FEBIANI BABUYA
JF-Expert Member
- Mar 5, 2022
- 1,916
- 3,850
- Thread starter
- #101
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 56
MADAM KATE
Lilikuwa nina maarufu ndani ya Black Market, jina ambalo liliheshimika na kuogopwa isivyokuwa kawaida. Ni kutokana na mambo ambayo alikuwa ameyafanya, mafanikio ambayo wengi waliamini kwamba ameyapata kutokana na biashara hizo zipatikanazo ndani ya soko jeusi. Licha ya kuwa maarufu sana huko lakini hakuwa akifahamika kwenye maisha halisi kwamba Madam Kate ni nani hasa.
Cersie Mhina ndilo lilikuwa jina halisi la mwanamke huyo, mwanamama ambaye alikuwa akiimbwa kila kona ya nchi kwa sababu alikuwa ni moja kati ya wanawake ambao walikuwa na mafanikio makubwa mno tofauti na mitazamo ya wengi ambavyo huwa ipo kwenye jinsia hiyo. Alikuwa amejikita zaidi kwenye biashara ya gesi pamoja na mitandao ya simu lakini pia alikuwa akijishughulisha na madini ya dhahabu. Mafanikio yake yalimfanya kuwa na ukaribu na viongozi wakubwa wa kiserikali kiasi kwamba akawa anahusishwa kwenye mipango mingi ya maendeleo ya nchi na hata kwenda kuiwakilisha nchi ilipokuwa inapata nafasi za uwekezeaji kimataifa kwa sababu alikuwa na uzoefu mkubwa kwenye biashara na uwezo mkubwa wa mikakati ya biashara kubwa ambapo hakuna mpango wake hata mmoja ambao ulikuwa umewahi kufeli chini yake.
Baada ya kutoka Bulgari mwanamama huyo alikuwa anahitaji kufanya mkutano, mkutano wa siri kati yake yeye na watu wake ambao alikuwa amewapa majukumu pamoja na viongozi kadhaa wa serikali. Usiku wa saa saba ndio ulikuwa muda wa kufanyika mkutano ndani ya jengo lake kubwa la biashara ambalo lilikuwa limejengwa maeneo ya Mikocheni Dar es salaam.
MHINA TOWER, majina ambayo yalikuwa yanang’aa yalilipamba jengo hilo na kuyafanya yasomeke vyema wakati huo wa usiku kiasi kwamba hata kama mtu angekuwa mbali basi maandishi hayo angeyaona kwa usahihi bila shaka. Ndani ya eneo la chini kabisa la jengo hilo, yalianza kupaki magari ya kifahari mno, ilikuwa ni ishara ya watu hao kuweza kukutana na kiongozi wao kujadili mambo mbalimbali yakiwemo maseke seke ambayo bado yalikuwa yanaendelea kutokea.
Zilipaki gari kadhaa na watu walikuwa wakionekana kuelekea kwenye lifti na kupandisha maghorofa ya juu. Zilipita kama dakika tano baadae ndipo ukaonekana msafara wa gari tatu ukiwa unaelekea eneo hilo, msafara huo ndio ulikuwa wa boss lady mwenyewe akiwa na walinzi wake kumi. Mmoja wa watu ambao walikuwa kwenye huo msafara alikuwa ni mwanaume Yohani Mawenge.
“Baadae natakiwa kuongea na wewe unipe mrejesho wa kazi zote ambazo nimekupatia uzikamilishe” mwanamama huyo aliongea kwa sauti ya taratibu akiwa anamwangalia kijana wake huyo mtu kazi Yohani Mawenge.
“Sawa bosi”
Chumba kikubwa ambacho kilipambwa na marashi ya kutosha pamoja na samani za bei ghali mno, kilikuwa kina wana wanaume watano ambao walikuwa wametangulia kabla yake madam Kate. Yeye aliingia humo ndani akiwa ameongozana na Yohani ambaye alikuwa ameishika begi ya mwanamama huyo. Baada ya kufika wote waliinuka kumpatia heshima kwani walionekana kumuogopa isivyokuwa kawaida, waliketi baada ya yeye kuketi kwenye kiti ambacho kilikuwa mbele ya hao wote tena katikati kabisa.
“Ni muda umepita sasa tangu niwe nje ya nchi, kuna mambo yanaendelea hapa nchini ambayo ni hatari kwa biashara yetu na kwa jamii yetu kwa ujumla na hatutakiwi kuruhusu kabisa yaendelee kutokea ndiyo maana nimewaiteni hapa leo tuweze kuyaweka sawa haya mambo kuhakikisha kila kitu kinaenda kama kilivyokuwa kimepangwa” aliongea akiwa anaivua miwani yake na kuiweka juu ya meza. Umri ulikuwa umekwenda lakini pesa ilimfanya bado aendelee kuvutia kwenye macho ya watu ambao walikuwa wanamtazama.
“Hili jambo ni kweli kwa sababu tangu lile tukio ambalo lilitokea pale uwanja wa ndege, ni kama lilikuja kwa wakati mbaya zaidi kumteka binti yule maana ujio wake umekuwa chanzo cha matatizo mengi hivyo naona anatakiwa kufa” Aliongea mwanaume mmoja mtu mzima lakini kwa bahati mbaya hakujulikana ni nani kwa sababu nyuso zao wote watano zilikuwa zimefunikwa kasoro mwanamama huyo pekee ndiye ambaye uso wake ulikuwa wazi. Hao wote hawakutakiwa kabisa kujuana ili kila mtu kuwa na amani na kila ambacho kilikuwa kinafanyika.
“Unamaanisha yule binti ambaye aliiba mzigo wetu?”
“Ndiyo madam”
“Yule atakufa ila sio kwa sasa”
“Kwanini?”
“Kwa sababu nafanya naye kazi”
“Hilo ni jambo ambalo haliwezekani bosi, inawezekanaje mtu ambaye ameiba mzigo wa mabilioni ya pesa ufanye naye kazi kirahisi tu hivyo?” aling’aka mwanaume mwingine kwa jazba ambayo ndani yake ilikuwa na heshima kwa mwanamke huyo.
“Kwa sababu naye anamtafuta mtu ambaye tunamtafuta sisi, alinihakikishia kwamba alikuwa anahitaji kuonana na mimi ili nimsaidie ndiyo maana akafanya lile jambo la kujikamatisha na sio mtoto wa Patrick Magembe kama alivyokuwa amedanganya bali ni mtoto wa mwanasheria wa zamani Aidan Semzaba na ni miongozi mwa watu ambao wana mafunzo ya kikomando”
“Unamaanisha kwamba yule komando Daniel ambaye alifia Somalia ni kaka yake wa damu?”
“Ndiyo”
“Kwahiyo hii ndiyo sababu ambayo imefanya amtafute Clyton Lameck?”
“Ndiyo hivyo kwa namna moja ama nyingine atatusaidia kazi kwa kiasi kikubwa na baada ya hapo atanipa mzigo wetu kisha nitamuua kwa mkono wangu mwenyewe” kauli hiyo ilionyesha kuwafurahisha wote humo ndani ambapo waligongesha mikono yao juu ya meza kuunga mkono jambo hilo lakini mmoja wao ambaye alivaa suti ya gharama ya kijivu alijikohoza kwa nguvu ili wenzake wampe umakini wa kumsikiliza.
“Bosi tunasubiri utupatie muongozo wa hatua zilizo chukuliwa, tulipo na tunapo elekea kwa sababu kama unavyo ona hali imekuwa mbaya hususani kwa yule mwanasheria yule ambaye hata jana amefika nyumbani kwa dokta Namaki Prasad hivyo kama tungechelewa kidogo basi huenda angepata siri nyingi ambazo hatakiwi kuzipata. Yule mtu huwa hazushi jambo bila kuwa na ushahidi hivyo mpaka anaongea hayo yote mitandaoni na kwenye vyombo vya habari basi ana mengi ambayo anayajua, tunataka kujua maamuzi ya jamii yetu ni yapi kuhakikisha sisi wote tupo sehemu salama na haya yanaisha” Mzee huyo aliuliza swali la maana kabisa ambalo huenda ndiyo ilikuwa sababu ya msingi zaidi ya kuweza kuwafikisha hapo usiku huo.
“Najua hicho ndicho kimetuleta hapa usiku wa leo, mambo yote yameenda kama yalivyopangwa, Keneth Lawi amekufa tayari Yohani aliifanya kazi vizuri nchini Uganda lakini wanatuma majasusi wao kuja kupeleleza na majasusi hao wanatakiwa kufa bila kuacha ushahidi wowote. Tukija hapa nyumbani, daktari tayari amekufa hivyo moja ya siri kubwa zinaendelea kuwa salama lakini shida ipo sehemu moja kwa yule kijana Damasi, yule alifanya kosa kubwa kuweza kuruhusu sura yake kuonekana jambo ambalo sasa gharama yake itakuwa kubwa kwani inatulazimu kuhakikisha shirika la kipelelezi la nchi haliendelei na habari yake ambayo kama ikija kuwa wazi zaidi itakuwa ni hatari kwetu. Nitalishughulikia lakini kama likifeli kabisa basi nitamuua mwenyewe hivyo msiwe na shaka kuhusu yeye” maelezo yake yalikuwa yamenyooka na kuwapa amani watu hao ambao walikuwa wameanza kupata wasiwasi kwenye mioyo yao.
“Sasa jambo la mhimu zaidi ni hatima ya huyo Lameck pamoja na JACK THE LAWYER, kuna kipi kitafanyika juu yao?”
“Hayo yote mimi nitawashughulikia ila ninacho kitaka kwa sasa, kama kuna mtu kati yenu bado ana biashara ambazo anaona sio sawa basi azisimamishe zote mara moja, nitawapa ratiba ya kuanza kuzifanya kwa mara nyingine. Hakuna kosa la kijinga ambalo linatakiwa kufanyika ila hao wawili ambao mmewaulizia ni kwamba wanatakiwa kufa mapema iwezekanavyo”
“Sawa bosi, na viongozi wakuu uliahidi kwamba tutawaona!” aliuliza mwanaume mmoja ambaye tangu aingie hapo ndani hakuwa ameongea jambo lolote lile. Madam Kate alimwangalia kwa muda kisha akatabasamu.
UKURASA WA 56 unafika mwisho.