Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Kijana wa masta...uko huku? Yeah weekend inakuwa ndefu sana bila ma episode ya mkuu SinganoJr. Mkuu Singano wabariki wana wape mashavu...hadith tamu sana, elimu ya dunia na sayansi, mapenzi...kila kitu kipo...Hongera sana Singanojr.
Nipo kiongozi maana mbali na soka pia ni mlevi wa simulizi.
 
Vijana tupo mkuu tumepanga foleni kwa hamu kusubiria. Tunajua kutuburudisha ni kazi bt unatufaa kiongozi. Big up
 
SEHEMU YA 281

Edna alikaa kimya kidogo pasipo kuongea huku akimwangalia Roma , alikuwa akiweka karata zake vizuri.

“Nitakuacha uendelee na wanawake wako wote kwasasa na sitokuingilia kwa chochote”Aliongea Edna na kumfanya moyo wa Roma kutabasamu na kuona yes dili hilo lilikuwa zuri , lakini hata hivyo aliwaza Edna na yeye ananufaika vipi kwenye hilo dili.

“Na wewe unapata nini?”

“Nitakaa na Lanlan kwa muda wa siku ishirini na tisa na kama babu yake hatajitokeza nitafanya maamuzi ya kumsajili kama mtoto wetu na kuhusu mkataba wa ndoa tutaurefusha kwa mwaka mmoja, najua hata kama kutatokea jambo la kutufanya tuachane ndani ya mwaka mmoja bado nitakuwa na uhalali wa kumlea Lanlan kama mtoto wangu”Aliongea Edna na kumfanya Roma avute pumzi baada ya kusikia meneno hayo , yaani kwa haraka haraka Edna alikuwa akimaanisha kwamba swala la kumlea Lanlan atalibeba yeye mwenyewe na haijalishi kama anapenda au hapendi huku yeye akifaidika kwa kuendelea na wanawake wake.

“Na kama nitakaa hili dili , nini kitatokea?”

“Utaachana na wanawake zako na tutaoana ndoa ya kihalali na tutatengeneza familia na Lanlan ataendelea kulelewa hapa kituoni , kama hutaki kuachana na wanawake zako basi tutaachana kwa talaka uwe unapenda au hupendi”Aliongea Edna akiwa siriasi na Roma alielewa kabisa mrembo huyyo hakuwa akitania hata kidogo , lakini hata hivyo hakuwa na cha kufikira kwani moyo wake una majibu yote, Roma alikuna kichwa chake kwa sekunde.

“Ninakuachia uishi na Lanlan baada ya siku hizo ishirini na tisa kama babu yake asipotokea tutamsajili kama mtoto wetu na tutamlea na mimi nitaendelea na wanawake wangu na wewe utakuwa mke wangu, lakini na mimi lazima niweke masharti yangu”Aliongea Roma na kumfanya Edna atingishe kichwa kumwambia aweke masharti mezani.

“Kwanza lazima uniahidi kwamba hutowaletea shida wanawake wangu na utaweka juhudi ya kuendana nao vizuri na mimi ninaahidi ndani ya mwaka mmoja nitakufanya kwa hiari yako mwenyewe kuoana na mimi kihalali na sio kwa mkataba na tutalala chumba kimoja”Aliongea Roma na Edna alifikiria kidogo na kisha aliona hana cha kupoteza, kwake aliamini kuwa na Lanlan kwenye Maisha yake atakuwa na furaha na Roma ataendelea kumpa ulinzi , lakini pia kama mwanamke alikuwa na shauku ni jambo gani ambalo Roma atalifanya mpaka yeye mwenyewe kukubali kuona nae kihalali.

“Deal”Aliongea Edna na kumfanya Roma kutabasamu.

“Wife unaonekana kumpenda sana Lanlan na upo tayari kufanya chochote juu yake”

“Nampenda ndio na kuna wito ndani yangu unaniambia Lanlan ni mtoto wangu , najua sijawahi kuwa mzazi lakini naweza kutafsiri ninachojisikia moyoni”Aliongea Edna na kunyanyuka kwa ajili ya kumuita Mama Issa na ndani ya dakika chache Mama Issa alifika.

“Mama Issa mimi na mke wangu tupo tayari kumchukua Lanlan kwa muda wa siku hizo ishirini na tisa na kama babu yake hatatokea basi tutamlea Lanlan”aliongea Roma na kumfanya Mama Issa kutabasamu

“Edna upo tyari kuanza malezi?”

“Mama Issa unanijua mwenyewe ninavyopenda Watoto , nipo tayari kumlea Lanlan”Aliongea Edna kwa furaha , ukweli aliona anacheleweshwa na alitaka kumuona Lanlan , alikumbuka mara ya mwisho alimtelekeza Lanlan kwa kumchagua Roma na ndani yake kuna hatia na alihitaji kujiponya.

Mama Issa hakuwa na kinyongo kazi aliokuwa amepewa ni kuhakikisha Lanlan anakuwa salama kwa niaba ya Master Chi, na aliamini Edna ni mtu sahihi kabisa wa kumlea Lanlan.

“Edna kama mpo tayari basi utaondoka na Lanlan siku ya leo , Master Chi amenieleza historia ya Maisha kwa ufupi ya Lanlan na kusema kwamba hana mama na hata baba yake hamfahamu na pia hajawahi kupelekwa shule , hivyo kwa mtazamo wangu kama mzazi naamini kabisa Lanlan anakuhitaji”Aliongea Mama Issa na kisha akanyanyuka na kuwpa ishara waongozane.

Dakika chache mbele walikuwa ndani ya nyumba ambayo Lanlan na Babu yake walikuwa wakiishi na ile wanakaribia tu mlango ulifunguliwa kwa spidi na akatokea Lanlan ambaye alionekana alikuwa akivalishwa Sweta kwani mkono mmoja haukua umetokezea na ilionyesha alipohisi tu uwepo wa Edna alitoka nduki.

“Maamaa..”Aliita Lanlan na kama mshale alimrurikia Edna kifuani na kama sio Roma basi Edna angedondoka kwani nguvu aliotumia Lanlan haikuwa ya kawaida kabisa na Roma alimshikilia Edna kwa nyuma.

Muda uleule na Qiang Xi alitoka akikimbia na alipomuona Edna na Roma alisimama na kuwaangalia , ni kama mtu ambaye hakuwa akiwafahamu na alianza kutembea taratibu.

“Mama , Lanlan amekumisi sana”

“Usijali Lanlan mama yako nimekuja kukuchukua”Aliongea Edna na kumfanya Lanlan kulipukwa na furaha.

“Aunt Qiang, Lanlan hawezi kuachwa tena na mama yake”Aliongea Lanlan na Edna alishitukia busu la kwenye shavu.

Vitendo vilivyokuwa vikifanywa na Lanlan vilimfanya Roma kushika kiuno na kumwangalia huyo mtoto , alijikuta akivutiwa na matendo yake na kumkera kwa wakati mmoja.

“Chubi unaonekana kuwa na furaha”Aliongea Roma na Lanlan alimwangalia Roma kwa macho makali.

“Lanlan sio Chubi , Lanlan anapenda jina lake”

“Qiang nishaongea na Miss Edna hapa Pamoja na Mr Roma na jiandae muweze kuondoka Pamoja kama Master alivyokupa maelekezo”Aliongea Mama Issa na kumfanya Qiang kuwaangalia Roma na Edna kwa sekunde na kisha alisimama wima na kuinamisha kichwa chini kama ishara ya salamu ya heshima na Edna alitabasamu.

Naam ndani ya dakika chache tu Roma na Edna walikuwa washachukua vitu vichache vya Lanlan Pamoja na vya Qiang na sasa walikuwa barabarani wakirejea nyumbani.

Ile hali ya huzuni aliokuwa nayo Edna ilikuwa imepotea kwa asilimia mia moja na roho yake ilikuwa nyeupe , hakuamini Lanlan karudi kwenye mikono yake na sasa anarudi nae nyumbani.

Roma aliekuwa akiendesha gari alijikuta akivuta pumzi na kuridhika baada ya kuona tabasamu la mke wake na kujiambia kama hiko ndio anachokipenda basi atamsapoti kwa namna yoyote ile.

“Mama Lanlan ana njaa na amemisi kula nyama”Aliongea Lanlan na kumfanya Edna amwangalie.

“Lanlan mwili wako ni mnene tayari , usipende sana kula nyama sawa”

“Lakini Lanlan anapenda kula nyama”Aliongea na kumfanya Edna kuvuta pumzi.

“Usijali mimi mama yako nitahakikisha unakula nyama”Aliongea Edna na kumfanya Lanlan kufurahi mno.

Upande wa Qiang alionekana kumwangalia Roma kila mara , inaonekana kuna jambo ambalo alikuwa akijaribu kulificha.

……….

“Baada ya siku ishirini na tisa nisiporudi utampa Roma hii barua?”Aliongea Master Chi jana yake usiku kabla ya kuondoka na hio ni mara baada ya kutoka kuongea na Mama Issa.

“Master unaenda wapi?”Aliuliza Qiang Xi kwa wasiwasi mno huku akimwangalia Master wake.

“Qiang najua tumekuwa karibu kwa Zaidi ya miaka miwili sasa na umejitoa sana kwangu na kwa Lanlan , lakini pia naelewa hisia zako juu yangu lakini siwezi kuzipokea hisia zako mpaka nikamilishe misheni yangu”Aliongea Master Chi na kumfanyaQiang kutoa machozi, ni kweli kabisa mrembo huyo wa kichina alikuwa akimpenda Master wake kimapenzi na alijitahidi kuonyesha lakini Master Chi hakuwahi kuonyesha utayari wa kuzikubali hisia zake.

“Lakini Master hujaniambia unaenda wapi , ninapatwa na wasiwasi”aliongea kwa kichina.

“Qiang Xi siwezi kukuambia kazi ninayokwenda kufanya , ila tambua kwamba ni kazi hatari sana na naweza kurudi ndani ya siku ishirini na tisa ama nisirudi kabisa milele na ndio maana nakupa hii barua , usiifungue ndani, nisiporudi ndani ya siku hizo mpatie Roma na atajua cha kufanya”Aliongea Master Chi na Qiang Xi aliipokea kwa huzuni kubwa.

Siku ya asubuhi baada ya kuamka hakumuona kabisa Master na hata baadhi ya nguo zake hazikuwepo ikiashiria kwamba ameondoka kimya kimya na hajamuaga Lanlan mjukuu wake.

Mrembo Qiang Xi alijikuta akikaa eneo la sebuleni akianza kulia mno huku akiwa ameshikilia barua aliopewa na Master Chi , kila akikumbuka kwamba Master wake anakwenda kupambana na anaweza asimuone tena, moyo wake ulijawa na wasiwasi mwingi, wasiwasi ambao ulimpelekea kuvunja ahadi na kufanya maamuzi ya kufungua barua iliokuwa kwenye mikono yake.

Baada kuchana bahasha iliohifadhia barua hio muda huu wa saa kumi na mbili za asubuhi, aliifungua vizuri na kuanza kuisoma na aijikuta machozi yakianza kumtoka na kushangaa kwa wakati mmmoja.









SEHEMU YA 282

Sasa Qiang Xi baada ya kusoma barua ile ndio anagundua mambo mengi sana , aligunuda Lanlan baba yake ni Roma na mama yake ni pacha wake na Edna , jambo ambalo lilimshangaza mno , lakini aligundua pia ndani ya barua hio kulikuw ana maelezo juu ya jina ambalo hakuwahi kulisikia jina lililosomeka ‘Athena’ kwa maelezo ya barua hio ni kwamba mama yake Lanlan yaani Seventeen ameuliwa na Athena na Master Tang Chi amejitoa kupambana na Athena ili kulipiza kisasi.

Jambo jingine alifahamu sasa kwanini Master Tang Chi Maisha yake yalikuwa ya kujificha kwani kwenye barua hio alionyesha Roma yeye anafahamu Master wake aliemfundisha mapigano miaka mingi nyuma aliuliwa na kikosi cha Dhoruba nyekundu, maneno alioyasoma Qiang Xi yalikuwa mazito sana na alijikuta akitetemeka.

“Hapana hii barua haiwezi kumfikia Mr Roma”aliongea Qiang Xi huku akiangalia barua hio kwa machozi.

Dakika kadhaa mbele Qiang Xi maneno yake yaliendana na vitendo kwani alichukua kiberiti na kuichoma ile barua, haikueleweka alikuwa akifanya nini , lakini alikuwa akivunja ahadi aliowekeana na Master Chi , ahadi ambayo alitakiwa baada ya siku ishirini na tisa kama Master Chi hataonekana basi barua hio ikabidhiwe Roma.

Sasa haikueleweka kwamba jambo hili analolifanya lilikuwa lina athari gani kwa Lanlan lakini yeye aliamini maamuzi yake ni sahihi kabisa.

Dakika chache mbele baada ya kukamilisha kazi yake na kuthibitisha majivu yamepotelea hewani alirudi ndani na kumuamsha Lanlan.

“Lanlan utanisamehe , najua Master dhumuni lake ni kukufikisha kwa baba yako na hili limefanikiwa kwa asilimia mia moja , Roma akijua siri nyuma ya kifo cha mama yako mzazi anaweza akashindwa kukulinda na mawazo yake yakahamia kwenye kulipiza kisasi kama Master alivyosasa”Aliwaza Qiang Xi

……..

Qiang xi aliekuwa kwenye mawazo alishindwa hata kuelewa ni muda gani waliweza kufika nyumbani kwa Edna , kwani alijikuta akiwa ndani ya ukuta , alionekana kujutia , lakini alijiapiza kama Master wake hatorudi ndani ya siku hizo ishirini na tisa basi siri ya barua alioacha atabaki nayo moyoni.

Alijikuta akishangazwa na ukubwa wa jumba ambalo anakwenda kuanza Maisha mapya , kila kitu kilichokuwa kwenye macho yake kilikuwa cha kifahari , Maisha hayo ndio aliokuwa akiota , kwanni licha ya kwamba alizaliwa kwenye taifa lenye uchumi mkubwa , lakini hakuwahi kuwaza kuishi sehemu ya kitajiri kama hio.

Sophia na Yezi ndio waliokuwa wa kwanza kushangazwa na ujio wa Lanlan , kwa upande wa Sophia alikuwa amkumbuka Lanlan kwani alishwahi kukutaa nae kituo cha kulelea yatima lakini alishangaa ujio wake hapo ndani.

“Sophia unamkumbuka Lanlan?”Aliongea Edna kwa tabasamu.

“Ndio kwanini nimsahau mtoto mzuri kama huyu”Aliongea Sophia na muda huu walikuwa nje.

“Tutaanza kuishi nae hapa ndani”Aliongea Edna na kumfanya Sophia kushangaa na sio kwake tu hata kwa Yezi.

Sophia alimwangalia Roma kama mtu anaejiuliza nini kinaendelea lakini Roma hakujibu Zaidi ya kutangulia ndani.

Edna aliwapa taarifa wanafamilia wote kwamba baada ya siku ishirini na tisa kama babu yake Lanlan atakuwa hajatokea , basi yeye na Roma wataanza taratibu za kumlea kama mtoto wao wa kwanza.

Jambo hilo hakuna ambaye alikuwa ni wa kupinga , Bi Wema alikubali na wengine wote walikubali , lakini upande wa Blandina alikuwa yupo nusu kwa nusu , ukweli hakupenda wazo la kumlea Lanlan kwnai aliamini Edna anao uwezo wa kumzalia wajukuu lakini hata hivyo alikuwa ahsakubaliana na Mama Issa juu ya mustakabali wa Lanlan jana yake lakini pia kwasababu ni wanandoa hao ndio wamekubali kumlea Lanlan basi yeye aliona asiweke pingamizi na kusubiria hizo siku ishirini na tisa zifike ili ijulikane kama Lanlan anaelelewa au anarudi kwenye familia yake.

Siku hio hio kabla haijaisha Mzee Kweka alimpigia simu Roma na kumwabia kwamba aanasubiria siku ambayo ataamua kumtembelea yeye na mkwe wake Edna na jibu la Roma lilikuwa jepesi tu kwmaba ataangalia maana hajawaza bado kurudi kwenye familia na hana mpango wa kubadili jina lake na kuitwa jina la ukoo.

“Mzee sina mpango wa kuitwa Roma Kweka , nimezoea jina langu la Roma Ramoni”hilo ndio jibu lake.

Naam ujio wa Lanlan ulichangamsha sana nyumba, kila mmmoja alifurahishwa na Lanlan na yote hayo ni namna ambavyo Lanlan alionesha hali ya kukomaa kimawazo licha ya kuwa mdogo.

Roma rasmi anajikuta akipata mshindani wake kwenye swala la chakula , mwanzoni wanafamilia wote walikuwa wakila chakula kidogo na kumwachia sehemu kubwa yeye , lakini ujio wa Lanlan ulibadilisha kabisa kiasi cha chakula kinachopikwa.

Kila mtu alishangazwa na uwezo wa kula wa Lanlan kwani licha ya wao kuwa watu wazima , lakini walikuwa wakizidiwa sana na Lanlan kwenye swala la msosi na swala hili lilimpa wasiwasi Edna lakini Qiang alijitahidi kueleza familia kwamba licha ya Lanlan kuwa mtoto lakini pia sio mtoto wwa kawaida na anayo mengi ya kuwashangaza.

“Bibi Lanlan ana ana njaa”Aliongea Lanlan siku ya jumatatu , siku ambayo Edna na Roma walikuwa washaenda tayari kazini na jukumu la kuhakikisha Lanlan amekula ni la Blandina na wanafamilia wengine.

Sasa kwasababu Blandina ndio alishinda na Lanlan , shida zote Lanlan alimueleza bibi yake.

Livha ya kwamba anajua fika Lanlan sio mtoto wa damu wa Roma , lakini alijikuta akimpenda sana na Lanlan alioneka kutokuwa msumbufu kabisa.

“Lanlan lakini sasa hivi ni saa tano na muda wa chakula bado”

“Lakini bibi Lanlan ana njaa”Aliongea na kumfanya Blandina kutamani kucheka , ilibidi atafute namna ya Lanlan kupata chakula japo muda wa kula chakula cha mchana bado.

Naam siku ya jumatatu Roma alikuwa ndani ya jengo la kampuni ya Vexto Media akiendelea na majukumu yake kama kawaida , majukumu ya kucheza gemu na siku hio alijikuta akiwa bize sana baada ya kuweza kupata gemu ambalo linamfanya kila akishinda kujipatia pesa , jambo hili lilimfurahisha mno na kuona afadhali sana hafiki kazini kupoteza muda bali anafika kazini na kucheza gemu kwa kulipwa.

Wakati akiendelea kucheza gemu kwa utulivu kabisa ndani ya ofisi hii ya kibosi ambayo amepewa na mke wake , mara simu yake ilitoa mlio wa sauti kuashiria kuna ujumbe wa meseji ambao umeingia na kumfanya kusubirisha gemu na kisha kuchukua simu yake iliokuwa juu ya meza na alijikuta akishangaa baada ya kuona namba ambayo haikuwa ya kitanzania namba ambayo iliambatana na ujumbe wa ‘Help me’ yaani nisaidie.

“Mh hii namba nikiangalia ni ya Japan , kwanini imenitumia ujumbe wa kuomba msaada?”Aliwaza Roma huku akiangalia meseji hio kwa dakika, ni meseji fupi sana ambayo haikuambatana na ujumbe wa aina yoyote ule wa ziada kwa mfano kujitambulisha jina na mengineyo.

Roma aliachana na simu yake na kuendelea kucheza gemu kwa nusu saa na meseji nyingine iliingia kwenye simu yake kwa mara nyingine na alisubirisha tena gemu na kuinua simu yake na kuangalia.

“Help me”

Ilisomeka tena hio mesji kwa mara nyingine na namba zinazofanana na kumfanya Roma kufikiria kidogo , aliona huenda meseji hio imekusudiwa kwake , lakini bado alihisi kwenye moyo wake meseji hio sio ya kwake.

Baada ya kutafakari kwa dakika alifanya maamuzi na kupiga namba ya Diego.

“Mfalme Pluto za muda huu?”

“Salama Diego , bado mpo kambini?”

“Ndio mfalme mafunzo yanaendelea na nimefurahishwa na jinsi vijana wanvyojituma na nadhani ndani ya mwezi huu tutakamilisha”

“Vizuri sana Diego , siku ya kuhitimu nitafika kuangalia kazi mlioifanya”Aliongea Roma.

“Sawa mfalme Pluto unakaribishwa sana na itakuwa heshima kwangu na kwa Adeline na Molin “

“Okey Deigo kuna namba imenitumia meseji muda huu na Napata hisia imelengwa kwangu nataka mjaribu kuifatilia”Aliongea Roma na Diego almwambia mfodiwe meseji na namba ili aongee na Bram kuendelea kuifatilia.

Na baada ya Roma kutoa namba hio alirejesha macho yake kwenye tarakishi na kuendelea kucheza gemu na baada ya nusu saa tu iliingia meseji ningine na alisubirisha na kisha akavuta simu yake na kuangalia na meseji ilisomeka tena.

“Help me” na namba ile ile na mpaka hapo aliamini hio namba imelengwa kwake kwa asilimia mia moja na alijikuta akikatishwa kufikiria na simu ya Diego.

“Diego mmepata nini?”

“Mfalme Bram anasema namba hio intaoa mawasiliano kutoka Hokkaido Japan”Aliongea Diego.

“Hokkaido!!””

“Ndio mfalme Pluto ,Bram kafanikiwa kupin point location na inaonekana inatoka ndani ya jumba linalomilikuwa na kampuni ya Emaar.

“Emaar!!”Roma aliongea na kuanza kufikiria kwa sekunde.

“Diego unamaanisha Emaar kampuni kutoka Dubai?”Aliuliza Roma.

“Ndio mfalme Pluto”

“Asante sana Diego , nitakupigia”aliongea Roma na kukata simu na palepale aliingia mtandao wa Google na kusearch kampuni ya Emaar , ukweli mpaka hapo kuna hisia ambazo zilikuwa zikimwambia mtu anaemtumia ujumbe ni Amina mrembo ambaye ashawahi kulala nae , hakujua hisia hizo zilikuwa zikitoka wapi lakini alikuwa na uhakika kwamba mtu ambaye anaweza akaomba msaada kutoka kwake na ambaye yupo ndani ya kampuni ya Emaar ni Amina pekee.

Roma baada yakuona mtandao haumletei majibu anayoyataka palepale alimpigia simu Diego na kumpa maelekezo ya kumwambia Bram ajaribu kutumia picha ya Amina ili kutambua mahali alipo na kwasababu Roma kwa kupitia jeshi lake la The Eagles walikuwa wakimiliki satilaiti ya Crogo , swala hilo lilikuwa jepesi sana , kwani walikuwa na teknolojia ya Facial Recognition na kama watasambaza signal ambazo zimeambatana na sura ya Aabasi ni rahisi ya kumpata hata akiwa ndani ya nyumba na Signal kuwa Reflected Kwenda kwenye satilaiti.

“Mfalme Pluto , Amina anaonekan kuwa Japani ndani ya Hokkaido , mpaka hapa naamini yeye ndio anakutumia meseji za kukuomba msaada”Aliongea Diego na Roma baada ya kusikia hivyo sasa alipata uhakika mtu ambaye anaomba msaada ni mrembo Amina.

Alifikiria kidogo na kupima uzito wa jambo lenyewe na kuona moyo wake ushakuwa mzito tayari na kama hatofanya maamuzi basi anaweza asiwe na amani.

“Wife nina safiri”Aliongea Roma mara baada ya kuinua simu yake na alionekana alikuwa akiongea na Edna.

“Kwenda wapi?”

“Nitaelekea Japani , lakini kwasasa sina ticket , nataka unisaidie kuipata kwa haraka sana kwa kutumia koneksheni zako , nataka ndege inayotoka sasa hivi”Aliongea Roma na Edna alionekana hajibu.

“Kuna shida gani Japani?”

“Nitakueleza nitakapo rudi , naomba ufanye kama nilivyokuomba”Aliongea Roma na kukata simu.

“Hapana siwezi kuteleport hapa mpaka Japani ni umbali mrefu sana na nitaviolate ‘Space Laws’ na kitu kibaya kinaweza kunikuta njiani”Aliwaza Roma na palepale alinyanyuka na kuchuku kila kilicho chake, alitoa maagizo kwa msadizi wake kwamba anasafiri na atarejea kazini akirudi nchin , jambo ambalo lilimshangaza Daudi , lakini hakuwa na jinsi kwanii Roma ndio boss.

Roma wakati anakaribia nyumbani tu , Edna alimpigia simu.

“Kuna ndege inaelekea Japani masaa matatu yajayo , nishakukatia tiketi na utakutana na Suzzane uwanja wa ndege”Aliongea Edna na Roma alitabasamu.

“Thank you babe”

“Sijui unachoenda kufanya huko Japani ni cha hatari namna gani , lakini urudi salama , hatujamalizaa”Aliongea Edna na kukata simu na kumfanya Roma kutabasamu.
 
SEEHEMU YA 283.

Roma alifanikuwa kufika uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere na akakutana na Suzzane ambaye alimkabidhi tiketi yake pasipo ya maneno mengi na
Suzzane ndio alirudi nyumbani na gari ya Roma.

Dakika ishirini zilimtosha kabisa Roma kufuata taratibu zote za kiusafiri ndani ya uwanja huu kwa ajili ya kuelekea Japani.

Tanzania hakukuwa na ndege ambayo ilikuwa ikiondoka moja kwa moja kwenda Hokkaido , hivyo ilikuwa ikimlazimu Roma kufika kwanza Tokyo na ndio apande ndege ya kwenda Chitose Airport ndani ya jiji la Sapporo katika kisiwa cha Hokkaido.

Kabla ya Roma kuanza safari ya kuja ndani ya uwanja huu wa ndege alikuwa ashawasiliana na Rafiki yake Makedoni kuttoka shirika la kijajusi la Israeli , yaani Mossad ili kumsaidia kutafuta ni kipi kinaendelea ndani ya familia ya Tajiri Khalifa kutoka Dubai na aliamini mpaka muda ambao atatua ndani ya uwanja wa ndege wa Haneda Tokyo, basi Makedoni atakuwa amekamilisha kazi ya kufatilia swala lake.

Unaweza ukashangaa kwanini Roma akamuomba Makedoni jasusi kutoka Mossadi , hii ni kwamba duniani matajiri wote wakubwa wanafauatiliwa kwa kila wanachokifanya , yaani kwanzia watu wanaokutana nao , miingiliano yao na serikali na mengine mengi, sasa zipo sababu nyingi ambazo idara kubwa za kijasusi kama MOSSAD au CIA kufuatilia matajiri wakubwa duniani na ndio maana Roma aliamini kwa asilimia mia moja lazima MOSSAD watakuwa na taarifa za Tajiri Khalifa na ndio maana aliona amtumie Makedoni.

Kutoka Tanzania mpaka Japani ni takribani maili 5973, na ndege zote za shirika la Qatar Airways zinatumia injini teknolojia mpya , spidi yake ni 567mph hivyo ili kufika Japani iatakulazimu kutumia takribani masaa kumi na mbili kama na nusu hivi , ukijumlisha na taratibu za uwanja wa ndege basi ni takribani masaa kumi na tatu.

Roma aliekuwa kwenye ndege alikuwa ashapiga mahesabu kabisa na aliona ajipumzishe kwenye siti yake , ukweli ni kwamba licha ya kwamba Edna ana baadhi ya madhaifu yake , lakini siti aliomkatia ilikuwa ni ya daraja la kwanza hivyo alikuwa akipata nafasi kubwa ya kupumzika kutokana na siti zilivyotegenezwa.

Ukitoka Tanzania kwenda Japani unapunguza muda , yaani Tanzania tuko mbele ya muda kwa masaa Zaidi ya matano na Japani Tokyo.

Wakati ndege ya shirika la Qatar Airways inaacha ardhi ya Tanzania ilikuwa ni saa tano kamili na Roma aliweza kufika Heneda Airport-Japani saa kumi na mbili za jioni, siku hio hio ya tarehe hio hio , tofauti ni kwamba wakati Roma anafika Tokyo , huku Tanzania ni saa tano usiku.

Heneda Airport ndio moja ya kiwanja pendwa sana ndani ya jiji hili kubwa la Tokyo ukiachana na kile kingine cha kimataifa cha Narita , moja ya sababu kubwa kwa ndege nyingi kutua ndani ya Heneda ni ukaribu wake na mjini Dowtown Tokyo.

Terminal namba tatu ndio inapokea wageni wa kimataifa ndani ya uwanja huu , na muda huu wa saa kumi na mbili Roma ambaye alikuwa ameshikilia kisimu chake kidogo alionekana akipitia taratibu zote ndani ya uwanja huu wa ndege kwa ajili ya kuingia mjini.

Baada ya taratibu zote kutoka alitembea huku akiangaza macho kulia na kushoto akifurahia uzuri wa jengo hilo , jengo ambalo lilikuwa likiashiria ukubwa wa nchi ya Japani kutokana na ukubwa wake na ugharama wake.

Watu mbalimbali walionekana kuingia na kutoka ndani ya jengo hili, Wazungu , Arabs na watu wa mataifa mengine , wote walionekana wakiingia na kutoka ndani ya hili jiji la pili kwa ukubwa Duniani.

Roma hakuwa na haraka sana kwani ilikuwa inakaribia saa moja na ndege ambayo inatoka Heneda kwenda New Chitose Airport-Hokkaido inatoka hapo saa mbili na nusu za usiku , hivyo kwa mahesabu ni kama alikuwa na masaa mawili mbele ya kusubiria.

Aliingia eneo la mapumziko(Lounge) huku akiwa na madhumuni kichwani ya kumtafuta Makedoni ili amwambie ni kipi amepata , hakutaka kwenda moja kwa moja ndani ya Hokkaido pasipo kufahamu ni nini kinaendelea.

“Makedoni umefanikiwa kupata taarifa gani?”Aliuliza Roma akiwa ameweka simu sikioni na ungeshangaa Roma anaweza kuwasiliana vipi wakati anayo laini za Tanzania , lakini ukweli ni kwamba Roma alikuwa akitumia laini maalimu ambayo ilikuwa na uwezo wa kuwasiliana ndani ya taifa lolote kwa kutumia mtandao wa International Mobile Services.

“Mfalme Pluto kwa taarifa za siri sana kutoka ndani ya familia ya Tajiri Khalifa ni kwamba kuna taratibu za ndoa ambazo zinafanyika kati ya mtoto wao mkubwa Dodi Fayez na Amina Kanani”Ilisikika sauti na kumfanya sasa Roma kuelewa kwanini alikuwa akipokea ujumbe wa kuombwa msaada , alijua lazima Amina alikuwa akilazimishwa kuolewa nje ya ridhaa yake.

“Makedoni ndoa hio inafungwa wapi?”

“Taarifa zinaonesha inafungiwa Ishikari Bay kwenye meli ya kifahari siku ya tarehe 21 mwezi huu wa kumi”Aliongea Makedoni na kumfanya Roma ahesabu na kugundua kuwa ndoa hio ina takribani siku nne mpaka tarehe yenyewe.

“Okey Makkedoni asante sana , nitakupigia simu kama kutakuwa na uhitaji”Aliongea Roma na kisha akakata simu..

“Ooh…. Sorry”Ilisikika sauti ya mwanamke kuomba msamaha sauti ambayo ilimshitua sana Roma kiasi cha kuangalia macho yake mbele, na katika harakati za kutafuta upande sauti hio ilipotokea ndio aligundua mbele yake kuna mwanaume ambaye aligongana na mwanamke mrembo maji ya kunde mrembo alievalia mavazi ya kitamaduni ya Japani.

Jambo ambalo lilimfanya Roma kushituka , kwanza ni sauti, halafu pili ni muonekano wa mwanamke aliekuwa mbele yake , ni kama alimuona mtu wa miaka mingi sana.

Mwanamke yule baada ya kuombwa msamaha na mwanaume wa kizungu ambaye amegongana nae alianza kupiga hatua kutoka eneo hili la ‘waiting lounge’ , lakini alivyofika mlangoni ni kama aligunguda kuna mtu anamwangalia kwa shauku , hivyo aligeuza shingo yake na kuangalia nyuma na hapo ndipo mshangao ulipo mpata Roma na kujihisi huenda ana ‘hallucinate’(kuchanganyikiwa kwa kuona sura za wafu)

“Seventeen….!!!”Aliita Roma kwa mshangao huku akinyanyuka na kwa upande wa yule mwanamke ni kama alikuwa akitaka sura yake ionekane vyema kwani baada nya kumwangalia Roma kwa sekunde kadhaa aliendelea kutembea kutoka eneo hilo haraka haraka.

Roma hakutaka kabisa kumpoteza huyo mwanamke kwani alikuwa akifanana kabisa na Seventeen , lakini pia alikuwa akifanana na Edna mke wake , utofauti wao ulionekana kuwa mdogo tu kwani mwanamke aliekuwa mbele yake sekunde kadhaa nyuma alikuwa akionekana kama wale wanawake ambao wameishi sana ndani ya bara la Asia na hata tembea yao kuathirika.

Roma alinyanyuka haraka haraka na kutoka eneo hilo la mapumziko na mita kama hamsini hivi alimuona yule mwanamke akipotelea kabisa nje ya jengo na kumfanya Roma akaze mwendo kumsogelea , na kwakua mwendo wake ulikuwa ni wa spidi aliweza kufika nje sehemu ambayo kuna maegesho ya magari ya Taksi na aliweza kumshuhudia yule mwanamke akigeuka nyuma na kumwangalia na kisha akaingia kwenye taksi na gari ikaondoshwa , Roma baada ya kuona mwanamke anaefanana na Seventeen kuondoka na gari ile na yeye pia alikimbilia taksina kutoa maelekezo ya kufukuziwwa gari iliotoka muda huo , na kwakua Roma aliongea kwa lugha ya kijapani , basi aliweza kueleweka na dereva aliandesha na kuanza kuitafuta gari hio

Ni kwa takribani dakika kumi na tano walikuwa washaiona gari ile na walikuwa wakiifatilia kwa nyuma na Roma aliridhishwa na uendeshaji wa dereva, barabara ilikuwa na magari mengi hivyo mpango wa Roma ni kuona gari hio inaenda kusimama wapi na yeye ashuke na amfuate yule mwanamke na kumuuliza kwaninia anafanana na Seventeen.

Wakati Roma akifikiria ile sura mara baadhi ya maeneno ya Zeo Kocav kule Ufaransa yalianza kuchipuka kwenye kichwa chake , lakini pia maneno ya Mellisa akiongea kwenye hoteli ya Kilimanjaro na yenyewe yalianza kuibuka kwenye kichwa chake na kuhisi huenda walichokuwa wakimwambia ni kweli.

Alijiambia kama ni kweli Seventeen alikuwa hai basi kosa la kwanza litakuwa lake kwa kutowaamini Mellisa pamoja na Zoe Kovac.

Ndani ya dakika kama ishirini tu baada ya kupita Kaneko hatimae gari ile ilikuja kukunja kushoto baada ya kuingia wilaya inayojulikana kama Yanaka , moja ya mitaa ambayo imetulia, na baada ya wao pia kukunja upande wa gari ile ilipoingia walikuja kuiona mbele imesimama mita kadhaa pembezeni mwa barabraba huku upande wa kulia kukiwa na nyumba ambayo imejengwa kama vile ni Temple , ulikuwa ni ujenzi wa staili ya zamani(Minka)

Baada ya gari ile kusimama mwanamke yule alitoka kwenye gari na kuingia ndani ya kigeti kidogo cha chuma ndani ya nyumba hio ambayo kwa nje imezungukwa na bustani kubwa ya maua.

Roma baada ya kuhakikisha mwanamke yule kaingia kwenye nyumba ile alimwamuru dereva kusimamisha gari na akalipa ujira wa dereva na kisha akaanza kupiga hatua kuelekea upande wa ile nyumba.

Roma alijaribu kufungua kile kigeti ambacho kilikuwa kama uzio na kuona kimefungwa kwa ndani, hakutaka kujisumbua kwani aliruka bustani na kwenda kutua ndani.

Kumbuka muda huu ulikuwa ni usiku na giza lishaanza kutanda maeneo yote na ni taa za umeme ndio zilimfanya kuona mazingira yote ya hapo ndani.

Upande wa ndani ya nyumba hio taa ilionekana kuwashwa mara baada ya Roma kuingia ndani ya eneo la nje na aliamini mwanamke ambaye ameingia hapo ndani ndio aliewasha hivyo akili yake ilimwambia kwamba asilimia mia moja mwanamke huyu atakuwa anaishi mwenyewe na jambo hili lilimpa uafadhali.

Ukweli ni kwamba licha ya kwamba Roma alikuwa akimfuatilia huyu mwanamke , hakuwa akiamini kabisa kama anaweza kuwa Seventeen , ni kweli kabisa mwanamke huyo alikuwa akifanana kwa asilimia mia moja na Seventeen kwanzia kila kitu lakini hakuamini kabisa kama ni yeye.

Jambo lingine ambalo lilimpa shauku ya kumfatilia huyo mwanamke ni kwamba kama ni kikundi cha Yamata Sect ambacho ndio kimeamua kutumia uchawi wao kuigiza kama Seventeen basi kuna uwezekano wa asilimia mia moja wa Seventeen kuwa hai, sababu ni kwamba moja ya uchawi wa kijapani ili uweze kufanikiwa, mathalani katika kuiga sura ya mtu ni lazima wakutane na huyo mtu mwenye hio sura.

Kwa maneno marahisi ni kwamba ‘Impersonation techinique’ itaweza kufanikiwa kwa kuwa na ukaribu na mtu ambaye sura yake inachukuliwa , huwezi ukaiga Sura ya Obama ilihali Obama yupo marekani , yaani ni lazima wasafriri wakutane na Obama ndio mbinu yao itakapoweza kufanyika , hivyo Roma aliamini uwezakano wa mambo mawili kutoka kwa huyo mwanamke , aliamini kama sio Seventeen halisi basi huyo feki atakuwa na ukaribu na Seventeen halisi, hivyo alijiambia wote wanaweza kumpatia majawabu anayo yataka aidha awe Seventeen Feki au halali atathibitisha atakapo kutana na huyo mwanamke.

Roma aligonga mlango kwa dakika kadhaa baada ya kuufikia na hatimae aliweza kusikia vishindo vya viatu vikisogelea mlango na mapigo yake ya moyo yalikuwa yakienda kasi mno , kuna hali flani alikuwa akihisi kabisa na kumwambia mwanamke yule anatoa ‘Aura; kama ya Seveenteen.

Ukumbuke Roma anauwezo wa nguvu za kiuchawi kutoka China na Japani kwa wakati mmoja , hivyo ilikuwa ni rahisi kwake kuweza kuhisi mtu kama ni hatari au ni wakawaida , hii hali ipo kwa viumbe vyote ambavyo vinatumia uwezo wa ziada , hata wachawi wanaweza kutambuana kutokana na uwezo wao , basi hata Roma aliweza kuhisi nguvu isio ya kawaida ikisogelea mlango.

“Thirteen..!!”Sauti ilimwita mara baada ya mlango kufunguliwa na kumfanya Roma kubun’gaa kwa muonekano wa mwanamke aliekuwa mbele yake , kila kitu kilichokuwa kwa mwanamke huyo kilikuwa kikimwambia kwa asilimia mia moja kwamba alikuwa ni Seventeen halisi.



SEHEMU YA 284

Kwa Upande wa mwanamke ambaye Roma anamuona kama Seventeen ni kama alikuwa akimtegemea kabisa Roma na ndio maana baada ya kufungua mlango , licha ya Roma kuonyesha hali ya mshangao yeye alimpa ishara ya kuingia ndani , yaani hakukuwa na maswali kama umekuja kufanya nini hapa na mengineyo, yaani ilikuwa ni kama mwanamke yule alikuwa akimfahamu Roma muda mrefu na haikuonyesha ishara yoyote kama walikuwa wamepotezana.

“Thirteen , kama huingii naomba uondoke”Aliongea yle mwanamke kwa liugha ya kingereza na Roma alimwangalia kwa sekunde kadhaa na pasipo kuongea neno , aliingia ndani na yule mwanamke akafunga mlango nyuma yake na kumtangulia Roma kwa mbele.

Nyumba ilionekana mbaya kwa nje lakini kwa ndani ilikuwa ni nzuri mno , katikati ya nyumba hii , sehemu ambayo Roma aliamini ni eneo la Sebuleni kulikuwa na boksi kubwa la kioo , boksi ambalo ndani yake kulikuwa ni kama kisiwa ambacho kimezungukwa na maji kila kona, katikati ya eneo hilo kwenye hilo boksi kulikuwa na miti mingi aina ya mikoko.

Ni mchoro wa kutengenezwa kabisa na kwa mtu yoyote ambaye anaweza kuona kwa jinsi kisiwa hiko kilivyotegenezwa ndani ya boksi hilo angeamini kwa asilimia mia moja eneo hilo hakuna mtu anaeishi , kwani hakukuonekana mitumbwi pembeni ya kisiwa hicho wala aina yoyote ya watu Zaidi ya Wanyama pamoja na ndege kama vile Tai zinazozunguka eneo hilo.

Roma alikagua mchoro huo kabla ya kuketi chini na kadiri alivyokuwa akiangalia jinsi mfano wa kisiwa hiko kilivyotengenezwa, kwake ni kama alikuwa akiona kitu halisi kabisa, yaani kwenye akili yake aliona mazingira ambayo yapo na ameyaishi , aliendelea kuchunguza mchoro huo kwa umakni na sasa anaweza kuona Watoto wawili ambao wapo katikati ya kisiwa hiko kwenye mikoko na wanaonekana kukimbia , walikuwa ni wa jinsia tofauti , mmoja akiwa mvulana na mwingine akiwa msichana na walionekana pia kuwa katika umri tofauti.

Dakika tano zote Roma aliweza kutumia kuangalia mchoro huo , huku yule mwanamke anaefanana na Seventeen akiwa pembeni yake, ni kama alikuwa akimuacha kwanza aone na kutafakari mwenyewe.

Roma baada ya kuridhika aligeukia upande wa kulia na kuona pia mchoro kama mchoro uliochorwa kwenye karatasi kama vile ni Ramani , ndani ya mchoro huo kunaonekana Watoto wengi ambao kwa haraka haraka aliona ni maiti za Watoto , huku kati ya maiti hizo Watoto wawili pekee ndio wanaonekana kuwa hai huku macho yao yote yakiangalia maiti za wenzao , jambo la kushangaza pia katika mchoro huo , Watoto hao wanaonekana kama vile wapo ndani ya pango , pango ambalo njia zote zimefungwa kwa milango wa chuma.

Yaani ni kama walikuwa wapo kwenye yale magereza ya kale(Dungeon) lakini sasa hili Gereza lilionekana kuwa kubwa ambalo lina uwezo wa kuingiza watu wengi kwa wakati mmoja.

Sasa Roma baada ya kuona picha hii ni kama ilimletea hisia mabazo ziliamza kumfanya kukumbuka Maisha yake ambayo ni kama aliyafuta kwenye kumbukumbu zake, kwa jinsi picha hio ilivyokuwa ikionekana katika macho yake , lilionekana hilo ni moja ya tukio la kutisha katika Maisha yake yote , haikueleweka pia kwanini mwanamke ambaye alikuwa na mwonekano kama wa Seventeen kuwa na picha kama hizo hapo ndani na Roma hakuelewa nini kinachoendelea kwa wakati huo.

“Sit Down , I`ll make you tea..”Alionge yule mwanamke baada ya kugnudua Roma anashangaa sana ,na kauli yake ni kama ilimfanya Roma kutoka kwenye mawazo na sasa kuanza kumwangalia mwanamke aliekuwa mbele yake.

“I didn’t expect my Seventeen to know haow to make tea other than killing”Aliongea Roma kwa kingereza akimaanisha kwamba hakudhania kama Seventeen wake anajua kutengeneza chai , tofauti na kuua.

“After being in Japan for more than a year , I forgot how to kill but learned how to make tea , Also I am not your Seventeen”Aliongea yule mwanamke na sauti na kila kitu kwa upande wa Roma ni kama Seventeen mwenyewe.

“Tabia yako haijabalika hata kidogo , najua unaweza kunilaumu na kunichukia sasa hivi lakini sikulaumu juu ya hilo , yote uliopitia yalikuwa ni kwasababu yangu, nilifikiria ushaniacha milele na sikuwahi kudhania kama ninaweza kukuta sehemu kama hii”Aliongea Roma.

“Sikuweza kudhania kama ninao uwezo wa kuepuka ile hali , na pia sikudhania kama nitaweza kuonana na wewe kwa mara nyingine”Aliongea huku akiendeleakutengeneza chai upande wa kushoto na alipokaa Roma, na hii ni kawaida sana, kwa tamaduni za kiasia mara nyingi unakuta kuna mashine kabisa za kutengenezea chai eneo la Sebuleni.

“Kwanini baada ya kuniona ulianza kunikimbia na kuonesha hali ya kutotaka kuonana na mimi?”Aliuliza Roma kwa Kingereza.

“Kama nilivyokwisha kusema , sikuwa na mpango wa kikuona hapa Japani na pia sijawahi kupanga kuonana na wewe”Aliongea na kisha alimuwekea Roma kikombe cha chai na yeye akaketi kwenye sofa.

Yaani huyu mwanamke alikuwa akifanana kabisa na Edna na kilichowafanya pia kuonesha utofauti wao ni unene Edna alikuwa mnene na huyu alikuwa mwembaba , Edna alikuwa na nywele ndefu na huyu alikuwa na nwele fupi , huo ndio utofauti wao.

“Vipi kuhusu sasa, nipo hapa”Aliongea Roma huku akiangalia picha ya kuchorwa iliotundikwa ukutani picha ambayo ilikuwa ikionyesha akiwa na Seventeen kwenye kisiwa huku wakikoka moto na mbele yao zilionekana aina ya samaki za kubanika na hata kwa mwanamke aliekuwa mbele yake ambaye alikuwa akifanana kwa asilimia mia moja na Seventeen katika macho yake alikuwa akiangalia picha hizo.

“Kunywa kwanza hio chai inapoa”Aliongea Seventeen na Roma aliangalia hio chai kwa muda kabla ya kuinywa.

“Nipe jibu langu kwanza”

“Nafikiri sikutakiwa kukimbia mar azote ambazo nilikuona , nilipaswa kukutafuta bara baada tu ya kupona kwenye lile janga”Aliongea na kumfanya Roma amwangalie mwanamke huyu kwa namna ya kumchunguza kwa kila kitu, ni kama alikuwa akitafuta dosari lakini bado hakuweza kumtofautisha mwanamke huyu na Seventeen anaemjua, lakini kubwa Zaidi kuhusu mwanamke huyu alionyesha kuwa na kumbukumbu za Maisha yao ya utotoni , kwa mfano picha ambazo amechora hapo ndani , lakini namna alivyotegeneza kisiwa feki na kuonyesha Maisha yao ndani ya kisiwa hiko , kila kitu kilionekana kilekile na Roma katika kumbukumbu zake alikuwa akimkumbuka Seventeen kama moja ya wanawake ambao walikuwa wakipenda kuchora sana , kwahio kwake haikuwa ajabu kwa picha hizo kuwa hapo ndani, na kama alivyokuwa akielewa mwanzo kwamba, kama mwanamke aliekuwa mbele yake alikuwa feki basi ni lazima kuna Seventeen orijino , lakini hata hivyo anakosa namna ya kumtofautisha huyo mwanamke na Seventeen halisi.

“The Tea is getting Cold , Drink it first”Aliongea

Seventeen na Roma aliangalia kikombe cha chai kilichokuwa mbele yake kwa dakika kadhaa na pasipo ya kujishaui mara mbili , alikibeba kwenye mikono yake na kisha akashusha kimiminika chote tumboni kwake , kwanza alikuwa akihisi njaa maana ni muda mrefu tokea aanze safari hajapata chakula, na hata aliposhuka kwenye ndege ndio alianza safari ya kumfatilia mwanamke aliekuwa mbele yake.

“Unatakiwa kunywa taratibu taratibu na sio kunywa yote kwa wakati mmoja kama maji”Aliongea.

“Sipo kwenye mudi ya kunywa taratibu taratibu..”Aliongea na kisha akavuta pumzi nyingi.

“Kwakua bado unaishi , vipi kuhusu mtoto wetu?”Aliuliza Roma.

“Now you think about the child , back then why didn’t you give the child any thought?”

“Naona sasa ndio unakumbuka kuhusu mtoto , kwanini kipindi kile hukuwa na mawazo yoyote kuhusu mtoto”Aliuliza Seventeen huku akianza kubalilika na sura yake kuanza kuonyesha kwamba alikuwa na hasira.

“My brain was akin to glue at that time , I couldn’t control myself…”Aliongea Roma akimaanisha kwamba akili yake ilikuwa ni kama gundi wakati ule na alishindwa kujidhibiti.

“Mh! Eti ulishindwa kujizuia , hivi ulishawahi kuwaza hata namna ya kujizuia kipindi kile , nilimuonea huruma mtoto wangu kuzaliwa na kukuta baba yake alikuwa na tabia za kishenzi vile , na kwasababu yako ndio maana mtoto aliondoka kwenye huu ulimwengu kabla ya kuzaliwa”Aliongea na kumfanya Roma kushikwa na mshituko.

“Le..! ,Left how!!”

“Do you think I will be completely unharmed when I fell into the ocean after the explosion without dying ?”

“Unafikri nisingeweza kupata madhara baada ya kudondoka kwenye bahari baada ya mlipuko ule”Aliongea na kumfanya Roma akili yake kuanza kukumbuka mambo yaliopita na alianza kupata maumivu ya kichwa ambayo yaliambatana na Maisha yaliowatokea nyuma yeye na Seventeen.
 
SEHEMU YA 285

Ni muda wa mchana juu ya bahari , inaonekana meli kubwa ya kivita ikiambaa ambaa kwenye ‘International water”, upepo na mawimbi ndio kitu pekee kilichoweza kusikika Zaidi kuliko injini zilizokuwa zikiendesha meli hio

Juu kabisa ya meli wanaonekana wanajeshi takribani ishirini hivi wenye vyeo tofauti tofauti huku wakiwa wamesimama kwa namna ya wasiwasi sana wakimwangalia mwanaume kijana aliesimama mbele yao.

Kwa jinsi walivyokuwa wakionekana ni kama wanajeshi ambao wamekamatwa na adui na sasa walikuwa wakisubiria adhabu ya kifo.

Kijana aliekuwa mbele yao aliwaangalia kwa kuwakagua mmoja mmoja kwa macho ambayo yalikuwa hayaonyeshi kuwa na hasira au furaha , yaani alikuwa akionekana kama mtu ambaye akili yake ipo lakini haipo ndani ya hilo eneo , alikagua kila mmoja kwa rangi zao tofauti , aliangalia waafrika walikuwepo , alikagua wazungu waliokuwepo na akakagua waarabu waliokuwepo , wote waliovalia nguo za jeshi zinazofanana.

“Since you guys took the money from someone else to deal with my people you should have expected this to happen , so stop giving me the look , I will give you all the chance to kill me too”

“Kwasababu nyie watu mmelipwa pesa ili kuja kudili na watu wangu , mlipaswa kutegemea hili kutokea , achene kuniangalia kwa macho yenu , Nitawapa nafasi ya kuniua na mimi pia”Aliongea, na kwa jinsi alivyoongea ni Dhahiri kabisa kwamba watu waliokuwa mbele yake walikuwa wamemchokoza kwa kuua baadhi ya watu wake na alikuwa juu ya meli hio kwa ajili ya kulipiza kisasi , lakini pia haikuwa hivyo tu ilionekana ndani ya meli hio kulikuwa na mateka wengine ambao wote hao walikuwa ni baadhi ya watu wake na alitaka awaokoke , lakini aikuwa akitaka kuwapa nafasi wanajeshi hao wachokozi wajaribu kumuua na yeye pia.

“Ni baadhi ya wanajeshi wachache sana kutoka kikosi chetu ambao wamehusika na kuuwa watu wako , lakini kwanini mpango wako ni kuua watu wote waliopo kwenye hii meli , lakini sio hivyo tu umeua pia familia zetu makao makuu”Aliongea moja ya mwanajeshi ambaye alikuwa na cheo cha Kanali , alikuwa ni mtu mzima kama miaka hamsini hivi.

“Huna chochote wewe kitu pekee kinachokusumbua ni kiu yako ya kutaka kuua watu kwa sababu zako za kipumbavu , wewe ni muyama na hupaswi kuwa katikati ya binadamu”Aliongea jamaa mmoja kwa lugha ya kijerumani akimnanga kijana aliekuwa mbele yao , alionekana kujiamini mno licha ya kumuogopa mtoa hukumu.

“Tunajua kwamba ni kweli unauwezo usio kuwa wa kawaida , lakini kitendo chako cha kuuwa watu bila hatia ni ushetani na naapa kwa kifo changu mbele ya maji haya , yote unayoyafanya sasa hivi yatakurudia”Aliongea kwa hasira na kabla hajasubiria jibu alijirusha baharini bila ya kusubiri adhabu yake na kufanya wenzake kuanza kupatwa na hofu Zaidi.

“Nilichosema kwenu ni kutumia mikono yenu kuniua na sio kunitamkia maneno ya laana”Aliongea kwa sauti na palepale alipotea alipo kuwa amesimama na kila anapoibuka yupo mbele ya mwanajeshi na ni damu pekee ambazo zilikuwa zikiruka hewani huku wanajeshi wale wakitenganishwa vichwa vyao kwa upanga, na zoezi lake lilichukua dakika mbili tu alikamilisha kila kitu , damu zilisambaa kwenye maji yote ya karibu na kufanya hata rangi yake kubadilika na kuwa nyekundu , kilikuwa ni kitendo cha kikatili mno ambacho kijana huyo alikuwa akikifanya na hakujali , alichokifanya ni kuinama na kuchukua kichwa cha mwanaume ambaye alimjua kama Jenerali wa jeshi hilo na kisha alitumia mkono wake na kupasua jicho lililokuwa likimwangalia kwa namna ya kumlaani kwa kumchinja na kisha akakitupa baharini.

Baada ya kuona karidhika na kazi yake ya chinja chinja alitoa kitambaa kilichokuwa kwenye mfuko wake wa suruali yake na kisha akajifuta damu zilizomchafua usoni na akamalizia na upanga wake na ile anatupa kitambaa kile chini , mlango wa meli hio ya kivita ulifunguliwa na anaonekana mwanamke mwenye tumbo kubwa akitoka , alikuwa ni mwanamke mrembo sana , lakini urembo wake ulififia kutokana na wasiwasi na mshangao aliokuwa nao , alimwangalia mwanaume kijana aliekuwa mbele yake na kisha macho yake akayahamishia kwenye miili na vichwa vya watu vilivyokuwa vimesambaa juu ya meli hio ya kivita na kujikuta akiziba mdomo na kuanza kutoa machozi , lakini licha ya hivyo mwanaume aliekuwa mbele yake hakumuhurumia hata kidogo wala kiguswa na machozi yake , yeye alikuwa akiangalia upanga wake na kuukinga na jua upande wa makali yake na kujikuta akitabasamu , ni kama moyo wake umeridhika sana kwa kitendo alichokuwa amekifanuya.

“Thirteen don’t kill anymore , haven’t you killed enough people ?”Aliongea akimaanisha kwamba Thirteen hupaswi kuua tena , kwani watu uliowaua hawakutoshi?.Aliongea kwa kuweweseka.

“My Dear Seventeen its not that I haven’t killed enough of them , there seems to be peaple constantly looking to die”

“Kipenzi changu Seventeen sio kwamba sijaua watu wa kutosha bali kuna watu ambao muda wote wanakitafuta kifo”Aliongea pasipo ya kujali.

“Miaka minne nyuma baada ya kuua wanajeshi wote wa Zero na kuharibu kambi yao , uliniahidi mwenyewe kama hautokuwa mkatili tena na kuuwa watu bila sababu , lakini kwanini .. kwanini kila mtu unaona anastahili kifo , hawa watu hawajakuchokoza na ni baadhi yao tu , kwanini ukaua familia zao zote na wao pia ?”Aliongea huku akianza kulia kwa kwikwi , alikuwa mrembo sana kiasi kwamba hata kulia kwake kulikuwa kukikipendeza lakini kijana aliefahamika kwa jina la Thirteen alionekana kutojali kabisa , kwanza hakujali ahadi yake aliowekeana na mrembo aliekuwa mbele yake, pili hakujali hisia zake wakati anapofanya mauaji”

“Seventeen unakumbuka mara ya mwisho nilikuuliza kwanini unapanda kuvaa mavazi ya rangi ya bluu mara zote na ulivyonijibu?”Aliouliza Thirteen lakini Seventeen hakumjibu Zaidi ya kuendelea kulia.

“You told me that when you were dressed in a blue clean looking shirt, you1`d feel a sense of achievement when blood got on your shirt”

“Uliniambia mwenyewe kwamba unapenda kuvaa vazi la bluu safi ili pale damu ya mtu inapokurukia kwenye nguo zako safi basi utajisikia mtu uliekamilisha jambo kubwa”

“Hayo mambo niliongea zamani , sasa hivi sitamani kabisa kuua binadamu mwenzangu napenda kuishi Maisha ya amani”Alionea Seventeen ambaye tumbo lake la ujauzito lilionekana wazi.

“Kama wewe unajihisi hupendi kuua kama zamani haimaanishi mimi sipendi, Seventeen najisikia vizuri sana pale matone ya damu ya moto yanaponirukia usoni mwangu, hizi hisia hazielezeki kabisa, kuchukua Maisha ya binadamu kwa mkono wangu huu ni kitu pekee ambacho hapa duniani kinanifanya nijihisi nimetimiza kusudi maalumu”

“You are the woman I trust the most also the woman I like the most , I’ll get really angry if you oppose me from killing , so I don’t allow you to try to stop me again”

“Wewe ndio mwanamke ninae kuamini sana na ndio mwanamke ambaye nakupenda kuliko , nitapatwa na ghadhabu kuu sana kama tu utanizuia mimi kuua , hivyo naomba usije ukajaribu tena kunizuia kufanya kitu ninachokipenda”Aliongea Thirteen na pasipo hata ya kusubiria jibu alitembea na kumpita Seventeen ambaye alikuwa akibubujikwa na machozi na kuingia ndani ya meli hio ya kivita. Alionekana sio mwenye kujali kabisa hisia za mwanamke huyo mjamzito na alikasirishwa na namna ambavyo anamzuia kuua.

………..

Ni siku nyingine juu ya meli hio hio ya kivita ndani ya chumba chenye kitanda kikubwa anaonekana Thirteen akijiinua kivivu na kilichomfanya kuamka ni njaa aliokuwa nayo , lakini pia alikuwa na ‘Hangover’ ya hatari kwani jana yake mara baada ya kumuacha Seventeen nje hakuongea nae tena na alishindia kunywa bia nyingi alizokutana ndani ya meli hio ya kivita ambayo hata haikuwa ya kwake.

Sasa baada ya kujiinua kivivu huku macho yake yakiwa bado na hali ya ukungu unaotokana na usingizi alijikuta akihisi kitu kigumu pembeni yake , aligeuza mkono wake na kushika kile kitu kigumu na kugundua ni karatasi mfano wa kama gazeti gumu kama yale ya kutegenezea kalenda , alilichukua kipande kile cha karatasi na kisha akakiweka mbele yake ili kuona kwanini kipo juu ya kitanda , baada ya kuangalia mbele yake alijikuta macho yake yakianza kuongezeka ukubwa , kwani karatasi hio ilionekana kuwa na maandishi ambayo yalimshitua mno.

“Thirteen mimi naondoka ,siwezi kuendea kuishi na wewe na kumfanya mwanangu alietumboni kuzaliwa juu ya damu zinazomwagwa kwa mikono yako , umesema huna mpango wa kuacha roho yako ya kikatili , roho ya kimauaji na mimi pia siwezi kuishi na muuaji , nitaenda kusihi mbali na wewe mpaka siku ambayo mtoto wangu atakapo zaliwa na kufahamu baba yake amebadilika. Kwa heri Thirteen”Hayo ndio maandishi yaliokuwepo kwenye barua hio na kumfanya Thirteen kukunja kunja karatasi hio kwa hasira kali mno , hakuamini karatasi hio likuwa na ujumbe wa Seventeen ambao ulikuwa ukimpa maneno ya mwisho ya kwaheri.

******

Masaa kadhaa mbele baada ya Thirteen kusoma barua ilioachwa na Seventeen na kumfanya kuomboleza kwa kuondoka kwake , kwenye kilele kimoja juu ya mwamba pembezoni mwa bahari ya Pasific wanaonekana watu baadhi wakionekana kuvuja damu nyingi mno huku wakiangalia maji yaliokuwa chini yao juu ya mwamba mkubwa waliokalia , sehemu ambayo kama ukidodonka tu basi moja kwa moja unakwenda kuzama kwenye kina kirefu cha bahari.

Watu hao ambao walikuwa wakihisi maumivu ya kuchanwa na kisu mwilini mwao walikuwa wakilazimishwa kujirusha juu ya mwamba huo kwenda chini baharini, na kwakua mtu aliekuwa akiwalazimisha alikuwa akigopesha hakuna mtu ambaye alikuwa na ujasiri wa kujiuliza mara mbilimbili , kila mmoja alijirusha chini ya mwamba huo uliokuwa juu mlimani kila ilipofikia zamu yake.

Thirteen aliekuwa na macho yaliokuwa yamebadilika rangi na kuwa ya kijani, hakuonyesha hali ya kuridhishwa na vifo vya watu ambao wamejirusha na sasa walikuwa wamebakia watu wawili ambao walionekana kuwa ndio viongozi katika kundi hilo la watu ambao amejeruhi kwa mapanga.

“Sijali sana nyie watu mnatokea kwenye kundi lipi la kigaidi , wala nguvu za giza mnazotumia , lakini mmefanya kosa kubwa sana kumteka mwanamke wangu”

“Thirteen even you kill all of us your woman and the child in her belly will be buried with us ,So what if we can’t defeat you even when we cooperate?,once we die while you are still alive you will suffer more than dying”

Ukweli ni kwamba kilichomfanya Thirteen kukamata watu hao ni kutokana na uepepelezi wake ambao ulimpa majibu kwamba baada ya Seventeen kumkimbia kwenye meli hio ya kivita , alitekwa akiwa kwenye meli ndogo na majambazi hao wa baharini (pirates) , sasa alichokuwa akitaka kwa hao watu ni kumueleza ni upande gani Seventeen walikuwa wamemficha , lakini hawakuwa tayari kuongea, ndio maana alianza kuua mmoja mmoja baada ya mbinu zake zote za mateso kukwama.

Wakati akiendelea kuongea na watu wawili wa mwisho ambao walimpandisha hasira za kutamani kuwaua muda huo huo mara mita kadhaa kutoka alipo aliweza kumuona mwanamke akiongea na simu ya upepo na ilionekana mwanamke yule alikuwa akifanya makusudi ili Thirteen aweze kuona na kusikia kwa wakati mmoja.

“Mission failed , initiate Explosion”Aliongea yule mwanamke ndani ya fukwe hii na palepale upande wa pili juu ya mwamba alionekana Seventeen akijirusha majini na wakati huo huo ulionekana mlipuko mkubwa eneo lilelile ambalo amejirusha na kufanya mawimbi ya maji kuongezeka kwa kiasi kikubwa , Thirteen alijikuta akitoa macho mara baada ya kushuhudia Seventeen akijirusha majini na sehemu ile kulipuka.

“Thirteen although our alliance failed to kill you this time, letting you go through the pain of losing the woman and child you love can be considered our victory”

“Thirteen ijapokuwa tumeshindwa kukufanya mtu wetu lakini kukuacha kuendelea kuishi ukiwa na maumivu kwetu ni ushindi pia”Aliongea mwanaume mmoja na pasipo kuruhusu Thirteeen kuwaua , walijirusha kwenye mwamba na kuambaa ambaa kwenda chini ya maji , huku Thirteen akiwa haamini macho yake kama Seventeen aliekuwa mjamzito ndio basi tena.

“Seventeen…. noooo…..!!!”Alijikuta akitoa kilio cha maumivu makali mno , hakuamini mwanamke ambaye alikuwa akimpenda kwa moyo wake wote ndio huyo ambaye amelipuliwa na bomu na kutumbukia kwenye maji

****

Roma alirudi kutoka kwenye kumbukumbu zake ambazo zilimkumbusha mbali sana na kujikuta moyo ukimuuma na kumwangalia mwanamke ambaye yuko mbele yake.

“Yalikuwa makosa yangu kukuacha kupitia maumivu makali kipindi kile , kutotaka kwako kuniona tena ijapokuwa ulikuwa unaishi na pia kupelekea mtoto wetu kufa , hayakuwa makosa yako , lakini hata hivyo nashukuru sana nimekuona ukiwa hai kwa mara nyingine”Aliongea Roma huku akinyanyuka kivivu.

“Thirteen naomba uondoke nyumbani kwangu , siku ya leo itakuwa mara ya mwisho ya mimi kuonana na wewe tena”Aliongea yule mwanamke hulu hasira zikionekana katika macho yake.

“Seventeen ijapokuwa najua nimesababisha yote yale , lakini baada ya tukio lile la ule mlipuko na namna ulivyomezwa na baada ya kudondokea baharini, nilijikuta nikifahamu mambo mengi sana , mambo ambayo yalinifanya nikabadilika kimtazamo kwa asilimia mia moja , niliomboleza kifo chako kwa muda mrefu na niliishi kwa majuto , na baada ya kuona siwezi kupona maumivu ambayo yalisababishwa na kifo chako nilifanya maamuzi ya kurudi nchini Tanzania ambako nilihisi ndio nilipozaliwa na nilivyoweza kukutana na mwanamke ambaye anafanana kama wewe kwa kila kitu , nilihisi ni Mungu pekee ndio aliemleta kwangu kama mbadilishano , lakini mwisho wa siku nilikuja kugundua mwanamke yule licha ya kwamaba mnafanana lakini nafasi zenu kwenye Maisha yangu ni tofauti kabisa , wewe ni kama wewe na yeye ni kama yeye , Seventeen niamini mimi nafasi yako kwenye Maisha yangu haiwezi kufutika

Roma baada ya kuongea risala zake alianza kugeuka na kupiga hatua kuondoka ndani ya nyumba hio , hakutaka kuongea na Seventeen tena.

“Thirteen”Aliita Seventeen na kumfanya Roma kugeuka na kumwangalia na pale ndipo aliposhuhudia machozi kutoka kwa mwanamke aliekuwa mbele yake na mwanamke yule pasipo ya kujiuliza alimkimbilia na kisha akamkumbatia.

“Naomba usiniache tena tafadhari”Aliongea yule mwanamke huku akimkiumbaita Roma na kumfanya kuhisi joto la mwanamke huyo lakini pia pumzi ilitoka katika pua za mrembo huyo mwenye kufanana kwa asilimia mia moja na Seventeen.,

Lakini sasa wakati Roma akijisikia faraja kukumbatiwa na mwanamke anaempenda , mwanamke anaenda kwa jina la Seventen , mara alijikuta akigundua kitu ambacho sio cha kawaida na hio ni mara baada tu ya mwanamke yule kutoka kwenye mwili wake.

Roma aliekuwa amesimama alishitukia kuna Kisu aina ya Dagger kikiwa kimetumbukizwa kwenye moyo wake , huku mwanamke ambaye alikuwa akiuonekana kwa asilimia mia moja kufanana na Seventeen akimwangalia kwa macho ya dharau ni kama vile alikuwa akimdhihaki.

Ni kwamba Roma alishindwa kuelewa ni muda gani ambao amechomwa na kisu hiko kwani mwanzoni hakuhisi aina yoyote yale ya maumivu , lakini baada ya mwanamke yule kuacha kumkumbatia ndio alihisi maumivu makali kutoka kwenye moyo wake na alianza kukosa nguvu na macho kuanza kujaa ukungu na sekunde sitini zilikuwa nyingi sana kwa Roma kwani damu zililoanisha shati lake na palepale akadondoka chini na kufumba macho na haikueleweka kama amekufa ama amefumba macho , ila kwa jinsi kisu kile kilivyozama eneo la moyoni ni dhahiri kabisa kuna uwezekano mdogo wa kuwa hai.

“Hahahahah….. hahahaha….”Alianza kucheka yule mwanamke kwa namna ya dharau kubwa na palepale sura yake ilibadilika na akaonekana kuwa mwanamke wa kijapani , mwanamke ambaye sasa alionekana kuwa ni mmoja ya wanawake kutoka kwenye kundi la Yamata Sect kutokana na aina ya mavazi yake.

“Hii mbinu aliopendekeza Chief sikuamini inaweza kuwa nzuri namna hii , Hades ulieaminika huwezi kufa hatimae leo nimeweza kutekeleza kifo chako , hahahaha….”Aliongea kwa furaha sana huku akijiona kama moja ya watu ambao wametekeleza jambo kubwa kwenye Maisha yake.

ITAENDELEA

ITAENDELEA SIKU YOYOTE , NICHEKI WATSAPP KAMA UMECHOKA KUSUBIRIA 0687151346
 
Hatariii
 
Nukta hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…