Simulizi: Nini maana ya mapenzi

Simulizi: Nini maana ya mapenzi

SEHEMU YA 346

Wakiwa njiani, Erica alimuuliza Erick kuwa wanaenda wapi kwanza,
“Tunaenda hotelini Erica kwani ulifikiri tutaenda wapi?”
Ni kweli Erica alikuwa amemmiss sana Erick lakini akaona asipokuwa makini basi yatamtokea mambo kama yaliyomtokea kwa Rahim, kupata mimba juu na kutukanwa malaya, kwahiyo akatafuta njia ya kumdanganya Erick ili asilale nae kwa siku hiyo,
“Ooooh Erick jamani, ungeniambia mapema ili nikupe mlolongo wa siku zangu, yani hapa nilipo nimeingia kwenye siku zangu”
“Mmmh Erica jamani, unataka kuninyina kweli?”
“Jamani eick hivi mimi naanzaje kukunyima wewe jamani! Hivi kwa jinsi ninavyokupenda hivi hadi mtoto nimemuandika kwa jina lako nikunyime kweli? Huniamini au?”
“Hapana nakuamini Erica”
Erica alifurahi sana kuaminiwa na Erick, aliamua kumshauri tu mule kwenye gari kuwa aende nyumbani kwao ili asikae kwenye mazingira ya vishawishi, basi Erick akamwambia,
“Hakuna shida, basi kwa muda huu tutafute mahali tukae, tule, tuongee halafu nitaenda nyumbani”
Basi wakatafuta mahali ambapo palikuwa na mandhari nzuri sana ya kwenda kukaa hapo ili kuongea kidogo, na kujikuta wakijadiliana mambo mbalimbali,
“Erica usijali kuhusu mimi lazima nitakuoa yani lazima nitakuoa tu, haijalishi nini kipo mbele yetu ila lazima nikuoe”
“Nitafurahi sana Erick, yani siku mimi nikiwa kwenye shela na wewe kwenye suti uwiiii sitaisahau hiyo siku katika maisha yangu”
“Usijali Erica, yani usijali kuhusu ndugu zangu wala mtu gani?”
“Ila kuna swali nataka nikuulize?”
“Niulize tu”
“Unajua wakati nimefika pale uwanja wa ndege nimekuona na mkaka mmoja na mdada ndio wanaondoka, ndugu zako wale?”
“Hapana, wale si ndugu zangu ila Yule kaka anaitwa Rahim, ni rafiki yangu kuna kipindi nilikuwa marekani nilikuwa nae, kipindi hiko nilikuwa nakunywa sana kwahiyo tulikuwa tunakunywa nae na yeye ndio alikuwa akiniunganisha kwa wanawake”
“Mmmh kumbe ni mlevi pia? Ila Erick ulikuwa balaa nadhani ushatembea na wanawake wakila rangi!”
“Yamepita hayo Erica usiyakumbushie, yani kama vile walokole wanavyosemaga yakale yamepita nimekuwa mtu mpya, mimi saivi ndio Yule Erick uliyemuhitaji maishani, Erica wewe ndio ulikuwa sababu ya yote haya, ila sio kwamba hao wanawake wote nilikuwa nalala nao hapana, wengine ni wa kwake huyo jamaa”
“Kwahiyo nae mlevi?”
“Tena bora ya mimi, yeye ndio mlevi balaa. Nimekutana nae leo tukajikuta tunakumbushiana mambo yaliyopita, nikamwambia mwenzie nimebadilika, ila yeye sasa hajabadilika wala nini maana Yule dada uliyetuona nae ni mwanamke wake”
“Kheee ana wanawake wengi sana eeeh!”
Erica alijikuta akiulizia sana habari za Rahim hadi Erick alimuuliza,
“Mbona unaniuliza sana habari za Yule mkaka, unamjua?”
“Mmmh hapana, na Yule aliyekuja kukupokea je una undugu nae upi?”
“Yule ana undugu na mama yangu huko kwenye ukoo wao, mie sina ukaribu nae sana wala nini”
“Tumaini anamfahamu?”
“Kumbuka Tumaini ni ndugu yangu mimi, halafu Yule na Tumaini ni watofauti maana Yule ni ndugu wa mama yangu, labda wafahamiane siku hizi. Halafu natamani kumuona Angel, sijui nije lini?”
“Wewe tu na muda wako unakaribishwa kuja kumuona”
“Ila Erica tuache masikhara, tunazungumza mengi sana ila mwenzio nina hamu tena sana”
“Erick, nivumilie tu siku zangu zipite na tutakuwa pamoja, mbona hakuna tatizo. Si ulikuwa unavumilia South sembuse usharudi jamani! Nivumilie Erick”
“Sawa nimekuelewa ila kaa ukijua nina hamu sana”
Erica aliamua kubadilisha mada kwani aliona ile mada ikiendelea basi anaweza kujikuta akiangukia kwenye uzinzi ambao hakuutaka kwa kipindi hiko.
Wakaongea ongea na muda ulipoenda ilibidi Erick arudi kwao akapumzike na alimkodia gari pia Erica na kumkodia gari arudi kwao.

Erica alimkuta mama yake nyumbani amefura hasira, akamsalimia ila mama yake hakumjibu na kuanza kumsema tu,
“Wewe mwanangu ndio huna akili yani huna akili huna akili kabisa, sijui niseme vipi ndio unielewe jamani. Haya umeenda kumpokea huyo Erick wako, umeshindwa kucharanga miguu kurudi nyumbani mpaka uende kulala nae? Yani kwa stahili tiyo utakuwa unadhalilika kila siku na kutukanwa na wanaume, hakuna jema kwenye macho ya mwanaume, utajitoa na kuona nimejitoa kwa mpenzi wangu ila bado atakuona malaya.”
“Ila mama umenifikiria vibaya tu, sijaenda kulala na Erick, nimeongea nae tu”
“Labda mdanganye Angel hayo maneno yako, mpaka muda huu ni maongezi tu hayo?”
Erica aliamua kumueleza mama yake vile alivyomdanganya Erick ili asilale nae, mama yake alimsikia na kumwambia,
“Siku nyingine hata usihangaike kumdanganya mwanaume, kuwa muwazi, sitaki sipo tayari. Kama kukuacha na akuache sio kutaka kukuharibia maisha, yeye katoka nje huko hata kusema mpenzi wangu tukapime hakuna, moja kwa moja twende tukalale, akikupa maradhi je! Ila napo umetumia akili kumwambia hivyo ingawa kuna wanaume wengine mathomaso atataka mpaka aone damu, yani mapenzi mwanangu ni kizunguzungu ila kama hujakubali namshukuru Mungu, najua ulikosea mwanangu ila ni muda wa kujitunza huu, acha yote jitunze”
“Sawa mama nimekuelewa”
“Kuzaa sio kugawa gawa kwa kila anayetaka, sio pipi ya kusema kila mtoto anyonye, tunza ujana wako, umezaa nje ya ndoa lakini ukijiheshimu utaheshimika na sifa mbaya juu yako zitapotea mwanangu”
“Asante mama”
Erica alienda kuoga na kwenda chumbani kwake huku akitafakari baadhi ya maneno ya mama yake, kuwa wanaume hawana shukrani hata umpe nini, ila akamkumbuka Bahati, huyu alikuwa ni mwanaume wa ajabu saba kwake maana anakumbuka siku ya kwanza kukutana na Bahati kimwili alionekana bikra mbele ya macho ya Bahati, na alipewa shukrani ambazo hata Babuu aliyemtoa bikra kweli hakuwahi kumpatia, kwahiyo aliona Bahati ni mwanaume wa ajabu sana kwake.
“Kwa mambo ya wanaume walivyo, ningekuwa na tuzo basi ningemzawadia Bahati maana ndio mtu pekee aliyeonekana kujali na kuthamini ulivyo. Ila sio wangu tena, ni wa mwingine mie wangu ni Erick, nampenda sana”
Basi alipotaka kulala aliwasiliana kidogo na Erick kisha akalala sasa.

Kulivyokucha tu, asubuhi na mapema Erica akapigiwa simu na Dora, kiukweli alikuwa akishangaa sana Dora alivyokuwa akishughulika nae,
“Erica unajua kilichopo kwako?”
“Kwangu kipo kipi?”
“Nasikia mzee Jimmy, kaweka shilingi milioni kumi kwenye akaunti ya mtoto wako”
“Kheee huyu mzee ana wazimu jamani, ana nitakia nini mimi?”
“Sijui ila ndio hivyo”
“Itabidi nikaangalie, sasa nifanyeje?”
“Mrudishie maana Yule mzee mmmh!”
“Nashukuru Dora, au unaonaje nikutumie wewe”
“Tena hapo utakuwa umefanya jambo la maana ili nitayarishe hela za kununulia sanda na jeneza langu”
“Yani Dora, unaongea kama ugonjwa wa kawaida huo!”
“Sasa nifanyeje wakati ninao tayari”
“Ngoja niende benki nikaangalie”
Erica alijiandaa kisha akamuaga mama yake na kutoka kwenda benki, alipofika benti alienda moja kwa moja huduma kwa wateja na kuulizia salio na kuona kweli kuna milioni kumi imeongezwa kwenye ile akaunti, akaomba apewe taarifa fupi ya akaunti ya mwanae, wakampa na akaiangalia vizuri sana na akaona kuwa kawekewa hiyo hela, akawaza kuwa hata kuirudisha atairudisha vipi ikiwa akaunti namba ya Yule mzee haijui halafu hawezi kutoa pesa zote hizo na kutembea nazo ili azirudishe ni hatari kubwa sana kwake, na pia hakuweza kuulizia akaunti ya Yule mzee pale huduma kwa wateja kwani alihisi ni kumchafulia sifa Yule mzee, kwahiyo aliamua kwenda kwa meneja wa ile benki.
Alimkuta na kuamua kuongea nae kirafiki tu, kwanza Yule meneja alimuomba msamaha sana kwa kutofanikisha swala la mwanae kuwa balozi,
“Nisamehe bure Erica, nilitamani sana Angel awe balozi wetu maana sifa zote anazo ila mamlaka ipo kwa mkurugenzi mkuu”
“Hamna usijali, naelewa ila kuna jambo nataka tuongee, kama ndugu yangu unipe ushauri”
“Sawa hakuna tatizo, ongea tu”
“Sikia nikwambie, huyu mkurugenzi mkuu nilikuwa namfahamu kabla ya kuonana nae hapa benki na alikuwa akinitaka kimapenzi ila nilimkataa, ndiomana swala la mwanangu kuwa balozi alivyoniona alinizungusha sana, sasa jambo lililonileta mpaka kuja kuomba ushauri ni kuwa nasikia amemuwekea mwanangu milioni kuzi, nimekuja kuhakikisha ni kweli na taarifa fupi ya akaunti ya mwanangu ni hii (Akamkabidhi lile karatasi lenye taarifa fupi) wazo lililonijia ni kumrudishia, sasa sijui akaunti namba yake, nimeona kuuliza pale mapokezi sio sifa njema ndiomana nimekuja kwako meneja ili nikuulize na unishauri”
“Kwanza kabisa nakupa hongera sana yani hongera mno, hakuna binti anayeweza kuchomoka akitongozwa na mzee Jimmy maana ana hela, ila wewe umechomoka hongera sana, halafu hakuna binti ambaye amewahi kuongwa hela nyingi hivi na mzee Jimmy, kwakweli wewe ndio wa kwanza, hongera sana. Jambo la kukushauri ni hili, hii hela hujamuomba sehemu yoyote, na ametuma kwenye akaunti ya mwanao, kwanini ujisumbue kumrudishia? Kwani hutaki mwanao ale vizuri, aishi vizuri afurahi? Hebu tumia hela hiyo kwa mahitaji ya mwanao, najua mwanao atakuwa na mahitaji mengi kama watoto wengine, tumia hela, karibia atakuwa Yule na ataenda shule, tunza hela hii imsomeshe badae, yani hata usihangaike kuirudisha tena jifanye hukujua kama amekutumia wala nini”
“Nisimrudishie eeh!”
“Usimrudishie ndio, na anayekushauri umrudishie anataka ufe masikini, hivi kwa usawa huu kweli mtu anakupa hela bila kuomba umrudishie? Weee hakuna kurudisha hiyo.”
“Kheee umenifungua macho sana, bora nimekuja kwako”
“Yani usiirudishe”
“Basi nikupe na wewe hela ya soda, nikupe ngapi?”
“Mwenzangu ile ni nguvu yako ya kupush mtoto leba, ila sababu umeamua kunipa hakuna shida. Nipe laki tu”
Basi Erica alitoka mule ofisini na kwenda kutoa hela kisha alimpa laki moja yule meneja na kuagana nae.
 
SEHEMU YA 347

Akiwa njiani alifikiria sana kuhusu ile hela, atafanyia nini milioni kumi ikiwa hata wazo la biashara hana ila aliona aitumie kidogo kidogo tu ili mwenye nayo akitaka amrudishie, sasa pale kwenye siti aliyokaa alisikia wamama wakiongea,
“Unajua hatuendelei kwasababu moja, unaiacha hela ikae tu badala ujishughulishe upate faida ya ile hela unaacha tu mwisho wa siku tunalalamika umasikini umasikini kumbe ni matatizo yetu”
“Umeongea vyema, nakumbuka mimi nilianza kukopesha vitenge na mtaji wa laki moja tu ila saivi mtaji wangu unagoja milioni mbili sababu sikukata tamaa”
“Haya sasa, ungeiacha hiyo laki ikae tu ungepata hizo milioni mbili?”
“Nadhani wengi tatizo linakuwa moja, mtu anakuwa na wazo la biashara na anahitaji sana kuifanya ila hajui namna ya kuanza biashara”
“Mimi mwenyewe nilikuwa hivyo hivyo ila nilisikia kuna semina ya wanawake wajasiliamali, sikuwa na biashara ila nilienda, jamani nilipata muhamko wa hali ya juu, kuna mambo yanafungua jaman I, yani ujinga tupa kule, nilifunguliwa haswaa kwenye ile semina, maana unasikia mwingine nilianza na mtaji wa elfu kumi niko mbali sasa? Nikajiuliza amewezaje? Ila mwingine akasema usiseme amewezaje ila sema kama Yule anaweza basi na mimi naweza, toka hapo nikafata tu mlolongo wa ile semina na ilipoisha nilianza kufanyia kazi kile nilichofundishwa basi nimekuwa mbali”
“Wengine unajua wanakosea nini, anaweza akahudhuria kama hivyo semina, anachanganyikiwa na kila ushuhuda wa mtu, anasikia natengeneza sabuni niko mbali, natengeneza batiki, napika tambi, nauza vikoi, sasa yeye sababu ndio anaanza anatakiwa aanze na kimoja kwanza basi utamkuta mara atengeneze batiki aache, atengeneze sabuni, humo humo vikoi anashangaa mtaji unakata anaanza kusema biashara haina faida”
Kwakweli Erica alijikuta akivutiwa sana na maongezi ya wale wakina mama, alitamani kuendelea kuwasikiliza ila ndio walikuwa wanashuka, basi aliendelea na safari ila maneno ya wale wamama yalikaa kwenye mawazo yake muda wote na kujikyta tu akitamani kuanza biashara ili afike mbali maana hata yeye alichoka kutegemea hela ya kuomba omba tu na kutegemea hela anayoingiziwa mwanae kama balozi, kwahiyo alikuwa anawaza vitu vingi sana. Alifika kwao na kushuka, kisha kuelekea nyumbani kwao.
Njiani alikutana tena na Johari na mume wake wanaondoka, Johari na Juma wakamsalimia Erick, muda huu Juma alitangulia mbele kidogo maana alienda dukani kununua vocha, kwahiyo Erica alibaki na Johari, akamuuliza,
“Inaonyesha mnapendana na mumeo eeeh!”
“Kwakweli tunapendana sana ten asana, namshukuru Mungu kwa kunipa mume mwenye hofu ya Mungu, usimuone hivyo mume wangu, si mlevi, havuti sigara na anafanya ibada vizuri sana”
“Wewe je unafanya ibada?”
“Nimebadilika Erica, Johari huyu si Johari Yule, hakika Juma kanibadilisha yani maisha yangu yamebadilika haswaaa, mwenzio siku hizi hadi Ramadhani nafunga”
“Kheeee kweli umebadilika Johari”
“Huyu mwanaume kanibadilisha, yupo vizuri sana. Hapa tunawahi kwenda nyumbani ila muda wa swala usimkutie kwenye daladala”
“Hongera sana Johari kwa kupata mume mwema”
“Asante, nawe Erica utapata mume mwema ila namkumbuka Erick, natamani siku moja mkutane na muoane”
Erica alicheka tu kwani ukwlei ni kuwa anawasiliana sana na Erick, Basi mume wa Johari alimaliza kununua vocha na kuweka kwahiyo Johari alimuaga Erica na kuondoka, Erica aliwaangalia hadi walipokuwa wanaishia stendi kisha yeye kwenda nyumbani kwao.

Njiani alijiuliza sana, kuwa Yule Juma hanywi pombe, havuti sigara na anapenda ibada mbona ni rafiki wa James sasa? Alijiuliza sana maana hakuona uwezekana wa James kuwa na rafiki kama Juma ikiwa Juma ni mume mwema tofauti na James.
Alifika nyumbani kwao na kushangaa sana kumuona Babuu kwenye geti lao, alifika na kumsalimia kisha akamuuliza,
“Umefata nini tena kwetu?”
“Erica jamani kwani haturuhusiwi kuja hapa?”
“Hapana, nimekuuliza tu”
“Nilikuja kukuona wewe Erica, nimekaa nyumbani nimeboreka ndio nikaamua kuja kukuona”
“Aaah karibu, nilimuona kwa mbali jana Rahim, vipi kasharudi nyumbani?”
“Erica, umeanza tena na Rahim? Yule sio mwanaume atakupoteza Yule”
“Hapana, sijaanza nae tena nimesemea tu”
“Kwanza hajafika nyumbani nahisi atakuwa na mwanamke tu na nyumbani atarudi hadi wiki iishe”
“Mmmh!”
“Mbona unaguna?”
“Naguna sababu nilikosea sana kuwa na Rahim kwakweli yani sijui hata nilianzaje jamani”
“Usijali ni mapito tu hayo”
“Haya, karibu ndani”
“Wapi? Mamako kanitimua kama mwizi, hata sitaki nishakuona kwaheri”
Basi Babuu akaondoka zake ila Erica hakuelewa ni kwanini Babuu atimuliwe na mama yake, kwahiyo aliingia ndani kwanza ili amuulize mama yake chanzo nini, alimkuta mama yake anacheza cheza na Angel, Erica alimsalimia mama yake na kumuuliza,
“Mama mbona umemtimua Yule kijana?”
“Ujinga ujinga kwenye nyumba yangu sitaki, anakuja kujitambulisha hapa oooh mimi ndio nilikuwa mwanaume wa kwanza kwa Erica, sasa ujinga huo unanihusu nini? Kuna mzazi anayefurahia kumuona aliyemuharibu mwanae? Hakuna mzazi anayekubali ujinga ujinga wa namna hiyo, ndiomana nimemtimulia mbali”
“Ila mama Johari nae ulimfukuza?”
“Ndio nilimfukuza, Yule rafiki yako alianza tabia za ajabu sana na ashukuru Mungu kapata huyo mwanaume wa kusitiri tabia zake, Johari alikuwa akitembea na kila mwanaume hapa mtaani yani hakutamanika Johari ndiomana nikamtimua pia”
Erica hakutaka kuendelea kumuhoji mama yake kwani anajua ambacho kingetokea baada ya kuendelea kumuhoji.
 
SEHEMU YA 348

Erica alikuwa amechoka kutokana na mizunguko ya siku hiyo sababu aliondoka kwao tangia asubuhi, kwahiyo alienda kujilaza tu, wakati kajilaza alipokea ujumbe toka kwa Erick, akafungua na kusoma,
“Erica nina hamu mwenzio hadi sina raha, nina hamu sana”
Ule ujumbe ulifanya asisimke mwili ila bado alishikilia msimamo wake kuwa asitembee na Erick kwanza kwa kipindi hiko, kwahiyo alimtumia ujumbe kuwa avumilie tu,
“Nivumilie hadi lini Erica?”
“Nivumilie jamani eeh! Nakupenda sana, nivumilie”
Erica alijaribu kumpa mpa maneno matamu pale na kulala, alilala usingizi mzito sana hadi akaanza kuota ndoto za ajabu ajabu tu, kuja kushtuka ni jioni kabisa na aliposhika simu yake alikutana na jumbe kadhaa za kutoka kwa Erick na kugundua alipolala, bado Erick alimtumia ujumbe ambao hakuujibu, jumbe za Erick zilionyesha ana hamu ya tendo la ngono tu, akaona hata akimpigia tena simu muda huo bado atamwambia jambo lile lile.
Basi akajiweka sawa na kwenda kufanya shughuli zake za jioni ile na alipomaliza walikuwa na kujiandaa kulala, mama yake akamwambia,
“hivi siku hizi unasikiliza mahubiri kweli?”
“Mmmh mama na wewe, nasikiliza”
“Usikilizage ni mazuri”
Basi alipoenda kulala, alifungua redio ila kuna stesheni ilikuwa na miziki mizuri sana akaamua aisikilize hata aache kufungua ile ya mahubiri maana aliona ile miziki ingempita, basi ile miziki ilivyoisha kulikuwa na kipindi cha wanawake, yani kuna mwanamke anaelimisha wanawake wengine waliokuwa katika ndoa, akaanza kusikiliza,
“Mwanamke unakuwa nyumbani, mumeo anarudi wala hujishughulishi kumpokea yani ndugu yangu huyo mume atakukimbia, ataenda kwa wenzako wanaomnyenyekea, mumeo akitaka mpe, yani ukimnyima ndio utamfanya aende kwa wengine, sio unajifanya umechoka, mpe mumeo haki yake, shauri yako utashangaa tu sio wako tena”
Erica akazima redio, maana akikumbua jumbe za mchana za Erick alipatwa mashaka, akaamua kumpigia Erick simu ila simu yake haikupatikana, akaamua kuchukua simu na kuingia kwenye mtandao wa kijamii, ile ameingia tu akaona ametumiwa ombi la urafiki na Sia, akashangaa sana ila akakubali lile ombi, mara ujumbe ukaingia,
“Erica, wewe umempokea ila sisi ndio tunafaidi”
Muda kidogo akaona picha zimetumwa na Sia, kuangalia zile picha akaona Sia yuko pembeni na Erick amelala inaonyesha amelala kwa uchovu wa mambo aliyokuwa akifanya na Sia.


Akaamua kuchukua simu na kuingia kwenye mtandao wa kijamii, ile ameingia tu akaona ametumiwa ombi la urafiki na Sia, akashangaa sana ila akakubali lile ombi, mara ujumbe ukaingia,
“Erica, wewe umempokea ila sisi ndio tunafaidi”
Muda kidogo akaona picha zimetumwa na Sia, kuangalia zile picha akaona Sia yuko pembeni na Erick amelala inaonyesha amelala kwa uchovu wa mambo aliyokuwa akifanya na Sia.
Kwakweli Erica alihisi kama kurukwa na akili hivi, yani hakujielewa kabisa, hakujua kama alie au afanye nini akajikuta akijisemea,
“Ndiomana mama anasemaga wanaume ni mbwa, loh kunifanyia hivi Erick jamani! Kumpenda kote huku!”
Hakujielewa na kahuweza kulala tena, alitamani awe anapajua kwakina Erick aende hata usiku huo huo, labda akapigane na Sia, ila muda mwingine akaona ujinga kugombea mapenzi, akawaza mtoto wake aliyembadilisha jina maana Erick kawa sio mtu sahihi tena kwenye macho yake, akajikuta akianza kulia, alilia sana, alinyamaza aliposikia mlio wa simu yake, akaichukua na kuangalia akaona namba mpya, ila alihisi pengine ni Erick anataka kunuomba msamaha, akapokea ili amsikilize, hakuwa Erick bali alikuwa ni Rahim, hata alimshangaa usiku huo kampigia simu ili iweje,
“Erica nimerudi mpenzi wako hata kunitafuta?”
Erica akatamani hata kumpa tusi sema hakuzoea kutukana kwahiyo alikaa kimya tu, Rahim akaendelea kuongea
“Mbona unanyamaza mpenzi wangu, nimekumiss sana. Kesho nitakutafuta tutoke na mtoto wetu tukatembee”
Aliamua kumjibu,
“Rahim, mimi sio mpenzi wako unikome”
“Mbona umekuwa mkali hivyo Erica? Mtoto anahitaji malezi ya baba na mama, na mimi ndio baba na wewe mama, tusimnyime haki mtoto wetu, au kama vipi njoo ili sisi wazazi tuyajenge”
“Rahim, nikome uyajenge na nani? Sio mimi, umeshindwa hata kufika kwa wazazi wangu halafu unaniita kuyajenga? Sitaki Rahim na siji”
“Erica usiwe mkali hivyo, kumbuka sisi ni wazazi, unanijua vizuri, nakujua vizuri, nimemiss vile unavyoliaga kitandani?”
Erica akachukia na kukata simu, alikuwa na hasira sana na ile simu akaizima kabisa, alikaa na kuendelea kulia huku akisema hamtafuti tena Erick, na hataki kuwa karibu na rahim bora awe mwenyewe tu, kwani hakuwa na raha tena hadi panakucha.
 
SEHEMU YA 349

Mama yake ndiye aliyemuita baada ya kuona muda mrefu umepita na mwanae hajatoka ndani, Erica alitoka na kumsalimia mama yake, mama yake alimuangalia na kumuuliza,
“Vipi mbona macho yamekuvimba hivyo?”
Erica hakuweza kujizuia kwa mama yake, alijikuta akimfata na kumkumbatia huku akianza tena kulia, mama yake akamwambia,
“Wewe vipi tena, kama babako kafa mara ya pili jamani? Kilio hiko vipi mwanangu eeeh!”
“Mama, leo nimeamini maneno yako kuwa mwanaume sio wa kumuamini”
“Eeeeh vipi tena? Ila kila siku nakuambia, mwanaume sio ndugu yako mwanangu”
“Kwakweli mama Erick kanifanyia kitu ambacho sielewi mpaka muda huu”
“Niambie mamako usinifiche, nilishakwambia mimi ni rafiki yako kwahiyo kuwa huru kusema chochote”
Erica alianza kumuelezea mama yake yaliyotokea kwa Erick na jinsi Sia alivyomtumia picha Erica,
“Ooooh katoto kangu jamani, kwanza tulia, tuliza akili zako, usipaniki, hayo mambo ni ya kawaida tu na huwatokea wengi sana. Tuliza akili, hakuna sehemu imeandikwa kuwa Erick ni mwanaume peke yake kwahiyo hakuna wengine, hapana wapo. Na sio kwamba nilivyosema wanaume hawajatulia basin i wote, hapana waliotulia wapo sema tu ni ngumu kuwatambua sababu tumezoea msemo kuwa samaki mmoja akioza basi wote wameoza”
“Lakini mama kwanini anifanyie hivi? Kwanini lakini? Kwanini nina mkosi hivi juu ya mapenzi? Sina raha mama, kwanini mimi?”
“Hapana, usijiumize kichwa sana. Ngoja nikuulize, hizo picha Erick alipigwa akiwa anachekelea kabisa kuwa na Sia au?”
“Hapana alikuwa amelala”
“Basi huna sababu ya kupata presha mwanangu, ingawa wanaume ni waongo ila bado anayetakiwa kukupa majibu ni Erick. Ndoa ni uvumilivu mwanangu, na uvumilivu unaanzia kwenye mahusiano. Sikia nikwambie, usipaniki wala nini, muulize Erick kwa upendo tu na atakwambia ukweli”
“Nitawezaje kumuuliza kwa upendo mama ikiwa nimeumia hivi?”
“Ndiomana nakwambia shusha presha, shusha hasira, ukiona upo sawa ndio umuulize. Kumbuka Sia ni rafiki mkubwa wa Tumaini, kwahiyo kuna uwezekano mkubwa hata Erick hajui kama alipigwa picha, kwahiyo wewe tulia na umuulize”
“Ikiwa kama ni kweli mama?”
“Ikiwa kweli maamuzi ni yako kusuka au kunyoa ila uvumilivu unaanzia kwenye mahusiano”
“Uvumilivu wa kumvumilia mwanaume muhuni mama?”
“Sasa kuna asiyekuwa muhuni?”
“Bahati mama ni mpole, hana hayo mambo”
“Kwahiyo unataka Bahati amuache mkewe na akuoe wewe, au unataka kuwa mke wa pili? Hebu nitolee ujinga mie, wewe mwenyewe ulikuwa unaimba wimbo hapa nampenda Erick, nampenda Erick, mvumilie ndio maradhi yako hayo”
Erica alizidi kunyong’onyea ila mamake alivyoona vile aliamua kumbembeleza, sasa maana alimuona kakosa raha kabisa,
“Aaah mwanangu jamani usijali, Erick ataongea nawe vizuri tu. Halafu mwanangu acha kupenda sana utaumia, nipende mimi mama yako niliyekubeba tumboni miezi tisa sio Erick aliyekufahamu ukubwani, usiwe kama Sia, kifo cha mama yake hajajaribu kujiua ila kuachwa na mwanaume amejaribu kujiua, na tena hata ajisikiliziii vizuri, kashapona na kwenda kwa mwanaume, Yule hana akili mwanangu, usiwe vile, sawa mama”
“Sawa mama, nimeelewa”
Basi mamake alimtaka Erica aoge na avae vizuri na awe na amani tu.

Mchana wa siku hiyo, Erica akiwa chumbani alisikia mama yake akimtimua mtu akataka kujua kuwa anayetimuliwa ni nani, akatoka na kushangaa ni Derick alifika na mama yake, alimsikia mama ake akisema,
“Wewe mama sina shida na wewe ila huyu mwanao simtaki kabisa hapa kwangu, mtoto mchawi huyu”
“Lakini kaja kuomba msamaha”
“Msamaha kitu gani wa kichawi, mtoto hafai huyo alitaka kumbaka mwanangu”
Inaonekana hata mama Derick hakulijua hilo kwani alishtuka sana kusikia mwanae alitaka kumbaka Erica, ilibidi amtulize kwanza mama Erica ili wakae wakizungumza, mwishowe mama Erica alikubali kuwakaribisha ila kiukweli hakupenda kabisa uwepo Derick mahali pale.
Erica alipowaona ni wao, alirudi zake chumbani kwake tu kwani hata yeye hakutaka uwepo wa Derrick ukizingatia kamuaibisha sana.
Basi akawasha tena simu yake, na muda huo huo Rahim akampigia simu tena, kiukweli hakujisikia kuipokea kwahiyo aliiacha iite hadi ikatike.
Kisha akajaribu tena kuipiga namba ya Erick napo haikupatikana na kuzidi kumtia simanzi, akachukia sana, huku asitamani hata kuongea na mtu mwingine kwa wakati huo, ila mama yake alimuita maana Derick alienda kuomba msamaha, kwahiyo muda huu Erica alienda kuwasikiliza sera zao, akawasalimia pale na kukaa, mama yake akaongea,
“Haya, wewe Derick, omba msamaha kwa Erica kwa hayo madudu uliyomfanyia”
“Erica, naomba unisamehe sana, nimefanya kitu ambacho hakitakiwi kabisa, sisi ni ndugu Erica na tuishi kindugu, sisi ni dada na kaka kwahiyo tupendane na tuishi vizuri”
Sababu erica hakutaka kuweka maongezi marefu akaamua kumsamehe tu, muda huo mtoto wa Erica aliyekuwa amelala aliamka na kulia kiasi na kuanza kwenda sebleni, kwahiyo Erica alimchukua mwanae na kumpakata, ila mama Derick akasema,
“Jamani huyu mtoto sikumuona alivyokua, daha kafanana na mtoto mtoto wa ndugu yangu anaitwa Rahim”
Derick akadakia,
“Ndio baba yake huyo, kumbe mama hujui?’
“Babake!”
“Ndio mama”
Mama Derick alimuangalia Erica na kumwambia,
“Kheee pole Erica, ulianzaje kuzaa na Yule? Yani matendo yake Yule si mazuri hata kidogo ila mamake huwa haamini kama mwanae mchafu hata umwambie vipi, sina cha kuficha wala cha kukupa moyo, kwakweli Rahim hakufai”
Erica akasema kwa aibu maana hakutaka mama Derick ajue ila mambo yote yako wazi,
“Ila nilishaachana nae huyo Rahim”
“Kwakweli pole yani pole sana, Yule ndugu yangu mtoto amepata ni John tu, ni mpole na anapenda kweli ila sio Rahim, hata mke wa kuoa hakujua amuoe nani, ikabidi babake amuolee tu mke, yani Rahim sijui labda akikuua ataacha ila pole sana”
Mamake Erica nae hakutaka hayo mambo ya kujadiliana kuhusu Rahim ilihali ni Rahim aliyeharibu maisha ya mwanae kwahiyo aliikatisha ile mada,
“Jamani sitaki kusikia habari za huyo mtu, huyu ni mjukuu wangu na atabaki kwenye himaya yangu, badilisheni mada kama zimeesha ondokeni”
Mamake Erica alionekana kuwa na kirirani tu kila muda. Basi waliongee ongea na kuaga ambapo walishikana mikono na kuagana.
Jioni ilipofika mama Erica alimuuliza mwanae,
“Kwanza Erica ni nani alikutumia picha na ujumbe kwamba Erick yupo na Sia?”
“Ni Sia mama”
“Aaah! Kumbe, mwenzio anataka kukurusha roho tu sasa wewe usionyeshe kama umeumia wala nini, onyesha kuwa upo kawaida kabisa, nay eye ndio atajisikia vibaya”
“Ila mama dah mapenzi haya, hapana kwakweli”
“Mapenzi ndivyo yalivyo mwanangu, kuna wakati utacheka na kuna wakati utalia, ndio mapenzi hayo”
Erica aliachana na mama yake na kwenda kufanya shughuli zake zingine.

Hadi usiku unaingia Erica hakutafutwa na Erick, swala hilo lilimuumiza moyo sana na kumfanya akose raha kabisa, hakuwa na usingizi ingawa ilikuwa ni usiku hivyo akachukua simu na kuingia kwenye mtandao ili kuone kama kuna jipya lolote labda Erick amemtumia ujumbe hakuona , ila leo aliamua kukagua akaunti ya Erick akaona hakuweka picha yoyote kwenye akaunti yake zaidi ya picha za maua na ujumbe ujumbe, akajiuliza kwanini hakuweka picha? Hakujua sababu, akaangalia na marafiki zake, akaona wote wale wa kwenye ofisi ya Erick ni marafiki zake, akiwemo na Sia, yani alijikuta akitamani sana kujua namba ya siri ya Erick ili ajiridhishe kuwa anaongeaga na nani mule kwenye mtandao. Akaona kuna jumbe Fulani kwenye ukurasa wa wazi wa Erick, akaona wa kwanza ukitoka kwa msichana,
“Erick nilikutafuta kweli, natumai wewe ndio Erick wangu wa kipindi kile”
Huo ujumbe ulitumwa jana, aliona moyo wake ukipasuka tu kwa wivu, akazidi kuangalia na kuona zingine za kawaida ila moyo ulikuwa unamuuma sana, mara akatumiwa ujumbe na Sia,
“Hulali shoga yangu, saa sita hii upo facebook! Pole sana, mapenzi yatakuua. Pole eeeh! Ila ndio ujifunze, sio kubambikia wanaume watoto, kwa taarifa yako shughuli niliyoifanya jana kwahakika nimepata mimba ya Erick na nitazaa nae uone kama atakufikiria wewe”
Erica aliumia sana ila alijiuliza kuwa huyu anayenishangaa silali, yeye amelala? Akamjibu
“Na wewe mbona hujalala? Na safari hii utakunywa sumu ya panya ufe kabisa, Erick ananipenda ingawa sijazaa nae ila ananipenda, unaweza ukazaa nae na asikupende, aliyekwambia kuzaa na mwanaume ndio kupendwa nani? Pole sana”
Aliamua nae kuwa na ujasiri kuliko kuendelea kujiumiza moyo, sia akamjibu tena
“Kama anakupenda mbona yupo na mimi?”
Erica akamjibu tena ili Sia aone kuwa hajaumia,
“Kuwa nae sio kwamba anakupenda sana, kuna watu hadi wanaolewa na hawapendwi kwahiyo kuwa nae wala sio sababu hiyo. Wewe hupendwi na ndiomana ukajaribu hata kujiua, ila mwenzio nina uhakika napendwa yani hata iweje Erick ananipenda sana, na kwa taarifa yako unafikiri kwa vipicha vyako ndio nitamuacha Erick! Hiyo haipo dada, tafuta njia nyingine”
“Yani Erica unanijibu hivyo?”
“Ndio, ulitaka nikujibu vipi? Na saivi hadi ndoa yani usage kabisa vichupa uchanganye na sumu ya panya unywe ili usiamke tena sababu kila ukishtuka tu utanikuta nae”
Sia hakumtumia tena ujumbe Erica, na kumfanya Erica ahisi kuwa Sian aye kaumizwa nay ale maneno, akaamua kuzima data sasa na kuweka simu pembeni ila kiukweli alikuwa akijikaza tu ingawa moyo ulimuuma sana kuhusu Erick.
Alijaribu kulala ila usingizi ulimpa kwa shida sana maana alilala saa kumi usiku.
 
SEHEMU YA 350

Kulivyokucha aliamshwa na mwanae maana alimletea swaga mpya kabisa alipoamka, kwanza alimfinya mashavu mama yake hadi akaamka na alipokaa tu akaanza kusema,
“Mama mpigie baba”
Alimshangaa mwanae maana hakumtegemea kama angemwambia vile kwa asubuhi ile, akamuuliza,
“Babako nani nimpigie?”
“Baba Erick, ataka ongea nae”
Kwakweli Erica alitamani sana kujua ni kitu gani Erick huwa anaongea na mwane kiasi kwamba mwanae amkumbuke asubuhi yote ile, basi akachukua simu na kujaribu kumpigia Erick akakuta hapatikani na kumwambia mwanae,
“Babako hapatikani”
Angel alianza kulia mpaka Erica ikabidi amsikilizishe kuwa hapatikani ndio akanyamaza na kutoka kwenda kwa bibi yake, kwakweli kwa kiasi Fulani Erica alichukia vile ambavyo mwanae alizoeshwa na Erick, sema hakuwa na la kufanya sababu mwanae alishazoeshwa hivyo.
Kwahiyo alitoka tu chumbani kwake na kwenda kufanya shughuli zingine.
Mama yake alimuaga kuwa kuna mahali anaenda kwenye shughuli zake za vikoba, ila akaongea nae,
“Ila mwanangu mamako nimechoka, maana shughuli hii nimeanza muda tu ila bado kuna watu wameendelea hadi natamani maendeleo yao. Kuna biashara haitanisumbua hata kichwa kuifanya ila sina mtaji”
“Biashara gani mama?”
“Natamani nianze kukopesha wamama, ningekuwa na milioni tano tu ingeniingizia faida nzuri sana halafu wala nisingetumia jasho sana”
“Ila biashara ya kukopesha mama utaiweza?”
“Naiweza ndio, idea zote ninazo sema sina hela tu”
Basi mama yake akaondoka zake, ila Erica aliona swala la mama yake ni swala zuri nap engine hela zake zitapata matuzimi, ila alijua akimwambia ukweli tu mama yake itakuwa tatizo kubwa sana. Basi mama yake alipoondoka tu na yeye akavaa na kuita gari kisha akaondoka na mwanae kuelekea benki, alikuwa akifanya haraka ili arudi kabla ya mama yake, na kweli alifika benki na kutoa zile hela, wakati anatoka pale benki akakutana na John, alitaka ampite ajifanye hajamuona ila John alimsogelea,
“Erica, unataka kunikimbia kweli?”
“Hamna bhana”
“Naona mtoto wa kaka anazidi kuchanua, mwenyewe karudi umeonana nae?”
“Hapana”
“Dah! Sio vizuri kwakweli, naenda kuweka hela ila ngoja nikupe kidogo kwa matumizi ya mtoto”
John alitoa laki tatu na kumpa Erica, ila kiukweli Erica alishangaa sana wasio na mtoto wana uchungu kuliko mwenye mtoto, Erica alichukua na kuondoka zake ambapo moja kwa moja alienda na ile gari nyumbani kwao.
Kufika tu kwao, mwanae alimuuliza,
“Mama Yule nani?”
Erica akaona mwanae kuna siku atamuumbua na maswali yake maana toka amejua kuongea amekuwa na maswali ya ajabu sana, kwahiyo hakumjibu bali alimgeresha tu na kuendelea na mambo mengine.

Ilikuwa ni Mchana na mama yake alikuwa hajarudi ila alisikia simu inaita akaamua kwenda chumbani kwake kuipokea, akakuta mpigaji ni Tumaini, akapokea hata hakumuogopa ingawa Erick alimwambia kuwa amblock Tumaini ila yeye hakumblock na alijipanga kumjibu kwa lolote atakalomuuliza,
“Hivi wewe Erica una akili kweli? Ndio nini kumjibu vile Sia?”
“Hivi wewe unahusika nini na ugomvi wa wake wenza? Unatakiwa kuwa mpole tu maana utake usitake ujue atakayeolewa na Erick ndio wifi yako”
“Aliyesema Erick atakuoa wewe nani?”
“Kumbe hujui!! Mimi ndio mke wa Erick”
“Hivi wewe Erica unajiamini nini wewe?”
“Najiamini sababu mimi ni mwanamke, na Erick atanioa mimi, kwaheri”
Erica akakata ile simu aliamua kufanya vile sababu ya jambo moja tu hakutaka kuona vile wakimsema wakati huo ameumizwa kuhusu swala la Erick na kutokupatikana kwake, kwahiyo alitaka na wao wajihisi vibaya kwa majibu yake.
Muda huu mama yake alikuwa amerudi na anajiongelesha mwenyewe tu kwa swala la kutokuwa na pesa, basi Erica akaenda na bahasha kwa mama yake na kumkabidhi, mama yake akahamaki,
“Nini tena?”
“Hela hizo mama”
“Zimetoka wapi?”
“Niliongea na Erick kuhusu swala la biashara unayotaka kufanya, ila sikumwambia kama ni wewe nilimwambia ni mimi ndio akaniletea hela za biashara hiyo”
“Kwahiyo pesa ngapi?”
“Ni laki tano mama”
“Weeee usiniambie, kumbe Erick ndio yupo hivi? Usimuache Erick mwanangu, achana na mada za wakina Sia”
Erica alicheka sana maana mama yake amekuwa kigeugeu baada ya kuona zile hela ila za mzee Jimmy hakuzitaka kabisa, kusikia za Erick alifurahi sana. Erica alishukuru mamake hajajua ukweli na akajua hawezi kumuuliza Erick kwani hajamzoea halafu amemwambia kuwa aliomba hela za kufanya biashara yeye kwahiyo hawezi kumuuliza.
 
SEHEMU YA 351

Jioni wakati Erica akiendelea na shughuli zake akasikia mlio wa simu yake na kwenda ndani kuipokea, alikuta ni Erick anapiga kwahiyo akapokea ili asikie uongo wake,
“Erica, najua utashangaa kuwa sio kawaida yangu na kweli sio kawaida yangu nilikuwa nje tu lakini haipiti siku nakupigia simu, iwe nchini kweli nishindwe kukupigia? Tafadhali Erica usinihisi vibaya, nakupenda sana. Naomba unisamehe”
“Nikusamehe umefanya kosa gani?”
“Sijakutafuta hewani, naomba unisamehe”
“Na mbona ulikuwa hupatikani?
“Erica hata sijui simu yangu iliwekwa wapi, ila kesho tuonane nikusimulie yaliyonikuta”
“Sawa, ila kesho nampeleka mtoto kliniki”
“Sawa, ukiwa kliniki utaniambia halafu mimi nitakuja kuwachukua wewe na mtoto, nataka nikueleze yaliyonisibu maana hata nikikwambia humu kwenye simu hautaelewa”
Erica alimuitikia tu ila alihisi tu maelezo atakayopewa na Erick ni uongo mtupu, akaagana nae.
Usiku ulipofika, mwanae akamuanzishia tena swala la kutaka kuongea na Erick, kwahiyo ilibidi ampigie na ampe mwanae aongee nae ambapo Angel alikuwa na furaha zaidi kumbe Erick alimwambia kuwa kesho wataonana.
Alivyomaliza Erica alichukua simu yake ile na kuweka pembeni kisha akachukua simu yake nyingine na kuingia nayo kwenye mtandao, alitaka kuona na siku hiyo Sia angemuandikia nini, ila kuna post aliiona akajikuta akiifatilia, ilisema
“Je mwanaume ukigundua kuwa mtoto wako amebadilishwa ubini na kupewa ubini wa mwanaume mwingine utafanyaje”
Aliona kama inamuhusu vile kwahiyo aliamua kuangalia watu waliochangia walikuwa na maoni gani, kwa bahati akakutana na maoni ya Rahim,
“Kwakweli kama ni mimi huyo mwanamke niliyezaa nae nitamuua kabisa hata asiwepo kwenye uso wan chi yani anibadilishie ubini mtoto wangu! Damu yangu! Naua kabisa”
Kwakweli hili oni lilimsisimua sana ukizingatia mtoaji wa oni hilo ndio muhusika ambaye mwanae kabadilishwa jina, aliamua kutoka kwenye mtandao kabisa akajiuliza,
“Hivi hawa watu wa mtandao ndio maswali gani hayo ya kuuliza watu? Mmmh sijui nifanyeje, Mungu wangu jamani”
Aliwaza sana ila alikosa jibu na kuamua tu kulala zake.

Asubuhi akajiandaa na kumuandaa mwanae kwaajili ya kwenda kliniki, aliondoka nyumbani na alifika na kuhudumiwa vizuri sana, ila sababu mwanae mtundu muwa wanaondoka akagoma kubebwa na kutembea, akamnyang’anya mamake pochi kisha akamwaga vitu vya kwenye pochi alikuwa na hasira sababu Erick alisema angeenda kuwachukua wakati wanaondoka ila akaona wanaondoka na mama yake bila baba yake kuja, wakati Erica ameinama kuokota vitu vya kwenye pochi yake, kuna mwanaume alitokea na kuinama pia kumsaidia Erica kuokota, alipoinua macho kumtazama alishangaa kumuona Rahim, wakati anamshangaa Rahim akamuona ameishika bima ya afya ya Angel akiiangalia, kisha Rahim akasema kwa mshangao,
“Angel Erick?”;


Asubuhi akajiandaa na kumuandaa mwanae kwaajili ya kwenda kliniki, aliondoka nyumbani na alifika na kuhudumiwa vizuri sana, ila sababu mwanae mtundu muwa wanaondoka akagoma kubebwa na kutembea, akamnyang’anya mamake pochi kisha akamwaga vitu vya kwenye pochi alikuwa na hasira sababu Erick alisema angeenda kuwachukua wakati wanaondoka ila akaona wanaondoka na mama yake bila baba yake kuja, wakati Erica ameinama kuokota vitu vya kwenye pochi yake, kuna mwanaume alitokea na kuinama pia kumsaidia Erica kuokota, alipoinua macho kumtazama alishangaa kumuona Rahim, wakati anamshangaa Rahim akamuona ameishika bima ya afya ya Angel akiiangalia, kisha Rahim akasema kwa mshangao,
“Angel Erick?”;
Erica akamnyang’anya Rahim ile kadi, Rahim akamuangalia Erica na kusema,
“Kweli Erica umeamua mtoto wangu umpe jina la huyo malaya mwenzio Erick?”
Ni wazi Rahim hakutambua kuwa Erick anayesemwaga na erica ni Yule Yule rafiki yake, Erica alikaa kimya tu kwa bahati alisogea karibu yao Salma na mimba kubwa sana inaonyesha Rahim alimpeleka Salma kliniki, halafu gafla Salma alianza kupiga kelele za maumizu, ilionyesha uchungu ulimsika kabla hata hajasema chochote, basi Rahim akainama kumsaidia Salma, Erica alitumia mwanya huo kuondoka mbele yao kwani hakutaka yaanze mengine.
Erica alitoka nje ya geti la ile hospitali, mara akamuona Erick ndio anashuka, cha kushangaza Angel alimkimbilia Erick na kumuwow kamavile alishawahi kumuona au aliambiwa kuwa Yule ndio Erick babake anayeongeaga nae, kwakweli hata Erica alibaki kaduwaa jinsi Angel alivyomkimbilia Erick, naye Erick alimdaka kwa furaha na kumbusu huku akisema,
“Aaaah binti yangu mzuri jamani, nakupenda sana”
Kisha akamuangalia Erica na kumwambia,
“Nisamehe kwa kuchelewa mpenzi”
Ila Erica hakujibu ambapo Erick aliwataka wapande kwenye gari ambayo alienda nayo, nao wakapanda ila bado kichwani kwa Erica kulikuwa na maswali mengi sana kuwa Angel amepatwa vipi na muunganiko na Erick ikiwa hakuwahi kumuona? Na kama damu nzito kuliko maji basi Angel alitakiwa amfurahie Rahim ila ndio kwanza alikuwa akishangaa tu Rahim akishangaana na mama yake, kwa hakika Erica hakuelewa kabisa. Basi walivyokuwa kwenye gari, Erica, Erick pamoja na Angel walikaa kiti cha nyuma na mbele ni dereva alikuwa akiwaendesha, Angel alipakatwa tu na Erick huku akimuuliza,
“Zawadi yangu baba”
Erica alizidi kushangaa kwakweli maana siku hiyo ni siku ambayo mwanae alimchanganya sana kupita siku zote.
Ile gari ilienda moja kwa moja ufukweni ambapo walishuka na kutafuta mahali pazuri na kukaa kisha wakaanza kuongea, ambapo Erica alimuuliza kwanza Erick,
“Imekuwaje Angel kakufurahia sana wakati hajawahi kukuona?”
“Ni kweli hajawahi kuniona kwa macho ila naamini amewahi kuniona ndotoni, damu ni nzito kuliko maji”
Erica akaguna maana hiyo damu nzito vipi wakati mtoto sio wake, kisha Erick akamwambia,
“Unajua ili mtoto akupende na akuzoee huwa inabidi upendo utengenezwe, kuna upendo wa asili na kuna upendo wa kutengeneza, mimi nipo kwenye upendo wa kutengeneza ambao mwisho utakuwa upendo wa asili, sitataka kumuona Angel akikosa raha, sitapenda kumuona Angel analia na siku zote nitampenda katika maisha yangu”
Kwakweli bado Erica haikumuingia akilini hata kidogo, gafla simu yake ikaanza kuita ila sauti ilikuwa ndogo sana, kuangalia mpigaji alikuwa ni Rahim, ikabidi amwambie Erick kuwa anaenda chooni ili akapokee hiyo simu ajue Rahim atasema nini, Erick hakuwa na tatizo kwani alibaki akicheza cheza na Angel.
 
SEHEMU YA 352

Erica alijiuliza sana kuwa Rahim anataka amwambie vitu gani, hofu ilikuwa kubwa sana kwake maana Rahim alishaujua ukweli kuhusu jina la mtoto, simu ikakatika na kuanza kuita tena, ikabidi aipokee,
“Hivi wewe mwanamke ambaye umehangaika dunia nzima na wanaume wote, leo hii unambadilisha mwanangu jina kwa misingi ipi? Yani naona post sijui ukikuta mwanao kaandikwa ubini mwingine najua tu ni mambo ya kawaida kumbe yapo! Niambie wewe malaya umeanzaje kumpa mwanangu baba mwingine?”
Erica akawa kimya tu na kumfanya Rahim aendelee kuongea,
“Erica, nadhani hunijui vizuri ulikuwa unaniona tu, mimi nina roho mbaya kuliko unavyofikiria. Mimi ni gaidi wewe mwanamke, nina uwezo wa kuteketeza wewe na familia yako kwa dakika, nina uwezo wa kuteketeza hicho kimwanaume chako kwa sekunde, mimi ni mafia, unawezaje kunifanyia kama hivi? Mwanamke mwenyewe hata hufai kutazamwa usoni kwahiyo umeuza mwanangu ili uolewe na hiko kibasha chako? Ni nani mwenye ujasiri wa kuoa mwanamke kama wewe mwenye kutembea na ukoo mzima, si atakuwa kaolea kijiji!”
Hakuna kitu kinachomuumaga Erica kama kutukanwa sababu ya kutembea na wanaume aliotembea nao yani hapo ndio huwa anaweza sema vibaya bila hata kuogopa maana maneno yale huwa yanamuumiza, akaanza kumjibu
“Rahim, nanyamaza kimya usifikiri mimi ni mjinga, nina akili zangu timamu. Kuhusu kumbadili mtoto jina sijakurupuka tu kama unavyodhani, hivi ulivyositisha huduma kwa mtoto ulifikiri atahudumiwa na malaika? Huna muda na mtoto, humjali, humthamini ila unajiita kuwa na wewe ni baba, hivi wewe ni baba kweli? Mtoto kakuona leo wala hajakushobokea sababu hakujui ila unaanza kufoka kuona bima ya afya ya mtoto, usipojiongeza kuwa watu watajiongeza kwaajili yako. Na kuhusu swala la umalaya hata wewe ni malaya ndio mana ulitembea na mimi mwanamke malaya, na kuhusu Angel kuwa Angel Erick ni sawa kabisa maana Erick sio wa ukoo wenu, na unajua fika toka siku ya kwanza nilikwambia mwanaume ninayempenda anaitwa Erick, kwahiyo usinichanganye, sitegemei chochote kutoka kwako”
“Hivi errica unapata wapi ujasiri wa kuongea hayo? Sihudumii mtoto sijui nini na nini, kipindi tupo kwenye mahusiano nilikuwa nakupa hela mara kwa mara, leo hii unadikiri kusema simuhudumii mtoto? Mbona huna akili wewe mwanamke, hela zote zile nilizokuwa nakupa, kwanini usingefanyia hata biashara eeeh! Umekalia tu kusema simuhudumii mtoto wakati nilikuwa nakupa hela kibao”
“Wewe ndio huna akili Rahim, usinitoe akili kabisa, wewe ndio huna akili namba moja. Sikatai ulikuwa ukinipa pesa ni nyingi tu na nilikuwa nakushukuru ila hazikuwa pesa kwaajili ya matumizi ya mtoto, zilikuwa peasa kwaajili ya matumizi yangu binafsi, na wakati nina mimba ilikuwa bado unanihudumia mimi, pindi mtoto kazaliwa ukasitisha huduma, hivi unategemea mtoto atakula nini huyo eeeh!”
“Ulishindwa hata kujiongeza ufanye biashara?”
“Ndio nimejiongeza sasa kwa mtafutia Angel baba mwingine wa kumlea, malaya anakuwaga na baba wa mtoto? Yeyote tu atakayetoa matumizi kwa mtoto ndio baba, yani Rahim usinitibue sijui utaiteketeza familia yangu kwa dakika siogopi yani jua kabisa siogopi, wewe ukiiteketeza yangu kwa dakika basi yako hata sekunde simalizi kuiteketeza, kumbuka nishatembea na ukoo wako mzima, achana na mimi, ulishasema mtoto wa malaya nae atakuwa hivyo hivyo kwanini sasa uhangaike na mwanangu? Muache kama alivyo, na Erick akishindwa kumlea nikipata mwingine nambadilisha vilevile, siri ya mtoto anayo mama, kwaheri.”
Kisha akakata simu na kuizima kabisa, alimjibu Rahim kiujasiri ila alikuwa amejawa na uoga vilivyo huku akijua kuwa ingekuwa ana kwa ana basi angepigwa atolewe ngeu siku hiyo lakini sababu kwenye simu aliamua kujibu anavyojisikia.

Erica akarudi alipowaacha Angel na Erick na kukuta Angel amelala kwenye mikono ya Erick kisha Erick akamjuuliza,
“Mbona umechalewa hivyo Erica, hiyo uwani uwani gani?”
“Ni tumbo linanisumbua gafla”
“Ooooh basi niwapeleke nyumbani”
“Itakuwa vizuri kwakweli”
Basi wakatoka pale na kwenda kupanda gari tena, huku Erica akimpa maelekezo Yule dereva kuhusu mahali wanapoelekea maana Erick hakupafahamu kwakina Erica, muda huu Erica hakukumbuka hata maswali ya kumuuliza Erick maana alikuwa ameshachanganywa na mambo mengi na kujikuta akiwa kimya kabisa hadi wanafika kwao, Erick alimuuliza,
“Mbona umekuwa hivyo Erica, kuna kitu nimekuudhi? Je nimekubore eeeh!”
“Hapana nit umbo tu”
Basi wakashuka ambapo Erick alishuka na Angel, na moja kwa moja waliingia ndani kwakina Erica na kumkuta mama Erica yupo ametulia tuli, basi wakamsalimia na Erica kumchukua Angel kwenda kumlaza yani hakuwa hata na wazo la kumtambulisha Erick kwa mama yake maana akili yake ilishavurugwa kabisa yani hakukumbuka chochote kile, maneno ya Rahim yalimchanganya vilivyo, alijikaza tu kumjibu lakini maneno yale yalimchanganya sana.
Pale sebleni alibaki Erick na mama yake Erica, kisha alianza kumuuliza,
“Wewe ndio Erick?”
“Ndio mimi mama”
“Haya, lini utakuja kumuoa mwanangu?”
“Mama, lazima nimuoe Erica yani lazima nimuoe, nitakuja rasmi hapa”
“Hujaogopa kufika muda huu?”
“Sijaogopa mama maana nia yangu kwa Erica sio mbaya, nina nia njema na Erica”
“Haya mwanangu, nakutakia mipango mizuri halafu nilisahau kukushukuru asante kwa zile pesa ulizompa Erica”
“Zipi hizo mama?”
“Si ile milioni tano, kwakweli nakushukuru sana maana kanipa karibia nitaanza biashara”
Erick hakujua kama aitikie au vipi, maana anakumbuka wazi kuwa hajawahi kumpa Erica hiyo hela sasa iweje ashukuriwe kwa hela ambayo hajawahi kuitoa? Alijikuta tu akijichekelesha ili Yule mama ashiwe na shaka nae ila alitaka sana kumuuliza Erica kuhusu huyo hela, wakatu huo huo mamake Erica akasema tena,
“Mbona unacheka tu baba eeeh! Nashukuru mamako kwakweli umetusaidia sana”
Erick akaamua kujibu tu,
“Hakuna tataizo mama”
Huku akiwa na mashaka kuwa huenda Yule mama anampa mtego ambapo akikubali ni tatizo ila aliamua kujitoa muanga na kukubali aone itakuwaje, ila Yule mama alikuwa akifurahi tu.
Wakati mama Erica akiongea na Erick, walishangaa ni muda mrefu sana Erica hakutoka ikabidi mama ke aende kumuangalia, akamkuta kumbe alilala pembeni ya Angel yani wakati ameenda kumlaza Angel nae akajilaza pembeni yake, ikabidi mamake Erica atoke na kumwambia Erick kuwa Erica amelala pamoja na mtoto, ilibidi Erick aage na kuahidi kwenda siku nyingine,
“Nitakuja tena Jumamosi mama”
“Sawa, karibu sana”
Basi Erick alitoka ila alijiuliza sana kuwa kuna kitu gani ambacho Erica anamficha maana hata ile hali ya siku hiyo hakuielewa kabisa, alishamweleza kuwa amwambie kila kitu lakini yeye anamficha, yani hakuelewa kabisa kuwa ni kwanini anafichwa na Erica. Basi aliondoka zake tu maana hakuwa na namna zaidi ya kuondoka.
 
SEHEMU YA 353

Ilikuwa ni jioni kabisa wakati Erica ameamka sasa maana alilala sana siku hiyo na hata hakujua kalala vile kwasababu gani, aliamka na kutoka nje ambapo alimkuta mama yake akifanya fanya shughuli zake, akamsalimia kisha mamake akamuuliza,
“Erica ndio tabia gani hiyo unakuja na mgeni hata umtambulishi?”
“Oooh nilisahau mama, yani nilisahau kabisa”
“Na kilichokusahaulisha ni nini eeeh! Yani leo unachanganyikiwa na kufikia hatua ya kusahau kama umekuja na Erick?”
“kwahiyo alijitambulisha mwenyewe?”
“Hamna nilihisi tu na kuanza kumuhoji maswali, haya wewe umevurugwa na kitu gani hiko hadi usahau mgeni?”
“Mama, leo wakati natoka kliniki nilipatwa na majanga”
“Majanga gani?”
Akajaribu kumsimulia mama yake kuwa alikutana na Rahim na jinsi Rahim alivyoona ile kadi ya bima ya afya ya mtoto na jinsi alivyomwambia kuwa ataimaliza familia yake, ila hakusema yeye ni majibu gani alimpa Rahim, mama yake alimuhurumia kwani kwa kiasi alimuona mwanae ana mapito,
“Ila mwanangu kosa lako ni moja tu”
“Lipi mama?”
“Huyo Rahim sababu aligoma kutoa matumizi ya mtoto yani kipindi kile kile ungemwambia bwana mimi nambadilisha mtoto jina maana umeshindwa kulea halafu ungeona angefanyeje, ila swala lingine je Erick najua kama Rahim ameanza kukufatilia?”
“Hajui mama”
“Mwambie ukweli, mwambie na vitisho alivyokupa, mwambie na jinsi alivyoona kadi ya mtoto, siku zote nakwambia ukweli huweka watu huru, ni bora kusema ukweli ili Erick ajue kuwa akikutana na Rahim basi akabiliane nae vipi, yani usimche, mwambie ukweli mtupu kuwa wewe na Rahim mko vipi, asishangae kusikia Rahim akikuita malaya, mwambie akupende ulivyo sio akupenda halafu akijua rangi yako halisi asumbue”
“Mmmh mama yani nimueleze yote hayo? Huoni kama nitampoteza Erick?”
“Basi usimwambie ila mwambie kama Rahim anakufatilia na ameshaona kadi ya mtoto, hilo ni la muhimu sana mueleze ukweli huo ajue”
“Sawa mama nitafanya hivyo”
“Na tena nimemshukuru Erick kwa ile milioni tano aliyokupatia”
Erica alishtuka kusikia hivyo maana mama yake alikuwa amemuongezea mabalaa, yani kumshukuru Erick wakati hajaitoa hela kwa Erick! Ulikuwa mtihani huo, mshtuko wake hata mama yake aliuona na kumuuliza,
“Wewe Erica vipi kushtuka hivyo?”
“Hapana sijashtuka mama”
“Niambie ukweli Erica, mshtuko wako huo sio wa kawaida”
“Hamna kitu mama ila sikujua kama umemwambia maana sikutaka ajue kama zile hela nilikupa wewe”
“Na mimi sijaona ubaya kumshukuru hata kama hakujua kama umenipa mimi, kushukuru ni jambo jema sana. Nimejifunza shukrani kwahiyo lazima nishukuru”
Erica alikaa kimya tu ila alitambua wazi kuwa mama yake kamuharibia tu.

Usiku uliingia na kwenda kulala ila Erick hakumtafuta kabisa hewani akaamua kumpigia yeye simu ila simu ya Erick iliita tu bila yan kupokelewa na kumfanya ajihisi vibaya sana kuwa Erick amechukia juu ya zile pesa, basi aliamua kutuliza mawazo yake kwa kuingia kwenye mtandao wa kijamii, aliingia tu na kukutana na picha ya Rahim akiwa ananyanyua chuma halafu kaandika,
“Katika mazoezi ya kumtoa mtu kafara mwaka huu”
Hakupenda kuendelea kuangalia ile picha maana aliona inamletea simanzi tu, kwani kila akifikiria maneno ya Rahim alihisi kichwa chake kuumia zaidi, basi alijitahidi tu na kuweza kulala.
Kulipokucha yani alfajiri kabisa alipigiwa simu na Dora na kuipokea ile simu na kuanza kuongea nayo,
“Erica, nilikwambiaje kuhusu hela za Yule mzee? Shauri yako, unadhani nakuonea wivu? Hapana nakuonea huruma”
“Sasa Dora, mi ningefanyeje jamani eeeh! Sikuwa na akaunti ya Yule mzee ningewezaje sasa kumrudishia?”
“Mi nilikwambia lakini bora hata ungezileta kwangu ningejua namna ya kukabiliana na huyu mzee lakini kuzitumia ni jambo litakalokutesa sana, una mtoto kumbuka”
“Na amejuaje kama nimezitoa?”
“Kumbuka Yule mzee ndio yuko pale benki kwahiyo anauwezo wa kufatilia taarifa za kila mteja halafu kajitapa kweli hela zake umeshazichukua?”
“Sasa nifanyeje Dora, yani unanishauri nini?”
“Sikia, wewe kama zile hela bado unazo kazirudishe halafu mimi nikafungue akaunti kwenye ile benki na kisha unihamishie ile pesa kama ilivyo yani aone kabisa kuwa zile pesa zilihamia kwangu”
“Dora jamani itawezekana vipi?”
“Itawezekana tu, ngoja le oleo nikafungue akaunti kwenye ile benki, jali maisha yako rafiki yangu, sitaki uteketee na uhangamie”
“Sawa nimekuelewa”
Basi akakata simu ila akawa na mawazo sana, anawezaje kumwambia mamake ukweli wa zile hela, na anawezaje kuzirudisha zile hela wakati kashampa mama yake na ameshaanza kuzikopesha? Yani akawa na maswali mengi sana, hadi anaamka na kwenda kufanya kazi alifanya kimawazo sana maana hakuelewa kwa usawa ule atatoa wapi milioni tano ya gafla na kwenda kuirudisha maana mama yake aliogopa kumwambia sababu kama akijua ni hela ya Yule mzee angemsema sana ila hakuwa na jinsi zaidi ya kuwa na mawazo tu.

Mchana wa siku hiyo hakuwa na namna nyingine zaidi ya kumpigia simu Erick, ingawa hakumuanza ila aliamua kumuanza yeye ili kujaribu kuongea nae, muda huo Erick alipokea simu ya Erica,
“Erick tafadhali nahitaji kuongea na wewe, usikatae nakuomba”
“Sawa, muda gani?”
“Hata muda huu, niambie popote ulipo nitakuja, nakuomba Erick”
Basi Erick alikubali na kumtajia sehemu ya kukutana nae, Erica alijiandaa na kumuaga mama yake kuwa kuna mahali anaenda ila hakumwambia tu ni wapi.
Basi aliondoka zake na kwenda kukutana na Erick, cha kushangaza Erick alifurahi sana kumuona Erica akamkumbatia kwa nguvu, na kwenda kukaa nae kuongea,
“Erick, mbona jana hukunitafuta na wala hukupokea simu zangu?”
“Erica lazima nijiridhishe kuwa kweli bado una upendo na mimi, kweli mtu gani wewe? Ulichonifanyia ni sawa/ Tunaenda kwenu halafu unaenda kulala bila kuniaga jamani? Ni sahihi hiyo?”
“Nisamehe Erick, najua si sawa ila si nilikwambia naumwa? Nisamehe sana”
“Hata kama unaumwa ila ulitakiwa kuniaga basi, halafu swali lingine umetoa wapi milioni tano na kumpa mama yako na kusema kuwa mimi ndio nimekupa? Una wanaume wengine Erica eeeh!”
“Ila nyie wanaume ni watu wa ajabu sana, yani mimi sijakuuliza kuhusu picha zako na Sia ila wewe unauliza kuhusu milioni tano ambayo huna hata uhakika kuwa nilipewa na mwanaume”
“Uitoe wapi? Huna kazi, upo tu, uitoe wapi Erica? Ungeniomba mimi sawa ila wewe kama wewe unaitoa wapi?”
“Ndio nimekutafuta nikueleze kuhusu hiyo hela, nisamehe sana kwa kutokukwambia mapema”
“Haya nieleze”
“Ni hivi, kuna baba mmoja huwa ananitaka na kulazimisha kuwa niwe mpenzi wake sema nilimkataa sasa alivyoijua akaunti ya Angel ndio akaenda kuweka hela hizo kwenye akaunti ya Angel, sasa mama aliponiambia ana shida na hela nikaona nikamtolee tu zile, ila kwasasa roho inanisuta balaa, na mama siwezi kumwambia anirudishie maana kashazifanyia kazi, nahitaji kumrudishia Yule mzee hela yake”
“Utamrudishia wapi?”
“Nitaenda kuomba akaunti yake na kumrudishia humo, hata hivyo mke wake nimemueleza kasema niirushe kwake”
“Sawa sawa, bora uiweke kwenye akaunti ya mke wake, na hiyo hela utaipata wapi?”
“Sijui, Yule mzee aliweka milioni kumi ndio nimetoa tano, zimebaki tano kwahiyo inabidi niirudishe hiyo tano nyingine ile mkewe nimtumie hizo kumi, ila mpaka sasa sijui hiyo tano naipata wapi? Nikamdai mama! Itakuwaje nikimdai sasa? Yani sielewi”
“Basi sikia, mimi nitakupa lakini kwa sharti moja”
“Sharti gani hilo?”
“Utaniletea fomu ya kumuhamishia huyo mke wake hela”
“Ooooh asante sana Erick, ninashukuru kwakweli”
“Aaaah usijali”
Basi wakaendelea na mazungumzo mengine, kisha Erica akakumbuka swala la Sian a kumuuliza Erick,
“Eeeeh Erick ndio kunifanyia nini vile?”
“Nini tena?”
“Erick kweli wa kunisaliti na Sia wewe! Yani Sia ananitumia kabisa picha mkiwa mmelala pamoja, halafu simu ukazima siku mbili kweli?”
“Halafu unajua ni zawadi gani nimekuletea kutoka nilipokuwa?”
“Erick, mbona unataka kubadilisha mada wewe, yani swali langu lingine halafu na wewe unaniletea swali lingine”
Mara simu ya Erick ikaita, akaipokea na kwenda pembeni kuongea nayo, kwakweli Erica alishangaa sana jinsi Erick anavyokwepa mada ya kuwa alilala na Sia, alipomaliza kuongea na simu alikuwa akitabasamu tu na kumwambia Erica,
“Twende”
“Wapi?”
“Yani leo imekuwa siku nzuri sana, ile zawadi niliyoagiza imefika”
“Zawadi gani?”
“Twende ukaione”
Kwahiyo wakaondoka pale na Erick na kupanda gari ambalo lilienda hadi bandarini, walishuka na kwenda ofisi za bandari ambapo Erick alimuonyesha Erica, gari mpya tena nzuri sana na kumwambia kuwa ni zawadi yake aliyomnunulia, kwakweli Erica alipagawa na ile zawadi, alijikuta akipata furaha isiyo kifani, akaiangalia ele gari na kufurahi sana, kisha wakakubaliana na Yule wa bandari kuwa,
“Mje muichukue Jumatatu, kuna mambo nakamilisha”
“Sawa hakuna shida, nilitaka tu mke wangu aone zawadi yake”
Yule mtu wa bandari aliwapongeza sana kuwa inaonyesha wanapendana sana,
“Endeleeni hivyo hivyo kupendana, ni vizuri sana”
Erica alitabasamu tu kisha Erick alimpeleka hadi kwao na kumuaga mlangoni tu na kumwambia kuwa alishamwambia mamake kuwa ataenda Jumamosi kwahiyo kesho yake ndio atafika mahali pale, wakaagana pale na kuingia ndani.
 
SEHEMU YA 354

Kiukweli Erica alikuwa na furaha sana kiasi kwamba hata akasahau kumwambia Erick kuhusu Rahim kwa furaha ya gari alilopewa na Erick, mamake aliiona furaha aliyokuwa nayo,
“Eeeh mwanangu, unafuraha sana leo. Yani umerudi na furaha tushirikishane basi”
“Subiri Jumatatu mama”
“Jumatatu nini? Ndio Erick anakuja kujitambulisha au?
“Hapana ila subiri utaona tu”
“Kupeana mshtuko huko, jambo la heri au shari?”
“Ni heri mama”
“Haya sawa kama ni jamboo la heri”
kwakweli Erica alikuwa na furaha sana hadi muda anajiandaa kulala alikuwa akitabasamu tu, Erick alimpigia simu na kuanza kuongea nae muda huo,
“Halafu nilisahau Erica. Ile hela nitakupa Jumatatu”
“Sawa, hakuna shida”
“Ila naamini Erica wale wanaume zako wa zamani ulishaachana nao wote, sitaki kusikia uchafu wowote unakufata”
“Erick, sina mwanaume mwingine zaidi yako mpenzi wangu”
“Yani Yule kijana niliyepigana nae siku ile simpendi jamani yani nilimchukia, nab ado namchukia hadi leo”
“Aaaah achana na Yule, kwanza ameoa Yule ana mke wake”
“Yani sitaki yoyote akufatilie Erica, wewe ni wangu”
“Hakuna mwingine Erick”
“Unajua uchungu wa mke eeeh! Mimi nina uchungu na wewe, nimekutoa mbali sana, tafadhali Erica nipende mimi tu”
“Nakupenda wewe tu Erick”
Alijikuta akiongea nae vingi sana vya kuhusu mapenzi yao na kusahau kila kitu kuwa alisalitiwa, yani hakukumbuka chochote ila alichowaza yeye ni kuwa Erick anampenda sana.
Hadi wanaagana na kulala, alilala na tabasamu zito sana.

Kulivyokucha alifanya kazi zake kama kawaida ila Dora alimpigia tena simu kumuwekea msisitizo wa zile hela,
“Nishafungua akauntui Erica”
“Basi Jumatatu au Jumanne nakutumia, nitumie akaunti namba na jina la akaunti”
“Sawa, nakutumia”
Basi ile simu ikakatika na muda kidogo tu Erica akapokea ujumbe toka kwa Dora wa namba na jina la akaunti, hakuwa na shida na ujumbe huo maana ni yeye mwenyewe ameutaka.
Wakati anataka kuweka simu pembeni akapigiwa na namba ngeni, akajua ni Dora pengine anataka kumpa maelezo mengine, akapokea akashangaa kumsikia Bahati,
“Erica, namba yako sikuikuta kwenye simu yangu yani nimehangaika sana kuipata, nimejaribu kupata kumbukumbu zangu na kuikumbuka ilikuwa kichwani mwangu, Erica nakupenda sana, mwanamke niliyemuoa simpendi mimi, nakupenda wewe erica”
“Kheee Bahati, niondoleee mabalaa jamani, si umeshaoa wewe, hebu tulia na mke wako”
“Hapana Erica, mke wangu simpendi, ninayekupenda ni wewe yani wewe ndio mwandani wangu, wewe ndio kila kitu kwangu”
Erica akaona huyu Bahati anamletea balaa tu, kwahiyo akaamua kumkatia simu na kumblock ili asimtafute tena. Basi akaenda kuendelea na kazi zake zingine za hapa na pale, kisha mchana mama yake alimuaga kuwa anatoka kuna mahali anaenda kuelimisha wamama kuhusu ujasiliamali, aliweza kuona ni jinsi gani mamake zile hela zimemchanganya hadi kawa muelimishaji wa ujasiliamali. Basi mama yake akaondoka na kubakia mwenye nyumbani na Angel.
Jioni ya siku hiyo aliamua kwenda kukaa nje kidogo kupata hewa ya nje, alipotoka tu alikuta Bahati ndio amefika, kiukweli alichukia kwani hakutaka Bahati tena afike kwao, ila Bahati alisogea na kumkumbatia Erica tena hakutaka kumuachia huku akidai amemkumbuka sana na sio kosa lake kuoa, muda huo huo wakati Bahati kamkumbatia Erica, ndio Erick nae alifika mahali pale na kuwashangaa.
 
SEHEMU YA 356

Kiukweli Bahati alienda nyumbani kwake huku akiwa na mawazo mengi sana, alifika na mkewe kumpokea ila alimsukuma pembeni bila kujali kuwa ana mimba wala nini, Nasma alimuuliza mume wake,
“Unanifanyia hivi mme wangu, nimekukosea nini?”
“Sikia wewe Nasma, sikupendi na sijawahi kukupenda. Nampenda mwanamke mmoja tu wa kuitwa Erica”
Lile swala lilimfanya Yule binti ajihisi vibaya sana, ila ukweli wa mambo aliujua na alichangia ingawa hakupenda mumewe abadilike vile, alimuangalia Bahati akikaa mwenyewe na kuonekana mwenye mawazo sana, alimfata tena na kujaribu kuongea nae,
“Inamaana siku zote hizi ulizoishi nami Bahati hujanipenda kweli?”
“Sikupendi Nasma na kamwe sitokupenda”
“Usiseme hivyo, kumbuka tumefunga ndoa”
“Ndoa gani hii? Ndoa batili hii, sijafunga kwa akili zangu, mwanamke ninayempenda mwingine nikakuoa wewe ambaye hata kwenye akili yangu sijawahi kukuwaza”
Nasma alijaribu kumsogelea mume wake ili ajaribu kumbembeleza, ila kile kitendo cha kumsogelea Bahati akamsukumiza, na hapo hapo Yule binti alianza kulia kwa kuugulia uchungu, ilibidi Bahati amuinue na kumpandisha kwenye gari yake kumpeleka hospitali.
Ilikuwa usiku ushaingia, wakampeleka leba na kumpima njia, kuona bado bado walimrudisha wodini na huko alikuwa akiugulia vilivyo, hadi kufahamiana na mwanamke mwingine aliyejifungua siku mbili kabla yake, walifahamiana kwa vile alivyokuwa akihangaika sana.
Alfajiri alijihisi tena uchungu mkali sana kwahiyo wakampeleka leba ambako hakukawia sana alijifungua, alifurahi sana kupewa mwanae mikononi kwani alikuwa ni mtoto wa ndoto zake, maana siku zote alitamani kumzalia mtoto wa kwanza mumewe awe wa kiume na mtoto Yule alikuwa wa kiume kwahiyo nilikuwa furaha sana kwake na kusahau yote ya jana yake kwani alijua upendo kwake utaonekana maradufu.
Akarudishwa wodini na kwenda kukaa na kichanga chake maana walimwambia ni baada ya masaa ishirini nan ne kupita ndio angepewa ruhusa ya kwenda nyumbani, Yule mwanamke waliyezoeana nae usiku alimpongeza sana na kumuuliza,
“Hongera, umejifungua mtoto gani mwenzangu?”
“Wa kiume, yani ndio mtoto wa ndoto zangu”
“Oooh kama mimi ila mimi nimejifungu kwa operasheni yani nilikuja kama siku ngapi zilizopita huko ila uchungu unakuja na kuacha kumbe nyonga ndogo ndio jana nimepasuliwa”
“Kheee hongera na pole”
“Asante, ila mimi naitwa Salma, sijui mwenzangu waitwa nani?”
“Naitwa Nasma”
Wakafurahi sana kufahamiana kisha wakaanza kufanya mazungumzo ya hapa na pale huku wakiangalia vichanga vyao.
Muda wa kuona wagonjwa ulipofika walikuja ndugu zao kuwaona na kuwaletea chakula na zawadi za watoto, baada ya muda kuondoka kwa ndugu zao walibaki wenyewe sasa, Salma alianza kuongea,
“Mimi nitaruhusiwa kesho hata wewe utaruhusiwa kesho, ila hongera ndugu yangu naona mumeo alikuja kukuona pia”
“Mmmmh mume aje wapi, jana yenyewe kanileta hospitali sababu hakuwa na namna ya kufanya ila hata kuniuliza tena imekuwaje hakuna, ingawa nimejifungua ila sijui mtiti wa nyumbani”
“Mmmh jamani wanaume hawa, mbona hawana huruma loh! Mimi nililetwa na mume wangu pia ila toka siku hiyo hadi leo hajaja tena hapa hospitali nadhani kaenda kufatilia kile kijanamke chake tulichokutana nacho hapa hospitali, yani wanaume hawana huruma jamani, kweli hali kama hii ambayo mtu unahitaji upendo na faraja ila wenyewe wanakuacha kwenye mataa kweli! Dah Mwenyezi Mungu atusaidie tu”
“Jamani wanaume hawa loh! Hadi kakutana na kimwanamke chake jamani tena hapa hapa hospitali! Loh”
“Yani mimi namchukia Yule mwanamke, namchukia maisha yangu yote”
“Kumbe unamjua mke mwenzio?”
“Ndio, ila hawezi kuwa mke mwenzangu nadhani bahati ya kuolewa hana. Ndiomana wanasemaga usililie uzuri lilia bahati, hiko kisichana kinaitwa Erica yani sikipendi kufa loh!”
“Kheee mbona wewe na mimi tumeanza kufanana sasa”
“Kwanini?”
“Mume wangu hanijali siku hizi, hataki kuniona sababu ya msichana mmoja anaitwa Erica”
“Kheee yukoje huyo msichana?”
Nasma alianza kumueleza Bahati kuhusu Erica alivyo kutokana na jinsi alivyomuona siku ile kliniki, kwakweli Salma alihisi kabisa Erica wanayemsema ni mmoja na kuchukia sana,
“Haiwezekani mwanamke mmoja asumbue akili za watu kiasi hiki, yani tushindwe kufurahia ndoa zetu sababu yake loh! Tuungane shoga yangu na tumtokomeze huyo Erica”
“Sawa, bora tuungane maana na mimi nachefuka haswaaa jamani mwanaume hata kufurahia nimemletea jembe jamani, ndio kwanza hata hospitali hajaja, yani kidudu mtu Erica namchukia pia”
Walijikuta wote wakieleza chuki za wazi wazi walizo nazo dhidi ya Erica.

Siku ya leo Erica aliamua kwenda tena kanisani na mama yake, na kama kawaida walimshangaa na Yule mtoto huku kila mmoja akisema lake, na walipotoka kwenye ibada kama kawaida walimfata na kumuuliza kuhusu mtoto aliyembeba,
“Ni wa nani huyo Erica?”
“Ni wangu jamani”
“Yani hata harusi hatujacheza umezaaa, kumbe umezaa nje ya ndoa”
“Bora mimi niliyezaa ila kwavile naonekana basi ndio mnaona ni mwenye dhambi kuliko watu wote, na je wanaotoa mimba kila kukicha, wao ni wasafi? Huyu mtoto ni wangu na sina sababu ya kumficha kwenu”
Basi wakamuangalia tu maana yale majibu yaliwashangaza sana na kuona Erica kabadilika haswaaa ukizingatia hakuwa na majibu ya aina hiyo.
Erica aliondoka na kurudi nyumbani, ila hakuongozana na mama yake kwani mama yake alienda kwenye vikundi vya wakinamama muwaelimisha kuhusu ujasiliamali na mikopo, Erica alikuwa akicheka tu na kujisemea,
“Yani mama yangu kamiliki milioni tano ila utafikiri anamiliki milioni mia, yupo kwenye semina kila leo kuelimisha wamama kuhusu mikopo, ikimuishia atakopesha nini? Hahahah mama nae”
Erica aliendelea na safari yake ya kwenda nyumbani kwao, siku hii hakupanda pikipiki wala bajaji, aliamua kutembea tu na mwanae.
Wakati anarudi kwao akakutana njiani na Rehema, alikuwa ni rafiki wa dada yake Bite hapo kitambo, Rehema alifurahi sana kumuona Erica na kumkumbatia kisha wakasalimiana pale na Rehema akasema,
“Yani nilitaka kuwaletea kadi ya harusi yangu ila siku nimekuja sikumkuta yeyote nyumbani kwenu na sikuwa na muda mwingine kwahiyo nilishafanya sherehe hadi nimesahau, mnisamehe bure”
“Usijali dada”
“Ila nilikutana na dada yako jamani, kheee Bite amekonda halafu hana raha kwani ana matatizo gani?”
“Sijui”
“Inaonyesha ana matatizo kwenye ndoa yake, nikipata muda nitakuja kuongea na mama yenu, unajua ndoa zina mengi sana yanoyotendekaga ndani ambayo kwa macho ya nje hatuyafahamu ila wenyewe wanandoa tu ndio wanayajua, kwakweli Bite kakonde, hana raha yani yupo yupo tu, ana gari nzuri lakini hana furaha”
“Ndio maisha hayo dada”
“Ila mdogo wangu cha kukushauri uwe makini sana kabla ya kuingia kwenye ndoa ili usije kujutia maisha yako yote, kuwa makini sana na mwanaume atakayekuoa, hakikisha mume anayekuoa anakupenda kweli hakika hutoteseka hata kama mmeolewa sita”
“Mmmh dada, ndoa za kuolewa wengiwengi sipendi”
“Hahaha nimesemea tu, ila kuwa makini usiolewe tu sababu wenzio wameolewa ila olewa sababu kuna nia ya kuoana wewe na mwenzio. NIkipata mida siku moja nitakuja kwenu kuongea na mama”
“Haya, karibu”
Erica aliondoka zake na kurudi kwao, ambapo alianza kufanya shughuli zake tu.
 
SEHEMU YA 357

Usiku ulipofika ndipo mama yake alirudi kutoka kwenye shughuli zake na kumkuta mwane, ambapo baada ya salamu Erica alimuuliza mama yake,
“Mama, hiyo milioni tano tu, ikiisha utakopesha nini?”
“Kheee mwanangu ishaisha ujue, halafu walioandikisha wanataka mkopo kwangu wapo wengi mpaka mama yako naishia kucheka tu, wangejua nilikuwa na milioni tano tu! Wenzio wanajua nina mahela mengi mengi, wengine wanataka wakope milioni mbili nimewakalia yani nimewakopesha wa elfu ishirini, elfu hamsini, laki na mwisho laki tano yani akiongeza tu simkopeshi”
Erica alicheka kweli maana mama yake alijifanya kibosile haswaaa na hela zenyewe zimemuisha, kisha akaanza kumuuliza,
“Mama na wewe jamani, jana ndio nini kunifanyia vile mwanao kwa Erick! Yani umenijoboa mweeeh hadi umenipigisha magoti mama”
“Kheee wewe mtoto hebu uelewe kula na kipofu, bila Erick hiyo milioni tano ningeipata wapi ndotoni au? Yani na Yule mjinga asije tena sitaki aweke kitumbua mchanga, tena hao wa kumroga wamroge tena ili asahau kabisa kuhusu wewe”
“Mama jamani!”
“Hakuna cha mama jamani, tunaangalia maendelea tu kwasasa, Erick ana akili sana halafu ana heshima yani nimempenda bure tena ukifanya ujinga nitakutembeza kwa magoti wewe kutoka barabarani kwenda kuomba msamaha kwa Erick, utapata wapi mwanaume kama yeye? Hebu acha ujunga huko, tuangalie maendeleo, na siku ukiona nipo halafu kaja Erick unatakiwa kunyenyekea, jana umeniudhi sana, hata chakula hukupika utajiondolea alama za ndoa ujue”
“Jamani mama, kwani ndoa ni mpaka kupika?”
“Ndio, unatakiwa ujue kupika, uwe msafi, uwe mpole, mnyenyekevu utafanya mume akupende mara dufu, akija hapa mnyenyekee, muulize atakunywa nini sio kukaa nae sebleni kama mabubu, akitaka kinywaji leta kwa unyenyekevu ikiwezekana na goti kabisa, unafikiri wanawake wa kijijini kwanini wanaolewa? Sababu ni wanyenyekevu, kila mwanaume anapenda kunyenyekewa, kusikilizwa na kuheshimiwa. Tena vijana wa ajabu ajabu marufuku kufika kwangu hapa sijui Yule wa kujitapa mimi ndio mwanaume wa kwanza kwa Erica, sitaki kumuona kabisa, umesikia!”
“Sawa mama, nimekuelewa”
Erica alimuitikia mama yake ili alitambua maneno yote hayo ni sababu ya hela zile alizoambiwa kapewa na Erick maana tangia hapo kampenda sana.

Basi muda wa kulala alienda kulala na mwanae ila akapigiwa simu na Dora, alikuwa akimkumbusha kuhusu swala la hela,
“Erica usisahau”
“Ni kesho Dora, hata sijasahau yani usijali”
“Sawa, nakuonea huruma ndiomana nakupigia pigia shoga yangu”
“Sawa, nimekuelewa”
Basi waliagana na Erica kuamua kulala.
Kesho yake mapema kabisa, alijiandaa na kumuaga mama yake kisha kwenda kwenye duka la Erick ambapo alimkuta Moses, aliyemkabidhi mzigo alioachiwa na Erick, basi alivyochukua akawa akiongea ongea na Moses ila Moses akamwambia,
“Erica, samahani siku ile kwa ile fomu niliyokusainisha haikuwa lengo langu nilitumwa na Tumaini kufanya vile halafu kuhusu kukupeleka dukani kwa Tumaini naomba unisamehe, yani hapa kwenye hili duka wengi huamini ni duka langu, maisha yangu yamebadilika sababu ya hili duka, sasa nisingependa nirudi nilipotoka, nakuomba Erica unisamehe”
“Sawa usijali”
Muda kidogo akapokea simu na alipomaliza kuongea nayo akamwambia Erica,
“Naomba uondoke maana kuna watu wanaagizwa na Tumaini na hawana nia njema kwako halafu usimwambie hata Erick kama nimekwambia hili la sasa hivi”
Erica hakutaka hata kuendelea kusikiliza zaidi kwani kwa muda huo maisha yake yalikuwa bora sana kuliko kingine chcochote, akaenda moja kwa moja benki na kukutana na Dora alishafika muda anamngoja tu, basi Erica akaenda kuweka zile hela na kuzihamishai kwenye akaunti ya Dora.
Yani waliondoka pamoja huku Dora anatabasamu tu na kumwambia Erica,
“Yani hutokuja kujutia kwa hiki ulichokifanya shoga yangu, nimefurahi sana kwa kuniamini. Yule mzee sio mtu mzuri”
“Sawa nimekuelewa Dora”
“Yani Erica wewe ndiomana unabarikiwa sana yani huna tamaa za kijinga, hela zinakufata lakini huna tamaa za kijinga na hilo swala litakuokoa”
“Kwahiyo wewe tamaa ndio zinakuponza?”
“Mmmmh mimi yani sijui mwisho wangu ni nini ila ulilolifanya leo Erica nakupongeza sana, wewe ni mwanamke shujaa”
Wakaagana na kuondoka, kwakweli Erica alishangaa sana zile sifa kedekede alizopewa na Dora ila alimuitikia maana ukweli wa mambo hakuujua zaidi ya Dora mwenyewe. Kisha Erica alirudi tu kwao akisubiria muda wa kufatwa na Erick kwaajili ya kufata gari.

Jioni kama alivyoahidi Erick alienda kumchukua Erica na kumkuta ashajiandaa kabisa na kuondoka nae, wakiwa kwenye gari akamuuliza,
“Mama umemwambia?”
“Hapana, nataka kumshtukiza tu”
“Ni vizuri sana”
Basi walienda na kufika bandari, wakati wapo kwenye makabidhiano mara alitokea mtu karibu yao na kuwasalimia, Erica alimuangalia mtu huyo alikuwa ni Rahim, aliogopa na kujiuliza kuwa Rahim kafata nini bandari.


Jioni kama alivyoahidi Erick alienda kumchukua Erica na kumkuta ashajiandaa kabisa na kuondoka nae, wakiwa kwenye gari akamuuliza,
“Mama umemwambia?”
“Hapana, nataka kumshtukiza tu”
“Ni vizuri sana”
Basi walienda na kufika bandari, wakati wapo kwenye makabidhiano mara alitokea mtu karibu yao na kuwasalimia, Erica alimuangalia mtu huyo alikuwa ni Rahim, aliogopa na kujiuliza kuwa Rahim kafata nini bandari.
Kiukweli Erica alipatwa na mashaka sana akikumbuka yale maneno ya Rahim kuwa anaweza kuwateketeza, muda huo huo Erica alijishika tumbo na kuanza kulalamika kuwa tumbo linamuuma sana, ila Rahim alicheka na kusema,
“Erica tumbo linakuuma wewe! Kwahiyo huyo Erick unayemsemaga ndio huyu!”
Erica alikuwa akiugulia tut umbo kitendo ambacho Erick hakufikiria kama Erica anaigiza ila alimuonea huruma, na kumchukua upesi upesi hadi kwenye gari yake na hata maneno ya Rahim kama anamfahamu Erica hakutaka kuyasikiliza, basi alipanda na erica kwenye gari yake na kuelekea hospitali wakati huo Rahim nae aliingia kwenye gari yake na kuwafata nyuma huku akisema peke yake,
“Huyu msichana asinitanie kabisa, na leo nitawavuruga”
Erick alimpeleka Erica hospitali ile ile ambayo Erica huwa anaenda kliniki, waliposhuka tu kwenye gari na kuelekea hospitali bado Erick aliona kama Erica ana hali mbaya maana alikuwa akiugulia tumbo hadi anatoa machozi, Rahim nae alikuwa amefika akiwafata nyuma.
Wakati wanaingia Erica na Erick wakapishana na Nasma na Salma maana walilazwa hospitali ile na muda ule walisharuhusiwa kutoka sema ndugu zao hawakufika kuwachukua, walikuwa wamebeba watoto wao huku wakiangalia kama kuna ndugu zao wanakuja kwahiyo walitoka ili kuangalia ndugu zao kisha kuondoka nao, kwahiyo kitendo cha Erick kupita huku amemshikilia Erica na tena akionekana analia kama anaumwa sana, ila walipopita karibu yao tu wote walijikuta wakisonya na kuangaliana kisha Salma akasema,
“Ndio erica Yule sijui limekuja kufata nini hapa hospitali kama sio uchawi tu wa kuturogea vitoto vyetu”
Muda kidogo akamuona Rahim akiwafata nyuma, pale ndio akachoka kabisa na kumwambia tena Nasma,
“Jamani ni mume wangu Yule ona alivyopita kama hanioni vile, na nimempigia simu kabisa kwamba nimeruhusiwa kasema yupo busy sana hawezi kuja kunichukua ila saizi yupo busy kumfatilia Erica jamani ni haki hii kweli?”
Aliongea kwa masikitiko sana, Nasma akamwambia,
“Pole mwaya, ila mie mume wangu na ubishi wake kaniambia anakuja nadhani muda sio mrefu atafika”
Kweli muda sio mrefu Bahati alifika ila alipitiliza na kwenda kule kule alipopelekwa Erica, kumbe muda Erica na Erick wanashuka yeye aliwaona maana ndio alikuwa anaingia hospitali kwahiyo alitaka ajue ni kitu gani kimempata Erica, kwakweli Nasma nae aliongea kwa masikitiko,
“Mungu wangu ona na mume wangu hata mimi hajaniona kaenda kule kule”
“Kheee Yule aliyepita ndio mumeo”
“Ndio yani hadi nashangaa, dada tusikalie kimya swala hili lazima tufanye jambo”
“Kweli sasa tufanyeje?”
“Hebu tupeane namba za simu baada ya arobaini za watoto wetu tushirikiane, haiwezekani huyu kiumbe mmoja Erica atukoseshe raha kiasi hiki, kwani yeye ana nini ambacho sisi hatuna eeeh! Lazima tufanye jambo”
Pale pale wakabadilishana mawasiliano yao ila kuna mmama pembeni alisikia mazungumzo yao, akawafata na kuwaambia,
“Jamani wanangu nimewasikiliza vizuri, najua ni kiasi gani inauma kuona mumeo anakuacha na kwenda kufatilia mwanamke mwingine, ila kabla ya yote mnachotakiwa kufanya sasa ni kufuata waume zenu na kuwalazimisha mrudi nyumbani na watoto halafu mengine yatafuata, mnitafute niwaambie cha kufanya maana hata mimi mume wangu alikuwa hivyo nikamdhiti”
Pale pale wakachukua namba za Yule mama kisha wakafata ushauri wake wa kwanza wa kufata waume zao, waliwafata na kukuta wapo nje katika chumba cha daktari ambapo ndani alikuwepo Erica na Erick, ila ilionyesha hata wao kama wamechanganyikiwa hivi wakitaka kujua hali ya Erica, kila mmoja alimfata mume wake na kumuomba warudi nyumbani, kwakweli Rahim alikuwa mkali sana kwa mkewe na Bahati nae ilikuwa hivyo hivyo,
“Huoni kama kuna mgonjwa nataka kujua hali yake hapa”
“Jamani Bahati kumbuka mimi ni mkeo na huyu ni mwanao, toka nimejifungua hujaja kutuona na leo tunatoka ukaahidi kuja kutuona kweli unadhani ni sahihi unachotaka kufanya kwangu?”
Wakati huo mke wa Rahim nae alikuwa akimlalamikia mumewe maana Rahim ndio alikuwa na majibu ya shombo balaa kwa mke wake, Bahati akamtazama na kugundua kuwa ni Rahim ambaye waliwahi kubishana kuhusu Erica miaka ya nyuma, alisogea na kumwambia,
“Wewe jamaa si ndio siku ile ulisema Erica hatutaki wote anamtaka mtu wake Erick, haya unasubiri nini sasa? Erica si ameingia na mtu wake humo!”
Rahim akamjibu kwa ukali,
“Achana na mimi”
Bahati akaona itakuwa shari hapo kwahiyo aliamua tu kuondoka na mkewe huku akisema kwamba ataenda kwakina Erica kujua hali yake, kwahiyo alibakia Rahim na mkewe,
“Jamani mume wangu siku zote huniambia kuwa humpendi Erica, alijipendekeza tu kwako sasa unamsubiri wa nini hapa?”
“Wewe ni mwanamke tu hujui lolote, kwanza nyie wanawake sio wa kuwaamini, kwani wewe unaweza kuwa na tofauti gani na Erica, si mwanamke mwenzio huyo”
“Mwamani mume wangu, nimekuzalia mtoto wa kiume”
“Kwani mtoto wa kiume ndio nini? Mtoto ni mtoto, kumbuka Erica ana mtoto wangu pia”
“Rahim nimechoka kwakweli, nitaanza kupiga kelele hapa hospitali uumbuke”
Rahim alizijua akili za mkewe kwahiyo ilibidi akubali tu kuondoka nae maana alijua kifuatacho ni kudhalilishwa tu, akaondoka nae ila alikuwa akilalamika njia nzima kuwa kwanini ameoa mwanamke wa dizaini ile,
“Ni kosa la baba kunitafutia mwanamke chizi, bora hata Erica”
Yani mkewe alimuangalia tu ila aliridhika sababu amekubali warudi nyumbani.
 
SEHEMU YA 358

Wakiwa kwa daktari Erica na Erick bado Erica aliendelea kulia sana, huku dakari akijaribu vitu vyote kumtuliza ilishindikana,
“Dada, tulia basi uniambie hata kwa kifupi nini kinakusumbua nielewe vizuri kisha nihudumia wagonjwa wengine”
“Ila Erica alichukua muda mrefu sana na daktari alishindwa kuwafokea au kuwatoa sababu walipoingia tu Erick alianza kwa kumpa hela ili amuhudumie mtu wake vizuri, basi daktari akaamua kumwambia Erica apande kitandani ili kujua tatizo ni nini, alipopanda tu kitandani Erica alimpa ishara Yule daktari kuwa amtume Erick nje ili amueleze basi daktari alitumia uelewa wake kisha akamtoa damu Erica na kuweka kwenye bomba kisha kumuandikia maelezo Erick kuwa aende maabara akapime damu hiyo na asubirie majibu, akawapigia wa maabara kuwa wampokee kwamaana hiyo Erica hakwenda hata maabara. Daktari alifanya vile maana hakukuwa na namna nyingine ukizingatia Erick aligoma kutoka kwenye chumba cha daktari kabisa. Erick alipotoka tu kupeleka kile kipimo, daktari alianza kumuuliza Erica vizuri,
“Eeeeh tatizo ni nini?”
“Daktari sina tatizo lolote ila naomba umwambie mchumba wangu kuwa nina vidonda vya tumbo, sasa vilinishika ndiomana kuongea nilikuwa siwezi. Naomba umwambie hivyo maana akigundua nimemdanganya ataniacha”
“Sawa hakuna shida, sasa wewe utanisaidiaje kwa kudanganya hivyo?”
“Nina elfu thelathini dada yangu, nitakupa”
“Aaaah elfu thelathini ni ndogo sana yani nifiche siri kwa hela ndogo hivyo hapana”
“Basi nikupe ngapi?”
“Labda laki”
“Sawa, nitakupa laki moja dokta, nakuomba nisitiri”
“Mmmh haya mambo, ila huwa tunakutana na mengi sana zaidi ya haya, sema sikufahamu ujue!”
“Ndio ila mimi naitwa Erica, na mwenzangu waitwa Dokta nani?”
“Naitwa Dokta Doroth”
“Sawa, nisitiri Dokta nakuomba”
Kwavile Yule ni dokta, alihisi kuna jambo limempata Yule binti kwahiyo aliamua kumbebea aibu yake, akamuuliza tena
“Na hiyo laki naipataje?”
“Nakutumia kwenye simu yako, tafadhali”
“Kwenye simu yangu lini?”
“Nakuomba niamini tafadhali”
“Nikuamini vipi?”
Alikuwa na elfu thelathini akamkabidhi Yule dokta ila bado dokta alitaka amaliziwe chake mapema, Erica alimsisitiza kuwa atammalizia,
“Sikia binti sikujui hunijui, nimalizie changu kabisa, la sivyo nasema ukweli”
“Sasa nitaitoa wapi hapa? Yani hela ipo nyumbani, nakuomba nisitiri mwanamke mwenzio, sikudanganyi nitakumalizia kweli tena”
“Hapana kwakweli na mimi nipo kazini hapa, nimalizie kabisa”
“Dada nakuahidi kuimaliza, basi naomba nikuachie simu yangu halafu kesho nikija kumaliza deni nitaichukua”
Daktari alikubali kuachiwa ile simu na Erica, basi Erick aliporudi na vipimo alikuta Erica yupo sawa na dakatari akamwambia kuwa kampa dawa ya kumtuliza, kisha akamuelekeza,
“Huyu ana vidonda vya tumbo kwahiyo asikae na njaa kwa muda mrefu na aepuke kula vyakula vyenye aside, akizingatia hayo atapona”
“Nashukuru daktari maana nilikuwa na mawazo sana”
Kisha Erica na Erick wakatoka pale hospitali na kupanda gari wakielekea nyumbani ila Erica alikuwa na mawazo sana maana yaliyotokea kwake siku hiyo ni makubwa sana, walitembea njia nzima na Erica alikuwa haongei chochote, sababu ilikuwa ni usiku Erick akamwambia,
“Erica, mpigie mama simu kuwa utachelewa kidogo maana nataka tupite kula”
Erica akajiuma uma maana simu hakuwa nayo, hadi Erick akarudia tena kumwambia, ndipo akaamua kujifanya anaitafuta na kushtuka,
“Kheee kumbe nimeiacha hospitali kwa Yule daktari”
“Erica jamani, umeanzaje kusahau simu jamani, ngoja turudi kuifata”
“Hapana Erick usisumbuke, nitaifata kesho”
“Hapana haiwezekani, yani jishindwe kuwasiliana nawe usiku sababu simu umesahau kwa daktari! Nageuza gari tukaifate”
Basi Erick aligeuza gari kitendo hiko kilifanya Erica ashikwe na mashaka balaa maana hakujua hata kitu gani atafanya alibakia tu kusema,
“Mungu nisaidie”
Maana uongo aliofanya siku hiyo hakutegemea kusamehewa na Erick kabisa, basi walifika hospitali yani Erick alivyosimamisha tu gari Erica alishuka na kumwambia,
“Erick usihangaike kuliingiza ndani na kupaki ngoja nikaichukue mara moja twende”
“Hapana bhana, hali yako bado si sawa, ukizidiwa huko je!”
Erica hakusikiliza haya maoni kwani alienda tu hospitali na moja kwa moja kuingia kwa Yule daktari na bahati hakuwa na mgonjwa, Yule Doroth alimshangaa na kumuuliza,
“Kheee umerudi tayari, si unaona usingeacha simu usingeniletea”
“Dada sio hivyo, yani jamaa yangu hataki kunielewa kabisa kuwa simu nimeacha hospitali nakuomba kesho nikuletee hiyo hela, naomba simu tafadhali”
“Unadhani naweza kukuamini kirahisi hivyo!! Sikujui hunijui, hiyo kitu haiwezekani, nipe change ndio uondoke”
Basi akapata wazo la kumpigia simu Bahati, akamuomba Yule dada simu ili apige kwa mtu wa kumtumia hela, basi Yule dada akampa na kuiwasha kisha kumpigia Bahati,
“Erica, nini tatizo mama angu eeeh! Nimesikitika sana sijakujulia hali hospitali”
Tena ikawa ni vyema kwa Erica kusikia kuwa amejua kwamba alikuwa hospitali, akamwambia
“Bahati naomba nitumie laki moja nina shida nayo muda huu”
“Shida gani tena?”
“Nitakwambia ila naomba unitumie, nakupa namba za kunitumia, nitumie nay a kutolea”
Kisha Erica akamtumia ujumbe Bahati wa namba ya simu ya Yule daktari kuwa amtumie hela kwenye hiyo namba, na muda kidogo tu Bahati alikuwa kashatuma hela, Erica alimpigia na kumshukuru sana kisha akakata ile simu na kumwambia daktari,
“Basi ile elfu thelathini yangu naomba”
“Aaaah sikupi, ile nimekata kwa usumbufu”
“Jamani daktari”
“Unafikiri kudanganya kazi ndogo eeeh! Sikupi”
Aliona simu yake inaita yani Erick alianza kumpigia simu kwahiyo aliamua kuondoka zake maana hakuwa na namna tena ingawa aliona Yule dokta kamfanyia unyama wa hali ya juu ingawa angeamua kuweka wazi yote yale yasingetokea.
Basi alirudi kwenye gari na kumpigia mama yake kuwa atachelewa kidogo,
“Mama nitachelewa kidogo, kuna mahali naenda kula na Erick”
“Ila kuwa makini mwanangu”
“Usijali mama, nipo makini”
“Nakujua unavyompenda huyo mwanaume na umejikuta kumuamini balaa ila narudia tena usimuamini mwanaume, siyo ndugu yako wa kuaminiwa hata mara moja”
“Sawa mama usijali”
Kisha safari ikaendelea na kwenda sehemu ya kula na Erick ila akaona ni vyema wakiwa wanakula abwage manyanga, aliamua tu siku hiyo aseme ukweli maana aliona vyema nafsi yake ibaki huru kwakuwa alikumbuka jambo moja kwamba ukweli humuweka mtu huru, kwahiyo aliamua siku hiyo aseme ukweli tu.
 
SEHEMU YA 359

Basi walifika kwenye hoteli nzuri sana na kushuka, kisha kukaa kwenye meza na kuagiza chakula ila Erica alikuwa na mawazo sana, kwanza hakupenda ambacho Yule daktari alimfanyia na pia hakupenda kushindwa kwake kupata gari sababu ya Rahim, ila hapo alitulia akijipanga kusema ukweli kwa Erick juu ya Rahim, walipoanza kula ni Erick ndio alimuuliza Erica,
“Hivi erica, unamfahamu Rahim?”
Erica alitulia kwa muda na kujibu,
“Ndio namfahamu”
“Erica, nakumbuka kuwa uliniuliza maswali mengi sana kuhusu Yule mtu, na mbona hukuniambia ukweli kama wamfahamu?”
“Nisamehe Erick ila sikujua ungechukulia vipi kama ningekwambia ukweli”
“Haya niambie mnafahamiana vipi?”
“Yule kijana ndio babake Angel”
Erick alijikuta akikohoa hadi chakula alichokuwa anakula kikaanguka, na kumuuliza tena Erica,
“Unasema!”
“Nisamehe Erick, ila Yule ndio babake Angel”
“Yani bora hata usingeniambia kama unamjua ila huna aibu Erica, unaniambia kabisa Yule ndio babake Angel ili iweje, na mimi ni nani?”
“Nisamehe Erick”
“Hivi Erica ulishindwa kuzaa na mimi ukaenda kuzaa na Yule kweli? Uliniona mimi malaya ila Yule akawa mtakatifu kwako kweli? Hivi Erica ni wewe ambaye nilikuwa nakuona shuleni kama binti mlokole au ni Erica mwingine? Sielewi Erica, hukuona wanaume wote wa kuzaa nao zaidi ya Yule?”
“Nisamehe Erick”
“Nikusamehe kitu gani? Yani unachojua wewe kusema ni nisamehe tu hata hufikirii jambo lingine zaidi ya nisamehe, nilikwambia tuzae ukagoma, nimerudi nimekwambia nina hamu umegoma ila kumpa Yule mjinga umeona sawa, kweli Erica wewe ni wa kutembea na Rahim jamani! Sijawahi kufikiria kama inaweza tokea siku moja mke wangu akawa amewahi kutembea na wanaume vichaa kama Rahim, nimejitolea kwa kila hali juu yako, nakupenda, nakujalo, nakuthamini lakini wewe ndio kunidhalilisha kiasi hiki kweli!”
“Ila Erick sijatembea nae kwa kipindi hiki, ilikuwa ni zamani alinidanganya”
“Inamaana na elimu yako hukuweza kutambua mwanaume wa kweli yupi na wa uongo yupi, hukuwa na maana ya kusoma basi. Ni afadhali ungezaa na mjinga mwingine kuliko mpumbavu kama Rahim, nilihisi tu nilivyomuona mtoto ila sikutaka kuongea. Kiukweli Erica umeniboa yani umeniboa sana hata chakula hiki siwezi tena kukila, kwaheri”
“Lakini Erick usinifanyie hivyo!”
“Nisikufanyie hivi nini, mtu hujielewi nakuomba mapenzi hutaki unajifanya kuumwa sijui siku zako kumbe unamtunzia Rahim, kwahiyo mimi nikuleee, na kukuhudumia halafu starehe apewe Rahim, mimi sio bwege kiasi hiko Erica, umeniboa sana kwaheri”
Erick akainuka huku amefura hasira na kuondoka, alimuacha pale kwenye hoteli Erica peke yake, kwakweli Erica alihisi kuchanganyikiwa alijikuta akiinama na kulia maana hakujua kuwa afanye nini kwa muda huo maana hakutegemea kama Erick angeweza kumuacha kiasi kile, kumuacha eneo lile ni bora hata angeenda kumuacha kwao, alijiangalia hakuwa na hela yoyote maana yote alitoa hospitali kwa Yule dokta, alijihisi kuchanganyikiwa, alipotaka kuinuka ili aondoke, muhudumu wa ile hoteli akamsimamisha na kumwambia,
“Dada, hamjalipia chakula bado”
Erica alijikuta akianza kulia huku akisema,
“Mungu wangu nitafanyaje mimi, uwiii Erica leo nimepatikana. Akajaribu kuongea na Yule muhudumu kuwa pesa hiyo apelike kesho ila muhudumu akagoma na kusema,
“Wakati mnaagiza vitu vya gharama hivyo mlikuwa mnategemea nini? Hapo mnadaiwa elfu ishirini na tano”
“Ila hatujala”
“Haijalishi maana mlishaagiza”
“Basi naomba niache simu yangu, kesho nilete hiyo pesa”
“Simu yako haina umuhimu kwetu, umesikia dada, unachotakiwa ni kulipa hiyo hela. Twende kwa meneja”
Erica alipelekwa kwa meneja wa ile hoteli ambaye nae alichukia kuambiwa chakula walichoagiza na hawajalipia,
“Sasa mdada unategemea nini?”
“Naomba niache simu yangu hii na nitakuja kulipa kesho”
“Unadhani simu yako ni muhimu kwetu? Cha muhimu ni pesa, nyie wadada ndio zenu hamjifunzi tu ukienda hotelini na mwanaume unatakiwa kuwa na hela yako ya ziada ili likitokea la kutokea uweze kujinasua ila wewe hukujua hilo unaenda matembezi na mwanaume na huna hela yoyote, sasa mimi nakupa cha kujifunza ili siku nyingine usirudie kutoka na mwanaume na kuagiza vitu vikubwa wakati huna hela mfukoni”
Kisha akamuangalia Yule muhudumu na kumwambia,
“Mpeleke akaoshe vyombo huyo, hatuna shida na simu yake”
Erica alipelekwa sehemu ya kuosha vyombo, macho yake yalijaa kwa machozi alijikuta akilia sana na hakutegemea kama jambo kama lile lingempata kwa siku hiyo ya furaha, maana gari hakupata ila kapata majanga juu ya majanga na kuweza kuelewa usemi wa Yule mama kuwa ana kimavi, alikosa raha kabisa.
Alikuwa akiosha vyombo huku amejawa na machozi kwenuye macho yake, muda kidogo simu yake ikaita, alihisi ni Erick anapiga labda kajirudi ila alichukua na kukuta mama yake anapiga, machozi yalizidi kumwagika na kupokea ile simu huku akilia, mamake akamfokea
“Wewe mtoto vipi? Hujarudi nyumbani halafu nakupigia simu unajitia kulia, Erica hebu acha ujinga wako huko, kwanini hujarudi nyumbani?”
Erica hakumjibu mama yake na kuendelea kulia, mama yake aliendelea kuongea,
“Erica, nakwambia kama umeanza ujinga wako tena wa kujirahisisha kwa wanaume usahau hapa nyumbani, ndio nakuozesha hivyo bila harusi, yani wewe kutoka kidogo na Erick ushaenda kulala nae! Na ukirudi hapa utanieleza, sio kujiliza kwenye simu, kwani unafikiri siujui uongo wako au!”
Erica aliweka simu pembeni na kuendelea kulia yani hakuwa na raha na wala hakuweza kuendelea kuosha vile vyombo, muhudumu akaenda na kumwambia,
“Dada, usilie osha hivyo vyombo”
“Dada, hivi huna huruma na mwanamke mwenzio, hivi nyie ni wanawake wa aina gani ambao mna roho mbaya kiasi hiki”
Aliongea huku akilia, Yule muhudumu akaenda kumuita meneja tena, meneja alifika na kumwambia Erica,
“Tutakupeleka polisi, hatutaki ujinga kabisa, tutakupeleka kuwa umetaka kututapeli, hebu osha vyombo hivyo”
Kwakweli Erica alilia tu ila wazo la kumpigia simu tena Bahati likamjia, ila alipiga simu haikupokelewa Yule muhudumu akamwambia,
“Huyo mwanaume ashakuacha, yani wanawake wengine nyie sijui akili zenu ziko vipi, mnashindwa kujifunza au? Tena ushukuru tumekupa kazi ya kuosha vyombo unapata hata pa kujistiri, tukikuruhusu kuondoka saa hizi saa saba si utabakwa huko useme tuna roho mbaya! Bora ung’atwe na mbu tu hapo uoshe vyombo”
Kisha wakaondoka na kumuacha ila Erica alikuwa na kilio cha hali ya juu na hakupenda ile hali.

Erick hakwenda kwao kwa mawazo aliyokuwa nayo ila alienda baa na kuanza kunywa sana, yani ni alikunywa hatari ila badae akakumbuka kuwa alimuacha pale Erica bila ya kumpa nauli wala kulipa ile bili, alidhani kuwa wangemsumbua sana Erica, ingawa alikuwa amelewa ila alimuonea huruma sana Erica, akataka kuinuka ila akamuangalie Erica pale, sema muda huo huo akapigiwa simu na Rahim na kupokea,
“Aiseee umenisikitisha sana Erick, yani kumbe erick aliyechukua majukumu ya kulea mwanangu ni wewe!”
“Bwana Rahim, achana na mimi”
“Sio niachane na wewe, hivi unamjua Yule mwanamke vizuri au unamsikia, unajua kwanini kazaa na mimi ila sijamuoa? Erica ni msichana mzuri sana ambaye kila mwanaume atatamani kuwa nae ila ni msichana asiye na akili, huwezi amini, Erica katembea na ukoo wangu mzima, nikikwambia vitu alivyofanya Erica huwezi kuamini”
“Sawa hakuna tatizo ila hayo yalipita, kama alitembea na ukoo wako mzima yalipita, nampenda Erica”
“Shauri yako, nakuonea huruma, nilivyorudi tu kesho yake au keshokutwa nilikuwa na Erica tukila raha, ndio mwanamke wa kujihesabia nae wewe”
Lile jambo ndio lilimuumiza zaidi Erick na kujikuta akikata ila simu na kuagiza pombe nyingine, alikunywa sana na kujikuta akilala pale pale Bar maana hakuwa na raha hata kidogo.
 
SEHEMU YA 360

Bahati alikuwa na mawazo tu tangia muda ule Erica kamuomba laki, hakujua ni jambo gani limempata Erica mpaka kawa vile maana sio kawaida kabisa, alikuwa na mawazo mno juu ya Erica, Nasma alitambua hilo ya kuwa mumewe ana mawazo juu ya Erica, alimzia mumewe kalala akachukua simu yake na kwenda kuiweka bafuni na ndiomana muda wote Erica anampigia hakupokea, Bahati alikuwa amelala kwenye kochi, kwenye mida ya saa kumi alfajiri alishtuka na kuanza kutafuta simu yake ila hakuiona, aliitafuta sana ila hakuiona popote pale, wazo likamjia kuwa huenda ni mke wake tu kaificha.
Bahati alimfata mkewe chumbani na kumuuliza ilipo simu ila mkewe akasema hajui ilipo, Bahati alifoka kwa hasira,
“Humu ndani tupo wawili tu, wewe, mimi na mtoto mdogo je simu achukue nani?”
“Tupo wawili sababu umekataa ndugu zangu wasije kuniuguza”
“Ulishindwa nini kusema nikupeleke kwa ndugu zako? Yani hapa sitaki ndugu zako wala ndugu zangu, hujui hii nyumba nimeipataje wewe. Haya simu iko wapi?”
“Sijui”
Bahati aliamua kutumia nguvu ili mkewe amuonyeshe simu ilipo, alimzaba vibao kadhaa mpaka mkewe akasema ukweli kuwa simu kaiweka bafuni.
“Mwanamke mjinga sana wewe, sijui nilianzaje kuoa mwanamke mjinga kama wewe”
“Jamani Bahati hunipendi, nimekuzalia mtoto ila hunipendi jamani kwanini unanitesa hivi!”
“Usinibabaishe nikaongea mengine bure”
Bahati akaenda kuchukua simu yake nakukuta alipigiwa na Erica mara mbili, alichukia sana na kumpigia Erica ila Erica alisema tu hoteli aliyokuwepo bila kusema tatizo ni nini, kwakweli Bahati hakusubiri kwani muda huo huo alijibeba na kuondoka kwakweli mke wake alikuwa na simanzi sana na kuona anaonewa maana hakufikiria kama mumewe wa ndoa angemfanyia hivyo.

Bahati alienda hadi hoteli aliyoambiwa na Erica, akamuulizia na kupelekwa alipowekwa kuosha vyombo ila vyombo vyenyewe aliosha vichache sababu ya kulia, Bahati akauliza kwanini Erica kafanyiwa vile,
“Huyu mwanamke kaja na mwanaume wameagiza chakula mwanaume kamkimbia, hana hela ya kulipa ndio tukampa kazi ya kuosha vyombo”
“Kwani mnamdai pesa ngapi?”
“Elfu ishirini na tano”
Bahati akatoa zile hela na kumuinua Erica aliyekuwa amekaa chini sababu ya kilio na kwenda nae nje kupanda gari yake kisha akampeleka moja kwa moja kwao, walipofika aliingia nae ndani na kwenda kugonga mlango wa nyumbani kwao maana ilikuwa mapema sana, saa kumi na mbili kasoro, mamake alitoka ila alichukia sana kuona Erica kaletwa na Bahati ila kabla hajasema chochote Erica alianguka miguuni pake.


Bahati akatoa zile hela na kumuinua Erica aliyekuwa amekaa chini sababu ya kilio na kwenda nae nje kupanda gari yake kisha akampeleka moja kwa moja kwao, walipofika aliingia nae ndani na kwenda kugonga mlango wa nyumbani kwao maana ilikuwa mapema sana, saa kumi na mbili kasoro, mamake alitoka ila alichukia sana kuona Erica kaletwa na Bahati ila kabla hajasema chochote Erica alianguka miguuni pake.
Ilibidi mama Erica ainame na kumuokota mwanae alikuwa kazimia, ni sababu ya kulia sana, huyu mama alimfokea sana Bahati,
“Umemfanya nini mwanangu wewe?”
“Sijamfanya chochote mama”
Mamake Erica alikuwa akihangaika na Erica pale ila Bahati alipotaka kusaidia alimtimua kabisa na kumwambia aondoke, hataki kumuona, ila bahati aliganda tu pale, wakati mama Erica akihangaika na Erica Bahati alienda kuchukua chupa ya maji kwenye gari yake na kummwagia Erica, akazinduka lakini alionekana kuwa na uchovu sana, mamake alimuuliza kama wampeleke hospitali ila Erica aligoma na kusema akalale tu, mamake akamshauri jambo moja kuwa kabla ya kwenda kulala akaoge kwanza, basi Erica alikuwa akijikongoja tu ikabidi mamake ampeleke na kummwagia maji kisha ndio akampeleka kulala. Muda huo wote Bahati alikuwepo tu sebleni. Mama Erica akarudi sebleni na kumwambia Bahati,
“Nashukuru sana kijana kwa kuniletea maradhi yangu ila nakuomba uondoke maana mwanangu sasa yupo kwenye mikono salama”
Bahati hakuwa na usemi na wala hakuweza kubishana na mama yake Erica, hivyo aliamua kutoka zake na kuondoka.
Mama Erica alibaki na maswali sana kuhusu kilichompata mwanae yani hakuelewa kabisa ila alimwacha apumzike kwanza kama mwenyewe alivyoomba kuwa apumzike kwanza.

Muda kidogo Bahati alirudi tena akiwa kabeba samaki na kuku wawili na kumwambia mamake Erica,
“Mama nimekuja kidogo kuleta hii ili Erica atengenezewe supu, samahani mama”
Kisha akaacha pale na kuondoka zake, kwa upande mwingine hata mamake Erica alimuhurumia ila tu ndio alishaoa. Akaamua kuandaa ile mboga kwaajili ya mwanae akiamka.
Kwenye mida ya mchana mama Erica alienda kumuamsha mwanae maana kila muda alikuwa akimchungulia ila akaona ni vyema muda huo amuamshe tu, Erica aliamka ila mwili wake ulikuwa umechoka sana, mamake akampa ushauri,
“Nenda kaoge mwanangu upate nguvu, sijui nini kimekukuta, sijui nini kimekukumba lakini najisikia imani, nenda kaoge tena upate nguvu mwanangu”
Erica alinyanyuka na kwenda tena kuoga kisha mamake akaenda nae mezani na kumuwekea supu na chakula ili ale, na kweli alikula kamavile hajawahi kula chakula, mama yake alikuwa akimuangalia tu mwanae anavyofakamia chakula, alipomaliza alikuwa na nguvu sasa, mama yake alikaa nae na kuzungumza nae,
“Eeeeh mwenzetu, kimekusibu kipi?”
Erica alitoa tena machozi ila mama yake alimbembeleza na kumwambia kuwa amwambie ukweli wote ilivyokuwa,
“Mama, jana niliamua kumueleza ukweli Erick kwamba mtoto nimezaa na Rahim, kumbe Erick na Rahim wanafahamiana, huwezi amini mama Erick amechukia sana na amediriki hadi kuniacha hotelini ikiwa bado hajalipia chakula”
“Sikuelewi mwanangu, hebu nieleweshe”
Erica akamueleza mama yake alichofanyiwa hotelini, jinsi walivyomuoshesha vyombo na jinsi alivyowasiliana na Bahati kwenda kumchukua,
“Hivi ni ya kweli hayo? Yani Erick akuache wewe!”
“Kweli mama, tena bora angeniacha sehemu nzuri kuliko kunidhalilisha vile”
“Amakweli mapenzi hayana dhamana, kila siku nakwambia mwanaume sio ndugu yako ila hunielewi mwanangu, na leo nakuongezea lingine, mapenzi hayana dhamana, usimuamini mtu kupitiliza kwani mtu anaweza kukugeuka kwa muda mfupi tu na usijielewe, mapenzi ni kitu kingine kabisa”
“Ila mama nakumbuka uliniambia ukweli humuweka mtu huru, ukweli ndio mzuri ila mbona mimi nimepata majanga kwa kusema ukweli?”
“Erica mwanangu, nishawahi kukwambia unaposema ukweli angalia ni ukweli kuhusu nini na mazingira gani unasema huo ukweli, yani ukweli mwingine kabla hujasema jifikirire kwanza wewe ukiwa Yule mtu utachukua maamuzi gani, je ulikuwa unajua kama Rahim na Erick wanafahamiana?”
“Nilikuwa sijui mama ila nikajua siku ile uwanja wa ndege maana niliwaona wote nikajificha”
“Je ulimuuliza Erick kuwa anafahamiana vipi na Rahim?”
“Nilimuuliza mama na akasema ni rafiki yake”
“Ooooh kama ni rafiki yake basi kuna siri nyingi sana wanafichiana, sasa mwanangu kwa mazingira hayo ungeniambia hata mimi nimwambie huyo Erick ukweli hata kama kupaniki angepanikia hapa nyumbani kuliko kukudhalilisha hivyo mwanangu, kuna watu sio waelewa yani huyu Erick anafanya nae nianze kumchukia loh!”
“Ndio hivyo mama, mwanao nimedhalilika sana ten asana, kwakweli alichonifanyia Erick siwezi kukisahau”
“Basi mwanangu tulia yaishe”
Basi mama Erica akachukua simu yake na kujaribu kumpigia Erick ila iliita tu bila ya kupokelewa , kwahiyo akahisi huenda ana mambo yake ndiomana hata simu yake hapokei, basi yeye akaendelea tu kuongea na mwanae na kumpa nguvu.
 
Back
Top Bottom