Simu Janja kama Mashine ya EFD - Nafuu kubwa kwa wajasiliamali na wafanya biashara

Simu Janja kama Mashine ya EFD - Nafuu kubwa kwa wajasiliamali na wafanya biashara

We twende tartiiibu !mbona kama sijaelewa??
Gharama elfu 50 kwa mwaka , si ndio? Hii laki 4 one time fee ni kitu gani?
Si bora ninunue efd machine kwa 580000, with no strings attached?
Ubabaishaji mtupu, hizi kazi za kupeana bado ni tatizo sana
 
Hongereni sana. Nilitoa hili wazo siku za nyuma. Kinachokera ni kwamba badala ya TRA kuja na hiyo application, wameruhusu (?) watu binafsi kutengeneza apps hiyo ndio maana mnatutaka kulipa hiyo shs 50,000 kwa mwezi au 400,000 kama one-time fee. Kwa hiyo tunalipia tena kama EFD machine tu.

TRA wapuuzi sana, hii kitu tuliipigia kelele sana. Hakuna haja ya kulazimisha matumizi ya EFD machine (hardware) nyakati hizi wakati inawezekana kabisa kuwa na software tu.
Huko TRA kumesheheni WAPIGAJI TUPU,mimi nitaanza kulipa kodi kikamilifu siku watakapohamia kwenye software ambazo kimsingi zinapaswa kuwa BURE KABISA.
 
Nadhani umeninikuu vibaya hii TRA wanatoa bure.. Pesa tunayochukua sisi... Tunaichukua sisi, Haiendi kabisa TRA wala hawatupangii kiasi. Yani wakati tunasajili kampuni tungesajili kama wamisionari tungekua tunatoa bure pia
 
Hapa unaweza pata PDF File au ukaituma kama picha.... Mteja wako kama hajaelimika anaweza kukulazimisha uwe na printer ila mwingine unamtumia tu na inakubalika na TRA
Mkifikia mnahitaji Printer, mnambie, ninazo Digital printer ndogo...
 
Mkifikia mnahitaji Printer, mnambie, ninazo Digital printer ndogo...
Ndio zitatufaa sana... Sisi tunatoa software pekeake kama unabei nzuri naweza recommend waje wachukue kwako... Naweza pata picha na bei?
 
Karibu mno.

kidonto nimekutumia PM. unaweza zituma hapa kwa manufa a wengine pia
Nilishawahi kuzitangaza hapa miaka ya nyuma, na sikupata mteja, muhimu ni kukubaliana na ww, then wewe ukiwa unaongea na wateja wako utawapa full package price iki include hiyo printer!
 
AMBWENE KONZO LIMITED WANAKUPA NAMNA , RAHISI, SALAMA NA NAFUU ZAIDI YA KUTOA RISITI ZA TRA KWA KUTUMIA SIMU,KOMPYUTA,POS AU MFUMO WAKO ULIONAO. HUNA HAJA YA KUNUNUA MACHINE.
ILIKUPATA HUDUMA UNATAKIWA KUWA NA:

  • NAKALA YA TIN CERTIFICATE YA BIASHARA
  • BARUA YA MAOMBI KWA TRA KUTOKA MMILIKI

JITENGENEZEE BARUA KWA KUTEMBELEA TOVUTI YETU, TUANDIKIE TUKUHUDUMIE
UNAWEZA ANZA NA SIMU ULIYONAYO KISHA UKANUNUA VIFAA VINGINE BAADAE.

[EDIT]
TRA ndio watapitisha ombi lako kabla hujaanza kutumia hivyo ni vizuri uwe umefanyiwa au umefanya makadirio ya kodi na unalipa au umeahidi kulipa.

240573377_372022187754977_391034581021199161_n.jpg

239437248_372017507755445_1946388517785372504_n.jpg

239698002_372019544421908_995944875179231592_n.jpg

Bando nayo je ni lazima?
 
Nilishawahi kuzitangaza hapa miaka ya nyuma, na sikupata mteja, muhimu ni kukubaliana na ww, then wewe ukiwa unaongea na wateja wako utawapa full package price iki include hiyo printer!
Ulitangaza wapi? Unaweza kuweka link?
 
Bando nayo je ni lazima?
Ndio, lakini sio wakati wote, walau mara moja kwa wiki ili mfumo utume mauzo yako TRA, unaweza ukatumia wi-fi au ukarusha hotspot pia au ukadandia internet yoyote utakayooipata.
Nilishawahi kuzitangaza hapa miaka ya nyuma, na sikupata mteja, muhimu ni kukubaliana na ww, then wewe ukiwa unaongea na wateja wako utawapa full package price iki include hiyo printer!

Ndio biashara zilivyo, watejawanataka waone tangazo lako mara nyingi mno ili waweze kukumbuka kununua kwako siku wakihitaji.
Ni kweli tuna nafasi kubwa ya kuuza kama pakage biashara nyingi bado zinataka kutoa karatasi.
 
TRA wanakubali hii ?, Yaani badala ya mtu kununua EFD kwa wale authorised dealers waliojiwekea mirija ya kujipa shavu yaani unatumia hii ?
Ndio wanakubali... Ni ngumu kuamini ila ipo hivyo... Tena sehemu yao wanafanya bure unatulipa sisi tu. Na kama una subira huenda wakafanya bure kila kitu hapo baadae. Ila kama unataka leo karibu sana
 
Ni ngumu kuamini ila ipo hivyo... Tena sehemu yao wanafanya bure unatulipa sisi tu. Na kama una subira huenda wakafanya bure kila kitu hapo baadae. Ila kama unataka leo karibu sana
Dah mkuu, bado hujafafanua vizuri kabisa yani
 
Dah mkuu,bado hujafafanua vizuri kabisa yani

Ni kweli jibu ni ndio TRA wanakubali ila lazima wafanye aproval kwanza, Ukisema panapokutatiza itakuwa rahisi kukufafanulia

We ni kutoa to risiti tu na kama mteja wako hajali unaweza mtumia tu bila kuchapa kama hivi...

Screenshot_20211021-1911142.png
 
Back
Top Bottom