Simulizi: Harakati za Jason Sizya

Simulizi: Harakati za Jason Sizya

View attachment 2275058
184

“Mmh, makubwa!” yule muuguzi aliguna na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.

“Kwa vyovyote utakuwa umenichanganya na mtu mwingine, dada!” nilimwambia baada ya kumwona akiwa ameduwaa akinitazama kwa mshangao kama aliyeona kitu fulani cha kustaajabisha. Kisha nikaongeza, “Kwani hapa nipo wapi?”

“Upo hospitali, na mimi ni muuguzi wa wadi hii!” yule muuguzi aliniambia huku uso wake ukionesha wasiwasi kidogo.

“Najua kuwa nipo hospitali, wodini… ila nataka kujua nipo hospitali gani?” nilimuuliza tena huku nikiilamba midomo yangu iliyokuwa imekauka.

“Hospitali ya Wilaya ya Kilosa,” yule muuguzi alinijibu kwa sauti tulivu. Macho yake yalitulia kwenye uso wangu.

“Kilosa? Tangu lini nimelazwa hapa?” nilizidi kumsaili yule muuguzi huku mshangao wangu ukizidi.

“Leo ni siku ya tatu tangu uletwe hapa na jamaa zako ukiwa huna fahamu,” yule muuguzi alinijibu kwa utulivu huku akiendelea kunitazama kwa tuo.

“Kwa nini niletwe hapa Kilosa?” nilimuuliza tena kwa mshangao.

“Kumbe ulitaka upelekwe wapi! Kwani unajua nini kilikutokea hadi ukaletwa hapa?” yule muuguzi aliniuliza.

“Najua…!” nilimjibu kisha nikaongeza, “Tulikuwa tunatoka Arusha kwenye fungate na tunakwenda Dodoma, tukapata ajali eneo la Makutupora. Ninachoshangaa imekuwaje kutoka Makutupora niletwe huku Kilosa badala ya Dodoma au hata hospitali iliyo karibu na hapo?”

Na hapo nilimwona yule muuguzi akinitazama kwa mashaka mno, kwa namna ambayo sikuweza kupata tafsiri kabisa! Macho yake yaliongezeka ukubwa na kuwa ya duara na uso wake ulionesha kupambwa na mashaka makubwa. Sikujua alidhani labda nilikuwa nimerukwa na akili zangu!

“Samahani… kwani mke wangu yuko wapi?” nilimuuliza tena yule muuguzi na kumwona akishtuka kidogo, huenda nilikuwa nimemzindua toka kwenye mawazo yake.

“Alikuwepo hapa mchana alipoletea chakula akidhani labda umezinduka,” yule muuguzi alinijibu na kuitazama saa yake ya mkononi. “Hata hivyo bado dakika chache tu ufike muda wa kuona wagonjwa. Vuta subira huenda yeye akakufahamisha vizuri.”

Niliposikia hivyo nikapata matumaini nikiamini kuwa kumbe Rehema alikuwa mzima, nikaamua kujipa subira nikiamini kwamba angenifafanulia kila kitu.

“Kwa hiyo yeye ni mzima wa afya?” nilimuuliza yule muuguzi nikitaka kuhakikisha Rehema hakuwa na majeraha.

“Yeye hana shida ila mtoto ndiyo anaumwa,” yule muuguzi aliniambia jambo ambalo lilinifanya nijikute nikishangaa mno.

“Mtoto gani?” niliuliza kwa mshangao.

“Mtoto wenu, Mariam… kwani huna mtoto?” yule muuguzi alisema.

“Hatuna mtoto, ndiyo kwanza tumetoka kuoana,” nilimjibu huku nikianza kupata mashaka kuwa huenda alikuwa amenichanganya na mtu mwingine.

Kwa kusema hivyo nilimwona yule muuguzi akifungua mdomo wake kutaka kusema neno kisha akasita na kunitazama kwa mshangao mkubwa. Katikati ya mshangao wake alibetua midomo yake huku akinitazama kwa mashaka, “Daah! Basi kuna shida kubwa sana! Itabidi niongee na daktari wako.”

Sikusema neno, nilibaki na mshangao. Yule muuguzi akapiga kofi dogo la mshangao na kuongeza, “Mara sijui jina lako ni Jason nani, mara ooh nimepata ajali Makutupora, mara tumetoka kuoana! Dah… haya sasa makubwa!”

Nami nilimshangaa sana yule muuguzi, nilihisi kuwa kama ni kuchanganyikiwa basi ni yeye aliyekuwa amechanganyikiwa na si mimi. Nilimwona akishusha pumzi za ndani kwa ndani huku akiendelea kunitazama kwa namma ambayo ilinidhihirishia kuwa alikuwa kama anaona kitu cha kustaajabisha sana.

Huenda alidhani jeraha nililopata kichwani lilikuwa limeichanganya akili yangu. Kisha alitingisha kichwa chake na kuanza kuondoka.

“Nesi, samahani…” nilimwita yule muuguzi kabla hajatokomea na kumfanya ageuke kunitazama kwa wasiwasi, uso wake ulikuwa umejaa mashaka.

Alinitazama kwa kitambo akionekana kama aliyekuwa akijishauri iwapo arudi au aendelee na safari yake, kisha nikamwona akishusha pumzi na kusema, “Unasemaje, nisubiri nakuja sasa hivi.” Kisha aliondoka haraka na kuniacha nikiwa nimeshangaa sana. Nilimsindikiza kwa macho wakati akiondoka.

“Bila shaka watakuwa wamechanganya majina! Mgeni Mwema ndiyo nani?” nilijiuliza mwenyewe huku nikigeuza shingo yangu kuwatazama wagonjwa wengine mle wodini.

Hata hivyo, niliamua kuupisha utulivu kichwani mwangu huku nikiyazungusha macho kutazama mle wodini kisha nikayarudisha tena kule alikoelekea yule muuguzi. Na hapo fikra zangu zikahamia kutafakari juu ya Rehema na jamaa zangu.

Nilijiuliza kama kulikuwa na dosari yoyote juu yangu au pengine ni kweli nilikwisha anza kuchanganyikiwa! Na kwa nini yule muuguzi asisitize kuwa jina langu ni Mgeni wakati nilijua fika kuwa si langu? Hadi wakati huo nilikuwa na uhakika wa asilimia mia moja kwamba nilikuwa sahihi.

Swali jingine likawa; ni kweli Rehema alikuja pale hospitali akiwa na mtoto anayeitwa Mariam? Huyo Mariam alikuwa mtoto wa nani? Kila nilipojaribu kuwaza zaidi nilihisi kuchanganyikiwa mno. Sasa nilimwomba Mungu anipe unafuu haraka ili nitoke pale hospitali na kurudi nyumbani.

“Mgeni!” nilishtushwa na sauti ya mwanamume aliyeita kwa furaha huku akiharakisha kuja pale kitandani kwangu. “Mungu mkubwa, hatimaye umeamka?”

Nilishangaa sana na kumtazama yule mwanamume aliyeyasema hayo, kwa umakini, alikuwa mrefu na mwembamba akiwa amevaa suruali ya bluu ya dengrizi na shati la mikono mirefu la rangi ya samawati. Mkononi alikuwa amebeba mfuko mwekundu.

Mwanamume huyo alikuwa ameongozana na wasichana wawili, warembo ingawa walionekana wamechoka, mmoja wao alikuwa na mtoto wa miaka takriban mitatu. Wote walikuwa wakinitazama kwa furaha wakiwa hawaamini macho yao. Yule msichana aliyekuwa na mtoto alinyoosha mikono yake juu kumshukuru Mungu kisha akaharakisha kuja pale kitandani na kunikumbatia kwa furaha huku akitokwa na machozi ya furaha machoni.

Mwanzoni nilidhani labda walikuwa wamenifananisha na pindi wakigundua wangeniomba radhi na kuondoka lakini nilipomwona yule msichana mwenye mtoto akizidi kunikumbatia kwa nguvu na kuning’ang’ania huku akisema, “Jamani mume wangu…” nikamtazama kwa mshangao kisha nikayahamisha macho yangu kutoka kwa msichana huyo na kuwatazama wale wengine wawili. Nao walinitazama kwa furaha wakiwa hawana wasiwasi wowote.

“Nyinyi ni akina nani?” niliwauliza wale watu kwa mshangao huku hasira zikianza kuchipua ndani yangu, niliwakazia macho kwani nilihisi kitendo kile cha kuchangamkiwa na watu nisiowajua kilikuwa ni cha kutaka kucheza na akili yangu.

Wale watu wakaonekana kushtuka kidogo baada ya swali lile na kunitazama kwa mshangao mkubwa, kisha wakatazamana.

“Mume wangu, inamaana umenisahau kama ni mimi Zainabu mkeo?” yule msichana mwenye mtoto ambaye sasa nilimtambua kwa jina la Zainabu aliniuliza kwa mshangao huku akijaribu kunishika begani lakini niliusukuma mkono wake.

Endelea...
Kweli haya ni zaidi ya makubwa, hata mimi nashangaa tu, maskini Zainabu nakuonea huruma maskini
 
Mgeni mwema.jpg

189

Basi siulizi tena




Saa 8:15 mchana…

NILIKUWA nimepitiwa na usingizi mzito kitandani wakati niliposhtushwa na sauti ya mtu aliyekuwa ananyonga kitasa cha mlango kwa papara. Nilikuwa nimelala usingizi mtamu kuliko siku zote tangu niliporudiwa na kumbukumbu zangu, usingizi ulionifanya niyasahau, kwa muda, masaibu yote niliyoyapitia.

Muda huo nilikuwa nimepumzishwa kwenye chumba maalumu ndani ya Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma kwa ajili ya huduma zaidi kwani hali yangu bado haikuwa nzuri kimwili na kisaikolojia.

Tukio la kile kitasa cha mlango kunyongwa na kisha mlango kusukumwa kwa ndani liliyavuta macho yangu kuutazama ule mlango huku nikishangaa maana moyo wangu ulianza kupoteza utulivu katika kiwango cha hali ya juu.

Mtu aliyeingia mle ndani baada ya ule mlango kufunguliwa alikuwa Daktari Lutta, daktari aliyekuwa akinihudumia tangu nilipofikishwa hapo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jioni ya siku iliyokuwa imetangulia. Kwanza daktari huyo alianza kwa kuchungulia ndani na kuyatupa macho yake pale kitandani nilipokuwa nimelala, baada ya kuhakikisha kuwa nilikuwa macho akageuza shingo yake kutazama nyuma yake akionekana kunong’ona jambo. Halafu akaingia akiongozana na Olivia, kaka Eddy na Mchungaji Ngelela.

Mchana huo Mchungaji Ngelela alikuwa amevaa suti nzuri ya kijivu na kola maalumu ya kichungaji na miguuni alivaa viatu vyeusi vya Ngozi. Eddy alivaa shati la kitenge lililokuwa na mikono mirefu, suruali nyeusi ya dengrizi na miguuni alivaa makubazi ya ngozi.

Nikiwa bado nawatazama kwa umakini mara akaingia Grace aliyekuwa binamu yangu, mtoto mkubwa wa Mchungaji Ngelela. Grace alipoingia tu aliyatupa macho yake kwa shauku kutazama pale kitandani nilipokuwa nimelala.

Grace alikuwa mrefu mwenye umbo uzuri, alikuwa amevaa gauni zuri la kitenge cha wax lililoshonwa kwa mtindo wa ‘Ankara midi tube dress’ likiishia kwenye magoti, likaushika vyema mwili wake na kulichora umbo lake. Nywele zake alizinyoa zikabaki fupi na akazichana vizuri. Miguuni alivaa viatu vyenye vikanyagio virefu vya mchuchumio na begani alining’iniza mkoba mzuri wa kike.

Nilipomwona Grace nikatarajia pia kumwona Rehema akiingia lakini sikumwona! Nikashtuka kidogo.

Ukiwaacha Daktari Lutta na Olivia waliokuwa wakinitazama kwa macho ya kawaida, niliwashuhudia wale wengine wakiduwaa huku macho yao yakionesha kukataa kabisa kuamini kama taswira ya mtu waliyekuwa wakimtazama mbele yao ni Jason. Kitambo kifupi cha ukimya kilipita kila mmoja akiwa kasimama kimya, hakuna alitesogea wala kutikisika, ni kama walikuwa wamepigiliwa misumali miguuni au miili yao ilikuwa imekufa ganzi! Na zaidi ya hapo walidhani labda walikuwa wanaona mzimu wangu.

Wakiwa bado wanashangaa, nikauona msirimbi wa kipaji cha uso wa Grace ukiumuka, milizamu ikatutusika chini ya masikio yake kama iliyopulizwa, shingo yake ikavimba na michirizi ya machozi ikapasuka machoni mwake. Alipotaka kuongea neno akashindwa na kuanza kulia kilio cha kwikwi, huku Mchungaji Ngelela na kaka Eddy wakibaki kimya huku wakinitumbulia macho. Kisha na wao machozi yakaanza kuwalengalenga.

“Kaka Jason!” hatimaye Grace aliita kwa mshangao huku akinisogelea pale kitandani nilipolala na kunikumbatia kwa nguvu bila kujali majeraha niliyokuwa nayo mwilini, alikuwa bado analia.

Tulibaki tukiwa tumekumbatiana kwa takriban dakika nzima huku nami nikijikuta nalia, kilio chetu kiliamsha simanzi kwa wengine, na wao wakajikuta wakitokwa na machozi pasipo kupenda. Sasa chumba chote kikachachatika vilio na nyuso zikafiringiswa katika viganja vya mikono.

Daktari Lutta na Olivia walibaki kimya wakitutumbulia macho, ingawa kuna muda Olivia alishindwa kujizuia, akatoa kitambaa chake toka kwenye mkoba wake, akapangusa macho yake kufuta machozi yaliyoanza kumlengalenga.

Baada ya kitambo kidogo tulinyamaza na hali ndani ya kile chumba ikarudi katika hali yake ya kawaida. Mchungaji Ngelela alishusha pumzi ndefu na kujifuta machozi huku akiomba dua, “Machozi yetu na yawe ya heri katika jina la Yesu Kristo, amen!”

“Amen!” Eddy, Olivia na Grace wakaitikia kwa pamoja.

“Kaka Jason?” Grace aliniita tena kwa mshangao huku akifuta machozi yake machoni.

“Naam!” niliitikia huku nikifuta machozi yangu.

“Hivi ni nini kilikutokea?” Grace aliniuliza kwa shauku huku tukitazamana kwa furaha.

“Daah… ni hadithi ndefu kidogo…” nilimjibu.

“Jason hawezi kukumbuka lolote, alikuwa amepoteza kabisa kumbukumbu za utambulisho wake kwa miezi yote hii tuliyodhani kuwa amekufa,” Olivia alidakia.

“Duh! Masikini, kaka yangu!” Grace alisema kwa masikitiko.

“Usijali, Grace, naamini lipo kusudi la Mungu ndiyo maana hadi sasa nipo hai,” nilisema huku nikimpa mkono. Na baada ya kuuachia mkono wake nilimtazama Mchungaji Ngelela.

“Mjomba, shikamoo!” nilimsalimia kwa unyenyekevu.

“Marhaba, Jason! Pole sana na masaibu yaliyokupata,” Mchungaji Ngelela aliitikia huku akifuta macho yake kwa kutumia vidole vyake.

“Ahsante, mjomba… Mungu ni mwema, bado ananilinda,” nilisema na kushusha pumzi za ndani kwa ndani. Kisha nikaongeza, “Shangazi hajambo?”

“Hajambo, nilikuwa naye muda mfupi tu uliopita, kaelekea kanisani maana leo wamama wana huduma,” Mchungaji Ngelela aliniambia.

Kisha nilisalimiana na kaka Eddy, halafu kitambo kirefu cha ukimya kikapita mle ndani huku kila mmoja wetu akionekana kuzama kwenye tafakuri juu ya mambo yote yaliyotokea katika miezi yote tangu ile ajali ilipotokea eneo la Makutupora.

“Vipi, kaka, unajisikiaje kwa sasa?” hatimaye Grace aliniuliza huku akiachia tabasamu pana usoni kwake.

“Najisikia nafuu kidogo hasa baada ya kuwaona, ila nitapona pindi nikimwona mke wangu. Kwani yuko wapi?” niliuliza kwa utulivu huku macho yangu yakiwa yametua usoni kwa Grace.

“Utamwona tu, yupo hapa hapa Dodoma, na jana tu katoka hapa hospitali…” Grace alisema huku akifuta machozi ya furaha kwa mgongo wa kiganja chake.

“Katoka hospitali kwani anaumwa?” nilimuuliza Grace huku nikimtazama kwa wasiwasi. Nikamwona akisita kidogo na kumtazama kaka Eddy.

“Unaweza kusema hivyo, ila yeye kwa sasa ni mama…” Eddy aliniambia, kisha akaongeza, “Mama Jason Junior.”

“Ki vipi! Mbona sielewi?” niliuliza kwa mshangao mkubwa huku nikimtazama Eddy.

“Utaelewaje na wewe ulikuwa unaishi maisha yasiyo yako?” Olivia alidakia.

“Ndo nieleweshwe sasa! Unasema yeye ni mama na baba wa mtoto ni nani?” niliuliza kwa wasiwasi huku nikiwatazama mmoja mmoja usoni nikijaribu kuzisoma nyuso zao.

“Inamaana hukumbuki kama ulimwacha akiwa mjamzito? Hukumbuki ulivyonipigia simu wakati niko Sweden ukiwa na furaha siku mnajiandaa kutoka Arusha kuja Dodoma? Au kumbukumbu zako zinarudi nusu nusu!” Grace aliniuliza maswali mfululizo akiwa na mshangao.

Endelea kufuatilia...
 
Mgeni mwema.jpg

190

Sasa nilikumbuka. Niliikumbuka vyema siku tulipokuwa tukijiandaa kutoka Arusha na hata tulipokuwa safarini jinsi nilivyokuwa namweleza Rehema furaha yangu pindi akinizalia mtoto. Nilikumbuka vyema kuwa kila dakika nilimkumbusha Rehema kuhusu manunuzi ya nguo za mtoto pindi tu tukifika Dodoma. Nilikumbuka pia nilivyompigia simu Grace, wakati huo akiwa nchini Sweden, na kumpa habari nilizoziita “habari njema.”

“Kajifungua lini?” hatimaye niliuliza baada ya kumbukumbu hizo kupita kichwani kwangu, nilivuta pumzi ndefu na kisha nikazishusha taratibu.

“Takriban wiki sasa, na amejifungua kwa operesheni,” kaka Eddy alinijibu.

“Kwani alikuwa anaishi hapa Dodoma?” niliuliza huku nikiwa na mshangao kidogo.

“Hapana, alikuwa anaishi Kahama kwenye nyumba yenu ila mama alikwenda kumchukua miezi miwili iliyopita baada ya kushauriana na baba,” Grace alisema, kisha akanisimulia ilivyokuwa.

Alisema kwamba ilitokea baada ya Mchungaji Ngelela, katika maombi yake, kupata maono kuwa Rehema alikuwa katika hatari ya kifo, akaongea na Mama na Baba waliokuwa Tabora kuwataarifu kuwa alikuwa na mpango wa kumchukua Rehema amlete Dodoma ili amfanyie maombi maalumu ya kumwepusha hatari hiyo.

Baada ya Mama na Baba kukubaliana naye akawasiliana na Rehema na kumwambia kuwa Mama Mchungaji angemfuata huko Kahama na kumleta Dodoma. Rehema alipoletwa Dodoma wakagundua kuwa alikuwa ameanza kupatwa na shinikizo la juu la damu na mwili wake ulikuwa unavimba.

Siku moja asubuhi Grace alishangaa kuona hadi saa nne asubuhi Rehema alikuwa hajaamka na haikuwa kawaida yake, alikwenda kumgongea chumbani kwake bila mafanikio kwani mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani, akampigia simu, nayo ilikuwa inaita tu pasipo kujibiwa. Akashtuka na kuhisi huenda jambo baya lilikuwa limemtokea.

Alisimama pale mlangoni akiwa na hofu kubwa, alitazama huku na huko kana kwamba alikuwa anatafuta kitu cha kumsaidia, hakuelewa afanye nini! Ndipo alipokumbuka jambo, akampigia simu mama yake, Mama Mchungaji, kwa sauti iliyoashiria kuwa alikuwa anatetemeka. Wakati huo Mama Mchungaji hakuwepo nyumbani, alikuwa amekwenda kanisani kwenye huduma.

“Mungu wangu!” Mama Mchungaji alisema kwa mshtuko, kisha kikapita kitambo kifupi kabla hajaongeza, “Subiri nakuja.”

Grace alibaki amesimama pale pale mlangoni akiwa hajui afanye nini, alikuwa amenywea utadhani kifaranga kilichonyeshewa na mvua.

Baada ya dakika ishirini Mama Mchungaji alifika nyumbani. “Vipi?” Mama Mchungaji alimsaili Grace huku akimtazama kwa wasiwasi.

“Hata sijui nini kimempata wifi Rehema… nimegonga sana mlango lakini kimya, nimejaribu kupiga simu yake pia inaita tu bila kupokewa…” Grace alisema kwa wasiwasi.

“Mmh!” Mama Mchungaji aliguna na kukunja uso wake, alifikiria kwa muda kisha akashusha pumzi za ndani kwa ndani.

“Hebu subiri…” alisema na kuchukua simu yake, akampigia simu mumewe, Mchungaji Ngelela na kumjulisha kilichokuwa kinaendelea pale nyumbani. Kisha alitoka na kuzunguka sehemu ya nyuma ya ile nyumba kulikokuwa na madirisha ya chumba alichokuwa analala Rehema.

Alichungulia huku akisikiliza kama angeweza kusikia kitu lakini hali bado ilikuwa ya ukimya mno. Pamoja na kwamba mapazia katika madirisha hayo yalikuwa yamefunikwa lakini kupitia uwazi mdogo pembeni ya dirisha aliweza kuona mle ndani. Hata hivyo hakuona dalili ya kuwepo mtu kitandani. Ila alishtushwa na sauti hafifu ya mtu aliyekuwa anakoroma mle ndani ingawa hakuweza kumwona.

Muda mfupi uliofuata Mchungaji Ngelela akafika na hapo wakajadiliana kwa dakika chache tu na kukubaliana wavunje kitasa cha mlango kwa kuwa hakukuwa na njia nyingine ya kuingia mle chumbani.

Muda mfupi uliofuata wakawa wamefanikiwa kuingia mle chumbani, na walichokiona kiliwashtua sana. Rehema alikuwa amelala sakafuni akiwa amepoteza fahamu na alikuwa anakoroma taratibu kwa maumivu na alihema kwa taabu sana. Kando yake, sakafuni, kulikuwa na matone ya damu.

Ukelele wa hofu uliwatoka Grace na mama yake, walimkodolea macho Rehema ambaye alikuwa amejikunyata na kushika tumbo lake kwa mikono yake miwili katika namna ya kupambana na maumivu makali ya tumbo. Alikuwa na kila dalili ya uhai.

Bila kuchelewa walimkimbiza hospitali ya jirani alikopatiwa huduma ya kwanza na baada ikashauriwa kuwa awahishwe Hospitali ya Rufaa ya Mkoa au Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa matibabu zaidi.

“Halafu siku hiyo tukiwa tunafika pale Benjamin Mkapa kwa gari maalumu la wagonjwa, nilishtuka sana baada ya kuhisi kumwona mtu kama wewe eneo lile akiwa amesimama akituangalia kwa umakini, nilitaka kumfuata lakini wauguzi wakawa wananiita…” Grace aliniambia. Nikabaki kimya nikimtazama kwa mshangao.

Daktari alipompima aligundua kuwa alikuwa na shinikizo la juu la damu na miguu yake ilikuwa imevimba kidogo hali ambayo kwa kitaalamu iliitwa ‘mild oedema’, daktari alimfungulia faili na kuandika vipimo vilivyopaswa kuchukuliwa na dawa maalumu ya kushusha na kuimarisha shinikizo la damu ili kunusuru maisha yake na ya mtoto aliyekuwa tumboni kisha alipelekwa haraka katika wadi maalumu ya wajawazito walio katika hatari kubwa, ‘high-risk pregnancies ward’, na kutakiwa awe chini uangalizi maalumu, wa karibu, muda wote.

Na hapo ndugu wakaambiwa kuwa Rehema alikuwa na viashiria vya awali vya kifafa cha mimba, ugonjwa unaowapata wajawazito hasa wenye ujauzito wa kwanza. Ili kuzuia hali hiyo isije kuwa tatizo kubwa zaidi ikabidi kumweka wodini chini ya uangalizi wa karibu muda wote kwani kama hali isingedhibitiwa angeweza kupoteza maisha pamoja na mtoto wake tumboni.

Siku tatu baadaye yalipotoka
majibu ya vipimo ikagundulika kuwa alikuwa na presha katika tumbo lake la uzazi na mlango wa kizazi ulikuwa umefunguka na kusababisha tishio la kujifungua kabla ya wakati. Hali ile iliwachanganya sana madaktari, na mambo yote yalionekana kutokea haraka na yalitisha sana…

Simulizi ile ilinifanya nishindwe kuendelea kuisikiliza, nilijikuta nikitokwa na machozi pasipo kupenda.

“Olivia, mbona hukuniambia habari hizi!” nilimuuliza Olivia huku nikifuta machozi yaliyonitoka machoni kwangu.

“Kwa mazingira na hali uliyokuwa nayo ilikuwa vigumu kukwambia kila kitu, kwanza nilitakiwa kuhakikisha afya yako inaimarika halafu mengine yangefuata,” Olivia aliniambia kisha akaongeza, “Si wewe tu, hata Rehema bado hajaambiwa kuwa upo hai, tunamfanyia counselling kwanza ili kumweka tayari kupokea taarifa hizi.”

“Halafu, huwezi kuamini, kaka! Mara nyingi tu Rehema alikuwa akiniambia kuwa haamini kama umekufa, mwanzoni nilimwona kama amechanganyikiwa! Na zaidi ya mara tatu alisema ameota ndoto kuwa uko hai na unaishi kwa mwanamke mwingine,” Grace alidakia huku akiketi kwenye ukingo wa kitanda.

“Jana tulipokuwa tunamrudisha nyumbani alisisitiza tena kuwa anataka afukue kaburi ili apime DNA, maana bado haamini kama kweli umekufa,” kaka Eddy naye alisema kwa huzuni.

“Dah, basi atakuwa na karama ya unabii ndani yake!” nilisema kwa mshangao.

Endelea kufuatilia...
 
Mgeni mwema.jpg

191

“Kwa kweli… japo hata mimi bado akili yangu haiamini kama ni kweli upo hai! Nahisi kama nipo na mzimu,” Grace alisema huku akinitazama usoni.

“Hebu leta mkono wako hapa,” nilimwambia Grace nikimwonesha paja langu la mguu wa kulia, naye bila kusita alinyoosha mkono wake akaupeleka kushika paja langu.

“Hiki umeshika ni kitu gani?” nilimuuliza huku nikimtazama kwa umakini. Watu wote walikuwa kimya wakitutazama.

“Hili ni paja,” Grace alinijibu huku akinitazama kwa mshangao usoni.

“Una uhakika kuwa umeshika paja?” nilimuuliza tena nikiendelea kumtazama kwa tuo.

“Ndiyo, kaka, hili ni paja. Kwani vipi?” Grace alisema huku akiendelea kunitazama kwa mshangao usoni.

Very good! Kama una uhakika kwamba hili ni paja basi mimi si mzimu. Hata mjomba anaweza kukwambia, mzimu ni roho na hivyo hauna nyama wala haupigi stori kama hivi,” nilisema na kuwafanya watu wote mle ndani waangue kicheko.

“Dah! itanibidi tu niamini maana sina namna!” Grace alisema na kushusha pumzi.

“Ndo hivyo, ni Mungu tu aliyeniokoa maana ile ajali ilikuwa inatisha,” nilisema kwa utulivu huku nikitabasamu.

“Tulipoambiwa kwamba uko hai kwa kweli tulishtuka sana na hakuna aliyeamini…” Grace alisema huku akinitazama usoni.

“Ndo hivyo ushaniona, hunabudi kuamini,” nilisema huku nikijiinua toka pale kwenye kitanda na kuketi nikajiegemeza kwenye mto laini uliokuwa ukutani.

“Hata mimi sikuamini nilipoambiwa kuwa imeshapita miezi tisa tangu ajali ilipotokea! Ni kama muda wote huo sikuwepo kabisa duniani au utadhani nilikuwa kwenye coma kipindi chote na nilipozinduka nikahisi kama ilikuwa juzi tu,” nilisema kwa huzuni.

“Ni kweli, kwa hali uliyokuwa nayo hukuwa tofauti na mtu ambaye hakuwepo duniani! Yaani mtu unaishi maisha yasiyo yako kwa miezi tisa ukiwa umepoteza utambulisho wako na huna uwezo wa kukumbuka taarifa zozote za nyuma, ni kama muda wote uko kwenye coma!” Olivia alisema kwa huzuni huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.

“Dah!” nilisema huku nikinyanyua juu mabega yangu kisha nikashusha pumzi. Halafu nikasema kwa huzuni, “Inaonekana kuna mengi yametokea wakati nikiwa katika ulimwengu mwingine, kwa hali hii ninaweza hata kuwa mgeni nyumbani kwangu mwenyewe!”

“Kila kitu hutokea kwa kusudi la Mungu kama ulivyosema, najua lipo kusudi la kukuondoa nyumbani kwako kwa miezi tisa na kisha kurudishwa tena,” kwa mara ya kwanza Mchungaji Ngelela alisema, kisha alimgeukia Olivia. “Ulisema ugonjwa uliompata Jason unaitwaje?”

“Huu si ugonjwa, ni tatizo la kusahau linaloitwa kitaalamu amnesia. Kuna aina mbili kuu za amnesia ambazo ni retrograde amnesia na anterograde amnesia,” Olivia alisema.

“Ndiyo zikoje hizo! Yaani tofauti yake ni ipi?” Grace aliuliza kwa shauku.

Retrograde amnesia, mtu anakosa kabisa uwezo wa kukumbuka taarifa zozote za kabla ya siku husika ya kutokea tatizo. Wengine kumbukumbu zinaweza kurudi nyuma miongo kadhaa, wakati wengine mtu anaweza kupoteza kumbukumbu miezi michache tu na pindi kumbukumbu zikirudi zinaanzia pale pale zilipoishia kwenye siku husika ya kutokea tatizo,” Olivia alielezea.

I see!” Grace alisema kwa mshangao. Mchungaji Ngelela na Eddy walitingisha vichwa kwa huzuni.

“Na anterograde amnesia ni kutokuwa na uwezo wa kuhamisha taarifa mpya kutoka kwenye hifadhi ya kumbukumbu za muda mfupi kwenda hifadhi ya kumbukumbu za muda mrefu. Watu wenye aina hii hawawezi kukumbuka mambo kwa muda mrefu,” Olivia alieleza.

“Duh! Kumbe ndiyo maana mtu anaweza kuanza maisha mapya katika utambulisho mwingine huku taarifa zote za nyuma zikitoweka!” Eddy alisema na kuongeza, “Kwa hiyo bila vurugumechi ya kudhaniwa mwizi pengine Jason angeendelea kuishi kwa utambulisho mwingine kabisa huku sisi tukiamini kuwa alishakufa!”

“We acha tu, na kinachoniuma zaidi ni aina ya maisha niliyokuwa nikiishi. Nimepiga sana vibarua kwenye kampuni ya Yapi Merkezi kujenga reli,” nilisema na hapo hapo, pasipo kupenda, yakaibuka mawazo juu ya Zainabu.

Pasipo hiyari yangu nilijikuta nikizama kwenye mawazo ya kumfikiria msichana huyo, kama nilivyosimuliwa, kwa maisha ya ukaribu wetu wa takriban miezi tisa tuliishi kwa furaha akinipokea katika mji wa Kilosa na kusaidiana kwa mengi ikiwemo kunitafutia kazi, kisha tukachangia na ladha ya ukaribu wetu ikaongezeka baada ya kuibuka kwa hisia za mapenzi kati yetu. Tukawa wapenzi. Katika mji wa Kilosa nani hakujua kama tulikuwa tunapendana? Haikuwa siri tena!

Lakini baada ya kurejea kwa kumbukumbu zangu za awali yakatokea ya kutokea, nikamsahau kabisa na jambo hilo likatufanya tutengane ingawa sikuwa na namna ya kumwepuka kabisa kwa sababu tayari alikuwa amebeba ujauzito wangu, na hata moyo wake uliendelea kuishi katika upendo wa dhati juu yangu…

“Umeyajuaje maisha hayo wakati kumbukumbu za maisha hayo zimetoweka akilini mwako?” sauti ya Grace ilinizindua toka kwenye mawazo yaliyoanza kuiteka akili yangu, aliniuliza huku akiachia kicheko hafifu.

“Nimesimuliwa! Kwani si nilikuwa naishi na watu… yaani ukisimuliwa ni kama unatazama sinema hivi!” nilisema.

“Nasikia kaka yangu ulioa binti wa Kikaguru ukapewa na zawadi ya mtoto juu! Sijui sasa una mpango gani na huyo wifi yangu?” Grace aliniuliza huku akiendelea kucheka. Alikuwa mcheshi sana.

“Halafu wewe Grace, hayo ndiyo maswali gani sasa?” Mchungaji Ngelela alimkaripia Grace huku akionekana kukerwa.

“Mwache tu mjomba, inaonekana alinimiss sana,” nilisema.

“Hata kama siku nyingi hamjaonana ndiyo maswali gani sasa hayo?” Mchungaji Ngelela alisema kisha akaongeza, “Mtu kapata matatizo badala ya kumfariji unaanza kumuuliza maswali yasiyo na kichwa wala miguu!”

“Basi siulizi tena,” Grace alisema katika hali ya kususa huku akijiegemeza kwenye ukuta.

“Ni heri ukakaa kimya badala ya kuuliza maswali kama hayo,” Mchungaji Ngelela alisema huku akimkazia macho Grace. Kisha kitambo kidogo cha ukimya kikapita huku kila mmoja wetu akizama kwenye tafakuri.

* * *

Endelea kufuatilia...
 
Mgeni mwema.jpg

192

Mwana mpotevu


Saa 8:00 mchana…

SIKU tano zilikuwa zimepita tangu nitoke Kilosa kuja Dodoma, na siku ya pili tangu niliporuhusiwa kutoka hospitalini baada ya afya yangu kuonekana imeimarika zaidi; kimwili na kisaikolojia.

Sasa nilikuwa nimeketi peke yangu kwenye kiti cha nyuma, kwa utulivu mkubwa, ndani ya gari aina ya Toyota Prado lenye vioo vyeusi vya tinted visivyomruhusu mtu aliye nje kuona waliomo ndani ya gari. Gari hilo lilikuwa mali ya Olivia na liliegeshwa ndani ya uzio wa nyumba ya Mchungaji Ngelela. Pia kulikuwa na magari mengine matatu yaliyoegeshwa mle ndani.

Nyumba ya Mchungaji Ngelela ilikuwa kubwa ya kifahari, ni nyumba ambayo kuanzia mchoraji wa ramani mpaka fundi mwashi aliyeijenga walisugua bongo zao kisawasawa na kuzitendea haki fani zao. Ilikuwa imezungukwa na miti mizuri ya vivuli na sehemu za wazi zenye bustani nzuri ya maua na nyasi za kijani kibichi zilizokatwa vizuri. Ilikuwa na uzio mrefu uliofungwa mfumo maalumu wa umeme wa kuzuia wezi juu yake usiomwezesha mtu kuona ndani.

Ilikuwa moja ya majumba makubwa ya kisasa ya watu wenye ukwasi yaliyozungushwa uzio na mageti makubwa yenye vifaa vyote vya usalama vya kuwahakikishia wakazi wake usalama wa hali ya juu, ikiwa ya ghorofa moja ilikuwa na madirisha makubwa ya kisasa ya vioo na baraza kubwa mbele yake iliyopangwa seti moja ya makochi ya sofa.

Upande wa Mashariki wa nyumba ile kulikuwa na banda la wazi la kuegeshea magari. Sehemu nyingine ya mandhari ya ile nyumba ilikuwa imezungukwa na miti mirefu na mikubwa ya kivuli, huku sehemu ya mbele ikizungukwa na bustani nzuri ya maua ya kupendeza na katikati ya bustani hiyo kulitengenezwa njia nzuri ya kutembea kwa miguu kwa vitofali vidogo vilivyovutia.

Kwa upande wa Magharibi wa ile nyumba kulikuwa na bwawa kubwa la kuogelea lililozungukwa na vitanda vizuri vya kujipumzisha chini ya miamvuli mikubwa ya kivuli. Nyuma ya nyumba ile kulikuwa na tenki kubwa la maji na kando yake kulikuwa na karo kubwa la kuoshea vyombo na kufulia.

Nikiwa nimeketi ndani ya gari la Olivia, muda wote macho yangu yalitazama kwenye geti kubwa la kuingilia, mapigo ya moyo wangu yalikuwa yakienda mbio isivyo kawaida na moyo ulipiga kwa nguvu mithili ya saa kubwa ya Jamatini.

Niliketi ndani ya gari hilo nikisubiri muda mwafaka wa kuingia ndani kuonana na Rehema, hii ilikuwa baada ya Olivia na Grace kumweka sawa Rehema kisaikolojia kabla ya ujio wangu. Asubuhi ya siku hiyo Olivia alikuwa amefika hapo nyumbani ili kuzungumza na Rehema.

Olivia aliniambia kuwa alilazimika kumweleza ukweli Rehema kwa namna ambayo hakuwa ameipanga hasa baada ya Rehema kuushtukia ujio wa Olivia kwamba haukuwa kwa ajili ya kumsalimia tu bali alikuwa na jambo zito moyoni!

Wakati Olivia akiongea na Rehema asubuhi ya siku hiyo, mimi na kaka Eddy tulikuwa tumeketi kwa utulivu mkubwa ndani ya gari hilo hilo la Olivia, tukifuatilia kila kilichokuwa kinaendelea kati ya Olivia, Grace na Rehema kupitia kamera ya siri aliyoivaa Olivia.

Kupitia ile kamera ya siri niliweza kumwona Rehema, alikuwa amepungua kidogo ingawa alionekana bado mrembo sana. pia niliweza kumwona mtoto Jason Junior aliyekuwa amepakatwa na Grace.

Ujio wa Olivia ulisababisha sebule kuwa kimya kabisa kwa kitambo fulani. Rehema alimtazama Olivia kwa namna ambayo ni kama alikwisha elewa kilichokuwa kimemleta pale, kisha alishusha pumzi za ndani kwa ndani huku akionesha wasiwasi kidogo. Baada ya kusalimiana ukimya uliendelea kutawala pale sebuleni, kila mmoja alionekana kuwa katika tafakari nzito.

Hivyo, kupitia macho yake nilibaini kuwa Rehema alikuwa na hisia za uwepo wa jambo lisilo la kawaida. Aliwatazama kwa kitambo Olivia na Grace bila kusema neno lolote akionekana kuwa na wasiwasi.

“Kwani vipi shosti, kuna nini leo?” Rehema alimuuliza Olivia huku akimkazia macho kwa wasiwasi.

“Kwani wewe umeona nini?” Olivia naye alimtupia swali Rehema huku akijiweka sawa kwenye kochi.

“Kwa vyovyote ujio wako leo una jambo kubwa ambalo huenda ni mimi tu nisiyeelewa…” Rehema alisema huku akimgeukia Grace na kumtazama kwa udadisi.

“Wasiwasi wako tu, wifi…” Grace alidakia huku akiachia tabasamu akijaribu kumzuga Rehema.

“Lakini wasiwasi ndiyo akili,” Rehema naye alidakia kisha akashusha pumzi za ndani kwa ndani.

Grace na Olivia walitazamana kisha kitambo kingine cha ukimya kikapita pale sebuleni. Baada ya sekunde kadhaa Olivia alikohoa kidogo kusafisha koo lake, jambo lililomfanya Rehema amtazame kwa shauku.

“Shosti…” Olivia aliita kwa sauti tulivu, “hivi zile ndoto zako za kumuota Jason akiwa hai bado zinakujia?”

“Kwa nini…?” Rehema aliuliza kwa shauku kisha akaongeza pasipo kusubiri jibu la Olivia, “Ndiyo, bado zinanijia. Tena kwa siku za karibuni zimekuwa zikinijia sana na zinakaribia kunitia wazimu. Sijui nifanye nini maana najua siwezi kumrudisha tena.”

“Unaamini katika miujiza? Yaani… ukuu wa Mungu?” Olivia aliuliza, sauti yake iliendelea kuwa tulivu.

“Najua Mungu ni mkuu…” Rehema alisema halafu akaonekana kusita, akawatazama Olivia na Grace kwa macho yaliyojaa udadisi. “Kwa nini umeniuliza hivyo, shosti, kwani kuna nini kinaendelea hapa?”

“Kwani kuna ubaya kutaka kujua?” Olivia aliuliza, sauti yake iliendelea kuwa tulivu. “Ila kwa vyovyote utakuwa na karama ya unabii maana…”

“Maana kitu gani?” Rehema alidakia huku macho yake yakiwa yametulia kwenye uso wa Olivia. Alimtazama kwa udadisi zaidi akijaribu kuyasoma mawazo yake kisha akayahamisha macho yake kumtazama Grace kabla hajayarudisha tena kwa Olivia.

Muda huo nilimsikia Olivia akishusha pumzi za ndani kwa ndani kabla hajaongea. “Shosti, naomba nikuulize…”

“Niulize tu pacha,” Rehema alisema huku akipitisha ulimi wake kulamba mdomo wake wa chini.

“Vipi kama utagundua kuwa ndoto zako zilikuwa na ukweli fulani, kwamba ni kweli Jason yupo hai?” Olivia aliuliza.

“Mbona leo unaniuliza maswali yenye utata! Naomba nieleze tu ukweli wa kinachoendelea hapa badala ya kuendelea kuniweka roho juu,” Rehema alisema huku akionekana kukerwa kidogo kisha akainuka na kusimama wima huku akiwatazama Grace na Olivia kwa zamu.

Grace alitaka kusema neno lakini akasita na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.

“Ujue leo siwaelewi! Kwani kuna kitu gani mnaficha hapa ambacho hamtaki nikijue?” Rehema aliendelea kuuliza huku akiwatazama wote kwa zamu.

“Hebu kaa kwanza, utaelezwaje wakati umesimama?” Grace alisema kwa sauti tulivu.

Rehema alishusha pumzi na kuketi lakini alikuwa makini zaidi kuwatazama wote kwa zamu. Huenda alijaribu kuyasoma mawazo yao. Kisha kikatokea tena kitambo kingine cha ukimya.

“Mbona unakuwa na wasiwasi… unajuaje pengine Mungu ametenda miujiza yake…!” Olivia alisema baada ya kusita sana.

“Sijaelewa. Mungu katenda miujiza ipi? Jason amefufuka?” Rehema alidakia huku akimtazama Olivia kwa tuo.

“Unaweza kusema hivyo!” Olivia alisema kwa wasiwasi kidogo. “Kwenye ile ajali tuliyodhani kuwa amekufa kumbe hakuwa amekufa…”

Endelea kufuatilia...
 
Mgeni mwema.jpg

193

Baada ya maneno hayo nikamwona Rehema akiduwaa, alimtazama Olivia kwa mshangao mkubwa kana kwamba alikuwa anaona kitu fulani cha kushangaza mno, kisha nilishuhudia jasho jepesi likianza kumtoka na machozi kumlengalenga machoni. Nami mapigo ya moyo wangu yakaanza kwenda mbio isivyo kawaida.

“Pamoja na kwamba alisalimika lakini ile ajali ilisababisha ubongo wake kuhama kutoka katika sehemu yake ya kawaida na hivyo kumfanya apoteze kumbukumbu zote. Hakuwa na uwezo wa kukumbuka taarifa zozote za kabla ya ajali hiyo,” Olivia alisema.

Nilimtazama Rehema kwa umakini nikahisi alikuwa amechanganyikiwa kwa taarifa zile, aliendelea kuwa mkimya kwa kitambo fulani akimtazama Olivia na kisha macho yake aliyahamishia kwa Grace akiwa ana mashaka kidogo. Kupitia macho yake nilihisi kuwa moyo wake ulianza kupoteza utulivu.

“Wewe umeyajuaje yote hayo?” hatimaye Rehema alimudu kumuuliza Olivia huku akiendelea kumtazama kwa umakini.

“Tulipata taarifa kuwa yupo Kilosa anaishi maisha magumu ya kufanya vibarua na huko anatumia jina la Mgeni Mwema! Yaani hakumbuki kabisa taarifa zozote za kabla ya ile ajali,” Olivia alisema na kuungwa mkono na Grace.

“Lini mmepata taarifa hizi?” Rehema aliuliza kwa sauti tulivu huku akizidi kuwatazama wote kwa udadisi zaidi.

“Siku ambayo wewe ulijifungua kwa operesheni,” Grace alisema huku akimgeukia Olivia. Kisha kitambo kingine cha ukimya kikapita.

“Mmejuaje kama huyo mtu ni Jason na si mtu mwingine anayefanana naye?” Rehema aliuliza kwa wasiwasi.

“Tumekutana na kuzungumza naye, hatuna shaka kuwa ni yeye… na tumeyajua yote haya baada ya yeye kupatwa na mkasa mwingine tena,” Olivia alisema.

“Mkasa gani?” Rehema aliuliza kwa pupa.

“Alivamiwa na watu wenye hasira alfajiri wakati akifanya mazoezi, walidhani mwizi wakampiga sana, na kipigo kile kikasababisha kuurudisha ubongo wake katika sehemu yake ya kawaida. Sasa kumbukumbu zote zimemrudia ndiyo maana tumejua kuwa yupo hai,” Olivia alisema.

Nilimwona Rehema akifungua mdomo wake kutaka kuongea lakini akasita, au labda alishindwa, huenda maneno yake yaliishia akilini mwake kwani hakuweza kutamka chochote. Kwa vyovyote hakuwa ametarajia kabisa kusikia habari zile…

_____



Nikiwa nimezama kwenye lindi la mawazo nikiyakumbuka mambo yaliyojili asubuhi nilishtushwa na mtu aliyefungua mlango wa mbele wa gari, nikainua uso wangu kumtazama. Na hapo macho yangu yakakutana na macho ya Olivia aliyekuwa akinitazama kwa tabasamu pana.

“Muda umewadia, twende ndani,” Olivia alisema huku akiendelea kutabasamu.

“Vipi, hali ni shwari kabisa?” nilimuuliza Olivia nikiwa na wasiwasi kidogo.

“Usihofu, kila kitu kipo sawa,” Olivia aliniambia kisha akaongeza, “Ila wewe kapitie mlango wa jikoni, upo wazi.”

Nilishuka kwa tahadhari kubwa toka kwenye gari na kukatiza katikati ya bustani nikaelekea nyuma ya nyumba kwenye mlango wa kuingilia jikoni, niliukuta ukiwa nusu wazi, nikaingia kwa tahadhari na kuchungulia sebuleni. Na hapo nikawaona watu wote wakiwa wameketi kwenye masofa isipokuwa Rehema, yeye alikuwa amesimama huku akionekana kuwa na mashaka kidogo.

Mara kwa mara aliwatazama watu wengine kwa namna ya udadisi kisha aligeuka kumtazama Olivia aliyekuwa akiingia pale sebuleni akitokea nje. Rehema alionekana kama aliyetaka kuongea jambo lakini akasita, kisha aliwatazama tena watu wengine kwa umakini.

Mbali na Olivia, pale sebuleni niliwaona Grace aliyekuwa amempakata mtoto, Mchungaji Ngelela na Mama Mchungaji, kaka Eddy, Mama, Mama yake Rehema, na watu wengine wawili ambao sikuweza kuwafahamu mara moja.

Ile sebule ilikuwa imepambwa kwa seti mbili za makochi ya sofa ya kifahari yaliyokuwa yamepangwa katika mtindo wa kuizunguka. Katikati kulikuwa na meza nzuri ya kioo iliyokuwa na umbo la yai ikizungukwa na stuli ndogo nne za sofa. Upande wa kulia wa ile sebule kwenye kona kulikuwa na runinga pana aina ya LG iliyofungwa ukutani na chini yake kulikuwa na meza fupi nyeusi yenye sistimu ya muziki, decorder na deki moja ya Dvd.

Ukutani kulikuwa na picha kubwa ya Mchungaji Ngelela na picha nyingine kadhaa za kuchorwa zilizovutia sana. Upande wa kushoto kwenye kona nyingine kulikuwa na meza fupi ya mapambo na jokofu. Pembeni ya meza ile kulikuwa na rafu kubwa iliyopangwa vitabu na majarida mengi na juu ya rafu hiyo kulikuwa na vinyago vya Kiafrika vilivyopangwa kwa ustadi wa hali ya juu.

Upande huo pia kulikuwa na ngazi za kuelekea juu na upande mwingine kulikuwa na ukumbi mdogo wa chakula wenye meza kubwa ya chakula yenye umbo la yai iliyozungukwa na viti sita nadhifu vyenye foronya laini. Jirani na ule ukumbi wa chakula kulikuwa na mlango mwingine upande wa nyuma wa ile sebule ulioelekea kwenye vyumba viwili vya chini vya ile nyumba.

Watu wote mle ndani walikuwa kimya wakimtazama Rehema bila kusema neno. Olivia aligeuza shingo yake kwa siri kunitazama kule nilikokuwa nimejificha kisha alinipa ishara kwamba niingie pale sebuleni. Nikajikuta nikikohoa na kuwafanya watu wote wageuke haraka kutazama upande nilikokuwa. Wote walikuwa na furaha isipokuwa Rehema peke yake, yeye alitazama kwa wasiwasi.

Nilitembea taratibu nikiingia pale sebuleni huku uso wangu ukiwa umechanua kwa tabasamu, na hapo nikahisi kuwa shughuli za mwili wa Rehema zilisimama kwa sekunde kadhaa na macho yake yalikataa kabisa kuamini kama taswira ya mwanamume aliyekuwa akimwona mbele yake ni mumewe Jason.

Nilimshuhudia akinitumbulia macho kana kwamba hakuwahi kuniona kabla, nilihisi kuwa kwa dakika kadhaa mwili wake ulikuwa umekufa ganzi na pengine alihisi ubaridi mwepesi ukimtambaa mwilini huku mapigo ya moyo wake yakibadili mwendo wake na kwenda mbio isivyo kawaida!

Huenda pia jambo lililomjia akilini mwake muda huo ni kuwa kile alichokuwa akikishuhudia mbele yake ilikuwa ndoto tu kama ndoto zingine na pindi akiamka kutoka usingizini angekuta kila kitu kikiwa cha kawaida.

Hata hivyo, tabasamu jepesi la upendo na matumaini alilokuwa akiliona usoni kwangu lilifanikiwa kuufanya moyo wake ulipuke kwa furaha isiyopimika, furaha iliyoichanganya zaidi akili yake na kuamsha hisia zisizoelezeka. Niliyajua yote hayo kupitia macho yake.

Nilikuwa katika mwonekano wa kupendeza japokuwa bado nilikuwa na plasta ngumu mkononi na bandeji kichwani kutokana na kipigo nilichokipata huko Kilosa.

Hakika Rehema alikuwa katika wakati mgumu sana, alishindwa kufanya chochote na hivyo aliganda bila kusogea, kutingishika wala kupepesa macho yake utadhani alikuwa amepigiliwa msumali sakafuni! Mara kikohozi kidogo kikamtoka na nyuma yake wimbi la machozi ya furaha lilikuja mbio.

Nilimshuhudia akijaribu kuyazuia machozi yasimtoke lakini akashindwa. Hakuwa na namna ya kuyazuia yasitoke na hivyo akaendelea kunitumbulia macho bila kusema chochote huku machozi yakimtoka.

Endelea kufuatilia...
 
Mgeni mwema.jpg

194

Nilizidi kumsogelea taratibu hadi karibu yake, nikasimama huku nikimtazama kwa tabasamu. Yeye aliendelea kusimama kama sanamu pasipo kupepesa macho jambo lililoanza kumshtua kila mtu aliyekuwemo pale sebuleni. Tulitazamana. Nilikuwa namtazama kwa umakini nikiwa siamini kama niliyekuwa namwona kasimama mbele yangu alikuwa mke wangu mpenzi, Rehema. Nilisimama pale nikiyashuhudia machozi yakiendelea kumtiririka mashavuni utadhani milizamu iliyopasuka.

Kwa sekunde kadhaa watu wote pale sebuleni walibaki katika taharuki wakitutazamana bila kusema neno, kisha kama aliyegutuka, Rehema alikweza khanga yake na kufuta machozi kwa kutumia pembe ya khanga na kisha akapenga kamasi zilizoanza kumtoka. Halafu akashusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani.

Na hapo nikapata nguvu na kuinua mikono yangu, nikamkumbatia. Yeye pia alinyanyua mikono yake akanikumbatia. Tulikumbatiana kwa furaha kwa muda tusioweza kuukumbuka, mioyo yetu ilikuwa inadunda kwa kasi na jasho jepesi lilikuwa linatutoka.

Wakati tukiwa bado tumekumbatiana nilimsikia Rehema akivuta pumzi ndefu kisha akazishusha taratibu huku akiwa amekilaza kichwa chake kwenye kifua changu. Hadi muda huo hakuweza kuongea neno lolote. Nilijikuta nikizama katika kuuajabia mwili wa Rehema, nikauhusudu urembo wake usiochujuka japo alikuwa ametoka kujifungua lakini bado aliweza kuonekana mrembo.

Kisha Rehema aliinua uso wake kunitazama na hapo akalihisi joto la pumzi zangu jambo nililoamini kuwa lilimfanya kuamini kuwa nilikuwa mtu hai na si mzimu.

Kwa muda wote huo hali ilikuwa ya taharuki kidogo ndani ya ile sebule, watu wote walikuwa kimya wakishuhudia kilichokuwa kikiendelea kati ya wanandoa tuliokuwa tumepotezana kwa takriban miezi kumi, huku mimi nikidhaniwa kuwa nimekufa.

“Rehema!” hatimaye nilimwita Rehema kwa sauti ndogo.

“Abee!” Rehema aliitika kwa sauti ya chini huku akinitazama usoni, uso wake ulikuwa na michirizi ya machozi yaliyolilowesha shati langu eneo la kifuani.

“Ni mimi Jason mumeo, niko hai… usilie mimi ni mzima kama unionavyo,” nilisema huku nikimpapasa nywele zake.

Maneno hayo yalionesha kumwingia sana Rehema, alinitazama kwa haya, alinitazama tangu unyayoni hadi utosini, kisha macho yetu yaligongana na kumfanya aachie tabasamu laini. Mashavu yake yakaonesha vishimo vidogo, pembe za midomo yake zikafinya na macho yake yakafanya kuelea. Midomo yake yenye maki ikafunguka na sauti iliyotoka humo ilitosha kabisa kumtoa nyoka pangoni mwake.

“Hata sijui niseme nini, mume wangu! Ila namshukuru sana Mungu kwa kukurejesha nyumbani ukiwa mwenye afya, karibu tena maisha kwangu,” Rehema alisema na kushusha pumzi ndefu kama aliyetoka kumaliza mbio ndefu za marathoni.

Kwa maneno hayo, mkondo wa umeme ulikuwa umepitishwa katika mwili wangu. Nilishusha pumzi na kumwachia Rehema kisha nikamsogelea Grace na kusimama nikimtazama Jason Junior aliyepakatwa mikononi. Kuona hivyo Grace akanyoosha mikono yake kunipa mtoto.

Nilimchukua mtoto na kumtazama kwa umakini, nikashusha pumzi za ndani kwa ndani na kumbusu kwenye paji la uso wake, kisha nikamkumbatia kifuani kwangu huku nikijitahidi kuyazuia machozi yaliyokuwa yakinilengalenga machoni.

Grace alinyanyuka toka pale alipokuwa ameketi na kunipisha, akaketi kwenye kochi jingine lililokuwa kando kabisa ya sebule. Niliketi huku nikiendelea kumtazama Jason Junior kwa umakini. Kitambo kirefu cha ukimya kikapita huku kila mmoja akiwaza lake na ukimya ule ulipokuwa mbioni kushika hatamu nikanyanyua uso wangu kuwatazama watu walioketi pale sebuleni.

“Habari za hapa?” niliwasalimia mle ndani huku nikivunja ukimya ulioanza kutawala pale sebuleni.

“Za hapa nzuri,” wote walijibu. Mama Mchungaji akaongeza, “Sisi hatujambo kama unavyotuona. Pole sana.”

“Nimekwisha poa,” nilijibu kisha nikamtazama Rehema, “Pole sana kwa maisha ya upweke na yote yaliyotokea wakati mimi sipo.”

“Hivi sasa sina tena upweke,” Rehema alisema huku akiangua kicheko hafifu cha kimahaba.

“Hata hivyo akili yangu inashindwa kukubali, ni kama vile mambo haya yametendeka ndani ya wiki moja tu tangu ile ajali itokee,” nilisema huku nikiutazama mkono wangu wa kushoto uliofungwa plasta ngumu.

Rehema aliyapeleka macho yake kuutazama mkono wangu wenye plasta ngumu kwa umakini huku akijitahidi kuyazuia machozi yake, kisha alinisogelea na kuketi sakafuni huku akiishika miguu yangu kwa upendo. Akamwagiza Grace alete maji kwenye kikombe kikubwa na beseni dogo.

Grace aliinuka na kuleta maji kwenye kikombe na beseni dogo na kumpa Rehema ambaye alivipokea na kunivua viatu na soksi, kisha akaniosha miguu yangu kwa upendo huku akiyakinga yale maji kwenye beseni, halafu akayanywa yale maji aliyonioshea. Kila mtu alimtazama kwa mshangao lakini yeye hakujali.

“Kwa miezi tisa nimeishi kwa ukiwa, sikujua kama ingetokea siku kama ya leo tukiwa pamoja na mtoto wetu Junior,” Rehema alisema huku akifuta machozi yaliyokuwa yanamlengalenga machoni.

Muda mfupi uliofuata Grace alielekea jikoni na kurudi akiwa amebeba sinia kubwa la mbao safi ambalo lilikuwa na majagi mawili makubwa ya kioo, moja likiwa na sharubati ya mchanganyiko wa embe na passion na jingine lilikuwa na sharubati ya parachichi. Akayaweka juu ya meza na kuondoka tena, akarejea na bilauri kadhaa. Kisha alimimina sharubati kwenye zile bilauri na kutukaribisha.

Kila mmoja alichukua bilauri ya sharubati kulingana na alivyopenda halafu tukagongesha bilauri zetu kutakiana afya njema na maisha marefu. Tukanywa taratibu huku tukiongea na kufurahi kwa pamoja.

“Haya ni maajabu kabisa! Hiki kilichotokea ni kama ile hadithi ya mwana mpotevu wa kwenye Biblia,” Eddy alisema huku akiachia kicheko hafifu. Watu wote walicheka kwa furaha huku wakionekana kuafikiana na maneno yake.

“Wala hujakosea, mimi pia ni mwana mpotevu, nilipotea na sasa nimepatikana. Nilikufa na sasa nimefufuka,” nilisema kwa furaha huku nikinyanyua bilauri yangu juu kisha nikapiga funda kubwa la sharubati.

“Ni kweli, wewe ni mwana mpotevu ila tofauti yako na yule wa kwenye Biblia ni kwamba, mwenzio aliondoka akiwa na fahamu zake na wewe uliondoka ukiwa huna kumbukumbu zako na ukaishi maisha ya kufikirika,” Grace alisema huku akiangua kicheko. Kisha aliinuka na kunifuata huku akinyoosha mkono wake wenye bilauri, tukagongesha bilauri zetu.

Cheers!” tulisema kwa pamoja na kuinua bilauri, tukapiga mafunda mfululizo kana kwamba tulikuwa kwenye mashindano.

Long live, my dear brother!” Grace alisema kwa sauti kubwa akiwa na furaha.

Long live, my dearest sister!” nilijibu mapigo huku nikiikita ile bilauri tupu juu ya meza kwa furaha.

“Na ninyi mkishakutana basi tabu tupu,” Eddy alisema huku akitabasamu.

“Wacha tufurahi, kaka… mwana mpotevu amefufuka na kurudi nyumbani,” Grace alisema huku akicheka kisha akaongeza huku akinitazama usoni, “Kwanza juice haipandi kabisa, hapa tungepata Castle baridi ingependeza zaidi, au vipi brother?”

“Hiyo pombe yenu mkainywee huko huko si ndani ya nyumba ya Mchungaji,” Eddy alisema kwa utani na hapo tukageuza shingo zetu kumtazama Mchungaji Ngelela aliyeketi kwa utulivu kwenye kochi.

* * *



Saa 11:30 jioni…

Jioni ya siku hiyo ilinikuta nikiwa nimesimama mbele ya kaburi ambalo ulizikwa mwili uliodhaniwa kuwa wangu, nililitazama kaburi hilo kwa huzuni kubwa huku mawazo yangu yakirudi nyuma miezi tisa iliyokuwa imepita siku tuliyopata ajali. Kisha nilijaribu kuwaza kuhusu maisha mapya niliyoishi kama Mgeni lakini sikuwa na kumbukumbu zozote.

Wakati nikilitazama lile kaburi nilishindwa kuyazuia machozi yangu hasa nilipoyaona maandishi makubwa yaliyokuwa yameandikwa juu ya msalaba wa zege, maandishi ambayo yalikuwa yanawakilisha jina langu, tarehe ya kuzaliwa na ya kufa.

Nilikuwa nimeambatana na Mchungaji Ngelela, Eddy na Grace waliosimama kando yangu huku wakinifariji. Nilisimama pale kwa dakika kadhaa nikilitazama lile kaburi kisha nikashusha pumzi ndefu na kufuta machozi yaliyokuwa yakinitoka. Halafu kwa kusaidiana na watu niliofuatana nao tuliuondoa ule msalaba kutoka kwenye lile kaburi.

Baada ya kuhakikisha kuwa sijaacha alama yoyote yenye kuonesha utambulisho wangu kwenye lile kaburi, niliinamisha kichwa changu kwa huzuni mbele ya kaburi lile na kufumba macho. Kisha nilimshukuru Mungu kwa kuniepusha na mauti na nikamwomba anipe nguvu na maisha marefu yenye heri, halafu nilimwombea marehemu aliyezikwa kwenye kaburi hilo ili Mungu ampumzishe mahala pema.

Nilipomaliza nikaondoka taratibu kwa huzuni huku nikifuatwa na jamaa zangu niliokuja nao.

* * *

Endelea kuufuatilia mkasa huu wa kusisimua...
 
View attachment 2280500
194

Nilizidi kumsogelea taratibu hadi karibu yake, nikasimama huku nikimtazama kwa tabasamu. Yeye aliendelea kusimama kama sanamu pasipo kupepesa macho jambo lililoanza kumshtua kila mtu aliyekuwemo pale sebuleni. Tulitazamana. Nilikuwa namtazama kwa umakini nikiwa siamini kama niliyekuwa namwona kasimama mbele yangu alikuwa mke wangu mpenzi, Rehema. Nilisimama pale nikiyashuhudia machozi yakiendelea kumtiririka mashavuni utadhani milizamu iliyopasuka.

Kwa sekunde kadhaa watu wote pale sebuleni walibaki katika taharuki wakitutazamana bila kusema neno, kisha kama aliyegutuka, Rehema alikweza khanga yake na kufuta machozi kwa kutumia pembe ya khanga na kisha akapenga kamasi zilizoanza kumtoka. Halafu akashusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani.

Na hapo nikapata nguvu na kuinua mikono yangu, nikamkumbatia. Yeye pia alinyanyua mikono yake akanikumbatia. Tulikumbatiana kwa furaha kwa muda tusioweza kuukumbuka, mioyo yetu ilikuwa inadunda kwa kasi na jasho jepesi lilikuwa linatutoka.

Wakati tukiwa bado tumekumbatiana nilimsikia Rehema akivuta pumzi ndefu kisha akazishusha taratibu huku akiwa amekilaza kichwa chake kwenye kifua changu. Hadi muda huo hakuweza kuongea neno lolote. Nilijikuta nikizama katika kuuajabia mwili wa Rehema, nikauhusudu urembo wake usiochujuka japo alikuwa ametoka kujifungua lakini bado aliweza kuonekana mrembo.

Kisha Rehema aliinua uso wake kunitazama na hapo akalihisi joto la pumzi zangu jambo nililoamini kuwa lilimfanya kuamini kuwa nilikuwa mtu hai na si mzimu.

Kwa muda wote huo hali ilikuwa ya taharuki kidogo ndani ya ile sebule, watu wote walikuwa kimya wakishuhudia kilichokuwa kikiendelea kati ya wanandoa tuliokuwa tumepotezana kwa takriban miezi kumi, huku mimi nikidhaniwa kuwa nimekufa.

“Rehema!” hatimaye nilimwita Rehema kwa sauti ndogo.

“Abee!” Rehema aliitika kwa sauti ya chini huku akinitazama usoni, uso wake ulikuwa na michirizi ya machozi yaliyolilowesha shati langu eneo la kifuani.

“Ni mimi Jason mumeo, niko hai… usilie mimi ni mzima kama unionavyo,” nilisema huku nikimpapasa nywele zake.

Maneno hayo yalionesha kumwingia sana Rehema, alinitazama kwa haya, alinitazama tangu unyayoni hadi utosini, kisha macho yetu yaligongana na kumfanya aachie tabasamu laini. Mashavu yake yakaonesha vishimo vidogo, pembe za midomo yake zikafinya na macho yake yakafanya kuelea. Midomo yake yenye maki ikafunguka na sauti iliyotoka humo ilitosha kabisa kumtoa nyoka pangoni mwake.

“Hata sijui niseme nini, mume wangu! Ila namshukuru sana Mungu kwa kukurejesha nyumbani ukiwa mwenye afya, karibu tena maisha kwangu,” Rehema alisema na kushusha pumzi ndefu kama aliyetoka kumaliza mbio ndefu za marathoni.

Kwa maneno hayo, mkondo wa umeme ulikuwa umepitishwa katika mwili wangu. Nilishusha pumzi na kumwachia Rehema kisha nikamsogelea Grace na kusimama nikimtazama Jason Junior aliyepakatwa mikononi. Kuona hivyo Grace akanyoosha mikono yake kunipa mtoto.

Nilimchukua mtoto na kumtazama kwa umakini, nikashusha pumzi za ndani kwa ndani na kumbusu kwenye paji la uso wake, kisha nikamkumbatia kifuani kwangu huku nikijitahidi kuyazuia machozi yaliyokuwa yakinilengalenga machoni.

Grace alinyanyuka toka pale alipokuwa ameketi na kunipisha, akaketi kwenye kochi jingine lililokuwa kando kabisa ya sebule. Niliketi huku nikiendelea kumtazama Jason Junior kwa umakini. Kitambo kirefu cha ukimya kikapita huku kila mmoja akiwaza lake na ukimya ule ulipokuwa mbioni kushika hatamu nikanyanyua uso wangu kuwatazama watu walioketi pale sebuleni.

“Habari za hapa?” niliwasalimia mle ndani huku nikivunja ukimya ulioanza kutawala pale sebuleni.

“Za hapa nzuri,” wote walijibu. Mama Mchungaji akaongeza, “Sisi hatujambo kama unavyotuona. Pole sana.”

“Nimekwisha poa,” nilijibu kisha nikamtazama Rehema, “Pole sana kwa maisha ya upweke na yote yaliyotokea wakati mimi sipo.”

“Hivi sasa sina tena upweke,” Rehema alisema huku akiangua kicheko hafifu cha kimahaba.

“Hata hivyo akili yangu inashindwa kukubali, ni kama vile mambo haya yametendeka ndani ya wiki moja tu tangu ile ajali itokee,” nilisema huku nikiutazama mkono wangu wa kushoto uliofungwa plasta ngumu.

Rehema aliyapeleka macho yake kuutazama mkono wangu wenye plasta ngumu kwa umakini huku akijitahidi kuyazuia machozi yake, kisha alinisogelea na kuketi sakafuni huku akiishika miguu yangu kwa upendo. Akamwagiza Grace alete maji kwenye kikombe kikubwa na beseni dogo.

Grace aliinuka na kuleta maji kwenye kikombe na beseni dogo na kumpa Rehema ambaye alivipokea na kunivua viatu na soksi, kisha akaniosha miguu yangu kwa upendo huku akiyakinga yale maji kwenye beseni, halafu akayanywa yale maji aliyonioshea. Kila mtu alimtazama kwa mshangao lakini yeye hakujali.

“Kwa miezi tisa nimeishi kwa ukiwa, sikujua kama ingetokea siku kama ya leo tukiwa pamoja na mtoto wetu Junior,” Rehema alisema huku akifuta machozi yaliyokuwa yanamlengalenga machoni.

Muda mfupi uliofuata Grace alielekea jikoni na kurudi akiwa amebeba sinia kubwa la mbao safi ambalo lilikuwa na majagi mawili makubwa ya kioo, moja likiwa na sharubati ya mchanganyiko wa embe na passion na jingine lilikuwa na sharubati ya parachichi. Akayaweka juu ya meza na kuondoka tena, akarejea na bilauri kadhaa. Kisha alimimina sharubati kwenye zile bilauri na kutukaribisha.

Kila mmoja alichukua bilauri ya sharubati kulingana na alivyopenda halafu tukagongesha bilauri zetu kutakiana afya njema na maisha marefu. Tukanywa taratibu huku tukiongea na kufurahi kwa pamoja.

“Haya ni maajabu kabisa! Hiki kilichotokea ni kama ile hadithi ya mwana mpotevu wa kwenye Biblia,” Eddy alisema huku akiachia kicheko hafifu. Watu wote walicheka kwa furaha huku wakionekana kuafikiana na maneno yake.

“Wala hujakosea, mimi pia ni mwana mpotevu, nilipotea na sasa nimepatikana. Nilikufa na sasa nimefufuka,” nilisema kwa furaha huku nikinyanyua bilauri yangu juu kisha nikapiga funda kubwa la sharubati.

“Ni kweli, wewe ni mwana mpotevu ila tofauti yako na yule wa kwenye Biblia ni kwamba, mwenzio aliondoka akiwa na fahamu zake na wewe uliondoka ukiwa huna kumbukumbu zako na ukaishi maisha ya kufikirika,” Grace alisema huku akiangua kicheko. Kisha aliinuka na kunifuata huku akinyoosha mkono wake wenye bilauri, tukagongesha bilauri zetu.

Cheers!” tulisema kwa pamoja na kuinua bilauri, tukapiga mafunda mfululizo kana kwamba tulikuwa kwenye mashindano.

Long live, my dear brother!” Grace alisema kwa sauti kubwa akiwa na furaha.

Long live, my dearest sister!” nilijibu mapigo huku nikiikita ile bilauri tupu juu ya meza kwa furaha.

“Na ninyi mkishakutana basi tabu tupu,” Eddy alisema huku akitabasamu.

“Wacha tufurahi, kaka… mwana mpotevu amefufuka na kurudi nyumbani,” Grace alisema huku akicheka kisha akaongeza huku akinitazama usoni, “Kwanza juice haipandi kabisa, hapa tungepata Castle baridi ingependeza zaidi, au vipi brother?”

“Hiyo pombe yenu mkainywee huko huko si ndani ya nyumba ya Mchungaji,” Eddy alisema kwa utani na hapo tukageuza shingo zetu kumtazama Mchungaji Ngelela aliyeketi kwa utulivu kwenye kochi.

* * *



Saa 11:30 jioni…

Jioni ya siku hiyo ilinikuta nikiwa nimesimama mbele ya kaburi ambalo ulizikwa mwili uliodhaniwa kuwa wangu, nililitazama kaburi hilo kwa huzuni kubwa huku mawazo yangu yakirudi nyuma miezi tisa iliyokuwa imepita siku tuliyopata ajali. Kisha nilijaribu kuwaza kuhusu maisha mapya niliyoishi kama Mgeni lakini sikuwa na kumbukumbu zozote.

Wakati nikilitazama lile kaburi nilishindwa kuyazuia machozi yangu hasa nilipoyaona maandishi makubwa yaliyokuwa yameandikwa juu ya msalaba wa zege, maandishi ambayo yalikuwa yanawakilisha jina langu, tarehe ya kuzaliwa na ya kufa.

Nilikuwa nimeambatana na Mchungaji Ngelela, Eddy na Grace waliosimama kando yangu huku wakinifariji. Nilisimama pale kwa dakika kadhaa nikilitazama lile kaburi kisha nikashusha pumzi ndefu na kufuta machozi yaliyokuwa yakinitoka. Halafu kwa kusaidiana na watu niliofuatana nao tuliuondoa ule msalaba kutoka kwenye lile kaburi.

Baada ya kuhakikisha kuwa sijaacha alama yoyote yenye kuonesha utambulisho wangu kwenye lile kaburi, niliinamisha kichwa changu kwa huzuni mbele ya kaburi lile na kufumba macho. Kisha nilimshukuru Mungu kwa kuniepusha na mauti na nikamwomba anipe nguvu na maisha marefu yenye heri, halafu nilimwombea marehemu aliyezikwa kwenye kaburi hilo ili Mungu ampumzishe mahala pema.

Nilipomaliza nikaondoka taratibu kwa huzuni huku nikifuatwa na jamaa zangu niliokuja nao.

* * *

Endelea kuufuatilia mkasa huu wa kusisimua...
Kweli mkasa unasisimua, ahsante Bishop
 
Nasubiri iishe niisome
I wish i was u ila subra ndo nimenyimwa everytime nakuja kuchungulia hola. Kuna namna mtu ukifaulu kusubiri iishe una faida sana maana wengine kususa tunatamani ila ndo hivo tena.....watunzi wazuri wanajua kutuweka roho juu honestly...
 
Back
Top Bottom