SIMULIZI: Nilipata nafasi ya kuongea na Gurus wawili wenye mitizamo miwili tofauti kuhusu Kuzaliwa, Kifo na uwepo wa Mungu pamoja na Dini

Okay mkuu.

Japo bado sijashawishika kama tunatumia base mbili tofauti lkn nnachoweza kusema ni kwamba wewe unatumia moja ya 'Abstraction' ilotengenezwa kuelezea hiki kitu.

Sina uhakika kama uko kwenye field ya computing lkn kwenye hii field kuna mfano mmoja ngoja nitoe labda unaweza kunielewa coz nataka kuelezea hio Abstraction ambapo kwako wewe unadhan ni base lkn sio bali ni abstraction tu.

Computer ni very complicated lkn ni very powerful pia, so inaweza fanya vitu vingi. Waliodizain computer walitengeneza vitu vinaitwa Abstractions ambapo sisi programmers hatuna haja ya kujua underlying mechanisms lkn tunatumia hizo interface za hizo abstractions kucommand computer ifanye kazi tofauti tofauti. Mfano mm nikitaka kuandika program ya kupiga picha kwa camera ya computer sihitaji wala kujua hardware details za hio camera lkn natumia interface ya abstraction ilodizainiwa na hao walotengeneza computer au operating system.

Sasa hizo abstrations na interface zao kwenye computing ziko za aina nyingi na zinaweza fanya kazi nyingi. Kazi moja inaweza fanywa na interface zaidi ya moja, so mm kama nimechagua interface X kupiga picha lkn mtu mwngne anaweza chagua Interface Y pia kufanya kazi hiohio, lkn base ni ileile japo tumekuja kutofautiana kwenye hizo abstractions tulizotumia. Ukienda mbali zaidi hizo interfaces na abstractions utakuta ziko tofauti kabisa coz zimeandikwa kwa languages tofauti tofauti. LAKINI to their lowest levels zina base moja.

Sasa nmeamua kutumia mfano huu kwa sababu ndo naona unaweza elezea situation hii kiurahisi, hatutumii base tofauti bali wewe unatumia Abstraction na hautaki kukubali kama ni abstraction kwa sababu umeshikilia dini yako.

Kama umesoma vzr bandiko langu la mwanzo kabisa hata mm niko hvohvo na ndo maana niliharibu kabisa kile kitabu beyond recovering, sikutaka kukubali abstraction nloitumia toka utotoni nije nii-question.

Tuishie hapo lkn nimejifunza kitu kwako na naamini pia umejifunza kitu kwangu.
 
Piah hili la ku interfere karma umeniongezea knowledge mkuu.
 
Aisee hii hali pia huwa inanipata naweza fika mahala au kufanya jambo kisha mawazo yanikuja na ninaona mbona hili jambo nilisha lifanya na hili eneo nilisha kuwepo kabla na huyu mtu nakumbuka nilisha kutana nae..
 
Maelezo yako haya yako sahihi kabisa nakubaliana na wewe. Kwenye physical world hizi abstractions unazozisema hapa zinafanya kazi.
Tofauti na mfano wako huu, hapa tunajadili mambo kwenye ulimwengu wa roho na si kwenye ulimwengu wa mwili. Kwa mfano, ulishawahi kuota ndoto? Kama ulishawahi, mimi hapa nilipo unaweza ukanihakikishiaje kuwa huwa unaota? Nikisema kuwa huwa huoti ndoto wakati kumbe huwa unaota, nitakuwa nimefanya makosa? Nilichokuwa najaribu kusema ni kwamba unatumia principles za physics kuelezea vitu ambavyo viko kwenye realm ambayo ni metaphysical
Still, nafurahi kwamba wewe ni programmer; utakuwa uko vizuri sana

By the way, hii issue ya wataalamu wa AI kutengeneneza computer inayokua (yaani yenye uwezo wa kujiongeza yenyewe akili mithili ya ambavyo binadamu huwa anafanya anapokuwa anakua kuanzia utotoni kwenda kwenye utu uzima), imefikia wapi? Maana nakumbuka mwanzoni mwa miaka ya 2000, hii ndiyo ilikuwa ni MAIN CHALLENGE ya CENTURY kwenye ulimwengu wa IT au AI
 
Mkuu hili somo ni zito na tunashukuru sana kwa kupata uelewa zaidi. Swali kidogo, umesema kwamba hizi energies watu wanazitape na kuzimanipulate kwa namna watakavyo wao, na pia negativity na matendo mengine uliyotaja hapa yanazififisha au kuziondoa kabisa! Nani anayedetermine matendo fulani ni negative? Na Kama ndivyo, tunaamini wachawi ndio wana negativity zaidi ya wengine kiafrika, kwa nini sasa wanaweza kuzichukua na kuzitumia pia? Au kuna namna pia nyingine? Ahsante kwa ufafanuzi
 
Hapo sasa utambaue jamaa kazungumzia nguvu za asili ambazo waweza kuwa nazo wakati mwingine usitambue kama unazo, na zile za kujipatia kwa kuforce, kama hizo za kishirikina.
 
Hii kitu wanaiita AI Singularity lkn bado hatujafikia huko coz kuna wanaharakati wanadai kwamba AI ikifikia hio level basi inaweza kuangamiza Humanity na ndo ukawa mwisho wetu. Hio ni kwasababu uwezo wa AI ni mkubwa sana na speed of operation ni kubwa sana. Kwenye system inayofanya kazi kutumia AI sekunde moja kwake ni kama mwezi mzima. So AI ikifikia level ya kujitambua na kufanya self-growth watu baadhi wanaogopa kwamba hizo system zitafanya mapinduzi na kutuua sisi binadamu, na hio vita hatutoiweza kamwe.

Matajiri na watu wenye ushawishi kama vile Elon Musk wanapinga sana hio kitu na kiukweli madhara yake yalishaonekana kwenye baadhi ya labs huko USA.
 
Nani anayedetermine matendo fulani ni negative? Na Kama ndivyo, tunaamini wachawi ndio wana negativity zaidi ya wengine kiafrika, kwa nini sasa wanaweza kuzichukua na kuzitumia pia? Au kuna namna pia nyingine? A
Okay swali challenging sana ambalo hata mm niliwahi kuuliza watu baadhi walokua wananifafanulia hili jambo, mwisho nikaja kupata maelezo ambayo naona yanakaribia kuwa jibu sahihi na kwa sasa kwangu hilo ndio jibu sahihi.

Iko hivi, kuna standards 2 unazoweza kutumia kujua kwa kitu fln ni neg au positive kwanza kuna kitu kinaitwa GOLDEN RULE, inasema kwamba USIMFANYIE MWENZAKO KITU AMBACHO HUTOTAKA WEWE KUFANYIWA.

Ya pili ni Natural Order, hii ni kwamba inabidi tufuate nature inachotaka. Nitie mfano kdg, nature inataka tuzaliane na ili kuzaliana lazima mtu mme na mke washiriki. Sasa ukienda nnje ya hapo ujue ni kosa na nature siku zote ni "Merciless and Unforgiving" so ukienda against natural order ujue kuna feedback utaipata tu. Angalia mambo yote yanayoenda against natural order then utatambua kuna mateso wahusika hupitia.
 
Kwa nini isiwe designed tu for experimtal purposes kwa muda huu halafu ikawa archived somewhere kwenye maabara ikisubiria muda muafaka utakapofika (kama itatokea hivyo) iweze kutumika? Huoni kuwa hili swala la NWO kuna uwezekano likaja likapunguza 1/2 of the entire wordl population? Huoni kwamba hiki kitu kikifikia hatua ya utelekezaji SUPERCOMPUTERS za aina hii zinaweza kuhitajika kuanza kutumika?
 
Pia kuna 4 virtues ambazo ukizi-cultivate zitakusaidia kujua kama kitu ni neg au positive, hizo ni WISDOM, JUSTICE, COURAGE and MODERATION
 
So AI ikifikia level ya kujitambua na kufanya self-growth watu baadhi wanaogopa kwamba hizo system zitafanya mapinduzi na kutuua sisi binadamu, na hio vita hatutoiweza kamwe.
AI is just a program, so one can simply programme it the way he likes. Kwa mfano, mimi ningeweza kui-programme iwe tofauti kidogo na mwanadamu; kwamba isiwe na hasira wala wivu, na izidi kuongeza upendo kwa binadamu kadri inavyokzidi kukua. Sasa hizi hofu zingine zinatoka wapi?

Isije ikawa ni challenge ambayo watu wame-ipose halafu uwezekano wa kuirtekeleza ukaksoekana halafu watu wakaanza kutafuta visingizio!
 
Ni sawa lakini kuna magroup mawili hapa, kuna wanaokubali Advancement ya AI na vilevile kuna wanaokataa. Na wote hao wanafanya harakati kwa vitendo pia kuonesha msimamo wao, nikimaanisha wanaokubali Advancement kwenye hii kitu bado wanawekeza mabilion ya fedha ili kuendeleza utafiti.

In my Opinion hii NWO haifuati natural order, so kuna adjustments tu zitafanyika na isitekelezeke au kama ikitekelezeka basi itakua ndio mwanzo wa mwisho wa hii phase ya humanity tuliopo sasa kama phase nyngne zilivyoisha na viumbe kuangamia. Kuna jamaa huwa anasema kwamba "If New World Order is not based on Natural Order then it's not something to last"
 
Ahsante kwa ufafanuzi mkuu, Kama ulivyosema hili challenging! Ukisikiliza wanazuoni wengine hasa wa manifestation kwa imagination wanasema neno linaumba na neno linatokana na thoughts be them negative or positive haijalishi so long as umeliumba in details na ukalijengea feelings! Some kind of confusion, Msikilize huyu Neville Goddard kwnye imagination creates reality! Anatoa mada complex kweli
 
Habari kali linux ni njia gani/zipi za kiroho zitakazoweza nisadia kucrack interview bila kujali ni wapi au ni lini?
Mkuu hii ina mambo mengi japo kwa mimi kilichokua kinanisumbua ni kwamba nilikua sina mvuto fln hv, kama nlivyosema hapo juu kuna nguvu (impure) ambazo mtu anaweza kuzaliwa nazo au akawekewa akiwa anaishi. Hizo zinaweza kuingia na kuharibu Nguvu asilia za kiroho ulizonazo then ukawa mtu wa mikosi, huna mvuto, etc....

Siwezi endelea zaidi coz sitaki watu waje kusoma na kunishutumu kwa kufanya endorsing ya baadhi ya vitu na mwisho ikaleta picha mbaya, pia hilo halikua lengo la mie kuleta huu uzi humu lakini natumaini nimekujibu kwa kiasi fln.
 
umenijibu kwa kiasi fulani, asante.
 
taarifa mhe speaker: uislamu unamtambua roho mtakatifu. rejea suratul qadri : 3
 
Thanks mkuu kwa kushea..... I wonder how comes sikuuona huu uzi almost a year now
 
Kali linux ,,naona umepotea kuna muendelezo ulisema utauleta umekua kimya sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…