NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA
MTUNZI :
Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILRINI NANE : Dakika kumi na tano baadae yakaingia magari matatu, aina ya STCAV (Special Force Team Carrier Amoured Vehicle) ambayo yalikuwa wazi, na kufanya Deus aweze kuwaona askari wa nne wenye silaha, kwa kila gari moja, kati ya magari manne, wakiwa wamevaa miwani, nyeusi zenye camera, zenye uwezo wa kurecord na kutuma matukio moja kwa moja, wakiongozwa na askari mwenye cheo cha luten. ENDELEA……
Mara baada ya kushuka tu, wakatanyika na kujigawa makundi mawili nane wakikaa katika muundo wa duara wakilizunguka eneo lile na mitutu ya silaha zao aina ya Micker galiry zikielekezwa kwenye vichaka na mapori tayari kukabiliana na chochote kitakacho jitokeza, huku wengine nane akiwepo kiongozi wao, yaani yule luten mwenye nyota mbili kila upande wa kola ya shati lake, (hii ni tofauti na Tanzania, wao cheo uweka kwenye ukosi wa shati) wakikagua na kuhakikisha kama kuna chochote kilichobakia eneo lile lililozungukwa na wenzao,
SA Special Force, wanafanikiwa kukagua kwa sekunde chache tu, kisha wanasimama na kutazamana kwa mshangao kabla hawaja mtazama Deus aliesimama akiwatazama, huku ameshikilia AK 47 mkononi mwake, wawili wakamsogelea Deus, akiwepo yule luten na mwenzie mwenye cheo cha koplo, na Deus alipoona wame msogelea akapiga salut “good after noon lieutenant?” alisalimia Deus, akimaanisha habari za mchana luteni, naomba niweke sawa hapo.
Katika nchi nyingi ambazo hazitumii lugha ya English wanajeshi huitana kwa vyeo vyao, na wanapo pokea amri huitikia kwa jina la mheshimiwa yani Sir, hiyo pia ni kwa baadhi ya nchi zinazotumia Kiswahili, ila kwa nchi kama Tanzania utumika neno afande neno ambalo halina tafsiri kwa lugha yote duniani, ila ni neno ambalo waswahili walilidadavua toka kwenye neno AFFENDI toka katika lugha ya kituruki, kupitia askari wa sudani walioshiriki vita vya kwanza vya dunia, likiwa na maana ya neno KUSAMEHEWA, hiyo ni endapo utaweka I mwishoni mwa neno, na ukitoa I ikabaki AFFEND maana yake ni MSHIKAMANO, wakati neno hilo hilo ukilitaja hivyo kwa lugha ya English lina maana ya KUUDHI.
Hivyo kwa Deus ambae alisha kaa nchi kadhaa akifanya mafunzo, na hata hapa nchini Congo, alikutana na mataifa mbali mbali, anafahamu jinsi wenzao wanavyoitana, tofauti na nchini kwetu, OC akutane na RPC halafu aseme habari za asubuhi RPC, au koplo akutane na captain aseme habari yako captain, hakika nikosa la kinidhamu, maana neno afande lipo na linapaswa kutumika, ila kumbuka ni afande siyo affend au affendi.
“priate Nyati were is your back up?” aliuliza yule Luteni ambae kifuani kwake kwenye mfuko wa kulia shati lake, lilikuwa na jina limeandikwa, HD Thabo wa AS mwenye kuongoza makomando wa south Africa ambae alisoma jina la Deus kwenye tag yake iliyowekwa kwenye shati, juu ya mfuko wa kulia, akimaanisha kuulizia watu waliokuja kuwasaidia, “no sir, there is no any back up, you and your team is the only backup here” alijibu Deus kwa lugha ile ya English, sina hakika kama nimeandika kama walivyokuwa wanatamka, ila Deus alikuwa ana maanisha kuwa hapa kuwa na watu waliokuja kuwasaidia, zaidi ni kwamba yule lutent na team yake, ndio msaada pekee uliofika, “you mean all this you did by you self?” aliuliza liuetinant Thabo, kwa saut ya mshangao akiuliza kuwa “unamaana haya yote umefanya peke yako?” kumbuka muda wote huo bado zile chopa zilikuwa zinaendelea kufanya doria kule juu ya anga.
Ilishangaza sana, hata wale wengine waligeuka kuwatazama mkuu wao na private Deus Nyati, na kabla Deus hajajibu mwenzao mmoja akadakia, “Deus Frank Nyati i know this man, i met him in cuba at SF intake 116, course, he is a most derous special force in Africa” alisema mmoja wao aliekuwa na cheo cha private kama Deus, ambae alidai kuwa anamfahamu Deus na walikuwa wote cuba kwenye mafunzo ya Sepcial Force kundi la 116, na kwamba ni komando hatari kuliko wote Africa, yaani yeye alivyo amini, nikama mtu anavyo amini yanga ni hatari kuliko simba na mwingine akasema simba ni hatari kuliko yanga, hapo Deus akamtazama na kumwona askari huyo aliesema anamfahamu, walipokutana macho Deus akatabasau kidogo, ni kweli alimkumbuka, “good job Private” alisema yule luten, akimpongeza Deus.
Naam baada ya hapo yule luten akatoa simu ya upepo aina ya motorora ya ya kisasa, akapiga Head Quarter na kuwa julisha kuwa tayari wameshafika eneo la tukio na kwamba hakuna mateka alieshikiliwa na waasi, na wao wamekuta eneo liposalama, ni baada ya waasi kudhibitiwa na Speciali Force DF Nyati, toka Tanzania, nae akapewa maelekezo ya kurudi kambini, “ok! five minutes, to clear every thing” alisema yule luten, na hapo askari wale makomando toka Africa ya kusini, wakaakusanya kila walichoona kinafaa ikiwa pamoja na miili ya wale waasi, ambayo waliipakiza kwenye KAMAZ.
Ilikuwa ni kazi ya dakika tano kweli, “ok! listen to me, get in car for RTB” alisema yule Luteni, akimaanisha kuwa waingie kwenye magari, kwaajili ya RTB, yani Return To Base (kurudi kambini) askari wakaingia kwenye magari, huku wawili wakiingia kwenye KAMAZ, akiwepo yule koplo mmoja akiwa na private akiwa ndie dereva, wengine wakaingia kwenye magari yao yale madogo, huku Deus akiingia kwenye Toyota land Cruize walilokuja nalo pamoja na madoctor wake, ambao bado walikuwa wanamtazama kwa macho ya mshangao na kutoamini kwa kile alicho kifanya muda mfupi uliopita na mpaka hapo hakuna aliesema asante.
Safari ikaanza huku chopa zikiranda angani, hakika ilipendeza machoni pa wapiganaji, huku wale raia wakifunguliwa njia na kuendelea na safari zao, kila mmoja alimchukulia Deus kama shujaa hawakujuwa kuwa huo ndio mwanzo wa kuufikia mwisho wa utumishi wake jeshini.*******
Mashariki mwa congo katika jiji la Goma, kivu ya kaskazini mwa DRC, linaonekana gari aina Nissan patrol linatembea kwa speed kwenye barabara kuu iendayo Rwanda, kupitia mpaka wa Gisenyi, huku ndani yake kukiwa na mtu mmoja tu, ambae ni mzee wamakamo, aliekuwa anaendesha gari hilo kwa speed sana huku simu ikiwa sikioni, “naamini tutafanikiwa Chief ondoa shaka andaa mpago wa kukabidhiwa fedha” aliongea yule jamaa ambae ni mtu mzima, huku anapunguza mwendo kuikaribia barabara iendayo Linda hotel na maeneo ya ziwa Kivu, “lakini hakikisha mpango unaenda kama tulivyo panga na uwe makini kufwatilia kila wanacho ongea, endapo watatuma askari kwenda kuwa komboa tujulishe kabla mpango haujaanza, sisi tunazidi kusisitiza habari kwenye redio na tv zote kubwa duniani, ilikuwapa msukumo MONUSCO wa kutoa hizo fedha haraka” iliskika sauti yenye msisitizo toka upade wa pili wa simu.
Wakati huo tayari mzee huyo alikuwa anakata kona kulia, kuingia upande wa Linda hotel, “Ni sawa haina shida nitafanya hivyo, naamini nitawakuta wanaandaa fedha, madoctor watatu na askari mmoja siyo mchezo, lazima wachanganyikiwe” alisema yule jamaa kisha wakacheka kwa pamoja, huku mzee yule anakata kona kulia kuifwata barabara inayoelekea upande wa Linda hotel mpaka ziwa Kivu, “lakini bwana Seve una uhakika jamaa watatoa fedha?” aliuliza jamaa upande wapili wa simu, lakini katika hali ya furaha na kujiamini.
Sasa mzee huyu alieitwa Seve, ikiwa ni kifupi cha Sevelin, alipunguza wendo kulikaribia lango la eneo la majengo ya ofisi za MONUSCO, “ondoa shaka chief, fedha inapatikana pamoja na dawa mingi sana, vijana hawato hangaika matibabu” alisema kwa kujiamini bwana Seve, huku anasimamisha gari, mbele ya lango kubwa la blue bahari na maandishi makubwa, ya rangi nyeupe MONUSCO DU NORD KIVU, ikiwa na maana ya kwamba MONUSCO KIVU YA KASKAZINI, “imekaa poa sana, cha msingi hakikisha kila kitu kinaenda kama tulivyo panga” alisisitiza mtu upande wapili wasimu, na wakati huo geti lika funguliwa, wakaonekana askari waliovalia mavazi ya kijeshi, yanayo watabulisha utaifa wao wakuwa ni watanzania, sambamba na bendera begani mwao, huku bunduki aina ya SMG zikiwa zimeshikwa imara mikononi mwao, kofia za chuma rangi ya blue bahari, na bullet pluff vifuani mwao, “sawa chief, nimeshafika nitakupigia baadae” alisema Seve, ambae kwa mkadirio alikuwa na miaka kati ya hamsini mpaka hamsini na nne na kukata simu.
Wakati huo askari wawili wakaonekana wakilisogelea gari lile mmoja akiwa ameshika mine detector ambae alianza kulikagua gari, kitendo ambacho Seve aliona kama anacheleweshwa kwenda kujuwa kinachoendelea hukondani, “kitambulisho tafadhari” alisema yule askari mwingine, hapo haraka sana Seve akaonyesha kitambulisho chake ambacho kilimtambulisha kama mfanyakazi wa umoja wa taifa ofisi ya msimizi wa mipango ya kiraia.
Baada ya hapo wakamruhusu apite, na hapo gari lile aina ya NISSAN likaingia ndani, huku mzee yule akionyesha kitambulisho chake na kuelekea moja kwa moja mpaka mbele ya ofisi za wasimamizi wa maswala ya kijeshi wa umoja wa mataifa, ambapo aliwaona wenzake wakitembea kwa haraka kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano, wakiwepo maafisa wa majeshi mbali mbali ambayo yanashiriki operation ile ya kuondoa waasi kivu ya kaskazini, pia na maafisa wa kiraia wakike na wakiume, “yes! mambo yanapamba moto” alijisemea Seveline, usowake ukijawa na tabasamu, huku anashuka haraka toka kwenye gari na kuungana na wenzake kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano.*******
Beni Mavivi, ndani ya eneo la uwanja wa ndege, mbele ya ofisi za MONUSCO walionekana watu wengi sana, askari kwa raia, wafanyakazi wa airport na wafanyakazi wa MONUSCO wa maitafa mbali mbali, wahindi waarabu faransa wa filipino, na wenyeji yaani waafrica, wakiwa wamekaa kwa vikundi vikundi, wakijadiri tukio la kutekwa kwa madoctor wa WHO, pamoja na askari mmoja wa Tanzania, hakika sura za watu wale zilionekana kunyongea sana kasoro kijana mmoja tu ambae anafahamika kwa jina la Kisonge, ambae shuguri zake ni usafi katika ofisi za MONUSCO, yeye alionekana kuwa katika hali ya kawaida kabisa, “NALU siyo wamchezo wanatisha wale watu” alisema yule kijana, ambae katika kumbu kumbu zetu ndie alieenda kumpelekea Deus karatasi.
Kauli ile nikama ilimchomoka tu, na hakuna alietegemea kusikia kauli ilee kutoka miongoni mwao, hivyo karibu watu wote pale waligeuka na kumtazama kijana huyo, hata major Felix aliekuwa karibu yake, alimtazama kwa macho ya mashaka kijana huyu, huku yeye Felix na maafisa wachache toka Tanzania wakiwa wanajuwa kuwa tayari kijana wao ameshamaliza kazi, alitamani kumweleza jambo kijana yule mfagizi wa maofisini lakini kabla hajasema lolote wakaona magari mawili madogo ya FARDC yakiingia kwa mwendo wa speed ya kutisha, speed ambayo ingekutambulisha kuwa huko walikotoka hakukuwa salama, hakuna alieshangaa kwanini yanarudi magari mawilikati ya matano yaliyoondoka pale mavivi.
Naam ile magari yale yana simama tu, askari wakashuka toka kwenye magari yao, kila mmoja akawasogelea, akiwepo Kisonge alieonyesha hamu kubwa ya kujuwa kilichotokea, akihitaji kujuwa kilichotokea huko pori la Ituli, “kwa kweli ilikuwa hatari sana” alisema yule major ambae nikiongozi wa msafari uliotekwa na IDFNALU, Felix na wenzake waliokuwa wanajuwa kinachoendelea walimsikiliza Major huyo aliefahamika kwa jina la Kashumba, “ilikuwaje chief mbona wengine hawapo?” aliuliza yule kijana, swali ambalo liliwashangaza watu waliokuwepo pale maana kila mmoja alikuwa anafahamu kuwa wametekwa.
Hapo major Kashumba, akaanza kusimulia kilichotokea, tofauti na vile tulivyo shuhudia sisi, major Kashumba alisema kuwa, wakiwa njiani wakashtuka waasi wa NALU wakiibuka toka porini na silaha zao na kuanza kulishambulia gari la mbele, bahati nzuri askari wakaruka toka kwenye gari, na kukimbilia kwenye magari ambayo haya kushambuliwa, “tukalazimika kugeuza magari na kukimbia tulishindwa kugeuza gari kubwa kutokana na ufinyu wa barabara, ila yule mtanzania sijuwi kwanini alishindwa kugeuka na kuondoka, wakati ilionyesha wazi tuna shambuliwa, maana hata gari la mbele lilipigwa kombora” alisema Kashumba kwa sauti ambayo ungesema alikuwa katika masikitiko makubwa.
Habari ile iliwasikitisha wengi ila habari ile ilikuwa burudani kwa wakina Felix, ambao, walichekea kwapani, “ule Tanzania ni mzembe sana anashindwaje kukimbia ambushi, anasababisha wale madoctor wanaingia mikononi mwa Nalu” alisema Kisonge akishusha lawama kwa Deus hapo Major Felix uvumilivu ukafikia mwisho, maana alimsogelea Kisonge, na alipomfikia akasogeza mdomo sikioni mwake, “Deus hajawai kupoteza, subiri matokeo” alisema Felix na kumfanya Kisoge ambae hakutarajia ujumbe huo, ashtuke na kumtazama Felix kwa mshangao, ambae alimwona akiwa anatabasamu. ….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa …
NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa
jamii forums