Simulizi: Nini maana ya mapenzi

Simulizi: Nini maana ya mapenzi

SEHEMU YA 394


Mara mdogo wake Dora alitoka kwenye chumba cha Sia na kusogea karibu kisha kumkumbatia Sia na kumwambia dada yake,
“Wewe ondoka zako tu maana mimi kwa Sia ndio nimefika”
Kisha akambusu Sia, haya mambo yote Tumaini aliyaona na kuyasikia kwakweli yalimstaajabisha sana.
Tumaini hakuamini kile kitu na kujihisi kama yupo ndotoni, aliamua kujitokeza katikati yao, kitendo kile cha Sia kumuona Tumaini mbele yao akamsukumiza Steve, kile kitu kilimsikitisha zaidi Tumaini na kusema,
“Sia hata usingemsukumiza huyo maana nimesikia kila kitu, ila mpaka muda huu nashindwa kuamini, hivi si ni wewe Sia uliyekunywa sumu kwaajili ya kaka yangu? Inamaana ulikuwa unaigiza kunywa sumu? Upendo uliousema unao dhidi ya kaka yangu uko wapi?”
Sia alianza kujitetea kwa kuomba msamaha
“Nisamehe Tumaini, mimi ni mwanamke mwenzio”
“Hebu nitolee ujinga mie, mwanmke mwenzangu kwenye mambo ya kijinga kama hivi! Nilikuwa nakuamini sana ila imani yangu umeipoteza.”
Dora alikuwa anaangalia tu na kushangaa aliyechukuliwa dawa alikuwa ni kaka wa Tumaini, sababu hakutaka umbea umpite akauliza,
“Huyo kaka yako ni nani Tumaini? Namfahamu?”
“Utakuwa unamfahamu ndio, anaitwa Erick”
“Kheee kumbe ni Yule Erick mpenzi wa Erica?”
“Ndio huyo huyo”
“Kheee kumbe Sia nilikubali kukupeleka kwa mganga ukamroge shemeji yangu jamani!”
Tumaini aliposikia kuwa Dora ndiye aliyempeleka Sia kwa mganga ndio akafunguka macho kabisa na kusema,
“Kumbe ni kweli alienda kwa mganga?”
“Ndio ni kweli, na bahati mbaya kakako hakula lile tunda ndio likaliwa na huyo mdogo wangu hapo ambaye hasikii kwasasa wala haoni anadai anampenda tu Sian a hakubali kuwa amerogwa”
Na kweli ingawa Steve alisukumiwa pembeni ila kusikia ile mada ya kurogwa alisogea karibu na Sian a kusema,
“Mimi sijarogwa, ni mapenzi yangu. Nampenda sana huyu mwanamke toka moyoni na ndio nitamuoa na atakuwa mke wangu daima”
Kwakweli Tumaini alizidi kushangaa sana yani alijikuta akimchukia Sia gafla maana hakutegemea kuwa Sia angeweza kwenda kwa mganga kwaajili ya kumroga Erick, kwahiyo kwa yale maneno ilikuwa kama ni uthibitisho. Alisikitika sana na kusema,
“Yani kwa ulichofanya leo Sia, sitaki tena kukuona kwetu. Sitaki tena urafiki na wewe”
“Wananisingizia Tumaini”
Tumaini hakutaka kumsikiliza Sia kwakweli maana alichokisikia hakupenda hata kidogo, moja kwa moja aliondoka. Na aliamua kwenda kwa mama yake ili amsimulie kidogo ndio aende kwao maana alihisi akili yake kutokuwa sawa kabisa.
Alifika na kumkuta mama yake, akamsalimia na kuanza kumsimulia yaliyotokea siku hiyo,
“Unaona sasa mwanangu, unagombana na kaka yako sababu ya mwanamke mshirikina. Huyo hakuwa anampenda kaka yako wala nini maana kama kumpenda asingemuendea kwa mganga maana kama mtu unampenda kweli hutotoka kumsumbua kwa madawa, utapenda akupende ule upendo halisia, na ule upendo halisia ni mzuri sana maana unajisikia kuwa unapendwa yani hata wewe unajihisi raha”
“Ila mama huyo msichana alikunywa hadi sumu sababu ya Erick”
“Hakumpenda Erick huyo mwanangu, na labda alikunywa sumu kuwapima imani tu, huyo kuna kitu alihitaji kwa Erick ndiomana kaweza kumwendea hadi kwa mganga, tena shukuru Mungu umegundua mapema kabla hajawa wifi yako maana ungejuta huyo, angefanya uone maisha machungu maana angemfanya kaka yako ndondocha yani kila ambacho ungemwambia asingekuelewa sababu yake. Mwanangu hakuna upendo mzuri kama upendo halisia, hakika hata mimi ningeangalia upendo halisia basi nisingezaa na baba yako ila hela zake zilinichanganya sana na kuhisi kuwa ananipenda na kuhisi nitaishi kama malkia kwenye himaya yake, kumbe hakuwa na upendo na mimi hata kidogo na nilimgundua baada ya kuzaa tu”
“Mmmh mama, hivi baba anampenda nani? Maana toka nikae nae sijawahi msikia akitaka kuoa wala akisema labda nimuoe mama yake Erick maana Yule mama nae anaishi mwenyewe”
“Yule baba yenu nadhani hajielewi, yupo yupo tu. Nilijua angenioa wapi, nimezaa ndio akanipiga teke kabisa, basi mama Erick nilijua atamuoa wapi, ndio kwanza amezaa nasikia hata hospitali hakwenda kumchukua yani Yule mwanamke kahudumiwa na mdogo wake mwanzo mwisho ndiomana anamthamini sana mdogo wake, Yule mzee ana wazimu Yule mpaka leo yupo yupo tu ila nasikia ana wanawake wengi balaa”
“Ila hajawahi kuwaleta nyumbani mama, baba yetu anajiheshimu”
“Angejiheshimu angeoa, pesa anayo, mali anayo, kitu gani kinamshinda asioe? Kaeni vizuri na baba yenu muulizeni vizuri kuwa kwanini haoi?”
“Sawa mama”
Tumaini aliongea ongea pale na mama yake kisha akajiandaa kurudi kwao tu maana siku hiyo alikuwa amechefuka haswaa na yale aliyoyaona kwa Sia.

Dora alimuangalia Sia bila kummaliza maana alijilaumu sana kumpeleka Sia kwa mganga kwanza kumbe ilikuwa ni kuharibu mahusiano ya rafiki yake na pia imepelekea kuharibu akili ya mdogo wake, kisha akaanza kumwambia,
“Hivi wewe Sia aliyekwambia kwamba penzi linatafutwa kwa dawa nani?”
“Na wewe hebu ukae kimya huko, kumbuka ni wewe mwenyewe ndio ulinipeleka kwa Yule mganga. Kama penzi halinunuliwi kwa mganga na wewe ulienda kufanya dawa upendwe ili iweje? Mimi bila kujua kama kuna dawa uliifanya ya kupendwa na wewe mwenyewe kunipa ushuhuda ningejuaje kama kwa mganga kuna dawa ya mapenzi? Unaponisema mimi nijiangalie na wewe kungwi”
“Sikatai ni kweli nilienda kwa mganga ila lengo langu na lako halifanani, niliamua kumfanyia James dawa sababu nilipanga kumkomesha na nilifanya vile sio sababu nilikuwa nampenda hapana, nilitaka kumchuna tu pesa zake. Sasa wewe shoga yangu kumfanyia dawa mwanaume ili akupende ni vipi hapo? Hivi unajisikiaje ukipendwa na mwanaume kwa upendo wa dawa? Inanoga kweli?”
“Bhana eeeh achana na mimi”
“Niachane na wewe kitu gani? Mdogo wangu akomboke huyu, uende kwenye maombi”
“Siendi popote, achana na mimi kwanza wewe ni mbaya sana ushanipotezea laki moja yangu jumlisha na zile hasara za nauli na chakula kwenda huko Bagamoyo ndani ndani, wala sijapenda kabisa, naomba tu uende”
“Siwezi kwenda na kumuacha mdogo wangu”
“Si umchukue, huyo hapo mchukue kama mtoto mdogo mbebe mgongoni”
Kiukweli Dora alichukia sana kama angeweza kupigana na huyu Sia kwa hakika angepigana nae ila uwezo wa kupigana na huyu Sia hakuwa nao kwani alionekana kuwa na nguvu kushinda yeye na ndiomana hata Tumaini hakuweza kumzaba vibao Sia maana amehisi kuwa pengine angepigwa yeye ndiomana alijiondokea tu.
Basi Dora akamwambia,
“Sia, subiri tu nione hivi hivi nilivyo ila hiko ulichomfanyia mdogo wangu utalipia nakwambia yani utalipia, nimeachana na mambo ya waganga ila naweza kurudi tena sababu yako kwaheri”
Dora aliondoka pale na hata mdogo wake hakujigusa kumuuliza kuwa mbona anaondoka akiwa amechukia vilke kwani yeye alijionea kawaida tu.
Dora akiwa njiani huku ananung’unika mwenyewe, kuna gari ilipaki karibu yake, kisha Yule wa kwenye gari alishusha kioo, basi Dora akamuangalia akakuta ni George akafurahi sana na kwenda kupanda kwenye gari ya George huku akimsalimia.
“Mmmh za siku George, inaonekana maisha yako mazuri siku hizi eeeh!”
“Kiasi chake kwakweli namshukuru Mungu, twende nikupeleke kwangu”
“Twende tu”
Kwa muda huo hata hakufikiria kuwa muda umeenda na anataka kurudi kwao ila aliondoka na George tu.
 
SEHEMU YA 395

Tumaini alifika nyumbani kwao ilikuwa ni kwenye mida ya saa tatu usiku, alipoingia getini alimuuliza mlinzi wao,
“Vipi Erick na Yule msichana wake wameondoka?”
“Ndio wameshaondoka”
“Na lile gari pale la nani?”
“Lile gari la mzee”
“Kheee leo kaja mapema hivyo?”
“Tena karudi toka saa kumi na mbili jioni, muda ule ule walipoondoka wakina Erick tu basin a yeye akaingia”
“Kwahiyo hajawakuta”
“Ndio hajawakuta”
Basi Tumaini akaachana na Yule mlinzi na kuingia ndani kwao, yani ni kweli baba yake alikuwa na magari mengi tu ambayo si yote alikuwa ameyakariri ila ile kumwambia baba yake kuwa anauhitaji na gari alishindwa kwani hakumzoea na vile vile toka wanakaa nae hapo, basi kuonana nae ni kwa nadra sana.
Aliingia ndani kwao, na kwa mara ya kwanza alimkuta baba yake sebleni akiangalia taarifa ya habari, Tumaini akamsalimia baba yake,
“Najua umenimiss mwanangu, karibu karibu tuongee”
Tumaini akasogea karibu na baba yake,
“Kaka yako yuko wapi?”
“Sijui ila nilimuacha, nadhani katoka, na leo mbona umerudi mapema?”
“Jamani kuna muda nakaa naikumbuka familia yangu mwanangu, ila leo niliwahi kwa lengo la kuwakuta wanangu nyumbani maana kuna habari nataka niwape”
“Habari gani hiyo baba?”
“Sasa ni vyema nikaongea nanyi mwenzio akirudi, basi asubuhi mwambie asitoke ili niongee nanyi sawa!”
“Sawa baba”
Tumaini akajikuta ana hamu sana ya kujua ni kitu gani ambacho baba yao anapanga kuongea nao, kitendo hiko kilimfanya alivyoenda chumbani kumpigia simu Erick kuwa baba yao anawahitaji nyumbani na anataka kuongea nao.

Basi George alifika na Dora nyumbani kwake na kumkaribisha ndani, kwakweli dora aliona jinsi gani George alivyojipanga akamsifia sana na kumuuliza,
“Hivi George bado tu hujaoa? Au bado unatafuta bikra?”
“Nyie wanawake mnbajielewa basi! Nilipenda sana nioe mke ambaye hajawahi kupitiwa na mwanaume yeyote yani mimi niwe mwanaume wake wa kwanza”
“Mwanamke awe hajawahi kupitiwa na yeyote ila wewe umepitia kibao hatusemi, huoni kama unachofanya sio sawa? Ila hata hivyo mabikra wapo bhana, tuseme hujawapata tu! Nyumba kama hii inatakiwa awepo mwanamke ndani, umerudio kutoka kazini kama hivi akupikie na kukupetipeti”
“Aaaah mabikra kweli wapo ila wengine wana bikra feki yani wenye bikra halisi hawajulikani karne hii, nilimpata mwanamke bhana akasema yeye ni bikra tukaja nae ndani uwiiii anajua kila kitu, jamani bikra gani anayajua mapenzi kiasi kile! Nikasema hapana hapa nauziwa mbuzi kwenye gunia”
“Kwani damu haikutoka?”
“Ilitoka ila Yule nadhani alikuwa muigizaji, nikajaribu kuangalia wa vijijini ni washamba hatari na mwingine anakwambia ni bikra ila anasema msifanye hadi ndoa, sasa mtu wa namna hiyo wa nini? Nitajuaje kama bikra kweli? Naamua kumbwaga tu, ila kwasasa wala sitaki cha bikra wala nini namtaka mwenye mapenzi ya dhati”
“Basi nipo mimi George jamani, au mimi umenisahau?”
“Wewe Dora nae loh! Wewe ni hawara yangu jamani”
“Ndio mimi ni hawara yako ndiomana huwa sina wivu na wewe na hata hivyo mahawara huwa hawaachani. Umesikia wapi mahawara wanaachana? Kwanza leo nafurahi sana nimekutana na wewe, nafurahi sana nimefika kwako, sasa unafikiri leo naondoka?”
“Kheee kwahiyo huondoki?”
“Siondoki ndio, huna mke halafu mimi niondoke kwa lipi na umewahi kuwa hawara yangu. Yani leo ndio nipo nawe hadi asubuhi nami nifaidi matunda yako ya mafanikio”
George alihisi furaha sana na aliona amepata haswaa yani alijiona ni mshindi kupita njia na kuonana na Dora, kwahiyo hakupinga zaidi zaidi kumfanya Dora kama mke kwa muda huo.

Erick alikuwa amemrudisha Erica nyumbani kwao ila kwa muda huo wakati anaaga kuwa anaondoka, Bite alitamani sana kumuuliza kuhusu zile hela ila mama Erica alimkatisha kwani alihisi kama ni swala la kujiaibisha kuhisi kuwa Erick anaweza kuchukua hela kama ile wakati ana hela nyingi tu, basi Erick aliaga na kuondoka zake.
Alifika nyumbani kwao ilikuwa saa tano usiku, na dada yake akamwambia azma ya baba yake ya kutaka kuongea nao asubuhi kwahiyo dada yake alimwambia kuwa asiondoke mapemaili asubuhi waweze kuongea na baba yao.
Basi Erick alikubali na kwenda zake kulala tu maana siku hiyo alikula kwakina Erica kwahiyo hakuwa na sababu tena ya kula, zaidi ya kuoga na kwenda kulala tu, ila alipigiwa simu na Sian a hakupokea ile simu kwani alikuwa na hisia mbaya na Sia huenda akaweka hata dawa kwenye simu ashangae akiongea nae tu aanze tena kumfatilia wakati kashaamua moyo wake kuwa kwa Erica.
Kulipokucha aliamka na kujiandaa kisha alienda kukaa sebleni ili kumsubiri baba yao, ambapo Tumaini nae alienda kukaa sebleni na muda kidogo baba yao alitoka ndani na kuanza kuongea na watoto wake, walimsalimia na akaanza kuwaeleza lengo lake,
“Nadhani Erick nishawahi kukugusia kuhusu swala hili, ni hivi nahitaji kuoa”
Tumaini akashangaa na kumuuliza baba yake kwa mshangao,
“Kuoa baba”
“Ndio, nahitaji kuoa. Katika maisha yangu sijawahi kuoa yani sijawahi kuwa na mke kabisa, ila kwasasa nimeona ni bora nioe yani kuwe na mama yenu hapa nyumbani ili baba yenu na mie niwe narudi nyumbani mapema, nashinda nyumbani kama baba wengine wenye familia, naomba mniunge mkono kwa hili wanangu”
Erick akamwambia baba yangu,
“Kwa upande wangu mimi sioni kama ni tatizo tena naona umefanya maamuzi ya maana sana baba maana sijawahi kuona au kusikia mahali kuwa baba uliwahi kuoa au kuwa na mke. Na sisi kwetu ni faraja sana kuona baba ukipata mke wa kukuhudumia na kukutunza. Au unasemaje Tumaini”
“Hata mimi naona ni sawa kabisa, ila swali ni kuwa huyo mama yetu ni nani? Na hiyo harusi ni lini?”
“Swala la mama yenu ni nani subiri tu mtamjua, maana kuna maswala nilikuwa nakamilisha na yashakamilika ila hivi karibuni nimepanga kwenda kutoa mahali kwa huyo mama yenu yani mwezi huu haupiti basi mtasherekea harusi yangu, na Erick si ulisema unataka kuoa eeeh!”
“Ndio baba nataka kuoa”
“Basi hakuna tatizo, baada ya harusi yangu ndio wewe pia utaanza mipango ya harusi yako tena nitaisimamia kila kitu maana harusi yangu nataka iwe ya kawaida tu ila harusi yako, nitagharamia sherehe yote mwanangu, kipindi hiko nipo na mama yenu yani ni furaha tele”
Wote wakafurahia haswaa Erick maana aliona ni jambo la kuvutia sana kwake kuambiwa na baba yake kuwa atagharamia shughuli yote ya harusi yake, hivyo akaombea tu harusi ya baba yake ipite salama ili yake ifanyike pia.
“Baba, mzee wangu yani mimi natoa heri zote za wewe kumpata mama yetu maana ni furaha kwetu pia. Natumaini hiyo Jumamosi itakuwa kweli na tutaenda wote ili tumfahamu na mama yetu”
“Yani msijali wanangu, maandalizi yapo vizuri kabisa, siku hiyo tutaondoka hapa pamoja kwenda kumaliza kila kitu ila ninachowaomba watoto wangu tutakapofika kwa huyo mama yenu mumpende na akifika hapa nyumbani mmuheshimu, baba yenu nimechelewa kuoa sababu katika maisha yangu sijawahi kumpata mwanamke nikampenda, huyu niliyempata sasa ni mwanamke wa kwanza kupendwa na mimi kwahiyo lazima nimuoe”
Tumaini akamuuliza baba yake,
“Je na yeye anakupenda?”
“Mwanangu Tumaini hivi unaendaga kanisani kufanya nini na maandiko huyajui? Je maandiko unayasoma vizuri kweli? Unayajua vizuri maandiko? Imeandikwa enyi wake watiini waume zenu nanyi wanaume wapendeni wake zenu, kwahiyo swala la kupenda ni swala la mwanaume yani limeandikwa kabisa kuwa mwanaume lazima apende kwa maana nyingine mwanaume anatakiwa aoe anachokipenda ila mwanamke hakuna tatizo maana mwanamke anajifunza kupenda yani mwanamke anaendana mazingira yanapompeleka, yakimpeleka kwa A basi atampenda A yakimpeleka kwa B vivyo hivyo, yani mwanamke anajifunza kupenda ila mwanaume ndio haswaa anayejua kupenda”
“Ila baba mbona wanasema mwanamke akikupenda ndio kakupenda kweli”
“Sababu mwanamke anajifunza kupenda kwahiyo kitu cha kujifunza lazima uwe nacho makini na ndiomana utakuta unamtongoza mwanamke ila anakukataa kataa ila cha kushangaza badae weee anakupenda kufa maana kashajifunza kwahiyo swala la mama yenu kunipenda au kutokunipenda lisiwape shida maana atajifunza kunipenda ndani ya ndoa na nitamfanyia kila kitu cha kumfanya anipende maana wanaume tunajukumu la kuwafanya wanawake watupende kwa kuwaonyesha upendo”
“Mmmh baba umenifungua”
“Ndivyo ilivyo hiyo yani usishangae kuona mwanamke alimkataa mwanaume ila alipomkubali na kuwa nae akampenda sana, au anaweza kumkataa ila kila yule mwanaume anavyomfatilia ndio yeye anapojifunza kumpenda mwanaume yule na kumkubali, maandiko yanasema enyi wanaume ishini na wake zenu kwa akili unafikiri ni akili gani hapo tunaambiwa? Ni akili ya kumfundisha mwanamke upendo maana akikupenda hawezi kukufanyia mambo ya ajabu ila ukikosa akili ya kumfanya mwanamke akupende hata usijisumbue kumuoa maana kuna siku atakuwekea sumu ya panya huyo ufe”
“Kwahiyo baba una uhakika huyo mwanamke atakupenda?”
“Jamani tumeandikiwa upendo yani lazima atanipenda, mbona nyie watoto mnakuwa watata hivyo? Tumaini vipi, hutaki nioe mama?”
“Hapana baba, nilikuwa nauliza tu”
“Au umeshangaa vile nilivyoweza kukuchambulia maandiko wakati siendagi kanisani? Enzi zangu za ujana wangu nilikuwa naenda kanisani, kuna mwanamke mmoja nilimpenda sana alikuwa mlokole, aaah habari hiyo nitawaeleza siku nyingine ila kwasasa tuwe makini tu na maandalizi ya harusi yangu”
Kisha akainuka na kuwaaga watoto wake na kuondoka kwenda kwenye shughuli zake. Walibaki ndani Tumaini na kaka yake ambapo naye Erick alikuwa akijiandaa kutoka ila Tumaini akamwambia kidogo kuhusu baba yao.,
“Unajua Erick leo nimemshangaa baba jamani, loh hata yeye maandiko anayajua makubwa haya”
“Kwani hujawahi kusikia kuwa hadi shetani anayajua maandiko”
“Kwahiyo baba ni shetani?”
“Sina maana hiyo ila ni kitu cha kushangaza jamani, hakuna dini anayoudhuria, hakuna kipindi cha dini anachoenda ila anatuambia habari za maandiko loh! Nimesema hivyo kama mfano tu”
“Sawa lakini, kheee imeshangaza yani baba anajua maandiko loh!”
Basi wakacheka tu pale kisha Erick kutaka kuondoka ila kabla hajatoka Tumaini akamsimamisha na kumwambia,
“Ila Erick mdogo wangu hebu nionee huruma dada yako eeeh! Nakaa tu nyumbani natia huruma haswaaa yani siendi kwenye shughuli ndiomana Napata na muda wa kuanza kufatilia mambo yasiyonihusu, nirudishe dukani jamani mdogo wangu eeeh!”
“Sawa, nenda kafungue duka ila sijakurudisha rasmi maana lile duka ni la Erica, wewe nenda kafungue tu halafu tutajua cha kufanya mbele ya safari”
“Sawa, nashukuru kwa hilo. Haya mdogo wangu na usafiri je! Unajua na mimi natamani kuendesha gari, nimechoka kutembea”
“Subiri, kuna gari ya baba ipo tu gereji imepaki najua vitu vingi vya baba huvijui sababu hutaki kujua basi hiyo gari italetwa leo jioni hapa nyumbani maana funguo ninazo mimi”
“Asante sana mdogo wangu”
Basi Erick akatoka na kumfanya Tumaini ajisikie vizuri na kuona pengine siku hiyo kaongea na kaka yake kwa upendo ndiomana kaka yake amemsikiliza tofauti na siku zingine.
 
SEHEMU YA 396


Dora aliamka nyumbani kwa George na kujiandaa kwaajili ya kurudi kwao, kwahiyo wakati George anaenda kazini akampitisha nay eye stendi na kumshusha, kisha Dora akamwambia,
“Ila George wewe mbahili loh! Nilijua umejifunza siku hizi kumbe huna lolote, mwanaume mbahili wewe, yani umeendelea siku hizi ila wapi ubahili tu hata kusema hela hii ya nauli hakuna! Mmmh George mbahili sana wewe”
Ila ndio kwanza George alisimamisha gari ili Dora ashuke tu basi Dora akashuka na kupanda daladala ya kurudi kwao huku akijisemea mwenyewe,
“Yani na Yule nimemkomesha, na nitamkomesha hadi naye apate ukimwi nilioupata mimi maana anajishauwa mtu gani hadi leo hajaoa eti anatafuta bikra, sasa sijui kama kuna bikra atamkubali na ukimwi wake. Kwanza janaume bahili kweli, sasa ukimwi utamkomesha mjinga Yule”
Kisha akaendelea na safari hadi kwao ambapo alimkuta mama yake akilalamika na malalamiko yale yale kuwa watoto wake wamebadilika,
“Dora, ulianza wewe kulala nje kwahiyo mdogo wako analala nje hata hushtuki jamani mnataka kunifanya nini mama yenu jamani? Watoto wenyewe ndio nyie wawili tu kwanini mnanifanyia hivi!”
“Mama, utanilaumu bure tu ila mimi nimekwambia kuhusu Steve twende kwenye maombi”
“Maombi gani nitakayoenda na wewe, hivi ni Mungu yupi atakayesikilkiza maombi yako wewe binti mchafu!”
“Maneno yako hayo mama ndio yanayofanya hata nisijirekebishe ujue, wewe ni mama yangu, niweke mwanao kwenye mstari, ni wewe ambaye hukunilea vyema, hivi mfano ungenifundisha kuishi katika misingi ya dini ningeacha si ingekuwa uzembe wangu mwenyewe? Ila mama hakuna ulichojaribu kwangu na Steve halafu unalalamika, nakwambia kuwa swala la Steve ni la kwenda kwenye maombi unasema hakuna Mungu wa kunisikiliza mimi. Yule mwanamaombi alinifundisha vizuri sana kuna mwanamke kahaba ila alilia miguuni pa Yesu na akasamehewa sembuse mimi! Jamani mama laiti ungejua kuwa wewe ndio unazidi kunipotosha mimi hata usingesema”
“Hebu nitolee ujinga wako hapa, unaanza hadi kujifananisha na makahaba kama na wewe sio kahaba ni nini! Kwani wewe na huyo mwanamke mnatofauti gani? Mtoto kama sijakuzaa mimi, yani hapo ulipo unanuka dhambi tu”
“Kheri mimi nanuka dhambi lakini nina hela”
“Yani unaongea kama binti ambaye hakusoma, jamani Dora umefika chuo wewe! Unaongea utumbo tu”
“Ni kweli nimefika chuo ila kumbuka kwenye elimu yangu kila hitaji nililokwambia ulisema nijiongeze, hivi mama ulitaka mwanao niwe vipi? Ndio nikajiongeza hivi”
“Unajua usiniambie hivyo mama yako mimi, nitakupiga ujue!”
Dora akaachana na mama yake ukizingatia alishachoka muda huo aliamua tu kwenda chumbani kwake kujilaza.

Siku hiyo Erica akiwa nyumbani kwao kwenye mida ya jioni jioni alienda Erick kama kawaida kumsalimia na kuangalia kama anaendeleaje maana ingawa alishampeleka kule kwenye duka ila hakutaka aanze kwa kipindi hiko mpaka awe sawa kabisa kwahiyo Erica alikuwa tu nyumbani ila huku ana uhakika na kile kinachoendelea juu yake.
Kwahiyo Erick alivyofika walitandika mkeka nje na kukaa huku wakizungumza mambo yao mbalimbali.
Basi Erick aliongea ongea nae pale na alimueleza pia lengo la baba yake kutaka kuoa,
“Hivi kwani baba yenu hajawahi kuoa?”
“Hajawahi hata mara moja mwenyewe anadai hakumpata mwanamke ampendaye ila sasa kapata ampendaye ndio anataka kuoa na ameniahidi kuwa baada ya harusi yake ndio atashughulikia yangu”
“Kwahiyo mimi na wewe Erick tutaoana mwaka huu huu!”
“Ndio mwaka huu tunaoana Erica”
Kwakweli Erica alifurahi sana kusikia vile kwani ndoto yake siku zote ni kuolewa tena kuolewa na mwanaume ampendaye kama Erick kwahiyo ilikuwa ni furaha sana kwake.
Basi baada ya maongezi yale ndipo Erick alipotaka kuondoka ila Erica alitaka ale kwanza,
“Hapana Erica, leo nahitaji twende restaurant tukale. Basi twende ukaage tu tuondoke muda huu”
“Ila mama hayupo, yupo dada Bite tu”
“Si ndio vizuri lakini maana mama nae akiwepo kutoa ruhusa ni balaa”
Basi Erica akacheka tu na kuinuka pale kutoa mkeka kupeleka ndani na kumuaga dada yake kuwa anatoka kidogo na Erick kisha yeye na Erick wakaondoka zao.
Pale nyumbani alibaki Bite akiendelea na kazi zake zingine, muda kidogo akaja mgeni na kugonga ikabidi Bite afungue, mgeni huyu alikuwa ni mtu mzima wa makamo halafu kaongozana na vijana wawili basi akawakaribisha na kuwauliza maana alikuwa akiwashangaa basi Yule mzee alijitambulisha,
“Naitwa mzee Jimmy”
“Kheee kumbe mzee Jimmy mwenyewe ndio wewe!”
“Ndio ni mimi, niliacha milioni tatu za posa ya Erica, niliacha na karatasi ndani kuonyesha nampenda Erica na leo nimekuja”
Bite akataka kuongea jambo ila huyu mzee alimzuia na kuendelea kusema,
“Leo nimeleta hii milioni moja ya chakula siku ambayo nakuja kutoa mahali na kumchukua mke wangu, jiandaeni na msifikirie kunifanyia ujinga kama mnaonifanyiaga maana posa yangu mmepokea kwahiyo mke wangu nakuja kumchukua, sitaki useme neno lolote kwasasa. Jua kwamba jumamosi nakuja kumchukua mke wangu”
“Kwahiyo kesho”
“Ndio, mjiandae yani kesho mapema kabisa nakuja kuchukua mke wangu”
Kisha Yule mzee na wale vijana wakaondoka, Bite alibaki tu kaduwaa na zile pesa mkononi maana hakujua hata anaanzia wapi na kuishia wapi na kuzirudisha kwa Yule mzee hakuweza maana alimuwekea vitisho.
Basi mama yake aliporudi alimpa zile pesa, ila alizipokea na kumuulizia Erica kwanza
“Erica yuko wapi?”
“Katoka na Erick mama”
“Yani huyu mtoto akipumzika siku mbili basi siku ya tatu lazima atatoka na Erick, kwahiyo hizi hela ni Erick kazileta?”
Basi bite akamueleza mama yake jinsi zile hela zilivyoletwa, yani mama Erica alizitupa zile hela chini huku akilalamika,
“Hizi hela ni hela za moto jamani, huyo mzee anatutakia nini jamani!”
“Mama nilisema Erick aulizwe kuhusu hiyo milioni tatu ila hajaulizwa hadi leo na habari ya hela jamani tutajuta humu ndani, na hivyo kesho ndio kasema anakuja kutoa mahali na kumchukua mke wake yani hiyo hela katoa ya chakula eti tusimtie aibu kwa wageni”
“Hivi huyo mzee ana wazimu au kitu gani jamani, ni wapi wanatoaga mahali bila mila za kabila hilo? Anajua kabila letu mila zake? Ni wapi wanatoaga mahali kinyemela hivi? Mbona huyu mzee anataka kulazimisha mambo?”
“Ndio hivyo mama, subiri mwanao Erica afike umueleze habari hizi labda ampigie huyo mzee kumzuia”
“Kheee jamani nimechoka kwakweli yani nimechoka haswaaa”
Basi kwenye mida ya saa nne, Erica alirudi nyumbani na mama yake alimfokea sana kwa kuchelewa kisha akamwambia habari za mzee Jimmy na kumtaka ampigie simu kumsitisha hiko anachotaka kukifanya, ikabidi Erica ampigie simu mzee Jimmy,
“Wewe mzee hivi unataka niongee kwa lugha gani unielewe? Sikutaki, achgana na mimi”
“Hunitaki nini wakati posa yangu nyumbani kwenu mmekula, kesho ndio utajua kama unanitaka au la”
“Sikutaki wewe mzee, achana na maisha yangu”
Erica alikata ile simu kwa hasira na kuamua tu kwenda kulala.
Kulipokucha waliendelea na mambo mengine huku kila mtu akiwa hana habari kwa chochote kile.
Kwenye mida ya mchana mama Erica alimuagiza Erica dukani kwahiyo Erica alitoka kuelekea dukani, wakati anatoka nje ya geti alishangaa kukuta pamepambwa sana kama kuna sherehe vile, aliamua kukimbia ndani kwenda kumuita mama yake.
 
SEHEMU YA 397


Erick, Tumaini na baba yao waliongozana kwenye gari moja wakienda huko kumchukua mke wa baba yao. Walikubali kwenda nae ingawa aliwashtukiza tu maana hakusema kuwa ni siku gani wao wataenda huko kwa mama yao yani mke mtarajiwa wa baba yao, walipokuwa kwenye gari Yule mzee aliwasisitiza wanae,
“Yani kama mkikuta familia ya Yule mwanamke inaleta vurugu msishangae sana ni hawataki mtoto wao nimuoe sijui washachukua mahali za watu wengi wengi ila baba yenu huwa sitaki hela yangu iende bure na mwanamke nampenda. Kwahiyo msishangae”
“Sawa baba”
Safari iliendelea ila Tumaini na Erick walishangaa sana kuona mitaa ambayo wanaelekea ni mitaa ya kwakina Erica ila wakajipa moyo, walifika mahali hapo pamepambwa sana ni vigumu kujua kama ile nyumba huwa wanakuja mara kwa mara, wakashuka huku wakishangaa shangaa, Erick akasema kwa mshangao,
“Jamani hapa si kwakina Erica!”
Tumaini akajibu,
“Ndio, na Erica mwenyewe Yule pale na mama yake”
Erick aliwaangalia huku akiendelea kushangaa.


Safari iliendelea ila Tumaini na Erick walishangaa sana kuona mitaa ambayo wanaelekea ni mitaa ya kwakina Erica ila wakajipa moyo, walifika mahali hapo pamepambwa sana ni vigumu kujua kama ile nyumba huwa wanakuja mara kwa mara, wakashuka huku wakishangaa shangaa, Erick akasema kwa mshangao,
“Jamani hapa si kwakina Erica!”
Tumaini akajibu,
“Ndio, na Erica mwenyewe Yule pale na mama yake”
Erick aliwaangalia huku akiendelea kushangaa.
Kumbe na wao wakina Erica walikuwa wakishangaa pia, Erick alimuacha pale baba yake na dada yake na kwenda alipo Erica na mama yake, bila salamu aliwauliza,
“Kuna nini?”
Wakajibu kwa pamoja,
“Hata sisi tunashangaa”
Erick akatulia kimya akiwaza kuwa mke anayesemwa na baba yake ni yupi kwenye hiyo nyumba, hakupata jibu maana hata wenye nyumba nao walijibu kuwa hawaelewi kinachoendelea, wakati wametulia wakishangaana tu walimuona Mzee Jimmy akiongoza kwa kupita getini kwakina Erica na kuingia ndani huku Dora akimfata nyuma, ilibidi na wao waingie, ila kabla mzee Jimmy hajafungua mlango wa nyumbani kwakina Erica, alisikika mama yake Erica nyuma yake,
“Hivi wewe mzee unataka nini lakini?”
“Nimekuja kumalizia mahari na kumchukua mke wangu”
“Mke wako yupi unayemuona kwenye nyumba yangu?”
“Mke wangu Erica”
Pale Erick na Tumaini walishangaa kabisa kuwa baba yao ni mzima au wazimu umemuingia, kisha mzee Jimmy akageuka nyuma na kumuona Erica na mama yake, akasema,
“Si jana nimeacha pesa hapa jamani, mbona hamjampamba mke wangu?”
Hata Erick alishangaa kusikia kuwa baba yake hadi aliacha pesa ili Erica apambwe, Bite pia alitoka ndani na kushangaa ule mzozo. Kwanza alishangaa kumuona mzee Jimmy, wakati huo huo alishangaa kumuona na Erick. Tumaini akamuuliza baba yake,
“Kwahiyo baba huyo mama yetu unayetaka kumuoa ni Erica?”
“Ndio, kwani mnamfahamu”
Ni pale pale Erick alipomwambia baba yake,
“ Ndio Baba, huyu Erica ndio mwanamke ambaye nilisema kuwa nataka kumuoa”
“Unasemaje wewe!”
“Ndio hivyo baba, nampenda sana Erica”
Cha kushangaza huyu mzee alianguka chini na kuzimia, ilibidi waite vijana waliokuwa wanapamba na kumpakiza baba yao kwenye gari kisha kumuwaisha hospitali maana inaonekana presha ilimpanda mzee Yule.
Kwahiyo pale ilibaki familia ya kina Erica tu yani Erica, mama yao na Bite na vijana wachache waliokuwa wanapamba. Mama Erica aliwatazama wale vijana na kuwaamuru kuwa watandue mapambo waliyoyaweka nje ya nyumba yake, ikabidi wale vijana waende kutandua maana mwenye shughuli ndio Yule alipelekwa hospitali.

Wakina Erica waliingia ndani ila siku ile ilikuwa ni siku ambayo kuna kitendo cha ajabu kimetokea kwenye nyumba yao, walipokaa Bite alimuuliza Erica kwa mshangao,
“Inamaana Yule mzee Jimmy ndio baba yake na Erick?”
“Ndio inavyomaanisha ila nashangaa sana”
“Sasa unashangaa nini? Inamaana kipindi chote hiki hukuwajua wazazi wa Erick? Yani kipindi chote hiki hukumjua hata baba wa Erick?”
“Kweli nilikuwa simjui”
“hata jina Erica? Wewe ni mtu wa aina gani? Hata jina basi la Mzee Jimmy lingekujulisha kuwa huenda ni baba wa Erick”
“Dada, utanilaumu bire lakini mimi sikujua kabisa, na wala sijui yani mpaka muda huu nashangaa tu”
“Ok, tuseme hujui kama ni baba yao haya hata hujui Erick anaitwa Erick nani? Wewe mbona mjinga hivyo eeeh! Hebu ona hii aibu, ingejulikana mapema ungejua namna ya kumpanga Erick ila sio kwa stahili hii”
Erica aliinuka na kwenda chumbani kwake na baada ya muda alirudi na cheti cha kuzaliwa cha Angel kisha akamwambia dada yake,
“Angalia hapo kwenye majina ya Erick kama kuna herufi J au jina Jimmy ndio unilaumu”
Bite aliangalia kile cheti kweli jina la Erick lilikuwepo ila halikuwa na uhusiano wowote na jina Jimmy mahali popote, ila Bite akaanza mada nyingine kwanza,
“Kwani Erick ndio baba wa Angel? Wewe si ulisema baba wa Angel anaitwa Rahim wewe?”
Mama yao akadakia,
“Bite mwanangu, hayo ndio maajabu ya mdogo wako yalivyo. Aliuza mtoto kwa Erick bila hata kufikiria ya mbele wala ya nyuma, halafu Erick nae kwanini hana majina ya baba yake Jimmy? Au nae alinunuliwa kama Angel? Wamama sisi tuna matatizo sana, si ndio mambo ya Angel nayo yatakuwa hivi hivi mnbele ya safari! Haya sasa kumbe Erick baba yake Jimmy na Yule mzee presha imempanda yani sijui kama kuna ndoa hapa kati ya Erick na Erica mmh sijui naona chenga tu.”
“Yani mama kama Yule ni baba yao na hadi kafikia hatua ya kuzimia hivi watoto wataelewa kweli? Hivi Erick anaweza kuacha baba yake awe na hali mbaya sababu ya Erica? Kwanza wewe Erica una akili gani mdogo wangu, toka lini mtoto akauzwa jamani, hivi nani mshauri wako wewe?”
“Mshauri wake ni mapenzi, yani huyu mtoto anaendeshwa na nguvu ya mapenzi, yakimpeleka huku anaenda yakimuhamisha yupo sijui ataishia wapi”
Wote walikuwa wakimsema na alikaa kimya tu kwani bado hakuona kosa lake na alihisi kuonewa tu, Bite akaongezea kwa kumuuliza,
“Hivi Erica hujatembea kweli na Yule mzee? Ameanzaje kuzimia jamani!”
Erica hakujibu ila mama yake akaongea,
“Inawezekana Erica katembea na yule mzee, hivi mwanangu unajisikiaje kuchanganya baba na mtoto? Nafsi yako inajihisi vipi? Ndiomana Rahim alikuwa akikulalamikia unachanganya ukoo, mwanangu nikajua wale wana roho mbaya, sasa umepata mume umeenda kutembea na baba yake”
“Jamani sijawahi kutembea na Yule mzee msinikandamize jamani”
“Wapi wewe, mzee wa watu azimie tu bila sababu. Lazima umetembea nae na umekula vyake vingi sana”
“Inawezekana hata zile hela nilizokuwa nakwambia uzirudishe hkuzirudisha, itakuwa umekula vingi sana vya huyu mzee Erica. Nashangaa mtoto wangu huna hata kinyaa, hivi ulianzaje kutembea na mbaba kama Yule jamani eeeh! Sidhani kama huyo Erick atakupenda tena mwanangu kwa uchafu huo”
Erica aliinama huku akilia kwa uchungu kwani hakutarajia kabisa na ndugu zake kumkandamiza kiasi kile haswaa mama yake.
“Hata ukilia lakini tunakwambia ukweli, tumesomesha ujinga yani wewe badala ya elimu kukutoa ujinga naona imekuongeza ujinga, unakuwaje na mahusiano na mtu hata hujui ndugu zake, hata huwajui wazazi wake, si mjinga wewe yani mjinga namba moja. Erica hujifunzi yani hujifunzi kabisa, mahusiano na wanaume matapeli unayatoa wapi? Yani mwanaume anawajua ndugu zako wote hadi wale wa pembeni anawajua ila wewe hujui hata wazazi wa huyo mwanaume na unajidai kuwa unapendwa, ndio upendo huo au kichefuchefu? Wanaopendwa wametambulishwa kwao sio nyie wa vichochoroni, ukipewa shilingi mbili basi unajiona umefika, unajiona kama umeokota dodo kwenye mwarobaini, huo ni ujinga Erica yani ni ujinga haswaaa. Mwanaume wa ukweli anayekupenda kwa dhati, atakupeleka wewe kwa ndugu zake wote, atakutambulisha kwa rafiki zake wakujue, atakuonyesha kwa watu wake wa karibu uwajue, kwa Rahim yamekutokea hay ohayo, na kwa huyu Erick hay ohayo, hujifunzi tu loh! Ukipata mwanaume kwasasa, kabla ya mambo yote akutambulishe kwa ndugu zake, akigoma achana nae. Nilikwambia niwe mshauri wako ila unaenda kuchukua ushauri kwa wajinga wenzio huko na unakuwa mjinga maradufu. Natamani hata nichukue bakora nikutandike sijui nimezaa vipi toto jinga kama wewe”
Erica alijisikia uchungu sana na hivyo alikimbilia chumbani kwake na kulia sana kwani hakutegemea kwa yale aliyoambiwa na hakutegemea kuhusu mzee Jimmy alilia sana huku akijisemea,
“Hakuna ninachotenda kiwe chema katika maisha, kila jambo langu ni baya mimi Erica jamani kwanini mimi!”
Alilia sana kwa muda huo.
 
SEHEMU YA 398


Tumaini na Erick walikuwa hospitali wakimngoja baba yao ambapo alikuwa akihudumiwa na madaktari walisema kuwa inaonekana presha yake ipo juu sana, Tumaini alimwambia kaka yake,
“Mmmh Erick, naomba niongee hili ila usinifikirie vibaya kiukweli Erica sio mtu mzuri yani anakuchanganya wewe na baba kweli?”
“Tumaini sidhani hiko kitu”
“Inamaana baba amechanganyikiwa kusema kuwa Erica ni wake? Na hadi baba kazimia lazima kuna kitu hapa Erick sio bure”
“Ila sidhani kama Erica alikuwa akinichanganya mimi na baba kiukweli”
“Ila wewe ni mbishi tu, kipindi tupo chuoni kulikuwa na sifa mbaya sana dhidi ya Erica kuwa anatembea na wanaume wengi, alibakwa, sijui katoa mimba yani ana kila aina ya sifa mbaya”
“yote hayo tumeyaona kama mapito kwenye mapenzi yangu na Erica maana tunapendana sana”
“Kwahiyo na hili la baba nalo ni mapito eeeh! Hebu fungua macho Erick, huyu ni baba na huna baba mwingine ila Erica ni mwanamke ambaye ukimuacha utapata mwanamke mwingine. Unapoongea chochote fikiria na maisha ya baba”
“Hivi Tumaini unafikiri mimi sifikirii? Ila na wewe unapoongea fikiria na furaha yangu, furaha yangu ni kuwa na Erica, yani Yule ndio manamke wa maisha yangu”
“Baba akifa sitakuelewa wewe wala huyo Erica”
“Sasa hizi mada zinatokea wapi jamani”
Daktari alitoka na kwenda kuwapa taarifa juu ya maendeleo ya baba yao,
“Imnaonyesha kuna habari ya mshtuko ambayo huyu mzee kaipata maana presha yake ilikuwa juu sana na tumejitahidi kwakweli kuweza kuishusha kiasi, sasa hata akija kuruhusiwa hawezi kuwa sawa kwa kipindi kidogo tena inabidi muwe nae makini sana yani msimpe habari ya kumshtua wala msimwambie kitu kibaya”
Tumaini akauliza,
“Je ameweza kuongea?”
“Hapana, bado amepumzika ila anaweza akaruhusiwa kesho. Kwahiyo kwa leo atalala tu hapahapa hospitali”
“Ila dokta, baba yetu hajawahi kuwa na presha hata mara moja”
“Inawezekana hamkujua ila ana presha tena ya kupanda”
Kwahiyo ilibidi wawe wapole tu maana tayari baba yao alikuwa amelazwa, kichwani kwa Erick kulikuwa na vitu vingi sana vinacheza kwa wakati huo na hakupata majibu ya chochote anachowaza, simu yake ikaita aliangalia mpigaji aliona ni Erica, alitamani kutokupokea ile simu ila aliamua kupokea tu, alisogea pembeni na kuongea na ile simu na kugundua kuwa Erica analia, akamuuliza
“Sasa unalia nini?”
“Najua Erick utanifikiria vibaya ila mimi sikuwa na mahusiano na baba yako kabisa”
“Kwahiyo baba yangu ni chizi kusema mwanamke wake ni wewe”
“Erick jamani, kumbuka niliwahi kukwambia kuwa kuna mzee ananifatilia na huyo mzee ndio huyo mzee Jimmy na hata sikujua kama ni baba yako Erick”
“Kwavile hukujua kama ni baba yangu ukaamua kutuchanganya baba na mtoto? Kwanini wanawake mnakuwa hivyo lakini, yani hata mpendwe vipi lakini ukimuona mwanaume ana dau kubwa unaamua kuhamisha majeshi kwake, sasa baba yangu kweli Erica!”
“Jamani Erick utanilaumu bure ila nilikueleza kuhusu huyo mzee kunifatilia jamani, sijawahi kuwa na mahusiano nae. Ila nimekupigia ili kuuliza anaendeleaje?”
“Sasa unamuulizia wa nini? Wakati ulipokuwa na mahusiano na mtu mzima kama huyu hukujua kama uanweza msababishia matatizo? Bado hajazinduka”
“Najua Erick huwezi kunielewa kwasasa, ila tuonane basi nikueleze”
“Yani nimuache baba yangu hospitali nije kuonana na wewe Erica? Inakuingia akilininhiyo kabisa? Si unakumbuka ulivyonieleza kwamba ulimpenda sana baba yako, inamaana mimi simpendi baba yangu?”
“Lakini Erick, mimi sikujua kama ni baba yako”
“Swala hapa sio kujua au kutokujua ila swala ni kwanini uchanganye mapenzi yangu na mtu mwingine? Ngoja baba azinduke ndio nitaongea na wewe vizuri ili nijue kisa na mkasa, lakini kwasasa hatutaelewana”
Kisha Erick akakata simu, kwa wakati huo hakutaka kumuelewa Erica kwa haraka kwani alitaka kujua ukweli kwanza na ukweli hawezi kuujua toka sehemu moja ni lazima apate sehemu zote mbili.

Kesho yake Mzee Jimmy alipewa ruhusa ya kurudi nyumbani ambapo alirudi na watoto wake ila hawakumuuliza chochote baba yao zaidi ya kwenda nae nyumbani tu, walipofika walimuacha akapumzike kwanza kisha Tumaini aliamua kwenda kwa mama yake ili akamueleze hali hiyo inayoendelea kwao.
Alifika kwa mama yake na kumkuta, na baada ya salamu tu alianza kumueleza yaliyojiri ila mama yake alionekana kucheka sana yani kama kasikia habari ya kituko wakati kamueleza kuwa na baba yao hali sio nzuri maana presha ilipanda, Tumaini alimuuliza mama yake,
“Mbona unacheka sasa mama?”
“Ananichekesha huyo baba yenu, hivi ujana wake ale na nani uzee amfie nani? Mzee akili zake mbili kweli huyo, kwamaana hiyo kama mwanamke mwenyewe ndio huyo huyo wa Erick kwahiyo ni binti mdogo ambaye ni lika lenu. Hivi baba yenu ana wazimu au kitu gani, mzee mzima kutaka kuoa watoto wake ndio nini? Mbona kuna wanawake wengi tu lika lake, kuna sie wajane, kuna Yule mamake Erick hajawahi kuolewa Yule si akamuoe kuliko kuanza kuaibika na kupandisha presha na uzee ule. Anataka tu kumkosesha mwanae furaha kwa ujinga wake”
“Kwahiyo mama unamshauri Erick aendelee na maswala ya ndoa na Yule binti?”
“Ndio mimi ningekuwa Erick wala nisingebabaishwa na huyo mzee, aende zake huko muda wake ulishapita”
“Mmmh mama jamani, baba akifa je!”
“Na afe tu, mzee hana akili hata kidogo alikuwa wapi kuoa kile kipindi chetu? Alijua kuchezea wanawake wala hakuwa na lengo la kuoa, iweje leo asikie mwanae anataka kuoa basin a yeye juu juu kutaka kuoa? Haya hatumkatazi kuoa, ila atafute mtu mzima wa lika lake, kilichempeleka kwa mtoto ni nini si alitaka presha ndio hiyo kaipata. Aishie zake huko”
“Jamani mama, jua unayemsema hapo ni baba yetu?”
“Kama angeithamini hiyo nafasi yake ya ubaba basi asingeenda kutafuta presha kwa kuwa na mahusiano na watoto. Simtetei hata kidogo huyo mzee yani hata kidogo, sema lingine tu Tumaini”
Kwakweli alikosa kingine cha kuongea na mama yake maana ilionyesha mama yake kuwa hana habari kabisa na ugonjwa wa baba yao, ila hakumlaumu sana kwavile hakujua kuwa baba yake alimtendea nini mama yake kipindi cha mahusiano.

Kwakweli Erica hakuwa na raha kabisa siku hii, ilikuwa ni jioni tayari na hakupata mawasiliano yoyote toka kwa Erick na alikuwa kila akimpigia simu Erick basi ile simu yake haipokelewi, kitendo hiko kilimfanya awe na mawazo sana. Dada yake Bite na mama yake kuna mahali walienda kwahiyo walimuacha yeye nyumbani kwa muda huo, mama yake akamwambia,
“Sio Erick wako anakuja unajifanya umepandisha shetani la upendo halafu uondoke na kuacha watoto ndani”
“Siwezi kuondoka na kuacha watoto mama”
“Nakwambia kabisa maana akili zako unazijua mwenyewe”
Kisha wakaondoja na kumuacha akiendelea na mawazo yake, muda kidog alifika rafiki yake Dora maana kipindi hiko alijifanya amejirekebisha na ni muda mrefu kidogo hakuja kumuona rafiki yake, Erica alimkaribisha vizuri tu ila aliamua kumwambia kile kinachomsibu au kumuumiza moyo,
“Dora rafiki yangu, mbona hujawahi kuniambia kuhusu watoto wa mzee Jimmy?”
“Kwani mzee Jimmy kafanyaje? Sasa mimi watoto wa mzee Jimmy nikwambie wa nini eeeh! Wananihusu nini, najua tu Yule mzee ana watoto wawili ila watoto wake siwafahamu”
“Mwenzangu, kumbe Erick ni mtoto wa mzee Jimmy kwahiyo Erick na Tumaini ndio watoto wa mzee Jimmy”
“Kheee kumbe!! Sasa ndio kama naanza kupata mwangaza wa mambo”
“Yapi hayo?”
Ndio Dora alianza kumueleza kilichompata mdogo wake na mpaka muda huo yupo kwakina Sia,
“Sasa nilishangaa kusikia kuwa Tumaini na Erick ni ndugu na Yule Sia alimpelekea Erick tunda halafu kalirusha nje na mdogo wangu akaliokota kumbe wale ni watoto wa mzee Jimmy!! Maana Yule mzee anaishi nmitaa ya kwetu kule, ule mtaa wa matajiri, kumbe ndiomana mdogo wangu kapata ujinga kirahisi kumbe wanakaa kule kule”
“Basi ndio huyo mzee wako kaniletea tafrani jana hapa nyumbani”
“Tena Erica usimkubali kabisa huyo mzee, ila kwavile kakuletea vioja vya kujifanya presha imepanda sababu umemkataa sijui nini na nini, nasikia watoto wa Yule mzee wanampenda sana baba yao, na kwavile ndio hao Tumaini na Erick basi inabidi ufanye kitu”
“Kitu gani sasa?”
“Wakina Erick wakikulazimisha uolewe na baba yao sababu baba yao kachanganyikiwa na wewe sijui, waambie swala moja kuwa kweli umewahurumia na unataka hali ya baba yao iwe imara ila waambie kabla ya ndoa ukapime ukimwi na baba yao. Erica Yule mzee kaathirika, asitake kukuingiza mkenge rafiki yangu, mwanzo nilifanya utani ila kiukweli Yule mzee kaathirika kabisa”
“Jamani nawezaje kukubali kuolewa na Yule mzee? Simpendi kabisa, hata kama angekuwa hajaathirika bado simpendi yani mimi nitaendelea kusimamia msimamo wangu tu wa kuwa na Erick, najua Mungu nae atanisimamia kwa hili. Sitaki kuwa kigeugeu yani huku na huku hapana kwakweli, nampenda Erick na ninamtaka Erick”
Kabla Dora hajajibu, kuna mtu aligonga mlango na Erica kumkaribisha, mtu huyo aliingia ndani alikuwa ni Derick, baada ya kutimuliwa kwa siku zote ila bado alifika. Akashangaa sana kuwa bado Erica ana urafiki na Dora, naye Dora alimshushua,
“Kwani kuna ubaya gani jamani mimi na Erica kuendelea na urafiki?”
“Ni vizuri ila mimi jlipita tu kukusalimia Erica, ila kama mama yako hayupo nashukuru ngoja niondoke sasa hivi asije akanikuta bure maana mama alivyo hanipendi huyu anaweza kunila mboga”
Basi Derick akaamua kuaga ila Dora nae aliaga pia sababu alimaliza kuongea na Erica na alihofia pia dada yake Erica kumkuta maana alihisi kuwa lazima huyo dada atakuwa na kisasi nae.
Kwahiyo Dora aliongozana na Derick na kuondoka pamoja.
 
SEHEMU YA 399

Walivyofika setendi Dora alimuuliza derrick,
“Kwani muda huu unaenda wapi Derick?”
“Kwani nina pakwenda basi, leo kuna mtu kaniboa kweli ndiomana nikaja kumuona Erica mara moja”
“Kakufanyaje mtu huyo?”
“Yani kuna mdada nilikuwa na mahusiano nae, na leo nilijipanga vizuri kabisa kuwa nae sijui vipi eti anasema hayupo kwenye mood ya kuwa na mimi. Nimeachana nalo huko, kaniudhi kweli yani”
“Pole sana, na wewe una hamu zako hapo!”
“Yani weee acha tu, nimekuja hadi huku basi tu”
“Ila usijali, unajua umeletwa huku ili kuonana na mimi maana katika umalaya wako wote hujawahi kutembea na mimi”
“Na wewe Dora vipi, mwanaume haitwi malaya bhana, hata hivyo sijawahi kutembea na wewe. Nikitaka utanipa?”
“Kwanini nisikupe sasa jamani wakati wewe ni rafiki yangu!”
“Mmmh Dora kweli?”
“Ndio kweli”
“Basi tukodi bajaji tutafute sehemu ya karibu guest tukajivinjari”
“Hakuna tatizo”
Muda ule ule Derick aliita bajaji na kuondoka na bajaji ile kwenda kwenye nyumba ya kulala wageni yani huko akawa na Dora mpaka asubuhi.

Dora alitoka pale asubuhi na kuanza safari ya kuelekea kwao ila alikutana na James akiwa anaenda kazini, James akasimamisha gari yake na kumpakiza Dora kisha akamuuliza kuwa ametoka wapi muda huo.
“Asubuhi yote hii Dora, unaonekana umechoka umetoka wapi?”
“Ngoja tu nikwambie ukweli, nimetoka guest”
“Guest! Kwahiyo ulikuwa na mwanaume?”
“Sasa Guest niende peke yangu nina wazimu au? Nilikuwa na mwanaume ndio”
“Ila Dora si umeathirika wewe, huoni kuwa si vizuri hivyo unavyofanya?”
“Hivi kwani ni mimi tu mwenye dhambi duniani hadi nikapata huu ugonjwa? Yani yoyote anayejilengesha kwangu twende, habari ndio hiyo na wale wanaume wote walionisumbua kipindi cha ulimbwende wangu nawapeleka na maji, si wanaume huwa hamkumbuki kinga eeeh! Yani akili zitawakaa sawa”
“Mmmh Dora, ila ujnajua ukimwi unazunguka? Unaweza tembea na mwanaume halafu akatembea na mdogo wako”
“Kwa bahati nzuri au mbaya sina mdogo wa kike kwahiyo imekula kwao na mdogo wangu kashalishwa limbwata huko kamganda mwanamke hataki hata kurudi nyumbani”
“Hivi Dora, limbwata ndio inakuwaje kuwaje?”
Dora alicheka sana kuona kuwa James kashasahau kuwa hata yeye alilishwa limbwata na pale alimwambia tu muda huo anarudi kwao ila James alijitolea kumpleka Dora kwanza ndio yeye kwenda kazini.
Dora aliingia kwao na kama kawaida mama yake alifoka huku akisikitika na kitendo cha kutokumuona mwanae,
“Mama, kunilalamikia mimi ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa. Nishakwambia cha kufanya, kama hutaki basi, ila hiko ndio cha kufanya”
Kisha Dora aliingia chumbani kwake, ila leo kabla ya yote aliamua kumpigia simu mzee Jimmy ili kusikia anasemaje ila ile simu ilipokelewa na Erick, na Dora aligundua baada ya kusikia ile sauti,
“Kheee Erick”
“Ndio, ni mimi wanifahamu kwani maana baba anaumwa”
“Nakufahamu, mimi ni Dora rafiki wa Erica nilikuwa nampigia simu mzee Jimmy”
“Kwahiyo na wewe unataka kujua hali ya shemeji yako sio”
“Hapana, huyo sio shemeji yangu kama unavyofikiria. Muulize vizuri kuwa Dora ni nani akueleze kuhusu mimi. Sio shemeji yake mimi”
“Baba yangu ni mgonjwa, siwezi kuondoka karibu yake maana hataki niende popote na siwezi kumuuliza swali hilo kwasasa mpaka awe sawa kabisa”
Kisha Erick akakata ile simu, ila Dora alihisi jambo kuwa mzee Jimmy anajifanyisha ili Erick asiwe karibu na Erica.
Tumaini alimuita kaka yake ambapo alitoka sebleni na kuanza kuongea naye,
“Nimekusikia ukiongea na simu nani huyo? Nikasikia shemeji”
“Ni Dora huyo, Yule rafiki wa Erica, itakuwa unamfahamu maana anajulikana sana kwa matendo yake”
“Kapata wapi namba ya baba?”
“Sijui, labda na rafiki yake Erica wamepeana huko”
“Hivi Erick sikuwahi kukuuliza, kwani Erica amewahi kukwambia habari zozote za kuhusu baba?”
“Hajawahi kuniambia zaidi zaidi aliniambia kuwa kuna mzee anamfatilia eti anasema ndio baba, ila swali linalonitatiza ni kuwa alisema kuna hela kapewa na huyo mzee sasa hazitaki na amezitumia milioni tano halafu mke wa huyo mzee anazitaka, yani nikatoa milioni tano yangu hivi hivi ili Erica asisumbuliwe na huyo mzee. Swali langu ni kuwa mke wa huyo mzee ni nani wakati baba yetu hana mke? Si change la macho lile nilipigwa na Erica?”
Mara baba yao akamuita Erica, kwahiyo ilibidi Erick aende kumsikiliza na kuacha kuongelea mada zake.

Ndugu wa Bahati leo walimuita nyumbani ndugu yao ili waongee nae kuhusu yale waliyoyasikia, Bahati alifika na kuwasikiliza tu wanachoongea ambapo dada yake alianza kwa kusema,
“Kwakweli Bahati utusamehe sana, hatukujua kuwa Nasma ni mbaya kwako na kukuozesha kwa huyo”
“Sawa hakuna tatizo, ila mimi nataka kumuoa Siwema kwasasa”
“Yani Bahati hujui tu ila bado nguvu ya dawa ipo kwako, yupo binti uliyekuwa ukimpenda sana”
“Yuko wapi huyo binti?”
“Anaitwa Erica, ulikuwa ukimpenda sana na alikuwa ni kila kitu kwako”
“Nina uhakika hata huyo binti hatonitaka tena kwa nilivyo sasa, ila nyie wenyewe si ndio mlikiri ya kwamba mlinipa dawa ili nimsahau huyo binti? Na kweli nimemsahau maana hayupo hata kwenye kumbukumbu zangu, kwahiyo haya ndio maisha ambayo mmenichagulia ndugu zangu”
“Hapana Bahati, sio hivyo yani sio kama hivyo unavyofikiria”
“Yani kuongea kwenu sidhani kama kunanisaidia maana kama kuharibika sasa nimeharibika vya kutosha, kwasasa sirudi nyumbani kwangu sababu nina tatizo lingine”
“Tatizo gani tena?”
“Nishatembea na mdogo wa huyo Nasma na sasa ana mimba yangu, nahitaji kumuoa Siwema. Ila nilirudi nyumbani kwangu na kumkuta Nasma yupo na mama yake yani mama mkwe wangu, ngoja niwaambie tu ukweli ndugu zangu nimejikuta nikianza kumpenda Yule mama tena nampenda kimapenzi”
Ndugu zake walishangaa sana, kisha Bahati akaendelea kuongea,
“Nikaamua kuondoka nyumbani kwangu na kwenda kulekule nilikompangishia nyumba Siwema sababu nikiishi pale nyumbani naweza nikambaka Yule mama mkwe, namtamani kabisa na kujizuia siwezi”
Kwakweli hii hali iliwafanya wawaze dawa ya kumfanyia Bahati mapema iwezekanavyo maana bila ya hivyo atachafua ukoo wa kina Nasma maana hali aliyokuwa nayo haikuridhisha kabisa.

Siku zilienda na Erica hakutafutwa na Erick kabisa, kwakweli kitendo hiko kilimpa mawazo sana. Halafu alianza kujihisi vibaya yani afya yake haikuwa vizuri, siku hiyo alijiandaa na kuaga pale kwao kisha akaenda zake hospitali kwa lengo la kupima malaria.
Majibu yakatoka na kuambiwa kuwa ni mjamzito, alishtuka kidogo ila alikubaliana na majibu yale kwani kabla ya ugonjwa wake anakumbuka kuwa aliwahi kukutana kimwili na Erick kwahiyo kwa vyovyote vile ile ni mimba ya Erick.
Basi akawa anatoka pale hospitalini ila kuna mtu alikumbana nae kikumbo na cheti chake kikaanguka, Yule mtu aliokota kile kicheti na kukishika. Alivyoinua macho kumtazama Yule mtu akakutana macho kwa macho na Sia yani Yule mtu alikuwa ni Sia, basi alisoma kile cheti cha Erica na kusema
“Kheee Erica, kumbe una mimba? Ya nani tena? Usije ukamsingizia Erick maana na mimi pia nina mimba ya Erick, cheti hiki hapa”
Akatoa cheti na kumpa Erica, ambapo alikisoma na kuona kweli Sia ana mimba.
 
SEHEMU YA 400

Basi akawa anatoka pale hospitalini ila kuna mtu alikumbana nae kikumbo na cheti chake kikaanguka, Yule mtu aliokota kile kicheti na kukishika. Alivyoinua macho kumtazama Yule mtu akakutana macho kwa macho na Sia yani Yule mtu alikuwa ni Sia, basi alisoma kile cheti cha Erica na kusema
“Kheee Erica, kumbe una mimba? Ya nani tena? Usije ukamsingizia Erick maana na mimi pia nina mimba ya Erick, cheti hiki hapa”
Akatoa cheti na kumpa Erica, ambapo alikisoma na kuona kweli Sia ana mimba.
Erica alimuangalia kwa makini Sian a kumuuliza kwa mshangao,
“Una mimba?”
“Kwani umeshindwa kusoma cheti hiko au? Mimi nina mimba ya Erick, sijui mwenzangu kama kawaida yako ya kupachika mababa watoto wako, sikuelewi!”
Erica akaona kuendelea kuongea na mtu huyu ni kujipa mawazo ya bure wakati mwenye ukweli ni mmoja tu ambaye ni Erick, basi Erick akachukua kile cheti chake kwa Sian a kumkabidhi kile alichompa akisome kisha kuanza kuondoka, ila Sia alimfata kwa nyuma na kumwambia,
“Mbona husemi lolote sasa?”
“Unataka niseme nini?”
“Wotw tuna mimba, na huonyeshi kushtuka kama kitu ulikuwa unajua au Erick kashakwambia kuwa nina mimba yake!”
“Sia, naomba uniache tafadhali kila mtu kaja hospitali kwa mambo yake. Kama wewe una mimba na mimi nina mimba tatizo nini sasa? Sisi ni wanawake na kubeba mimba ni haki yetu”
Sia akaanza kucheka na kusema kwa kebehi,
“Ni haki yetu ndio ila tunatakiw akubeba mimba kwa malengo, yani wewe mtoto wa kwanza umezaa bila malengo na sasa wa pili huyo hujui hata baba wa mtoto ni nani na hujui hata atachukua uamuzi gani”
Erica hakumuangalia tena wala nini sababu alihisi akimchefua tu nay ale maneno yake, alitoka zake na kwenda kupanda gari lake na kuondoka ambapo alienda moja kwa moja ufukweni ili atulize mawazo kidogo.

Erica alifika ufukweni huku akiwaza na kuwazua, akafika eneo moja wapo na kulikumbuka vizuri, lilikuwa ni eneo ambalo alikutana na Bahati kwa mara ya kwanza na alikuwa akiwaza jinsi alivyoachwa na George, aliangalia lile eneo ila hakutaka kukaa tena maana aliogopa kukutana na mwanaume mwingine king’ang’anizi kama Bahati ingawa kwa upande mwingine alimkumbuka Bahati, mwanaume ambaye huwa haoni kosa kwa Erica yani kila kitu kinachofanywa na Erica kwake ni sawa tu, alitabasamu alivyomkumbuka na kurudi kwenye gari kisha kuchukua simu na kumpigia Erick kwani aliona anahitaji sana kuongea na Erick, ile simu ilipokelewa na Erica alianza kuongea,
“Erick tafadhali nina maongezi na wewe, naomba tuonane”
“Si unajua baba yangu anaumwa Erica? Nitamuachaje baba yangu?”
“Erick kumbuka ahadi uliyonipa kwenye mapenzi yetu sasa kuwa hakuna kitu kitakachotutenganisha, ulisema hatupaswi kusikiliza maneno ya watu yani sisi tukae na swala moja la kupendana tu sasa vipi leo umesahau ahadi yako?”
“Kwahiyo Erica, unataka mimi nimuache baba yangu sababu ya ahadi ambayo niliahidi kipindi cha nyuma?”
“Nina jambo muhimu nahitaji kuongea na wewe”
“Hapana, sio kwasasa”
Erick alikata simu, kitendo hiko kilimuuma sana Erica, aliamua tu kurudi nyumbani kwao ambapo mama yake alimuuliza alichoenda kuambiwa hospitali kuwa kinamsumbua ni kitu gani,
“Haya mwali wetu, nini kinakusumbua?”
Erica aliwaza kuwa akisema ni mimba itakuwa ni balaa kwa mama yake maana hatomuelewa kabisa ukizingatia maswala ya mapenzi kashamkataza sana, kwahiyo alimdanganya tu,
“Wamesema eti nina UTI”
“Oooh pole mwanangu, eeeh dawa walizokupa ziko wapi?”
Hapo ndio ukawa mtihani sasa maana uongo ule hakujipanga nao sababu ya mawazo ya Erick, alijikuta akikaa kimya kwa muda na kumuangalia tu mama yake ambapo mama yake alirudia swali,
“Dawa walizokupa ziko wapi? Au hawajakupa dawa?”
“Waliniandikia dawa kuwa nikanunue duka la madawa”
“Karatasi uliloandikiwa dawa liko wapi?”
Alianza kuhisi kuwa pengine mama yake kamgundua maana si kwa maswali yale ya mitego, ila bado aliendelea kumficha mama yake,
“Nilienda duka la madawa ila Yule nesi niliyemkuta amenipa ushauri mzuri sana. Kuwa nisijisumbue kumeza madawa maana unaweza ukameza na UTI ikakurudia, kwahiyo kanishauri nanze dozi ya vitunguu swaumu”
“Dozi ya vitunguu swaumu? Weee Erica ni mzima kweli?”
“Ndio dozi ya vitunguu swaumu, niwe natwanga halafu nameza kama dawa”
“Yani umezunguka kunitafutia uongo wa kuniambia hadi umeupata huo loh mwanangu uongo utaacha lini wewe? Nilikuwa nakuangalia tu wakati unatoka, mwanaume toka sakata la baba yake hapa hajawahi kukanyaga mguu wake tena ila wewe kiguu na njia kumfata fata, unachokitaka utakipata nakwambia, na usiniletee mimba tu, huo ujinga wa kuzaa watoto wawili nyumbani tena bila ndoa siutaki. Umesikia!”
“Nimesikia mama”
Kisha Erica akainuka na kwenda chumbani kwake huku akiwaza sana maana kama mimba tayari anayo, sasa Erick akiendelea kuzingua tu kwake itakuwa ni mtihani mkubwa sana.

Kwa upande wa Sia, alipotoka hospitali moja kwa moja alienda kwakina Tumaini na kumkuta Tumaini akiwa amekaa nje leo. Akasalimiana nae na kuanza kuongea nae, kiukweli Tumaini alitaka kumtimua Sia ila alishangaa akimuangalia tu bila kumtimua, basi Sia akampa Tumaini kile cheti cha kuonyesha kuwa ni mjamzito, Tumaini akamuuliza kwa mshangao,
“Una mimba?”
“Ndio nina mimba, ya kaka yako”
“Hebu acha zako Sia, hiyo mimba iliingia kwa upepo au? Nakumbuka tulisema uigize kuwa una mimba ila haikuwa kweli”
“Tumaini sikupima tu ila kiukweli nina mimba, na cheti hiki hapa. Huyu nimembeba ni mtoto wa Erick”
“Mmmh na Yule unayeishi naye pale kwako?”
“Yule siishi nae kama unavyofikiria ila analalaga pale nje kwetu”
“Unafikiri nina hamu na wewe? Toka nimejua kuwa wewe ni mshirikina basi sina hamu na wewe tena”
“Tatizo Tumaini hukunielewa, ila ndio nina mimba ya kaka yako”
“Sikia Sia, swala la wewe kuwa na mimba siwezi kukubali wala kukataa ila muhusika ndio atasema ukweli maana ndio mnajuana. Mimi siwezi kujua kuwa mlikutana muda gani”
Baba yao na wakina Tumaini alikuwa nje pale akinyoosha nyoosha miguu na aliwasikia wakati Tumaini na Sia wanaongea, basi akafika na kusema kuwa atambulishwe Sia kuwa ni nani? Kwa kipindi hiko wakina Tumaini walikuwa wapole wana kwa baba yao maana hawakutaka kumkera wala kumpa habari za kuudi, kwahiyo Tumaini akamtambulisha Sia kuwa aliwahi kuwa na mahusiano na Erick, halafu Sia nae akasisitiza pale pale kuwa katoka kupima ana mimba ya Erick huku akimpa baba yao cheti kinachoonyesha kuwa ana mimba. Cha kushangaza mzee Jimmy alionekana kufurahia sana ile habari na kumkaribisha Sia ndani kwao ambapo kwa muda huo Erick alikuwa ametoka kuna dawa alienda kumtafutia baba yake.
Mzee Jimmy alimkaribisha Sia huku akimuhoji maswali mbalimbali kama ana mpango gani na Erick,
“Natamani siku moja Erick awe mume wangu, yani nitafurahi sana”
“Basi usijali, siwezi kuacha mjukuu wangu alelewe bila ya baba yani lazima Erick akuoe na sherehe yote nitaigharamikia mimi”
Tumaini alikuwa jikoni kwa muda huu ila kwakweli alishangaa sana kwa baba yao ambaye siku zote toka ameanguka alionyesha kutokuwa na furaha na aliongea kwa shida kiasi kwamba Erick ndio alikuwa akimpokelea simu zake ila leo ilikuwa ni ajabu sana maana aliongea kwa furaha mno kama hakuwahi kuumwa hapo kabla.
 
SEHEMU YA 401

Erick wakati anatafuta dawa za baba yake alijikuta akifika mpaka mitaa ya kwakina Erica, ingawa ilikuwa ni usiku tayari ila kwa upande mwingine alitamani kujua ni kitu gani erica alitaka kumwambia, kwahiyo alimpigia simu muda huo ambapo kwa muda mchache tu Erica alipokea simu hiyo kisha Erick alimuambia aende kituoni kwao akaongee nae.
Erica alitoka kwao kwa gia ya kwenda dukani kisha akaelekea kituoni ambako Erick alisimamisha gari yake yani siku hii hakutaka kwenda kwakina Erica kabisa maana kwa amjuavyo mamake Erica basi inaweza kuwa balaa kwake akijitokeza pale wakati hajajipanga.
Erica alifika na Erick alikuwa amesimama tu nje ya gari, Erica alimsogelea na kumkumbatia ambapo Erick hakuweza kuacha kukumbatiwa na Erica ila naye alimkumbatia pia na kugundua kuwa Erica alikuwa akitokwa na machozi, alimuuliza kwa upole kuwa tatizo ni nini ila bado Erica alionekana akilia ikabidi aingie nae kwenye gari ili aongee nae vizuri.
Alikaa nae kwenye gari huku akimkumbatia na kumbembeleza na kumuuliza kwa upole,
“Kwani Erica tatizo ni nini?”
“Nilikuwa sipo vizuri kwa hivi karibuni, nikaamua leo kwenda hospiatali. Nimekutwa na ujauzito Erick”
Erick akamuweka kwanza pembeni Erica na kumuuliza,
“Erica una mimba? Usiniambie ni mimba ya baba yangu maana sijui nitafanya nini muda huu”
“Erick, najua nitasema sana ila unaweza ukaniamini au usiniamini ila mimi sijawahi kutembea na baba yako, ni kweli kanifatilia kwa kipindi kirefu sana ila sijawahi kutembea nae. Kama huamini naomba hata uchukue muda wako umuulize Dora, mimi sijawahi kuwa na mahusiano na baba yako. Hii mimba ni yako Erick”
“Kwa mara moja tu Erica jamani! Yani mara moja tu umepata mimba yangu?”
“Ndio Erick, hii mimba ni yako yani una mashaka bure tu ila hii mimba ni yako Erick, naogopa kusema nyumbani, naogopa kumwambia ukweli mama maana sijui kama atanielewa kubeba mimba mbili nyumbani”
“Sawa, nimekuelewa Erica. Ila nina ombi moja kwako”
“Niambie Erick”
“Naomba usiitoe hiyo mimba tafadhali, naomba usiitoe. Huyo mtoto nitampenda kama nimpendavyo Angel, haijalishi ni wa nani ila nitampenda”
“Erick, huyu mtoto ni wako hutakiwi kuwa na mashaka. Ni mtoto wako huyu Erick, niamini tafadhali”
“Sawa, nimekuelewa basi ngoja nikurudishe kwenu”
“Kabla ya kunirudisha kwetu, naomba nikuulize jambo”
“Jambo gani?”
“Erick, una majina mengine kabisa hata nikashindwa kuelewa kuwa mzee Jimmy ni baba yako. Kwanini hutumii majina ya baba yako?”
“Erica, nilitaka kukwambia kuhusu mimi zamani sana ila kwavile tu mambo yaliingiliana ndiomana sikuweza kukwambia. Toka kipindi nimekwambia Angel aitwe jina langu na sikuona kama ni tatizo maana mambo kama hayo hutokea kwenye jamii. Sema historia yangu ni ndefu kidogo ila nitakwambia kwa kifupi”
“Niambie tu nitaelewa”
“Sikia nikwambie, mama yangu aliponizaa mimi, Yule baba umuonaye nasikia alizingua hivyo mama aliishi kwao ndipo babu yani baba mzaa mama akasema niitwe kwa majina yake yani hakutaka majina ya baba yawe kwangu, toka hapo niliandikishwa shule kwa majina ya babu kwahiyo vyeti vyangu vyote vina majina hayo. Na mwishowe mimi niliishi kwa mama mdogo ndio kipindi kile wakati nasoma, sasa nilivyotimuliwa pale shuleni, mamdogo alimwambia mama kuwa hatoweza tena kunilea maana nimekuwa mtukutu, kipindi hiko mama yangu alikuwa Marekani akifanya kazi za ndani, kwahiyo ujumbe ule ulichelewa sana kumfikia mama. Toka nifukuzwe shule niliishi nyumbani tu kwa mamdogo maana alisema hanitafutii shule nyingine tena, kidogo hapo katikati nina historia ndefu ndiomana mamdogo hakutaka kunitafutia tena shule na alisema ile ni shule ya mwisho kwangu. Nilikuwa napenda maisha mazuri hivyo kila akinipeleka shule zisizoeleweka nilianza kumsumbua ndio akanileta ile shule, akasema ni nzuri na kweli niliipenda na kumuahidi sitamsumbua tena na nitakuwa mtoto mzuri kwahiyo nilipofukuzwa na pale mamdogo alizira kunitafutia shule nyingine, babu naye hakuwa na uwezo wa kunisomesha ingawa nina majina yake, maana alisema ni bora kutumia majina yake anayenijali kuliko kutumia majina ya baba ambaye wala haonyeshi kunijali. Nilikaa mwaka mzima nyumbani nikiwa sijielewi wala nini yani nipo nipo tu maana tulikuwa tunangoja majibu ya mama kuwa tufanye kitu gani ila kwa kipindi hiko niliondoa matumaini ya kusoma kabisa. Siku moja katika pita pita zangu mitaani ndipo nikakutana na baba na alinisaidia bila kujua kuwa mimi ni mwanae, sasa siku naenda kumpokea mama uwanja wa ndege nikakutana tena na baba ambaye kuna ndugu yake alikuwa anaenda kumpokea pia, akanipa lifti tulipofika uwanja wa ndege ndio akakumbana na mama na palepale mama alishangaa kuona mimi na baba tulifahamiana, basi ikabidi atutambulishe vizuri na hapo ndio maisha yangu yakabadilika kwani nikaanza kuishi na baba huku nikisaidiana nae kwenye biashara zake mbalimbali, yani mimi nilikuwa nasoma huku nafanya biashara na baba, na kiukweli zile pesa zilinipa kiburi maana nilianza kuwa na wanawake wengi wengi sababu nilijua ulinikaa sababu nilikuwa sikupi pesa sasa nilikuwa na hela na kupata wanawake mbalimbali sema tu sikuwapenda kama nilivyokupenda wewe”
“Kheee kumbe, kwahiyo Tumaini ulikutana nae kwa baba yako?”
“Ndio Tumaini alikuwa akiishi kwa baba ila alikuwa akiishi sana kwa mama yake, nilipohamia mimi kwa baba ndipo na yeye akaja kuishi kwa baba na hapo ndipo alipojua historia yangu ya kufukuzwa shule sababu ya mwanamke maana mamdogo alikuwa akimsimulia kila mtu kuhusu mimi kufukuzwa shule sababu ya mwanamke, na ndio hapo Tumaini alipochukia sana kuhusu mwanamke aliyesababisha nifukuzwe shule maana mimi hadi kuendelea zaidi na masomo niligoma, unajua kitendo cha mimi kukaa mwaka mzima nyumbani bila ya kusoma kilinichukiza sana, mwishowe nilipokutana na baba nilisoma tu kutoa ujinga ila sio kusoma kwa malengo ndiomana wakati Tumaini yupo chuo mimi sikuwa chuo na usinione hivi sijafika chuo wala nini.”
“Kwahiyo mama yako alikuwa akifanya kazi za ndani?”
“Ndio mama yangu alikuwa akifanya kazi za ndani huko Marekani, watu wengi walipojua walitukebehi na kutucheka ila sasa ndio wanaoomba misaada maana mama kawa na hela hatari, anafanya atakacho, anaenda atakapo yani saivi kawa kama sio yule wa zamani. Na ni kipindi hiko aliporudi maisha yake yalibadilika moja kwa moja, nadhani alijiwekeza”
“Sasa wewe huishi na mama yako, kwahiyo anaishi na nani?”
“Mama anapenda sana kusaidia, ukienda kwake utakutana na watu mbalimbali tu ndugu zake, mimi kwasasa nishazoea kuishi kwa baba kwani kwa kiwango kikubwa sana kabadilisha maisha yangu, mama nae kabadilisha maisha yangu. Kwahiyo mimi nipo katikati, ni jicho la mama na pia baba ananitazama sana, toka amenitambua huwa hataki kunikosea na ndiomana na mimi sitaki nkumkose. Baba yangu amepatwa na presha kwasasa kwahiyo siwezi kumwambia kuwa Una mimba sijui yangu maana ninaweza msababishia matatizo zaidi”
Erica akapumua kidogo kisha akasema,
“Ila ukweli ni kuwa sijawahi kutembea na baba yako, muulize Dora ndio anajua ukweli wote maana Dora ndio alikuwa akitembea na baba yenu”
Hapo Erick alishangaa zaidi kwani hakutegemea kusikia kuwa baba yake anaweza kutembea na msichana kama Dora, aliona kweli mzee wake kaingiliwa basi alienda mbele kuendesha gari ili kumrudisha Erica kwao na kumwambia kuwa wataongea zaidi na watajua cha kufanya.
Alifika nae getini kwao, kisha Erica alifungua mlango wa gari ili aondoke ila kabla hajaondoka Erick alimuita na kushuka kwenye gari kisha akambusu Erica na kumuaga halafu akarudi kwenye gari na kuondoka zake.

Erica hakujua wakati anaingia pale getini kwao kumbe mama yake alikuwepo na alimuona pale wakati Erick anamuaga, kwahiyo Erica aliingia ndani bila kujua kuwa mama yake naye alikuwa nje.
Basi aliingia na kumkuta dada yake akiwa anamshangaa,
“Yani Erica kweli! Ndio duka gani hilo tangu umeondoka hadi muda huu jamani!”
Erica alikuwa kimya, akijipanga na majibu yake kama kawaida kisha dada yake akaendelea kumwambia,
“Mama yupo nje huko, ameenda kukutafuta madukani maana ni mud asana umechukua, toka uondoke hadi saa hizi! Halafu ni usiku huu ujue”
Basin a mama yao akaingia ndani na kumwamgalia Erica kwa gadhabu sana huku akisema,
“Natamani ungekuwa bado mdogo, yani leo ningekufinyanga upya mjinga wewe. Haya nidanganye kuhusu duka uliloenda mpaka muda huu”
Erica sababu mama yake alishaenda dukani kumuangalia pia, akaamua tu kusema ukweli,
“Mama, samahani nilitoka niende dukani kweli ila nikakutana na Erick njiani akiwa anakuja huku kwahiyo nikapanda kwenye gari lake na kuongea, tulipomaliza mazungumzo ndio nikarudi nyumbani”
“Sio ukarudi, sema akakurudisha. Au unafikiri sijawaona hapo mlangoni kwangu mkiwa mnalambana lambana, yani Erica unasahau kabisa jinsi Yule mwanamaombi alivyokufundisha kuenenda kiimani, yani umesahau kabisa kabisa na unafanya unavyotaka wewe, huyo Erick kila nikimfikiria kuwa ndiye mtoto wa lile balazuri najikuta kukosa tumaini nae kabisa, ndiomana alianza kukutongoza toka uko shuleni kumbe karithi tabia za baba yake mpaka shule ile ikakushinda sababu yake ila umesahau kabisa unaendelea tu kuendekeza mapenzi na yeye”
Bite alidakia na kusema,
“Kumbe ni huyu aliyesababisha Erica aje kusoma kwangu?”
“Ndio huyu mwanangu, yani Yule kijana sijui alimpa nini mdogo wako na alivyo mjinga ataanza kumfata fata hadi abebe mimba yake maana anafikiri kubeba mimba ndio kupendwa”
Hapo Erica alitulia kimya kabisa kwani kama mimba tayari alikuwa nayo, ila sasa alijitahidi kwa kila hali ile mimba isigundulike mapema nyumbani kwao labda mpaka atomize swala la yeye na Erick kuoana.
Basi akaamua tu kwenda kulala maana hakufurahia vile alivyokuwa anasemwa.

Erick alikuwa kwenye gari, ila kilichompeleka hadi mitaa ya kwakina Erica hazikuwa dawa za baba yake ukweli ni kuwa alitamani sana kuonana na Erica, na muda huo roho yake ilikuwa imeridhika sana na jinsi alivyoongea siku hiyo na Erica alijihisi raha sana kwenye moyo wake kiasi kwamba alikuwa akiendesha gari ila mawazo yote kwa Erica tu.
Alifika kwao na kuingiza gari ndani kisha kushuka, muda ulikuwa umeenda sana, ilikuwa ni saa tano usiku ila alipoingia ndani alimkuta Tumaini bado yupo macho akiangalia tu Tv, alipoingia tu alimsalimia na kukaa ili kuulizia kama baba yao amelala sababu dawa kachelewesha,
“Mmmh baba kashalala maana nimechelewesha dawa balaa”
“Wewe nawe kununua gani dawa huko toka saa kumi na moja jioni hadi muda huu ndio unarudi kweli?”
“Aaah sijui nikwambie vipi ila nilimkumbuka sana Erica, nikaamua kupita kwenye mitaa yao ili nimuone tu”
“Mmmh huyo Erica, sijui alikupa nini. Vipi lakini umeonana nae?’
“Ndio nimemuona na moyo wangu umeridhika na tena kanipa habari hiyo kama ina ukweli basi ni furaha kubwa kwangu”
“Habari gani tena hiyo?”
“Kwanza niambie, baba kalala?”
“Alale wapi? Baba leo kapona yani kaondoka kumpeleka Sia kwao, baba kawa mzima gafla”
“Kivipi yani”
“Ni hivi, ulivyoondoka tu alikuja Sian a kunipa taarifa kuwa ana mimba yako”
“Ana mimba yangu?”
“Ndio alivyosema, na cheti kanionyesha kuwa ana mimba yako. Sasa baba alisikia weee yani huwezi amini baba kapona muda huo huo na kumuita Sia sebleni ameongea nae kwa muda mrefu sana na ulikuwa unangojwa wewe, sema umechelewa sana, ndipo Sia alipoaga basi baba kaamua ampeleke Sia kwao yani baba anaonekana anataka umuoe Siam lee mtoto wenu”
“Huo ni ujinga sasa, sijategemea mambo ya kijinga kama hayo kutokea kwenye familia yangu, huyo Sia nitaenda kwao kesho asinitanie”
Erick aliinuka na kwenda chumbani kwake kwani alihisi kuwa na hasira iliyopitiliza, ni alichukia sana kwa muda huo yani baba yake kapona baada ya kusikia habari kuwa Sia ni mjamzito, alichukia sana kwakweli. Aliamua kulala kwa hasira hata kula hakutaka kabisa.
 
SEHEMU YA 402

Kulipokucha, Erick aliamka akaoga na kujiandaa basi akataka kwenda kumuangalia baba yake kwanza kabla ya kuondoka ila hakumkuta, alitoka nje na kumkuta dada yake Tumaini akiangalia gari lake, akamuuliza,
“Inamaana baba hakurudi jana au?”
“Alirudi yani wewe nay eye mlipishana kama nusu saa tu ila leo mapema kabisa katoka, kaniaga kuwa anaenda kwenye kazi yake”
“Kwahiyo baba kapona eeeh!”
“Itakuwa”
Erick alisikitika sana kwa mwenendo wa baba yake, kisha akamuaga Tumaini kuwa muda huo ameamua kwenda kwakina Sia,
“Na mimi natoka muda sio mrefu, naenda kule dukani”
“Sawa, tutaonana badae basi maana baba mwenyewe tuliyekuwa tunamuuguza ndio huyo kapona”
Basi Erick aliondoka zake na moja kwa moja alienda kwakina Sian a kumkuta Sia yupo tu ametulia nje kwao, alipofika yeye kuna mwanamke alikuwa nakatisha pia na kikapu kichwani, Sia alimuita na kununua embe bichi kisha kuanza kulitafuna pale, Erick alimuangalia huku akitikisa kichwa, ila Sia alimwambia,
“Usisikitike, ni mwanao huyu kataka embe muda huu”
“Hebu nitolee balaa lako huko, hiyo mimba yangu uipate wapi? Ndotoni au?”
“Unajifanya umesahau kama ulikutana na mimi kimwili? Ndio nikapata mimba hii, tena safari hii siwezi kuitoa hata usemaje, nishatoa mimba zako nyingi sana ila hii siitoi umesiki? Tena nadhani nitazaa mapacha”
Halafu akacheka, Erick alikuwa amechukia sana na kumuuliza,
“Hivi wewe mwanamke una kichaa au? Mara ya mwisho nilikutana na wewe nikiwa na hasira zangu hata hivyo nilitumia kinga maana sikuwa na mpango wa kuzaa na wewe, iweje useme ni mimba yangu?”
“Hujui kama kinga huwa zina pasuka? Nenda kagoogle uone jinsi wanawake wanavyopata mimba na kinga ilitumika. Mimi nina mimba yako, ukubali au ukatae yani utake ni mimba yako, hutaki ni mimba yako, sasa maswala hayo ya kushangaa yanatoka wapi?”
“Sia, huwezi kuwa na mimba yangu”
Sia akatoa kile cheti chake kumuonyesha kuwa ni mjamzito,
“Sasa bishana na cheti hiko kuwa Sia hana mimba. Nimekwambia nina mimba yako, unakataaje? Nakusingiziaje kwa mfano? Nimekaa kimya kwa mud asana ila sasa nimeamua kusema maana kitumbo kitaenda mbele bure sijakwambia kuwa nina mimba yako, kipindi chote nahangaika ili unipende sababu nahitaji tulee mtoto pamoja. Erick, hii mimba ni yako na wala usibishe”
“Nakataa Sia, huna mimba yangu yani hilo napinga kabisa na tutaenda kupima kwakweli huyo mtoto. Hiyo mimba sio yangu, sikutambui Sia. Huyo mtoto akizaliwa tutaenda kupima”
“Tena sio mtoto akizaliwa, ni watoto maana watakuwa mapacha tena wakike na wakiume. Mmoja ataitwa Erick na mwingine Erica, si itapendeza eeeh!”
“Achana na mimi”
Erick aliondoka mahali pale na kupanda gari yake ila alikuwa na mawazo mengi sana, bado hakukubaliana na swala kuwa ile mimba ni yake maana akikumbuka mara ya mwisho na Sia alitumia kinga, na muda mrefu tayari ulishapita kwakweli hakukubaliana na hilo swala.
Muda huo aliamua kuondoka kwenda kwa Yule rafiki yake daktari ili kumuuliza vizuri.

Leo Steve alikuwa amepooza sana maana tangu jana hakutoka nyumbani kwao, ilibidi Dora amuulize mdogo wake kuwa ana tatizo gani maana toka alitokomea kwa Sia ni jana tu ndio alilala nyumbani kwao,
“Mdogo wangu, nikikwambia umerogwa unakataa haya nakubali hujarogwa ni mapenzi yako kwa Yule dada. Haya leo vipi upo nyumbani na mawazo kibao”
“Sia kaniambia niondoke kwake na nirudi nikiwa nimepata kazi maana hawezi kuishi na mwanaume asiye na kazi”
“Huyo Sia wakati anakuachia wewe kula tunda lenye dawa hakujiongeza kuwa huna kazi? Yani wanawake bhana wana mambo ya ajabu sana. Kashachanganya akili yako na bado anaendelea kukuchanganya zaidi. Eeeeh kazi wewe utaipata wapi?”
“Nitafutie kazi basi dada”
“Mi mwenyewe unavyoniona hivi ni kazi yani sina mbele wala nyuma ila nitakuulizia mdogo wangu ila dah Sia angekubali kwenda kwenye maombi mdogo wangu ungefunguka yani ungefunguka kabisa kabisa, sema hutaki kukubali kuwa umerogwa”
“Ndio sijarogwa mimi”
“Basi ondoa hayo mawazo, yule Sia asikubabaishe wewe siku mvizie akiwa na watu unajitokeza mbale yao umesikia”
“Nijitokeze vipi?”
“Unawaambia watu kuwa unamahusiano na Sia”
Mara simu yake ikaita na kuipokea na alipomaliza kuongea nayo alimuaga mdogo wake kuwa anatoka kidogo,
“Unaenda wapi dada?”
“Mimi mtoto wa kike kumbuka, siwezi kuulizwa ninapoenda”
Basi alienda kujiandaa kisha akaondoka, ile simu ni James alimpigia kwahiyo alienda kukutana nae, kwa kipindi hiko James aliona mtu pekee wa kumgfariji ni Dora maana yeye hakujua kuwa Dora ndio alimletea ugonjwa ule sababu alikuwa na wanawake wengi kwahiyo hata aliletewa ugonjwa na nani hakujua kabisa, kwahiyo alimuita Dora ili wale wanywe kisha ndio warudi kwenye nyumba zao.

Rahim leo alienda mwenyewe kuonana na Zainabu maana mar azote huwa anaenda na Babuu, na huwa ni Babuu ndio anaongea. Basi alimsalimia na kuanza kuongea nae,
“Zainabu, samahani kama nakukosea ila nimeshindwa kuvumilia kwa hakika nakuhitaji, yani nahitaji uwe mke wangu wa ndoa, nakupenda sana”
Zainabu akacheka sana na kumwambia,
“Naomba nitajie aya moya ya kwenye Kuran”
“Yametoka wapi mambo hayo jamani eeeh! Mi nakwambia mambo mengine na wewe unasema vitu vingine”
“Ila si ulisema wewe ni Mwislamu safi, sasa mbona nimekuuliza kitu chepesi sana ambacho hata mtoto mdogo anajua. Inamaana wewe hukusoma Madrassa?”
“Nisome wapi, baba na mama ni kweli ni Waislamu ila hawakuishi pamoja wala hawakuoana ilipelekea mama yangu kuishi na mwanaume mwingine ambaye ni baba wa mdogo wangu, Yule mwanaume alikuwa Mkristo, huko Madrassa ningeenda muda upi? Na mama kaja kuolewa kabadili na dini kabisa, mambo mengine unanipa tu mitihani ambayo ni wazi siwezi kuifanya”
“Haya, Msikitini je? Maiwaidha hujawahi kusikiliza wewe?”
“Mimi nimeshi Marekani, hayo mawaidha ningeyasikia wapi?”
“Hakuna mji ambao hauna Misikiti labda kama ulikuwa huendi Msikitini!”
“Zainabu, habari hizo hapana unajua nikiwa na wewe nitaweza kuyajua yote hayo! Na utafanya niwe Mwislamu safi sasa, kuliko kuniuliza maswali ya kunikandamiza kwa kipindi hiki. Mimi nakupenda na ninahitaji uwe mke wangu, tafadhali usiniletee propaganda zingine”
“Sawa, jambo rahisi kabisa njoo kwa wazazi wangu na ufanye taratibu zote unioe maswala ya kuniimbia nyimbo za nakupenda wala sitaki kuyasikia”
Zainabu akaondoka zake na kumuacha Rahim mwenyewe, alifikiri Rahim anashindwa kufanya kile alichokisema, ni kinyume maana Rahim aliondoka pale muda ule ule na alikuwa na lengo la kwenda kuongea na mama yake juu ya swala hilo.
 
SEHEMU YA 403


Erick alienda hadi kwa rafiki yake hospitali na kumkuta baada ya kumalizana na wagonjwa sasa, alienda kukaa na rafiki yake kuongea nae,
“Yani Tom bhana nina tatizo”
“Lipi hilo”
“Yule msichana wangu wa zamani wa kuitwa Sia si unamkumbuka Yule!”
“Namkumbuka ndio, kwani kafanyaje?”
Basi Erick alianza kumueleza kuhusu Sia, yani kuhusu mimba aliyosema anayo ili asikie ushauri kutoka kwa rafiki yake huyo, basi Yule rafiki yake alianza kumshauri,
“Cha kukushauri huyo binti mkapime ultrasound ili ujue tu mimba ina muda gani wala usisubiri mtoto azaliwe sijui nini, yani wewe kapime nae tu hiyo utajua uongo wake maana unajua vizuri toka umekutana nae ni kipindi gani kimepita halafu yeye anasema ana mimba ni ya muda gani tena mlete hapa hapa tumpime wala asitake kukudanganya rafiki yangu”
“Sawa nashukuru sana Tom, yani huyu binti sina hamu nae loh! Kajua mimi nimerudiana na mchumba wangu basi ndio wivu mpaka kutaka kunisingizia mimba”
“Kwanza Kondomu ililetwa kwaajili ya kuzuia mimba, yani asilimia mia moja kondomu kazi yake ni kuzuia mimba ila wala tusizunguke yani tupime muda wa mimba tu muache ajidai ila muda wa mimba utamuumbua”
“Na kama alipata mimba kipindi ambacho yupo nami ila alipata kwa mwanaume mwingine?”
“Erick rafiki yangu, vipimo vipo tutajua tu.Usiwe na mashaka rafiki yangu”
Basi Erick alifurahi pale na kuondoka akiagana na rafiki yake kwani kwa asilimia mia moja alikuwa na uhakika kuwa ile mimba ya Sia sio ya kwake.
Wakati anaondoka alikutana na Dora njiani na kusimamisha gari lake ili asalimiane nae, alimpakiza kwenye gari lake kwani alitaka pia kuulizia maendeleo ya mdogo nwake,
“Mwenzangu Steve ndio kazamia kwa Sia balaa, majuzi ndio kamfukuza mdogo wangu eti mpaka apate kazi maana hawezi kuishi na mwanaume asiye na kazi”
“Kwahiyo huyo mdogo wako alikuwa anaishi kwa Sia?”
“Ndio, wanapika na kupakua yani waliishi kama mke na mume”
Hapo akili ya Erick ilifunguka kiasi, kisha alianza kumuuliza Dora kuhusu baba yake,
“Eeeh na mzee Jimmy una mahusiano nae yapi?”
“Yule baba yako ni buzi langu”
“Buzi lako kivipi?”
“Yani ni mpenzi wangu”
“Haiwezekani Dora, baba yangu atembee na wewe!”
“Ukatae ukubali habari ndio hiyo, Yule baba yako alikuwa akimtaka Erica ila Erica hakuwahi kumkubali basi babako akaamua kumalizia hamu zake kwangu”
“Unaongea utumbo tu, hebu shuka kwenye gari yangu”
“Huniamini ila nitakuaminisha, siku sio nyingi utaamini niyasemayo”
Kisha Dora alishuka kwenye ile gari ya Erick na kuondoka zake.

Erick alienda kwao huku akiongea mwenyewe kuwa haiwezekani baba yake awe na mahusiano na Dora, hata Tumaini alipofika alimueleza jinsi alivyokutana na Dora na jinsi Dora alivyomwambia.
“Dora ni mjinga sana, hivi baba yetu anaweza kuwa na mahusiano naye?”
“Haiwezekani yani haiwezekani kabisa Tumaini, hata kama baba alitaka kumuoa Erica ila haiwezekani kuwa na mahusiano na baba yetu”
“Au katumwa na Erica akwambie hivyo?”
“Hapana napo nakataa, Erica hawezi kufanya huo upuuzi”
“Mmmh unavyomkatalia huyo Erica kama malaika vile na hawezi kutenda lolote baya. Ila tutaona”
Basi waliongea ongea na siku hiyo baba yao aliwahi kurudi na kuwaita ili kuongea nao tena,
“Kwasasa baba yenu naendelea salama kabisa, jamani yaliyopita sitaki kuyasikia kwenye nyumba yangu. Ile familia hamjui tu ni kiasi gani imenila, mimi sikuwa mjinga kutaka kuoa pale. Ila tuachane na mambo hayi kabisa, nilichowaitia ni kuhusu harusi yako Erick na Sia”
Erick alishangaa sana na kumkatalia baba yake kuwa hawezi kumuoa Sia ila baba yake alimwambia jambo moja tu,
“Ukitaka utamuoa Sia, usipotaka utamuoa. Mambo ya mjukuu wangu kulelewa mbalimbali kama malezi mliyoyapata nyie sitaki. Nimemaliza”
Kisha baba yao akainuka na kuondoka zake, Tumaini alimuangalia Erick na kumuuliza,
“Eeeeh sasa utachukua maamuzi gani?”
“Sina maamuzi yoyote, si yeye anababaishwa na mimba ya Sia! Basi Erica pia ana mimba yangu”
Baba yao alitoka ndani na kuuliza kwa mshangao,
“Unasema nini?”


Kisha baba yao akainuka na kuondoka zake, Tumaini alimuangalia Erick na kumuuliza,
“Eeeeh sasa utachukua maamuzi gani?”
“Sina maamuzi yoyote, si yeye anababaishwa na mimba ya Sia! Basi Erica pia ana mimba yangu”
Baba yao alitoka ndani na kuuliza kwa mshangao,
“Unasema nini?”
Tumaini na Erick wakaangaliana kwa muda, kisha Tumaini akaamua kuua ile habari kwani ilikuwa ni usiku na akadhani kusema kuwa Erica ana mimba ni kumuongezea ugonjwa huyu baba yao, basi akasema
“Hamna kitu baba, tulikuwa tunaongelea mambo yet utu”
“Mambo yenu wakati nimesikia mkisema Erica!”
“Hamna baba hatujamtaja mbona”
“Nyie watoto nadhani hamuelewi maumivu yangu ndiomana mnasema sema tu hapa. Mimi huyo Erica kamwe siwezi mtambua kama mke wa Erick ila nitamtambua kama mke wangu mtarajiwa, wewe Erick kama unahitaji kupata radhi zangu endelea kucheza na mama yako Erica, nimemaliza”
Erick alitaka kujibu kitu ila Tumaini alimzuia, alipoondoka baba yao alimtaka tu kaka yake akalale na waongee kesho kuhusu yale mambo.
Erick aliingia chumbani kwake akiwa amechukia sana maana pale ndio ilitokea udhihirisho kabisa kuwa baba yake hataki yeye awe na Erica, akajisemea,
“Na atataka tu, Mungu nae anajuaga mambo yani mara moja tu Erica kadaka mimba yangu na ile mimba ndio itakuwa kigezo kizuri cha mimi na Erica kuoana. Yeye kama anataka kuchangia mwanamke na mimi akamuoe Sia huko”
Alichukia hadi alijikuta akiongea hovyo na kulala ila alilala huku amechukia sana.
Kitendo kile kilifanya siku hiyo Erick acheelewe kuamka, sema sababu biashara zilikuwa zake kwahiyo hakupata mawazo sana, akaoga na kutoka nje akamkuta dada yake Tumaini yupo mezani akinywa chai ambapo alimsalimia na Tumaini akamwambia wajumuike pamoja kunywa chai.
“Unafikiri najisikia basi hata kunywa chai, sijisikii hata chai naiona ya uchungu”
“Erick usifanye hivyo kaka yangu, hebu njoo kwanza tuongee kama familia”
“Na wewe utaniambia nini na humpendi Erica!”
“Hivi hujui kama nimebadilika, hata nisingemtaka Erica ni wazi nisingemtaka na Sia pia. Njoo tuongee bhana, sisi ni familia inatakiwa letu liwe moja ndio tutashinda”
Basi Erick alikaa pale mezani ambapo Tumaini alimmiminia chai na kumuwekea ili apashe tumbo na kuanza kuongea nae,
“Eeeh hebu tuongee vizuri, kwahiyo Erica ana mimba yako?”
“Ndio Erica ana mimba yangu”
“”Ila una uhakika Erick? Isije ikawa kakudanganya tu au ana mimba ya mtu mwingine?”
“Tumaini sikia, nampenda sana Erica yani nampenda sana. Kumbuka nimejitolea kumlea Yule mtoto wake Angel, nimeamua kujitoa na kumfanya kama mwanangu wa kumzaa, hivi Erica awe ni mwanamke wa aina gani anisingizie mimba mwanaume ambaye nina utu kama mimi? Kwani akisema amebeba mimba ya mtu mwingine unafikiri nitamuacha? Nitachukia ila nampenda sana kumuacha siwezi”
“Mmmmh mapenzi ya hivyo sijawahi kuyaona toka dunia iumbwe, basi tuachane na hayo. Tuzungumzie swala la baba sasa”
“Halafu wewe usiku umeleta kidomo domo chako, mimi nilitaka kumueleza ukweli Yule mzee”
“Tatizo sio kumueleza ukweli, tatizo mzee wetu ana presha na unalijua hilo”
“Kwahiyo presha ya huyo mzee ni kwa habari za Erica tu au?”
“Erick, Yule ni baba yetu hivi jana ungemwambia angepandisha tena presha ingekuwa tatizo kwa nani? Kama sio sisi tungehangaika tena, tunaweza kuongea mengi kwasasa sababu tunamuona, unaweza sema hata bora afe sababu tunamuona ila akifa tutashikana mashati hapa, ukisikia kuwehuka ndio hapa, hatukatai kufa kupo basi afe kwa ahadi yake ila kisije kuwa kisingizio kuwa sisi tumesababusha kifo cha mzee wetu, sio picha nzuri kwakweli”
“Sasa Tumaini, hebu niambie cha kufanya yani huwa najikuta natamani tu kumjibu huyu mzee”
“Cha kufanya ni kuongea kwa busara na huyu mzee, kwasasa tunatakiwa kuweka nae ukaribu na tumuulize kuwa kwanini anamng’ang’ania Erica, halafu tujue jinsi ya kumuweka sawa ili ajue kuwa Erica hamuhitaji, anayekuhitaji ni wewe yani tujue jinsi ya kuweka sawa saikolojia ya baba yetu. Bado tunamtegemea huyu mzee Erick, wala usitumie hasira mdogo wangu najua inauma ila tu kuwa makini”
“Sawa nimekuelewa, basi leo jioni akirudi nitajaribu kuwa nae sawa”
“Hivyo ni vizuri mdogo wangu”
Basi Erick alimaliza ile chai na kuagana na dada yake maana nae alikuwa akijiandaa kutoka.
 
SEHEMU YA 404

Kwa kipindi hiko Erica alikuwa kwao ila hakuwa na raha kabisa yani ukimuona unajua kabisa kuwa huyu mtu anasumbuliwa na mawazo, basi siku hiyo alifika dada yake Mage na walianza kumueleza yaliyotukia.
Erica alikuwa chumbani na kusikia yale ambayo Mage anaelezewa, basi akaitwa na alijua tu kuwa anaenda kusemwa,basi akatoka ili kuwasikiliza, ambapo Yule dada yake mkubwa alianza kuongea,
“Erica, katika pitapita zangu zote sijawahi kukutana na majanga aina yako. Hivi nikuulize tu, hujawahi kutembea na huyo baba mkwe wako?”
“Sijawahi dada”
“Tutaaminije ikiwa ndugu yako Derick tu ulitembea nae na nikakuuliza ukakataa katakata kuwa hujawahi kutembea nae kumbe ulitembea nae. Na kuhusu huyo mzee tutajuaje?”
Ndio hapa Bite naye akasikia vizuri swala la Erica kutembea na Derick, basi akasema kwa mshangao,
“Kheee Erica kumbe ulitembea hadi na Derick ndiomana mama anamtimuaga hapa, loh mdogo wangu mchafu wewe”
Mage akaongezea,
“Kwani unafikiri ni mchafu kidogo, mengine si mama yake anamfichia hapa. Unaambiwa huyo ukoo wa huyo Rahim yani baba yake Angel kashaumaliza wote, inawezekana kaka wa watu alihitaji kumuoa ila kila akikumbuka kuwa Erica kamaliza ukoo wao wote hana hamu. Yani huyu Erica usimuone hivi, ana maovu kushinda wote humu”
“Khee kwa mtindo huo anafikiri huyo Erick atamuoa? Kila mwanaume anapenda kupata mwanamke aliyetulia ila macho juu juu kama unatafuta mitambo kuna atakayekuhitaji? Yani utajikuta unazeekea nyumbani”
“Ni kweli Bite, asipoangalia huyu kazi yake itakuwa kusherekea harusi za wenzie tu, kamuendekeza Yule shoga yake malaya wa dunia”
“Ila ukitembea na mwizi na wewe ni mwizi, yani huyu Erica kanivunja maini kabisa, hakuna cha ndoa hapa wala nini”
Mama yao ilibidi aingilie kati maana walikuwa wakimkandamiza sana mdogo wao
“Hivi na nyie toka muanze kuaongea hamna mada nyingine za kujadili jamani eeeh! Sijui ndoa hamna, sijui hajatulia, sijui nini na nini haya sasa nyie mliotulia ndoa zenu ziko wapi? Wewe Bite imekushinda hiyo, na wewe Mage unaishi tu kwa taratibu za kidini ila ndoa yako ilishakata roho, hebu muacheni mwenzenu. Mimi Erica swala langu kwako ni moja tu, nahitaji kumuona tena Erick hapa niongee nae mwenyewe, nadhani unanielewa”
“Nimekuelewa mama”
Erica aliinuka na kwenda chumbani ila alikuwa na uchungu sana moyoni mwake, aliamua muda huo kumpigia simu Erick ili angalau apooze moyo wake.
“Erick nimekumiss”
“Hata mimi nakumiss sana Erica, ila nashindwa kuja kwenu kwasasa. Basi naomba uje tukutane, nikuone tu kipenzi change”
“Basi njoo mitaa ya kwetu”
“Sawa. Nikifika mitaa ya kwenu nitakupigia simu uje”
Basi Erica alikata ile simu huku akitabasamu na kusahau yote waliyokuwa wakimsema sebleni.

Jioni ilipofika Erick alimtafuta Erica kisha alienda kuonana nae kama ambavyo alipanga kukutana nae, ila kwasasa ilionyesha kuwa Erick kakubaliana na hali halisi kuwa ile mimba ya Erica ni yake maana alivyokaa nae tu kwenye gari cha kwanza alimuuliza,
“Mtoto wetu wa tumboni hajambo?”
Erica alitabasamu na kuitikia kuwa hajambo, kisha Erick aliulizia na maendeleo ya Angel,
“Kiukweli Angel kakumiss sana”
“Dah! Kweli sijatoka siku nyingi na mwanangu, basi lini upo tayari tutoke?”
“Hata kesho”
“Hahaha, basi muandae Angel tutoke nae. Twende mahali tukafurahi pamoja kama familia, yaliyotokea kati yetu tusiyazungumzie kwasasa ila tujali afya za watoto wetu”
Erica alitabasamu kwani aliona raha sana kwa wakati huo, ila muda ule ule simu ya Erick iliita na alipoitazama aliona ni baba yake anapiga, aliamua kuipokea na kuongea nayo
“Erick, nakuhitaji nyumbani muda huu”
“Ila nipo mbali baba”
“Nimekwambia nakuhitaji nyumbani muda huu”
Kisha akakata simu, na kumuacha Erick akimuangalia tu Erica kisha akamwambia
“Ni baba yangu huyo, anahitaji niende nyumbani sijui ana lipi la kusema”
“Mmmh!”
Erica aliguna tu ila Erick aliongea,
“Katika pitapita zangu zote sikuwahi kukutana hata na ndugu yako na nimekuwa makini sana kwani uliishi sana moyoni mwangu na niliamini siku moja utakuwa mke wangu, ila mwenzangu bado najiuliza ulimkubali vipi mtu mzima kama baba yangu? Je hela zake ndio zilikuzuzua?”
“Erick, tafadhali usinikandamize nakuomba, kwetu wanikandamize, nahitaji faraja kwako ila nawe unanikandamiza unataka niwe mtu wa aina gani eeeh! Usinikandamize nakuomba. Nishakwambia ukweli, sijawahi kuwa na mahusiano na huyo mzee ila bado unakazania kitu hiko hiko”
“Erica, Napata maswali sana sababu ulinilamba milioni tano ukasema kuwa Yule mzee alikupa hela na ukatumia kwahiyo mke wake anataka, baba yangu hana mke kwahiyo ulinipiga change la macho?”
“Sikukupiga change la macho Erick, ni kwavile tu siku ile mambo yaliingiliana ukashindwa kuniuliza risiti ila nitakuletea risiti hiyo kesho tunavyoonana, nilisema mkewe ila hakuwa mke ni hawara ambaye ni Dora na alinidai hela za Yule mzee sababu ni wake”
“Kwahiyo kweli baba yangu alikuwa na mahusiano na Dora?”
“Sio alikuwa, hadi sasa bado ana mahusiano na Dora”
“Weee haiwezekani, sema kingine Erica ila kwavile hapana na nikigundua hivyo Yule mzee sitajali presha yake, yani nitafunga ndoa na wewe haraka sana”
Erica alitabasamu kwani ule ulikuwa ni ukweli kwahiyo ataolewa na Erick, lilikuwa jambo la furaha sana kwake. Basi kwa muda huo Erick alimrudisha Erica kwao kisha kuagana nae na yeye kurudi kwao.
Erica aliingia kwao huku akitabasamu na familia yake ilikuwepo, alianza mama yake kumuuliza,
“Haya mwenzetu hiyo furaha ni lazima umetoka kukutana na Erick”
Bite akachangia,
“Jamani Erica hukomi tu, ukipata kimimba kingine ndio akili itakukaa sawa maana utatulia”
Erica aliwaacha na kuelekea chumbani kwake ambapo Mage aliuliza,
“Jamani huko kukimbilia chumbani ni kawaida au kuna kitu?”
“Kitu gani unakihisi Mage?”
“Mmmh sijui, jamani ngoja niage. Naenda kwangu, nitakuja tena”
Basi Mage akawaaga pale na kuondoka zake.
 
SEHEMU YA 405


Erick alifika kwao na kumkuta baba yake yupo sebleni na Tumaini kwahiyo alimsalimia na kujumuika nae kwenye maongezi,
“Yani Erick umejichelewesha huko balaa, nilihitaji kumaliza mambo leo leo ila wewe umechelewesha mambo”
“Mambi gani baba?”
“Nishaenda Kanisani kuandikisha ndoa yako na Sia”
Erick alimshangaa baba yake, kuwa amechanganyikiwa au vipi, akamuuliza
“Baba, kwanini ufanye maamuzi bila kunishirikisha mwenyewe?”
“Nishaongea na Mchungaji kwahiyo kesho tutatoka hapa kwenye mida ya saa nne tutaelekea kumchukua Sia kisha tutaenda kanisani maana kuna maswali mtaulizwa kwanza”
“Baba jamani hata kama hujawahi kuoa ila ndoa sio kama hivyo ufanyavyo wewe”
“Kwani wewe tatizo lako nini, nisjhakwambia sitaki mjukuu wangu apate malezi kama mliyoyapata nyie kwa kutokuishi na baba na mama. Nahitaji mjukuu wangu apate mapenzi ya wazazi wawili”
“Hapana baba, siwezi kumuoa Sia”
“Kwanini huwezi kumuoa Sia? Kwasababu ya Erica eeeh!”
Erick akawa kimya tu , kisha baba yake akaendelea kuongea,
“Erick, ujinga kwangu sitaki. Hivi wewe mtoto una laana au ni kitu gani? Hivi upite palepale alipopita baba yako, mbona ni laana hiyo?”
Tumaini na Erick wakaangalia na kuona wakiendelea kuongea na huyo mzee wao basi kuna maneno mengine atayazungumza ambayo sio sawa kabisa, ila Yule mzee akainuka na kusema,
“Erick, utake Sia utamuoa, na hutaki utamuoa. Nimemaliza, saizi natoka kidogo nitarudi baadae”
Tumaini akamwambia,
“Lakini baba muda umeenda saa hizi?”
“Acha nitoke kidogo akili yangu iwe sawa, watoto mnanichanganya nyie, sasa mimi sina mke, nataka kuoa mnaniletea mambo ya ajabu na kuzua magonjwa ya ajabu kwenye mwili wangu nab ado mnaendelea kumtaja huyo mtu katika masikio yangu. Yani nyie watoto hapana aisee”
Basi akaondoka zake, na kubaki Erick na Tumaini, kwakweli Erick alianza kulalamika,
“Yani huyu mzee ndio cha kuniitia hiki upesi upesi jamani, aliona wapi kuna harusi ya kulazimishana hivi eti kesho tunaenda kwa Mchungaji kuzungumzia ndoa jamani, huyu mzee ndiomana alikurupuka kwenda kwakina Erica bila kujitambulisha kwanza, hajafuata mila wala kitu gani yeye anajipeleka tu kuchukua mke, tuseme tatizo ni kutokuwahi kuoa au kachanganyikiwa tu jamani!”
“Usiseme kwa nguvu Erick, ila wewe cha kumkomesha baba kesho nenda nae huko Kanisani halafu Mchungaji akiuliza unagoma kabisa kwamba kuoa hutaki ili asiandikishe hiyo ndoa”
“Tumaini, siendi cha Kanisani wala nini kujisumbua, kwanza kesho nimepanga kwenda kutembea na kipenzi cha moyo wangu. Huyu mzee wakati wake umepita, hivi sikukuuliza mama yako ulivyomwambia habari za huyu mzee kutaka kumuoa Erica alisemaje?”
“Jamani mama kacheka balaa, kasema huyu mzee ujana wake wote alikuwa wapi kuoa. Eti anakumbuka shuka wakati kumeshakucha”
“Na shuka lenyewe tushajifunika wengine, halafu akasema nini kuhusu mchumba ambaye mimi namtaka na baba anamtaka”
Basi Tumaini akaanza kumuelezea Erick jinsi mama yake alivyosema kwa kicheko kikubwa sana.
“Kwahiyo mamako angekuwa mimi angeoa bila kujali!”
“Yani kasema angeoa kumkomesha, yani mama yangu kacheka sana. Yani sijui baba alimfanyaga nini mama kwenye ujana wake maana anavyomsemaga vibaya balaa. Ila hata mamako Erick huwa hampendi baba”
“Ni kweli hampendi tena hampendi kabisa, tena umenikumbusha jambo. Mama si anamchukia Erica, nikitaka ampende nitamwambia hili swala la baba kutaka kumuoa Erica, subiri arudi tu nimwambie najua kwajinsi mama anavyomchukia baba basi atafanya kila jitihada ili mimi na Erica tuoane”
“Huyu baba sijui ana matatizo gani, sio kitu cha kawaida kwa mama zetu wote kumchukia lazima kuna kitu kibaya aliwatenda”
“Tena mama yangu ndio zaidi maana inaonyesha hata hamu ya kuolewa tena hakuwa nayo ndiomana hadi leo nipo mwenyewe. Ngoja arudi nimwambie habari hizi, huyu mzee tutaona hiyo presha yake.”
Wakacheka sana pale ndani maana kwa kipindi hiko Erick na dada yake Tumaini walipatana vilivyo.

Erica kabla ya kulala alifikiria jambo, akaona ni vyema ampigie simu Dora kwani yale maneno ya Erick kuwa akigundua babake ana mahusiano na Dora basi atamuoa haraka iwezekanavyo, kwahiyo kuliko mimba igundulike wakati yupo nyumbani aliona ni vyema amwambie Dora afanye jambo na mzee Jimmy agundulike kwa watoto wake ili Erick amuoe kwa haraka.
Basi alipiga simu muda huo na Dora alipokea simu ile,
“Niambie Erica, kuna jipya leo maana siku hizi hunipigii simu?”
“Aaah Dora, nisaidie familia yam zee Jimmy ijue ukweli maana wanahisi kuwa ni mimi ndiye nilikuwa na mahusiano na mzee Jimmy. Nisaidie wajue kuwa ni wewe”
“Nimewaambia ila wananibishia, sema subiri kuna bomu nimeliandaa yani hilo mzee Jimmy hachomoki kabisa, nitahakikisha hao watoto wake wanaomtetea wanaona mambo ambayo baba yao huyatenda. Tena kuna dada huyo ndio alikuwa anatembea na mzee Jimmy, nimemjua pia si unajua mimi ni kama mpelelezi”
“Nakuaminia Dora, yani huyu mzee ananipa mawazo sana kwakweli”
“Punguza presha rafiki yangu, ile milioni kumi huwa siisahau hadi kesho kwahiyo kuwa mpole tu ndugu yangu yani hivi karibuni huyo mzee ataumbuka”
Erica alifurahi sana kusikia hivyo na kuagana na rafika ila akakumbuka kuhusu habari za mdogo wake Dora ilibidi amuulizie pia,
“Vipi Steve nae?”
“Weee yani Yule ndio haoni wala hasikii, tulikuwa nae hapa siku zote kapooza hatari maana kaambiwa na Sia kuwa atafute kazi kwanza ila leo hajakubali kaenda hivyo hivyo jamani huyu mtu ataanza hadi kuniibia hela zangu ndani apelike kwa Sia. Najuta na habari za waganga jamani dah! Usiniulize sana ila ndio hivyo najuta, kwaheri Erica ngoja nilale tu”
Basi Erica alikata simu ila alifurahi kuongea na Dora maana wale walikuwa wanamkosesha raha sana. Akaamua kulala sasa.
Palivyokucha aliwasiliana na Erick kuwa ajiandae anaenda kumchukua, alishangaa kuona ni mapema vile, alimuandaa na mwanae na kumwambia mama yake kuwa anaenda kliniki, hakutaka kumwambia ukweli muda ule maana alijua wazi kuwa ni lazima angemrudisha kuwa asiende popote. Alipanga badae ndio ampigie simu kuwa atachelewa kurudi.
Basi Erick alivyofika karibu na kwao, aliaga vizuri na kutoka na mwanae kisha Erick alipanda nae kwenye gari na kuondoka zao.
Na moja kwa moja walienda kwenye hoteli ambayo ilikuwa na michezo mbalimbali ya watoto ili kumfurahisha Angel.

Mzee Jimmy aliamka na kujiandaa vizuri kabisa kwaajili ya kutoka na Erick wampitie na Sian a waende Kanisani, alishangaa alimuita bila kuitikiwa ikabidi amuite Tumaini na kumuuliza,
“Katoka asubuhi sana, sijui kaenda wapi”
“Mtoto mjinga sana huyu, yani tunapanga hivi halafu anafanya vile”
Basi Mzee Jimmy akaondoka zake na moja kwa moja alienda kwakina Sia, alivyofika alimkuta Steve yupo nje akiosha vyombo ila kabla hajaongea nae vizuri alitoka Sian a kumsalimia Yule mzee ambapo aliulizia kuhusu Yule kijana,
“Ni mdogo wangu huyu”
“Aaah! Sawa basi njoo kidogo tuongee”
Sia akasogea pembeni na Mzee Jimmy ambapo Mzee Jimmy alimueleza lengo lake la kutaka yeye na Erick waoane na kutaka siku hiyo waende kwa Mchungaji ili kusaini kuhusu ndoa yao.
“Tulipanga vizuri ila Erick leo kaondoka asubuhi kabisa jamani, yani akjifanya kusahau kama nimepanga nae kuhusu hili swala”
“Dah yani Erick anachanganywa sana na Erica Yule anasahau kuwa mimi ndiye mwenye mimba yake halali”
“Kwani Erica nae ana mimba?”
“Ndio, Erica ana mimba sasa nadhani Erica kamdanganya Erick kuwa ile mimba ni yake ndiomana kamchanganya akili. Erick anaacha kuhudumia mimba yake ya halali huku anaenda kuhudumia mimba feki”
Yule mzee alianza kuondoka bila hata kuaga mpaka Sia alishangaa ila kilichomfanya aondoke vile ni kwamba swala la kusema kuwa Erica ana mimba lilimchanganya sana.
 
Back
Top Bottom