Simulizi: Harakati za Jason Sizya

Simulizi: Harakati za Jason Sizya

ufukweni mombasa.JPG

259

Wakati tukifungua milango ya nyuma ya teksi ile na kuzama ndani macho yangu yalikuwa makini kutazama kila mahali katika namna ya kuchunguza kuwa hapakuwa na mtu yeyote aliyekuwa akitufuatilia nyendo zetu. Muda ule ule ile teksi ikaondoka na kuingia barabarani huku yule kijana dereva wa teksi akijitia uchangamfu wa kila namna katika kuhakikisha kuwa ananizoea, nafasi ambayo kamwe sikutaka kumpa.

Muda wote nilikuwa makini kuchunguza kama tungefungiwa mkia na gari nyingine nyuma yetu lakini hilo halikujitokeza hadi tunafika katika mgahawa maarufu wa Acapulco Club & Restaurant uliopo barabara ya Nyali kwa ajili ya kupata chajio (dinner). Ulikuwa mgahawa mzuri wa kisasa wenye huduma zote muhimu kama aina ya vyakula mbalimbali vya watu wa mataifa tofauti na utulivu wa kutosha.

Tulipoingia pale kwenye mgahawa nikagundua kuwa kulikuwa na watu wa daraja la kati na la juu na wengi walikuwa raia wa kutoka nje ya Kenya. Mle kwenye mgahawa tulitafuta meza moja iliyojitenga kwenye kona moja ya mgahawa na kuketi. Sehemu ile tuliyoketi ilituwezesha sote kuona nje ya mgahawa ule kupitia vioo.

Mhudumu mmoja wa mgahawa ule alikuja kutusikiliza nikaagiza ugali na makange na saladi ya mboga za majani. Merina yeye aliagiza chips kuku na saladi ya mboga za majani. Vyakula vile vilipoletwa na mhudumu tukaanza kuvishambulia huku kila mmoja akionekana kuwa na njaa. Tulipomaliza kupata mlo tukaagiza sharubati ya mchangayiko wa embe na pasheni, tukashushia taratibu huku kichwani nikitafakari kuhusu kazi iliyokuwa mbele yangu.

Baada ya kupata chakula pale Acapulco Club & Restaurant tulikodi teksi nyingine iliyotupeleka katika ukumbi wa maraha wa Bamburi Beach Villa uliopo kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi. Tuliingia kwenye ukumbi wa Bamburi Beach Villa mnamo saa tatu na nusu usiku. Ulikuwa ukumbi mkubwa wa kisasa kabisa wenye kila aina ya vionjo vya daraja la kimataifa wenye jukwaa zuri linalotazamana na viti vingi vya kisasa kwa ajili ya kufanyia matamasha ya muziki na mikutano mbalimbali.

Pia kulikuwa na ukumbi mwingine mkubwa kwa ajili ya kujipatia vyakula vya asili na vya kimataifa wenye meza ndefu za kisasa zilizozungukwa na viti vizuri vya sofa vyenye foronya laini na kila ukumbi ulikuwa umejitenga na hivyo kutengeneza mgawanyo mzuri wa starehe tofauti zenye utulivu zinazoweza kufanyika kwa wakati mmoja.

Siku hiyo kulikuwa na onesho maalumu kutoka kwa msanii wa Afrika Mashariki anayetoka nchini Tanzania, Ali Kiba, ambaye alikuwa anasindikizwa na wasanii wengine maarufu kutoka Kenya. Merina alikuwa ameniomba twende Bamburi Beach Villa kwa kuwa, kama ilivyokuwa kwa wakazi wengi wa Mombasa, alikuwa shabiki mkubwa wa Ali Kiba.

Tulipoingia ndani ya ukumbi wa Bamburi Beach Villa tukatafuta sehemu nzuri, kwenye kona, na kuketi ili tuweze kuona vyema onesho. Lakini pia niliichagua sehemu ile kwa sababu za kiusalama ili niweze kumwona kila mtu aliyeingia ukumbini. Wengi tuliowakuta mle ukumbini walikuwa ni watu wa kipato cha kati na cha juu. Alipofika mhudumu niliagiza mvinyo ghali mwekundu aina ya Pinot Noir na Merina akaagiza kinywaji baridi cha Leapfrog cocktail na tulipoletewa tukawa tunakunywa taratibu huku tukifuatilia onesho jukwaani.

Wakati wote nilikuwa makini kuwachunguza watu walioingia na kutoka mle ukumbini, na hata waliokuwa wameketi ili kuona kama kulikuwa na yeyote wa kumtilia shaka.

Hadi inafika saa tano usiku mwanamuziki Ali Kiba alikuwa bado hajapanda jukwaani. Ni muda huo nilipotaka niinuke nielekee maliwato nikajikuta nikisita baada ya macho yangu kuvutiwa kumtazama msichana mmoja mzuri na mweupe ambaye alikuwa amevaa suruali ya bluu ya dengrizi iliyolichora umbo lake la msichana wa Kiafrika mwenye kiuno chembamba kiasi.

Juu alikuwa amevaa blauzi nyepesi nyekundu iliyozionesha vizuri chuchu zake nyeusi zilizotuna na shingoni mkufu unaometameta uliizunguka vizuri shingo yake ndefu na nyembamba huku ukipotelea katikati ya matiti yake. Mkufu huo ulinishtua na kunifanya nimtazame vizuri usoni na kumtambua.

“Miriam!” nilijikuta nikimaka kwa mshangao kwa sauti ya chini. Hata hivyo Merina alinisikia kwani nilimwona akigeuza shingo yake kutazama upande ambao macho yangu yalielekea.

“Usitazame huko, kuna mmoja wa watu wabaya sitaki atushtukie,” nilimwambia Merina, akanielewa haraka na kugeuka haraka kutazama upande mwingine.

Muda huo Miriam alikuwa amesimama akiyatembeza macho yake taratibu kutazama kila meza iliyokuwa mle ndani kama aliyekuwa anamtafuta mtu na wakati alipogeuka upande wetu niliwahi kuinamisha kichwa changu chini kama niliyekuwa natafuta kitu chini ya meza. Merina naye aliinama kutazama chini akidhani labda nilikuwa nimedondosha kitu.

“Kuna kitu umedondosha?” Merina aliniuliza huku akiyakodoa macho yake kutazama pale sakafuni.

“Hapana, yule mtu sitaki anione,” nilimjibu Merina huku nikiwa bado nimeinamisha kichwa changu na wakati huo huo nikimtazama Miriam kwa chati na kumwona akianza kuondoka na kuufuata uelekeo wa mlango wa kutokea, na hapo nikatambua kuwa alikuwa anaondoka. Nyuma yake alikuwa anafuatwa na mwanamume mmoja mrefu aliyevaa suti maridadi nyeusi.

“Mtu gani?” Merina aliniuliza huku akinitazama kwa wasiwasi.

“Ngoja kwanza, n’takwambia…” nilisema huku nikiinua uso wangu na kuangaza macho yangu huku na kule kutazama kama kungekuwa na mtu mwingine ambaye nilikuwa namfahamu au kumtilia shaka. Sikuona. Hata hivyo sikutaka kupoteza hata sekunde, nami nikainuka.

“Samahani, Merina… nakuja ila nakuomba chukua tahadhari, usimwamini mtu yeyote. Na kama sijatokea baada ya saa moja chukua teksi utangulie nyumbani, hakikisha hakuna mtu anayekufuatilia…” nilimwambia Merina kwa maneno ya msisitizo huku nikimpa noti kadhaa ambazo niliamini zingemtosheleza kwa nauli na mambo mengine. Nikamwona akiingiwa na wasiwasi, akataka kupinga wazo langu la kuondoka nimwache lakini hakupata nafasi kwani tayari nilikwisha mshikisha zile fedha na mimi nikaanza kupiga hatua kuelekea nje ya jengo.

Nilipiga hatua kadhaa na kugeuka kumtazama Merina nikamwona akiwa amesimama akiniangalia kwa wasiwasi. Nikaendelea na safari yangu pasipo kujali wasiwasi wake. Nilitembea kwa tahadhari huku nikijaribu kuwachunguza watu wote waliokuwemo mle ukumbini na hata wale niliopisha ili kuona kama kulikuwa na yeyote wa kumtilia shaka. Nilipohakikisha kwamba hakukuwa na wa kumtilia mashaka nikaharakisha kuelekea nje.

Tayari Miriam alikwisha toka nje na sikutaka aniache mbali sana hivyo nilipotoka tu nje nikaangaza macho yangu kutazama huku na kule sikumwona Miriam lakini nikajikuta nikimwona yule mwanamume mrefu ambaye sasa nilimtambua kuwa ni yule aliyekuwa akiendesha gari aina ya Jeep iliyotufungia mkia wakati tunatoka Serena Beach Resort kabla hatujapata ajali iliyosababisha kifo cha dereva wa teksi.

Alikuwa ni mwanamume mwenye asili ya Kisomali na alikuwa anamalizia kuongea na simu kisha akalifuata gari lake aina ya Range Rover jeusi. Nikiwa bado nashangaa nikaliona lile gari aina ya Range Rover likaanza kuyaacha maegesho ya magari ya pale Bamburi Beach Villa kwa mwendo wa taratibu, kisha likaingia barabarani. Mara nikamwona Miriam akiwa amesimama kwa mbele.

Gari lile lilienda kusimama hatua chache pembeni yake na hapo nikaelewa ni nini kilichokuwa kikiendelea mbele yangu. Lile gari liliposimama tu Miriam akafungua mlango wa nyuma na kuingia ndani na hapo safari ikaanza lile gari likiufuata uelekeo wa barabara ya Jomo Kenyatta Beach.

Sikutaka kuzubaa nikaharakisha kuiendea teksi moja iliyokuwa eneo lile na kumkuta dereva wa teksi, mtu mzima mwembaba wa wastani, ana nywele nyingi zilizochanganyika na mvi na ndevu za wastani akiwa tayari kwani alikuwa ameniona tangu nilipokuwa mbali nikiharakisha kuelekea eneo lile.

Nilipoifikia teksi ile nikafungua mlango wa nyumba na kuingia na kabla yule dereva hajaniuliza uelekeo wangu nikamwambia alifuate lile gari aina ya Range Rover jeusi lililoondoka pale kwenye yale maegesho muda mfupi uliokuwa umepita. Dereva yule alinielewa na bila shaka kumbukumbu ya uelekeo wa lile gari ilikuwa bado ipo vizuri kichwani mwake kwani muda ule ule aliingia na kuliwasha gari lake, likagoma kuwaka.

Oh shit!’ niling’aka kwa hasira, na wakati huo huo yule dereva akawa analalamika, “Aah! Matatizo yameanza tena!”

“Vipi, gari lako bovu?” nilimuuliza huku akili yangu ikiwa inawaza namna nyingine ya kufanya ili niwawahi akina Miriam na yule dereva wake.

“Aaah vijana wa Mombasa wanatumia sana uchawi, hawataki mimi nipate fedha kama wao,” yule dereva alilalamika.

“We mzee acha imani za kishirikina, we sema gari lako bovu!” nilisema kwa hasira huku nikishuka toka ndani ya gari lake. Kisha nikaikimbilia teksi nyingine ambayo dereva wake alikuwa kijana na alikuwa akiniita baada ya kugundua ile teksi niliyotoka imegoma kuwaka.

Niliifikia nikafungua mlango wa nyuma na kuingia. “Una petroli ya kutosha?” nilimuuliza yule dereva wa teksi kwa wasiwasi.

“Kwani we unakwenda mbali?” yule dereva aliniuliza huku akiingia na kuketi kwenye usukani.

“Sijajua…” nilimjibu. “Nataka ulifuate lile gari aina ya Range Rover jeusi lililoondoka maeneo haya muda mfupi uliopita.”

Yule dereva alielewa na muda ule ule akayaacha yale maegesho ya teksi na kuingia barabarani akiufuata ule uelekeo wa lile gari aina ya Range Rover.

“Ni akina nani wale? Au hayanihusu?” yule dereva aliniuliza na hapo hapo akajishtukia mwenyewe. Nikacheka kidogo kumtoa wasiwasi na kusema kwa sauti tulivu, “Ni mchumba wangu yuko na jamaa mwingine, nataka nikafumanie.” Yule dereva hakuuliza tena.

“Ila naomba kuwa mwangalifu sana, sitaki wajue kuwa wanafuatwa,” nilimwonya yule dereva. Akanielewa na wakati huo tukiingia barabara ya Jomo Kenyatta Beach. Dereva akakunja kulia na kuifuata barabara ile na mwendo mfupi baadaye tukaifikia Barabara ya Malindi.

Tulipoingia barabara ya Malindi tukaliona lile gari aina ya Range Rover likiwa linakikaribia kiwanda cha simenti cha Bamburi. Dereva wangu akaongeza mwendo na wakati tukifika pale Bamburi Cement lile Range Rover lilikuwa limechepuka kulia na sasa lilikuwa limeufikia mzunguko wa barabara jirani na ofisi za Azam.

Baada ya hapo sikujua ni barabara zipi tulizokuwa tukizipita zaidi ya kuona dereva akikunja kona moja baada ya nyingine kulifuata lile gari, hata hivyo bado tulikuwa makini kuhakikisha hawagundui kama wanafuatwa.

* * *

Inaendelea...
 
ufukweni mombasa.JPG

260

Liwalo na liwe…

Saa 6:50 usiku…

TULIFIKA kwenye mtaa wenye nyumba aliyokuwa akiishi Miriam Mutua ikiwa inaelekea kuwa saa sita usiku. Sikujua eneo lile liliitwaje lakini ulikuwa mtaa uliokuwa kimya sana, ni majumba makubwa na machache yaliyojipanga upande huu na ule. Tukaliona lile gari aina ya Range Rover jeusi lilipunguza mwendo na kusimama mbele ya geti kubwa jeusi kwenye nyumba moja kubwa ya kifahari.

Tulisimama umbali fulani toka pale lilipokuwa lile gari aina ya Range Rover na hapo nikakumbuka kumuuliza dereva wangu alikuwa akinidai kiasi gani kama malipo ya umbali wa kutoka kule Bamburi Beach Villa hadi hapo. Akaniambia kiasi na bila kupoteza muda nikamlipa takriban mara mbili zaidi na kumtaka ageuze gari lake na aende akanisubiri kule mwanzo kaabisa wa mtaa kabla ya kuchepuka na kuingia kwenye mtaa huo alioishi Miriam.

Kisha nilimwahidi kuwa ningerudi baada ya nusu saa na endapo angeona muda huo umepita bila ya mimi kutokea basi alikuwa huru kuondoka. Wakati huo lile Range Rover lilikuwa linaingia ndani ya uzio wa ile nyumba.

Nilishuka haraka nikiiacha ile teksi ikigeuza na kurudi kule tulipotoka. Wakati huo moyo wangu ulikuwa unanienda mbio. Kisha nilianza kutembea taratibu kuifuata ile nyumba ambayo lile gari aina ya Range Rover liliingia huku nikiwa tayari nimeishika bastola yangu mkononi.

“Liwalo na liwe,” nilisema huku nikizidi kujongea kwenye ile nyumba. Kisha niligeuka kutazama huku na kule kwa tahadhari lakini sikuweza kumwona mtu yeyote niliyemtilia shaka. Nikashusha pumzi na kuendelea na safari yangu bila kuonesha wasiwasi wowote nikiwa kama mtu aliyekuwa anapita zake.

Wakati napita niliitupia jicho la wizi nyumba ile kuutathmini usalama wa eneo lile. Mwanga wa taa kubwa juu ya ukuta wa ile nyumba uliniwezesha kwa kiasi fulani kuyasoma mazingira ya eneo lile. Na hapo nikaiona kamera moja kubwa iliyokuwa juu ya geti yenye uwezo wa kunasa picha ya kitu chochote mbele ya nyumba.

Nilitembea hadi mwisho wa ukuta wa ile nyumba kisha nikawa kama ninayeivuka kuelekea nyumba nyingine iliyokuwa inafuatia lakini nikasita na kugeuza shingo yangu kutazama huku na kule kwa tahadhari, sikuona mtu. Nikachepuka na kusogea karibu na mti mkubwa wa kivuli uliokuwa mwisho wa ukuta na matawi yake yalikuwa makubwa yaliyotengeneza kichaka kilichosababisha kiza fulani.

Nilisimama pale kwenye kiza kwa tahadhari huku hisia zangu zikiniambia kuwa mtu yeyote mwenye hila angeweza kujibanza kwenye mti ule na kuitimiza adhma yake mbaya. Nilipojiridhisha kuwa hali ilikuwa swari nikaukwea kwa tahadhari ule mti na kufanikiwa kufika juu kisha nikachungulia ndani.

Nyumba ile ilizungukwa na mazingira mazuri. Ilikuwa nyumba ya kisasa iliyozungukwa kwa bustani nzuri ya maua na nyasi zilizokatwa vizuri. Mle ndani kulikuwa na magari mawili yaliyokuwa yameegeshwa. Moja ni lile Range Rover jeusi na lingine lilikuwa Nissan Patrol la rangi ya maruni. Niliruka kwa tahadhari kuelekea mle ndani ya ule ukuta kisha nikatua kwa ndani kwa kunyata kama paka pasipo kufanya kishido.

Nikaelekea moja kwa moja kwenye baraza ya nyuma ya nyumba huku macho yangu yakiwa makini kuangaza huku na huko. Niliusogelea mlango ambao nilihisi ulikuwa wa kuingilia jikoni na kusimama kwa utulivu nikisikiliza kama ningeweza kusikia chochote lakini hali bado ilikuwa ya ukimya mno.

Nilijaribu kutafuta japo upenyo ili niweze kuchungulia ndani lakini sikuweza kwa sababu ndani kulikuwa kumefunikwa na mapazia mazito. Taratibu nikausogelea mlango na kushika kitasa, nikakinyonga taratibu kile kitasa ili nione kama mlango ulikuwa wazi, haukufunguka.

Nikasogea kwenye dirisha na kujaribu kukisukuma kioo, nikashangaa kuona kikisogea na kuniruhusu kuingia. Nikahisi ulikuwa mtego na hivyo nikajionya kuchukua tahadhari zote. Ghafla nikahisi nikiguswa na kitu cha baridi kichwani.

“Dondosha bastola yako chini taratibu,” sauti nzito ya mwanamume iliniamuru. Ilikuwa sauti yenye lafudhi ya Kisomali. Kijasho chembamba kikaanza kunitoka na wakati huo huo nikaidondosha chini taratibu bastola yangu.

“Weka mikono kichwani na usogee mbele hatua mbili na usijaribu kuleta ujanja,” nikaamuriwa tena na mtu yule aliyekuwa nyuma yangu. Bila ubishi nikaweka mikono yangu kichwani na kusogea mbele hatua mbili. Yule jamaa akawa amepata nafasi ya kuiokota ile bastola yangu. Nilikuwa nimekamatika kirahisi mno.

Kisha nikaongozwa hadi sebuleni ambako niliwakuta Miriam na wanaume wengine wawili, mibaba iliyoshiba, wakiwa wamekaa katika masofa kwa kuizunguka meza moja ya kioo ambayo ilikuwa na chupa mbili kubwa za mvinyo, mabunda ya noti na bastola mbili, moja ilikuwa aina ya 45 Colt na nyingine aina ya FNX 45 Tactical zote zikiwa zimewekwa kiwambo cha kuzuia sauti. Wale watu wakanitumbulia macho macho makali yaliyoashiria kila aina ya ukatili uliokithiri.

I’m so sorry, my dear…” Miriam aliniambia kwa dharau huku akiachia tabasamu. “Hata hivyo haya umeyataka mwenyewe kwa kupenda kufuatilia mambo yasiyokuhusu. Nasikitika sana kwa kijana mtanashati kama wewe kufa kifo kibaya kama utakachokufa, tena unafia ugenini!” Miriam aliniambia kwa kebehi huku tabasamu lake likikataa kwenda likizo.

Niliwatazama wale jamaa, hawakuonesha kuwa na wasiwasi hata chembe. Bado waliendelea kunywa mvinyo taratibu kana kwamba hawakuwa na habari zozote kuhusu mimi. Mtu yule aliyekuwa nyuma yangu ambaye sasa nilitambua kuwa ni yule jamaa aliyekuwa akiiendesha ile Jeep iliyonifungia mkia wakati natoka Serena Beach Resort mchana, sasa akatoa pingu na kunifunga mikono yangu kwa nyuma. Sikuwa na ujanja wowote wa kuweza kujiokoa tena baada ya mikono yangu kufungwa.

Nilijilaumu kwa nini sikuwa nimemtaarifu Leyla huenda angekuja kuniokoa. Hata hivyo niliamua kuendelea kuvuta muda kwa kujaribu kumwongelesha Miriam aliyeonekana ndiye mkuu wa kikao kile na mwenye amri.

“Miriam, tambua kwamba unalisaliti taifa lako. Unaiuza nchi yako kwa magaidi na hatimaye utasababisha maisha ya watu wengi wasio na hatia kupotea bure…” nilisema kwa sauti tulivu huku nikimtazama Miriam.

“Ahaa, kumbe unalifahamu vizuri jina langu!” Miriam alisema kwa mshangao. “Nikadhani ungeniita Zuena… you’re very smart, my dear.”

“Si wewe tu, nawafahamu wote mliopo kwenye sindicate hii akiwemo Abshir na bosi wenu Abdoulkader Omar… nafahamu kuwa ni wewe uliyeleta ule ujumbe wa vitisho pale hotelini Serena Beach Resort,” nilimwambia Miriam kwa utulivu, kisha nikaongeza, “Nakuomba achana na mambo haya, damu za watu zisizo na hatia zitakulilia toka udongoni. Hivi ni kitu gani kimekufanya uwe hivi? Ni hizo fedha?”

Miriam hakujibu bali aliinuka toka pale kwenye sofa alipokuwa ameketi na kunisogelea. Japokuwa nilikuwa nimefungwa mikono kwa nyuma lakini nilikuwa namsubiri kwa hamu anisogelee karibu zaidi halafu ningemfanyia shambulizi la hatari la kushtukiza, sikuwa na ujanja hivyo nilishaamua kujitoa mhanga. Ni kama aliyeyasoma mawazo yangu, aliogopa kunikaribia karibu zaidi.

Inaendelea...
 
ufukweni mombasa.JPG

261

Alisimama akanitazama akiwa na uso uliojaa hasira kisha akasema kwa ukali, “Don’t be stupid, Jason. Hizi kazi tunafanya kwa sababu tunatafuta kuwa na maisha mazuri. Sasa kama fursa imekuja ambayo itakufanya uishi maisha mazuri kwa nini usiitumie?”

“Maisha yepi mazuri wakati unaua Wakenya wenzio? Unadhani…” nilimwambia Miriam kwa uchungu lakini akanikata kauli.

“Mambo ya Kenya yanakuhusu nini, sioni sababu ya kuendelea kujibishana na wewe hapa wakati si muda mrefu utakuwa umekufa? Nilidhani ungeutii ujumbe wangu na kuondoka zako kurudi kwenu kumbe wajitia jasusi mbobevu! Ona sasa umekamatika kijinga sana tena bila vurugu yoyote,” Miriam alitamba kisha akaangua kicheko kikubwa huku akinitazama kwa dharau.

“Najua nitakufa na siogopi, lakini kabla sijafa wewe na genge lote la maharamia mtakuwa mmeshafungwa na wengine kutangulia chini futi sita,” nilisema kwa hasira na kumfanya Miriam apandwe na ghadhabu.

Alinisogelea karibu zaidi pasipo kuchukua tahadhari na kuninasa kibao kikali cha kike. Hilo likawa kosa kubwa. Kwa kuwa hasira zilikuwa zinachemka ndani yangu sikuweza kuhisi maumivu yoyote, ilikuwa kama vile alikuwa amenipapasa tu kwenye shavu langu.

“Mpumbavu kama wewe utanifanya…” alianza kuongea kwa nyodo lakini hakumalizia sentensi yake nikawa nimefanya tukio hatari la kushtukiza.

Niliruka juu na wakati huo huo nikijikunja na kuipitisha chini ya miguu mikono yangu iliyokuwa nyuma ili ije kwa mbele, kisha kabla sijatua chini nikajitupa kumvamia Miriam, nguvu niliyoitumia ilitufanya sote tukapiga mweleka na kuanguka chini.

Miriam alipoanguka akatua juu ya ile meza ya kioo iliyokuwa na chupa za mvinyo, mabunda ya fedha na zile bastola na kuivunja vipande vipande. Kiuno chake kikapata hitilafu na mkono wake wa kulia ukavunjika na kumfanya apige yowe kali la maumivu.

Shambulizi lile hatari lilikuwa la ghafla mno na liliwakuta wale jamaa wakiwa hawajajiandaa na hivyo wakapigwa na butwaa kwa sekunde kadhaa. Nikaitumia nafasi hiyo ya taharuki kuiwahi bastola moja aina ya FNX 45 Tactical iliyokuwa imeanguka karibu yangu na kuishika kwa mikono yangu iliyofungwa pingu. Nikageuka kumwelekezea bastola yule mwenye asili ya Kisomali aliyekuwa nyuma yangu.

Na hapo nikawaona wale jamaa wenye miraba minne wakizinduka, na kabla sijafanya chochote mmoja wa wale jamaa wa miraba minne akaruka na kunipiga teke kali lililonirusha na kunitupa sakafuni huku ile bastola ikinitoka mikononi, na wakati huo huo yule mwenye asili ya Kisomali aliyekuwa nyuma yangu akaielekezea bastola.

Ghafla bila kutegemea nikamwona akianguka kwa kishindo huku akitoa yowe la uchungu. Wote tukapigwa na butwaa kwa kitendo kile lakini kabla hatujang’amua nini kilikuwa kinaendelea nikamwona jamaa mwingine kati ya wale wanaume wa miraba minne ambaye muda huo alikuwa ameiwahi bastola yake na kuielekeza kwangu naye akianguka kwa kupigwa risasi. Na hapo nikagundua kuwa kulikuwa na mtu ambaye alitumia bastola yenye kiwambo cha kuzuia sauti.

Kwa kasi ya aina yake nilijitupa chini na kuviringika kuifuata bastola ya yule jamaa aliyepigwa risasi huku mikono yangu ikiwa bado imefungwa pingu. Bila kutegemea yule jamaa aliyekuwa amebakia aliruka juu na ghafla nilijikuta nikipigwa teke kali la tumbo lililonifanya nishindwe kutimiza azma yangu ya kuifikia ile bastola. Nilijikunja nikisikia maumivu makali kupita kiasi kwa sababu teke lile lilikuwa ni kali mno. Kama ningekuwa mtu legelege sidhani kama ningeweza kuamka.

Niligugumia kwa mauimivu makali wakati yule jamaa akiruka hewani na kutua karibu kabisa na mlango kisha akageuka kwa kasi na kuelekeza bastola yake upande wangu, nikachupa na kutua nyuma ya sofa na wakati huo huo ukasikika mlio wa risasi. Nikafumba macho. Nilipoyafumbua sekunde kadhaa baadaye sikuamini kile nilichokuwa nikikiona.

Macho yangu yalimwona Miriam akiwa amelala chini akivuja damu kifuani. Yule jamaa aliamua kumtwanga risasi Miriam na kummaliza kabisa na tayari alikwisha tokomea zake. Kwa mara nyingine tena nikaamini kwamba nilikuwa napambana na watu hatari mno kuliko hatari yenyewe.

Wakati nikiwa katika mduwao nikahisi kusikia sauti ya mtu akitembea mle ndani, nilipotazama upande ule nikamwona Leyla akiwa kasimama mlangoni akiwa na bastola inayofuka moshi, nikapigwa na butwaa nisijue alikotokea.

Jason, are you okay?” Leyla aliniuliza huku akinitazama kwa umakini.

Yeah! I’m okay!” nilijibu huku nikijiinua toka pale nilipojificha.

“Mshenzi amefanikiwa kutoroka,” Leyla alisema huku akimsogelea yule mwenye asili ya Kisomali aliyekuwa amenifunga pingu na kuanza kumpekua mifukoni, akazipata funguo za ile pingu na kunifungua.

“Pole sana, Jason,” Leyla aliniambia huku akimwendea Miriam pale alipokuwa amelala huku akivuja damu nyingi kifuani. “Hawa jamaa ni watu hatari mno.”

Alipomfikia Miriam akamgeuza ili aangalie kama angeweza kuongea lolote lakini akagundua kuwa tayari alikwisha kufa. Nilisimama nikamtazama Miriam kwa uchungu. Umbo lake la kuvutia lilikuwa limelala kwenye dimbwi la damu.

“Dah! Haya ndiyo malipo ya usaliti. Mdada mrembo kama wewe hukustahili kabisa kufa kifo cha namna hii!” niliiambia maiti ya Miriam kisha nikashusha pumzi na kuiokota bastola yangu.

“Hivi ulijuaje kama nipo hapa?” nilimuuliza Leyla kwa mshangao mkubwa.

“Ni hadithi ndefu… ila nakuomba uondoke haraka, mkuu wangu na askari wengine wapo njiani kuja hapa nisingependa wakukute,” Leyla aliniambia kwa msisitizo. “Kesho saa nne asubuhi nitafute.”

“Kesho au leo kutakapokucha?” nilimuuliza huku nikiinua mkono wangu kuitazama saa yangu ya mkononi, ilionesha kuwa ilikuwa saa sita na nusu usiku, nikaanza kupiga hatua kuondoka.

“Ooh ni leo kweli… hata hivyo nadhani umenielewa,” nilimsikia Leyla akisema, wakati huo nilikuwa natoka.

* * *

Mambo yanazidi kunoga, endelea kufuatilia...
 
View attachment 2339670

“Dah! Haya ndiyo malipo ya usaliti. Mdada mrembo kama wewe hukustahili kabisa kufa kifo cha namna hii!” niliiambia maiti ya Miriam kisha nikashusha pumzi na kuikokotaa bastola yangu.

Inawezekana Leyla akawa mtu mzuri kwa Jason
 
We nae si upande ndege urudi kwenu tuhangaike wote na tozo mwisho ufie huko utupe shida kuchanga kukusafirisha kata tiketi leo panda basi la alfajiri kesho mfyuuuu
 
Iko poa sanaa ,, asante Bishop

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
We nae si upande ndege urudi kwenu tuhangaike wote na tozo mwisho ufie huko utupe shida kuchanga kukusafirisha kata tiketi leo panda basi la alfajiri kesho mfyuuuu
Haha! Anatafuta sifa matokeo yake zimtokee puani[emoji23][emoji23]...
 
Ntafurahi haswa, af Rehema aje kuolewa na Warari
Haha! Warari atawezana kweli na jasusi ofisa kificho? Rehema anaweza kuonekana mjinga lakini kila.mara ndiye anaibuka mshindi...
 
Ujue bishop nataka nikuulize lini tena utashusha mzigo ila naogopa
 
Haha! Umeanza lini tabia ya kuniogopa?...

Ila dah, katika mfululizo wa Harakati za Jasom Sizya hii season ya tano "Ufukweni Mombasa" na ile inayofuata yaani ya sita "Taharuki" zimenitesa sana kuziandika maana kuna wakati nilijikuta naandika mambo yasiyopaswa kuongelewa hadharani...
 
Nimeanzia kwenye ufukweni kuna namna nakuogopa nahisi unaweza hata kunikamata na kunifunga bila kosa maskini mie na hapo ulivosema zimekutesa kuandika ndo natamani nikuombe japo kesho
 
Sasa bwana Bishop Hiluka unaogopa nni kuweka hayo mambo?? Huoni unatunyima baadhi ya vitu?? Ama huoni nafsi yako unakusuta kwa kutuibia??

Weka mambo wazi kiongozi acha kufutafuta
 
Nimeanzia kwenye ufukweni kuna namna nakuogopa nahisi unaweza hata kunikamata na kunifunga bila kosa maskini mie na hapo ulivosema zimekutesa kuandika ndo natamani nikuombe japo kesho
Dah! Mwogope jasusi Jason, mimi si lolote![emoji23] ngoja nione kama nitaweza kutupia kesho maana nipo busy kinyama, kuna report ya kazi fulani naiandaa kwani inatakiwa haraka sana...
 
Back
Top Bottom