Simulizi ya kijasusi: Nafsi zilizotelekezwa

Simulizi ya kijasusi: Nafsi zilizotelekezwa

HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 25

Kwangu ilikuwa bahati ya mtende kuwa ndani ya idara, idara ambayo kila mwanajeshi kambini alikuwa akiiimba kila siku na kutamani kuwa huko ila ni mimi ambaye niliipata hiyo nafasi. Nilikumbuka nilikotoka sikutaka kufanya makosa, nilitamani kumfanya mama yule aliyenilea ajivunie huko aliko hivyo nilihitaji kufanya kazi kwa juhudi zangu zote na kweli nilitimiza hilo. Huko kwenye idara nilipewa kesi nyingi na nilizitimiza kwa asilimia zote miamoja na kwa moyo wote baada ya mafunzo ya muda mrefu.

Sikuwahi kumsahau baba yako, alikuwa ni mtu maarufu tayari nchini, niliona ni muda sahihi wa kumtafuta rafiki yangu wa damu. Kumpata kwake akiwa na mke na mtoto tayari alinitupia lawama nyingi kwa kuamua kumkimbia ila alinielewa kwa sababu maana yangu haikuwa mbaya. Maisha yangu ni siri kubwa ila niliamua kumuweka wazi juu ya kazi yangu mpaka nilipo fikia wakati huo, akanipongeza na kunifurahia rafiki yake, urafiki wetu ukarudi japo kwa siri kwani haikutakiwa kujulikana kwa mtu yeyote, wote tungekuwa hatarini.
Nikiwa ndani ya idara ndipo lilipokuja kutokea jina la mrembo IRINA ESPANOVICH, haikuchukua muda mezani likaja jina la LS (The LUNATIC SOCIETY) tukiwa tunaendelea kulifuatilia kwa ukaribu ndipo raisi akaja kufariki ghafla, ukawa msiba kwa taifa. Tulibaki tumeduwaa lakini viongozi wa ngazi za juu wakawa hawana presha yoyote kana kwamba walikuwa wanajua kilichokuwa kinaendelea, jambo hilo kama mzalendo lilinigusa mno, licha ya baba yako kunipa maelekezo juu ya kilichokuwa kinaendelea upande wake; kama mzalendo niliamua kuingia kwenye maktaba za taifa kuusaka ukweli ambao ulikuwa nyuma ya jambo hilo.
Nilicho fanikiwa kukijua kinatisha, hakikuwa salama kwangu hata kidogo kama ningeamua kukifikiria, jambo la kwanza nilishangazwa na ukweli kwamba raisi aliuawa na mdogo wake wa damu Novack Nyangasa ambaye alikuwa mpenzi wa mrembo ambaye aliiasi idara yake ya KGB, Irina. Ujio wake Tanzania ndio ulikuwa mwanzo wa kuanzishwa kwa jamii hiyo ya siri ambayo kwa wakati huo yeye na mpenzie Novack Nyangasa ndio walikuwa viongozi.
Hata baada ya raisi kufariki, walimpa nafasi hiyo aliyekuwa makamu wa raisi mwanamama Daniela Lopa akakaimu nafasi hiyo. Mwanamama huyo alikaa hapo kuwawakilisha wao hivyo taifa likaingia kwenye mikono yao rasmi kwa kutumia akili ya mwanamke huyo. Kwa bahati mbaya baadae ilikuja kugundulika kwamba hata mimi nilikuwa nawafuatilia kwa ukaribu hivyo nikawa nipo kwenye mahesabu yao ya kunifanya niwe mtu wao au wanipunguze duniani kwani kukusanya taarifa zao nyingi lilikuwa ni tatizo kubwa ambalo lingekuja kuwaharibia mbeleni kwenye hiyo mipango yao.
Wakati mambo yote hayo yanafanyika ndio wakati ambao baba yako alikuja kwangu na kutaka mimi nikutafute wewe na mama yako kwa kupotea ghafla huku yeye akidai anaelekea Israeli. Aliniachia mtihani mzito mbele yangu, mimi mwenyewe nilikuwa nimeshaharibu kwenye idara kwa kufukunyua taarifa ambazo hazikuwa zikinihusu halafu ndio wakati ambao rafiki yangu alinifuata na kuhitaji nimtafutie familia yake na kuihifadhi mahali ambapo ni salama. Nina uhakika ukikaa sehemu yangu utaona ni ugumu kiasi gani ambao nilikuwa nao, lakini ningefanyaje na mimi ndiye mtu pekee ambaye baba yako aliniamini kiasi cha kuniachia hata miliki zake na mali zake zote? Ningegoma nisingekuwa na cha kujibu mbele ya mwenyezi Mungu siku ya mwisho kikaoni, nikakubali kuifanya kazi ya kukutafuta wewe na mama yako, kazi ambayo ilinishangaza na kuyafanya maisha yangu kubadilika.
Nilifanya kila namna kuhakikisha nawapata japo sikuwa na mwanzo wa kujua mliko potelea wala kuwepo kwa wakati huo ila jambo ambalo lilinishangaza kwenye upelelezi wangu juu ya maisha yako ni baada ya kugundua kwamba mama yako alikuwa ni mwanachama wa jamii hiyo ya LUNATIC SOCIETY na ndiye ambaye alikwenda huko mbarali kuwapa sumu familia ya baba yako kwa sababu alikuwa akiaminika huko. Hilo ni jambo ambalo lilinishangaza na siwezi kusema niliamini bali nilibaki nimetahamaki nisijue ni kipi nilitakiwa kukifanya, mtu ambaye nilitakiwa kumlinda na mwanae ndiye alikuwa nyuma ya hiyo mipango. Ulimwengu uliwahi kunishangaza ila siku ile ulinipa somo kuhusu wanadamu. Sasa ni wakati wa wewe kujua sababu ya msingi hasa kwamba ni kwanini watu hawa wanaisaka roho yako kwa udi na uvumba kuliko hata pesa inavyotafutwa na maskini, wapo tayari kutumia mabilioni ya fedha kukuua wewe na kukupoteza ulimwenguni kwa sababu wewe ni miongoni mwa viumbe hatari vichache vilivyo bakia duniani na uhatari wako unawahusu wao wakiogopa kwamba siku ukiujua ukweli utafanya mambo ya kutisha kwa upande wao lakini pia wanaogopa zaidi wewe kuvujisha taarifa hizo ukizipata.
Simulizi ndefu imhusuyo yeye na maisha yake ya nyuma ilikuwa imefika kati kati, ilikuwa inasisimua, inaliza na kushangaza. Alikuwa amepewa nusu yake na sasa alikuwa anaelekea kwenye sehemu ya mhimu zaidi akiwa anashangaa kuambiwa kwamba mama yake mzazi alikuwa mwanachama wa jamii hiyo ya siri ambayo ndiyo kwanza alikuwa ameiskia kwa mara ya kwanza ambayo ilidaiwa kuwa nyuma ya mipango miovu ya serikalini ikiwepo kumuua raisi wa nchi, kumtoa baba yake kafara lakini kuiteketeza familia yake yote. Edison alihema kwa nguvu akiwa mwingi wa hofu, jasho lilikuwa linashuka usoni kwake akiwa hana uwezo wa kulizuia. Aligusisha kidole chake mdomoni ili kupata mate ya kufungulia kurasa mpya ambazo alitakiwa kuanza kuzisoma sababu za msingi za yeye kuishi maisha ya sasa, aliifunua kurasa hiyo iliyo fuata;
Juu iliandikwa KIFO CHANGU MKONONI MWANGU. Hakuelewa maneno hayo yalikuwa na maana gani na yalihusiana nini na simulizi ya maisha yake, kitabu alikuwa nacho, alichagua kuzizuia hasira na kuwa mpole ili aelewe mchezo mzima ulikuwaje.

“MAGAIDI WATISHIA AMANI TANZANIA KWA KUMWAGA DAMU ZA WATU, MMOJA ATEKWA. KUNANI NYUMA YA PAZIA? TANZANIA SI SALAMA TENA. JNIA HALI TETE”
Kichwa cha gazeti kilizipamba kurasa za mbele kabisa za magazeti ambazo zilifanya taasisi za usambazaji wa magazeti kupata wateja wengi siku hiyo kuliko ilivyo kawaida. Tukio la jana yake usiku lilikuwa la namna yake, tukio lilikuwa la kusisimua huku likitokea ndani ya uwanja ambao unategemewa na taifa zima.
Habari hiyo ilisambaa kwa kasi kila eneo na kuzua mijadala mikubwa, wengi walihusisha jambo hilo na shambulio la kigaidi wakiamini kwamba huenda Tanzania kuziunga mkono baadhi ya nchi ilikuwa inaenda kuleta matatizo makubwa nchini, kama kawaida ya wananchi wengi lawama walizielekezea upande wa serikali na kuona kama serikali haifanyi kazi sawa sawa kama inavyopaswa. Wengine hawakuishia hapo tu, walitaka wale ambao walikuwa wazembe kwenye hizo sehemu zao walitakiwa kuchukuliwa hatua kali kwani uzembe wao ulifanya watu wengi kuumia vibaya kwa kukimbia, ulileta shambulio na nafsi kwa wahanga ambao walikuwepo eneo hilo lakini lilikuwa shambulio hatari la kuhatarisha maisha ya watu hao.
Eneo la Banana njia ya kuelekea Kitunda, watu walikuwa wameketi pembezoni mwa barabara karibu na kilipo kituo cha dala dala za kwenda huko wakiteta yale ya jana.
“Mimi huwa nasema kila siku, hawa wajinga wanakula kodi zetu tu hakuna kitu wanakifanya huko zaidi ya kuwaza kuwavua warembo chupi na kujaza matumbo yao. Haiwezekani eneo kama lile ambalo sisi tunaamini kwamba ni moja ya sehemu ya kujivunia ya taifa, eneo ambalo tunaamini kwamba linalindwa na ni salama! Watu wanavamiwa na kuuawa halafu inasemekana hakuna hata mmoja aliye kamatwa? Huu ni ujinga mtupu, haki ya Mungu siji kwenda kupiga kura tena” Kijana mmoja alifoka! Hasira zilikuwa zimempanda huku akiwa anahema kwa jazba. Haikueleweka kama alikuwa na hasira zake za kupigwa na maisha au ni mtu ambaye alivurugwa asubuhi hiyo, ilibidi mwenzake mmoja ampe maji kwanza apooze koo, alipaniki isivyo kawaida mpaka akawa anawashangaza wenzake.
“Abraham Linkoln aliwahi kusema USIHUKUMU HAUTAHUKUMIWA, kabla ya kuwarushia lawama kwanza inabidi ukae kwenye nafasi yao halafu ujiulize kama ungekuwa wewe ungefanyaje! Hata wewe mwenyewe kuna mazingira familia yako tu inakushinda kuifanyia maamuzi sasa kwanini unavamia tu na kuanza kutukana kuwasema viongozi bila kutumia upembuzi mzuri wa hoja? Maliki punguza kukurupuka mwanangu. Hakuna taarifa kutoka mamlaka za usalama nchini hivyo subiri watoe taarifa zao walipo fikia ndipo ulaumu, ni ngumu kushindana na watu ambao hujui wanapanga nini dhidi ya nchi yako, ni sawa na wewe hapo uvamiwe na kuchomwa kisu ghafla ukiwa kwenye utafutaji wako badala ya kutafuta sababu iliyo mfanya mtu huyo akushambulie unaanza kujilaumu kwa kushambuliwa, huo ni ujinga mwanangu” kijana ambaye alionekana kuwa mwerevu alimpa somo mwenzake, alitakiwa kuacha kukurupuka bali kuwa mtu wa kutumia zaidi akili.

UKURASA WA 25 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 26


“Umeongea jambo la maana Innocent, sioni sababu ya kuilaumu serikali, hata wao hawapendi mambo kama haya yatokee kwani huwavua nguo na kuwachafua. Ni wao ambao hawapendi haya mambo yatokee ili wapate kujinadi vyema kwenye siasa, jambo la mhimu ni kuendelea kuliombea taifa letu na kila mtu kuwajibika kwa nafasi yake. Mtu mmoja mwenye busara aliwahi kunukuliwa akisema “LAWAMA NI TAMU SANA UNAPO ITOA MDOMONI LAKINI PEKEE HAITAPELEKA MKONO KINYWANI”, gari imefika twendeni tukapakie kwanza haya mambo mengine tutaendelea nayo baadae” kwa mazungumzo yao walionekana kabisa walikuwa ni wapiga debe kwenye hilo eneo.
Huo ndio ulikuwa uhalisia wa mtaani kupitia tatizo hilo, kila mtu alikuwa na jambo lake huku wengine wakianza kuhoji kuhusu usalama wa maeneo mengine, hawakuona kama watu hao wanaweza kushindwa kuvamia maeneo mengine kama walifanikiwa eneo ambalo linapokea wageni wa kila aina kutoka duniani kote. Serikali ilitoa tamko tu kwamba ni kweli tukio hilo limetokea ila muda sio mrefu wahusika wangeweza kukamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Simu za wakubwa zilikuwa zinaita kila wakati kwa kamanda wa jeshi la polisi kiasi kwamba zingine akawa anazipotezea, usiku mzima hakulala kabisa Raymond Kono. Akiwa ndani ya ofisi yake, sigara ilikuwa ikipotea taratibu mdomoni, hakuwa anavuta kwa sababu alikuwa na hamu nayo bali kwa sababu ilikuwa inampa ahueni ya mawazo, alikuwa anaukadiria moshi ambao alikuwa anaupuliza juu bila kupata jibu la alichokuwa anakihitaji. Usiku mzima aliutumia kuchora michoro yake ya kujua ni wapi angeanzia kulifanya jambo hilo lakini hakufanikiwa kupata majibu.
Akiwa ndani ya mawazo mazito, simu yake ilianza kuita kwa fujo, aliipotezea kwa sababu ni mara nyingi ilikuwa ikiita asubuhi hiyo ya mapema tangu awasili ofisini kwake. Alitoka kwenye mawazo fikirishi baada ya kugundua kwamba iliyokuwa inaita haikuwa simu ya ofisini bali ya mfukoni kwake, alisonya baada ya kuona mtu ambaye alikuwa anampigia. Afisa usalama wa mkoa ndiye alikuwa anampigia wakati huo.
“Habari ya asubuhi bwana Kono”
“Sio njema “
“Nalielewa hilo, nitumie taarifa za awali hii kesi tunaichukua kuanzia hapa maana wakubwa wanapiga simu nyingi na wametoa masaa kadhaa tu majibu yawe yamepatikana”
“Unamaanisha hii kesi mimi sihusiki tena?”
“Ulipewa muda tangu jana lakini hakuna ulicho kifanya, hata simu za IGP haupokei kwahiyo nitumie taarifa za ulicho kipata mpaka sasa ili tuanzie hapo na wewe utakuwa nje ya jambo hili. Hili sio ambi Raymond” Alisonya na kukata simu, aliihitaji hiyo kesi kwa sababu kuwa chini yake kama ingefanikiwa ingempa jina kubwa kwa wakubwa wake wa kazi ila muda haukuwa rafiki. Hakuwa na namna zaidi ya kutuma taarifa hizo huku akijiapiza kufuatilia jambo hilo kwa ukaribu ajue kulikuwa na mchezo gani ambao ulikuwa unafanyika.
Taarifa zilifika ndani ya ofisi kubwa ya afisa mpelelezi wa mkoa, AZIKIWE POSTA. Ndani ya jengo hilo ndimo alikuwepo kiongozi huyo ambaye aliwahi kufika hapo asubuhi na mapema baada ya jana yake usiku kufika uwanja wa ndege na kupata dondoo chache juu ya kile ambacho kilifanyika.

JULIUS MBANDU
Kijana aliye upenda umaarufu, alipenda jina lake liandikwe kila sehemu. Hakuwa mtu ambaye alipenda jina lake liwe nyuma gizani ndiyo sababu aliutumia muda wake kuwafurahisha wakubwa zake. Julius alikuwa kijana mpelelezi na mchapakazi, maisha yake aliyaelekeza kwenye kazi ya kujenga taifa japo kwake ufahari wa kusifiwa na kupata jina kubwa wa wakubwa zake ndicho kilikuwa kipaumbele cha maisha yake. Nani hautaki ufahari kwenye haya maisha? Kila mtu anautamani ila huenda wengine hawautaki kwa sababu wanajua hawawezi kuupata na hata kama wataupata gharama ya kuutunza ni kubwa na ngumu.
Ilikuwa ni tofauti kwa Julius, alikuwa akifanya kazi kwa ukaribu na afisa usalama wa jiji la Dar es salaam na alikuwa kijana ambaye alifikia hatua ya kumuamini vilivyo. Imani haikuja kwa bahati mbaya bali kwa kazi kubwa ambayo alikuwa anaifanya na ikaonekana. Asubuhi hiyo ni yeye ambaye alikuwa anaingia ofisini kwa bosi wake baada ya kupokea taarifa ya kuhitajika, ni yeye ambaye alikuwa anapewa kijiti cha kwenda kuchunguza kuhusu tukio ambalo lilitokea uwanja wa ndege kisha alete majibu haraka, yalikuwa yanahitajika ofisi kuu ya nchi, nazungumzia Ikulu kwa raisi pamoja na wakubwa wa vyombo vya usalama.
Alifika kwa katibu muhtasi wa mheshimiwa Bosco Ndatu na kuruhusiwa kuingia. Aliingia na kutoa heshima kwa mkubwa wake kama ilivyo utaratibu
“Julius nimekuita hapa asubuhi hii kwa sababu nakuamini, nakuamini sio kwa kukupendelea mbele ya wenzako bali kwa mafanikio ambayo umeyaonyesha kwa kazi kadhaa ambazo umefanikiwa kuzifanya. Hii kesi ipo mamlaka za juu lakini kwa sababu hii ofisi ni sehemu ya mamlaka hayo hususani ya usalama na upelelezi wa taifa, nimeomba niifanyie kazi na kuahidi kutoa majibu haraka iwezekanavyo lakini mimi kufanya haya ni kwa sababu nakutafutia nafasi kubwa maana unastahili na kama ukifanikiwa kwenye hili basi utatengeneza jina kubwa kwa wakubwa na kwa wananchi, utaimbwa kila sehemu na taratibu ndoto zako zitaanza kutimia bila tatizo”
“Nimekuelewa bosi, nashukuru kwa kuniweka mbele siku zote, naahidi kuto kukuangusha kwenye hili”
“Mwisho wa siku ahadi ni maneno tu, una masaa kumi na mawili ya kukamilisha hii kazi na kuja na majibu kamili. Zaidi ya hapo hii kesi inaenda moja kwa moja kwa idara ya usalama wa taifa na hakuna mtu mwingine atapewa nafasi nyingine ya kuishughulikia. Angalia kwenye simu yako kuna taarifa zote za kuanzia nimetuma kwenye barua pepe yako, baada ya huo muda nahitaji majibu kamili ya kwenda kuyafikisha baadae kwa wakubwa”
“Sawa bosi” alinyanyuka na kutoa heshima kisha akatoka humo ndani. Julius, aliingia ofisini kwake na kutulia kwanza, alihitaji kutuliza akili ili asiweze kukosea hata hatua moja. Lengo lake kubwa alihitaji kujua wapi pa kuanzia na wapi atamalizia, hiyo kazi kwake ilikuwa ni zaidi ya kushiriki michuano ya kombe la dunia, ilikuwa ni nafasi ya pekee kutengeneza maisha ya ndoto zake, hakutaka kucheza nayo. Alizifungua taarifa za tukio hilo na kuzisoma kwa umakini
“Damasi Kazimoto” ndilo jina pekee ambalo alilitaja, kupitia mwanaume huyo angeweza kutambua sababu ya jambo lile kutokea na kuwapata wahusika pia. Kesi ya Leyla kutekwa haikuwa ikimuumiza kichwa kwa kuwa aliamini akipata jibu kumhusu Damasi Kazimoto ambaye alidaiwa kufa na mwisho wa siku akaonekana kuwa hai, angepata jibu la moja kwa moja hivyo akajua kabisa kwamba alikuwa anaua ndege wawili kwa wakati mmoja. Julius aliwachukua askari kadhaa wa kuongozana nao eneo la tukio, walikuwa na kazi yao askari hao. Alitoweka mjini baada ya kupata vibali maalumu vya huko alikokuwa anaenda na hao polisi wake.
Safari yake ilikuwa ni kuelekea Tambani Mkuranga, nyumbani kwa akina Damasi Kazimoto. Alikuwa na taarifa kwamba kamanda wa polisi alifika eneo hilo lakini hata yeye alilihitaji pia kwa sababu ndipo siri ya tukio zima ilipokuwa imejificha. Alifika hapo majira ya saa mbili ya asubuhi, alishuka kwenye gari akiwa na wenzake na kuzichukua hatua zao kuelekea ilipokuwepo nyumba ya mzee Kazimoto mwenyewe ambaye alikuwa baba mzazi wa Damasi.
“Mzee heshima yako?”
“Salama vijana wangu karibuni”
“Asante, mimi sio mkaaji na wenzangu ila kuna jambo zito ambalo limetuleta hapa, huenda lisiwe sawa kwako na kwa familia lakini hakuna namna mzee wangu kwa sababu ni mambo ya usalama wa nchi na raisi anasubiria majibu kutoka kwa kile ambacho kitapatikana hapa leo” maneno ya Julius yalimtisha mzee Kazimoto, akayameza mate yake kwa shida akiwa mwingi wa hofu moyoni. Dalili za mvua ni mawingu, aliliona wingu hapo kilichokuwa kinasubiriwa ni mvua tu kunyesha.
“Jambo lipi hilo?” aliuliza midomo yake ikiwa inatetemeka, hakuwa na uhakika na kile ambacho kilikuwa kinaenda kufanyika ama kuendelea hapo mzee Kazimoto.
“Nimekuja na kibali cha kufukua kaburi la mwanao, serikali itailipa familia kwa usumbufu huo lakini hakuna namna kwa sababu ni mambo ya usalama”
“Hapana, hilo ni jambo ambalo haliwezekani”

UKURASA WA 26 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 27

“Unaweza kuitamka hiyo kauli mbele ya raisi na watu wamekufa huku mamia ya watu wakiwa wanasubiri taarifa kutoka serikalini mzee wangu ili nikupeleke Ikulu muda huu?”
“Kwanini mnayatumia mamlaka vibaya kuwanyanyasa raia namna hii? Mwanangu ni miaka miwili sasa tangu azikwe, jana tu mwenzako kaja kunisumbua hapa nikamsikiliza, leo wewe unakuja hapa na habari zile zile, muacheni mwanangu apumzike tafadhali”
“Vipi kama mwanao yupo hai mzee?” hayo maneno yalimshtua mzee huyo, mshtuko wake Julius aliuona vyema japo hakumwambia, ni kama mzee huyo kuna jambo alikuwa analifahamu ila aliamua kulihifadhi kwenye moyo wake.
“Kijana hii ni familia ambayo ina heshima yake, usitake kutukumbushia machungu ambayo watu tumeyasahau kuwa makini na kauli zako, hivyo vyeo ambavyo mnavipata mkiwa wadogo visiwasahaulishe mkajiona dunia mmeishika kwenye mikono yenu” Julius alitabasamu kwa sababu kauli hiyo akiitoa kama chombeza ili mzee huyo atoe taarifa za ndani.
“Nisamehe mzee wangu, naomba utuonyesha kaburi lake lilipo tafadhali kwa sababu jinsi ninavyozidi kuchelewa, watu wa Ikulu wataifika hapa wao wenyewe na kama nikiwapa taarifa kwamba umegoma kutoa ushirikiano familia yako inaweza kuingia kwenye matatizo” mzee Kazimoto alimpa jicho la kufuga kisasi kijana huyo mbele yake ila hakuwa na namna, alifanya kile ambacho aliambiwa bila shuruti kwa sababu lilikuwa ni jambo la usalama wa nchi.
Kaburi lilifukuliwa upya, ikachukuliwa mifupa kadhaa kwa ajili ya kwenda kumpima DNA, Julius alihitaji kuhakikisha kama je kweli yule aliyekufa alikuwa ni Damasi mwenyewe au kulikuwa kuna jambo lingine nyuma yake? Kama angekutwa ni yeye basi njia ya upelelezi ingekuwa ni kazi bure kumhusisha yeye ila kama asingekuwa yeye basi angekuwa amepiga hatua kubwa kwenye upelelezi wake ambao alikuwa anaufanya. Baada ya kukamilisha zoezi hilo walifukia kaburi hilo na kuahidi kulifanyia matengenezo yenye ubora mkubwa pindi wakirudisha zile sampo za mifupa ambayo waliibeba kwa ajili ya kwenda kuifanyia uchunguzi japo mzee yule hakuambiwa kwamba walikuwa wanaipeleka wapi. Hakuwa na namna zaidi ya kukubaliana na uhalisia wa kile ambacho kilitokea.
Wakati Julius na watu wake wanaondoka kwenye ile eneo, kuna kitu alikishuhudia kwa mzee yule. Aliitoa simu yake mfukoni akiwa ana wasiwasi mwingi na kuipiga mahali, alitamani angemsikia ila walikuwa mbali, yeye alikuwa amelifikia gari tayari na hata mzee Kazimoto alipo yageuza macho yao yakagongana, alionyesha mshtuko ambao ulimpa Julius mashaka, akajua kwamba lazima kulikuwa kuna jambo nyuma ya hofu ile, mtu mzima hawezi kuwa na mashaka ya namna ile bila sababu ya msingi ya kufanya hivyo. Hata hivyo hakuwa na namna zaidi ya kuupa muda nafasi.
Julius safari yake ilikuwa ni mpaka kwa Mkemia mkuu, alimhitaji mtu huyo amsaidie kufanya vipimo vya mifupa ambayo alimpelekea na sampuli ya DNA ambayo alimpatia. Watumishi wa umma kama wanajeshi sampuli zao huwa zinachukuliwa na kuhifadhiwa kwenye hifadhidata ya nchi hivyo kukiwa na tatizo kubwa kama hilo kuzipata ni zoezi la muda mfupi ndiyo maana Julius hakuhangaika kuhusu hilo.
Lilikuwa ni zoezi la masaa kadhaa tu kwa sababu lilikuwa ni jambo la nchi, maabara ilisimamisha kazi zake zote na wataalamu wakalishughulikia jambo hilo. Majibu ambayo yalipatikana yalimshangaza Julius pakubwa, sampuli ya ile mifupa ilikuwa ni tofauti kabisa na Damasi. Alitabasamu kwa tumaini baada ya kugundua kwamba aliyekuwa amezikwa hakuwa Damasi Kazimoto bali ulikuwa ni mwili wa mtu mwingine tofauti, hapo akakumbuka ile hofu ambayo ilikuwa imepenya kwenye nafsi ya mzee Kazimoto, akawa na uhakika kwamba mzee yule alikuwa anayajua mambo mengi ambayo aliamua kuuficha ulimwengu. Kabla ya kutaka kuyajua mambo hayo, kichwa chake kililichuja swali moja ambalo aliliona ni la mhimu na kubwa kwa wakati huo, Kwanini? Ilikuwaje mtu huyo adanganye kuhusu kifo chake? Akaacha nafasi kwa sababu hakuwa na uwezo wa kulijibu hilo.
Julius hakuwa na kingine cha kufanya zaidi ya kutoa amri mzee Kazimoto akamatwe haraka kwa ajili ya mahojiano. Akiwa na tumaini la ushindi mbele yake, alimfuata mwenyewe mzee huyo na kumkamata kisha kuondoka naye kwenda kumhoji, huyo ndiye ambaye angempa maelekezo ni wapi angefanikiwa kumpata mwanae aliye danganya kifo bila sababu za msingi kuweza kujulikana.
“Miaka miwili ambayo imepita, Damasi Kazimoto alikuwa miongoni mwa wanajeshi bora ndani ya taifa hili. Alikuwa miongoni mwa watu ambao walikuwa wanatarajiwa kulifanyia makubwa taifa hili, sifa hizo zilikuja kutokana na kazi yake tukuka ambayo aliifanya kipindi chote ambacho alilitumia vazi la jeshi. Alikuwa na ufanisi mkubwa kazini, alikuwa mlenga shabaha bora, wakuu wake wakaweka mararajio makubwa kwa mwanaume huyo ndiyo sababu akawepo kwenye ule msaafara wa kuelekea Somalia”
Alienda kwa uwezo wake na sio bahati mbaya, na rekodi zinaonyesha kabisa familia mlikabidhiwa posho za mpendwa wenu kwenda kwenye hiyo safari ambayo muda mwingine huwa inalazimu mtu kurudi akiwa maiti kikubwa kulipambania vazi lake la thamani lililopo mwilini. Kwa bahati iliyo mbaya ilirudi maiti yake yeye na wenzake, Damasi hakuwa tena yule shababi na shupavu ambaye aliondoka kwa furaha badala yake alirejesha majonzi kwa familia. Naikumbuka vizuri ile siku tupo pale uwanja wa ndege kuipa heshima ya mwisho miili yao mbele ya mheshimiwa raisi, nilisikitishwa hasa nilipo lisikia jina lake kwa sababu ni moja ya watu ambao walikuwa kama kioo kwetu sisi vijana.
Jambo la kusikitisha ni kwamba hayo yote yalikuwa maigizo, hakukuwa na ukweli wowote kuhusu haya ambayo nimeyaelezea na kumpatia sifa binadamu huyo. Alitufanya watanzania wote wapuuzi, akawatusi viongozi kwa kupoteza muda wao kuupa thamani mwili ambao haukuwa wake huku yeye akiwa sehemu anatusanifu na kuicheka serikali. Damasi yupo hai! Kwanini imekuwa hivi mzee wangu? Nini tatizo mpaka mmeamua kuifanya serikali kuonekana wajinga wakati mwanao yupo hai? Julius aliteta na mzee Kazimoto akiwa kwenye chumba cha mahojiano, alielezea kwa urefu ili mzee huyo atambue kwamba alikuwa mbele ya mtu ambaye alikuwa na taarifa za kutosha.
Ukweli kuhusu maigizo ya kifo cha mwanae ulikuwa mkononi mwa kijana huyo mchapakazi aliye lipenda jina lake kuwa juu na umaarufu! Kwanini asiupende wakati unavutia watu kuwa karibu yako? Julius alimpatia maelezo mzee huyo kumhakikishia kwamba alitambua kuwa mwanae yupo. Mzee huyo hakuwa na papara wala taarifa hizo hazikuonyesha kumshtua, alitabasamu akiwa na utulivu kwenye uso wake, hakuwa na haraka na kijana huyo muda ulikuwa upande wake.
“Kijana wangu nadhani hauna kazi za kufanya, kwanini usiingie hata mtaani kwenda kukamata vibaka wavuta bangi? Hilo jambo ambalo unaliongelea huoni kama ulimwengu utakuona wewe kichaa?” aliongea kwa majivuno mzee huyo kuonyesha maelezo yote hayo hayakumpaparisha kabisa.
“Nitaonekana kichaa mpaka pale ulimwengu utakapo ufahamu ukweli” Julius alijibu kwa kujiamini huku akitua mezani nyaraka mbili ambazo zilikuwa na maelezo ndani yake. Alizingua na kumsogezea mzee Kazimoto karibu ili ajionee;
“Hayo ni majibu ya uthibitisho kwamba mwanao yupo hai, upande wa kulia ni vipimo vya DNA ya mwanao akiwa jeshini lakini upande wako wa kushoto ni vipimo vya ile mifupa ambayo nimeondoka nayo kwako asubuhi. Ubaya wa hivyo vipimo ni kwamba vina majibu tofauti kumaanisha kwamba aliyezikwa pale sio mwanao Damasi bali ni mwili wa mtu mwingine, je mpaka hapo bado unaamini mimi ndiye nitaonekana kichaa mzee wangu?” Julius aliona ushindi mbele yake, kwanini? Mzee Kazimoto jasho jembamba liliutembelea uso wake na kumpa hofu, hakuwa na ujasiri wa kutamba tena bali mitetemo ya midomo yake yote miwili huku akiwa kama mtu ambaye anataka kuteta jambo ila nafsi ilimsaliti. Julius aliwasha sigara na kumpatia mzee huyo kisha naye akaketi upande wa pili na kuiwasha yake moja kisha wakawa wanavuta taratibu huku wakiwa wanaangaliana.
“Kuna watu wakimpata mwanao kabla yangu wanaweza kumuua ila kama nikimpata mimi nakuahidi atakuwa salama na kuna uwezekano akapata nafasi ya kuachwa kabisa kama atakubali kutoa ushirikiano juu ya kile ambacho kilitokea na kutueleza walipo wenzake pamoja na yule mwanamke ambaye walimteka” mzee Kazimoto alicheka sana baada ya kusikia ngonjera kutoka kwa kijana Julius.
“Bwana mdogo nadhani hata hauelewi kwamba ni kitu gani ambacho unataka kupambana nacho, unayo nafasi bado kawaambie wakubwa zako kwamba hii kesi binafsi imekushinda watafute watu wengine wenye uwezo. Wewe hapo bado ni mdogo, nina uhakika hata familia bado hauna hivyo usiyakatishe maisha yako kwenye umri kama huo kwa kuutafuta umaarufu ambao utaupatia ukiwa kaburini mwanangu” ya kale ni dhahabu ila maneno ya mzee huyo Julius aliyaona kama taka taka, alimuona mzee huyo kama mfa maji ambaye alikuwa anatapatapa tu kujaribu kumtisha ili mwanae awe salama huko aliko.

UKURASA WA 27 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 28

“Mzee wangu, nimewahi kupewa nasaha nyingi nikiwa bado mtoto mdogo ila kwa bahati mbaya mimi ni mtu ambaye nauishi zaidi uhalisia wangu kuliko ushauri wa watu. Naangalia moyo wangu unataka nini au kichwa changu kinaamini nini ndicho nakifanya, sijali ambacho unataka kunilazimisha nikiamini hapa kutoka kwako ila naomba unijibu nilicho kuuliza. Nakuheshimu kulingana na umri wako ni kama mzazi kwangu ila haimaanishi kwamba siwezi kukufanya kama wengine, nina ruhusa ya kukuhoji kinguvu kama ikibidi na hilo unatakiwa kulielewa kwa usahihi”
“Ukimpata Damasi unataka kumfanya nini?”
“Hakuna jambo litamtokea zaidi ya kukamatwa na kuhukumiwa kwa kile ambacho amekifanya”
“Nakusikitikia kijana wangu. Miaka miwili ambayo imepita ni kweli mwanangu aliondoka na ukarudi mwili wake, kwa mara ya kwanza hata mimi niliamini hilo lakini nililazimisha sana kumuona mwanangu kabla hajazikwa. Lilikuwa ni jambo gumu kwani jeshi lilisimamia kila kitu ila nililazimisha mpaka nikafanikiwa kuuona mwili wake na kwenye familia ni mimi tu pekee ambaye nilifanikiwa kuuona mwili hivyo naweza kusema ni mimi pekee ambaye ninajua kwamba bado mwanangu yupo hai” alitulia mzee Kazimoto na kuendelea;
“Ule uso licha ya kuwa na sura ambayo ilifanania na mwanangu ila niligundua kwamba yule hakuwa yeye kwa sababu kipindi akiwa mdogo niliwahi kumchapa na waya shingoni karibu na sikio ukamuachia alama ndogo nyeusi, haikuwa kubwa ila nilikuwa nikiangalia tu najua kwamba ni yeye au sio lakini kwenye mwili ule ile alama haikuwepo kabisa hivyo nikapata jibu kwamba hakuwa Damasi. Jambo lile lilinishtua na kupata udadisi wa kutaka kujua kwamba iweje niletewe mwili ambao sio? Nikawaza labda mwili wake uliharibika wakaufanyia upasuaji upya? Jibu likawa ni hapana, nikiwa bado kwenye hayo maswali mengi ulikuwa ni wakati wa kwenda kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele”
“Sikumshirikisha mtu yeyote juu ya jambo hilo mpaka pale ambapo nilihisi kwamba pembezoni kidogo umbali wa mita kadhaa kutoka pale kaburini kulikuwa na mtu ambaye alikuwa ananiangalia kwa ukaribu. Sikutaka kumzingatia kwa sababu mwili ulikuwa unashushwa kaburini ila baada ya kukamilisha zoezi lile nilitamani nimfuate mtu yule nimfahamu ila kwa bahati mbaya watu walikuwa wameanza kutawanyika eneo ile japo ilibahatika kumuona wakati akigeuka, alikuwa ni Damasi mwenyewe, sikumuona vizuri usoni kwa kuwa alitumia ndevu za bandia, kofia kubwa na miwani ya jua ila wakati anageuka niliona ile alama shingoni, ikanipa jibu la moja kwa moja kwamba alikuwa ni yeye bila shaka”
“Nilizongwa na mawazo mengi, sikujua lile jambo ilikuwa ni ndoto na hofu iliyo nitawala kwa kumpoteza mwanangu au kulikuwa na shida gani ila kwa baadae nilikuja kuamini kwamba ilikuwa ni kweli. Siku ile usiku, nilifuatwa na watu wawili ambao sikuwahi kuwafahamu kabisa wala kuwaona na baada ya siku ile sijawahi kuwaona tena kwenye maisha yangu. Wanaume wale waliniletea begi, begi ambalo ndani yake lilikuwa limejaa pesa, nikabaki natetemeka na kushangaa nisijue pesa zote zile zilikuwa za nini. Mmoja wao aliiona hofu yangu, akaniwahi na kuniambia kwamba walikuwa ni watu wa serikali na walikuwa pale kwa niaba ya mwanangu ambaye bila shaka walijua kwamba nimetambua yupo hai baada ya kuukagua ule mwili hivyo nilitakiwa kuifanya siri ndani ya moyo wangu hakuna mtu mwingine alitakiwa kuifahamu hata mke wangu wa ndoa ambaye alikuwa mama yake.”
“Watu wale walisisitiza kuhusu jambo hilo na hawakuwa na sababu ya kunipa kwamba ni kwanini yale yote yalikuwa yanatokea zaidi ya kunipa maelekezo kwamba keshoyake usiku nilitakiwa kwenda Mtoni Kijichi usiku nisimame pembezoni mwa lami, ningefanikiwa kukutana na mwanangu na huenda angeyajibu maswali yangu mengi ambayo nilikuwa nayo. Sikuipuuza taarifa ile nikaenda, nilimuona mwanangu akishuka kwenye gari moja ya kifahari akiwa makini ili mtu yeyote asije akamshtukia, alinichukua mpaka ndani ya gari ili tufanye mazungumzo”
“Bila shaka alitambua maswali ambayo nilikuwa nayo ila alinijibu kifupi tu kwamba yeye alifanya yote yale kwa ajili ya familia yake, kama angekataa basi familia yote ingeuawa. Nilitamani kujua sababu ambayo ilimfanya mpaka kufikia hatua ya kuigiza kifo, hakuwa tayari zaidi ya kuniachia namba ambayo aliniambia kukiwa na dharura au shida yoyote niwe naipiga. Kwahiyo hata mimi sijui nini kinaendelea nyuma ya pazia ila mwanangu ni kweli bado anaishi na ni mzima wa afya” hakuwa na namna mzee Kazimoto zaidi ya kuueleza ukweli ambao alikuwa anaufahamu kwa sababu kuficha jambo hilo kungezidi kutengeneza kelele ambazo zingeifichua siri hiyo.
“Ndiyo maana wakati naondoka pale kwako ulipiga simu kumtaarifu kuhusu hilo?”
“Ndiyo”
“Naomba mawasiliano yake”
“Haina haja, anajua kwamba unaenda kumtafuta”
“Wapi?”
“Ukifika Ununio ufukweni kabisa kule, kunja kulia kwako kama unaanza kurudi Bahari Beach, ukipita sehemu yenye migahawa ile na sehemu za watoto kuchezea kuna eneo utaona hakuna watu kabisa na kuna miti miti mingi mithili ya nyika, atakuwa kule anakusubiri hivyo kama una ubavu unaweza kwenda japo binafsi sikushauri uende utakuwa na maisha mafupi” Maelezo yaliyo jitosheleza yalimpa cheko Julius, umaarufu ulikuwa unanukia mbele yake sasa kivipi tena ausikilize ushauri wa mzee huyo ambaye alikuwa anamsisitiza asiweze kwenda huko? Aliona kama mzee huyo alikuwa anampigia kelele.
“Mzee wangu shukrani ziende kwako, nakuahidi ndani ya masaa matatu utaenda kumuona mwanao akiwa amelazwa hospitali na baada ya hapo utajua kwamba ulikuwa unafanya mazungumzo na kijana wa namna gani, mimi sio mtu wa kawaida kama ninavyo onekana nikiwa natabasamu na wewe, nimekamata wahalifu walio shindikana kwenye nchi hii wapo Segerea kwa sasa, nimekutana na wanaume wa shoka itakuwa mwanao ambaye alikuwa mwanajeshi tu wa kawaida? Hapana mzee wangu, nisubiri hapa ili uniamini” hakuwa na muda wa kupoteza tena, alijiamini mno Julius. Aliangalia saa yake, ilikuwa ni jioni tayari na kwa mahesabu yake alijua kabisa kwamba angechelewa kufika huko na kurudi hivyo akatuma taarifa kwa bosi wake na kumpa maelekezo kwamba anaenda kumchukua mtuhumiwa wake wka sababu ana taarifa zote hivyo anaweza akapitiliza muda kwa masaa mawili ila atakaporudi atakuwa amekamilisha kila kitu ila hakujua aina ya mtu ambaye alikuwa anamfuata huenda angemsikiliza mzee Kazimoto.

Julius aliingia kwenye gari baada ya kutoka mahali ambapo alikuwa anamhoji mzee Kazimoto, kwenye kontena lake la siri ambalo alikuwa analitumia kwa kazi hizo maeneo ya Kurasini. Aichagua kuzungukia Bagamoyo road ambayo aliamini ingemfikisha ndani ya eneo hilo kwa muda mfupi zaidi lakini matarajio yake hayakuwa kama alivyo hitaji kulikuwa na foleni kidogo hali ambayo ilimfanya azidi kukerwa na kuwatupia lawama askari wa barabarani kwa kushindwa kuimudu hali hiyo.
Hatimaye alifanikiwa kupenya penya mpaka akafanikiwa kufika eneo la Ununio, alikunja mkono wake wa kulia kushika njia ambayo moja kwa moja ilikuwa inaenda baharini, alisimama sehemu ambayo wenye magari huwa wanatozwa ushuru ili kuingia baharini, alionyesha kitambulisho chake cha kazi akaruhusiwa bila bugudha yoyote. Alitembea taratibu na gari yake aina ya Lexus mpaka nje ya bar moja ambapo aliiacha hapo na kushuka kuanza kutembea kwa mguu, alikatisha katikati ya bar hiyo ambayo ilikuwa imenakshiwa pembezoni kwa picha za asili za kuchorwa za watu mashuhuri wa zamani ambazo zingine zilikuwa zikiuzwa.
Hakuwa na muda nazo wala hakujali kelele za wapiga picha ambao walikuwa wakimzonga na kujinadi kwamba walikuwa wana uwezo wa kumpiga picha kali ambazo hakuwahi kuzishuhudia kwenye maisha yake. Haikuwa siku ya wikiendi hivyo kulipoa na kigiza kilikuwa kimesha anza kuchukua nafasi yake kwa mbaali. Baharini kulikuwa na watu wachache wakiwemo ambao walionekana kuwa wapenzi kwa sababu walitulia kwenye maji wakiwa wanakiss na kuonekana walizama mahabani, alilaani kitendo hicho cha watu kufanyia mapenzi baharini wakati hoteli zilikuwa zimejaa mtaani ila haikuwa biashara yake.

UKURASA WA 28 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 29

Alikunja mkono wake wa kulia kuanza kuelekea sehemu ambayo haikuwa na kitu chochote zaidi ya miti ambayo ilikuwa imeanzia pembezoni mwa bahari na kutengeneza eneo kama nyika ya asili. Upande huo haukuwa na mtu yeyote na hilo alilithibitisha baada ya kuzipita sehemu za migahawa, pamoja na sehemu za watoto kuchezea michezo yao, kitu pekee ambacho alikuwa anakipata ni upepo wa bahari na utulivu wa sauti za mbali za muziki ambazo zilikuwa zinapiga nyuma alikokuwa ametoka huku watu wachache waliokuwepo wakiwa wanaifurahia hali ile. Baharini ni sehemu ya kutuliza akili japo kwake hakuwa hapo kutuliza akili, yeye alikuwa amemfuata mtuhumiwa wake ambaye aliamini kwamba angempatia jina kubwa na umaarufu wa kumfanya aandikwe kile sehemu kwa kumkamata mtu ambaye aliigiza kama amekufa kwa miaka miwili.
Bastola yake ilikuwa kiunoni, kujiamini kwake ndiko ambako kulimfanya aelekee ndani ya eneo hilo bila kujiuliza mra mbili akiamini kwamba uwezo wake ulikuwa ni zaidi ya kila kitu hivyo hakuna kitu kibaya ambacho kilikuwa kinaweza kumtokea kwenye maisha yake. Mikono yake alikuwa akiiamini kwa asilimia kubwa, uzoefu wake kwenye hiyo kazi yake ulimtoa shaka na kuamini kwamba mtu huyo hata kama angekuwa na wenzake bado asingeshindwa kumfikisha kituoni. Alijitwika ugwiji Julius, kujiamini kukazidi uhalisia, akawa hana hofu.
Wakati anaanza kuingia eneo ambalo lilikuwa na hiyo miti mingi, aliitoa sigara kwenye mfuko wake na kuirushia mdomoni, midomo yake yote miwili ikaidaka kisha akakiwasha kiberiti chake cha gesi na kukisogeza ilipo sigara. Alisimama na kuuvutia moshi kwa juu kwa hisia kali ambazo zilijionyesha ndani yake, aliangaza kila upande sigara yake ikiwa bado mdomoni lakini hakuona mtu yeyote hivyo akaamua kusogea mbele zaidi ambapo alitembea kwa dakika moja tu pekee.
Aliivuta sigara yake taratibu kwa dakika tano mpaka ilipo teketea yote, bado hakuona mtu. Nafsi yake ilianza kukata tamaa akihisi kwamba mzee yule huenda alikuwa amemdanganya, aliichanganua akili yake kama inawezekana baba mzazi amuingize mwanae kwenye hatari ya namna ile? Jibu lilikuwa ni hapana, hapo akagundua kwamba alikurupuka kuweza kuyaamini maneno ya mzee yule isingekuwa rahisi namna hiyo kumuingiza mwanae ambaye dunia nzima iliamini kwamba amekufa kwenye mkono wa sheria kirahisi namna hiyo. Akajumlisha kwamba alidanganywa bila kutumia akili, moyo wake ukaghafilika, aligubikwa na hasira za wazi ambazo zilijionyesha baada ya kutukana tusi zito kwa sauti ya chini huku akimlaani mzee Kazimoto ambaye ni hakika angeenda kumkoma akirejea kwa sababu muda ambao alikuwa amepewa na mkubwa wake ulikuwa unaelekea tamati hivyo asingeupata wakati mwingine tena.
Aligeuka na kuanza kuzitupa hatua zake kurudi kule alikokuwa ametokea lakini alisita, alisita kwa sababu masikio yake yalimtekenya. Ule mtekenyo ambao aliupata haukuwa wa hisia bali alisikia hatua za miguu ya mtu ambazo bila shaka zilikanyaga kwenye mti mkavu ambao ndio ulipiga kelele. Aliivuta bastola yake taratibu kuitoa kwenye kiuno chake kisha akajibanza kwenye mti mmoja akisubiri kuhakiki kama kile ambacho alikiwazia kilikuwa ni cha kweli au ni hasira zake zilimfanya ahisi jambo hilo.
Mjongeo wa sauti za mtu kuja upande ule ziliongezeka kadri sekunde zilivyokuwa zinazidi kwenda, mapigo yake ya moyo nayo yalizidi kukita kwa nguvu asijue ni kwa namna gani alikuwa anaenda kumhimili mtu ambaye alidanganya kifo. Akiwa kwenye hiyo taharuki sauti za ile mijongeo zilikoma ghafla, alitulia kwa dakika nzima lakini hakusikia chochote kikija upande wake hivyo akaamua kuchomoka kwa umakini bastola yake ikiwa kwenye mkono wake ili kuweza kukabiliana na hatari yoyote ile ambayo angekutana nayo mbele yake.
Kuchomoka kwake ni kama alikuwa anasubiriwa, umakini wake kwenye uchomokaji ulizingatia zaidi usalama wake kwani hakujua bado kama kulikuwa na mtu alisimama maeneo ya karibu na hata kama alikuwa hapo hakujua kama ni mtu mmoja au kulikuwa na watu zaidi ya mmoja ndiyo maana alihitaji kwenda kwa mahesabu kwenye kila maamuzi ambayo alikuwa anayafanya hapo. Kuchomoka kwake ilikuwa ni hatari zaidi kwa upande wake kwa sababu alishangaa kuna kitu kinakuja kwa kasi kuelekea ile sehemu ambayo alikuwepo. Alijitahidi kukwepa lakini ni kama alichelewa kiasi, kisu kilikuwa kimelenga kwenye kile kiganja chake ambacho alishikilia bastola yake.
Bahati kwake wakati anauvuta mkono wake kisu kilikita kwenye bastola ambayo ilirushwa mbali. Tukio hilo alilishuhudia kupitia mwanga ambao ulikuwa unazidi kufifia wakati kiza kinataka kuichukua anga nzima. Alinyanyua uso wake huku akiwa anavinyoosha vidole vyake ambavyo vilivuruzwa kidogo na kile kisu na kuifanya dole gumba kuchubuka na kutoa damu, alipo yainua macho yake; mbele yake alikuwa amesimama mwanaume ambaye usoni kwake alikuwa amevaa hood, hakuwa anaonekana vizuri sura kwa sababu hood ilimfunika vizuri mpaka kwenye macho yake.
Alivaa suruali aina ya track ikiwa ni kama ishara ya mtu ambaye alitoka mazoezini wakati huo, chini alivaa raba aina ya Adidas ambazo huwa wanapenda kuzitumia wana mazoezi kutokana na uimara wake bila kusahau namna inavyokuwa inamkaa mtu vyema kwenye miguu yake. Mwanaume huyo alisogea hatua kadhaa kuelekea pale alipokuwepo Julius ambaye hakuwa na wasiwasi zaidi ya kumshangaa mwanaume huyo, hakuwa na presha kwa sababu aligundua kwamba mtu huyo alikuwa pekeyake hivyo wangeongea kikubwa zaidi wakiwa wenyewe huko mitini.
Mwanaume huyo baada ya kuhakikisha amebakisha hatua kadhaa kumfikia Julius, aliitoa hood yake usoni na kubakia kichwa wazi. Julius alihisi bado yupo ndotoni, hakuamini kile ambacho alikuwa anakiona mbele yake, ni kweli kabisa alikuwa Damas mwenyewe, mwanaume ambaye miaka kadhaa nyuma sifa zake ziliimbwa kila sehemu na kuchukuliwa kama mfano kwa vijana wazalendo wapatikanao jeshini na ndani ya jeshi la polisi. Damasi alitabiriwa makubwa na kuja kuwa moja kati ya wanajeshi bora zaidi ndani ya nchi ya TANZANIA lakini mwanaume huyo miaka miwili iliyokuw aimepita, maiti yake ndiyo ilirudi kitu kilichofanya azikwe ila wakati huo Julius alikuwa anamshuhudia kwa macho yake mawili akiwa wa afya njema kabisa mbele yake.
Kichwani kwake alikuwa amefuga rasta ambazo alizifungia kwa nyuma, Damasi alikuwa mbele ya Julius, si alitamani kumkamata? Basi ilikuwa imebakia kazi kwake kuweza kuondoka naye na kwenda kuupata umaarufu ambao alikuwa akiuhitaji.
“Ni miaka miwili sasa tangu taifa liweze kuomboleza kifo chako wewe na wanajeshi wengina lakini upo salama kabisa unaishi na hauna tatizo lolote lile, Kuna kitu gani hasa ambacho kimekupelekea mwanajeshi mwadilifu kama wewe kubadilika namna hiyo na kuishia kuwa mhalifu huku ukidanganya kifo chako” Julius aliuliza akiwa amezongwa na hasira kwenye uso wake, hasira ambazo zilimfanya mapigo yake ya moyo kuongezeka. Damasi kabla ya kumjibu Julius, aliiwasha saa yake na kuitazama kisha akainua macho yake kumuangalia Julius;
“Una dakika tano za kuondoka hapa ukiwa hai, kama utafanikiwa kutoka hapa basi usije kujaribu kuuliza maswali ya kipumbavu tena kama hayo kwenye maisha yako yote. Ukiishi leo basi tafuta kijiji chochote ambacho hakifuatiliwi tena na watu kaishi huko na dunia isije kutambua kama uliwahi kuishi na kuwa hai”
“Unanitisha mimi?”
“Kwa sababu hata nikikuacha hai bwana mdogo kuna watu watakuua tu ndani ya nusu saa ijayo”
“Nijibu maswali yangu, kwanini unayafanya hayo yote?”
“Umekuja kunikamata ili ukanihoji sio kuanza kunibembeleza mimi nikujibu bwana mdogo, umefanya kosa kubwa la kutambua kwamba nipo hai kwa sababu inatakiwa ufe wewe na wenzako wote ambao ulikuwa nao siku ya leo”
“Unamaanisha nini?”
“Mpaka muda huu baba yupo njiani kurudi nyumbani, askari wenzako wote tayari wamekufa kule ulipo waacha, hili ni jambo ambalo kila anaye zipata hizi taarifa lazima afe” Damasi maelezo yake yalikuwa yanafuatiwa na hatua zake kusogea pale alipokuwepo Julius, hakutakiwa kuendelea kuongea tena kwa sababu alitambua kitu ambacho kilikuwa kinafuata hapo.

UKURASA WA 29 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 30

Ngumi kali ilirushwa kwenye uso wake, akasogea nyuma, aliteleza bila kutarajia kwani ilikuwa ni ghafla. Aliupanga mkono wake akiwa anakuja kwa hasira na jaziba kali, aliukunjua mkono wake kwa mara ya kwanza akiwa amerusha ngumi nzito ambayo iliishia kwenye tumbo la Damasi, alihisi amepiga chuma kwa sababu tumbo lilikuwa limekomaa vya kutosha. Aligeuka kwa teke moja maridadi ambalo lilitua kwenye shingo ya Damasi, mguu wake ulipata maumivu kiasi kwani alionekana kutoukaza zaidi na baada ya kukita kwenye shingo hiyo ambayo ilikazwa kiasi chake aliumia.
Alirudi nyuma akiwa anachezesha chezesha mguu wake, alimkimbilia Damasi ila hatua zake zilikuwa taratibu mno. Damas aliubetua mguu wake wa mbele na kujirusha sarakasi ya nyuma kwa kasi ambapo wakati yupo hewani alijisogeza mbele hali ambayo ilifanya miguu yake kukita kwenye kifua cha Julius na kumfanya adondoke chini kwa kujibamiza. Alinyanyuka haraka akiwa anajipinda kujinyoosha, aligeuka kuangalia bastola yake ilikuwa mbali, hakuona kama alikuwa na uwezo wa kushindana na mtu huyo zaidi ya kuifanikiwa kuipata bastola hiyo ambayo ilikuwa mbali. Kupiga mahesabu ya ile bastola kulimpotezea umakini mpaka alipo shtuka kuona mchakacho wa mtu akija kwa kasi upande wake, aliinama chini teke likamkosa juu, aliuzoa mguu mmoja wa Damasi ambao ulisalia chini na kumkita Damasi ngumi ya mbavu.
Kwa namna alivyo mzoa alitakiwa kudondoka vibaya lakini haikuwa hivyo Damasi alidunda kwenye mti ambao ulikuwa pembeni yake kisha akatua chini kwa mkono mmoja, alijigeuza na kusimama kama hakuna kitu kilitokea. Hakuamini alicho fanyiwa na askari huyo ambaye alikuwa ameanza kuzipiga hatua zake kuelekea ilipo bastola yake. Alikimbia na kudunda chini kwa sarakasi ya mbele akatua mbele ya Julius ambaye alishtuka ila mshtuko wake ulikuwa hauna faida baada ya kupigwa na kiganja kikali cha shingo na kumfanya aishike shingo yake. Alichotwa miguu yake ghafla bila kutarajia akiwa anaambaa ambaa hewani Damasi alijigeuza hewani kisha akatua kwenye mwili wa Julius na flying kick nzito ambayo ilimpata kifuani.
Hakuwa na balansi zaidi ya kujibamiza kwenye mti mmoja na kudondoka chini akiwa anahema kwa nguvu na mashaka mengi, maisha yake yalikuwa hatarini hivyo akajilazimisha kivivu kuweza kusimama kujipigania. Muda ulikuwa umetumika mwingi mno, Damasi alikuwa mbele yake tayari kumuwahisha alikokuwa anastahili kuwepo, aliona ngumi inakuja usoni, akajisogeza pembeni hali ambao iliifanya ngumi hiyo kutua kwenye mti na kubandua ganda lake. Wakati anahema aligundua kwamba tumbo lake lilikuwa kwenye maumivu makali, alijigusa tumboni na kugundua kwamba alikuwa amechomwa na kisu mpaka yeye mwenyewe akabaki anashangaa kwa sababu lilikuwa ni tukio la ghafla.
Wakati bastola yake inakutana na kisu na kurushwa mbali, kisu kile kilijichomeka kwenye mti hivyo wakati amepigwa na kudondoka kwenye ule mti juu yake ndipo kilikuwa kimekita kisu kile, kufanikiwa kuikwepa ile ngumi kulimfanya Damasi kuchomoa kisu kile na kumkita nacho tumboni. Alisimama akiwa anayumba yumba kwa maumivu ya mwili na tumbo lake ambalo kwa wakati huo lilikuwa linatoa damu ya kutosha, alijitahidi kuhitaji kujiokoa au kuyapambania maisha yake wakati huo ikiwezekana akimbie lakini alikuwa amechelewa kwa sababu Damasi hakumpa hiyo nafasi. Kila alipo jaribu kurusha ngumi alikutanishwa na kisu, ndani ya dakika moja mwili wake ulikuwa umechomwa visu kila sehemu hali ambayo ilimpa wakati mgumu hata kwenye upumuaji wake, aliishia kudondokea kwenye mti mmoja na kuuegamia huku akiwa anahema kwa shida.
Damasi alimsogelea kwenye ule mti akiwa anamwangalia kwa masikitiko kijana yule, alichuchumaa karibu yake akiwa anamwangalia usoni;
“Bwana mdogo hii dunia haipo kama ambavyo unataka wewe iwe na haiwezi kuja kutokea kuwa hivyo. Hii dunia ipo sio kwa sababu ya kila mtu ila kuna watu mnaletwa duniani kusaidia wengine kuishi na kukamilisha mambo yao. Haukutakiwa kuendelea na hii kesi lakini kwa sababu uliuhitaji umaarufu basi ukaamua kujitwika ufahari ambao haujui umeanzia wapi na unaishia wapi. Swali ambayo ulipaswa kujiuliza kabla ya kuanza kulifuatilia jambo hili ni kwamba, kuna sababu gani hasa ya msingi ambayo inamfanya mpaka mtu anaigiza kifo na kuamua kujitoa kwenye uso wa dunia ambayo kila mtu anautaka umaarufu? Ungekaa na kutafakari kwa umakini ukalipata jibu la hilo swali basi binafsi tusingefikia hapa ulipo muda huu” Damasi aliyaonyesha masikitiko yake akiwa anamwangalia Julius usoni kiza kikiwa kinafunika kabisa pande zote na taa zikiwa zinang’aa kutokea kila pande ya jiji la Dar.
“Kwanini unayafanya haya yote?”
“Ili niishi”
“Kuishi kwa kuua wengine?”
“Ungekuwa na muda wa kuishi ningekwambia kajifunze kuhusu maisha ya wanyamapori, kuna wanyama ili waishi lazima waue wanyama wengine na ipo hivyo kwa wanadamu pia; ili baadhi ya watu tuishi basi hatuna budi kuyachukua maisha ya watu kama nyie”
“Hili litakuwa na mwisho Damasi, siri yako ilishafichuka tayari na kumbuka hakuna baya ambalo huwa linaikwepa aibu baadae”
“Basi ngoja tuone hiyo aibu inakuja vipi ila kwa wewe haustahili kuendelea kuishi kwa wakati huu, nenda kajitetee juu ya dhambi zako ambazo umeziacha hapa duniani” Aliongea kwa msisitizo akiwa anaukaza mkono wake wenye kisu. Alikiinua kwa nguvu na kukita kwenye koromeo la Julius kisha akakizungusha hali ambayo ilifanya shingo yake kuchanika chanika vibaya. Roho ilikuwa imeacha mwili, umaarufu ulikuwa umemponza Julius na kumfanya afe akiwa na ndoto nyingi kichwani. Hakujua njia ya kwanza ya mtu kuishi inatakiwa kwanza ujifunze namna ya kuishi na mifumo mpaka pale unapokuwa na nguvu kubwa ndipo uchukue maamuzi magumu. Tamaa ya mafanikio ikayakatisha maisha yake kupitia mkono wa Damasi ambaye baada ya kukamilisha jambo hilo, alitoweka kwenye hilo eneo kukiwa na kiza kinene tayari akiwa na kisu chake mkononi taratiiibu akiufurahia upepo wa bahari ambao ulikuwa unapuliza kwa mbali.

Asubuhi sana wakati ambao muokota makopo mmoja alikuwa anazunguka baharini kujitafutia makopo kwa ajili ya kujipatia ridhiki yake, alishtushwa na sauti za mbwa wakipiga makelele. Alitamani kudadisi kujua kilichopo huko ndipo alipo shangazwa baada ya kuona mbwa wakiwa wanagombana karibu na mti, aliwarushia mawe na kuwafanya wakimbie eneo lile huku akizidi kusogea taratibu. Alipiga yowe kali baada na kutupa mfuko wake baada ya kugundua kwamba aliyekuwa pale alikuwa ni binadamu asiye na uhai.
Yowe lake lilisindikizwa na utimuaji mkali wa mbio ambao uliwafanya hata wale mbwa ambao walikuwa karibu kukimbia kwani walihisi mtu yule alikuwa akiwafuata kule ambako walikuwepo. Bwana yule mbio zake ndizo ambazo ziliwashtua watu wengine ambao walikuwepo asubuhi hiyo ya mapema pale ufukweni hususani wafanyakazi na baadhi ya watu wachache wengine wakiwemo wazungu. Iliwalazimu kumfuata na kumkamata ili awaeleze alicho kiona kiasi kwamba aanze kupiga makelele kiasi kile kwa hofu kubwa.
Aliwasogeza mpaka lile eneo ambapo wengi wao walishangaa kuona mwili wa mtu ukiwa umeuliwa kikatili namna ile, hawakuelewa ni kipi hasa kilitokea na mtu yule alikuwa ni nani mpaka mfanyakazi mmoja alipofanikiwa kumtambua. Alieleza kwamba bwana yule jana yake alifika na kupaki gari yake ambayo mpaka wakati huo ilikuwepo ila hakujua kwamba alikuwa amekuja kufuata kitu gani ndani ya lile eneo. Kuna baadhi ya watu walianza kurekodi video na kuzisambaza huku mwanaume mmoja mzungu akisogea pale ulipokuwepo mwili ambao shingo iliharibika vibaya na eneo lile kutapakaa damu kila kona. Alimkagua kwenye mifuko yake na kubahatika kukuta vitambulisho vyake, sigara, kiberiti cha gesi na waleti ambayo ilikuwa na pesa za kutosha ndani yake.
Kitambulisho kilionyesha wazi kwamba alikuwa ni askari bwana yule hivyo wakafanya jitihada za kupiga simu polisi ambapo muda mfupi ulio fuata polisi walifika kwa wingi eneo lile na kuligeuza kuwa crime scene (eneo la tukio la uhalifu) huku wakizuia watu kufika pale na kumpongeza yule mzungu kwa msaada wake wa kupiga simu wakimtaka pamoja na yule muokota makopo kwa ajili ya maelezo zaidi. Lakini kwa bahati mbaya kuna watu tayari walikuwa wamesha isambaza video hiyo kwenye mitandao ya kijamii baada ya kurekodi lile tukio mahali pale hali ambayo ilianza kuzalisha taharuki kwa wananchi juu ya kifo cha askari yule.

UKURASA WA 30 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 31

Mr Ndatu, alikuwa ndani ya ofisi yake maeneo ya Posta akiwa mwingi wa tafakari ambayo ilimfanya akose raha. Kukosa kwake raha ilikuwa ni baada ya kupokea taarifa mbaya za kifo cha kijana wake ambaye alimuamini, kijana ambaye alikuwa akimsaidia kwa kiwango kikubwa ili aweze kuzitimiza ndoto zake. Kufa kwake kwa namna fulani hata yeye alijiona kuwa na hatia ya kuhusika na tatizo hilo kwani huenda asingemchagua au kumtuma kwenye kesi hiyo basi angekuwa hai mpaka wakati huo. Alijihisi hatia..
Akiwa hapo alikumbuka jana yake usiku akiwa anamsubiri kijana huyo ofisini kwake, alisubiri bila mafanikio huku muda aliopewa ukiwa unayoyoma. Alipokea meseji ikimtaarifu kwamba kuanzia wakati huo alitakiwa kukaa mbali na kesi hiyo. Zoezi hilo lilikuja baada ya kupiga simu nyingi kwa kijana wake huyo bila mafanikio ndipo akaamua kufuatilia kilichokuwa kinaendelea kuanzia kesi hiyo inaanza mpaka wanafikia hatua hiyo. Alipata taarifa kwamba Julius alienda kumkamata mzee Kazimoto hivyo akasafiri mpaka huko kwa ajili ya kupata dodoso lakini habari ambazo alikutana nazo kwa mzee huyo ni kwamba kijana huyo alimchukua kwenye gari akamhoji kisha akamrudisha tena kwake hivyo hakujua kilicho endelea.
Alihitaji kwenda kwenye kaburi la Damasi, alipelekwa huko na kukuta likiwa limejengewa vizuri kabisa pamoja na kuwekewa malu malu ambayo ilikuwa inang’aa, hakuwa na lingine zaidi ya kuondoka eneo hilo. Asubuhi alipata taarifa kwamba kijana huyo alionekana kwenye ofisi ya mkemia mkuu wa serikali ambapo baada ya kufanya nao mawasiliano alipewa maelezo yote juu ya vipimo vya DNA ambavyo alivifuata huko na majibu yake. Akawa njiapanda asijue kwamba alikuwa anafanya vipimo vya kujua habari ya nani maana jioni yake alimuaga tu na kumpa taarifa fupi kwamba kesi yake ilikuwa imekamilika na wakati huo alikuwa anaenda kumfuata mhusika.
Sasa huyo mhusika alikuwa ni nani? Alikosa jibu sahihi juu ya hilo swali lake. Aliingiwa na wasiwasi kwamba huenda labda alifanikiwa kuipata mifupa ya mwili wa Damasi? Lakini hilo halikuwa jibu sahihi kwani alilishuhudia kaburi la mtu yule likiwa limejengwa vizuri tu akaishia kuchanganyikiwa kiongozi huyo. Akiwa ndani ya ofisi yake na maswali mengi ndipo akapokea taarifa nyingine kwamba Kurasini imekutwa miili ya maaskari watatu ikiwa imeuliwa kwa risasi kwenye kontena moja ambalo liliachwa wazi hali ambayo iliwafanya watu kadhaa ambao walikuwa kulewa wakati wanarejea asubuhi kukutana na damu nje ya kontena hilo na baada ya kuangalia ndani ndipo wakakutana na miili ya hao askari wakaamua kuripoti polisi.
Alibaki ameduwa asijue ni wapi alikuwa anapaswa kuanzia na ni kitu gani hasa kilikuwa kinatokea, jambo ambalo lilimchosha zaidi ni baada ya kupata taarifa kwamba askari hao kwa mara ya mwisho kuonekana walikuwa na Julius ambaye alikutwa ameuliwa kikatili huko ufukweni. Alibeba koti lake la suti na kutoka ndani ya ofisi yake, kiti hakikuwa kikikalika tena asubuhi hiyo na uwezo wa kuifuatilia kesi hiyo hakuwa nao, akaamua kwenda kulewa tu.





TANDALE KWA TUMBO.
Alionekana kijana mmoja ambaye uso wake ulikuwa umesawajika, uso uliokata tamaa ya maisha. Hiyo haikusababishwa tu na chozi ambalo lilikuwa likimdondoka kutoka kwenye macho yake ya thamani, lahasha! Bali namna alivyokuwa ameuweka uso wake, ni wazi kichwani kwake ni mengi yalikuwa yanapita kama sio kumuelemea, alionekana kufikia hatua ya mwisho kabisa ya uvumilivu wake ndiyo maana aliamua kujipooza kwa chozi ambalo huenda lilishuka bila yeye mwenyewe binafsi kupenda kufikia kwenye hali hiyo.
Aliketi kwenye kivaranda kidogo ambacho kilikuwa ng’ambo ya kibanda kimoja kibovu, kibanda ambacho kilijaa masizi. Kilikuwa kibanda cha kuchomea dagaa wauzwao kwa bei rahisi kwenye mitaa ya waswahili ambao kukamilisha milo mitatu kwa siku kwao ni zaidi ya kuishi Masaki. Alivaa shati kubwa mithili ya mtu wa Arusha ikiwa imechoka, kisha pensi ambayo ilikuwa imekomaa kwa sababu ya kutofuliwa kwa muda mrefu ilikuwa imeziba sehemu zake za siri na kumsitiri. Miguu yake haikuwa peku, alivaa kandambili ambazo moja ilikuwa imetoboka upande wa nyuma kwa sababu iliisha kwa kiasi kikubwa, zilikuwa ni dalili kwamba ilikuwa ikivaliwa mara nyingi zaidi.
Kutoboka kwake kuliifanya kuruhusu maji machafu kupenya kwenye mguu wake ila hata hivyo hakujali kama sio kukosa namna ya kufanya kwa sababu uchumi ulimchumu. Kandambili nyingine ilikuwa imeshonwa mbele kwa nyuzi nyingi, nyuzi ambazo nazo zilikuwa zimeoza, alikatisha tamaa kijana yule kumwangalia. Alikuwa amejishika tama akiwa anaiangalia dunia ilivyokuwa ikimzomea hali ambayo ilimfanya kuchukia kila ambacho kilikatiza mbele ya macho yake. Alijikuta anawachukia kwa kiwango kikubwa walimwengu, alimchukia kila ambaye alikatiza kwani alimuona kama ndiye chanzo cha matatizo yake! Hakika moyo wake ulikuwa na mengi ya kuusimulia ulimwengu lakini angemsimulia nani kupunguza machungu kwenye jiji hili ambalo kila mtu huwa anajiangalia yeye tu? Alizubaa, alishindwa kujiokoa, msaada pekee ambao ulikuwa karibu kwake ulikuwa ni kutoa machozi.
Kilio chake kilisababishwa na mwanadamu ambaye yeye alimpenda, alimnadi kwenye moyo wake na kumpatia soko kubwa lakini ajira zilimpita kwa mtu huyo. Aliyaangaza maisha ya familia za Montague na Capulate kule kwa waitaliano basi akajipa u-Romeo na huyo mtu ambaye alimpenda akampa u-Juliete. Ugwiji wa kujihisi anajua zaidi kuinadi biashara ya moyo alijivika ushujaa wa Jack kwa Rose wa Titanic akasau kwamba wanadamu hawana kumbukumbu hivyo inatakiwa kuwa na kiasi cha kutenda wema kwa ajili ya usalama wake binafsi. Akazama jumla jumla kwa kumkopesha imani binadamu aliyezaliwa na mwanamke, malipo yake akawa anatia huruma kwa walimwengu ila hakuna ambaye alikuwa na muda naye.
Joel John ndilo lilikuwa jina la kijana huyo, mtaani kwake wengi walipenda kumuita Double J lakini jina lililompa umaarufu likawa ni Joh yaani kufupisha mambo yasiwe mengi lakini kwa wakati huo alikuwa kama mfiwa. Kwenye harakati zake za upambanaji wa maisha kwenye viunga hivyo ambavyo wanaishi watu wenye maisha ya hali ya chini sana, sehemu ambazo watu wanafanya chochote ili tu waishi, sehemu ambayo wanawake hawaoni taabu kabisa kufanya biashara za miili yao tena kwa bei ya supu tu mtaani kikubwa wanacho jali ni kutia mkono kinywani. Joh alikuwa ni mtoto wa mtaani haswa, alizijua kona nyingi za mtaani hapo na kumfanya kuwa maarufu kwa kila mtu na kwa ucheshi wake akawa kipenzi cha wengi japo hakuwa na chochote cha kumpa ufahari wala heshima. Wengi walimpenda kwa sababu alikuwa akiwachekesha ila hakuna ambaye alimheshimu, mjini inaongea pesa bwana! Ndivyo wengi walikuwa wakitamka, yeye hakuwa na thamani kabisa mbele yao, hakuwa na pesa Joh.
Joh, alibahatika kumpata mtoto mmoja wa kienyeji mtaani, mwanamke ambaye alikuwa na maisha ya chini kama yeye. Joh alikuwa anajituma na kupata vibarua kadhaa ambavyo vilimfanya kumpatia angalau pesa za supu mrembo huyo wa mtaani, mwanamke ambaye huenda hakuijua thamani yake kwa sababu ya maisha mabaya ambayo yalikuwa yanamzonga. Hakuwa na namna zaidi ya kuolewa na kijana Joh ambaye walidumu kwenye mahusiano kwa mwezi mmoja tu pekee ndipo wakaamua kuishi kama mume na mke.
Joh alimpenda mwanamke huyo, kila siku iliyokuwa inaenda alizidisha mapenzi kiasi kwamba akawa tayari kufanya lolote lile ili mkewe afurahi. Mwanzoni yalikuwa kama mapenzi ya ahadi ambayo yameandikwa kwenye tenzi za maandiko matakatifu, hali hiyo ilimfanya Joh ajinyime, Joh hakupendeza hata kidogo, Joh alikuwa wa hovyo lakini alihakikisha mkewe angalau anapata kanga kadhaa, alijikakamua kununua madera ya kuvaa ili aendapo kwenye shughuli za wenzake mkewe asihangaike wala kupata aibu. Mwanaume akayavaa majukumu, akazibeba changamoto na kuamua kuishi nazo kifuani kwake bila kuendekeza malalamiko kutoka sehemu yoyote ile maana msaada wake zilikuwa nguvu zake mwenyewe.
Kumpa kipaumbele mkewe na kujisahau yeye, kumfanya mkewe malkia na kumpatia kila ambacho alikitolea jasho, likawa kosa kubwa la maisha yake! Kosa ambalo lilimfanya aishie kukaa kwenye kile kivaranda karibu kabisa na kwa mama muuza dagaa. Ule uzuri wa mkewe ambao ulijificha kwenye maisha magumu ukaanza kujionyesha taratibu, licha ya kupata vipodozi vya bei rahisi ndani ya soko la Manzese na mwanamke huyo kuwa na uwezo wa kubadili nguo angalau kila siku japo za soko la Karume na Manzese! Taratibu ule uzuri wake ukaanza kujifunua.

UKURASA WA 31 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 32

“CHEMA CHAJIUZA, KIBAYA CHAJITEMBEZA”, walisema hivyo wahenga, mkewe akaanza kuongelewa chini chini na watu mtaani, akaanza kuzua gumzo kila akipita mahali. Kuongelewa kwake kukamfanya kuanza kupata jina na umaarufu kwenye vinywa vya watu. Sio kila binadamu huwa anapenda kuhadithiwa, kuna watu huwa wanapenda kujionea vitu kwa kujaribu! Mke wa Joh akaingia kwenye mtego wa wanaume ambao wengine kwao pesa haikuwahi kuwa tatizo kabisa hivyo kumlipa au kumuahidi pesa likawa jambo dogo na kupitia ufukara wa kuzidi kipimo wa mumewe! Wengi walijua watampata tu.
Vishawishi vikaanza kutia doa penzi lake, mkewe akawa anatongozwa na wanaume ambao walisifika kwa biashara kadhaa ndogo ndogo Tandale na Manzese. Ndipo hapo ile tabia halisi ya mkewe ikaanza kujionyesha wazi. Mwanamke huyo likawa pumzikio la kila mwenye pesa huku mumewe asijue jambo, wanaume wenzake walikuwa wanamng’ong’a mtaani kwa sababu walizijua mpaka rangi za chupi za mkewe, walimsaidia mkewe kufika kileleni, nani angemheshimu? Joh hakujua bado akawa anajinadi kuwa na mke merembo! Mke? Mke au jike? Nafsi yake bado iliamini kuwa anapendwa, maskini Joh!.
Mkewe sasa akawa na uwezo wa kuzishika pesa kuliko yeye, hapo ndipo dharau za wazi zikaanza, vituko vikawa haviishi ndani. Mke akaanza kudai mahitaji ambayo alijua kabisa Joh hana uwezo wa kuyatimiza, licha ya Joh kuahidi kumfanyia mwanamke huyo kila kitu hakuna kilicho badilika ikawa leo ni afadhali ya jana, Joh akaamini kwamba ni mambo ya kawaida yangetulia! Alikuwa mjinga wa mahaba. Akawa anapata simulizi fupi fupi mtaani kumhusu mkewe, aliambiwa mkewe karibia kila mtu mtaani hapo ambaye alimtaka basi alikuwa amemvua chupi tayari, yeye alikuwa anawatunzia wenzie wanakuja kula pipi bila maganda. Alighafilika moyoni, alishikwa na jazba ila hakuwa na cha kufanya ikambidi kumuuliza mkewe kwa upole lakini alicho ambiwa ni kwamba hana uwezo wa kuhudumia hivyo awaache wenye uwezo wajilie kwa raha zao.
Kauli ilimvunja moyo, iliurarua moyo wake, alihisi kuna mtu anampiga na pasi ya umeme moyoni ila hakuwa na la kufanya. Alijaribu kujifariji lakini ilishindikana, aliamua kujipa moyo kwamba mkewe alikuwa anataka kumuumiza tu ila taarifa hizo hazikuwa za kweli lakini stori zilizidi kila sehemu mpaka alipo gundua kwamba hata marafiki zake walikuwa wanamvua chupi mkewe. Alitahamaki huku dunia ikiwa inamcheka, hakuwa na uwezo wa kufanya kazi tena, akawa kama mtu anaye tapa tapa huku na huko kwa wiki kadhaa mpaka siku moja alipo mkuta mkewe akiwa na wanaume kwenye chumba kimoja kibovu kibovu ambacho alipanga na alikuwa anakitumia kuishi na mwanamke huyo.
Alimfumania mwanamke huyo akiwa uchi kabisa huku akiwa anafurahia kufanya mapenzi na wanaume wawili kwa wakati mmoja. Alidondoka chini kwa presha lakini hakuna aliye mjali, sio kwamba hawakumuona lahasha! Bali hakuna mtu ambaye alikuwa ana muda naye, alilia sana kwa uchungu ila hakupata msaada. Alinyanyuka kwa taabu akiwa anajivuta kwa kujikongoja mithili ya mtu ambaye alikuwa amechanganyikiwa na kwenda kuishia kwenye kile kivaranda ambacho alikuwepo wakati ule. Alikuwa amelia kwa masaa matatu lakini bado chozi halikuacha kulalamika kwa kushuka kwenye mashavu yake.
Watu walikuwa wanampita sio kwamba hawakuwa wakimuona bali ndio wale ambao wengine walishiriki kumuumiza, watu wakawa wanamuona yeye ni mwanaume mjinga asiye na akili hivyo wengi walimcheka na kwenda zao akabaki mwenyewe akiwa anamlaumu muumba kumleta hapa duniani. Moyo wake ulikuwa na mengi ya kuyaandika ila kwa bahati mbaya aliukosa wino wa kuelezea hisia zake hali ambayo ilimfanya faraja pekee ibaki kutoa machozi akitamani kujiua.
Akiwa amekata tamaa, akiwa amewaza kwenda kuyatoa maisha yake kuliko kuishi dunia yenye ushenzi na uonevu kiasi kile, pale alipokuwepo alihisi kwamba kuna mtu mwingine alikuwa ameongezeka. Hakuwa amemuona kwa sababu alikuwa amejiinamia mikono yake akiwa ameipitisha kichwani, ni harufu ya manukato ya gharama ndiyo iliziumiza pua zake na kumfanya atambue kwamba kulikuwa na mgeni aliyeongezeka ndani ya eneo lile. Marashi hayo yalikuwa ya gharama mno kiasi kwamba aliamini kwa mtaa ule hakuna mtu ambaye angefanikiwa kuyamudu ndiyo sababu ambayo ilimfanya kuinua uso wake uliokuwa umejikunja kwa kulia kwa muda mrefu huku chozi likiwa linachuruzika taratibu.
Pembeni yake alikuwa ameketi mwanaume mmoja aliyekuwa amependeza na kuvutia mno, mwanaume huyo alikuwa ndani ya suti ya gharama huku pale alipokuwa ameketi akiwa amekiweka kitambaa safi ili suti yake isichafuke. Alikaa mkao wa kukunja nne huku kwenye uso wake akiwa na miwani myeusi na cigar ya bei ghali kwenye mdomo wake akiwa anaivuta taratibu na hapo ndipo Joh aligundua kwamba hakuipata harufu kali kutokana na kwamba ilikuwa ya bei ghali tofauti na zile sigara za mtaani. Katikati yao ilikuwa imewekwa briefcase (begi ambazo zinatumiwa zaidi na wafanya biashara hasa kuwekea vitu vya thamani).
Akiwa bado ameduwaa asijue sababu ya mtu huyo kuja hapo alipo, mwanaume huyo aliitoa cigar nyingine kwenye mfuko wake wa koti na kumpatia Joh. Aliogopa kuipokea ila mtu huyo alionyesha msisitizo usoni kwake baada ya kuivua miwani, aliipokea huku akiwa anatetemeka mno lakini mwanaume huyo hakujali zaidi ya kutoa kiberiti cha gesi cha gharama na kumuwashia. Akawa anaufaidi moshi wa gharama ambao aliuwa ameuona mara kadhaa kwenye tamthilia tu.
“Hiyo unayo ivuta muda huu bei yake ni shilingi laki tano za kitanzania” alishtuka baada ya kusikia sauti nzito ya mwanaume huyo. Ilikuwa ni sauti ya mamlaka tena kavu yenye kukwaruza kidogo. Ilimfanya kuhitaji kuirudisha kwa sababu bei aliyo tajiwa kama angeambiwa alipe hapo alikuwa anafia jela, hiyo ni pesa ambayo alikuwa anaiskia tu ikitajwa kwa watu wengine halafu yeye leo alikuwa anauchezea moshi wa laki tano? Hakutaka makuu akataka kuirejesha ila aliambiwa aendelee kuifaidi kwani mtu huyo hakumpa kwa mkopo bali alimsaidia.
“Nikiwa bado kijana na umri kawa wako, nimewahi kuwa mjinga na mpumbavu kama wewe kwa kuwapa watu wengine umuhimu kwenye maisha ambayo hayawahusu. Matokeo yake nilijikuta napoteza muda wangu kuwajali watu wengine nikawa najisahau mimi mwenyewe hali iliyo nifanya niishie kwenye maumivu makali mpaka nikaenda kujirushia kwenye maji ila kwa bahati nzuri wasamalia wema waliniokoa lakini hawakuniacha hivi hivi. Walinitandika viboko vingi kwa ujinga wangu hasa baada ya kunisikiliza kwamba nilikuwa nahitaji kujiua kwa sababu ya mapenzi, kwa sababu ya mtu ambaye nimekutana naye ukubwani, kweli hata mimi nilijiona mpumbavu ambaye nilistahili kupigwa hata kuuawa na watu wale waliokuwa na hasira kali ya kuyapambania maisha yao halafu mimi nawaza kujiua kisa uchi wa mwanamke!” Alitamka bwana yule akiwa anauvuta moshi wake vizuri na kutulia kisha akageuka kumwangalia usoni Joh, alimpulizia moshi uliokuwa kwenye pua yake, akasikitika kidogo na kuendelea;
“Kabla ya kujipa umuhimu kwa watu wengine unatakiwa uijue sababu ya wewe kuwepo duniani, ukiitambua hiyo sababu utagundua kwamba hauna sababu yoyote ya kupoteza muda kumlilia mwanadamu mwenzako. Unamlilia malaya kwani ni mama yako yule? Ni dada yako yule? Malaya ambao wamejaa mjini huko tena warembo wa ngazi ya dunia, wewe unahangaishwa na mpumbavu mmoja huku ambaye hana hata uhakika wa kumiliki kiwanja kibaha japo cha milioni moja? Mwanaume wa kweli anawaza kuwa na nguvu, nguvu kipesa na mamlaka. Ukiwa na hizo nguvu hapa duniani kila mtu atakutii, kila mtu atafanya kile ambacho unataka Joh, maisha ni marahisi sana ila watu ndio wagumu. Mtaalamu Mark twain aliwahi kusema “THERE ARE TWO MOST IMPORTANT DAYS IN YOUR LIFE, THE DAY YOU WERE BORN AND THE DAY YOU FIND OUT WHY”
“Hayo ndiyo mambo ya msingi mwanaume unatakiwa kuwaza, ujue sababu ya wewe kuzaliwa na kuwepo duniani ili uzitimize kwa usahihi. Kuna sheria za kumfanya mtu afikie huko ila kwa bahati mbaya watu wengi hawazijui na wengine wanazijua ila hawawezi kuzifuata hali ambayo huwa inawafanya wanaishia njiani hususani kwa kupotea kabisa au kuweza kuuawa. Ukijijua kwamba hauna huo ubavu wa kuvimbiana na wenye uwezo, inamisha kichwa chini, watii kadri watakavyo wao, fuata kile ambacho wanakuambia, kuwa mbwa mtiifu mpaka siku ambayo utaijua mifumo kwa usahihi, hapo na wewe utaingia kwenye mifumo na kumiliki nguvu kubwa ambayo itakufanya ufike unapo takiwa kufika” mwanaume huyo alionekana kumjua vizuri kijana huyo tena kiundani, alikuja hapo kama malaika wake kwa kumpa maneno magumu namna mwanaume wa shoka anavyo takiwa kuwa.
“Umenifahamu vipi mimi na kwanini umenifuata?” Joh aliuliza akiwa anatetemeka.

UKURASA WA 32 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 33

“Hilo begi hapo ni lako, ndani lina pesa za kutosha. Kuanzia sasa kaishi maisha ambayo ulikuwa unayaota, kale unacho kitaka, katafute wanawake wa kila hadhi ambao unawataka wewe ila sio yule mbwa ambaye amekusaliti kwa sababu yule utakuja kumuua kwa mkono wako mwenyewe kwani akiendelea kuishi yule atakuwa udhaifu mkubwa kwako. Mimi nitakuja kukuchukua popote ulipo baada ya mwezi kama utakuwa tayari kufanya kazi na mimi, nataka nikutengeneze uwe miongoni mwa wanadamu hatari zaidi kuwahi kuishi ambaye utakuwa na kila kitu na hautatoa machozi kijinga tena kwenye maisha yako mpaka unakufa” hakutaka kujitambulisha kwamba yeye ni nani, alikuwa na uhakika na mambo yake ndiyo maana hata majibu yake yalionyesha kabisa kwamba alikuwa akimjua kiundani Joh kiasi kwamba akawa na uhakika wa kumpata muda wowote ambao angemhitaji huku akimuahidi kufika baada ya mwezi mmoja kupita.
Joeli akiwa bado amezubaa akihisi kama kilicho tokea ni ndoto, kuna gari ya kifahari ilifika maeneo ya karibu na maeneo yale ambayo ilimfanya mwanaume yule kunyanyuka na kuzitupa hatua zake taratibu kuelekea ilipo ile gari bila wasiwasi.
“Wewe ni nani?” alijikuta ameropoka akiwa mwingi wa hofu, jasho lilikuwa linamshuka kwa kasi akasahau hata kama ni yeye ambaye alikuwa analia kwa sababu ya mapenzi, mwanaume yule aligeuka akiwa anatabasamu.
“We are LS” akaingia kwenye gari, gari ikatoweka hilo eneo kwa kasi. Joh alibaki ameduwaa, aliifungua ile begi na kuyaona mabunda ya pesa yakiwa yamepangana. Aliangaza kila upande na kugundua kwamba kiza kilikuwa kimeingia na hakuna mtu alikuwa na muda naye kwa sababu watu wenyewe alikuwa akipita mmoja mmoja. Alicheka kicheko kikali, aliifunga ile begi na kuondoka nayo huku akikimbia kwa kasi kuelea ilipokuwa stendi ya magari. Ni yeye pekee ambaye alikuwa anajua mahali ambapo alikuwa anaelekea wakati ule, pesa ilirejesha lile cheko ambalo lilipotea huku akiahidiwa kwamba mtu huyo angekuja kumtafuta baada mwezi mmoja kuisha.
Hizo zilikuwa kumbukumbu za Yohani Mawenge, aliyakumbuka maisha yake ya nyuma, alitoka sehemu ambayo ilikuwa inatisha sana. Wakati huo alishtuka baada ya kuitwa na mhudumu wa ndege binafsi ambayo waliipanda na vijana wake kutoka Entebbe Uganda mpaka KIA, walikuwa wamefika tayari akiwa ameikamilisha kazi ya kumuua kijana ambaye alionekana kuwa kwenye mstari wa hatari wa kuweza kutoa siri zao na wakati huo alikuwa ndani ya ardhi ya Tanzania kwa mara nyingine tena.

SURA YA NNE
SAKATA LA EDWARD PANDE
Nilikuwa na jukumu zito kwenye mkono wangu, kukutafuta wewe na mama yako huku nikijua kabisa kwamba mama yako ndiye miongoni mwa watu ambao walikuwa nyuma ya lile jambo ambalo lilitokea. Nilikuwa na uchungu mkali na hasira kwenye moyo wangu juu ya mama yako, sikujua ni kitu gani ambacho ningemfanya siku ambayo ningemtia kwenye mkono wangu lakini mpaka wakati huo sikujua nianzie wapi kumpata ukizingatia walikuwa wamesha anza kunitoa kwenye mfumo.
Kete yangu ya bahati ilikuwa ni kwa kijana mmoja aliye itwa Danken, huyu alikuwa ni mtaalamu wa komputa ndani ya shirika letu, alikuwa bwana mdogo tu ambaye alikuwa amemaliza chuo muda mfupi lakini kutokana na uwezo wake mkubwa aliokuwa nao, aliajiriwa moja kwa moja hivyo kupitia yeye niliamini kwamba ningepata taarifa na kujua kwamba ni wapi ambako nilikuwa nastahili kuanzia kukutafuta wewe. Nilikutana naye, nikamdanganya kwamba nazihitaji taarifa za Zulpha Mazipa ambaye alikuwa ni mama yako mzazi, kijana yule alisita kunipa zile taarifa lakini hakuwa na namna kwa sababu alikuwa na machaguo mawili, kunipa na kuendelea kuishi au anipe kwa lazima kisha nimuue. Akanipatia taarifa za mama yako ambapo baada ya kunipa taarifa zile nikawa na uhakika kwamba mwanamke huyo yupo kwenye mfumo kwa muda kwani haikuwa rahisi mtu itokee tu bahati mbaya taarifa zake nyeti zikawepo ndani ya mfumo bila kuwa na umuhimu.
Mama yako alikuwa amekuchukua wewe ambaye haukuwa na taarifa yoyote juu ya kile ambacho kilikuwa kimetokea kwa familia ya baba yako pamoja na baba yako kutolewa sadaka huko Mossad na kukimbilia ndani ya jiji la Mbeya mpaka pale ambapo mambo yangetulia basi angerudi ndani ya jiji hili la starehe kuyaishi maisha yake akiwa amekamilisha kazi ambayo alipewa kuifanya. Sikuwa na namna zaidi ya kusafiri kwa ndege kwa siri kutoa hapa mpaka Mbeya, jiji lenye utajiri mkubwa wa chakula na watu wakarimu mno ndani ya nchi hii huku wao wakiliita GREEN CITY kwa sababu ya ufahari wake wa kupendeza na ukijani ambao unaashiria utajiri wa uoto wa asili.
Nilifika salama. Sikuwa na muda wa kupoteza zaidi ya kuchukua Tax kunipeleka mpaka Iwambi ambako ndiko mama yako nilipewa taarifa kwamba amehamia kwenye jengo jipya. Ni eneo ambalo linakua kwa kasi kutokana na kwamba watu wengi wenye pesa wanakimbilia kujenga huko kwa sasa hivyo niliamini lazima ningempata kwa namna yoyote ile. Baada ya kufika eneo hilo nilitafuta dalali wa kunipatia nyumba nzima ya kupanga ambapo lilikuwa suala la muda mfupi tu na bahati nzuri nilipata nyumba moja ndogo ambayo ilikuwa imemalizika muda mfupi tu kujengwa.
Sikuchukua nyumba kwa sababu nilijua kwamba nitakaa muda mrefu huko, lahasha! Bali nilifanya hivyo ili nisilete mashaka kwa wenyeji kwani kuwepo bila sababu kungefanya watu waanze kuwa na mashaka na mimi na taarifa huwa zinasambaa haraka kitu ambacho huenda kingefanya utambulisho wangu ujulikane jambo ambalo halikutakiwa kutokea. Nilikuwa mpelelezi mbobevu hivyo nilijua namna sahihi ya kuweza kuifanya kazi yangu, licha ya kuwa na namba sahihi ya nyumba ambayo mlikuwepo lakini sikuwa na haraka, kwanini? Kwa sababu moja nilitaka kujua hali ya usalama lakini nilitaka kupata namna sahihi ya kukupata wewe kwenye mazingira ambayo ni salama pia.
Ndani ya siku mbili nilifanya upembuzi kupitia watoto wa jirani na maeneo yale ambao mara kadhaa niliwaona wakicheza mpira kwamba nyumba ile, ilikuwa kila jioni inatoka gari nyeusi na hawakujua ilikuwa inarudishwa saa ngapi, nikapata jibu kwamba huenda huwa wanaenda nayo kwenye starehe. Je kama ni hivyo watakuwa wanaenda na mtoto? Sikukurupuka nikahitaji kujua aina ya ulinzi ambao ulikuwepo eneo lile. Kwenye kupekenyua kwangu, niligundua kuna walinzi wanne ambao walikuwa wanamlinda mama yako mzazi pamoja na wewe mwenyewe.
Niliamua kuvamia ndani ya ile nyumba usiku wa saa saba, nilikuwa nimejipanga kwamba ni lazima siku hiyo niondoke na wewe na mama yako lazima aniambie kinacho endelea na sababu ambayo ilimfanya afanye hayo matukio. Wakati naingia mle ndani nilikutana na wanaume wawili ambao nilitumia dakika tano tu kuwaua, niliingia ndani na kutafuta kila chumba sikuona mtu yeyote hapo nikashtuka, wakati hayo yanaendelea nilisikia muungurumo wa gari kwa mbali nje huku baada ya muda mfupi honi ikianza kupigwa. Kwenye mkono wangu nilikuwa nimeshika bastola huku nikiwa makini, nilijua ni yeye amerudi eneo lile.
Baada ya kuona geti halifunguliwi, nilisikia mlango wa gari ukibamizwa nikajua mwanaume mmoja ameshuka ili kuufungua, kwa sababu niliwaua wawili basi nikatambua wengine wawili ndio ambao walikuwa naye huko alikotoka. Hatua zake wakati analikaribia geti lile nilizisikia vizuri, bastola niliiweka kiunoni kisu changu kikiwa mkononi, nilikuwa namsubiri kwa hamu kama ule mpira wa penati. Aliligusa geti na kutahamaki likiwa halijafungwa lakini wakati anayachukua maamuzi hayo alikuwa amechelewa kwa sababu kichwa chake kilivutika ndani akiwa ameshikwa na butwaa ya kulifungua, nilizamisha kisu kwenye sikio lake la kushoto.
Alipiga kelele ila sikumpa nafasi, nilimzoa na buti kali ambalo lilimkosesha balansi akajikuta anapiga yowe huku anashuka chini ila hakuipata nafasi ya kulia vizuri kwa sababu nilimchana chana shingoni kabla hajatua chini. Alikuwa amekufa lakini wakati hilo linatendeka nilimuona mama yako akiwa amejishika mdomo kwa mshangao, alikuwa ameshuka kwenye gari mwanamke yule hivyo nikawa namwangalia kwa hasira ila kabla sijafanya maamuzi ya kumfuata niligundua kwamba mwanaume mmoja alikuwa nyuma yake mkononi akiwa na bastola.
Niliwahi kumdaka yule ambaye nilimuua pale chini na kumnyanyua ili kumtumia kama ngao, plani yangu ilifanya kazi vizuri kwa sababu bwana yule aliziachia risasi mpaka pale zilipo isha na zote ziliishia kwenye mwili wa yule mwenzake hivyo nikawa salama huku mkononi mwangu nikiwa na kisu kinavuja damu. Alikuja kwa nguvu zote na jazba, nilimkwepa akatua kwenye ukuta, ngumi yake ilitoboa ukuta ule, sikugeuka kijinga kwani wakati anakita kwenye ukuta, naye pia aligeuka akiwa na hasira, lile lilikuwa ni kosa vitani kutumia mihemko badala ya akili. Alikutana na kisu uso kwa uso ambacho kilikita kwenye jicho lake.

UKURASA WA 33 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 34

Nilikichomoa kwa nguvu na kukizamisha kwenye moyo kisha nikamsindikiza kwa ngumi nzito ya shingoni, nilisikia vyema ile mifuta ikiwa inakatika. Alijibamiza kwenye ukuta akiwa anagala gala na kuhitaji msaada ila sikuwa na huruma naye, nilimfuata pale karibu na ukuta nilimtwisha goti la kifua nikauvunja uti wa mgongo ambao ulikuwa umeegamia ule ukuta! Hakuwa hai tena, nafsi ilimsaliti. Nikajua sasa amebaki mama yako ambaye nilitakiwa kudili naye wakati huo ila wakati nageuka kumbe nilichelewa kufanya maamuzi wakati namuua yule mwanaume wa mwisho, mama yako aliliondoka gari pale kwa kasi kubwa ambayo sikuitegemea.
Nilitukana chini chini kwa sababu sikujua ningempata wapi kama ningempoteza kwenye jiji kubwa kama lile. Niliingia ndani na kuangaza huku na huko, kama bahati niliona pilipiki ikiwa pembezoni mwa ile nyumba kubwa na funguo yake. Bila shaka ni dalili kwamba miongoni mwa wale wanaume ambao niliwakuta mle ndani kuna mmoja wao alikuwa ametoka sehemu muda sio mrefu ndiyo maana funguo ilikuwepo pale. Ile nyumba haikuwa mbali na barabara hivyo na mimi nilitoka kwa pupa ila wakati naangaza upande wa barabara nilimuona mama yako akiwa ameshuka kwenye gari mkononi amebeba kitu kama furushi kubwa ambalo alitweta nalo kwa muda. Hakunitambua mimi ni nani kwa sababu hakuwahi kunijua ila nadhani ile kamari ambayo aliicheza wakati ule ilimlipa.
Nikiwa nakaribia nilimuona akiwa anarushia lile furushi kwenye gari moja ya ambayo ilikuwa na mzigo nyuma. Kwa namna alivyo lirusha ni wazi kwamba hazikuwa takataka bali kitu kizito, nikawaza kwa haraka nikagundua huenda yule ni mtoto wake, sasa kwanini afanye vile? Sikuwa na jibu zaidi ya kufanya maamuzi ya haraka. Wakati nafika barabarani alikuwa amepanda kwenye gari na kuishika Njia ya Iyunga, nilikuwa na uwezo wa kumkamata lakini swali likawa ni kwamba naweza kufanikiwa hilo na nisifanikiwe kukipata kile ambacho baba yako ameniagiza, akili yangu ikaamua kulifuata lile gari ambalo lilikuwa linaelekea kwenye ule mteremko hatari wa Iwambi kwenda Mbalizi.
Lilikuwa kwenye mwendo mkali hali ambayo ilinifanya nilikutie Mbalizi, nililisimamisha na kumtaka dereva ashuke hali ambayo ilinipa nafasi ya kulishusha lile furushi kubwa kiasi na kulifungua. Ndani ulikuwepo wewe ukiwa usingizini haujitambu, yule dereva na wenzake walihitaji kuwapigia simu ila niliwaonyesha kitambulisho changu na bastola ikawalazimu kuwa wapole. Nikawa nimekupata rasmi huku mama yako akiwa amepotea na sikujua ningekuja kumpatia wapi kwa mara nyingine na hivyo ndivyo ulivyo ingia kwenye mikono yangu kwa mara ya kwanza.
Nilirudi Dar es salaam nikiwa nimekupata tayari na kumkosa mama yako. Haukuwa sawa, hata nilipo kupeleka kwa daktari iligundulika kwamba ulikuwa umechomwa sindano nyingi za kukufanya uwe unasahau matukio mhimu kwenye maisha yako na zingekuathiri kama usingepata tiba ya haraka. Hilo ni jambo ambalo lilinipa maswali mengi kuhusu malengo ya mama yako mpaka kumfanyia mwanae wa kumzaa hivyo kwahiyo nikaja na mpango mwingine, mpango wa kuhama na wewe ambapo niliamua kuondoka Dar es salaam na kwenda ndani ya mkoa wa Shinyanga vijijini huko ambako nililazimika kuua mtu asiye na hatia ili kukulinda wewe.
Mtu ambaye nilimuua alikuwa ni daktari, daktari huyo ni ambaye mimi nilimuajiri kwa kukuweka wewe sawa na kujitahidi ili urudi kwenye hali yako lakini pia kunitengenezea mimi sura bandia ambayo ilikuwa na mfanano na mtu mmoja aliyekuwa anatoa huduma ya MUNGU, mwanaume huyo nilimsoma kwa umakini kule kijijini ambako alikuwa anaishi kama mgeni lakini kutokana na huduma yake alipendwa na watu.
Iselemagazi ndiko ambako tulikuwa tunaishi, kwa zamani mnamo miaka ya 1879 yalikuwa makao makuu ya Mirambo. Ulitibiwa ukaanza kurudi kwenye hali ya kawaida lakini kitu pekee ambacho kilikuwa changamoto kwako ilikuwa ni kukumbuka matukio ya nyuma na daktari alisema kwamba hilo linaweza kufanikiwa taratibu japo linaweza kuchukua miaka mingi na huenda usije kukumbuka mambo yote kwa kuathirika na dawa ambazo mama yako alikuwa anakupatia. Mimi kumuua yule daktari ambaye nilienda naye kule kwa siri sio kwa sababu ya kukutibia wewe, hapana! Wewe nilijua utakua na kubadilika sura kiasi kwamba watu hawatakuja kukutambua tena lakini shida ilikuwa kwangu, nililazimika kumuua yule mtumishi wa MUNGU na kuishika ile nafasi yake hasa baada ya kupata sura yake bandia ambayo ilitengenezwa na yule daktari.
Duniani siri ni pale unapokuwa nayo mwenyewe ila kipindi ambacho inakuwa kwa mtu zaidi ya mmoja basi sio siri tena hiyo. Nilijua kwamba daktari yule kuna siku angekuja kuropoka hivyo ili kuilinda ile siri nikaamua kumuua kisha nikahamia nyumbani kwake alipokuwa anakaa na wafanyakazi wake ambao niliwakuta niliamua kuwaondoa kwa kuwapatia mitaji na kutafuta wengine huku nikikuchukua wewe kwa mgongo wa kwamba mlezi wako hakuwa na uwezo ndiyo maana niliamua kukusaidi jambo ambalo lilinipa imani kubwa wa waumini, nikatafutiwa na wafanyakazi wengine na ndipo hapo ambapo huduma yangu rasmi ya kumtumikia Mungu ilianzia hapo nikiwa najifunza maneno ta Mungu kwa bidii ili nisije kugundulika.
Siku zilikatika, miezi ikapita na miaka ikasonga, nilikupeleka shule. Shule ulisoma kule kule kijijini nikikupa na utambulisho mpya wa Clyton Lameck na ndilo jina ambalo umekua nalo ukijua ni lako ila haikuwa hivyo bali nilitumia kama njia ya kukufanya usije ukatambulika mahali popote pale. Lengo langu nilitaka ubadilike kabisa kisha nikupeleke jeshini kwani elimu haikuwa kichwani mwangu. Kwanini jeshini? Kwa sababu nilikuwa naielewa dunia, dunia kwa wakati ule haikuwa rafiki kwako kwa sababu tu una elimu bali ilihitaji mtu ambaye unaishi kwenye nyakati zozote ngumu ambazo zitakukuta. Wakati nasubiri hilo sikukufanya kuwa lege lege, nilianza kukufunza mazoezi mimi mwenyewe binafsi nyumbani kila uliporudi shule na mimi kumaliza ibada ambayo nilikuwa naigiza tu ila sikuwahi kumaanisha.
Mazoezi yale magumu ilikuwa ni kwa usiri mkubwa na sikutamani mtu hata mmoja aje kuelewa lolote ambalo lilikuwa linaendelea kwako. Zaidi ya miaka kumi na kitu ilipita mpaka ulipo vuka miaka ishirini, haukuwa mtoto tena bali mwanaume shupavu, mwanaume wa maana kabisa mwenye kila namna ya ubora lakini sikusahau kukufunza kuhusu kanuni za maisha. Kanuni za kuwa mtu wa kawaida unapokuwa unakitaka kitu fulani mbele ya watu wajuaji. Ulikuwa umebadilika kila kitu na hakuna mtu ambaye angeweza kukutambua tena kwani sura yako ilibadilika na ndipo nilipo kutafutia nafasi jeshini na kwa sababu nilikuwa mtu wa Mungu kwangu nafasi ilipatikana kirahisi. Ikawa safari yako ya kwanza kwenda Msangi Tabora kwa ajili ya mafunzo ya jeshi.
Mpaka wakati ule ulikuwa unaamini kwamba wazazi wako walikuwa wafu, hawakuwepo duniani kitu ambacho hakikuwa sahihi maana sikuwa na uhakika kama hawakua hai japo mama yako nilikuwa na uhakika kamba bado alikuwa hai. Kanuni za maisha nilikufunza vyema, ulikuwa mwanaume ambaye ulikamilika mno lakini ukawa mstaarabu huko jeshini na kujifanya kama hakuna ulijualo, kujituma kwako na sifa nzuri ulizo zitengeneza zinakufanya upate nafasi ya kujiunga na mafunzo ya Ukomando Morogoro ukiwa miongoni mwa vijana kumi ambao mlikusanywa kwenye kila pembe kwenda mahali huko.
Baada ya kukamilisha hayo mafunzo huko Morogoro tena baadae ukapata nafasi nyingine ya kwenda Cuba ambako ulikaa mwaka mmoja na nusu na uliporudi ulikuwa mtu na binadamu mwingine hatari kuliko ilivyo kawaida. Wakati huo nilikuwa nimepata uhamisho wa kuishi ndani ya jiji la Dar es salaam kikazi. Hakukuwa na tatizo ukaendelea kulitumikia taifa lako lakini bahati iliyokuwa njema mkabataika kukutana tena na wale wenzako tisa ambao mliachana wakati kila mtu anapangiwa sehemu ya kwenda wakati mnatoka Morogoro na ukachaguliwa kuwa kiongozi wao kwa vigezo ambavyo uliwazidi wote kwenye ubora na mafunzo yako ambayo uliyapata kila ulipokuwa umepita.
Muda ulizidi kwenda, sikutaka kukukumbushia yale maisha ya nyuma kwa sababu nilijua yangeanza kukutesa. Niliamua kuufanya utafiti mimi mwenyewe binafsi ili kupata taarifa zozote zile kuhusu baba yako lakini sikufanikiwa kupata chochote hivyo binafsi nikajumlisha kwamba alishakufa kwa sababu kama angekuwa hai lazima angenitafuta, najua ingekuwa ngumu kwani nilikuwa naishi kwenye sura ya mtu mwingine ila kuna dalili ambazo mimi ningeziona, zingenifanya nitambue juu ya uwepo wake. Lakini kuhusu mama yako? Sikuwa na taarifa yoyote juu ya uwepo wake na ndiye hasa ambaye nilikuwa namhitaji pakubwa ili niweze kumpata kwani alikuwa na mengi ya kuweza kunijibu ila bado sikumpata.
UKURASA WA 34 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 35

Nikashawishika kuzidi kuchimba zaidi ili kuhitaji kujua kuhusu ile jamii! Jamii ya LUNATIC SOCIETY, ni muda mrefu ulikuwa umepita nikiwa sina taarifa zao hivyo nikaona kwamba ulikuwa muda mwafaka wa mimi kuanza kulifuatilia jambo hilo. Sikuwahi kuisikia popote tena stori ya mwanamama yule wa Urusi, IRINA ESPANOVICH. Nikapatwa na shauku ya kumtambua kwa wakati huo alikuwa wapi na anafanya nini. Sikutaka kukurupuka, niliajiri mpelelezi binafsi wa kuweza kuchunguza jambo hilo, nadhani kwa wakati huo nilifanya moja kati ya makosa makubwa sana.
KILL ON MISSION (KOM), ndilo lilikuwa kundi la makomando kumi, makomando ambao wewe ndiye ulikuwa kiongozi wao. Ni kundi ambalo halikuwahi kutambulika kwa raia zaidi zaidi ni kwa viongozi wa ngazi za juu tu ndio ambao walikuwa wanalifahamu kundi hilo. Uwepo wa kundi hilo ilikuwa faida kubwa ndani ya taifa hili lakini haikuwa habari nzuri kwa baadhi ya wakubwa na ukizingatia nchi ilikuwa imeenda kwenye mikono ya huyo mwanamama. Kwanini haikuwa habari njema kwake? Hicho kikosi hawakukitengeneza kwa mipango yao wao, walijua ilivyo ngumu kumshawishi komando ambaye amekula kiapo kwa ajili ya kuipigania bendera ya nchi yake hivyo wakawa na uhakika kwamba wasingeweza kirahisi kukishawishi kikosi hicho labda wajaribu kumuua kiongozi wake ambaye ni wewe hapo.
Wakati hayo yote yanatokea nina uhakika una picha mfukoni, picha ya mwanamke ambaye huenda mpaka sasa hauelewi kwamba ni kwanini unatembea na picha yake. Huyo ni mkeo, mkeo wa ndoa kabisa, Patricia Leonard ndilo lilikuwa jina lake. Binti mrembo ambaye ulimpatia kanisani kwangu, siku moja moja ambazo ulikuwa unakuja kusali, ulibahatika kukutana na mwanamke yule ambaye niliwakutanisha naye huku watu wasijue historia yetu mimi na wewe. Mlipendana sana kiasi cha kufikia kufunga ndoa huku mimi ndiye nikiwasimamia mpaka zoezi hilo kuweza kufanikiwa, akiwa mjamzito Patricia ndipo usiku wa giza ulipo anza kutawala nikashindwa kumlinda mwanamke yule. Nimeishi nikiwa nazijutia zile siku na yale maisha kwani kushindwa kwangu kumlinda, kulifanya ushindwe kumuona mwanao ambaye angezaliwa muda wowote kwa wakati ule.
Ni wakati ule ambao mimi nilikuona wewe ukiwa unafanya mauaji, mauaji ambayo hakuna binadamu angependa kuyashuhudia kwa macho yake. Ulikuwa unawaua watu ambao walitumwa waje kukumaliza wewe kama kiongozi wa KOM, wanaume ambao walitakiwa kuondoka na roho yako ili kukimaliza nguvu kikosi chako ambacho huenda watu hao waliogopa kwamba baadae kinaweza kuja kuwa tatizo kwao kama mngeyajua yale ambayo yalikuwa nyuma ya pazia. Mimi sikuwa na haraka ya kukujulisha lolote bado wakati ule ambao kumbukumbu zako hazikuwa zimerejea bado ili nikulinde, ungeujua ukweli huenda ungekurupuka ambapo ungeishia kuuawa.
Ule usiku niliushuhudia uhalisia wako ulio nao, ulichinja na kuua watu kikatili hadi shetani mwenyewe alistahili kujifunza ila roho ngumu kwako na sio wewe kujifunza kwake. Kufeli kwa ule mpango wao ukawa mwanzo wa safari nyingine, najua unaikumbuka! Hapa nazungumzia ile safari ya kwenda Mogadishu ambako kulienda kuyabadilisha maisha yako jumla na kukufanya uanze kuishi kama mkimbizi.
Kwa sababu ilitakiwa mfe wote kumi haikuwa rahisi kuweza kulitekeleza hilo mkiwa ndani ya nchi ikabidi waangalie namna ya kuwatuma wote kwenye kazi. Ni wakati ule ambao AL-SHABAAB walivamia ndani ya Kenya kwenye chuo na kusababisha maafa, ikawa imepatikana sababu ya kwenda, kwanini? Kwa sababu wakati jambo lile linafanyika, AL-SHABAAB waliteka baadhi ya watoto na wanafunzi na kukimbilia nao huko Somalia ambako kuna makao yao makuu. Serikali iliingia makubaliano na Kenya kwa ajili ya kutoa msaada huku wakiwahadaa nyie kwamba kuna raia wa Tanzania walikuwa wametekwa huko pia hivyo walitakiwa kurudi salama nyumbani.
Walitunga uongo kwa kudai kwamba wanajeshi wengi walitumwa huko wakauawa hivyo wangekufa wengi zaidi mpaka pale ambapo mlitumwa nyie makomando. Jambo la kuwatuma wote kumi sehemu moja na kwa wakati mmoja walijua kabisa kwamba lingewashtua hata nyie mkachukua tahadhari hivyo walicho amua kukifanya ni kuwagawa, kivipi? Watano walitakiwa kuingia nchini kongo kupigana na Jeshi la kihalifu kusaidiana na serikali ambayo ilikuwa madarakani huku watano mkitakiwa kwenda Somalia. Haya yote nilikuja kuyajua baada ya nyie kuondoka nchini huku ukimuacha mkeo wa pekee kwenye mikono yangu na mwanamke huyo nilimkabidhi Issa aweze kumlinda. Si unakumbuka niliwahi kukwambia kwamba hata ikitokea siku sipo yupo Issa wa kukusaidia? Ndiye huyo Issa ambaye nilimhusisha bila kumpa maelekezo kwamba Patricia Leonard ni mkeo. Issa aliwahi kufanya kazi na Ls lakini baadae akaondoka kwa siri baada ya kukutana na mimi hivyo hakuwa upande wao tena.
Turudi kwenye kosa ambalo nililifanya. Kuanza kufanya upelelezi wangu juu ya yale ambayo yalikuwa yanaendelea lilikuwa tatizo lingine, kijana yule mpelelezi ambaye nilimpa kazi hakuwa makini nadhani kwa kujiamini ama kutojua watu ambao alikuwa anawafuatilia. Jambo lile lilifanya aweze kukamatwa, hayo nilikuja kuyatambua baada ya kukutana na mwili wake ukiwa umekatwa katwa kwenye gari yangu huku kukiwa na barua. Barua ilinitaka kuwa makini na hatua ambazo nilikuwa nazipiga kwani sio muda mrefu kuna mtu angekuja kunitembelea ili nimpe majibu ya sababu za kufuatilia yale mambo ambayo yalikuwa yametokea huko nyuma. Yaani mimi nilikuwa nani hasa na nilijuaje mambo hayo kiasi cha kufikia hatua ya kuweza kuajiri mpelelezi? Na baada ya kuyajua nilikuwa nataka kuyafanyia nini hasa? Nikajawa na hofu.
Utambulisho wangu ulikuwa umeanza kuwa uchi, nikajua yule mpelelezi wangu alifanya makosa kitu ambacho kilinifanya nitafute kundi moja ya wauaji kutoka Kenya na kuwafanya kuwa walinzi wangu ili kama likitokea tatizo niwe naweza kujilinda na wakati huo niliendelea kutoa huduma ya kanisa bado. Jioni moja nikiwa kanisani pekeyangu, nilikuwa pekeyangu kwa sababu sikuwahi kuhitaji watu wajue kama mimi nalindwa ndiyo maana walinzi wangu walikuwa wakionekana usiku tu. Siku ile nilipokea ugeni, ugeni wa mwanaume ambaye sikuwahi kumuona kwenye maisha yangu yote.
Alikuwa ndani ya suti ya kijivu, umri wake ulikuwa umeenda kidogo. Hakuwa na papara baada ya kuingia pale ndani akiwa pekeyake na kofia yake akiwa ameishika na kuizungusha mkononi. Nilikuwa nimeketi mbele madhabahuni, hata hakuhangaika kuweza kuniangalia au kunifuata, alichagua kiti cha katikati kabisa ya kanisa, akaketi katikati yake. Nilijua tu alikuwa mgeni wangu hivyo nikamsogelea pale alipokuwa ameketi, mazungumzo yake ndiyo yalianza kunionyeshea hali ya hatari mbele yangu.
Kwanza alinionyesha picha yangu, picha ambayo ilinishtua moyoni japo sikuonyesha ule mshtuko wazi wazi kiasi kwamba atambue juu ya hilo. Ile ilikuwa ni picha yangu kipindi nipo ndani ya shirika letu la kijasusi la IBA, aliniangalia kwa umakini usoni, bila shaka alikuwa ananikagua na kuweza kujiridhisha kama sikuwa na mshtuko lakini nilikuwa ngangali ila moyoni nilikuwa natetemeka, kuweza kujulikana lilikuwa kosa kubwa ambalo lingefanya nijutie kila nilicho kilinda kwa miaka mingi kwa sababu lingekuwa suala la muda tu kabla hawajajua kuhusu wewe.
“Unamfahamu huyu mtu?” Aliuliza kwa sauti kavu mithili ya mtu ambaye alikuwa ametoka kuvuta sigara.
“Mimi ni mtumishi wa Mungu siwezi kuwakariri watu wote wanao kuja hapa, kuna jambo labda unahitaji nikusaidie la kiroho?”
“Sijaja hapa kwa ajili ya ubatizo mchungaji, nina uhakika hata wewe unalitambua hilo. Bado haujajibu swali langu”
“Ndiyo kwa mara ya kwanza naiona hiyo sura, unaweza ukaniambia kwamba ni nani labda huyo mtu?”
“Huyu alikuwa kwenye idara nyeti ya usalama wa taifa, alikuwa mtu wa kutegemewa lakini mwisho wa siku aliliasi taifa lake kwa kuanza kuuza taarifa za ndani kabisa ambazo zingeliweka taifa kwenye hatari”
“Naweza kuijua sababu ya msingi ya wewe kuniambia hayo yote?”
“Mimi na wewe wote tunajua kwamba wewe haupo hapa kwa ajili ya neno la Mungu, unaweza ukaniambia sababu ya msingi ya kuajiri mpelelezi binafsi?”
“Mbona sikuelewi, mtumishi wa Mungu na wapelelezi wapi na wapi?” mwanaume yule baada ya mimi kuonyesha kuwa mbishi hakuongea tena bali akaingiza mkono kwenye mfuko wake na kunipatia kitu. Ilikuwa picha ambayo mimi nilikuwa napishana na yule kijana mpelelezi kwenye moja ya mgahawa mkubwa upatikanao katikati ya jiji. Moyo wangu ulipiga kite kwa nguvu nikatamani kubadilika palepale ila niliamua kujipa utulivu kwa sababu ule haukuwa ushahidi wa kuamini hilo.

UKURASA WA 35 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 36

“Hiyo picha imekutwa kwenye picha za marejeo ya kamera zilizopo katikati ya mji”
“Nakutana na kupishana na watu wengi hivyo kwakweli siwezi kujua lolote kuhusu haya ambayo yanaendelea” alitabasamu na kuzirudisha picha zake kwenye mfuko wa koti na kusimama.
“Nadhani tutakutana siku nyingine mtumishi wa Mungu” aliongea bila kusubiri nimjibu akatoweka. Sikuelewa nifanye nini, nilibaki nimechanganyikiwa, licha ya kuishi kwa ule usiri ambao binafsi nilijiaminisha kwamba utakuwa mkubwa na nitakuwa salama, nilijiona nipo uchi kwa watu hao kwa sababu ni wazi yule kijana alisema ukweli kwamba ni mimi nilimtuma hivyo usiku huo nilihitaji kwenda kwa siri kwa mkeo ili kumpatia taarifa ya kwamba sitakuwa naonana naye tena kwa sababu ya kutingwa na majukumu. Sikutaka aingie kwenye wasiwasi, hilo likawa kosa lingine kwa sababu nilikuwa nafuatiliwa tangu mtu yule aondoke kule kanisani bila kulitambua hilo, nikaingia kwenye mtego mwingine kwa kuwapa urahisi wa wao kutambua kuhusu Patricia. Nadhani walifuatilia kwa undani na hasa baada ya kugundua kwamba mwanamke huyo anasali ndani ya kanisa langu wakaamua kuichimba historia yake.
Baadae ndipo waligundua kwamba Patricia alikuwa amefunga ndoa na wewe, ndoa ambayo ilifungwa mbele ya watu wachache tu pekee kanisani bila kuwashirikisha watu wengi. Sasa kama Patria alikuwa mkeo, kwanini mfungie harusi kwangu na baadae mimi jina langu lijitokeze kwenye kufuatilia siri zao? Nikaingia kwenye listi ya watu ambao walitakiwa kufa, lakini wangeniua vipi na hawajapata majibu ya maswali yao? Mimi nikawa chambo bila kulitambua hilo na ndipo ukaanza kuchunguzwa bila hata kujua.
Miongoni mwa makomando wenzako wote tisa ambao walikuwa kwenye kikosi chao, historia za maisha yao na familia zao zilikuwa zinatambulika vizuri baada ya kupitia historia zao za nyuma kasoro wewe tu. Wewe haukujulikana historia yako zaidi ya ile ambayo ulianzia jeshini huko Msangi, watu hao wakatuma watu kupeleleza huko na ndipo wakatoa maelezo uliko tokea huko Shinyanga vijijini. Historia ya kule ikawa ya ubabaifu ambayo iligundulika kwamba mimi ndiye ambaye nilikuchukua na kuanza kukulea kwenye mikono yangu. Sasa wakaunganisha matukio na kugundua kwamba kulikuwa na mtego kama sio mchezo mbaya ambao ulikuwa unaendelea kati yangu mimi na wewe.
Siku chache baadae nilipata ugeni mzito, ugeni wa kiongozi wa shirika la kijasusi la IBA, Lionela Philson. Nilishtuka kumuona mwanamama huyo Lionela kwa sababu kuonekana kwake kulionyesha uzito wa jambo ambalo lilikuwa linaendelea kwangu. Mwanamke yule alinitaka nimpe ukweli wa kijana ambaye alikuwa anaitwa Clyton Lameck ambaye kwa taarifa ambazo walizifuatilia ni kwamba mimi ndiye niliye mlea tangu nikiwa huko Shinyanga. Ushahidi ulikuwa wazi sikuwa na namna ya kukataa zaidi ya kukubali na kueleza kwamba mimi nililetewa na mtu ambaye sikuwa namjua hivyo nilimpokea na kumlea.
Kuhusu kukupelekea jeshini lilikuwa ni swali lingine gumu ambalo pia ilinilazimu kudanganya kwamba ni wewe ulikuwa ukiipenda kazi hiyo ndiyo maana ikawa rahisi zaidi kuifanya kwa moyo wako wote. Hakuridhika na maneno yangu, alidai angenitafuta kwa mara nyingine kwa sababu kama angeondoka na mimi ingeleta sifa mbaya kwao kwa kiongozi wa dini kukamatwa kiholela hivyo ule mlango wa dini ukawa umenibeba kwa kiasi fulani japo nilijua kwamba saa na wakati unakaribia, kukutana na yule mwanamama lilikuwa ni jambo la hatari mno kwa sababu nilimjua vizuri, ni mwanamke hatari mno, anakuua huku anakuchekea usoni ukiamini kwamba upo salama.
Kuondoka kwake niliamini kwamba lisingeishia pale bali ule ulikuwa ni mwanzo tu. Nilitamani nikupe taarifa ya kukimbia ila tayari ulikuwa umesha toweka kwani mlikuwa mmesha ianza safari ya kwenda Somalia tayari na wenzako wengine walienda Kongo. Jambo ambalo sikulifahamu ni kwamba Issa aliitwa na wakubwa zake kisha akapangiwa safari ya kwenda Msumbiji ya kijeshi huku akikatiwa mawasiliano ghafla, hivyo sikujua yuko wapi ila nikaamini kwamba alikuwa anaendelea na kazi yake ya kumlinda mkeo, nilitambua hilo nikiwa nimechelewa.
Jambo pekee ambalo sikulitambua ni kwamba yule mwanaume wa kwanza wakati anakuja kunitembelea pale Kanisani alikuwa na mkasi, wakati anatoka alinipia nyuma yangu! Sikutambua kwamba aliondoka na nywele zangu, nywele ambazo zilienda kuuweka wazi ukweli wa juu ya kwamba mimi ni nani. Nywele zangu zilikuwa zimeenda kuwafanikishia kujua kwamba mimi ni yule mpelelezi wa zamani wa IBA ambaye nilikimbia na kupotea ghafla kwenye macho yao, mwanaume ambaye nilikuwa natafutwa kwa udi na uvumba na taarifa za kutafutwa kwangu nilikuwa nazo.
Hilo halikuwa hatari kwangu, hatari zaidi ni kwamba wakati naondoka ulipatikana ushahidi wa picha mara kadhaa mimi nikiwa na Christian Edison baba yako, wakajua kwamba mimi nilikuwa karibu naye na hata ile siku ya mwisho kabla ya kuondoka wakati anakuja kuniaga nadhani kuna mtu alikuwa anamfuatilia akafanikiwa kutupiga picha. Picha ambazo waliamini kwamba ziliashiria Christian aliniachia maagizo ya kumlinda mwanae, ukijumlisha na yale matukio ya Mbeya ndiyo moja kwa moja nina uhakika walijua kwamba mimi ni nani ila wakaamua kunikaushia. Walitambua kwamba mimi ndiye ambaye niliondoka na wewe siku ile kwa sababu mama yako mzazi aliiona sura yangu nikiwa namuua yule mwanaume pale nje. Mimi na wewe wote hatukuwa salama tena Edison ila sikujua hilo.
Baada ya kufuatilia hayo wakawa na uhakika asilimia tisini kwamba wewe ndiye yule mtoto wa Christian ambaye mimi nilikuteka Mbeya, hivyo Lionela kuja kuniuliza ni kwamba alikuwa anahitaji uhakika wa asilimia zingine kumi ambazo zilikuwa zimebakia juu. Wakati nyie mnaenda kwenye hiyo misheni, kuna vikosi viwili vilitumwa nyua, vikosi hivyo mliambiwa kwamba vinakuja kuwaokoa na kutoa msaada ila haikuwa kweli, vilikuwa ni vikosi kwa ajili ya kuja kuwaua wote kwani mngeonekana kwamba mlifia kazini na hata wananchi wasingekuwa na maswali mengi kusikia wanajeshi wamefia kazini na vikosi hivyo vikagawanywa Somalia na Kongo.
Kupata taarifa kuhusu wewe ziliwapa uoga, ulikuwa ni mtu hatari mwenye mafunzo makali na baada ya uchunguzi waligundua hakuna unacho kijua juu ya kilicho tokea hivyo wakawaza kwamba endapo ukaja kujua huhusu hilo basi ingekuwa tatizo kwako hivyo wewe ukatakiwa kuuawa kwa namna na kwa gharama yoyote ile. Haukutakiwa kurudi tena Tanzania hata kwa bahati mbaya, kwahiyo licha ya kutuma kikosi cha kwanza lakini ikawalazimu kutuma wanaume wengine watatu ndani ya jiji la Mogadishu ambako ndiko mlitakiwa kuweka kambi kwa muda wote ambao mngekuwepo kwenye lile jiji. Walifanya hivyo ili kusije kukatokea na makosa yoyote yale ya wewe kurudi ukiwa hai.
Usiku nilipata meseji, meseji kutoka kwa Patricia akihitaji msaada kwa sababu alikuwa kwenye hali mbaya. Nilishangaa kwanini anipe taarifa yeye badala ya Issa? Ndipo nikapiga simu kwa Issa lakini haikupatikana, haikuwa kawaida jambo hilo likanipa taarifa mbaya kichwani na kuamini kwamba hakukuwa salama. Licha ya kuhisi kwamba mkeo lazima alikuwa ameanza kusumbuliwa na tatizo la mimba ambayo ilikuwa imebakia muda mchache tu ili ajifungue lakini nilijawa na hofu kwamba huenda kuna zaidi ya hilo. Niliingia kwenye gari yangu ili kuwahi kuko nikiwa napiga simu ambayo haikuwa ikipokelewa mpaka ilipo acha kupatikana kabisa.
Kutoka Sinza Lego mpaka Mikocheni sikutumia muda mwingi lakini nilichelewa kufika. Kitu ambacho unatakiwa kukijua na kujikaza kiume ni kwamba mkeo alibakwa usiku ule, mimba yake iliharibika na yeye menyewe aliuawa na watu wale. Lile jambo liliniuma isivyokuwa kawaida, niliogopa sana na ndipo nilipokumbuka kuhusu wewe, niliwaza mpaka wameamua kumuua mkeo maana yake hata wewe ulikuwa kwenye hatari ya kufa kwenye ile misheni yako. Sasa hapo ndipo nikaamua kutumia plani yangu ya pili, plani ambayo niliiandaa kwa muda mrefu wa kuhakikisha nakulinda.
Hapa unakutana na mtu mpya, mtu ambye hata nitakapokuwa nimekufa basi utambue kwamba yupo hai mpaka leo bado naishi. Huyu ndiye ambaye alikuokoa wewe mpaka leo umefanikiwa kukisoma kitabu hiki ukiwa na afya njema, huyu ndiye atakuwa na majibu ya maswali ambayo huenda utatamani kuyauliza kwa sababu mimi siwezi kukujibu kwani wakati unasoma kitabu hiki nitakuwa nimekufa tayari.
Kabla ya kukwambia kuhusu mtu huyo unatakiwa kutambua kwamba kupitia hiyo safari yako basi ulitengeneza adui mpya, adui ambaye sina taarifa zake nyingi lakini anadaiwa naye kukutafuta isivyokuwa kawaida. Sio wa kiume bali ni wa kike anaitwa Nicola Aidan Semzaba, huyu binti anahitaji kukuua kwa gharama yoyote ile kwa sababu miongoni mwa wale makomando wanne ambao ulienda nao Somalia, mmoja wao alikuwa kaka yake wa damu na walizaliwa wawili tu pekee. Ubaya wa jambo hilo ni kwamba kaka yake alikutwa amekufa na risasi ambazo zilitumika kuubeba uhai wake ni risasi za silaha ambayo ulikuwa unaitumia wewe hapo hivyo wamemuaminisha kwamba wewe ndiye muuaji. Sasa ilikuwaje mpaka haya yote yakafanyika?

UKURASA WA 36
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 37

Zilirudi taarifa mbaya kutoka huko Congo kwamba kikosi cha makomando watano ambao walienda huko kwa bahati mbaya wakiwa kwenye gari, gari yao ililipuliwa na vikosi vya waasi hivyo yakarudi majivu bila watu husika. Kuna mengi yalitokea huko ila sitayaeleza haya, mtafute Issa akupatie frashi ambayo ndani yake ina kila kitu, ina taarifa za mhimu za matukio hayo namna yalivyo tokea na majina ya watu ambao wanaweza kukifikisha sehemu nzuri kwenye uchunguzi wako, lakini kuna siri za LUNATIC SOCIETY hivyo hakikisha unaipata.
Zilikuwa zimebakia taarifa za huko Somalia ambako mlifikia Mbamali Mogadishu pembezoni mwa bahari ya Hindi. Kwenye kambi yenu ambayo mlifikia mlipokea taarifa muda mfupi kwamba kulikuwa na kikosi ambacho kilikuwa kinafika hapo kuwapa taarifa za mhimu juu ya wapi ambapo mlitakiwa kueleakea na hatua ambazo mlitakiwa kuzifuata lakini haikuwa kweli. Ulitoka nje ukiwa na vijana wako kutoka kwenye lile jengo ambalo mlifikia ili kuupokea ugeni huo kutoka Tanzania ila kwa bahati tu simu iliita ndani hivyo aliyekuwa ndani akatoa taarifa ya simu ambayo ulikuwa unaitumia kufanyia mawasiliano kuita ikakulazimu uawaache nje na kuingia ndani.
Ukiwa ndani ndipo ulisikia milio ya magari yakiingia pale ambapo kilicho fuatia ni milio ya risasi nyingi ambazo ziliyachukua maisha ya vijana wako wote. Jambo lile lilikushangaza lakini haukuwa na muda wa kusubiri zaidi ya kujitetea, ulijitahidi sana kupambana nao mpaka ukafanikiwa kuwaua wote na baadae ukajaribu kufanya mawasiliano kwani ulikuwa umeshangazwa na kuuawa na wanajeshi ambao ni watanzania na walitumwa kuja kuwaokoa nyie huku ukiwa umewapoteza wenzako wote wanne.
Ukiwa kwenye ile taharuki ndipo waliingia wale wanaume watatu ambao walikuja kwa ajili yako kuhakikisha kama zoezi limeenda vizuri, hao walitumwa kuhakikisha hauishi kama kuna makosa yangefanyika kwa wale wa kwanza kushindwa kukuua. Ulitamani kupambana nao lakini walikuzidi kwa sababu walikuwa na silaha za moto ambapo ulipigwa risasi mbili kifuani, mwanaume mmoja alisogea ili akuue lakini wakati ule alidondoka chini kwa kuuawa na kisu. Mtu ambaye nilimuandaa kama mpango wa pili alifika pale na kuua wanaume wale wote watatu kisha akaondoka na wewe ukiwa kwenye hali mbaya isiyo na matumaini.
JACK THE LAWYER, ndiye mwanaume ambaye alikuokoa wewe, ni kama mlokole ukimuangalia usoni ila ni binadamu hatari na ni miongoni mwa watu ambao nimetumia gharama kubwa kuwatengeneza kwa ajili ya kuja kukulinda na haya atakwenda kukusimulia yeye mwenyewe mkionana. Huyu ni mwanasheria mbobevu lakini pia ni daktari na ndiye ambaye alikufanyia wewe upasuaji wa kukuondoka zile risasi mpaka ukafanikiwa kuishi kwa mara ya pili ila kuja jambo nilitaka alifanye.
Nilihitaji azifute kumbukumbu zako kichwani, yaani usikumbuke kuhusu maisha ambayo uliyapitia mwanzo ili tuandae mazingira ya wewe kuja kurudi kwa mara ya pili ukiwa sawa. Ningekupa taarifa ya mambo ya nyuma na kukwambia kwamba mkeo mjamzito amekufa, nina uhakika usingeweza kuwa mvumilivu lakini kingekupelekea kufa kwa sababu hasira zingekuendesha vibaya. Ule ndio ukawa mwanzo wangu wa kukutaka wewe uwe unaishi maisha ya chini mtaani, maisha ambayo yangekufanya usiwe kwenye midomo ya watu kwa sababu hakuna maskini ambaye anazingatiwa kabisa kwenye haya maisha.
Na ndipo mara ya kwanza nikakushauri uishi maisha ya kubangaiza na ya kimaskini sana ili uwe salama, ile ahadi ambayo nilikuahidi kwamba ningekueleza kabla sijafa naona imenishinda hivyo kitabu hiki kinakupa majibu kwa niaba yangu. Nina uhakika utanisamehe kwa kila kitu kwa sababu nilishindwa kuitunza ahadi yangu kwa kushindwa kumlinda baba yako, mke wako lakini hata mwanao ambaye bado hakuzaliwa. Mimi nilijitahidi kadri ya uwezo wangu na sikujua kama kulikuwa na lingine la kufanya zaidi ya yale ambayo niliyafanya. Mama yako nina hisia kwamba bado yupo hai na ni mzima wa afya ila kuhusu wewe kumtafuta hilo ni juu yako kama utahitaji.
Mtafute JACK THE LAWYER kama unahitaji kurejeshewa kumbukumbu za maisha yako kwenye kichwa chako, huyo atakujibu maswali yako yote ambayo unayo na unatamani kuyajua majibu yake kwa sababu huyo ni IMPOSTER ambaye anaishi kwenye sura ya mtu mwingine ila ni mtu ambaye ana sura kama yako kwenye uhalisia wake, ukitaka kujua sababu ya kutengenezwa mtu wa aina yako basi yeye atakuwa na majibu zaidi ila huyo ndiye ambaye ataichukua nafasi yako na kufa kwa ajili yako ili kuwaaminisha watu ambao wanakutafuta wewe kwamba umekufa ilihali wewe utaendelea kuishi.
Unaweza ukawa na maswali mengi kuhusu mimi kwamba kwanini hawakuniua mapema? Hawakuniua kwa sababu walikuwa wana imani kwamba kupitia mimi siku moja wangekuja kukupata. Kuukosa mwili wako kule Somalia licha ya kuikuta damu yako, walikuwa na uhakika kwamba upo hai bado hivyo wakajua kupitia mimi wangekupata ndiyo maana wakaniacha hai kwa muda mrefu zaidi licha ya kunifahamu. Kwa matukio ambayo yalitokea Somalia na Congo, wewe ndiye ulitengenezewa kesi ya kuwauaza wenzako wote tisa kwa tamaa ya pesa na wakaishia kuuawa huku wale wa Somalia ukidaiwa kwamba wewe ndiye ulihusika na mauaji yao hivyo unatafutwa sana ndiyo maana nilitaka uishi huko vichochoroni mpaka pale ambapo mambo yangetulia, na miongoni mwa hao watu ambao wameaminishwa hilo ni Nicola anaye kutafuta ili akuuee” Ni maneno mazito ambaye aliyasoma kwenye hicho kitabu. Mpaka anakimaliza, hakujua aishike njia ipi, hakujua ashike lipi na kuliacha lipi, alijihisi kuchanganyikiwa huku kichwa kikiwa kizito mno.








JACK THE LAWYER
(THE IMPOSTER)
Jack the Lawyer ni nani na na anahusika vipi na Edison kiasi kwamba jina lake likatokea kwenye kile kitabu ambacho E.C (Edison Christian aliachiwa)?

JACK THE LAWYER, lIlikuwa jina maarufu la gwiji wa sheria ndani na nje ya Tanzania. Hilo ni jina ambalo alijipa yeye binafsi kutokana na sababu ambazo alizijua yeye mwenyewe. Jack alikuwa mbobevu kwenye tasnia hiyo ya sheria, aliijua sheria kuliko hata zile harufi ambazo zilikuwa zinaliwakilisha jina lake. Jack halikuwa jina lake halisi, jna lake la kuzaliwa alifahamika kama CHRISPIN MWAMBANO, mtu mwenye asili ya Mbeya, ardhi inayo aminika kutoa vichwa vilivyo shiba maarifa ya kutosha.
Mwanasheria huyo alikuwa amesimamia kesi hamsini na mbili za ndani na nje ya nchi na alishinda kesi hamsini na moja, kesi moja ambayo kwake ilihesabika kama kaipoteza ni kesi ambayo wahusika walienda kumpigia magoti ili aweze kuifuta ndipo akaifuta hivyo kwenye miaka yake isiyo pungua thelathini, hakuwahi kupoteza kesi hata moja japo kwa bahati mbaya.
Umaridadi wake huo ulimfanya awe maarufu, akawa na jina kubwa mwanasheria huyo kijana ambaye hakuna kesi ya aina yoyote ile ingekatiza mbele yake halafu ikamshinda, akawa maarufu na umaarufu wake ukafanya kuwa kipenzi cha watu. Hakuwa mtu mwenye majivuno licha ya kupata mafanikio ya kesi zake hizo ambazo alizishughulikia. Hakuwa mtu ambaye alipenda maskini kuonewa, siku zote sehemu ambayo sheria ilivunjwa alijitokeza mstari wa mbele kupinga jambo ambalo lilizidi kumpa nafasi kubwa na ushawishi wa hali ya juu kwa jamii na wananchi, wakamuona mkombozi.

UKURASA WA 37 Unafika mwisho
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 38

Miaka mitano ilikuwa imepita tangu litokee tukio ambalo lilileta pigo kwenye jeshi la nchi. Makomando kumi ambayo walitumwa kutoa msaada pamoja na kufanya oparesheni ya ukombozi walikufa kabla ya kuanza kwa mission ambayo iliwapeleka huko na kupelekea majukumu hayo kufeli hata wananchi ambao walitakiwa kukombolewa hawakuwahi kuonekana tena. Jambo hilo baada ya kuvuja kwa waanchi lilileta mjadala mkubwa kutokana na taarifa ambazo zilipatikana zikiwa zinaeleza kwamba komando mmoja ndiye alihusika na maafa hayo huku akifanikiwa kukimbia na serikali iliahidi kumtafuta na kumtia kwenye mkono wa sheria.
Licha ya wananchi kuchukizwa na jambo hilo na kumhitaji mtu huyo aweze kupatikana lakini kuna wengine hawakuziamini taarifa hizo hali ambayo ilizua gumzo kubwa kila pande ya nchi. Kuna baadhi ya wananchi na watu wasomi walikuwa wakihoji kwamba kama mtu huyo alihusika, ilikuwaje yeye alikuwa somalia ahusike pia kuua watu ambao walikuwa Kongo? Majibu yake yalikuwa mepesi kuna watu hawakuyakubali, eti kwamba aliuza taarifa kwa waasi ndio wakajua mpango huo na kuwalipua makamando huo kabla hawajafika eneo la kazi!
Wengi walikubaliana na huo ukweli ila kuna watu wanajielewa, huwa wanawaza nje ya box hivyo hawakuziamini taarifa hizo, wakawa na maswali mengi na kuhisi kwamba kuna mambo yalikuwa yanafichwa, huo haukuwa ukweli kamili. Hata hivyo wale ambao walionekana kuhoji sana waliuawa na kupotezwa kwa siri hali ambayo ilifanya kila mtu aanze kuogopa kulizungumzia jambo hilo hivyo likaanza kupotea taratibu mpaka pale ambapo kelele zikaisha kabisa na wananchi wakaanza kusahau huku wengi wakiwa wanalikumbushia mara moja moja mitandaoni hasa kwenye magroup yao ya WhatsaAAP na baadhi ya majukwaa ya jukwaa la Jamii Forums.

Ukiwa umepita ukimya wa miaka mitano, kila mtu akiwa amesha lipotezea jambo hilo na watu wakiwa wameacha kabisa kuhoji kulihusu ndipo anaibuka mwanasheria nguli JACK THE LAWYER ambaye anadai kuhitaji kuifungua upya kesi hiyo. Mwanaume huyo anajipambanua kwa kusema kwamba hiyo ni kesi ambayo ilifanyika kihuni na viongozi, viongozi walileta usela kwenye mambo nyeti ambayo yalibeba hatima za roho za watu ambao waliacha familia na ndugu walio wategemea.
Habari hiyo ilianza kusambaa kama utani kwenye gazeti ambalo kwa chini chini lilidaiwa kumilikiwa na mwanasheria huyo, gazeti la THE TRUTH-UKWELI. Hakuna ambaye alikuwa na uhakika wa habari hizo lakini gazeti hilo mara nyingi lilikuwa likitoa taarifa za kweli japo lilikuwa linachelewa kutoa taarifa zake. Yaarifa hizo ndizo zilizalisha tena minong’ono kwa mara nyingine, watu walianza kupiga kelele mtaani kuhusu mwanasheria huyo huku watu wakianza kupata munkari wa kuhitaji kujua kwamba mtu huyo ni jambo gani ambalo angelifanya baada ya hapo na wengi walihitaji kumfanyia mahojiano ili athibitishe taarifa hizo kama zilikuwa ni za kweli au ulikuwa ni uzushi tu magazeti yanalitumia jina lake ili kuweza kuuza habari zao hizo.
Saa kumi ya usiku JACK THE LAWYER alitoka ndani ya nyumba yake akiwa kwenye taulo na sendo mguuni. Kutoka kwake nje ni baada ya kuona kuna kijana amekaa hapo kwa muda mrefu akiwa na kamera yake shingoni na mwenzake ambaye alishika vifaa vingine huku akiwa ameegamia ukuta na kulala. Walikuwa ni waandishi wa habari ambao waliamua kumsubiri mtu huyo nje ya nyumba yake mpaka pale ambapo angeamka asubuhi wajaribu kumhoji kama wangepata jambo lolote lile.
Alikuwa anakaa nje ya mji, Gongo la Mboto njia ya kuelekea Pugu lakini vijana hao wasanga tonge hawakujali umbali wala hatari ya usafiri mpaka huko, walifanikiwa kufika eneo hilo. Kijana ambaye alikuwa macho akiwa na hamu kubwa ya kukutana na mwanasheria huyo alikumshtua mwenzake ambaye naye alikurupuka huku wakiwa wanatetemeka, mwanasheria huyo ilikuwa ni adimu kumpata, hata ufanyaji wake wa kazi ulikuwa ni wa kutoonekana mara nyingi ndiyo maana hata kesi zake zilikuwa za gharama kubwa. Hali hiyo ilimfanya asiwe mtu wa kuzoeleka kirahisi hivyo watu wa hali ya chini kukutana naye haikuwa kawaida ndiyo sababu vijana hao walikuwa wakitetemeka hapo mtu huyo kuwajia mbele yao.
“Navutiwa na vijana ambao mnapenda kuutafuta ugali kwa namna yoyote kama hivi, hamkujali kama ningewagomea kukutana na mimi ila mliamini kwenye ndoto zenu na kuja kunisubiri hapa kuweza kufanya kazi. Fungeni vifaa vyenu tufanye mahojiano na kuniuliza maswali ambayo mnayataka, inaweza kuwa fursa kwenu kutengeneza maisha mazuri kwa sababu mkiwa makini, habari hii itaenda kuuza kwa ukubwa usio wa kawaida lakini kwa kujitoa kwenu wakati mnaondoka hapa ninawapa zawadi ya milioni hamsini za kitanzania” aliongea akiwa ametulia na kuwaangalia vijana hao ambao ni kama walikuwa hawaamini bado. Midomo yao ilionyesha cheko, cheko la furaha lililo mpelekea mmoja wao kushangilia kwa sauti kubwa, hawakuamini.
“Kuna habari inasambaa kwenye gazeti la UKWELI kwamba unataka kuifufua upya ile kesi ya miaka mitano, kesi ambayo ilifutwa na kufungwa kabisa kwa sababu yalionekana kuwa mambo ya ndani ya nchi na usalama wa ujumla, je kuna ukweli wowote juu ya jambo hilo?”
“Ndiyo”
“Kwanini unahitaji kulifanya jambo hili na kuanza kulifuatilia kwa sasa na sio miaka ambayo ilikuwa imepita huko nyuma?”
“Muda ndilo jambo ambalo huwa linaamua ufanyaji wa mambo kwa usahihi, niliiacha serikali ifanye jambo hilo na niliwapa muda ili nione kama kweli walikuwa wanalifuatilia kama walivyo sema lakini mwisho wa siku waliamua kuudanganya umma na jambo ambalo wao walilisema halikuwa la kweli”
“Huoni kama jambo hili linaweza kuleta machafuko kwa nchi hii?”
“Vipi kama baba yako mzazi ndiye angekuwepo kwenye ile safari, akafa halafu hakuna kitu ambacho kinafanyika bado ungeniambia kuhusu machafuko? Haki ya mtu haitakiwi kupoteza kipuuzi namna hii na wahusika wapo, unajua kwanini hawapo tayari kulipigania jambo hili? Kwa sababu ile haikutokea bahati mbaya bali ulikuwa ni mpango wa serikali yenyewe kuhakikisha wale watu wanakufa” Aliongea jambo ambalo lilimtisha hata mwandishi, alishindwa kuuliza akabaki anajiuma uma, mambo yalikuwa mazito alianza kuhofia usalama wake.
“Kijana haya maisha yapo tofauti na wewe unavyo yaona, hii nchi haipo huru kama ambavyo huwa unadanganywa kwenye vyombo vya habari na hao wapiga porojo ambao ni wanasiasa wanao angalia matumbo yao tu halafu utasikia vijana hivi, mara vijana vile wakati wao wenyewe ndio wahuni na wapigaji watupu. Watu wengi wameuawa, watu wengi wamepotezwa, watu wengi wamesingiziwa kesi huku wenye makosa wakiwa wanatamba mitandaoni na magari ya kifahari kwa kujivuna kwamba wana pesa nyingi, nani anajali? Hakuna mtu anawajali maskini wanyonge ambao wanapoteza haki zao, hakuna muda mwenye uchungu na wao kuwapoteza ndugu zao ila mpaka ndugu wa mwanasiasa au kiongozi mkubwa akiguswa hata kwa maneno tu hapo ndipo utaiona nguvu ya dola! Hili sio taifa la mtu, nchi ni mhimu kuliko maslahi ya mtu mmoja na siwezi kuruhusu hilo likafanyika;”
“Ni kweli nimeamua kuifungua kesi hii dhidi ya serikali, nawahitaji wasimame na mimi mahakamani waje kuthibitisha kwamba sio wao ambao waliwaua wale makomando tisa ambao walitumwa kwenye oparesheni ya kijeshi na ukombozi na kama wakiwa na huo ushahidi basi waje wajibu wameishia wapi na zoezi hilo ambalo wamelipotezea? Walicheza mchezo hatari kama huo halafu wakaamua kumpakazia kesi komando mmoja ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa makomando hao”;
“CLYTON LAMECK, kivipi mtu ambaye alijitoa miaka mingi, alijitoa kwa ajili ya vijana wake kirahisi tu aje kuwasaliti kwa sababu aliongea kiongozi fulani? Hawajawahi kuwa ushahidi na hawana uwezo wa kuthibitisha hilo ila ni mpuuzi mmoja akiwa juu ya kiuno cha mpenzi wake aliamua kuupika huu uongo na watu wakaamua kuuamini kama kawaida yao kukurupukia mambo ya kwenye mitandano. Nina faili la kesi ambalo nimelifungua na file hilo nimeamua kulipa jina la NAFSI ZILIZO TELEKEZWA”;
“Nimeamua kuipa kesi hii hilo jina kwa sababu; ni nafsi za watu ambazo ziliihitaji serikali kuzisaidia, kuziponya na kuzipa tumaini ya kuwa wazalendo wa taifa hili lakini serikali ikaamua kuudanganya umma, serikali ikaziacha nafsi hizo zikiangamia bila msaada wowote ule kwa kuzitelekeza, nafsi hizo zisinge telekezwa basi mpaka leo zingekuwa kwenye miili ya watu hao nao wangekuwa hai. Na kama wanajua kwamba jambo hilo ni moja basi wanapaswa kujiandaa vitu vya kujibu kwa sababu nafsi ya kwanza ambayo wanatakiwa kuitolea ufafanuzi sahihi ni wapi alipo EDISON CHRISTIAN, moja kati ya wanasayansi bora kuwahi kutokea ndani ya nchi hii lakini waliamua kumtoa sadaka mtu huyo kiasi kwamba haujawahi kupatikana ushahidi wa wapi alikwenda na kama yupo hai au amekufa ila wao wanajua walicho kifanya na MOSSAD hivyo wapeni taarifa kwamba nakuja” Alimaliza mahojiano yake na kuwapatia vijana hao kile ambacho alikiahidi na kuwapa maagizo kwamba walitakiwa kuachia habari ile kama alivyo ongea, hawakutakiwa kupunguza hata herufi wala neno moja na kama wangefanya hivyo basi yeye binafsi angeweza kuwatafuta ili kuwaonyesha yupo vipi kwenye huo upande wake mwingine.

UKURASA WA 38
 
Monsters are not born? Mazingira yanacreate monsters...
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 39

Asubuhi wakati kunakucha, nchi iliamka na habari hizo, habari ambayo ilianza kusambaa kwa nguvu kutokana na aina ya mtu ambaye alikuwa ameitoa taarifa hiyo. Mwanasheria nguli zaidi nchi ndiye alitoa hizo taarifa, mtu ambaye jamii ilikuwa ikimuamini kwa jambo lolote ambalo lilikuwa linatoka kwenye mdomo wake. Watu walianza kutoa lawama kwa serikali hususani suala la kupotea kwa mwanasayansi mashuhuri ambaye ni miaka mingi sana ilikuwa imepita lakini serikali haikuwahi kuonyesha kuguswa na jambo hilo hata kidogo lakini pia watu waliihitaji serikali itolee ufafanuzi juu ya tuhuma kutoka kwa mwanasheria huyo za kuhusika kwenye mauaji ya hao makomando tisa na mmoja ambaye alisadikika kuwa hai bila kujulikana alikuwa wapi ambaye aliuziwa hiyo kesi.
Taarifa hiyo ilifika mpaka ndani kabisa kwenye shirika la kijasusi ya nchi, IBA (INVESTIGATION BREAUCRACY AGENCY). Haikuwa habari njema kwao, ilikuwa ni habari mbaya ambayo ilikuwa inaenda kuwachafua wao, ofisi ya raisi lakini mpaka jeshi la nchi kwa wote kuoekana kutowajibika vya kutosha juu ya mambo ya hatari ambayo yalikuwa yanatokea nchini ukizingatia ni siku chache tu zilikuwa zimepita tangu kutokea kwa utekaji na mauaji uwanja wa ndege na bado watu hawakuwa wamepata taarifa zozote za kuridhisha, haukupita muda tena askari ambaye aliishika ile kesi ya kufuatilia jambo lile alikutwa akiwa ameuawa na wenzake wakiwa wameuliwa eneo jingine. Hali hiyo iliwafanya wananchi waanze kuandamana na kudai kwamba viongozi wa juu walitakiwa kutoa majibu na kama hawakuwa na majibu basi walitakiwa kuachia nafasi zao kwani hawakuwa na sifa stahiki za kuweza kuisimamia nchi yao na kupigania haki za watu wanyonge maskini.
Taarifa hiyo ambayo haikuwa njema ndiyo ilimtoa mwanamama Lionela Philson ambaye alikuwa mkurugenzi wa shirika la kijasusi la IBA nyumbani kwake na kumuwahisha ofisini akiwa mwingi wa hasira. Ofisi hizo za shirika hilo zilikuwa mita chache kutoka kilipo chuo cha mafunzo ya usalama wa taifa wa nchi huko Mbweni ambako wanapatikana watu wenye ukwasi wa kutosha hasa wale viongozi wa ngazi za juu serikalini na wafanya biashara wakubwa. Aliingia ofisini akiwa anawahitaji vijana wake ambao alikuwa anawaamini awakute wamejikusanya kwenye ukumbi wa mikutano.
Jengo lilikuwa ni kubwa la ghorofa mbili, lilitengenezwa kwa uzio mrefu na pembani yake hakuna mtu ambaye aliruhusiwa kujenga nyumba ya ghorofa kwa sababu wizara ya ardhi ilipiga marufuku kwa kudai kwamba eneo hilo halikuwa salama kulingana na aina ya udongo wake hata hilo ghorofa ambalo lilikuwepo lilikuwa kimakosa lakini watu wa maeneo ya mbali na eneo hilo walikuwa wanaruhusiwa kuweza kujenga nyumba ya aina yoyote ile kulingana na ukubwa wa mfuko wako. Lengo la kuzuia ujengaji wa majengo marefu, hawakuhitaji mtu yeyote aweze kutambua kitu ambacho kilikuwa kinaendelea humo ndani.
Mambo yao mengi yalikuwa yanafanyika chini ya ardhi ambako kulikuwa na vyumba na maofisi mengi na kila kitu kilimalizikia huko huku juu watu wachache wakiwa wanazuga kama wanayaendeleza maisha ya kila siku ambapo hata kama kwa bahati mbaya mtu angehoji basi asingekuwa na taarifa za jambo lolote ambalo lilikuwa linafanyika humo ndani. Akiwa amefura kwa hasira ambazo zilijidhihirisha kwa ndita zilizo jichora kwenye uso wake, alifika ofisini kwake na kuutua chini mkoba wake mdogo huku akiwa amevaa suti ya blue na koti lake akiwa amejifunikia tu bila kulivaa! Simu yake iliita.
Baada ya kuangalia vizuri aligundua kwamba simu ambayo ilikuwa inaita haikuwa ya ofisini bali namba yake binafsi, aliisogelea mahali ambapo alikuwa ameibwaga na kuipokea baada ya kugundua kwamba ilikuwa inapigwa na CDF.
“Kichwa changu hakipo sawa, tutaongea baadae”
“Hili jambo ni mhimu halihitaji hata kusubiri, sio muda hapa raisi atahitaji taarifa kwa skendo hii chafu ambayo inaendelea hivyo nahitaji kujua kama kuna taarifa zozote za mhimu ambazo unazo?”
“Hapana, hata mimi nimeshangazwa na taarifa hizi, huyu mwanasheria hajawahi kuonyesha dalili zozote za kulijua jambo hili sasa iweje aibuke tu ghafla baada ya miaka mingi kupita tena akiwa anaongelea habari za ukweli na kudai kwamba ana ushahidi wa kutosha? Hili sio bure kuna namna na hatari kubwa inaweza kuwa inajisogeza hali ambayo inaweza kuliingiza taifa kwenye majanga makubwa mbele ya macho yetu”
“Nadhani huyu anapaswa kuuawa” CDF alitamka kwa sauti ya nguvu
“Halafu?”
“Habari hiyo itakuwa imeishia hapo”
“Muda mwingine uwe unatumia akili, umepewa jeshi uliongoze nina imani sio kwa bahati mbaya. Huyo ni mtu ambaye anapendwa na watu na kwa hili ambalo limetokea kama akipata tatizo lolote lile basi moja kwa moja tutadhihirisha kwamba serikali imehusika moja kwa moja kwenye hilo jambo. Halafu ukizingatia yule ni gwiji wa sheria hauna huo uwezo wa kumkamata kijinga namna hiyo hivyo kwa sasa anatakiwa kuachwa kama alivyo”
“Yaani tumuache aendelee kufanya hiki anacho kifanya?”
“Jambo la msingi tunatakiwa kujua sababu ya yeye kuyaleta haya yote ni ipi na alikuwa wapi wakati wote mpaka ajitokeze saivi? Kuna kitu ambacho huenda hukifahamu kwa huyu bwana. Kuna taarifa zinadai kwamba ni mtu ambaye anaishi kwenye sura ya mtu mwingine na taarifa hizi kuna vyanzo vinadai kwamba alizivujisha yeye mwenyewe makusudi hivyo kabla ya kukurupuka kuna mengi ambayo tunatakiwa kuyajua kumhusu yeye. Ni muuji pia wa kutisha wa siri ambapo haijulikani haya mambo alijifunzia wapi lakini pia ni daktari mzuri tu na hilo wanalijua watu wachache”
“Hivi unamzungumzia ni huyu mwanasheria JACK THE LAWYER au mtu mwingine?”
“Ndiye huyo huyo mwenyewe, ndiyo maana nakwambia kwamba hatutakiwi kukurupuka huenda anajua kwamba tutafanya hivyo ili afanye anacho kitaka. Watu wenye akili ni hatari sana kama ukiamua kutumia mihemko kupambana nao hivyo kwa sasa usije ukathubutu hata kutuma watu wako kwake kwa sababu utazua mambo mengine ambayo siyo. Kuhusu raisi naenda kuongea naye kuhusu hili mimi mwenyewe” mwanamama huyo alikata simu baada ya kuona CDF anazidi kumhoji utadhani alikuwa mtuhumiwa wake. Alichukua kifaa chake kidogo cha mawasiliano mithili ya kalamu ya wino na kuelekea nayo kwenye chumba cha mkutano.
“Nadhani wote mnakumbuka vyema tukio la miaka mitano iliyopita, tukio ambalo lilileta mtikisiko mkubwa kwenye idara na nchi kwa ujumla baada ya makomando tisa kufariki na mmoja kupotelea kusiko julikana na kupewa kesi ya kuhusika na mauaji ya wenzake pamoja na kuuza siri za nchi. Jambo hilo limerudi tena kupitia mwanasheria JACK THE LAWYER” Aliweka kituo huku akiibonyeza ile kalamu yake katikati ambayo ilikuwa kama rimoti. Kwenye ukuta mkubwa paliwaka pakiwa na picha ya mwanasheria huyo ambaye alikuwa ndani ya suti ya gharama akiwa mwingi wa tabasamu. Mama huyo aliyaanzisha mazungumzo hayo bila hata kujibu salamu ya vijana wake wanne ambao walikuwa wakimsubiri ndani humu, watatu walikuwa wa kiume na mmoja wao ambaye ndiye alikuwa kiongozi wao alikuwa ni mwanamke! Aaliyah Beka.
“Anaadai kwamba kesi hii inatakiwa kufunguliwa upya na serikali ndiyo mshtakiwa, hili ni jambo baya kwa sababu kama serikali ikishindwa kwenye kesi hii ni kwamba viongozi wakubwa watahitajika kuachia nafasi zao na watu wengi watakosa kazi huku wengine wakitakiwa kufungwa. Ukiachana na jambo hilo, jambo la hatari zaidi ni kwamba nchi itapata mpasuko mkubwa ambao utakuwa ni hatari kwani unaweza ukachochea vurugu nyingi kama sio kuleta vita vya wenyewe kwa wenyewe”
“Sanjari na hilo, mwanasheria huyu huwa haongei vitu kwa kubahatisha, mpaka amefikia hatua ya kuongea mambo mazito kama hayo basi jua ana ushahidi wa kutosha. Kilicho zidi kueleta hofu kubwa ni baada ya kuifufua kesi ya miaka mingi iliyopita, kesi ya mwanasayansi Christian Edison ambaye serikali ilikubali kumpeleka huko MOSSAD kwa ajili ya kwenda kulisaidia taifa la Israeli kutengeneza nyuklia ila mpaka sasa haijawahi kurudi taarifa yoyote kumhusu na jambo hili halieleweki liliishia wapi ila mtu huyu anadai yeye anazo taarifa”

UKURASA WA 39 unafika mwisho.
 
Back
Top Bottom