Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 439.

Rufi aliwahi kuamka mara tu baada ya kufikishwa hospitalini na kupokelewa na madaktari , ilionekana hakuumia sana zaidi yakupata michubuko kidogo tu jambo ambalo hata Edna lilimshangaza kidogo na kushukuru kwa wakati mmoja.

Baada ya nusu saa ya Edna na Innocent kusubiri nje ya chumba cha wagonjwa wa dharula hatimae waliruhusiwa kuonana na mgonjwa wao ambaye tayari alishazinduka.

Edna baada ya kumuona mgonjwa wake alishangazwa na mwonekano wake , kwanza alikuwa mzuri lakini kitu cha pili alionekana kuwa na rangi mchanganyiko ambayo ilimfanya amuone kama ni Yezi , utofauti pekee kati ya Yezi na mgonjwa wake ni kwenye macho , mwanadada aliekuwa mbele yake alikuwa na macho kidogo ambayo kwa haraka haraka aligundua alikuwa ni mchina.



Edna alimsalimia mgonjwa kwa kuanza na lugha ya kiswalihi na ndipo alipogundua hakuwa akijua lugha ya kiswahili kabisa na ilibidi atumie lugha ya kingereza na hapo ndipo alipomfahamu kwa jina la Rufi Wangsi.

Jambo la kwanza ambalo Edna alitaka kulifahamu kutoka kwa Rufi mara baada ya kuomba msamaha ya kumgonga na gari ilikuwa ni kutaka kujua ndugu zake hapa Tanzania ili waweze kutaarifiwa kufika kumuona lakini jibu ambalo Ruffi alitoa lilimfanya Edna kushangaa.

Kwanza kabisa Rufi alisema hakuwa na wazazi kwani baba yake alikwisha kumtelekeza lakini pia mama yake hakuwa akimfahamu na hata ujio wake hapo Tanzania ilikuwa ni kujaribu kuangalia fursa zinazopatikana aweze kujiendeleza kimaisha.

Maneno ya Rufi yalimshangaza Edna lakini kwa wakati mmoja aliweza kuyaamini kwani Rufi alionekana kabisa hakuwa akidanganya . lakini ukweli ni kwamba Rufi alikuwa akidanganya kwnai ujio wake ndani ya Tanzania sio kwa ajili ya kutafuta maisha bali ni kwa ajili ya kumtafuta mwanaume anaefahamika kwa jina la Roma , mwanaume aliekutana nae ndani ya jiji la Los Angeles.

Haikueleweka mara moja kama Rufi alitokea kumpenda Roma au alikuwa na shauku ya kumjua zaidi kutokana na kuweza kumponyesha sumu iliokuwpo kwenye mwili wake miaka na miaka lakini uhakika ni kwamba Rufi alikuwa akimjua vizuri tu Edna kama mke wa Roma na huenda hata kugongwa na gari ilikuwa sehemu ya mipango yake.

Sasa wakati Roma anafika ndani ya hospitali hio upande wa Innocent alikuwa ashaondoka kwa kupewa maelekezo mengine na Edna , hivyo Edna kutokanna na kuguswa na stori ya Rufi ndipo alipoweza kuwasiliana na Roma na kumwambia kile kilichotokea lakini kubwa zaidi ni kama Edna alitaka na Roma aweze kusikia stori ya Rufi jambo ambalo Rufi alifurahi mno.

Edna alikuwa ni moja ya wanawake wanaoguswa kirahisi na matatizo ya watu hivyo kwa mwonekano wa Rufi kuweza kufanana na wa Yezi , lakini pia udogo wa umri wa Rufi vilimfanya kumuonea huruma , hakujua kwanini Rufi aliamua kuja Tanzania na sio kwenda kwenye mataifa yalioendelea kwa ajili ya kutafuta maisha.

“Kwanini ukaamua kuja Tanzania kutafuta maisha na sio nchi nyingine ambazo zina fursa nyingi?”Aliuliza Edna mara baada ya Rufi kumaliza kuelezea kwa ufupi stori yake ya uongo na kweli.

“Nimechagua kuja Tanzania kwasababu pia naamini ninaweza kumpata mama yangu”Aliongea Rufi na kumshangaza Edna.

“Mama yako ni Mtanzania?”Aliuliza Edna ijapokuwa Rufi alikuwa na rangi mbili ya kiafrika na ya Kiasia lakini hakuweza kudhania Rufi mzazi wake upande wa mama angeweza kuwa mtanzania.

“Ninachofahmu mama ni mtu wa Afrika mashariki , kwa maelezo ya baba mama alinitelekeza mara baada ya kutimiza mwaka mmoja”Aliongea Rufi na kuendelea kumshangaza Edna lakini ndio muda ambao Roma aliweza kufika ndani ya wodi hio.

Roma mara baada ya kuingia hakuamini mwanamke aliekuwa akiongea na mke wake ni Rufi maswali kibao yalimjia , kwanza kabisa mwanamke huyo alianza na kudukua kampuni yake katika mitambo ya kurushia matangazo lakini swala la pili mwanamke huyo huyo ndio majeruhi aliegongwa na gari mke wake , mpangilio wa matukio hayo ulimchanganya kiasi cha kumfanya aanze kuona haiwezekani kuwa bahati mbaya , huenda yote ilikuwa mipango ya Rufi.

Roma mara baada ya kuambiwa na Eda aingie ndani asisimame mlangoni kama sanamu alijikuta akijongea huku macho yake yote yaikuwa kwa Rufi , alikuwa na wasiwasi ni kitu gani ambacho Rufi alikuwa akiongea na Edna lakini kwa muonekano wa Edna aliamini kabisa Rufi hakugusia swala la wao kukutana nchini Marekani.

“Rufi huyu ni mume wangu anaitwa Roma…., Roma huyu ndio muhusika ambaye nimekuambia tumemgonga maeneo ya Kivukoni lakini kwa bahati nzuri hakuumia sana zaidi ya kupata michubuko na kutegua mguu(Soft tissue injury)”Aliongea Edna.

Upande wa Rufi aliishia kumwangalia Roma kwa macho ya kawaida akijifanyisha kama ndio kwanza wanaonana lakini moyoni alijiona mshindi maana kwa macho ya Roma yalivyokuwa yakimwangalia kwa wasiwasi aliona kabisa atakuwa ashapata kujua yeye ndio mdukuzi.

“Pole sana Rufi”

“Asante sana Mr Roma nimefurahi umekuja kuniona”Aliongea Rufi kwa Kingereza.

“Nisingeshindwa kuja hapa wakati mke wangu kipenzi yupo kwenye shida , hivyo usijali sana ujio wangu”Aliongea Roma na kumfanya Edna amuangalie Roma na kujiuliza kwanini anaongea kauli kama hio , lakini upande wa Rufi aling’ata meno kwa hasira, alijua kauli ya Roma kwake ni kama tahadhari ya kwamba asifanye chochote cha kijinga , alikuwa na akili hivyo kwake ilikuwa rahisi sana kuelewa kauli zenye zaidi ya maana.

Edna ilibidi amuelezee Roma simulii fupi ya maisha ya Rufi kwanini alikuwa Tanzania, hivyo haraka haraka alimwambia kwamba Rufi hakuwa na ndugu hapa Tanzania , pili alikuwa hapo kwa ajili ya kutafuta maisha pamoja na kumtafuta mzazi wake.

Kila alichosema Edna kilimshangaza Roma , kwanza kabisa alishindwa kuelewa kama maneno hayo ni ya kweli , kwani hata mara ya kwanza kukutana na Rufi ilikuwa ni kwasababu mrembo huyo alitaka kumtapeli hivyo haraka haraka Roma aliona kabisa na mke wake kadanganywa , lakini kwasababau hakutaka dhambi alioifanya Marekani ifahamike aliona atulie tu na asubiri muda muafaka aweze kumuonya Rufi kutomfatilia.

“Kwahio Wife unapanga kufanya nini juu ya mgonjwa?”

“Atakua chini ya uangalizi wangu mpaka atakapo pona kabisa na kuendelea na shughuli zake , nitakuwa mkatili nikumuacha msichana kama huyu akiishi bila msaada wowote”

“Unataka kumsaidia kivipi , mimi nashauri tumpe pesa kiasi itakayomsaidia kwenye mambo yake ya kimatibabu , kuhusu mzazi wake sio jukumu letu”Aliongea Roma kwa kingereza.

“Miss naomba tafadhali usinitelekeze… sina msaada wowote wa mtu ninae mjua hapa Tanzania , nataka kumtafuta mzazi wangu lakini sijui pa kuanzia..”Aliongea Rufi huku akianza kutoa machozi na kumfanya Roma akasirishwe na maigizo yake.

Kitendo cha Rufi kutoa machozi mbele yake kilimhuzunisha Edna , alijua msichana mdogo kama huyo alikuwa akipitia wakati mgumu.

“Huna haja ya kutoa machozi Rufi sawa nitakusaidia kwa kila hatua , ijapokuwa itakuwa ngumu kumpata mzazi wako kutokana na humjui hata kwa sura wala sehemu anayoishi , lakini Mungu siku zote ni mkubwa na kwa wakati wake utampata mama yako”Aliongea Edna huku akimpeti peti Rufi kwa kuzishika nywele zake ndefu na kumfanya Roma aone kazi anayo , mke wake kaingia moja kwa moja kwenye mtego pasipo ya yeye kujua.

Muda huo huo Edna simu yake ilianza kuita na alipoangalia jina la mtu anaepiga aligundua ni Recho sekretari wake.

“Boss saa saba kamili una ratiba ya kuonana na muwekezaji kutoka kampuni ya Kiboko Enterprises , naulizia kama ratiba inaendelea kama ilivyopangwa au nifanye mawasiliano kuweka miadi siku nyingine”Aliongea Recho kwenye simu.

“Ninakuja ofisini muda si mrefu , weka miadi afike moja kwa moja ofisini kwangu”Alijibu Edna.

“Sawa Madam”Aliongea Recho na kisha simu ilikatwa na Edna aliangalia muda na kuona zimebaki kama dakika therathini kuweza kuonana na muwekezaji kutoka kampuni ya Kiboko.

“Unaweza kwenda tu kazini nitahakikisha mgonjwa namsaidia kadri ya uwezo wangu”Aliongea Roma mara baada ya Edna kukata simu na Edna alitabasamu na kutingisha kichwa.

“Kama kuna lolote la ziada utaniambia, Rufi nitaenda ofisini mara moja ila baadae nitapitia kukuona sawa?”

“Okey , Asante kwa mara nyingine Miss Edna”

“Usijali”Alijibu Edna na kisha alimuaga Roma na kutoka.

Baada ya Edna kutoka Roma alifungua mlango na kuchungulia nje kuona kama Edna kashatokomea na baada ya kuhakiki Edna ashaondoka kabisa alifunga mlango na kurudi ndani huku akimkazia Rufi macho, lakini Rufi wala hakumhofia kabisa kwanza kabisa alijiegamiza bila wasiwasi.

“Rufi najua kila ulichomuelezea mke wangu ni uongo , hivyo niambie umekuja Tanzania kufanya nini?”Aliongea Roma huku akiweka sura yenye usiriasi na Rufi alitabasamu na kuufanya uzuri wake kuonekana vizuri.

“Wapi unahisi nimeongea uongo?”

“Acha kujibu kwa kuuliza maswali , ni jibu kwanini upo Tanzania?”

“Usiniangalie hivyo bwana unanitisha”

“Rufi naomba unisikilize , mimi na wewe hatudaiani kabisa na najua upo hapa nchini kwa ajili ya kunitafuta ndio maana ukafanya utundu wa kudukua kampuni yangu , hivyo kama shida ni pesa nitakupatia pia nitakusamehe kwa kosa la kudukua mawasiliano ya Tv Chaneli ya kampuni , hivyo nitahitaji ufute Vidio ile , pili uondoke Tanzania”Aliongea Roma akiwa siriasi.

Roma hakutaka kwa namna yoyote kujihusisha kabisa na Rufi , ni kweli alikuwa ashafanya nae ngono lakini siku ile alimchukulia kama kibudurisho tu cha muda na hata hivyo alishakwisha kumlipa kwa kumponyesha sumu iliokuwa mwilini mwake kwa mabadilishano ya kumtoa Bikra hivyo ni kama hakuwa na deni na mrembo huyo , alijaribu kumshawishi Rufi kwa kutumia pesa kwanni aliamini huenda mrembo huyo ndio alichokuwa akihitaji kutoka kwake , hivyo aliamini anaweza kumaliza hilo tatizo kwa kumpa pesa ili mke wake asijue kile alichokifanya na yeye.

Rufi alimwangalia Roma namna anavyoongea na alijikuta akiishia kucheka kwa sauti , kicheko ambacho hakikuonyesha kama ni cha dharau bali kilionyesha ni kama amefurahi kumuona Roma katika muonekano aliokuwa akitegemea , kwake aliona ni kama ushindi.

“Usicheke nipo siriasi Rufi sitaki nilichofanya mimi na wewe kimfikie mke wangu , mpango wako wa kujigongesha uonekane umepata ajali , lakini pia kudukua chaneli yetu hilo nakubali ni mpango safi lakini kwasasa unapaswa usikilize ninachokuambia”.

“Mr Roma Ramoni najua una pesa nyingi sana na kama mpango wangu ni kuhitaji unipatie pesa zako basi nisingekwenda mbali mpaka kutengeneza ajali kwa kutumia gari ya mkeo lakini pia kufanya udukuzi kwenye kituo cha televisheni, ninachotaka ni kingine kabisa na sio pesa”Aliongea Rufi

“Kama hutaki unahitaji nini kutoka kwangu?”

“Swala la kwanza nimefurahi kukuona kwa mara nyingine , tokea ulivyoondoka nilikuwa nilikuwazia sana , hivyo ni ngumu kwa yale ulionitendea kuweza kuyasahau mara moja na kuendelea na maisha yangu, swala la pili nilichomwambia mke wako sijadanganya, najua nilikuambia nilikuwa na babu yangu ni mgonjwa lakini ile ilikuwa ni uongo”Aliongea na kumfanya Roma kukuna kichwa.

“Niambie unachoitaji ni nini ambacho ni zaidi ya pesa”

“Nadhani swali la kwanza uniulize kwanini nilikuwa na sumu nyingi ndani ya mwili wangu , ni wapi nimetokea , kwanini nina ngozi nyeusi na nyeupe , je nilichomwambia mkeo ni sahihi au sio sahihi , unatakiwa kuniuliza maswali ya namna hio”Aliongea Rufi huku akianza kuwa na uso uliokuwa siriasi na kuonyesha namna ya huzuni na kumfanya Roma kuvuta pumzi kidogo.

“Mr Roma Ramoni sipo hapa kwa ajili ya kukugombanisha na mke wako , bali nipo hapa kumtafuta Mama yangu mzazi, nilipokutana na wewe Loss Angeles nilishakufahamu tayari kwa majina yako kamili na wapi unapotokea”Aliongea Rufi na kumfanya Roma kidogo kushangaa lakini Rufi hakumjali zaidi ya kuchukua mkoba wake na kisha akaufungua na kutoa picha na kumpatia Roma.

Roma alishangazwa na picha hio , ilikuwa ni picha ambayo ilipigwa kipindi cha shindano la Kizazi nyota ni picha ambayo alionekaa yeye , Edna mke wake pamoja na Christen Stewart msanii kutoka Marekani.

“Hio picha ndio ilionifanya nikahamia Loss Angeles kutoka New York, sababu kubwa ya kuhamia Loss Angeles ni kuweza kukutana na Miss Christen ili aweze kuniunganisha kwako”Aliongea Rufi na kumfanya Roma kukunja sura.

“Kwanini ulitaka kuonana na Miss Christena na akuunganishe kwangu?”

“Kama nilivyosema nipo hapa nchini kumtafuta Mama yangu mzazi, kuhusu kutaka kuunganishwa kwako ni stori ndefu sana ila kwa ufupi sana sina ndugu huku duniani wala mzazi wa aina yoyote nipo mimi kama mimi Rufi na nimeishi miaka mitano nchini Marekani kwa kurubuni watu, maisha yangu yalikuwa ya maumivu makali na sikuwahi kuwa na amani hata kidogo , kila siku kwangu nilikitamani kifo lakini sikuweza kufa niliishi kwa mateso makali , lakini mpaka leo siamini mateso yangu yote yaliisha mara baada ya kukutana na wewe , uliiponya maumivu nilioishi nayo tokea nikiwa mdogo…..”Alijikuta akiishia njiani na kuanza kulia na kumfanya Roma kuzidi kuchanganyikiwa kwa kutojua namna ya kumsaidia lakini hata hivyo hakutaka kumuamini Rufi moja kwa moja ,alikuwa ashamjua ni mwanamke mjanja lakini kwenye swala la maumivu ni swala la kweli kabisa kwani yeye mwenyewe ndio aliemsaidia kupona.

“Okey haina haja ya kulia tena , kama kweli umekuja hapa kwa ajili ya kumtafuta mama yako kwanini ukamu’approach’ mke wangu , lakini pia kwanini ukadukua Tv Chaneli yetu?”Aliuliza Roma lakini Rufi hakujibu zaidi ya kuinama chini.

Roma alijikuta akimwangalia Rufi kwa namna ya kumwangalia , ijapokuwa msichana huyo alikuwa na urembo wa kupitiliza lakini hakutaka kujihusha nae alikwisha kujiapiza asingeongeza mwanamke mwingine kabisa kwa namna yoyote, lakini hali ya upweke ya Rufi ilimfanya kumuonea hjuruma kwani hisia alizokuwa akipitia mrembo huyo ni hisia ambazo hata yeye mwenyewe amekwisha wahi kupitia , maisha ya kutokuwa na mzazi wa kumtegemea maisha ya kuwa mpweke ni maisha ambayo Roma aliweza kuishi nayo kiwa miaka mingi kabla ya kufanikiwa kuijua familia yake.

“Kama unataka nikusaidie na niruhusu ukae hapa Tanzania lazima utii masharti mawili matatu”Aliongea Roma mara baada ya kumuagizia Chakula na Rufi alimwangalia Roma kwa shauku ya kujua hayo masharti.

“Kwanza kabisa sitaki kujihusisha na wewe kimapenzi , hilo niweke wazi kabisa , sipendi ugomvi na mke wangu , mimi na wewe deni letu liliisha hivyo kama una chembe ya shukrani lazima unaelewa nilichokufanyia usingeweza kufanyiwa na mtu yoyote yule , swala la pili ufute Vidio zote za sisi tukifanya mapenzi, swala la tatu ijulikane kwamba hatujawahi kukutana mahali popote, Je upo tayari kutii masharti?”Aliongea Roma na kumfanya Rufi kufikiria kidogo na kisha akamwangalia Roma usoni na akaishia kutabasamu kinyonge.

“Nipo tayari”Aliongea

Ushaonja tayari kitumbua changu ni swala la muda tu utanihitaji tena, nitazidi kujenga ukaribu na wewe mpaka unitake mwenyewe, , Rufi Mission accomplished without Hitch hehe..”Alijiwazia kwenye akili yake , ilionekana mpaka hapo alichokuwa amekipanga kimekamilika kwa aslimia mia moja.

Ni kweeli kabisa kwanza kabisa mrembo Rufi baada ya kufika Tanzania na kuchukua Chumba ndani ya hoteli , mpango wake wa kwanza ni kutafuta namna ya kujenga ukaribu na Roma lakini pia na mke wake , hakutaka kutumia mbinu ya kumtishia Roma kwa kutumia Vidio alizorekodi pasipo ya Roma kujua wakati wakifanya mapenzi kutokana na kwamba alishajua Roma sio mtu wa kawaida na angetaka kuzichukua kutoka kwake ingekuwa ni rahisi sana na mpango wake usingefanikiwa , hivyo alichofikiria cha kwanza ni namna ya kuweza kujenga ukaribu na Edna na wakati huo huo akijitambulisha kwa Roma kwa namna ya kipekee , katika kuwaza kwake namna ya kufanikisha jambo lake ndipo moja kwa moja alipopata wazo la kutumia uwezo wake wa akili na taaluma yake.

Rufi n kweli aliishi Marekani kwa miaka mitano na katika miaka yote hio aliweza kujifunza vitu vingi kwa namna isiokuwa rasmi , yaani kwa njia ya mtandao.

Kwanza kabisa alijifunza lugha ya kingereza na kuielewa vizuri na baada ya kukamilisha kujifunza lugha hio alianza kujikita kwenye kujifunza matumizi ya kutumia Kompyuta na ndipo alipochagua somo la Computer Science kwa kuchukua kozi maalumu kwenye mtandao wa Udemy pamoja na alijikita kwenye kujifunza lugha zaidi ya nne za Programing , alijifunza PHP, Python , JavaScript pamoja na C++.

Aliweza kujifunza kwa haraka kutokana na kwamba alikuwa na uwezo mkubwa wa kiakiri wa kukariri vitu na kutovisahau lakini pia kilichomsaidia zaidi ni mara baaada ya kujenga urafiki na moja ya wanafunzi wa chuo cha Columbia.

Njia rahisi ya kupata marafiki ndani ya jiji kubwa kama New York ni ule upekee ambao mtu kwenye jambo husika , kwa mfano kama unao uwezo mkubwa sana wa kucheza na masoko ya hisa basi ni rahisi kupata marafiki wanaopenda maswala ya hisa, kama unapenda maswala ya komputa katika maswala ya ubunifu na ukawa vizuri kwenye kazi yako basi ni rahisi sana kupata marafiki wa kada hio, ijapokuwa Rufi hakuwa amesoma elimu rasmi lakini uwezo wake ndio uliomtambulisha kwa watu waliosoma kutoka vyuo mbalimbali kama Columbia na Queens University.

Baada ya kuiva ndipo alipojiingiza katika kufanya kazi mbalimbali kwenye makapuni kwa njia ya ‘freelancing’ kazi mbalimbali ambazo zilikuwa zikihitaji ujuzi zaidi kuliko vyeti , hivyo njia hio ilimpatia pesa za kulipia kodi na kuishi ndani ya New York, lakini hata hivyo njia hio haikumpatia pesa za kutosha kukidhi kiu yake hivyo ndipo alipoanza kujiingiza kwenye kazi ya kutapeli watu kwanjia mbalimbali na kazi hio ilimpatia pesa nyingi sana kuliko hata ya kupata ‘gig’ mtandaoni.

Roma alijikuta akivuta pumzi mara baada ya Rufi kumuelewa , ijapokuwa aliona swala hilo linaweza kumletea shida mbeleni lakini hakutaka kumnyima Rufi nafasi ya kumtafuta mama yake mzazi , alijiambia mwenyewe moyoni kwmaba atajitahidi kuwa makini ili mazoea yake na Rufi yasiwe na ukaribu zaidi kiasi cha kuwa wapenzi.

Edna mara baada ya kutoka kazini moja kwa moja alikuja hadi hospitalini na Rufi aliomba ruhusa ya kuondoka siku hio hio kwani hakupenda kukaa hapo hospitalini kwa muda mrefu.

“Umefikia wapi hapa Tanzania?”Aliuliza Edna.

“Nilifikia hotelini lakini nimefanikisha kununua Apartmeng kwa msaada wa rafiki yangu”Aliongea Rufi na kumfanya hata Roma kusangaa.

“Kumbe unarafiki hapa Tanzania?”

“Ndio nilikutana nae kupitia mtandao wa Speaky”

Mtandao wa Speaky ni mtandao maarufu ambao unaunganisha watu wa tamaduni nyingi duniani kwa ajili ya kufundishana lugha , kwa mfano kama utahitaji kujifuza kiarabu na pia kuna mtu anataka kujifunza kiswahili basi mtaombana urafiki na kusaidiana kufundishana.

Kwa maelezo ya Rufi rafiki yake ni mwenyeji wa mkoa wa Kahama ambaye anasomea chuo cha CBE, kauli hio ilimfanya Roma kuwa na ahueni kwani aliamini huenda mke wake angemuambia Rufi akakae nyumbani.

Basi ilibidi Rufi awasiliane na rafiki yake , ambaye ndani ya muda mfupi aliweza kufika hospitalini hapo, Roma alishangaa mara baada ya kugundua rafiki aliekuwa akizungumziwa na Rufi alikuwa mwanaume tena kijana ambaye alikuwa Sharobaro kutokana na mavazi yake na mkato wa nywele , alionekana kama kijana muhuni muhuni lakini Roma hakutaka kutoa maoni yake na hata kwa Edna alionyesha wasiwasi lakini upande wa Rufi alionekana kumuamini rafiki yake.

Alikuwa kijana ambaye pia hela ilionekana kuwa sio tatizo kwani alikuwa akiendesha gari nzuri kweli ya kifahari aina ya BMW X6 toleo jipya.

Baada ya Rufi kuondoka , Roma na Edna waliamua kurejea nyumbani huku Edna akimuahidi Rufi atamsaidia kumtafutia namna ya kuishi Tanzania kama mgeni kwani Viza yake alioingia nayo nchini kama mtalii ilionyesha kuisha ndani ya mwezi mmoja.

“Kesho kuna mahari nataka twende pamoja”Aliongea Edna wakati wakiwa kwenye gari na Roma wakielekea nyumbani.

“Nipo tayari kwenda na wewe hata kuzimu mke wangu nitahakikisha naongoza njia kabisa”Aliomgea Roma kwa namna ya utani na kumfanya Edna amshangae Roma na uropokaji wake mpaka kujisikia kucheka.

“Kesho kuna graduation UDSM, Profesa Clark na mimi ni moja ya watu tulioalikwa , lakini pia ndio siku ambayo projekti ya kampuni yangu kwa kushirikiana na chuo itatangazwa rasmi ili kuruhusu wanafunzi wenye sifa za kuomba kushiriki kuanza rasmi, naomba unisindikize kwasababu kwanza wewe ndio upo na ukaribu zaidi na Profesa Clark hivyo itakuwa vizuri kama utamsapoti”

“Okey wifey umeongea pointi , tutahudhuria pamoja siwezi kukuacha uende mwenyewe na maprofesa wakaanze kukodolea macho nitahakikisha wanaelewa nini maana ya mwanmke mrembo kama wewe kuwa ‘taken’”.

“Yaani Roma..”Alijikuta akiongea na kufumba macho.

Ilikuwa ni muda wa usiku baada ya chakula Roma wakati akiwa amekaa sebuleni akicheza na Lanlan simu yake kubwa ilianza kuita kwa kutetema na kumfanya kuitoa ili kuangalia nani aliekuwa akipiga na aligundua namba inayompigia ni kutoka Uingereza , alishangaa kidogo na kisha alitoka nje kwa ajili ya kuipokea

“Who is this?”Aliuliza Roma mara tu baada ya kuipokea .

“Little Roma Roma it’s me” Ilisikika sauti ya kimagizo yenye kuumiza masikio na kumfanya Roma mwili wake kushikwa na msisimko.

“Catherine!!” Aliongea Rima baada ya kuitambua sauti ni ya Catherine mama yake mzazi Profesa Clark , kwani ni yeye pekee ambaye alikuwa akizungumza nae kwa namna ya kitoto na kurudia rudia jina lake.

“Nilikumisi sana kwanini hukunipigia tokea mara ya mwisho tuonane , kila wakati unapenda kuniacha nikiwa na huzuni na hamu ya kukuona tena kila unavyomaliza kunichezea”

“Huna tabia ya kunipigia simu , labda iwe kwa shida maalumu unaonaje ukienda moja kwa moja kwenye shida yako”Aliongea Roma.

“Oh! sikujua unanifahamu hivyo?”

“Kadri utakavyobakia kwenye uhalisia wako nitaendelea kukufahamu”Aliongea na Catherine alitoa kicheko kidogo.

“Roma nadhani ushakutana na Clark huko Tanzania , ameondoka huku bila ya kuaga na kuja huko nataka umrudishe nyumbani haraka”Aliongea Catherine na kumfanya Roma kushangaa hata hivyo alishajua tokea mwanzo kuna kitu hakikuwa sawa kwa Profesa Clark ghafla tu kuja Tanzania kwa ajili ya kazi ya kufindisha.

“Unamaanisha nini kumrudisha nyumbani , mmefanya nini mpaka akawakimbia?”Aliuliza Roma.

“Ameondoka pasipo ya kuaga mara baada ya familia ya Rothchild kumtaka aolewe na mchumba waliomwandaa”Aliongea na kumfanya Roma kushangazwa na kauli hio.
 
SEHEMU YA 440

Ijapokuwa ni swala la kawaida sana kwa familia za kifalme kuwaozesha watoto wao kwa maslahi mapana ya kuendeleza kizazi lakini hakuaminni ingekuwa haraka hivyo.

“Roma naomba unisaidie kumrudisha nipo kwenye wakati mgumu ,ukoo wote wamekasirishwa na kitendo chake cha kutoroka kuja Tanzania kwa kuandaa projekti ambayo hakupaswa hata kuifanya yeye ili kupata sababu, nimekupigia kwasababu kila mmoja ana wasiwasi na uwepo wako nchini Tanzania kama tutatumia nguvu kumrudisha hivyo nataka unipe ruhusa yako kama nikituma watu waje kumsindikiza kumrudisha Wales usiingilie”Aliendelea kuongea.

“Clark aliyaokoa maisha yangu kwa mara nyingi sana na mpaka sasa naendelea na miash yangu ya kawaida kwasababu alijitolea kunisaidia,, kama hataki kuolewa na mtu asiempenda lakini pia hataki kurudi Uingereza basi hakuna mtu wa kumfosi kufanya hivyo kwani sitoruhusu”Aliongea Roma kwa Kingereza na kufanya sauti ya Catherine kuwa ya kinyonge.

“Mimi na Edward tulijua tu utaingilia ndio maana hatukutaka kuchukua hatua lakini inaonekana Clark ni mwerevu mno kuzidi hata mimi mama yake , ameshakuja kwako akiamini hatuwezi kufanya lolote”

“Sio siwezi kufanya lolote ninachoongea ni ukweli , sijui mmepangia aolewe na nani lakini nawasihi muheshimu kile anachokipenda la sivyo hakutakuwa na maelewano baina yangu na nyie”Aliongea Roma huku akiona hana haja ya kuwarembesha.

Hata hivyo alijua Clark hakuwa mtoto tena kwa msingi wa kisheria za jumba la kifalme , hivyo kwa umri wake ilitakiwa awe tayari ashaolewa au iwe ishajulikana wazi ni mwanaume gani anapaswa kuolewa nae kama ilivyo kwa watoto wengi wa kike wa kifalme.

“But Roma hear me out, Clark is a girl from Royal family , She is expected to carry on ou bloodline , Her Marriage is inevitable , I have been meaning to call fo while now .Please persuade her to reconsider , She has to stop living in her fantansy and start facing reality”

“Lakini Roma Clark ni mtoto kutoka koo ya kifalme na ni matarajio kwamba lazima aendeleze damu yetu, Ndoa yake haiepukiki , nilikuwa nikijishauri nikupigie simu kwa muda mpaka sasa , naomba ujaribu kumshawishi afikirie upya , anatakiwa kuacha kuishi kwa fantansia na aanze kukabiliana na uhalisia”

“Okey nitaongea nae kesho lakini naomba nikutahadharishe kwamba hakuna mtu wa kumfosi kufanya kile asichopenda”Aliongea Roma na kumfanya Catherine kuvuta pumzi na kisha akakata simu.

Usiku huo Roma alishindwa kabisa kupata usingizi kwani alianza kufikiria kwanzia siku ambayo aliweza kukutana na Clark , Roma tokea mara ya kwanza anakutana na Clark alishaona ni wa kipekee mno kwenye macho yake, lakini licha ya hivyo hakutaka kufanya jambo lolote kwake kutokana na kile kilichokuwa kinaendelea kati yake na mama yake.

Siku iliofuata Roma na Edna hawakuenda kazini zaidi ya kwenda moja kwa moja UDSM kwa ajili ya kuhudhutia mahafali ya 52 ya chuo hicho.

Ndani ya madakika kadhaa tu waliweza kufika Mlimani na kupokewa huku baadhi ya watu wakiwashangaa kwa aina yake , Tokea Edna aweke mahusiano yake wazi na Roma , lakini pia Roma kutangazwa kama mtoto wa Raisi wa Tanzania basi ni kama wameingizwa kwenye nafasi ya ‘Maceleb’ moja ya watu wanaofuatiliwa zaidi hivyo hata waandishi wa habari hawakuacha kuchukua picha mara baada ya kuwaona.

Ilionyesha kuhudhuria kwa Profesa Clark ndani ya chuo hicho kwenye hayo mahafali kulipewa heshima ya kipekee kwani picha zake pia zilikuwa zimewekwa katika njia ya kuingia eneo lote la chuo.

Baada ya nusu saa tu ya Roma kufika hatimae msafara wa Jane uliweza kufika ndani ya eneo hilo la chuo na kufanya waandishi wa habari kutaka kuruka fensi ili kuweza kupiga picha nyingi , lakini hata hivyo mabodigadi na watu wa usalama walifanya kazi kubwa ya kuzuia watu , hata hivyo siku hio mheshimiwa Senga pia alikuwa ni mgeni rasmi katika Mahafali hio , hivyo itifaki za ki usalama zilikuwa za hali ya juu kabisa.

Baada ya wote kwa pamoja kuingia ndani ya ukumbi wa Nkurumah na kuonyeshwa sehemu ya kuketi , Edna alianza kusogelewa na wafanyabiashara wakubwa wa jiji na kusalimiana nae kwa heshima yake , ilikuwa nafasi nzuri kwao kwanni ndio namna ya kujitengenezea konekshenni za kibiashara , wale baadhi ya wafanyabiashara pia ambao mwanzoni hawakumheshimu Roma kama mke wa Edna walijitahidi pia kumsogela na kumsalimia kwani walishajua ni mtoto wa raisi , watu walimsogelea zaidi ni wanasiasa.

Roma alishangazwa na jambo hilo lakini hata hivyo alichukulia kawaida na kusalimiana nao.

Muda mchache mbele hatimae mgeni Rasmi wa kuongoza mahafali hayo alifika na ufunguzi wa mahalafi ukaanza rasmi , ukumbi wote huo na ukubwa wake ulijaa wahitimu wengi mno , ikionyesha namna ambavyo chuo hicho kilikuwa kikubwa nchini.

Clark na Edna walikaa meza moja za mbele kabisa sehemu maalumu ya wageni wa heshima walioalikwa , uzuri wa Clark na Edna ulifanya Kamera muda wote kuwamulika na kufanya kuonekana kwenye ukumbi wote kwa wale waliokuwa eneo la nje na ndani pia ambao walikuwa mbali , kila mmoja alijaribu kufananisha uzuri wao , lakini hata hivyo ilikuwa ngumu kupata kujua nani kamzidi mwenzake kwani wote ni wa rangi tofauti , Edna alikuwani mweusi huku Clark akiwa mzungu.

Baada ya mahafali kuanza hatimae zamu ya Clark kuongea ilifika na watu walimshangalia mara baada ya kuanza hotuba yake na kuelezea dhumuni lake la kutaka kufundisha ndani ya chuo hicho kupitia Projekti maalumu, kingereza chake cha kizungu kiliwaacha wale walioweza kumuelewa kufurahi lakini wale ambao hawakumuelewa kusikiliza tafisiri ya mkalimani.Mwishon kabisa mwa hotuba yake:

“That is all I have to say regarding the project , lastly I would like to thank each of you . I know many of you might not have understood what I said , its complete;y normal since my student didn’t understand it either , But thank you all for not falling asleep during my speech”

“Hivi ndivyo ninavyoweza kusema kuhusiana na Project , mwisho kabisa niwashukuru ninyi wote , najua kati yenu kuna ambao hamjanielewa moja kwa moja nilichozungumza lakini niwaambie ni kawaida sana , hata wanafunzi wangu hawakunielewa , niwashukuru kwa kutosinzia wakati wa hotuba yangu”Aliongea huku akitabasamu na kufanya wanafunzi waliovalia majoho akiwemo Raisi Senga kupiga makofi.

Baada ya hotuba yake ilifuatia makamu mkuu wa chuo ambaye alikaimu nafasi ya mkuu wa chuo ambaye alikuwa ni Mheshimiwa Kigombola aliekuwa nje ya nchi na alimkaribisha waziri wa dhamana na kisha waziri akamkaribisha mheshimiwa Raisi kwa hotuba yake ya mwisho.

Roma hakukaa kabisa kusikiliza kile alichokuwa akisema raisi Senga kwani aliondoka na kwenda kukaa nyuma kabisa ya bustani kwenye kimbweta na huku akiangalia bustani za majani akionekana kuwaza baadhi ya mambo.

Ijapokuwa Catherine hajaongea mambo mengi kuhusu swala la ndoa ya Clark lakini moyo wake ni kama uliguswa na swala hilo hususani mara baada alivyomuona Clark akitoa hotuba kwa kujiamini na kufanya urembo wake kuzidi kujidhihirisha.

Roma hakuwahi kufikiri kumfanya Clark kuwa mpenzi wake kabisa lakini swala la kuambiwa anataka kuolewa na mwanaume mwingine ni kama moyo wake uligoma kumuachia kwenda kwa mwanaume mwingine.

Baada kama ya lisaa kupita wakati Roma akiwa akiwaza hili na lile hatimae aliweza kusikia hatua hafifu zikimsogelea eneo ambalo amekaa na aliweza kugundua kadri mtu huyo alivyokuwa akimsogelea.

Na baada ya kugeuza shingo ndipo alipomuaona mrembo huyu alievalia gauni la rangi ya bluu kumwangalia kwa tabasamu na kisha akaenda kuketi pembeani yake.

“Huogopi mapaparazzi?”Aliuliza Roma kidogo kwa wasiwasi.

“Nimetumia upande ule wa nyuma kuja mpaka hapa , nilikuwa nikiotea mahali ulipo na bahati imeniangukia nimekuona”Aliongea baada ya kukaa huku akivua viatu vyake vya high heels ambavyo vilionekana kumchosha kuvaa.

“Usingekuja Tanzania , mama yako unampa wakati mgumu”

“Kati ya hisia za mama na za kwangu zipi unatanguliza kuzijali?”

“Yeye ni mzazi wako , sina haja ya kuzingatia hisia zako wala za kwake”

“Hapana Roma nakuuliza kama mwanamke , kama unajali hisia zangu mimi au za mama yangu?”Aliongea na kumfanya Roma kufikiria namna ya kujibu.

“Sijui namna ya kukujibu lakini mara baada ya kupigiwa simu na mama yako sikuweza kulala kwa amani”Aliongea Roma na kumfanya Clark kutabasamu kwa furaha.

“Nimependa jibu lako , angalau nimekufanya ushindwe kulala kwa amani”

“Wewe na mama yako mmekuwa watu muhimu sana kwangu , tumeishi pamoja kwa kipindi kirefu , mna sehemu yenu ya pekee kwenye moyo wangu”

“Kwahio unasema sisi ni wa pekee ambao tupo ndani ya moyo wako?”

“Siwezi kuongea zaidi juu ya hilo lakini hata hivyo wewe una akili nyingi kuliko hata mimi , tatizo tu ni kwmaba hata kama una akili vipi lazima ukubaliane na uhalisia kwamba wewe ni Princess wa Wales ambaye lazima uozeshwe kwa matakwa ya familia”Aliongea Roma lakini Clark alionekana kutoridhishwa zaidi na jibu lake na alichokifanya ni kuweka kichwa chake kwenye bega lake huku akiacha kujali watu waliokuwa wakiwaangalia kwa mbali.

“Lakini Roma unajua kabisa kwanini nimekimbilia kuja Tanzania”Aliongea na kumfanya Roma kuvutya pumzi nyingi na kuzishusha.

“Clark unajua kila ninapokuona na kuchukulia kama Almasi ambayo haijachakachuliwa , almasi ambayo imekatwa kwa namna ya upekee kabisa , kisi cha kunifanya nisiiguse kwa kuogopa kuichafua kwa kuamini kwamba itaendelea kuvutia na kung’aa milele , uzuri wake ni mkamilifu kwenye moyo wangu lakini kama nitaigusa na kuichafua nnitakuwa mbinafsi , lazima niiache ili wengine wapendezwe na uzuri wake”

“Kama ni hivyo kwanini usiache ikaendelea kung’aa ikiwa karibu ya macho yako , ilinde huku iking’aa hata bila ya kuigusa lakini ukihakikisa ipo salama bila ya kuchukuliwa na mtu mwingine, huenda ikawa na furaha zaidi”Roma alijikuta akishindwa kujibu na kuishia kukunja ngumi .

“I like you Roma Ramoni , I really do , I m very sure of it”

“Nakupenda Roma Ramoni , ni hakika nakupenda, nina uhakika na hisia zangu”Aliongea na kumfanya Roma kushangazwa na maneno ya moja kwa moja ya Clark lakini hata hivyo alishindwa kujibu.

“Ila usiwaze sana kuhuhusu hisia zangu , siku ambayo nilizama penzini ni muda ambao kila kitu kuhusu mimi kilibadilika niligundua kwamba nipo kwenye ulimwengu wa kiza kinene nikitumainnia kuna mwangaza unanisubiri upande mwingine wa ulimwengu ”

“Clark mimi si wa thamani kupendwa na mwanamke kama wewe”

“That is my call to make”

“Hio ni juu yangu”Aliongea Clark kwa namna ya ukibuti wa kutokubali kushindwa

“Clark sitaki kukuficha chochote kwako na wewe pia unaweza kuchangia mawazo yako kuhusu mimi , tupo hapa tumekaa kwa kukaribiana”

“Lakini unavyosema tupo tumekaribiana kwanini nahisi kama tupo kwenye dunia mbili tofauti”Aliongea lakini Roma alikaa kimya na Clark aliendelea.

“Roma tafadhari naomba usinifukuze kama hunihitaji, sina mahali pengine pa kwenda , naomba uniahidi angalau niwe tu karibu yako”Aliongea na kumfanya Roma kuguswa na maneno yake na kumwangalia.

“Okey nakuahidi siwezi kukufukuza”Aliongea Roma na kisha akasimama na kuondoka eneo hilo kwani macho yaliokuwa yakiwaangalia ni mengi.

Roma mara baada ya kurudi ukumbini sherehe ilikuwa ndio inakaribia kuisha kwa ugawaji wa zawadi na wageni walipaswa kukusanyika kwenye ukumbi mwingine kwa ajili ya chakula, Roma alikutana na Edna mlango wa kutokea.

“Ulienda wapi wakati mahafali yakiendelea ,usiniambie ulikuwa ukinisaliti?”Aliuliza Edna

“Usiwe na wasiwasi sikuwa ‘interested’ na kilichokuwa kikiendelea hivyo nilienda kukaa nje kupata ka usingizi kidogo”

“Mh warembo wote hao waliopo ndani ya hiki chuo hawajakufuata kweli?, maana ukizingatia na umaarufu wako lazima wavutiwe lakini pia mwonekano wako umekaa kipesa zaidi , hata hivyo natania tu kukuuliza , nakuamini”Aliongea Edna huku akiweka tabasamu.

“Hehe Babe nina haja gani ya kuangalia warembo wengine wakati mke wangu wewe umewazidi kwa kila kitu?”

“Kama ni hivyo ulikuwa ukifanya nini na Profesa Clark kule nyuma?”

“Kumbe ulituona?”

“Kwanini nipoteze tageti zangu , nimekuleta hapa kwasababu nakuamini , usije ukanisaliti na Profesa Clark , ukifanya hivyo nitahakikisha hii projeti tunayofanya ninaifuta na baada ya hapo nitamfukuza kurudi kwako na kuhusu wewe nitahakikisha unaisoma namba”

“Edna mke wangu sio unavyofikiria , tulikuwa tukiongea mambo ya kawaida tu haraka haraka”Alijitetea Roma.

“Naomba iwe hivyo, sina uwezo wa kuzuia matendo yako lakini lazima uelewe kwamba najitahidi kuhakikisha mahusiano yangu na wewe yanaendelea vizuri bila migogoro, wewe mwenyewe ndio umekubali tukishafunga ndoa ndio tutalala pamoja na nitajikabidhi kwako, hivyo ole wako uongeze mwanamke mwingine , nitakuonyesha ukatili wangu ambao sijawahi kuuweka wazi ohoo , Roma umenielewa?”

“Ndio malkia wa moyo wangu”Alijibu Roma.

Wakati wanataka kwenda kujiunga na wageni wengine kwa ajili a chakula cha mchana Roma simu yake palepale iliiita kwa hasira kama zote na alipoangalia jina lilisomeka Benadetha , alishangaa kwani si kawaida kwa mrembo huyo kumpigia simu.

“Benadetha vipi ?”Aliongea Roma mara baada ya kupokea simu.

“Roma naomba unisamehe kwa kupigia simu lakini sijui cha kufanya na nimeongea na baba na amenilazimisha nikupigie simu na kukuomba msaada….”Aliongea na kumfanya Roma kukunja sura kwani sauti ya Benadetha haikuwa ile alioizoea , alionyesha kuwa kwenye wasiwasi.

“Nini kimetokea niambie”

“Kaka yangu ametekwa , haonekanni tokea jana usiku”Aliongea .

“Unasema!!?”Aliongea Roma na kumfanya Edna aliekuwa pembani ya Roma akisikiliza mazungumzo hayo kukunja sura hakuwa na amani kwa Benadetha kumpigia mume wake.

Inayokuja kesho Safari ya kwa Putin kuua mtu….

Anyway nilikumbwa na shida ya kibinadamu mnisamehe kwa kutowapa mrejesho wa aina yoyote , itaendelea back to back.





SEHEMU YA 441

Kwa maelezo ya Benadetha ni kwamba kuna mgogoro wa kifamilia uliokuwa ikiendelea baina ya kaka yake ambaye ni wa mama tofauti , mgogoro ambao ulipelekea kaka yake kutoroka nyumbani na kuelekea kusikojulikana.

Kaka yake huyo ambaye anaitwa Mika ni mwanafunzi wa chuo cha IFM na kwa maelezo ya marafiki zake ni kwamba hakuwa akipatikana kabisa hewani na hata mahali ambapo alikuwa akiishi gari yake ilikuwepo jambo ambalo sio kawaida kwa Mika kuondoka bila gari yake.

Roma baada ya kusikiliza kwa dakika kadhaa alifikiria kidogo na kuona ngoja tu amsaidie Benadetha , ijapokuwa hakupenda kufanya hivyo lakini kwasababu mwanadada huyo kaomba aliona huenda aliamini anageweza kusaidia.

“Edna unaweza kuongozana na Jane tu , Benadetha kaka yake anaonekana kuwa kwenye matatizo”

“Kama kaka yake kwenye matatizo kwanini akuombe wewe msaada huwezi kuondoka na kuniacha hapa mwenyewe tumekuja wote itakuwaje ukiondoka ghafla na kila mtu anajua wewe ni mume wangu”

“Ngoja nimsaidie , tutaongea nyumbani sawa”Aliongea Roma na bila kujali Roma aliondoka na kumuacha Edna akiwa amesimama haamini kama kweli Roma anamuacha , hata hamu ya kwenda kupata chakula na wageni rasmi ilimwishia palepale.

Roma akiwa njiani alimwambia Benadetha amtumie picha ya huyo kaka yake kwani hakuwa akimfahamu kwa sura na baada ya picha kutumwa kwa mtandao wa watsapp Roma alishangaa kwani huyo kijana alikutana nae siku ya jana tu , ndio rafiki aliekuja Agakhani kumchukua Rufi , ilibidi Roma amuambie Benadetha atume pia namba yake ya simu na ilipotumwa aliwapa maelekezo The Eagles kujaribu kufatili namba hio.

Ndani ya nusu saa tu The Eagles walikuwa na majibu , na kwa maelezo yao ni kwamba waliweza kudukua simu yake na ilionekana siku ya jana usiku Mika aliwasiliana kwa njia ya meseji na namba yenye usajili wa jina la Shendrack Kengeu na meseji ilionyesha Shedrack Kengeu akimwambia Mika afike hotelini kwake kuna warembo wa Kizungu kutokea Urusi wanarafuta mtu wa kukesha nae.

“Mmefuatilia ni wapi Hoteli hio inayozungumziwa?”Aliuliza Roma akiwa kwenye gari ameliegesha kando ya barabara.

“Ndio mfalme Pluto, Shedrack ni mmiliki wa hoteli maarufu inayofahamika kwa jina la Bagamoyo One , ni hoteli ambayo pia inaendesha Club na Casino kubwa ndani ya wilaya ya Bagamoyo , nadhani atakuwa hapo lakini mfalme Pluto kuna jambo kidogo nadhani napaswa pia niliweke wazi kuhusu huyu Shedrack Kengeu”

“Jambo gani?”

“Tumejaribu kuchimba taarifa za ndani kabisa zinazomuhusu kwani umri wake na ukubwa wa hoteli ya Bagamoyo one vilitupa mashaka , ineonekana kwanza ndio kiongozi wa taasisi ya LGBTQ hapa Tanzania”Aliongea Diego na kumfanya Roma kuguna alikuwa na uelewa mkubwa ya maswala ya upinde lakini hakuwahi sana kujihusisha nayo kabisa.

Baada ya kumaliza kuongea na Diego na kuelekezwa eneo ambalo Hoteli hio ilipo aliendesha gari lake kuelekea Bagamoyo na ndani ya dakika therathini tu aliweza kufika ndani ya hoteli hii ambayo ilijengwa nyuma kidogo kabla ya kufika Bagamoyo mjini.

Lilikuwa ni eneo pana mno, barabara iliokuwa ikiingia ndani ya hoteli hio ilikuwa imejengwa kwa ustadi wa hali ya juu kiasi cha kumfanya Roma ajiulize inakuwaje mdogo wake Benadetha akawa na urafiki na kiongozi wa Mashoga ndani ya Tanzania au na yeye ni shoga , lakini hata hivyo alijiambia angejua huko ndani , kipaumbele chake kwa muda huo ni kumrudisha Mika nyumbani kwao.

“Sir huwezi kuingia bila kadi ya uanachama”Sauti ya mlinzi getini ilimuonglesha Roma baada ya kupiga honi kutaka kuruhusiwa kuingia.

“Hapa ni hotelini kwanini niingie kwa kadi ya Uanachama?”Aliuliza Roma.

“Huo ndio utaratibu uliopo haingii mteja ambaye hana kadi ya uanachama ndani ya hoteli hii”Aliongea na Roma alijikuta akikuna kichwa kwa muda.

“Nahitaji kuonana na bwana Shedrack Kengeu , mnaweza kuwasiliana nae mara moja na mueleze Roma Ramoni yupo getini anataka kuingia hotelini”Aliongea Roma na walinzi wale wawili wa kiume waliangaliana na yule aliekuwa akiongea na Roma alimpa ishara mwenzake kufanya mawasiliano.

Baada ya dakika chache tu geti lilifunguliwa na Roma aliruhusiwa kuingia bila shida yoyote na kwenda kuegesha gari lake kwenye eneo maalumu na baada ya kutoka nje ya gari alijikuta akishangazwa na baadhi ya watu waliokuwa ndani ya eneo la bustanini , alijikuta akitingisha kichwa kwa namna ya kuonyesha huzuni.

“Mr Rama Ramoni Right?”Aliuliza mhudumu mmoja wa kiume ambaye sauti yake ilikuwa ya kike na Roma aliitikia kwa kichwa.

“Boss katoa maagizo kwamba unaweweza subiri aneo la mapokezi na hurushusiwi kuingia Club au ndani ya Casino”

“Huo muda wa kusubiri sina , nitaenda huko huko ndani ya Casino na hakuna mtu wa kunizuia”Aliongea Roma kwa vitisho , ukweli hakupenda kukaa hapo ndani hata sekunde moja kwani watu wake walimfanya hata ngozi yake kuota vipele, ijapokuwa ashawahi kufika kwenye maeneo yenye mfanano na hapo lakini siku zote hakuwa ni mwenye kupendezwa na aina hio ya maisha.

Baada ya mkwara ule kuutoa Roma moja kwa moja alitembea kuingia kabisa kwenye jengo hilo ambalo halikuwa refu sana kwenda juu bali likuwa refu kwenda mbele(Horizontal) unaweza kufananisha na hoteli ya Hyatt Kilimanjaro , ilikuwa na ghorofa kama tano kwenda juu , lakini pia lilikuwa na ghorofa mbili kwenda chini ardhini , ni jengo ambalo kwa haraka haraka Roma aliamini huenda lilijengwa kwa ufadhili wa matajiri wa nje , alikuwa akielewa namna ya jamii ya watu hao wanaojiita LGBTQ walivyokuwa wakiishi kwa misaada kutoka kwa mataifa yalioendelea na aliamini hata uwepo wa hoteli hio ni kwa ajili ya kuhamasisha.

Roma alifuatwa na mhudumu mwingine na moja kwa moja aliongozwa mpaka kwenye Lift ambayo ilimpeleka mpaka ndani ya Club na baada ya kuingia ndipo mwanaume alievalia pensi akiwa kifua wazi alimsogelea, alikuwa ni mwanaume jamii ya msomali alikuwa ameshikilia Glass yenye kimiminika cha rangi ya njano.

Itoshe kusema kwamba hapo ndani yaliokuwa yakiendelea yalimshangaza Roma kuyaona ndani ya Taifa kama Tanzania , lakini kwasababu sio kilichomleta lakini pia The Gods treaty ilikuwa ikimzuia kutoingilia maswala ya binadamu wa kawaida , basi hakuwa ni mwenye uwezo wa kujaji baadhi ya mambo.

Ilikuwa mchana ndani ya eneo hilo , lakini ndani ni kama usiku kwani eneo hilo pana lililojengwa kwa usanifu wa hali ya juu halikuruhusu mwanga kuingia ndani na kufanya taa maalumu zinazotumika kwenye Club kufanya eneo lote kupendeza , lilionekana ni eneo maalumu la starehe kwa wale waliokuwa wakipendelea zaidi kufana mapenzi ya jinsia moja.

“’Nipo hapa kwa ajili ya kumchukua Mika , nina taarifa yupo ndani ya hii hoteli”Aliongea Roma.

“Mr Roma Ramoni nakutambua kabisa kama mtoto wa Raisi wa Taifa hili la Tanzania ndio maana nimeweza kutoa ruhusa uweze kuingia bila kadi ya uanachama lakini inanishangaza kumfuata Mika Bindamu yangu , naweza kufahamu una uhusiano gani na Mika?”Aliuliza yule bwana na kwa haraka haraka Roma alitambua huyo bwana pia ni Shoga kwani sauti yake ilikuwa imekwisha kulegea tayari.

“Huna haja ya kufahamu jina langu , nionyeshe kijana alipo”Aliongea Roma na kumfanya bwana Kengeu kumwangalia Roma kwa wasiwasi na kisha alimpa ishara amfuate na Roma aliongozana nae huku Shedraki Kengeu kwa namna ambavyo alikuwa akitembea ilisikitisha kwa mwanaume kuwa hivyo.

Baada ya kupita upande wa pili aligundua kulikuwa na eneo lingine ambalo lilikuwa ni Club pia lakini eneo hilo lilikuwa na vyumba maaalumu ambavyo watu hufurajia maisha wakiwa hawana usumbufu ni eneo ambalo kwa haraka haraka Roma aligundua ni la watu VIP.

Baada ya mlango wa chumba kufunguliwa na ndipo alipokutana na sura za wazungu waliokuwa wameketi kwenye masofa, huku kuna waliokuwa wakishikana shikana na kudendeka wanawake kwa wanawake lakini pia kulikuwa na wanaume waliokuwa wakishikana wao kwa wao , kati yao Mika pekee ndie aliekuwa akimshika shika mwanamke mmoja ambae Roma baada tu ya kumwangalia alijua mwanamke huyo ni Mrusi.

Mika mdogo wake Benadetha mara baada ya kumuona Roma alijawa na wasiwasi hususani pale alipomuangalia kwa macho yenye hasira.

“Binadamu Mr Roma kakufuata , nimeshangazwa ukiwa una fahamiana na mtu mkubwa kama huyu na hautuambiani”Aliongea Kengeu.

“Bro sina uhusiano wa karibu na Mr Roma lakini nakiri kwamba nishawahi kukutana nae , unakumbuka nilikuelezea kuhusu mrembo flani wa kichina kupata ajali siku ya jana , basi ndio nilifahamiana na Mr Roma kwani mke wake ndio aliemsababishia ajali”Aliongea Mika kwa wasiwasi huku akimwashiria yule mwanamke wa Kirusi kuacha kumshika shika.

“Nimekuja hapa kukurudisha nyumbani na jiweke sawa tuondoke kabla sijachukua hatua ya kukufosi kufanya hivyo”Aliongea Roma kwa usiriasi na kumfanya Mika kukunja sura mpaka hapo alishajua kwanini Roma amefika hapo.

“Mr Roma naomba nibakie hapa hapa , siwezi kurudi, Mzee wangu ni shetani kamuua mama yangu mzazi kwa kumpiga risasi”Aliongea huku akianza kuonyesha hali kukasirika.

“Sijaja kusikiliza maelezo yako”Aliongea Roma na kisha alimsogelea Mika na kisha alimkwida kwenye mkanda wa suruali na kisha akamtoa ndani ya eneo hilo na kufanya watu kumshangaa kwa vitendo vyake vya fujo, wale wanawake wa kizungu waliishia kuangalia na kisha wakatabasamu.

Dakika chache tu Roma alishatoka na kumsukimia Mika kwenye gari na kisha akaingia na yeye na kuliondoa hapo ndani.

“Mr Roma ni nani aliekutuma kuja kunichukua huku?”

“Nimekuja kwa kumsaidia dada yako ambaye anaonekana kwenye wasiwasi na sipo hapa kwa kutumwa”Aliongea Roma huku macho yake yakiwa yamekazia barabara.

Waliendesha kwa kilomita kadhaa baada ya kupita kiwanda cha Kemeli kilomita moja mbele,lakini Roma akili yake ilihisi hatari kwenye gari na ni baada tu ya kuboneza kitufe cha kuwashia mziki.

***********

Upande wa hotelini mara baada ya Roma kuondoka na Mika , bwana anaefahamika kwa jina la Kengeu aliketi kwenye sofa huku akimwangalia mwanamke wa kirusi ambaye jina lake anafahamika kwa jina la Aishapova .

“AishaPova kuna jambo mpaka muda huu bado sijaelewa na nahitaji kukuuliza”Aliongea Kengeu huku akiketi karibu na mwanamke yule wa kirusi.

“Jambo gani hujaelewa?”

“Najua kwamba mabosi kwa muda mrefu wana angazia namna ya kulishinda kundi la waasi kule Congo ili kuweza kutawala migodi ya eneo hilo, lakini siamini kama nguvu ya kundi la ZoaZoa kutoka Kahama linaweza kuwa na nguvu , ni sababu gani mkaamua kumtageti mtoto wa Doni Samweli Nguluma?”Aliuliza na kumfanya Aishapova kutabasamu na kisha alimpokonya glasi ya mvinyo alioshikilia na kunywa kidogo.

“Kuna zaidi ya kazi ambayo imetuleta hapa Tanzania , mathalani inayohusiana na mwanaume uliemuona amekuja hapa, mpango wa kumtumia mtoto wa bosi wa kundi la ZoaZoa kama majaribio ya siraha ya kibailojia ni robo tu ya mpango wote , kufa kwa Mika ni makosa alioyafanya baba yake mzazi kwa kutotimiza maagizo yetu na kumuua mke wake”Aliongea kwa kingereza.

Lakini muda huo huo waliokuwa wakiongea ndipo walipohisi mtikisiko wa ajabu ambao ulifanya hata waliopo ndani ya eneo la Club kuweza kuusikia , Kengeu ndie aliekuwa wa kwanza kushituka kwa wasiwasi.

Muda huo huo mabodigadi wawili waliingia wakiwa na sura za kupaniki, wakimfuata Shedrack.

“Boss kuna kuna dharula nje?”

“Unamaanisha nini?”

“Kuna mtu kaingia na gari na kugonga geti na kisha akagonga pia eneo la mapokezi na mpaka sasa eneo lote limeharibika na kufuka moshi”Aliongea Bodigadi na kumfanya Shedrack Kengeu kujawa na wasiwasi na ilibidi awatafsirie wale wazungu na wote kwa pamoja walipaniki na kuondoka eneo hilo , ilionekana pia baadhi ya watu waliokuwa ndani ya hoteli hio walishituswa na kile kilichotokea hivyo walikimbia kutoka nje kuokoa maisha yao kwani kengele ya Alarm inayoashiria hatari ya moto ilikuwa ikitoa mlio jengo zima.

*******

“BOOM!!”

Ni mlipuko wa aina yake ulitokea na kuteketeza gari ya Roma , kama sio uwezo wake basi hakika wangefia kwenye gari,

Roma alifanikiwa kutoka kabla ya mlipuko akiwa amembeba Mika mkononi na kwenda kumuweka pembeni ya barabara

Alijikuta aking’ata meno kwa hasira , alijua kabisa kuna uwezekano wakari alivyokuwa ndani ya Club basi kuna watu walitegesha bomu chini ya gari lake.

Mika aliekuwa kwenye mshituko alijikuta akitoa mkojo palepale kwani ukubwa wa mlipuko uliotokea ni kama hakuamini amini bado alikuwa hai , alikuwa kwenye majani kando ya barabara lakini hakujua hata amewezaje kufika hapo.

Roma aliangalia gari yake ilivyokuwa ikitekea kwa moto na alijikuta aking’ata meno kwa hasira na kujiambia kwenye nafsi yake lazima alipize kisasi.

Muda huo huo wakati gari ikiendelea kuteketea ilisimama gari kubwa aina ya Semitrailer ambalo halina bodi nyuma kampuni ya Swift Transit , ni gari ambayo nyuma ilikuwa imefungwa mzigo ambao kwa haraka haraka Roma aligundua ni Cement na ilikuwa ikielekea upande wa Bagamoyo.

Gari ile mara baada ya kusimama dereva alishuka kutoka kwenye gari na alionekana alikuwa na Kondakta wake na Roma hakutaka kuchelewa kwani baada wote kushuka yeye alipanda kwenye gari lile.

Wenye gari lao walishtushwa na kitendo cha Roma kupanda gari yao na kushindwa kuelewa alikuwa akitaka kufanya nini na Konda ndio aliekuwa wa kwanza kutaka kuingia lakini kabla hajachukua hatua alipoteza fahamu kwa namna isioelezeka na sio kwake tu hata kwa Dereva pia alidondoka chini, kitendo kilichomshangaza Mika na kuanza kumuogopa Roma kwa wakati mmoja kwani alichoshuhudia ni maajabbu ambayo hakuwahi kufikiria angeweza kuyaona laivu.

“Ingia kwenye gari wewe mtoto”Aliongea Roma kwa kuamrisha na Mika aliekuwa kwenye mshituko aliingia haraka haraka kwenye gari na Roma aliendeesha kwa kukwea gari yake ilikuwa ikiteketea kwa moto na kurudi Bagamoyo.

Haikueleweka alikuwa akipanga kufanya nini lakini mara baada ya kukaribia barabara ya kuingia hotelini alimwamrisha Mika kushuka na atembee wa mguu kumfuata.

“Papaaaa…. Papaaaaa “Roma alibonyeza honi kwa nguvu huku akizidi kukanyaga pedeli ya kuongeza spidi kiasi cha kumfanya aliekuwa nyuma Mika kuziba mdomo wake na viganja vya mikono walinzi waliokuwa getini baada ya kuona gari hio inakuja uelekeo wao ikiwa na spidi kubwa walitoweka wote kwa kulikimbia geti.

Roma hakusuburi hata geti kufunguliwa kwani aliingia nalo moja kwa moja na kulidondosha chini kiasi cha kufanya gari lile kuyumba yumba na eneo lote kuwa vumbi bahati tu ni kwamba ni gari ambalo lilitengenezwa kwa ngao mbele , hivyo vioo havikupasuka.

Kitendo kile kilifanya watu waliokuwa ndani ya eneo hilo kuhaha kwani ni tukio ambalo hakuna ambaye alilitegemea , lakini upande wa Roma hakujali kabisa baada ya gari kupita na geti aliendelea kukanyaga mafuta huku akipiga honi na kwenda kuingia na mlago wa kioo wa kuzunguka uliokuwa ukiunganisha eneo la mapokezi hakujali ni nani angejeruhiwa yeye alijiambia atawakomesha kwa uchokozi wa kutaka kumuua kwa bomu.

Ilikuwa bahati sana kwa baadhi ya watu kujihami mapema lakini kama si hivyo wangejeruhiwa wengi,

Roma baada ya kuridhika na uharibifu aliofanya moja kwa moja alishuka kwenye gari.

Alikagua namna eneo lilivyosambaratika na alionyesha hali ya kuridhika na kile alichokuwa amekifanya , hata hivyo hakufurahishwa na kile kilichokuwa kikiendelea hapo ndani , hivyo kitendo cha kumchokoza kwa kumtegea bomu kwenye gari yake alijiambia ilikuwa ni haki kuhakikisha eneo hilo analiharibu.

Muda huo ndio Shedrack Kengeu na baadhi ya wageni waliokuwa ndani ya hoteli hio walitoka mpaka eneo la nje kwa kutumia mlango wa dharula kwani eneo la mapokezi lililikuwa likifuka moshi mzito uliosababishwa na gari kugonga eneo hilo na kuharibika vibaya sana

Hoteli yote kwa nje ilifuka moshi kutokana na tukio ambalo lilitokea , baada ya walinzi kutoa maelezo ya awali kwa Shedrack ndipo walipogundua muhusika ni Roma Ramoni.

Wote walishangaa na kuangaliana huku wakitembea kuelekea upande wa mbele kwani walitokea mlango wa nyuma , baada ya kufika ndio muda ambao Roma alikuwa akitokezea kutoka ndani ya jengo hilo huku akijifuta vumbi.

Shedrack Kengeu mara baada ya kumuona alijikuta aking’ata meno kwa hasira na kumwangalia kwa hasira kali kwani kwa uharibifu uliofanyika aliamini itachukua muda kukaratabati eneo la mapokezi hivyo biashara lazima kusimama.

“Roma nakuapia nitakuua”Aliongea kwa hasira huku akimwangalia lakini walinzi wenyewe walishangazwa na ujasiri wa aina yake wa Roma , kwani hakuna mtu wa kawaida mwenye akili timamu kuweza kufanya kitendo kama hicho ambacho kingehatarisha maisha yake.

“Mr Kengeu pole kwa mshituko , sijakufa kama mlivyotarajia nimekuja hapa na kuondoka kistaarabu lakini mkaamua kunichokoza wenyewe”Aliongea Roma huku akiweka koti lake la suti Versace kwa namna ya kuihurumia kwani mke wake Edna ndio aliemletea kwa ajili ya kuivaa lakini imebadilika mwonekano wake kwa kujaa vumbi .

“Nina furahi kukuona bado unaendelea kuishi , lakini leo ndio mwisho wako mpuuzi wewe unafikiri tutakuogopa kwasababu ya kuwa mtoto wa raisi, mshambulieni”Aliongea akiwaamrisha walinzi kumshambulia Roma kwa siraha zao , lakini kabla hata hawajafanya maamuzi Roma alishawafikia na kuanza kuwashambulia yeye kwa spidi ya haraka sana na ilikuwa ni kufumba na kufumbua wote walikuwa chini wakiugulia maumivu.

Wale wazungu walijikuta wakiangaliana kwa mshangao baada ya kuona namna Roma alivyodhibiti wale walinzi , lakini muda huo huo kutoka eneo la nyuma waliongezeka wasichana wengine ambao walikuwa wana siraha nzito walionekana kama wanajeshi na wote walikuwa ni kutokea urusi, jambo hilo lilimshangaza Roma kwani hakuamini hoteli hio ingekuwa na wazungu wengi kiasi hicho.

“Aishapova nadhani nikushukuru kwa uwepo wako siku ya leo , naamini huyu mpuuzi leo hachomoki”Aliongea Shedrack Kengeu huku tumaini likibuuka upya mara baada ya Roma kuzingirwa na wanawake wa kizungu walioshikilia bunduki.

“Ni ngumu sana kama tutafanikisha kudili nae kama ameweza kuepuka mlipuko wa bomu lakini pia kugonga geti na hoteli bila ya kupata majeraha”Aliongea Aishapova.na palepale aliwapa ishara wanawake wale waliokuwa na siraha kumshambulia Roma.

“BANG! , BANG! , BANG!, BANG…”

Waliziachia risasi kama vichaa kwa kupokezana , lakini hakuna risasi ambayo ilimpata Roma hata moja kwani kuna zilizokuwa zikipinda na zile zilizomsogelea karibu ni kama kuna nguvu iliokuwa ikizizuia kutokumgusa kwani ziliishia kudondoka chini kama vile ziligonga kwenye chuma kigumu.

“Kuwa makini nyuma yakooo..!!”Aliongea Aishapova kwa kutoa sauti na hio ni mara baada ya Roma kutokezea nyuma ya wale wanawake wenye siraha kwa namna ambayo hawakutegemea kwani ni kitendo cha kufumba na kufumbua.

CRACK!

Sauti yake ilikuwa imechelewa kuchukuliwa hatua kwani mwanamke aliekuwa mwisho kabisa shingo yake ilivunjwa.

Wale waliobaki baada ya kugundua wanapambana na mtu ambaye hakuwa wa kawaida walitupa siraha chini na kujipanga kwa mashambulizi ya kupigana moja kwa moja.

Lakini ilimchukua Roma dakika moja tu kumalizia waliobaki kuwavunja shingo kwa urahisi kabisa na baada ya kummalizia mwanamke wa mwisho wa kizungu alijongea kumsogelea Aishapova.

“Usisogee mbele ..”Aliongea Shedrack Kengeu kwa sauti yake ya kulegea lakini hata hivyo Roma hakuogopeshwa na kitisho chake zaidi ya kumwangalia kwa dharau.

“Handsome wewe ni aina ya adui mwenye nguvu ambaye sijawahi kukutana nae kwenye maisha yangu , lakini naamini bora usingetuchokoza , unaweza ukadhania mpaka sasa umeshinda lakini nadhani hali yenyewe huelewi ilivyo”Aliongea Aishapova kwa Kingereza akijairbu kumzuia Roma kutochukua hatua zidi yake..

Roma alimwangalia huyu mwanamke wa kirusi kwa namna ya kumchunguza na kugundua hakuwa mbaya sana , alikuwa na urembo ambao si haba lakini hakuwa akimfikia Clark wala mke wake.

“Kama hutanipa sababu ya kunishawishi kukuacha hai nitakuua kama wenzako”Aliongea Roma

“Nadhani umefanikisha kumuokoa Mika kutoka kwenye mlipuko , lakini nikuambie tu bora hata ungemuacha akafa kwa mlipuko kuliko tulichomfanyia kwani ni bomu linalotembea”Aliongea

“Unamaanisha nini?”

“Usiku kucha alikuwa akifanya mapenzi na wenzangu hivyo naweza kukuambia hakuwa akifutahia mapenzi anayopewa ila alikuwa akikifurahia kifo chake”Aliongea Aishapova.

“Unamaanisha kwamba kuna dawa mliomuwekea?”Aliuliza Roma

“No!, Techically it’s our new genetic weapon and he is our first black experimental subject”Aliongea akimaanisha kwamba hawajamuekewa dawa lakini kilichofanyika ni kwamba ameingiziwa siraha ya kibailojia kwenye mwili wake na hivyo kuwa mtu wa kwanza mweusi kujaribiwa nayo.

Genetic weapon ni aina flani ya sayansi ambayo inaweza kuingizwa kwenye mwili wa binadamu na kushambulia Genes za mwili ili kuzibadilisha , sasa siraha zinaweza kuwa za aina mbili kuna Genes ambazo zinaweza kutengenezwa kuua watu , lakini kuna zingine zinafanyiwa kwa watu ili kuwafanya miili yao kuwa na uwezo usiokuwa wa kawaida.

Umoja wa mataifa ulipigia sana kelele ili wanasayansi wasijihusushe na uundaji wa Genetic Wepon kutokana na kwamba kama itaingizwa kwenye mwili na seli za mwili na zikashindwa kufanya mchakato wa ‘Mitosis’ basi moja kwa moja mtu hupoteza maisha ni kama ilivyotokea kipindi cha chanjo ya Covid19 watu kuhofia kwamba inaweza kuwabadilisha DNA , sasa hofu yote hio iliibuka kutokana na uwepo wa hizi siraha maarufu zinazofahamika kwa jina la Genetic weapon.

Roma alikuwa akijua dunia ilikuwa imefanikisha kwa kiwango kikubwa sana katika udhalishaji wa hizi ‘genetic weapon’ , kwa mfano alikuwa akifahamu kuna baadhi ya siraha hizo ambazo zimetengenezwa kwa ajili ya kuifanya miili ya binadamu kuwa dhaifu kwa miaka kadhaa na hatimae kufa ,ni moja ya mipango ambayo siku zote alikuwa akiitafsiri kama ya kishetani kwani aliamini ilikuwa na lengo la kuua watu na kupunguza idadi ya watu ndani ya uso wa dunia, licha ya Umoja wa mataifa kukemea juu ya hizo siraha za kibailojia lakini ukweli ni kwamba ilikuwa geresha tu kwani kila uchao zinatengenezwa na nyingine zikihifadhiwa lakini nyingine mpaka sasa zipo kazini kuingiziwa kwenye miili ya binadamu kwa ajenda za muda mrefu , lakini hata hivyo mambo kama hayo yanaishia kubakia kuwa fununu kwani hakuna ushahidi wa moja kwa moja.

“Kwa mwonakano wako Mr Roma naamini tayari ushafahamu ninachomaanisha , hivyo kama hutoweza kupata ‘Genetic Code’ ndani ya muda basi Mika anakwenda kufa ndani ya masaa 72 yajayo kama seli za mwili wake zitashindwa kupitia mchakato wa mitosis, lakini kama unataka kumuokoa basi nakushauri ufanya maamuzi sahihi”Aliongea Aishapova.

“Ndio Mr Roma anachozungumza Aishapova ni sahihi kabisa , unaweza kutuchukulia wepesi , lakini labda nikuambie kuna watu wakubwa sana ndani ya Tanzania na mataifa makubwa ambao wapo nyuma yetu ndio maana mpaka sasa hivi licha ya uwepo wetu ndani ya Tanzania maisha yetu yameendelea kuwa ya amani licha ya kupigwa vita na watu wengi”Aliongea wa kujitapa

“Bto huwezi kunifanyia hivyo, ninakwenda kukuua sasa hivi”Aliongea Mika ambaye muda wote alikuwa amejificha katikati ya watu na kumvaa Shedrack kwenye shingo lakini ni kama alitegemewa kwani Shedrack alisogea pembeni na kumfanya Mika kupita mzima mzima na kudondoka chini.

“Mika wewe ni mjinga , unafikiri kutaka kunishambulia kutakuponya”Aliongea na kumfanya Mika kuwa na wasiwasi wa afya yake.

“Mr Roma ni kweli jana nilikuwa na hawa wazungu lakini sikufanya chochote nao zaidi ya mabusu ya rasharasha”Aliongea na kumfanya Roma amuangalie Mika na kuona hamnazo kabisa na ilionekana wazazi wamemuharibu sana.

“Acha kunidhalilisha, kukufuata mwenyewe mpaka hapa kumenipotezea muda mwingi na kama sio kwa ajili ya Benadetha ningekuacha ufe tu”

“Mr Roma naomba unisaide tafahdari sitaki kufa..’Aliongea huku akianza kutokwa na machozi huku watu waliokuwa wamewazunguka wakishindwa kusogea karibu zaidi ya kuangalia kwa mbali na kushindwa kusikia vizuri maongezi.

Roma alimwangalia Mika huku akionekana kufikiria kwa muda , aliona kama Aishapova alichokuwa akiongea ni sahihi basi kama atamuua huenda ikaleta shida kwa upande wa Mika, hivyo kipaumbele kwanza aliamini ni kuhakikisha anakuwa salama na baada ya hapo lazima atafute namna ya kumuua Aishapova , aliamini lazima kuna mpango unaendelea hivyo lazima atajaa kwenye kumi na nane zake.

“Mr Roma naomba utuache hai nitahakikisha baada ya kuwa salama dawa inayoweza kumponyesha Mika inamfikia kwa muda muafaka , nitatuma vijana wangu”Aliongea Shedrack kwa wasiwasi akihofia Roma anaweza kuwaua kama alivyoua wengine.

“Niandalieni gari niondoke hili eneo, mmelipua gari langu kwa bomu hivyo mnatakiwa kunilipa la sivyo siwezi kuwasamehe”Aliongea Roma baada ya kuwaza kwa muda na Shedrack alijikuta akivuta pumzi za ahueni.

“Kalete ile Audi R8 gereji tumpatie Mr Roma”Aliongea kwa kuamrisha mmoja wa mhudumu aliekuwa mita kadhaa kutoka waliposimama.

“Sitaki tena Audi wala BMW nataka gari nzuri na Brand tofauti”Aliongea.

“Tunayo Lexus ES toleo la mwaka huu Mr Roma , ni zuri na linakufaa”Aliongea.

“Okey fanya haraka liletwe hapa la sivyo nitabadili maamuzi”Aliongea Roma na Shedrack Kengeu alimpa ishara muhudumu kwenda gereji kuleta gari aina ya Lexus haraka haraka.
 
SEHEMU YA 442

Roma mara baada ya kubeba bunduki aliangalia kama ilikuwa na risasi na baada ya kuona zipo za kutosha alimgeukia Mika.

“Dogo unajua kutumia bunduki?”Aliuliza Roma na kumfanya Mika kutingisha kichwa kwamba alikuwa akijua kutumia na Roma alitegemea hilo kwani alikuwa akielewa kama Samweli Nguluma ambaye ni baba yake Benadetha alikuwa bosi wa kundi la kiharifu la ZoaZoa basi Mika asingekosa mafunzo muhimu ya namna hio.

“Shika lipiza kisasi kwa kumuua Shedrack”Aliongea Roma baada ya kumrushia ile siraha huku akiwa na uso uliojaa usiriasi.

“Lakini Bro kama nitamuua dawa nitapataje?”Aliuliza huku akionyesha wasiwasi.

“Wewe niamini mimi dogo”Aliongea Roma.

Baada ya Kengeu kusikiliza yale maongezi jasho lilianza kumtoka ,kwa upande wa Aishapova licha ya kwamba hakuwa akijua lugha ya kiswahili lakini kwa picha iliokuwa ikiendelea alijua ni kipi kinaenda kutokea , lakini aliamini Roma hakuwa mjinga mpaka kumuua kwani ni kweli kabisa Mika alikuwa amewekewa sumu ambayo inakwenda kushambulia vinasaba vya damu.

“Mika fikiria vizuri ukiniua mimi huwezi kupona tena , nimeyashikilia maisha yako”Aliongea Kengeu kwa namna ya kujitetea huku hata sauti yake iliolegea ikianza kutoa mikwaruzo.

“Mika usimsikilize huyo nina kuhakikishia afya yako itakuwa sawa , lipiza kisasi kwa kumpiga risasi tuondoke”Aliongea Roma na kauli yake iliogopesha baadhi ya watu.

Mika ijapokuwa baba yake amemfundisha kutumia siraha , lakini kwenye maisha yake hakuwahi kuua kabisa na siku hio kwake ni kama inakwenda kuwa mara ya kwanza , mikono yake ilimtetemeka mno.

“Dogo acha kupoteza muda , muue tuondoke”Aliongea Roma huku upande wa Aishapova akitamani kujinasua , lakini kutokana na uwezo wa kimaajabu aliokuwa nao Roma , aliona hata kama atakimbia basi angekamatika tu na huenda angekufa hata kabla hajatoweka hivyo aliishia kusubiri kuona hatima yake..

“Paaa!!.. Paa.!!.”

Risasi mbili zilitoka kwenye siraha alioshikilia Mika na kumpiga Shedrack Kengeu kifuani na kudondoka palepale, hakuweza hata kujitetea kabisa, lilikuwa ni tukio ambalo lilifanya watu wachache waliobakia hapo ndani kukimbia.

Mika alidondoka chini huku akianza kuhema kwa tabu , ilikuwa ni kama mtu ambaye amekimbia maili nyingi sana.

Kuua mtu kwa mara ya kwanza ni jambo kubwa sana kwenye maishaya binadamu , lakini ukifanikisha kuua huwezi kuwa mtu wa kawaida tena , hio ndio laana inayotokana na kumuua binadamu mwenzio.

“Vipi dogo mbona unatapika?”Roma alijikuta akitamani kucheka kwani mara baada ya Mika kumaliza kumpiga Shedrack Kengeu kwa risasi alianza kutapika, lakini hata hivyo alishindwa kujibu zaidi ya kuanza kutoa kilio palepale..

“Nadhani unaona kwamba kuua sio jambo rahisi kwenye maisha ya binadamu Dogo, umesema baba yako amempiga mama yako risasi si ndio?”Aliuliza Roma na Mika alitingisha kichwa kuitikia.

“Kama wewe umeona ugumu wa kumuua mtu ambaye huna ukaribu nae sana , je unahisi baba yako amejisikiaje kumuua mama yako ambaye ameishi nae kwa muda mrefu , mwanamke ambaye amempenda?”

“Viba.. vibaya..”Aliongea huku akitetemeka akiangalia maiti ya Shedrack Kengeu iliokuwa ikiloewa kwenye dimbwi la damu.

“Unachojisikia sasa hivi mara baada ya kumuua adui yako ambaye amehatarisha maisha yako ni zaidi ya mara kumi anachojisikia baba yako mara baada ya kumuua mke wake , naamini kuna sababu ambayo imemfanya kumuua , tofauti na kukimbilia huku kwenye hoteli iliojaa mambo ya ajabu ungetafuta sababu kwanini mama yako mzazi kapigwa risasi, kuja eneo hili ni kuharibu maisha yako ya baadae”Aliongea Roma kwa kufoka.

“Bro nimekuelewa sitorudia tena kujichanganya na maswala kama haya…”Aliongea kwa namna ya kujitetea na Roma alimgonga gonga kwenye mgongo kumtuliza.

Roma mara baada ya kuangalia alipokuwa amesimama Aishapova aligundua ameshatoweka hata hivyo hakutaka kujihangaisha nae.

“Bro nawezaje kupona sasa , yule mwanamke kakimbia?”

“Kuna mtu naamini anaweza kukusaidia kukutibu , kuhusu Aishapova nikimuua sitopata majibu ninayotaka , kama ameweza kutengeneza siraha za kibailojia na kuingia nazo Tanzania naamini kuna jambo kubwa linaendelea”Aliongea Roma na kumfanya Mika kushangaa kidogo lakini Roma hakutaka kuendelea kubaki nani ya hilo eneo , alimpa ishara ya kuingia kwenye gari na kuondoka eneo hilo..

Ukweli Roma alitaka kwenda kuthibitisha kama kwenye mwili wa Mika kuna hiko kinachoitwa ‘Genetic weapon’ na mtu pekee ambaye angeweza kuthibitisha hilo ni Profesa Clark.

Roma alipokuwa anaingia eneo la Mapinga alimpigia simu Profesa Clark ili kujua yupo wapi na alijibiwa kwamba yupo sehemu inayoitwa Makongo juu , sehemu ambayo ndio atakapo ishi kwa muda wote atakaokuwa hapa Tanzania.

Roma ilibidi amueleze Profesa Clark juu ya mtu aliekuwa nae ambaye alikuwa akihitaji msaada kutoka kwake ndani ya masaa 72 na baada ya Profesa Clark kumsikiliza kwa umakini alimwambia aje moja kwa moja mpaka nyumbani.

Ndani ya dakika chache tu aliweza kufika eneo la Makongo Juu na haikumpa shida kuipata nyumba ya profesa kwani nyumba zote za jiji la Dar zilikuwa na mfumo wa anuani ambao umeunganishwa moja kwa moja kwenye GPS hivyo aliendesa mpaka nje ya jumba lenye geti na ukuta mrefu uliozungushiwa nyaya za umeme na kupiga honi na geti lilijifungua lenyewe.

Aliingiza gari mpaka ndani na kwenda kuliegesha mbele kabisa na mlango wa kuingia na kisha akamwamuru Mika kushuka..

Lilikuwa jumba kubwa mno la kifahari la ghofora mbili , lenye bustani nzuri zilizozunguka pande zote na kuifanya nyumba kuwa katikati.

Mika alijikuta akipagawa mara baada ya mwanamke mrembo wa kizungu kutoka ndani ya nyumba hio

“Roma hakika unajua kunifanya niwe bize , nipo hapa kwa siku mbili tu lakini tayari ushanitafutia mtu wa kumfanyia majaribio”Aliongea kwa Kingereza huku akimwangalia Mika ambaye alikuwa akimwangalia kwa namna ya kushangazwa na uzuri wake

“Nadhani siingilii pia ratiba zako zingine na kampuni isije nikakosana na mke wangu”

“Hakuna cha kuniweka bize , ni kazi nyepesi sana ambayo mwanafunzi wangu yoyote yule angeweza kuifanya , lakini kwasababu sikutaka Catherine na Rothchild kunifanya bidhaa kwa faida yao ndio maana nipo hapa Tanzania , muda huu huenda ningekuwa nimejichimbia ndani ya maabara nikifanya majaribio, lakini hata hivyo najisikia vizuri ninakuona mara kwa mara”

“Huko kuniona mara kwa mara ndio kunanisababishia matatizo na familia yangu”

“Ooh! tena nimekumbuka mkeo mchana alionekana alikuwa na hasira sana kiasi ambacho kiliniogopesha na sio mimi tu kila mmoja alimuogopa hata kumsogelea na kumuongelesha , sijawahi kukutana na mwanamke mrembo lakini kauzu kam mke wako”Aliongea huku akicheka.

“Haha..nitajitahidi kwenda kumuweka sawa , Unaweza kuchukua damu yake hapa hapa au ni mpaka maabara?”Aliuliza Roma.

“Hapa hapa panafaa zaidi, Kuna kitu nataka pia nikuonyeshe ndio maana nilikuambia umlete moja kwa moja , nifuateni”

Walitembea hadi kwenye mlango uliokuwa kushoto baada ya kupita sebuleni na kuingia kwenye chumba kikubwa ambacho kilionekana kama ofisi ya kujisomea kwani kilikuwa na mpangilio wa vitabu vingi pamoja na meza na tarakishi, kwa haraka haraka Roma aliamini huenda Clark alikuwa akisoma kwani kwenye meza kulikuwa na kitabu ambaco kimefunguliwa, lakini pia alijiambia huenda nyumba hio inakaliwa na zaidi ya mtu mmoja.

Profesa Clark alichukua kadi kama zile za benki kwenye meza , lakini hii ilikuwa na utofauti kidogo ni kadi ambayo ilikuwa na michoro myeupe kama ya radi rangi ya silver upande mmoja , baada ya kuichukua alisogea mpaka mwanzo wa kabati upande wa kulia mwa chumba na kusogeza vitabu na kilionekana kifaa kama simu iliobandikwa ukutani na alichukua ile kadi na kuibandika juu yake kwa sekunde tano tu , kulisikika mlio wa lock za mlango kuachiana na hapo upande mmoja wa kushoto wa kabati ulionyesha kufunguka na kuacha uwazi na kumfanya Roma kuguna.

“Hii nyumba imekaa kijasusi jasusi inaonekana sio ya kawaida ,inaonekana ina mambo mengi ya siri”Aliongea Roma.

“Sio wewe tu , hata mimi nilishangazwa pia na hii nyumba, lakini inaleta maana kwani ni nyumba iliokuwa chini ya umiliki wa siri wa Profesa Shelukindo”

“Unamaanisha nini?”

“Dear Roma naona upo kwenye mshangao mkubwa, katika maisha yangu ya kimasomo nadhani mimi ndio nilikuwa mwanafunzi wa pekee kutoka kwa Profesa Shelukindo na alinipenda haswa kutokana na kwamba tulikuwa tukifanana kwenye mambo mengi sana likija swala la taaluma ya uvumbuzina hilo linanifanya kumpa heshima yake”

“Kuna siku moja wakati nawasiliana nae alianimbia kama nitabahatika siku moja kutamani kuishi Tanzania na yeye hayupo hai basi kuna mtu napaswa nimtafute, sikuwahi kumzingatia sana kwani licha ya kuwa mwalimu wangu lakini pia alikua mtani wangu , hivyo hata baada ya kuniambia hivyo sikuweza kuchukulia sana jambo hilo kwa usiriasi mpaka leo ulivyo ondoka kule chuoni”Aliongea na kisha akaendelea

“Roma unajua kwanini mara baada ya kusikia kifo cha Profesa Shelukindo nilifanya safasi siku hio hio?”

“Kwasababu ni mwalimu wako na mlikuwa mkishirikiana kwenye mambo mengi”Alijibu Roma.

“Ukiachana na kushirikiana kwetu , Profesa Shelukindo aliniahidi nitakuja kumrithi kazi zake zote na kuendeleza kile ambacho hakukikamilisha , unaweza kusema kwamba alitaka kuniachia mikoba yote ya tafiti zake na kuendeleza , lakini nilihuzunika sana mara baada ya kugundua alikufa bila hata ya kutimiza ahadi yake , nilikuwa ni mwenye shauku ya kujua ni hatua gani aliokuwa amefikia katika maswala ya sayansi , lakini nilijikuta nikirudi Uingereza nikiwa mwenye huzuni”Aliongea Profesa wakiwa wamesimama kwenye chumba hicho pasipo ya kuingia, Roma alishangazwa na maneno hayo.

“Clark mbona unaongea ukiwa umebadilika ghafla na furaha kutoweka machoni mwako?”

“Kwasababu ninayofuraha na huzuni kwa wakati mmoja, lakini huzuni imenizidia kwa wakati huu”

“Kwanini?”

“Kwasababu niliishi kwa huzuni kwa kuamini Profesa Shelukindo hakutimiza ahadi yake , lakini ukweli ni kwamba ahadi yake aliitimiza , huzuni yangu ni juu ya muda wote ambao niliupoteza kwa kumlaumu kwa kutoikamilisha ahadi yake kwangu”Aliongea na pale pale hakumpa Roma nafasi ya kuuliza swali , alisukuma mlango na akatangulia kuingia kisha akafuatia Roma halafu Mika.

Roma aligundua mlango huo ulikuwa ukiwaruhusu kwenda chini kwenye vyumba vya ardhini.

Baada ya kufika chini Clark alitumia kadi ileile kufungua mlango mwingine na ulipofunguka ndipo Roma alipo onyesha mshangao wake.

********

MASAA MACHACHE NYUMA

Ni mara baada ya wageni rasmi kumaliza kupata chakula cha mchana , ikiwa ni muda wa saa tisa za adhuhuri, Profesa Clark alionekana kupiga picha na wanafunzi mbalimbali ambao ni wahitimu ndani ya chuo hicho.

Wanafunzi waliokuwa wakihitaji kupiga picha nae walikuwa wengi hivyo ilichukua zaidi ya lisaa limoja mpaka pale makamu mkuu wa chuo alipomfuata na kuondoka nae kitendo ambacho pia kilimpa ahueni Profesa Clark kwani alikuwa ashaanza kuchoka.

Muda huo Edna alikuwa ashaondoka mara baada ya kufuatwa na Innocent dereva wake wa kampuni hivyo Profesa na yeye alitakiwa pia kurejea hotelini kwake kusubiria taratibu zingine za kuonyeshwa mahali ambapo angetakiwa kuishi kwa muda wote atakaokaa hapo Tanzania.

“Profesa samahani najua umechoka sana , lakini kuna daktari mmoja ambaye anahitaji kuonana na wewe japo kwa dakika chache”Aliongea Bi Asha Abdulah ambaye ndio makamu mkuu wa chuo cha UDSM akiwa na yeye pia profesa wa chuo hicho.

“Profesa kwasababu wewe ndio umeomba nadhani atakuwa ni mtu muhimu ninaepaswa kuonana nae”Aliongea Profesa Clark huku akitabasamu.

“Usije ukanifikirai vibaya Profesa lakini ukweli ni kijana wangu , hivyo katumia ukaribu kupata nafasi ya kuonana na wewe , alionyesha hali ya kuwa na jambo muhimu hivyo niliona nikuelezee ufanye maamuzi , anafahamika kwa jina la Dr Issai Singano”Aliongea.

“Dr Issai Singano!!!!”Alimaka

Hili jina sio geni kwangu nililisikia wapi?”Alijikuta akijiwazia kwenye kichwa chake

“Ndio Profesa kwa muonekano wako naamini ushawahi kusikia jina lake , hata yeye alianiambia kama nitakutajia jina lake utamfahamu”Aliongea na kumfanya Profesa Clark kusimama na kufikiria kidogo , jina la Issai singano halikuwa geni kwake na baada ya kufikiria kwa dakika kadhaa aliweza sasa kupata mwanga na aijikuta akimwangalia Makamu Mkuu wa chuo kwa namna ya kumshangaza.

“Oh! My God , nilishasahau kabisa kuhusu hili jina , nimekuwa mjinga sana nimewezaje kusahau”Aliwaza tena huku akionekana anajilaumu.

“Makamu asante sana , nadhani nitaonana nae kwenye gari yangu haina haja ya kwenda mpaka kwenye ofisi yako”Aliongea Profesa Clark huku mwonekano wake ukibadilika na kuwa na uchangamfu lakini na shauku kwa wakati mmoja.

Bi Asha Abdullah mwenyewe alishangazwa na mabadiliko ya Profesa Clark ,wakati alipoombwa msaada na Dr Singano alisita sita , lakini kwa kubembelezwa sana alikubali na hio yote ni kutokana na ukaribu wa familia ya Dr Singano upande wa wakwe zake na familia yake.

Zilipita kama nusu saa zingine ilibidi Profesa kuagana na baadhi ya viongozi na watu mashuhuri ndani ya chuo hicho ndipo alipoweza kuelekea kwenye gari yake iliomleta na kabla hata hajaingia ndipo aliposogelewa na mwanaume mwenye mwonekano wa kijana mweusi mrefu wa saizi ya kati alievaa suti ya rangi nyeusi.

“Dr Issai Singano Right?”Aliongea Profesa mara tu baada ya kusogelewa na huyo mwanaume.

“Yes Professor , Nice to meet you”Aliongea na wakapeana mkono huku Clark akionyesha hali ya furaha mara baada ya kuonana na Dr Singano.

“Dr Singano nadhani tunayo mengi ya kuzungumza , je umefika hapa na gari?”Aliuliza Profesa na Dr alimuonyeshea upande wa pili gari yake aina ya Range rover V8 .

Kwasababu gari iliomleta Profesa Clark mpaka hapo ilikuwa ni ya hoteli aliofikia basi ilibidi ampe dereva maelekezo ya kutangulia na yeye ataongozana na Dr Singano na kuingia kwenye garri yake.

“Nikiri niliposikia jina lako nilipata mshituko , Mtu alienitajia jina lako miezi michache iliopita ni Profesa Shelukindo , Mwalimu wa heshima kwangu, kwa maelezo yake aliniambia nikutafute kama nitafika Tanzania lakini nikasau kabisa kutokana na siku tuliokuwa tukiongea tulikuwa katikati ya kutaniana”Aliongea Profesa Clark.

“Ndio hata Profesa pia alishawahi kunipatia maelekezo maalumu , ambayo aliniitaji niyafikishe kwako”

“Kweli!! ,Profesa Shelukindo alikuwa nani kwako?”

“Sijui niwekeje ila naweza kusema ni ndugu yangu wa mbali kwa upande wa bibi yangu mzaa baba, niliweza kukutana nae kwa mara ya kwanza kwenye msiba wa baba yangu mzazi na kuanzia hapo ndio ukaribu kati ya mimi na Profesa ulianza”Aliongea na kisha alivuta mkoba uliokuwa siti ya nyuma na kuufungua na kuibuka na Notebook kubwa ya rangi nyeusi na kisha akamkabishi Profesa Clark.

‘Hio ni Diarybook yake ambaye aliniambia nikupatie, lakini pia alinipa maelekezo kama ukifika nchini nikupeleke kwenye nyumba yake ambayo alikuwa akipendelea kupumzika”Aliongea na kumfanya Clark kushangaa lakini alifungua ile Diary taratibu taratibu na ilionekana ilikuwa na maandishi mengi ambayo yalionekana yapo kisayansi zaidi , alisoma baadhi na alionekana kuyaelewa lakini hakuona kitu cha maana zaidi , lakini alipofika katikati ndipo alipoona kadi katikati ya Notebook hio na aliinua juu na kutoa macho , alionekana alikuwa akiijua.

“Nipeleke kwenye nyumba yake ya mapumziko”Aliongea Profesa na Dr Singano hakuuliza mara mbili na aliwasha gari na wakaondoka eneo hilo kwa haraka na ndani ya madakika kadhaa ndipo walipokua kufika Makongo Juu.

********

Ilikuwa ni maabara ndogo ya kisasa , ijapokuwa haikuwa na vitu vingi lakini ilikuwa kwenye mpangilio mzuri sana na ilikuwa na vifaa muhimu vyote.

Kwa maelezo ya Profesa Clark ni kwamba maabara hio ilikuwa ikitumiwa na Profesa Shelukindo mara chache sana, lakini kubwa zaidi ni kwamba ilikuwa imebeba asilimia miamoja ya taarifa zote zilizokuwa zikihusiana na tafiti zote ambazo Profesa Shelukindo amefanya kwenye maisha yake mpaka alipofikia.

Kwa maana rahisi ni kwamba kila kilichokuwa humo ndani alielengwa kukimiliki ni Profesa Clark.

Roma alishangazwa na uwezo mkubwa wa Profesa mpaka kutunza siri zake za tafiti na kuweka mpango ambao ulikuwa madhubuti kiasi kwamba kumfikia mlengwa , lakini swali lingine liliibuka.

“Kama umesema alikusudia wewe kupata taarifa zake kupitia maabara hii , je ni kipi ambacho Yan Buwen alipata kutoka kwake?”

“Hilo siwezi kujua , lakini nilichokipata humu naweza kusema kwamba Profesa alikiandaa kwa ajili yangu na ni kazi zake zote ambazo amefanya miaka kwa miaka pale aliposhia lakini pia matarajio yake ya mbelemi”Ilishangaza sana , lakini hata hivyo Roma hakutaka kuuliza sana.

Mika ilibidi achukuliwe damu yake hapo hapo kwenye hio maabara ili Profesa kuifanyia majaribio na baada ya kazi hio kumalizika wote walitoka nje huku Profesa akiahidi kufanyia kazi ndani ya muda mfupi.

“Lakini Roma vipi kama nikishindwa kupata Genetic Codes na kuweza kudhalisha Antidote yake ndani ya masaa sabini na mbili maana maswala yanayohusiana na DNA yanahitaji muda”Aliongea Profesa.

“Clark nakuamini utapata majibu ndani ya muda mfupi, hivyo usiwe na wasiwasi na wewe fanya kazi yako”Aliongea Roma na Profesa Clark alivuta pumzi na kuzishusha.

“Okey nitajirahidi kadri ya uwezo wangu ili kabla masaa yote hayajaisha niwe nimepata majibu”

Roma ilibidi awasiliane na Benadetha na kumuambia yupo na kaka yake aje kumchukua.

Nyumbani kwa Benadetha ni Tabata hivyo Roma ilibidi wakubaliane na Benadetha wakutane Mwenge.

“Vipi yule rafiki yako?”Alivunja Roma ukimya akimuulizia Rufi.

“Bro unamaanisha yule mrembo Rufi?”

“Ndio”

“Yule nilimsaidia mpaka kununua Apartment kule kwa Warioba , lakini hakutaka hata kunikaribisha mara baada ya kuhamia , hivyo nilimuacha jana ileile ndipo nilipoanza safari ya kwenda Bagamoyo”Aliongea Mika na kumfanya Roma kuitikia kwa kichwa.

Baada ya dakika chache tu Benadetha alievalia suruali na blazier aliweza kufika eneo la Mwenge akiendesha gari aina ya Harrier.

“Roma naomba unisamehe kwa kusumbua , sikuwa na jinsi baada ya baba kunilazimisha..”Aliongea Benadetha kwa upole.

“Usijali Benadetha wewe ni mfanyakazi wa kampuni ya mke wangu , hivyo kukusaidia ni wajibu wangu pia , ukiwa na mawazo huwezi kumsaidia Edna kwenye kazi zake vizuri”Aliongea Roma na Benadetha aliitikia kwa kichwa.

Roma baada ya kumkabidhi Mika kwa dada yake huku akimpa maelekezo mengine kuhusu kilichomkuta , basi aliagana nao na kuanza kuitafuta safari ya kurudi nyumbani kutatua mgogoro wake na mke wake, lakini ndio muda ambao simu yake ilianza kuita mfululizo na alipoangalia jina aligundua ni Mage.

“Roma una tabia mbaya sana wewe mwanaume?”

“Babe kwanini unaongea hivyo?”

“Acha kujifanyisha hujui, yaani wewe mwanaume umeshindikana”

Roma aliijikuta akitabasamu kwa uchungu na kugundua kosa alilolifanya , tokea alivyomuacha Mage kule hotelini hakuwa amemtafuta kabisa kujitolea maelezo kwanini Video yake ya ngono ilikuwa kwenye kile chumba cha mdukuzi.

Ilikuwa ni saa moja na nusu kwenda saa mbili za usiku na Roma ilibidi tu amuambie Mage waweze kuonana usiku huo ili aweze kumwelezea kilichotokea, alijua alitakiwa kuwahi nyumbani kumpoza Edna , lakini pia alikuwa na deni kwa Mage.









SEHEMU YA 443.

Mage ni kama alipata nafasi ya kumshikilia Roma usiku mzima na hata pale kulipokucha Mage alimwambia Roma amsindikize Mlimani City kununua baadhi ya nguo za kufanyia mazoezi na Roma kwasababu hakuwa ametumia mua mwingi na mrembo huyo ilibidi tu akubaliane nae.

Walitoka pamoja hotelini na kwenda mpaka Mlimani City ambapo Mage alinunua mahitaji yote alioyahitaji akisaidiwa kuchagua na Roma na mpaka wanakuja kutoka eneo hilo ilikuwa ni saa nne za asubuhi.

Roma hakusahau pia kununua zawadi kwa ajili ya mke wake , aliamini ingekuwa rahisi kwake kuomba msamaha akiwa na zawadi.

Baada ya kumpeleka Mage hadi nje ya nyumba yao hakutaka kuingia ndani zaidi ya kuondoka huku mpango wake ni kunyoosha moja kwa moja mpaka kwenye kampuni ya mke wake , kwani aliamini hata kama angeenda muda huo nyumbani asingemkuta.

Roma mara baada ya kufika aliweza kukutana na Recho ambaye alikuwa amekumbatia mafaili na alionekana alikuwa akitoka kwenye ofisi ya bosi wake.

“Roma upo hapa kwa ajili ya Bosi?”Aliuliza Recho mara baada ya kumuona Roma.

“Ndio”

“Mhmh nikajua umekuja kwa ajili yangu”

“Hehe.. hio ni kazi ya boyfriend wako sio ya kwangu”Aliongea Roma.

“Mhmh… ila nakushauri ni bora ukaja muda mwingine maana bosi anaonekana kuwa ni mwenye hasira mno mpaka nimeshindwa kua na amani, nilijikuta nikiwa natetemeka kama nipo chumba cha barafu”Aliongea na kumfanya Roma kufikiria kidogo

“Kama tunaishi pamoja sina jinsi zaidi ya kutafuta namna ya kumpoza, jana ni kweli nilikosea lakini ilinipasa kutoa msaada pale ulipokuwa ukihitajika, lakini kutokurudi nyumbani daa..! nitajua bwana”Aliwaza Roma kwenye kichwa chake.

Roma mwenyewe alijishangaa mno kwenye maisha yake hakuwahi kumuhofia mwanamke , kwa mfano usiku wa jana aliweza kuyamaliza kirahisi na Mage , lakini likija swala la Edna alionekana kuwa na hofu mno na kuona hakika maisha yake yamepiga hatua kubwa.

Roma alisogelea mlango wa ofisi ya CEO huku akisikilizia sauti hafifu ya AC iliokuwa ikipuliza na kisha akavuta pumzi na kugonga mlango.

“Come in”Sauti hafifu iliitikia kutoka ndani na Roma alisukuma mlango na kuingia ndani huku akifikiria namna ya kumlegeza Edna.

“Ooh jamaniii.. haijalishi ni mara ngapi namuona CEO akiwa ameketi kwenye kiti chake cha ubosi , lakini niseme kwamba uzuri wake ni wenye kuyawasha macho yangu muda wote, ni hasara kweli kweli uzuri kama huo kuuficha ndani ya hii ofisi , dunia inahitaji uzuri wako na hata kuwa balozi wa bidhaa nyingi za urembo huenda zingeuza sana”

Wanawake siku zote wanapenda kusifiwa kuhusu mwonekano wao hata kama mazingira hayaruhusu kufanya hivyo na ndio mbinu pekee ambayo Roma aliona inaweza kumlegeza mke wake kidogo, Roma alijiambia pasipo ya kuwa Chawa asingetoboa , lakini licha ya hivyo aliona kabisa mbinu yake imegoma kwani mwonekano wa Edna ulikuwa wa aina yake.

Edna hakuinua kabisa macho yake kumwangalia zaidi ya kuendelea kupekua makaratasi yaliokuwa kwenye meza yake , ni kama alikuwa peke yake ndani ya ofisi.

“Tafadhari zungumza shida yako iliokuleta”Aliongea Edna kwa sauti kavu na kumfanya Roma kukuna kichwa.

“Aah, Edna najua unafanya mazoezi kila siku asubuhi hivyo leo nimepitia dukani kukunulia zawadi”

“Director Roma if you don’t have pressing matters in hand please leave my office”Aliongea Edna kwa Kingereza na mpaka hapo Roma aliona kazi anayo , mpaka Edna akikubadiishia lugha inamaanisha kwamba kuupata msamaha isingekuwa jambo jepesi.

“Okey ngoja tusizungumzie hili sasa hivi , Edna najua umekasirishwa na kitendo changu cha jana kukuacha peke yako lakini kulikuwa na dharula kweli , nilihitajika kuyaokoa maisha ya mtu”

“Ni vizuri kusikia hivyo Mr Superhero, najua kabisa ujasiri wako kati ya wanaume wote ambao nimekutana nao na imenishangaza sana kuweza kuwa na mwanaume wa aina yako, lakini hilo sio tatizo kwangu kwani sihitaji sana ujielezee , ni bora ukajizuia ili kuyatoa kwa mtu ambaye ameathirika”

“Halafu naamini wewe ni mwanaume ambaye huna haja ya kujielezea kwa mwanamke licha ya kwamba uliniacha mwenyewe bila ya kujali watu walichukuliaje lakini pia ukalala nje kwa raha zako , usijielezee maana nahisi utakuwa ni mwenye kutia huruma”

“Edna sio kama unavyofikiria , yaani usiku wa jana ulikuwa ni wa kashikashhi sana , Benadetha mdogo wake alipatwa na matatizo makubwa mno na ilinipasa kumsaidia, ni jambo ambalo lilinifanya nichukue muda mwingi kushughulikia, hivyo nikakosa muda wa kurudi nyumbani, lakini nashukuru nimeweza kufanikisha na kumrudisha akiwa salama salimini”

“Okey endelea nakusikiliza..”Aliongea Edna huku akimwangalia Roma kwa macho yasio na furaha.

“Ndio nishamaliza , ilikuwa ni kama hivyo”

“Okey vizuri sana , ni jambo zuri kwa binadamu kusaidian , hivyo Mr Roma Ramoni naomba utoke kwenye ofisi yangu”Aliongea na Roma kwa muonekano wa Edna aliona akijitetea zaidi ni kuharibu.

“Edna vipi hii zawadi ambavyo nimekuchukulia”

“Sihitaji”Aliongea na Roma aliishia kuachama na kutoka nje kinyonge.

Edna alikuwa na hasira kweli kwanza kabisa yeye ndio aliependekeza kwenda na Roma kwenye sherehe ili kwenda kujigamba kwa kuonyesha ameolewa , lakini kabla hata sherehe haijaisha akaachwa mwenyewe tena bila hata ya usafiri kadhia iliomfanya kupiga simu kufuatwa , lakini sio kuachwa kwa sababu nyingine bali ni kwasababu ya mwanamke kapiga simu , lakini haya mwanamke huyo kamshikilia mume wake mpaka asubuhi na mume wake pasipo kujali hata kutoa taarifa..

Wivu na hasira vilimfanya kutamani kupasua tarakishi yake aliokuwa akiitumia muda huo , uwepo wa michepuko ulikuwa ukimtesa , lakini licha ya hivyo mume wake haonyeshi kabisa hatia, kwanini asiwe na hasira.

Roma baada ya kutoka ofisi ya mke wake na mfuko wa zawadi alionunua ,hamu ya kwenda kazini kwake ilimwishia hivyo moja kwa moja alitoa maagizo kwa wanajeshi wa The Eagles kuhakikisha usalama wa Profesa Clark.

Roma mara baada ya kurudi aliweza kumkuta mama yake akitengeza bustani kwa kupanda mbegu za maua na kumwangalia , Blandina mara baada ya kumuona Roma ndio kwanza anaingia alijikuta akishindwa kuelewa moyo wake na kujiambia ni kheri kumpa Roma vidonge vyake.

Kitendo cha kutokurudi kwake jana usiku kilimfanya yeye na Bi Wema kuwa katika hali zisizoelezeka .

“Roma nini kilitokea jana na ukashindwa kurudi , kiasi cha kumfanya Edna kuwa na sura ambayo tulikuwa tukianza kuisahau, Usiniambie umetafuta mwanamke mwingine wewe mtoto mtukutu? Ndio sababu hukurudi”Aliongea Blandina.

“Mama sio hivyo , kwanini kila mtu anaona kila mwanamke ninaekutana nae ni mwanamke wangu”

“Sasa uniambie kwanini Edna anaokana kukasirika mno?” Aliongea na ilibidi Roma aeleze kilichotokea.

“Sasa kwanini ukaamua kulala huko huko na usirudi numbani hata kama ulichelewa, Roma unavyofanya sio vizuri mkeo anajaribu kujitahidi kuweka ukaribu lakini wewe kutwa kumchokoza , utaniua kwa presha mimi kwa makosa yako”

“Nilikosea najua lakini niliweka kipaumbele kuomba msamaha kwa kwenda ofisini kwake , lakini hakutaka hata kuniangalia usoni licha ya kumletea zawadi”

“Zawadi gani umempelekea?”

“Nilimnunulia Headphone ambazo zingemsaidia kusikiliza mziki akiwa anachukua mazoezi”

“Mh bora angalau ukampelekea kile anachopenda kuliko kwenda kumpoza na zawadi ya namna hio , hata ni mimi ningekataa,Yaani Roma jamanii”Aliongea Blandina huku akirudia kazi yake.

Roma siku yote alikaa nyumbani huku akiisikiliza mziki kwa kutumia Headphone zake alizomnunulia Edna na zikakatiliwa, muda wa chakula cha mchana aligundua Lanlan hakuwepo pamoja na Qiang Xi.

“Mama Lanlan na Qiang Xi siwaoni hapa?”

“Babu yako kaja kumchukua na kuondoka nae na kasema atamrudisha kesho ilinibidi nimpigie Edna simu kumpa taarifa maana alikuwa ashaondoka tayari kwenda kazini”

“Hakuna kitu kingine alichosema zaidi ya kumchukua Lanlan?”

“Hakuna alichosema , alimpigia simu Edna tu na kumpa Lanlan aombe ruhusa kwa mama yake na wakaondoka”

“Kwanini hajanipigia mimi”

“Kama unajijua ni baba kwanini hurudi hata nyumbani kwa kuwahi na kujua mtoto kalala vipi , unaitwa baba lakini bado huchukulii cheo hicho kwa ukubwa wake, Lanlan anaweza asiwe mtoto wako wa damu lakini tayari anakuita baba hivyo una jukumu kubwa kwake, huoni babu yake anajitahidi kumkubali kama mjukuu”Aliongea na kumfanya Roma kujisikia hatia.

“Lakini mama unanisema sana leo , ila Lanlan namchukulia kama mtoto wangu wa kumzaa na nitahakikisha nampa malezi yote kama baba mengine yalikuwa dharula tu”

“Sawa nimekusikia baba na nakuamini katika , ila mimi ile sura ya Edna ikiwa kwenye ukauzu ndio inanikosesha amani , hivyo jitahidi kumuweka sawa”

“Hahaha..Mama bwana nikajua naigopa mwenyewe kumbe tupo wengi”Aliongea Roma

Nyumba ilikuwa imepooza kweli maana Sophia hakuwa mtu wa nyumbani tokea awe maarufu na hata muda huo alikuwa Afrika ya kusini ambako alienda kwa ajili ya kutengeneza Vidio ya wimbo wake mpya anaopanga kuachia mapema kabla ya mwezi wa nne.

Muda wa usiku Edna hakurudi na Roma aliamini Lanlan angekuwepo huenda angerudi, lakini hata hivo alijua huenda ni kwasababu bado alikuwa na hasira, lakini alikaa kama nusu saa tu Edna aliweza kurudi na Roma alimwangalia kutoka juu na kutabasamu huku akifikira namna ya kuyamaliza.

Siku iliofuata baada ya kuamka na kushuka chini kusalimiana na wanafamilia wengine pamoja na kumuulizia Edna , aliambiwa katoka kwenda kuchukua mazoezi.

Roma baada ya kupata taarifa hio alienda mpaka gereji ya magari na kuchukua baiskeli ambayo alifanya kuiagiza mtandaoni na kuletwa jana yake mchana ikiwa ni mwendelezo wa kufikiria namna ya kumpoza mke wake.

Alitoka na baiskeli hio na kuendesha uelekeo ambao aliamini Edna angekuwa akichukulia mazoezi na ni kweli ndani ya dakika chache tu za kuendesha alimuona akiwa anakimbia akiwa amevalia suruali ya track Suit na jezi ya Wananchi(Yanga) , Roma alijikuta akitabasamu kwa namna Edna alivyokuwa ameimarika kwenye swala la mazoezi , kwani mwili wake ulionekana kuanza kukomaa na hata ule unyonge kuanza kupotea na alikuwa mwepesi kwenye kukimbia.

Wanaume aliokuwa akipishana nao Edna waliishia kugeuka nyuma na kuangalia kazi ya uumbaji.

Ilikuwa ni siku ya tano tokea Edna kuanza kukimbia ndani ya mtaa wa Ununio kila asubuhi na katika siku zote hizo aliweza kusogelewa na wanaume takribani wanne waliokuwa wakichukua mazoezi na kujaribu kumuongelesha lakini matokeo yake hakuna ambaye hata alipewa nafasi kwani waliishia kughairi baada ya kuona ukauzu wa Edna.

Kati yao kuna wazungu wawili ambapo pia walikuwa wageni ndani ya hilo eneo ambao walijaribu bahati zao lakini waliishia kutolewa nje na ilipelekea mpaka kuanza kujaribu kutaka kumjua zaidi mrembo huyo asie taka shobo na majibu walioyapata yaliwafanya wasimsogelee tena.

Hivyo Edna hakusogelewa tena baada ya kugundulika ni mke wa bwana Roma Ramoni mtoto wa Raisi wa Jamhuri , lakini pia waligundua wao ni vikapuku tu kwani Edna alikuwa tajiri mkubwa nchini kiasi kwamba mwanzoni waliamini wangeweza kumpata kwa kumhonga pesa , lakini walipokuja kugundua alikuwa na hela zaidi ya uchafu wa jiji la Dar walichoka kabisa na kukata tamaa.

Edna hakupenda macho yaliokuwa yakimwangalia lakini hata hivyo alikuwa akitaka na yeye kujifunza mbinu za kijini , ndio maana hakujali sana waliokuwa wakimkodolea macho na kuendelea na mazoezi yake.

Edna asubuhi hio alikuwa akikimbia kwa spidi kuliko siku zote na hio yote ni kutokana na kwamba kichwa chake hakikuwa sawa kwa yale yaliokuwa yakiendelea kati yake na Roma.

“Babe kunywa maji kidogo , jua lishaanza kuwa kali?”Aliongea Roma mara baada ya kumfikia Edna, lakini hakupokea zaidi ya kusimama huku akihema akiangalia chupa ya maji na kisha kugeukia baiskeli ambayo Roma alikuwa akiendesha Roma na kujiuliza kaitoa wapi , Edna hakuwahi kuiona hio baiskeli na hata hivyo hakujua kuendesha.

“Vipi unaionaje hii baiskeli , nilinunua kwa kuiagiza jana Kupatana na kumwelekeza muuzaji ailete nyumbani kwangu , niliona inafaa kabisa ukiwa umechoka kukimbia nikupandisha na kukurudisha nyumbani, Edna mke wangu umechoka sasa unaonaje ukapanda nikakurudisha nyumbani?”Aliongea Roma na kumfanya amwangalie, aliona ni jambo la aibu kwake kupanda baiskel , hiyo bila kumjibu chochote Roma aliendelea kukimbia.

Roma alijua hawezi kumlainisha Edna kirahisi kutokana na alivyo , hivyo ilibidi aendeshe akiwa upande upande na yeye.

“Edna naomba unisamehe , najua sio mara ya kwanza lakini siwezi kurudia tena , sitokuacha tena mwenyewe”Aliongea Roma lakini Edna ni kama hajamsikia kwani alizidi kukimbia akijifanyisha kiziwi

“Edna mpenzi wangu , usipo nisamehe na kuendelea kuninunia nitaongea kwa sauti ya juu kila mtu asikie nakuomba msamaha”Aliongea Roma na kuufanya moyo wa Edna kupiga kite , watu wengi walikuwa wakiwaangalia na wale ambao wasiomjua Roma waliamini mshikaji alikuwa akibembeleza kukubaliwa.

Edna alimwangalia Roma kwa ishara ya kumwambia asije akafanya anachotaka kufanya kwanni hatomsamehe.

“Edna usinifanyie hivyo , kama usipo nisamehe nitapiga magoti chini hadi unisamehe, niongeleshe hata kidogo basi angalau nisikie sauti yako”Alibembeleza Roma lakini Edna aliendelea kukimbia , lakini hata hivyo alikuwa akifurahi namna Roma alivyokuwa akiteseka kuomba msamaha.

Edna hakuwa na hasira tena ila hakutaka kumsamehe Roma kirahisi , hata hivyo alijua hawezi kuachana nae , hivyo ni wajibu wake kumsamehe lakini hakukubaliana na Roma alivyokuwa akiomba msamaha aliamini kadri atakavyoteseka kuupata msamaha wake ndio itamfanya siku nyingine kutorudia.

“Babe usiponiongelesha chochote nitakuomba msamaha kwa kupiga makelele , unanijua sina aibu hivyo swala dogo kama hilo halinishindi”Aliongea Roma lakini Edna alikuwa na wasiwasi , ni kama aliamini Roma angefanya kweli

“Mpenzi wangu Ednaaa… , naomba unisamehe nimekukosea mimi mume wako” Roma aliongea kwa sauti kubwa ambayo ilisambaa kweli na kufanya hata wale ambao hawakuwa na habari nao kugeuka na kuwaangalia.

Edna alijikuta akisimama huku akimwangalia Roma kwa mshangao , hakuamini kama angeweza kuongea kwa sauati namna hio

“Darling mimi ni mbwa..”Roma alitaka kuendelea lakini alishitukia akizibwa mdomo na mkono , Edna alitaka kukasirishwa na kitendo chake lakini kwa wakati mmoja alitamani kucheka.

“Roma umechizika , kwanini unaropokasauti mbele za watu?”

“Kwanini nijali watu , Kama yangu mbinu inafanya kazi inafanya kazi” Edna alijikuta akivuta pumzina kutamanni kumpiga Roma ngumi kwa jinsi alivyosababisha watu kuwaaangalia.

“Umeshinda baba , umeshinda daah!, sijaona mtu asie na aibu kama wewe”

“Edna naomba unisamehe sijali watu wananichukuliaje lakini nataka unisamehe siwezi kuendelea kukuangalia ukinichunia, nakuapia sitokukasirisha tena”

“Niachie mikono sasa watu wanatuangalia Roma.. hasira zangu zimeisha hata hivyo”

“Babe unamaanisha umenisamehe?”

“Siwezi kuendelea kukasirikia , lakini Roma ukinifanyia kitendo kama cha jana na kunifanya nione aibu mbele ya watu nakuapia nitahakikisha unajutia kwa maisha yako yote”

“Mpenzi usnitishie hivyo bwana mwenzio , sitorudia tena naapia”Aliongea Roma na Edna alitabasamu na kutingisha kichwa kwamba amemsamehe , Roma aliachia tabasamu hakuamini mambo yanekuwa marahisi hivyo , alijiambia inabidi awe makini siku za usoni hata kwenda kulala na wanawake zake.

Edna alipokea maji alioletewa na kunywa kidogo , hata hivyo alishachoka na watu walikuwa wakiwakodolea macho hivyo aliona ni muda wa kurudi nyumbani.

“Edna vaa hizi headphone masikioni , ni nzuri sana na zitakusaidia kuwa mwepesi wakati wa kukimbia zimetengenezwa mahususi kwa ajili ya watu wanaofanywa jogging asubuhi”Aliongea na Edna alizishika na kuziangalia kwa muda na kisha ilibidi tu avae, hata hivyo hakuwa mpenzi sana wa mziki.

Roma baada ya kumvalisha alimpa ishara ya kupandisha kwenye baiskeli aliokuja nayo ili amrudishe nyumbani, Edna alimwwangalia Roma aliekuwa akibembeleza kwa macho ya kulegea na alijikuta akitamani kucheka , alijiambia muda mwingine inafurahisha mwanaume mgumu kuamua kujishusha kwa ajili ya mwanamke.

Edna mara baada ya kupanda kwenye baiskeli Roma aliendesha kwa kuchanga pedeli kuelekea nyumbani huku Edna akiwa amemkumbatia Roma kwenye kiuno ili asije akadondoka.

Upepo wa baharini ulikuwa ukipuliza vizuri mno na kufanya Edna kufumba macho huku akifurahishwa na mziki, ilikuwa mara yake ya kwanza kupanda baiskeli kama hivyo na Roma alilitambua hivyo kuna buda alikuwa akishika breki makusudi ili kumfanya Edna azidi kumkumbatia.

Edna mwenyewe aligundua Roma alikuwa akimfanyia makusudi, lakini aliishia kuangalia kisogo cha Roma na kisha alimkumbatia vizuri.

Upande wa Roma hakuamini maisha yake yangefikia katika hatua hio ya kumuendesha mwanamke anaempenda kando kando ya bahari , ilikuwa ni ndoto ambayo aliamini isingeweza kutimia kutokana na namna watu walivyokuwa wakimwandama , maumivu ya kumpoteza Seventeen miaka iliompita yalimfanya kuamini haitotokea siku akarejewa na furaha na kuishi kama binadamu wa kawaida.

Alijikuta akivuta pumzi ndefu na kuzisuha huku akiserereka na baiskeli kueleleka nyumbani.

“Asante sana Edna mke wangu”Aliongea Roma na kumfanya Edna ambaye alikuwa akisikiliza mziki kuhisi Roma alikuwa akimuongelesha na kumfanya kupeleka mkono mmoja na kuvua zile headphone bila Roma kujua.

“Edna hivi unajua kwenye maisha yangu nimekutana na kila aina ya mwanamke kutokea nilipokua mdogo mpaka umri huu niliokuwa nao kwa kuzunguka karibia kila nchi? , mara baada ya kukuona kwa mara ya kwanza nilikuchukulia kama mwanamke tu mwenye sura ya kirembo ambaye unapaswa kutumiwa kwa starehe ya muda mfupi , safari yangu ya kuja Tanzania haikuwa kwa ajili ya kuoa lakini nilikubali kuona na wewe kwasababu tu ulikuwa ukifanana na Seventeen kwa kila kitu, Edna wewe ni mzuri lakini niseme tu huna Vibe kabisa , nilikukuta hujui kupika , muda wote umekaa kikauzu mno , haupo Romantic mpaka muda mwingine najiuliza ni kipi unachofikira kichwani kwako”

“Ukiachana na uzuri wako sikuwa na sababu yoyote ya kuendelea kubakia kama mumeo , wewe ni mgumu mno , ukauzu wako unafanya maisha kuwa magumu na kuna muda niliona huenda wanawake wengine ni ‘Wife material’ kuliko hata wewe…”

Edna alijikuta aking’ata meno yake kwa hasira huku machozi yakimtoka mfululizo kwa kauli ya Roma , alijihisi amekosewa kweli , alijiuliza ni kweli yote hayo yanayosemwa , inamaana tofauti na uzuri wake wote hakuna kitu kingine cha kuvutia kuhusu yeye,alimuona Roma anamuonea.

“Lakini Edna licha ya yote hayo siwezi kukataa kwamba wewe ndio uliehusika katika kunifanya nifikirie upya kuhusu maisha yangu na kuachana na mambo yaliopita , umenifanya nimeanza kuyaangalia maisha kwa namna ya utofauti kabisa , na sasa hivi nashindwa hata kuelewa ilikuwaje mpaka nikakubaliana na wewe kwa kila kitu tokea tulivyokutana , najiuliza kwanini sasa hivi nahisi maisha yangu bila wewe hayawezi kuendelea, najihisi kama nimerogwa kiasi kwamba muda wote sura yako inapita mara kwa mara kwenye akili yangu , Edna natamani maisha yangu kuendelea hivi mpaka mwisho wa maisha yangu hapa duniani , najua mara kwa mara nakukasirisha , lakini nataka utambue kwamba hata kama siku ikatokea hatuongeleshani kwa kukoseana , nitaendelea kubaki nyuma yako ili ukigeuka uweze kuniona , Edna asante kwa kuja kwenye maisha yangu na kunifanya nipate nafasi tena ya kuyaangalia maisha kwa namna ya tofauti , Edna nakupenda mno kuliko mwanamke yoyote yule”

“Kama mini ni wa muhumu kwenye maisha yako na unanipenda kwanini unanikasirisha mara kwa mara”Aliongea Edna na kumfanya Roma kutaka kudondosha baiskeli.

“Roma kua makini utanidondosha”

“Edna nilijua hunisikiii?”

“Niliacha kusikiliza , mziki wenyewe ulioniwekea mbaya”

“Dah .. kwahio umeweza kusikia nini nilichozunguma?”

“Nimesikia ukini nanga , umesema ninaboa , sina Vibe kabisa , sipo romantic muda wote nipo na ukauzu , naona umetokea kunanijua vizuri sana”

“Babe kwanini unachagua maneno mabaya tu , sikiliza voko yangu mwishoni nilihitimisha vizuri bwana”

“Endesha acha kuongea sana”Aliongea na kumfanya Roma kuongeza spidi kuelekea nyumbani.

Edna alijikuta akitoa tabasamu bila kupenda , aliangalia mgongo wa Roma kwa macho ya huba na kujikuta akivuta hewa huku akizidi kumkumbatia Roma, alijihisi mapenzi yake kwa Roma yalikuwa yakimkolea siku hadi siku.

Roma na Edna mara baada ya kufika nyumbani walikuta sehemu walipoegesha magari yao yameongezeka mawili , moja ikiwa ni Aud A8 na Benz SL 550.

Mpaka hapo walijua kuna ugeni ambao umefika , lakini Roma alijiuliza ni mtu gani ambaye anafika kuwatembea asubuhi asubuhi tena nyumbani

“Roma hio Lexus ni ya kwako . niliona wakati naenda mazoezini?”

“Ndio , lakini hayo magari mengine sio ya kwetu , unatammbua ni ya nani?” aliuliza Roma na kumfanya Edna atingishe kichwa kujibu kwamba hayatambui.

“BMW yako ipo wapi?”

“Jana ililipuka , nimesahau kukuambia, hio Lexus nimeichukua kwa mtu”Aliongea Roma kirahisi tu lakini alimfanya Edna kumwangalia kwa wasiwasi.

“Kulipuka kwa gari sio jambo la kawaida , Roma unafanya mambo mengi ya hatari ndio maana mama haishiwi na wasiwasi kila ukitoka nyumbani”

“Usijali kuna tukio lilitokea katika harakati zangu nitakuelezea”

“Okey! Lakini unaweza kuchukua gari lingine ukaachana na hili la kijapani , linaonekana vizuri lakini huwa sipendi brand yak…”

“Edna njooni kuna wageni kutoka serikalini wanawasubiria…”Sauti ya Bi Wema kutoka ndani iliwaita na walijikuta wakiangaliana na kisha walipiga hatua kuingia ndani.

ITAENDELEA-WATSAP 068715134
 
Kwanza kabisa nikushuru mkuu singanojr . Dude limesimamia kucha hili! Nimerudi kuisoma upya! Ilimradi nipate raha dunian kama nilivyorudia riwaya kadhaa kwa mfano anga la washenji na peniala! Back to the vipande vya leo! Rufi akapambane na amina huko vexto media! Kumuwin hades! Halaf hades ana kula mkuyati?? singanojr si unajua battle ya mkuyati na k? Mkongo ukasome tena kuanzia nasari kabisa
 
Kwanza kabisa nikushuru mkuu singanojr . Dude limesimamia kucha hili! Nimerudi kuisoma upya! Ilimradi nipate raha dunian kama nilivyorudia riwaya kadhaa kwa mfano anga la washenji na peniala! Back to the vipande vya leo! Rufi akapambane na amina huko vexto media! Kumuwin hades! Halaf hades ana kula mkuyati?? singanojr si unajua battle ya mkuyati na k? Mkongo ukasome tena kuanzia nasari kabisa
 
Kwanza kabisa nikushuru mkuu singanojr . Dude limesimamia kucha hili! Nimerudi kuisoma upya! Ilimradi nipate raha dunian kama nilivyorudia riwaya kadhaa kwa mfano anga la washenji na peniala! Back to the vipande vya leo! Rufi akapambane na amina huko vexto media! Kumuwin hades! Halaf hades ana kula mkuyati?? singanojr si unajua battle ya mkuyati na k? Mkongo ukasome tena kuanzia nasari kabisa
 
Kwanza kabisa nikushuru mkuu singanojr . Dude limesimamia kucha hili! Nimerudi kuisoma upya! Ilimradi nipate raha dunian kama nilivyorudia riwaya kadhaa kwa mfano anga la washenji na peniala! Rufi akapambane na amina huko vexto media! Kumuwin hades! Halaf hades ana kula mkuyati?? singanojr si unajua battle ya mkuyati na k? Mkongo ukasome tena kuanzia nasari kabisa
 
Kwanza kabisa nikushuru mkuu singanojr . Dude limesimamia kucha hili! Nimerudi kuisoma upya! Ilimradi nipate raha dunian kama nilivyorudia riwaya kadhaa kwa mfano anga la washenji na peniala! Rufi akapambane na amina huko vexto media! Kumuwin hades! Halaf hades ana kula mkuyati?? singanojr si unajua battle ya mkuyati na k? Mkongo ukasome tena kuanzia nasari kabisa
 
Ila huyu Roma ni msenge, mpaka Sasa anashindwa kugundua kuwa lan lan ni mwanae, kashindwa kugundua Edina ni pacha wa demu wake seventeen.


Ila mwandishi Kuna kipande umetupilia mbali kinqchohusu hao maraisi was Kenya na Tanzania kuliwa matakule
 
SEHEMU YA 432

Ni kama nusu saa au na zaidi , katika maabara iliopo ndani ya bara la barafu , yaani Antarctica alionekana Naira alievalia mavazi ya kitabibu huku akiwa ameshikilia kalamu mfano wa Marker pen , akiwa anaandika kwenye ubao kwa kasi ya ajabu mno kiasi kwamba kila baada ya sekunde sitini alikuwa akirekebisha miwani yake.

Aliandika kwenye ubao ule ambao haukuwa wa kawaida , ambao ni dhahiri ulikuwa ubao wa kieletroniki kwa zaidi ya dakika kumi na ukawa wote umejaa maandishi ya kimahesabu ambayo hayakueleweka kwani kulikuwa na miingiliano ya kanuni nyingi za kimahesabu , zikiwa ni zile ambazo huenda mwanafuzi wa kidato cha sita au wa chuo aliesomea hesabu kushindwa kuzitafutia ufumbuzi.

Baada ya kumaliza kuandika , ndani ya chumba hiko kilichojaa mwanga mweupe usionyesha chanzo chake , alijikuta akishika kiuno kwa namna ya kuyafanyia upembuzi maandishi yake huku akigonga kichwa kwa kutumia ile marker pen ya kisasa kabisa ambayo inafanana na zile za simu.

Wakati akiwa kwenye mawazo alijikuta akijikatia tamaa na palepale aliponyeza ile karamu kwa juu kwa namna ya kuminya na dole gumba na palepale yale maandishi yalipotea huku uso wake ukionyesha kutopata jawabu ambalo alikuwa akihitaji na alisogelea ubao akihitaji kuanza upya , lakini kabla tu ya kuanza mlango wa chumba hicho ulijifungua kwa namna isioelezeka kama vile umeyeyuika hewani na akaonekana mrembo Clelia Allisanto akiingia hapo ndani na kumfanya Naira kukakamaa kwa kumuangalia.

Clelia alionekana kutabasamu pasipo kuongea lololote na kisha alimpa ishara Naira ya kumpatia ile Marker Pen au kalamu na kisha akampa ishara ya kurudi nyuma na Clelia alibonyeza ile karamu juu na kisha alisogelea ule ubao ulioshikilia ukuta wa chuma na kisha aliandika maneno kwa lugha ya kingereza makubwa kwa haraka na kisha akasogea pembeni na kumpa nafasi Naira kuyasoma.

Naira ambaye hakuwa akijua anachokusudia Athena , alisoma maandishi yale huku akionyesha mshangao kwenye uso wake akiwa kama mtu aliechanganyikia.

The Devil’s smile au tabasamu la shetani ndio neno ambalo lilisomeka kwenye ule ubao wa kieletroniki na kumfanya Clelia kumgeukia Athena na kumwangalia kwa namna ya kushangaa.

“The Devil’s smile kwanini ukaandika hivi?”Aliuliza na Athena ambaye hakujali mshangao wa Naira alitabasamu pasipo ya kumjibu na kisha alimpa ishara ya kuangalia tena ule ubao wa kieletroniki na pale pale yale maneno yalififia mpaka kupotea kabisa na ule ubao ulibadirika rangi na kutengeneza picha ya mwanamke mrembo , mwenye rangi ya kiafrika aliekaa kwenye kiti ambacho ni kama cha Enzi , yaani kiti cha kifalme huku kichwani akiwa na taji la kimalkia lakini ambalo lina urembo wa ncha yake juu uliotengenezwa na madini kama vigololi flani vya rangi ya kung’aa sana.

Ilikuwa ni picha ambayo hakika haikuwa ya kupigwa na kamera za kisasa na kama utaangalia kwa umakini ni kwamba picha hio ilikuwa kama mchoro lakini uliokuwa kwenye ukamilifu wa hali ya juu na kama itakuwa ni mchoraji ndio aliekamilisha kazi hio basi atakuwa ni kiwango cha juu.

Naira aliangalia picha ile kwa namna ya kushangaa sana kiasi cha kutoa macho , alisogea karibu zaidi kuichunguza ile picha na kuangalia watu waliokuwa pembeni ya mwanamke huyo aliechorwa amekaa kwenye kiti cha kifalme cha enzi alikuwa akionekana kutabasamu lakini tabasamu lake lilikaa vibaya mno, ni sahihi kusema ni tabasamu la kishetani maana haliashirii mzaha wa aina yoyote wala nia njema lakini kwa wakati mmoja likivutia kwa aina yake kutokana na urembo wa mwanamke.

Ukiachana na vazi ambalo lilionekana kuwa la gharama ambalo limevaliwa na mwanamke malkia aliekuwa kwenye picha , lakini pia mbele yake kuna wenye mavazi tofauti na rangi tofauti wakiwa wamezika vichwa vyao chini wakionyesha hali ya kusujudu , ni kama watu hao walikuwa wakiogopa kumwangalia mwanamke aliekuwa kwenye kiti cha enzi na yule mwanamke ambaye alionekana kuwa malkia aliwaangalia watu wake waliomsujudia kwa namna ya tabasamu ambalo sio la kawaida. The Devil’s smile au tabasamu la kishetani ndio uhalisia wa picha yenyewe , lakini hilo sicho kitu kilichomshangaza Naira , kilichomshangaza ni mwonekano wa utambuzi wa mtu mwenyewe.

“Siku zote umekuwa ukijiuliza kwanini mwili wa Seventeen nimeuhifadhi kwenye Cryosleep na nikakujibu nitautumia baadae , leo hii nataka kukufunulia ukweli , ili uweze kufikisha asilimia tano za kufahamu kila kitu kuhusu mimi, lakini kabla ya yote nataka unielezee mchoro unao uona , kwanzia sura ya mwanamke anaeonyesha tabasamu na watu waliokaa pembeni yake wanaashiria nini”Aliongea kwa lugha ya kingereza na kumfanya Naira kumeza mate.

Mrembo Naira licha ya kwamba amekuwa ni mwenye ukaribu na Athena lakini hakumjua kabisa kila siku aliweza kumuona mwanamke huyu kwa mwonekano na wasifu tofauti lakini sura ile ile na hili lilitengeneza ile hali ya muda wote kumuogopa , lakini kinachomtia wasiwasi zaidi na kumhofia ni kwamba tokea wawe na ukaribu na kuendeleza misheni zote kwa maagizo yake , alichojua kuhusu Athena kwa kila kitu ni asilimia nne tu , inamaana kuna zaidi ya asilimia tisini na sita hamjui Athena kiundani na mambo yake yote kuhusu ulimwengu na mipango yake.

“Namuona mwanamke mwenye mwonekano wa Seventeen akiwa zaidi ya malkia, naona utukufu uliokuwa juu yake , mbele yake na nyuma yake , naona mamlaka lakini naona tabasamu la ushindi unaoashiria utawala,lakini nashindwa kuelewa tabasamu lake kwani linaonyesha kuelezea mambo mengi”Aliongea kwa lugha ya kingereza.

“Hahaha…Hahaha..”Athena alicheka na kisha akasogela mbele.

“Unachokiona ndio maisha ya baadae, unachokiona ndio misheni yangu tokea siku nilioweza kumiliki huo mchoro, kadri huyu mwanamke atakavyoendelea kutabasamu , inamaanisha mipango yangu katika misheni zote inaendelea vizuri na ni asilimia kubwa ya matumaini nitayafikia mafanikio”Aliongea

“Unamaanisha nini kusema kadri mwanamke huyu kuendelea kutabasamu ndio mafanikio ya mipango yako?”

“Elewa kauli yangu ya mwanzo ni rahisi kugundua ninachomaanisha , kwa maneno marahisi ni sawa nikisema picha hii imepigwa miaka mingi mbeleni ambayo sijui wakati wake”Aliongea.

“Hii picha ni ya Seventeen , sura ya mwanamke kwenye Cryosleep , ina uhusiano gani na mipango yako?”

“Umekosea swali na sio kawaida yako Naira , swali lako linatakiwa kuwa hivi tokea mwanzo , kwanini kati ya sura za wanawake woote ndani ya dunia nikachagua mwili wa Seventeen? , jibu langu kwako ni hio picha ndio picha”

“Naira unajua ni kwanini kati ya vitu vyote ndani ya dunia ni ngumu sana kuelezea neno Muda kwa maneno marahisi , kuliko inavyoelezewa sasa?”

“Kwasababu kilichopangwa kutokea kulingana na muda ndio hutokea”Aliongea lakini Naira bado alikuwa njia panda.

“Hii picha ni wewe ukiwa kwenye mwili wa Seventeen na imepigwa miaka ya mbeleni hivyo naweza kusema unaichukulia kama unabiii ambao unaotarajiwa kutokea au naweza kusema kuna mtu aliefanikisha kwenda mbele ya muda na kupiga picha na kurudi nayo wakati wa sasa hivyo kukuwezesha kujua nini kitakajokucha kutokea nadhani ndio unachojaribu kuelezea”

“Upo sahihi kwa maneno yako , lakini hata hivyo maneno yako yanaweza kutokuwa sahihi vile vile, labda nikueleze picha hii iliweza kuwa chini ya umiliki wangu kwanzia karne ya kwanza na imekuwa kama tumaini pekee kwangu na maneno yako yanaweza kutokuwa sahihi kwasababu sura ya mwanamke unayoiona inaweza kuwa ya Seventeen au Persephone lakini pia inaawezekana nikawa mimi kwenye mwili wa Seventeen , lakini kwasababu Seventeen roho yake ishacha mwili makisio yanabakia kuwa mawili , inawezekana kuwa mimi au Persephone”Aliongea na kumfanya Naira kuelewa nusu.

Alichokuwa akimaanisha Athena ni kwamba picha anayoiona inaweza kuwa ya Seventeen au pia ikawa ya Edna yaani Persephone kutokana na sababu kwamba wanawake hao wanafanana kwa kila kitu kwani wote ni mapacha , lakini pia kwasababu alikuwa na mwili wa Seventeen ambao ana mpango wa kuutumia hapo baadae.

Mwanamke kwenye picha anaweza kuwa yeye akiwa ameuvaa mwili huo lakini pia anaweza asiwe yeye kwasababu yupo Edna ambaye ni pacha wake na Seventeen na hana namna ya kutofautisha ambaye yupo kwenye picha ni Seventeen au ni Edna.

Lakini pia picha hio anasema ilianza kuwa chini ya umiliki wake wakati wa karne ya kwanza na inaonyesha maisha ya miaka mingi mbeleni zaidi ya miaka ya sasa , miaka ambayo sasa mwanamke huyo inaonyesha kusujudiwa kwa kuashiria dunia yote ipo chini ya miguu yake na yeye ndio mtawala kwani kitendo cha watu kuzika vichwa vyao chini kwa namna ya kusujudu ni kuashiria kwamba mamlaka ya mwanamke huyo ni makubwa kuliko hata Mungu mwenyewe.

Ni rahisi kusema kwamba Athena alikuwa ni mwenye kuchanganyikiwa kwa kutojua picha hio ni yeye akiwa kwenye sura ya Seventeen au ni Edna.

Maelezo yale yalimshangaza Naira na kugundua sasa , kwanini Athena alikuwa akiumiliki mwili wa Seventeen, lakini hata hivyo anashangaa kwani ni swala kubwa mno kulifahamu siku hio.

“Kwahio ndio sababu unalinda maisha ya Edna , lakini pia wakati huo huo umehifadhi mwili wa Seventeen? Ni kwasababu huna jibu la moja kwa moja sura hio inamwakilisha nani kati yako na Edna?”Aliuliza na kumfanya Athena kutabasamu.

“Ni rahisi pia kufikiria hilo kwa haraka kwasababu lipo wazi , lakini swali hilo litakuwa ni sahihi kwasasa tu, kwenye maisha yangu yote mara baada ya kumiliki hii picha , nilijiuliza maswali mengi ni wakati gani wakati wa hio picha ungeweza kutimia niliweza kutaifsiri picha lakini nilishindwa kutafsiri muda”

“Picha hii kuimiliki inaelezea tafsiri nyingi , lakini tabasamu la huyu mwanamke ndio misheni yangu , je unafahamu ni changamoto gani nilipitia ilionitengenezea mawazo kwa muda mrefu?”Aliuliza Athena aliekuwa kwenye mwili wa Clelia Allisanto.

“Ni wakati gani huo?”

“Ni wakati mwanamke huyo akiwa anatoa machozi na watu wanaosujudu kuonekana kumkimbia”Aliongea Athena na kumfanya Naira kutoa macho.

“Unamaanisha picha hii ilishawahi kubadilika?”Aliuliza akiwa kama haamini.

“Ndio ilishawahi kubadilika kwa zaidi ya miaka ishirini mpaka pale lilipotokea tukio kubwa sana kwenye uso wa dunia ndio tabasamu la huyu mwanamke liliporudi vilevile future timeline imerudi kuwa vilevile”

“The choice we make today can shape the future timeline, However future is not determined by the present but rather shaped by a complex interplay of many different factors”Aliongea akimaanisha kwamba maamuzi ya sasa ndio yanatengeneza yanayokuja laini hata hivyo sio mambo ya wakati huu tu ambayo yanaamua yatakayokuja bali kuna mambo mengi yakuzingatiwa.
Ohooooooo
 
Back
Top Bottom