Simulizi: Nini maana ya mapenzi

Simulizi: Nini maana ya mapenzi

SEHEMU YA 330


Muda huu sasa alimfata mama yake kwani alihitaji kujua mapenzi ni nini ikiwa kila anachofanya kinamuumiza tu katika mapenzi,
“Mama, nimemaliza sasa nahitaji kujua mapenzi ni nini?”
“Kwanza kwanini unataka kujua mapenzi ni nini? Tuanzie hapo ndio nitaweza kukuelewesha kidogo”
“Mama, mwanao nimekuwa nikipata changamoto mbalimbali za mapenzi, nimekuwa nikikutana na watu mbalimbali wakidai wananipenda ila kumbe si kweli walikuwa na lengo lao tu, yani mpaka nachanganyikiwa hapa kuwa mapenzi haya ni kitu gani na kwanini mimi yananiumiza hivi”
“Mwanangu pole sana, ila mara nyingine ni kosa langu kutokukaa na wewe na kukuelimisha kuhusu swala zima la mapenzi kwani sikufikiria kuwa mwanangu umekuwa sasa, ila mwanangu mapenzi yamejaa unafki sana, kwanini nasema hivi sababu mtu anaweza kukuonyesha anakupenda hadi unaweza hisi nikimuacha huyu atakufa, kumbe kuna kitu anahitaji toka kwako ndiomana anaonyesha anakupenda, haya yuko wapi baba Angel? Si ulisema alikuwa hadi anakutumia pesa? Ziko wapi hizo pesa sasa? Angekuwa mwingine si ndio angekujali sana hivi una mtoto wake? Yani mapenzi kila mtu anayatafsiri kwa namna yake ila yakikupitia ndio unajua haswaa mapenzi ni nini, ndiomana nimekuuliza hujawahi kuumizwa na mapenzi? Kama umewahi, unawezaje kumuamini mtu asiye mume wako? Ingawa hata kwenye swala la ndoa kuna watu wanaingia kwenye ndoa sio sababu ya mapenzi ila kuna kitu anahitaji, yani mapenzi ni swala pana kidogo”
“Mama, jana nimetukanwa sana mwanao na huyo unayemsema baba Angel, ndiomana nashindwa hata kuelewa mapenzi ni nini. Huyu mwanaume aliniambia kuwa ananipenda kuliko msichana yeyote humu ulimwenguni, ila jana alivyonitukana kama si yeye aliyesema maneno yale kipindi kile”
Mama yake alicheka kama anamcheka mwanae vile, kisha akamwambia amuonyeshe alivyomwambia, kwavile Erica alishaamua kuwa mkweli kwa mama yake hakuona kama ni tatizo kumuonyesha alichoandikiwa na Rahim, alienda kuchukua ile simu yake na kufungua mtandao wa kijamii kisha kumuonyesha mama yake zile jumbe ambazo Rahim alikuwa akimtumia jana,
“Yani kaniita malaya kweli!”
“Hajakosea, wewe ni malaya ndio ndiomana ukamkubali shetani kama yeye bila hata kujiuliza, kumbe ulikuwa ukiniongopea nasafiri halafu unaenda kukutana na shetani kama hili! Watu wanagombana ila sio kufikia hatua ya kutukanana na kuhisi mmoja hafai, Erica mwanangu nilikufundisha kama naimba nyimbo, mwanangu jitunze hadi ndoa ila wapi ukaona natwanga maji kwenye kinu, umeona asante ya mwanaume eeeh! Yani mwanaume anakupa na mbinu ya kutoroka kwenu ila mwisho wa siku anakuona malaya kwa starehe yake mwenyewe, ila mwanangu usijali wala usiumizwe na maneno ya huyu Rahim, mi ninachokuombea ni uolewe tu mwanangu na huyu Rahim na familia yake yote tutawaalika kwenye harusi yako, wala maneno yake yasikukatishe tamaa, yani kuna mijitu haina akili hata kidogo, mwanamke kajitoa kubeba mimba kwaajili yako, kazaa kwa uchungu na analea mtoto wako kwenye mazingira ya kusemwa kila siku kuwa kazaa nje ya ndoa halafu unashindwa hata kufikiria mazingira anayopitia Yule mwanamke unafurahi tu kumuita malaya! Nimechukia sana, simpendi huyo Rahim yani simpendi kabisa, nimechukia sana. Acha tu mwanangu uendelee kujifariji kwa huyo Erick, natumaini atakuwa wako kweli”
Kwahiyo alijikuta na mama yake mada yako ya kuelezana mapenzi ni nini imeishia hapo kusikitishwa na majibu ya Rahim tu, maana hata mama yake Erica hakufikiria kama Erica angepata tabia za kuweza kuitwa kwa jina baya vile, alimuangalia mwanae na kusema tena,
“Unajua nakuangalia Erica sikumalizi, hivi ni kweli ni wewe niliyekulea katika maadili yote? Mtu anafikia kusema hakuna mwanaume atakayekuoa mwanamke kama wewe, kwaini aseme hivyo? Najiuliza sana, hivi ulianzaje kutembea na familia nzima? Najiuliza bado, ulianzaje kutembea na shetani kama Derick? Unajua ninavyokuangalia na haya mambo yanayokuhusu hakika huendani nayo, hivi ilikuwaje Erica! Aaah kama sikukulea mimi vile dah! Najaribu kukufikiria nakosa jibu, si utakuwa umemaliza kijiji mwanangu wewe, na sijui kama huyo Mzee Jimmy hukutembea nae kweli! Wewe uliweza hata kutembea na Yule Bahati kipindi kile anavua samaki hukuona hata kinyaa mmmh! Ila mwanangu ni mchafu wewe loh! Bora nikalale mie, nisije kuongea na mengine”
Erica nae alijisikia vibaya sana, ilikuwa ni usiku tayari alienda chumbani kwake.
 
SEHEMU YA 331


Alipofika chumbani kwake aliinama na kutoa machozi kwa hakika alitamani siku zirudi nyuma na awe Erica mpya, alijikuta akijuta sana kwa yale matendo yaliyopita nyuma,
“Najuta kumfahamu Babuu maana ndio kanifanya niyajue mapenzi, najuta kumfahamu pengine nisingemfahamu ningeweza kujitunza hadi ndoa ila kwavile nilishaharibu sikuweza tena kujitunza. Najuta mimi Erica, ila nimebadilika sema natazamwa kwa yale matendo ya nyuma tu”
Alijikuta akilia sana, simu yake iliita tena alipoitazama ni Erick alikuwa akipiga tena, akapokea huku akiendelea kulia na kumfanya Erick ajue pengine Erica analia kwa kitendo chake cha kulewa jana yake,
“Erica nisamehe mpenzi wangu, nilikwambia nitakuwa nakunywa kistaarabu, naomba unisamehe Erica tafadhari, sitarudia tena”
“Silii hicho Erick ila nalia sababu mimi nimekuwa mwanamke asiyefaa”
“Nani kasema wewe ni mwanamke usiyefaa?”
“Erick, wanawake wanaofaa wote wanaolewa wakiwa bikra ila sio kama mimi”
“Erica, hebu achana na hizo desturi potofu, kwani ukiwa na bikra au usipokuwa nayo ndio nini katika maisha eeeh! Tunachoangalia ni upendo, Erica kuna wasichana wengi wadogo wanatamani kuwa na mimi, kuna wasichana wengi waliobikra na hawana watoto wanatamani kuwa na mimi ila mimi siwataki nakutaka wewe, unajua kwanini? Sababu moyo wangu upo kwako, wewe ndiye mwanamke wa maisha yangu, wewe ndiye nikupendaye kwahiyo hata utokee mlolongo wa wasichana ujipange kwaajili yangu siwezi kuchagua yeyote maana kwangu upo wewe tu. Erica usilie wala usiwe na mawazo, kuzaa nje ya ndoa si kusema kwamba ni malaya, hapana, tena mimi naweza kukuita wewe ni mwanamke shujaa maana najua ni vikwazo vingapi umekumbana navyo wakati wa mimba ya Angel, Erica mama yangu usilie ila furahi kuwa na Angel na ufurahi kuwa na mimi, kwa pamoja tutamlea Angel na kumuweka katika maadili yanayofaa”
Kwakweli maneno ya Erick yaliupa faraja moyo wa Erica kwani alijikuta akitabasamu tu na kusema,
“Erick nakupenda”
“Hunifikii mimi malkia wangu, nakupenda sana”
Yani Erica kila akiongea na Erick alikuwa akijihisi raha sana, basi akaagana nae na kuweza kulala, kwakweli alilala kwa tabasamu zito sana, yani hata hakumuuliza Erick kuwa kwanini jana yake alilewa ila alilidhika tu na kubembelezwa na Erick.
 
SEHEMU YA 332


Kulivyokucha, mama Erica alijua kama kawaida kuwa angemkuta Erica amevimba macho kwa kulia kwa yale maneno aliyomwambia jana ila alishangaa sana kuona Erica ameamka na tabasamu huku akifanya kazi za hapa na pale, alimsalimia mwanae na kumuuliza,
“Nipe siri ya tabasamu lako”
“Hamna mama, nimefurahi tu”
“Mmmh Erica, najua tu kipo kilichokufurahisha”
Simu ya Erica ilikuwa mezani na ikaanza kuita, mama yake akachungulia na kuona mpigaji ni Erick kisha akona Erica akichukua simu na kwenda kupokelea chumbani huku akiwa amejawa na tabasamu, kwakweli hapo ndio akaelewa furaha ya mwanae imekuwa Erick,
“Ila huyu Erick anagombewa na Sia, mmmh sijui itakuwaje? Ngoja nitulie mie”
Ilibidi tu aka echini akimsubiri huyo mwanae amalize kuongea na simu, basi Erica nae alikuwa akiongea na simu,
“Jana nilisahau kukwambia Erica, kuna mzigo mpya umeingia, kwahiyo Jumamosi uwende na Angel”
“Mmmh umesahau kuniambia au ulitaka kuongea na mimi tu!”
“Nilisahau kukwambia kweli, kwani jana nilikwambia?”
“Hapana hujaniambia, ila si Moses yupo angeniambia”
“Erica bhana, ila kiukweli nilimiss tu kusikia sauti yako kipenzi change, ngoja nifanye kazi zangu huku nahitaji tuishi maisha ya furaha sana. Nakupenda Erica”
“Nami nakupenda pia”
Kisha akakata simu na kwenda sebleni kwa mama yake ambaye alisema,
“Nimesikia nakupenda pia, hahaha penzi likiwa change unajihisi kama una miliki dunia”
“Jamani mama, usiseme hivyo. Niombee tu mwanao nifike mbali na Erick”
“Unafikiri sikuombei mwanangu, mafanikio yako ndio mafanikio yangu”
Wakasikia mtu akibisha hodi, ikabidi mama Erica ainuke kwenda kufungua kwani muda huo huo Angel alikuwa akilia kwahiyo Erica alienda kumbeba mtoto wake, alipofungua mlango alishangaa kumuona Sian a Tumaini, hakutaka kuongea nao vibaya mlangoni kwahiyo aliwakaribisha ndani na kuanza kusikiliza kilichowaleta, baada ya salamu Tumaini alianza kuongea,
“Mama, samahani sana usione kama tunakusumbua ila huyu wifi yangu kwasasa yupo kwenye hali mbaya sana, tafadhali mwambie Erica amuache kidogo Erick aweze kuwasiliana na familia yake.”
Sian aye akaongea,
“Mama, nipo chini ya miguu yako, Erick ndio kila kitu kwangu, Erick ndio pumzi yangu, siwezi kitu mimi bila Erick nampenda sana, nisaidie mama yangu, ongea na Erica ni mwanamke mwenzangu anielewe ninakopitia mwenzie”
Mama Erica baada ya kuwasilikiliza kwa makini akaanza kuwajibu, muda huo Erica alipogundua ni wao alijibanza chumbani hakutaka kwenda sebleni kuonana nao, Yule mama alianza kuwaeleza,
“Nimewasikia yote, toka jana nimewasikia ila kuna swali nataka nikuulize wewe Sia”
“Niulize tu mama”
“Kati ya mama yako mzazi na huyo Erick nani ni muhimu kwako?”
“Mama jamani, mama yangu mzazi ameshakufa kwahiyo Erick ndio amebaki katika maisha yangu kwasasa”
“Tuchukulie mfano mama yako bado yupo, je kati yake aliyeingia leba kukuleta wewe mtoto mpumbavu na huyo Erick nani wa muhimu kwako?”
“Sasa mbona unanitusi mama?”
“Sikutusi ila nakwambia ukweli, ungekuwa mjinga wewe ungeelimika ila wewe ni mpumbavu, yani hujui umuhimu wa aliyeingia leba kupigana na maisha yake sababu yako, ila unajua umuhimu wa mwanaume unayekutana nae kwaajili ya atarehe za kimwili tu. Wewe mama yako kafariki juzi, jana hapo tumezika, leo kiguu na njia kuja kugombania mwanaume, hivi una akili wewe? Ndio nyie wazazi wanawazaa kutoa change tumboni tu maana ungebaki kwenye tumbo la mama yako basi ungemuua kwa uvimbe”
“Jamani mama”
“Hakuna cha jamani hapa, wewe Sia huna akili hata robo, unakuja kwangu kwa sura ya huruma sijui Erick ndio uhai wangu, sijui ndio pumzi yangu, siwezi ishi bila yeye, Erick ni nani katika maisha yako? Unakuja kunieleza mimi kuhusu Erick kukuchanganya ili nikusaidiaje? Unajua nyie watoto wa siku hizi hamna akili kabisa, unaendekeza mapenzi, unaacha kumthamini mama yako aliyehangaika na mimba yako miezi tisa, bado akaenda kuteseka leba kwa uchungu na kukulea kwa shida, leo bila aibu unakuja kuniambia ujinga kuwa Erick ndio wa muhimu kwako? Saivi ulitakiwa kutulia huko ukiomboleza kifo cha mama yako, ukikumbuka mazuri ya mama yako na kuyaenzi ila wewe kiguu na njia kuja kutafuta penzi, jana nimekustai tu pale nilijua utajirekebisha kumbe hamna kitu. Haya nigeukia upande wako wewe Tumaini, huna mama wewe?”
“Ninae”
“Huna mpenzi?”
“Ninae”
“Mpenzi wako na mama yako nani muhimu zaidi?”
“Mama ni muhimu zaidi”
“Sasa kama unatambua hilo kwanini unamfundisha ujinga huyu mwenzio, ulitakiwa umwambie rafiki yangu, sijui wifi yangu, huu ni muda wa kuomboleza kifo cha mama, mapenzi yapo tu jamani, nyie watoto wa siku hizi mkoje? Mbona mnatupa simanzi wazazi wenu, naombeni muondoke sasa hivi, Sia rudi katafakari mambo mema ya mama yako uyafate, ujinga ujinga muache”
Hawakuwa na neno la ziada zaidi ya kuaga na kuondoka zao, na walivyoondoka tu Erica ndipo akatoka chumbani na kwenda kwa sebleni kwa mama yake kwani hakuamini kama mama yake angewatimua hao watu.
“Kheee mama umewafundisha vizuri”
“Ndio ujinga sitaki, hivi nyie watoto hamjui uchungu ambao mama anapitia au? Hivi Angel huyo awe mkubwa halafu aseme aliyekutana nae ukubwani ndio muhimu zaidi kushinda wewe, atakuwa anawaza kwa kutumia nini jamani? Yani hawa nimewaangalia sana na ujinga wao toka jana”
Erica akacheka tu kwani alijua akiendelea kumwambia chochote kwa muda huo mama yake basi mada itamgeukia yeye.
Basi akaendelea na shughuli zingine hadi muda wa kulala, na kuchukua simu yake kumpigia Erick, alimuuliza pia swala la kazi ambayo alisema angemtafutia,
“Vipi kuhusu yule mtu wa kazi?”
“Kuna jambo lingine nimelifikiria Erica”
“Jambo gani hilo?”
“Nimewaza kuhusu kazi, nimeona itakufanya ukose muda wa kuwa karibu na mtoto ila nilikuwa nafikiria namna ya kukusaidia, unaweza kufanya biashara?”
“Mmmh sijawahi, ila kila kitu ni kujaribu, sidhani kama nitashindwa”
“Sawa basi kesho utaniambia ni biashara gani unafikiria kujaribu kuifanya”
Kisha wakaongea mada mbali mbali na kuagana.
 
SEHEMU YA 333


Kesho yake Erica alijifikiria sana, maana mwanzo alifikiria kuhusu biashara ya vifaa vya watoto ila akajifikiria tena kuwa mbona ndio biashara kwenye duka la Erick, akawaza tena na kukumbuka maneno ya Rahim kuwa hakuna mwanaume anayeweza kumpa kiasi cha pesa alichowahi kuomba, aliwaza hilo jambo, hakuwa na wazo la biashara yoyote ila akajisemea kuwa Erick akimpigia atajaribu kumuomba hela hiyo asikie kuwa naye atasemaje.
Mchana wa siku hiyo Erick alipiga na kuongea nae vizuri sana kisha akamuuliza,
“Umeshafikiria biashara ya kufanya?”
“Hapana, ila nimefikiria mtaji wa kuanza nao”
“Unataka kuanza na kiasi gani?”
“Ningependa nianze na milioni kumi na tano”
“Biashara gani hiyo Erica ya milioni kumi na tano?”
Akafikiria na kuamua kujibu kama wazo lake la mwanzo,
“Nilifikiria kufanya biashara ya kama lile duka lako la vitu vya watoto na nguo”
“Mmmh mbona mtaji uliofikiria ni mdogo sana?”
“Nilikwambia lakini sina ujuzi vizuri wa biashara”
“Basi ngoja, kuna kitu nitafanya, tulia tu”
“Mmmh nini hiko Erick?”
“Sikwambii ila hiyo siku utakijua, subiri tu ila nadhani kuhusu kazi ungevumilia kidogo tuangalie na michakato mingine hii inasemaje”
“Sawa, nimekubali”
Basi aliongea nae kwa tabasamu zito sana, kisha kukata simu.
Alipokata ile simu tu ikaingia simu nyingine, kuangalia ni Tumaini alikuwa akipiga, Erica akapokea na kuongea nae,
“Erica unajua ulichosababisha kwa Sia?”
“Nimesababisha nini kwani?”
“Huna huruma na msichana mwenzio, wewe binti hufai hata kidogo”
“Sikuelewi Tumaini”
“Utanielewa tu, subiri”
Kwakweli Erica hakumuelewa Tumaini kuwa ana maana gani, muda huo alimsikia mama yake akimkaribisha mgeni, akatoka na mwanae kwenda kumuona huyo mgeni, alikuwa ni Yule mama ambaye mama yake alikuja nae kutoka msibani kwa mama Sia, Erica akamsalimia huyu mama ila Yule mama alionekana kumshangaa sana mtoto wa Erica, hadi mama Erica akamuuliza,
“Vipi mbona umemshangaa hivyo?”
“Jamani, duniani wawili wawili yani huyu mtoto kafanana na mjukuu wangu balaa”
“Aaah! Mjukuu wako, baba yake ni nani?”
“Usingeniambia kuwa mwanao ana mchumba ningefikiria ndiyo Yule mjinga kazaa nae pia”
“Nani huyo?”
“Mjinga mmoja hivi anaitwa Rahim”
Kwakweli mama Erick alishtuka kidogo na kutambua tabia ya Rahim.
 
SEHEMU YA 334


Erica akamsalimia huyu mama ila Yule mama alionekana kumshangaa sana mtoto wa Erica, hadi mama Erica akamuuliza,
“Vipi mbona umemshangaa hivyo?”
“Jamani, duniani wawili wawili yani huyu mtoto kafanana na mjukuu wangu balaa”
“Aaah! Mjukuu wako, baba yake ni nani?”
“Usingeniambia kuwa mwanao ana mchumba ningefikiria ndiyo Yule mjinga kazaa nae pia”
“Nani huyo?”
“Mjinga mmoja hivi anaitwa Rahim”
Kwakweli mama Erick alishtuka kidogo na kutambua tabia ya Rahim.
Mama Erica akauliza tena kwa makini,
“Unasema Rahim?”
“Ndio mjinga mmoja hivi anaitwa Rahim, hebu fikiria mtoto anatimiza miaka minne sasa, Yule Rahim hajawahi kufika nyumbani”
“Kheee pole mwenzangu”
“Asante”
“Ila wewe ushawahi kumuona?”
“Nimewahi ndio, kipindi hicho anamdanganya danganya mwanangu na vihela vyake, kumbe Yule mjinga anapewaga hela na wanawake wengine, ila tuachane na hizo habari, nimekuja kukuaga tu”
“Karibu ukae basi, ndio wima wima jamani!”
Mama Erica alikuwa akiongea ila moyoni mwake alikuwa anajisikia vibaya sana kutokana na kusikia habari za Rahim, basi Yule mama akakaa kidogo na kufanya maongezi ya hapa na pale na mwenzie maana ni kipindi kirefu ila hakuweza kuongea nae sana sababu alikuwa na haraka zake, basi muda huo huo aliamua kuaga ila wakati anaaga gafla akapigiwa simu, na kuipokea ila ilionekana kama hiyo simu imemchanganya kidogo, kwahiyo alivyokata ilibidi mama Erica amuulize kuwa kulikoni,
“Mwenzangu, eti mtoto wa marehemu kalazwa”
“Kalazwa? Anaumwa nini tena?”
“Eti alitaka kujinyonga, jamani huyu mtoto mbona anatutafutia makubwa sisi! Ngoja niende huko hospitali, nishachanganyikiwa sasa hivi”
Ilibidi mama Erica nae avae mara moja na kuondoka na Yule mwenzie wakielekea hospitali.

Erica alibaki nyumbani na mwanae ila alijisikia vibaya sana kwani yale maongezi ya Yule mama na mamake aliyasikia yote, akajiuliza sana kuwa au ndio ile simu aliyopigiwa na Tumaini kuwa kuna kibaya kimetokea kwa Sia,
“Yani Sia alitaka kujinyonga sababu ya mapenzi kweli? Inamaana Sia anampenda zaidi Erick kuliko mimi ninavyompenda? Hapana haiwezekani, mbona mimi nampenda sana Erick ila hata nilipoachana nae sikuthubutu kujidhuru, siamini kama Sia anampenda Erick kuliko mimi. Ila lawama naletewa mimi, kweli mimi nimsababishie kifo jamani? Mbona naonewa sana?”
Erica aliwaza sanahuku machozi yakimklenga lenga ila alipokumbuka mambo ya Rahim, hakutaka kuwaza tena maana mambo ya Rahim yalimchefua sana, yani kijana aliyekuwa akiifiwa na mama yake kuwa ni kijana mtulivu kumbe ndio kijana mchafu hafai, ingawa siku ile alimtusi ila alijipanga kuwa siku hiyo usiku amtafute hewani amsikie sera zake za kukimbia watoto.
Jioni alijifikiria akaona ni vyema awasiliane na Erick ili ajue kama anajua kuwa Sia alitaka kujinyonga, basi akampigia simu Erick kama kawaida Erica alivyoanza kuongea tu mwanae alimpora ile simu kwahiyo Erica alimuangalia tu mwanae aongee na Erick, alipomaliza ndio alimpa mama yake, Erica alicheka na kumuuliza Erick,
“Hivi huwa unaongea nini na huyu mtoto hadi anachanganyikiwa hivi?”
“Mambo ya baba na mtoto yaache tu, wenyewe tunajua tunachoongeaga, hivi hujui? Mtoto wa kike ni wa baba na wa kiume ni wa mama kwahiyo huyu lazima anipende baba yake”
“Yani wewe loh! Tuachane na hizo habari, ila umesikia?”
“Kusikia nini?”
“Majanga yaliyotokea?”
“Yapi hayo?”
“Nasikia Sia alitaka kujinyonga eti”
“Nani kakwambia?”
“Tumaini alinipigia simu”
“Kwanza Erica, huyo dada yangu mblock kwenye simu yako wala usiwasiliane nae tena, nadhani hana jema na penzi langu, Erica nakupenda, tafadhali usisikilize maneno ya watu, ajinyonge sababu yangu ni mumewe mimi? Lini nimeoa labda ndio kanifumania na kuchukua uamuzi mbaya, yani mtu kama huyo wala asikuchanganye Erica wangu akili, achana nao kabisa. Mimi nakupenda wewe yani hadi dunia nzima iwe kinyume na mapenzi yangu kwako bado nitasimama na kusema nakupenda wewe, kwanini Erica unashindwa kusimama kwaajili ya penzi langu? Huyo dada yangu labda akikutafuta na namba nyingine mwambie malalamiko aniletee mimi maana mimi ndiyo nimependa ila wasisumbue akili yako kabisa”
“Ama kweli Erick unanipenda sana, hadi najihisi raha”
“Erica, wewe nenepa tu upo na mimi. Yani katika akili yako tambua kwamba hakuna mwanaume anayekupenda kama anavyokupenda Erick”
“Asante sana nami nakupenda”
Kiukweli Erica alipata ahueni ya moyo kwani hakutegemea kama Erick angempa moyo kiasi kile, ila alifurahi sana kuzungumza na Erick.
 
SEHEMU YA 335

Hadi muda wa kulala ulifika ila mama Erica alikuwa hajarudi kiasi kwamba Erica alikuwa na mashaka na kusinzia sebleni akimsubiri mama yake, muda kidogo alirudi ila alionekana kuchoka sana kiasi kwamba hakutaka kuhojiana maswali na kwenda kuoga, kula na kulala. Erica nae aliamua kwenda chumbani kwake, ila muda huu usingizi ulikata maana alikumbuka ahadi yake ya kuingia kwenye mtandao ili amseme Rahim, na kweli alipoingia tu alimkuta Rahim yupo hewani kama kawaida, akamsalimia na kumuuliza,
“Hivi wewe Rahim, watoto wangapi umetelekeza?”
“Niondolee balaa mimi huwa sitelekezi mtoto”
“Unajua wewe mamako anakuona msafi sana, kumbe ni mchafu mchafu hufai, sikukujua vizuri, nasema tena sikukujua vizuri, kumbe kutelekeza watoto ndio kawaida yako loh! Mwanaume hufai wewe”
“Erica, usitake niongee maneno machafu, sasa wewe unafaa kwa lipi? Umetembea na familia yangu nzima, ndio unafaa wewe? Kumbe umetembea hadi na kaka yako, ndio unafaa wewe? Ushatoa mimba ya Derick, ndio unafaa wewe? Hapo ya Derick tu ndio tunaifahamu, ila nahisi ushatoa mimba zaidi ya kumi hata huyo mtoto umezaa kwa kuhurumiwa tu, Erica nikija kumchukua huyo mwanangu itabidi nikapime DNA”
Yani Erica ingawa ni yeye alianzisha mada ili amseme Rahim ila ilimshinda maana hakuweza kuendelea kuongea nae ukizingatia kila alichosemwa na Rahim kilimshika vilivyo, alijihisi vibaya sana moyoni mwake, alijikuta tu akimuandikia,
“Usiku mwema”
“Unalala? Kweli siku hizi huna soko Erica, hivi wapo wanaobabaishwa na wewe tena kweli? Nakwambia hata ndotoni huwezi kuwa mke wangu Erica, maana nitakuwa naoa uchafu tu, mwanamke umepitiwa na kila aina ya mwanaume, hapana kwakweli”
Erica akazima mtandao na kuamua kulala tu kwani alijihisi maumivu haswa kwenye moyo wake, kuna muda alitamani kuyachukia mapenzi ila alipofikiria kuhusu Erick alitabasamu tu na kuamua kuendelea kuyapenda mapenzi.

Kulivyokucha Erica aliamka na kufanya shughuli zake za hapa na pale ila muda kidogo mama yake alimuita na kuanza kuongea nae,
“Erica, sikuwahi kuwaza kuwa kuna watu wanasumbuliwa na mapenzi kiasi hiki, Sia ametaka hata kujiua sababu ya Erick! Tena unaambiwa mama Erick ndio aliyemuokoa, ila hatukumkuta hospital alishaondoka, Erica mwanangu kama mzazi nimejihisi vibaya sana. Ngoja nikuulize kitu”
“Niulize mama”
“Ni kiasi gani unampenda Erick?”
“Nampenda Erick mama, sijui ni kiasi gani ila nampenda sana”
“Kwanini unampenda?”
“Sina sababu mama ila nampenda tu yani Erick amekaa kwenye moyo wangu mama”
“Na je huyo Erick anakupenda kama wewe unavyompenda?”
“Ndio mama Erick ananipenda sana”
“Ila mwanangu Erica mapenzi unayajua vizuri kweli? Wanaume wanabadilika kama kinyonga, hata Sia aliamini kuwa Erick anampenda sana na hawezi kumuacha mwisho wa siku kamuacha, Erica mimi ni mama yako na ndio naujua uchungu wako, mimi ndiye nikupendaye kwa dhati mwanangu. Unanielewa Erica?”
“Nakuelewa mama”
“Naomba uachane na Erick”
“Hapana mama,nampenda sana Erick”
“Kumbuka kuna mtu alijaribu kujiua sababu ya Erick, je moyo wako utakuwa na amani iwapo Sia akifa?”
“Hapana mama, ila je wewe utakuwa na amani iwapo mimi nikifa?”
“Kwanini unasema hivyo sasa?”
“Mama, mkiniachanisha na Erick basi sina sababu ya kuishi pia”
“Wewe mtoto ni punguani sana, hebu nitokee mbele ya macho yangu hapa tafadhali. Erick, Erick ni nani kwenye nyumba yangu? Aah watoto wa siku hizi, tuzaa basi tu”
Erica aliondoka na kwenda kuendelea na shughuli zingine ila alishukuru vile alivyomwambia mama yake ukweli kuwa hawezi kuachana na Erick.
Jioni ya siku hiyo kuna simu ilimpigia Erica, alipoiangalia kwa makini akaona ni namba ya mzee Jimmy, hakutaka kupokea ila aliipokea tu,
“Erica, hupendi kuishi kwenye nyumba ya kifahari nay a kisasa?”
“Unazungumzia nini kwani?”
“Aaah nilikuwa nakusalimia tu, binti chaurembo”
“Haya asante, kwaheri”
Erica akakata simu kwani hakutaka kutumia muda wake mwingi kuongea na Mzee Jimmy wakati hamtaki.
 
SEHEMU YA 336

Siku moja jioni, wakati Erica akifanya shughuli zake, alishangaa kupata ugeni na mgeni huyo alikuwa ni Dora, ila Erica alimkaribisha tu sababu hakuwa na ugomvi nae kwa kipindi hiko, kwao alimkaribisha ila mialiko ya Dora hakuitaka.
Dora alianza kuzungumza na Erica,
“Erica nimeamua kuja kukwambia jambo hili sio unicheke au unione kuwa sina akili hapana, nimekuja kukwambia tu ili na wewe ujilinde”
“Jambo gani hilo Dora, siwezi kukucheka”
“Erica nimetangatanga sana, yani mimi nadhani nimetembea na wanaume wa kila rangi ila siku zote nilikuwa naenda kupima na kujikuta niko mzima tu, kiasi kwamba nilihisi ukimwi haupo duniani, niliona watu wanaosema tuna ukimwi hajajifikiria vizuri, ila kipindi hiki yamenitokea puani, huwezi amini, nimeenda kupima wiki iliyopita nimekutwa nimeathirika, Erica Yule mzee jimmy ameathirika”
Kiukweli Dora alikuwa akiongea kama mtu anayejutia sana na alitia huruma, hata Erica akamuonea huruma sana, Dora aliendelea kuongea,
“Erica, Yule mzee si mtu mzuri, anaambukiza mabinti wengi sana, Yule mtu mzima kumbe ana lengo lake la kuua vijana, hadi huwa najuta vile nilivyokuwa nakulazimisha utembee na Yule babu, Erica nisamehe rafiki yangu”
“Usijali nishakusamehe”
“Jambo lingine Erica, tena ngoja nikwambie kabla sijasahau”
“Jambo gani hilo?”
“Kama una mpenzi Erica, usitaje jina la mpenzi wako kwa huyu mzee, yani alichomfanya mpenzi wangu dah!”
“Kamfanyeje?”
“Nitakwambia tu siku moja ila kwa leo yanatosha hayo niliyokwambia”
“Mmmh Dora ungeniambi kidogo”
Dora aliamua kubadilisha mada kwani hakutaka kujadili kile ambacho mpenzi wake alifanywa na mzee Jimmy.
“Ila uwe unakuja kunitembele, mwenzio sina raha kabisa kabisa Erica”
“Sawa usijali, pole sana”
Kisha Dora hakukaa sana aliondoka zake, kwakweli Erica alitafakari sana na akatafakari kama ingetokea siku hiyo Yule mzee angembaka ingekuwaje,
“Kwakweli Mungu alinisaidia sana jamani, Mungu nilinde hadi niolewe na Erick”
Alikuwa akijisemea tu, giza lilipoingia alienda chumbani kwake na kusikia simu inaita, kuangalia ni namba ngeni, akapokea na kukuta ni mzee Jimmy, Yule mzee baada ya salamu tu akaanza kumwambia Erica,
“Usisikilize maneno ya Dora, Yule binti ni mjinga sana sijapata kuona”
“Mbona sikuelewi?”
“Kaniambia kuwa anakuja kukwamabia kwamba mimi nimeathirika, Yule binti ni mpumbavu na wivu tu unamsumbua, kisa kaona kuna nyumba nzuri nimenunua na nimesema nataka nikupe wewe zawadi kwenye siku yako ya kuzaliwa basi yeye kasikia wivu akaniambia ooh siku zote unakuwa na mimi halafu ukampe zawadi Erica kweli? Akasema anakuja kukwambia kuwa mimi nina ukimwi ili unichukie ila si kweli Erica”
“Iwe kweli au si kweli, bado sina mpango na wewe nampenda sana mpenzi wangu”
“Anaitwa nani huyo mpenzi wako?”
Erica akakumbuka maneno ya Dora kuwa huyu mzee hata akikuuliza jina la mpenzi wako usimwambia sababu ana hela, anaweza akamfanyia jambo lolote baya, basi Erica akamwambia,
“Hapana, sikwambii na sio muhimu wewe kumfahamu”
“Ila Erica, kumbuka nakupenda sana hata ukisema vipi ila upendo wangu kwako uko pale pale”
Erica aliamua kukata simu tu kwani alihisi ni kizunguzungu.
Muda kidogo aliitwa na mama yake maana na siku hiyo alitoka pia, Erica alienda kuongea na mama yake,
“Nilienda tena kumuona Sia, mwanangu Sia anatia huruma sana, ila kuna kitu sielewi kabisa”
“Kitu gani mama?”
“Yule binti ni mjinga sana, hivi kupendaje huko hadi utake kudhuru maisha yako sababu ya mwanaume loh! Watoto wetu mmepotea kwakweli, ila ngoja nikuulize tena na wewe”
“Niulize mama”
“Utawezaje kuishi na mwanaume ambaye ndugu zake wote hawakutaki?”
“Mama, ngoja niseme mambo ambayo huwa yananitokea, sijawahi kupata mwanaume yoyote ambaye ndugu zake wakanipenda, je sitaolewa? Nashukuru Mungu ingawa ndugu wa Erick hawanitaki ila Erick ananipenda”
“Ushawahi kujiuliza kwanini ndugu huwa hawakutaki?”
“Huwa sielewi mama ila hakuna ndugu wa mwanaume amewahi kunipenda mimi, anaweza kunipenda ila akisikia tu nina mahusiano na ndugu yake basi upendo wake unaishia hapo”
“Je mama yake Erick umewahi kuonana nae?”
“Ndio nimewahi mama, yani Yule mama alikuwa akinipenda sana mwanzoni ndio kazini kwake nilikuwa nafanya kazi ila gafla Yule mama aliposikia kuwa nina mahusiano na mtoto wake akanichukia tena kanichukia haswaa bila hata sababu, je wewe umeonana nae?”
“Hapana sijaonana nae ila kwa inavyoonyesha Yule mama hakutaki kabisa kutokana na maelezo niliyopata kwa Tumaini, tena anasema kuwa umemroga mtoto wake. Ila Erica ningekuwa mimi ni wewe nisingeendelea na huyo mtu”
“Mama samahani kwa hili nitakalokuuliza, umewahi kusema hata uliiba ng’ombe kwenu ili uolewe na baba, si inamaana ulimpenda sana kiasi kwamba hukujali lolote lile, mbona mimi unanikataza kumpenda Erick mama? Nampenda sana Erick, labda aniache yeye ila mimi sina mpango wa kumuacha”
“Kweli hapa mtoto sina jamani, haya nimechoka hayo maneno yako ya nampenda nampenda nampenda, mwambie aje hapa nyumbani na tufanye harusi, maswala ya kupendana siyataki”
“Atakuja mwezi ujao”
“Ndio alivyokudanganya hivyo! Haya bhana, nenda kalale tu maana kila nikiongea nawe nachefuka”
Basi Erica aliondoka ila alikuwa na imani kuwa ipo siku Erick atamuoa, kipindi hiko aliamua kujitoa kwa hali zote kuwa amsubirie Erick tu bila kujali kama Erick akibadilisha maamuzi atamuumiza kwa kiasi gani, kichwani mwake aliona bora amuwaze Erick tu.
Aliingia chumbani kwake na kujisemea,
“Kwa kipindi hiki nitakomaa na Erick hadi kieleweke, hata akiniacha najua na Mungu naye atanipigania ila siwezi kutangatanga tena na mapenzi, imetosha kuitwa majina ya ajabu, nimekuwa Erica mpya. Dunia haina usawa kabisa hii, mtu anakutongoza na kukuonyesha dalili zote za kukupenda, unaamua kumkubali na kuwa naye, unamuheshimu na kumpenda, eti kesho na keshokutwa anakuita malaya kweli? Malaya sababu ulimpenda, malaya sababu ulijitoa kwaajili yake? Rahim nimemvumilia, nilikuwa naumia ila nakazana kwani niliamini ndiye mume wangu, ila leo ananiita malaya kweli? Ananiita mwanamke nisiyefaa kwenye jamii sababu nilitunza mimba aliyonipa na kuzaa? Wanaume hawa, ila nampenda Erick hata iweje nampenda Erick”
Aliwaza sana na kutaka kulala, ila kabla hajalala akapigiwa simu na Erick na kutabasamu vilivyo, alipopokea simu ya Erick akamsalimia,
“Mambo Erick”
“Mmmh unatakiwa uanze kujifunza sasa Erica”
“Kujifunza nini?”
“Uwe unaniambia uhali gani mume wangu, unajua mimi ndio mumeo eeh!”
Erica akatabasamu tu yani kiukweli alikuwa akisikia raha sana kuongea na erick.
“Kuna kitu nataka kukuuliza Erica”
“Niulize tu”
“Hivi umezaliwa tarehe ngapi na mwezi gani? Nataka kujua siku yako ya kuzaliwa”
Erica akatabasamu na kumjibu Erick maana kipindi chote amekuwa akiwasiliana na Erick ila hawajawahi kuulizana kuhusu tarehe zao za kuzaliwa, leo ilikuwa ni mara ya kwanza yani Erica alihisi labda kuna kitu Erick anataka kufanya kwaajili ya siku yake ya kuzaliwa, alimjibu kwa bashasha kubwa sana,
“Nimezaliwa tarehe nne mwezi wa nne”
“Kheee Erica, hapana kwakweli”
“Hapana nini?”
“Unajua na mimi nimezaliwa tarehe ngapi?”
“Ni ngapi ndio”
“Tarehe nne mwezi wa nne yani tarehe hiyo hiyo na mwezi huo huo uliozaliwa wewe, kwakweli tunahaki ya kupendana Erica, sisi ni wa tofauti ujue”
Erica alitabasamu tu ila kiukweli hakupendezewa kuwa na tarehe moja ya kuzaliwa na Erick maana alianza kuhisi vitu vingi sana. Ila aliongea tu kama kawaida na kuagana na Erick.
Alipokuwa analala akajiwa na wazo,
“Mungu wangu isije kuwa Erick nae ni ndugu yangu, kwanza nafanana nae majina, halafu nimezaliwa nae tarehe moja mmh! Jamani nina mashaka na hivi watu wanaibaga watoto uwiii, naomba asiwe na undugu na mimi jamani nampenda sana”
Alisubiri pakikucha amuulize kwa mitego mama yake.
 
SEHEMU YA 337

Palivyokucha, alifanya shughuli zake na alipomaliza alitaka kuongea na mama yake ila hakuwepo kumbe alidamkia tena hospitali kumuangalia Sia, kwenye mida ya mchana mchana ndio akarudi ndipo Erica aliongea na mama yake,
“Hivi mama hujawahi kuzaa mapacha wewe?”
“Mmmh sijawahi, hata kwetu hakuna historia ya pacha. Kwanini umeuliza hivyo?”
“Napenda sana mapacha, natamani siku moja nizae mapacha”
“Ili uwaite Erick na Erica sio, maana umeona mwanaume mnafanana kidogo majina basi ndio umekufa umeoza”
Erica akacheka tu na kumuuliza tena mama yake,
“Hujawahi kuzaa mtoto mwingine wa kiume zaidi ya kaka Tony?”
“Kwakweli Tony, ndio mwanangu pekee wa kiume. Nilipokuwa na mimba yako nilijua labda atakuwa wa kiume ila wapi, nikajifungua wa kike ila nawakubali watoto wangu ambao Mungu amenipa”
“Mama hujawahi kuwaza kuwa pengine mimi niibadilishwa hospitali!”
“Nibadilishiwe kwa lipi? Wewe ni change langu na nimekukubali, mimi nimezaa kawaida kabisa, na mtoto nimempokea mwenyewe, nabadilishiwaje sasa, halafu wewe badala uniulize habari za hospitali unakazana kuniuliza maswali ya kijinga”
“Jamani mama”
“Sio, jamani mama badala uulize Sia anaendeleaje wala hujishughulishi kujua wala nini?”
“Nilisahau mama, anaendeleaje?”
“Mpaka nikuseme loh! Roho mbaya hiyo, Sia anaendelea vizuri ila nashangaa kwakweli huwa wanasema mama Erick anampenda sana Yule binti ila tangia nianze kwenda hospitali sijawahi kukutana na huyo mama Erick hata kidogo, ndio upendo ule hapana. Sasa mwanangu ile sio familia kama mtu wanatempenda ndio wanamfanyia hivyo, je wewe wasiyekupenda itakuwaje, tafakari chukua hatua mapema, sina mengi ya kusema ila kuwa makini”
Erica alimsikiliza mama yake ila kwa muda huo alishakata shauri la kumpenda tu Erick hata iweje.
Jioni ya siku hiyo Erica alipigiwa simu na Dora, akapokea na kuanza kuongea nae,
“Erica sina nia mbaya na wala si wivu unaofanya nikwambie haya, Yule mzee kanunua nyumba ya kukupa wewe ila kuna siri nzito sana katika hiyo nyumba”
“Ila Dora si nilikwambia kuwa simtaki huyo mzee wala chochote chake, au hukunielewa jamani! Huyo mzee hata anipe dunia simtaki”
“Erica, Yule mzee ana akili sana usifikiri hajui kuwa utaikataa ila mpango alioweka kwako ni kabambe, utajikuta ukikubali mwenyewe”
“Kheee Dora ushindwe na ulegee”
“Yani wewe badala ya kusema ni nini eti unasema nishindwe, nilitaka nikusaidie ila sababu hutaki kusaidiwa basi kwaheri”
Dora akakata ile simu ila Erica alibaki na maswali mengi sana, sema aliamua kupotezea kwani hakuhisi kuwa kuna lolote baya juu yake ukizingatia Yule mzee hakumtaka.
Basi wkati wa kulala aliamua kumpigia simu Erick ili kuongea nae tu kwani baada ya kuwa na uhakika si ndugu yake alijikuta akiwa na upendo nae maradufu,
“Eeeh Erick kwanini jana uliuliza kuhusu tarehe yangu ya kuzaliwa?”
“Subiri uone kuna kitu nitafanya siku hiyo, na hivi ni tarehe moja na yangu nataka iwe siku ya kumbukumbu kwenye maisha yetu:”
“Kitu gani hiko?”
“Hapana sikwambii Erica ila ni kitu cha kukushtukiza tu”
Erica alimbembeleza sana amwambie ila hakumwambia, kwahiyo alibaki tu kungoja kuwa ni kitu gani kitatokea siku hiyo, aliagana nae na kulala.

Ilikuwa siku ya Erica kumpeleka mwanae kliniki, kwahiyo alijiandaa kisha akampeleka mtoto wake kliniki, wakati anatoka akakutana na mwanamke akiwa na mimba kubwa tu ameongozana na mumewe, basi akajikuta akigongana macho na Yule mwanaume, akashangaa sana kuona kuwa yule mwanaume ni Bahati ila kile kitendo cha Erica kugongana macho na Bahati kilikuwa kama kimewehusha akili ya Bahati, kwani alionekana kama mtu aliyeshtuka toka usingizini na kusema,
“Erica”
 
SEHEMU YA 338

Ilikuwa siku ya Erica kumpeleka mwanae kliniki, kwahiyo alijiandaa kisha akampeleka mtoto wake kliniki, wakati anatoka akakutana na mwanamke akiwa na mimba kubwa tu ameongozana na mumewe, basi akajikuta akigongana macho na Yule mwanaume, akashangaa sana kuona kuwa yule mwanaume ni Bahati ila kile kitendo cha Erica kugongana macho na Bahati kilikuwa kama kimewehusha akili ya Bahati, kwani alionekana kama mtu aliyeshtuka toka usingizini na kusema,
“Erica”
Erica alimuangalia tu bila kusema chochote, ila Bahati alimsogelea Erica na kumshika yani kama mtu anayechunguza jambo Fulani, kisha akasema
“Erica, kumbe ni wewe”
Akamkumbatia, mkewe alikuwa pembeni tu akimuangalia ila alikuwa amechukizwa sana, na Erica aliweza kuiona chuki ya Yule msichana, ikabidi ajigeleshe na kumwambia Bahati,
“Wewe Bahati kwani vipi?”
Ile sauti ya Erica ni kama iliongezea kumshtua Bahati kiasi kwamba Bahati akumbuke hadi Yule mtoto wa Erica aliahidi kuwa atakuwa wa kwake,
“Erica, mwanetu hajambo? Nipe Angel nimbebe”
Mke wa Bahati akasogea karibu na kuingia kati yale maongezi ya Bahati na Erica, akamwambia Bahati,
“Mme wangu tumekuja kliniki au umekuja kuongea na wanawake zako jamani?’
Bahati aliongea kitu cha kumjibu Yule mkewe hadi Erica alishangaa kwakweli,
“Hivi mimi nimekuoaje wewe Nasma, naanzaje kukuoa wewe na kumuacha Erica? Sikutambui”
Erica akaona kutakuwa na mgogoro hapo kwahiyo akaamua kuondoka ila Bahati alimuacha mke wake pale na kumfatilia Erica hadi nje ya ile hospitali, Erica alitaka kupanda bajaji ila akamzuia na kusema,
“Kwanini upande Bajaji wakati mimi nipo nina gari?”
“Bahati, nenda kwa mkeo kule anakusubiri”
Erica akasimamisha bajaji na kupanda kisha akaondoka na kumuacha Bahati akiwa ameduwaa pale.
Bahati alionekana kama kuchanganyikiwa hivi kwani alikuwa hata haelewi imekuwaje amuoe Nasma wakati anayempenda ni Erica? Akaamua kwenda kwenye gari yake ili aende kwakina Erica maana alikuwa anakufahamu ila hajaelewa tu imekuwaje mpaka kipindi chote hiko hajawahi kwenda kwakina Erica.
 
SEHEMU YA 339

Wakati Erica yupo kwenye bajaji, Moses alimpigia simu na kumwambia kuwa afike dukani mara moja, kwahiyo Erica alimuelekeza Yule wa bajaji ampeleke dukani ili aonane na Moses ajue anamuitia nini.
Alipofika alimkuta Moses akimsubiria nje, Erica alishuka na mwanae, Moses akamsalimia na kumuuliza,
“Imekuwaje upande bajaji?”
“Hahaha, tunapanda kile ambacho tunaweza kugharamia”
“Erick anajua hilo?”
“Kwanini umeniuliza hivyo?”
“Nimeuliza tu, karibu”
Basi Erica aliongozana na Moses hadi kwenye ofisi ya duka, kisha alianza kumsikiliza kuwa ni kitu gani alichomuitia,
“Kuna faili unatakiwa usaini”
“Linahusu nini?”
“Kwani Erick hajakueleza?”
“Hapana, hajaniambia chochote”
“Kuna event ipo tarehe nne mwezi wan ne, unatakiwa usaini ili niipeleke kwa wahusika”
“Wahusika ndio wakina nani hao?”
“Wewe isaini halafu muulize hayo maswali Erick atakujibu”
Basi Erica alichukua kweli na kusoma, akaona muhusika wa hilo jambo ni yeye na Erick, hakuelewa ni jambo gani sema sababu alimuamini Erick aliamua kusaini bila mashaka yoyote, kisha akataka kuondoka ila Moses alimwambia kabla hajaondoka anataka ampeleke kwenye duka lingine la Erick, kwakweli Erica alishangaa kidogo na kukubali, kisha walitoka pale na Moses na kupanda gari ya Moses wakielekea huko.
Kwenye gari Erica aliamua kumuuliza Moses kimtego,
“Kwani Erick kakuambia mimi ni nani yake?”
Moses alicheka kisha akamjibu,
“Kasema wewe ni partner wake”
Erica akatabasamu, ila Yule Moses akamuuliza,
“Niambie kama kuna cha zaidi?”
“Hamna bhana, ndio hivyo hivyo”
“Ila mbona Tumanini anakuchukia sana?”
“Sijui kwanini”
“Na kwenye hilo duka yupo yeye”
Erica alivyosikia hivyo alihisi akikosa muelekeo kabisa, maana hakuna kitu alichokuwa anakiogopa kama kukutana na Tumaini, akamwambia Moses kuwa asiende tena, ila Moses alikazana kusema ni lazima Erica afike kwenye hilo duka.
“kwani unamuogopa nini Tumaini, lile ni duka la Erick, Tumaini anakusumbua nini sasa?”
“Hapana, sikutaka tu kuonana nae kwasasa”
“Usijali, mimi nipo”
Moses alimshawishi Erica hadi akakubali kwenda kwenye hilo duka.
 
SEHEMU YA 340

Bahati alifika nyumbani kwakina Erica na kugonga, alifunguliwa mlango na mama yake Erica ambaye alionyesha kushangaa sana ujio wake, Bahati akamsalimia na kumuulizia Erica, ila huyu mama alimkaribisha ndani kwanza ili amuhoji, Bahati akaingia na kukaa, kisha mama Erica akaanza kuongea,
“Haya leo umekumbuka nini, si niliambiwa umeoa wewe?”
“Mama, nimemuona Erica, naye anasema nimeoa niongozane na mke wangu, kwakweli mama sielewi hata imekuwaje hadi nimeoa mwanamke mwingine, mwanamke ninayempenda ni Erica tu na itabaki hivyo siku zote”
“Sasa mwanangu atakuwa mke wa pili?”
“Nipo tayari kumuacha huyu niliyemuoa”
“Weee usilete laana kwenye ukoo wetu, yani umuache huyo umuoe mwanangu! Haipo hiyo, kwanza Erica hayupo?”
“Yuko wapi?”
“Wewe si ulioa? Erica nae kaolewa, kwahiyo yupo kwa mume wake”
Mama Erica alimdanganya Bahati maana alishajua alivyoking’ang’anizi ila Bahati alijihisi vibaya saba kuambiwa kuwa Erica kaolewa, alitamani hata ardhi ipasuke, akaanza kulia,
“Mama, kwanini mmenifanyia hivyo lakini? Erica wangu nampenda sana, kwanini mama?”
“Weee usinichulie, mara ya mwisho umekuja hapa na familia yako mkaongea maneno ya kejeli sana, halafu baada ya hapo hukuja tena eti leo hii ndio unafika na kilio kuwa unampenda sana Erica, umechelewa kwakweli tena umechelewa haswaa, ulikuwa ukiishi huko kwa raha zako hata mwanangu humkumbuki, leo hii eti Erica ndio mwanamke wa maisha yangu. Hebu nitolee balaa mimi, ulimwaga mboga, na sisi tukamwaga ugali, umeoa na Erica ameolewa kwaheri”
Kwakweli Bahati aliinuka na kuondoka ila alikuwa anajisikia vibaya sana, kiasi kwamba hakuweza hata kwenda nyumbani kwake kwa muda huo na kuamua kwenda ufukweni ambako alikutana na Erica kwa mara ya kwanza.

Walifika dukani na kushuka, kiukweli Erica hakutaka kabisa kuingia kwenye duka ambalo yupo Tumaini maana akifikiria na matatizo aliyoyapata Sia ndio akazidi kuwa na mashaka. Walivyoshuka tu Erica aliomba kuonyeshwa uwani ili akajisaidie, na aligoma kuacha mkoba wala mtoto wake, ikabidi Moses amuonyeshe,
“Ukizunguka hapo nyuma tu utaona vyoo vya kulipia”
Basi Erica akazunguka ila hakuingia chooni badala yake alisimamisha bodaboda na kupanda na mwanae kisha ile bodaboda ikaondoka.
Walipofika mbele mbele, bodaboda iliishiwa mafuta kwahiyo Yule wa bodaboda akapita sheli ili kuweka mafuta, wakati yuko pale sheli alitokea mtu mmoja na kumshika bega, Erica alipogeuka Yule mtu alikuwa ni Babuu, basi akasalimiana nae huku akihisi lazima Babuu ataongea nae maneno machafu tu, ila Babuu alianza kusema,
“Erica huyu mtoto anazidi kufanana na Rahim”
“Sitaki uendelee kumfananisha mwanangu na mwanaume ambaye hajui umuhimu wa mtoto”
“Sijasema kwa ubaya wala kwa kejeli ila nimesema ukweli, ila Erica kupanda pikipiki na mtoto sio vizuri ujue”
Yule bodaboda alipomaliza kujaza alimwambia Erica apande tena waondoke, ila Babuu akamuuliza Yule bodaboda,
“Kwani unamdai shilingi ngapi hadi hapa?”
“Elfu mbili”
Babuu aliitoa ile hela na kumpa bodaboda, kisha Yule dereva akaondoka zake, kisha Babuu akamwambia Erica,
“Hata kama Rahim hataki kumuhudumia mtoto ila bado sio sababu yaw ewe kupanda pikipiki na mtoto, ni hatari sana. Baba zake wadogo tupo, tuambie tutamuhudumia, ila naumia sana maana huyu mtoto angekuwa damu yangu kabisa, yani mimi badala ya kuwa bamdogo ningekuwa baba”
“Achana na mimi kabisa”
Erica akataka kwenda kusimamisha usafiri mwingine aondoke, ila Babuu alimuitia usafiri na muda kidogo tu gari la kukodi lilifika kisha Babuu akafungua mlango ili Erica na mtoto wapande na walipopanda tu na yeye akapanda na kumuelekeza dereva kwakina Erica ili awapeleke.
Erica alimuangalia Babuu maana alimshangaa ule moyo wa huruma vile kautoa wapi,
“Kwanini umeamua kufanya yote haya?”
“Erica, kiukweli nimekaa nikafikiria na kuona kwamba katika maisha yako nina sababu kubwa sana ya kujilaumu na mimi kuliko kukulaumu wewe, kukuita malaya sijui hufai sio maneno yanayofaa kwani kwa kiwango Fulani ni mimi nimesababisha yote”
“Kwanini unasema hivyo?”
“Erica, mimi nina makosa kwako nina uhakika kama ningekutambulisha ndugu zangu basi isingetokea iliyotokea kuwa ungetembea na ndugu zangu. Erica, siwezi kukuweka kwenye kundi la wanawake malaya ila najua kuna kitu kilisababisha tusiwe pamoja, na kama hatukuwa pamoja tena isingekuwa rahisi kwa wewe kuishi tu bila mtu, yani umetembea na ndugu zangu imeniuma ila kosa ni langu kwa kutokukutambulisha ndugu zangu. Mapenzi yetu tulikuwa tunayajua wenyewe, Erica hukumfahamu ndugu yangu hata mmoja wala rafiki yangu, wala mawasiliano yao kwahiyo mimi kukulaumu kuwa umetembea na ndugu zangu nitakuwa nafanya makosa maana ulifanya vile kwa kutokujua.”
“Na mimi samahani sana kwani sikusikiliza ushauri wako, nakumbuka siku ile niliyoenda kukutana na Rahim sikutaka hata kukusikiliza kuwa unazungumzia nini, nilimuamini sana Rahim, niliamini ni mwanaume atakayenifaa yani sikuhisi kama kuna kipindi Rahim atabadilika kama sasa”
“Usijali Erica, ila kuhusu huduma za mtoto uwe unatuambia hata sisi, ili mradi tunajua ukweli kuwa ni mtoto wa ndugu yetu, tuambiage tumuhudumie”
“Niwaambie wakati mama yenu hajaonyesha kujali hadi leo?”
“Muache Yule mama kapagawa sasa hivi, kaletewa watoto watatu wa Rahim pale kwake yani haamini maana alimuona Rahim ni mpole sana, kumbe bora ya sisi”
Erica akashangaa sana, kuwa Rahim kapelekewa watoto watatu? Akawaza na mke wa Rahim anajihisi vipi,
“Na mke wake je kakubali hiyo hali?”
“Akatae vipi sasa, ila yupo kama kachanganyikiwa, anagombana na kila mwanamke anayehisi ni mwanamke wa Rahim, na hivi ana mimba ndio balaa”
Walifika kwakina Erica na kusha, kisha Babuu akaagana nae kurudi kwenye lile gari halafu Erica akaingia ndani kwao.
 
SEHEMU YA 341

Alimkuta mama yake ambaye alimuuliza,
“Kheee kliniki gani mwenzetu hadi saa hizi?”
“Aaaah mama, kulikuwa na foleni”
“Basi alikuja mumeo wa zamani”
“Nani huyo tena mama?”
“Si Yule muuza samaki”
Hapo ndio Erica akapata picha kuwa Bahati alijua ameenda kwao ndiomana akamfata, ila alishindwa kuelewa kuwa akili zimemrudi au vipi, kisha akamuuliza mama yake ambacho kilisemwa na Bahati, na mama yake akamueleza Bahati alivyosema, Erica alimsikitikia sana,
“Masikini Bahati, kweli alirogwa Yule”
“Ila sio kosa letu, ni kosa la ndugu zake”
“Ndio mama, ila kwanini ndugu hufikia hali kama hiyo jamani! Ona sasa atahisi kuchanganyikiwa Bahati”
“Kwahiyo wewe unamtaka Bahati au Erick?”
“Erick nampenda ila Bahati namuonea huruma, hata kuachana nae ningeachana nae kwa amani ila sio kwa njia waliyoitumia ndugu zake, unajua amemuacha mkewe hospitali na kunifata mimi? Yani nimekutana nae kliniki, wakati natoka ndio kanifatilia”
“Haya mbona yeye aliwahi kufika na wewe ndio unaingia saivi?”
“Nilipita kwenye lile duka la nguo mama, lile Angel amekuwa balozi, waliniita mara moja”
“Mbona mwanzo umenidanganya kuwa kliniki kulikuwa na foleni?”
“Nisamehe mama”
“Yani uongo huachi! Hebu jifunze kuwa mkweli Erica, kwa mtindo huo utamuingopea hadi mumeo na muanze kugombana bure, jifunze kuwa mkweli”
“Sawa mama, nisamehe”
Kisha Erica akaenda chumbani kwake ila habari ya Bahati ilimuuzunisha sana, hakuelewa ni kwanini Bahati alipomuona alistuka,
“Au zile dawa hazikutaka aonane na mimi? Ningejua toka ile siku anafunga ndoa si ningejionyesha anione? Nampenda Erick ila namuhurumia Bahati, ningeweza kuachana nae kwa amani na angetafuta mwanamke anayempenda kweli na sio mwanamke wa kuvutiwa kwa madawa, kwakweli ndugu zake wamefanya dhambi sana.”
Akaendelea kufanya mambo mengine tu.
 
SEHEMU YA 342

Usiku ulivyofika akampigia Erick, na kusalimiana nae na kuongea nae kisha akamuuliza,
“Erick, kwanini kutaka kunipeleka mimi dukani kwa Tumaini na unajua sipatani nae?”
“Muda gani nilitaka kukupeleka dukani kwa Tumaini?”
Erica akamueleza Erick ilivyokuwa hadi kutaka kwenda dukani kwa Tumaini na kukimbia,
“Erica, unaniambia Moses alikupa fomu usaini?”
“Ndio, kasema wewe ndio umeagiza eti nisaini sijui kuna event ya tarehe nne mwezi wa nne, kasema nisaini kuna mahali inapelekwa”
“Na Moses huyo huyo akataka kukupeleka dukani kwa Tumaini?”
“Ndio”
“Huyu Moses vipi katumwa au nini? Subiri niwasiliane nae ili nijue kwanini kafanya hivyo, hakuna kitu ulichotakiwa kusaini, kwanini kafanya hivyo jamani? Aaaah yani penzi letu kila kukicha linavamiwa na vidudu mtu tu, huyo Moses nitamuuliza asiponipa majibu ya kuridhisha namfukuza”
“Hapana Erick usifanye hivyo, jua yeye ndio anasimamia vyema”
“Hata kama, sijamtuma aingilie maisha yangu binafsi mimi, subiri kesho”
Kisha akaagana nae na kukuta simu, kiukweli hata Erica alikuwa akijiuliza haswaa kuwa kama Erick hajatoa hayo maelezo ni kwanini sasa Moses afanye hivyo? Hakuelewa na kuamua kulala, ila kabla hajalala akapokea ujumbe, kuangalia ulitoka kwa Rahim,
“Erica, umeamua kunidhalilisha kwa ndugu zangu kuwa simuhudumii mtoto? Ingia kwenye mtandao tuongee”
Erica aliangalia ule ujumbe mara mbili na kuweka simu pembeni kisha akalala kwani hakutaka hata kujisumbua kuingia kwenye mtandao.

Kulipokucha aliamka na kufanya shughuli zake za hapa na pale, mchana akapigiwa simu na namba ngeni, alipopokea alikuwa ni Sia akasema,
“Erica, niachie Erick tafadhali, nakufa kwaajili yake”
“Sia, niachie Erick tafadhali nakufa kwaajili yake”
Yani Erica alimgeza Sia yale yale maneno aliyoyaongea, ila hakujua kama hiko kitendo kimemkera sana Sia kiasi kwamba aliamua kukata simu sababu aliona ni kejeli, ila alipokata simu Erica alijisemea,
“Kwani sisi wengine ndio hatujui kufa au? Na mimi nakufa kwaajili yake asinibabaishe”
Kwakweli Erica alikuwa kashachoshwa na mada za malalamiko na lawama ndiomana akafanya vile, muda kidogo akapigiwa na namba nyingine ngeni na kupokea, ilikuwa ni sauti ya Tumaini,
“Hivi wewe Erica unajiona una nini wewe? Yani wewe wa kunigombanisha na mdogo wangu?”
“Nimekugombanisha nini?”
“Kwanini umwambie kuwa kuna fomu ulikuja kusaini?”
“Sasa Tumaini, nisaini fomu halafu nisimwambie muhusika nitakuwa mzima kweli? Yule ndio muhusika ndiomana nimemwambia”
“Halafu Sia anakupigia unamjibu kwa jeuri, msichana una kiburi sana wewe”
“Labda una mambo yako tu ila mimi sina ubaya wowote na wewe wala na huyo Sia”
“Subiri nitakufundisha somo”
Kisha akakata simu, kuna mambo mengine Erica alikuwa akishangaa tu, maana Tumaini anaonekana anafanya kila hali ili kakake asiwe na Erica, ila Erica hakutaka kabisa kuwaza hayo yote, akamshangaa Sia pia kutoka hospitali tu na kuanza kuwaza kuhusu maswala ya mapenzi yale yale yaliyomsababisha ajaribu kujiua,
“Ndiomana serikali ukijaribu kujiua tu unafungwa kuepeka watu wenye akili mbovu kama Sia”
Kisha akaendelea na shughuli zake.
 
SEHEMU YA 343

Jioni ya siku hiyo akiwa ametulia zake huku akicheza na mwanae, akapigiwa simu na Dora, na kuamua kupokea hivyo hivyo ingawa anapataga kukereka sana kutokana na maneno ya Dora,
“Erica, sikuonei wivu na wala usione nakusumbua ila nataka nikuponye”
“Uniponye vipi wakati nishakwambia huyo mzee simtaki!”
“Sawa ila kuna jambo nataka nikwambie la kukusaidia”
“Jambo gani hilo”
“Erica, nasikia kuna siku huyo baba alikutumia vocha ya shilingi elfu hamsini, kama una hela nenda kaweke vocha na umrudishie”
“Kwanini?”
“Erica, mzee huyu atatumia hilo swala, kukuumiza na kukutesa. Nakupenda rafiki yangu naomba ufanye hivyo”
Erica aliamua kusikiliza ushauri wa Dora na kuamua kwenda kuchukua hela ndani kwao, kisha akamuacha mtoto na mama yake halafu yeye akaenda kununua vocha, kwakweli hakutaka mchezo na Yule mzee kabisa maana mambo yake yanajulikana yalivyo.
Alienda dukani na kununua vocha, ila wakati anarudi alikutana na rafiki yake Johari, ni kitambo sana hakukutana nae, alimkumbatia pale na kuanza kuongea nae ambapo Johari akamwambia,
“Erica umekuwa adimu sana, jamani nilikuja kwenu mamako alinitimua balaa”
“Aaaah pole mwaya, vipi bado unaishi na Yule mume wako?”
“Ndio, na anakuja ndio tunaenda nyumbani kusalimia. Subiri umuone shemeji yako”
“Oooh nitafurahi sana kumfahamu”
“Anakuja, kwakweli namshukuru sana Mungu baada ya kupitia machungu yote akatokea wa kunifuta machozi yangu, baba wa wanangu, nampenda sana maana kanifichia aibu yangu. Si nilikusimulia Yule mwalimu alichofanya eeeh! Ila Mungu mwema nimempata mume wangu, amenifichia aibu yangu, nimezaa nae mtoto mmoja ila anamlea na Yule mtoto wa mwalimu, huwezi kutofautisha kwani anawapenda wote kama wanae”
Basi huyo mtu alifika na Johari kuanza kumtambulisha Erica kwa shemeji yake,
“Huyu anaitwa Erica ni rafiki yangu sana, Erica huyu anaitwa Juma ndio mume wangu”
Erica akampa mkono Juma, ila alijisikia vibaya sana kwani huyu Juma ndio Yule jamaa wa TRA ambaye alimtengenezea leseni na ndio Yule alimjibu vibaya kwenye daladala, ila hakutaka Johari ajue kama ameshawahi kumjibu vibaya huyo kaka, akaongea ongea nao kidogo na kuagana nao.
Alirudi kwao na sura ya aibu sana kwani hakutegemea kukutana tena na Juma zaidi ya ofisini kwa shemeji yake,
“Kumbe kijana wa watu ni mpole tu, kweli usimfikirie mtu ubaya kwa kumuona, kumbe Juma ana moyo wa upendo. Mungu amzidishie kwakweli”
Erica alifika kwake na kuweka ile vocha kisha muda ule ule akamtumia mzee Jimmy na kuendelea na mambo yake mengine.
 
SEHEMU YA 344

Usiku wake akapokea simu kutoka kwa Dora akimuuliza kama ile vocha ameshaituma,
“Tayari nimeshairudisha”
“Basi akikuuliza mwambie mpenzi wako kaiona kwahiyo kasema uirudishe”
“Sawa, lakini kwanini hivyo?”
“Erica, ipo siku nitakwambia kwanini ila kwasasa fanya hivyo, usitake vocha ya elfu hamsini tu ikuponze”
Erica alimuitikia kwani hata yeye alipatwa na uoga kiasi falani.
Wakati wa kulala alipokea simu ya Erick, na kusalimiana nae kisha kuongea nae,
“Unajua Erica, kuna mambo yanatendeka sijui sababu niko mbali ila ningekuwa karibu nina hakika ysingetokea. Wiki ijayo nakuja”
“Erick kweli?”
“Ndio ni kweli, wiki ijayo nakuja”
“Wow, nimefurahi sana basi utaniambia ni lini ili nije kukupokea”
“Sawa na mimi nitafurahi sana kupokelewa na wewe maana nimekukumbuka sana”
“Sawa Erick, tuko pamoja”
Erica alionekana kufurahi sana kwani alikuwa akitamani kila siku Erick arudi, kisha akaagana nae na kulala, ila kabla hajalala alipigiwa simu na namba ngeni, hakutaka kupokea ila alipokea akihofia labda kuna maelekezo ya ile vocha aliyoituma kwa mzee Jimmy, na kweli alikuwa ni mzee Jimmy,
“Mbona umenirudishia ile vocha?”
“Ulinitumia nyingi sana”
“Ndio kuamua kuirudisha yote kweli?”
“Ndio maana mpenzi wangu aliiona na kuuliza vocha nimetumiwa na nani? Akaniamuru niirudishe”
Yule mzee akakata simu na Erica alilizika tu maana alikata simu kwa matakwa yake, alishukuru kwa Dora kumpa yale maelekezo,
“Dora ni mbaya ila mara nyingine ni mtu maana angeniacha niangamie, ninayosababu ya kumshukuru kwakweli”
Aliwaza hilo na kulala.
Kulipokucha alikuta kuna ujumbe kwenye simu yake ukitoka kwa Rahim,
“Erica, ingia kwenye mtandao, kuna jambo la muhimu sana nataka kukwambia”
Kiukweli Erica hakuwa na hamu kabisa ya kuwasiliana na Rahim kwahiyo hakuingia kwnye mtandao wala nini.

Siku hiyo ilikuwa ya kurudi Erick kwahiyo alijiandaa kwenda kumpokea, alijiandaa vizuri sana na kumuaga mama yake kisha akaenda uwanja wa ndege kumpokea Erick, alifika na kukaa mahali ili amsubirie, alivyoona karibia muda unafika alienda kusimama karibu karibu ili amsubirie Erick, na kweli alipoangalia mbele alimuona Erick ila alikuwa ameongozana na kijana mmoja na waliongea kama wanafahamiana vile, alipomuangalia vizuri Yule kijana alishtuka sana kwani alikuwa ni Rahim, hofu ilimjia kuona Erick na Rahim wanafahamiana.
 
SEHEMU YA 345


Siku hiyo ilikuwa ya kurudi Erick kwahiyo alijiandaa kwenda kumpokea, alijiandaa vizuri sana na kumuaga mama yake kisha akaenda uwanja wa ndege kumpokea Erick, alifika na kukaa mahali ili amsubirie, alivyoona karibia muda unafika alienda kusimama karibu karibu ili amsubirie Erick, na kweli alipoangalia mbele alimuona Erick ila alikuwa ameongozana na kijana mmoja na waliongea kama wanafahamiana vile, alipomuangalia vizuri Yule kijana alishtuka sana kwani alikuwa ni Rahim, hofu ilimjia kuona Erick na Rahim wanafahamiana.
Akaamua arudi nyuma na kujificha kwani alihisi angejitokeza basi habari ingekuwa nyingine, alikuwa akiwaangalia tu na walionekana wakiongea mambo mbalimbali, kisha akamuona Erick kachukua simu akimpigia, akaangalia mkononi akaona namba ya Erick ya nchini, akaacha tu iite maana haikuita kwa sauti, aliona akipokea anaweza kuzua mengine, yani alikuwa akiwaangalia tu Rahim na Erick, mara akatokea binti mwenye asili ya kishombeshombe pia, alimkumbatia Rahim na kusalimiana na Erick, yani muda wote huo Erica alijibanza tu akiwaangalia, kisha akaona Erick akimpigia tena simu ila hakupokea na badae akaona Rahim na Yule binti wakikodi gari na kuondoka, wakati huo Erick nae alionekana kukodi gari kwani alitaka kuondoka tu baada ya kuona Erica hapokei simu ile gari alilopanda Erick lilivyoanza kwenda tu akampigia simu Erick,
“Erick, nimefika uwanja wa ndege huku uko wapi?”
“Mbona nimekupigia sana simu Erica?”
“Nisamehe kulikuwa na foleni, halafu simu ilikuwa kwenye mkoba na gari nililopanda lilijaa sana kwahiyo sikuweza kupokea”
Erick alisikika akimsimamisha Yule dereva huku akimuuliza Erica alipo ili wamfate, ila Erica aliwafata yeye kwani ni muda tu alikuwa akiwaona, alivyofika pale Erick alishuka kwenye gari na kumkumbatia sana Erica maana alimmiss sana, kumbe kuna mtu alikuwa akiwaangalia vile wanavyokumbatiana, alikuwa ni George na alitumwa na mama yake Erick ili akampokee Erick, aliamua kuwafata, na kuwasalimia ila alikuwa na kitu moyoni mwake, kisha akamwambia Erick,
“Nimetumwa na mama yako nije kukupokea”
“Mama nae, mimi ni mkubwa sana kwasasa, nimepokelewa na mpenzi wangu kwahiyo wewe rudi tu. Hata hivyo nimeshakodi gari”
Kisha George akamuuliza Erick,
“Kwani una undugu wowote na huyu binti? Labda huko kwa baba yako?”
“Huyu ni mpenzi wangu sio ndugu yangu”
Kisha George akamuangalia Erica na kusema,
“Erica kumbe hunitaki tena sababu ya Erick? Unajua mimi na Erick tukoje?”
Erica alikaa kimya kwanza alikuwa akiwaza mambo mengi tu kuwa kakimbia moja halafu la pili limemjia kwa namna mbaya sana, Erick alimuangalia Erica na kumuuliza,
“Unamfahamu huyu?”
Erica leo hakutaka kabisa maswahibu ya George yamuharibie siku, alijibu kwa uso mkavu kabisa,
“Simfahamu”
Kisha Erick akamwambia George,
“Bhana George tusiharibiane siku, mwenyewe kasema hakufahamu, kama umemfananisha shauri yako. Erica twende”
Akamfungulia mlango wa lile gari Erica akapanda kisha nay eye kupanda na kuondoka.
 
Back
Top Bottom