Simulizi: Nini maana ya mapenzi

Simulizi: Nini maana ya mapenzi

SEHEMU YA 208

Alivyofika kwao alishangaa kuna ugeni, alishangaa kumuona kaka yake ambaye kwa siku nyingi sana alikuwa akiishi kwa mjomba wao, alimsogelea na kukumbatiana kwa nguvu na kaka yake,
“Kheee Erica mdogo wangu umekuwa mkubwa jamani hadi una mtoto! Wakati kaka yako wala sina”
Erica alikuwa akitabasamu tu, kisha kumkaribisha vizuri kaka yake nyumbani,
“Kaka Tony, karibu sana ndio ulizamia Arusha jamani utafikiri ulikuwa nchi nyingine ambavyo hukutaka kurudi nyumbani. Karibu sana”
Walifurahiana nae na kuongea mambo mbalimbali kwa furaha kisha Erica aliinuka na kwenda chumbani kwake, alifunga mlango wa chumba chake kwani alikuwa na mawazo sana na alihitaji apate hata muda kidogo wa kulia.
Alivyojifungia mlango alianza kulia huku akijilaumu jinsi alivyoyafanya maisha yake, maneno ya mama yake kuwa yeye ndiye aliyekuwa na uwezo wa kuchagua maisha yake yalimrudia akilini na kuanza kujisemea,
“Kama mimi ndio nilikuwa na uwezo wa kuchagua maisha yangu, mbona maisha yangu nimechaguliwa? Nilikuwa nawasiliana vizuri sana na John hadi tukaahidiana mambo mbalimbali ila kitendo cha mimi kusahau simu mezani ikawa ndio mwisho wa mawasiliano yangu na John kwani hata niliporudi bado majanga, mama alisema simu kaitumbukiza kwenye maji na laini imevunjika. Sikuweza kuwasiliana tena na John. Kumbe alinitafuta sana, huenda ndio angekuwa mume wangu na wala yote haya ya kukutana na watu wa ajabu ajabu yasingetokea, mama yangu kachangia pakubwa sana kuharibu maisha yangu ila hataki tu kukubali ukweli. Asingeleta vurugu shuleni wala usikute hadi leo ningekuwa na Erick na wala nisingetangatanga na wanaume, akaniharibia kwa Erick, akaniharibia kwa John na pia akaniharibia kwa Bahati halafu bado anajitoa kuwa hakuna alichoharibu kwangu eti nimejiharibia mwenyewe”
Akainama tena na kulia sana, ila muda huu alikuwa hajamchukua bado mtoto wake, kwahiyo mama yake alienda kumgongea ili amchukue mtoto wake, Erica alifuta machozi na kwenda kufungua mlango,
“Kheee nimekusikia saa nyingi sana kuwa umerudi na ulikuwa ukiongea na kaka yako, kumbe hujaoga hata kuoga! Hebu nenda kaoge huko umnyonyeshe mjukuu wangu, sio umnyonyeshe na majashojasho yako ya huko njiani”
Erica alienda kuoga ila bado alikuwa na mawazo sana, kwani kimsingi maisha yake mengi yameharibika na chanzo kikubwa ni mapenzi, na sasa alikuwa akihitaji mtoto wake apate malezi ya baba na mama, ila atajielezeaje kwenye familia ya John kuwa alikuwa na mahusiano na Rahim yani hapo ndio palimshinda na kumfanya hata siku hiyo ashindwe kujieleza maana kilishatokea kitu cha kumuwekea pingamizi.



 
SEHEMU YA 209


Usiku wake alijaribu tena kuingia kwenye mtandao, ila leo alimkuta Rahim yuko hewani. Kabla hata ya salamu, Erica alimuuliza Rahim swali kwani hakuona umuhimu wa salamu,
“Kwahiyo ndio umemaliza honeymoon leo umekuja hewani sio?”
“Honemooy ipi Erica? Unajua mara nyingine sikuelewi yani unatoaga lawama tu”
“Si ulishaoa kwahiyo ulikuwa kwenye mapumziko ndio leo umekuja hewani”
“Sasa nimemuoa nani?”
“Si umemuoa Salma wewe”
“Hivi Erica una tatizo gani kwani? Huyo Salma hata kumuona kwa macho sijawahi zaidi ya kutumiwa picha zake, sasa kumuoa nimemuoa saa ngapi? Au umeanza tena maongezi na mama yangu kwahiyo kashakuchanganya akili!”
Erica akaona atumie nafasi hiyo hiyo kumwambia kuwa alikutana na mama yake na kamuhakikishia kuwa ameoa,
“Mama yako mwenyewe kanihakikishia kuwa umeoa”
“Si ungemwambia akupe picha za harusi uzione, unajua wanawake msiwe na tabia ya kukurupuka. Hujauliza kuwa nilikuwa na tatizo gani, mbona sikupatikana siku zote hizo ila wewe unakuja tu kuniparamia na lawama eti sijui nimeoa nimetoka honeymoon, Erica mke gani wewe mwenye lawama kila kukicha?”
“Haya basi ulikuwa wapi?”
“Ungeanza na swali hilo mwanzoni ndio ningekujibu ila kwasasa siwezi kukujibu wakati swali nimekupa mwenyewe. Vipi mwanangu anaendeleaje?”
“Hivi wewe Rahim unajua ni kwajinsi gani unaumiza moyo wangu? Unajua unavyonitesa?”
“Nakutesa kwa lipi? Je nilikataa mimba? Hapana, je nimekataa mtoto? Hapana, sasa nakutesa kwa lipi. Mbona hutumii akili Erica”
“Kwahiyo unaona unachofanya ni swa? Yani mimi sielewi hatma yangu, sijui kama nitaolewa na wewe au la, yani umenifanya niwe njiapanda”
“Kwani Erica jamani una miaka mingapi hadi uwe na mawazo ya ndoa kiasi hiko? Si nilishakwambia kwenu nitakuja kwani wewe tatizo ni nini jamani? Kwani sikutumii hela za kumtunza mtoto? Unataka nini sasa? Unajua nilijua nimepata mwanamke mwanachuo atakuwa anajitambua sana ila kitendo cha kuona bado hujitambui Napata shida ya kuelewa shahada uliyochukua”
yani majibu ya Rahim yalikuwa yakimtia hasira Erica hata akatamani angekuwa karibu maana sio kwa kumtia hasira vile kwa majibu yale,
“mapenzi hayana usomi, unaniumiza Rahim”
“Nilishakwambia kaa mbali na mama yangu, Yule mama atakupa kichaa bure. Nimeambiwa kuwa mdogo wangu John alikuwa anamvalisha mchumba wake pete ndio wakafanya sherehe, ila wewe uliambiwa mimi naoa loh! Ni maswala ya ajabu hayo Erica, narudia tena kaa mbali na mama yangu. Atakuchanganya akili Yule mama”
“Kiukweli Rahim sikuelewi yani sikuelewi kabisa”
“Naomba ulale na ukiamka utanielewa kwa urahisi zaidi ila hivyo unavyobisha tu itakuwa ngumu sana kunielewa”
Erica alituma ujumbe mwingine ila hakujibiwa na Rahim, ilibidi tu alale huku akiwa amechukia vilivyo moyoni mwake maana aliona kama Rahim anamfanyia vitu vya makusudi.
Alilala huku akiwa na mawazo mbalimbali kuwa pengine mambo yake katika maisha yatabadilika.


 
SEHEMU YA 210

Kesho yake alifika James nyumbani kwakina Erica, akiwa ameongozana na Mage, alikuwa na lengo la kuomba msamaha ila kiukweli Bite aligoma kabisa kuongea nae, aliwakuta sebleni ila Bite hakuitikia hata salamu yake.
Ila James alishangazwa kumkuta Erica na mtoto akicheza nae sebleni, aliuliza kwa mshangao,
“Mtoto wa nani huyo Erica?”
“Wa kwangu”
“Kheeee kumbe Erica una mtoto? Mbona mimi sijui”
Hapo ndio Bite alipomjibu mume wake,
“Utajulia wapi na siku zote upo busy na malaya wako”
Ikabidi Mage aingilie maana alijua ni mzozo mwingine utaibuka,
“Mmmh Bite mdogo wangu jamani, hata kama mtu kakukosea vipi ila usimwambie maneno makali hivyo”
“Sasa neno kali nillolitamka ni lipi? Kumwambia ukweli ndio neno kali?”
“basi yaishe, ila pokea msamaha wa mwenzio”
“Sitaki, tena naongea mbele ya wote hapa. James kuanzia leo mimi na wewe basi”
“Bite, kumbuka tumefunga ndoa ya kanisani na tulikula kiapo kuwa hatutaachana mpaka kifo kitakapotutenganisha”
“Usinibabaishe na hayo maneno, ambacho hutaachana nacho mpaka kifo ni mwili wako tu ila sio mimi tena unikome”
Ilibidi Mage amtoe kidogo James na kwenda kuongea nae kuwa arudi siku nyingine maana inaonyesha Bite bado alikuwa na hasira sana.
Ila kabla James hajaondoka aliomba kidogo kuongea na Erica, na aliongea nae jambo moja tu,
“Erica nitakutafuta ili unisaidie swala la kurudiana na mke wangu, najua wewe unajua kuwa mimi nifanye nini ili Bite akubali”
“Sijui mimi, hebu nipishe wasije hisi unanitongoza tena bure”
“Erica najua unajua, na nitakutafuta tu”
Kisha James aliondoka zake, na Erica kurudi ndani ila dada yake alimkata jicho hilo ambalo lilimtisha na kumwambia dada yake,
“Mbona unaniangalia hivyo dada?”
“Ngoja utakapoolewa halafu ufanyiwe ninayofanyiwa mimi na James uweze kuona moyo wako unavyokuwa”
Erica alikuwa kimya tu kwani bado kuolewa ila moyo wake ulikuwa na maumivu ya hali ya juu maana hata hakujua kuwa ni nani atakayemuoa.


ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 211



Baada ya wiki kaka yao aliwaita ndugu zake wote na kuwaeleza dhumuni la kwenda nyumbani kwao kwa kipindi hiko,
“Jamani nimepata mchumba, nikaona ni vyema nije kumtambulisha nyumbani”
Walimpa hongera pale, na mama yake akamwambia kuwa ni uamuzi wa busara kumtambulisha mchumba wake, kwahiyo aliwaambia kuwa Jumamosi ya wiki hiyo ndio wajiandae kumpokea huyo mgeni ambaye ni mchumba wake, basi wakafurahi na kusema kuwa watajiandaa.
Siku ya Jumamosi, walikusanyika wote nyumbani yani mama yao, Mage, Bite na Erica huku wakimsubiri kaka yao amlete huyo mchumba aliyempata.
Muda kidogo kaka yao alifika na mgeni na kuanza kumkaribisha, muda huo Erica alienda chumbani kumlaza mtoto wake, ila aliposikia mgeni amefika alimlaza haraka mwanae na kwenda kumuona mgeni.
Alipofika tu sebleni alishangaa akigongana macho kwa macho na Dora, kwahiyo Dora ndio mchumba wa kaka yake.


Muda kidogo kaka yao alifika na mgeni na kuanza kumkaribisha, muda huo Erica alienda chumbani kumlaza mtoto wake, ila aliposikia mgeni amefika alimlaza haraka mwanae na kwenda kumuona mgeni.
Alipofika tu sebleni alishangaa akigongana macho kwa macho na Dora, kwahiyo Dora ndio mchumba wa kaka yake.
Erica alimtazama Dora na kuanza kucheka sana hadi ndugu zake wakamshangaa kuwa imekuwaje, mama yake akamuuliza,
“Vipi Erica, mbona unacheka hivyo baada ya kumuona mgeni?”
Muda huu Dora alikuwa akitazama chini tu, kisha Erica akasema,
“Ukisikia usiyempenda kaja ndio leo loh!”
“Erica hatukuelewi”
Erica akamsogelea Dora, na kuinama alipo kisha akapitisha mkono wake na kumshika tumbo halafu akamuuliza,
“Vipi shoga yangu, ile mimba ulishaitoa?”
Familia nzima ilikuwa ikishangaa tu, hakuna aliyeelewa haswa Tony na ilimbidi amuulize Erica kwa hasira,
“Wewe Erica, mbona unamfanya hivyo wifi yako jamani? Mbona unakosa heshima wewe?”
“Kaka sikia, huyu mwanamke sio mara ya kwanza kumuona huyu Dora namjua vilivyo tena alikuwa rafiki yangu”
Kisha akamuangalia mama yake na kuwaangalia dada zake na kusema,
“Jamani huyu ni mtu aliyefanya nione chuo kichungu, huyu ndio alipanga na watu wanibake ila hawakufanikiwa nab ado akatangaza chuo kizima kuwa nimebakwa. Kaka kama unaamua kuishi na huyu mwanamke ni juu yako ila nakwambia ukweli huyu mwanamke ni shetani”
Mama yao akamuuliza swali Erica,
“Na mimba uliyomuuliza ni ipi?”
“Huyu Dora nimekutana nae hivi karibuni tu, alikuwa anatafuta daktari wa kumtoa mimba akidai kuwa kabeba mimba bila kutarajia na kapata mchumba sasa itakuwa so huyo mchumba akijua, dah inaniuma sana kuona mchumba mwenyewe ni kaka yangu jamani! Kaka hivi hujaona wanawake wengine kweli?”
Dora alikuwa ameinama ila aliinuka bila kuongea na yeyote na kutoka nje, yani ni Tony ndiye aliyeanza kumfata nyuma Dora huku akimuita ila Dora hakuitika kwani kiukweli alishaaibika.
Ikabidi Tony aendelee tu kumfata Dora ili akazungumze nae.

 
SEHEMU YA 212

Ndani walibaki wenyewe kwenye familia huku wakisikitika yale mambo waliyoyasikia,
“Jamani Erica, usingekuwa unamjua huyo msichana si ndio kaka yako angekuwa anadumbukia kwenye mdomo wa mamba?”
“Kweli mama,yani Erica asingemjua wala tusingekuwa na wasiwasi nae maana anaonyesha ni mpole kweli”
“Hata mimi nilipoanza urafiki nae chuoni nilijua ni mpole yani hata sikudhania kama ana mambo ya ajabu kiasi hiki, ila jamani mama na dada zangu mambo ya mapenzi yalivyo utashangaa kaka anapewa uongo na Yule mwanamke hadi sisi tunaonekana wabaya”
Bite akacheka na kumwambia Erica,
“Kweli umekuwa mdogo wangu naona unaanza kuelewa maana ya mapenzi, yani mapenzi bhana ni kweli usemayo yani inawezekana wote tukaonekana maadui hapa sababu ya mtu mmoja tu. Ila bora umesema mdogo wangu ili leo na kesho likibumbuluka tutamwambia si tulikwambia, ila usingesema ingekuwa ni lawama tu kwanini hukusema”
Walijadiliana pale ila hawakujua kilichoendelea kwa kaka yao, ila mama yao alionekana kuwa na misimamo yake ya kumkataa huyo msichana hata iweje, ili mradi tu kajua kuhusu huyo mwanamke hamtaki tena.
Jioni ilifika kisha Mage akaondoka na kuwaacha wakibaki wenyewe pale nyumbani, wakaendelea na maongeze mengine na usiku kufika wakalala ila Tony hakurudi.

Kesho yake wakiwa wanajadiliana kuwa Tony mbona hakurudi nyumbani ndio alifika, kwakweli mama yao alimsema sana maana hakupendezewa na lile jambo kabisa.
“Mama jamani, nampenda Dora na hana tabia hizo, huyu mwanao Erica anamsingizia tu”
Erica akadakia,
“Nilijua tu, ila kaka kama ukiamua kujiweka kwenye mdomo wa mamba shauri yako ila mimi nishakwambia ukweli”
Mama yao aliendelea kuongea,
“Tony, huyo mwanamke simtaki katika nyumba yangu yani simtaki kabisa na kama unaamua kumuoa basi utajuana na mjimba wako ila huyo mwanamke simtaki”
“Mama jamani, kwanini mnanifanyia hivyo? Erica aliyekutia aibu hapa kwa kuzaa nyumbani wala huna tatizo nae ila mimi ninayeweka heshima kwa kumtambulisha wangu humtaki”
“Hivi wewe mtoto uambiwe vipi jamani eeeh! Tushakwambia Yule msichana hakufai, au mpaka siku akuletee mtoto wa kipemba kama dada yako ndio akili ikukae sawa. Haya na jana ulilala wapi?”
“Mmmh nilijua tu, muulizeni dada Mage, nililala kwake”
Kisha akainuka na kwenda chumbani kwake, kwakweli mama yao aliona Erica na kaka yake ni watu wanaomchanganya sana akili.

 
SEHEMU YA 213

Siku hiyo walimuita tena Tony kuongea nae habari za kusema Dora hawamtaki, ila na yeye alionekana kuanza kuelewa elewa,
“Mama, jana sikuwaaga ila nilienda kwakina Dora dah nimemkuta na mwanaume amesimama nae halafu mazingira sikulizika nayo kabisa, eti kaniambia ni kaka yake mmmh Napata shida kwa huyu mwanamke ila nampenda”
“Sitaki hiyo habari ya kumpenda huyo mwanamke asiyefaa”
Tony akainuka na kuondoka, mama yao akamtazama Erica sasa, ikawa zamu ya Erica, kama kawaida yake hakuacha kuongelea swala la mume wa Erica,
“Haya wewe mtoto, huyo mwanaume anakuja lini?”
Hili swali huwa linammaliza nguvu kabisa Erica, yani huwa anakosa raha akiulizwa swali la namana hii, muda ule ule alinyong’onyea na kumfanya mama yake aongee
“Nilijua tu utanywea, hivi Erica unataka sura yangu hii niiweke wapi? Tunafanya siri kila kukicha, hivi mtoto ana siri? Unafikiri watu hawajui kama una mtoto? Shida sio kwa majirani ila ndugu wakijua, jamani nitaweka wapi sura yangu mimi? Erica, fanya juu chini umlete huyo mwanaume, ni afadhali wakigundua niseme mwanaume yupo kuliko hivi. Umenisikia”
“Sawa mama”
“Yani sio unanijibu sawa tu, kinachotakiwa ni vitendo. Waje hapa wajitambulishe na kumuona mtoto wao, waniambie hatma yako kwa huyo mwanaume. Inamaana huyo mwanaume hana ndugu jamani, maana hatujawahi kuona ndugu yake wala rangi ya ndugu yake”
Muda kidogo mtoto wa Erica aliamka na leo alitoka mwenyewe hadi sebleni, Bite alisema,
“Kheee Angel mjanja jamani yani katoka mwenyewe chumbani kuja sebleni”
Mama yao akadakia,
“Sio ujanja tu, hiyo ni kuonyesha kama mtoto amekua. Huyu Angel amekua sasa”
Erica akamchukua mwanae na kumpakata, mama yake akasema,
“Erica, hivi huoni aibu? Mtoto anazaliwa, anakaa, anatambaa na sasa anatembea na wiki ijayo anaenda kufunga mwaka ila hakuna mwanaume wala rangi yake. Hapo ulipo hata mahafali ulishindwa kuhudhuria sababu ulikuwa unanyonyesha, Hivi iko wapi elimu yako? Iko wapi sifa yangu ya kusema mtoto anasoma? Umenitia aibu Erica, haya huyo mwanaume yupo nje, ndugu zake je? Huyo mwanaume hana ndugu? Basi sio binadamu wa kawaida kama hana ndugu. Kiukweli umenitia aibu Erica jamani yani umenitia aibu balaa, haya baba wa mtoto yuko wapi? Yani sitaacha kuuliza swali hili hadi nitakapomuona. Nilikuuliza toka mtoto mchanga ukanijibu atakuja, atakuja hadi leo kimya na wiki ijayo mtoto anatimiza mwaka ila baba hola, aua ulidanganyika siku ile niliposema kuwa Yule muuza samaki ndio baba Angel? Kama umekubaliana nae basi mlete ajitambulishe rasmi na akuoe maana sina muda wa kukwambia mwanaume gani anafaa kukuoa kwasasa, ukizingatia ushaharibu maisha yako. Fanya ufanyavyo ila nahitaji kumjua baba wa huyu mtoto. Erica, mtoto anahitaji malezi ya baba na mama, hivi hutamani ukiona baba na mama wameongozana wakiwa wamebeba kitoto chao hutamani? Erica nahitaji jibu, huu mwezi usipite mwanangu, huyu mtoto amekua sasa sio muda wa kucheleweshana huu. Nadhani umenielewa”
“Nimekuelewa mama”
Erica alikuwa mpole sana na kuinuka na mwanae kisha kwenda nae ndani, ila alipoingia chumbani kwake alijifungia na kulia kama kawaida ingawa alijua wazi kilio chake hakimsaidii kitu.
Alilia sana na kujikuta akilaumu sana kuhusu Rahim, ingawa maneno ya mama yake yalimchoma ila kuna muda aliona kuwa mama yake alikuwa na ulazima wa kuyasema maana asingeweza kuacha mwanae ateketee.

 
SEHEMU YA 214


Usiku wake kama kawaida alianza kumtafuta Rahim hewani maana akisemwa semwa ndio anapoteza raha kabisa, alimtafuta na kumkuta tu hewani akamtumia ujumbe maana siku hizo ilikuwa tofauti na zamani kuwa Rahim ndio alikuwa anamtafuta Erica, kwa siku hizo ni Erica ndio wa kumtafuta Rahim tena anaweza kutuma jumbe hata nne ndio akajibiwa, ile kitu ilimuumiza sana Erica.
“Rahim kwanini lakini unanifanyia hivyo jamani! Lini utakuja kumuona mtoto?”
“Erica, kwani kitu gani unataka haswaa maana huwa sikuelewi”
“Rahim jamani, kumbuka sisi ni wazazi. Na mtoto anahitaji mapenzi ya baba na mama”
“Kwani niliwahi kukwambia simpendi huyo mtoto?”
“Hapana Rahim sio hivyo, ila mbona umebadilika sana jamani Rahim yani sio Yule ambaye nilikujua jamani”
“Erica, hebu zungumza unachotaka kusema sio kuanza kueleza eleza vitu visivyokuwa na kichwa wala miguu. Sasa kitu gani ambacho nimebadilika mimi, mbona unaeleza vitu visivyoeleweka, wewe sema unataka nini kwangu. Maana kama pesa za kumtunza mwanangu huwa nakutumia haya kitu gani unataka”
“Rahim, kumbuka nimezaa nje ya ndoa na nyumbani hawakufahamu”
“Kwahiyo unataka nini?”
“Nataka nyumbani wakufahamu na unioe”
“Hahahaha unanichekesha Erica, unataka ndoa? Hiyo ndoa utaiweza wewe au unaitaja tu ilimradi umeitaja”
“Jamani Rahim kweli ndio maneno ya kuniambia hayo? Kuna mwanamke asiyeweza ndoa hapa duniani? Rahim, kumbuka ahadi zako kwangu, kumbuka uliniambia nini”
“Si nilikwambia ubadili dini nikuoe”
“Rahim, dini sio kigezo cha wewe kushindwa kunioa. Kuna ndoa za bomani, watu wanafunga na dini tofauti”
“Hahahah hivi sharia zetu unazijua wewe? Hebu ulizia vizuri uelezwe kama ulishawahi kuona mtu kama mimi kafunga ndoa ya bomani au kabadilisha dini. Hivi wewe ni mwanamke gani usiyemuelewa? Hujui kama mwanamke hana dini? Ukitaka nikuoe badili dini nikuoe mwisho. Kama hutaki jua kwamba hakuna kitu kinachoitwa ndoa baina yangu na wewe”
Erica aliona machozi yakitoka machoni mwake, alijisikia uchungu wa hali ya juu, kisha akabadilisha ujumbe wa kumwambia Rahim,
“Sawa, nimekubali hakuna ndoa basi njoo nyumbani uonekane. Umuone mtoto na ndugu zangu wakufahamu, mama ananiuliza sana maana hata ndugu zako hujawaambia kuhusu mimi na mtoto una maana gani?”
“Ila nilishakwambia mama yangu alivyo, yani siwezi kumwambia mama aje kwenu maana namjua vizuri. Pili mimi nitakuja tu, sasa usinipangie siku ya kuja, jua nitakuja tu. Huyo mtoto sijamkataa, ni wangu na ninampenda kwahiyo nitakuja tu hata usiwe na mashaka kuhusu swala la mimi kuja”
“Kwahiyo ni lini?”
“Nimekwambia Erica usinipangie, nitakuja tu”
Hapa Erica alipumua na kuweka simu pembeni maana alianza kulia tena na alilia hadi alihisi kichwa kumuuma na kujiona kama ametupwa duniani na hana uelekeo kabisa, alikosa raha.
Akikumbuka maneno ya mama yake, na akiwaza kile alichoambiwa na Rahim alihisi kupata kizunguzungu kabisa, alilia sana na kulala huku akilia kwani hakuweza tena kuongea na Rahim alihisi kuendelea kuumia tu.
 
SEHEMU YA 215


Asubuhi palivyokucha ni dada yake alienda kumgongea mlango na kisha kuinuka na kufungua, Bite aliingia ndani na kumuangalia mdogo wake akamuuliza,
“Nini tatizo Erica, mbona macho yamekuvimba hivyo?”
“Hakuna tatizo dada”
“Hakuna tatizo wapi, ulikuwa unalia wewe”
Erica alikuwa kimya tu na kukaa kitandani kisha Bite nae akakaa kitandani na kuendelea kuongea na mdogo wake,
“Erica mdogo wangu, unalizwa na maneno ya mama kweli? Yani unakosa raha sababu ya maneno ya mama jamani?”
“Hapana si maneno ya mama”
“Basi kipi kinakuliza”
Erica alijikuta akianza tena kulia maana alishindwa kujizuia na kusema,
“Dada, nakubali kuwa nimefanya makosa tena makosa makubwa sana ila dada sikutegemea kama ingekuwa hivi katika maisha yangu. Yani mama anahitaji niolewe ila mwanaume hataki kunioa, ina niuma dada tena inaniuma sana”
“Usiumie mdogo wangu, wala sijaona sababu yaw ewe kuumia. Bado mdogo wewe, huyo mwanaume mwache aende zake na utapata mwingine wa kukuoa. Halafu usikimbilie ndoa mdogo wangu, zina mambo mengi sana yani unaweza hadi kuchanganyikiwa sababu ya ndoa. Niangalie dada yako, si niliolewa mimi na harusi na vigelegele kabisa ila kiko wapi? Hata nikirudi bado nitakuwa na maumivu moyoni, mdogo wangu wewe ni binti mdogo, angalia maisha yako. Ukikosea usikae kwenye makosa ila inuka na usonge mbele”
“Sasa nitasongaje mbele dada? Mwanaume hataki hata kujionyesha nyumbani”
“BHivi wewe si kuna Yule muuza samaki, ongea nae aje yeye kujitambulisha kama unahisi kupungukiwa na kitu ila ningekuwa ni wewe hata nisingeusumbua moyo wangu”
Maneno ya dada yake kidogo yalimtia moyo, na dada yake akamtaka akaoge ili awe na nguvu na aweze kumuogesha mwanae na kumlisha, kwahiyo alifanya hivyo na kuwa na nguvu.
 
SEHEMU YA 216

Mchana aliamua kuwasiliana na Bahati, ila kabla hajaongea nae lengo lake Bahati akamwambia,
“Erica, tena bora umenipigia maana kuna jambo nataka kukwambia”
“Jambo gani hilo?”
“Nimeshawaambia ndugu zangu kuwa nimezaa na wewe, na wanataka kuja kumuona mtoto”
Erica akafikiria kwa muda kuwa itakuwaje, kisha akamuuliza Bahati
“Kwanini umechukua uamuzi huo wakati unajua mtoto sio wako Bahati?”
“Mtoto wako wewe ndio wangu Erica, kumbuka mimi ni mwanaume wako wa kwanza kwahiyo lazima nichukue jukumu hilo. Erica, nishawaambia ndugu zangu naomba usiniaibishe mpenzi wangu. Ndugu zangu wote wanajua nimezaa na wewe mtoto wa kike, mama amefurahi sana hata zile tofauti na wewe zimeondoka, naomba waje kumuona mtoto”
“Sasa ndugu zako hawatashtuka kama tunawadanganya Bahati?”
“Erica, kitanda hakizai haramu. Nahitaji kukuoa tena swala la mtoto itakuwa ndio kigezo kikubwa sana maana nitasema nataka kumuoa mama wa mtoto wangu. Erica, huyo mtoto ni wa mimi na wewe, haijalishi yukoje ila ni mtoto wetu”
“Sawa kama umeamua hivyo”
“Nakupenda Erica, tafadhali mwambie mama kuwa keshokutwa nakuja na ndugu zangu kumuona mtoto na tutajitambulisha siku hiyo maana nitakuja na mshenga kabisa na barua ya kuomba mke”
“Sawa nitamwambia”
“Nakupenda sana Erica”
Kisha wakamaliza yale maongezi, kwa upande wa Erica alijihisi amani kidogo kwenye moyo wake kwani kwa wakati huo hakuangalia kupenda sana wala nini, ilimradi mtu afike kwake na lengo la kumuoa basi huyo alimfaa.
Alipomaliza kuongea nae, alienda kumwambia mama yake kuhusu ujio wa Bahati na barua ya uchumba,
“Kwahiyo huyo ndio baba Angel?”
Erica alikuwa kimya, na mama yake akamuuliza tena,
“Huyo ndio baba Angel?”
“Ndio mama”
“Siri ya mtoto unayo wewe, ulisema baba yake anaitwa Rahim, saivi Bahati unataka kutupiga changa la macho kwa Yule muuza samaki eeeh! Au umemdanganya mtoto wake!”
Erica alikuwa kimya tu, mama yake akasema tena,
“Sawa nimekubali, ila tutakuwepo familia tu hapa. Nitawaambia dada zako basi, tutakusanyika hiyo keshokutwa kuwapokea”
Kitu ambacho hakumueleza mama yake kuwa wanakuja na kumuona mtoto ila alimwambia tu wanakuja kujitambulisha.
 
SEHEMU YA 217

Usiku wake aliamua tena kumtafuta Rahim hewani, akamsalimia leo na kumuuliza,
“Rahim, kwahiyo unaniruhusu niolewe na mwanaume mwingine?”
“Hahaha hebu usinichekeshe Erica, nikupe ruhusa au nisikupe kwani nimekuoa? Mwenye maamuzi ni wewe mwenyewe ila mimi siwezi kutoa maamuzi juu yako”
“Rahim, hivi huna wivu hata kidogo na mimi?”
“Erica, hata nikiwa na wivu itasaidia nini? Niko mbali mie sasa unadhani kuna ninachoweza kufanya? Wewe fanya unachoona ni kizuri kwako, ukiamua kuolewa haya, ukiamua kutokuolewa haya, ukiamua kunisubiri mie haya ila sikupi ruhusa yoyote maana mimi sio wa kukupa ruhusa wewe. Hiyo ruhusu ichukue kwenye moyo wako”
“Dah”
Erica aliona akidharaulika balaa na kila siku aliyoongea na Rahim alikosa raha kabisa, maana mawazo yalizidi maradufu kwake.
Alilala kwa shida sana usiku ule maana aligubikwa na mawazo, hata kesho yake usiku hakuweza tena kumtafuta Rahim kwani alijua atamuongezea mawazo maradufu.

Wote leo walitulia wakisubiri ugeni walioambiwa na Erica, na muda kidogo ugeni uliwasili, alikuwepo Bahati akiwa ameongozana na mbaba wa makamo kisha na mama yake Bahati na dada zake waweli. Mama Erica aliwakaribisha kwa vizuri kabisa, kisha kuanza kusalimiana nao na walionyesha kuwa na furaha tu.
Walikaa na Erica akaitwa, alitoka bila mtoto ila alipofika tu sebleni mtoto wake nae alimfata nyuma, na alikuwa ndio ameanza anza kuongea, Yule mtoto akawa anamuita Erica,
“Mama, mama”
Pale sebleni wote walikuwa wakimuangalia Angel, muda huo Bahati alionyesha tabasamu kubwa na kumwambia Angel
“Njoo mama”
Basi Angel akawa anamsogelea Bahati na alipofika pale Bahati alimuinua na kumpakata, ila kabla hawajafanya maongezi mengine alisikika mama Bahati akiuliza,
“Kwahiyo Bahati, mtoto wako mwenyewe ndio huyo?”
“Ndio mama, ndio huyu anaitwa Angel”
Huyu mama alisimama na kung’aka,
“Wewe mtoto hebu nitolee uchizi mimi, hata kipofu hawezi kudanganywa kuwa huyu mtoto ni wake maana hata akimpapasa nywele tu atajua si mtoto wake. Wewe mwenye macho mawili kabisa unaanzaje kusema huyu mtoto wa kiarabu ni wako?”
Wote walinyamaza kimya, Erica alishindwa hata aseme nini maana mambo kama yale aliyahisi tu.
 
SEHEMU YA 218

Huyu mama alisimama na kung’aka,
“Wewe mtoto hebu nitolee uchizi mimi, hata kipofu hawezi kudanganywa kuwa huyu mtoto ni wake maana hata akimpapasa nywele tu atajua si mtoto wake. Wewe mwenye macho mawili kabisa unaanzaje kusema huyu mtoto wa kiarabu ni wako?”
Wote walinyamaza kimya, Erica alishindwa hata aseme nini maana mambo kama yale aliyahisi tu.
Yule mama aliwaangalia ndugu zake na kusema,
“Tulihisi tu kuwa tunaenda kupigwa changa la macho maana huyu binti hawezi kuwa mkweli kamwe. Tuondokeni”
Kisha akamuangalia mwanae na kusema,
“Acha ubwege, weka mtoto chini twende”
Kiukweli hili swala hata Bahati hakulipenda kwani aliona kama amedhalilishwa, kwahiyo aliinuka na kutoka na familia yake nje maana ilikuwa ni aibu kwake na wala hakufikiria kama familia yake ingeweza kufanya kitu kama kile, haswa mama yake. Na wakati wanatoka, mama na dada zake Bahati walimuangalia Erica na kumsonya yani kila mmoja alikuwa akimsonya. Kitendo hiki kilimkera sana mama yake Erica, aliinuka na kuwazuia kutoka nje,
“Hivi nyie mmepata wapi ujasiri wa kuongea shombo zenu kwenye nyumba yangu? Na ubaya zaidi kumsonya mtoto wangu, kuna sababu gani nyie ya kumsonya mwanangu? Nawauliza? Kama mwenye matatizo hapa si kijana wenu na sio mtoto wangu, tena sikieni leo ndio iwe mwanzo na mwisho kwa nyie kukanyaga katika nyumba hii. Haya ondokeni”
Muda huu wakati mama Erica anaongea hakuna aliyethubutu kumjibisha maana hata ndugu wa Bahati waliogopa kuanza varangati kwenye nyumba ya mtu, wataonekana wakorofi ila kiukweli angekuwa kwenye eneo lao wangeanza kumchamba kama kawaida yao, mama Erica akawapisha watoke nao walitoka ila Bahati alirudi nyuma na kwenda kupiga magoti kwa mama yake Erica,
“Mama, naomba nisamehe mimi. Sio wale watakaoishi na Erica ila ni mim, nampenda sana Erica mama usinichukie mimi”
“Inuka na uende na nduguzo tafadhali”
“Mama nisamehe”
Mama Erica hakujibu na kwenda kukaa ila hakujua tabia ya Bahati kuwa anaweza akapiga magoti pale mpaka kesho yake asubuhi asipopewa jibu kuwa amesamehewa, na kweli ndugu wote wa Bahati na Yule mshenga walikuwa wameondoka ila Bahati alibaki amepiga magoti tu ndani kwakina Erica.
Bite alimfata mama yao na kumwambia kuwa Yule kijana bado kapiga magoti, mama yao alishangaa sana,
“Mpaka muda huu!”
Erica alikuwa akijiinamia tu ila swala la kusikia Bahati bado amepiga magoti ikabidi amuombe mama yake akamwambie kuwa amemsamehe aende,
“Kwahiyo wewe umeridhika na kile walichofanya ndugu zake?”
“Sijaridhika nacho mama, ila Bahati namfahamu mama. Yani anaweza piga magoti hapo hadi asubuhi”
“Kheee mkubwa”
Mama yao aliinuka na kumwambia Bahati kuwa amemsamehe na aende, ndipo Bahati aliinuka na kuondoka.
 
SEHEMU YA 219

Ndugu wa Bahati walichukizwa sana na kitendo cha Bahati kubaki ndani akipiga magoti kwa kuomba msamaha, walipokuwa pale nje kabisa na nyumba ya kina Erica maana walitoka nje kabisa, walijadiliana ambapo alianza dada yake Bahati,
“Hivi mama huyu kijana wako ana nini jamani, kwanini anakuwa hivi?”
“Hata mimi nashangaa dada, mama inabidi tufanye kitu. Haiwezekani Bahati akawa bwege kiasi hiki, au huyu msichana kamapa dawa ndugu yetu?”
“Inawezekana maana sio hali ya kawaida, mtu unaona kabisa mtoto sio damu yako ila unakazana kusema mwanangu. Hivi kwani Bahati ana shida gani kwasasa? Kila kitu anacho, biashara nzuri hadi gari hii kanunua (akionyesha gari aina ya Noah waliyoenda nayo kwa kina Erica), kanunua kwa pesa yake mwenyewe. Sasa kitu gani kinamfanya amng’ang’anie huyu mwanamke? Saivi ameanza ujenzi na nyumba karibia inaisha”
“Sio karibia, ni imeisha ila mjinga Yule kasema akimuoa huyu mwanamke wake ndio ataenda kuishi nae kule. Kwahiyo bado anakaa kwenye chumba cha kupanga sio kwamba nyumba haijaisha, imesha ila mjinga kasema mpaka akaishi na Erica, sijui Yule mtoto nimfanye nini jamani”
Mshenga alikuwa akiwasikiliza kwa makini sana na alikuwa kimya muda wote, ila sasa ndio akaongea,
‘Unajua leo ndio nimeshangaa, kumbe Bahati ana maendeleo kiasi hiki! Unajua tulivyokuwa tunakuja na gari hii nilijua labda kaomba rafiki zake kama kipindi kile alivyokuwa anaomba bodaboda, kumbe ni yake jamani huyu kijana loh! Kumbe na nyumba amejenga! Kweli ana kila sababu ya kuoa, sasa tunaweza kulalamika bure hapa kuwa inakuwaje ila kwa mazingira yalivyo ni wazi kuwa Bahati kapewa dawa na huyu msichana. Sasa mimi nina ushauri kama mtaafiki”
“Ushauri gani huo?”
“Kumbuka nina binti yangu, Yule Nasma ndio kamaliza kidato cha nne mwaka jana. Kwanini Bahati asimuoe huyo?”
Wakatazamana, kisha mama Bahati akasema,
“Itakuwa vizuri, ila itawezekanaje?”
“Sikia niwaambie, sababu Bahati kapewa madawa itakuwa ngumu sana kwa kumwambia hivi hivi ila inatakiwa tumuendee kwa mtaalamu kisha apewe dawa. Najua kwenu ndio itakuwa rahisi kumfanyia dawa hiyo na atajikuta akikubali kumuoa Nasma, na akikubali tu yani ndoa tunaifanya haraka haraka tusipoteze muda kabla mambo hayajaharibika, nitampaka binti yangu akiingia ndani tu abebe mimba maana hata dawa za Yule zikianza tena Bahati hawezi kumrudia sababu Nasma atakuwa na mtoto nae. Au mnasemaje kuhusu hilo?”
“Dah! Hilo swala zuri sana, kwanini hatukupanga siku nyingi? Dah! Asante Mungu maana mwanangu atapata pumziko la moyo sasa”
Wakaendelea kujadiliana pale, mpaka Bahati alipotoka ndani kisha kupanda nao kwenye gari na kuondoka nao maana hakutaka hata kuongea nao jambo lolote ukizingatia walishamdhalilisha.
 
SEHEMU YA 220

Nyumbani kwakina Erica walianza kumsema Erica, haswa mama yake,
“Hivi Erica, angalia aibu uliyonitia mama yako jamani! Hivi ulishindwa kupanga na huyu muuza samaki wako, kwani hukuelewa kuwa ndugu zake wangefika wangeshtushwa na mtoto? Wangapi wanaolewa wakiwa na watoto tayari? Ni wengi tu lakini wanakuwa na makubaliano na wenza wao yani hilo linajulikana wazi, bora hata mtoto angekuwa wa Kiswahili, tatizo mtoto ni wa kiarabu Erica yani hapo ndio kuna shida mwanangu dah hata sijui inakuwaje”
Erica aliinuka na kwenda chumbani kwake maana yeye alipata aibu kushinda ile aliyoipata Tony kwa kumleta Dora.
Alifika chumbani na kumuweka mwanae pembeni ila machozi yalimtoka, kitendo hiko kilionekana kinamuumiza pia mtoto wake kiasi kwamba hata mtoto wake alianza kulia, ikabidi Erica anyamaze na kuanza kumbembeleza mtoto.
Alitulia kimya sasa ila baada ya muda kidogo dada zake yani Bite na Mage walienda chumbani kwa Erica kuzungumza nae,
“Erica, usisononeke kwa hili lililotokea ila sisi tunaelewa mdogo wetu ulikuwa tu ukitaka kutuliza haja ya moyo wa mama ila ukweli upo wazi kuwa Yule mwanaume si muhusika wa huyu mtoto, si ndio?”
“Ndio”
“Basi kama ni hivyo, inamaana yote haya uliyategemea mdogo wetu. Sidhani kama ni jambo jema kwako kuendelea kuwa na mawazo”
“Sawa dada zangu nimewaelewa”
“Ila hebu leo tuongee kirafiki, baba wa Angel yuko wapi? Na huwa anasema nini kuhusu swala la ndoa wewe na yeye? Na huwa anasemaje kuhusu kumuona mtoto? Kuwa muwazi mdogo wetu”
“Dada zangu ngojeni tu niongee, baba wa mwanangu nadhani nilifanya makosa sana kumuamini mwanaume kiasi hiki ila kiukweli kanitamkia wazi kuwa hana mpango wa kunioa mpaka nibadili dini”
Erica akainama na kulia, ila dada zake wakamtuliza,
“Eeeh swala la kutokukuoa bado sio tatizo, unaweza kuolewa na mtu mwingine. Vipi kuhusu kumuona mtoto?”
“Yani siku zote huwa ananiambia nitakuja na hataki kusema atakuja lini?”
“Na vipi kuhusu kumuhudumia mtoto?”
“Huwa anamuhudumia”
“Basi sio tatizo”
“Ni tatizo dada, yani kiukweli Rahim kabadilika sana siku hizi. Zamani kabla sijawa na mtoto alikuwa akinitumia hela nyingi sana, hata wakati naenda kujifungua alinitumia hela nyingi ila siku hizi kabadilika kwanza shida ya hela hadi nimwambie halafu hanitumii kwa kiwango kile alichokuwa ananitumia mwanzoni. Yani siku hizi naweza nisimpate hewani hata mwezi na nusu halafu akiibuka nikimwambia nashida na hela basi anatuma laki mbili, na hapo nikimtumia ujumbe mwingine wa kumuomba hela hajibu ujumbe wangu. Ndiomana namuuliza mara kwa mara atanioa lini? Pengine nikiishi nae atamuhudumia vizuri mtoto wake”
“Mmmh ila Erica, hebu tuambie ukweli unajua wewe hata mtu akikusikiliza kuhusu swala la mwanaume kutokukutumia pesa hatokuamini kabisa, kwanza toka mtoto kazaliwa huyu hujawahi kupanda nae daladala, unaendaga kliniki ya mbali kabisa na unaenda na tax na kurudi na tax. Hufanyi kazi wala biashara Erica, nina uhakika hata mama hajawahi kukupa hela ya tax ila ni hela zako. Kama huyo mwanaume kabadilika siku hizi basi mwanzoni alikuwa anakutumia hela nyingi sana si ndio? (Erica akatingisha kichwa kumuitikia dada yake) Haya sasa, alikuwa akikutumia kama kiasi gani?”
“Mara nyingine milioni moja, mbili au tatu na akituma laki tano basi ndio ametuma hela ndogo”
“Mmmh kwa aina hiyo ya mwanaume mdogo wetu ulikuwa na haki ya kubabaika ila ungetushirikisha dada zako na tungekufundisha mbinu za kula na kipofu, haya sasa hizo hela nyingi umefanyia nini?”
“Nifanyie nini dada? Nilikuwa natumia tu”
“Unatumia milioni tatu, sijui mbili kwa matumizi gani hayo? Erica mdogo wangu hata hukuwaza kuanzisha biashara!”
“Dada, kipindi kile nilikuwa nasoma wala wazo la biashara sikuwa nalo. Kwanza nilijua nikimaliza chuo basi nitaanza kazi, kwahiyo sikuwa na wazo la biashara kabisa kichwani”
“Sasa hizo hela ziko wapi? Inamaana zote umekula?”
“Dada, hela niliweka benki ila kwa matumizi yangu na mtoto zimebaki kidogo sana na nikimwambia yeye ananitumia hela za mawazo hadi kichwa change kimevurugika na sijui cha kufanya”
“Watu huwa wanafurahia mapenzi kabla ya ndoa na kabla ya kuzaa, ungetuuliza kwanza dada zako. Yani kabla hujachukua uamuzi wa kubeba mimba, ungetuuliza kwanza, huyo kaka inaonyesha ana hela, mwanaume afikie hatua ya kukutumia milioni tatu ya matumizi tu! Huyo ni tajiri, sasa mdogo wangu ungeuliza ila cha ajabu hizo hela hata dada zako hatujawahi kuziona. Kumbe ndiomana ulikuwa huoni shida kukodi gari kutoka nyumbani hadi chuoni, kumbe ulikuwa na hela!”
“Nisameheni dada zangu, ila mnanishauri nifanyeje kwasasa?”
“Cha kukushauri maana ulishakosea tena ulikosea kabisa ila unatakiwa tu kuwa mpole, yani huyo mwanaume wasiliana nae kwa upole kabisa, ila kwavile kasema hatokuoa hadi ubadili dini ujue hapo ndoa hakuna”
Bite akatoa ushauri mwingine,
“Sasa dada, mdogo wetu akitaka apate tena hela za Yule mwanaume ajifanye anakubali kubadili dini ndio atamchota vizuri”
“Bite mdogo wangu, unafikiri kuna muowaji kweli hapo? Yani kuhusu dini ni kisingizio tu, yani hapo hamna cha ndoa wala nini ila Erica shukuru Mungu umeshaujua ukweli halafu usonge mbele. Saivi angalia jinsi ya kutunza mtoto wako tu, usihofu kuhusu mume utapata tu”
Erica alianza kuwaelewa dada zake na kuishiwa maumivu kidogo yale aliyokuwa anayawaza moyoni.

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 221

Usiku wake Erica aliwaza sana kuhusu yale aliyokuwa akizungumza na dada zake kwa siku hizo, ila neno la dada yake Bite lilimuingia akilini kuwa amwambie Rahim kuwa anakubali kubadili dini kwani kiukweli bado Erica alikuwa na wazo la ndoa licha ya kumwambia kuwa aachane na wazo hilo.
Aliingia kwenye mtandao na kumtumia ujumbe Rahim, ambapo kwa leo alianza na salamu kisha Rahim alimuitikia halafu Erica akaandika tena ujumbe mwingine,
“Rahim, nipo tayari kubadili dini unioe”
Akamtumia huku akisubiri majibu, ila alikaa kama nusu saa bila ya kujibiwa na kujiuliza kuwa imekuwaje maana hakuelewa sababu alijua lile jambo lazima lingemfurahisha Rahim, alipoona kimya akatuma ujumbe mwingine,
“Mbona kimya Rahim”
“Kimya nini?”
“Si nimekutumia ujumbe, mbona hujanijibu”
“Ujumbe gani?”
“Si nimekwambia nipo tayari kubadili dini unioe”
“Sasa hilo ni swali umeniuliza au ni nini maana sijaelewa ndiomana sijakujibu”
“Rahim jamani, mbona unakuwa hivyo. Yani nakwambia kitu kingine unanijibu vingine. Kwanini lakini?”
“Sijakuelewa”
“Si ulisema nibadili dini ndio unioe? Nipo tayari kubadili dini sasa, lini utakuja kunioa?”
“Ila wewe Erica hebu muda mwingine uniache nipumue jamani, kila siku hakuna vitu vya msingi tunavyozungumzia zaidi ya ujinga ujinga tu. Kwanza mwanangu anaendeleaje?”
“Yani wewe mwanaume laity ungeingia kwenye moyo wangu na kujua jinsi gani naumia sijui kama ungekuwa unanifanyia hivyo, huyu mwanao unataka kujua anaendeleaje unampenda kweli? Kama ungempenda si ungekuja kumuona? Yani Rahim kuanzia leo sitakwambia tena habari za mtoto”
“Sasa Erica huko unafika kubaya, kumbuka wewe ndiye mwandani wangu, kumbuka tumezaa Erica, huyo mtoto anatuhitaji wote wawili sasa ukisema hutoniambia tena kuhusu mtoto wangu utakuwa hunifanyii vizuri”
“Ungeujua umuhimu wa huyu mtoto basi ungejua na umuhimu wa mama yake”
“Erica, nielewe ninaposema nitakuja. Tatizo lako unapenda nifanye vitu ambavyo sina uwezo navyo kwasasa, kuwa muelewa basi Erica. Kesho nitakutumia pesa”
Rahim alitumia swala la kumwambia Erica kuwa atamtumia pesa ili kumpooza maana alimuona ameshapaniki, naye Erica hakuweza kuendelea kuongea nae zaidi, kwahiyo aliamua kulala tu.
 
SEHEMU YA 222

Alipoamka aliendelea na kazi zingine ila akatumiwa ujumbe na Rahim kuwa ametumiwa pesa,
“Nimekutumia laki moja na nusu”
Erica alisoma ule ujumbe na kuona kweli Rahim kabadilika maana mwanzoni ilikuwa akimtumia hela kubwa kubwa ila kwa ile hali inamaana kuwa kuna siku atatumiwa elfu tano, ila kwavile alikuwa na shida alishukuru hata hiyo aliyoipata maana kwa siku hizo Rahim alikuwa akimtumia moja kwa moja kwenye akaunti yake.
Muda kidogo akaitwa na mama yake, kisha mama yake akaanza kumwambia,
“Haya Erica mwanangu, umeona jana ulivyoniaibisha mama yako? Umeona?”
Erica aliitikia kwa kichwa tu, kisha mama yake aliendelea kuongea,
“Una mpango gani sasa? Una mpango gani na maisha yako? Au unasubiri huruma za kudhalilishwa kiasi hiki hadi lini? Hujishtukii mwanangu?”
“Mama, nakuomba mama yangu usinikandamize”
“Sikukandamizi mimi ila ujinga wako ndio uliokukandamiza, sijakutuma ulete mwanaume mwingine halafu umsingizie mtoto. Hapa usinione hivi, nimechanganyikiwa, wiki ijayo wajomba zakowanakuja sijui hata nitaweka wapi sura yangu”
Kiukweli Erica hakujua cha kumjibu mama yake na kujikuta akiwa kimya tu na kumuacha mama yake aongee hadi anyamaze.
Mchana wa siku hiyo alifika James na kumkuta Erica na mama yao maana Bite hakuwepo siku hiyo, alienda nyumbani kwa Mage kwahiyo James alipata upenyo wa kwenda kuzungumza pale.
James alikaa sebleni na Erica akizungumza nae, ni wazi James alihitaji sana kusamehewa na mke wake,
“Erica, niambie nifanye nini ili dada yako anisamehe”
Erica akawaza kuwa dada zake waliposikia alikuwa anatumiwa pesa nyingi na Rahim walionyesha kumpenda sana na hata kuona mdogo wao hajafanya makosa kuzaa na Rahim kwahiyo dada zake bado walihusudu pesa. Pia akakumbuka dada yake aliwahi kulalamika kuwa ameambulia kigari kisichoeleweka kwahiyo inamaana akipata gari nzuri zaidi atamsamehe mume wake,
“Shemeji, najua hela unayo ila kwanini usimnunulie mkeo gari nyingine? Mshtukize kwa kumletea gari nyingine hapa, najua atakusamehe tu”
“Sasa gari gani?”
“Yoyote nzuri, yani gari utayoona imezidi ubora ile gari ya mwanzo maana huwa anailalamikia sana ile gari.”
“Una uhakika Erica, nikifanya hivyo dadako atanisamehe?”
“Fanya hivyo kwanza halafu uone kama atakusamehe au la”
James aliona aage mapema kabla mkewe hajarudi na kumkuta hapo nyumbani, kwani hakutaka mkewe ajue kama alifika kwao.
 
SEHEMU YA 223

Usiku kama kawaida, Erica alianza kwa kumtafuta Rahim na leo alimuuliza,
“Mbona siku hizi hunitumii hela kama zamani?”
“Hela nyingi wewe unataka za nini?”
“Jamani, kuna vitu vingi. Mtoto ana mahitaji mengi kwahiyo ndiomana nahitaji pesa”
“Yani wewe Erica ni bure kabisa, umesoma lakini ni bure yani ndio nyie ambao elimu haijawakomboa. Nilijua utaniambia nitumie hela nyingi nifanye biashara ila wewe umekazania kusema tu una mahitaji mengi. Ndio mke wewe? Loh!”
“Rahim acha kunisema vibaya, najua mimi sio mke kwako. Nitakuwaje mke na wewe umeshaoa?”
“Ushaanza kuota tena, aliyekwambia nimeoa nani? Erica acha mawazo mgando, mke wangu ni wewe”
Katika siku alizotabasamu tangu awe na mtoto basin i leo toka alipoambiwa kuwa mke wangu ni wewe yani alijihisi kuwa na furaha iliyopitiliza kiasi kwamba hakuendelea tena kumtumia ujumbe mwingine Rahim zaidi ya kumtakia siku njema na kulala huku akitabasamu na kuwaza kuwa yupo ndani ya nyumba akiishi yeye, Rahim na mtoto wao.

Kulipokucha, alifanya shughuli za nyumbani kwao. Siku hii ilikuwa ni siku ya kumpeleka mwanae kliniki kwahiyo alimuandaa vizuri nay eye kujiandaa kisha kuita gari kwaajili ya kwenda kliniki.
Gari lilifika na alipanda na kwenda kliniki, ambapo alihudumiwa vizuri tu, wakati anatoka akakutana uso kwa uso na Mrs.Peter akiwa ameongozana na Yule Salma yani Erica alishindwa hata kujificha ila kwa bahati muda huo mtoto wake alikuwa mgongoni amelala.
“Kheee Erica, mtoto wa nani huyo?”
“Wa dada yangu”
“Aaah ndio umemleta kliniki! Mwenyewe yuko wapi?”
“Kaenda kazini”
“Aaah! Mimi nimekuja na mkwe wangu hapa, ana mimba change basi inamsumbua balaa, ndio nimemsindikiza aanze kliniki”
Swala la kuambiwa Salma ana mimba lilipasua moyo wa Erica.
 
Back
Top Bottom