliwa ni nini?
2. Kigezo kikubwa cha ubakaji ni ridhaa. Je hiyo inayodaiwa kuwa historia ya mhanga huyu inaondoa ridhaa yake juu ya mwili wake mwenyewe? Kuna jambo lolote lile ambalo mtu akilifanya leo, basi linamuondolea uwezo wa kubakwa? Hujawahi kusikia kitu kinaitwa marital-rape?
Kama Mke halali wa ndoa bado ana full right ya mwili wake, kwa nini unadhani binti huyu hana haki ya kudai amebakwa kwa sababu aliwahi kubakwa before?
3. Nimepitia hiyo kesi ingawa kwa juu juu. Bado sioni hoja yoyote ya maana. Binti alikuwa 16 years old, na kwa sheria zetu alikuwa ni minor, boda boda alishtakiwa for statutory rape. Shitaka hili la statutory rape lilifeli kutokana na kushindwa kufikia standard ya proof beyond reasonable doubt, sio kwamba dunia nzima haijui kuwa bodaboda alikuwa analala na huyu binti. Binti angepata mimba kusingekuwa na mashaka, au labda coincidentally wangekamatwa wakiwa ndio wametoka kufanya ngono, ushahidi wa actual penetration ungepatikana. Hii ndio maana bado akafungwa kwa shitaka la pili la abduction ambalo hilo lilikuwa na ushahidi usiopingika. In short Bodaboda ameponea technicality tu, he was guilty!
Mlalamikaji kwenye hiyo kesi alikuwa ni nani? Binti ndie aliyekwenda polisi kudai amebakwa? au binti alikuwa anatafutwa akakutwa kwa Bodaboda?
Umeniangusha learned brother!
 
All in all Hilo tukio ni baya mno, hata kama umesingiziwa sijui unajioshaje....Bora kubaka kuliko kutuhumiwa kula ndogo, jamii haiwez kukuelewa.
 
Uyo binti anamatatizo ila hapo kwa uyo jamaa boda boda sikuungi mkono kabisa, hawa jamaa ni waharibifu mno kama unabinti yako au wadgo zako wa kike utakubaliana na mimi. Ukiisoma hadi mwisho mshkaji hakuhukumiwa kwa kesi ya kubaka ila kwa kosa la kumtorosha mtoto wa watu (below 18 hana uwezo wa kufanya maamuzi alishawishiwa) mwamba alihukumiwa kwa miaka 7.
Binafsi natakaga wapigwe hata miaka 30 tu hawa jamaa wanatia sana hasira
 
Swali, kwa nini anayesababisha kesi awe ni yule yule?
 
Sikuwahi kufikiria kwamba kuna siku serikali itakuja kuwapeleka watanzania kwenye siasa za Tigo.
Ikaanza kidogokidogo kwa waliokuwa wakitekwa sababu ya kuipinga seriksli wakawa wanawapenya ili kuwaharibu kisaikolojia, lakini sasa imeshafanywa kuwa kawaida kiasi cha kuwa habari ya kitaifa kuliko hata msina kwa jirani, kuliko hata hotuba ya bajeti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…