Simulizi: Nini maana ya mapenzi

Simulizi: Nini maana ya mapenzi

SEHEMU YA 361

Jioni ya siku hiyo, mama Erica alitoka kidogo na kumuacha mwanae nyumbani, muda kidogo alikuja mgeni na kugonga mlango, Erica alipoenda kufungua alikuwa ni Tumaini hata akamshangaa kuwa siku hiyo kafata nini kwao, Tumaini bila salamu alimuuliza Erica,
“Mama yupo?”
“Mama yangu wa nini?”
“Nimekuuliza tu yupo? Nijibu”
“Hayupo katoka”
Erica akashtukia kapigwa kibao, cha kwanza na cha pili kwakweli Erica hakumuelewa kabisa Tumaini kumbe aliulizia kuhusu uwepo wa mama yake Erica ili aweze kumpiga Erica, aliamua kumuuliza,
“Haya umenipiga, umenipigia nini sasa?”
“Unaona ulichomtendea kaka yangu ni sahihi? Umefanya kajifungia ndani na kusema Erica Erica, umekuwa nani wewe katika jamii?”
“Tumaini naomba uondoke maana nisije kuongea maneno mengine ya karaha ukashindwa kuvumilia hapa, naomba uondoke”
“Hebu ongea hayo maneno yako ya karaha nikusikie”
“Hivi wewe Tumaini una nini na mimi lakini? Kama unamtaka kaka yako si ukatembee nae”
“Unasemaje wewe”
Tumaini akataka kumvaa Erica ila akatokea Bahati na kuingia katikati yao, alishangaa sana kuona ule ugomvi na akamuuliza Erica kuwa kuna nini, ila Erica alijibu kwa kujiamini,
“Namshangaa huyu dada, toka nipo na kaka yake kutwa kufatilia maisha yangu, sijui haridhishwi huko kwingine! Kama unamtaka kaka yako kamchukue uone laana itakavyokufatilia”
Kwakweli Tumaini alifura hasira kitendo ambacho Bahati aliamua kumuingiza Erica ndani na kumwambia Tumaini aondoke kisha yeye kuingia ndani, akaanza kuongea na Erica,
“Kwanini uwe na mwanaume ambaye ndugu zake wanakunyanyasa hivi wakati mimi nipo!”
“Usinichekeshe na wewe, ndugu zako si ndio ukoo mzima hawanitaki sasa hiyo wewe upo ndio nini?”
“Erica, mimi nipo tayari kwa chochote hata ukitaka leo hii naenda kumuacha Yule mwanamke wala simpendi wala nini, nakupenda wewe Erica, naomba ukubali nikuoe”
“Bahati ushachelewa, Yule mwenyewe nilikuwa namjibu tu ila kwasasa sitaki mahusiano ya aina yoyote bora niwe mwenyewe tu, sitaki mwanaume yeyote, nitalea mwanangu tu”
“Erica usiseme hivyo wakati mimi nipo na ninakupenda sana, Erica nilishasema hata dunia nzima iseme kuwa wewe malaya na unajiuza ila mimi nitaendelea kukupenda tu. Maana nimefundishwa kupenda na si kitu kingine, nitakupenda maisha yangu yote”
“Asante Bahati ila kwasasa hapana, mimi na wewe tubaki tu marafiki au ndugu”
Basi Bahati alikuwa akijitahidi pale kusema ya moyoni mwake ila ilikuwa ngumu sana kueleweka kwa Erica.

Muda huu mke wa Bahati alikuwa na mawazo sana ya jambo la kufanya aliamua kumpigia simu Salma ili ajaribu kumshirikisha anachowaza,
“Salma ndugu yangu mwenzio nimefikiria nimeona tukingoja mpaka arobaini iishe tutakuwa tumeumia sana, huyu Erica ni ana nitesa vilivyo”
“Eeeeh kafanyaje tena?”
“Hebu fikiria nimetoka kujifungua ila mume hanijali wala nini yani, hataki ndugu zangu waje kuniuguza hapa wala ndugu zake anasema nikitaka kuuguzwa niende ila sio ndugu kuja hapa, na mimi siwezi kuiach nyumba yangu nimeamua kuvumilia tu, jamani jana tumerudi nyumbani hata sikuwa na raha muda kidogo simu, sijui Erica anapiga, mwanaume anahaha huku na kule, muda kidogo simu sijui Erica anataka nini, nikaamua kuficha simu bafuni, ndugu yangu alivyogundua nimeficha simu, nimepigwaje? Yani nimepigwa hatari na tangu aondoke hiyo alfajiri hajarudi hadi muda huu, hebu fikiria mume wa mtu kweli anafanya hivi jamani!”
“Sikia Nasma, mimi niliongea na Yule mmama akasema kuna dawa sijui ya kumfunga mume ila kwa upande wangu huyu mume wangu sijui kama atafungika jamani, na ndugu zake wakijua nimemfunga yani wataniharibu maana hapa naishi kwao tena sababu ya mama mkwe ana roho nzuri, sasa sijui tufanyeje?”
“Mimi nina wazo Salma”
“Wazo gani?”
“Tumfanye Erica kuwa chizi, yani wote watamkimbia, huyo mumeo atamkimbia na Bahati wangu atamkimbia, yani awe chizi kabisa abaki kuhangaika na familia yake”
“Mmmh hilo swala zuri, ila inawezekanaje?”
“Kuna mtaalamu namfahamu yani kinachotakiwa ni kupata majina matatu ya Erica basi kazi imeisha, sasa sijui hayo majina tuitayapata wapi maana mimi hata kumuuliza mume wangu siwezi, nitapigwa hadi nishangae”
“Hiyo sio kazi kwangu, nina shemeji yangu ana undugu na Erica yani yeye ndio atanitajia majina matatu ya Erica hata usiwe na shaka. Nakwambia huyo Erica habari yake imekwisha maana akiwa kichaa nani tena atamtaka?”
“Hakuna, yani tutamkomesha. Basi nakutegemea, tufanye haraka maji ya shingo yamenifika dhoga yangu”
“Aaaah usijali, ndani ya siku mbili hizi atakuja tu Yule shemeji kuniona nitakupa majina ya Erica sio kazi kuyapata”
Basi walifurahia na kupongezana kwa ajenda yao.
 
SEHEMU YA 362

Usiku mama Erica alirudi na Bahati akaondoka, kwahiyo Erica akaongea ongea na mama yake na kumwambia maamuzi yake aliyoamua kuwa hataki tena kujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi, basi wakaongea na kwenda kulala.
Kabla ya kulala Erica alipigiwa simu na Derick akaipokea simu ile,
“Erica, dada yangu kipenzi nimekumiss”
“Asante”
“Mmmh erica, hata kusema nimekumiss pia jamani hakuna”
Erica alicheka tu na kumuuliza,
“Haya niambie kilichofanya unipigie usiku usiku huu”
“Kwani kuna ubaya ndugu kwa ndugu kupigiana simu?”
“Hakuna ubaya ila undugu wako wewe nina mashaka nao, haiwezekani ukawa na mawazo finyu kama unayokuwaga nayo”
“Jamani Erica, basi tuachane na hayo, ila naomba tuonane nina maongezi na wewe”
“Njoo tuongee nyumbani kwetu, kwakweli siji popote utakaposema nije”
“Mbona una roho mbaya hivyo Erica?”
“Nadhani huna cha kuongea na mimi, kwaheri”
Erica akakata ile simu na kulala zake kwani hakutaka kujiumiza kichwa kwa wakati huo.
Kulipokucha aliamka mapema kabisa na kujinyoosha mwili katika kazi za hapa na pale, akapigiwa simu na Fetty na kuanza kuongea nae,
“Shoga yangu nina shida, nina shida, nina shida”
“Shida gani tena?”
“Nina shida ya laki tatu, naomba unikopeshe tafadhari”
Erica akakaa kimya kwa muda na kuwaza zile hela alizozituma kwa Dora, maana zingekuwepo kwake basi asingeshindwa kumtumia Fetty, na kumwambia hana aliona sio swala zuri sababu alishamwambia mwanae amekuwa balozi kwahiyo lazima ahisiwe kuwa na hela, akamwambia
“Fetty, subiri kidogo kuna mahali nikuulizie halafu nitakutaarifu”
“Nashukuru sana ndugu yangu, nashukuru kwa kunusitiri”
Basi simu ile ilivyokatika, Erica akapata wazo la kumpigia simu Dora ili amuombe hela kidogo, alipiga iliita hadi kukatika, akapiga tena hivyo hivyo, akapiga tena ndio Dora akapokea na alikuwa akiongea sauti ya usingizi kabisa,
“Kheeee Dora, inaenda saa nne hii hujaamka?”
“Niamke mapema nina shida gani? Wenye shida ndio wanaamka mapema ila sio sisi wenye raha zetu”
“Mmmmh mna raha ya nini?”
“Raha ya kila kitu maana dunia ya sasa kuwa na hela ndio kila kitu, unaenda unapotaka, unafanya unachotaka, unakula unachotaka, kwahiyo acha niburudike mie.”
“Mmmmh hujampa mzee Jimmy zile pesa?”
“Nimpe nina wazimu?”
“Si ulisema bora nikupe wewe”
“Ndio bora unipe mimi nitumie, Erica Yule mzee kashanitumia sana nishampa mapenzi sana ila hakuna nilichoambulia kwake zaidi ya vilaki laki halafu wewe usiyempa chochote ndio anakujazia mavitu, kwakweli roho iliniuma yani kazi nifanye mimi na faida upate wewe, kwahiyo hii ni haki yangu hata mzee Jimmy akifanya chochote hakitanipata maana hii ni haki yangu”
“Ila wewe jamani, si ulisema lengo la mzee Jimmy ni bay asana?”
“Ila wewe Erica hujiongezi! Huna huruma wewe, yani matatizo yote niliyokwambia ninayo sababu ya mzee Jimmy ila bado ukataka ule hela yake usiyoitolea jasho! Nimeenyeka mwenzio, nimekukuruka ach anile matunda ya kazi yangu, jana na juzi nilikuwa kwenye starehe tu ndiomana nimeamka na uchovu”
“Haya bhana ila nisaidie kitu, mwenzio sina hela yoyote yani hakuna kitu mfukoni kwangu, naomba unisaidie laki tatu”
“Shoga yangu laki tatu tu, sio kitu kwangu nitakupa ila tukutane kesho mahali nikupatie maana kuna jambo nahitaji kuongea nawe”
“Sawa hakuna tatizo kwahiyo muda gani?”
“Iwe kwenye saa kumi kumi Erica wangu sawa mama eeeh! Ninakupenda shoga yangu uuuh yani ushoga wetu hudumu daima”
“Sawa bhana maana mimi mjinga kukupa wewe hela zote”
“Hata sio mjinga shoga yangu umefanya cha maana sababu ulijiona hustahili kumiliki hizi pesa, sasa ni mimi ndio nastahili kuwa nazo ndiomana ukanipatia, acha mwenzio nijifute jasho kwa kazi niliyoifanya siku zote hizi kwa Yule mzee”
Erica aliongea ongea nae na kukata simu ila alijiona ni mjinga sana kumkabidhi pesa Dora ila kwa upande mwingine aliona acha tu atumie aliyezihangaikia.
Akampigia simu Fetty na kumuahidi kuipata hiyo pesa kesho kutwa, na Fetty alimshukuru sana maana alikuwa na shida haswaaa na ile pesa.

Basi jioni yake Erica alipigiwa simu na Erick kwa hakika hakutaka kuipokea na kuifanya iite mara nyingi nyingi bila ya kuipokea hadi Erick alipopiga simu kwa mara ya tatu ndipo Erica alipokea ile simu na akamwambia,
“Ongea kilichokupigisha simu”
“Usiwe mkali hivyo Erica, hujui ni kitu gani kimetokea?”
“Kitu gani kunidhalilisha vile? Hivi Erick una akili kweli, mwanamke unayempenda unaweza kumdhalilisha kiasi kile? Erick sikutaki tena kuanzia leo”
“Erica usiseme hivyo kumbuka mimi na wewe tuna mtoto”
“Tuna mtoto kitu gani? Ungetambua hilo ungenidhalilisha kiasi kile kwenye ile hoteli? Ungefanya mimi nionshe vyombo usiku kucha? Kwakweli Erick nakuchukia yani nakuchukia haswaa”
Erica akakata simu ila kiukweli yale yote alikuwa akiongea kwa hasira tu kwani moyo wake ulijaa habari za Erick tu nay eye peke yake aliyekuwa anampenda, alitamani muda wote Erick ampigie simu kumuomba msamaha ila mpaka usiku unaingia na kulala, Erick hakupiga simu tena yani kitu hiko kilimuuma moyo zaidi na kujisemea,
“Hivi kwanini wanaume wana roho mbaya hivi? Ndio huyu aliyekuwa anasifiwa kuwa anajua sana kubembeleza jamani? Mbona hamna kitu chochote maana sioni kubembelezwa wala nini jamani, aaah Erick hanipendi”
Akawaza sana na kukosa raha kabisa, hadi analala na kuamka asubuhi hakupata simu yoyote ya Erick zaidi ya kumpigia simu Dora ili ajue ni wapi atakutana nae kwa siku hiyo kama walivyopanga.
 
SEHEMU YA 363

Mchana wa siku hiyo Erica aliamua kumshirikisha mama yake ambayo aliongea na Rehema alipokutana nae,
“Mama nilikutana na Da Rehema kasema Da Bite kakonda sana hadi amemuonea huruma”
“Jamani watoto wangu sijui mna matatizo gani jamani, hivi Bite anaacha kuja nyumbani hapa kunieleza shida zake mpaka anaonekana na watu huko kuwa ana matatizo jamani!”
“Yani Da Rehema kaniambia siku akipata muda atakuja ili muongee vizuri maana hali ya Da Bite imemshtua sana”
Kwakweli mamake hakuweza kuvumilia zaidi akaamua kumpigia simu Bite ili kujua tatizo ni nini, akampigia na kumsalimia kisha kumuuliza,
“Mnaendeleaje Bite?”
“Salama mama, tunaendelea vizuri”
“Kila siku nikikupigia simu ni swala hilo hilo la kuendelea vizuri, hivi Bite mwanangu una matatizo gani? Hutaki kuja nyumbani, ndio ulichukia ujinga aliofanya mumeo? Huyo mumeo tunajua mambo yake kwahiyo hata habari zake zisikuogopeshe kuja nyumbani, kwanza niambie tatizo ni nini, usinifiche mimi ni mama yako”
“Mama, ni bora hata ningekuwa mwanamke malaya yani ni bora ningekuwa hivyo kuliko ninachofanyiwa na huyu mwanaume jamani, mama huyu mwanaume ananitesa tena sio kwa kipigo ila ananitesa kisaikolojia, mama hadi nachanganyikiwa”
“Vipi ni kuhangaika na wanawake tena au?”
“Ndio hiyo tabia hajaacha wala nini mama, halafu kinachoniumiza zaidi nimeanza kuumwa na ugonjwa wa ajabu”
“Ugonjwa gani huo?”
“Nimeenda kupima, wameniambia nina ugonjwa wa kansa ya shingo ya kizazi, mama ugonjwa huu husababushwa na ngono yani mwanaume anautoa kwa mwanamke mwingine na kuuleta kwa mwanamke wake, yeye hadhuriki ila mwanamke ndio nadhurika, jamani huyu James kwanini anataka kuniua jamani kosa langu nini”
“Bite, akili zako zifanye kazi, kwani ugonjwa huo hautibiki? Utapona tu mwanangu, ila rudi nyumbani, kwanza una uwezo wa kuishi maisha yako mwenyewe cha msingi kuwa na msimamo tu kuwa umeondoka na haurudi tena, asikubabaishe James bhana, mtu alitaka hadi kumbaka mdogo wako, ni mtu huyo kweli? Kwakweli mwanangu ni muda wa kufanya mabadiliko huu, usikubali kuumizwa kiasi hiko”
“Sawa mama nimekuelewa”
Basi pale mama Erica aliongea ongea na mwanae maneno ya kumpa moyo kwa kile alichomwambia kuwa asijihisi vibaya, awe kawaida tu na achukulie ni ugonjwa wa kawaida usimpe presha sana.

Salma alimpigia simu Nasma na kuongea nae,
“Nimepata majina matatu ya Yule mtu”
“Eeeeh nitajie”
“Nakutumia kwenye ujumbe, unajua nimetumia ujanja gani kuipata?”
“Eeeeh niambie umetumia ujanja gani?”
“Basi bhana Yule shemeji yangu nikaongea nae kuhusu majina akaniuliza kwani vipi, sikutaka kumwambia ukweli ila akasisitiza nimwambie ikabidi nimwambie kumbe nae ana ugomvi na huyo mwanamke tena kaniambia ndio vizuri tena umfanye chizi kabisa aokote makopo yani asijitambue”
“Sawa sawa, yani mimi ninapoipeleka kazi wala sio sehemu ya kugushi ndani ya wiki hii hii utasikia matokeo”
Mara Bahati akatokea na kumkuta mkewe akiongea na ile simu akamuuliza kwa makini kuwa anaongelea kuhusu nini,
“Hamna kitu mme wangu”
“Unajua nyie wanawake mkipigwa mnasema mmeonewa, hivi mwanamke umempata mwanaume kwa ushirikina hivi unawezaje kujisifia kuwa huyu mwanaume ni wangu? Kwanini unashangaa nikimtaka nimpendaye? Halafu simu unayoongea nayo hapo ni ushirikina mtupu, unajua najuta kukuoa Nasma, yani hata kama ndugu hawakumtaka Erica basi wangenizesha hata kwa Sakina Yule dada katulia ila sio wewe, yani hapo ulipo unanuka ushirikina tu”
“Hamna mume wangu sifanyi ushirikina wowote”
“Yani Nasma nikigundua kuna ujinga wowote unafanya utaondoka huku unatambaa nakwambia, na kwa taarifa yako hata Erica agome kuolewa na mimi basi wewe nitakuolea hata wake sita maana siwezi kuishi na mwanamke mshirikina kama wewe”
Nasma alikaa kimya tu ila bado wazo lake la kumfanya Erica kuwa kichaa lilikuwa kichwani ingawa mumewe kamtishia kwahiyo wazo hilo lilikuwa likimjia na kumtoka.

Wakati Erica anajiandaa huku akingoja simu ya Dora kuwa wakutane wapi, akapigiwa simu na Erick, kwa muda huu hakuweza kujizuia kutokuipokea kwani alikuwa akiacha kuipokea anaumia moyo sana, akaanza kuongea nae, Erick alimuomba waongee kwahiyo Erica alimwambia sehemu anayoenda kukutana na rafiki yake,
“Huyo rafiki yako ni muhimu sana hadi unakutana nae?”
“Ndio ni wa muhimu sana, ni rafiki yangu mkubwa”
“Sawa, na mimi sipo maeneo ya mbali na sehemu hiyo, ukifika basi utanikuta”
“Sawa, hakuna tatizo”
Erica alimaliza kujiandaa kisha akamuaga mama yake na kuondoka zake, alifika kwenye ile hoteli na kumkuta rafiki yake Dora ameshafika kwahiyo walikaa nae na kuanza kuongea nae,
“Erica, kabla ya yote jamani nimekutana na mkaka mmoja hapo nje huwa namfahamu fahamu jamani ila sina mazoea nae, Yule kaka ni mzuri, sijategemea leo kumuona, mkaka ni mzuri Yule nilitamani hata nikambusu ila sijamzoea halafu hanipendagi”
“Dora nawe, hakupendagi kwani anakufahamu?”
“Ananifahamu ndio na ndiomana siwezi kuwa nae karibu ila nampenda balaa, natamani angekuwa wangu, mkaka Yule ni mzuri”
“Mmmh Dora tuachane na habari hizo, hebu tuongee ya kwetu bhana”
Muda kidogo Erica akapigiwa simu na mpigaji alikuwa Erick, ilibidi Erica amuelekeze walipokaa ili aende hapo. Basi akakata simu na kuendelea kuongea na Dora,
“Sasa Erica, ninachotaka kuongea nawe ni kuhusu shemeji yako James”
“Kafanyaje tena shemeji yangu James?”
Gafla akamwambia Erica ageuke nyuma,
“Wow, Erica geuka nyuma Yule mkaka mzuri nilikwambia anakuja kwenye meza yetu sijui ananifata!”
Erica akageuka na kumuona anayekuja ni Erick, kwakweli alimuona rafiki yake Dora anatamaa sana, Erick alifika pale ila kabla ya salamu alimuuliza Erica kwa mshangao huku akimuonyeshea Dora,
“Yani Erica, huyu ndio rafiki yako!”
 
SEHEMU YA 364

Gafla akamwambia Erica ageuke nyuma,
“Wow, Erica geuka nyuma Yule mkaka mzuri nilikwambia anakuja kwenye meza yetu sijui ananifata!”
Erica akageuka na kumuona anayekuja ni Erick, kwakweli alimuona rafiki yake Dora anatamaa sana, Erick alifika pale ila kabla ya salamu alimuuliza Erica kwa mshangao huku akimuonyeshea Dora,
“Yani Erica, huyu ndio rafiki yako!”
Erica alikuwa kimya tu kwani hakuelewa toka mwanzo kuwa mwanaume aliyekuwa anasemwa na Dora ni Erick, ila pale pale kabla hajajibu Dora akasema,
“Kheee Erica huyu kaka mzuri kumbe ndio mpnzi wako!”
Erick alimuangalia Erica bila hata kucheka na kumtaka waondoke, sasa Erica hakuwa na maamuzi zaidi ya kufata kile anachokisema Erick kwahiyo ilibidi ainuke na kuanza kufatana na erick, kwakweli Dora alimshangaa Erica na kumwambia,
“Kwahiyo ile hela hutaki tena?”
Kiukweli hela alikuwa anataka lakini wakati huo huo hakutaka kumkera Erick, alitoka nae hadi nje na kupanda gari ya Erick ambapo kwenye gari Erick alianza kuongea,
“Unajua Erica muda mwingine mwanaume anampiga mwanamke sio kwasababu huyo mwanaume anapenda kupiga, hapana ila ni sababu ya vitendo vya huyo mwanamke. Hivi Erica Yule ndio rafiki yako kweli?”
“Ngoja nikueleze ukweli kuhusu Yule mtu”
“Haya nieleze”
Erica alimueleza Erick jinsi alivyokuwa na urafiki na Dora wakati yupo chuo ila akamueleza jinsi alivyoacha urafiki nae, alimwambia ni sababu ya kumsingizia maneno ya uongo ila hakusema tatizo kubwa kuwa lilikuwa ni George, alimueleza na jinsi kaka yake alivyotaka kumuoa na yeye alivyokataa,
“Erick naelewa kabisa kama Dora hana tabia nzuri ila nipo nae karibu kipindi hiki si sababu ni rafiki yangu bali kuna rafiki yangu mwingine alinituma kuchukua hela kwa Dora”
“Na mbona uliniambia mimi ni rafiki yako?”
“Nimekosea kusema hilo sababu sikujua niseme kitu gani ila Erick najua umetafuta sababu tu, hivi unadhani ulichofanya kwangu siku ile ni sawa? Kuniacha mimi bila kulipa hoteli? Kuniacha nioshe vyombo? Unafikiri ni sawa, wewe mwenyewe ulisema kuwa tusahau yote yaliyopita, nilikwambia ukweli kuwa nina mtoto ukakubali, na sasa nikakwambia baba wa huyo mtoto halafu unathubutu kuniacha hotelini kweli?”
“Erica, nilikuwa na hasira sana kumbuka nakupenda”
“Hata kama unanipenda ndio kunifanyia vile kweli?”
“Erica, niliumia sana umeacha kunipa mimi mapenzi umeenda kumpa Rahim kweli? Nimerudi na kukwambia kuwa mpenzi wangu nina hamu ila ukanipa kisingizio kuwa upo kwenye siku zako, na Rahim umeenda kumpa”
“Erick, sijawahi kutembea na mwanaume yeyote toka nijifungue, mimi sio kichaa wa kusema nibadili mwanaume huyu mara huyu, nina akili zangu timamu mimi. Nilisema yaliyopita ilikuwa zama za ujinga, nilihisi ndio njia ya kupanda penzi la kweli, sasa nimejua ukweli nianza tena kutembea na wanaume jamani! Huyo Rahim ni muongo”
“Basi kama muongo naomba unipatie haki yangu”
“Haki gani?”
“Unajifanya huelewi Erica jamani? Si nilikwambia nina hamu, nahitaji mapenzi”
“Hapana Erick, mimi nilikuwa nataka tufanye hadi ndoa”
“Hahaha usinichekeshe Erica, hivi siku hizi ni nani anayengoja ndoa? Hamu ipo muda wote kweli mtu utasubiria ndoa? Siku hizi hata mwanamke bikra anajaribishwa kabla ya ndoa sembuse wewe Erica ambaye ushazaa jamani! Hata hivyo kwani mimi na wewe ni mara ya kwanza kufanya? Hebu usinifanyie hivyo mwenzio, naomba haki yangu Erica tafadhali, mimi ni mpenzi wako niende wapi tena?”
“Sawa hakuna tatizo, ila naomba jambo moja”
“Hayo ndio maneno sasa, haya jambo gani?”
“Naomba tukapime”
“Kwahiyo Erica huniamini? Yani kipindi chote hiko huniamini?”
“Usipaniki Erick maisha yamebadilika sana, nasema tukapike sababu ya kukuokoa wewe na kujiokoa na mimi, kumbuka…..”
“Basi usiendelee kusema, tumalize mjadala, kesho nakuja kukuchukua tukapime”
“Basi fanya kesho kutwa maana kesho haitawezekana”
Erica alikumbuka ahadi aliyotoa kwa Fetty kwahiyo alitaka aitumie siku ya kesho kutimiza ahadi yake kwa Fetty, ila Erick akamuuliza
“Kwanini haiwezekani?”
Erica akawa anajiuma uma kisha Erick akaongea,
“Ooooh nimekumbuka kitu, ngoja kesho nikafatilie tena ile gari bandarini unajua Erica ulinichanganya sana siku ile, basi kesho nitaenda kufatilia mwenyewe halafu keshokutwa twende tukapime”
“Sawa hakuna tatizo”
“Halafu tukitoka hapo tunaenda kufanya”
“Mmmmh!”
“Usigune, ujue mimi na mwanaume na wewe ni mwanamke tumetofautiana maumbile, ukinibania mimi unataka niende wapi?”
Erica alikaa kimya tu na kumuomba kuwa anataka kurudi nyumbani, wakati huo hata ile laki tatu kwa Dora hajaipata na hajaweza kusikiliza kuwa ni nini Dora alimuitia kuhusu shemeji yake, na pia aliogopa kumuomba Erick hiyo hela maana alikuwa anataka Erick ampe mwenyewe na sio amuombe, kwahiyo Erick akageuza gari na kuanza safari ya kwenda kwakina Erica huku akimpapasa papasa,
“Mmmh Erick usifanye hivyo bhana, tupo barabarani ujue”
“Hata barabara inaelewa ni jinsi gani nakupenda”
Erica hakupenda kushikwa vile maana alikuwa akipatab msisimko na hakuutaka huo msisimko sababu alihisi ungechochea kufanya mapenzi kitu ambacho hakukitaka kwa wakati huo.

Walifika nyumbani kwakina Erica, na kabla Erica hajashuka Erick aliomba kuongea nae tena kidogo,
“Usijifikirie vibaya mimi kushangaa urafiki wako na Yule msichana, Yule msichana labda hanifahamu vizuri ila mimi namfahamu vizuri sana sana, Yule msichana hana tofauti na changudoa kwa kifupi Yule msichana hafai, yani anawafata wanaume kwaajili ya pesa, ile sio aina ya kuwa na urafiki nao Erica, wewe ni msichana unayejielewa, unayejithamini, unayevutia usianze kuzunguka nay ale makorokoro, sawa mama eeeh!”
“Sawa nimekuelewa”
“Halafu kitu kingine nakupenda sana, siwezi kuingia ndani kwenu maana kama umemwambia mama yako sijui nitaweka wapi sura yangu, ila keshokutwa nikija kukuchukua lazima nije nionane na mama”
“Sawa hakuna tatizo”
Kisha Erick akashuka na kumfungulia Erica mlango wa gari akambusu na kumuaga, halafu Erica akaingia ndani kwao ila akiwa na mawazo sana kuwa hiyo laki tatu aliyomuahidi Fetty atampaje mpaje, akaingia ndani tu na kumsalimia mama yake kisha kwenda chumbani kwake, alijisemea,
“Sisi wasichana kitu kinachotusumbua sana ni hela, unakuwa na mpenzi kama Erick unajua kabisa hela anayo ila hakupi na ukiomba atauliza ya kazi gani yani hapo ndio panakuwa pagumu! Nilianguka kwa Rahim sababu alikuwa mtoaji sana kwangu, alikuwa akinihonga sana ila sikujua kisa na mkasa cha kuhongwa vile na mwisho wa siku nimeambulia maumivu, hivi kweli Erick anaweza kutoa milioni tano kwaajili ya mimi kulipa deni anauwezo wa kutoa pesa kwaajili ya kuninunulia gari, anashindwaje kutoa pesa kwaajili ya matumizi yangu?”
Erica alijiuliza sana ila alipotulia tulia aliamua kumpigia simu Dora ili kujaribu kuongea nae kuhusu ile hela aliyomuomba,
“Yani Erica ukaacha kunisikiliza mimi sababu ya Yule, hajakupa hela?”
“Hajanipa?”
“Halafu mjinga ana hela kweli Yule sema bahiri tu ndio tatizo lake”
“Unajua sana eeeh!”
“Namfahamu ndio ila Erica hongera, umepata mwanaume mzuri balaa hadi natamani kama angekuwa wangu”
“Basi tuachane na hayo mambo, vipi kuhusu hela?”
“Erica, nilitaka kukupa hela ya kuonana kabisa ila hela ya kutuma hapana, labda nikutumie laki”
“Mmmmh Dora wewe”
“Ndio, kubali tu nikutumie laki”
“Sawa basi nitumie hata hiyo”
“Halafu unajua jana ulivyoniacha pale nini kilitokea?”
“Aaah Dora, usiniletee habari zingine bhana, nitumie hiyo laki”
“Basi ngoja nikutumie”
Erica alikata simu akisubiri kutumiwa hiyo laki maana hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali hiyo hiyo huku akiwaza mahali pa kumtafutia Fetty laki mbili maana katika marafiki zake alimuona Fetty kuwa rafiki mwema kwake ingawa kuna vichache anampeleka sipo ila kwa kiasi Fulani aliona kuwa ni mwema na anakila sababu ya kumsaidia.
Alivyomaliza kuongea na Dora alipigiwa simu na Erick na kuongea nae tena Erica hakuongea nae kwa raha kwani alikuwa na shida na hela halafu kumwambia hakuweza,
“Erica nakupenda sana”
“Nashukuru kwa kunipenda ila Erick sina kazi ujue?”
“Najua mpenzi wangu, nilikwambia hilo hata lisikupe shida nitakutafutia cha kufanya yani kuwa na amani tu”
Erica alikuwa akichukia kwani alitamani aulizwe hela unayo aseme sina ili aweze kupewa hela anayoitaka, hakutaka kutoa hela za kwenye akaunti ya mwanae kwani hakutaka kuendelea kuimaliza akaunti hiyo ukizingatia hela nyingi anazozitumia ni kutoka kwa mwanae, kwahiyo aliendelea tu kuongea na Erick haku akicheka ila hakuwa na furaha wala nini, hadi wanaagana na kulala bado hakuwa na furaha sababu Erick hakuweza kujiongeza kumpatia hitaji lake.
Kulipokucha bado alikuwa akiwaza kuwa hiyo hela ataipata wapi aweze kumsaidia Fetty, akapata tena wazo la kumpigia Bahati, kwahiyo akampigia Bahati na kuanza kuongea nae,
“Nina shida na hela mwenzio”
“Unataka kama pesa ngapi?”
“Nina shida na laki mbili”
“Mmmmh kwani Erica una tatizo gani mpenzi wangu? Ila usijali, ngoja niende nikaangalie mahali nikutumie”
“Sawa, nashukuru sana Bahati”
Kwakweli kwa Bahati ilikuwa ni afadhali yake kwani Bahati ingawa hakuwa na hela nyingi lakini alikuwa hodari sana wa kumsikiliza Erica ana mahitaji gani, na kwa upande wa Erica ilikuwa rahisi sana kwake kumuomba hela Bahati kuliko mtu mwingine yoyote, alishukuru sababu alijua ni lazima Bahati angemtumia kama alivyoahidi.
 
SEHEMU YA 365

Nyumbani kwa Bahati, mkewe alimuona vizuri Bahati akiongea na Erica ile asubuhi kuhusu maswala ya hela, kiukweli hakupendezewa na swala lile hata kidogo na chuki kwake dhidi ya Erica ikaongezeka, basi Bahati alivyotoka tu yeye naye akamuandaa mtoto na kutoka naye bila kujali kuwa bado ni mdogo sana, kwa muda huo aliona ni vyema afanikishe mambo ya ndoa yake kwanza.
Alifika kwa babake ili aongee nae, babake alisikitika sana kuona mwanae akitembea mwenyewe na kichanga, Nasma aliamua kumueleza babake kila kitu na jinsi Bahati alivyobadilika asivyotaka ndugu yeyote kufika nyumbani kwake,
“Pole mwanangu”
“Baba, mmeniozesha kwa mtu mwenye tabia za ajabu sana, kwakweli nateseka baba yangu”
“Pole sana mwanangu, lakini kwanini anafanya hivyo?”
“Sina raha na ndoa yangu baba, yani kila muda ni Erica tu, tukilala tukiamka ni Erica jamani hakuna hata amani baba, sasa leo asubuhi kaongea tena na erica, jamani Bahati ameondoka pale nyumbani haihai ndio sijui anaenda kumtafutia hela huyo Erica, baba natamani tufanye kitu juu ya Erica ili kukomesha tabia ya wanawake kama wale wanaopenda kutembea na waume za watu”
“Kwahiyo tufanyeje mwanangu?”
“Nataka Erica awe kichaa baba yangu, yani awe chizi kabisa”
“Unayajua majina yake matatu ndio”
“Ndio, kuna mtu kanitumia”
“Basi hiyo kazi rahisi”
“Yani sina raha baba yangu kila kitu nikishika ndani nambiwa hiko cha Erica, nyumba eti ya Erica, kitanda sijui jiko, makochi, tv vyote naambiwa vya Erica, sina raha baba”
“Usijali mwanangu, kazi rahisi sana hapa, huyo Erica atajuta kufahamu ukoo wetu. Kesho nitafanyia kazi hili swala hata usiwe na mashaka mwanangu Nasma”
“Sawa, baba ngoja nirudi nyumbani kwangu”
“Aaaah usirudi, yani naanza nay eye, atakuja kukuchukua mwenyewe hapa na safari hii utaenda na dadako kumuhudumia mtoto na Yule mumeo tutamkoroga zaidi ya pale, yani wakati Erica anaugua uchizi na yeye hata hajui kama kuna kiumbe anaitwa Erica katika hii dunia. Yani safari hii nitamfanyia dawa hivyo hatoisahau, maishani mwake maana akija kushtuka anakuta Erica alishakufa kwa uchizi huko”
“Sawa baba nashukuru”
Kwahiyo Nasma akasikiliza ushauri wa babake kuwa asiende popote maana Bahati atamfata mwenyewe pale kwao.

Erica alitumiwa ile hela na Bahati kwahiyo alishukuru sana kisha akamtumia rafiki yake Fetty ambapo Fetty nae alimshukuru sana maana amemuonyesha upendo,
“Erica nakushukuru sana kwa kuthamini shida yangu”
“Usijali tupo pamoja”
“Yani sijui niseme nini, nashukuru sana. Nitakuja kwenu wiki ijayo”
“Karibua”
Kisha akakata ile simu na sasa akapata amani na kwenda kuongea na mama yake, mama yake alianza kumsimulia kuhusu ugonjwa anaoumwa mwanae Bite,
“Yani hawa wanaume jamani hata sijui wako vipi? Kashampa mwanangu hilo gonjwa, ila nimemwambia Bite asiwe na wasiwasi atapona tu”
Wakati akiongea vile na mama yake, alifika Mage na kuwasalimia ila mama yake alimwambia,
“Mtoto mbaya wewe, ulivyojua umefanya makosa ya kumpeleka mdogo wako kwenye matambiko huko ukaona bora usije”
“Hapana mama, ila mambo yaliingiliana”
“Mambo yaliingiliana wapi? Unashindwa kweli kuja kumsalimia mama yako sababu ya mambo kuingiliana?”
“Nisamehe mama, ila hiko sio kilichonileta”
“Haya, kimekuleta kipi?”
“Jana, kulikuwa na sherehe ya rafiki yangu, kwahiyo nilienda kwenye sherehe na mume wangu, huwezi amini mama wakati tunarudi usiku kwa macho yangu haya nimemuona shemeji James akiwa na Dora Yule rafiki wa erica, wakitoka guest”
Mama Erica alishangaa sana, na kuuliza kwa mshangao
“Unasema!”
“Ndio hivyo mama, kwakweli tumeshangaa yani mume wangu alikuwa anasema kila siku Erica mbaya kumuumbua James ila kwa alichokiona jana alisema amakweli James ni mchafu, tena mama bora ingekuwa wanatoka tu ukasema hakuna kilichofanyika ila tuliwaona wakitoka na kusimama nje huku wakinyonyana midomo”
Kwakweli mama erica, alijikuta akiishiwa na la kusema kabisa,
“Mungu wangu wanafanya uchafu huo nje!”
“Ndio hivyo mama”
Erica alikuwa amekaa kimya kwa muda ila yale maneno yalimuumiza vilivyo maana Dora alishamwambia kuwa ameathirika, alijikuta akisikitika sana na kuwaambia,
“Jamani Dora aliwahi kuniambia kuwa ameathirika”
Ndio mama yao alipiga nay owe kabisa,
“Uwiiii James kaniulia mwanangu mimi jamani, hata sijui nifanyeje”
Mage aliamua kumtuliza mama yao maana ilionekana ameshachanganyikiwa,
“Mama usipaniki hivyo na wala usiongee na Bite kwa kupaniki hivyo, muite Bite uongee nae taratibu na atakuelewa,
“Jamani hivi nawezaje, huyu James huyu nimfanye nini? Kwanini anifanyie vitu vya ajabu hivi kwa mwanangu, kampa ugonjwa wa kansa ya shingo ya kizazi kaona hautoshi kampelekea na ukimwi kweli? Hapana jamani”
“Mama, usipaniki naomba keshokutwa nije na Bite najua haendi kazini, nitamfata tuje hapa nyumbani na uongee nae kirafiki tu”
“Je naweza kuvumilia hadi kesho kutwa?”
“Vumilia mama, nakuomba vumilia na jipe moyo yote yanawezekana”
Mage alijaribu pale kumpa moyo mama yake hadi akakubali maana hakuweza kuvumilia yale maneno kuwa James alikuwa na Dora.

Babuu alionekana yupo na Rahim akimshauri kuhusu mtoto aliyezaa na Erica,
“Najua Rahim ndani kwenu wanaogopa kukwambia ila hakuna kitu kibaya kama kutokuhudumia damu yako, mimi mwenyewe nilitamani sana kuzaa na Erica ila sababu hakuchagua kuzaa na mimi simlaumu kwani sijui ni kwanini aliamua kuzaa na wewe, basi wewe onyesha kumjali mtoto”
“Ila Babuu hujui tu, Yule mwanamke ana dharau sana, nishampa hela nyingi mno angekuwa ni mwanamke mwingine ningemkuta na biashara kubwa sana kwasasa, na alichonikera ni swala la kukazania ndoa na mimi wakati huku kwetu nishawekewa mke, yani Erica ni msichana mzuri kimtazamo ila ana matatizo sana, hujui tu Babuu”
“Sasa mimi namjua Erica kushinda wewe unavyomjua, mimi ndio nilikuwa mwanaume wake wa kwanza”
Rahim hakupenda kusikia vile, yani Babuu alipenda kujisifia kuwa mwanaume wa kwanza kwa Erica ila kila aliyemwambia alionekana kutokupenda kabisa swala lile ingawa aliendelea kuongea,
“Mimi ndio nimemfundisha erica mapenzi”
“Hebu na wewe nyamaza huko kama huna cha kuongea, muda mwingi nilikuwa nikiwaza kuibiwa Erica ndiomana sijawahi kupata wazo la kumuoa kabisa, tatizo ukioa mwanamke mzuri sana jua umeolea wenzio”
“Hapana sio hivyo, ila Erica hukumuelewa tu”
“Nimekwambia nyamaza kama huna cha kuongea”
Mdogo wake Salma alikuwa karibu na kuwasikia wakimuongelea Erica, kwahiyo alienda kumwambia dada yake, kitu kilichomkasirisha zaidi.
“Natamani hata huo uchizi Erica umpate hata muda huu, yani baada ya kukaa kuzungumzia mada za maana wanakaa wakimzungumzia Erica, msichana aliyewatia aibu kwa kutembea na ukoo mzima, namchukia Erica”
Yani Salma alikuwa na chuki za wazi wazi kabisa dhudi ya Erica.
 
SEHEMU YA 366

Erica alirudi ndani na kumpigia simu Dora maana zile habari kuwa alikuwa na shemeji yake zilimtisha kidogo, alimpigia na Dora alipokea muda ule ule,
“Dora nasikia ulikuwa na shemeji James?”
“Umejuaje?”
“Kuna mtu kawaona Dora, kumbe umeanza na shemeji yangu”
“Sikia Erica, Yule shemeji yako alivyonibaka niliumia sana moyo, yani mimi katika kuhangaika kwangu kote sikuwahi kufanya kinyume na maumbile ila Yule shemeji yako kajitia kunibaka mbele na nyuma nab ado mahakamani akashinda kesi kuwa si yeye aliyenifanyia vibaya ingawa ushahidi wote ulikuwepo. Tena jana nilitaka nikupe habari za shemeji yako sema ndio hivyo ukaondoka, Erica nilikwambia mimi Yule James akiingia kwenye kumi na nane zangu ninae maana nimedhalilika sababu yake, na kweli kaingia kwenye kumi na nane zangu na atajuta”
“Jamani Dora, si umeathirika wewe?”
“Kuathirika kitu gani? Tena ndio vizuri na yeye aupate kwa umalaya wake, wengine tumeupata sababu ya tamaa ila sio umalaya, na yeye aupate sababu ya umalaya wake, kwahiyo kwasasa tupo kwenye mahusiano na shemeji yako”
“Kheee Dora”
“Tena sikukwambia, ana mpango wa kunipangishia na nyumba kabisa ili tuishi kama mke na mume. Na zile hela za mzee Jimmy ulizonipa ni kama nikapata kismati maana nilimuendea shemeji yako kwa mtaalamu, nimemkoroga haswaaa yani kwangu hasikii wala haoni”
“Kheee Dora, sasa madawa yako kwa waganga shemeji yangu yalimpataje”
“Ukiwa na pesa katika maisha ndio kila kitu duniani, kuna dawa hiyo nilipewa, nimuwekee kwenye tunda nikawaza ni njia gani nitatumia, nikanunua sindano nikaiweka dawa maji nikaiingiza kwenye sindano na kuichoma, kwenye tunda la apple, shemeji yako si malaya, nikamchombeza siku hiyo hadi akakubali kwenda na mimi kula ndipo nikampa tunda lile akala yani ikawa kwisha habari yake, baada ya hapo nilimualika kwetu akaja nikamuwekea dawa hiyo funga kazi ambayo lazima niitumie kunawa kwanzq sehemu za siri ndio nimuwekee kwenye chakula, nikafanya hivyo basi toka hapo Yule shemeji yako kama zuzu unajua hiyo dawa nimemfanyia jana asubuhi ndio nikashangaa usiku ule kanitafuta hawezi kulala bila kuniona, nimemkomesha shemeji yako”
“Jamani Dora, ndio umemlisha shemeji yangu uchafu”
“Ndio akome, yani mambo yote haya ni ndani ya siku tatu tu, asante Erica kwa kunipatia hela za Mzee Jimmy maana nimeweza kulipa kisasi changu”
Kwakweli Erica hakuwa na la kuongea zaidi ya kumuhurumia dada yake tu kwani shemeji yake kaponzwa na umalaya wake kwa maana hiyo asingekuwa malaya basi Dora asingempata tena.

Jioni yake Erica alipigiwa simu na Erick huku akimsisitiza kuhusu siku ya kesho,
“Erica, kumbuka kesho ni siku yetu nitakuja kukufata mama yangu”
Erica hakuweza kukataa maana ameshamzungusha Erick kwa muda mrefu sana na akaona kuzidi kumzungusha ndio kupelekea zaidi mapenzi yao kuwa pabaya, alikubaliana nae na muda wa kwenda kumchukua kisha wakaagana.
Usiku wakati wa kulala, leo Erica alipigiwa simu na Yule mwanamaombi, alipokea na kumsalimia kisha kuanza kuongea nae,
“Erica, toka jana nilikuwa najiwa na ndoto na maono kuhusu wewe, Erica kwa swala lililopo mbele yako inatakiwa kufunga na kuomba”
“Kufunga na kuomba?”
“Ndio kufunga na kuomba, tena mfungo huo itabidi tuufanye kwa siku saba yani kula jioni tu, Erica mimi nitafunga huku ila nawe ufunge huko na muda wa maombi tufanye wote ila itakuwa vyema zaidi kama ukija kanisani kwetu”
“Sawa nimekuelewa, kwahiyo inabidi kuanza lini?”
“Ni kesho Erica, haya maombi si ya mchezo, yanataka haraka, kesho tuanze mfungo na maombi”
“Mmmh!”
“Mbona unaguna Erica, hujawahi kufunga?”
“Hapana, nimewahi ila ni gafla mno”
“Maombi mengine ni ya gafla na yanatakiwa kufanyiwa kazi muda huo huo, unapofunga epuka zile dhambi ambazo unahisi zitakutenga na uwepo wa Mungu kama uzinzi na uasherati”
“Mmmh!”
“Mbona unaguna Erica?”
“Hapana, nimeguna tu na nimekuelewa”
“Basi naomba kesho tuanze hilo jukumu mimi na wewe la kufunga na kuomba, sijui nini kipo mbele yako ila naambiwa moyoni tufanye hivyo”
“Sawa, nimekuelewa”
Kwakweli Erica alijuta kutoa namba yake kwa huyu mwanamaombi maana hakuelewa hata kesho yake kuwa atamwambia kitu gani Erick amuelewe, ila moyo mwingine ukamshauri kuwa ni bora aanze huo mfungo kesho kutwa maana kesho alikuwa na ahadi yake, ila akajisemea atajaribu kuongea na Erick kama atamuelewa. Akaamua kulala tu muda huo.

Kulivyokucha akafanya kazi zake kama kawaida, na Erick alimpigia simu kuwa ajiandae na alijiandaa kabisa, kwenye mchana Erick alifika pale kwao na kumkuta mama Erica, kwakweli mama Erica alimfokea sana kwa kitendo alichomfanyia mwanae ila Erick alimuomba msamaha mama Erica kisha akamuuliza,
“Mama, vipi ile biashara yako inaendaje?”
“Aaah wamekopa zote nimemaliza, saivi nakusanya madeni tu”
“Basi ngoja nikuongezee hizi mama”
Erick alimpa mama Erica milioni tano nyingine, kwakweli mama Erica alifurahi sana na kusahau kama huyu kijana ndiye aliyemuacha mwanae kwenye mataa, na muda huo Erick aliomba kutoka na Erica ambapo mamake alimruhusu bila tatizo lolote, tena alimuita viuri kabisa,
“Erica mama fanya upesi mwenzio anakungoja”
“Sawa mama”
Erica alitoka kisha yeye na Erick wakaondoka na safari ilikuwa ni moja kwa moja hospitali kupima, majibu yakatoka na kukutwa wote ni wazima kitu kilichomfurahisha sana Erick, na kuondoka tena na kwenda na Erica moja kwa moja hotelini, Erica alijaribu kukataa ila Erick alimuonyesha sura ya huruma sana ikabidi akubali na kwenda nae chumbani, kisha akajaribu kuongea nae tena,
“Ila Erick, mimi leo nimefunga si vizuri kufanya zinaa”
“Hebu Erica acha zako, Watu kibao wanafunga na kufanya wanafanya, hakuna tatizo lolote kwenye kufanya”
“Erick zinaa ni dhambi”
“Erica, ushatenda dhambi ngapi katika maisha yako sembuse zinaa? Je kutoa mimba si dhambi? Yani kutoa mimba ni sawa na kuua ila zinaa peke yake ndio unaona dhambi”
“Hayo yalipita Erick, sasa nataka kuwa mpya. Subiri unioe tutafanya”
“Mambo gani hayo Erica? Kumbuka mimi ni mwanaume, unataka hamu zangu nimalizie wapi? Kwanini unanifanyia hivi lakini? Hunipendi tena eeeh!”
“Nakupenda sana sana ila ningeomba unisubiri”
“Hapana Erica, kila siku unanipa visingizio visivyoeleweka, kama kupima tushapima na wote ni wazima, kwanini tusifanye? Kwanini unanikosea Erica?”
“Hapana Erick, sitaki kukukosea ila sitaki kufanya hiko kitendo”
“Ila Rahim ndio anafaa kufanya na wewe eeeh!”
“Hapana sio hivyo”
“Basi nipe mimi, unataka niende wapi Erica eeeeh!”
Erick alianza kumpapasa papasa Erica ili kumtia hamasa Erica, alijikuta tu akisema sitaki huku akikubali yote anayofanyiwa na Erick, kwakweli Erick alifurahi sana kuona Erica amekubali na walipomaliza aliinuka ili apige simu mapokezi wawaletee chakula ila alishangaa kuona Erica akiwa amelala tu vile vile hata kuinuka hakuna, akahisi labda anataka waendelee bila ya kula, akamuuliza,
“Erica, tuendelee”
Ila Erica alikuwa kimya, ikabidi amsogelee na kumbusu gafla akashangaa Erica akianza kutapatapa kama mtu mwenye kifafa.
 
SEHEMU YA 367

Erick alianza kumpapasa papasa Erica ili kumtia hamasa Erica, alijikuta tu akisema sitaki huku akikubali yote anayofanyiwa na Erick, kwakweli Erick alifurahi sana kuona Erica amekubali na walipomaliza aliinuka ili apige simu mapokezi wawaletee chakula ila alishangaa kuona Erica akiwa amelala tu vile vile hata kuinuka hakuna, akahisi labda anataka waendelee bila ya kula, akamuuliza,
“Erica, tuendelee”
Ila Erica alikuwa kimya, ikabidi amsogelee na kumbusu gafla akashangaa Erica akianza kutapatapa kama mtu mwenye kifafa.
Kwakweli Erick alichanganyikiwa maana si kitu alichokitarajia na wala hakuhisi kama Erica anaweza kuwa na ugonjwa wa aina hiyo, alijaribu kumshtua lakini Erica alikakamaa sana na kuwa kama mgonjwa wa degedege, akaona akiita watu kwaajili ya msaada wakati bado hajamvalisha Erica ni kumdhalilisha kwahiyo ikabidi amvalishe kwanza akiwa vile vile anatapatapa kisha akataka ambebe ili ampeleke hospitali huku akijiuliza hapo hotelini watamuonaje, alijihisi vibaya sana na ile siku ikawa mbaya kwake kupita siku zote. Mara kidogo simu ya Erica ikaita, Erick aliichukua na kuipokea huku akitetemeka na huku jasho likimtoka, mpigaji lilitokea jina la Fetty,
“Hallow Erica”
“Samahani, mimi ni mpenzi wa Erica ila nipo nae mahali kapatwa na matatizo”
Fetty akashtuka na kuuliza kwa mshangao,
“Matatizo gani?”
Erick alimueleza kwa kifupi ambavyo Erica alianza kutapatapa na kumwambia uamuzi wake wa kutaka kumpeleka hospitali,
“Unajua kuna hisia Fulani zimenijia kwenye kichwa change nikahisi kama Erica hayupo sawa ndiomana nikapiga simu muda huu, sasa naomba nikuombe kitu”
“Niambie”
“Naomba usimpeleke hospitali bora umrudishe kwao tu, Erica hana huo ugonjwa napatwa na hisia mbaya, naomba usimpeleke hospitali, mrudishe kwao na mimi mtanikuta nimefika dah! Jamani rafiki yangu”
Erick akawaza jinsi ya kutoka na Erica pale hotelini maana lazima watamshangaa, kwahiyo alimsubiri atulie na mwili wake ulegee kisha akamuona amefungua macho akiangalia tu akajaribu kumtikisa na kumuita ila Erica hakusema chochote ikabidi Erick ambebe kama mtoto mikononi kiasi kwamba waliowaona nje walihisi kuwa pengine ni aina ya mapenzi tu ndiomana wamebebana vile, na uzuri ni kwamba Erica alikuwa akiangalia tu ila hakusema chochote kile, basi alifika nae nje na kumuingiza ndani ya gari, akamkalisha vizuri na kumfunga mkanda kisha yeye akapanda na kuanza safari ya kwenda kwakina Erica huku akiwaza sana moyoni kuwa atasema nini akifika na Erica nyumbani kwao, aliwaza sana huku akiendesha gari na kuhisi kuchanganyikiwa kabisa.
Wakati anaendesha gari na mawazo akapigiwa simu na Rahim, muda huu Rahim alitaka kusema mengine kuhusu Erica ila Erick alimzuia,
“Rahim, tafadhali acha maneno yako Erica anaumwa”
“Nini tena?”
“Jua anaumwa tu, nini sijui”
Erick akakata ile simu maana alikuwa na mawazo kibao ya jinsi ya kumfikisha Erica nyumbani kwao.

Alifika nyumbani kwakina Erica huku kigiza giza kikianza kuingia maana kidogo alienda hoteli ya mbali sana na Erica, basi akamshusha na kumbeba kumuingiza ndani kwao huku akiwaza jinsi mama yake atakavyomuuliza kwa hamaki, ila alifika pale, akakuta mlango upo wazi akaingia ndani na kumkuta mama yake Erica amekaa chini na binti mmoja hivi, hakuelewa Yule binti ni nani maana hakumjua, alisogea moja kwa moja kwenye kochi na kumuweka Erica kwa kumlaza kisha akamsogelea mama yake Erica ili amuombe msamaha, ila kabla hajasema chochote mamake Erica alimzaba kibao Erick na kumwambia,
“Ndio ulichokuwa unakitaka, naona roho yako imefurahi sasa”
“Hapana mama”
“Hapana kitu gani na umeniletea mzoga nyumbani kwangu”
Mama Erica alimsogelea Erica na kumuita ila Erica alimuangalia tu mama yake bila kusema chochote ndio kumuumiza kabisa huyu mama, akamuangalia binti aliyekuwepo na kumuuliza,
“Fetty ndio unasema asipelekwe hospitali?”
Ndio hapo Erick akaelewa kuwa Yule ndio Fetty ambapo Fetty akajibu,
“Ndio mama asipelekwe, nina hisia mbaya kuwa Erica katupiwa jinni, kwahiyo mkimpeleka hospitali akichomwa sindano basi tunampoteza ndiomana nilimwambia hata huyu shemeji asimpeleke hospitali. Halafu mama huu si wakati wa kulaumiana ila ni wakati wa kujua tufanye kitu gani kunusuru maisha ya Erica.”
“Sikuelewi hata kidogo, mwanangu ana hali kama hii kweli nawezaje kukuelewa Fetty?”
Erick alikuwa kimya kabisa maana alihisi hata angechangia ni angezidisha hasira kwa mama yake Erica maradufu.
Mama Erica alimuangalia Erick na kumwambia,
“Yani wewe ndio chanzo ila huongei chochote maana nina uhakika kama mwanangu asingetoka na wewe yasingempata haya yaliyompata”
Wakati wanaongea ongea pale, simu ya Erica ilianza kuita na ilikuwa kwa Erick kwahiyo aliitoa na kumpa mama Erica aongee nayo, mamake aliichukua na kuangalia mpigaji akaona jina limeandikwa ‘Mwanamaombi’ Mama Erica akaipokea na kuanza kuongea nayo,
“Erica, sasa kuna maombi ya muongozo tutakayoenda nayo katika huu mfungo. Una peni na karatasi hapo nikwambie uyaandike!”
Mama Erica aliongea nae kwa sauti ya unyonge sana,
“Erica ni mgonjwa yani yupo akituangalia tu ila haongei chochote”
Yule mwanamaombia alishangaa sana kuwa imekuwaje tena kwa Erica kuwa vile, ikabidi aongee na mamake Erica jinsi walivyokubaliana na Erica kuwa afunge siku hiyo maana alikuwa anaona vitu sio vizuri kwa Erica, basi mamake Erica alisikitika sana vyenyewe hakushirikishwa na mwanae kuhusu hayo maombi, labda angemshirikisha basi angemuhimiza kufunga na asingemruhusu kutoka, ikabidi wakubaliane kuwa waendelee kumfanyia maombi Erica kisha Yule mwanamaombi akasema kuwa ataenda,
“Mama, najua unaamini kwamba Mungu anaweza”
“Ndio naamini”
“Basi mtoto wako usimpeleke kwa waganga kwani watamzidishia tu”
“Siwezi kwenda kwa mganga”
“Tukazane na maombi tu mama yangu, ningekuwepo mjini basi kesho ningekuja ila mpaka wiki ijayo, sema nitaendelea kuomba kwaajili ya Erica na atakuwa mzima kabisa kama mwanzoni. Pole sana mama yangu”
“Asante”
Basi ile simu ilikatika mamake Erica akawaeleza jinsi mwanamaombi huyo alivyowaambia, Erick alijilaumu kimoyo moyo maana aliona kosa ni lake kulazimisha kulala na Erica wakati alimwambia kuwa yupo kwenye mfungo, na bila kujua mwenzie kafunga sababu gani ila akamlazimisha kufanya ngono, yani alijilaumu sana, ila hakuweza kusema pale mbele ya mama yake Erica maana ingekuwa balaa zaidi, aliumia tu moyoni mwake kwa kutokumsikiliza Erica.
 
SEHEMU YA 368

Nasma aliitwa na baba yake kupewa taarifa ya kitu kilichofanyika,
“Mwanangu tumeshamtengeneza huyo Erica, ulisema kuwa tumfanye awe chizi na ndio lengo letu lilivyokuwa yani awe chizi akimbie hovyo, avue nguo barabarani, wa kumbaka wambake, aokote makoto na mwisho wa siku agongwe na gari na kufa maana kumshikilia chizi ni ngumu sana, ila imeenda kinyume”
“Imekuwaje baba?”
“Badala ya kuwa chizi kawa taahira kwahiyo mataahira si unajua wanavyokuwaga, yani wale mazezeta, yani Yule atakuwa akifanyiwa kila kitu na familia yake kwamaana hiyo hatoweza kutoka kwao maana ni taahira”
“Ila hata hivyo sio mbaya baba”
“Ila ingekuwa vizuri sana kama angekuwa chizi, yani anewehuka akili zake yani pangine mpaka kesho angekuwa ameshabakwa na vijana hata kumi, yani hata akija kupona anajiona hana thamani tena katika maisha”
“Kwahiyo atapona baba?”
“Kwa dawa tulizofanya mwanangu Yule haponi, yani haponi kabisa hata ndotoni Yule haponi ataugua hadi kufa”
“Sawa, na mume wangu kuja kunichukua”
“Usijali atakuja, yani tushamkorogea dawa ya kumuita kwahiyo atakuja na nitakupa dawa nyingine ya kumuwekea kwenye chakula yani hiyo ndio atakuwa hasikii wala haoni kwako, ngoja nikakuletee”
Basi Yule mzee alienda kumletea mwanae dawa na kumkabidhi, kisha akamwambia
“Kipindi kile hatukufanya dawa kali sana sababu ya ndugu zake, ila dawa ya sasa hivi ndio kiboko yani anakuwa ni kwako kabisa, ila tuliyomvuta ni kwamba hata wazo la kukufukuza tena wewe lisiwepo sasa hii ndio funga kazi yani mwanangu hii dawa Bahati anakuwa wako milele hata usijali”
“Asante sana baba”
Kisha akamkabidhi dawa ile na kumpa masharti ya kufanya na ile dawa,
“Sasa hii dawa mwanangu inaitwa funga kazi, yani usisahau masharti yake maana ukikosea kidogo tu unaweza kumfanya awe ndodndocha hata ashindwe kutafuta hela, sasa usikosee masharti ya hii dawa, unaichanganya na maji kisha unaenda kunawa sehemu za siri unakinga bakuli maji yamwagikie humo, halafu unampikia mumeo chakula na kumuwekea maji hayo kwenye chakula kisha unamkaribisha ale, akishakula tu hakikisha hii nyingine unaitemea mate na kuichanganya na maji ya kuoga, yani akimaliza kula atataka mwenyewe kuoga basi aende kuoga, baada ya hapo mwanangu hata ukikohoa atakuuliza unataka nini, na ndio mwanzo wa kutujengea gorofa wazazi wako maana mumeo ana hela huyu”
“Asante baba, ila nina shida nyingine, najua baba yangu unanipenda sana na utanisaidia”
“Sema mwanangu, usiogope”
“Yani baba, Bahati ni mgumu kufanya tendo la ndoa na mimi, mpaka nimlazimishe, toka akili zake zimerudi ndio kabisa anasema yeye anataka kufanya na Erica tu”
“Ngojea mwanangu”
Yule mzee akainuka na kurudi na dawa nyingine, akamkabidhi mwanae na kumwambia,
“Sasa hii unainyunyiza kitandani, yani akishakula, akioga atakwenda kujilaza ili dawa ifanye kazi, baada ya hapo mwanangu utaniambia, mumeo atakuwa kama jogoo. Ila sasa mwanangu usiwe unamnyima mumeo maana atakuwa na hamu kila mara, isingekuwa hizi dawa za mwanzo basi angetoka sana nje ya ndoa ila sababu ya hizi dawa za mwanzo atakuwa anavumilia tu humo humo na kulia kwahiyo uwe unampa”
“Hakuna shida baba, nashukuru sana”
Nasma alifurahi sana, na alifurahi zaidi wanavyoshirikiana na baba yake katika mambo mbali mbali, na kweli baada ya muda mfupi tu mara akamuona Bahati huyo amekuja kwao akiomba kuondoka na mke wake huku akitubu kweli kuwa hatomkosea tena mke wake, huyu mzee kama alivyopanga kuwa Nasma aondoke na ndugu yake mmoja ili akamsaidie kulea mtoto, akaona vyema kumuita mdogo wake Nasma ili aondoke nae,
“Basi mkeo ataondoka na huyu mdogo wake Siwema maana ndio kabakia mwenyewe nyumbani, hasomi huyu wala nini toka afeli darasa la saba mwaka juzi yupo nyumbani tu. Kwahiyo mtaondoka nae, ataenda kumsaidia dada yake kulea mtoto”
“Sawa baba hakuna tatizo”
Bahati aliitikia vizuri sana, na alikuwa mnyonge kupita maelezo ya kawaida, kisha akasubiri Nasma na mdogo wake Siwema wajiandae kisha wage vizuri na kuanza dafari ya kurudi nyumbani kwao.
Walifika na kukuta Bahati alishapika chakula kwahiyo walikula tu na kwenda kulala huku nasma akijipanga kuanza kufanya dawa zake siku ya kesho.

Muda ulipoenda ilibidi Fetty aage na kuondoka ila Erick hakujihisi kuondoka kabisa, alitamani siku hiyo alale hapo kwakina Erica maana ni yeye aliyesababisha mambo ya vile kwa Erica, ila mama Erica alimwambia aondoke tu maana alishawapigia simu wanae wengine wanakuja ila Erick aliamua kusubiri kwanza wakifika ndio aondoke, kiukweli mama huyu aliumia sana moyo kumuona binti yake Erica akiwa kwenye hali hiyo, alikuwa kila muda akiingia kwenye maombi kwaajili ya kumuombea binti yake alijikuta akiishia kulia tu yani hakuwa na raha kabisa haswaaa akimsikia mtoto wa Erica akisema,
“Bibi mbona mama hasemi kitu”
Roho ilikuwa inamuuma sana, ilibidi Erick achukue jukumu la kumbembeleza Angel kwa siku hiyo hadi alipolala na kwenda kumlaza maana alionyeshwa tu chumba cha Erica na kwenda kumlaza Angel, muda kidogo alifika Mage na Bite, kwakweli Bite alikuwa amekonda sana ila kitendo cha kumuona mdogo wao katika hali ile walijikuta wakiangusha machozi kwa uchungu maana si kitu mtu yeyote alikitarajia, walipofika tu mama Erica akamruhusu Erick aondoke, kwakweli Erick aliondoka huku akiwa na mawazo sana kwani hakuwa na raha hata kidogo.
Pale nyumbani walijikuta wakilia tu bila ya kufanya chochote kile na kushauriana kila jambo la kufanya ila mama yao alibaki na msimamo ule ule wa kusema ashikilie maombi.
Siku hiyo walilala sebleni yani watoto tu ndio walienda kuwalaza chumbani, kulipokucha waliamka na kumchukua Erica kwenda kumuogesha kisha kumrudisha na kuanza kumlisha chakula ambapo kile chakula kilikuwa kinarudi tu na kufanya waumie zaidi, mpaka wamuinamishe ndio waweze kumlisha, ile asubuhi asubuhi Erick alifika tena kamavile alilala getini, kiukweli Erick hakuwa na raha kabisa kwani kwa kiasi kikubwa alijiona kuwa yeye ndio kasababisha kwa kumlazimisha Erica kufanya mapenzi wakati alikataa na kumwambia kuwa amefunga, yani Erick alijiona mkosaji sana, aliumia jinsi Erica alivyokuwa akila kwa shida na kuamua kutoa ushauri kuwa amlete daktari amfundie Erica mifumo ya kuingizia chakula huku wanaendelea na maombi, Mage aliafiki na kuona hilo swala ni zuri nap engine daktari afike pale na kumgfanyia uchunguzi kuwa ana ugonjwa gani.
Kwakweli Erick hakuchelewa kwenda kumtafuta daktari na mida kidogo alifika na daktari ambaye alimchukua Erica vipimo na kuangalia uwezekano wa kumuwezesha Erica kupata chakula kwa muda huo, daktari aliondoka na vipimo kwanza huku akiwaambia kuwa anawalete majibu.
Majibu yalipokuja ilionekana Erica hana ugonjwa wa aina yoyote na kuzidi kupata jawabu kuwa kuna kitu ambacho si cha kawaida kimempata Erica. Wote ilibidi waegamie kwenye maombi tu ingawa walipata na ushauri mbalimbali ila ilibidi wakae kwenye maombi tu.
 
SEHEMU YA 369

Kwenye mida ya saa kumi na mbili siku hiyo, Nasma alifanya matayarisho ya dawa yake, amapo alimuwekea kwenye chakula, kwenye maji ya kuoga na kunyunyiza ile ya kitandani, akawa akimngoja tu Bahati atoke kwenye shughuli zake, na kweli baada ya muda Bahati alifika nyumbani, na moja kwa moja Nasma alimkaribisha mezani ili ale, akaoge na alale ila Bahati akamwambia Nasma,
“Nimechoka sana leo, nataka kupumzika tu”
“Basi ule kidogo, ukaoge ndio ukapumzike, na leo nimepika kile chakula unachopenda”
“Nasma, jioni hii hii nimekula, kuna jamaa alileta chakula pale ofisini nimekula, kwahiyo labda badae shibe ikiisha”
“Kheee jamani mme wangu”
Bahati ndio kwanza aliinuka na kwenda chumbani na kujilaza, kwakweli Nasma alihisi dawa zimefanywa ndivyo sivyo, akawa na mawazo sana ila kila alipomuamsha Bahati alikuwa hana habari zaidi ya kulala usingizi fofofo.
Alipoamka ilikuwa ni usiku tayari, ila bado Nasma alikuwa na swala moja la kumlazimisha mumewe akale,
“Basi mume wangu twende ukale”
“Aaaah nimeshiba sana Nasma”
Basi Nasma aliendelea kumbembeleza mume wake kuwa akale, ila badala yake Bahati alimtaka mke wake kimapenzi kwa muda huo,
“Ila mume wangu si unajua nimetoka kujifungua!”
“Kama hutaki basi ila mimi nataka”
“Subiri nimalize arobaini basi mme wangu, nitakupa hadi uchoke”
Bahati aliamua kuendelea kulala, kwakweli Nasma hakupatwa na usingizi alikuwa na mawazo mengi mengi maana kile kitendo cha Bahati kutaka mapenzi alihisi huenda zile dawa zimeanza kufanya kazi, yani alijilaumu sana kufanya kitu bila kufikiria madhara yake kwanza.
Palivyokucha tu, Bahati aliamka na kujiandaa kisha akaondoka yani hata kuoga hakuoga, kitu ambacho kilimchanganya sana Nasma.

Rahim alikuwa na mawazo sana baada ya kuambiwa kuwa Erica anaumwa, yani hakuwa na raha kabisa, alijikuta akitaka kufahamu kuwa Erica anasumbuliwa na tatizo gani, ila tatizo lake hakupafahamu vizuri kwakina Erica, kwahiyo aliamua kumuomba Babuu amsindikize, kwakweli Babuu alishangaa sana kuona siku hiyo Rahim akitaka kwenda kwakina Erica, ila alikubali kumpeleka kama kawaida wakati wanajadili mdogo wake Salma alisikia maongezi yale na kumpelekea dada yake,
“Dada, nimewasikia wanapanga kwenda kwakina Erica, eti anaumwa”
“Kheee jamani nifanye kitu gani ili Rahim awe anamaanisha maneno yake kuwa Erica hampendi tena! Nachukia Erica mimi, namchukia sana”
Wakati anasema hivyo mke wa John alimsikia na kwenda kuongea nae maana wote walikuwa wanakaa nyumba moja maana mama yao mwenyewe aliwaambia waoe na kuwataka wote aishi nao nyumbani kwanza mpaka familia zao zikitanuka, mke wa John aliyeitwa Neema alisogea na kuongea na Salma,
“Sikia Salma, usimchukie hivyo Erica ila jua kwanini Erica anapendwa hivyo na si wewe, ila swala la kumchukia Erica sio suluhisho”
“Wewe Neema hujui tu, unajua Rahim kakazana sana na kwa Erica yani mapenzi kwangu hayapo nkabisa yeye na Erica tu. Wewe huumii kama mimi”
“Tena bora wewe hata Rahim anakudanganyaga danganyaga kuwa hamtaki Erica, jamani mimi john mara ya kwanza kabisa aliniambia kuna msichana alikuwa akimpenda sana alikuwa anaitwa Erica, nilikuwa sijui yukoje ila nilitaka kujua ni kwanini alimpenda sana, nikawa napeleleza kwa John nijue ni kwanini alimpenda sana Erica, mbona nilivyojua basi na mimi niakjaribu kuenenda hivyo mbona John hata alimuona tena Erica hakumfatilia maana aliamini kwa mimi mke wake, sasa wewe Salma kumchukia Erica sio mwisho maana Rahim atakudanganya huku akiendelea kumpenda Erica”
“Sasa wewe uligundua ni kitu gani John alimpendea Erica?”
“Kwanza Erica ni mpole, hakuna mwanaume anayependa mwanamke machachari, mwanamke anayeongea kama cherehani hana kituo hakuna mwanaume anayependa, hakuna mwanaume anayependa mwanamke mwenye gubu, huwa wanavumilia tu lakini hakuna anayependa, tunaona Erica akipendwa na wote hawa ni sababu ya upole wake, hata sura yake inaonekana ni ya kipole na mtaratibu, halafu Erica sio mkorofi, sidhani kama huwa anagombana na watu kwa kutukanana nao au kuchambana nao, halafu Erica ni mcha Mungu, kila mwanaume anapenda apate mwanamke mcha Mungu, maana wanaume wengi wanahofia wakipata mapepe watarogwa, kwahiyo Salma jaribu kusimama kwenye nafasi yako, acha kuwaza kuhusu Erica sijui ana bomoa nyumba yako, mwanamke mpumbavu hubomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe, usiwaze hayo, mimi nilikuwa mkorofi ila nilivyosoma John hapendi mwanamke mkorofi nilianza kubadilika taratibu na sasa huwezi kunikuta nikigombana na watu au kumjibisha kitu kibaya John, nilikuwa sisali ila siku hizi nasali na kumuhimiza mume wangu twende kanisani ingawa humu ndani tupo dini tofauti”
“Sasa mbona nasikia na huyo Erica hasali!”
“Unaweza sikia hivyo ila swali wewe unasali? Jamani toka nimefika huku ndani sijawahi kukusikia hata mara moja ukienda Msikitini, nina hakika hata umesahau Misikiti ikoje, tena sijawahi hata mara moja kukuona unaswali sijawahi ila nakuonaga mara nyingi ukijifukiza, hapo utasema mbaya wako ni Erica? Mbaya ni wewe mwenyewe Salma unatakiwa kujirekebisha”
“Kwahiyo muonekano wa mtu ndio unaharibu, sina sura ya upole mimi kwahiyo niitengeneze? Siwezi kukaa kimya mtu akinisema mimi sio mjinga kiasi hiko, wewe Neema endelea hivyo hivyo ila mimi nitahakikisha mpaka jina la Erica linapotea kwenye masikio ya Rahim”
Kwakweli Neema ilibidi anyamaze tu kwani aliona kila anachomuelekeza mwenzie alikuwa haelekezeki.

Rahim na Babuu walienda hadi nyumbani kwakina Erica kumuona Erica, walifika na kuwakuta dada zake na Erica maana waliamua kukaa pale pale kwanza kumuhudumia mdogo wao sababu alikuwa akuhitaji kuhudumiwa kila kitu, kwa upande wa Erick ilikuwa kama pale ni eneo lake la kazi maana kila siku alionekana kwenye nyumba ile, kwahiyo hata Rahim na Babuu walivyofika walimkuta Erick yuko pale na alikuwa akimbeba Angel, walifika na kusalimia huku wakiulizia hali ya Erica na kuambiwa anavyoendelea ingawa kila siku kulikuwa kunaonekana maendeleo juu ya Erica kwahiyo nao wakaambiwa kuwa wamuonavyo ni anaendelea vizuri maana mwanzo alikuwa hawezi kukaa ila kwa hizo siku mbili aliweza kukaa, kilichomshangaza Rahim ni kuwa Yule mtoto hakumtaka kabisa yeye, yani alimtaka Erick tu, kile kitu kilimuumiza sana moyoni kuona mtoto wake mwenyewe akimpenda baba mwingine, aliumia sana roho.
Ila mama Erica alivyorudi na kumuona Babuu hakutaka kabisa, akamtimua na alivyotambulishwa kuwa Yule ndiye Rahim alimtimua pia,
“Sitaki kuwaona nyie vijana, sitaki kuwaona kabisa, haswaaa wewe Rahim, ondoka kwenye nyumba yangu, kwanza ulishamtishia mwanangu, kwahiyo umekuja kiunafki tu. Ondoka kwenye nyumba yangu”
Ilibidi Rahim na Babuu waondoke zao maana hawakutakiwa tena mahali hapo.
Muda kidogo alifika Fetty na kuanza kuongea na mama yake Erica na ndugu zake wengine pale,
“Mama, kuna mtu anaona ameniambia kuwa waliokuwa wakimtesa Erica ni wanawake wawili yani hao wana visasi vikubwa sana na Erica”
Mama Erica alishtuka sana na kusema,
“Wanawake wawili! Sian a Tumaini hao, jamani kwani mwanangu kawakosea nini?”
Erick alichukia pia kusikia vile kuwa dadake na msichana wake wa zamani wameamua kufanya kitu kibaya kwa Erica, yani muda huo huo aliaga na kuondoka maana hakupenda kabisa na aliwaona kuwa wabaya sana hadi kufikia hali ile aliona ni mbaya kwakweli.
 
SEHEMU YA 370

Erick aliondoka mpaka dukani ambako Tumaini alikuwa akisimamia, alimfata na kumwambia,
“Tumaini kuanzia leo sitaki tena uguse duka hili”
“Erick imekuwaje tena? Si ulisema hili unaniachia mimi na lile ndio unabaki nalo wewe, imekuwaje unanifukuza tena?”
“Nimesema toka kwenye duka langu, yani kuanzia leo ni mwisho na kesho naleta msimamizi mwingine, umeniudhi sana Tumaini”
“Kosa langu ni lipi lakini?”
“Kamfate baba akupe na wewe mali zako uanze kuziendesha sio zilizoendeshwa na wenzio ufurahie tu kuzifanya, fanya zako. Na sitaki kukuona tena, yani wewe wa kumroga Erica! Sitaki tena kukuona”
“Jamani Erick, nimemroga Erica saa ngapi? Kumbuka wewe ni ndugu yangu”
“Tumaini, ole wako Erica afe yani sahau kama umewahi kuwa na ndugu kama mimi. Kwaheri”
Erick aliondoka na kumuacha Tumaini akiwa na mawazo mengi sana kuwa yeye kamroga Erica muda gani yani hakuelewa kabisa.
Erick muda huo aliondoka na kwenda kwakina Sia, kwakweli Sia alifurahi kumuona na kwenda kumkumbatia ila Erick alimsukuma pembeni na kumwambia,
“Sitaki unipigie simu, sitaki unitumie ujumbe, sitaki ukanyage kwetu”
“Kwani Erick nimefanyaje?”
“Na ole wako Erica afe ndio utanijua vizuri mimi”
Kisha Erick akaondoka hakutaka hata kurudi kwao, yani toka Erica aanze kuumwa alikuwa akishinda kwakina Erica na kulala hotelini, na hivyo alivyoambiwa kuwa wabaya wa Erica ni wanawake wawili ndio kabisa akawachukia Tumaini na sia, na hakutaka kuonana wala kuongea tena na Tumaini zaidi ya pale dukani alipomfukuza.

Ilipita wiki toka Erica apate matatizo, mamake alikuwa akialika watu mbalimbali kuja kumfanyia maombi pale nyumbani kwahiyo Erica alikuwa akiombewa kila siku na kufanya afya yake ianze kuwa imara, siku hiyo Erick akiwa amekaa pembeni ya Erica, akamuita
“Erica”
Erica akageuka na kumuangalia huku akitabasamu, kitendo hiko kilimfanya Erick ashangilie utafikiri kaona kitu gani, familia yote iliingia ndani, na walijaribu pia kumuita Erica, aliwaangalia na kutabasamu yani wote walikuwa na furaha sana, mama Erica aliamua muda ule ule kumpigia simu Yule mwanamaombi,
“Kwakweli Mungu ni mwema, leo Erica tunamuita anatuangalia na kutabasamu”
“Ooooh hiyo habari njema sana, tuingie kwenye maombi sasa tukimshukuru Mungu kwa kutenda makuu kwa Erica”
Alivyokata simu aliwataarifu wote, yani siku hiyo hata Erick ambaye huwa hawezi kuomba aliomba kwa furaha ya kumuona Erica akitabasamu tena.

Ilikuwa mida ya jioni ambapo Nasma alikuwa ameenda dukani mara moja, wakati anatoka dukani akakutana na mdada mmoja ambaye alimsimamisha kisha akamsalimia na kuanza kumwambia,
“Dada, wewe ni mwanamke mwenzangu nimeona nikwambie hili”
“Niambie tu”
“Jamani mumeo kabadilika yani kabadilika haswaaa”
“Kivipi?”
“Hadi tunakuonea huruma, jamani mumeo anatongoza hovyo, anatembea na wanawake hovyo hadi tunakuonea huruma, ile gari yake imekuwa kama guest yani mumeo anafanya mapenzi na wanawake ndani ya gari, kwakweli ni aibu. Samahani kama nimekosea kukwambia, ila nimeshindwa kuvumilia”
Kwakweli Nasma aliondoka pale akiwa na mawazo sana maana hakutegemea kama mumewe atakuwa muhuni wa kiasi kile, basi akarudi nyumbani kwake akiwa na mawazo sana.
Akafika na kukuta nyumba ipo kimya sana, akaweka vitu jikoni na kuelekea sebleni, akashangaa kumkuta Bahati na Siwema wakiwa sebleni wanafanya mapenzi.

Kwakweli Nasma aliondoka pale akiwa na mawazo sana maana hakutegemea kama mumewe atakuwa muhuni wa kiasi kile, basi akarudi nyumbani kwake akiwa na mawazo sana.
Akafika na kukuta nyumba ipo kimya sana, akaweka vitu jikoni na kuelekea sebleni, akashangaa kumkuta Bahati na Siwema wakiwa sebleni wanafanya mapenzi.
Alijikuta tu akisema kwa mshangao,
“Yani mume wangu na mdogo wangu mnanisaliti?”
Ila wala walikuwa hawamsikilizi kabisa, hadi ikabidi awafate karibu na kumvuta Bahati huku akisema,
“Yani hamna hata aibu! Naonekana hapa mnaendelea tu, heshima iko wapi jamani! Eeeeh Siwema, heshima iko wapi mdogo wangu?”
Siwema alikuwa akivaa kwa aibu tu, ila Bahati alienda chumbani na kujilaza, kwakweli Nasma alikuwa amechukia sana na kumfata Bahati huku akimuuliza kwanini amefanya vile na mdogo wake,
“Hebu wewe mwanamke tulia, nishakwambia nina hamu umesema hadi umalize arobaini kweli nitasubiri arobaini iishe? Ushaambiwa kizuri kula na nduguyo, sasa kuna ubaya gani wa mimi kulala na Siwema?”
“Hebu niondolee balaa mie Bahati, umenitia aibu haswaaa yani umenitia naibu sana”
Kisha akarudi kwa mdogo wake na kumfokea kuwa kwanini kamfanyia hivyo,
“Dada, nilikuwa nakusaidia tu maana shemeji alisema ana uhitaji”
“Mjinga wewe, nimeomba msaada wako mimi? Nakwambia na kwangu hapa unaondoka mjinga wewe”
“Jamani dada nisamehe, nimefanya na shemeji mara mbili tu sirudii tena”
“Mjinga wewe, kumbe ndio mchezo wenu eeeh! Na kwangu unaondoka kapaki vitu vyako uende, yani nikafuge mbwa ndani kwangu siwezi, sikufikiria kama una tabia mbaya kiasi hiko”
Basi ilibidi Siwema ajiandae kwaajili ya kuondoka kwa dada yake.
Nasma hakutaka tena kumuona mdogo wake maana alihisi akiondoka ndio itakuwa afadhali kwake na familia yake ili apambane tu na wanawake wa nje ambao Bahati atakuwa nao.
Mdogo wake Nasma wakati anaondoka, muda ule ule Bahati nae alitoka, kwakweli Nasma hakuelewa kuwa ni kipi kimeendelea ila Bahati hakumruhusu Siwema kurudi nyumbani na badala yake alienda kumpangishia chumba ili awe mke wake wa pili.
 
SEHEMU YA 371

Nyumbani kwakina Erica ilikuwa ni mabadiliko ya kila siku juu ya uzima wa Erica kwani saivi alikuwa akielewa kila kitu kilichokuwa kikizungumzwa na kuna baadhi ya mambo alikuwa akiyafanya kama kumshika mwanae tofauti na mwanzo ambapo hakuweza kufanya chochote, ila tu hakujibu kitu lakini alionekana kuelewa kila kitu, kitu kile kilimpa matumaini na Erick na kuweza kuendelea na kazi zake zingine kwahiyo alikuwa akitoka kwenye kazi zake jioni ndio anapitia kwakina Erica kuangalia hali yake na kisha kurudi hotelini kulala.
Siku hiyo walibaki nyumbani Bite na Mage huku Mage akijiandaa andaa kwenda kuona familia yake, na mama yao hakuwepo, na muda kidogo Mage akaondoka zake kwahiyo alibaki Bite na Erica, muda kidogo wakapata ugeni na mgeni huyo alikuwa ni Dora, ambaye alifika na kugonga mlango na kukaribishwa na Bite, alishangaa kumuona Dora maana anakumbuka mara ya mwisho ni kipindi kile wakati ametimuliwa kwao baada ya kuletwa na Tony kama mchumba, ila yeye hakumtimua bali alimkaribisha ambapo Dora aliulizia Erica,
“Yani nampigia simu hapokei, natuma ujumbe hajibu ndiomana nikaamua kuja tu”
“Erica anaumwa, siku zote hizi”
Akaingia ndani na kuonyeshwa Erica aliyekuwa sebleni, akashangaa anamuitwa Erica ila anamuangalia tu bila kusema chochote,
“Kheee kwahiyo hasemi”
“Mbona ni afadhali hapo, alikuwa na hali mbaya sana yani watu wa maombi wamefanya kazi kubwa”
“Kheeee kaanzaje?”
“Yani nasikia alianguka kama kifafa, baada ya hapo ndio akaanza hivyo, alikuwa anakakamaa mwili kama mtu mwenye degedege”
“Kheeee nguvu za giza hizo”
“Kwanini umesema hivyo?”
“Erica, hajawahi kuumwa kifafa, mtu ambaye kifafa hakijawahi kumpata halafu kimpate gafla huwezi sema ni kitu cha kawaida, halafu sijui akakamae kama anaumwa degedege jamani huo ugonjwa huwa unawapata watoto tena wale wasiopewa chanjo, aje kuupata Erica kweli! Kwanza ugonjwa wenyewe huo hata ukimpata mtoto huwa unashirikishwa na nguvu za giza, wanasemaga ni jinni na ndiomana wakikosea tu tiba kwa mtoto mwenye degedege anapotea. Ila mbona hamkuniambia kama rafiki yangu kipenzi anaumwa hivi?”
“Kumbe bado ni rafiki yako eeeh!”
“Ndio, tena urafiki wangu na wake saivi umekuwa zaidi, yani wa kiwango kingine. Mngeniambia kwakweli”
“Basi ndio hivyo, ila saivi anaendelea vivuri tofauti na mwanzo alikuwa na hali mbaya zaidi”
“Kwahiyo tiba gani mmepata?”
“Watu wa maombi huja kumuombea kila mara yani Erica anaimalika sababu ya maombi”
“Ila hamuoni kama mnamchelewesha na hayo maombi”
“Kivipi?”
“Yani mngeniambia mapema, kuna mtaalamu huyo yupo Bagamoyo yani huyu Erica angechemshiwa jungu siku mbili tu angerudi kwenye hali yake, huyo mtaalamu kiboko na angesema nani kamfanyia hayo mambo, yani nyie mnakazana na maombi tu jamani!”
“Wewe acha maneno hayo, maombi yana nguvu. Kwani kuna watu wangapi tunasikia habari zao kuwa wamefia kwa waganga? Kupona kwa maombi ni kupona milele, nguvu ya Mungu ni kubwa sana kupita unavyoielewa, yani wewe ni dini gani usiyejua mambo ya maombi?”
“Mimi ni mkristo ila huwezi kunipeleka kwenye maombi maana hao wachungaji wanapenda pesa tu, kidogo utasikia sadaka, tunadanganyana tu hao wachungaji ndio wanaongoza kwenda kwa waganga, mnamchelewesha Erica hapa yani tungeenda nae kwa babu huyu mbona angekuwa mzima kabisa ila hizo habari hapana aisee”
“Wewe ndiomana tulikutimua kipindi kile sijui Erica ameanza vipi tena na urafiki na mtu kama wewe hata usiyejua uwepo wa Mungu”
“Najua vizuri kuwa Mungu yupo ila hata hao waganga wanatumia Mungu, mi ngoja niondoke maana hatutaelewana hata nishauri vipi ila nakuahidi natoka hapa kesho safari Bagamoyo kwa babu halafu nitaleta dawa uone kwa sekunde tu Erica mzima”
Bite aliamua kumtimua tu Dora na hapo hakujua kama huyo ndiye mwizi wa mume wake,ila alijikuta akimchukia tu gafla kwa maneno yake.

Kiukweli Salma hakufurahishwa na mwenendo wa Rahim kwani ilionyesha wazi Rahim toka ametimuliwa nyumbani kwakina Erica hakuwa na furaha kabisa na vile mtoto wake alivyoonekana kumpenda zaidi Erick ndio kulimfanya azidi kupata mawazo, kufikia hatua ya kuaga anaenda kwenye kazi ila alikuwa akienda kwa wanawake zake wengine na kulala huko siku mbili ndio anarudi nyumbani, hali hiyo haikumpendeza kabisa Salma, ukizingatia kila alipomueleza mama mkwe wake ila huyu mama alionekana kumtetea kabisa mtoto wake na kila Salma alichosema alionekana kumuonea,
“Mama, Rahim anakunywa pombe”
“Hebu Salma acha maneno yako Rahim na pombe wapi na wapi?”
“Kweli mama, na ana wanawake”
“Mwanangu kuzaa na Erica sio alikusudia ila ni bahati mbaya tu, mwanangu hana wanawake wengi kama usemavyo, mara nyingine jifikirie Salma, mwanangu kazunguka nchi mbalimbali lakini kaja kukuoa wewe, jiulize una kipi ambacho wanawake wengine hawana? Ila unaweza kuja kumsingizia kuwa ana wanawake kweli? Nimewapa ile nyumba pale muwe mnakaa sababu sitaki kukaa mbali na wanangu ndiomana kwenye nyumba ile mnakaa nyie tu yani wewe na mumeo na Neema na mumewe, sitaki kukaa mbali na wanangu na ningewaweka humu ndani mngeona nawabana oooh mama mkwe anatubana, haya mwanamke wa watu sitaki matatizo ile nyumba niliijenga kwaajili ya wanangu na ni wao na nyie ndio mmeanza kukaa pale, kipindi chote hiki hakuna anayekaa kwenye ile nyumba, mnapika wenyewe, mnaongea wenyewe leo hii uje uniambie mwanangu ana wanawake wengi? Hakuna hiyo kitu, mwanangu namfahamu”
Kwahiyo Salma akaona hakuna ushirikiano kabisa kati yake na mama mkwe wake, akaamua kurudi ndani kwake, ila akapata wazo la Yule mmama waliyekutana nae hospitali aliamua kumpigia simu ili kupewa maelekezo ya kitu cha kufanya,
“Sasa binti yangu itakuwa vyema ukija huku kwangu ili nikupe hiyo dawa na maelekezo”
“Sawa, nitajitahidi nije maana huyu mwanaume sasa anataka kunichanganya akili yangu, nitakuja unisaidie nahitaji kumtuliza huyu mwanaume”
“Sawa karibu sana binti yangu”
Salma aliona ni afadhali amfanyie mumewe dawa maana aliona mwenendo wake haujatulia kabisa.
 
SEHEMU YA 372

Mama Erica alirudi nyumbani kisha Bite kumpa ujio wa Dora,
“Kumbe Yule Dora na Erica walianza tena urafiki?”
“Yani Erica nilishamkataza mara nyingi na Yule rafiki ila yeye alikataa kuwa na urafiki naye, ndiomana hata siku zake nikuwa sipokei”
Basi Bite akamueleza mama yake ambaye Dora aliyasema, ndio mama yake akakumbuka pia kuhusu mahusiano ya Dora na Bite, aliamua kumuuliza mwanae,
“Hivi mwanangu, ulishawahi kupima na ukimwi?”
“Ndio, nilipojigundua nina ugonjwa wa kansa ya shingo ya kizazi niliamua kupima na ukimwi ila sikuwa nao”
“Hongera, na mumeo ulipima nae?”
“Yani James alikataa kata kata kwenda kupima”
“Mmmh kapime tena mwanangu”
“Mama, toka kipindi nimejigungua nina kansa ya shingo ya kizazi sina raha kabisa, nikamwambia James tukapime aligoma basi toka kipindi hiko sishirikiani nae tendo la ndoa nilimwambia hadi akubali kwenda kupima magonjwa yote, ila hana aibu ananiambia eti ugonjwa nimeupata kwenye umalaya wangu, mama wewe ni mama yangu siwezi kukuficha, toka nianze na James sijawahi kuwa na mwanaume yeyote ndiomna roho inaniuma sana, kwakweli nimechoka kuishi na James nimechoka kabisa, anapigiwa simu na wanawake hadi usiku tukiwa tumelala mama yani hana heshima na mimi jamani”
“Kwakweli pole sana mwanangu, naelewa jinsi yanavyoumiza mambo hayo, tafadhali usishirikiane na mumeo mpaka akapime ukimwi, hajatulia kabisa Yule, yani usikubali kabisa mwanangu.”
“Siwezi kukubali mama”
“Nadhani Mage hajakwambia, waliwahi kumuona mumeo akiwa na huyo shetani aliyekuja leo Dora, tena walikuwa wakitoka nyumba za wageni”
Bite alijikuta akimchukia Dora maradufu,
“Kumbe msichana Yule ni mchafu vile?”
“Ndio, na Erica alisema kaambiwa na Dora kuwa ameathirika”
“Uwiii mume wangu jamani”
“Hebu acha uchuro na wewe, Yule ni mume au kopo? Mwanaume wa kumtaka hadi ndugu yako, sio mwanaume kabisa, nasikia mumeo alikuwa na kesi ya kumbaka Dora”
“Hiyo kesi hakutaka hata nijue mwenendo wake na sikuelewa kama ni huyu rafiki wa Erica, sasa mbona alikuwa anakataa?”
“Huwajui wanaume mwanangu? Ila Dora nae sio wa kumlaumu pengine kataka kutuonyesha kweli James alimbaka ndiomana saivi wamekubaliana nae wako wote”
“Itakuwa kweli mama, yani huyu James huyu dah najuta kuwa nae jamani, najuta kumuamini aina yake ya mwanaume. Kuna Yule mkaka alikuwa akinifatilia sana labda ningeolewa nae saivi ningekuwa nafurahia maisha ila kwa huyu James nimekosea namba kwakweli”
“Ila mwanangu usichukulie hasira sana, haya mambo yanaenda taratibu sema huyu mumeo sasa hivi sio wa kumchekea”
“Yani mama najuta, najuta mimi kuolewa na James”
Bite aliongea kwa uchungu kwani hakuwa na raha kabisa yani aliona kamavile dunia imemuonea sana.

Tumaini aliamua kwenda kwa Sia maana walipigiana simu na kujikuta wote wakiwa na janga moja, walikutana na kusalimiana kisha kujadili, Tumaini alimuuliza Sia,
“Kwani unajua kuwa huyo Erica anaumwa na nini?”
“Hata sijui mwenzangu yani nashangaa tu kuwa kwanini Erick kaja kunifokea hivi”
“Mwenzio sasa nimefukuzwa dukani, yani Erick kanifukuza kwenye lile duka lake ambalo nimeliendesha miaka yote hii eti ananiambia nikafate mali kwa baba, halafu baba mwenyewe ni jibu kabisa maana aliwahi kuniambia mali ni za mwanaume eti mimi nitumie tu, ona mwanae alichonifanya kisa mwanamke”
“Sasa Tumaini, mimi naona ni vyema ukazungumze na baba yenu yani umueleze kila kilichotokea, unajua sijui ni kwanini Erick atusingizie sisi”
“Pengine ni sababu ya kumchukia sana Erica”
Wakajipanga cha kufanya ila hawakufikia hata hitimisho, basi Tumaini akawa anaondoka na Sia kumsindikiza huku wakipanga siku moja kwenda kwakina Erica ili wajue nini kinaendelea, wakati wanatembea njiani Tumaini akamuona Dora akamkumbuka kuwa aliwahi kuwa rafiki wa Erica, akamsimamisha na kumsalimia kisha kumuuliza kuhusu Erica,
“Erica rafiki yangu anaumwa kuna wajinga wamemroga rafiki yangu ila nawaendea kwa mtaalamu”
Tumaini akauliza kwa mshangao,
“Kwa mtaalamu! Ndio atafanya nini huyo mtaalamu?”
“Yani kuna babu yupo Bagamoyo ni kiboko huyo, nakwambia Yule Erica mbona siku mbili tu kapona. Mie alinipa dawa nimemteka mwanaume huyo hafurukuti kwangu kwa siku moja tu yani mpaka leo mwanaume haoni pengine”
Tumaini akaona huyu Dora analeta stori sio zenyewe, ikabidi aagane nae na kumuacha akiendelea na safari yake kisha yeye akamuaga Sian a kuita bajaji ili aondoke zake, Sia akamwambia,
“Ila Tumaini unajiachia tu, babako ana hela, mdogo wako ana hela hivi inashindikana kununuliwa gari kweli?”
“Mmmh weee acha tu, baba ana mambo mengi sana na huyo Erick sasa ndio balaa kila nikimwambia kuwa nahitaji gari anasema nitakununulia tu”
“Unajua sielewagi, baba yenu ana hela sana, Erick ana hela sana ila wewe unaishi maisha ya kawaida kwanini? Si ilitakiwa wewe na Erick muwe na mali sawa!”
“Sia familia yetu ni pan asana kuielewa ila kwa kifupi Erick ana hela za sehemu mbili, yani sio baba peke yake anaefanya Erick awe na hela bali na mama yake nae ana hela sana halafu Yule mama mtoto wake ni Erick tu kwahiyo ni mtoto wa pekee na kwa baba nako mtoto wa kiume ni Erick tu hapo ndio kuna utofauti kati yetu. Ila usijali Erick alisema kwasasa mambo yake hayajakaa sawa ataninunulia sasa na hilo swala la Erica kuumwa duh hadi kichwa kinanichemka, tupange tu siku twende kwakina Erica”
Bajaji ilifika na Tumaini kupanda huku akiagana na Sia ila Tumaini alivyoondoka tu Sia akajikuta akimkimbilia Dora na kumuita, yani swala alilosikia kuhusu mtaalamu lilimvutia sana, Dora alisimama na kumsubiria, Sia alikimbia hadi alipo Dora,
“Samahani kuna jambo nataka kukuuliza”
“Bila samahani”
“Wakati tunaongea pale nimesikia kuhusu mtaalamu anavuta mpenzi hadi anakuwa wako, swali ni je hata kama huyo mpenzi hakutaki?”
“Yani hata kama hakutaki baada ya hiyo dawa anakutaka mwenyewe tena anakupenda balaa, atakuhonga hadi usahau”
“Kheee jamani na mimi nilikuwa namtaka huyo mtaalamu”
“Sawa, kesho nataka niende basi chukua namba yangu ili tuwasiliane twende wote”
“Nitafurahi sana, asante”
Wakabadilishana namba pale kisha kuagana, mawazo ya Sia kwa wakati huo yalikuwa kumpata Erick tu kwa hizo dawa, aliwaza kumvuta kwa dawa, aliwaza kummiliki na kufurahi sana.
 
SEHEMU YA 373

Salma kama alivyopanga na Yule mama, akajiandaa vizuri na kumuachia mdogo wake mtoto kisha yeye kuonana na huyo mama, ambapo alimkuta pale alipomwambia,
“Sasa wewe unataka dawa ya kumtuliza mume, au dawa ya mume kukusikiliza kila unachosema, au dawa ya kumfanya mume awe anakupa hela zote yani wewe ndio unatoa bajeti na matumizi ndani ya nyumba”
“Kiukweli nataka dawa zote yani mume wangu asifurukute kabisa mbele yangu yani mimi niwe kila kitu kwake”
“Sawa hakuna shida, masharti utayaweza?
“Nitayaweza ndio”
Akampa dawa nyingine ya kujifukiza na nyingine ya kuweka kwenye chakula, na nyingine ya kuweka kwenye maji ya kuoga, kwakweli Salma aliifurahia sana ile dawa na alitakiwa kuifanya muda ambao mumewe hayupo,
“Yani vizia wakati mumeo kaondoka nyumbani ndio uifanye hii dawa, unawashamkaa unachukua kidogo kwenye sufuria halafu unaenda nao chumbani na kuanza kuchoma huku unanuizia hata aje kukuita nani usiinuke wala usiitike ndiomana nakwambia ni vizuri ukiwa mwenyewe yani baada ya hizi dawa mumeo atatulia hawezi tena kuhangaika nakwambia”
“Nashukuru sana, ila kuna mwanamke mmoja hivi anapendwa sana na mume wangu, mwenzangu alimfanyia dawa, tulitaka awe chizi ila nasikia ilisindikana kuwa chizi akawa tahira, sasa mume wangu anashinda huko huko hadi nakosa amani”
“Sasa huyo mto ni ndondocha ila bado mumeo anashinda huko, basi ngoja nikupe dawa”
Salma akaisubiria hiyo dawa,
“Sasa nakupa dawa ukamsalimie, wakati hiyo dawa umeishika mkononi yani utampa mkono na dawa hiyo hapo ni kwisha habari yake”
“Ila mimi siwezi kwenda nyumbani kwakina huyo msichana, naweza kumuagiza mtu?”
“Inawezekana ndio”
Mtu ambaye alimuwaza kwa muda huo ni Derick tu ndio aliona wa kumsaidia kwa kile alichokipanga, kisha akaagana na Yule mmama na kuondoka zake kurudi kwao, alipofika kwao alimuona mumewe Rahim akiongea na Neema, hakutegemea kumkuta nyumbani mumewe muda huo ila ndio alimkuta hakuwa na cha kufanya zaidi ya kuwa mpole kwanza, alisogea ili aingie ndani na kuwasalimia, Rahim akamuuliza,
“Weee Salma, umetoka wapi muda huu?”
“Aaaah nilienda hapo dukani”
“Hivi wewe mwanamke una akili? Yani mtoto bado mdogo umeanza kuzurula, haya niambie umetoka wapi? Hata kazini kwenyewe hutoa miezi mitatu ya mapumziko mtu akitoka kujifungua sembuse wewe mama wa nyumbani? Niambie umetoka wapi muda huu?”
Salma hakusema chochote na kuingia ndani, Rahim akamfata ndani na kumuuliza tena kuwa ametoka wapi,
“Jamani Rahim mbona uko hivyo! Mimi mbona sijawahi kukuuliza wewe kuwa umetoka wapi jamani? Kila mtu awe huru humu ndani”
“Wewe Salma usinipande kichwani, mimi ni mumeo nina haki ya kujua mapito yako yote, usinijibu hivyo nitakupiga sasa hivi”
“Kama unaona kupiga dili nipige basi”
Huku akimsogelea mwilini kama anayetaka kupigwa, Rahim nae hakumuachia na alimpiga kweli na kumuacha akipiga kelele tu ndani ya nyumba kisha Rahim akatoka na kuondoka, neema aliingia ndani kumbembeleza rafiki yake, alimkuta chini akilia na kuanza kumbembeleza, salma alikuwa akisema,
“Yani wanaume wana roho mbaya jamani, mimi nina mtoto mdogo halafu yeye ananipiga! Najuta kuolewa nae”
“Ila Salma usifikie kujuta, jiulize kwanza kwanini kakupiga”
“Na wewe hebu nenda huko, yani hapa ndani mtu huruhusiwi kutoka au ni kitu gani? Mbona yeye anatoka simuulizi”
“Usishindane na mwanaume”
“Wewe subiri tu huyu Rahim dawa yake inachemka tuone kama atanipiga tena na ujinga wake”
Neema alijaribu kuongea nae ila ilikuwa ngumu sana kwa Salma kumuelewa ikabidi neema atoke.
Ila alimkuta tu Rahim amekaa nje, akamfata tena na kumuuliza,
“Kwani shemeji vipi jamani mpaka umempiga Salma?”
“Yule mwanamke ni mjinga sana, huwa sipendi mwanamke anijibishe hata mara moja, mimi sio mpigaji ila alivyokuja mwilini alitaka nimfanye nini?”
“Mmmh ila shemeji hujawahi kuishi na Salma kama kipindi hiki, unatakiwa kumuonyesha upendo na sio hasira”
“Mwanamke mjinga sana, najuta kutafutiwa mwanamke, bora ningemuoa Erica wangu mimi tungelea mtoto wetu”
Salma alikuwa dirishani na kusikia yani hapo ndio hasira zilimpanda alitamani hata dawa aifanye muda huo ila kwavile tu aliambiwa ni hadi jioni.

Siku hiyo Erick alikaa na Erica akiongea nae, yani Erica hakujibu ila Erick aliongea nae kwa furaha kwani aliona jinsi Erica anavyotabasamu na kumpa moyo kuwa Erica ni mzima na karibuni atakuwa sawa kabisa,
“Erica, ile zawadi ya gari bado ipo yani usijali mpenzi wangu, siku ukipona kabisa nitaileta hapa yani nitakukabidhi hapa mpenzi wangu, ile ni zawadi yako kabisa, na unajua kitu kingine kuna zawadi kubwa nimekuandalia najua hii ndio utaipenda zaidi maana si gari tena ila ni zaidi ya gari. Nakupenda sana Erica”
Erica alikuwa akitabasamu tu na kumfanya Erick afurahi zaidi, muda huo akafika mgeni pale kwakina Erica, mgeni huyo alikuwa ni Fetty kwahiyo alifurahi sana kuwaona pamoja, Bite na Mage nao wakasogea karibu alivyofika Fetty maana mwanzo walimuacha tu Erick aongee ongee na Erica.
Bite aliamua kumuuliza Fetty,
“Eeeh leo una ujumbe gani Fetty?”
Fetty akacheka tu na kusema,
“Sina ujumbe ila watu huwa hawanielewi mimi yani mimi kama nina madudu kichwani yani huwa yananiambia vitu nisivyovielewa kabisa, ndiomana nikienda kupeleka ujumbe huwa nasema kuna mtu kaniambia ila ni madudu yangu kichwani, bite alicheka sana baada ya kusikia Fetty ana madudu kichwani, mama Erica nae alitoka ndani akiwa amesikia hiyo habari ya Fetty kuwa na madudu kichwani ila mama Erica akamshauri,
“Unatakiwa uombewe hayo madudu yatoke, huoni kama yanakusumbua?”
“Hapana hayanisumbui wala nini ila huwa yananipa habari”
“Mmmh ila ningekuwa ni wewe ningeyatoa, kuishi na madudud hapana kwakweli. Ni muda gani sasa unayo?”
“Ni ukubwani hapa hapa ndio hii hali imeanza maana nilipokuwa mdogo wala hakuna kitu”
Wakati wanaongea alifika mgeni mwingine ambaye ni nadra sana kufika mahali hapo, alifika Derick, na alionekana kuwa na lengo la kumuona Erica ila alishangaa sana kumuona Erica ameshikiliwa na Yule kijana aliyemkuta, hakumjua ni nani ila alihisi atakuwa mpenzi wa Erica tu, alikaribishwa na baada ya salamu tu aliamua kuulizia na kujifanya anayaka kumsalimia sheej yake, Mage alimtambulisha pale kwa Erick, kitu kilichomuumiza sana moyo kumfahamu Erick, yani yeye hakupenda Erica awe na Erick, kwakwe ilikuwa ni bora Erica awe na mwanaume mwingine ila sio Erick sababu tu alijua huyo mvulana anapendwa sana na Erica, Badi Derick akamsalimia pale halafu akaulizia chanzo cha ugonjwa wa Erica, kisha Mage alimueleza kwa kifupi. Kisha Derick akasogea karibu ili amguse Erica, Gafla Fetty aliinuka na kwenda kumzaba kibao Derick, kwakweli Derick alichukia sana na kuuliza,
“Wewe Fetty una nini wewe? Kwanini unipige?”
“Wewe ni mnafki, hauna lolote umesababisha pia kuumwa kwa huyu”
Derick alishangaa na wote pale walishangaa, kwakweli Derick hakutegemea kama Fetty angesema vile na hakujua kwanini alisema vile, kisha Fetty alisogea katikati yani yeye ndio akawa katikati kiasi kwamba Derick asiweze kumuona tena Erica, kisha akasema,
“Ondoka Derick, hakuna kumsalimia Erica, ondoka upesi”
Wote walikuwa wakishangaa ila kwavile mama Erica hampendagi Derick aliamua kutumia ile ile nafasi kumtimua maana huwa anamuhisi muda wote ni mnafki toka mambo ya chuo ambayo mwanae alimsimulia na mambo ya kule kwenye tambiko basi huyu mama ndio hakutaka kabisa kumuona Derick ila alimuona tu sababu ya Erica kwahiyo muda huo akapata nafasi ya kumfukuza pia.
Kwahiyo Derick hakuwa na jinsi zaidi ya kuondoka tu, na baada ya Derick kuondoka ndipo mama Erica nae akaondoka kwenda kwenye shughuli zake.
 
SEHEMU YA 374

Jioni hii Salma nae aliwasha moto ili afanye ile dawa kwani aliamini sababu ya ule ugomvi wa mchana ni ngumu mumewe kurudi nyumbani, akampa mdogo wake mtoto ambebe na ambembeleze ambapo mdogo wake alimbeba na kwenda nae kwenye nyumba ya mama yao na wakina Rahim. kwahiyo aliona ndio muda pekee wa kuanza kufanya ile dawa yake, kisha kuchukua moto wa mkaa kwenye sufuria na kwenda nao ndani kunuiza kile alichofundishwa na Yule mmama, akaanza kufukiza dawa zake huku akinuiza, Neema alikuwa akiona tu moshi ukitoka kwenye kile chumba cha Salma, kiukweli alisikitika sana maana aliona anachofanya mwenzie sio sawa, kisha akamuona Rahim kama anakuja, akatamani amzuie ila hakuweza maana Rahim alishafika, Rahim hata hakumsalimia Neema kwani moja kwa moja aliingia ndani, akafungua mlango wa chumbani na kuona mgumu kufunguka, akagundua umefungwa kwa ndani na vile aliona moshi moshi alihisi tu kuna kitu si cha kawaida kwenye nyumba yake, Sema alikuwa na funguo ya ziada mfukoni ya kile chumba, akaingiza na kuangusha funguo ya ndani kisha kufungua mlango, alishangaa kumuona Salma kajifunikiza akinuizia dawa, alimuuliza kwa ukali,
“Salma, unafanya nini?”
Salma hakujibu kitu kwani alikuwa akifuata masharti, kwakweli Rahim alichukia na kujikuta akianza kumpiga Salma, alimpiga Salma hadi Salma akazirai.

Jioni ilipoingia sana Fetty akaaga na kuondoka na Erick nae kuna kazi alisema kuwa anaenda kuimalizia, Bite alimuuliza,
“Kwahiyo utarudi?”
“Ndio, nitakuja kuwaaga”
“Sawa”
Bite aliitikia ila aliweza kuona huyu kijana alikuwa na upendo wa aina gani kwa mdogo wake kwajinsi alivyoonyesha kumjali. Muda kidogo simu ya Erica iliita, dada yake Bite aliichukua na kuona ni namba ngeni akaamua kuipokea maana hakujua ni nani na anahitaji nini kwa Erica. Alipokea maana alihisi huenda akawa ni mtu wa maana, alimuuliza kwanza ni nani,
“Mzee Jimmy anaongea hapa!”
“Mzee Jimmy? Yupi na unashida na nani?”
“Shida yangu ni Erica, maana naona sauti sio ya Erica hii, yuko wapi nina shida nae haswaaa”
“Erica anaumwa”
“Anaumwa? Nini tena?”
Bite akamueleza kwa kifupi juu ya kinachomsumbua Erica, basi Yule mzee aliahidi kwenda, na kweli kwenye mida ya saa mbili usiku Yule mzee alifika, na kugonga mlango akatoka mama yake Erica maana muda huo alikuwepo,
“Eeeeh wewe mzee usiye na haya kimekuleta kipi hapa nyumbani kwangu?”
“Nimekuja kumuangalia Erica”
“Hatuna haja ya wewe kuja kumuona, sikia nikwambia yani nakuchukia wewe mzee basi tu naomba uondoke nyumbani kwangu”
“Unanichukia bure ila jua mimi ndio mkweo”
“Huwezi kuwa mkwe wangu kamwe, siwezi kukubali mwanangu aolewe na mzee kama wewe”
Mama Erica akafunga mlango na kuingia ndani, kwahiyo mzee Jimmy aliamua kuondoka ila kuna mzigo aliacha mlangoni kwakina Erica.
Muda kidogo alifika Erick kwa lengo la kuaga, akaona bahasha mlangoni kwakina Erica, akaichukua na kuifungua akaona ina hela na kuna karatasi limeandikwa ‘Nakupenda sana Erica’



Sepa nayoooo.......!!!!!!
Mama Erica akafunga mlango na kuingia ndani, kwahiyo mzee Jimmy aliamua kuondoka ila kuna mzigo aliacha mlangoni kwakina Erica.
Muda kidogo alifika Erick kwa lengo la kuaga, akaona bahasha mlangoni kwakina Erica, akaichukua na kuifungua akaona ina hela na kuna karatasi limeandikwa ‘Nakupenda sana Erica’
Erick alisoma mara mbili mbili ule ujumbe ila kwa haraka haraka akajua umetumwa na Rahim maana Rahim ndio alifukuzwa hapo kwakina Erica, kwahiyo akahisi kutumia njia hiyo ili aweze kumpata Erica maana kwajinsi alivyomsoma mama yake Erica alionekana kupenda hela kwahiyo alihisi lazima Rahim katumia njia hiyo ili aruhusiwe kwenda tena kwakina Erica, basi akaamua kuweka kwenye begi lake ambalo huwa anatembea nalo, kisha akagonga kwakina Erica ambapo mama yake Erica alienda kufungua huku akiongea,
“Umerudi tena weee mjinga”
Alipofungua akakutana na Erick, kidogo huyu mama alihisi haya, Erick alimuuliza,
“Kwani kuna nini mama?”
“Hakuna kitu mwanangu, karibu”
Akamkaribisha ndani, ambapo Erick alikaa na kuongea ongea kidogo tu maana Erica alikuwa amelala, kisha akaaga na kuondoka.
Alipofika hotelini yani alijikuta akimchukia Rahim huku akisema,
“Kwanza kaniharibia Erica wangu, kamuongopea na kumzalisha bila malengo halafu sasa anataka tena kumchukua, siwezi kukubali hilo jambo hata kidogo. Huyu Erica ni wangu tu”
Akatoa ile bahasha na kuhesabu zile hela, akakuta zipo milioni tatu, basi akaziweka tu pembeni akasema hampelekei ila atamwambia kuwa pesa zake alichukua yeye, kisha akampigia simu muda huo huo ila simu iliita tu bila ya kupokelewa, alipiga kama mara tatu haikupokelewa na kuamua kuachana nayo.
 
SEHEMU YA 375

Muda huo Rahim alikuwa hospitali maana ilibidi ampeleke mkewe hospitali baada ya kile kipigo cha haja, mama yake Rahim nae alikuwa hospitali ila walihonga madaktari ili Yule mgonjwa ijulikane alianguka na sio kupigwa.
Mrs.Peter alirudinyumbani na mwanae kwenye mida ya saa tano usiku ila muda huo huo hakujali kama muda umeenda wala nini, aliamua kuongea na mwanae,
“Hivi Rahim umeanzaje kumpiga mwanamke? Hivi unajua kama mwanamke hapigwi? Na kumpiga mwanamke ni dhambi?”
“Sikia mama, laity ningekuwa najua kuwa wanawake wa kutafutiwa wako hivi kwa hakika nisingekubali baba anitafutie Salma, kuna wanawake wengi tu nilikuwa nawaona, wenye tabia njema ila sio tabia kama za huyu Salma”
“Mwanangu, Salma hana matatizo ila unajua nini? Hakuna mwanamke duniani asiyekuwa na tabia za kike sema cha muhimu ni kumrekebisha, hata huyo unayemdhania ndio angefaa sana bila kumrekebisha hafai, na kumrekebisha mwanamke sio kumpiga, ni kumwambia tu kuwa hiki sipendi na hiki sipendi”
“Mama hujui tu, ni mengi naficha ya huyu mwanamke, kipindi kile nimerudi nilikaa nae kwa siku chache tu hata wiki haifiki ila safari hii nimeishi nae sana, kwakweli kanichosha”
“Kwani kipi hupendi kwa Salma? Maana mimi nilimuona kuwa ni msichana mzuri na aliyetulia kwani kipi hupendi kwake?”
“Mama, Salma ni msichana mbishi na hataki kuelekezwa hata umwambie nini haelekezeki, mara nyingi nimemwambia sipendi dawa za kuchoma choma zenye harufu mbaya, angekuwa anachoma udi nisingekuwa nagombana nae maana una harufu nzuri lakini sijui alikuwa na dawa gani zinaacha harufu mbaya kwenye nyumba anadai ni kinga kaletewa na ndugu zake kumkinga na mimba na mtoto atakapozaliwa. Nikavumilia, ukimwmbia kitu anataka mabishano yani kwenye nyumba haijulikani mwanamke nani mwanaume nani, namuangaliaga tu. Leo mapema nilimpiga kidogo na ndio ilikuwa mara ya kwanza kumpiga sababu ya majibu yake ya shombo na kuja mwilini nimpige, na jioni ile nimemkuta kajifungia ndani akichoma dawa gani sijui huku akiongea ongea maneno ya ajabu, mama siwezi kuishi na mwanamke mshirikina kama huyu”
“Sasa unatakaje?”
“Mama nampa Salma talaka, bora nioe mwanamke mwingine”
“Usiniambie unataka kumuoa Erica, eeeeh!”
“Erica nae ni mwanamke mama, naweza nikamuoa hata yeye”
“Hebu niondolee wazimu wako mie, Erica ni mwanamke ndio ila hana heshima hata kidogo yani hapa atatembea hadi na baba yenu, simtaki huyo mwanamke. Na kama unawazo la kumuacha Salma ili uoe huo uvchafu wako unisahau kabisa kama mimi ni mama yako”
Rahim aliondoka na kumuacha mama yake pale, kisha yeye kwenda kulala tu.

Kulipokucha mapema kabisa, simu ya Erica ilianza kuita ikabidi tena Bite apokee simu ile ya mdogo wake maana namba ilikuwa ngeni pia,
“Mzee Jimmy anaongea hapa”
“Mbona jana sikukuona tena?”
“Nilikuja ila mama yenu alinitimua”
“Aaaah kumbe ndio wewe asiyekutaka mama”
“Ndio mimi ila ananichukia bure tu kwa makosa ya miaka ya nyuma kabisa, mwambie hata maandiko yamesema samehe sabab mara sabini. Ila siyo lengo hilo, lengo ni kuwauliza kuwa ule mzigo nilioacha jana mlangoni mmeupata?”
“Mzigo? Hapana bhana hakuna mzigo tulioupata”
“Kuna mzigo niliacha jana, niliacha pesa kwenye bahasha kiasi cha milioni tatu”
“Mmmh ngoja niulize”
Bite akaenda kumuuliza mama yake maana kwa muda huo ndani walikuwa wawili tu,
“Mmmmh mbona nje mimi nimefagia sijaona kitu”
“Anasema eti aliacha mlangoni”
“Sasa nani achukue? Ingekuwa getini sawa, sasa mlangoni nani achukue?”
Bite akawaza jambo na kumuuliza mama yake,
“Kwani huyo mzee na Erick nani alitangulia kuja?”
“Yule mzee ndio alitangulia na alivyoondoka tu, muda kidogo ndio akaja Erick ila jana hajakawia sana kuondoka”
“Mmmmh nina hisia mbaya mama, sio Erick kachukua hizo hela kweli?”
“Mmmh mwanangu, Erick hana hiyo shida, yani nakataa kabisa, yani Erick achukue milioni tatu za nini? Hana hiyo shida Erick, labda huyo mzee muongo”
“Hapana mama, nina hisia ni Erick tu. Kwanza Yule kijana mdogo unamsifia ana hela, anatoa wapi hizo hela kijana mdogo vile? Mama mara nyingine kuwa makini, isije kuwa Yule kijana ni mwizi au anauza madawa ya kulevya, tunafurahia hela zake hapa kumbe tunachukua hela haramu mama yangu, kuwa makini”
“Kheee na wewe Bite, kwani James ni mkubwa? Mbona ana hela?”
“Ila sio hela nyingi kama za huyu kijana unazosema, James familia yake inajiweza, James ana kampuni yake kaachiwa na baba yake, huwezi kumfananisha na huyo Erick, hatujui ndugu zake, hatujui rafiki zake wala jamii yake, hizo hela anazitoa wapi?”
“Yule Erick nae familia yake ina hela, Yule kijana usimuingize katika hizo biashara haramu wala nini, na hawezi kuchukua hela za huyo mzee. Mwanangu huyo mzee humjui tu ila huyo mzee hafai hata kidogo, kwanza usikute ni muongo na wala hajaacha hizo hela na kama ameacha kweli basi zimesombwa na upepo ila swala la kusema Erick kachukua halipo kabisa”
“Mmmh sawa mama, nakubaliana nawe”
Hakuweza kubishana zaidi na mama yake ila kiukweli Bite hata alitamani nusu ya upendo aliokuwa nao Erick ndio ungekuwepo kwa James maana mumewe kuanza kumpenda yeye ni mpaka asemwe na watu.
 
Back
Top Bottom