🙏🙏🙏Nala kwanza nikimaliza naleta
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
🙏🙏🙏Nala kwanza nikimaliza naleta
hawa waleta hadithi wa JF kuwa wanaanza kwa kumwaga moto balaa non stop.. ila wakishapata wafuasi tu wanaanza kudengua visingizio vingi mwisho wanapotea ni suala la muda tu makelele ya lawama yataanza humu.!Leo umetuchuda sana
Ka episode kamoja tu.
Ni 🔥 🔥 🔥 🔥NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA THELATHINI NA MOJA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA THELATHINI : Haraka sana Kisonge akachungulia na macho yake yakaona magari sita yakiingia pale kwenye ofisi za UN, manne yakiwa ni STCAV, na moja Toyota Land Cruizer jeupe la UN na lile KAMAZ, lililoondoka na mizigo ya WHO, “haoooo wanaingia ni kweli wamerudi na kila kitu” alisema Kisonge kwa sauti ya kukata tamaaa…….endelea….
Huku bado anaendelea kuchungulia, ambapo aliona yale magari yakipitiliza na kuzunguka upande wa nyuma kabisa wa jengo la ofisi za MONUSCO, wakipita kwenye gate dogo lililoshikizwa kwenye kuta za uzio mdogo wa ofisi hizo. wenye eneo la mita za mraba arobaini kwa thelathini, “Imekuwaje wameweza kuchomoka hao! mbona taarifa za huyo mtanzania hazielezi kuwa ni mtu hatari hivyo! au walikuwa na silaha wakati haluhusiwi?” aliuliza Seveline kwa sauti ya nshangao iliyo hamaki, “kwakweli hata mimi nashangaa, yaani ukimwona mtu mwenyewe, utajiuliza amewezaje kupambana na wakina Kabhago” alisema Kashimba kwa sauti yakutilia mashaka, “kwahiyo unataka kusema lazima kuna msaada aliupata sehemu?” aliuliza Seveline kwa sauti ya ung’amuzi “pengine mpango ulisha gundulika na wakaamua watangulize majeshi, lakini kwa yule mmoja asingeweza kupambana na Kabhango” alisemama Kashumba kwa sauti yenye kuonyesha kuwa anaamini anachokisema, “hawawezi kuwa wajanja zaidi yetu, lazima walipie hii kuanzia huyo mtanzania mpaka MONUSCO kwa ujumla” alisema Seveline na kukata simu.********
Siku kama hizo huko #Mbogo Land, nyakati za mwisho za utawala wa king Eric wa pili, ambako mpaka mwaka huu wa 2014 walikuwa na jeshi imara, ambalo lilikuwa limesha shiriki kazi nyingi za nje ya nchi kwa ushirikiano wa nchi nyingine za umoja wa nchi za Africa, yaani AU, na hata za umoja wa mataifa, UN, moja ya operatio waliyoshiriki ilikuwa ni ile ya visiwa vya Comoro, miaka ya 2006/ 2007 nyingine ni huko Sudan, operation Darfu, pia siyo operation zote walikuwa wanapeleka askari nyingine walikuwa wanachangia vyakula na dawa, kwa chini shiriki.
Hii ilikuwa ni miaka minne toka King Elvis, aanze kutawala nchi hiyo ndogo na tajiri, king Elvis akionekana mwenye wasi wasi mwingi na mashaka juu ya jambo flani, alikuwa peke yake, ndani ya chumba chake kikubwa mfano wa ukumbi mdogo wa mikutano, chumba chenye kila kitu, licha ya kitanda kikubwa cha futi nane kwa nane, kilicho nakishiwa na uji wa dhahabu, kwenye kingo na miguu yake pia kulikuwa na seatting room, swimming poor, ofisi ndogo, na sehemu nyingine ambazo ni nimuhimu kwa maisha ya kila siku ya binadamu, kamavile dianing table, bar counter ndogo yenye shelfu zilizojaa vinywaji vya kila aina,
King Elvis wakwanza, aliekuwa amekaa peke yake chumbani mwake, mbele ya meza kubwa ya ofisi ndogo ya mle chumbani kwake, sura yake iliyojawa na mashaka akiwa ameinamisha kichwa kwenye meza akikodolea macho file (jarida) lililopo mezani kwake, jarida ambalo ni maalumu kwaajili ya taarifa toka katika jeshi lake la ulinzi la nchi yake yani ML Army ikiwa na maana ya #Mbogo_Land Army, ni wazi ilionyesha kuwa, taarifa ya leo haikuwa nzuri kwake, “inawezekana vipi haya mambo yanaendelea mpaka leo, imaana waziri wa ulinzi hawa kumwelewa tu, mbona changamoto zao zimesha tatuliwa?” alijiuliza King Elvis, kwa sauti ya chini yenye kuchanganyikiwa, huku akitazama karatasi ndani ya jarada lile, lenye majina hamsini na nane, yaliyopo chini ya kichwa cha habari, askari waliotoroka ML ARMY NA ML SA MWAKA 2013/14 “kwanini haya mambo yanatokea wakati huu wa uongozi wangu” aliongea Elvis mfalme kijana, mwenye umri mdogo kuwahi kungoza #mbogo_land, toka kuanzishwa kwake, akionyesha kushtushwa na taarifa ile.
Ukweli nikwamba kwa kupindi cha miezi kumi sasa kumekuwa na taarifa ya kuzuka kwa utoro mfululizo wa askari wa majeshi ya ulinzi na usalama wa nchi hiyo ya kifalme, yaani utoro huo ulikuwa kwa askari wa jeshi la ulinzi na wale wa kitengo cha usalama wa taifa wa nchi hiyo, na kilichoshangaza zaidi ni kwamba, kati ya hamsini na nane waliotoroka kwa upande wa jeshi la ulinzi ni thelathini na mbili, na kati yao kumi na moja tu, wakiwa ni askari wa vyeo vya chini, yaani kuanzia private mpaka sajent, na maafisa ishirini na moja, maafisa wakuu kuanzia cheo cha major mpaka kanali, wakiwa sita, na wengine ni kuanzia luteni usu, mpaka captain.
Miongoni mwao wakiwa askari na maafisa wazuri na mahili kiutendaji, walioshiliki operation mbali mbali za ndani na nje ya nchi, kati yao akiwepo Afisa mpelelezi mwenye cheo cha luteni kanali, bwana Ramadhan Mbwambo, ambae licha upelelezi wake lakini katika operatio Comoro, aliongoza vyema kikundi cha wapelelezi sita waliofanikisha kwa kiasi kikubwa, kubaini maficho ya kiongozi muasi wa Comoro mwaka 2007, ukiachana na kanali Mbwambo, pia mtoro mwingine aliemshtua King Elvis, ni Major Zaid Tambwe, ambae umahili wake katika majukumu ya kijeshi chini ya umoja wa mataifa huko Africa ya kati, ulimfanya apande cheo toka luteni mpaka major, ni baada ya kuongoza platoon yake, katika operation kadhaa na kumaliza operation hizo, kwa mafanikio makubwa.
Mwingine alikuwa ni kijana mdogo aliekuwa katika kitengo cha usalama wa taifa, huyu ni kijana Enock Kafulu, aliezaliwa mwaka 1987, hapo Trench Town, ambae taifa la #Mbogo_Land, lilimwandaa kuwa mtendaji mzuri, kwa kumpeleka vyuo mbali mbali vya kiusalama, katika nchi mbali mbali duniani, huku serikali hiyo ikitumia gharama kubwa kuhakikisha kijana wao lilimgharamia katika mafunzo makubwa ya nchi mbali mbali, Israel, ambako alienda kujifunza ujasusi.
Ufaulu wake wa hali ya juu, ulimfanya king Elvis ajivunie kijana huyo na kukubaliana na wazo la mkuu wa kitengo cha ML SA, bwana Dickson Chitopelah kwa kuchukuwa uamuzi wa kumpendekeza kijana huy akapate mafunzo hayo, maalumu ya kijasusi na upelelezi wa siri, “inakuwaje miaka mitatu tu, anaacha kazi bila sababu za msingi?” alijiuliza King Elvis, ambae mwaka mmoja uliopita alibadili waziri wa ulinzi, kutokana na sababu kama hizi za mienendo mibaya ya uongozi katika vyombo vya ulinzi na usalama na kumweka bwana Chitopelah, ambae wakati huo alikuwa mkuu wa kitengo cha MLSA, “kwanini haya mambo yanaendelea?” alijuliza tena king Elvis, kwa sauti ambayo ungesema anaongea na mtu mwingine pale alipo.
Naam baada ya kuwaza na kuwazua kwa dakika kadhaa, ndipo Elvis alipopata wazo la kwenda kupata ushauri kwa mfalme aliemtangulia, yaani king Eric wa pili.*******
Yap! sasa turudi mashariki mwa DRC, jijini Goma, pembezoni mwa ziwa Kivu, ndani uzio wa eneo la ofisi za MONUSCO, bado kikao kilikuwa kinaendelea ndani ya jumba la mikutano, kikao kilicokuwa kinaendeshwa na brigedia Thabo, ambae alisha pokea simu ya toka Ben Mavivi, kwamba madoctor wa WHO na askari toka Tanzania wamewasili mavivi wakiwa salama kabisa na hakuna kitu kilichoibiwa kati yao, nae akatoa maagizo kuwa madoctor wale wapelekwe Goma haraka kwa usafiri wa ndege, maana yule askari wa Tanzania angekuja na wale maafisa walioenda kule Ben.
Wakati hayo yanaendelea huko ndani, huku nje bwana Seveline akiwa ndani ya gari lake akiongea na na mtu aliemwita Chief kwa kutumia simu yake, “imemshangaza kila mmoja hata wao wenyewe wameshangaa hyo kijana amewezaje kupambana na vijana wetu” alisikika Sevelie akiongea na chief kupitia simu yake, “kwahiyo tutakaa tu pasipo kuwaonyesha kuwa sisi siyo wadhaifu?, na vipi kuhusu watu wetu wa FADRC, unampango gani kuhakikisha hawaingizwi kwenye hili?” iliuliza sauti upande wapili, “kuna mambo nimesha yafikiria, kwanza tuna hakikisha lawama zote zinaenda UN, ili kumchafua mtanzania, kabla hatuja mfyekelea mbali, hilo litakuwa ni somo kwao na hawataenda tofauti na kile tutachowaambia” alisema Seveline na yule anaeitwa chief akahitimisha kwa kukubaliana na Seveline kisha wakakata simu.*******
Deus alipongezwa sana na makamanda wenzake wa jeshi ambao ndio pekee walio ruhusiwa kuingia mle ndani ya uzio wa ofisi ya MONUSCO, “umetisha dogovhiyo ndiyo inatakiwa, wakileta ujuwaji ni kucheza nao tu” alisema mmoja kati ya makamanda huku Felix akidakia, “yani kila safari ya nje nitaomba uwe Dereva wangu” alisema Felix, na wote wakacheka, kasoro Deus alieishia kutabasamu, wakaendelea kuongea hili na lile.
Wakati huo wote yule doctor wakike wa kihabeshi, aliekuwa amesimama na wenzake, mita chache toka pale walipo wakina Deus, wakikaguliwa na madoctor wenzao kuhakikisha kama hawajapatwa na madhara yoyote,, muda wote macho ya mrembo huyo, yalikuwa yameelekea upande walipo wakina Deus, ambae muda wote alionekana kutabasamu, tofauti na wenzake waliokuwa wanacheka kwanguvu, ukweli ni vigumu kufahamu mschana huyu, alikuwa anawaza nini pale alipokuwa ana mtzama Deus, ila kilichoonekana ni macho ya mshangao na kama vile kuna jambo alikuwa anahitaji kumweleza kijana wetu.
Wakati doctor wa kike anaendelea kumtazama Deus Frank Nyati, kijana aliewakomboa toka kwenye mikono hatari ya waasi wa IDF, mara akamwona muhudumu mmoja wa airport, akifika pale walipokuwepo wao, na moja kwa moja akaenda pale kwake, “Maadam, checkup imekamilika na ndege yenu imebakiza dakika kumi kuondoka” alisema yule mhudumu wa airport, “sawa” aliitikia yule mwanamke mrembo sana, kisha akageuka kutazama kule walikokuwepo wakina Deus, ambapo safari hii, macho yao yakakutana, kila mmoja alimtazama mwenzie kama vile anataka kumweleza jambo flani, lakini nikama walishindwa la kufanyiana, hivyo kila mmoja akageuka kuwa tazama wenzake, pasipo hata kutabasamuliana, “jamani tunatakiwa kuingia ndani ya ndege, zime bakia dakika kumi tu” alisema, yule doctor wakike, “hooo safari ya goma tayari?” aliuliza doctor wa Kenya, kwa sauti ya kushangilia huku anainuka toka sehemu aliyokaa, kama mwenzie toka burudi alivyofanya, “maadam naomba dakika moja, nikamuage yule jamaa” alisema Doctor toka Burundi, akionyesha kidole alipokuwa Deus, “ni sawa unaweza kufanya hivyo” alisema yule doctor wakike ambae toka mwanzo tuliona kuwa nikama kiongozi wao.
Hapo mara moja, yule doctor toka Burundi akaanza kutembea kumsogelea Deus ambae alikuwa bado amesimama na wakina Major Felix, wakiendelea kuongea, “wacha na mimi nikaseme asante, alifanya kazi kubwa sana” alisema doctor toka Kenya, huku na yeye anaelekea kule alikokuwepo Deus, doctor kusikia maneno hayo ya mganga mwenzake, doctor wa kike anageuka kumtazama Deus, kule alikokuwepo.…….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
Tukutane Mchana Kwaajili Ya Episode Moja Zawadi Ya Mwaka Mpya Kwa Udhamin Wa Maadamu Doctor 💊 😅
HapaNYUMA YA MLANGO WA ADUI

TuendeleeTunaendelea