Simu ya mpenzi wako kuwa Bize usiku mnaitafsiri vipi wakuu?

Markomx

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2016
Posts
809
Reaction score
981
Hodi wana jamvi,

Katika pirika za maisha japokua tunapambana kutafuta maokoto
Kunamda tunahitaji faraja angalau kutibu stress.ndipo pale tunakua na binadamu eva(mwanamke) ili kuweka msawazo wa uumbaji

Unakutana na binadamu ifikapo mida ya saa 3 usiku simu iko Bize,mbaya zaidi yupo kwao hana biashara za kuagizwa na wateja

Ila kunamda simu inatumika hadi saa 5 usiku unajiuliza,Hii simu ni ndugu gani wa kupiga usiku tu?

Najua Hii hali imenisumbua muda mrefu majibu ninayo ila nataka nanyinyi wakuu mnipe uzoefu

Hii hali hua mnaichukuliaje wakuu ukikuta mtu wako awe mwanamme au mwanamke kunamida simu yake inakua Bize muda wa kulala hua mnaitafsiri vipi?

Kifupi japo nakaribia kutoa mahali huu mchongo nataka kupiga chini .kupitia hizi simu sijawahi muamini kiumbe eva,japo hatujawahi suguana kesi nyingine zaidi ya simu za usiku
 
Kweli hii Hali imekusumbua muda kwa muda mrefu, na mpaka sasa ndio maana umekosa usingizi mpaka saa hizi, mkuu pole sana. Au haupo tz?
Any way it rains everywhere, watu wana watu wao.
 
Jibu ulilonalo laweza kuwa sahihi kwa %kubwa.

Milango ya fahamu ya mwanadamu ni zaidi ya masikio na macho.

Binadamu macho yetu na masikio yetu ni mafupi, ni rahisi kukingwa kwa hadaa.

Lakini mlango wa hisia na ufahamu, waweza kuona vizuri zaidi ya macho makavu.

Haujasikia: 'watu kuolewa ili kuondoa mikosi'?

Ama: 'ndoa ya hawara huwa haivunjiki' na misemo mingineyo kama hiyo?

Wewe sijui umewekwa katika hadhi gani katika group aliloliunda moyoni mwake.

Maana mnaweza kuwa wengi lakini wewe ukapewa hadhi ya juu sana na hadhi hiyo haikuzuii kuyajua yaliyopo nyuma ya pazia kutokana na hisia na ufahamu uliopewa.

'Tuishi nao kwa akili', uamzi ni wako mkuu.
 
Pole sana ila ukweli ni kwamba mpenzi wako ana mpenzi wake na wanapendana Sana hivyo wanapokuwa wote wewe huwekwa kwenye black list kwa muda!
 
Ukimuoa utampangia sheria zako,lakini sasa ni wa wote. Ukimchunguza sana bata...... Wewe muoe mkuu usimuache eti kisa 'anaongea sana na simu usiku' ukishamuweka ndani nyang'anya simu,muwekee sheria zako la sivyo hutaoa maana wanawake hasa mabinti wapo hali moja.
 
You may want to say Niebuhr’s serenity prayer:

"God grant me the serenity to accept the things I cannot change; courage to change the things I can; and wisdom to know the difference.“
 
Ndio maana nashindwa kufanya maamuzi magumu ,unaweza fanya maamuzi bila ushahidi ukapoteza
 
Hapo ujue hamna mke.kama ulikuwa na mpango wa kumuoa achana naye kimyakimya.Kikawaida kama anakupenda ikitokea umempigia na ikawa inatumika muda kuanzia saa nne usiku na kuendelea lazima akate na akusikilize wewe yofauti na hapo piga chini
Asante kwa ushauli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…