HADITHI: BADO NINAISHI (ASHRAFU NDILO JINA LANGU)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL:
thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
SEHEMU YA AROBAINI NA MOJA
"Sioni kama hayo maelezo yanahusiana kwa namna yeyote na yeye kuwa mlezi wa Ashrafu"
"Miaka ishirini huko nyuma iliyopita kuna siku nilifanikiwa kwenda kwake bila taarifa majira ya usiku ndipo nilimkuta akiwa anambembeleza kijana wa miaka kama kumi na tano hivi na alipo niona tu alimficha kijana huyo chumbani kabla hata sijafanikiwa kumfahamu. Nilimshangaa sana kumuona na yule mtoto kwa sababu kwenye maisha yake hakuwahi kupenda watoto tangu siku aambiwe kwamba hakuwa na uwezo wa kuzaa hivyo akawa kama amewachukia watoto wote, kumuona na mtoto yule lilikuwa ni jambo la ajabu sana hivyo ikabidi nimkalishe chini aweze kunijibu maswali yangu"
"Maria huyu mtoto ni nani na umemtoa wapi?"
"Sio biashara yako kuweza kujua"
"Ni biashara yangu kwa sababu ni jukumu langu kuhakikisha usalama wa hii nchi na unalijua hilo, huyu mtoto anaweza kuwa anatafutwa kwao huko unasemaje kwamba hainihusu?"
"Kwa sababu hana kwao huyo mtoto, mimi pekee ndilo tumaini ambalo limebakia kwenye maisha yake. Wamekufa wote" aliongea akiwa analia kwa uchungu sana, nikawa namshangaa kwa maana sikumuelewa, sikuwahi kumuona mdogo wangu anamlilia mwanadamu yeyote yule zaidi ya yule mpenzi wake ambaye alikufa.
"Nani amekufa?"
"Familia yake yote"
"Ni nani huyu mtoto?"
"Ashrafu Dominic Sawa sawa" jibu lake lilinifanya nikae chini kwanza, Dominic Sawa sawa alikuwa ni moja ya watu maarufu sana nchini kwa kipindi hicho kwa sababu alikuwa ni tajiri mkubwa na ni kweli siku kadhaa nyuma alikuwa ameuawa huku ikisemekana kwamba familia yake yote iliuliwa.
"Huyu mtoto ameponaje wakati inasemekana kwamba familia nzima ilikufa?"
"Hapana huyu aliishi kwa sababu nilienda kumuokoa mimi"
"Ulienda kumuokoa? Ulijuaje kwamba hilo litatokea?"
"Dominic aliniomba msaada"
"Ulikuwa unafahamiana na Dominic?"
"Ndiyo"
"Kivipi"
"Alikuwa mpenzi wangu"
"Maria!!!!!" majibu yake yalinishangaza sana, sikuwahi kujua kama mdogo wangu alikuwa hawala wa Dominic Sawa sawa.
"Alikuwa ni mpenzi wangu kwa muda mrefu sana, tulikutana nikiwa kwenye kazi naye akiwa kwenye biashara huko Mwanza na ndipo mahusiano yetu yalianza ghafla sana. Aliniweka wazi kwamba alikuwa ni mtu mwenye familia na aliipenda sana familia yake lakini kwangu halikuwa tatizo kubwa kwa sababu nilikuwa nimeamua kumpenda kwa namna yoyote ile nikakubali kuwa nae hivyo hivyo. Yule ndiye mwanaume pekee kabisa ambaye alikuja kunirejeshea furaha kwa mara nyingine tena kwenye maisha yangu."
"Siku ile ambayo aliuawa na familia yake alinipigia simu akiwa mwenye wasiwasi mkubwa sana, sauti pekee ambayo niliisikia kutoka kwake ni kwamba naomba uwasaidie wanangu. Nilimuuliza kama yuko wapi lakini sikupata jibu lingine hivyo nilichukua gari ya jeshi haraka sana na kuitraki simu yake ambayo ilinionyesha alikokuwepo. Kwa bahati mbaya sana wakati nafika pale nilikuwa nimechelewa kwani yeye alikuwa amekufa tayari ila niliona Ashrafu akiwa hai bado na kuna mtu alikuwa anataka kumpiga risasi hivyo nilimuwahi mwanaume yule na kumuua pale pale kisha nikaondoka na Ashrafu maana baada ya kuondoka tu niliona kuna watu wengine nyuma wakiwa wanafika lile eneo, sikutaka tena kuendelea kukaa pale zaidi nikaamua kuondoka na mtoto kwa sababu alikuwa hai hivyo nitamlea mimi kama mwanangu wa kumzaa"
"Maria kwanini hukuniambia kuhusu hili jambo?"
"Unataka kumuua mtoto? kwa sababu kama ni hivyo unatakiwa kuniua mimi kwanza"
"Maria umefanya jambo kubwa lakini ni la hatari sana kwa sababu maisha yako yanaweza kuwa hatarini muda wowote ule nadhani huyu mtoto itakuwa ni vizuri kama ukinikabidhi mimi niondoke naye"
"Hilo ni jambo ambalo haliwezekani Cleopatra na kuhusu maisha yangu tangu lini umeanza kujali mimi kuwa hai? Acha kunienjoi dada angu"
"Kumbuka wewe ni mdogo wangu wa damu na tupo wawili tu"
"Sijali kuhusu hilo. Kama kweli unanipenda mimi kama mdogo wako wa damu, kuna jambo naomba unisaidie na itakuwa shukrani yangu ya maisha kwako"
"Nakusikiliza"
"Naomba sana hili jambo ubaki nalo kwenye kifua chako, ulimwengu usije ukajua kuhusu huyu mtoto wala mtu yeyote yule, mimi nitamlea kwa siri sana na hakuna mtu atajua, nitampa kila kitu lakini pia nitamtengeneza kuwa mwanaume haswa ili hata huko baadae aje kujilinda mwenyewe kwenye huu ulimwengu usi na huruma"
"Unamaanisha unataka kumtengeneza ili aje kulipa kisasi?"
"Hilo ni juu yake yeye wala halinihusu mimi na kama akitaka hivyo siwezi kumzuia kulipa"
"Maria tafadhali usifanye hilo jambo, naweza kukuruhusu kumlea kwa siri kama unavyo hitaji wewe na hata msaada nitakupa lakini usimkuze kwa kumlisha hiyo sumu ni jambo ambalo linaweza kuja kuwa hatari sana kwa hapo baadae na tunaweza kuingia kwenye mgogoro ambao utakuja kunilazimu nimuue kwa mikono yangu"
"Cleopatra utalikubali ombi langu nililokuomba au utaendelea kunipatia risala hapa?"
"Naomba nimuone kwanza" aliitwa akiwa anatetemeka sana yule kijana, huruma ilinishika sana kwa sababu alipatwa na jambo baya sana akiwa bado ana umri mdogo.
"Unaitwa nani?"
"Remy Claude ndilo jina langu" nilishangaa sana na kumgeukia mdogo wangu lakini aliishia kutabasamu tu hapo nikagundua kwamba ni yeye ambaye alikuwa amembadilishia hilo jina.
"Nitailinda hii ahadi yangu mdogo wangu. Mlee kwa namna ambayo utaona kwamba inakupendeza wewe" ile kauli yangu baada ya miaka mingi sana kupita nilimuona mdogo wangu akinifurahia na kunikumbatia hivyo niliamua kuondoka na kumuachia yule mtoto amlee anavyotaka yeye" mkurugenzi aliitema siri ambayo aliishi nayo moyoni mwake kwa zaidi ya miaka ishirini, siri ambayo Suzane ilimtoa machozi sana kwa kuisikia historia fupi ya Ashrafu waweza kumuita Remy Claude.
"Kwa maana hiyo huyo ndugu yako ndiye aliye mtengeneza huyu mtu?"
"Yeah, kwa sababu mdogo wangu ana mafunzo ya kikomando na ni mtu ambaye alikuwa hatari sana kwenye mambo ya mapigano mpaka wenzake wakawa wanamuogopa sana, hivyo ni yeye mwenyewe kwa mkono wake aliye mtengeneza Ashrafu kama alivyokuwa ameniahidi"
41 BYE.