Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Huyu jamaa sometimes frequency hazishiki
Siyo hivyo mkuu, hii ni kwa sababu anatumia muda mrefu kuifasiri na kuiongezea vionjo, ili ifiti kwenye muktadha wetu na nyingine ni delay technique, ili kujipatia maokoto kwa yeyote asiye na subira. Sisi wengine tulishaisoma kule alikoichota na kuileta humu JF. Ila nampongeza kwa uwezo wake wa kuifasiri, kuongezea vionjo na hata kuijengea mandhari ya Tanzania, badala ya China. Kwa heshima yake sitataja link na jina la hiyo Novel.
 
NILIMHDANIA KAHABA KUUMBE BIKRA

MTUNZI: SINGANOJR

Mono no aware

SEHEMU YA 751.
Mkuu wa miliki ya Panas, Gefu mara baada ya kuulizwa na viongozi wa Hongmeng kama wapo hapo kwa ajili ya kuomba msaada alitabasamu na kisha akawaangalia wenzake na kukubaliana kwa macho kisha akawageukia.
“Kiongozi mkuu ni kama nilivyosema , mnadhani Hongmeng peke yake inao uwezo wa kushindana na miungu wakati sisi miliki nyingine tumeshindwa , sio kwamba nadharau uwezo wa wakuu wa Hongmeng lakini kaka yangu Anjiu na baba yake wote kwa pamoja wapo katika levo ya kuipita dhiki ya radi na hakuna jini yoyote ambae anauwezo wa kuwashinda hapa Hongmeng lakini wao wameshindwa kuwadhibiti miungu”
“Ninakiri kwamba ni kweli Anjiu uwezo wake ni mkubwa kuliko wa kwetu lakini mnapaswa kutambua kwamba sisi tunalindwa na safu ya ulinzi wa mababu zetu , hawawezi kutufanya chochote kama tutakuwa ndani ya miliki yetu , walishajaribu kuingia huku miaka mingi iliopita na wakaambulia kushinidwa”
“Kiongozi mkuu nadhani uache maigizo , kwasababu umeshawaondoa watu wako wa daraja la chini ongea sababu yako’
“Oh , inaonekana unajua mengi kuhusu sisi?”Aliongea Wucheni huku akipepesa macho kulia na kushoto.
“Kwasababu safu yenu ya ulinzi ilitengenezwa na mababu wa enzi hizo waliokuwa na akili kubwa ni kweli kwamba nguvu yake ya ulinzi ni kubwa kama sio hivyo isingeweza kushikilia roho za majini waovu ndani ya gereza lenu la Roho kwa miaka mingi , lakini je naweza kusema au wewe unaweza kusema mnao uwezo wa kuutumia ulinzi huo , je mnajua namna ulinzi huo unavyofanya kazi?, kwa kile ambacho nakijua mimi ni kwamba majini wa miliki yako wanasema wao ndio wanaosapoti ulinzi huo kwa kuingiza nguvu yao ya mbingu na ardhi , lakini ukweli ni kwamba inaonekana safu hii ya ki ulinzi imetengenezwa kuvuna yenyewe nishati za mbingu na ardhi na hakukuwa na haja ya kuiongezea nguvu”
“Sidhani kama ni sahihi kwa wewe kufanya makisio yako juu ya maswala yetu ya ndani”Aliongea Wucheni.
“Ni kweli , lakini matumaini yetu ni nyie kuweza kujua namna ya kuendesha safu yenu ya ulinzi na kujilinda zidi ya miungu lakini kulingana na hali ilivyo inaonekana kabisa hamuwezi kwani hamjui busara iliopo nyuma ya ulinzi huo”
Wale majini wanne ambao ni viongozi wote walikaa kimya wakimwangalia Gefu ambaye alikuwa akiongea.
Ukweli ni kwamba walikuwa wakijua sana namna nguvu ya miungu ilivyo mara baada ya kuwachakaza majini hao huko katika ulimwengu wa binadamu.
Sasa kama miungu wote kumi na moja watashambulia miliki ya kijini hawatoweza kujilinda na ni hakika kwamba watashindwa.
Katika swala la nguvu haikujalisha miungu ilikuwa upande wa dunia inayoonekana lakini kama nguvu zao zikirudi kikamilifu ilimaanisha kwamba lazima wangetaka kujipima uwezo na washindani sahihi ni hao majini , isitoshe pia miungu hio ina kinyongo na majini kwa muda mrefu.
Ilikuwa ni swala la muda tu kurudia kile ambacho walitaka kufanya miaka mingi iliopita mara baada ya kutua katika uso wa dunia.
“Mwisho wa yote inaonekana kabisa mlichokijia hapa sio sisi kuwasaidia bali mnatafuta kura ya pamoja ili walinzi wa umoja wa majini kuchukua hatua”Aliongea Yanyun na ilikuwa ni kama vile amepatia kile ambacho Gefu na wenzake wamekijia hapo Hongmeng.
Ijapokuwa ni kweli kwamba kulikuwa na umoja wa ki ulinzi wa pamoja wa majini ulioundwa maiaka mingi iliopita lakini miliki nyingi za kijini hazijawahi kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na jini mkuu namba moja ambaye ndio kiongozi wa umoja huo.
Hivyo Gefu na wenzake walikuwa wakijua kwamba mkuu wa umoja wa majini lazima atakuwa na mawasiliano na Hongmeng ndio maana wakafika hapo.
Hawakuenda Hongmeng kwa ajili ya kuomba msaada wa kivita ukweli ni kwamba Hongmeng ni miliki dhaifu ambayo isingekuwa na mchango mkubwa kumshambulia Roma.
Inaaminika kwamba mkuu namba moja wa umoja wa majini ndio jini ambaye ana nguvu kubwa za kijini na ambaye ameishi muda mrefu sana hivyo kama yeye na wajumbe wake wa ulinzi wa baraza la umoja huo wataingia katika vita na Roma ni hakika kwamba Roma asingeweza kushinda kwa namna yoyote ile.
Jini mwenye nguvu ambaye alikutana na Roma jijini Dodoma ndio ambae anazungumziwa hapo , ndio jini ambaye anadumisha muungano wa pamoja wa ki ulinzi wa ulimwengu wa kijini na wa kibinadamu.
Haikuwa sheria ya ‘The Gods treaty’ tu ambayo ilikuwa ikiwazuia majini kutoka katika ulimwengu wa kawaida na kufanya fujo , ukweli ni kwamba mkataba huo wa The gods treaty ulikuwa ni wa maslahi wa pande mbili tu na binadamu kwa namna moja ama nyingine hanufaiki kwa namna yoyote na mkataba huo.
Mkataba huo ulikuwa ukiwapa ruhusa miungu kushughulika na majini wote wanaovuka mipaka na kujitokeza katika ulimwengu wa kawaida lakini hakukuwa na kipengele cha moja kwa moja ambacho kilikuwa kikisema kwamba majini wakiua binadamu miungu inapaswa kuchukua hatua.
Umoja wa muungano wa pamoja wa ki ulinzi ndio ambao ulikuwa na sheria ya moja kwa moja ya kuwazuia majini au viumbe wote wenye nguvu za mbingu na ardhi kushambulia binadamu ambao hawana uwezo wa nguvu hizo au kutoka katika ulimwengu na kutaka kutawala binadamu hio ndio sheria ambayo ilikuwepo mara baada ya vita kati ya majiini pepo, binadamu na majini watu.
Hivyo mkuu namba moja alikuwa akiishi katika ulimwengu wa kawaida na kazi yake kubwa ni kulinda mpaka wa kisheria kati ya majini na binadamu lakini wakati huo huo akiwa na jukumu la kulinda miliki za kijini pale tu itakapotokea hatari ambayo majini hawawezi kuizuia wenyewe.
Sasa miliki hizi za Panas , Kekexil na Xia zilitaka kuwaamsha wajumbe wa muungano wa pamoja wa ki ulinzi wakiongozwa na mkuu namba moja mwenyewe wa umoja huo wa majini kumchukulia Roma hatua.
“Kama hichi ndio kilichowaleta basi hatuwezi kuwasaidia , ukweli ni kwamba hatuwezi kukutana nao pale tunapohitaji na hata sura zao hatuzijui kwani hawajawahi kujionyesha “Aliongea Shombeli.
“Najua pia hatuwezi kukutana nao , lakini ukweli ni kwamba lazima watakuwa wanajua kile kinachoendelea , kama wajumbe wa ulinzi wa pamoja watakataa kutusaidia sidhani kama pia wanaweza kuisadia miliki yenu pale itakapokuwa hatarini , hivyo kwasasa ni sawa na kusema wote tupo kwenye tatizo moja , taarifa za siri ambazo tunazo mpaka sasa Roma ameshakutana na mkuu wa umoja mara baada ya kutibua amani ndani ya familia ya Sharif sehemu ya wafuasi wa majini pepo kutoka miliki ya Braki, mnadhani hii tafsiri yake ni nini?”
Kauli yake ilibadili hali ya hewa palepale hakuna ambaye aliamini kama kweli Roma alikuwa amekwisha kukutana na mkuu wa umoja sehemu ya wajumbe wa ulinzi.
Ukweli ni kwamba mara nyingi umoja huo haujawahi kuamulia majini hao cha kufanya , ni umoja ambao haujawahi kuingilia maswala ya majini na binadamu na hata pale inapotokea migogoro hawajitokezi mpaka waone kuna ulazima.
Kuna uwezekano mkuu wa umoja alikutana na Roma kumpa onyo kutokana na kuchokoza miliki ya Braki , miliki ya majini pepo , majini ambao ni hatari kama wataingia katika ulimwengu wa binadamu.
Tokea siku nyingi Hongmeng ilitaka kusafiri kwenda Afrika kumshambulia Roma lakini ukweli sio kwamba walishindwa au sheria ilikuwa ikiwazuia kufanya hivyo ila ni kwamba walikuwa wakimuogopa Roma.
Hata pale taarifa zilipowafikia hivi majuzi mara baada kutuma mjumbe wao kuja ulimwengu wa kawaida kutoa msimamo wao na Roma kumuondolea nguvu za kijini hawakuwa na cha kufanya licha ya kwamba walitafsiri kitendo hicho kama uchokozi wa wazi ambao Roma ameufanya.
“Kwasasa haiwezekani kuwasiliana na mkuu wa umoja na wajumbe wake wa ulinzi , kama kweli wangekuwa tayari kutusaidia wangekuwa washafanya wenyewe bila ya kutafutwa , hata kama miliki zetu zote zitaingia kwenye matatizo nina wasiwasi wanaweza wasijali , wanachokilinda wao sio majini bali ni asili ya usalama wa ulimwengu”Aliongea Umini.
“Umini wewe ndio ambae ushawahi kukutana na mkuu wa umoja unakadiria vipi uwezo wake?”Aliuliza Wucheni.
“Sina uhakika lakini kulingana na mkandamizo wa msisimko anaozalisha inaonekana ana uwezo mkubwa kuliko hata Anjiu , watu ambao hawajionyeshi kama wao sidhani kama kuna mmoja kati yetu anaweza kushindana nao”Kauli yake iliwashangaza na kuwaogopesha.
Ukweli ni kwamba hata huyo Umini aliwahi kukutana na mkuu wa umoja wakati wa kupewa msisitizo wa kimaagizo.
“Wajumbe wote wa ulinzi wa pamoja hawajawahi kujitokeza mpaka sasa kwasababu hawapo tayari kutusaidia , hatuwezi kukaa na kusubiria na lazima tupambanie maisha yetu , wazee kwasasa tunayofursa , tunaweza kumuua Roma kama ataingia kwa mara nyingine katika ulimwengu wa majini ili mradi tu Hongmeng mtatoa ushirikiano wenu kwetu , kama mtaendelea kusita sita na kukataa kutoa msaada mtakuwa mmechelewa kutuomba msamaha mara baada ya Roma kuja kuwashambulia , mkumbuke tu kwammba balozi wenu Xuan Jizi alifanyiwa kitendo cha aibu sana na Roma Ramoni hii inamaanisha Roma ameshatangaza vita yake na Hongmeng”
Kikao kilikuwa ni cha moto na adui namba moja ambaye alikuwa akizungumziwa ni Roma , ukweli ni kwamba hawakuwa na habari hata na miungu kuwa na nguvu kubwa kwa wakati huo , hofu yao kubwa ilikuwa ni Roma kuja kuwashambulia.
Kutokana na kutokuwa na uhakika juu ya kutokea kwa viongozi wa umoja wa majini, Hongmeng kabla ya kukubaliana na miliki nyingine waliona kwanza wakae wao kwa wao wajadiliane na wakishafikia maamuzi watawapatia msimamo wao.
Hivyo wakuu hao wa miliki walipelekwa katika kisiwa cha maua ya Lotus kwa ajili ya mapumziko wakisubiria maamuzi.
“Kwanini hawa vikongwe bado tu wanasita sita , Roma tayari amekwisha kuua balozi wao hivyo moja kwa moja ametangaza vita nao lakini bado tu wanaamini Roma hawezi kuwashambulia , kama tutaendelea kuruhusu Roma uwezo wake kuongezeka Hongmeng ushawishi wao katika dunia utashuka kwa viwango”
“Hey! Menyu huna haja ya kuwa na wasiwasi si bora ufuruhie zako kwani ndio kwanza umeweza kupata cheo cha ukuu wa miliki ya Kekexi?”
“Menui kifo kilikuwa kikimtafuta , nani angedhania kifo chake kitatokea katika ulimwengu wa binadamu , hii nafasi nilistahili kwa muda mrefu haina haja ya kuwa na furaha kwani ni haki yangu”Aliongea Menyu kijeuri na kumfanya Gefu na Anjjiu kuangaliana na kisha walicheka.
Ukweli ni kwamba Anjiu alikuwa akimkubali sana Menyui kuliko kaka yake Menui na ni marafiki wa muda mrefu na ndio ambaye alimpasha habari juu ya kuwekewa sumu ya Taouwu.
Mara baada ya Menui mkuu wa miliki ya Kekexil kuuliwa na Apollo moja kwa moja nafasi yake ilirithiwa na Menyu ambae ni mdogo wake , pengine kungekuwa na mgogoro nani arithi nafasi yake lakini kutokana na vifo vya Mohena na Mohi kiti hicho cha uongozi kilikuwa wazi na moja kwa moja nafasi ikamwangukia Menyu kwa urahisi kabisa.
Yalipita kama masaa kadhaa hivi wakati wakuu wa Hongmeng wakjjadiliana huku upande wa wageni waliokuja kuomba ushirika wakiwa katika eneo la mapumziko.
Mkuu wa kikosi cha ulinzi wa mipaka alifika katika nyumba ambayo anaishi Nefi mtendaji wa shughuli za miliki , bwana huyo alionekana kuwa na taarifa ya haraka ambayo mkuu wake anapaswa kuifahamu.
“Mkuu kuna mvamizi ambae amejeruhiwa sana yupo nje ya uzio , nini tunapaswa kufanya?”Aliongea yule mkuu wa vikosi vya ulinzi wa mipaka mara baada ya kumfikia Nefi.
“Mzamiaji!! , mmegundua anatokea wapi na kwanini amejeruhiwa?”
“Amesema anataka kuonana kwa haraka na kaka yake mkubwa ili kumpa taarifa ya kinachotokea katika miliki yao , ni mdogo wake Gefu mkuu wa miliki ya Panas lakini amepoteza fahamu hivyo tumeshindwa namna ya kudili nae”
“Nipelekeni kwa huyo mtu haraka”Aliongea Nefi mara baada ya kuwaza jambo.
Dakika chache tu Nefi aliweza kuchukuliwa mpaka seheu ya wazi ambayo ni mpakani mwa Hongmeng na kukuta majini wawili ambao wanalinda mtu ambaye amejeruhiwa.
Mtu huyo alikuwa ni wa ngozi nyeusi lakini mweupe na alikuwa amelala ardhini akiwa na sura iliokuwa ikionyesha ni kwa kiasi gani yupo kwenye maumivu.
Nefi ni moja ya majini ambao walikuwa na taarifa nyingi sana kuhusiana na miliki karibia zote na alikuwa akijua baadhi ya majini waiopo katika nafasi za uongozi wa juu katika miliki zote hivyo mara baada ya kumchunguza majeruhi huo palepale aliweza kumjua jina lake , alikuwa ni Gegu Master namba tatu kutoka miliki ya Panas.
“Gegu nini kimekutokea?”Aliuliza Nefi mara baada ya kumfikia yule majeruhi kwa haraka sana.
“Haraka … haraka ..”Aliongea na palepale aliinua mkono wake na kumshika Nefi kwa nguvu huku akiongea kwa shida.
“Mwambie kaka … Roma … Roma anaua watu wetu .. mwambie amevamia Panas”Aliongea kwa shida lakini taarifa yake ilieleweka.
Nefi na baadhi ya majini wa Hongmeng walishangazwa na kauli ile , walikuwa wakijua ndio Roma na Panas hakukuwa na maelewano mazunri lakini hawakutegemea angevamia miliki ya Panas mapema hivyo na kuanza kushambulia.
Mara baada ya kuona Gegu angepoteza maisha kama asingemfanyia huduma ya kwanza palepale alitoa kidonge cha daraja la kati ambacho kazi yake ni kuponya , ijapokuwa kilikuwa cha thamani lakini kwa wakati huo aliona ndio njia pekee ya kumuokoa Gegu.
Baada ya kumuwekea mdomonni alimsaidia kumponyesha na nguvu zake za kijini na hatimae majeraha yake yalipona na kumpa nafasi ya kuanza kukusanya nguvu za nishati ya mbingu na ardhi ili kurejewa na uwezo wake
Ndani ya sekude tu nguvu zake zilirudi na angalu macho yake yalirudi katika hali ya uhai.
“Nitakupeleka katika kisiwa cha anga kwa ajili ya kuonana na baba na wengine”Aliongea Nefi.
Nefi baba yake alikuwa ni Wucheni mkuu wa hadhi ya juu kabisa katika miliki hio ya Hongmeng.
“Nyie wengine nendeni mkatoe taarifa kwa mkuu wa miliki ya Panas haraka”Alitoa maagizo kwa wale wengine .
Katika dakika hio hali ya wasiwasi iliwafunika kila mmoja na raia hao wa Hongmeng walikimbia kwenda kutoa taarifa kwa haraka sana
Mara baada ya Nefi kumfikisha Gegu juu ya kisiwa moja kwa moja alienda mpaka katika eneo la mkutano unapofanyikia na aliweza kugundua tayari Anjiu na wenzake wamekwisha kufika.
Gefu mara baada ya kuona hali aliokuwa nayo Gegu macho yake yalisinyaa huku hasira ikianza kumvaa na haraka sana aliuliza kile kilichotokea.
Gegu ambaye alikuwa akihema kwa nguvu kama mbwa aliekimbia maili nyingi alielezea kila kilichotokea.
Ilionekana lisaa limoja lililopita Roma aliweza kuvamia miliki ya Panas , mara baada ya kugunduika na walinzi ni adui hakuwachelewesha na kuanza kuwashambulia , anasema ni kama vile anga linatema moto ambao ulikuwa ukiunguza makazi yao.
Gegu ambaye aliponea chupuchupu ndio aliweza kukimbia kuja katika miliki ya Hongmeng kwa ajili ya kutoa taarifa.
Anasema kama sio kusaidiwa na walinzi wa miliki waliokuwa katika levo ya maji ya upako na pamoja na Dhana asingeweza kukimbia kwani Roma alikuwa akimshambulia kwa kasi.
“Pumbavu!! , Kwannini Roma kutushambulia sisi Panas kwanza?”Aliongea Gefu kwa hasira huku akijizuia hata kuwazia kile ambacho kinaendelea wakati huo katika miliki yake.
“Gefu unamaanisha nini , kwahio ulitaka aanze kutushambulia sisi Kekexi kwanza?”Aliongea Menyu kwa jazba.
“Ndio ninachomaanisha kwanini asingeanza na nyie”
“Wewe mwanaharamu!!!”
“Inatosha , huu sio muda wa kulumbana , Roma ameenda miliki ya Panas kwasababu moja tu miliki ya Panas ipo katika bara la Afrika sehemu ambayo ipo karibu na Ulaya tofauti na miliki zetu ambazo kimahesabu ni kama zipo katika bara la Asia”Aliongea Anjiu.
“Nin!!”
Gefu na Menyu walishangaa lakini waliona alikuwa sahihi , ukweli ni kwamba kwa njia ya mkato inachukua dakika tano kamili kutoka Tanzania kuingia katika miliki ya Panas.
Lakini swali bado liliibuka katika kichwa cha Gefu , Roma amejuaje njia ya kuingia katika miliki yao maana kuna mahesabu ambayo wanatumia katika kufungua mlango unaoteganisha ulimwengu wa binadamu na miliki yao.
“Viongozi bado tu mtanzamo wenu ni wa kujijengea ukuta.?”Aliuliza Anjiu.
“Roma tayari amechagua kushambulia Panas kwanza kwasababu hakutaka usumbufu na miliki zetu za Xia na Kekexil na hii inaonyesha nia yake ni kushamblia miliki zote , hajali hata ni chuki ya namna gani anaitengeneza kwa kutushambulia , je bado mnaamini ataiacha na miliki ya Hongmeng au mnaamini mtaweza kumdhibiti baada ya miliki zetu kushambuiwa , mkumbuke kwamba ana Dhana ya Cauldron na roho ya Chaosi iliopo ndani yake inaweza kumeza nguvu ya aina yoyote ile na kadri anavyozidi kumeza nguvu za majini wengi ndio anavyozidi kuongezeka nguvu”
Viongozi wa Hongmeng wote walionyesha hali ya wasiwasi wao kwenye macho mara baada ya Anjiu kumaliza kauli hio.
Gefu palepale ni kama wazo lilimwingia na alimgeukia Gegu na kumuuliza swali.
“Gegu dada yetu wa tatu yupo wapi , je ndio anapambana na Roma muda huu?”Aliuliza akimaanisha Rozu.
“Hapana… Dada wa tatu hajaonekana na haijulikani ni wapi alipo , ki ufupi ni kwamba kapotea”Aliongea Gegu.
Hawakujua siku zote Rozu hakuwa mwenzao , alikuwa katika miliki za kijini kwa ajili ya kujipatia nguvu ya unabii maarufu kama Darubini ya Kichawi ya unajimu ambayo ingemsaidia kujua maisha ya mbele yapoje kupitia unabii ili kuweza kumshinda Athena na Hades.
“Okey , ili kutenda haki na kuondoa hii roho ya uovu, nitatupilia mbali unafiki wangu na kuungana na Wabobezi wa miliki zote tatu kumuua huyu shetani Roma Ramoni’Aliongea Wucheni.
Kauli hio ilimfurahisa Anjiu na wenzake na alijua sasa wana nafasi kubwa ya kumdhibiti Roma kama wataunganisha nguvu.
“Kama ndio tumekubaliana, basi bado hatujachelewa tutaita Wabobezi wote na kuianza safari ya kuelekeaPanas”Aliongea Anjiu.
“Amitabbha , awamu hii huyu mzee wenu hata ambatana na nyie , nitaungana na walinzi wa mipaka ili kutengeneza safu ya ulinzi wa jini pepo KingKong ili kuilinda Hongmeng , mniwie radhi”Aliongea Yanyun.
“Usiwe na wasiwasi tunaelewa”Aliongea
Ijapokuwa Yanyun hakuungana nao lakini bado Hongmeng walikuwa na wataalamu watatu wa mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi lakini pia waliunganisha nguvu na majini wote ambao walikuwa katika daraja la mbingu.



SEHEMU YA 752.
PANAS
Yale majengo ya kisasa ambayo yalikuwa yameenda hewani , yaliokuwa yamejengwa kwa msingi imara yaliikuwa yamekatwa katikati huku mengine yakidondoka kwanzia chini kabisa kwenye msingi na kutengeneza kifusi.
Moto mkubwa uliokua ukiwaka katika kila pande ya makao makuu ya miliki hio ya Panas ulikuwa ukizidi kuongezeka katika kila kona huku ukivuka mpaka kwenye msitu uliokuwa karibu na eneo hilo.
Anguko la mikili ya Panas lilikuwa likikaribia muda wowore na kubakia katika historia.
Walinzi na majini wa Panas walikuwa wamepata majeraha makubwa mno na ni wachache sana ambao walikuwa wamefanikiwa kukimbia.
Damu iliotengeneza mfereji ilikuwa ikitiririika kuelekea katika mto uliopita katikati ya jiji la miliki hio na kufanya maji yake kubadilika rangi, ilikuwa ni vigumu kabisa kuelezea namna eneo hilo lilivyokuwa mwanzo kutokana na uharibifu uliotokea.
Hali ilikuwa ikitisha kweli kweli , kulikuwa na miguu pamoja na vichwa vilivyoachana na miili vimesambaa katika kila kona ya eneo hilo , ilikuwa ni ngumu kuona maiti ya jini ikiwa na viungo vyore.
Panas ilikuwa na majini wengi lakini maiti zao zilikuwa chache ikimaanisha kwamba asilimia kubwa ya majini hao walikuwa wamekwisha kuungua na wengine wamemezwa na chungu .
Ijapokuwa muda mfupi ujao eneo hilo lingefunikwa na nguvu ya giza kutokana na kuzama kwa jua lakini ilionekana kama vile ndio kwanza imefika mchana.
Roma alikuwa amesimama katikati ya mbingu na ardhi , macho yake yalikuwa sio ya ubinadamu kabisa , ilikuwa ni kama vile kuna roho abayo imemvaa kwa wakati huo.
Nguvu ya chungu kilichokuwa kikizunguka na kutoa makelele kilimeza nguvu ya upepo ndani ya eneo hilo.
Baada ya kuchinja na kuvunja vunja majini wengi mpaka wakati huo alikuwa amemeza nguvu za majini waliovuka levo ya dhiki wengu sana , kwa kujumlisha na uwezo wake wa mapigo mengi ya radi ilikuwa ni swala la muda tu kuingia katika levo nyingine.
Ukweli hakupata ukinzani wowote mara baada ya kuanza mashambuizi yake , alitegemea pengine Panas ingekuwa na nguvu kuliko Kekexil au Xia lakini hakuna jini yoyote ambaye alikuwa levo zake na kwake aliwaona kama viumbe dhaifu sana.
Wakati huo ni kama uwezo wake umeongezeka maradufu mara baada ya kufyonza nguvu za majini hao.
Dhana ya Chaos Cauldron na yenyewe haikuwa nyuma katika kujiimarisha nguvu kwa kumeza majini.
Chungu hicho kadri kilivyokuwa kikimeza ndio kilivyotengeneza mzingo mkubwa wa kani mvutano.
Mpaka dakika hio ni majini wawili tu wa miliki ya Panas ambao walikuwa wamesimama upande wa kulia na kushoto kwake wakijaribu kupambana nae.
Roma mpango wake ulikuwa ni kuimaliza kabisa miliki ya Panas na kuifutilia mbali , ukweli sio Panas tu alikuwa na mpango wa kumaliza majini wote na kuwatufilia mbali ili aweze kuishi kwa utulivu na amani.
“Wewe mhalifu , umeamsha hio roho ya kishetani na sasa inakwenda kumaliza ulimwengu , hakika lazima utakufa”Aliongea Gezi , mzee mmoja jini chotara ambaye alikuwa ni moja ya wazee wa umri mrefu ndani ya miliki hio , alikuwa na madirio ya umri wa miaka mia tatu na ushee, muda huo alikuwa akitema damu, huku mkononi akiwa ameshikilia siraha ya Dhahabu iliokuwa katika umbo la koni , alikuwa katika levo ya kati ya maji ya kiroho na Dhana hio ilionekana alikuwa akitumia kwa ajili ya kujilinda.
Ilikuwa ni Dhana ya kati ambapo katika elimu ya majini Dhana hio ilikuwa imebeba roho ya jini pepo aliekuwa na nguvu kubwa aliefahamika kwa jina la Tanywi.
Moja ya nguvu ya siraha hio ni kwamba ilikuwa na uwezo wa kubusti uwezo wa mtumiaji kwa kukusanya kiwango cha ziada cha nguvu ya kijini katika mazingira , lakini sio hivyo tu ilikuwa pia na uwezo wa wa kurahisisha mtiririko wa nguvu hizo kutoka katika senta ya hifadhi ya nishati.
Ilikuwa na uwezo wa kuzuia mashambulizi makubwa na hata kama ikishindwa kutokana na ukubwa wa shambulizi ilikuwa na uwezo wa kupunguza kasi ya mashambulizi.
Sasa ilionekana ndio ambayo iliweza kumlinda mzee huyo na kutokufa katika muda huo maana ilikuwa imetengeza uzio wa rangi ya Dhahabu wa mzingo wa futi kumi na iliweza kumlinda Geyu pamoja na Gezi kwa wakati mmoja.
Lakini wazee hao wote wawili hawakuwa na uwezo wa kujilinda muda mrefu kwani nguvu ya Roma ilikuwa kubwa mno na hawakuonyesha hali ya utulivu , ilikuwa ni kama muda wowote wangeweza kukumbwa na kifo kabla ya msaada wa majini wengine kufika.
”Hata kama nisingeacha kuwaua nyie mngekuja na kutaka kuua familia yangu , haya yote yanayowatokea yametokana na uchokozi wenu”
Roma hakuwa katika mudi kabisa ya kuwasikiliza wala kuwaonea huruma, alikuwa tayari amekwisha kufanya maamuzi ya kuangamiza miliki zote za kijini ,hakujali ni damu kiasi gani angekwenda kumwaga lakini kwasababu asipo fanya hivyo wangemrudia wao basi hakuona haja ya kuwasamehe.
Ilikuwa ni ukichaa lakini ndio mbinu pekee ambayo ni ya moja kwa moja aliona inaweza kumsaidia kuliko kumalizana na majini hao kwa njia ya kidiplomasia.
Chungu cha machafuko kiliendelea kushindana na ngao ile ya wale majini na dakika chache tu hatimae ngao ile iliweza kutengeneza upenyo.
Kutokana na wote wawili walikuwa wakiendesha ile Dhana ili kujumlisha nguvu yao mwanamke aliefahamika kwa ina la Geyu alitema damu mara baada ya ngao hio kutengeneza ufa.
“Geyuu…!!”Gezi alipiga yowe lakini kabla hata hajaiitikia Roma alikuwa ashatuma mashambulizi zaidi ya kumi katika ule upenyo.
Licha ya kwamba waliunganisha nguvu zao lakini uwezo wao bado ulikuwa ni wa chini sana kulinganisha na wa Roma na hata hivyo ilikuwa ni ujasiri na ujuzi wa aina yake ambao wametumia kuweza kumihili mashambulizi ya Roma mpaka wakati huo ili kusubiria msaada.
Kitendo cha kutuma shambulizi ilimtengenezea Roma mwanya mwingine wa kutuma mashambulizi ya moto wa Zambarau na kumshambulia yule mwanamke.
“Ni mwaka wa elfu kumi sasa mpaka kuanzishwa kwa miliki ya Panas , je leo ndio anguko lake”Aliwaza Gezi huku akimwangalia mwenzake namna pumzi inayyoachana na mwili.
Gezi alikuwa akijua kabisa miliki yao ilikuwa na wataalamu wa juu tu wabobezi lakini mpaka muda huo hawakuwa wamejitokeza na moja kwa moja alijua pengine walishajua hawana uwezo wa kushindana na Roma hivyo wakaamua kukimbia.
Alijua hata kama vita hio iishe muda huo ni ngumu sana Panas kurejea katika ukuu wake waliokuwa nao mwanzo kwani hasara ilikuwa ni kubwa mno ambayo haikuwahi kutokea wala kuwaziwa itakuja kuikumba miliki hio.
Roma upande wake aliona kuendelea kuwaangalia majini hao wakijificha chini ya ngao aliona ni swala la kupoteza muda na palepale alikipa kazi chungu na kiliwasogelea kwa kasi na kuwanza kuwavuta katika kila pande.
Gezi alijitahidi kushindana na kasi ya mvutano huo lakini alishindwa hata kusogea , upande wa Geyu yeye alikuwa amekwisha kujeruhiwa muda mrefu hivyo alikosa uwezo wa kuhimili nguvu ya mvutano na aliamua kujitoa tu kafara na kugeuka kuwa chakula.
Gezi aliishia kutoa machozi ya damu mara baada ya kushuhudia kifo cha rafiki yake wa muda mrefu.
Muda uleule wakati Roma akijiandaa kummeza na Gezi ghafla tu vitu kama mawe yaliokuwa meuzi yalirushwa kuelekea upande wake kwa spidi kubwa kama vile ni vimondo.
Roma palepale sura ilijikunja mara baada ya kuweza kuhisi ujio wa kundi kubwa la majini wanaomsogelea.
“Naona wamekuja kuongeza nguvu , vizuri wamenirahisishia kazi ya kwenda kuwatafuta”Aliwaza Roma.
Mara baada ya kugeuka aligeuza nguvu zake za kijini na kuwa kama vile ni shuka na kuyakinga yale mashambulizi yote.
Dakika hio hio Anjiu , Gefu na Wucheni walijitokeza mmoja baada ya mwingine huku wakifuatiwa na kundi kubwa la majini kutoka miliki ya Xia , Kekexil na Hongmeng.
Wale majini watu ambao Roma alikuwa akiwasubiria kwa muda mrefu kujitokeza hatimae walikuwa mbele yake.
Gefu chozi la maumivu lilimtoka mara baada ya kuona makao makuu ya miliki yake yalikuwa yameharibika kwa kiwango ambacho hakivumiliki na palepale hasira zilimvaa na nia ya kumuua Roma iliongezeka kwa zaidi ya mara elfu moja.
“Huyu moto ni katiri mno , inaonekana kama vile ametawaliwa na roho ya Chaos na kugeuka kuwa muuaji”Aliongea Shombeli.
“Nguvu ya huyu binadamu sio ya kawaida kabisa , ndio kwanza ana miaka ishirini hivi , inasikitisha kwamba ameruhusu shetani amtawale , kama tukishindwa kumuua leo hii hakika atakuja kuwa tatizo kubwa kwetu”Aliongea Menyu.
Muda huo Gezi aliweza kufanikiwa kukimbia kwenda upande wa wenzake na kuanza kuelezea hali ilivyo kwa mkuu wake.
Kwa maelezo ya Gezi ni kwamba mpaka wakati huo Roma amekwisha kuua majini wengi sana ikiwemo viongozi watatu wa juu sana na taarifa hio ilizidi kumkasirisha sana kiasi kwamba alitamani hata kutema damu.
Kitu ambacho kilimshangaza ni namna uzio wa kuingia katika makao makuu hayo ulivyovunjwa.
Roma aliangalia mamia ya majini hao ambao asilimia kubwa wote walikuwa ni wale wabobezi na walionekana kuwa na ari kubwa ya kutaka kumuua , hakuna hata mmoja aliekuwa akimwangalia kwa macho mazuri.
“Haina haja ya kuongea ujinga , haijalishi ni maamuzi gani ninachukua lakini hamna haki ya kutafsiri matendo yangu watu kama nyie mnaojitafutia umaarufu kupitia migongo ya wengine , Mungu anaangalia kila maamuzi mnayochukua na kila hatua mnayopiga na kilichotokea siku ya leo ni kutokana na tamaa zenu , mimi Roma Ramoni muwakilishi wa binadamu dhamiri yangu ni ya wazi , angalau mimi sikatati pale ninapoua mtu wala ninapofanya makosa , ninachotaka sasa hivi ni kuwaueni wote na damu yenu kusafisha ulimwengu huu wa majini , kama uwezo mnao pambaneni na mimi vinginevyo msinilaumu kwa kutowapa nafasi ya kuonyesha uwezo wenu , nataka kuona ni kipi mnachoweza kunifanya leo hii”
“Wewe kibinadamu hakika una majigambo sijapata ona , hivi unaamini una nguvu kubwa kuweza kupambana na majini mia moja kwa wakati mmoja ,pengie leo hii ningekupa tu adhabu kwa kuzingatia asili yako lakini ulichokifanya leo hakisameheki”
Roma alishangazwa na kali ya Wucheni kusema maswala ya asili lakini hakutaka kujua anamaanisha nini maana alikuwa mvivu wa kufikiria.
Wucheni palepale alisogea mbele na mwili wake wote ni kama vile umefunikwa na gamba lingine la ngozi huku nguvu za kijini zikimtoka kama vile ni ukungu wa asubuhi na ghafla tu siraha ndefu sana ilitokea katika mikono yake.
Siraha hio ilikuwa ni nyeusi tupu na rangi ya bluu huku ikiwa na michoro ya kustaajabisha ya kikale iliokuwa imechorwa , ilikuwa ni mwishoni katika makali ndio kulikuwa na rangi ya bluu bahari.
Siraha hio ilikuwa kubwa kwa futi kama kumi hivi na ilikuwa na upana mkubwa mno , ilikuwa ni siraha kubwa mno ya kimaajabu lakini mbele ya jini huyo haikuonekana kama siraha nzito kuishikilia.
“Wucheni kiongozi wa hadhi naona namna ambavyo upo siriasi mara baada tu ya kufika ushatoa huo upanga wa kimilenia”
“Lazima nifanye hivyo ninaeshindana nae hapa tayari ashaivuka radi na anatumia Dhana ya kihistoria ya Chaos Cauldron , ijapokuwa siraha yangu ilitumiwa na jini aliekuwa na nguvu na imejaa r nguvu ya roho ya kukatisha tamaa lakini bado haina nguvu kama Cauldron”
“Ni ngumu kutabiri pia , hapa kuna damu nyingi imemwagika na chanzo cha nguvu ya upanga huo ni damu , nadhani nguvu yake itaongezeka kwa kasi”
“Lakini kiongozi uwezo wake…”
“Kwanini unajaribu kukadiria uwezo wa adui yetu?”Aliongea Shombeli akimkatisha moja ya majini kutoka Hongmeng ambaye alikuwa akitaka kuongea..
“Siraha ya uungu wa Nebula!!”
Shombeli aliongea kwa nguvu na palepale nguvu zake za kijini ni kama zilikuwa zikijikusanya na kufumba na kufumbua siraha ya rangi iliweza kutokea mbele yake .
Dhana hio ilikuwa ni ya kimaajabu ya daraja la kati la kimaajabu na mashambulizi yake ni yale ya kutokutabirika , kutokana na uwezo wake wa kutumia siraha basi nguvu yake haikuwa ya kupuuzwa.
Kulikuwa na Dhana ya upanga mweusi na kushoto kulikuwa na siraha ya kinebula , majini wengine na wenyewe hawakuzubaa walikusanya kila walichokuwa nacho na kumzingira Roma.
Anjiu na Gefu pia waliungana pia pamoja na wafuasi wao kwa ajili ya kushambulia , ilionekana hawakuwa na sababu ya kushambulia mmoja mmoja bali wote walitaka kufanya mashambulizi.
Roma macho yake yalisinyaa na palepale hisia zake zilimwambia pengine hao majini wamekuja na mbinu ya kutaka kummaliza mapema na kama atakurupuka kushambulia mmoja wapo anaweza kuzidiwa hivyo alisubiri kuona wanachokipanga na kuangaia namna ya kuwadhibiti mmoja baada ya mwingine.
“Nafsi pepo kutoka Kaskazini, Shibe mmiliki wa barafu”
“Utupu wa mzimu katika anga ya Nebula!!”
Ule upanga wa Wucheni ulifyatuka kwenda agani na kugeuza chini na kuanza kutengeneza mapanga mengi na kumshukia Roma kama mishale.
Silaha ya kiuungu ya Nebula ilitengeneza kitu kama shimo ambalo halina hewa ndani yake na kumshukia Roma na kumuweka kati.
Roma alishangazwa na namna ambavyo Wucheni na Shombeli walivyokuwa spidi ya kufanya mashambulizi.
Dakika ileile kulitokea boma la barafu kubwa ambalo lilikuwa ikijjijenga kwenda juu , kitendo kile kilimfanya Roma kukumbuka aina hio ya ngao na mawazo yake yalimrudisha kwa mtu aliemshambulia kule Australia.
Palepale akili yake ilimwambia mtu ambaye aliemshambulia akiwa kule Arnhem Australia akiwa katika vazi la Mask pengine ni Wucheni jini wa miliki ya Hongmeng.





SEHEMU YA 753.
Roma hakuwa na uhakika pengine labda amuulize yeye mwenyewe , maana siku ile alikuwa amevalia Mask lakini nywele zake zilikuwa tofauti kidogo siku hio hivyo hakuwa na majibu sahihi kama mtu aliemshambulia wakati akitafuta miti shamba ni huyo huyo Wucheni.
Roma hakuwa na muda wa kuwaza kwani aliona ni kama vile anatengenezewa gereza la kukamatiwa katikati.
Roma pia hakutaka kuttubutu kuruhsu nguvu ya mashambulizi ya siraha ile ya Nebula kumfikia na palepale alitumia Chungu kukinga mashambulizi yote , ijapokuwa chungu kilikuwa kipipitia mapigo ya nguvu hio lakini kutokana na udhibiti wake aliweza kukinga mashambulizi yote mawili ya Wucheni na Shombeli.
Hakukuwa na ubishi majini hao wanne walikuwa ndio mhimili wa Hongmeng kutokana na uwezo wao na ili kuhakikisha wanashinda pambano walitumia uchawi wa kilevi na kufawafanya majini hata wale wa levo ya chini kuingiwa na hali ya kujiamini na hofu ya kifo iliwatoweka.
“Roho usie na mipaka ,Vifungo vva kuzimu”Aliongea Shombeli
Wakati ule Roma alipokuwa akitaka kufanya shambulizi kuvunja boma la barafu lisilioelezeka , zile panga za nguvu za kijini ambazo zilitumwa na Wucheni kumshambulia hazikumffikia moja kwa moja bali zilikuwa zikizunguka hewani na kutengeneza mfumo wa ajabu mno.
Roma palepale alijua nini kinatokea , ilionekana zile panga zilikuwa zikifyonza nguvu ya damu ya majini iliokuwa imemwagika katika ardhi ili kujiongezea nguvu.
Roma palepale aliona ashambulie panga zile kabla hazijaendelea kujikusanyia nguvu zaidi na zaidi lakini sasa ile anataka kufanya mashabulizi zilifyatuka kwa namna ya kutawanyika na kisha zilielekea kwenda ardhini kwa kasi kubwa mno.
Ilikuwa ni kitendo cha sekunde tu zile panga zote ziliungana na kutengeneza mkuki mmoja wa nishati ya mbingu na ardhi na kumsogelea Roma kama mshale kwa spidi kubwa mno
“Bang , Bang , Bang!!”
Ile siraha iliokuwa kama mkuki kabla haijamkaribia Roma kulitokea mlipuko na kufumba na kufumbua kulitokea mapanga marefu mengi zaidi ya nishati na kuungana kwa namna ya kipekee na kutengeneza kitu kama kijumba hivi ambacho kilimfanya Roma kuwa ndani yake kama vile ni kijumba cha mbwa.
Ilionekana ni gereza la nishati ya mbingu na Ardhi ambalo siraha zile imetengneza kwa ajili ya kumkamata Roma.
Roma alishangazwa na uwezo wa kimaajubu aliokuwa nao Shombeli na Wucheni , ulikuwa ni uwezo wa kichawi ambao aliweza kuuona katika vitabu mara baada ya kutembelea dhehebu la Tang kule China milima ya Shushan.
Lakini licha ya kumtengeneza gereza lile la visu lakini bado nguvu yake haikuwa kubwa zaidi kumzingira Roma.
Roma mwili wake ulikuwa umemezwa na roho ya hasira , ya vifo na uozo, ilikuwa ni kama vile visu vile vilikuwa vimepakwa sumu ya nyoka.
Visu vilizid kuungana katika gereza lile kwa kasi kumzingira Roma lakini hata hivyo bado kigereza hicho kilikuwa dhaifu kuhimili moto wa rangi ya zambarau.
Ilimtumia Roma sekunde tu kujinasua katika gereza la visu na alichokuwa akitaka ni kuweza kupitisha mashambulizi yake katika boma ya barafu aliotengeneza Wucheni lakini ni kama alikuwa akisubiriwa kwani ile Dhana yake ya Lindi(Abyss) ilikuwa ikikusanya nguvu za giza kutoka katika kila pande na kuifanya kuwa hatari zaidi na zaidi.
“Hii ni…”
Roma macho yake yalisinyaa kutokana na uelewa wa nguvu za giza , Roma uwezo wake wa kuhisi roho ya kimizimu ulikuwa ni mkubwa mno kuliko mwanzo.
Sasa kilichokuwa kikifanyika ni kwamba wale majini ambao walionekana kufariki roho zao bado hazikuwa zimekimbia mbali zilikuwa zikizunguka ndani ya eneo hilo na ile siraha ya Wucheni ndio ilikuwa ikikusanya nguvu za roho hio na kutengeneza lindi kubwa la makali(ferrocius)kutoka katika hio Dhana.
“Haha… wewe pia ni shetani, unatuhubutu vipi kuniambia mimi nikichaa niliepotoka wakati siraha yako hio ya maajabu imefanikiwa kukusanya roho za hao majini waliokwisha kufa , hata kama hao majini wamekwisha kufa bado hawawezi kukupatia nguvu kubwa ya kushindana na mimi”
Aliongea Roma na palepale alifyatuka kuelekea chini ya ardhi ikiwa kama vile anafanya mawasiliano ya anga na ardhi na palepale aligeuza nguvu zake za kijini na kuwa donge la moto wa nguvu ya giza na kisha alimsogelea Wucheni kwa spidi kwa kutaka kumshambulia nalo.
“Pepo barafu wa Kaskazini , mvua ya mishale barafu,visosi mia moja vya barafu kutoka madhabahu ya Shibe!!”
Wucheni ambaye alikuwa juu ya Roma alifyatua ile siraha yake na ilitokea vitu kama mishale ya midogo ya barafu na kumvaa huku vitu kama vile ni visahani vya barafu vilienda kumvaa Roma kwa spidi kubwa.
Ilionekana Wucheni alikuwa ametumia nguvu kubwa kumshambulia Roma lakini ukweli ni kwamba Roma alikuwa na nguvu kubwa mno kuweza kujeruhiwa na shambulio la namna hio.
Mpango wa Shombeli na Wucheni ni kumkamata Roma ili asiweze kutumia nguvu zake za kijini na kisha Anjiu na wenzake waanze kumshamblia lakini kila namna ambavo walikuwa wakifanya ilikuwa ngumu kwao kumkamata na mashambulizi ya namna yoyote ile.
Walitumia mbinu lakini hawakuweza kumfanya Roma chochote kwani kila mtego waliokuwa wakijaribu kumkamata nao ulishindikana kabisa.
Baada ya kuona wameshindwa Gefu alimpa ishara Shozi aingie na yeye kazini kutekeleza mpango wao.
Wucheni roho ilikuwa ikimtoka , kitu pekee ambacho waliweza kufanikisha ni kumfanya Roma kutokufanya mashambulizi kwani walikuwa wakishambulia kwa spidi kubwa.
Sasa mara baada ya Shozi kuingia kazini kitu cha kwanza kabisa alichokifanya kilimshangaza Roma kwani alianza kutokwa na damu kama vile ni mgonjwa wa Ebola kwani damu ilitoka katika kila tundu la kichwa chake.
Sijapambana nae lakini ashaanza kutoa damu kila tundu , anajaribu kufanya nini?”Aliwaza Roma akiwa kwenye mshangao lakini ni ndani ya muda uleule aliweza kukisia kinachokwenda kutokea , ilionekana kuna mbinu ya kimaajabu ambayo ili kuamka lazima atumie damu yake.
Roma alipata wazo mara baada ya kuona hakuwa akitema damu tu bali kulikuwa na vitu kama vile ni vijisumari vidogo vidogo ambavyo mara baada a damu kukauka nguvu ya ajabu ilianza kusambaa , ilikuwa ni msisimko wa nguvu ya ajabu mno na ilikuwa ni kitendo cha kufumba na kufumbua lilitokea fuvu la kiumbe cha ajabu katika mkono wa Shozi ambalo limetapakaa damu.
Ilikuwa ni dakika ileile Roma sasa alweza kujua alichokuwa akifanya mara baada ya vile vitu kuongezeka ukubwa , misumari ile ilikuwa jumla yake ni tisa
Shozi mwili ulikuwa ukimtetemeka mno na damu kuzidi kumtoka na ilikuwa ni ndani ya sekunde chache tu yalitokea mafuvu tisa .
Roma hakutaka kujiluliza mara mbilimbili mara baada ya kuona ile misumali ya skeletoni inamsogelea kwa kasi kubwa mno huku ikizalisha nguvu ya ajabu.
Lakini sasa Roma alijua pengine inakwenda kumshambulia lakini mara baada ya kumkaribia ilitawanyika katika umbali wa futi kama kumi na mbili hivi na kufumba na kufumbua ile misumari tisa ya mifupa iliungana na yale mafuvu na kutengeneza umbo la Dimenssion tatu.
Ilikuwa ni kufumba na kufumbua Roma alijikuta akiwa ndani ya boksi la damu , ilionekana dhamira ya shambulizi lile sio kwa ajili ya kumshambulia bali kumkamata.
Roma aliishia kukunja ndita kwani hakutemgemea tukio la namna hio , ilionekana majini walikuwa na vitu vingi mno vya kuonyesha kabla ya pambano kuisha.
Roma hakutaka kulembesha alijua hakuna namna anaweza kufungiwa katia mtego wa namna hio na palepale aliandaa bomu la nguvu za mbingu na ardhi na kujaribu kulipua lile boksi.
“Boom!!
Mara baada ya mlipuko mkubwa wa kuumiza masikio kutokea Roma alijikuta akilia ndani kwa ndani mara baada ya kuhisi maumivu makali sana.
Roma alihihisi ni kama vile yupo kwenye chumba ambacho kuta zake zote zimejengwa kwa vioo vya kujiangalia na kila anachokifanya ni kama vile kinamrudia.
Yaani lile shambulizi lake lilidunda katika kuta na kisha likamrudia yeye mwenyewe na kumuunguza.
“What the hell!!!”
Roma alipiga yowe mara baada ya kuuguzwa na moto wa rangi ya zambarau ambao alitumia kushambulia
Roma aliishia kusambaratisha moto ule ili usimuunguze bahati nzuri ni kwamba hakuogopa moto wa namna hio kutokana na mbinu yake ya adiko
Mara baada ya kuona ni kama Roma anajishambulia mwenyewe baada ya kuingia katika mtego waliomwandalia majinii hao walianza kuangua kicheko kikubwa mno na wote walionyesha ishra kwamba wanakwenda kushinda hilo pambano.
“Wewe mtoto Roma hivi unadhani hakuna mtu ambaye anaweza kupambana na wewe , , yaani unakuja kwenye ulimwengu wa majini kwa ajii ya kushindana na sisi wabobezi wa nishati za mbingu na ardhi , ni majigambo ya namna gani hayo kutuchukuliwa kiwepesi namna hio”Aliongea Menyu.
“Hakika Shozi unastahili kupewa sifa ya uti wa mgongo wa usalama wa miliki ya Panas”Aliongea Umini akimsifia Shozi.
“Hey! .. khoo ..koho”
Shozi alishia kucheka lakini alionekana kupaliwa na kikohozi mfululizo na kulikuwa na damu iliokuwa ikimtoka pembeni kwenye midomo.
Uso wake ulikuwa umepauka sana lakini alizidi kubadilika na kuwa kama mti mkavu na nguvu yake ya kijini ilionekana kupungua kwa kiasi kikubwa.
“Gefu awamu hii uliniambia nije na nishafanya ulichoniambia , kwasasa nishakuwa dhaifu tayari hivyo unapaswa kunilinda , isitokee baadhi ya wahalifu wakatumia udhaifu wangu kunishambulia”a
“Usiwe na waswasi Shozi, leo hii hawa wote waliokuwa mbele yako wapo hapa kwa ajili ya kushuhudia kifo cha Roma Ramoni na wewe ni muokozi wetu”Aliongea Gefu
Shozi aliishia kucheka na alisema hivyo ili kila mmoja kuweza kusikia ili kama ikitokea yoyote kumshambulia ili moja kwa moja iwe ni aibu kwake.
Ilikuwa ni wakati huo macho yao yote yalikuwa yakimwangalia Roma aliekuwa kwenye boksi la damu , Roma alikuwa akitumia kila mbinu ili kujitoa katika mtego wa boksi ambalo amewekewa , alijaribu hata kuvuta boksi hilo na Cauldron lakini kila alivyokuwa akijaribu kushambulia mapigo yalimrudia yeye mwenyewe kitendo ambacho kilimfanya kupata majeraha makubwa ambayo ameyasababisha yeye mwenyewe.
Ilikuwa kwa bahati nguvu ya andiko la urejesho wa azimio lilikuwa na spidi ya kumponya.
Roma alijaribu kutumia upanga kushambulia ukuta wa kingo za boksi lile na alikuja kugundua kila alivyokuwa akishambulia kuna vitu kama vile vipele vya damu vivyokuwa vikisambaaa katika mwili wake na kisha hugeuka na kuwa kama vipele vyeusi na kupasuka kisha kufutika.
Roma alijiuliza au ni tindikali lakini mara baada ya kuangalia kwa umakini aliweza kugundua kwamba ukuta huo ulikuwa ukiongezeka nguvu kutokana na kwamba ile damu ambayo ilikuwa ikigusana na mwili wake ilikuwa ikinyonya nguvu yake kwa kukausha damu.
Roma alijua kama ataendelea na mbinu hio hio hawezi kuondoka hapo kwani kadri atakavyokuwa anashambulia ukuta huo basi ndio nguvu zake zitakvyokuwa zinaisha na ukuta kuzidi kuimariaka.
“Kijana usihangaike sana , nitakufanya ufe kwa amani , hio ni Dhana ya misumari tisa ya mfupa wa Dragoni na mafuvu yake, ijapokuwa ni Dhana ya daraja la kati lakini ilitengenezwa na mababu zetu wa enzi hizo kwa ajili ya kukamata majini pepo wenye levo kubwa kufikia levo ya kuidhibiti radi pale wanapokiuka sheria
Hii dhana ya kimajabu inafanya kazi kwa kunyonya damu ya mzee wa miaka mia tatu na kila inapotumika itatumia kiasi kikubwa cha damu lakini inao uwezo wa kufukuza na kukamata adui , ukishakamatwa na mtego wake kazi yake ni kunyonya damu kila mara inapokutana na nguvu za kijini , ijapokuwa uwezo wangu sio mkubwa sana lakini unatosha kabisa kukukamata mtu kama wewe ambaye umekwisha kuipita dhiki ya radi, haijalishi Chaos Cauldron ina nguvu namna gani lakini hakiwezi kuvunja huo mtego”
Roma mara baada ya kusikia maelezo hayo aliishia kuchukia , ilionekana majini wa enzi hizo walikuwa na juhudi kubwa katika kushambulia wenzao waliokuwa levo za juu mpaka kuunda Dhana hio.
Lakini alijiuliza kama Dhana hio ni ya zama za kale imewezaje kufika katika mikono ya Shozi.
Ukweli ni kwamba hio Dhana ilikuwa mali binafsi ya Shozi na sio ya Panas na kabla ya kuja katika miliki hio alikuwa nayo tayari haiikueleweka aliipata vipi lakini ilikuwa na nguvu kubwa mno.
Shida kubwa ni kwamba Dhana hio ili kuendelea kuwa na nguvu lazima inyonye damu na kwasababu hio Shozi alikuwa ameua majini wengi sana kwa ajili ya kulisha hio Dhana.
Ilikuwa ni Dhana hai ya kijini ambayo ina tabia kama za Vampire bila damu haifanyi kazi na inalishwa damu hio kila baada ya siku therathini katika kipindi cha mwaka mzima , uzuri ni kwamba damu haijalishi hio ina nguvu za mbingu ili mradi iwe ni damu tu lakini damu ya jini mwenye nguvu kubwa ndio faida huwa kubwa.
Kama ilivyokuwa kwa Dhana ya Cauldron kutaka kumvaa Roma basi dhana hio pia ilikuwa ikimfanya Shozi kukonda kwani ilikuwa ikifyonza damu yake kila siku na ndio maana ngozi yake ilionekana kuwa kavu na kuwa kama vile amechakaa.
Roma hakutaka kuamini kirahisi maneno ya Shozi hivyo alijaribu kuita nguvu za kijini kushambulia boksi hilo ili kuchoropoka.
“Mnasubiri nini , ili kumzuia kabisa asipate nafasi ya kutoka kwanini msiunganishe nguvu zenu za kijini katika misumari yangu ili tumkaushe damu na kumuua kwa haraka “Aliongea Shozi.
Anjiu na wenzake mara baada ya kusikia kauli hio hawakutaka kuzubaa na kila mmoja alishikilia msumari wake wa Dragoni katika kila fuvu na kisha wakapitisha nguvu zao za kijini ili kuongezea nguvu Roma asiweze kuchoropoka.
Kadri walivyokuwa wakilisha nguvu ile misumali ya skeleton lile boksi lilizidi kukorea rangi na kuwa la damu tupu na kumfanya Roma kutokuonekana kwa nje.
Roma hakujua nguvu ya boksi hilo mara ya kwanza lakini hatimae sasa alijua nini kinafanyika , kwani ngozi yake ilianza kuota vipele vyeusi vingi sana kwa kasi kubwa na nguvu zake za kijini ni kama vile zinapungua kila mara baada ya vipele hivyo kupasuka na kukauka.
“Pumbavu kabisa inaonekana huu ndio ulikuwa mpango wao tokea mwanzo ndio maana wakakusanya majini wengi namna hio”
Aliwaza Roma na pale karibia majini yote waliunganisha nguvu zao na kuzichaneli katika ile misumari na kadri walivyokuwa wakifanya hivyo lile boksi lilizidi kuwa jekundu kama vile karatasi ambalo limeloa damu na kuta zake kuzidi kuwa pana.
Roma vipele vilizidi kumtoka na vilikuwa vikitoka kwa awamu na kisha vinapasuka na damu inapotea na kisha jeraha linapona na vinaota tena kwa kasi kubwa huku akihisi maumivu makali mno.
ITAENDELEA.
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA .

MTUNZI SINGANOJR.

Mono no aware

SEHEMU YA 754.
Roma aliishia kukunja sura akiwa ndani ya Kizimba(Cage) amekunja ngumi kwa hasira huku akiwa kimya wakati vipele vikienelea kuota katika mwili wake na kunyauka kwa kasi.
Wakati Roma akionekana kama vile amejikatia tamaa kabisa majini wale walishangilia na kuridhika kabisa.
“Haha..ulikuwa na maringo sana lakini sasa hivi umekuwa mpole kama mbwa , unaonaje ukipiga magoti na kuomba msamaha?”Aliongea Menyu mkuu wa miliki ya Kekexil huku akicheka kicheko cha furaha.
“Nadhani anaogopa sana hapo kiasi cha kushindwa kuongea chochote , ndani ya lisaa limoja na nusu huyu shetani atakuwa amekwisha kufa”Aliongea Gefu akiwa katika hali ya kutabasamu
“Uhai wa raia wa Panas zaidi ya elfu moja umepotea katika mikono yako hivyo ni damu yako inakwenda kulipia deni”Aliendelea kuongea.
“Haina haja ya kupoteza maneno yetu , tumuueni kwa nguvu zetu zote ili kusitokee tatizo kabisa”Aliongea Anjiu.
Majini hao hatimae walikaa kimya lakini hakuna ambaye alijali kwani asilimia mia moja wote walikuwa wakitaka kuona kifo cha Roma.
Dhana ya fuvu la misumari tisa ya mfupa wa Dragon iliendana na jina lake , majini hao katika vitabu vyao walisoma na kuelewa kwamba ambao washawahi kutumia Dhana hio wengi wao wamekwisha kufa kutokana na kunyonywa damu.
Ukweli ni kwamba hata kwa Shozi ambaye alikuwa mdhibiti wa Dhana hio, kama akifanikiwa kumkamata Roma katika kizimba hicho cha damu baada ya hapo kuna uwezekano mdogo sana wa kuendelea kuishi muda mrefu , hio Dhana athari yake kubwa ni kupunguza urefu wa maisha kutokana na kwamba inanyonya uhai kupitia damu.
Roma alikuwa amesimama katikati ya boksi hilo , chungu chake cha maafa kilikuwa pia kipo ndani kikielea katika kichwa chake, ule ukali wa chungu hicho ulionekana kupungua kabisa.
Dakika iliofuata baada ya Roma kunyanyua kichwa chake uso wake haukuonyesha ishara yoyote ya wasiwasi lakini viashiria vya kukata tamaa vilionekana kwa mbali.
“Inanishangaza kuona bado unao uwezo wa kutumia huo mkono…”
Majini hao waliokuwa wamezunguka kizimba hicho cha gereza la damu hawakumwelewa Roma anachomaanisha na walioamini anaongea ujinga.
Roma mara baada ya kuwaza kwa dakika kadhaa palepale aliweka kila alichokuwa amekishikilia katika hifadhi ya pete na kisha mkono wake mmoja wa kulia alibadilisiha nishati za mbingu na ardhi kwa kutengeneza moto wa rangi ya zambaranu na mwingine akatengeneza moto wa rangi ya bluu na madonge yale ya moto yalizidi kuongezeka ukubwa kadri sekunde zilivyokuwa zikisonga.
“Dogo bado tu unahangaika , unachokitafanya ndio kitakuua mapema”Aliongea Umini.
Roma alimpotezea kabisa na wakati moto ule ukiwa unawaka katikam mikono yake alifanya kitu kama vile anapiga makofi ili kuunganisha ule moto kwa pamoja.
“BOOM!!
Moto wa rangi ya Zambarau na wa bluu uligongana na kusababisha kishindo cha aina yake , ilikuwa ni kama vile aina hizo mbili za nishati zilikuwa zikiumana na kujaribu kumezana kwa wakati mmoja.
Ilichukua sekunde kadhaa tu kama vile kemikali zimeungana hatimae kulitokea matokeo mengine kabisa ambayo ni ya kimaajabu mno.
Roma mikono yake ilikuwa ikitetemeka kwa nguvu kama vile inaungua na alitumia nguvu ambayo sio ya kawaida kujaribu kuhakikisha nguvu hizo mbili za moto zinaungana ili kutengeneza kitu kingine.
“Buzz. Buzzz, Buzzz!!!!”
Ilikuwa ni cheche za umeme ambazo zilitoa sauti flani hivi kama ile ambayo inasikika wakati wa mafundi wakichomelea chuma na umeme lakini yenye sauti kubwa mno.
Mwanga wa ajabu uliweza kutokea pia katikati ya viganja vya mikono ya Roma na kuna kitu ambacho ni kama vile kinafutuka kana kwamba muda wowote kinakwenda kulipuka.
“Hicho ... hicho ni……!!!!!”
Anjiu ndio aliekuwa wa kwanza kuhamaki mara baada ya kuhisi kitu cha ajabu , macho yake yalikuwa yamepanuka kiasi kwamba yanataka kumchomoka.
Wucheni na wenzake pia walianza kuhisi nguvu ya ajabu ikitoka katika eneo ambalo amesimama Roma , ilikuwa ni nguvu ambayo hawakuwahi kuihisia katika maisha yao yote na ilionekana nguvu ile ilikuwa ikianza kula ukuta wa kizimba cha damu.
Mwanga uliokuwa ukionekana katikati ya mikono ya Roma ulizidi kuongezeka na kuzidi kuwa na nguvu sekunde hadi sekunde.
“Hehe.. hahaha simaanishi ,,, kila kitu kilichopo chini ya nguvu ya radi ya mapigo mengi , moto wa mbingu na maji ya kiroho hayana nguvu.. dah .. ninashauku .. kama nguvu ya radi ya mapigo tisa athari zake zilivyo”
Roma alikuwa akibwabwaja mwenyewe maneno ambayo hayakuwa yakieleweka ilionekana ni kama vile kuna ufunuo anaupata.
Palepale aliinua sura yake juu kama vile anaangalia anga huku akitunisha kifua na ghafla tu mikono yake ilijiachia.
“Hey!!”
Ghafla tu shoti ya radi ya mwanga wa bluu na zambarau ilitoka katika mikono yake na kutengeneza umbo kama la mkuki uliopinda pinda huku ukitoa cheche.
Mwanga wake ulikuwa ni mkali mno na ndani ya sekunde tu Roma alikuwa amefunikwa na mwanga ule na sehemu aliosimama ilionekana kama vile ni jua la rangi ya bluu zambarau na ngurumo kubwa ilianza kugonga na mwanga ulikuwa ukizidi kuongezeka na kuwa mkubwa sekunde hadi sekunde.
Upande wa Roma alikuwa akiendelea kuzalisha moto wa bluu na wa zambarau katika mikono yake na kuunganisha kwa spidi kubwa na kadri alivyokuwa akifanya hivyo ni kama yeye mwenyewe anageuka na kuwa nishati ya ajabu vile.
Ndani ya sekunde chache tu kile kizimba cha damu kilibadilika rangi na kufunikwa na mwanga na ngurumo za radi zilizidi kuongezeka na shoti za rangi ya urujuani zilianza kutoka.
“Haiwezekani … radi ya Zambarau!!!?”
Gefu ndio aliekuwa wa kwanza kuhamaki , huku majini wengine wakiwa ni kama hawaamini kile ambacho wanakiona mbele yao.
Unachopaswa kuelewa ni kwamba moto wa bluu unatokana na mapigo tisa ya radi yaani kwa lugha nyepesi ile nguvu ambayo unaipata baada ya kupitia mapigo tisa ya radi ndio inakufanya kuweza kudhibiti moto wa bluu , upande mwingine mapito tisini na tisa yanakupa uwezo wa kutengeneza moto wa zambarau.
Sasa kwa haraka haraka Roma ni kama ameunganisha nguvu ya radi ya mapigo tisini na tisa na nguvu ya radi ya mapigo tisa na kufanikiwa kudhibiti radi ya rangi ya urujuani(Violet).
Sasa majini walishangaa mara baada ya kuona Roma amegeuza moto wa bluu na wa zambarau kutengeneza radi ya zambarau.
Shozi ambaye ndio alikuwa akidhibiti kizimba cha misumari na mafuvu tisa ya mfupa wa Dragoni alianza kutetemeka kwa maumivu ,ilikuwa ni kama vile mwili wake unakwenda kupasuka kutokana na presha kubwa iliokuwa ikimwingia.
“Haraka ongezeeni nguvu ya nishati za mbingu kuimalisha ulinzi , anataka kujinasua!”Aliongea Shozi kwa kubweka.
Haikujalisha aliongea kwa sauti kubwa namna gani lakini majini hao mioyo yao ilikuwa imetingishika kabisa na kukosa ujasiri.
Moja ya udhaifu wa majini ni radi(Wenyewe wanaita moto wa mbingu) , wanaiogopa radi kuliko kitu chochote kile na ndio adhabu yao kubwa ambayo ukiipita wanakupa heshima.
Kile kizimba kilishindwa kumnyonya Roma damu tena na sekunde baada ya sekunde kilikuwa kikipoteza nguvu.
Anjiu macho yake yalionyesha hali ya kusita kulikokithiri , alikuwa pia ni jini ambaye amepitia mapigo ya radi hivyo swali liliibuka kwanini Roma kuwa na mwili wenye utimamu wa namna hio mpaka kufanikiwa kuidhibiti radi , alishakuwa katika mshangao kwa uwezo wake wa kudhibiti moto wa bluu , Wa zambarau na maji ya kiroho lakini wakati huo amefanikiwa pia kuidhibiti radi ya rangi ya urujuani.
Alijiambia hapana haiwezekani sio ujuzi pekee wa Roma katika kung’amua siri za mafunzo ya mbingu za ardhi na mbingu tu , pengine ametawaliwa na nguvu ya roho ya andiko la Urejesho.
Kadri alivyokuwa akiwaza ndio namna ambavyo alizidi kuwa na hasira , alijiambia kwanini sio yeye mwenye kumiliki mbinu hio ya andiko la urejesho wa azimio, kwanini ashindwe na binadamu ambaye amejifunza utamaduni wao.
Yeye ni jini kikamilifu kwanini ashindwe na binadamu ambaye hana damu ya kijini.
Pengine Roma angeangua kicheko kama angejua kile ambacho Anjiu alikuwa akiwaza , mbinu hio ya mafunzo ilikuwa amepatiwa ndio lakini hakuwa akiwaza watu wanavyoichukulia wala kuamini uwezo wake.
“Kama nilivyotarajjia , ijapokuwa hichi kizimba chenu kinaweza kuwa kama gereza kwa jini mwenye kuipita radi lakini ni ngumu kuhimili shambulizi la radi ya Urujuani ambayo hata jini ambaye amepitia mapigo elfu moja anaogopa”Aliongea Roma.
Aliangalia kizimba hicho ambacho tayari kilikuwa kikitetema na alijitingisha kidogo tu radi ile ya Zambarau ilitoka kama vile ni mshale na mara baada ya kugusana na kingo za kizimba kile kilipasuka na kuharibu kabisa ile Dhana.
Roma ni kama vile hakuwa na uwezo wa kudhibiti uwezo wake na kama angejua nguvu ya radi hio ilikuwa na nguvu namna hio asingetumia kiharibu Dhana hio kwani angeipata huenda ingekuwa na matumizi kwake hapo baadae.
Lawama alizipeleka kwa jini Shozi kwa kutokuwa na nguvu za kutosha za nishati ya mbingu na ardhi ndio maana shambulizi lake moja limeharibu Dhana hio.
Shozi mara baada ya Dhana yake kuharibiwa ilikuwa ni kama moyo wake ndani umepasuka na alitema damu nyingi sana na uso wake ulikuwa mweupe kama vile ni karatasi kutokana na kukosa damu na hakuendelea hata kusalia katika anga kwani alidondoka chini kama kifusi akiwa katika hali ya kukata tamaa kabisa.
Dhana ya misumari na mafuvu tisa ya mfupa wa dragoni ndio uikuwa ni kiini cha uhai wake na kitendo cha kuharibiwa na pigo la radi ya bluu zambarau haikuwa tu nguvu zake za kijini kumpotea lakini pia kifo kilimpata .
Hatimae Roma alikuwa amechoropoka kwa mara nyingine katika mtego wao wa kizimba cha damu na sasa alirudi na kusimama katikati ya mbingu na ardhi, kwa jinsi mwili wake ulivokuwa ukipumua ni kama kila sehemu ya mwili wake kulikuwa na moyo unaosukuma damu.
Roma sasa alikuwa ameijua siri ya radi ya zambarau , yaani alikuwa kama ule mnara wa kuingia katika ulimwengu wa majini pepo , radi na Roma ilikuwa ni kitu kimoja.
Anjiu na majini wenzake wote walionyesha hali ya hofu katika macho yao , walikuwa wamemzingira kwa umbali mrefu sana na hakuna ambaye aliweza kuthubutu kusogea karibu hata kwa nchi moja , wote walikuwa wakiogopa nguvu ya radi iliokuwa ikimtoka Roma.
Radi ilikuwa na uwezo wa kuharibu sio mwili tu bali mpaka roho na nafsi na kupotea katika anga.
“Inaonekana tayari umekwisha kufanikiwa kubobea katika kuidhibiti radi ya Zambarau ?”Aliongea Anjiu , ijapokuwa alikuwa kwa mbali lakini sauti yake ilikuwa ikisikika kwa ukaribu.
Roma alinyanyua mkono wake mmoja na ile anafungua kiganja ilikuwa ni kama vile kuna mnyororo wa radi unamtoka na kwenda angani na kutengneza kitu kama upinde.
“Kama ilivyokuwa siku ile nilivyoficha kete yangu ya ushindi leo pia ni hivyo hivyo , kama ningekuambia nimeweza kugundua siri ya kuidibiti radi ya zambarau ungenichokoza?”Aliongea Roma akiwa katika hali ya utani.
Ukweli ni kwamba ile siku mara baada ya kufanikiwa kuinyonya nguvu ambayo Chaos alikuwa ameificha aliweza kugundua mambo mawili matatu namna ya kudbiti radi , alichokuwa amekosa tu ni changamoto ya kufungua mawazo yake.
Ili kupanda levo Roma alikuwa akihitaji changamoto na ndio maana aikuwa akizitafuta sana , wakati majini wakiwaza kumuua Roma yeye alikuwa akichukulia changamoto hizo kama mbinu ya kufungua mawazo yake na hio ndio siri kubwa ambayo ipo katika nguvu ya andiko la Urejesho.
Andiko la Urejesho ni kama njia ya kupokea maono na ili iweze kukupatia maono lazima ukidhi vigezo vya kimazingira ambavyo ni kuwa katika changamoto , pale linapotokea giza kubwa la changamoto mbele yako ndio maono yanapotokea.
Yaani utofauti wa mbinu nyingi za majini wanazojifunza katika kupanda levo na kuvuna zaidi na zaidi nishati ya mbingu na ardhi ni kufanya mazoezi kila siku na kutamka maneno maalumu lakini kuhusu andiko la urejesho ni kama vile ni ahadi ambayo Mungu amemuwekea binadamu kwamba pale ambapo utakuwa katika changamoto atamletea maono ya kutatua changamoto hio.
Unapaswa kuelewa andiko la urejesho wa azimio jina hilo sio jina lake bali ni jina ambalo Roma aliamua kuliita , mwalimu wake ambaye alimfundisha kuhusu mbinu hio alimwambia aipatie jina analotaka yeye na ndio jina la Andiko la urejesho wa Azimio lilipozaliwa.
Sasa siku ambayo Anjiu alipitia dhiki ya Radi upaande wa Roma iikuwa ni kama vile maono yalimjia na kuona radi ambayo alikuwa akipitia Anjiu ilikuwa na rangi mbili yaani rangi ya bluu na Zambarau hivyo moja kwa moja Roma aliamini pengine ni muunganiko wa elementi za moto wa bluu na elementi za moto wa zambarau na matokeo yake yalikuwa ni kama vile alivyokuwa amewaza.
Roma hatimae alikuja kuelewa pengine kinachomtokea katika maisha yake ni mambo yaliopangwa na Mungu tokea mbali , hakuwahi kuamini sana katika Mungu lakini kila kinachomtokea kilikuwa katika fumbo la namna yake na njia ambazo anapitia ni kama vile zimekwisha kuandaliwa.
Ukweli ni kwamba katika sheria za kikanuni za matokeo ya radi katika rangi tofauti tofauti ukizungumzia radi ya urujuani ni matokeo ya muunganiko wa elementi zinazozalisha mwanga wa bluu na zambarau ki ufupi ni kanuni zilezle za kisayansi .
Bila shaka haikuwa kama vile unafanya majaribio ya kikemikali kwamba lazima kutokee makosa kwanza mpaka unapofikia mafanikio.
Mbinu za mbingu na ardhi zilikuwa ni za tofauti kidogo , ufunuo ukishakutokea na ukaufahamu basi ukiufanyia kazi matokeo yake ni sahihi na namna ya kupata maono ni kujua asili ya dunia ilivyo , kila kitu kipo kwa sababu kiwe na uhai kisiwe na uhai , kila tukio la asili linatokea kwa sababu na hio ndio njia rahisi ambayo ilimuwezesha kupata ufunuo.
Sasa Roma kutokana na uzoefu wake wa kijamii ulimwambia kwamba asili ya moyo wa kiumbe chenye utashi siku zote ni Dhambi kwanza kabla ya kupitia utakaso na ndio maana hakutaka kuambia mtu yoyote kwamba ameweza kufanikiwa kujua siri iliopo katika kuidhibiti radi.










SEHEMU YA 755.
Roma sasa alikuwa na hali ya kujiamini na alijiambia akishaingia katika levo ya mapigo ya radi elfu moja atakuwa na uwezo wa kutumia moto wa bluu na elementi za moto mweusi na kufanikiwa kutengeneza radi ya mapigo elfu moja.
Unachopaswa kuelewa ni kwamba Roma ameweza kudhibiti radi ya mapigo tisini na tisa , hii haikumaanisha kwamba Roma anaweza kutengeneza mapigo tisini na tisa lakini katika kanuni za nguvu za mbingu na ardhi inamaanisha kwamba anao uwezo wa kutengeneza radi yenye nguvu mara 9 katika awamu 11 na ndio hutokea hesabu ya 99.
Nishati za nguvu ya radi zinaenda katika kanuni hii tatu mara tatu , tisa mara kumi na moja , tisa mara mia na kumi na moja na kuendelea.
Maana yake ni kwamba unaweza ukapigwa na awamu tatu za radi yenye nguvu sawa ya mapigo matatu ambapo moja kwa moja utakuwa umepitia mapigo tisa , au unaweza kupigwa na mapigo kumi na moja yenye ujazo wa nguvu ya mapigo tisa hivyo kimahesabu utakuwa umepigwa na mapigo tisini na tisa au mapigo mia moja kumi na moja hapo utakuwa na uwezo wa kupigwa na mapigo mia tisa tisini na tisa , kanuni hii inabadilika lakini majawabu yanakuwa yanafanana, inategemea sana namna anga lilivyokasirika na mbinu yako ya mafunzo kwa mfano Anjiu na Rozu wao walipitia mapigo matatu tu ambayo ni sawa na mapigo tisa lakini kwa Roma alipitia awau tisa na awamu tisini na tisa katika mnara
Kila pigo lina rangi yake , asilimia kubwa ya mapigo tisa rangi yao ni bluu , tisini na tisa ni zambarau na kuendelea.
Roma sasa mara baada ya kuangalia majini waliokuwa mbele yake , aliona kabisa hana cha kuogopa licha ya kwamba walihesabika kama wabobevu wa nguvu za mbingu na ardhi katika ulimwengu huo.
“Nilikuwa nikipasha mwili joto na nishamaliza sasa , ni muda wa kuanza kazi..”
Mara baada ya kuongea kauli hio alitengeneza wimbi kubwa la radi ambazo shoti zake ziligawanyika na kuwa kama mishale midogo na kuwarushia wale majini.
Ngurumo iliosikika ni kama vile dunia imegongana na sayari nyingine na kabla hata majini hao wa Hongmeng na miliki nyingine masikio yao hayajatafsiri sauti hio walikwisha kufikitwa tayari na boriti za radi na kuwayeyusha.
Kwa Roma lilikuwa pigo la kawaida tu lakini athari zake hazikuwa za kawaida kwani majini waliokuwa katika levo za maji ya kawaida wote walipotea.
Majini wote ambao wamekwisha kuijua nguvu ya radi ya zambarau walijua namna ilivyokuwa ni hatari kuguswa na radi hio ukiwa hujajiandaa , hata Anjiu mwenyewe ambaye alikuwa na uwezo wa juu alitumia chungu cha Roma kuweza kuipita radi.
“Kimbieni!”
Sauti ilisikika kusikojulikana kama vile ni ya binadamu , meza ilikuwa imepinduliwa kibabe na kitu pekee ambacho majini hao waliona ni aidha kukwepa au kukimbia na sio kufanya mashambulizi.
Majini wa levo za chini waliosalimika walikimbia kwa kutawanyika lakini Anjiu , Gefu, Wucheni walikuwa wamebakia.
“Mnataka kukimbia , kukimbia kwenda wapi?”Aliwaza Roma akiwaangalia majini hao wa levo ya majji ya kiroho.
“Nyie vipi mbona hamkimbii kama wenzenu?, nimetoa kionjo tu show yenyewe haijaanza”
“Mh Tukimbie! ,unataka tukimbie kwenda wapi , unataka turudi katika miliki zetu ili utufuate huko huko ukaondoe mizizi ya vizazi vyetu kama ulivyofanya hapa Panas”Aliongea Menyu katika uchungu mkubwa na Roma hakukataa kwani ndio alichokuwa akiwaza.
“Hujakosea , isitoshe kama mnataka nianze kuwatafuta mmoja baada ya mwingine ni usumbufu ni kheri kama kutakuwa na mmoja wenu ambaye atakuwa ananielekeza njia”
“Ni kweli unataka kuua majini wote? , Roma kwa nguvu zako unaweza kutawala dunia nzima wewe mwenyewe na hatutanii katika hili… hatuwezi kukuchokoza tena kama utatuacha tuondoke leo hii .. au kama huridhiki na hivyo sisi kama miliki ya Panas tupo tayari kuwa chini yako , itakuwa ni kutuambia tu unachokitaka na sisi tutakutimizia”Aliongea Gefu akiwa na tabasamu pana kwenye uso wake.
“Ndio bro Roma , tunaomba msamaha kwa kukuchokoza , Mungu anatutaka kuishi maisha mazuri na nia yako ya kimauaji ni kubwa mno na inaenda kinyume na sheria za ulimwengu , sasa hakuna haja ya kuuana sisi kwa sisi kwanini unataka kwenda mbali namna hio?”Aliongea Umini.
“Sio wewe ambaye ulikuwa ukitaka kuniua muda huu , sasa nipo katika nafasi ya kukuua ndio unaniambia huo ujinga , kwasababu mmeamua kubakia na kufa basi sina haja ya kuwachelewesha”Aliongea Roma na palepale radi ya zambarau ilianza kumzingira katika mwili wake kwa namna ya ajabu kabisa na haikuwashambulia moja kwa moja bali ilichomoza na kwenda kugongana na wingu.
Wakati huo wingu kubwa juu angani lilikuwa likizunguka kwa kasi mno katika usawa aliosimama Roma na cheche za moto kugongana zilikuwa zikionekana.
Anga kati ya mbingu na ardhi lilikuwa giza tupu likiwa limefunikwa na ngurumo za radi sauti ilikuwa kubwa kana kwamba Mungu amaemua kuharibu sayari nzima.
Katika mabadiliko ya spidi ambayo ilikuwa ikionekana kwa macho ya kibinadamu , mawingu ya ngurumo yalitengeneza kizingia kikubwa ambacho kilizngira mzingo wa maili mia moja , katika maeneo mengi mbali na miliki hio kulikuwa na Dhoruba kubwa ya upepo.
Sasa katikati ya kizingia hicho ndio mahali ambapo Roma alikuwa amesimama , ilionekana alikuwa akiivuta radi kutoka juu kuja chini , haikuwa uwezo wakudhibiti radi tu lakini alikuwa na uwezo wa kuyasuguanisha mawingu kwa moto wa bluu na zambarau kutengeneza radi.
“Hivi bado tunaweza kusema huyu ni binadamu kweli…!”’Majini waliokuwa wakitetemeka kwa hofu wakiwa hawaaini kile wanachokiona waliongea , kilichokuwa mbele yao ilikuwa ni zaidi ya uhalisia wa kiumbe binadamu.
“Kulingana na vitabu vyetu, majini wa enzi hizo walikuwa na uwezo zaidi ya huo, hivyo nguvu hio ni nusu ya nguvu zao”Aliongea Shombeli.
Ubaridi wa maji ya mvua uligonga uso wa Anjiu na aliishia kukunja ngumi tu huku macho yake yakiwa yamejaa husda.
“Andiko la urejesho wa Azimio …hii ni mbinu ya namna gani, kuna siri gani iliopo nyuma yake?”
Anjiu ambaye alikuwa na tamaa kubwa ya kupanda levo mara baada ya kuhisi nguvu ya ajabu iliokuwa ikiongezeka kila sekunde na namna ambavyo Roma analizungusha wingu na kufanya linavyotaka alijikuta akishindwa hata kujua ni hisia gani anazipata.
Roma alikuwa katika levo za juu kabisa na kwa wakati huo hakuwafikiria majini hao kama washindani wake , moyo wake ulikuwa ukiimba wimbo wa; ‘Athena njoo nikushikishe adabu’.
Roma alijiua pengine hisia anazozipata hata Athena alikuwa amezipata kwa muda mrefu sana , pengine Athena hakuwa akiigiza kuwa na ukiburi na ukauzu , vile vitu ambavyo watu wengi walikuwa wakiviona vya thamani kwake havikuwa vya thamani na hisia hizo ndio alizokuwa nazo Roma.
Ni kama vile mtu mzima kutokuvutiwa na midoli ya kuchezea watoto basi ilikuwa ni kama yeye vile kutokuvutiwa na vitu kama vile pesa na madaraka , Roma hakuwa hata na tamaa tena ya kuua viumbe dhaifu tena.
Roma alikuwa na uwelewa na hisia hizo mwanzoni lakini katika nguvu ya namna hio aliweza kufikiria kama vile alivyokuwa akifikiria Athena,
Mabadiliko ya kimtazamo na kiakili ilikuwa ni hatua ya ukuaji kwake ambao ulimpa hali ya kujiamini , Roma sasa alijiambia hawezi tena kuogopa yule mkuu wa umoja wa majini aliekutana nae Dodoma tena.
Mambo mengi alikuwa akiyafikiria katika kichwa chake na alikuwa ameshasahau kuna kundi la majini chini yake ambao linasubiria hukumu yake.
Katika wakati huo Roma sasa alikuwa katika hali ya utulivu kabisa na macho yake hayakuonekana kama yale ya fujo tena kama alvyoweza kuingia katika ulimwengu huo , ilikuwa ni kama vile amebatizwa na kuwa kiumbe kipya.
Roma alikiwa amesimama juu angani alinyanyua mkono wake na kunyoosha kidole upande wa aliposimama Menyu na wenzake.
“Boom!!”
Kitendo cha kunyossha kidole ni kama ishara ya kuruhusu pigo kwani wingu lililokuwa likizunguka juu yake lilishusha radi na kwenda kupiga katika eneo lile alilonyooshea kidole.
Ijapokuwa radi hio haikuwa kubwa kama ya mapigo tisa lakini ilikuwa na nguvu kubwa mno ya kugeuza majini wa nne wa levo ya maji ya kiroho kuwa majivu.
Anjiu na wenzake waliweza kukwepa shambulizi lile lakini ile wanakuja kumgeukia Menyu na baadhi ya majini walikuwa wamebadlika na kuwa moto wa rangi ya bluu na roho zao na nafsi zao ziliunguzwa .
Ijapokuwa walijua hawakuwa saizi ya Roma tena lakini walishangazwa na uwezo wake wa kuua majini wa levo ya kati ya maji kwa pigo moja tu.
BOOM!!
Radi nyingine ilishuka bila hata ya tahadhari , na awamu hio wazee wakuu wa miliki ya Xia walishambuliwa na kuuliwa palepale.
Roma alihisi ni kama vile ameanza kutumia radi miaka mingi iliopita namna ilivyokuwa rahisi kushambulia, moto huo wa mbingu aliweza kuita kama vile akili yake imetawaliwa na mdudu ambaye anawezesha hayo yote.
Gefu na wenzake waliona kabisa hali sio nzuri kwao kabisa na alipanga kuchukua baadhi ya watu wake kukimbia , hata kama angeamua kucheza kamari lakini ni kheri kuishi kwa muda mrefu kidogo kuliko asili yao kufutwa.
“Tawanyikeni , jiokoeni”Aliongea na baadhi ya wazee wa miliki ya Panas mara baada ya kusikia kauli hio walianza kukimbia kuelekea pande tofauti tofauti.
Roma hakuwaangalia kabisa na palepale aliita moto wa mbingu na kisha kunyoosha vidole upande wao na palepale walishukiwa na mashambulizi na kumezwa ndani ya sekunde ikiwemo Gefu mwenyewe.
Majini wote wa miliki ya Panas walipotea na kilichoweza kubakia ni Dhana ya kiuungu ya mkuki peke yake , ilikuwa ni dhana ya kilijendi hivyo haikuharibika kirahisi.
Ikawa Roma amekwisha kuua mkuu wa miliki ya Panas na mkuu wamiliki ya Kekexil.
Katika kifo cha Gefu hakuna jini ambaye alikuwa hata na habari ni wapi Dhana yake ya kiuungu ilipokuwa imedondikea.
Anjiu aliishia kung’ata meno yake na katika hali kama hio aliamua kuita pepo lake la ndani la kijeshi na mwili wake wote ulifunikwa na nguvu ya moto wa ndege wa dhahabu wa miguu mitatu.
“Msikimbie ni vizuri kupigana nae kuliko kushambuliwa wakati wa kukimbia , sidhani kama anao uwezo wa kuhimili uharibifu wake mwenyewe kwa kutuua wengi namna hii’
“Anjiu upo huru kufa mwenyewe , wewe ndio umetuleta katika hali hatarishi namna hii”Umini alitoa alimwangushia lawama kwa hasira , huyu kijana wa miaka mia mbili hatimae alijua kwamba tayari kifo kinamuita.
Kinyume chake Wucheni na Shombeli na wenzake wote walikuwa katika muoenekano wa utulivu kabisa , ni kama wamejiandaa kufa kimya kimya.
Roma aliweza kuoneysha kejeli katika macho yake na wakati kama huo alichopata kuona kati ya majini hao ni Anju peke yake ambaye alikuwa na muonekano wa kishujaa.
Mbele ya israeli mtoa roho Anjiu alikuwa bado akionyesha hali ya kujiamnni , ni kama hakutaka kufa kama muoga bali alitaka kufa kama mwanajeshi.
Pengine hio ndio sababu ya kumfanya Anjiu kuwa maarufu katika ulimwengu wa majini , Roma alijiambia kama sio Anjiu mwenyewe kutaka kumchokoza pengine angeweza kumfanya kuwa rafiki yake kwani kuna vitu vingi wanafanana.
Ni dakika kadhaa wakati Roma akijiandaa kumalizana na Wucheni hatimae aliweza kuhisi nguvu za majini zikisogea katika eneo hilo huku akisikia sauti ikimwita.
“Master Roma naomba usimuue mjomba tafadhari ,, usimuue”
Roma aliweza kuijua sauti hio kutokea mbali , ni kama vile alishawahi kuisikia na kufumba na kufumbua aliweza kuona wanawake wawili pamoja na mwanaume mmoja wakisogea katika eneo hilo.
“Bi Zenzhei!!”
Roma alishangaa mara baada ya kumuona ni Zenzhei , ijapokuwa Zenzhei alikuwa amebadilika na kuwa msichana lakini Roma alikuwa akimtambua kwani alionana nae wakati akiwa anaondoka.
Lakini alishangaa Zenzhei kusema mjomba wake asiuliwe



SEHEMU YA 756.
Roma mara baada ya kumjua Zenzhei alionyesha hali ya kuwa na furaha , ukweli licha ya kwamba alikuwa ni msichana lakini hakujizuia kumuita bibi.
Watu aliokuwa ameambata nao ni Nefi pamoja na Yiyu ambao ni watoto wa Wucheni.
Zenzhei mara baada ya kusikia Roma akimuita Bibi , Zenzhei alishindwa kujizuia na kutokwa na machozi ya furaha neno bibi lilikuwa na maana kubwa kwake , ilimaanisha Roma alikuwa akimheshimu.
“Master Roma siamini kama kukutana kwetu kutakuwa kwa namna hii , mambo yanaendaje nyumbani Tanzania?”Aliuliza Zenzhei.
“Mambo kwanini yasiwe shwari wakati nipo , nina vitu vizuri kwa ajili ya yule mzee na umri wake kwasasa sio tatizo, usiwe na wasiwasi kabisa”Aliongea Roma akiwa katika tabasamu la furaha kumuona Zenzhei kwa mara nyingine.
“Ndio , nimesahau kama tayari unao uwezo wa kutengeza vidonge”
Baada ya kumuona Zenzhei anamsogelea Roma , Nefi na Yiyu walienda kwa baba yao wakiwa katika hali ya wasiwasi.
“Zenzhei usimsogelee atakuuwa huyo”Wucheni alibweka lakini Zenzhei aligeuza sura yake na kumtingisha kichwa mjomba ake na kisha akamgeukia Roma.
“Mr Roma Zenzhei anajua kwamba Hongmeng wamefanya makosa , nilipofika nilipata kujua ukweli wa mambo menginyuma ya vifo vya wazazi wangu kutoka kwa mjomba Wucheni na nimejua ni maamuzi gani ambayo nilipaswa kufanya muda mrefu juu ya kisasi changu , Mjomba ana makosa ndo lakini bado ana majukumu makubwa , najua nakosa aibu kukuomba hili kulingana tulivyokubaliana lakini naomba unikubalie hili ombi moja , muache aondoke ..nimeweza kusikia kutoka kwa baadhi ya wenzetu waliokimbia hapa kwamba tayari unao uwezo wa kudhibiti radi , hata kama Hongmeng wanatamani kukuchokoza hawatothubutu kwani wanajua unao uwezo mkubwa tayari”
Majini wa Hongmeng wote walikuwa kimya na walikuwa na taarifa ya Zenzhei kuishi katika taifa la Tanzania tokea akiwa mdogo hivyo ni kama ni raia wa Tanzania.
Lakini hawakuwa wakijua kama wakati Roma anaingia katika levo ya nafsi mara baada ya kukamilisha mzunguko wa Andiko la urejesho msaada mkubwa aliupata kutoka kwa Zenzhei.
Kutokana na kujua hayo Shombeli , Umini na wengne walijua pengine kuna tumaini la kubakia hai kwa kumtegemea Zenzhei.
“Acha kumbembeleza , hata kama watoto wangu na mabinti zangu watakufa hawawezi kukupigia magoti , mimi Wucheni ijapokuwa siwezi kujiita shujaa lakini sio mjinga ambae ninaweza kuishi kwa kuchekwa na kuomba kuhurumiwa”Aliongea Wucheni akionyesha hali ya kujisikia vibaya kwa Zenzhei kumuombea msamaha kwa Roma.
“Bi Zenzhei huna haja ya kunibembeleza , kama unataka nimuachie mjomba wao nitamuacha , sitaki kukuona ukinibembeleza”Aliongea Roma akimwangalia Zenzhei ambaye alikuwa na muonekano wa kinyeyekevu.
Majini wote ambao walikuwa hawampendi Roma walishangaa mara baada ya kuona Roma kweli alikuwa akijali maneno ya Zenzhei.
“Usishangae sana , wewe kwangu ni mwanafamilia na umekuwa mkarimu kwangu kwa muda mrefu sana na bado sijalipa yale yote ambayo umeyafanya kwa familia yetu , ijapokuwa mjomba wako alitaka kuniua lakini bila shaka nitamuacha aende lakini hii itakuwa ni mara yake ya mwisho kumpa nafasi nyingine , awamu nyingine akinichokoza ajue kwamba ndio mwisho wa uvumiivu wangu”
“Binadamu ulielaaniwa wewe acha kunibebesha uovu , hata kama nitakufa mimi na uzee wangu huu huwezi kunisingizia vitu ambavyo sijafanya , ni lini nikataka kukuua?”Aliongea Wuchen.
“Kwahio unataka kusema sio wewe uliekuja Australia katika nyika ya Arnhem na kutaka kuniua?”
“Australia!!. , unaongea nini?, Lini nikaja Australia na kutaka kukuua miii?”Aliongea Wucheni akiwa katika hali ya kushangaa.
“Roma! Baba yangu siku zote ni mtu mwema asie tayari kuvunja sheria , kama kweli alitaka kukuua unadhani ungeweza kumshinda wakati huo?”Aliongea Nefi.
“Nilishambuliwa na mtu aliekuwa amevalia Mask ya chuma na kutaka mbinu yangu ya mafunzo , mtu huyo alikuwa na uwezo wa kutumia kinga ya boma la barafu na kuita pepo wa kikaskazini , vipepeo wa kufikirika na mbingu nyingine , mtu huyo uwezo wake wa kijini ulikuwa mkubwa mno , kama sio Wucheni je ni nani kama sio mmoja wenu ndani ya miliki yenu?”
Mara baada ya kuongea kauli hio wazee hao wa Hongmeng walijikuta wakishangaa , ilikuwa haiwezekani Roma kumsingizia mtu kwasababu alikuwa na uwezo wa kumuua mtu yoyote ambae hakuwa akimfurahisha.
Dakika ileile macho yao yote yaliokuwa katika hali ya hasira yalimgeukia Anjiu.
“Anjiu unathubutu vipi kutumia mbinu ya familia yangu kujifanyisha ni mimi katika kufanya uovu wa namna hio , una moyo uliojaa hila, je ulikuwa ukinitafutia matatizo kati ya Roma na miliki yetu?”
“Nini , Anjiu!?, kwanini Anjiu aweze kutumia mbinu yenu?”
“Mr Roma mjomba hajahusika kabisa na kinachoendeea ni kama kilichoitokea familia yangu , kuna baadhi ya majini wa jamii yetu walijua siri ya mbinu yetu ya mafunzo lakini walikufa wote na mpaka sasa aliebakia katika ulimwengu wetu ni Anjiu pekee , alijua mbinu yetu kwa njia ya kumhadaa kimapenzi binamu yangu Yiyu ndio maana mpake leo hii kuna ugomvi mkubwa baina yao”
“Ushachelewa kufahamu hili, vyovyote vile lazima unapaswa kujiona mwenye bahati , nilitumia hii mbinu kwa ajili ya kukugombanisha na Hongmeng lakinni inasikitisha kwamba hukuchukua hatua na badala yake ukaja katika miliki yangu na kuanzisha vurugu, nadhani nilikosea mahesabu yangu”
“Kama ni hivyo wakati nilipokuwa kwenye Dhehebu la Tang , mtu ambaye alikuwa akiwatala kiakili wale wazee jr wewe pia?, je ambaye alijaribu kumtumia Tang luyi kwa kumleta binti wewe pia unahusika?”
“Ndio ni mimi, usisahau ilikuwa rahisi sana mimi kukuua wakati ule na usione inaweza kuwa rahisi kuniua leo hii”
“Kama ni hivyo basi utakuwa unamjua binti wa damu wa Tang Luyi, hivyo sema binti yake yupo wapi?”
Tang Luyi ni Master yake na Magdalena kutokea milima ya Shushan katika ngome ya Tang sasa siku ile Roma alivyoenda katika ile ngome alikuta wazee wote wakiwa katika kutawaliwa kimawazo na kutaka kumshambulia.
“Kwanini nikuambie?”Hali ya muonekano ya Anjiu ilibadilika.
“Haijalishi kama hutaki kujibu, hivyo nitakuuliza tena swali lingine, Je umejuaje nilikuwa nikitumia mbinu ya Andiko la Urejesho , je swala hili linahusiana na mtu ambaye alikuwa akimfukuza Master wangu Tang Chi na kutaka kumuua?”Aliuliza Roma.
Ukweli ni kwamba Roma alikuwa akijiuliza swali la namna hio kwa muda mrefu na kukosa majibu na hio yote ni kukosa mtu wa kumuuliza , hata alivyokutana na Tang Chi kwenye ulimwengu wa majini pepo hakumpa habari juu ya ubini wa adui ambaye alikuwa akimfukuza.
Kitu kingine ni kwamba asilimia ya majini wote ambao wapo katika ulimwengu wa majini watu hawakuwa na uelewa na mbinu hio aliokuwa akitumia , jambo ambalo lilimfahamisha kwamba hawakuwa wakijua mbinu ya andiko la Urejesho ni mara baada ya kukuta karatasi lenye andiko linalofanana na kwake japo majina tofauti.
Hivyo moja kwa moja lazima kuna mtu ambaye aliwaambia majini kwamba Roma anatumia mbinu ya Andiko , mbinu ya kijini ambayo hawaiujui ndio maana miliki zote zilikuwa zikihitaji kupata mbinu hio.
“Kama nikijibu maswali yako je utaniacha hai?”
“Huna jinsi zaidi ya kujibu maswali yangu au ufe , usifikiri pepo lako la ndani linaweza kudili na mimi awamu hii , ninao uwezo wa kukuua na radi kabla hata hajafanya shambulizi”
Anjiu mara baada ya kusikia maneno hayo aling’ata meno kwa hasira na kisha alimwangalia Roma na sura iliokuwa ikicheza cheza kwa hasira.
“Kama ni hivyo basi jibu langu ni kwamba sijui chochote, nasema hivi kwasababu mtu ambaye aliniambia kuhusu mbinu yako alikuwa ni wa ajabu sana haieleweki alikuwa ni mwanamke au mwanaume lakini nilichoweza kukuta ni barua katika meza yangu nyakati za usiku ambayo imeachwa na mtu huyo , sikujua hata kama kuna mtu aliingia katika ofisi yangu , kutokea siku hio huyo mtu alionekana sio wa kawaida hivyo sikumuwazia sana … kuhusu swala la kumfukuza Master wako na kutaka kumuua sijui hata kama una master wa jina hilo , hivyo sina majibu unayotaka na unaweza kuamini unachotaka”
Haikujalisha Roma alisikiaje jibu hilo lakini alihisi ni kama vile ni ujinga lakini kwa kumwangalia Anjiu haikuonekana alikuwa akidanganya
Mara baada ya kuona Roma yupo kwenye mawazo kila mmoja aliona hakuwa na nia tena ya kuendelea kuua na hatimae waliweza kupata ahueni ya kupumua.
Shombeli na Umini waliangaliana na kisha walipeana ishara ya maelewano na kwa haraka sana waliondoka na kundi la majini wa miliki ya Hongmeng.
Roma hakujali hata kuwafukuzia , mpaka wakati huo alikuwa na uwezo wa kuua jini yoyote kwa muda wowote anao taka laikini aliona kabisa kuua majini hao hakuna faida kubwa kwake
Iwe ni kwa kuua sana au kuua kidogo kwake hakukuwa na utofauti wa aina yoyote zaidi ya kujisumbua tu.
“Hakuna siku niliodhalilika kama leo , sijawahi kupitia huu uzoefu , umeniumiza na kisha ukachukua Dhana yangu , nipo tayari kufa nikipigana kuliko kukimbia ninakataa kushindwa lakini mimi Wucheni nachagua kuishi leo hii kwa ajili ya familia yangu .. mimi Wucheni nina deni la uhai kutoka kwako na kwanzia leo hii natangaza Hongmeng haitokuja kuwa na uadui na wewe kama ili mradi nitaendeea kuwa hai”Roma mara baada ya kusikia maneno hayo almwangalia Wucheni na palepale alijikuta akiangua kicheko.
“Sawa mzee , ndio uondoke wakati huu ambao nimekuruhusu na sitaki uchukulie mimi kukuacha hai ni kama deni , kama nilivyosema mwanzo nimekusamehe wewe na watu wako kwa ajili ya Bi Zenzhei , viumbe kama nyie ni swala la mimi kujiuliza kama niwaue au niwaache hai hivyo usijifanyishe kama utakuja kuwa na manufaa kwangu , kwangu muwe maadui msiwe maadui kwangu haibadilishi kitu kwanni mtabakia kuwa viumbe dhaifu mbele yangu”
Maneno yale ya Roma yalitaka kumfanya Wucheni kubadilika na kuonyesha hasira zake lakini mtoto wake Nefi na Yiyu walikuwa na hofu mno ya Roma kuwachukulia hatua.
“Zenzhei alimwangalia Roma na kisha akamwangalia Anjiu lakini kwa jinsi alivyokuwa akimwangalia Roma hakuonyesha aina yoyote ya hofu.
“Mr Roma nadhani sina haja ya kuwa na wasiwasi tena kwa mafanikio yako naamini yule mtu alifanya chaguzi sahihi , kwa mara nyingine niseme asante sana kwa ukarimu wako wa leo”
“Bibi kama upo tayari unaweza kurudi Tanzania na nitahakikisha hakuna anaeweza kukurudisha katika huu uimwengu wakifanya hivyo naua wote”
Zenzhei alifurahishwa na maneno yake , alikuwa na muonekano wa kijana na kwa Roma ni kama vile alikuwa akilinganga nae umri licha ya kwamba alikuwa akimwita bibi na aliishia kutingisha kichwa tu na palepale aliondoka kwa kupotea.
Sasa aliebaki alikuwa ni Anjiu peke yake , sio kwamba hakutaka kuondoka lakini alijua Roma anaweza kuwaacha wote waondoke lakini yeye asimruhusu
“Kusema ukweli sina uhakika kama ulichoongea ni ukweli kwasababu ya hilo najikuta nakuona wa hatari sana , kama unachochote unachotaka kuongea ongea kabla ya kifo chako”
“Nishajua unakwenda kuniua muda mrefu hivyo sogea tupambane , ijapokuwa nafasi yangu ya kushinda ni ndogo lakini siwezi kufa”
Mara baada ya kuongea hivyo aliita pepo lake la ndani na palepale ni kama vile kivuli cha mtu kinamtoka na kusimama mbele yake , kilikuwa ni kivuli kinacholingana kila kitu na yeye na kufumba na kufumbua kivuli kile kilimsogelea Roma kwa kasi.
Roma alikuwa tayari amekwisha kujindaa na aliita chungu cha maaafa na kwenda kugongana na kwa ana na lile pepo.
Lakini kwa nguvu ya Chaos ilivyokuwa kubwa ilikuwa ni mchezo wa kitoto sana kwa pepo wa namna hio kuweza kushindana na chaos kwani palepale mara baada ya kukaribiana na mdomo wa chungu lilipuka. Kama bomu.
Roma aliishia kupiga yowe kwenye moyo wake , ilionekana Anjiu hakuwa na nia ya kutumia pepo hilo kushambulia bali alilitoa kafara na kulitumia kama bomu la moshi.
Pepo la namna hio hata kama lilipuke ilikuwa ni swala la muda tu kwa Anjiu kulirudisha licha ya kwamba inaweza kumgharimu nguvu nyingi za mbingu na ardhi.
Sasa mara baada ya mlipuko ule wa pepo ambao ulitengeneza wingu Anjiu alitumia nafasi hio kukimbia lakini Roma ni kama alitegemea anachotaka kufanya na hakuwa na mpango wa kumuacha akimbie kizemba namna hio.
Uelekeo aliochukua Anjiu ilikuwa ni kuelekea katika miliki ya Xia na ilionekana alikuwa akitaka kuita wasaidizi wake
Ijapokuwa Roma alikuwa na spidi kubwa lakini spidi ya majini haikuwa ya kawaida hawakuwa wakipotea bali walikuwa wakisafiri kwa kasi mno kiasi kwaba wanaonekana kama wanapotea na ndani ya sekunde tu Anjiu alikuwa maili nyingi sana akiwa amemuacha Roma na hio ilimfanya Roma kutokuweza kuita radi kumshambulia tena.
Kilichomshangaza Roma ni uwezo wa Anjiu kukimbia huku akiacha kinga nyuma za barafu kama maboma
Ilimchukua Roma dakika kama tano kuweza kumfikia Anjiu lakini ile anataka kumzuia kwa mbele na kumshambulia na pigo la radi ghafla tu alihisi msisimko wa nguvu za kijini ukiongezeka kwa kuwasogelea na kufumba na kufumbua walitokeza majini waliokuwa katika kundi kutoka katika miliki ya Xia wakiongozwa na msichana mdogo Xiao .
“Mnafanya nini hapa?”Anjiu alikuwa amekasirika mno mara baada ya kumuona binti yake Xiao.
Roma alitaka kutumia ile nafasi kuwashambulia na pigo moja la radi na kuwaua lakini mara baada ya kumuona Xiao alisita.
Msichana huyo nusu jini nusu binadamu alimpa Roma ugumu wa kumshabulia , pengine ni kutokana na kwamba Rufi alikuwa na deni nae na yeye pia alikuwa amemshuku zaidi ya mara mbili.
“Baba wewe unaweza kuondoka , mimi binti yako nitamzuia huyu mtu mbaya”Aliongea Xiao na kisauti chake cha kuumiza masikio na palepale alisogea mbele ya Roma na kumkinga baba yake.
“Wewe mhalifu mkubwa niue sasa kama uwezo huo unao , hujatosheka kunichokoza mara kibao lakini na sasa hivi unataka kumuua baba yangu, dhamiri haikusuti?”
Roma aliguswa na maneno ya Xiao , yalikuwa ni kama vile ni shambulizi la radi , ijapokuwa alikuwa na uwezo wa kuua majini kwa kufikiria tu lakini alijikuta akiwa mzito sana kumuuiza huyo mrembo.
“Sogea pembeni , Mimi na Rufi tuna deni kwako ndio , lakini kinachotokea hapa ni kati yangu na baba yako , kama nisipomuua leo hii ataniua mimi”
“Unaongea ujinga, kama kweli una deni kwangu kwanini unataka kumua baba yangu , hii ndio namna ya kulipa hilo deni?”
“Hili ni tofauti..”
“Ni tofauti kivipi?”
Anjiu macho yake yaliongezeka ukubwa , palepale aligundua Roma alikuwa akimjali sana binti yake.
Kama ingekuwa ni zamani angemtumia Xiao kama mateka ili kumzuia Roma asimuue lakini tokea siku ambayo alirudi kutoka katika ulimwengu wa kawaida alianza kumchukulia kama binti yake kipenzi.
Siku hio ndio Anjiu aliweza kumjua Roma vizuri , alikuwa ni katili ambaye anao uwezo wa kuua miliki karibia zote hivyo alijua mtu wa aina hio anaweza kumuua hata kama atakubali kutokumuua kwa ajili ya binti yake
Anjiu hakutaka kumuona binti yake akijihatarisha kwa ajii ya kumuokoa.
Kuna vitu nadhani alisahau kuvijua kuhusu Roma , ukweli ni kwamba alijua kama Roma hakuwa akimjali Xiao basi mpaka wakati huo angekuwa ashawaua yeye na binti yake na kuwageuza majivu.
Roma hakuwa bado amefanya maamuzi , alikuwa akiwaza namna ya kutokumdhuru Xiao lakini amuue Anjiu kwani ni tishio kwa usalama wake na watu wake.
Mara baada ya kuona Roma anawaza wale majini wengine walianza kumbembeleza Anjiu kuondoka lakini yeye aliwafaokea kwa kumruhusu Xiao kuja nao.
“Mkuu tulikuwa na wasiwasi juu yako , taarifa za vita imesambaa katika miliki zote za majini , mkuu aliepita bado hajapona tutafanya nini kama na wewe tutakupoteza”
“Baba ondoka , nitamzuia asikudhuru , huyu nanamdai fadhila hivyo siwezi kumruhusu kukudhuru”
Xiao aliacha kumwangalia baba yange na alikuwa akijaribu kumsukuma Roma kurudi nyuma bila ya hofu yoyote , pengine ni hisia zake za kimapenzi ndio zinamfanya kutokumuogopa Roma.
Anjiu alitaka kumzuia Xiao lakini wazo lilimwingia , alijiambia kama ataendelea kumshikilia si nitangia katika mtego wa Roma labda anapanga kumtumia kama mateka ili kunikamata.
Kutokana na mawazo hayo alishindwa kuchukua maamuzi ya kukikimbia.
Ukweli ni kwamba Roma hakuwa hata na mpango wa kumtega Anjiu,alikuwa na uwezo wa kutokumdhuru Xiao na kisha kumuua Anjiu lakini matendo ya Xiao yalimfanya kutokuchukua hatua yoyote.
Xiao alienda mbali na kumshikilia Roma kiuno kwa kupitisha mikono kwa mbele ili kumzuia asisogee , vitendo hivyo vilimfanya Roma kushangaa na kuishia kucheka kwani vilikuwa vya kitoto sana
Licha ya kwamba uwezo wake ulishafikia levo ya nafsi lakini bado matendo yake yalikuwa kama ya msichana mdogo.
Upande wa Anjiu alikuwa na wasiwasi mno kwa kuogopa Roma kumuua binti yake.
“Baba kimbia basi”
Aliongea Xiao akiamini kwa namna alimvyomshikilia Roma hawezi kuchoropoka.
“Haka kajinga kanadhani Roma hawezi kuniua kwa kufanya vile”Aliwaza Anjiu.
Roma palepae alitoa tabasamu la kifedhuli na alimgeuza Xiao kama karatasi na kumshikilia na kwapa la mkono na kabla hata hajaleta ukinzani alikuwa tayari ashamzimisha.
Roma mpango wake ulikuwa ni mwepesi , alijua kama ataondoka na kurudi nae anaweza kumjua vizuri Xiao ni nani na kama ni mtoto wa Tang Luyi angempeleka kwa mama yake lakini pia asingekuwa na wasiwasi kuivamia Xia na kuisambaratisha.
Anjiu hakuweza kumuokoa binti yake na aliamua kukimbia huku akiamini Roma hawezi kumdhuru.
Upande wa Roma alikuwa mzito mno kumuacha Anjiu akimbie na alijaribu kumshambulia kwa kumrushia shoti za radi na mkono mmoja lakini kwasababu alikuwa amembeba Xiao alishindwa kubomoa ngao yake ya kijini ya barafu.
Roma aliweza kukiri ngao ya barafu ya pepo wa kaskazini ilikuwa sio ya kawaida kabisa , ilikuwa na nguvu mno kwani iliweza kumsaidia Anjiu kutoroka.
Lakini licha ya kwamba Roma hakuweza kumpata Anjiu na shambulizi lake lakini wale majini waliofika hapo waliweza kupatwa na mashambulizi hayo na kupoteza maisha.
Roma hakutaka kumwangalia tu akipotea katika macho ake na aliamua kumfukuzia kwa nyuma kwa kasi kubwa huku akiwa bado amembeba Xiao.
Anjiu alichukua uelekeo wa Kaskazini mashariki na alikuwa na spidi ya kasi mno lakini Roma licha ya kumfukuzia kwa kasi hakuwa na wasiwasi wa kumpata.
Roma alijiambbia hata kama asipomkata Anjiu miliki yake anaifahamu hivyo angeenda Xia na kuilipua na aone kama hatojitokeza.
Wakati Roma akiwa nyuma anaendelea kumfukuzia Anjiu alihisi kitu kisichokuwa cha kawaida kimeamka , ilikuwa ni kama vile kuna kitu kinataka kumtoka katika mwili wake , Roma mara baada ya kujichunguza alikuja kugundua ni kitu ambacho kilikuwa ndani ya hifadhi yake ya pete na jambo lile lilimshangaza sana.
Kabla hata hajagundua ni kitu gani hicho baada ya kufungua hifadhi hio kivuli cheusi kilitoka kwa kasi na kumvaa , kivuli hicho kilikuwa na nguvu ya giza , na kimejaa roho ya ukichaa , kifo na baadhi ya hisia hasi ambazo hazikuwa zikielezeka.
“Ni ile Hazina ya majini pepo!!!”
Roma alishangaa mno kwani ilikuwa ndio mara ya kwanza hazina hio ikawa hai na kutoka katika hifadhi bila ya ridhaa yake.
Kubwa zaidi ni kwamba hajawahi kujua kazi ya hazina hio ni nini na tokea mwanzo hakuweza kuhisi kama ilikuwa na nguvu zozote zile.
“Kwanini ghafla tu imeamua kuzalisha nguvu ya ajabu ya namna hii ya giza?”
Roma alijiuliza na kabla hata hajapata majibu kivuli kile kilichokuwa kimemzingita kiligeuka na kuwa kama vile ni kizingia au kimbunga na kuanza kumzunguka kwa kasi mno huku kikielekea juu angani zaidi na zaidi huku ncha yake juu kabisa kukiwa na ile hazina nyeusi.
Msuguano wa nisahti za mbingu na ardhi na nishati za hazina ile ziliongezeka kwa kiasi kikubwa na kuanza kumsukuma Roma kwenda juu angani , ilikuwa ni kama vile alikuwa amefungwa kamba kiunoni na kulazimishwa kwenda juu kwa kuvutwa.
Nguvu ilikuwa ni kubwa mno na Roma hakuweza kujinasua kwa kadri alivyokuwa akijitahidi , alijaribu kutumia chungu cha maafa kuweza kumeza nguvu inayotokaana ile hazina lakini alishindwa kabisa , alijaribu uwezo wake wote wa nguvu za kijini katika levo ya radi lakini pia ilishindikana na alijikuta akitoa macho.
“Hii nguvu ya hazina mbona kama inanyonya nguvu zangu?”
Roma aligeuza macho yake juu angani na palepale aliona katika anga ni kama vile kuna shimo kubwa jeusi ambalo anga yake ilikuwa ikichemka kana kwamba ni mafuta meusi yanayochemswa na moto mkali.
Roma kutokana na uwezo wake wa kuelewa kanuni za anga aligundua kilichokuwa juu yake ni Lango(Portal) la shimo ambalo ndio lilikuwa likimvuta.
Ilikuwa ni ndani ya sekunde tu ilikuwa ni kama alivyowaza kwani akiwa amemshikilia Xiao aliweza kutumbukia katika lile shimo refu na hakujua hata kinachomtokea ni kitu gani , kila kitu kwake kilikuwa cha maajabu.
Roma alijiuliza au pengne Hazina hio haikuwa na uwezo wa kuzalisha nguvu yoyote bali kazi yake ilikuwa ni kuamsha malango ya anga.
Kilichokuwa kimemtokea ni kama vile alivyovutwa na mnara na kupelekwa katika ulimwengu wa majini pepo na ndio kitu cha namna hio hio ndio kilichokuwa kikimtokea tofauti tu ni kwamba alijihisi ni kama vile anatumbukia kwenye shimo lefu la giza huku akishindwa kujizuia.
Roma mara baada ya kutumbukia mzima mzima katika shimo hilo ndio sasa anakumbuka kwenye mikono yake alikuwa memshikilia Xiao.
“Ni kitu gani hichi kinanitokea , kwanini nina bahati mbaya namna hii , au majini pepo waliniwekea mtego , au hii hazina yao ilikuwa ni ufunguo wa kuteleport kwenda ulimwengu mwingine , kama ningejua ningerudisha hazina yao mara moja”
Roma alianza kujilaumu wakati akiwa ndani ya giza totoro asijue ni wapi anaelekea , alichokuwa akijua tu ni kwamba nguvu inayomvuta ilikuwa ni kubwa sana kiasi kwamba hawezi kufanya lolote.
Anjiu ambaye alikuwa akikimbia kwa kasi kuokoa maisha yake hakujua ni kipi ambacho kinamtokea Roma na mara baada ya kuhisi nguvu ya ajabu alijiuliza au kuna mbinu nyingine Roma anajaribu kufanya ili kumuua.
Kitendo cha kugeuka nyuma aliona kitu kama duara nyeusi ambalo linapungua ukubwa kwa namna ya kusinyaa na ilikuwa ni kwa haraka sana kidoti kile cheusi kilipotea na hakuhisi tena msisimko wa nguvu za Roma wala za binti yake Xiao.
Ilikuwa ni kama vile Roma na Xiao walikuwa wamepotea katika anga jembamba , aliishia kukunja ndita na alirudi kwa kasi nyuma na kujaribu kumtafuta Roma , alijaribu kutumia nguvu zake za kijini za utambuzi ili kumuona binti yake lakini hakukuwa na dalili yoyote.
Roma kapotelea wapi au ndio mpango wa Athena kumpoteza Roma kukamilisha mambo yake.
Hatima ya Lekcha na Aoiline ni nini.
ITAENDELEA.
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI :SINGANOJR

Mono no aware.

SEHEMU YA 758.

Anjiu mara baada ya kujiuliza kwa dakika kadhaa ni kama sasa alikuwa anapata uelewa ni kitu gani kimetokea.
“Jicho la Anga!!!’
Mara baada ya kuangalia eneo ambalo yupo ni kati ya mpaka wa miliki ya Xia na Panas na ndio eneo ambalo jicho la anga hufunguka alipata wazo hilo, ijapokuwa muonekano wa jicho hilo hutofautiana kila linapofunguka lakini ilikuwa ni sehemu hio , sasa alijiuliza je kile kidoti cheusi alichoona angani ndio lango la jicho la anga lakini kwanini lifunguke wakati huo ilihali tarehe ya kufunguka kwake ilikuwa mwakani.
Hakukuwa na ishara ya furaha katika macho ya Anjiu wakati akijaribu kuchunguza eneo hilo na aliishia kuonyesha hali ya wasiwasi na majonzi.
*****
Anga lilikuwa ni la kijivu huku ukungu wa ajabu ukiwa umetanda katika kila kona.
Ni ulimwengu ambao ni kama umetelekezwa uliojaa ukiwa na ukale , ardhi ambayo haikuwa na dalili ya mti ilikuwa imetawaliwa na harufu mbaya sana ya uozo huku ardhi yake ikiwa ni ya rangi ya kahawia iliokolea iliokuwa na chembechembe za mchanga mwekundu.
Hewa ilikuwa na unyevunyevu kiasi kidogo sana na mara moja moja upepo wa nishati ya nguvu hasi ilikuwa ikizingira katika eneo hilo.
Kulikuwa na vilio vya ajabu na min’gako ambayo ilikuwa ikisikika kutokea pande zote lakini ukisikia sauti upande huu na ukigeuza macho na kuangalia inatokea wapi sauti ile hukoma mara moja.
Eneo hilo lilikuwa ni nusu kuzimu , iijapokuwa kulikuwa na mwanga usiokuwa na chanzo cha jua lakini bado ilionekana kama vile ni alfajiri.
Wakati huo Roma alionekana akiwa amesimama katika ulimwengu huo ambao hakuwa akijua ni ulimwengu gani akiwa amempakata Xiao ambaye bado hakuwa katika fahamu zake.
Kitu pekee ambacho Roma aliona ni unafuu katika eneo hilo ni kwamba uwezo wake wa nishati za mbingu na ardhi haukuwa umepungua kama wakati alivyongia katika ulimwengu wa majini pepo.
Ijapokuwa nguvu ya giza ilikuwa kubwa mno kuliko katika ulimwengu wa kawaida lakini bado haikuwa imemuathiri.
Lakini licha ya Roma kuona uwezo wake anao lakini ilikuwa salama kukiita chungu chake cha maafa na kukifanya kielee juu ya kichwa chake kama kinga ya ulinzi.
Katika mazingira kama hayo ambayo kuna nguvu ya giza kubwa kitu pekee ambacho kinaweza kupambana na nguvu hizo ni chungu hicho ambacho asili yake pia ni nguvu za giza.
Kutokana na uwepo wa ukungu mzito Roma alijaribu kutumia uwezo wake wa utambuzi kupima eneo hilo na aligundua ni eneo ambalo lilikuwa na ukubwa mpana sana ambao alishindwa kujua mwisho wake.
Hakuweza kuona mbali zaidi kwani ilikuwa ni kama juu angani kuna tabaka ambalo linamfanya nguvu zake za kijini kutokufanya kazi na hata kanuni za anga hazikumfanya kwenda juu angani zaidi , ilionekana kabisa hazikuwa zikifanya kazi na alijua lazima anga hilo limefungwa.
Lakini hisia za Roma zilimwambia pengine bado yupo ndani ya anga la dunia isingekuwa ni hivyo asingeweza kutumia uwezo wake wa nishati za mbingu na ardhi.
Roma aliamua kutoka katika eneo hilo na kujaribu kusafiri kwa umbali wa kilomita kadhaa kwenda mbele na alikuja kutua katika ardhi ambayo ilionekana kama vile ni ya kijangwa yenye mchanga mwembamba sana na mlima uliochakaa ambao haukuwa na miti.
Kitu kingine alichoweza kugundua ni uwepo wa mifupa mikubwa sana ya wanyama , ilikuwa ni mifupa isiokuwa ya kawaida kama vile ya wanyama ambao wamepotea katika dunia au waliaminika kuwepo na wakapotea lakini pia aliweza kuona baadhi ya Dhana ambazo zilionekana kukatika hivyo kukosa matumizi.
Roma mara baada ya kutembea kwa muda hatimae alipata wazo ambalo hakuwa na uhakika nalo.
Alikumbuka wakati alipokuwa katika miliki ya Kekexil majini watu walikuwa wakijiandaa mwakani kuingia katika jicho la anga na pengine eneo hilo alipo ndio jicho lenyewe la anga.
Tabia za ulimwengu huo ni kunyonya kiasi kikubwa cha nguvu zake za kijini na kitendo cha kuona Dhana na siraha mbalimbali pamoja na mifupa ya majini pepo waliokufa aliona tabia hizo zinalingana na kile walichosema.
Kuhusu namna alivyoweza kufika katika ulimwengu huo yote hayo yalichangizwa na hazina ya majini pepo kutoka Braki ambayo ilikuwa chini ya familia ya mzee Sharif.
Kokoto ile bado alikuwa nayo lakini katika wakati huo ilionekana kutokuwa na nguvu ya aina yoyote , ilikuwa imebakia katika hali yake ileile ya mwanzo ya kikokoto.
Roma alijaribu kuifanyia mizengwe ya namna nyingi lakini haikuonyesha kutoa nguvu ya aina yoyote na alijikuta akikosa cha kufanya na kuamua kuirudisha katika hifadhi yake.
Kitu kingine ambacho kilimshangaza Roma ni kwamba alishindwa kuhisi roho za nguvu za majini pepo , kinadharia ilitakiwa roho hizo ziwepo kulingana na namna majini walivyokuwa wakiuita ulimwengu huo , lakini amesafiri kwa zaidi ya kilomita mia moja lakini hajahisi nguvu yoyote ya kiumbe hai iwe ni ya kishetani au ya kawaida.
Ulimwengu huo ulikuwa ni mkubwa mno na ilikuwa ngumu hata kujua uelekeo , Roma alikuwa hata hajui alikuwa katika eneo gani ndani ya huo ulimwengu na kilichomshangaza ni kwamba ardhi yake ilikuwa haina viumbe hai wa namna yoyote , lakini hata hivyo aliamini lazima kuna viumbe wanaoishi hapo kama ni hivyo kwanini bado anavuta pumzi kama kawaida , kwanini kuna uwepo wa oksijeni.
“Nini kitatokea kama nitaishia kukwama katika ulimwengu huu , nini kitatokea kwa familia yangu na Lanlan?”
Roma wasiwasi ulianza kumvaa kutokana na kutokujua namna ya kurudi katika ulimwengu wa kawaida na aliishia kulaani majini pepo wa Braki kwa kutokuchukua hazina yao lakini hata hivo aliona anapaswa kuwa na utulivu lazima angepata njia.
Katika wakati huo wa mawazo hatimae Xiao na yeye alishituka kutoka kwenye usingizi na kuanza kuangaza kwa mshituko katika ulimwengu ambao alikuwepo na mara baada ya kuona sura ya Roma imempakata alijikuta akipiga ukulele.
Roma alijua ni hali ya kawaida kwani alikuwa amerejewa na kumbukumbu hivyo alimwacha atulie yeye mwenyewe , na aliishia kumaka na kisha kuanza kuongea maneno yasioeleweka mpaka akaja kutulia.
“Ushamaliza?”Roma aliuliza akiwa katika sura ambayo haikuwa na furaha wala huzuni.
Xiao aliishia kukohoa kwani koo lake lilikuwa linauma kutokana na kupiga yowe, na mara baada ya fahamu zake kuweza kutafsri harufu aliokuwa akinusa aliishia kujaribu kuziba pua kwani ni kama vile anga linatoa mashuzi lakini angalau alikuwa amekwisha kutulia.
Roma aliishia kuvuta pumzi ya ahueni na alijiambia angalau wapo wawili na wanaweza kuibua wazo la kujitoa katika huo ulimwengu..hivyo aliamua kumwelezea Xiao namna ambavyo wamefika katika eneo hilo.
Xiao mara baada ya kusikia baba yake alikuwa hai alifurahi lakini muda huo wasiwasi ulianza kumvaa mara baada ya kusikia kuna uwezekano wapo ndani ya ulimwengu wa jicho la anga.
Akiwa ameshikilia Roma alianza kumsindilia ngumi za lawama na kumlaumu kumleta huku bila kujua namna ya kurudi.
“Acha kunipigia makelele hujichukii tu?, tayari ushakuwa mtu mzima lakini bado unajifanyisha kama mtoto ..nipigie makelele uone kama sitokuacha mwenyewe”
Xiao alishangazwa na kufokewa na Roma lakini alinywea haraka na kuangalia chini.
“Sawa nimetulia , naomba usiniache mwenyewe…”Aliongea na palepale akaanza kuangua kilio cha kwikwi jambo ambalo lilimshangaza Roma.
“Unalia nini sasa , sijasema nataka kukutelekeza nimekuambia utulie , kama ningetaka kufanya hivyo ningekuwa nishafanya muda mrefu , usilie na ongea kawaida tu”Roma alikuwa sio mvumilivu mbele ya machozi ya mwanamke.
Ukweli ni kwamba muda mwingine alijiona sijui ni mwenye bahati ya namna gani , kila anapoingia katika eneo nje ya hiyari yake lazima awe na mwanamke , wakati alipokuwa katika ulimwengu wa majini pepo alikuwa na Sophia na sasa wapo katika ulimwengu wa jicho la Anga yupo na Xiao.
“Mh.. ba.. Roma najua unanijali sana na huwezi kunitelekeza hehe…”Xiao kilio chake kilikuwa cha kinafiki tu ili kumuona Roma atamwangalia vipi , ukweli alishajua hakuna namna Roma anaweza kumtelekeza , ilikuwa ni mbinu za kike tu.
Mabadiliko ya mrembo huyo yalimfanya Roma kukosa usemi , tokea siku ambayo amekutana nae mpaka wakati huo tabia yake haikuwa imebadilika.
“Kwasasa sijui vizuri huu ulimwengu ulivyo hivyo inatupasa kuuelewa kidogo kidogo , nifuate kwa adabu na nitahakikisha unatoka ukiwa salama , sina ombi lolote kwako hivyo usiniletee matatizo tu , sawa?”
“Sawa nitakuwa mwema”
Mara baada ya kuona alikuwa na mtu mwenye nguvu kama Roma hakuwaza kuondoka kwa haraka katika ulimwengu huo wala hakuona hofu ya aina yoyote ile.
Alikuwa na furaha ili mradi tu hawawezi kukwama katika ulimwengu huo.
Ukweli ni kwamba asingekuwa na msaada mkubwa kwa Roma kwani hakuwa mwenye kutamani sana kuvuna nishati za mbingu na ardhi , xiao ni wasichana ambao walijifuza kwa ajili ya kudumisha muonekano wao na kuishi maisha marefu.
Roma mara baada ya kuona utulivu wa msichana huyo alijiuliza au alikuwa amemsahau baba yake , maana hakuuliza chochote.
Kutokan na kwamba Roma alikuwa akitafuta kitu chochote cha kumfanya kuelewa ulimwengu huo hivyo alijitahidi kujibu baadhi ya maswali huku wakiwa wanazurura.
Katika safari yao hio aliweza kupata Dhana ya daraja la juu pamoja na andiko ambalo lugha yake licha ya kwamba hakuilewa vizuri lakini aliona linaweza kuwa la muhimu kwake.
Upande wa mrembo Xiao alikuwa akichunguza kila Dhana aliokuwa akiona , baadhi hakuzipenda lakini nyingine zilimfurahisha na alifurahia safari hio kwani kwake alichukulia kama vile ni safari ya kitalii ya kusaka hazina.
Baada ya muda mrefu sana Roma alikuja kugundua anga linazidi kuwa giza , ijapokuwa hakukuwa na mwanga mkali mwanzoni lakini kadri saa zilivyokuwa zikiongezeka ndio giza lilivyokuwa likiongezeka na walijua lazima kuna nyakati za usiku na mchana hata katika ulimwengu huo,
Sasa wakati ambapo giza hilo lilivyokuwa likiongezeka hali ya nguvu za giza na msisimko wa ajabu ulizidi kukithiri na palepale ni kama Roma anapata uelewa kwamba au viumbe wa ulimwengu huo mchana wanalala na giza likiingia ndio wanaamka.
Roma alikuwa sahihi katika makisio yake , kwani mara baada ya giza kuwa kubwa ni kama miguu yao imeshikiliwa na kani ya mvutano na ilikuwa ngumu sana kupiga hatua na kama sio uwezo wao wa nguvu ya nishati ya mbingu na ardhi ingekuwa ngumu kusonga mbele.
Roma aliamua kuachia nguvu zake za kijini na kuzifanya zimuongoze katika kutambua hatari katika mzingo wa kilomita kumi lakini mara baada ya kitendo hicho palepale sura yake ilijikunja.
Xiao mara baada ya kubadilika kwa muonekano wa Roma alionyesha wasiwasi na kumuuliza Roma nini tatizo.
“Roma kwanini una mabadiliko?”
“Simama mkabala na mimi na hakikisha sio umbali wa hatua tatu , unaelewa”Aliongea Roma kwa namna ya tahadhari.
Wakati msichana huyo akiwa katika hali ya mshangao wa maneno yake aliweza kuona vitu ambavyo vinawasogelea na alijikuta akipatwa na hali ya kupaniki.
“Ni viumbe gani hao , wanaonekana kuwa wengi wanatusogelea”Aliongea Xiao kwa hofu .
Wakati akiongea kauli hio vitu kama moshi mweusi ulianza kujikusanya kutoka katika pande zote na kusogelea katika eneo walipo huku vikitengeneza maumbo ya ajabu.
Mara baada ya kuangalia kwa umakini katika moshi ule ungeweza kuona viumbe vya ajabu sana ambavyo vinasura ya ukali vilivyokuwa vikiwasogelea.
Baadhi ya viumbe hao walikuwa wameshikilia vitu kama mifupa ya kibinadamu na wengine walionekana kuwa na mifupa ambayo haikueleweka wanyama wake .
Kwa msichana kama Xiao ambaye nyoka tu inamtisha katika wakati huo mkojo ulitaka kumtoka.
Chungu cha maafa kilianza kunesa nesa na kuonyesha kustuka na kudhalisha kiwango kikubwa cha nguvu ya giza ambayo ilizingira eneo kubwa katika muundo wa duara.
Chungu hicho kwa namna kilivyokuwa kikicheza cheza ni kama vile kilikuwa katika furaha ya kunasa uwepo wa viumbe wa namna hio.
Ijapokuwa roho ya mnyama huyo alikuwa akiitawala lakini kwa namna fulani bado ufahamu wake alikuwa upo katika akili ya Roma.
Chaos alionekana kutokuweza kumtawala Roma kiakili lakini ilikuwa ni kama vile anasubiria muda nuafaka wa kujiimarisha na kisha kumteka Roma na kutumia mwili wake.
Kabla Roma hajajua hali ilivyo hatimae roho wa giza walimsogelea karibu zaidi na zaidi wakielea kutoka kilomita kadhaa kutoka walipo.
Ghafl tu ilikuwa ni kama vile ni kimbunga cheusi ambacho kilikuwa kinaendesha zile roho kuwasogelea na tofauti na kusinyaa kwa kile kiwingu cheusi kilikuwa kikipanuka na kuwa kama wingu jeusi.
Roma aliweza kugundua kwamba roho hao wa kishetani hawakuwa na nguvu kubwa kutokana na kwamba walikosa miili, haijalishi wakati wakiwa na miili walikuwa na nguvu namna gani lakini kwa wakati huo walikuwa dhaifu mbele ya viumbe wenye miili.
Mwili ndio unafanya mtu kuhifadhi nguvu ya nishati ya mbingu na ardhi na ndio huo huo unaomfanya jini kuweza kupanda levo za dhiki na mengineyo , ukiwa jini katika roho au pepo moja kwa moja unakosa ile sifa ya kuweza kuhifadhi nguvu za nishati ya mbingu na ardhi hivyo athari zako zinakuwa ni za kiroho zaidi tofuati na kuwa za kimwili.
Roma kwa haraka haraka aliweza kujua roho hizo za kishetani kama ni kupima uwezo wao kwa kufananisha na namna nguvu za anga zinavyopimwa basi ni majini ambao watakuwa katika levo ya maji meupe hivyo ni dhaifu sana kuwa tishio kwa Roma.
Kitu kingine ambacho Roma aligundua ni kwamba hizo roho hazikuwa na akili ya namna yoyote na zilikuwa zikitembea kwa kutuia utashi tu wa kihisia na zilianza kuzingira kwa mbali kama vile zilikuwa makini katika kumsogelea.
Roma aliona pengine sio kwasababu roho hao waovu wanamuogopa , ukweli ni kwamba majini wengi ambao waliingia katika ulimwengu huo wa jicho la Anga mara nyingi wanakuwa katika levo ya maji ya kiroho hivyo ilimaanisha kwamba viumbe au roho walizokutana nazo katika ulimwengu huo waliweza kuzimudu.
“Hizi roho zinaonekana zinaogopa roho ya Chaos”Ijapokuwa Chaos alikuwa amepoteza mwili wake lakini ukali wake na nguvu zake hazikujificha.
Kama ilivyo katika ulimwengu wa wanyama , wale wanyama wadogo wadogo walikuwa wakiogopa wale wanyama wakubwa ndio ilivyokuwa kwa roho hizo.
Lakini licha ya hivyo hawakutaka kupotezea tageti yao , ilionekana walikuwa wakitafuta namna ya kushindana na roho hio ili kumvamia Roma na Xiao.
Roa mara baada ya kuona roho hao wa kishetani wanamwangalia kwa macho ya tamaa aliamua kumalizana nao kwa kuruhusu chungu kuwameza , lakini wale roho mara baada ya kuhisi nguvu ya roho ya mnyama ya mvuto wote walianza kukimbia lakini hata hivyo chungu hicho kilikuwa na uwezo mkubwa hivyo roho hao hawakufanikiwa kukimbia.
Ilikuwa ni kama vile moshi mweusi unatoka angani na kuingia katika chungu kile wale roho wote walimezwa na mng’ako wa chngu hicho uliongezeka kadri ilivyokuwa ikimeza hao roho.
Roma aliweza kuhisi nguvu ya ajabu ikiingia katika mwili wake na kufanya senta za nguvu zake za kijini kusinyaa na kupanuka kwa wakati mmoja.
Roma alionekana kufurahi , kilichomfurahishwa ni kwamba ijapokuwa hizo roho hazikuwa katika miili ya kibinadamu lakini chungu chake kilikuwa na uwezo wa kubadiisha nishati yao ya kiovu na kuwa nishati safi na kumwingia Roma na kumfanya nguvu zake kuongezeka.
Roho wale wa giza walikuwa wengi mno na walijaribu kukimbia katika mvuto wa chungu lakini walishindwa kutoka katika mvutano wa roho ya mnyama.
Xiao ambaye alikuwa akiona tukio zima aliishia kuvuta hewa ya amani na kugundua roho hao wa kishetani hawakuwa na uwezo wa kuwasogelea lakini alishangaa kuona Roma alikuwa na tabasamu la ajabu katika uso wake.
Lakini hata hivyo alijua Roma asingejali maoni yake , kwa akili ya kawaida alijua ni nini ambacho Roma anafanya , alijua kabisa anajilisha na nguvu za hayo mapepo.
Ijapokuwa roho na mapepo katika ulimwengu huo walikuwa wengi lakini haikumaanisha kwamba wote wangemsogelea Roma na kumshambulia hivyo idadi ya waliokuwa wakifyonzwa na chungu ilizidi kupungua.
Roma alikuwa akihisi kabisa uwezo wake unaongezeka , kimahesabu kwasababu alikuwa tayari katika levo ya radi ya mapigo tisini na tisa kwa nguvu hizo aliokuwa akipata ni kama nguvu ya ziada tu.
Sasa mara baada ya kuona hakukuwa na roho na pepo nyingine za kumeza walianza kujiandaa kuelekea eneo lingine ili kutafuta mapepo mengine ili kuyanyonya , kwake ni kama ardhi hio ya ulimwengu wa jicho la anga wa mapepo na roho ilikuwa ni kama nchi ya ahadi ya maziwa na asali.
Ijapokuwa hakujua bado namna ya kutoka lakini sio mbaya kama ataendelea kuongeza nguvu zake.alijiambia pengine anaweza kupanda hata levo akiwa ndani ya ulimwengu huo.
Wakati wakijiandaa kuondoka mara aliweza kuhisi mkandamizo wa nguvu ya ajabu , ilikuwa ni nguvu kubwa kuliko wale mapepo wa mwanzo ikiwasogelea kutokea mbali.
“Wewe ni nani unaethubutu kuua watu wangu?”
Sauti iliokuwa kama ya kishetani iliweza kuzifikia ngoma za masikio yake kutoka mbali , ilikuwa sauti kubwa ilioweza kusambaa karibia eneo lote.
Sauti hio ilimshangaza Roma kwani mapepo hayo ya awamu hayo yalikuwa na maumbo ya ajabu lakini mpangilio wa kibinadamu kama vile ni mizuka.
Roma mara baada ya kuangalia kwa umakini aligundua lazima sauti ile ilitoka kwa kiumbe ambaye alikuwa na mwili mkubwa na alieenda hewani mno kwa mita kama nne hivi.
Alikuwa akitisha pamoja na wenzake na alikuwa amevalia mavazi machakavu kama ya ngozi ya mnyama huku akiwa amejifunga na vito flani kama goroli katia mikono yake.
Alikuwa ameambatana na roho nyingine ambazo zilikuwa na maumbo ya kibinadamu lakini sura mbaya zilizokuwa katika mavazi ya kufanana na ilionekana walikuwa ni walinzi.
Roma macho yake yalisinyaa mara baada ya kugundua Mzuka huo ulikuwa na nguvu kulingana na jini ambaye yupo levo ya radi ya mapigo tisini na tisa na walinzi wawili waliokuwa wakimlinda walikuwa katika levo inayolingana na radi ya mapigo tisa na wengine ni sawa na levo ya maji ya kiroho.
Roma alishangaa na kujiambia pengine ndio maana walionekana kuwa na akili.
Unapaswa kuelewa kwamba kila kiumbe ambacho kinapatikana katika ulimwengu huo wa jicho la anga ni viumbe ambao walikufa na roho zao zikaja kuishi katika huo ulimwengu.
Sasa Roma anashangaa kuona mizuka hio kuwa na nguvu kubwa namna hio mara baada ya kufa.
Roma mara baada ya kukumbuka ulimwengu wa jangwa tenganifu ulikuwa na umri zaidi ya miaka elfu hamsini hivyo na ulimwengu huo utakuwa na miaka mingi na kama kweli roho za majini wanaokufa walikuwa wakikimbilia katika ulimwengu huo basi kutakuwa na roho ambazo zilikufa zikiwa katika levo ya kudhibiti radi na kuweza kupitia levo za dhiki ya radi elfu moja.
Wakati Roma akiwa haongei ule Mzuka mkubwa wa kipepo ulisogelea Chaos Caulrdon na macho yake ya kipepo yalikuwa katika hali ya mshangao kama vile hakutegemea kuona kitu kama hicho.
“Hii ni Chaos Cauldron , wewe ni nani mpaka kumiliki Dhana hii ya kilijendi ya Kale?”Aliongea kwa sauti kubwa na nzito sana.
Sauti hio ilikuwa na mwangi na ilikuwa ni kama vile upo katika shamba kubwa la migomba na ujaribu kuongea kwa sauti, lakini licha ya hivyo sauti yake haikuwa ya kuogofya bali ilionekana kuwa ya heshima mbele ya Chungu cha Chaos.


SEHEMU YA 759.
Roma alishangazwa na ukarimu ule, mwanzoni alikuwa akiwaza kama anaweza kushinda kama ataishambulia hio mizuka lakini ilionekana haikuwa na mapngo wa kumshambulia.
“Nyie ni wakina nani na kwani kumiliki Chaos Cauldron ndio nini?”Aliuliza Roma.
“Mimi ndio ‘Mramu’ wa miliki hii naitwa Uramu Hantu ,nimekuja hapa mara baada ya kugundua kundi kubwa la mapepo limepotea , nadhani utakuwa umewameza na hii Dhana ya Chaos Cauldron”
Uramu maana yake ni cheo cha Lord au Bwana katika lugha ya kihangaria na Hantu ni neno pepo au mzuka katika lugha ya Kimalay.
Sasa Roma mara baada ya kusikia neno Uramu na Hantu alishangazwa na majina hayo lakini kitu ambacho hakuwa akifahamu ni kwamba hilo sio jina lake halisi wakati akiwa hai ila ni jina la kutambulisha jamii yake , majini mara nyingi wanakuwa na majina ambayo yanaendana na tabia zao.
“Kwahio umekuja kulipiza kisasi ?”Aliuiza Roma akiwa hana ishara ya hofu kabisa.
Lakini sasa ghafla tu ule mzuka uliangua kicheko kikubwa na kadri ulivyokuwa ukicheka ndio ulivyokuwa ukitisha zaidi na zaidi kwasababu sura yake ilikuwa ni kama lijiskeleton.
“Umenielewa vibaya , waliokufa ni kundi la wasio na faida kwangu na kuna mapepo wengi sana hapa , kwanini nishindane na wewe kwa ajili yao?”
Roma aliona wasiwasi mara baada ya kumuona pengine Uramu Hantu anamuoopa , sasa alijuliza pengine anachomuogopea sio uwezo wake kwani ni kama vile wanalingana ki uwezo lakini pia alikuwa na kundi la watu wake ambao wana uwezo hivyo ilipaswa wasimuogope.
“Au wanadhani mimi ni moja wapo ya wakuu wa enzi hizo kutokana na kumiliki chungu cha maafa?”Aliwaza Roma.
“Nimefika hapa katika ulimwengu wa jicho la anga kwa ajali mbaya na sitaki kugombana na yeyote hivyo usiwe na wasiwasi”
“Je naweza kujua ni ajali gani imekupata?”Uramu Hantu aliuliza huku akionyesha wasiwasi wake.
“Kulingana na maarifa yangu jicho la Anga linafunguka huko katika ulimwengu wa nje kila baada ya karne moja na huu sio muda bado , hivyo imekuwaje ukaingia huku?”Roma aliona kwasababu anauliza maswali anaweza kumjibu lakini lazima na yeye ajibiwe.
“Nitakupa majibu lakini unapaswa kunijibu mimi kwanza”
Uramu Hantu alishangaa lakini palepale alitoa kicheko kidogo na kuonyesha kukubali.
Mapepo hayo ya kijini pengine yamekwisha kufa muda mrefu lakini yaliendelea kuwa hai kutokana na kuendelea kung’ang’ania uwezo wao..
Uramu Hantu alijibu maswali ya Roma yote kwani hakuwa na sababu ya kumficha.
Ilionekana kwamba ulimwengu huo wa jicho la anga ulikuwepo tokea enzi na enzi na kuhusu alieutengeneza haifahamiki lakini kinachofahamika ni kwamba alieugundua ni jini aliekuwa na nguvu kubwa aliefahamika kwa jina la Demok wa enzi hizo.
Ni nafasi katika anga ambayo inajitegemea kabisa kama ilivyokwa ulimwengu wa jangwa tenganifu.
Anasema kwamba wakati wa vita Demok mara baada ya kugundua uwepo wa hilo eneo aliwatega majini pepo wa kishetani ambao walikuwa ni maadui zao na kuwaingiza katika ulimwengu huo na kufanya maamuzi ya kiharibifu kwa kujilipua yeye mwenyewe na kutokana na kitendo hicho majini pepo jamii ya mashetani wa anga waliishia kufa kwani alikuwa ni kama bomu.
Sasa kitendo cha majini wale kufa roho zao hazikufariki bali miili yao ilikuwa ndio iliharibika , sasa wakati roho hizo zilipokuwa zikijaribu kutoka katika ulimwengu huo kwenda ulimwengu wa nje ilishindikana na kwanzia hapo ndio ikawa makazi yao.
Sasa anasema ambacho kinaonekana katika anga ya majini watu kila baada ya miaka mia moja sio mlango bali ni kama ufa ambao huruhusu majini hao kuingia katika ulimwengu huo.
“Nikueleze ukweli tu kwamba tokea niingie katika huu ulimwengu sijawahi kuona roho yoyote inatoweka , huu ni ulimwengu ambao naweza kusema hauna mipaka na haijalishi unaweza kusafiri kwenda umbali kiasi gani lakini tukio la ajabu ni kwamba utaishia kurudi palepale ulipotokea”
Roma alishangaa sana na ndio maana aliona ni kama vile ni ulimwengu usiokuwa na mwisho.
“Umesema kwamba ufa huo hutokea katika kila miaka mia moja , lakini si kuna majini watu wanaingia wakati huo kwa ajili ya kujitafutia hazina na Dhana , kwanini usitumie nafasi hio kutoka kwani uwezo wako ni mkubwa?”
“Kama niivyosema mwanzo hakuna uwezekano wa kutoka katika huu ulimwengu kwasababu moja, kila mara ufa unapojitegneneza kiwango cha nishati hasi ambayo ndio kama chanzo cha nguvu yetu hupungua kwa kiwango kikubwa sana hivyo hutufanya kuwa dhaifu na tunakuwa kama tupo kwenye usingizi mzito , kabla ya ufa kutokea tunachofanya ni kujificha kwanza katika mashimo ili tusije kushambuoliwa na majini watu wanaokuja , hata kama wasipokuja hata kama twende katika ufa hio kuna nguvu kubwa ya chanya ambayo tukiisogelea hatuwezi kuihimili na tunaishia kupotea”Aliongea.
Nguvu hasi inamaanisha nguvu ya giza au nguvu ya kipepo na nguvu chanya ndio nguvu ya nuru au nguvu ya Kimungu.
Ulimwengu wa kawaida upo katika uwiano wa nguvu hasi na nguvu chanya ndio maana viumbe wanaishi katika mchanganyiko lakini katika ulimwengu huo wa jicho la Anga nguvu hasi ambayo ni ya giza ndio kubwa zaidi.
Sasa Roma ndio anajua kumbe ndio maana majini watu walikuwa wakija katika jicho hilo na kutoka bila shida yoyote , ilionekna nguvu ya mapepo hao ilikuwa ni dhiafu mno katika wakati wa kujitengenza kwa ufa ndio maana walishindwa kutoka.
Walijua hata kama wanaweza kutoka katika ulimwengu huo hawawezi kuishi katika nishati ya jua ambayo ina kiwnago kikubwa cha nishati chanya.
Ukweli ni kwamba kama wasingekuwa katika ulimwengu huo ambao ulikuwa na hali ya hewa tofauti na dunia wangekufa muda mrefu.
Roma zamu yake aliongea kila kitu na alimuonyesha Uramu Hantu ile hazina ya familia ya Sharifu na kumuuliza kama ashawahi kuona mahali.
Lakini mapepo hayo hayakuweza kuigundua kazi ya hio hazina lakini walifurahi mara baada ya kujua ni kitu ambacho kiliachwa na watangulzi wao.
“Hiki kitu kinashangaza hakina nguvu yoyote na sijawahi kuona na hata malighafi iliotumika kutengenezea siijui”Aliongea Uramu.
“Kwasababu umekuwa katika huu ulimwengu kwa muda mrefu lazima utakuwa umekutana na majini pepo , je naweza kupata taarifa yoyote kutoka kwake?” Roma mara baada ya kuuliza Uramu alionyesha ishara za hasira.
“Ingawa sikuwa katika levo ya juu ya mapigo elfu moja wakati nafariki lakini wakati huo sikuwa na kinyongo na koo ya majini pepo…”Aliendelea kuongea na Roma aliweza kujua alikuwa ni jini pepo wa kishetani yaani wale majini ambao huzaliwa wakiwa kama wanyama wa kutisha.
“Je nawezaje kutoka katika huu ulimwengu?”Aliuliza Roma kwa shauku.
“Njjia ya kutoka ni moja tu , inakupasa kusubiri mpaka mwaka unaofuatia wakati wa kutokea kwa ufa , isitoshe wote mna miili na una nguvu kubwa hivyo utaweza kutoka bila shida , kama hutojali unaweza kukaribia nyumbani kwangu na kuchukua hifadhi kwa muda”Aliongea
******
MIEZI MIWILI BAADAE
Katika nyumba iliojengwa kwa mawe iliokuwa katikati ya kisiwa kikubwa ndani ya fungu la visiwa hivyo vva wafu , moto ulikuwa ukiwaka kwa hasira kutokana na kuni kuwa kavu na cheche za moto zilikuwa zikionekana zikiruka ndani ya jiko katika eneo hilo la sebuleni.
Tv ya nch 83 ya teknolojia ya Oled iliokuwa imetundikwa ukutani ilikuwa ikionyesha taarifa ya habari za kimataifa kwa kile kinachoendelea ulimwenguni hususani katika mataifa ambayo yapo upande wa Kaskazini mwa dunia.
Chaneli hio ilikuwa ni kama vile imechagua kuonyesha kile kinachoendelea katika nchi kubwa kubwa kama China na Japani na baadhi ya mataifa mengine katika mabara husika.
Katika runinga hio alionekana mwandishi wa habari ambaye anaripoti kutoka katika aneo la tukio ambaye amevalia koti kubwa lililomfunika kutoka juu hadi chini , lipsi zake zilikuwa za zambarau kutokana na baridi kali na alikuwa ni mwanamke, alikuwa amesimama akinyooshea kidole upande wa bandari kubwa ya kusafirishia mzigo kaskazini mwa China.
Theluji ilikuwa ikidondoka kwa kasi mno kama vile ni mvua na kufunika ardhi yote kiasi cha kuifanya ardhi ni kama imefunikwa na zuria pana jeupe.
“Kama mnavyo ona , maji yote kuja katika bandari hii yameganda , hii bandari haijawahi kuganda katika historia yake yote lakini katika nyuzi joto -37oC maji yamegeuka na kuwa barafu , meli zimekwama kufika katika bandari na wafanyakazi wameshaondoka muda mrefu, kulingana na serikali ya China wameshaanza kuingia makubaliano na nchi kumi na moja zilizopo katika bara la Afrika upande wa kusini kwa ajili ya kuhifadhi raia huku taratibu nyingine za kuokoa binadamu zikiendelea…”
Aliekuwa akiangalia Tv ni Bi Wema na alikuwa amejifunika na Blanket kubwa ambalo alikuwa akijifunika vizuri kila sekunde na alijaribu kubadilisha chaneli na karibia chaneli zote za kisimbuzi lakini zilikuwa zikitangaza habari zinazofanana , yote hayo ni kile kinachoendelea katika dunia.
Watu katika mataifa mengi walikuwa katika hali ya taharuki kwa kile kinachotokea duniani.
Bi Wema mara baada ya kuona hakuna chaneli inayoonyesha tamthilia aliishia kuzima na kumgeukia Sui na Rufi.
“Yaani nimebadilisha chaneli zote habari zinafanana tu , dunia ipo katika taharuki sijui ni kitu gani kinaendelea usiku nakosa hata usingizi”
“Mama si uachane kuangalia habari naona zinakuongezea wasiwasi tu , ni kama kinachoendelea hapa Mediterranian ni swala la muda tu na bahari yetu kuganda”
“Ndio kwanza ni mwezi wa saba kwenda wa nane huu lakini hali ipo hivi , kama ikiendelea watu ambao watapoteza maisha kutokana na baridi watakuwa wengi sana.. Mwenyezi Mungu ukoa watu wako”
Sui ambaye alikuwa kimya muda wote alitaka kuongea neno lakini muonekano wake ulionekana kubadilika.
“Wamerudi”Aliongea
Muda uleule mlango ulifunguliwa na kufanya upepo wa baridi kuingia ndani na kumfanya Bi Wema na Rufi kutetemeka.
Wanawake warembo waliokuwa wamevalia ‘trench Coats’ waliingia , alikuwa ni Edna , Amina na wengine wote na miili yao ilikuwa imefunikwa na kiasi cha theluji..
“Naona huko nje mvua ya theluji imeanza , ona ulivyojaa chembe theluji“Aliongea Bi Wema akijaribu kumpangusa Edna kichwa chake
Kwa kuangalia kwa nje tu ungeweza kuona namna miti ilivyokuwa imenyauka , kila kitu kilikuwa cha kutisha.
“Nje hakuna theluji Bi Wema , tumepitia China ndio kuna theluji ya kutisha”Aliongea Edna.
“Oh! ,,, nikajua ni huko nje , hebu kaeni kwanza mniambie habari za Tanzania’Aliongea Bi Wema kwa shauku.
Siku chache zilizopita warembo hao walisafiri kwenda Tanzania kuona hali ilivyo na baada ya hapo wakaelekea katika maeneo ya China na Japani kujaribu kumtafuta Roma.
Upande wa Edna , Neema Luwazo na Amina walikuwa na makampuni mengi tu ambayo yana wafanyakazi wengi ,yaan Vexto, Kanani Group na Maple zote
Kutokana na kwamba wao ndio viongozi wa juu wa makampuni hayo hawakuwa na sababu ya kujitokeza mara kwa mara kazini hivyo walienda kwa ajili ya kazi ambazo ziliihitaji uwepo wao.
Ukweli ni kwamba wote walirudi kutokana na biashara yao ya Real Estate na hio ni kutokana na kwamba matajiri wengi walikuwa wakitoka mataifa ya Kaskazini mwa dunia na kuja katika nchi za Ikweta ambazo baridi yake ilikuwa chiin.
Serikali ya Tanzania ni moja ya nchi ambazo zimekubali kupokea baadhi ya raia kutoka katika mataifa makubwa ikiwemo China , Japani na Marekani na hawa raia ambao wanakuja walihitaji sehemu za kuishi na makampuni makubwa ambayo yanamiliki mahoteli na Apartment ilikuwa ndio biashara sasa kwa wakati huo ambayo ilikuwa na thamani kubwa.
Sasa Edna , Neema na Amina ni moja ya wamiliki wa kampuni hizo ambazo zinamiliki biashara za kukarimu watu , wakati Neema yeye akiwa na mahoteli karibia nchi nzima na Afrika mashariki na kati yote upande wa Edna yeye alikuwa na Apartment za kutosha katika kila nchi na baadhi ya hoteli na projekti za ujenzi wa hoteli nyingi katika nchi ya Afrika mashariki yote na kati yote ulikuwa ukiendelea.
Hivyo ilikuwa ni swala la kuchangamkia fursa , Amina yeye kampuni yake pia ilikuwa ikijihusisha na mahoteli pamoja na vyakula hivyo pia ni kama amepitiwa na upepo wa fursa.
Sasa mara baada ya kusaini mikataba mingi ya ujenzi moja kwa moja wote walienda Hongkong kwa ajili ya kusaini mikataba na makampuni ambayo inasafirisha raia kuja nchi za hali ya joto na baada ya hapo walielekea Beijing China kwa ajili ya misheni maalumu.
Ijapokuwa joto lilikuwa likishuka kwa kasi katika mwambao wa kaskazini lakini nchi ambazo zilikuwa katika mwambao wa kusini na ikweta na baadhi ya nchi za Afrika nyingi zilikuwa bado hazijapitia hali ya baridi kali na mazingira yake bado yalikuwa mazuri kwa kusapoti maisha ya viumbe hai.
Yaani kwa siku kadhaa baadhi ya nchi nyingi zilizokuwa katika bara la Afrika na baadhi ya nchi za Amerika ya kusini zimegeuka kuwa nchi ambazo nyumba na ardhi zimekuwa za thamani kuliko hata dhahabu.
Changamoto kubwa ambayo inaikumba dunia ni swala la usafirishaji , baadhi ya bahari nyingi zilikuwa zimeganda na reli nazo hazikuruhusu treni kupita hivyo usafirishaji wa chakula kuwa mgumu mno na hii inasababisha serikali nyingi kufanya juhudi kubwa kuzia uhalifu.
Ijapokuwa maeneo ambayo bado yapo salama ni mengi lakini maeneo hayo kilimo chake kilikuwa hakitoshelezi watu wote , kwa mfano nchi kama Tanzania haijitoshelezi katika kilimo chake , sasa kwa wingi wa watu ambao wanaingia nchini inafanya nchi kukosa chakula.
“Nasikia nusu ya nchi za China , Urusi na Japani zimeganda na matajiri wengi wanakimbilia nchi ambazo zipo katika mstari wa ikweta na baadhi ya maeneo ya kusini na hali ikiendelea hivi na maeneo ya kusini pia joto lake linaweza kufikia nyuzi sifuri “Aliongea Rose
“Sasa nini kitatokea jamani, kama hali hii itaendelea watu wengi watakufa”Aliuliza Bi Wema.
“Wasiwasi wangu ni kwamba kama watu hawatokufa kwa baridi bali watakufa kwa njaaa au kupigana wao kwa wao mpaka kufa , katika maeneo mengi maduka ambayo yalikuwa chini ya uendeshaji binafsi yanaendeshwa na wanajeshi wa kiserikali ili kuzuia uhalifu lakini bado haitoshi , kiwango cha uhalifu kimeongezeka sana ,imekuwa bahati kwa nchi nyingi za Afrika hali sio mbaya lakini bara la Asia na Ulaya ndio kwenye hali mbaya zaidi lakini hili linaweza kuwa swala la muda tu”Aliongea Magdalena
Hali ilikuwa mbaya wale wa imani kali wanatangaza ni wakati wa kiama huku baadhi ya watumishi kutoka Afrika wanasema abara ya Asia , Ulaya na Amerika ya Kaskazini yanaadhibiwa kutokana na kufanya dhambi sana ikiwemo kuruhusu ndoa za jinsia moja.
Ki ufupi kila mtu alikuwa akiongea lake na wale ambao hawakuwa wakiamini uwepo wa Mungu walikuwa wakikimbilia makanisani na msikitini.
“Vipi wakwe zako , Blandina na Mzee Kweka?hujaenda kuwasalimia?”Bi Wema alimuuliza Edna.
“Nimeenda na wapo salama mama na babu wote wapo Dar Mzee anasema baridi Iringa imezidi, sijawaeleza chochote kuhusu Roma”Aliongea Edna kinyonge.
“Tukiachana na hayo vipi kuhusu Mr hakuna taarifa yoyote ambayo mmeweza kuipata?”Aliuliza Bi Wema.
Ijapokuwa walienda China kibiashra lakini pia walienda kwa misheni ya kuweza kujua Roma yupo wapi , ukweli ni kwamba kitu ambacho Roma hakuwa akijua ni kwamba muda ulivyokuwaukihesabika katika ulimwengu ule aliopo ulikuwa ni tofauti katika ulimwengu wa kawaida.
“Tumefanikiwa kwenda China na kuonana na mkuu wa jeshi la kitengo cha Iron Flame Brigade kwa msaada wa serikali ya Tanzania na tumeweza kuonana na Jenerali Cai Yuncheng ambaye alituunganisha na mjumbe wa Hongmeng , na taarifa zinasema kwamba Anjiu ndio ambaye alipambana na Roma mara ya mwisho na taarifa za chini ni kwamba hakukuwa na uwezekano wa Hubby kushindwa na jini Anjiu lakini Anjiu yupo hai na yeye kapotea”Aliongea Mage
‘Hongmeng na wenyewe wanasema wapo na wasiwasi na wanatafuta msaada wa Roma kwani Anjiu ashaanza kushambulia miliki zote na kutaka ziwe chini yake na kutokana na Hongmeng kupoteza watu wao wengi hofu yao ni kwamba akimaliza miliki nyingine anaweza akaja kwao pia”Aliongea Magdalena.
“Ni shetani yule lazima kuna mbinu ametumia kumuumiza mpenzi wetu , lakini uhakika wangu ni kwamba Roma atarudi”Aliongea Rufi
Na warembo hao wote walilazimisha tabasamu , ijapokuwa walikuwa wakitamani kuona Roma anarudi akiwa salama lakini hawakuwa na uelewa alikuwa kaenda wapi , mtu pekee ambae anaweza kuwaambia mahali alipo Roma ni jini Anjiu lakini wasingeweza kwenda ulimwengu wa majini na kumuuliza.
“Kwasasa haina haja ya kuwa na wasiwasi , kitu pekee tunachoweza kufanya ni kumuanini na kumsubiri arudi.. Bi Wema simuoni bini yangu Lanlan kakimbilia wapi?”Aliongea Edna mara baada ya kuwatuliza na ndio wakati ambao alimkumbuka binti yake.
“Wale dada zetu wameenda kutembelea baadhi ya nchi kadhaa za karibu na kama unavyojua Lanlan ametokea kuwapenda sana hivyo walimchukua na kuondoka nae , wameniambia nisikuambie maana ungekataa , niliamni atakuwa salama akiwa nao hivyo nimekubali waondoke nae tu”Alijibu Bi Wema lakini sura ya Edna ilijikunja.
Usikose ni ya moto sana ijayo.
ITAENDELEA KESHO AU JUMAMOSI
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI :SINGANOJR

Mono no aware.

SEHEMU YA 758.

Anjiu mara baada ya kujiuliza kwa dakika kadhaa ni kama sasa alikuwa anapata uelewa ni kitu gani kimetokea.
“Jicho la Anga!!!’
Mara baada ya kuangalia eneo ambalo yupo ni kati ya mpaka wa miliki ya Xia na Panas na ndio eneo ambalo jicho la anga hufunguka alipata wazo hilo, ijapokuwa muonekano wa jicho hilo hutofautiana kila linapofunguka lakini ilikuwa ni sehemu hio , sasa alijiuliza je kile kidoti cheusi alichoona angani ndio lango la jicho la anga lakini kwanini lifunguke wakati huo ilihali tarehe ya kufunguka kwake ilikuwa mwakani.
Hakukuwa na ishara ya furaha katika macho ya Anjiu wakati akijaribu kuchunguza eneo hilo na aliishia kuonyesha hali ya wasiwasi na majonzi.
*****
Anga lilikuwa ni la kijivu huku ukungu wa ajabu ukiwa umetanda katika kila kona.
Ni ulimwengu ambao ni kama umetelekezwa uliojaa ukiwa na ukale , ardhi ambayo haikuwa na dalili ya mti ilikuwa imetawaliwa na harufu mbaya sana ya uozo huku ardhi yake ikiwa ni ya rangi ya kahawia iliokolea iliokuwa na chembechembe za mchanga mwekundu.
Hewa ilikuwa na unyevunyevu kiasi kidogo sana na mara moja moja upepo wa nishati ya nguvu hasi ilikuwa ikizingira katika eneo hilo.
Kulikuwa na vilio vya ajabu na min’gako ambayo ilikuwa ikisikika kutokea pande zote lakini ukisikia sauti upande huu na ukigeuza macho na kuangalia inatokea wapi sauti ile hukoma mara moja.
Eneo hilo lilikuwa ni nusu kuzimu , iijapokuwa kulikuwa na mwanga usiokuwa na chanzo cha jua lakini bado ilionekana kama vile ni alfajiri.
Wakati huo Roma alionekana akiwa amesimama katika ulimwengu huo ambao hakuwa akijua ni ulimwengu gani akiwa amempakata Xiao ambaye bado hakuwa katika fahamu zake.
Kitu pekee ambacho Roma aliona ni unafuu katika eneo hilo ni kwamba uwezo wake wa nishati za mbingu na ardhi haukuwa umepungua kama wakati alivyongia katika ulimwengu wa majini pepo.
Ijapokuwa nguvu ya giza ilikuwa kubwa mno kuliko katika ulimwengu wa kawaida lakini bado haikuwa imemuathiri.
Lakini licha ya Roma kuona uwezo wake anao lakini ilikuwa salama kukiita chungu chake cha maafa na kukifanya kielee juu ya kichwa chake kama kinga ya ulinzi.
Katika mazingira kama hayo ambayo kuna nguvu ya giza kubwa kitu pekee ambacho kinaweza kupambana na nguvu hizo ni chungu hicho ambacho asili yake pia ni nguvu za giza.
Kutokana na uwepo wa ukungu mzito Roma alijaribu kutumia uwezo wake wa utambuzi kupima eneo hilo na aligundua ni eneo ambalo lilikuwa na ukubwa mpana sana ambao alishindwa kujua mwisho wake.
Hakuweza kuona mbali zaidi kwani ilikuwa ni kama juu angani kuna tabaka ambalo linamfanya nguvu zake za kijini kutokufanya kazi na hata kanuni za anga hazikumfanya kwenda juu angani zaidi , ilionekana kabisa hazikuwa zikifanya kazi na alijua lazima anga hilo limefungwa.
Lakini hisia za Roma zilimwambia pengine bado yupo ndani ya anga la dunia isingekuwa ni hivyo asingeweza kutumia uwezo wake wa nishati za mbingu na ardhi.
Roma aliamua kutoka katika eneo hilo na kujaribu kusafiri kwa umbali wa kilomita kadhaa kwenda mbele na alikuja kutua katika ardhi ambayo ilionekana kama vile ni ya kijangwa yenye mchanga mwembamba sana na mlima uliochakaa ambao haukuwa na miti.
Kitu kingine alichoweza kugundua ni uwepo wa mifupa mikubwa sana ya wanyama , ilikuwa ni mifupa isiokuwa ya kawaida kama vile ya wanyama ambao wamepotea katika dunia au waliaminika kuwepo na wakapotea lakini pia aliweza kuona baadhi ya Dhana ambazo zilionekana kukatika hivyo kukosa matumizi.
Roma mara baada ya kutembea kwa muda hatimae alipata wazo ambalo hakuwa na uhakika nalo.
Alikumbuka wakati alipokuwa katika miliki ya Kekexil majini watu walikuwa wakijiandaa mwakani kuingia katika jicho la anga na pengine eneo hilo alipo ndio jicho lenyewe la anga.
Tabia za ulimwengu huo ni kunyonya kiasi kikubwa cha nguvu zake za kijini na kitendo cha kuona Dhana na siraha mbalimbali pamoja na mifupa ya majini pepo waliokufa aliona tabia hizo zinalingana na kile walichosema.
Kuhusu namna alivyoweza kufika katika ulimwengu huo yote hayo yalichangizwa na hazina ya majini pepo kutoka Braki ambayo ilikuwa chini ya familia ya mzee Sharif.
Kokoto ile bado alikuwa nayo lakini katika wakati huo ilionekana kutokuwa na nguvu ya aina yoyote , ilikuwa imebakia katika hali yake ileile ya mwanzo ya kikokoto.
Roma alijaribu kuifanyia mizengwe ya namna nyingi lakini haikuonyesha kutoa nguvu ya aina yoyote na alijikuta akikosa cha kufanya na kuamua kuirudisha katika hifadhi yake.
Kitu kingine ambacho kilimshangaza Roma ni kwamba alishindwa kuhisi roho za nguvu za majini pepo , kinadharia ilitakiwa roho hizo ziwepo kulingana na namna majini walivyokuwa wakiuita ulimwengu huo , lakini amesafiri kwa zaidi ya kilomita mia moja lakini hajahisi nguvu yoyote ya kiumbe hai iwe ni ya kishetani au ya kawaida.
Ulimwengu huo ulikuwa ni mkubwa mno na ilikuwa ngumu hata kujua uelekeo , Roma alikuwa hata hajui alikuwa katika eneo gani ndani ya huo ulimwengu na kilichomshangaza ni kwamba ardhi yake ilikuwa haina viumbe hai wa namna yoyote , lakini hata hivyo aliamini lazima kuna viumbe wanaoishi hapo kama ni hivyo kwanini bado anavuta pumzi kama kawaida , kwanini kuna uwepo wa oksijeni.
“Nini kitatokea kama nitaishia kukwama katika ulimwengu huu , nini kitatokea kwa familia yangu na Lanlan?”
Roma wasiwasi ulianza kumvaa kutokana na kutokujua namna ya kurudi katika ulimwengu wa kawaida na aliishia kulaani majini pepo wa Braki kwa kutokuchukua hazina yao lakini hata hivo aliona anapaswa kuwa na utulivu lazima angepata njia.
Katika wakati huo wa mawazo hatimae Xiao na yeye alishituka kutoka kwenye usingizi na kuanza kuangaza kwa mshituko katika ulimwengu ambao alikuwepo na mara baada ya kuona sura ya Roma imempakata alijikuta akipiga ukulele.
Roma alijua ni hali ya kawaida kwani alikuwa amerejewa na kumbukumbu hivyo alimwacha atulie yeye mwenyewe , na aliishia kumaka na kisha kuanza kuongea maneno yasioeleweka mpaka akaja kutulia.
“Ushamaliza?”Roma aliuliza akiwa katika sura ambayo haikuwa na furaha wala huzuni.
Xiao aliishia kukohoa kwani koo lake lilikuwa linauma kutokana na kupiga yowe, na mara baada ya fahamu zake kuweza kutafsri harufu aliokuwa akinusa aliishia kujaribu kuziba pua kwani ni kama vile anga linatoa mashuzi lakini angalau alikuwa amekwisha kutulia.
Roma aliishia kuvuta pumzi ya ahueni na alijiambia angalau wapo wawili na wanaweza kuibua wazo la kujitoa katika huo ulimwengu..hivyo aliamua kumwelezea Xiao namna ambavyo wamefika katika eneo hilo.
Xiao mara baada ya kusikia baba yake alikuwa hai alifurahi lakini muda huo wasiwasi ulianza kumvaa mara baada ya kusikia kuna uwezekano wapo ndani ya ulimwengu wa jicho la anga.
Akiwa ameshikilia Roma alianza kumsindilia ngumi za lawama na kumlaumu kumleta huku bila kujua namna ya kurudi.
“Acha kunipigia makelele hujichukii tu?, tayari ushakuwa mtu mzima lakini bado unajifanyisha kama mtoto ..nipigie makelele uone kama sitokuacha mwenyewe”
Xiao alishangazwa na kufokewa na Roma lakini alinywea haraka na kuangalia chini.
“Sawa nimetulia , naomba usiniache mwenyewe…”Aliongea na palepale akaanza kuangua kilio cha kwikwi jambo ambalo lilimshangaza Roma.
“Unalia nini sasa , sijasema nataka kukutelekeza nimekuambia utulie , kama ningetaka kufanya hivyo ningekuwa nishafanya muda mrefu , usilie na ongea kawaida tu”Roma alikuwa sio mvumilivu mbele ya machozi ya mwanamke.
Ukweli ni kwamba muda mwingine alijiona sijui ni mwenye bahati ya namna gani , kila anapoingia katika eneo nje ya hiyari yake lazima awe na mwanamke , wakati alipokuwa katika ulimwengu wa majini pepo alikuwa na Sophia na sasa wapo katika ulimwengu wa jicho la Anga yupo na Xiao.
“Mh.. ba.. Roma najua unanijali sana na huwezi kunitelekeza hehe…”Xiao kilio chake kilikuwa cha kinafiki tu ili kumuona Roma atamwangalia vipi , ukweli alishajua hakuna namna Roma anaweza kumtelekeza , ilikuwa ni mbinu za kike tu.
Mabadiliko ya mrembo huyo yalimfanya Roma kukosa usemi , tokea siku ambayo amekutana nae mpaka wakati huo tabia yake haikuwa imebadilika.
“Kwasasa sijui vizuri huu ulimwengu ulivyo hivyo inatupasa kuuelewa kidogo kidogo , nifuate kwa adabu na nitahakikisha unatoka ukiwa salama , sina ombi lolote kwako hivyo usiniletee matatizo tu , sawa?”
“Sawa nitakuwa mwema”
Mara baada ya kuona alikuwa na mtu mwenye nguvu kama Roma hakuwaza kuondoka kwa haraka katika ulimwengu huo wala hakuona hofu ya aina yoyote ile.
Alikuwa na furaha ili mradi tu hawawezi kukwama katika ulimwengu huo.
Ukweli ni kwamba asingekuwa na msaada mkubwa kwa Roma kwani hakuwa mwenye kutamani sana kuvuna nishati za mbingu na ardhi , xiao ni wasichana ambao walijifuza kwa ajili ya kudumisha muonekano wao na kuishi maisha marefu.
Roma mara baada ya kuona utulivu wa msichana huyo alijiuliza au alikuwa amemsahau baba yake , maana hakuuliza chochote.
Kutokan na kwamba Roma alikuwa akitafuta kitu chochote cha kumfanya kuelewa ulimwengu huo hivyo alijitahidi kujibu baadhi ya maswali huku wakiwa wanazurura.
Katika safari yao hio aliweza kupata Dhana ya daraja la juu pamoja na andiko ambalo lugha yake licha ya kwamba hakuilewa vizuri lakini aliona linaweza kuwa la muhimu kwake.
Upande wa mrembo Xiao alikuwa akichunguza kila Dhana aliokuwa akiona , baadhi hakuzipenda lakini nyingine zilimfurahisha na alifurahia safari hio kwani kwake alichukulia kama vile ni safari ya kitalii ya kusaka hazina.
Baada ya muda mrefu sana Roma alikuja kugundua anga linazidi kuwa giza , ijapokuwa hakukuwa na mwanga mkali mwanzoni lakini kadri saa zilivyokuwa zikiongezeka ndio giza lilivyokuwa likiongezeka na walijua lazima kuna nyakati za usiku na mchana hata katika ulimwengu huo,
Sasa wakati ambapo giza hilo lilivyokuwa likiongezeka hali ya nguvu za giza na msisimko wa ajabu ulizidi kukithiri na palepale ni kama Roma anapata uelewa kwamba au viumbe wa ulimwengu huo mchana wanalala na giza likiingia ndio wanaamka.
Roma alikuwa sahihi katika makisio yake , kwani mara baada ya giza kuwa kubwa ni kama miguu yao imeshikiliwa na kani ya mvutano na ilikuwa ngumu sana kupiga hatua na kama sio uwezo wao wa nguvu ya nishati ya mbingu na ardhi ingekuwa ngumu kusonga mbele.
Roma aliamua kuachia nguvu zake za kijini na kuzifanya zimuongoze katika kutambua hatari katika mzingo wa kilomita kumi lakini mara baada ya kitendo hicho palepale sura yake ilijikunja.
Xiao mara baada ya kubadilika kwa muonekano wa Roma alionyesha wasiwasi na kumuuliza Roma nini tatizo.
“Roma kwanini una mabadiliko?”
“Simama mkabala na mimi na hakikisha sio umbali wa hatua tatu , unaelewa”Aliongea Roma kwa namna ya tahadhari.
Wakati msichana huyo akiwa katika hali ya mshangao wa maneno yake aliweza kuona vitu ambavyo vinawasogelea na alijikuta akipatwa na hali ya kupaniki.
“Ni viumbe gani hao , wanaonekana kuwa wengi wanatusogelea”Aliongea Xiao kwa hofu .
Wakati akiongea kauli hio vitu kama moshi mweusi ulianza kujikusanya kutoka katika pande zote na kusogelea katika eneo walipo huku vikitengeneza maumbo ya ajabu.
Mara baada ya kuangalia kwa umakini katika moshi ule ungeweza kuona viumbe vya ajabu sana ambavyo vinasura ya ukali vilivyokuwa vikiwasogelea.
Baadhi ya viumbe hao walikuwa wameshikilia vitu kama mifupa ya kibinadamu na wengine walionekana kuwa na mifupa ambayo haikueleweka wanyama wake .
Kwa msichana kama Xiao ambaye nyoka tu inamtisha katika wakati huo mkojo ulitaka kumtoka.
Chungu cha maafa kilianza kunesa nesa na kuonyesha kustuka na kudhalisha kiwango kikubwa cha nguvu ya giza ambayo ilizingira eneo kubwa katika muundo wa duara.
Chungu hicho kwa namna kilivyokuwa kikicheza cheza ni kama vile kilikuwa katika furaha ya kunasa uwepo wa viumbe wa namna hio.
Ijapokuwa roho ya mnyama huyo alikuwa akiitawala lakini kwa namna fulani bado ufahamu wake alikuwa upo katika akili ya Roma.
Chaos alionekana kutokuweza kumtawala Roma kiakili lakini ilikuwa ni kama vile anasubiria muda nuafaka wa kujiimarisha na kisha kumteka Roma na kutumia mwili wake.
Kabla Roma hajajua hali ilivyo hatimae roho wa giza walimsogelea karibu zaidi na zaidi wakielea kutoka kilomita kadhaa kutoka walipo.
Ghafl tu ilikuwa ni kama vile ni kimbunga cheusi ambacho kilikuwa kinaendesha zile roho kuwasogelea na tofauti na kusinyaa kwa kile kiwingu cheusi kilikuwa kikipanuka na kuwa kama wingu jeusi.
Roma aliweza kugundua kwamba roho hao wa kishetani hawakuwa na nguvu kubwa kutokana na kwamba walikosa miili, haijalishi wakati wakiwa na miili walikuwa na nguvu namna gani lakini kwa wakati huo walikuwa dhaifu mbele ya viumbe wenye miili.
Mwili ndio unafanya mtu kuhifadhi nguvu ya nishati ya mbingu na ardhi na ndio huo huo unaomfanya jini kuweza kupanda levo za dhiki na mengineyo , ukiwa jini katika roho au pepo moja kwa moja unakosa ile sifa ya kuweza kuhifadhi nguvu za nishati ya mbingu na ardhi hivyo athari zako zinakuwa ni za kiroho zaidi tofuati na kuwa za kimwili.
Roma kwa haraka haraka aliweza kujua roho hizo za kishetani kama ni kupima uwezo wao kwa kufananisha na namna nguvu za anga zinavyopimwa basi ni majini ambao watakuwa katika levo ya maji meupe hivyo ni dhaifu sana kuwa tishio kwa Roma.
Kitu kingine ambacho Roma aligundua ni kwamba hizo roho hazikuwa na akili ya namna yoyote na zilikuwa zikitembea kwa kutuia utashi tu wa kihisia na zilianza kuzingira kwa mbali kama vile zilikuwa makini katika kumsogelea.
Roma aliona pengine sio kwasababu roho hao waovu wanamuogopa , ukweli ni kwamba majini wengi ambao waliingia katika ulimwengu huo wa jicho la Anga mara nyingi wanakuwa katika levo ya maji ya kiroho hivyo ilimaanisha kwamba viumbe au roho walizokutana nazo katika ulimwengu huo waliweza kuzimudu.
“Hizi roho zinaonekana zinaogopa roho ya Chaos”Ijapokuwa Chaos alikuwa amepoteza mwili wake lakini ukali wake na nguvu zake hazikujificha.
Kama ilivyo katika ulimwengu wa wanyama , wale wanyama wadogo wadogo walikuwa wakiogopa wale wanyama wakubwa ndio ilivyokuwa kwa roho hizo.
Lakini licha ya hivyo hawakutaka kupotezea tageti yao , ilionekana walikuwa wakitafuta namna ya kushindana na roho hio ili kumvamia Roma na Xiao.
Roa mara baada ya kuona roho hao wa kishetani wanamwangalia kwa macho ya tamaa aliamua kumalizana nao kwa kuruhusu chungu kuwameza , lakini wale roho mara baada ya kuhisi nguvu ya roho ya mnyama ya mvuto wote walianza kukimbia lakini hata hivyo chungu hicho kilikuwa na uwezo mkubwa hivyo roho hao hawakufanikiwa kukimbia.
Ilikuwa ni kama vile moshi mweusi unatoka angani na kuingia katika chungu kile wale roho wote walimezwa na mng’ako wa chngu hicho uliongezeka kadri ilivyokuwa ikimeza hao roho.
Roma aliweza kuhisi nguvu ya ajabu ikiingia katika mwili wake na kufanya senta za nguvu zake za kijini kusinyaa na kupanuka kwa wakati mmoja.
Roma alionekana kufurahi , kilichomfurahishwa ni kwamba ijapokuwa hizo roho hazikuwa katika miili ya kibinadamu lakini chungu chake kilikuwa na uwezo wa kubadiisha nishati yao ya kiovu na kuwa nishati safi na kumwingia Roma na kumfanya nguvu zake kuongezeka.
Roho wale wa giza walikuwa wengi mno na walijaribu kukimbia katika mvuto wa chungu lakini walishindwa kutoka katika mvutano wa roho ya mnyama.
Xiao ambaye alikuwa akiona tukio zima aliishia kuvuta hewa ya amani na kugundua roho hao wa kishetani hawakuwa na uwezo wa kuwasogelea lakini alishangaa kuona Roma alikuwa na tabasamu la ajabu katika uso wake.
Lakini hata hivyo alijua Roma asingejali maoni yake , kwa akili ya kawaida alijua ni nini ambacho Roma anafanya , alijua kabisa anajilisha na nguvu za hayo mapepo.
Ijapokuwa roho na mapepo katika ulimwengu huo walikuwa wengi lakini haikumaanisha kwamba wote wangemsogelea Roma na kumshambulia hivyo idadi ya waliokuwa wakifyonzwa na chungu ilizidi kupungua.
Roma alikuwa akihisi kabisa uwezo wake unaongezeka , kimahesabu kwasababu alikuwa tayari katika levo ya radi ya mapigo tisini na tisa kwa nguvu hizo aliokuwa akipata ni kama nguvu ya ziada tu.
Sasa mara baada ya kuona hakukuwa na roho na pepo nyingine za kumeza walianza kujiandaa kuelekea eneo lingine ili kutafuta mapepo mengine ili kuyanyonya , kwake ni kama ardhi hio ya ulimwengu wa jicho la anga wa mapepo na roho ilikuwa ni kama nchi ya ahadi ya maziwa na asali.
Ijapokuwa hakujua bado namna ya kutoka lakini sio mbaya kama ataendelea kuongeza nguvu zake.alijiambia pengine anaweza kupanda hata levo akiwa ndani ya ulimwengu huo.
Wakati wakijiandaa kuondoka mara aliweza kuhisi mkandamizo wa nguvu ya ajabu , ilikuwa ni nguvu kubwa kuliko wale mapepo wa mwanzo ikiwasogelea kutokea mbali.
“Wewe ni nani unaethubutu kuua watu wangu?”
Sauti iliokuwa kama ya kishetani iliweza kuzifikia ngoma za masikio yake kutoka mbali , ilikuwa sauti kubwa ilioweza kusambaa karibia eneo lote.
Sauti hio ilimshangaza Roma kwani mapepo hayo ya awamu hayo yalikuwa na maumbo ya ajabu lakini mpangilio wa kibinadamu kama vile ni mizuka.
Roma mara baada ya kuangalia kwa umakini aligundua lazima sauti ile ilitoka kwa kiumbe ambaye alikuwa na mwili mkubwa na alieenda hewani mno kwa mita kama nne hivi.
Alikuwa akitisha pamoja na wenzake na alikuwa amevalia mavazi machakavu kama ya ngozi ya mnyama huku akiwa amejifunga na vito flani kama goroli katia mikono yake.
Alikuwa ameambatana na roho nyingine ambazo zilikuwa na maumbo ya kibinadamu lakini sura mbaya zilizokuwa katika mavazi ya kufanana na ilionekana walikuwa ni walinzi.
Roma macho yake yalisinyaa mara baada ya kugundua Mzuka huo ulikuwa na nguvu kulingana na jini ambaye yupo levo ya radi ya mapigo tisini na tisa na walinzi wawili waliokuwa wakimlinda walikuwa katika levo inayolingana na radi ya mapigo tisa na wengine ni sawa na levo ya maji ya kiroho.
Roma alishangaa na kujiambia pengine ndio maana walionekana kuwa na akili.
Unapaswa kuelewa kwamba kila kiumbe ambacho kinapatikana katika ulimwengu huo wa jicho la anga ni viumbe ambao walikufa na roho zao zikaja kuishi katika huo ulimwengu.
Sasa Roma anashangaa kuona mizuka hio kuwa na nguvu kubwa namna hio mara baada ya kufa.
Roma mara baada ya kukumbuka ulimwengu wa jangwa tenganifu ulikuwa na umri zaidi ya miaka elfu hamsini hivyo na ulimwengu huo utakuwa na miaka mingi na kama kweli roho za majini wanaokufa walikuwa wakikimbilia katika ulimwengu huo basi kutakuwa na roho ambazo zilikufa zikiwa katika levo ya kudhibiti radi na kuweza kupitia levo za dhiki ya radi elfu moja.
Wakati Roma akiwa haongei ule Mzuka mkubwa wa kipepo ulisogelea Chaos Caulrdon na macho yake ya kipepo yalikuwa katika hali ya mshangao kama vile hakutegemea kuona kitu kama hicho.
“Hii ni Chaos Cauldron , wewe ni nani mpaka kumiliki Dhana hii ya kilijendi ya Kale?”Aliongea kwa sauti kubwa na nzito sana.
Sauti hio ilikuwa na mwangi na ilikuwa ni kama vile upo katika shamba kubwa la migomba na ujaribu kuongea kwa sauti, lakini licha ya hivyo sauti yake haikuwa ya kuogofya bali ilionekana kuwa ya heshima mbele ya Chungu cha Chaos.


SEHEMU YA 759.
Roma alishangazwa na ukarimu ule, mwanzoni alikuwa akiwaza kama anaweza kushinda kama ataishambulia hio mizuka lakini ilionekana haikuwa na mapngo wa kumshambulia.
“Nyie ni wakina nani na kwani kumiliki Chaos Cauldron ndio nini?”Aliuliza Roma.
“Mimi ndio ‘Mramu’ wa miliki hii naitwa Uramu Hantu ,nimekuja hapa mara baada ya kugundua kundi kubwa la mapepo limepotea , nadhani utakuwa umewameza na hii Dhana ya Chaos Cauldron”
Uramu maana yake ni cheo cha Lord au Bwana katika lugha ya kihangaria na Hantu ni neno pepo au mzuka katika lugha ya Kimalay.
Sasa Roma mara baada ya kusikia neno Uramu na Hantu alishangazwa na majina hayo lakini kitu ambacho hakuwa akifahamu ni kwamba hilo sio jina lake halisi wakati akiwa hai ila ni jina la kutambulisha jamii yake , majini mara nyingi wanakuwa na majina ambayo yanaendana na tabia zao.
“Kwahio umekuja kulipiza kisasi ?”Aliuiza Roma akiwa hana ishara ya hofu kabisa.
Lakini sasa ghafla tu ule mzuka uliangua kicheko kikubwa na kadri ulivyokuwa ukicheka ndio ulivyokuwa ukitisha zaidi na zaidi kwasababu sura yake ilikuwa ni kama lijiskeleton.
“Umenielewa vibaya , waliokufa ni kundi la wasio na faida kwangu na kuna mapepo wengi sana hapa , kwanini nishindane na wewe kwa ajili yao?”
Roma aliona wasiwasi mara baada ya kumuona pengine Uramu Hantu anamuoopa , sasa alijuliza pengine anachomuogopea sio uwezo wake kwani ni kama vile wanalingana ki uwezo lakini pia alikuwa na kundi la watu wake ambao wana uwezo hivyo ilipaswa wasimuogope.
“Au wanadhani mimi ni moja wapo ya wakuu wa enzi hizo kutokana na kumiliki chungu cha maafa?”Aliwaza Roma.
“Nimefika hapa katika ulimwengu wa jicho la anga kwa ajali mbaya na sitaki kugombana na yeyote hivyo usiwe na wasiwasi”
“Je naweza kujua ni ajali gani imekupata?”Uramu Hantu aliuliza huku akionyesha wasiwasi wake.
“Kulingana na maarifa yangu jicho la Anga linafunguka huko katika ulimwengu wa nje kila baada ya karne moja na huu sio muda bado , hivyo imekuwaje ukaingia huku?”Roma aliona kwasababu anauliza maswali anaweza kumjibu lakini lazima na yeye ajibiwe.
“Nitakupa majibu lakini unapaswa kunijibu mimi kwanza”
Uramu Hantu alishangaa lakini palepale alitoa kicheko kidogo na kuonyesha kukubali.
Mapepo hayo ya kijini pengine yamekwisha kufa muda mrefu lakini yaliendelea kuwa hai kutokana na kuendelea kung’ang’ania uwezo wao..
Uramu Hantu alijibu maswali ya Roma yote kwani hakuwa na sababu ya kumficha.
Ilionekana kwamba ulimwengu huo wa jicho la anga ulikuwepo tokea enzi na enzi na kuhusu alieutengeneza haifahamiki lakini kinachofahamika ni kwamba alieugundua ni jini aliekuwa na nguvu kubwa aliefahamika kwa jina la Demok wa enzi hizo.
Ni nafasi katika anga ambayo inajitegemea kabisa kama ilivyokwa ulimwengu wa jangwa tenganifu.
Anasema kwamba wakati wa vita Demok mara baada ya kugundua uwepo wa hilo eneo aliwatega majini pepo wa kishetani ambao walikuwa ni maadui zao na kuwaingiza katika ulimwengu huo na kufanya maamuzi ya kiharibifu kwa kujilipua yeye mwenyewe na kutokana na kitendo hicho majini pepo jamii ya mashetani wa anga waliishia kufa kwani alikuwa ni kama bomu.
Sasa kitendo cha majini wale kufa roho zao hazikufariki bali miili yao ilikuwa ndio iliharibika , sasa wakati roho hizo zilipokuwa zikijaribu kutoka katika ulimwengu huo kwenda ulimwengu wa nje ilishindikana na kwanzia hapo ndio ikawa makazi yao.
Sasa anasema ambacho kinaonekana katika anga ya majini watu kila baada ya miaka mia moja sio mlango bali ni kama ufa ambao huruhusu majini hao kuingia katika ulimwengu huo.
“Nikueleze ukweli tu kwamba tokea niingie katika huu ulimwengu sijawahi kuona roho yoyote inatoweka , huu ni ulimwengu ambao naweza kusema hauna mipaka na haijalishi unaweza kusafiri kwenda umbali kiasi gani lakini tukio la ajabu ni kwamba utaishia kurudi palepale ulipotokea”
Roma alishangaa sana na ndio maana aliona ni kama vile ni ulimwengu usiokuwa na mwisho.
“Umesema kwamba ufa huo hutokea katika kila miaka mia moja , lakini si kuna majini watu wanaingia wakati huo kwa ajili ya kujitafutia hazina na Dhana , kwanini usitumie nafasi hio kutoka kwani uwezo wako ni mkubwa?”
“Kama niivyosema mwanzo hakuna uwezekano wa kutoka katika huu ulimwengu kwasababu moja, kila mara ufa unapojitegneneza kiwango cha nishati hasi ambayo ndio kama chanzo cha nguvu yetu hupungua kwa kiwango kikubwa sana hivyo hutufanya kuwa dhaifu na tunakuwa kama tupo kwenye usingizi mzito , kabla ya ufa kutokea tunachofanya ni kujificha kwanza katika mashimo ili tusije kushambuoliwa na majini watu wanaokuja , hata kama wasipokuja hata kama twende katika ufa hio kuna nguvu kubwa ya chanya ambayo tukiisogelea hatuwezi kuihimili na tunaishia kupotea”Aliongea.
Nguvu hasi inamaanisha nguvu ya giza au nguvu ya kipepo na nguvu chanya ndio nguvu ya nuru au nguvu ya Kimungu.
Ulimwengu wa kawaida upo katika uwiano wa nguvu hasi na nguvu chanya ndio maana viumbe wanaishi katika mchanganyiko lakini katika ulimwengu huo wa jicho la Anga nguvu hasi ambayo ni ya giza ndio kubwa zaidi.
Sasa Roma ndio anajua kumbe ndio maana majini watu walikuwa wakija katika jicho hilo na kutoka bila shida yoyote , ilionekna nguvu ya mapepo hao ilikuwa ni dhiafu mno katika wakati wa kujitengenza kwa ufa ndio maana walishindwa kutoka.
Walijua hata kama wanaweza kutoka katika ulimwengu huo hawawezi kuishi katika nishati ya jua ambayo ina kiwnago kikubwa cha nishati chanya.
Ukweli ni kwamba kama wasingekuwa katika ulimwengu huo ambao ulikuwa na hali ya hewa tofauti na dunia wangekufa muda mrefu.
Roma zamu yake aliongea kila kitu na alimuonyesha Uramu Hantu ile hazina ya familia ya Sharifu na kumuuliza kama ashawahi kuona mahali.
Lakini mapepo hayo hayakuweza kuigundua kazi ya hio hazina lakini walifurahi mara baada ya kujua ni kitu ambacho kiliachwa na watangulzi wao.
“Hiki kitu kinashangaza hakina nguvu yoyote na sijawahi kuona na hata malighafi iliotumika kutengenezea siijui”Aliongea Uramu.
“Kwasababu umekuwa katika huu ulimwengu kwa muda mrefu lazima utakuwa umekutana na majini pepo , je naweza kupata taarifa yoyote kutoka kwake?” Roma mara baada ya kuuliza Uramu alionyesha ishara za hasira.
“Ingawa sikuwa katika levo ya juu ya mapigo elfu moja wakati nafariki lakini wakati huo sikuwa na kinyongo na koo ya majini pepo…”Aliendelea kuongea na Roma aliweza kujua alikuwa ni jini pepo wa kishetani yaani wale majini ambao huzaliwa wakiwa kama wanyama wa kutisha.
“Je nawezaje kutoka katika huu ulimwengu?”Aliuliza Roma kwa shauku.
“Njjia ya kutoka ni moja tu , inakupasa kusubiri mpaka mwaka unaofuatia wakati wa kutokea kwa ufa , isitoshe wote mna miili na una nguvu kubwa hivyo utaweza kutoka bila shida , kama hutojali unaweza kukaribia nyumbani kwangu na kuchukua hifadhi kwa muda”Aliongea
******
MIEZI MIWILI BAADAE
Katika nyumba iliojengwa kwa mawe iliokuwa katikati ya kisiwa kikubwa ndani ya fungu la visiwa hivyo vva wafu , moto ulikuwa ukiwaka kwa hasira kutokana na kuni kuwa kavu na cheche za moto zilikuwa zikionekana zikiruka ndani ya jiko katika eneo hilo la sebuleni.
Tv ya nch 83 ya teknolojia ya Oled iliokuwa imetundikwa ukutani ilikuwa ikionyesha taarifa ya habari za kimataifa kwa kile kinachoendelea ulimwenguni hususani katika mataifa ambayo yapo upande wa Kaskazini mwa dunia.
Chaneli hio ilikuwa ni kama vile imechagua kuonyesha kile kinachoendelea katika nchi kubwa kubwa kama China na Japani na baadhi ya mataifa mengine katika mabara husika.
Katika runinga hio alionekana mwandishi wa habari ambaye anaripoti kutoka katika aneo la tukio ambaye amevalia koti kubwa lililomfunika kutoka juu hadi chini , lipsi zake zilikuwa za zambarau kutokana na baridi kali na alikuwa ni mwanamke, alikuwa amesimama akinyooshea kidole upande wa bandari kubwa ya kusafirishia mzigo kaskazini mwa China.
Theluji ilikuwa ikidondoka kwa kasi mno kama vile ni mvua na kufunika ardhi yote kiasi cha kuifanya ardhi ni kama imefunikwa na zuria pana jeupe.
“Kama mnavyo ona , maji yote kuja katika bandari hii yameganda , hii bandari haijawahi kuganda katika historia yake yote lakini katika nyuzi joto -37oC maji yamegeuka na kuwa barafu , meli zimekwama kufika katika bandari na wafanyakazi wameshaondoka muda mrefu, kulingana na serikali ya China wameshaanza kuingia makubaliano na nchi kumi na moja zilizopo katika bara la Afrika upande wa kusini kwa ajili ya kuhifadhi raia huku taratibu nyingine za kuokoa binadamu zikiendelea…”
Aliekuwa akiangalia Tv ni Bi Wema na alikuwa amejifunika na Blanket kubwa ambalo alikuwa akijifunika vizuri kila sekunde na alijaribu kubadilisha chaneli na karibia chaneli zote za kisimbuzi lakini zilikuwa zikitangaza habari zinazofanana , yote hayo ni kile kinachoendelea katika dunia.
Watu katika mataifa mengi walikuwa katika hali ya taharuki kwa kile kinachotokea duniani.
Bi Wema mara baada ya kuona hakuna chaneli inayoonyesha tamthilia aliishia kuzima na kumgeukia Sui na Rufi.
“Yaani nimebadilisha chaneli zote habari zinafanana tu , dunia ipo katika taharuki sijui ni kitu gani kinaendelea usiku nakosa hata usingizi”
“Mama si uachane kuangalia habari naona zinakuongezea wasiwasi tu , ni kama kinachoendelea hapa Mediterranian ni swala la muda tu na bahari yetu kuganda”
“Ndio kwanza ni mwezi wa saba kwenda wa nane huu lakini hali ipo hivi , kama ikiendelea watu ambao watapoteza maisha kutokana na baridi watakuwa wengi sana.. Mwenyezi Mungu ukoa watu wako”
Sui ambaye alikuwa kimya muda wote alitaka kuongea neno lakini muonekano wake ulionekana kubadilika.
“Wamerudi”Aliongea
Muda uleule mlango ulifunguliwa na kufanya upepo wa baridi kuingia ndani na kumfanya Bi Wema na Rufi kutetemeka.
Wanawake warembo waliokuwa wamevalia ‘trench Coats’ waliingia , alikuwa ni Edna , Amina na wengine wote na miili yao ilikuwa imefunikwa na kiasi cha theluji..
“Naona huko nje mvua ya theluji imeanza , ona ulivyojaa chembe theluji“Aliongea Bi Wema akijaribu kumpangusa Edna kichwa chake
Kwa kuangalia kwa nje tu ungeweza kuona namna miti ilivyokuwa imenyauka , kila kitu kilikuwa cha kutisha.
“Nje hakuna theluji Bi Wema , tumepitia China ndio kuna theluji ya kutisha”Aliongea Edna.
“Oh! ,,, nikajua ni huko nje , hebu kaeni kwanza mniambie habari za Tanzania’Aliongea Bi Wema kwa shauku.
Siku chache zilizopita warembo hao walisafiri kwenda Tanzania kuona hali ilivyo na baada ya hapo wakaelekea katika maeneo ya China na Japani kujaribu kumtafuta Roma.
Upande wa Edna , Neema Luwazo na Amina walikuwa na makampuni mengi tu ambayo yana wafanyakazi wengi ,yaan Vexto, Kanani Group na Maple zote
Kutokana na kwamba wao ndio viongozi wa juu wa makampuni hayo hawakuwa na sababu ya kujitokeza mara kwa mara kazini hivyo walienda kwa ajili ya kazi ambazo ziliihitaji uwepo wao.
Ukweli ni kwamba wote walirudi kutokana na biashara yao ya Real Estate na hio ni kutokana na kwamba matajiri wengi walikuwa wakitoka mataifa ya Kaskazini mwa dunia na kuja katika nchi za Ikweta ambazo baridi yake ilikuwa chiin.
Serikali ya Tanzania ni moja ya nchi ambazo zimekubali kupokea baadhi ya raia kutoka katika mataifa makubwa ikiwemo China , Japani na Marekani na hawa raia ambao wanakuja walihitaji sehemu za kuishi na makampuni makubwa ambayo yanamiliki mahoteli na Apartment ilikuwa ndio biashara sasa kwa wakati huo ambayo ilikuwa na thamani kubwa.
Sasa Edna , Neema na Amina ni moja ya wamiliki wa kampuni hizo ambazo zinamiliki biashara za kukarimu watu , wakati Neema yeye akiwa na mahoteli karibia nchi nzima na Afrika mashariki na kati yote upande wa Edna yeye alikuwa na Apartment za kutosha katika kila nchi na baadhi ya hoteli na projekti za ujenzi wa hoteli nyingi katika nchi ya Afrika mashariki yote na kati yote ulikuwa ukiendelea.
Hivyo ilikuwa ni swala la kuchangamkia fursa , Amina yeye kampuni yake pia ilikuwa ikijihusisha na mahoteli pamoja na vyakula hivyo pia ni kama amepitiwa na upepo wa fursa.
Sasa mara baada ya kusaini mikataba mingi ya ujenzi moja kwa moja wote walienda Hongkong kwa ajili ya kusaini mikataba na makampuni ambayo inasafirisha raia kuja nchi za hali ya joto na baada ya hapo walielekea Beijing China kwa ajili ya misheni maalumu.
Ijapokuwa joto lilikuwa likishuka kwa kasi katika mwambao wa kaskazini lakini nchi ambazo zilikuwa katika mwambao wa kusini na ikweta na baadhi ya nchi za Afrika nyingi zilikuwa bado hazijapitia hali ya baridi kali na mazingira yake bado yalikuwa mazuri kwa kusapoti maisha ya viumbe hai.
Yaani kwa siku kadhaa baadhi ya nchi nyingi zilizokuwa katika bara la Afrika na baadhi ya nchi za Amerika ya kusini zimegeuka kuwa nchi ambazo nyumba na ardhi zimekuwa za thamani kuliko hata dhahabu.
Changamoto kubwa ambayo inaikumba dunia ni swala la usafirishaji , baadhi ya bahari nyingi zilikuwa zimeganda na reli nazo hazikuruhusu treni kupita hivyo usafirishaji wa chakula kuwa mgumu mno na hii inasababisha serikali nyingi kufanya juhudi kubwa kuzia uhalifu.
Ijapokuwa maeneo ambayo bado yapo salama ni mengi lakini maeneo hayo kilimo chake kilikuwa hakitoshelezi watu wote , kwa mfano nchi kama Tanzania haijitoshelezi katika kilimo chake , sasa kwa wingi wa watu ambao wanaingia nchini inafanya nchi kukosa chakula.
“Nasikia nusu ya nchi za China , Urusi na Japani zimeganda na matajiri wengi wanakimbilia nchi ambazo zipo katika mstari wa ikweta na baadhi ya maeneo ya kusini na hali ikiendelea hivi na maeneo ya kusini pia joto lake linaweza kufikia nyuzi sifuri “Aliongea Rose
“Sasa nini kitatokea jamani, kama hali hii itaendelea watu wengi watakufa”Aliuliza Bi Wema.
“Wasiwasi wangu ni kwamba kama watu hawatokufa kwa baridi bali watakufa kwa njaaa au kupigana wao kwa wao mpaka kufa , katika maeneo mengi maduka ambayo yalikuwa chini ya uendeshaji binafsi yanaendeshwa na wanajeshi wa kiserikali ili kuzuia uhalifu lakini bado haitoshi , kiwango cha uhalifu kimeongezeka sana ,imekuwa bahati kwa nchi nyingi za Afrika hali sio mbaya lakini bara la Asia na Ulaya ndio kwenye hali mbaya zaidi lakini hili linaweza kuwa swala la muda tu”Aliongea Magdalena
Hali ilikuwa mbaya wale wa imani kali wanatangaza ni wakati wa kiama huku baadhi ya watumishi kutoka Afrika wanasema abara ya Asia , Ulaya na Amerika ya Kaskazini yanaadhibiwa kutokana na kufanya dhambi sana ikiwemo kuruhusu ndoa za jinsia moja.
Ki ufupi kila mtu alikuwa akiongea lake na wale ambao hawakuwa wakiamini uwepo wa Mungu walikuwa wakikimbilia makanisani na msikitini.
“Vipi wakwe zako , Blandina na Mzee Kweka?hujaenda kuwasalimia?”Bi Wema alimuuliza Edna.
“Nimeenda na wapo salama mama na babu wote wapo Dar Mzee anasema baridi Iringa imezidi, sijawaeleza chochote kuhusu Roma”Aliongea Edna kinyonge.
“Tukiachana na hayo vipi kuhusu Mr hakuna taarifa yoyote ambayo mmeweza kuipata?”Aliuliza Bi Wema.
Ijapokuwa walienda China kibiashra lakini pia walienda kwa misheni ya kuweza kujua Roma yupo wapi , ukweli ni kwamba kitu ambacho Roma hakuwa akijua ni kwamba muda ulivyokuwaukihesabika katika ulimwengu ule aliopo ulikuwa ni tofauti katika ulimwengu wa kawaida.
“Tumefanikiwa kwenda China na kuonana na mkuu wa jeshi la kitengo cha Iron Flame Brigade kwa msaada wa serikali ya Tanzania na tumeweza kuonana na Jenerali Cai Yuncheng ambaye alituunganisha na mjumbe wa Hongmeng , na taarifa zinasema kwamba Anjiu ndio ambaye alipambana na Roma mara ya mwisho na taarifa za chini ni kwamba hakukuwa na uwezekano wa Hubby kushindwa na jini Anjiu lakini Anjiu yupo hai na yeye kapotea”Aliongea Mage
‘Hongmeng na wenyewe wanasema wapo na wasiwasi na wanatafuta msaada wa Roma kwani Anjiu ashaanza kushambulia miliki zote na kutaka ziwe chini yake na kutokana na Hongmeng kupoteza watu wao wengi hofu yao ni kwamba akimaliza miliki nyingine anaweza akaja kwao pia”Aliongea Magdalena.
“Ni shetani yule lazima kuna mbinu ametumia kumuumiza mpenzi wetu , lakini uhakika wangu ni kwamba Roma atarudi”Aliongea Rufi
Na warembo hao wote walilazimisha tabasamu , ijapokuwa walikuwa wakitamani kuona Roma anarudi akiwa salama lakini hawakuwa na uelewa alikuwa kaenda wapi , mtu pekee ambae anaweza kuwaambia mahali alipo Roma ni jini Anjiu lakini wasingeweza kwenda ulimwengu wa majini na kumuuliza.
“Kwasasa haina haja ya kuwa na wasiwasi , kitu pekee tunachoweza kufanya ni kumuanini na kumsubiri arudi.. Bi Wema simuoni bini yangu Lanlan kakimbilia wapi?”Aliongea Edna mara baada ya kuwatuliza na ndio wakati ambao alimkumbuka binti yake.
“Wale dada zetu wameenda kutembelea baadhi ya nchi kadhaa za karibu na kama unavyojua Lanlan ametokea kuwapenda sana hivyo walimchukua na kuondoka nae , wameniambia nisikuambie maana ungekataa , niliamni atakuwa salama akiwa nao hivyo nimekubali waondoke nae tu”Alijibu Bi Wema lakini sura ya Edna ilijikunja.
Usikose ni ya moto sana ijayo.
ITAENDELEA
 
NILIMDHANIA KABAHA KUMBE BIKRA

MTUNZI: SINGANOJR

WATSAPP: 0687151346.

Mono no aware.

SEHEMU YA 760.
Tokea siku warembo wa kijini pepo yaani Latina , Weni na Yunu wakubali kulinda familia ya Roma walikuwa wakifanya kama walivyokuwa wameahidi na walitumia muda mwingi kuishi ndani ya visiwa hivyo isipokuwa tu walikuwa wakirudi mara chache sana katika ulimwengu wao wa jangwa tenganifu.
Ingawa walikuwa katika mshangao kwanini Roma hakuwa amerudi lakini waliendelea kuwa wavumilivu wakiamini kwamba ndani ya ulimwengu wa majini watu hakuna mtu ambaye anaweza kumshinda Roma.
Kwa majini pepo ambao wameishi miaka elfu moja kukaa kisiwani hapo kwa miezi miwili ilikuwa ni kama siku moja tu.
Sasa wakati Edna alivyosafiri alimuacha Lanlan kutokana na kwamba aliona atakuwa bize na kazi , hivyo wakati wa Lanlan akiwa hapo kisiwani alitumia muda mwingi na majini hao.
Ulimwengu wa jangwa tenganifu haukuwa na mazingira ya kushangaza kama ilivyokuwa kwa ulimwengu wa kawaida na ndio maana kila kitu kiliwashangaza na walitaka kujua mengi kuhusu ustaarabu wa binadamu , hivyo Latina na wenzake walielekea katika baadhi ya nchi za karibu kwa ajili ya kutembea kwani hakukuwa na tatizo lolote ambalo lilikuwa limetokea kwa zaidi ya miezi yote miwili , ukweli ni kwamba ni kama hawakuwa wakijali kile kinachoendelea katika dunia.
Ijapokuwa Bara la Ulaya maeneo mengi yalikuwa yameganda kwa barafu waliweza kufika maeneo ambayo hayakuwa na milima , isitoshe majini hawaathiriki na baridi na hata kwa Lanlan ambaye tayari ana nguvu za kijini hakuwa akiathirika na baridi kama binadamu wa kawaida.
“Edna usiwe na wasiwasi . wale dada zetu hawana shida lazima atakuwa salama”Aliongea Nasra.
“Umenielewa vibaya , wasiwasi wangu sio kwamba atakuwa katika hatari lakini akiwa katika furaha iliopitiliza anaweza kusababisha matatizo”Aliongea Edna lakini ndio muda huo huo simu ya familia hio ilianza kuita.
Bi Wema ndio alieamka na kuipokea mara baada ya kuona aliekuwa akipiga ni Ron.
“Mr Ron kuna kitu unataka nikusaidie?”
“Madam Wema , Mrs Roma bado hajarudi?”Aliuliza Ron akimlenga Edna.
“Ndio amerudi sasa hivi , kama una jambo la kumwambia unaweza kuja wote wamerudi wapo hapa”Aliongea Bi Wema,
“Hapana , jambo lenyewe ni kwamba Kamanda wa kikosi cha Phantom, Brewester katuma ujumbe kututaarifu kwamba meli za kijeshi kutokea Uingereza , Ufaransa ,Ujerumani , Italia na Hispania Ziimeonekana katika maji ya karibu na visiwa vetu , sio kawaida hivyo nataka kumuuliza Mrs Roma kama tunaweza kuchukua hatua ya kushambulia”
Bi Wema alijikuta akishangazwa na kauli hio kwani hakuwa akijua chochote kuhusu jeshi la Roma na kwa haraka sana alimpatia Edna simu.
Kwasababu Roma hakuwepo kisiwani vikosi vyote vya jeshi la Sea Eagles walikuwa wakimchukulia Edna kama kiongoi wao na wangetoa ripoti moja kwa moja kutoka kwake na kutaka maamuzi yake ni kikosi cha Phantom ndio kilichokuwa kikihusika na ulinzi wa visiwa.
Edna mara baada ya kusikiliza ripoti hio kutoka kwa Ron aliinamisha kichwa chini akionekana kuwaza.
“Mr Ron tageti yao sio sisi bali ni Clark , mwambie Kanali Brewester asichukue hatua”
“Princess Clark!!”
Ron alionekana kushangaa lakini hakuwa na wasiwasi juu ya maamuzi ya Edna na palepale alitoa ‘affirmative’ na kisha akakata simu.
“Hivi Clark Amerudi?”Aliuliza Edna mara baada ya kumaliza maongezi akimuuliza Bi Wema.
“Amerudi ndio siku kadhaa zilizopita , tokea arudi kutokea Uingerea alikuwa ana mudi mbaya kweli na hajatoka katika maabara yake”Alijibu Bi Wema na wengine wote waliangaliana kama vile walikuwa wakijua nini kinaendelea.
“Edna kwanini umesema wapo hapa kwa ajili ya Clark?“Aliulia Mage.
“Nadhani unaweza kuotea sababu”Alijibu Amina na Edna alitingisha kichwa kukubaliana nae.
“Lazima itakuwa ni juu ya kile kinachoendelea”
“Edna acha kuzunguka zunguka basi , hebu tuambie nini kimetokea”AliongeaMage kibabe.
“Clark mwenyewe ndie atakuja kuelezea ndio atahusika kuongea na hao wanajeshi pia”Aliongea Edna na haikuchukua hata dakika chache Clark aliweza kufika akiwa amevalia koti la kimaabara, nywele zake zilikuwa zimechanguka ikionyesha hakuwa amepata muda wa kupumzika kutokana na utafiti.
“Wanapata uhubutu gani kuja huku ilihali nishawakatalia waziwazi”Aliongea ikioneysha ni kama alikuwa akijua kinachoendelea.
“Nadhani hawaogopi kuingia katika hatari , wakati wa kupambania maisha utafanya vitu hata vya hatari ili mradi tu kujiokoa na kwao wewe ndio tumaini lao”Aliongea Edna huku akinywa chai ya moto.
Wengine wote walionyesha kutokuelewa wanachomaanisha ni nini na Clark alicheka na kisha akaanza kuwaelezea nini kilitokea.
Ilionekana kwamba Clark alikuwa amealikwa na kitengo cha usalama na wanachama wa kitengo cha ‘Royal Society’ ili kuhudhuria kikao cha baraza la kimataifa la usalama wiki moja iliopita.
Wahudhuriaji katika kikao hicho ni viongozi wa mataifa ambayo yamekwisha kuendelea na baadhi ya mataifa ambayo yanaendelea.
Vilevile watu maarufu na wamiliki wa makampuni makubwa duniani na wale matajiri walipewa nafasi ya kuhudhuria kikao hicho, ikiwemo familia kubwa duniani kama vile Morgani ,Rockfellers na Rothchild.
Lakini pia wengine ambao wamealikwa ni wanasayansi maarufu na watu majiniasi wenye vipaji maalumu kutoka pande zote za dunia.
Kikao hicho kilikuwa ni cha siri mno na licha ya kwamba kilionekana kuandaliwa na umoja wa baraza la usalama wa kidunia lakini ukweli ni kwamba nyuma ya pazia waandaaji ni Zeros organitision.
Ajenda ya kikao hicho ilikuwa ni kujadiliana kile ambacho kitatokea kwa binadamu kama joto la dunia litaendelea kushuka zaidi na zaidi.
Sasa baada ya majadiliano ya muda mrefu hatimae waliamua mpango ambao hata Clark mwenyewe aliona sio wa kawaida.
Viongozi wote waliweza kupiga kura ya ndio juu ya mpango huo na ni kura chache tu ambazo ziliharibika hivyo moja kwa moja mpango ukaidhinishwa rasmi na mpango huo ulipewa jina la Noah Ark Project yaani projekti ya ujenzi wa Safina ya Nuhu.
Yaani maamuzi yaliofikiwa ni kwamba nchi zote zenye nguvu pamoja na matajiri kutoka katika familia mbalimbali kuunganisha rasilimali zao zote kujenga meli kubwa ya usalama wa juu katika kipindi cha miezi sita tu.
Kulingana na teknolojia ilionekana ni ngumu kufanya ujenzi wa makazi katika orbit(mzingo) ya dunia kupitia msaada wa ‘Space station’ na nafasi yao pekee ni kutumia nishati ya nyuklia , hydrojen , Solar na vyanzo vingine vya nishati ili kujenga ngome kubwa ya chuma ambayo itakuwa na uwezo wa kuwafanya watu kadhaa waendelee kuishi juu ya barafu kama hali itaendelea kuwa mbaya na dunia kukosa sifa ya kusapoti maisha..
Kulingana na mahesabu ya kitafiti , kama joto litaendelea kupotea katika kiwango kilekile ndani ya mwaka mmoja basi joto katika mwambao wa kusini mwa dunia mpaka Ikweta litashuka kwa zaidi ya nyuzi kumi zaidi chini ya sifuri na wakati huo dunia yote itakuwa ni barafu.
Yaani kwamba hata maeneo ya Afrika mashariki ambayo mataifa yake yapo katika mstari wa ikweta na kupata mwanga wa jua kwa kiasi kikubwa baridi itafikia nyuzi hasi kumi hali ya hewa ambayo itakuwa ngumu sana kwa binadamu ambaye hajazoea kuishi katika mazingira ya namna hio.
Sasa ili kuzuia kiumbe binadamu asipotee kabisa katika uso wa dunia iliamuliwa mara baada ya projekti hio kukamilika wasichana na wavulana wenye vipaji mbalimbali na uwezo mkubwa wa akili, wanasayanansi na mafundi ndio watapanda katika safina hio kuepuka janga la dunia na watakuja kutoka dunia itaporudi kwenye hali yake.
Bila shaka , ujuzi , hela na rasilimali zingehitajika kujenga meli hio hivyo ilimaanisha sapoti kutoka kwa matajiri ilikuwa ikihitajika , hivyo wale mabilionea wenye pesa nyingi ndio ambao wangepewa kipaumbele kuingia wa kwanza.
Hayo ndio maamuzi yaliofikiwa katika kikao hicho , yaani kama huna hela angalau uwe na akili na ndio unaweza kubahatika kuingia katika safina
Mara baada ya kumsikiliza Clark wanawake hao walijikuta kimya mno kila mtu akiwaza lake , ilioneknna ni kama vile ni stori ya maisha ya baadae au filamu ya kisayansi wakati dunia ikiingia matatizoni lakini haikuwa ndoto wala filamu bali ni uhalisia kabisa.
Kwa lugha nyepesi ni kwamba Clark ndio moja ya wanasayansi ambao walitegemewa kusanifu na kujenga safina ambayo itaweza kuokoa uzao wa kibinadamu.
“Nilikataa pendekezo hilo kwasababu nafikiri hata kama nitaweza kusanifu na kujenga Safina, haitokuwa na maana kama hatutodili na chanzo cha tatizo , kama sikosei miungu ndio ipo nyuma na hiki kinachoendelea na njia pekee ni kuwazuia waache kufanya wanachopanga ili kuokoa binadamu , lakini hawakutaka kukubaliana na mimi na hawaamini kama binadamu tunaweza kupigana na miungu , na sasa wamepotea na hatujui ni wapi pakuanzia kuwatafuta”
“Hio ndio ipo wazi binadamu hawawezi kuwafanya chochote hata kama wajue miungu ndio sababu”Aliongea Edna huku akitabasamu kama vile yeye sio binadamu.
“Ila si uliongea na nchi za magharibi kuhusu nguvu ya jua kunyonywa katika ncha ya Kaskazini , wamekupa jibu lolote?”Aliuliza Edna.
“Hilo ndio tatizo kubwa kwa sasa , Marekani , Urusi na Canada walituma vikosi vya makomandoo lakini mpaka sasa hawapatikani hewani mara baada ya kutua katika ncha ya kaskaizini , meli pia ambazo zilikuwa zikielekea huko zimezama zote na hakuna aliepona na sababu juu ya matukio hayo hayafahamiki”Clark aliendelea kuongea.
“Inaonekana ni miungu hao ndio wapo huko Ncha ya Kaskazini na ndio wameua hao wanajeshi , hii inamaanisha Athena ameamua kwa asilimia mia moja kufufua moyo wa Gaia na anataka kupunguza joto la dunia kufikia kiwango ambacho binadamu atapotea katika uso wa dunia.”Aliongea Yezi.
“Haijalisihi itakuwaje lakini hakuna nchi ambayo ipo tayari kwasasa kutuma wanajeshi kwenda huko tena mara baada ya kilichotokea , ndio maana kitu pekee ambacho wanaona ni sahihi kufanya kwa wakati ni ujenzi wa Safina, inaeleweka kwani ndio tumaini pekee ambalo limebakia”Aliongea Edna.
“Hicho ndio nilichofikiria pia , ndio maana nimekuwa mzito kwenda huko ncha ya kaskazini na kuangalia kinachoendelea lakini kama kweli miungu ipo huko hata kama tuunganiishe nguvu zetu bado hatuwawezi na hatuwezi kubadilisha chochote zaidi ya kujitafutia matatizo tu”Aliongea Clark
“Tusiende huko jamani itakuwani hatari sana , nadhani mliona mara ya mwisho namna ambavyo Apollo na Artemis walivyokuwa na nguvu , Hubby pia amesema uwezo wao umeongezeka sana na unaendelea kuongezeka hivyo hatuwawei na kama hawatomchukulia Hubby kama mwenzao wanaweza kutua mara moja baada ya kutuona”Aliongea Rose.
“Tena Edna hivi wewe na Amina mliweza kupokea mwaliko wa kuwekeza katika projekti ya ujenzi wa Safina ya Nuhu, nyie si ndio mabilionea?”Aliuliza Nasra.
“Ndio lakini nimekataa, ukinilinganisha mimi na matajiri wengine wenye hela nyingi hela zangu hazina umuhimu mkubwa kwao , nadhani Amina anaweza kuwa katika orodha yao”
“Ndio walituletea mwaliko lakini baba alikataa na mimi pia nilikataa kwani niliona haina maana , Sister Neema wewe haujapokea mwaliko?”
“Hawajanipa mwaliko na hawawezi kufanya hivyo kwa namna yoyote ile”Aliongea Neema na jawabu lake liliwashangaza wengi.
“Unamaanisha nini kusema hivyo?”Aliuliza Dorisi kwa mshangao lakini kabla hajatoa jibu muda huo mvumo wa helicopter kutua karibu na nyuma yao iliwashitua wote.
Ilikuwa ni Chopa ya kifahari mno na watu ambao walikuwa na uhusiano na Roma ndio ambao walikuwa na uwezo wa kuingia kisiwani hapo bila kuzuiwa na wanajeshi hivyo haikuwapa hofu.
Sasa wakati wakiwa katika shauku ya kutaka kujua nani kafika kwenye chopa hio Clark alionekana ashajua ni nani.
“Naona wameleta mjumbe mwigine”Aliongea Clark na dakika hio hio mlango wa Chopa ulifunguliwa na akatoka mwanaume mtanashati, mzungu mwenye nywele zake nyeupe alievalia koti la kijeshi kubwa , alikuwa ni Edward Rothchild ambaye ni mrithi wa familia hio.
Ilionekana Ron na Brewester waliacha waingie baada ya kugundua ni Chopa yao.
Warembo hao ukimtoa Edna na Amina karibia wote hawakuwa wakimjua Edward na walishangaa mara baada ya Edna kuwatambulisha.
“Edward kama upo hapa kwa ajili ya kunishaawishi unapaswa kuondoka, nina uhakika unajua kwamba huwezi kunifanya niondoke hapa kwa lazima”Aliongea Clark moja kwa moja.
Edward alionyesha mshangao wake mara baada ya kuona kundi kubwa la wanawake , mara baada ya kusikia maneno ya Clark aliishia kutoa tabasamu na alionekana hakuwa na haraka ya kujibu na badala yake alimsogelea Edna na kumuinamia kwa namna ya kuonyesha heshima yake na baada ya hapo alisalimiana na wengine kawaida.
Haijalishi yupo katika hali gani lakini alipaswa kudumisha ustaarabu wa familia yake kama mrithi wa damu ya kifalme , hata kama ilimaanisha dunia imefikia mwisho.
“My dear Cousin , do you think I’m one who enjoys doing things in vain or one who is oblivious to your temper”
“Binamu yangu mpendwa hivi unadhani mimi ndio napenda kufanya vitu visivyofaa au sijali hasira zako”
Clark aliishia kusinyaza macho yake ya bluu na muonekano wa mshangao kati yao ulionekana.
Ingawa Edward alikuwa na akili lakini hakumfikia Clark hata kidogo , haikuhitajika kuuliza tayari amekwisha kujua mambo ambayo hayapo sawa kutoka katika maneno yake.
“Kwanini wafanye hivyo?”Aliulia Clark kwa hasira.
“You should’ve guessed this earlier, shouldn’t you ?, This isn’t a daydream where you can let your imaginations run wild , this is doomsday , the sign of human extinction , in order to survive they would do anything”Aliongea akimaanisha kwamba Clark alipaswa kuotea mapema kwani sio kama anaota ndoto na kumfanya impelekeshe , bali wakati huo ni wa mwisho , ishara ya kupotea kwa binadamu na ili kuendelea kuishi watafanya lolote.
“Wao !? , wewe si mmoja wao pia?”Aliongea Clark.
“Clark haijalishi unaniamini au lah , ila nasimamia msimamo wa kutokufungamana na pande zozote wa familia yetu , sijashiriki katika kupiga kura kuunga mkono”Aliongea.
Maongezi yao yaliwafanaya wengine wasielewe wanachomaanisha ni kitu gani.
“Clark mnaongea nini jamani , nini kuhusu kupiga kura?”Aliongea Mage na Clark alivuta pumzi kabla ya kuanza kueleea.
“Kwasababu ya uwepo wa jeshi la Sea Eagles kikosi cha Phantom hata kama NATO na Urusi washirikiane kushambulia hapa kisiwani ili kunilazimisha wataishia kupata hasara kubwa , isitoshe wengi wetu hapa tuna uwezo usio wa kawaida , hata bila ya uwepo wa Latina mkuu wa Dhehebu na wenzake itakuwa ngumu kwa mataifa haya makubwa kunilazimisha kuongoza ujenzi wa Safina , hivyo ujio wa Edward hapa kama mjumbe ni zaidi ya kunishawishi , lazima watakuwa na kete ya majadiliano ambayo kwa hakika lazima itanifanya nikubali kuwasaidia”
“Kete gani hio , sidhanni kama unakosa kitu , embu subiri au unataka kusema wamemteka malkia Catherine?”Aliuliza Mage kwa hamaki.
“Nisingekuwa na wasiwsi kama ni hivyo isitoshe hawana uwezo wa kufanya hivyo na hata kama wakifanya hivyo ninao uwezo wa kwenda kumuokoa”
“Kama sio hivyo kwanini inaonekana kama wana kitu cha kukutishia , tuna watu wengi hapa hata kama watatumia mabomu ya nyuklia uwezo wa kukimbia tunao na hatuna kitu cha kuogopa”Aliongea Mage akichochea.
“Binadamu..!!”Aliongea Edna kwa herufi kubwa utadhani yeye sio binadamu.
“Edna yupo sahihi , hawana haja ya kuumiza familia yangu au marafiki zangu ili niwasaidie , ijapokuwa NATO na Urusi so marafiki lakini wakiungana inamaanisha wanadhibiti asilimia tisini ya siraha zote za teknolojia ya juu ulimwenguni , kwa rasilimali hizo wanao uwezo wa kushambulia nchi ndogo kwa bomu la nyuklia na kuuwa watu wengi na wataendelea hivyo hivyo ili mradi nikubaliane nao”
“Wamekuwa vichaa , kwahio wanataka kutokujali maisha ya binadamu wengine kwa ajili ya wao kuishi?”
“Sio kama hawajali , kama mambo yakiendelea hivi masikini watageuka na kuwa barafu au kufa njaa na kila mtu atakuwa hana kinga tena ya kifo , kama wanao uwezo wa kumpata Clark kuwasaidia kujenga safina kwa mabadilishano ya uhai wa mabilioni ya watu basi wapo tayari kufanya lolote”Aliongea Edward
“Huo ni Udhalimu sasa , kama Clark akikataa inamaanisha wanakwenda kuuwa watu wasiokuwa na hatia””
“Hakuna cha maadili wala amani mbele ya kifo badala yake sheria ya msituni ndio inafanya kazi , wanapaswa kujilaumu wao kwa kuwa dhaifu katika mnyororo wa mfumo wa kimaisha ”Aliongea Edward.
“Clark inabidi uende tu , kama Roma angekuwepo angefanya maamuzi ya kuwaua hao washenzi lakini ni zaidi ya miezi miwili sasa hajulikani alipo na hakuna anaejua ni lini atajitokeza , wewe sio yeye na hakuna mtu yoyote hapa anaweza kupotezea uhai wa binadamu wengine kama yeye , haijalishi nini kitatokea baadae lakini hatuwezi kuona mamilionni ya taia kufa”Aliongea Edward na kumfanya Clark kuwa katika hali ya kimawazo.
Ukweli ni kwamba Edward ni mnafiki tu na kati ya watu ambao watakuwa wa kwanza kuingia kwenye safina hio pengine ni yeye wa kwanza ni aina ya watu ambao hawajali kabisa binadamu wengine.
“Basi sawa , ninaweza kukubaliana nao niwasaidie katika ujenzi wa safina lakini kwa sharti moja , katika wakati huo hawaruhusiwi kuteka maeneo ya joto hususani nchi za Afrika na kuuwa watu , kama nikijua nitua watu wote wanaotaka kuja kuingia katika hio safina”
Asilimia kubwa ya watu ambao walikuwa wakiishi katika mazingira ya joto walikuwa ni masikini , sasa ukichukua kile kinachoendelea, kimahesabu matajiri na nchi zenye nguvu ni swala la muda tu kuvamia nchi hizo na kuzitawala hata kuua baadhi ya watu ili kupata nafasi ya kuishi.
“Usijali tupo tayari kukubali sharti lako ili mradi utakuwa tayari kutusaidia”Aliongea Edward.
Baada ya kuona hakukuwa na namna ya kukataa ombi hilo ilibidi Clark aondoke na Edward kuelekea kwenye kambi ya jeshi la Marekani hatimae kupelekwa eneo ambalo Safina hio ilipasw akujengwa.
Unajua ni wapi inajengwa?


SEHEMU YA 761.
Weupe ulikuwa umetanda kwa kuelekea angani katika eneo la ncha ya Kaskazini lakini katika eneo la katikati kulikuwa na ardhi ya dhahabu.
Mti Mama(Mother Tree) ulikuwa umeongezeka ukubwa mara mbili ukilinganisha na miezi miwili iliopita na ulienea mamia ya kilomita ukifanuka anga na kuunda ulimwengu wa dhahabu uliojitokeza kusikojulikana.
Hera alikuwa amelala kwa muda mrefu sana katika moja ya tawi , macho yake aliyafumbua taratibu na alikaa kitako kwa namna ya kimapozi kabisa na kuanza kuweka nywele zake sawa.
Mara baada ya kuvuta hewa kiasi kikubwa , hewa iliokuwa imechanganyika na harufu ya mti mama alionyesha hali ya ridhiko.
“Harufu ya nyumbani inavutia sana kuliko kitu chochote kile”Aliongea mwenyewe na kisha kwa namna ya kupaa kama malaika alishuka chini ya kivuli cha mti huo kuwafuta wenzake maana tawi ambalo alikuwa amelalia lilikuwa limerefuka kwa kilomita nyingi.
Ukiachana na Ares na Aphrodite ambao walikuwa wakikaa chini ya mti huo , Hermes , Apollo , Artemis na Poseidon walikuwa wameongezeka pia.
Mara baada ya kumuona Hera ameshuka kutoka juu mtini miungu hao wote sita walisogea katika upande mmoja ili kumruhusu kuona kitu ambacho kilikuwa kimejitokeza katika moja wapo ya tawi.
Lilikuwa ni ua la dhahabu ambalo linaanza kuchomoza , ambalo lilikuwa likitoa mnunurisho wa nguvu za kimaajabu kama za kiroho hivi huku ua hilo likiwa kama kitenesi cha mwanga wa jua , lilionekana kuwa hai kwa namna ambavyo lilikuwa limezungukwa na majani.
Hali ya furaha ilikuwa ikionekana katika uso wa Hera lakini ile ambayo haijazidi.
“Its finally .. born”Aliongea Hera akimaansiha kwamba hatimae imezaliwa.
Ijapokuwa wenzake walikuwa na muonekano usio kuwa wa kawaida lakini pia walionekana kuwa na furaha.
Katika wakati huo kila mmoja alionekana kufurahia kwa namna yake.
“This is first flower bud , I believe more will appear on Mother Tree in no tme , we we will then gain a new life”Aliongea Aphrodite huku akionyesha tabasamu akimaanisha kwamba hilo ni ua la kwanza kutokea na anaamini mengi yatatokea katika Mti Mama huo muda wowote na hatimae wataweza kupata maisha mapya.
Mara baada ya kufikiria kitu Hera aliita nguvu zake za kijini na palepale maandiko ya bluu yalionekana katika hewa kama holograph vile mara baada tu ya kuchezesha vidole vyake , ilikuwa ni mbinu ya kufanya ‘deduction’ kwa kutumia nguvu za mbingu na ardhi.
“Nyie watu mlikuwa mkifanya kazi kubwa wakati nilipokuwa nimelala .. naona mmeharibu meli nyngi za kivita na kuuwa wanajeshi”Aliongea huku akionyesha tabasamu la dharau.
“Itakuwa ni matatizo tu kama tutaruhusu binadamu kusogelea Mti wetu wa uzao, kuwa wakatili ndio njia pekee ya kuwazuia kutokutusumbua”Aliongea Ares.
“Haha.. humans are creating the so called Noah Ark .. what a bunch of stubborn low live “Hera alicheka kwa dharau kubwa na kumfanya Aphrodite kumwangalia na macho ya huzuni.
“Sijategemea kuona mbinu yako ya kuangalia matukio yaliopita na ya mbele kuwa sahihi namna hio , kwanini usijaribu kuangalia ni wakati gani Athena atafika hapa , nina uhakika lazima atakuwa na hamu ya kuona chipuo katika Mti Mama”Aliongea Aphrodite.
“Nitatumia tu nguvu zangu nyingi kujua nyendo zake na isitoshte naweza kukosea pia” Hera alikataa.
“Naona hatimae unakubali utofauti uliopo kati yako na yeye , Hera usijali muda si mrefu tunakwenda kuamka tena na mchango wa Athena hauwezi kupotezewa , ijapokuwa anaweza akawa ameenda mbali kwa baadhi ya vitu lakini amefanya yote kwa ajili yetu , huoni furaha kuona dalili ya kuchipuka kwa ua , hii inamaanisha kwamba sisi wote ni sawa , tofauti na kushindana na Athena kwanini usitumie mawazo yako katika kufikiria neema ya utukufu wetu ujao”Aliongea Apollo na Hera aliishia kupindisha midomo tu ikiwa ngumu kujua kama alikuwa akikubaliana na maneno yake.
“Kama tungepata moyo wa Gaia miaka ile wakati tunakuja duniani na kuufufua mapema mambo yangekuwa tofauti sasa hivi”
“Nani angejua uwepo wa kundi lile la mashetani kati ya kiumbe dhaifu kama binadamu na kuharibu mipango yetu”Aliongea Hera.
“Hebu kwanza ongeeni mambo yajayo , hivi mnadhani Hades akirudi atakuja kuwa rafiki yetu au adui yetu?”Aliuliza Hermes na kufanya kama wote kuwaza kitu.
“Hades?, tena nini kimemtokea huko kwenye ulimwengu wa majini?”
“Hatujajua ni nini kimetokea mpaka wakati huu , wewe si unambinu yako ya kujua yaliopita na yanayoenda kutokea , kwanini usitumie kujua yupo wapi”Aliulia Aphrodite.
Hera hakufikiria sana kuhisi hilo na wala hakuongea lakini matokeo yalimfanya sura yake kujikunja.
“Nini tatizo?, Hades yupo katika hatari?”Aliuliza Artemis akiwa katika hali ya wasiwasi.
Lakini palepale muonekano wake ulibadilika na aliishia kulamba lipsi zake na kukaa kimya.
“Yupo katika ulimwengu wa jicho la Anga”Sauti ya tofauti ilisikika.
Miungu wote walishangazwa na sauti hio kabla ya kugeuza sura zao zote kuelekea upande sauti ilikotokea.
Mwanamke aliekuwa katika umbo la kirembo aliweza kuoenekana katika hewa , alikuwa ni Athena ambaye alikuwa amevalia gauni flani hivi kama vile anatokea katika tamaduni za Roma ya kale , ni vazi ambalo lilikuwa limemuacha wazi shingo yake ambayo ilioneknaa ni dhahiri hakuwa mzungu wala mtu mweusi , sura yake haikuonekana na ndani ya sekunde tu aliijitokeza mbele ya miungu wenzake.
Hakuna ambaye alikuwa na uwezo wa kuongea chochote kwani akili zao ni kama vile amezishikilia.
Kama ilivyokuwa imetarajiwa , uwezo wake ulikuwa umeongezeka kwa kiasi kikubwa mno kiasi kwamba iliwashangaza mno , ijapokuwa walikuwa wakimjua Athena tokea katika sayari yao kuwa na nguvu kubwa ilikuwa ni muda mrefu kwa mungu huyo wa vita kuwa na uwezo wa namna hio katika mazingira ya dunia.
“Hata kama usingejibu najua yupo katika anga lingine , haina haja ya kujifanyisha unajua kila kitu”Aliongea Hera.
Miungu wenzake walijua kabisa Hera hakuwa akitaka kuonekana mnyonge mbele ya Athena lakini mbinu ya Athena kujua yajayo na yaliopita ilikuwa ina nguvu mno na sahihi zaidi kuliko hata ya Hera.
“Ili mradi hunichokozi tena na kujifanyisha ni mimi nitajizuia kutokuingilia mambo yako”Aliongea Athena ambaye haijulikani yupo katika sura ya nani.
Alichokuwa akimaanisha ni kwamba alikuwa akijua ni kipi ambacho Hera alikuwa akifanya katika kipindi chote na amechagua kutokumchukulia hatua.
Ndio katika wakati mrefu sana Hera alikuwa akijifanyisha ndio Athena na matukio mengi alikuwa amefanya kwa kujifanyisha ni Athena.
“Acha kujiona kijogoo , hili halijafika mwisho bado hata kama unabii wako unaweza kuwa sahihi kwa asilimia tisini na tisa kuna asilimia moja kila kitu kikabadilika kama ilivyotutokea katika sayari yetu kuamini kwamba tupo salama kwa asilimia tisini na nane lakini asilimia mbili tu zikatufikisha hapa duniani na kuishi kwenye miili dhaifu ya viumbe binadamu”Aliongea Hera kwa jazba lakini Athena alionekana kutokumzingatia kabisa na hatua moja tu alikuwa ashafikia katika tawi ambalo kuna chipuko la ua linaloanza.
Kwa hali ya upole sana alinyoosha mkono wake na kwenda karibu na ua lile kama vile alikuwa akisikilizia uhai uliokuwa ndani yake.
Miungu hao walikuwa kimya na ilikuwa ni kama vile wanahisi kuna nafsi nyingine katika akili zao licha ya kwamba Athena alionekana kuwa katika hali ya utulivu.
“Athena ni lini utaenda kumtafuta Zeus?”Aliuliza Poseidon mara baada ya kimya kifupi.
“Haina haja, atajitokeza mwenyewe muda si mrefu”Alijibu Athena.
“Nini!?”
“Anachomaanisha ni kwamba Zeus huko alipo na yeye uwezo wake utakuwa umerudi na ataweza kujitoa katika gereza la safu ya majini”Aliongea Hermes.
“Miaka elfu ishirini iliopita mimi na yeye uwezo wetu ulishuka mpaka kufikia asilimia therathini , sheria za ki ulinzi ambazo zipo katika safu ya ulinzi wa gereza la majini hao ni kali mno na kunifanya kushindwa kufanya unabii wa lini atatoka au ni nguvu kiasi gani zimemrudia , lakini ndani ya miezi sita ijayo uwezo wetu utarudi kwa asilimia mia moja na mpaka wakati huo itakuwa ni rahisi kutoroka , ukweli ni kwamba ninakwenda kulipa kisasi kwa wale wote waliokula njama mpaka kutufanya kupitia mateso yale”Aliongea Athena akiwa siriasi.
“Inafurahisha, lakini wewe na Zeus je mtaweza kumshinda yule binadamu mwenye nguvu za kijini wa wakati ule hata kama mtaunganisha nguvu zenu , kama ni hivyo kwanini ukaamua kumtengeneza Hades mpya kuwa nusu binadamu nusu sisi na kumfanya afuate ramani ya mipango yako?”Aliuliza Hera.
Mara baada ya kusikia kauli hio wengine wote walishangazwa na swali la Hera lakini Athena alibakia kuwa kimya tu bila ya kujibu na aliangalia mmoja mmoja.
“Sio lazima ujue kila kitu”Aliongea.
“Hehe..Au ni kwasababu hata wewe hujui kinachoendelea , mpaka sasa mambo yamefikia hatua hii hivyo moja kwa moja kila kitu kitakuwa kinaendelea kama ilivyotabiriwa na hakuna unachoweza kufanya kwasasa kubadilisha ukweli , unajaribu kuepuka hii topiki kwasababu wewe mwenyewe ndio unajua mwanzo ulivyo na mwisho ulivyo , Kesho ya Hades mpaka sasa haifahamiki na kulingana na mbinu yangu ya unabii wa kinajimu na hata pia Almanaki ya Hades wa zamani hatima yake mpaka sasa haitafsiriki , haijalishi una nguvu kiasi gani katika kufanya unabii wa mambo yajayo ila haupo mbali sana na mimi wala Hades wa mwenzetu”
Katika kauli ya kichokozi ya Hera , Athena alionekana kutokujali kabisa kuongea zaidi na mara baada ya kumwangalia kwa kejeli alipiga hatua mbili tu na kisha akapotea.
Mara baada ya kuona Athena ameondoka bila kujibu maswali yake mrembo huyo mwenye nguvu za kijini alijikuta akifubaa huku aking’ata meno yake kwa hasira.
“Bit*ch , ninachukia tabia yake ya kutokuchukulia wengine siriasi”
“Hera mmejuana na Athena kwa miaka mingi sana na unaijua tabia yake ilivyo ,wewe ndio unamfanya aonekane kuwa na nguvu kuliko sisi,kwanini unalazimisha akuambie kila kitu ilihali hayupo tayari ,tena kwa tabia hio unayoionyesha mbele yake”
“Kuna tatizo gani na tabia yangu , mimi sio kama nyie viumbe waoga waoga , kinachotokea hapa si kuzaliwa upya kwa nguvu ya Gaia , kwa namna yoyote ile hiki sio kitu cha kujivunia ni kitu cha kuumiza ambacho hatupaswi kufanya, kuna haja gani ya kuona anajua zaidi ya sisi , yaani mnataka tujishushe kwa kila kiutu kwasbaabu tu kafanikisha kufufua moyo wa Gaia kitu ambacho hata mimi ningeweza?”
Hera alionekana kukasirika mno na mara baada ya kuwaangalia wenzake kwa macho makali na yeye alipotea ikionekana kabisa anatafuta mahali pa kupunguzia hasira zake.
Baada ya kuwaacha wenzake nyuma walionekana kuwa na wasiwasi mno hususani juu ya Hades ambaye ilionekana hata Athena mwenyewe hakujua hatima yake ni ipi.
Unadhani hatima ya Roma ni ipi , je atachukua maamuzi gani.













SEHEMU YA 763.
Upande wa ulimwengu wa jicho la Anga mara baada ya Roma kukaribishwa na Uramu Hantu kwenda katika makazi yao kwa ajili ya hifadhi alionyesha hali ya kusita sita hususani namna mazingira yalivyo aliona pengine anajiingiza kwenye mtego.
Lakini Uramu Hantu alimtoa hofu na kumwambia Roma kwamba hana haja ya kuogopa kwani tayari anamiliki Dhana ya Cauldron , na ilionekana ni sahihi kwani Uramu Hantu alionekana kuihofia sana ile Dhana.
Roma mara baada ya kujihakikishia hana cha kugopa aliamua kumchukua Xiao na kuongozana nae kuelekea katika makazi yao.
Mwanzoni Xiao alikuwa katika hali ya uoga juu ya viumbe hao lakini hakuogopa tena kisi cha kumshangaza Roma , pengine aliona ni kwasababu ya uwepo wake.
Iliwachukua kilomita mia moja tu ya kumfuata Uramu Hantu na hatimae waliweza kufika mwisho wa safari na kuchipukia katika ardhi ambayo haikuwa na kitu kabisa , Roma alishangaa na kujiuliza hayo makazi yao yapo wapi mbona hayaonekani. Lakini mara baada ya Uramu Hantu kufanya mazingara ya kimaajabu palepale vitu kama moto vilimtoka katika macho yake na maneno flani ya herufi yalionekana na ilikuwa ni kufumba na kufumbua ardhi ilikuwa ni kama vile inatetemeka na palepale kulitokea mpasuko wa ardhi na kutengeneza shimo kwa kutenganisha pande mbili.
Roma alishangazwa na jambo lile hasa pale ambapo aliweza kuhisi nguvu hasi nyingi zikitoka katika ufa huo lakini hakuweza kuona chochote kilichokuwa chini yake kwani kulikuwa ni giza totoro.
“Nifuateni wageni”Aliongea Hantu na palepale yeye akitangulizana na watu wake wakijirusha katika ufa huo wa shimo na kupotelea chini lakini Roma mara baada ya yeye kutaka kuruka Xiao alimshikilia mkono huku akionyesha hali ya wasiwasi kwa kutetemeka.
“Nini tatizo?”
“Hio sehemu inaonekana kuogopesha”
“Wewe sio ndio ulionyesha hamu ya kuja , unaogopa nini sasa?”AliongeaRoma.
“Lakini sikujua kutakuwa kunaogopesha hivi , nilijua tunaenda kuingia kwenye ngome ya kifalme ila sio kwenye shimo la giza kama hivi”Aliongea Xiao kwa kulalamika na ilimfanya Roma kuona ni kama vile anajibizana na binti yake wa kumzaa.
“Acha kufikiria sana na twende ndani”Aliongea Roma na palepale alimshikilia Xiao na kisha akajirusha nae kwenda chini.
Ni ndani ya sekunde tu kwa nje ule ufa ulijiziba kabisa na hakukuonyesha dalili kama kulikuwa na shimo ambalo watu wameingia ndani.
Kadri walivyokuwa wakienda chini ndio namna ambavyo nguvu hasi ilikuwa ikiongezeka kiasi cha kumfanya Xiao kuzidi kutetemeka , kwake ilikuwa ni kama vile alikuwa kwenye ndoto kadri alivyokuwa akizidi kwenda chini lakini kutokana na uwezo wake wa nguvu ya mbingu na ardhi ilimfanya kushuka kama vile yupo kwenye lift.
Xiao hakuwa katika levo ya kuipita Dhiki bado hivyo uwezo wake wa kuhimili nguvu za giza ulikuwa mdogo na ilimfanya kuwa kama binadamu wa kawaida kutokana na mapigo yake ya moto yalivyokuwa yakienda kasi lakni kwa Roma alikuwa na utulivu na Roma aligundua namna ambavyo msichana huyo alivyokuwa mdhaifu mbele ya nguvu hizo na palepale ilikuwa ni kama anamvalisha koti ambalo limemziba mwili mzima na kuwa ngao yake.
Xiao alijihisi joto la ajabu na hata ile hofu aliokuwa nayo ilipotea sasa na kutokana na kufanyiwa hivyo na Roma moyo wake ulijiambia lazima Roma atakuwa anampenda sana , lakini ukweli upande wa Roma sio kwamba alikuwa akimchukia Xiao kutokana na tabia ya baba yake,alikuwa akimuonea huruma na alijiambia lazima amtoe katika ulimwengu huo kwa namna yoyote ile.
Mara baada ya kushuka futi elfu moja kwenda chini katika giza totoro hatimae mwanga ulianza kuonekana katika macho yao , ilikuwa ni eneo la kushangaa na hata kwa mtu kama Roma ambaye amezoea kuona vitu vya kiajabu ajabu alipigwa na mshangao.
iIikuwa ni nafasi kubwa chini ya ardhi ambayo ilikuwa kubwa mno kwa zadii ya kilomita za mraba kwa upana wake na mamia ya mita kwenda juu, ni sehemu ambayo ilikuwa ngumu kusema ni pango bali ni sawa na kusema ni ulimwengu chini ya ardhi.
Katika kuta za eneo hilo kulikuwa na mawe ya ajabu kama madini hivi ambayo yalikuwa yakitoa mwanga wa ajabu ambao ulifanya eneo hilo kuwa na uangavu wa rangi ya bluu.
Ulimwengu wa Bluu ndio labda neno sahihi ya kuita eneo hilo, ilikuwa ni kama underground Bunker.
Sasa mbele yao kulikuwa na jengo katikati ya eneo hilo ambalo usanifu wake ni ngumu kusema ni Ngome ila kwa haraka haraka ungesema ni eneo la makazi na kutokana na ukubwa wake ungesema ni makazi ya kifalme au ya kiongozi.
“Hakuna haja ya kushangaa Braza mdogo Roma , kama nilivyokwisha kusema mwanzo kila mara ufa unapojitokeza nishati chanya huongezeka maradufu na kupelekea nishati hasi kuongezeka , tuliwea kujenga hii kambi yetu kwasababu mbili , kwanza kuweza kuendelea kuvuna nguvu za giza kwa amani na pili kujilinda sisi wenyewe kutoka kwa nishati chanya na zaidi ya yote ni sehemu inayotusaidia kuepukana na wavamizi”Aliongea.
Nishati hasi ni nguvu za giza na nishati chanya ni nguvu za nuru sasa katika dunia nguvu za giza na nguvu za nuru zipo katika usawa au uwiano lakini siku zote nguvu ya nuru ina nguvu kuliko ile ya giza.
Uramu Hantu alikuwa ashajua umri wa Roma hivyo katika kuongea nae alikuwa na utulivu , ijapokuwa alikuwa na umri mdogo lakini kutokana na uwezo wake aliamua kumuita Braza au kaka.
Baada ya kuongea maneno machache alimchukua Roma na Xiao mpaka kwenye jengo hilo na mara baada ya kuingia ndani Roma alishangazwa kwani kulikuwa na majini roho wengi sana ,mizimu na mapepo na wote walikuwa na akili kama ilivyokuwa kwa Uramu.
Kulingana na Uramu ulimwengu huo wa jicho la anga umetawaliwa na mizimu ya roho za majini pepo jamii ya mashetani miaka mingi iliopita kabla ya kufa na kupoteza miili.
Sasa kutokana na kwamba uwezo wao ni kama unalingana baina yao na wamekwama katika ulimwengu huo, Ma’Uramu wote hawakupigana wao kwa wao na kila mmoja alikuwa katika makazi yake wakiishi pamoja kwa amani.
Sasa ijapokuwa roho za majini pepo wanaweza kuzalisha kiasi cha nguvu hasi lakini hawakuwa na manufaa makubwa na inasemekana kila Uramu ana miliki mizimu ya majini roho wa kishetani zaidi ya elfu moja ambao wapo chini yake na ni wachache sana ambao walikuwa na akili.
Hivyo licha ya kwamba walikuwa wengi lakini ngome hio ilikuwa kubwa sana kutokana na kwamba hawana miili hivyo kwa mtu wa kawaida ungeingia hapo ndani ungeona labda ni ngome ambayo ilikuwa haikaliwi na mtu kwa macho ya kibinadamu lakini Roma na Xiao walikuwa na uwezo wa kuona roho hizo na mapepo hayo.
Sasa Roma kwasababu alikuwa akitaka kujua kuhusu ulimwengu huo na pia hakuwa na pakwenda aliona akae hapo na viumbe hao wa kutisha kwa siku kadhaa, siku kadhaa ambazo ziligeuka na kuwa zaidi ya miezi.
*****
Ni miezi kadhaa sasa Roma wakati akiwa amejikalisha juu ya paa la ngome akiangalia ulimwengu huo wa chini ya ardhi ambao ulikuwa umetanuka kwa kilomita kadhaa , ulimwengu ambao alikuja kugundua ulikuwa chini ya Mfalme Nether au Uramu Hantu.
Ukweli ni kwamba hakuna mfalme katika eneo hilo bali ni Uramu pekee sasa , Xiao ndio aliamua kumbatiza Uramu Hantu na kumuita Mfalme Nether(Tutamke Neza) yaani mfalme wa kuzimu
Roma kwa mahesabu ya haraka haraka alijua lazima ametumia zaidi ya miezi miwili .
Katika moyo wa Roma alizidi kuona wasiwasi , mawazo yake ni kile ambacho kilikuwa kimeitokea familia yake , ijapokuwa Latina na wengine walikuwa wameahidi kumlinda mke wake na binti yake lakini Roma alijiambia kama hatorudi nyumbani mapema basi hatoweza kupata taarifa yoyote ya kinachoendelea na majini hao jamii ya Mbweha wanaweza kujikatia tamaa na kurudi kwenye ulimwengu wao.
Katika kipindi chote Roma alichokuwa akiishi chini ya ardhi aliweza kufahamina na zaidi ya Ma’uramu kumi na mbili wa ulimwengu huo wa jicho la anga.
Isitoshe ilikuwa ni ngumu kwa Uramu hao kutoshindwa kushituka ilihali binadamu ameweza kuonekana kaitka ulimwengu wao , tena binadamu ambaye alikuwa akimiliki Dhana ya kilijendi ya Chaos Cauldron ambayo ilikuwa ikijilisha nguvu za giza kila sekunde.
Karibia ma’uramu wote walikuwa si chini ya levo ya kuipita dhiki ya radi ya mapigo tisini na tisa na kuna ambao walikuwa mpaka juu ya mapigo elfu moja lakini licha ya hivyo kutokana na kwamba walikuwa katika maumbo ya kiroho tu hawakuwa na uwezo wa kutumia nguvu ao zote.
Kwa mfano ukimjulisha Mfalme Neza(Uramu Hantu) ambae ndio wa kwanza Roma kumjua lakini pia aliweza kufahamiana na Uramu Haku , Uramu Ngeki mkuu wa jumba na wengineo ambao Roma alikuwa na mazoea nao.
Kama ilivyokuwa kwa mfalme Neza hao ma’uramu hawakuwa na uadui na Roma.
Kitu kingine ambacho kiliwafanya majini hao roho na pepo kumpigia Roma magoti ni mara baada ya kuonyesha uwezo wake wa kutengeneza radi ya mapigo tisini na tisa.
Kutokana na uhatari wa Roma walimchukulia yeye na Xiao kama vile ni wageni wao wa VIP na wengi wao walimhonga Roma madini pamoja na baadhi ya Dhana za kijini pamoja na nyenzo kwa ajili tu ya kupata taarifa juu ya ulimwengu wa nje.
Kwa lugha nyepesi ilionekana jicho la anga kama kuzimu ya majini pepo hao , zilikuwa ni roho ambazo zimefungiwa ndani ya ulimwengu huo na hawakuwa na namna ya kutoka na kama zingeweza kutoka moja kwa moja pengine binadamu wangepata shida sana kwani zingetaka kutawala miili yao.
Sasa Roma alichoka sana katika siku zote hizo kwani ni kama alikesha kuelezea habari nyingi sana kuhusu majini na majini pepo na viumbe hao walitaka kusikia vitu vingi na kujifunza.
Lakini kwasababu walikuja na hongo Roma alipokea tu na kisha kujibu maswali yao , katika hatua hio Roma aliweza kupata Dhana nyingi sana zenye nguvu na kati ya Dhana ambazo aliweza kupata ni Shoka la kimaajabu ambalo liliitwa Pangu, lilikuwa Shoka kubwa mno na zito.
Roma wakati mizimu hao wanaelezea kuhusu uwezo wa Shoka hilo alikuwa haamini kabisa katika uwezo wake lakini mara baada ya kujaribu uwezo wake ulimshangaza sana haikuwa Dhana yenye nguvu kushinda Cauldron lakini ilikuwa na faida zake za kipekee sana.
Ilionekana kuwa Dhana ya kipekee sana ambayo uwezo wake sio kwa ajili ya kushambulia tu lakini ni kwa ajili ya kupasua anga , yaani kwa mfano ikitokea Roma anashindana na na miungu anao uwezo wa kupasua mashambulizi yao ya kikanuni kwa kutumia Shoka hilo.
Hio Dhana ni moja ya vitu vya thamani sana ambavyo Roma aliweza kupata katika ulimwengu huo wa jicho la anga .
Sasa majini roho hao waliweza kumpatia Roma Dhana hio kutokana na kwamba hazikuwa na matumizi kwao kwani walikuwa katika maumbo ya kiroho , hawakuwa na miili kwamba wanaweza kushika Dhana hizo na kushambulia.
Ukiachana na kujibu maswali pamoja na kukusanya Dhana mbalimbali Roma alikuwa amefanya utafiti wa kutosha katika ulimwengu huo na kutafuta namna ya kutoka akiwa yeye na Xiao lakini bado hawakufanikiwa.
Na muda ambao walikuwa amekaa juu ya jengo la kifalme la mfalme Nether alikuwa ndio ametoka katika ulimwengu huo wa shimo na kwenda nje kutafuta njia ya kurudi lakini hakuweza kupata namna ndio maana alikumbwa na hali ya kimawazo.
“Roma Mjomba Neza anakuita , ana kitu anataka kuongea na wewe”Aliongea Xiao ambaye alipaa mpaka kufika alipo Roma.
Xiao mwenyewe ndio aliamua kumuita mfalme huyo wa mapepo na roho kwa jina la Mjomba Neza yaani ilikuwa balaa tupu tokea woga umwishie
Roma mwenyewe alikuwa amejichokea na tabia ya Xiao kwani kila kitu kwake alikuwa akirahisisha , alikuja muda mfupi lakini kwa wakati huo alikuwa ni kama vile amezaliwa ndani ya eneo hilo kwani alikuwa ashajitafutia na marafiki kabisa., kwa mfano kuna mizimu aliokuwa akiita Babu Haku , kuna mjomba ake mwingine alikuwa akimwita Kwato kutokana na ubaya wake , na akajipatia na dada kabisa aliemua kumwita jina la Dada Yode.
“Wanataka nini tena , si muda si mfupi nilikuwa nikiwajibu maswali yao na wamesema wameridhika”Aliongea Roma akionyesha hali ya kukasirika kutokana na stress.
“Sio kwamba wanataka kukuuliza amswali tena juu ya ulimwengu wa biandamu bali wanataka kuongea na wewe kitu muhimu sana kuhusu ulimwengu wa jicho la Anga , kitu ambacho kinaweza kutusaidia kutoka”Aliongea
Mara baada ya Roma kusikia kauli hio haraka sana nguvu zake zilimrudia na aliruka na kuja kutua katika baraza la jumba hilo akiwa na xiao.
Katika baraza hilo la kifame kulikuwa na mizimu , mapepo na mizuka yenye vyeo vya uramu zaidi ya kumi na tano na wote walikuwa wakielea angani katika mkusanyiko wakionekana kujadiliana kitu.
“Braza mdogo Roma kuna kitu tumekumbuka na tulitaka kukuelezea”Aliongea Mfalme Neza huku akiwa ni mwenye kucheka.
“Xiao kasema ni kitu ambacho kinaweza kututoa katika huu ulimwengu na kurudi , tafadhali nendeni moja kwa moja kwenye topiki”
“Hahaha..Braza mdogo Roma naona umekosa uvumilivu sasa au unataka kuendelea kubakia hapa kwa miezi kadhaa”Aliongea Ngeka.
“Kama hakuna kinachoweza kunitoa kwasasa , sidhani kama nitakuwa na haraka ya kuondoka ni kwamba tu wasiwasi wangu ni kwa familia , kama watapatwa na tatizo sitoweza kuhimili”Aliongea Roma akiwa na tabasamu lililojaa wasiwasi.
“Ukweli ni kwamba tunaweza tusikusaidie sana lakini kesho tunaenda Shimoni kwa ajili ya kuvuna nguvu za giza , hivyo tunauliza kama mtaongozana na sisi”
“Shimoni , ndio wapi huko?”Aliuliza Roma kwa mshangao kwani alikuwa ametafuta kila kona katika ulimwengu huo lakini alishindwa kuona kitu kama shimo.
“Braza mdogo Roma usiwe na wasiwasi , hebu msikilize mfalme na atakuelezea taratibu”Aliongea Yode.
Alikuwa ni jijni mzimu wa kike na alipenda kuongea mno na ndio aliekuwa akitawala maongezi katika kila kikao.
Roma ilibidi asikilize kwa umakini wanachotaka kumwambia na alikuja kujua kwamba katika ulimwengu huo wa jicho la anga kuna sehemu hutengeneza shimo kubwa sana kila baada ya miezi mitatu katika eneo hilo hilo.
Shimo hilo linasemekana kwamba halina mwisho na sio pana sana pia lakini kikawaida lina upana wa futi kama nane hivi.
Wanasema kwamba ndani ya shimo hilo kuna nguvu ya giza inatoka kwa kasi sana kila linapojifungua na mizimu hao sasa walikuwa wakienda kukaa karibu ya hilo shimo na kuvuna nguvu hizo za giza.
Shimo hilo hufunguka kwa siku moja tu tena wakati wa mchana na hio mizuka ya majini pepo itacheza ngoma hapo kwa muda mefu kama mbinu ya kunyonya hizo nguvu mpaka litakapojifunga.
Lakini sasa wanasema kwamba haikuwahi kutokea kwa roho yoyote ambayo iliweza kuingia katika shimo hilo , ijapokuwa ndani zaidi kulikuwa na nguvu za giza kubwa lakini kwao ni kama vile binadamu unavyoipenda bahari utaipenda katika maeneo yasio na kina kirefu tu kwa kuogelea lakini hutopenda kwenda katika kina kirefu na kuzama ndani .
Wanasema sio kama hawakujaribu , mmoja wapo alijaribu kwenda ndani ya shimo hilo kwa ajili ya kujua nini kipo ndani lakini alirudishwa juu kwa kutemwa kama vile kafyatuliwa na bomu na kupoteza fahamu.
“Hatukukuelezea kuhusu uwepo wa hili shimo kwasababu nguvu inayotoka hapo ni ya giza na haiwezi kuwa na uhusiano na ulimwengu wa binadamu , tunaamini kwamba ni shimo ambalo linakusanya pepo kutoka chini na kuwaleta katika ulimwengu wetu kwa kipindi maalumu na ndio maana hulipuka”
Yaani wanachoamini ni kwamba kila linapofunguka na kulipuka kama volkano shimo hilo hutema roho , mapepo na mizimu ya majini waliokufa.
Roma alisikiliza kwa umakini lakini alijikuta akijikatia tamaa kiasi , kwani haikujalisha namna alivyosikia lakini alijua pengine ni muundo wa tabia asili ya ulimwengu huo kama uwepo wa mapango makubwa katika ulimwengu wa binadamu ndio hivyo hivyo katika ulimwengu huo kuwa na shimo la namna hio.
Lakini kutokana na Roma kuwa na shauku ya kuona shimo hilo aliona akubali kwenda na mapepo hayo kujionea mwenyewe.
Baada ya kukubaliana mizuka hio ilitaka sasa Roma aendeleze stori a ulimwengu wa nje na Roma hakukataa aliwaelezea kulingana na maswali yao.
Siku saba mbeleni Roma alimchukua Xiao na kuungana na mizuka hio pamoja na mapepo na kuelekea Shimoni.
Xiao alikuwa karibu na Roma sana sana ,ijapokuwa woga ulikuwa umeumuishia lakini aliamini kama asingekaa na Roma karibu huenda angeweza kutoweka kimuujiza na kisha kumuacha ndio maana alikuwa amemganda sana.
Katika siku zote hizo lile jiwe la hazina ya mzee Sharif ya majjini kutoka braki halikuwa limeonyesa dalili yoyote ya uhai.
Roma alisafiri huku akichunguza mzingira na kitu ambacho kilikuwa kikimshangaza Roma ni uchafu wa eneo hilo kwani ni kama vile ni jalala na kama kuna watu wanaokuja kutema takataka hapo , ilifanya baadhi ya maeneo kuwa kama vile ardhi yake ni mbolea lakini hakukuwa na dalili yoyote ya kuota kwa mmea.
Anga halikuwa kama la dunia na ilikuwa ni kama vile anga lote limefukwa na wingu na kuonyesha dalili ya mvua ndio namna ulimwengu huo uliyokuwa ukioneakna nyakati za mchana, hakukuwa na chanzo cha jua lakini ajabu pia hakukuwa na baridi wala upepo , ilikuwa ni kama vile ni sayari ya Mars.
Xiao na Roma ukaribu wao ulikuwa umeongezeka sana kwa kipindi chote walichokuwa pamoja, ukweli ni kwamba walikuwa wakilala eneo moja , ijapokuwa hawakuwa wapenzi , Roma alimchukulia Xiao kama mdogo wake tu lakini kwa Xiao mambo yalikuwa tofauti , alikuwa akimpenda sana Roma kimapenzi na alijua pia Roma alikuwa akimpenda ila anamficha ndio maana hakuwa akikataa kukaa nae karibu na kumkumbatia usiku ili kumlinda na nafsi za mizimu wabaya.
“Braza mdogo Roma unachokiona chini yako ndio eneo shimo linapofunguka na hicho kimbunga kama upepo inamanisha muda wowote litafungika”Aliongea Neza.
Dakika hio hio ilikuwa ni kama vile kuna tetemeko kubwa la ardhi linatokea kwa chini kiasi kwamba ardhi yote ni kama vile inataka kudondoka na kadri muda ulivyokuwa ukisogea ufa ulikuwa ukionekana katika eneo moja ukiongezeka taratibu taratibu.
Ilikuwa ni kama vile Mungu anatumia upanga kuchimba shimo kwenda chini ardhini .
BOOM!!”
Ilikuwa kama vile ni Volkano inavyolipuka katika eneo lile kulitokea mlipuko wa aina hio na kurusha mchanga hewani kwa umbali mrefu sana na kutengeneza moshi mweusi tii kiasi kwamba ulifanya eneo lote kuwa giza.
Roma aliweza kuhisi uwepo wa nguvu ya giza iliolipuka kutokea katika shimo hilo ilikuwa mara tatu zaidi ya kawaida na kwa haraka sana alikuwa ameshamzingira Xiao na nguvu zake za kijini ili asije kuathirika kiroho.
Kwake licha ya kwamba mlipuko huo ulikuwa na nguvu kubwa ya giza lakini haukuwa na madhara hata kidogo.
“Haha.. Braza Mdogo Roma wewe kaa kwanza hapa utusubiri sisi twende tukanyonye nguvu za giza kwanza, usije ukasahau ile stori ya jana ulioishia katikati juu ya vita ya falme tatu”Aliongea Haku jini mzimu na aliruka na uramu wenzake kwenda chini.
Muda huo huo Roma aliweza kujulishwa katika akili yake na nafsi ya Chaos Cauldron kuomba ruhusa ya kunyonya nguvu hizo za giza , lakini Roma hakutaka kuuhuusu , ijapokuwa alijua nguvu hio ya giza ni chakula cha chaos huyo lakini kulikuwa na nafsi za kishetani katika nguvu hizo hivyo Roma alipotezea ombi la chaos.
Lakini sasa kitendo tu cha kuzima ombi la Chaos palepale ile kokoto ya kihazina ilipata uhai kwa mara nyingine na kumfanya Roma kushituka kwani alikuwa ametumia sayansi ya kila namna kujaribu kulirudisha uhai ili kumrudisha duniani katika miezi miwili mfufuluzo lakini halikuamka.
Roma hakutaka kuchezewa na kitu hicho tena na palepale alimshika Xiao na mkono moja na kisha alisubiri ile kokoto ijitoe yenyewe katika hifadhi yake na sekunde chache tu ilifyatuka uelekeo wa lile shimo na mkono wa Roma ulikuwa mwepesi mno kwani aliidaka ile hazina na kuikamatia kwenye mkono wake.
Ilikuwa ikipambana kujitoa katika mkono wa Roma lakini hata hivyo Roma hakuweza kuona nguvu yoyote inayotoka kwenye jiwe hilo , ilikwua ni kama vile kitu ambacho kinavutwa na sumaku lakini hakina nguvu yoyote.
Roma alishangazwa na jambo hilo , kwani awamu hio sio kama alikuwa akivutwa tena kama ilivyomtokea kwenye ulimwengu wa majini , lakini kitu hicho kilionekana kama vile kinataka kwenda kutafuta kitu flani.
Roma alijiuliza au ndio walichokuwa wakimaanisha wale majini kwamba jiwe hilo ndio ufunguo wa kutafuta watangulizi wao.
“Nini kinaendelea na hio kokoto mbona imecharuka?”Aliuliza Xiao.
“Sijui lakini nina uhakika ili tuweze kutoka katika hili eneo hiki kitu ndio ramani yetu , usisogee na nishikilie kwa nguvu bila ya kuniachia”Aliongea Roma.
Palepale Roma aliachia ile Hazina na mara baada ya kutoka kwenye mkono wake ilipaa kuelekea upande wa mlima wa shimo lile lilipo na Roma aliifukuzia kwa kasi sana akiwa amembeba Xiao.
Mara baada ya hazina ile kufikia usawa wa lile shimo lile jiwe ilishuka kwa kasi sana kwenda chini.
“Bro Roma unafanya nini , ni hatari”Wale roho wa kijini walimwita Roma kwa nguvu kumtahadharisha kwani waliona kabisa ni kama anataka kutumbukia katika hilo shimo kitu ambacho ni hatari.
“Nina dharula wakuu , nataka kuona hii kokoto inaelekea wapi , msiwe na wasiwasi nina mpango kichwani”Aliongea Roma.
Lakini majini roho hao licha ya kuwa na wasiwasi haikuwa rahisi kwa Roma kumsikiliza na hawakutaka kusogea karibu na shimo hilo kwani wasingeweza kujilinda
Ukweli Roma mwenyewe alikuwa na wasiwasi kama wao tu lakini alijiambia hawezi kukosa fursa kama hio kwani anaweza akachelewa
Licha ya kubeba mzigo kama Xiao , ataweza kuwa salama na uwepo wa Cauldron lakini pia na uwezo wa kutengeneza radi hivyo kama likijifunga angeweza kutengeneza njia.
Nguvu zake zilikuwa ni zile za nuru na radi yake hivyo hivyo na mbele ya nguvu za giza hakuwa akishikika kabisa lakini kubwa zaidi ni kwamba alikuwa na mwili wa ajabu uliomulikwa na jiwe la kimungu.
“Hii hazina haikupata uhai tokea tufike hapa lakini mara baada ya kufnnguka kwa shimo ndio imepata uhai , pengine ndio kitu ilichokuwa ikisubiria ili kunitoa katika huu ulimwengu”Aliwaza Roma na ndio wakati ambao alikuwa akipotelea katika lile shimo ambalo lilikuwa na giza kali sana kiasi kwamba haikuwezekana kuona kinachomsubiria chini.
Unadhani atakwenda kuibukia wapi , Kwanini Neema yeye hajaalikwa kama Edna na Amina kufadhili ujenzi wa Safina?
Otea Dhana ya Shoka itampasua nani wa kwanza.
ITAENDELEA
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI:SINGANOJR

Mono no Aware

SEHEMU YA 764.
Ni muda wa jioni ndani ya mji wa kisasa , mji huu ambao upo chini ya kampuni ya Vexto umekuwa ghali sana kwa siku za hivi karibuni na yote hayo ni kutokana na kile kilichokuwa kikiendelea duniani.
Watu wengi kutoka mataifa mbalimbali duniani walikuwa wakiingia nchini Tanzania kwa ajili ya kuomba hifadhi na asilimia ya watu waliokuwa wakifika nchini ni wale ambao wana ukwasi wa pesa.
Sasa eneo la mji huo wa kisasa tokea mwanzo ni eneo ambalo lilijengwa kwa ajili ya kukarimu familia na mazingira yake yalikuwa ni bora sana hivyo umaarufu wake ulipaa ndani ya siku chache tu na kufanya matajiri wengi kufika na familia zao kwa ajili ya makazi.
Mpaka kufikia tarehe kumi ya mwezi wa nane majengo yote yalikuwa yamejaa na projekti za ujenzi wa majengo mengi zaidi zilikuwa zikiendelea mita kadhaa kutoka katika mji huo.
Lakini ukiachana na hayo kwenye nyumba ambayo ndio kitengo cha Athena hupatikana maisha yalikuwa yakiendelea na hakukuwa na mabadiliko makubwa sana.
Suzzane ni kwa muda mrefu alikuwa nchini Tanznai tokea mara ya mwisho kusafiri kwenda Afrika ya Kusini kwenye kikao akiwa na rafiki yake Nadia Alfonso na tokea arudi alikuwa akiendelea na majukumu yake ya kawaida ya kusimamia taasisi ya misaada ya Edna Foundation kama mwenyekiti msaidizi.
Lakini sasa siku hio yote nzima alikuwa na hamu kubwa ya kimatarajio hususani katika wakati huo ambao dunia ni kama vile ilikuwa mwisho.
Ijapokuwa mrembo huyo hakuwa amesafiri lakini haikumaanisha kwamba hakuwa na misheni yoyote kama mwanachama wa jamii ya siri ya Ant- Illuminat.
Wakati huo wa jioni alionekana akitoka kwenye lift akisogelea mlango wa uyumba yake mpaka pale simu yake ilivyoanza kuita na alipoangalia jina la mpigaji alikuwa ni Nadia Alfonso na alishangaa mara baada ya kuona Nadia anampigia na namba ya kitanzania kwa kuamini kwamba yupo nchini.
“Hello! Nadia”
Aliongea Suzzane huku akiweka vizuri mkoba wake begani na kuingiza nywira katika mlango wa apartment yake.
“Sikutegemea kama usharudi mapema hivi … Oh,,, ndio upo njiani , basi sawa utanikuta karibu best”
Hivyo ndio ambavyo Suzzane alikuwa akiongea na Nadia na ilionekana mgeni wake alikuwa njiani na muda wowote angefika nyumbani kwake kulingana na maongezi yao.
Baada ya nusu saa mbele Suzzane alikuwa amemaliza kuoga na sasa alikuwa eneo la sebuleni akiangalia runinga huku akiwa ameshikilia mvinyo na ndio muda huo huo kengele ya mtu kubisha hodi ilisikika na alitabasamu na kisha alitembea na kufungua mlango.
Kutokana na usalama wa jengo hilo hakuwa na wasiwasi wa kuangalia kama aliekuwa akigonga ni nani , alikuwa na miadi ya kufika kwa Nadia hivyo alijua lazima atakuwa ni yeye kwani alimwambia anafika ndani ya nusu saa tu.
Suzzane mara baada ya kufungua mlango aliishia kutoa tabasamu ambalo limeambatana na mshangao kidogo.
Hio yote ni kutokana na kwamba hakuwa ni Nadia tu ambaye alikuwa mbele yake bali alikuwepo Zoe Kovac mwanamama kutoka Hungary.
Suzzane alikuwa akimfahamu maana aliwahi kukutana nae mara kadhaa kama moja ya mwanachama wa jamii yao ya siri.
“Suzzane!!”
“Madam!!”Aliongea Suzzane na kisha alikumbatiana na Zoe na kisha akahamia kwa Nadia na kuwakaribisha ndani.
Zoe Kovacic ilikuwa ndio mara yake ya kwanza kufika ndani ya makazi hayo na alionekana kushangaa.
“Huu mji unavutia, sijategemea Tanzania kuwa na sehemu nzuri kama hii”Aliongea Zoe wakati akiketi.
“Ni kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Vexto chini ya Raisi Edna Adebayo”Aliongea Nadia huku akitoa tabasamu na kumwangalia Zoe usoni kana kwamba anatafuta kuona kitu katika sura yake.
“Edna..!!”Alionyesha mshangao kidogo na wote wakaangaliana kwa namna flani hivi ya kuongea kwa ishara na wakatabasamu.
“Suzzane nadhani hujategemea kama nakuja na mgeni, sina haja ya kukutambulisha kwake kwani unamfahamu , lakini ili tusichelewe kuungana na wenzetu katika kikao naomba nikutambulishe kazi ambayo imemleta Zoe Kovac nchini Tanzania”Aliongea Nadia huku Suzzane akipanga glass mezani kwa ajili ya kumimina mvinyo.
“Miss Zoe yupo Tanzania kama kiongozi wa misheni yetu mpya”Aliendelea kuongea Nadia .
“Misheni mpya!!”
“Ndio Suzzane na ndio maana nimerudi haraka nchini Tanzania”
Suzzane hakushangaa kwani ilikuwa ni swala la muda tu kupewa misheni mpya lakini hakutemgemea Zoe kuwa moja ya viongozi ambao watakwenda kuongoza misheni hio.
“Suzzane ulifanya kazi nzuri kwenye misheni yako iliopita na jina lako limependekezwa katika kusimamia mpango B katika ukanda wa Afrika mashariki na kati”Aliongea Zoe .
“Suzzane misheni yetu ni kuwatambua wafadhili wa umoja wetu kuelekea utekelezwaji wa Projekti Binamu Island”Aliongea Nadia.
“Unamaanisha nini kuhusu Projekti Binamu Island na hawa wafadhili unaowazungumzia tunawatambuaje?”Aliuliza Suzzane kwa kingereza.
“Swali zuri Suzzane nadhani mpaka sasa umekuwa ukijiuliza ni mipango gani inaendelea katika umoja juu ya hiki kinachoendelea dunani , kulingana na Kalenda hili ni swala ambalo limetegemewa na tokea siku ya kwanza kuonekana kwa mvua ya theluji nchini Morocco umoja uliingia katika msingi wa malengo ya kuanzishwa kwake”Aliongea Zoe na kisha alimpa ishara Nadia ambaye alitoa kishikwambi maalumu na kumpatia Suzzane.
“Unachokiona ni ramani ya misheni yetu na maelezo machache ya Projekti , kwa muda mrefu sana Ant- Illuminat ilikuwa ikipokea michango kutoka kwa wafadhili ambao ni ‘Non-Active member’ na kazi yetu itakuwa ni kuwatambua rasmi”
“Kama walikuwa ni wafadhili kwanini tunapaswa kuwatambua ili hali hali taarifa zao zipo?”
“Upo sahihi lakini je kama dunia ikiendelea hivi kwa kipindi cha mwaka mzima nini kitatokea, Pojekti Binamu Island ni mpango B kama mpango A utafeli kulingana na Kalenda, hii inamaanisha kwamba kama mpango A ukifeli dunia haitoweza kurudi katika hali yake ya kawaida ndani ya miezi kumi ijayo na mpaka wakati huo uwezekano wa binadamu kuwa hai ni mdogo sana n msingi wa umoja wetu ni kulinda binadamu asipotee”Aliongea Nadia.
“Anachojaribu kukuelezea Nadia ni kwamba kama mpango wa kalenda utafeli inamaanisha kwamba hatuwezi kuokoa binadamu wote na ni baadhi ya hawa wafadhili watakaokidhi vigezo vya ki utambuzi ndio watajumuishwa kwenye Projekti Binamu Island”
“Kwahio kinachokwenda kufanyika ni uchambuzi wa hawa wafadhili si ndio mnachomaanisha?”Aliuliza na kuwafanya Zoe na Suzzane kuangaliana kwa ishara wakionyesha kuridhika.
“Hii ni misheni ambayo inafanyika kila taifa katika kila bara na inatakiwa kukamilika ndani ya miezi sita ijayo yaani baada ya tarehe ya Kalenda ripoti iwe kamili, tutafanya Purposive na Stratified Sampling kulingana na taarifa tulizonazo na baada ya hapo kazi kubwa ni kufikia kwa siri tageti husika bila ya familia zao kujua , changamoto iliopo mpaka sasa ni kwamba hawa wanachama sio hai na baadhi yao tayari wapo katika mpango wa Noah Ark na hiki ni kigezo namba moja cha kukosa sifa”Aliongea.
“Kama huu ndio mpango mbadala je tuamini kufanikiwa kwa tukio la Kikalenda ni asilimia ngapi?”Aliuliza Suzzane na swali lake liliwafanya Zoe na Nadia kuangaliana , ilikuwa ni kama vile Suzzane kavuka mpaka wa taarifa ambazo anapaswa kufahamu lakini Nadia alionekana kumtingishia kichwa kuonyesha kukubaliana nae jambo.
“Kutokana na usalama siwezi kukupatia jibu la moja kwa moja Suzzane ila unachopaswa kuelewa katika matukio ya kilenda yote yaliopita asilimia za kufanikiwa ilikuwa ni themanini lakini tukio kubwa la mwisho ambalo ndio msingi wenyewe wa umoja kufanikiwa kwake ni asililimia therathini , hii inamaanisha asilimia sabini dunia itaendelea kuwa katika hali mbaya kwa muda mrefu”Alijibu Zoe.
“Utekelezaji wa Projekti Binamu Island ni sehemu ya mipango mingi ya Dharula iliopo katika kuokoa binadamu”
“Kwa maelezo ambayo nimesoma hapa inaonyesha hakuna anaejua kilichopo nyuma ya mpango huu wa Binamu Island , hii ni taarifa ya siri au ni mimi tu nisie kidhi vigezo vya hadhi ya uanachama kujua taarifa zake?”
“Nadia hio ni taarifa ambayo hata viongozi wenyewe hawajui ni mpango wa namna gani na kitu pekee ambacho kinafahamika ni uwepo wa mwanachama ambaye anakwenda kutambulishwa mwishoni kati ya wanachama ishirini waliokuwa na mihuri, ndie ambaye amebeba ujumbe wote wa mpango Binamu Island”Aliongea
Suzzane alikuwa akielewa wanachama ishirini wa hadhi ya juu wote walikuwa na mihuri maalumu, kati ya hao aliokuwa akiwajua ni Mellinda , Phill knight na Linda kutoka Rwanda na inasemekana katika umoja huo kila mmoja alibeba au amebeba ujumbe maalumu, kwa mfano Chriss alikuwa amebeba ujumbe maalumu wa mchoro wa unabii kabla ya kifo chake na ndio sehemu ya viongozi hao wenye nembo ya mihuri.
Kwahio mpango Binamu Island ni mpango mbadala kama mpango wa tukio la kikalenda lisipotokea na anaejua mpango huo ni mwanachama wa mwisho ambaye bado hajajitambulisha ambaye pia ni alikutana moja kwa moja na Hades wa zamani.
Itaendelea hapa kipande cha 767.











SEHEMU YA 765.
Mrembo nusu jini nusu binadamu alikuwa katika hali ya hofu kweli , alikuwa amemng’ang’ania Roma kwa nguvu huku akiwa amefumba macho akimuacha ampeleke popote pale , hakutaka hata kuangalia kile ambacho kinawasubiria chini ya shimo hilo.
Mara baada ya kuingia umbali wa mita kama kumi hivi chini ya shimo hilo , Roma alihisi nguvu kubwa ya uovu iliokuwa ikitokea chini na kuzidi kuongezeka hatua kwa hatua kila alivyokuwa akielekea chini zaidi na zaidi na ilikuwa ikiogofya kweli.
Ilikuwa ni kama vile ni visu visivyohesabika ambavyo vinamkata kata katika akili yake.
Kwa bahati nzuri ni kwamba uwezo wa Roma ulikuwa mkubwa sana , nguvu ya mbingu na ardhi ilikuwa haina mwisho ijapokuwa ngao yao ilikuwa ikilika na nguvu hizo lakini alikuwa na uwezo wa kuiongezea kila inapopungua.
Lakini sasa kwa ajili ya kuchukua tahadhari Roma aliamua kukitoa kafara chungu chake ili kupunguza makali ya nafsi hizo za kimizimu ambazo zilikuwa zikimzingira.
Chaos Cauldron ni Dhana ambayo inameza kila kitu , haichagui nguvu za nuru wala za giza hivyo katika eneo kama hilo ni mahali pa kufakamia kwa uwezo wake wote.
Kilichomfurahisha Roma ni kwamba Cauldron kwake ilikuwa ni Dhana ambayo ni kama chombo cha kubadilisha nguvu za giza na kuwa safi kwani aliweza kuhisi joto likiongezeka katika mwili wake ikimaanisha kuna nguvu safi inamwingia.
Ghafla tu Roma aliweza kugundua kitu cha ajabu , ile hazina mbele yake ilikuwa imetengeneza kitu kama nafasi hivi ya wazi , kana kwamba ni nguvu ya kimiuujiza , ilikuwa ni nafasi ambayo ni kama vile inasukuma zile roho za kimizimu kusogea pembeni kupisha njia.
Ilionekana kama vile ni kitu ambacho hakikuwa kikiathirika na nguvu hizo za giza na kila inapopita itapishwa njia
Wazo hilo lilimwingia Roma kwa haraka sana na mara baada ya kufikiria kitu alimchukua Xiao na kumshikilia kwa nguvu na kisha aliongeza spidi na kuishikilia ile hazina mkononi kwa mara nyingine.
Mara baada ya Roma kushikilia ile Hazina walijikuta wakiwa kama vile ni kwenye puto ambalo moja kwa moja liliweza kuwakinga na nguvu zile za giza na kwanzia hapo nguvu hizo hazikuwa na madhara kwao.
Wakati huo Roma alijaribu kukadiria alikuwa amesafiri zaidi ya futi mia moja chini ya shimo hilo na mazingira ndani ya eneo hilo bado yalikuwa ni ya giza na hakuweza hata kuona vidole vyake kwa macho ya kawaida.
“Kama hii hazina ina uwezo huu inamaana hata hio mizimu ya ki uramu inaweza kupita katika hili shimo kwa kutumia hii hazina?”Roma aliwaza.
Lakini mara baada ya wazo hilo Roma aliachana nalo kwa kuona kwamba hata kama wanaweza kupita inawea isiwe salama kwa dunia kama watatoka maana walikuwa wamekwisha kufa.
Kuna kitu kilikuwa kikimwambia Roma pengine hio hazina haikuwa tu kwa ajili ya familia ya Sharif wafuasi wa majini pepo kutoka Braki , bali asili yake ilikuwa na maana kubwa ambayo ni siri.
Roma aliona hana cha kupoteza , ijapokuwa hajaaga huko kwenye ulimwengu wa jicho la Anga lakini hawezi kurudi tena , anapaswa kuendelea kufuata hazina hio inapompeleka na kutokana na hilo alizidi kwenda chini zaidi ya shimo hilo.
Kutokana na ulinzi wa hazina ile Roma hakuona wasiwasi tena wa kuogopa usalama wake , na alikipa chungu chake ruhusa kuendelea kunyonya nguvu hasi za kutosha.
Roma alijua kama Cauldron itaendelea kunyonya nishati hasi ikifika katika mazingira ya nuru moja kwa moja kitaweza kutengeneza uwiano wa nishati hizo ikimaanisha kwamba itapaswa kinyonya nishati za mbingu na ardhi nyingi sana kufikia uwiano na hio ilimaanisha nguvu zake zingeongezeka zaidi na zaidi.
Madakika yalisonga kwa spidi yake na ilimfanya Roma kupatwa na hofu ni wapi anakwenda kutokea , ilikuwa ni kama vile ametoboa dunia na sasa yupo katikati ya kiini chake kwani hofu iliizidi kuongezeka.
Bila kujua, kimahesabu ya dunia Roma aliweza kusafiri kwa zaidi ya siku saba mfululizo katika shimo hilo bila ya kuona mwisho wake , yaani bado tu hakuweza kuona mwisho wa shimo hilo.
Kitu ambacho Roma aliweza kujua ni kwamba kutokana na muda mrefu aliotumia kusaifiri kwenda chini hatokuwa kwenye shimo tena.
Katika eneo alipo kulikuwa na nguvu kubwa ya giza na alishindwa kutumia uwezo wake wa utambuzi kujua kingo za eneo hilo zilivyo kwani ilikuwa ni hatari zaidi.
Roma alijiuliza au ndio yupo kwenye kiini cha ulimwengu huo wa jicho la anga kama ilivyokuwa kwa kiini cha dunia
Lakini mawazo yake yalimwambia hapana , kwanini hakuna mwisho, kitu kingine ambacho kilimpa Roma ufahamu kwamba pengine alikuwa ametoka kwenye ulimwengu wa jicho la anga ni kwamba wakati akwia juu ya uso wa ulimwengu huo alikuja kugundua kitu kimoja ulimwengu huo ulikuwa ni kama vile ni mwezi uliokuwa katika umbo la mviringo ndio maana kila alivyokuwa akisafiri umbali mrefu alikuwa akirudi kwenye eno moja.
Sasa mawazo mengi yalipita katika akili yake na kujiuliza au mwisho wa shimo hili kuna muunganiko wa ulimwengu mwingine.
Roma hakuwa na majibu kwa wakati huo na hakuweza kufanya chochote isipokuwa tu kuendelea kushuka chini akifuata uelekeo wa haizna , aliamini asingeweza kupata majibu kwa kuwaza bali kwa kuona.
“Hawa majini pepo nadhani wameniingiza mtegoni tu”Roma aliongea kwa hasira huku aking’ata meno yake.
“Romaa..!!”
Ghafla tu Xiao ambaye alikuwa amemkumbatia Roma mgongoni kama kaganda aliita.
“Umeamka?”Aliuliza Roma huku akimgeukia na kumwangalia msichana huyo kwa hatia kutokana na mambo anayopitia kwa ajili yake.
Katika kipindi chote hicho Xiao yeye alikuwa kimya tu huku akilala na kushituka na akishituka angeongea na kisha kupotelea usingizini , lakini kadri walivyokuwa wakienda chini hakuwa na hamu ya kuongea tena.
Isitoshe katika maisha yake hakuwahi kupitia magumu ya namna hio , kukaa gizani kwa zaidi ya siku saba ni kitu ambacho kilikuwa ndoto kwake.
Roma mara baada ya kuona Xiao anazidi kuogopa alimpatia usingizi wa pono ili asiendelee kuona vitu vya kutisha katika shimo hilo.
Roma katika wakati huo alikuwa mpole sana mbele ya Xiao , kwani tokea walivokutana kwa mara ya kwanza ilikuwa ni matatizo tu mpaka wakati huo ambao alimlazimisha kuja katika ulimwengu asio ujua.
“Vipi imeshindikana kutoka tu?”Xiao aliuliza kwa wasiwasi na kwa upole kama vile anaogopa Roma atakasirika.
“Nadhani tutatokea tu , hiki kitu bado kinavutwa kwa mbele , nadhani hili eneo ni refu sana kwenda chini na nimeshindwa pia kuongeza spidi kwa kuogopa hatujui tunapoelekea”Aliongea.
“Kama ni hivyo .. unaweza kuniacha tu kama kuna hatari ili nisiwe mzigo ..niache tu usiwe na wasiwasi”Aliongea Xiao Kinyonge na kauli ile ilimshangaza Roma.
“Unaongea ujinga gani , tumekuwa pamoja kwa siku nyingi hivi halafu nikuache?”
“Ijapokuwa siwezi kujiita nina akili au busara lakini mimi sio mjinga , hii hali tuliopo huna uelewa nayo kabisa na vipi kama tutapatwa na matatizo mbeleni , uwezo wako ni mkubwa na unayo nafasi ya kijilinda lakini mimi ni laini sana na nguvu zangu ni ndogo hivyo sina uwezo wa kukusaidia ,… itakuwa vizuri kama utajiangalia mwenyewe kwanzia sasa kuliko kuwa na mimi”
Roma hakujua ni nini anajisikia kwenye moyo wake , lakini hali ya kusita na wasiwasi ilikuwa imemvaa alijua kabisa ikija kwenye hali ya maajabu na mambo ya kutokutegemea kama hio nguvu zake pekee zinaweza zisitoshe.
“Usiwe hivyo basi , chochote kile kitakachotokea tutapitia pamoja”AliongeaRoma huku akilazimisha tabasamu.
Xiao alionekana kukata tamaa kabisa, na alipelekea mkono wake kiunoni na alivuta kitu na kisha akakiweka katika mikono ya Roma.
“Hiki kidani ni cha nini?”
Roma aliweza kuona namna kidani hivyo kilivyokuwa na hali ya joto na unyevunyevu na kwa kutumia uwezo wake aliweza kugundua ni kidani kilichotengenezwa kwa madini adimu sana ya Jade.
Binadamu wa kawaida anaweza kuyachukuia madini ya Jedi kama kitu cha kawaida lakini ni moja ya madini adimu sana , ukiachana na uzuri wake wa kuvutia kwa macho lakini inaaminikina kwamba madini haya hubeba nguvu ya ajabu ndani yake.
Yaani kama ilivyo kwa Waafrika wengi kufunga hirizi viunoni kwa ajili ya kuamini ni ulinzi flani kwa madini ya Jade yenyewe ilikuwa tofauti japo haikufanana na hirizi ambayo imebeba nguvu ya kishirikina.
Jade mara nyingi ni madini ya kiroho zaidi kuliko ilivyokuwa dhahabu.
Kwa namna kidani hicho kilivyotengenezwa Roma aliweza kushangaa mno kwani ni utalamu wa aina yake.
Sasa Roma alikichunuguza kidani hicho kwa macho yake ya nguvu za mbingu na ardhi na hakujua kwanini Xiao ameamua kumpatia.
“Hiko ni kidani ambacho baba amenipatia , nilivyokuwa mdogo nilifahamika kwa jina la Leili na ndio maana ya mchoro unao uona , ni kidani ambacho baba amesema ni cha thamani sana na nivae popote pale niendapo”
Roma alishangazwa na maneno hayo , ilionekana ni Anjiu mwenyewe alietengneza kidani hicho na kumpatia binti yake kama zawadi na kutokana na namna Xiao alivyoongea ilimfanya Roma kuwa na wasiwasi.
Hata yeye alikuwa tayari ni baba na aliona ni kwa namna gani Anjiu aliweka hisia zake katika kutengeneza kidani hicho kama zawadi kwa binti yake , mwenyewe Roma ashawahi kuwaza likija swala la Lanlan kutaka kitu hata kama kinapatikana mwezini anaweza kufanya mpango kwenda kutafuta.
“Kwasababu umepewa na baba yako , kaa nacho kama alivyotaka , isitoshe hii sio hazina wala kitu cha thamani kwangu kwanini unanipatie?”
“Nataka ukae nacho kama ikitokea nikashindwa kutoka kwenye hili giza .. nataka ukafikishe ujumbe wangu kwa baba kupitia hiki kidani kwamba ninaomba kwa mara ya mwisho aache ugomvi na Roma”
Roma alishangazwa na kauli hio , msichana huyo aliona ni kama mjinga kwani hakuchukulia siriasi ugomvi uliopo kati yake na baba yake.
“Unadhani baba yako yupo tayari kuacha anachokifanya kwasababu ya kuomba kwako . isitoshe hata kama nikitaka kumuua baba yako unajua kabisa haniwezi”
“Najua .. lakini sitaki kuona mmoja kati yenu akifa ,, baba amefanya vitu vingi viovu lakini mimi namjua sio mtu mbaya , amepotoka tu kwa muda”
“Sio rahisi kama unavyofikiri”
“Naomba unisikilize , baba yangu sio kama mnavyomuona , baba alikuwa ni mtu ambaye ananijali sana na kunilinda tokea nikiwa mdogo .ijapokuwa nimezaliwa nusu jini nusu binadamu familia yangu haijawahi kunichukulia siriasi lakini baba hajawahi kwenda matembezini akiwa na kaka , mimi kila siku atanichukua na nitaenda nae katika maeneo tulivu katika milima na kucheza na wakati mwingine ananitoa hadi ulimwengu wa binadamu na kucheza milimani na chini ya bahari … wakati huo kaka yangu yeye alikuwa akimeza vidonge na madawa kwa ajili ya kupandisha uwezo wake , mimi sijawahi hata kujifunza kuvuna nishati za mbingu na ardhi mpaka nilivyofikia umri mkubwa … familia yangu na baadhi ya watu waliona yote hayo ni kwasababu Baba hakuwa akinipenda kwasababu ya mchanganyiko wa damu yangu lakini yote hayo alikuwa akifanya kwa ajili ya kunilinda .ni sawa na kusema maisha yangu ya utotoni yalikuwa ya furaha zaidi kuliko kaka yangu ambaye muda wote alihimizwa kujifunza , sikuwa na mama lakini mapenzi ya baba yalinifanya nisiwe mpweke… mara baada ya kufikia miaka sita baba alinielekeza namna ya kuvuna nishti za mbingu na ardhi na kisha akanitoa kuja ulimwengu wa kawaida ili kufanya waone kama hanijali …niliishi peke yangu lakini baba alikuwa amenipatia kadi ya benki ambayo ina hela nyingi sana ambazo zilikuwa zikiongezeka kila siku na niliweza kusoma mpaka nikahitumu na safari yangu ya kwanza kitaaluma ndio ilinifanya tukakakutana nchini Tanzania……”
Xiao alielezea mengi mbele ya Roma kuhusu baba yake na ilionekana ni kweli Anjiu alikuwa akimpenda sana binti yake na Roma aliweza kuliona hilo.
IjapokuwaAnjiu alionekaa kuwa mkali muda mwingi mbele ya Xiao lakini ndio namna yake ya kuonyesha kwamba alikuwa akimpenda.
Roma aliweza kuelewa , ilikuwa ni kama yeye tu , pengine mbele ya Lanlan anaweza kuonekana kama baba mkatili lakini kwenye moyo wake ni aina ya baba ambao wanaweza kufanya chochoe kile kwa ajili yake.
“Inatosha sasa…”
Roma hakutaka kuendelea kusikiliza namna Xiao anavyomtetea baba yake mpaka kuanza kuangua kilio.
“Nakuahidi kama tukitoka salama nitampa baba yako nafasi , kama ataacha mambo yake na kuacha kuwa adui yangu basi sitomgusa”Aliongea Roma na jibu hilo lilimfurahisha Xiao kiasi cha kuanza kulia tena.
“Unalia nini tena sasa , si nishasema nitampa baba yako nafasi ya kujirekebisa ,siwezi kumuacha baba yako aniue mimi halafu nisimue , nina mke , watoto na familia inayonitegemea pia”Aliongea na ilimfanya Xiao kuwa na furaha sasa.
“Sio kama nalia kwa huzuni ni kwamba nina furaha sana , Roma najua unanipenda , ninaweza kuhisi mapenzi yako kwangu”
Roma alijikuta akiona aibu ya kauli hio na kumuondoa karibu kwani kidogo tu abusiwe mdomoni.
“Umenielewa vibaya…sifanyi hivyo kwasababu ya unavyofikiria”
“Huna haja ya kujielezea , najua wewe ni mwanaume mwenye aibu muda mwingine , ijapokuwa kwa kiasi gani umekaa kihuni lakini moyoni una maadili .. mwanaume mrahisi kuelezea hisia zake kwa mwanamke huyo sio wa kuaminika”Aliongea na kuanza kucheka.
Kwa jinsi walivyokuwa gizani ungewaoana ungesema mizimu inatongozana.
Roma mara baada ya kuona Xiao kasharudi kwenye hali ya furaha alivuta pumzi na kuzishusha.
“Labda ni nakupenda ndio maana ninaweza kuvumilia kusikiliza ujinga wako ..nani kakufundisha kuongea ujinga?”
“Na wewe ongea ni lini umeanza kunipenda?”
“Aa..”
Roma uso wake ulicheza na kujiambia kwanini uelewa wa msichana huyo ni tofauti na watu wengine.
“Kama unashindwa kujibu . je unajua ni lini nilianza kukupenda na kwanini?”
“Sitaki kujua”
“Kwanini?”
“Nimesema tu sitaki kujua”Aliongea Roma na kumfanya Xiao kuvuta mdomo.
“Ninachotaka kujua kwa wakati huu ni namna ambavyo nitakutoa kwenye hili giza ,, hivyo usiongee ujinga tena na tulia na uamini kwamba tutatoka salama”Aliongea huku akimfinya .
Roma moyoni alikuwa akimchukulia Xiao kama mdogo wake , lakini kutokana na mazingira hayo na namna ambavyo Xiao alikuwa mwepesi kubadilika kihisia aliona ngoja kwanza watoke amuweke wazi kwamba hana mpango wa kumfanya mpenzi.
Roma aliendelea kusemezana na Xiao ili tu kuondoa hofu mioyoni mwao kwa muda mrefu , mazunguzo hayo yalimfanya Roma kuja kugundua Anjiu alimdanganya Xiao kwamba mama yake ni muafrika lakini ki uhalisia mama yake mzazi alikuwa ni Master yake Magdalena.
Kilichomfanya Roma kuja kugundua ni mara baada ya Xiao kusema baba yake ana kidani hicho hicho ambacho herufi zake zilizokuwa zimeandikwa katikati zinatimia mpaka vidani vyote vitatu vinapokuwa pamoja.
Yaani kwa haraka haraka Roma aligundua Anjiu alitengeneza vidani vitatu ambavyo maana yake sio kamili mpaka vyote viwe pamoja , sasa kwa maelezo ya kidani cha Anjiu na kidani cha Tang Luyi Master yake Magdalena ilipata maana lakini Roma aliona ngoja atoke ataenda kujua vizuri ukweli wote.
Safari iliendelea , shimo lilikuwa ni kama vile linaongezeka urefu kadri walivyokuwa wakienda chini na kitu cha kushangaza ni kwamba Roma alihisi ni kama vile ile Hazina imezidi kuwa na nguvu na spidi yake kuwa kubwa.
Maada ya kupita kama masaa matano hivi hatimae kwa mbaali kulionekana kitu kama kijidoti cheupe na kwa haraka haraka Roma aliweza kugundua ni mwanga.












SEHEMU YA 767.
Ilionekana kama nyota kutokana na udogo wake lakini Roma alijua lazima itakuwa ndio mahali wanapoenda kutokea.
Sasa mara baada ya Roma kuona kuna mlango wa kutokea palepale alimshikilia Xiao vizuri na kusaifi kwa kasi kuelekea eneo hilo na kwa bahati nzuri kadri walivyokuwa wakisogelea ndio ambavyo eneo lile liliongezeka ukubwa na kuwafanya kuwa na shauku ya kuona kilichopo nje.
“Kadri nilivyokaribia karibu niliweza kuona ni kama vile ni pazia la mwanga ambapo sikuweza kuona mwisho wake”Aliongea Roma wakati akihadithia.
Ilikuwa ni kama vile ni ukuta ambao ulifanya nguvu za giza kushindwa kupita na kuchanganyika na mwanga huo.
Roma mara baada ya kufika alijihisi ni kama vile yupo juu ya kilele cha mlima wa kisiwa maeneo ya chini alichokuwa akiona sio ulimwengu bali ni bahari ya mwanga uliotanga kama shield.
“Tuko wapi hapa ?”Aliuliza Xiao kwa mshangao kwani alichokiona kilikuwa kinashangaza.
“Sijui hapa ni enoe gani lakini inaonekana kabisa hii hazina haijakosea kutuleta hapa . lakini inaonekana huu mwanga ni kama tabaka linalotenganisha hili shimo na upande wa chini ndani na kutufanya tushiwe kupita”Aliongea Roma akiwa amekuja sura kwani kila alivyokuwa akijaribu kwenda chini ilishindikana kupita.
“Kwanini usitumie mbinu yoyote kuvunja hili pazia la mwanga na tukapita”Aliongea Xiao.
“Hapana , hii sehemu haieleweki na siwezi kuhisi uwepo wa nishati yoyote , ninaweza kufanya hivyo na kusababisha matatizo mengine”
Aliongea Roma yaani licha ya kwamba wapo juu ya pazia la mwanga lakini kwa chini hawakuona chochote kile ni kama macho yao yamefika ukomo lakijni Roma alichoweza kuhisi ni kwamba bado hazina ilikuwa ikifurukuta kwenye mkono wake, lakini awamu hio haikufurukuta kwenda chini bali uelekeo wa tambarare.
Kwasababu Roma alishindwa kwenda chini aliamua kufuata uelekeo wa ile hazina kwa kusafiri kwenda njia mlamlo na muda huo haikuwachukua muda mrefu kwani walijikuta wakifika sehemu ambayo kwa mbali waliona kitu kama vile ni kisahani aina ya CD za zamani(Lacquered disk) ukubwa mara tatu wa beseni la kuogea na kisahani hicho cheusi kilikiwa kikizunguka kwa kasi mno kana kwamba kuna nguvu iliokuwa ikifanya kizunguke, kilikuwa ni kitu cha kushangaa ambacho binadamu wa kawaida angeogopa kufa.
Kitu ambacho pia kilimpa mshangao zaidi Roma ni kwamba ule weusi wa kile kisahani ulifanana kabisa na weusi wa jiwe lake , yaani malighafi ambazo zimetumiwa kutengenezea hio sahani kubwa inayozunguka ni vilevile ilivyo kwa hazina hio.
“Damn ,kwahio huu mwanga wote unadhibitiwa na hicho kisahani kidogo hivyo?”Roma aliwaza huku akipatwa na hali flani ya wasiwasi.
Ilikuwa ikizunguka kwa kasi kubwa na kulikuwa na vitu kama herufi(Runes) ambazo hazikueleweka maana yake , ilionekana ni lugha ngeni.
Herufi hizo zilikuwa zikifanana kabisa na ambazo zilikuwa zimechorwa kwenye Dhana yake mpya ya Shoka la Pangea.
Roma alijiuliza nani alitengeneza kitu cha teknolojia ya kimaajabu namna hii , ilionekana kabisa ni kitu ambacho hakikutengenezwa jana wala leo , kilionekana kutengenezwa zamani sana , lakini akili iliotumika hapo haikuwa ya kawaida kabisa .
Roma aliishia kusimama na hakujua afanye nini lakini ile hazina mkononi mwake ilikuwa bado ikifurukuta , Roma aliamua kutoa chungu na kukiweka mbele yake kwa namna ya kumlinda yeye na Xiao na kisha aliachia ile hazina.
Kitu kilichofuatia baada ya hapo kilimshangaza ziadi na zaidi na kuwafanya wote kuzuia pumzi zao.
Mara baada ya Hazina ile kuwa huru ilienda moja kwa moja mpaka eneo la katikati ya kisahani kile na ilizama katika eneo la katikati na kuifanya ionekana nusu kama hemisphere.
“Inaonekana hilo jiwe lako jeusi lilitolewa katika hilo eneo , au ni ufunguo wa kufungua hili pazia la mwanga”Aliongea Xiao.
Roma hata yeye alifikiria hivyo hivyo lakini wakati huo alipatwa na wasiwasi kwenye moyo wake akiogopa kwambe pengine anafanya makosa makubwa ambayo yanaweza kumgharimu yeye au wengine.
Kitendo cha lile jiwe la mviringo kukaa katika kile kisahani zile herufi zilizokuwa zikionekana kwa juu zilififia mara moja na kisahani kile kiliacha kuzunguka taratibu na mwanga mkali wa rangi nyeupe kabisa ulianza kuonekana ukitokea chini , yaani ni kama vile kunapombazuka na pazia kuonyesha mwanga wa nje.

Mara baada ya kisahani kile kufunga breki kabisa ilikuwa ni kama vile wingu linavosambaratika hewani mara baada ya mvua kumaliza kunyesha ndio namna ambavyo mwanga lilivyoanza kujiachia na kutengeneza shimo kiasi cha kufanya wale Roho wa giza na nafsi za kishetani kuanza kushuka kwa kasi kwenda chini kwenye mwanga.
Ndani ya muda mchache tu lile pazia lilikuwa limetengeneza njia kama vile ni shimo la mlango wa hewa inaochemka eneo la katikati na mlango ule haukuongezeka kabisa ukubwa lakini bado Roma hakuona chini yake kulikuwa na nini.
“Unafikiri ilikuwa ni sahihi kuja hapa na kufanya hivi?”Aliuliza Xiao kwa wasiwasi mara baada ya kuona giza la shimo lile likiporomoka.
“Tushafika tayari na hatuna pa kwenda zaidi ya kuingia”Aliongea Roma huku akiona kwa mbali mwanga flani wa Zambarau.
Roma alijaribisha kusogelea kile kisahani na kusukuma kwa ndani ile hazina na mara baada ya kufanya vile ni kweli ilisogea kwenda chini na palepale mwanga uliokuwa ni wa Zabarau umezingira kwa chini ulianza kupotea na hatimae waliweza sasa kuona kilichokuwa chini.
Kulikuwa na nafasi kubwa iliokuwa chini yake ambayo imejengwa kwa kutumia mawe yaliochongwa na kuwa kama matofauri makubwa huku ikishindiana kueleweka ni kwa namna gani yamegandishwa pamoja , mawe hayo yote yalikuwa na herufi za lugha isiofahamika.
Roma alitumia uwezo wake wa utambuzi kukagua eneo hilo na uso wake ulibadilika palepale na alishindwa kuhimili mshangao wake na kubweka.
“Huu si ule mnara ndani ya ulimwengu wa majini pepo!!!”
Roma ambaye ashawahi kuingia kwenye mnara ule mara baada ya kuvutwa kwenye ulimwengu wa majini pepo aliweza kufahamu mara moja mazingira yake.
Ndio maana hizo herufi zilikuwa zikimjia akilini kaziona mahali kumbe ni ndani ya huo mnara.
Ukweli ni kwamba pengine Roma angekuwa ashajua nini kinafuatia kabla hata hajafungua , tatizo tu ni kwamba herufi zile zilionekana ziikuwa ni maandishi yanayomaanisha kitu flani lakini alishindwa kujua tafsiri yake.
“Unamaanisha nini kusema mnara , unapajua hapa?”Aliuliza Xiao kwa shauku.
Roma alikuwa katika hali ya kuchnganyikiwa na hakuwa na muda hata wa kumwelezea Xiao , kwani hakuelewa kwanini wamekuja kutokea kwenye huo mnara, Roma alijiuliza au kulikuwa na muunganniko wa sehemu hizo mbili yaani ulimwengu wa jicho la anga na ulimwengu wa majini pepo.
Roma alijiuliza kama ni hivyo imekuwaje , je kuna mtu alitengeneza hii njia au ilikuwepo yenyewe tokea mwanzo?
Roma alimuwazia Aoiline palepale ambaye aliingia nae katika mnara huo wakati wa kupambana na Lekcha na ili kumsaidia yeye na Sophia kuondoka aliamua kujitoa kafara yeye mwenyewe.
Roma hakujua nini kimemtokea mrembo huyo wa kijini na kwasababu alikuwa yupo hapo aliona ni vizuri kama akienda hadi chini kujua kinachoendelea.
“Nifuate”AliongeaRoma na wote wawili waliingia katika mnara huo , ilionekana juu ya mnara huo tokea mwanzo kulikuwa na mfuniko ambao unaunganisha ulimwengu mwingine na hazina ile kuwa ufunguo.
Yaani kwa lugha nyepesi inaonekana ni mnara unaounganisha ulimwengu wa binadamu , ulimwengu wa majini pepo na ulimwengu wa jicho la anga ambapo ni makazi ya mizimu ya majini.
Sasa unachopaswa kuelewa Roma hakuwa kwenye mnara wa upande wa dunniani kwani muonekano wake ulikuwa tofauti bali alikuwa kwenye mnara wa ulimwengu wa majini pepo ambao katika ulimwengu huo ulikuwa umeenda sana hewani kiasi kwamba ilikuwa ngumu kuona mwisho na kwa maelezo ya Aoiline hakuwa akijua mwisho wake ulivyo.
Msisimko wa eneo hilo ulikuwa umebadiika na ulimwengu wa nje , ilikuwa ni hali ya kipekee ambayo unaweza kusema inapatikana katika mnara huo tu.
Roma mara baada ya kuwa ndani alikuja kugundua pazia la mwanga nyuma yake halikuwa limejifunika na palepale ni kama vile Roma anakumbuka kitu alichosahau.
Alijuliza kama hazina hio ilitolewa katika eneo hilo inamaanisha kwamba kuna jini ambalo liliweza kufika hapo na kuondoa hilo jiwe ,kama ni hivyo inamaanisha kuna jini pia ambaye alifika ulimwengu wa majini pepo na kisha akatoka.
Wazo hilo lilimshangaza mno Roma kwasababu Aoiline ndie aliesema kwamba hakuna kiumbe chochote ambacho kiliingia katika ulimwengu huo wa majini pepo na kurudi na yeye ndio ambaye aliishi kwa miaka mingi sana.
Ilipaswa kuaminika kwamba Aoiline ndio jini ambaye ameishi muda mrefu sana , pengine kabla hata ya miungu kufika duniani hivyo hakuna kitu ambacho hakuwa akijua , sasa anashindwaje kujua kama kuna mtu alifanikiwa kuingia kwenye ulimwengu huo na kisha akatoka.
Kama ni hivyo Roma aliamini labda ni kabla ya majini hao kumezwa kwenye ulimwengu huo ndio mtu huyo aliingia na kutoka na aliweza hata kuhimili mapigo tisini na tisa ya radi.
Kama ni hivyo Roma aliona ilikuwa ikileta maana , Aoiline atakuwa hajui historia yote.
Roma mara baada ya kuwaza kidogo aliamua kuchuka mpaka kwenye floor ya kwanza ambayo ni ya juu kabisa akiwa na Xiao na ukweli hakujua kama alikuwa floor ya mwisho au ya katikati kwasababu umbo lake halikuwa likieleweka kabisa ni eneo la kimaajabu mno ambalo muundo wake ni kama unabadilika badilika
Roma kwa wakati huo hakuwa akiogopa tena radi ya rangi ya zambarau isitoshe pia aikuwa na Caulrdon hivyo alijua kabisa lazima ataweza kumlinda Xiao.
Roma mara baada ya kutua chini kabisa ilikuwa ni kama vile eneo limeongezeka ukubwa na floor yake haikuwa ya kawaida kabisa , ilikuwa ni kama vile chuma cha madini ya dhahabu ambacho kilikuwa katika umbo la duara ambacho kilikuwa na michoro inayokutana katikati.
“Inaonekana hapa ndio floor ya juu kabisa ya huu mnara … kwahio inamaanisha kuna uwezekano wa kuwepo kwa milango miwili ya kutokea?”
Roma alikuwa sahihi kufikiria hivyo mara ya mwisho wakati alivyokuwa akitoka hakufika katika eneo hilo na kama angefika moja kwa moja angeenda ulimwengu wa jicho la anga , kwa hio moja kwa moja aliaini kuna mlango mwingine ambao unampeleka moja kwa moja mpaka kwenye ulimwengu wa kawaida.
Xiao mara baada ya kujua kwa uchache kuhusu eneo hilo na ulimwengu wa majini pepo aliishia kushanga na kutabasamu kwa wakati mmoja.
“Tunaweza kutoka?”
“Lazima uwezekano huo upo , hebu njoo kwanza tuone kama kuna mlango mwingine ,ijapokuwa hii floor ni kubwa lakini haifanani kabisa na floor za chini yake , hapa hatuoni mwisho kwani ni kama vile upana wake unaongezeka hivyo kuwa makini kutafuta ishara yoyote”
Xiao aliishia kutingisha kichwa huku akionyesha furaha yake baada ya kupata tumaini la kuweza kurudi dunaini.
“Hawa majini pepo inamaana walichokuwa wakimaanisha ni kwamba sio kufufua jamii yao bali ni kuruhusu majini pepo kurudi duniani””
Ukumbuke asili ya majini hao ilikuwa ni duniani kabla ya kuanza kuvutwa katika ulimwengu huo na kwao ilikuwa ni kama gereza na ilikuwa adhabu kwao kwa kuua sana binadamu.
Ilikuwa ni kazi ya Mungu kutenganisha viumbe wote katika ulimwengu tofauti tofuati , kwa mfano kulikuwa na ulimwengu wa majini watu , ulimwengu wa majini pepo na ulimwengu wa mizimu ambao ni wa jicho la anga , lakini pia ulimwengu wajangwa tenganifu.
Ukifikiria hayo yote inaonyesha kwamba sio mambo ambayo yametokea kwa bahati mbaya , kuna uwepo wa kiumbe mwenye uwezo wa kutisha ambaye alifanikisha.
Kama majini pepo haya yatatoka na kuingia ulimwengu wa kawaida uwezo wao utaongezeka zaidi ya mara nne”Aliwaza Roma kwani alijua fika ulimwengu huo ulikuwa ukiwazuia kuwa na uwezo wao wote , ukweli ni kwamba ni kama walikuwa kwenye gereza.
Kwa mfano Aoiline na Mfalme Zao wote walikuwa ni wabobezi wa levo ya tisa ya mafunzo yao ya kuamsha mapepo yao ya ndani ambapo ni sawa na kupitia mapigo tisini na tisa ya radi.
Roma kuna vitu viwili vilivyomjia akilini ,aliamini kwanza asili ya ulimwengu wa majini pepo ilionekana ilikuwa imewekwa makusudi kwa ajili ya kutotafuta namna ya kutoboa na kujiokoa , maana kama wangekuwa na uwezo wao wote basi ni dhahiri wangeweza kupita.
Kitu cha pili Roma alichowaza labda mtu ambaye amewafungia huko alikuwa hataki watoke kwa kuepusha hatari , kwa mfano Roma aliamini kama wale majini joka watatoka basi kwa tabia zao lazima dunia isingekuwa salama.
Lakini swali likaja kama ni kweli kwanini hazina yao tokea mwanzo iwe katika mikono ya majini pepo.
Ukweli ni kwamba kwa majini pepo ilikuwa ni sawa na mtu akupatie kitu akuambie hiki kina thamani kubwa kwako lakini thamani yake hujui ilivyo , ilionekana ni mara baada ya kupotea kwa majini pepo enzi hizo hazina hio iliondolewa na kukabidhiwa kwa majini wa jangwa tenganifu na kupewa maelezo kwamba ni kitu cha muhimu kwao kuwarudishia wakuu wao waliopotea lakini hawakujua kwa namna gani ni muhimu.
Ilionekana lilikuwa ni tumaini ambalo limepandwa kwao ili mradi kutunza hazina hio sasa Roma anajitokeza aiaiiba na sasa anajua kazi yake rasmi.
Roma aliamini kuna siri kubwa ambayo bado haijui na pengine yupo karibu kuijua hivyo hakutaka kujipa maumivu ya kichwa sana.
Roma alikuja kushituliwa kutoka katika mawazo mara baada ya kusikia ngurumo kubwa ya radi kutoka floor za chini ya mnara huo.
Eneo ambalo walikuwepo hakukuwa na radi ya aina yoyote ilikuwa ni kama ilivyokuwa chini kabisa ya mnara katika floor ya kwanza.
Roma alijua kabisa mnara huo haupigi radi labda iwe tu kuna mtu anaejaribu kutoka sasa alijiuliza au kuna mtu ambaye yupo ndani ya mnara , alishangaa kwani anachojua ni kwa miaka sitini ndio unafunguka na kama sio hivyo itakuwa kuna mtu aliekuwa ndani ya mnara huo kwa muda mrefu.
Roma alijikuta akimeza mate , ijapokuwa aliamini haiwezekani lakini ilimpa hali ya kuamini pengine ni kati ya Aoiline au Lekcha.
Sasa Roma hakujali atakuwa nani alijiambia hawezi kupotezea
Wakati huo Roma aliamini alikuwa na uwezo wa kwenda mpaka floor ya kwanza na kurudi chini bila shida yoyote hivyo anapaswa kwenda kuangalia.
Na alijiambia kama ni Aoiline ambaye bado anapambana na Lekcha basi hawezi kumuacha.
“Xiao bakia hapa na hakuna radi yoyote hivyo ni eneo salama , mimi nitaenda chini kuangalia hali ilivyo , kama nisiporudi ndani ya siku moja tafuta njia ya kutoka , lazima kutakuwa na mlango humu ndani kwenye hizi kuta.
Roma hakutaka kumchukua Xiao kwenda nae chini kutokana na wasiwasi wa kuumia.
Xiao mara baada ya kusikia kauli hio ya Roma alimshika Roma kwa nguvu huku akianza kutetemeka kwa hofu.
“Wewe.. naomba usiniache , Roma jamani si ulisema popote tunaenda pamoja mpaka tutoke , mimi naogopa mwenzio”Aliongea huku hali ya kulia ikianza kujionyesha.
Roma mara baada ya kuona hali ya msichana huyo kutaka kulia ilibidi amweleze hali ilivyo huko chini na ilikuwa ni vizuri zaidi akienda peke yake , mara baada ya kuongea kila kitu Xiao alimwachia kwa hiari yake mwenyewe na kukubali kusubiri.
Lakini mishscnaa huyo alikuwa na kiburi na alimwambia Roma kama hatorudi basi na yeye haondoki hapo , kauli yake ilimfanya Roma kuwa na hatia.
Lakini Roma hakuwa na jinsi kwa namna yoyote ile alitaka kwenda kuangalia kinachoendeea , kwani asingefanya hivyo ataendelea kumuwazia Aoiline hali yake ilivyo na ataendelea kujilaumu.
Lakini kubwa zaidi wale majini kutoka ulimwengu wa jangwa tenganifu walikuwa na hamu ya kutaka kukutana na mtangulizi wao , hivyo kama nafasi ipo aliona anapaswa kuitumia wakati huo.
Roma aliamini kutokana na kuishi muda mrefu , Aoiline sio mkatili tena kiasi cha kusababisha matatizo kama atatoka duniani.
“Aoiline naamini utakuwa salama dada yangu..”Aliwaza Roma na kisha aliruka kuelekea chini.
Chungu hakikuwa nyuma kudhalisha nguvu yake ya giza na kuanza kumshambulia Roma ubongo wange , ilionekana roho hio ya mnyama ni kama ilikuwa ikifurahia mazingira.
Roma mara baada ya kupita floor ya kwanza palepale alishitukiwa na safu ya ulinzi na palepale radi iligonga na kumshambulia pale alipokuwepo.
“BOOM!!
Radi iliokuwa juu kabisa ndio ilikuwa tishio lakini wakati huo Roma uwezo wake ulikuwa mkubwa kwani alikuwa na uwezo wa kuidhibiti.
Mara baada ya radi hio ya bluu na zambarau kuigia katika mdomo wa Cauldron , cheche za shoti zilionekana zikitoka na kupotea palepale kwa namna ya kumezwa na ziligeuzwa na kuwa nishati ya kiroho na kuingia katika mwili wa Roma na katika nafsi ya Cauldron.

Ilikuwa ni kama vile Dhana hio ilitengenezwa kwa ajili ya kuingia kwenye mnara huo na kunyonya nguvu ya radi , kwani ilimeza kila kitu na haikumsababishia Roma maumivu ya aina yoyote yale.
Lakini hata hivyo ni nguvu kidogo sana ambayo Roma alikuwa akifaidika nayo alikuwa mwishoni tayari mwa levo ya radi ya mapigo tisa hivyo , hivyo ilimaanisha kwamba hawezi kunyonya tena nishati hio kwani ilikuwa ni kama vile amejaa.
Roma aliweza kupita floor moja moja hakukuwa na ngazi katika mnara huo, ilionekana ni dhaihiri mnara huo haukutengenezwa kwa ajili ya binadamu wa kawaida.
Kadri alivyokuwa akishuka chini ndio urahisi ulivyoongezeka na dakika chache tu alikuwa chini kabisa ni sawa na kusema alikuwa katikati ya mnara huo sio chini sana wala sio juu sana.
Na Roma mara baada ya kutumia macho yake ya X-ray kuchunguza kilichokuwa kikiendelea chini yake alijikuta akishangaa mno.
Katika floor ya kwanza kulikuwa na mkusanyiko mkubwa wa nishati ya Ant-matter isio ya kawaida ambayo ilikuwa ikipigana na kamba za muundo wa hariri za nguvu ya kijini.
“Aoiline na Lekcha bado wanapigana tu!!“Aliongea Roma huku akiwa haamini kwani ni kama vile ameuwaacha hapo jana na karudi leo ili hali mwaka ulikuwa unakaribia kuisha.
ITAENDELEA.
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI: SINGANOJR

Mono no aware

SEHEMU YA 767.
Haikuwa na ubishi kabisa Roma aliweza kuona namna ambavyo Lekcha uwezo wake ulivyokuwa umeongezeka , kwa mahesabu ya haraka haraka ilikuwa tayari ni mwaka na Roma alishangazwa kwa namna ambavyo Lekcha ameimarika na ukweli ni kwamba hakuwa binadamu , alionekana kama kiumbe ambacho kipo katika umbo la nishati.
Aoiline upande wake alikuwa amechanguka na alionekana alikuwa akihangaika sana kujilinda na ngao ya kijini , yaani ilionekana uwezo wa kushambulia hakuwa nao zaidi ya kujilinda.
Nywele zake zilizokuwa za kirembo zilikuwa zimejikunja kunja kunja huku gauni lake likiwa limechanika chanika, mikia yake yote tisa ilikuwa ikionekana na kuwa kama kinga kwake.
Kama sio kwa uzuri wake wa uso ingekuwa ngumu kudhania mwanamke huyo alikuwa na hadhi kubwa kati ya majini wa jamii ya Mbweha.
Wawili hao pia walionekana kuhisia uwepo wa Roma na mara baada ya kumuona akishuka kutoka juu haikuwa kwa Aoiline tu lakini hata kwa Lekcha mwenyewe alikuwa katika hali ya mshangao.
“Ni wewe!, Wewe mjinga hukuweza kufanikiwa kutoka wakati ule?”Aliongea Aoiline akipandisha sauti na ni wakati uleule alifanya uchunguzi wa haraka haraka wa kumkagua Roma na uso wake ulikunja ndita.
“Embu subiri kwanza… naona uwezo wako umeimarika sana!?”Aliongea akiwa katika hali ya hamaki.
Roma nae alikuwa kwenye mshangao baada ya kugundua watu hao walikuwa katika floor hio kwa mwaka mzima wakiendelea kupigana.
“Hahaha…Hades wewe mpuuzi muoga muoga umekuja wakati muafaka, usije ukakimbia awamu hii wakati ukijiona unataka kufanya hivyo”
Lekcha alionekana kufurahi mno kama vile ameokota hela na ari yake ya kutaka kupigana ilipanda maradufu , nguvu ya Ant- matter ambayo ilikuwa ni kama mlima iliweza kuongezeka zaidi na zaidi.
Roma alijua wakati huo sio wa kujielezea na aliruka na kwenda kutua upande aliopo Aoiline huku akijilinda na Chaos Cauldron.
“Nitajielezea baadae , kwasasa rekebisha hali yako ya kimwili na niachie nidili na hili”Aliongea Roma.
Aoiline hakuwa msichana mdogo ambaye uwezo wake wa kufikiria ni mdogo , ijapokuwa uwezo wake ulikuwa ukizuiwa na kanuni za kifizikia za ulimwengu huo lakini uono wake haukuwa mdogo.
Hivyo alipanga kumpatia Roma nafasi kudili na maswala yao , isitoshe Lekcha alifika katika ulimwengu huo kwasababu ya ugomvi wake na Roma na yeye ni kama alinunua vita hio.
“Kijana, mimi Master wako nimeweza kushindana na huyu mshenzi kwa zaidi ya mwaka sasa hivyo usiniangushe”Aliongea.
Aoline alimwangalia Roma kwanzia chini na hali isiokuwa ikielezeka ilionekana katika uso wake na aliishia kutoa tabasamu hafifu sana na kisha alisogea pembeni kuangalia pambano.
“Sijawahi kuwaza juu ya uwezo wako lakini ushaanza kuniwazia vibaya , ngoja nikuonyeshe kwamba nilichokuwa nikifanya huko nje hakikuwa kitu cha kupuuzwa”Aliwaza Roma.
Kutoka kuwa chokoraa anaelala chini ya daraja mpaka kuwa mtu mwenye nguvu wa kuweza kushindana na Aoiline kwa zaidi ya mwaka mzima si jambo dogo na Roma alijikuta akimkubali Lekcha bila ya wasiwasi , maana uwezo wake sio wa kawaida.
Wakati Roma akiingia ulimwengu wa majini pepo na kukutana na Aoiline kwa mara ya kwanza alishindwa kabisa kushindana nae , lakini Lekcha aliishi katika ulimwengu huo kwa muda mfupi sana lakini alikuwa ameweza kupandisha uwezo wake kwa viwango vya juu hivyo kwake aliona kabisa hakuwa mtu wa kawaida lakini hata hivyo Roma wakati huo uwezo wake sio wa kawaida na alitaka kumuonyesha Lekcha maana ya nguvu halisi.
Unaweza kusema kwamba Lekcha alifika katika uwezo huo kwasababu ya Roma kumsukumia Kizwe kwake.
Yaani kama Roma asingempa adhabu Kizwe ya kubakwa na machokoraa basi ni hakika Lekcha asingeweza kukutana na Kizwe na hatimae kumuua Yan Buwen na kurithi uwezo wake.
Roma hakutarajia athari ya kile alichokifanya ingemfikisha katika hatua hio, wanasema kila unachokifanya leo kina athari mbeleni na ndio ambacho Roma aliweza kushuhudia na kwa namna yoyote ile kwasababu yalikuwa maamuzi yake wakati ule hakuwa na budi ya kuyakabili matokeo.
“Kwa vyovyote vile kwasababu Mungu amenileta na kukutana nae hapa ,, basi ni wakati wa kuhitimisha huu uhusiano mbaya kwa mikono yangu miwili”Aliwaza tena Roma.
“Inaonekana umekula vitu vingi ndani ya huu mnara”Aliongea Roma akiwa na tbaasamu.
“Kuna haja ya kuuliza , au ndio ushaanza kuniogopa , hivi unadhani mwaka wote niliokuwa ndani ya huu mnara nilikuwa napoteza muda , ijapokuwa nimeshindwa kumuua huyo mbweha lakini ilikuwa ni swala la muda tu .. majani ya kiroho na matunda yaliopo ndani ya huu mnara yamenifanya kuwa wa tofauti kabisa”Aliongea Lekcha akiwa katika hali ya kujiamini kabisa.
“Basi tuchukulie hii ni bahati maana hata mimi nimekuwa wa tofauti kuliko mwanzo , ngoja tuone nani alikuwa akipoteza muda”
Mara baada ya Roma kuongea tu mazingira yaliokuwa yakimzunguka ni kama vile yanaganda na kusababisha msuguano mkali wa elementi za hewa na kufumba na kufumbua radi ya Zambarau ilianza kujitengeneza kama vile ni transfoma la umeme linapiga shoti ambazo ziliruka kwa kunyongorota kama umbo la nyoka.
“Radi ya zambarau!!!”
Aoline ambaye alikuwa akiangalia kwa mbali alimaka huku akiingia katika tafakari nzito, ni kitu ambacho hakutegemea kukiona kwa Roma.
Roma licha ya kuonyesha karata yake hio kwa Lekcha hakubadilika hata kidogo na aliishia kutoa tabasamu la dharau katika uso wake na mkono wake ulibadilika na kuwa kama mkono wa chuma uliotengenezwa na nishati ya Ant- Matter, Shoti za nguvu ile zilikuwa zikitisha mno na ziiongezeka kila sekunde na kutaka kummeza Roma.
Ilikuwa ni sawa kusema mwili wa Lekcha kwa wakati huo ulikuwa ni nguvu ya Ant Matter na ilionekana ni kama vile alikuwa ashapata ufuno wa namna ya kuendeleza kuziongeza maradufu.
Kama sio kwa mnara huo kutokuwa wa kawaida , nguvu ambayo alikuwa akidhalisha Lekcha mnara huo ungekuwa umedondoka muda mrefu sana.
Roma ili kupambana na nguvu ile ya nishati isio maada palepale alibadilisha radi ile na kuwa kama mkuki na kisha alimrushia Lekcha ule mkuki kumchoma.
Nguvu ya radi haikuwa ya kawaida kabisa pia , ijapokuwa nishati ya Lekcha kila ilipokutana na radi ambayo huundwa na maada kulitokea ‘annihilation’ yenye nguvu kubwa kiasi kwamba uwiano ulikosekana.
BOOM, BOOM, BOOM!
Mlipuko mkubwa wa nishati zote mbili kukataana ulikuwa mkubwa mno na ulilipuka katika mfululizo na shambulizi la Lekcha likawa limesabaratishwa namna hio
Lekcha macho yake yalionyesha hali ya kukasirika , hakuamini shambulizi lake hilo ambalo alikuwa ameliongezea nguvu kwa muda mrefu lingeweza kusambaratishwa na nguvu ya radi.
Roma alikuwa mjanja mara baada ya kusambaratisha pigo la Lekcha alikuwa ameongezea nguvu kubwa mno shambulizi lake na mara baada ya mlipuko kutokea mshale mwingine uliweza kutoka na kumpata Lekcha katika kifua na kutengeneza shimo lakini hakukuwa na damu yoyote ilioweza kutokea zaidi ya nishati ambayo iliziba shimo lile haraka sana .
“Hey ..hahaha…Good .. what a powerfull move”Lekcha aliongea kwa kingereza huku akitingisha kichwa chake na kushika eneo la kifua chake ambacho kilitobolewa.
“Inasikisha kwamba huwezi kuniua kizembe namna hii na viradi vyako”
Roma aliishia kukunja sura , aliamini pengine shambulizi la radi lingeweza kumyeyusha lakini ilionekana nguvu ya Ant Matter ilikuwa kubwa mno na kufanya mwili wa Lekcha kuwa na kinga ilio imara.
Lekcha mara baada ya kupona palepale macho yake yalibadilika na aligeuka na kuwa kama lichuma lililotengenzwa kwa uji uji na ilikuwa ni kama mwili wake unaungua kwa shoti na kuzisambaza katika eneo lote.
Roma hakutaka nishati zile kumpata na alijikinga kwa kutumia Chaos Cauldron , chungu kile ni kama kilikuwa kikisubiria fursa hio kwani ile roho ya mnyama iliokuwa ndani yake iliweza kujitokeza kuonyesha ukali wake na kani kubwa ya mvutano ilidhalishwa na kutaka kummeza Lekcha.
“Aaah..ni yale yale , unadhani nitakuogopa kwa kutumia hilo lijichungu lako?”
Lekcha alitoa kicheko kama mwehu na bila ya kukwepa chungu kile alikisogelea na kukivaa na mara baada ya kufikiana na mwili wa Lekcha alilipuka kama bomu la nyuklia.
“Bang!!
“Hoooo…!!!
Ile nafsi ya Chaos ilinguruma kwa sauti kubwa mara baada ya kufunikwa na mlipuko wa nishati ile isiokuwa ya kawaida na kisha kiliachiwa na Lekcha alirudi katika umbo lake la kawaida.
Roma alijikuta akishangazwa na kitu kile , Dhana hio ya Cauldron ilikuwa imeunganishwa na nguvu zake na kama kikipigwa na kuathirika na yeye alikuwa akiumia.
Kilichomshangaa Roma ni mara baada ya roho ile ya mnyama kujificha mara baada ya kuachiliwa na nguvu ya nishati ya ant- matter na hii ilimaanisha kwamba Lekcha alikuwa na nguvu kubwa kiasi kwamba Dhana hio imekuwa sio tishio kwake tena.
“Unashangaa nini wewe ndio unaefuatia baada ya kuharibi chungu chako”Aliongea Lekcha.
Ilikuwa ni muda uleule Lekcha alitengeneza ngome ya nishati ya Ant- Matter na kuifanya iwe ni kama gunia na kutaka kumfunika nalo Roma.
Roma alishangazwa, nishati ile nyingi haikumtoka Lekcha bali ilikuwa ni kama vile ameitengeneza katika mazingira , yaani likuwa ni kama vile yeye alivyokuwa na uwezo wa kukusanya nishati za mbingu na ardhi ndio alichokifanya Lekcha.
“Nenda kuzimu mshenzi wewe”
Lekcha aliongea kwa sauti na palepale lile boma la nishati alilotengeza lilipuka na kuwa kama vile ni fataki na zile cheche zote kumvaa Roma huku zikiwa zimechanganyika na nguvu nyingine ambayo Roma hakuweza kuitambua lakini ambayo ni hatarishi.
Lekcha alikuwa akibweka kama vile alikuwa kwenye maumivu , chuki yake yote ya zaidi ya miaka aliokuwa nayo zidi ya Roma alionekana aliiwekeza katika ngurumo aliokuwa akitoa
Muonekano wake ulikuwa umebadilika kabisa na kuwa kama mtu mwingine na alionekana kabisa alikuwa akipambana kwa ajili ya kulipa kisasi.
Yaani ile hamasa aliokuwa nayo wakati akipambana na Aoiline ilikuwa ni tofauti wakati huo alivyokuwa akipambana na Roma.
Roma hakutaka kuwa mzembe , aliamua kukiongezea nguvu chungu chake na kisha akakipa kazi ya kunyonya nishati ile ya Ant Matter ili kuipunguza nguvu isimdhuru kwa kiasi kikubwa.
Lakini hata hivyo hakikuweza kuimeza yote na pale ilipomwangukia ilimfanya kujihisi ni kama vile anashambuliwa na nyuki.
Maumivu aliokuwa akihisi hapo yalikuwa ni mara mbili na yale ambayo aliyahisi wakati akiwa ndani ya kizimba cha Dhana ya mafuvu na misumari tisa ya Joka.
Katika hali hio ya kupambana na nguvu kubwa hata ule ugonjwa wake ni kama vile umeshituka kiasi cha kufanya macho yake kuanza kubadilika rangi na kuwa ya kijani..
“Arghh…!!”
Roma alitoa mguno mkubwa mno huku mishipa yake ya damu ni kaa vile inataka kumpasuka na mwili wake ulionyesha hali ya kutaka kupitia mabadiliko , ilionyesha ni dhahiri virusi ambavyo vilikuwa vimelala kwenye mwili wake viilitaka kuamka na kumfanya kuwa jitu.
Lakiini hata hivyo lilikuwa shambulizi dogo sana la kuweza kummaliza Roma kwani maumivu yale ni kama vile yalimfungua ubongo na kujikuta akiingiwa na utashi wa kutaka kufanya shambulizi kubwa zaidi.
“Radiii…!!
Roma alibweka na palepale kimbuka cha nishati ya nguvu ya mbingu na ardhi kilijikusanya juu na kugeuka kuwa moto wa zambarau na wa bluu na mara baada ya kuunganika tu radi ilimshukia Lekcha kutoka pande zote na kuanza kupambana na ile nishati ya Ant- Matter.
Roma nguo hakuwa nazo tena kwenye mwili wake na alikuwa yupo uchi kabisa na mwili wake ni kama vile unapigwa na shoti ya radi kwani ulikuwa ukitetema sio mchezo.
Wakati radi ikishambuliana na nishati ile ya nguvu isiokuwa maada Roma alishuka chini kama vile ni kimondo na mara baada ya kujipigiza chini aliweza kutengenza wimbi kubwa mno la nishati ya nguvu za kijini liloambanta na nguvu ya radi na kumshambulia Lekcha kwa chini.
Roma hakuishia palepale alifyatuka kama mshale huku akiwa amekunja ngumi na kumsogelea Lekcha kwa kasi na kumchapa ngumi ya kichwa iliokuwa na uzito wa tani nyingi mno.
“Pfff!!”
Lekcha alijikuta akipokea mashambulizi matatu kwa wakati mmoja na kufanya nguvu yake ya nishati ya anti-matter kusambaratika lakini wakati uleule ikiyeyushwa na shoti za radi.
Roma mpango wake ulikuwa mwepesi , alijua nishati ya Lekcha ilikuwa na kikomo na kwasababu dunia ki asili ni maada basi uwezo wa Lekcha kuidhibiti nguvu hio ilimhitaji uwezo mkubwa hivyo alimshambulia Lekcha kwa kasi kusambaratisha nguvu zake huku akitumia shoti za umeme wa radi kuziyeyusha ili zismrudie.
Mashambulizi yale ya haraka yalimfanya Aoiline aliekuwa akiangalia kwa mbali kuwa katika hali ya kutokuamini kile alichokuwa akiona.
Alikuwa ni jini wa uwezo wa juu sana ambaye alishawahi kuwepo na alikuwa ameona vitu vingi na mbinu nyingi ambazo majini wanazotumia lakini havikumshangaza , lakini upande wa Roma kila alichokuwa akifanya kilikuwa kipya kwake na kumfanya kushangaa.
Unachopaswa kuelewa hata ukiwa ndani ya mnara huo bado sheria za ulimwengu wa mapeppo zilikuwa zikitumika hapo hivyo kufanya uwezo wake kuwa wa chini , lakini sasa kama kwa nusu ya uwezo wake aliweza kupigana na Lekcha kwa mwaka mzima lakini hakufanya shambulizi kubwa kama ambalo Roma amefanya bali alimuona ameimarika nje ya matarajio yake.
Hivyo kimahesabu ni kwamba Roma na yeye alikuwa akitumia nusu ya uwezo wake na moja kwa moja aliona lazima Roma atakuwa amemuacha mbali sana hata kama akitoka katika ulimwengu wa kawaida na kurudiwa na uwezo wake wote.
Mbaya zaidi alichoona ni kwamba Roma anaonekana uwezo wake huongezeka kila ndani ya dakika.
“Huyu kijana ubora na utimamu wa kimwili unafaida kubwa kwake, kautoa wapi huo mwili?”Alijiwazia.
Aoiline aliamini mwili wa Roma ndio chanzo cha kuweza kufunikiwa kwa muda mfupi na alimfananisha na ukoo wa majini joka wa zama zile.
Kadri ambavyo Roma hakuwa akimpa nafasi Lekcha kujikusanya ndio ambavyo alikuwa akizidi kupoteza nishati yake ya Ant- Matter na ilichukua muda mfupi ilionekana Lekcha alibakiwa na nguvu kidogo sana.
Nishati ya Ant matter inaweza kuwa na nguvu lakini ni ghali sana , hii inamaanisha kwamba ni muda mwingi sana unahitajika kwa ajili ya kuikusanya tofauti na nishati ya mbingu na ardhi ambayo mara nyingi haina kikomo ili mradi tu ubongo wako unafanya kazi vizuri, hasara kubwa ya nishati hio ni kwamba asili yake sio ya kidunia hivyo huharibika kwa kasi.
Lakini sasa wakati Roma akiwa na mawazo kwamba amemzimisha Lekcha mpaka kuwa dhaifu Lekcha alirudi katika umbo la kawaida na kumfanya Roma amuone ni kama ndoto ambayo hawezi kuifuta.
Lekcha mara baada ya kurudi katika umbo la mfanano wa kibinadamu alianza kukunja shingo yake kama vile anaweka mwili sawa kana kwamba anamwambia Roma pigo zako ni za kitoto.
“Vipi tena bwana mdogo Roma Ramoni A.k. a Hades dhaifu, hicho ndio ambacho unaweza kujivunia , hii radi yako inaonekana kuwa na nguvu kweli lakini athari zake kwangu ni ndogo”Aliongea Lekcha huku akitoa tabasamu la uovu.
Roma moyo wake ulisinyaa , alidhania akitumia mahesabu ya kikanuni ya nishati ya nguvu hio anaweza kummaliza Lekcha kwa kumshambulia bila kukoma kwa kasi lakini ilionekana kuna kitu ambacho hakukitambua kutoka kwa Lekcha.
“Roma usichokijua na wasichokijua wanasayansi ni kwamba wakati wa nishati ya matter na anti matter zinapogongana hakutokei kitu kinachoitwa Annihilation kama wanavyoamini bali asilimia mia moja kunatokea nishati nyingine yenye tabia tofauti , nishati hii ndio ilionifanya uwezo wangu kuimarika maradufu kadri nilivyokuwa nikipambana na yule Mbweha , bomu la nyuklia ambalo hutengenezwa kwa kurutubisha viini vya atomu ni sawa na asilimia moja tu ya nishati inayotokea wakati wa kugongana kwa nishati hizi mbili , hivyo ninao uwezo wa kuharibu kisiwa kwa kukadiria tu uwezo nishati ninayotaka itokee , sasa hebu jiulize gunduzi yangu hii ndio nataka kuiajaribisha kwako”
Aliongea Lekcha na palepale alitengeneza kitenesi cha nguvu ya nishati ya Ant-Matter na kukirusha aliposimama Roma kwa kasi.
Roma alitaka kutumia Chaos Cauldron kuweza kukijikinga na shambulizi lile lakini Chaos alionyesha hali ya kunywea kutokana na ukubwa wa shambulizi lile.
Roma alijikuta akikosa chaguo lingine na kung’ata meno yake kwa hasira na kisha palepale kwa spidi ya haraka sana alichoropoa lile Shoka kutoka katika hifadhi yake ya pete.
Inasemekana katika ulimwengu wa majini kulikuwa na Dhana kumi na saba ambazo zilikuwa na nguvu sana enzi hizo na kati ya Dhana hizo ni Shoka hilo la Pangea ambalo halikueleweka namna linavyofanya kazi , kuna tetesi kwamba linaweza kuingia katika shimo jeusi la anga na kutoka.
Kitu kingine ni kwamba nguvu yake pia ni kama ilivyokuwa kwa Cauldron, shoka hilo linaonyesha uwezo wake kulingana na uwezo wa mtumiaji. Lakini kitu cha uhakika ni kwamba Shoka hilo lilikuwa na uwezo wa kuchana anga na kwenda kinyume na kanuni za anga.
Katika kanuni za kifizikia kutoka kwa mgunduzi Einstein anasema anga ni kama kitambaa, ijapokuwa hakumaanisha kitambaa kama kitambaa lakini ndio namna rahisi ya kuelewa kwamba anga linaweza kuharibika kikanuni.
Sasa Shoka hilo lilikuwa na uwezo wakuchana hiko kitambaa ambacho ni kama anga sasa kwa kukiuka sheria za anga.
Unaweza kushangaa hizi Dhana zinafanyake kazi lakini teknolojia ambayo ipo nyuma yake ni nje ya uelewa wa fahamu za kibinadamu na hata viumbe wenye akili sana kama majini na hata miungu hawakuwa wakijua siri iliopo nyuma ya uhunzi wa Dhana hizo..
Chukulia mfano safu ya ulinzi ya gereza la Roho katika miliki ya Hongmeng mpaka wakati huo sio Athena wala kiumbe chochote aliweza kujua teknojia ya safu hizo za ulinzi zinafanyaje kazi.
Hivyo hata kwa Roma mwenyewe hakuwa akijua namna Dhana hizo zilivyotengenezwa alichokuwa akijua ni namna ya kutumia tu.
Sasa Roma aliamini kwasababu kanuni za anga hazikufanya kazi vizuri katika ulimwengu huo kutumia Shoka hilo ambalo linaenda kinyume na kila sheria ya asili ndio tumaini pekee la kuhimili nguvu ya Ant- matter.
Kitendo cha Shoka lile kutua katika mkono wa Roma na kuliingizia nguvu za kijini lilibadilika palepale muonekano wake na zile herufi ambazo zilikuwa zimechorwa katika Shoka hilo ziling’aa.
Ijapokuwa lilionekana kama shoka la kawaida lakini uzito wake haukuwa wa kawaida na pengine hata Rose ambaye yupo mwishoni mwa levo ya Nafsi asingeweza kulishika mkononi.
Kwa namna ambavyo liliamshwa na nguvu za mbingu na ardhi za Roma ilikuwa ni kama vile shoka hilo lilikuwa likitawaliwa na nafsi lakini ukweli ni kwamba hakukuwa na nafsi yoyote , ilikuwa ni kama kifaa tu ambacho kimelala na muda huo kimepata nishati na kuingia katika matumizi.
Roma hata yeye ndio inakuwa mara yake ya kwanza kujaribisha shoka hilo na kitendo cha kuamka kwake ile sehemu aliosimama ni kama vile upepo unakimbia , msisimko ulioweza kutoka ilikuwa ni kama vile kiumbe mwenye nguvu sizizokuwa za kawaida anawavamia.
“Arghh…!!!”
Roma alipiga yowe na kwa kutumia nguvu zake zote za kijini aliinua lile shoka juu na kisha akalipigiza chini ndani ya sekunde.
BOOM
Wimbi la nguvu iliotokana na shoka hilo ilikuwa ni kama vile inakwenda kutenganisha mlima wa gereza la nafsi za giza na kuziachia.
Shambulizi lile la Lekcha mara baada ya kugongana na msisimko wa nguvu ya lile shoka mwanga wake ulibadilika katika rangi zisizokuwa zikihesabika na shambulizi lake nikama vile limetumbukia kwenye shimo.
Aoiline ambaye alikuwa mbali aliweza kuhisi msisimko usiokuwa kawaida kutoka kwa nguvu ya nishati ya Ant-matter iliotengenezwa na Lekcha , aliamini kama Lekcha angetumia shambulizi hilo kumshambulia basi angepatwa na majeraha makubwa mno, lakini sasa alishangaa pale Roma akitoa kitu kilichomwacha mdomo wazi.
Licha ya kwamba aliishi miaka mingi hakutegemea kuona Roma angeweza kumiliki kitu cha ajabu kama hicho , alikuwa akisikia kuhusu shoka hilo lakini hakuwahi kuona katika uhalisia.
Unajua bwana majini wengi wana historia kama ilivyokwa binadamu lakini utofauti wa majini na binadamu ni kwamba majini wa zamani walikuwa na akili nyingi sana na kufanya vitu vya ajabu kuliko hawa wa sasa lakini kwa sisi binadamu uwezo wetu wa akili unaongezeka kulingana na muda.
Yaani wakati binadamu akiendeea kutafuta siri za dunia kwa kupanua uwezo wa kufikiria upande wa majini wao wanataka kufikia levo za kufikiria za watangulizi wao.
Sasa katika vitabu vya kihistoria vya majini walikuwa wakisoma uwepo wa Dhana kumi na saba na kati ya Dhana hizo ni Chaos Cauldron , Shoka la kipangea , kioo cha nafsi, Fimbo ya muujiza na zinginezo lakini licha ya kuishi miaka mingi sana hakuwahi kushuhudia hizo Dhana.
Sasa alijjiuliza Roma amewezaje kumiliki Dhana mbili kati ya Dhana kumi na saba za kihistoria. Alijiambia huyu mtoto katoa wapi vitu hivyo.
Lakini licha ya kuwa kwenye mshangao hakuonyesha hali ya kufurahi mara baada ya kuona nguvu halisi ya shoka hilo , hakujali nguvu yake itauathiri vipi mnara lakini alitaka kuona matokeo tu.
Ile sehemu ambayo amesimama Roma kulionekana hali ambayo haikuwa ikielezeka ilikuwa ni kama vile kataratasi ya nailoni linaungua katikati na kutengeneza ufa katikati.
Roma mwenyewe alishangazwa na kitu kile na palepale wazo lilimwingia na kuhamaki na kujiambia kwahio kuchanika kwa anga ndio kupo hivi.
Roma alishangazwa na jambo hio radi yake ilikuwa ikileta machafuko lakini shoka hilo ilionekana ni kweli ilikuwa ikiharibu anga na kumfanya yeye kuwa kati , yaani ni kama lile shoka linaharibu anga na wakati huo huo kunatengenezeka anga lingine jipya ambalo ndio anaonekana yupo yeye sasa.
Roma alijua kabisa anga la ulimwengu huo sio ‘Parallel dimension’ kama ilivyokuwa kwa ulimwengu wa majini watu, bali ni tofauti kabisa ndio maana ukiwa katika huo ulimwengu huwezi kufanya mawasiliano kwa namna yoyote ile na ulimwengu wa kawaida, pili kanuni zake za anga hufanya kazi kitofauti.
Kama anga la uimwengu huo lilikuwa la kawaida basi majini hao wasingeweza kufungiwa kirahisi hivyo.
Moja kwa mmoja ilimaanisha kwamba Shoka hilo lilikuwa na sheria zake za ufanyaji kazi.
Kuna kitu kilikuwa kikimwambia kuna uwezekano wa Roma kubadilisha utendaji kazi wa ulimwengu huo kwa kutumia hilo shoka , ikimaanisha kwamba ameshikilia ufunguo ambao unaweza kuruhusu njia ya kutokea.
Yaani ni kama ilivyokuwa kwa mfalme Wuja mkuu wa majoka kutengeneza Dhana ambayo itakuwa na uwezo wa kutengeneza njia ya kutokea ulimwengu wa kawaida ndio ambavyo Roma alihisi uwezo wa shoka lake ulivyo.
Shambulizi ambalo Lekcha aliamini kwamba linaweza kuharibu kisiwa lilisambatatishwa na Sururu la Roma na moja kwa moja alijihisi kukasirika mno kwani hakutegemea hilo.
“Haiwezekani… Hadae nasema haiwezekani ukapangua shambulizi langu namna nyepesi hivyo”
Lekcha aling’aa meno yake kwa hasira, nguvu yake ya nishati ambayo ilikuwa kama dhoruba baharini ilijikusanya upya katika mkono wake na kwa mara nyingine alijaribu kumshambulia Roma.
Roma baada ya kuona utukufu wa shoka lake hali ya kujiamini iliongezeka na kujiambia yes ni muda wa majaribio na palepale alifyeka anga na shoka lake kutengenza wimbi lingine la mchaniko uelekeo wa shambulizi la Lekcha.
Shambulizi la Lekcha lilikuwa kubwa kweli lakini shoka lile liliteneneza hali ya kuyumba kwa anga hivyo kufanya shambulizi lake kusambaratika , kwa bahati nzuri ni kwamba anga lina nguvu ya kinishati kubwa sana hivyo hata kama shoka hilo lilikuwa na uwezo wa kubadilisha utedaji kazi wa kawaida wa anga ilikuwa ni eneo dogo tu hivyo athari zake zilikuwa katika mzingo mdogo na pia ile sehemu ambayo huonekana kuharibika inarudi upya kwa kasi.
Lekcha alikasirika mno mara baada ya kuona ana mashambulizi yenye nguvu lakini bado hakuweza kumfanya chochote Roma kutokana na shoka lake na aliamua kupotezea kila kitu na kuanza kukusanya kiwango kikubwa cha nishati ya ant matter.
Roma alijua Lekcha yupo katika hali ambayo ni ngumu kumuua , alikuwa ni kama nishati na ili kumaliza lazima kuyeyusha nishati yake hivyo alitumia Chungu , radi na shoka kushambulia kwa wakati mmoja.
Wakati huo ni kama Cauldron imeweza kutambua uwepo wa shoka na hali ya roho ile ya mnyama kujiamini ilirudi.
Wakati huo sasa katika floor hio ukiangalia kwa juu ni kama vile kuna nishati mbili ambazo zilikuwa zikivamiana huku watu waliokuwa wakidhalisha nishati hizo hawaonekani.
Aoiline aliekuwa akiangalia pambano hilo uwezo wake ulikuwa umerudi lakini hata hivyo hakutaka kuingilia.
Sio kwamba hakutaka lakini nguvu ya kimauaji iliokuwa ikimtoka Roma ilimfanya kuona kabisa hana haja ya kuingilia.
Lakini hata hivyo Roma asingependa maana katika maisha yake hakupenda kumtumia mwanamke kama chombo cha mafanikio yake ndio maana tokea amuache Aoiline ndani ya mnara huo roho iikuwa ikimsuta.
Kadri Roma alivyokuwa akishindana na nguvu ile ya Ant-Matter ni kama vile kichwa chake kinakuwa kizito mno kiasi kwamba ule ugonjwa uliokuwa umempotea ulianza kurudi kwa kasi na kufanya macho yake kuwaka taa nyekundu.
Ilikuwa ni kama vile ile nishati ya Ant- matter inashitua hali flani ya utendaji wa mwili wake.





SEHEMU YA 768.
Wakati huo huo vita hio ikiendela katika ngome ya makao makuu ya kambi ya kitafiti ya Zeros organisation alionekana Madam Dyana akiwa na tabasamu la aina yake usoni huku akiangaia kitu kwenye skrini , ilikuwa ni kama vile alitamani kuona kitu cha namna hio kwa muda mrefu.
Dyana ni mwanamama ambae ni Chief wa kitengo cha usimamizi wa maendeleo ya mpango LADO yaani idara ya PLMC.
Kitengo hicho kwa muda mrefu sana kilikuwa kimya sana na hakukuwa na dalili yoyote ya taarifa kutoka kwa ajent wao na hata wale wanasayansi ambao walikuwa wakihusika walikuwa wakilala tu muda mwingi lakini siku hio ilionekana kuwa tofauti katika miezi mingi.
Licha ya kwamba ulimwengu ulikuwa katika hali ya sinfofahamu lakini kazi zilikuwa zikiendelea kawaida ndani ya kambi hio na ukweli ni kwamba ubize ulikuwa umeongezeka kwa kiwango kikubwa sana.
Sasa ni miezi kadhaa tokea Dyana kupokea maagizo kutoka kwa mheshimiwa Barack Mabo.
Unajua katika jumuia yoyote ambayo inahusisha viumbe binadamu lazima kuna wale ambao wana mtazamo tofauti na hio ilionekana ndani ya umoja wa Zeros organisation.
Inaaminika kwamba Barack Mambo ndio moja ya wanachma wa vyeo vikubwa ndani ya jumuia hio ya siri tena akiwa mkuu chini ya The First Black lakini ndio mtu pekee ambaye alikuwa na mawazo tofauti na malengo ya Zeros.
Mpango LADO ni mpango ambao una sahihi yake na sio kwake tu karibia kwa maraisi wote waliopitia katika nyumba nyeupe mpango huo hujumuishwa katika viapo vyao ili kuulinda na kuudumisha.
Ki uhalisia haukuwa mpango mbaya kwani malengo yake yalikuwa wazi , malengo ya mpango LADO hayakuwa kwa ajili ya kumtengeneza ajent mwenye nguvu pekee lakini ukweli ni kwamba ni mpango ambao uliundwa kwa ajili ya kupata binadamu mwenye DNA tofauti, yaani kwa lugha nyepesi kilichokuwa kikilengwa ni kutengeneza kizazi kipya.
Illuminat ndio jamii ambayo ‘ideology’ yake imepewa kipaumbele katika zeros organisation kuliko jamii yoyote ile , waliamini ili dunia izidi kuwa salama kuelimika kwa binadamu lazima kuendane na kasi ya muda na ili hilo kufanikiwa lazima kuwepo binadamu wenye uwezo tofauti wa kufikiria na huo ndio utakuwa mwanzo wa gunduzi mpya tofauti na mwendelezo wa teknolojia zilizopo.
Upande wa Ant-Illuminat wao umoja wao ulianzishwa kupinga ‘ideology’ za Illuminat kwamba ii dunia iendelee kuwa salama maendeleo ya teknolojia yanatakiwa kuendelea katika spidi sawa na ukuaji wa kifikra wa kibinadamu , yaani kusiwe na ‘hacking’ ya aina yoyote ile ya kujaribu kuharakisha ukuaji wa kufikiria kwa binadamu.
Sasa Barack Mabo katika mawazo hayo mawili yeye ni vuguvugu, ikimaanisha kwamba nusu anakubali ajenda za illuminat na nusu anakubali ajenda za Ant-Illuminat na hili ndio ilimfanya kujikuta kuwa na mawazo tofauti.
Kati ya watu ambao anafanana nao kimawazo ni Dyana mwanamama ambaye ndio aliepewa jukumu la usimamizi wa maendeleo ya mpango LADO.
Sasa ni miezi kadhaa tokea yatokee mabadiliko ya hali ya hewa duniani , moja ya watu ambao hawakuwa na utulivu na kile kilichokuwa kikiendelea alikuwa ni yeye.
Na wasiwasi ulimfanya kufanya vikao vingi sana na wadau wengi kuzungumzia kile kinachoendelea na nia halisi ya viumbe hao kutoka sayari nyingne zidi ya binadamu.
Ijapokuwa ni kweli Athena aliwahakikishia kwamba ili kuibadilisha dunia kutoka katika hali ya sasa ya Dystopia na kwenda kuwa ulimwengu wa Utopia kuna kafara itahitajika lakini bado haikutosha kumuamini moja kwa moja na kutokufanya chochote au kutokuchukua tahadhari.
Ieleweke kwamba Athena licha ya kuanzisha umoja huo hakuwahi kujionyesha hadharani na hata pale alipokuwa akijionyesha ni katika hali ya kuogofya pengine hii iliwafanya watu kuwa na imani dhaifu juu ya mipango yake.
Ukweli ni kwamba hakuanzisha Zeros kwa njia ya moja kwa moja bali ni binadamu wenyewe ambao walitoa pendekezo na yeye akaingiza ushawishi wake na mwisho wa siku ikaonekana ni kama yeye alieanzisha.
Sasa Barack Mabo na wanachama wengine walikuwa katika vikao vya kila siku na ajenda kubwa iliokuwa ikizungumziwa katika vikao hivyo ni kufumbua fumbo gumu ambalo Athena amelitega.
Fumbo lenyewe ni kwamba kama Athena alikuwa na nguvu kubwa kwanini akataka mpango LADO kufanikiwa kwa silimia mia moja na kumfanya Roma kuendelea kuwa na nguvu kila uchao.
Yaani viongozi hao na wanasayansi hao waliona kabisa hakukuwa na uhusiano wowote uliopo kati ya mipango ya Athena na kupanda madaraja ya ki uwezo kwa ajent Thirteen.
Athena aliwaambia kufanikiwa kwa Roma ni kwa ajili ya kutengeneza uzao mpya , binadamu ambaye atakuwa na uwezo wa kufikiria tofauti lakini kwanini inaonekana ni kama vile Athena anataka kuua binadamu wote.
Yamkini ni kwamba binadamu hao ambao wanajiita ndio watu waliokuwa karibu na mwishoni mwa piramidi la uongozi wa dunia walikosa majibu , walikosa majibu kutokana na kwamba waliekuwa wakimuuliza maswali hakuwepo na hakujisumbua hata kujitokeza kwao.
Walijikuta kama vile ni viumbe ambavvyo vimetelekezwa kwani hali ya dunia ilizidi kuwa mbaya lakini hakukuwa na majibu kwamba hali hio ingedumu kwa muda gani na matokeo yake ni nini ,walijuliza je hali hio ndio dunia ambayo Athena anataka kutengeneza lakini kimahesabu wanaonna hakuna namna Athena akawa na nia nzuri kwa binadamu.
Mwisho wa maamuzi ya vikao ndio wengine wanashauri kujengwa kwa Safina kuokoa binadamu asipotee , huku kundi la watu wakipinga pendekezo hilo na kutaka kushindana na miungu.
Moja ya watu ambao waliona kujenga Safina sio suruhu ni mstaafu Barack Mabo na kutokana na kuwa na mawazo ya tofauti aliamini mtu mmoja pekee ambaye anaweza kutatua kitendawili kilichokuwa kikiwasumbua wengi ni Hades pekee kwani alikuwa ni nusu binadamu na nusu viumbe hao.
Sasa ule wakati ambao walikuwa wakitamani Roma aingilie kati ndio wakati ambao Roma ametoweka ghafla tu na asijiulikane alipo.
Ni muda wa mchana usiokuwa na jua nchini Marekani , licha ya kwamba dunia ilikuwa katika hali ya baridi kali lakini baadhi ya raia waliokuwa wakijiweza kiuchumi hawakuwa na hali mbaya.
“Dyana nipe ripoti , naamini simu hii sio ya bure kuna matokeo chanya?”Aliongea Raisi Barack Mabo akiwa nyumbani kwake na hio ni mara baada ya simu yake kuita na kupokea kwa haraka haraka.
“Ndio mheshimiwa tumeweza kupata dalili ya mabadiliko ya kimwili ya Ajent 13 na taarifa zimeingia katika mfumo wetu dakika chache zilizopita”
“Nini! Dyana unamaanisha mmepata Hades?”
“Mheshimiwa tokea tuanze kutafuta taarifa za Hades alikopotelea ni leo tu mifumo yetu imeonyesha uhai , vijana walikuwa macho kutokokosa hata viashiria kidogo ndani ya mfumo na juhudi zao za kuwa macho leo hii zimezaa matunda, inaonekana Hades yupo katika hali ya mapambano makali na signal za sayansi ya Devine light zimetuma taarifa hatujui kwa uhakika ni nini kinaendeea na katika lango lipi la anga lakini ni dalili nzuri”Aliongea Dyana na Mheshiimiwa Barack Mabo alionekana kuonyesha hali ya mabadiliko kidogo katika wasiwasi wake.
“Dyana nataka kujua kama Hades anaweza kurudi?”
“Mheshimiwa ili mradi yupo hai naamini atarudi , ndio tegemeo letu kwasasa kujibu maswali ya kinachoendelea, Barrack mpaka sasa umeshindwa kuwaamini watu wa Vatican?”
“Sio kama siwaamini lakini wamekuwa ni watu wa njama sana na mitego , wanasema kuna unabii unaopaswa kutimia ndio maana hawachukui hatua yoyote lakini mpaka leo hii hawatupi maelezo”Aliongea na kumfanya Dyana kutulia.
“China na Japani msimamo wao upoje , nasikia hawakushiriki katika vkao vyote vya kimataifa vya dharula lakini walikuhitaji kama mjumbe wao”Aliongea na kumfanya Barrack Mabo kukumbuka namna alivyofuatilia kikao cha viongozi wa China.
*****
Wiki kadhaa ndani ya Zhongnahai Beijing kulikuwa na kikao kizito ambacho kilihusisha viongozi wote wa juu wa taifa hilo na wale wastaafu waandamizi(Country senior’s).
Kiongozi mkuu namba moja mwandamizi ndio ambaye alikuwa akiongoza kikao hicho , pembeni yake kulikuwa na viongozi akiwemo Li Moshen waziri wa ulinzi , YangChen mkuu wa majeshi , Cai Yuncheng mkuu wa kikosi cha wachawi na Ning Guanyao ambaye ni waziri mkuu hao ni baadhi tu.
Katika watu waliokuwa na wasiwasi ndani ya kikao hicho ni Cain Yuncheng huyu ndie ambaye ni kama anahusika na utendaji wa Hongmeng katika ulimwengu wa kawaida na wasiwasi wake ni kwamba Hongmeng inaweza kukosa nguvu kutokana na kwamba Anjiu mkuu wa miliki ya Xia alikuwa akiwashambulia.
Ijapokuwa baridi ilikuwa kali sana ndani ya taifa hilo lakini China ni moja ya nchi ambazo zina hakiba kubwa ya chakula lakini pia limeeendelea katika urahisishaji wa social service delivery kwa raia wake.
Yaani haikuwa na haja kwa raia kutoka nje kwa ajili ya kwenda sokoni wala dukani bali teknolojia ilirahisisha kazi hio hivyo kufanya nchi hio yenye watu wengi zaidi duniani kwa mara ya kwanza kuonekana kama vile haina watu.
Bila shaka sio kwamba watu wote hawakutoka , kuna wafanyakazi walitoka lakini ilikuwa kwa tahadhari maalumu na hata wale wenye vipato kidogo walikuwa wakisaidiwa.
Baada ya kimya kirefu cha mkuu wa nchi hio hatimae alianza kuongea.
“Hatuwezi kuendelea kukalia mikono yetu zaidi , kwanzia sasa tutajitegemea sisi wenyewe na sio wengine”Aliongea lakini hakuna ambaye aliongea kwani wote walikuwa kimya wakimwangalia , licha ya kwamba dunia ilikuwa katika hali isiokuwa ya kawaida lakini tabasamu halikumtoka.
“Kutokana na janga hili linaloendelea nchi yetu yote na hata kwa binadamu tunapitia changamoto , kama unachochote cha kuongea waziri Ning tafadhari sema, kwanini upo kimya sana siku hizi?”
“Mheshimiwa ulimwengu wa majini sasa hivi upo kwenye machafuko kutokana na vita inayoendelea , miliki ya Xia kwa kutumia watu wao ambao wamefikia levo ya radi wanajaribu kuvamia miliki nyingine , ikumbukwe Xia ipo ndani ya bara la Asia na kwa muda mwingi wamekuwa na wivu na Hongmeng , je uhakika tunao kama wakiiteka Hongmeng hawatotaka kuchukua nafasi yao na kuingilia maswala yetu?”
“Usiwe na wasiwasi , hawawezi”Alijibu Raisi na kisha akaendelea.
“Ijapokuwa miliki ya Xia imepanda na kuwa na nguvu ndani ya ulimwengu wa majini kuliko miliki zote , kutumia nguvu zao kutaka kuingilia maswala ya ulimwengu wa kawaida hakutowasaidia chochote , zaidi ya kujiingiza hatarini kwa kuwachokoza wajumbe wa muungano wa ulinzi wa dunia na ulimwengu wao,sidhani wanaweza kuwa wajinga hivyo”
Mara baada ya kutajwa wajumbe wa ulinzi wa umoja kila mmoja alionyesha hali ya msisimko.
Haikuwa kwa majini tu ambao walikuwa wakijua uwepo wa umoja wa ulinzi wa dunia , ukweli ni kwamba historia hio haijawahi kufutika katika uso wa dunia tokea siku ambayo viumbe kutoka sayari nyingine kutua duniani.
Ni wajumbe hao hao wa umoja ndio waliohusika na ambao waliendelea kushikilia ulinzi wa usalama wa dunia.
Katika hali kama hio ya dunia kuwa hatarini na vilevile kupotea kwa Roma kitu pekee ambacho binadamu wenye kuelewa siri ya uwepo wa wajumbe hao waliomba waingilie kati.
Walinzi wa dunia au The Guardians jukumu lao kubwa ni kuhakikisha dunia inaendelea kuwa salama na wajumbe hao wa ki’umoja hawakujali maswala ya nchi na nchi , ukweli ni kwamba hawakujihangaisha na maswala ya kiserikali ya kibinadamu wala majini.
Hawajali Israeli kumvamia Mpalestina wala Mchina kumvatia Mtaiwani au Mrusi kumvamia Ukraine , ajenda yao kuu ni kulinda uwiano wa usalama wa kidunia hii ikimaanisha katika malango yote ya dunia , iwe ni ulimwengu wa kawaida ama ulimwengu wa ajini pepo au ulimwengu wa majini watu lakini vilevile kuzuia jamii moja ya viumbe kushambulia viumbe wengine.
Majini wa Panas , walitakiwa kubakia Panas na majini wa Xia walitakiwa kubakia Xia na kama wataamua kushambuliana wao kwa wao hakuna tatizo lakini kama watashambulia binadamu na kutaka kuteka nchi ndio tatizo hutokea ambalo lilipaswa wajumbe hao kuingilia.
Lakini kilichokuwa kikiwasumbua sio serikali ya China tu bali serikali zote ambazo ziikuwa zikijua historia ya uwepo wa watu hao ambao haikueleweka ni majini , binadamu au malaika ni kwamba hawajui walikuwa na ajenda gani na pili hawafahamika kwa sura ni wakina nani na wanatokea nchi gani au wanaishi nchi gani.
Inasemekana ni matiafa makubwa duniani tu ambao wameweza kukutana na mmoja ya wajumbe hao yaani Mkuu namba moja na mara nyingi alijitokeza kwao kwa ajili ya kutoa onyo tu na haikuwa vinginevyo.
Nchi pekee ambayo ni ndogo na mkuu namba moja alijitokeza kwa kiongozi wake ni Rwanda tu na hio yote ni kutokana na Jeremy kushikirikiana na miliki ya Panas kutaka kuingilia maswala ya kibinadamu,
Mtu binafsi tu ambaye aliweza kukutana na mkuu namba moja ambaye huunda baraza la usalama wa ulimwengu ni Roma pekee.
Ki ufupi ni kwamba Master Namba moja mwenyewe alikuwa na nguvu sana kiasi kwamba alikuwa na uwezo wa kukutana na raisi wa Urusi kwa kutumia sura ya Singanojr na vilevile akakutana na raisi wa Korea Kaskazini kwa sura ya mtu mwingine , ili mradi amefikisha ujumbe haikujalisha ni sura ya nani inatumika.
Sasa Raisi wa China na baadhi ya watu tofauti tofauti ndio walijua siri hio ya uwepo wa hivyo viumbe lakini hawakujua ni wakati gani watachukua hatua hivyo tofauti na kusubiri waendelee kuteseka ni bora kujitegemea wao kwa wao.
Wakati kikao hicho kikiendelea upande mwingine Raisi Barack Mabo alikuwa akifatilia kila kitu, ni kama alipewa ruhusa ya kuangalia namna kikao hicho kinavyoendelea.
Ukweli ni kwamba Raisi Barak Mabo alikuwa akiamini kwamba wajumbe hao wa ulinzi wa dunia walikuwa na mawasiiano na taifa la China na hio yote ni kutokana na uwepo wa Hongmeng lakini matokeo yake ni kwamba hata raisi mwenyewe wa China hakuwa na mawasiliano nao lakini licha ya hivyo Barack Mabo hakumuamini na ndio maana mheshimiwa alimpa nafasi ya kuangalia kikao chake na vongozi wake waandamizi ili aweze kuamini maneno yake.
“Mheshimiwa dunia nzima ipo katika hili janga la baridi na miungu wanaendelea kutukandamiza , Hongmeng ambao ni tegemeo letu wenyewe wapo na matatizo , je hakuna uwezekano wowote wa hawa walinzi kutusaidia ?”Aliuiza mkuu wa kikosi cha uchawi.
“Bado hamjanielewa tu nilichojaribu kuwaelezea..?”Aliongea na kisha akawaangalia mmoja mmoja na kisha alivuta pumzi na kuendelea.
“Sio mimi tu ambaye nimejaribu lakini wenzangu wengi wamejaribu lakini hakuna uwezekano wowote ambao nimeweza kuwasiliana nao”
“Kwaho hii inamaanisha hawana mpango wa kusaidia binadamu?”Aliuliza Ning.
“Hilo sijui lakini na wenyewe wana falsafa yao mpaka kuamua kuingilia maswala ya kibinadamu, pengine wanaona dunia haipo hatarini”
“Hawana lolote hao nina uhakika wanawaogopa miungu”Aliongea waziri mkuu Ning kwa hasira.
“Waziri chunga mdomo wako”Aliofokewa na mheshimiwa Raisi
“Kila kitu kinatokea kwasababu maalumu mheshimiwa waziri , mzunguko wa kimaisha unatafsiriwa kutoka kuzaliwa mpaka kufa , uwezekano wa hawa watu kuwepo ni kweli lakini haijalishi kama wapo au hawapo , hatua ambayo binadamu tumefikia haijatokana na wao , ni kwa maarifa yetu na upumbavu wetu wenyewe , dunia ilipofikia sio kwa msaada wa kiumbe chochote bali ni sisi binadamu wenyewe na ndio sisi ambao tunapaswa kuipambania kurudi katika hali yake ya kawaida”Aliongea mkuu wa majeshi.
“Mr Yang upo sahihi katika hali kama kila taifa linataka kujitegemea hatuna budi na sisi kujua namna ya kujilinda”
Kwa mheshimiwa Barack Mabo ilikuwa ni kama vile anaangalia filamu , alichokuwa akitarajia hakukipata ijapokuwa kwa namna flani alijua ni kweli kuna uwepo wa hao viumbe lakini bado hakuamini.
Na swali hata yeye kwake lilibakia je ni kweli kama inavyosadikika kwamba kuna viumbe wasiofahamika wanaojiita walinzi wa dunia kama wapo ni lini watajitokeza na ni viumbe wa namna gani.
Mpaka mwisho hakuwa na majibu na alijikuta akirudi nchini kwake akiwa mnyonge.












SEHEMU YA 768.
Ilikuwa ni vita ya wanaume wawili na ingekamilika vizuri kama mmoja kati wao angeshinda bila kuongezewa nguvu ndio maana Aoiline hakutaka kuingilia.
Vita hio ya Roma na Lekcha ilikuwa sio ya kawaida kabisa iliojaa mizungusho , kurushiana makombora ya nishati na kuoteana.
Radi ya zambarau na bluu ndani ya mnara huo ilikuwa ikipiga mara kwa mara lakini katika floor hio ya kwanza haikufika
Roma alizidi kuwa jasiri kila sekunde ilivyokuwa ikisonga na alijiua licha ya kwamba akili yake ni kama vile imetawaliwa na mdudu na kufanya macho yake kubadilika rangi mara kwa mara lakini uungu wake ulikuwa imara mno na haikuwa kama kipindi cha nyuma ambapo hakuweza kujitawala kiakili.
Roma aliweza kuhisi mwili wake ukipitia maumivu mara baada ya kupigwa na mlipuko wa nishati ya ant-matter na kuhisi kupoteza kiasi flani cha nguvu ya nishati ya mbingu na ardhi lakini hata hivyo alijiponyesha kwa haraka sana.
Kwa jinsi mwili wake ulivyokuwa ukifanya kazi , illikuwa ni kama vile alikuwa na mawasiliano na kila kiungo cha mwili , hata pale seli ambazo zilikufa na kujitengeneza zingine ni kama vile alikuwa akijua kinachofanyika.
Hisia za namna hio katika wakati huo zilikuwa ni za kipekee sana na ilimfanya kuhisi ulimwengu uliokuwa mbele yake ulikuwa sio , ilikuwa ni kama vile yupo katika lango jipya la anga.
Kila kitu ambacho kilionekana kuwa halisi katika macho yake ni tofauti..
“Hahaha…”
Roma wakati akiwa anahangaika ni kama vile alipata utashi flani hivi uliomfanya kucheka na hakujua hata ni kwa namna gani alisogea na hakujali ni shambulizi gani ambalo Lekcha atampiga nalo.
Kwa wakati huo upande wa Roma vita hio haikuwa ya kifo na uhai bali furaha mpya ili ujaza moyo wake, ni kama vile alikuwa akifurahia kinachoendelea katika wakati huo.
“Mvulana mjinga huyu … anacheka nini sasa”
Hata kama uwezo wa kufikiria wa Aoiline ni mkubwa kuliko wa Roma lakini hakuweza kuelewa ni kitu cha namna gani Roma alikuwa akipitia , hakuelewa hisia zake zilikuwa zikimaanisha nini.
Baada ya muda mfupi Aoiline alikunja ndita na aliangalia juu katika sehemu walipokuwa wakipambana Lekcha na Roma.
Kipande cha anga katika eneo waliopo ni kilikuwa kikiharibika kwa kasi , kwa macho ya kawaida unaweza usione kinachoendelea lakini kwa macho ya kijini au ya kiuungu lazima uone kinachotokea na kufanya nishati ya Ant-Matter aliokuwa akizalisha Lekcha kuwa na mawasliano na ulimwengu wa nje ya mnara hhuo.
Ilikuwa ni mnara huo umetengeneza ufa ambao ulikuwa ukipitisha hewa kwa juu.
“Hii nii…”
Aoiline aliwaza lakini macho yake yalichanua kama vile alikuwa ametegemea kitu ambacho kinakwenda kutokea.
Roma ambaye alikuwa akipambana na Lekcha alikuwa akicheka kama vile ni kichaa na uso wake ulikuwa umejaa hali ya kujiamini, hali flani ya utambuzi na ukuu kama vile ni mtawala mbele ya watawaliwa.
Lekcha ambaye alikuwa akipambana na Roma alijikuta akikasirika sana mara baada ya kutumia njia zote kujaribu kumfikia Roma kimashambulizi na kushidwa , kilichompa kero zaidi moyoni ni namna ambavyo Roma hakumchukulia siriasi.
“Siwezi kushindwa , siwezi kushindwa nimetoka mbali kufika hapa siwezi kushindwa leo , lazima nikumalize leo Hades”
Lekcha alibwatuka kama vile ni kichaa lakini sauti yake ilimezwa na ngurumo ya radi kubwa sana ambayo ilisikika kutoka nje ya mnara.
BOOM!!
Ilikuwa ni sauti kubwa ya kuumiza masikio ambayo ni kama vile mnyama ananguruma katika lindi la ukiwa wa milele au kama vile ni Mungu anafungua makufuli ya mateso k wa viumbe wake binadamu.
Ilikuwa ni ngurumo ambayo haikuwa ya kawaida , ambayo kwa haraka haraka haikuwa na asili ya mnara huo na kufanya waliokuwa wamesikia ni kama vile masikio yao yanasikia Kengele ya tahadhari .
Na ile sehemu ambayo walikuwa wamesimama Roma na Lekcha palikuwa na tundu ambalo limejitokeza kwa juu kupitia kwenye ule ufa ambalo lilikuwa na mawasiliano na ulimwengu wa nje.
“Hio ngurumo ya Dhiki ya mapigo elfu moja ya radi!! , Aisee huyu mtoto hazuiliki , kijana umefanikiwa vipi kuelewa haraka hivi tamaduni zetu na kupanda levo kila unapokuwa kwenye changamoto?”
Ailione ambaye alikuwa tayari amekwisha kupitia adhabu ya mapigo mengi ya radi alikuwa akijua kani ya radi ya mapigo mengi , alikuwa amepitia adhabu ya mapigo zaidi ya elfu moja hivyo asingeweza kushindwa kujua kinachoendelea.
Lakini sasa umri wa Roma ni miaka ishirini kwenda therathini kitu ambacho sio cha kawaida kwa umri huo kuweza kusababisha radi ya mapigo mengi.
Alijiambia mtoto huyo ambaye alionekana kuwa na tamaa ya pesa na maisha ya anasa haijalishi nini amefanya au wapi ametokea uwezo wake wa kutambua siri za mbingu na ardhi ni mkubwa mno kiasi kwamba unamfanya yeye mwenyewe kuona wivu.
Lekcha alijikuta akihamaki kwani hakutgemea mabadiliko ya namna hio.
Alikuwa akielewa kuhusu radi na mateso yake tokea siku ambayo aliweza kuuvaa mwili wa mkuu wa majoka mfalme Wuja , ijapokuwa alikuwa akijiamini kutokana na nguvu yake ya nishati ya Ant -matter lakini hakuwa na uhakika kama anaweza kupona kama atapigwa na radi ya mapigo elfu moja.
“Muda wowote radi itafika ndani ya hili eneo , je bado unataka kuendelea kushindana na mimi?”Aliuliza Roma huku akiona ishara ya wasiwasi kutoka kwa Lekcha
Lekcha alijikuta akiona ni kama vile anadhalilishwa na aliishia kutoa tabasamu la kejeli akionekana hataki kushindwa.
“Inaonekana umekasirisha anga na muda wowote radi inakuja kukupa adhabu yako ,hivi wewe mwenyewe unao uwezo wa kupona kabla ya kuniuliza , nina ngungu ya ant-matter ambayo inawea kulinda mwili wangu , unadhani radi hio itaweza kunifanya nini?”Aliongea Lekcha kwa kujiamini.
Roma hakuwa akipanga kumkasirisha Lekcha ukweli ni kwamba alijua kumdhibiti Lekcha lilikuwa ni swali la muda tu.
Hata kama hatomuua Lekcha Roma bado alikuwa na uwezo wa kutumia shoka lake na kumfungia katika space crack au kumpoteza mazima katika malango ya anga.
Lakini kwasababu Lekcha alionekana kuwa na hamu ya kupitia uzoefu wa nguvu ya radi akiwa na yeye hakuona haja ya kumjali
Mara baada ya kusita kidogo palepale alikiita chungu chake cha maafa kwa mara nyingine lakini hakutumia kwa ajili ya kujikinga na radi ambayo inatarajia kushuka alisimama na kisha alikizibia na mwili wake
Yaani alichokifanya Roma ni tofauti kabisa na mwanzo , kwani ili kupita dhiki hio ya mapigo mengi alitakiwa kukiweka chungu hicho juu ake kama kinga lakini awamu hio ni kama anakilinda chungu hicho na radi.
Kitendo kile kilimfanya Aoiline kuwa katika hali ya mshangao na alitaka kumuuliza Roma anajitafutia kifo lakini mara baada ya kufikiri kwa haraka alioneakna kupata wazo ambalo Roma anajaribu kufanya na macho yake yalijaa mshituko na kuamua kukaa kimya akitarajia namna Roma anavyokwenda kupita dhiki hio.
Upande wa nje mnara wote ulifunikwa na dhoruba ya wingu zito mno kiasi kwamba ni hakika wale ambao wapo karibu na mnara huo wasingewea hata kuuona kwani ulifunikwa mpaka kwenye maji na ni cheche tu na ngurumo ambazo zilikuwa zikisikika.
Katika ile floor ambao walikuwepo Roma ile ufa ambao umejitengeneza ulionekana muda wowote unakwenda kuporomoka kutokana na presha ambayo inajiandaa kuingia ndani.
Hali ya giza ilizidi kuongezeka ndani ya mnara na hakukuwa na mwanga tena kama mwanzo.
Roma upande wake hakuwa na muda tena wa kumfirikia Lekcha , ukweli ni kwamba aliacha kabisa kupambana nae.
Kulikuwa na nafasi ndogo sana kwa Lekcha kuweza kukwepa radi ile kwani alikuwa amekaribiana sana na Roma.
Ilionekana ni dhahiri baada ya Dhiki hio ambaye atafanikiwa kutoka hapo wa kuipita hio dhiki basi moja wa moja anaweza kuwa mshindi.
Boom!!
Palepale mwanga ulionekana ndani ya eneo lile mara baada ya shoti ya radi iliokuwa katika mwanga wa rangi ya fedha(silver), yaani ni mwanga ambao haukuwa mweupe sana wala mweusi sana.
Shoti ile ilianza kidogo kidogo na kwa nje ilikuwa ni kama vile anga linashambulia ule mnara na radi na kutaka kuangusha kwani wingu lilikuwa likizunguka kwa kasi kubwa mno , ni kama vile kuna panya yupo shimoni na paka anatafuta namna ya kupita ndo ilivyokuwa kwa namna wingu hilo lilivyokuwa likizunguka kupata upenyo wa kumpa Roma anachostahili.
Kitendo kile kilifanya mnara wote kuwa na hali flani ya umeme ambao ulikuwa endelevu , yaani ni radi ambayo haikukoma ni kama vile umeme umewashwa kutoka mawinguni na kuingia ndani ya mnara huo.
Upande wa Roma na Lekcha walikuwa wamefunikwa na shoti za radi ambazo ni kama hazina mpango wa wa kuwaachia na kuwafanya hata miili yao isionekane.
Zile nguvu za nishati ya Ant-Matter ambazo zilikuwa zimesambaa zote ziliyeyushwa na shoti za radi na kupotea mara moja , ikionekana kabisa hakuna uwezekano wa kuhimili nguvu yake.
“Arghhhh…uwiii!!”
Lekcha alipiga yowe kubwa mno la kilio cha kusaga meno na hio yote ni kutokana na kuyeyuka kwa kasi kwa nishati yake ya Ant Matter na kugeuka mvuke ambao ulipotelea angani. Alikuwa akibabuka kama vile ni magamba ya mti.
Upande wa Roma hakuonyesha ishara yoyote kama alikuwa akipitia maumivu .
Ukweli ni kwamba ile radi ilikuwa imemfunika Roma sio kwamba ilikuwa ikimshambulia lakini ni kama vile ilikuwa ikimzingira na kushidwa kupita katika mwili wake hivyo kutokumsambabishia maumivu yoyote.
Ilikuwa ni kama vile inamuogopa Roma kumshambulia kabisa tofauti na ilivyo kwa Lekcha.
Katika mkono wa kulia wa Roma alikuwa akibadilisha kwa kiwango kikubwa nishati za mbingu na ardhi na kutengeneza moto wa rangi nyeusi huku mkono wa kulia alikuwa ametengeneza kiwango kikubwa cha moto wa rangi ya bluu.
Moto ule ulikuwa ukimzingira na kutengeneza kitu kama gamba la radi ya rangi ileile ambayo ilikuwa ikisukumana na ile ya radi ya Dhiki.
Yaani ilikuwa ni kama vile nguvu ambayo Roma anadhalisha ilikuwa ikikataana na dhiki ile ya radi ndio maana ilitengeneza ‘magnetic field’ ambayo ilifanya radi ile kumzunguka Roma na kutokumgusa.
Ushawahi kuona filamu ambayo binadamu yupo msituni na anakutana na Dubu na yupo katika hali ya kutoweza kukimbia na anafumba macho kusubiria kuraruliwa na lile Dubu lakini ajabu mnyama yule aina ya Dubu anapiga magoti na kukusujudia basi hali hio ilikuwa ni kama vile kwa radi ile ya mapigo mengi.
Kitendo cha Roma kudhalisha moto mweusi na bluu na kisha kuunganisha kulimfanya kuweza kutengeneza radi yenye tabia sawa na ile ya Dhiki na kumfanya isihindwe kumsogelea.
Kifizikia kilichokuwa kikitokea ni sheria ya Ki’Electrostatic , sheria ambayo inaelezea kwamba kunapotekea chaji mbili zinazofanana ziwe aidha ni chanya au hasi ili mradi ziwe zimefanana basi zitakataana na kama zikitofautiana zitavutana.
Kwa lugha nyepesi ni sawa na kusema hakuna mvutano wowote kati ya mwanaume na mwanaume bali kuna mvutano mkali ambao huleta madhara pale mwanamke na mwanaume wanapokutana sasa chukulia radi aliotengeneza Roma ni radi dume na iliotaka kumuadhibu ni radi dume pia hivyo ki asili zitakataana.
Sasa ni kwamba kabla ya radi hio kushuka Roma alishajua kwamba akiunganisha elementi za moto mweusi na moto wa bluu atatengeneza shoti ya radi ya rangi ya fedha ambayo ndio rangi hio hio ya Dhiki.
Unachopaswa kuelewa ni kwamba radi ya mapigo tisini na tisa ilikuwa na rangi yake na radi ya mapigo tisa ilikuwa na rangi yake vilevile na radi ya mapigo mia tisa tisini na tisa ilikuwa na rangi yake vilevile.
Utofauti huu wa rangi inamaanisha namna inavyotokea kuna utofauti mkubwa wa elementi za chaji.
Roma hakuhitaji chungu kujilinda na radi tena hio yote ni kwamba anao uwezo tayari wa kutengeneza radi ya rangi ya silver kwa kuunganisha moto wa rangi nyeusi na moto wa rangi ya bluu na matokeo yake ni kwamba akawa anafanana na radi ya mapigo mia tisa tisini na tisa na kama sheria kifizikia ya asili inavyosema radi ile ilimtambua Roma kama mwenzake kutokana na kudhalisha nguvu inayolingana na kwake na matokeo yake ilishindwa kumdhuru.
Upande wa Lekcha yeye ni kama vile alikuwa Chanya na radi ilikuwa hasi na sheria ya asili inaelezea kwamba ikitokea nguvu mbili hazifanani basi zitavutana na ikitokea hizo nguvu mbili moja ni dhaifu basi itamezwa na ile iliokuwa na nguvu.
Hivyo ant Matter ilikuwa ni dhiafu na radi ilikuwa na nguvu hivyo moja kwa moja nishati ile ilifunikwa.
Radi ile ilikuwa ni endelevu , pengine ni aina ya radi ambayo binadamu wa kawaida hajawahi kuishuhudia na kadri ilivyokua ikiendelea kushambulia upande wa Roma alikuwa akipitia steji mbili muhimu sana ambayo ya kwanza ni Soul Evolution(Kukua kwa nafsi) na pili ni Soul Cleansing(Usafi wa nafsi) ambazo steji hizi zote mbili ukiziunganisha majini wanaita Ubatizo wa moto wa mbingu(heavenly fire baptism) ama ubatizo wa radi katika lugha ya kibinadamu.
Ukumbuke majini hawaiti radi kama radi bali kwao radi ni sawa na moto wa mbingu au moto wa Mungu na wao wanaamini kwamba moto wa mbingu ndio huwatengeneza au ni kama chanzo cha kukua kwao.
Katika hatua za juu kabisa za uwezo wao au unaweza kusema levo ambazo majini wa viwango vya juu sana ambao walipitia ni katika hatua ya ubatizo wa moto wa mbingu.
Lakini sasa tokea enzi zile hakuna jini ambaye ashafanikisha kupitia hatua ya ubatizo wa moto.
Roma hakupata faida ya kusafishwa kwa nafsi au kukua kwa nafsi pekee bali pia alipata usafisho wa mwili , yaani ni kama vile mwili wake uliondolewa kitu ambacho kilikuwa kikimsumbua kwa muda mrefu na kumfanya kuzidi kuwa imara.
“Hatimae imetokea… huyu mtoto amekwisha kupata ufunuo wa radi ya mapigo mengi na namna unavyotokea , hii radi ya kimungu haina tena madhara kwake zaidi ya kuwa ndugu aisee sijatarajia baada ya maisha yangu marefu kushuhudia kitu cha namna hii”Aliongea Aoiline mwenyewe .
Huku hisia mbalimbali zikipita katika moyo wake , ilionekana kwamba ukiachana na Roma kuweza kujua siri ambayo ipo katika adhabu ya mapigo tisini na tisa ya radi lakini pia alikuwa amefahamu siri iliopo nyuma ya mapigo mia tisa tisini na tisa ya radi.
Kwa mtu wa kawaida anaweza kusema kwanini majini waogope radi ilihali Roma anaweza kuwaambia siri ya radi hizo lakini ukweli ni kwamba ili waweze kufanikisha hilo lazima wakaanze moja katika hatua za uvunaji wa nishati za anga kwa kutumia mbinu ya andiko la urejehso.
Roma aliweza kudhibiti siri ya radi hizo kutokana na kwamba alikuwa amepitia njia ndefu ya mafunzo hayo ambayo ndio kama msingi na hii ilimpelekea kuwa na uwezo wa kutengeneza moto adimu sana ambayo una elementi zote za kutengeneza radi , mfano wa moto wa bluu , maji ya kiroho na moto mweupe.
Siraha za namna hio ni majini wachache sana ambao wanaweza kutengeneza au hakuna kabisa ndio maana tokea mwanzo miliki zote za majini watu zilikuwa zikimuwekea Roma njama ya kutaka kumpa siri hio.
Ikumbukwe kwamba katika hatua za andiko la urejesho mbinu ya hatari zaidi ni ile ya kufa na kufufufuka , yaani steji ya kifo na uhai.
Kwahio basi mpaka muda huo Roma aliweza kupitia hatua muhimu ambayo ya kwanza ni mapigo tisa ya radi ambayo steji hii alitumia uwezo wa mwii wake kujiponyesha kwa haraka na andiko la urejesho , hatua ya pili ya dhiki ni mapigo tisini na tisa ambayo aliyapata katika mnara huo wakati wa kutoka kwa msaada wa Cauldron na hatua ya tatu ni mara baada ya kumshuhudia Anjiu akipitia levo ya mapigo ya radi alikuja kufahamu siri ya kutengeneza radi ya zanbarau na hatua nyingine ni hio ya sasa ya kupitia mapigo mia tisa tisini na tisa lakini awamu hio hakuumia zaidi ya kwamba aliidhibiti ile radi kwa kujifananisha nayo ili sheria ya asili(law of nature) ifanye kazi.
Wakati Roma akifurahia namna ambavyo radi ya mapigo mengi ilivyokuwa ikimzunguka na kuendelea kunyonya nishati yake Lekcha yeye alikuwa katika kilio cha kusaga meno.
Ilikuwa ni ngumu sana kwake kujiokoa katika hali ambayo alikuwepo , iapokuwa radi ya Zambarau ilikuwa na uwezo wa kuharibu mwili wake lakini ukubwa wa nguvu ya ant matter iliuwa na uwezo wa kumrejesha lakini awamu hio radi ya rangi ya fedha haikuwa mchezo kabisa , sio tu kuharibu mwili lakini pia ilianza kuharibu na nafsi yake.
Haikujalisha nishati ya Ant Matter ilikuwa na nguvu namna gani lakini hakuweza kulinda kitu muhimu sana ambacho ni roho au nafsi , ilimaanisha kwamba Lekcha alianza kukosa ufahamu wa kujiendesha na kuwa kichaa na kadri sekunde zilivyokuwa zikisonga angepotea moja kwa moja.
Alijitahidi kukusanya kiwango kikubwa cha nishati kulinda roho yake lakini hakufua dafu kwani nishati yake ilikuwa na kikomo lakini kwa mapigo elfu moja ya radi hakukuwa na kikomo cha ukubwa wake.
Aliweza kuona kabisa nguvu ya radi hio ilikuwa ni kubwa sana kiasi kwamba hawezi kuvumilia tena na kifo kilikuwa kikimsogelea kwa kasi ya 5G.
BOOM
Awamu ya pili kubwa zaidi ya pigo la radi ilishuka , haikueleweka pigo moja lina uzito wa nguvu kiasi gani kukamilisha hesabu ya 999 lakini ni dhahiri mapigo yasingekuwa moja moja.
Roma alikuwa katika hali ya furaha ya ubatizo wa radi hio na mabadiliko ya kiakili aliokuwa akipitia ilimfanya kumpotezea kabisa Lekcha aliekuwa akilia kama mtoto.
Ajabu ni kwamba ni nje ya mahesabu ambayo Roma alitarajia kwani alipitia mapigo matatu tu ambapo kila pigo moja lilidumu kwa dakika kumi na tano.
Haikueleweka ni kwa namna gani majini waliweza kutoka na hesabu ya mapigo tisini na tisa katika awamu tatu lakini kutokana na ukubwa wa radi hio na nguvu yake Roma aliamini inawezekana awamu tatu kukamilisha mapigo yote mia tisa tisini na tisa.
Mara baada ya dakika kumi na tano kumalizika za pigo la mwisho hali ya hewa ilirudi katika hali yake ya kawaida kwa kasi sana.
Na hata ule mwanga wa rangi ya silver ambao ulidumu ndani ya mnara huo kwa dakika arobaini na tano ulirudi katika hali ya kawaida.
Hali ya hewa ndani ya mnara huo ilikuwa ni harufu flani hivi kama ya baruti iliochanganyika na kuungua kwa mimea na kuyeyuka kwa baadhi ya dhana zilizopo ndani humo.
Roma alivuta pumzi nzito na kisha alishuka taratibu na kukanyaga floor hio ambayo ilikuwa imepata moto , chungu cha machafuko kilimzhuguka Roma kwa namna flani hivi ya kumlaki kikimuelezea kwamba licha ya kumkinga na radi lakini pia kimefaidika .
Roma palepale aliamua kuficha Shoka lake la kimaajabu na chungu kile kwani hakuwa na uhitaji navyo kwa muda huo.
Mwili wake ulikuwa ukitoa harufu flani hivi isiokuwa ikielezeka lakini kwa mbali ni kama vile kuna cheche za shoti zilizokuwa zikionekana katika mwili wake uliokuwa umetuna kwa mazoezi.
Hakuwa na nguo hata moja wakati huo alikuwa uchi wa mnyama na kwanzia vidoleni mpaka chini alikuwa akitoa shoti za umeme na ilikuwa ni kama vile mwili wake unapo kwani shoti zile zilikuwa zikififia.
Roma alishangazwa na nguvu ya radi hio lakini alijua kabisa hapo sio mwisho , inasemekana majini wa enzi hizo walipitia mpaka hatua ya mwisho kabisa ya mapigo 9999 , sasa alijiuliza kama ni hivyo waliwezaje kupita hatua hio au na wao walikuwa kama yeye tu walijifananisha na radi hio na matokeo yake radi ilifuata kanuni ya asili.
Roma mara baada ya kuwaza kwa muda hatimae sasa akili yake iliwaza kuna Lekcha na aligeuka palepale na alipoangalia sehemu Lekcha alipo aliona vijicheche kwa mbali ambavyo vilikuwa vikipotelea.
Kama ilivyo kwa Roma mwili wake kupoa upande wa Lekcha alikuwa amerudi kawaida na mwili wake ulikuwa umepoa kabisa kwa kupoteza nishati yote ya Ant-Matter.
Ilionekana radi yote ilikuwa imekula nishati yake na kumbakisha mweupe na kuwa kama binadamu wa kawaida tu.
“Hukutakiwa kuwa na kiburi…. Vinginevyo ungeweza kupata nafasi ya pili , isitoshe mwili wako unaonekana kutokuwa wa kawaida”
Roma aliongea huku akitembea kumsogelea Lekcha aliekuwa akitetemeka kama vile mgonjwa wa Malaria kali.
Lekcha aliepiga goti alijikuta akivuta pumzi nyingi na kisha kwa unyonge aliinua kichwa chake , alikuwa amefubaa kama karatasi lakini hata hivyo hakupoteza ile hali ya ukejeli kwenye uso wake , ilikuwa ni kama vile hakujali tena kifo.
“Acha kunionyesha hio tabia yako ya kujiona unajua kila kitu , hivi unajua kinachonifanya kukuchikia zaidi ni nini , kinachonifanya ni kuchukie sana ni tabia yako ya majigambo”
“Inaonekana una chuki binafsi zidi yangu lakini niwe tu mkweli sijawahi kukuchukulia kama tishio kwangu lakini hata hivyo umenishangaza , sijui kuhusu mengine lakini kitu ninachojua ni kwamba sijali namna yoyote ile unavyonifikiria”
“Hahahaha… , kwaio ndio unajigamba , naona mwishoni nimekushindwa kama alivyoshindwa yule mjinga Yan Buwen na mjinga wake Denisi , mpaka mwishoni inaonekana hakuna ambaye anakuweza na yamkini hapo mwenyewe unajihisi sio wa kawaida lakini Roma ngoja nikuambie kitu , mimi Lekcha a.k.a Joseph Bikindi hujanishawishi juu ya uwezo wako wala siwezi kukubali, hata kama nikifa siwezi kukuruhusu ujione shujaa au kukufanya ufikirie umeniweza .. kitu pekee ambacho kimenifanya kuwa katika hali ya kushindwa ni bahati basi , najiuliza kwanini sikuwa na bahati ya kupata fursa ya kukutana na master ambaye ni mzuri kwangu , kwanini niligeuzwa na kuwa mtumwa , kwanini kuna watu nyuma yako ambao wapo tayari kukusaidia ,, Hades umefanikiwa hayo yote kwasababu bahati ilikuangukia na ukawa upande mzuri , tokea ulivyozaliwa Mungu alishakuandikia utafanikiwa kwa kutuchukulia sisi kama ngazi , lakini hebu jiangalie sasa hivi unavyojiona mwenyewe, sio juhudi zako pekee zilizokufikisha hapo mwanaharamu wewe”
Lekcha alitumia kadri ya uwezo wake wote kuongea kwa sauti lakini hata hivyo sauti yake ilionekana kunyongea sekunde hadi sekunde.
Roma aliishia kucheka kivivu kama vile ashajichokea hata kumgusa Lekcha lakini hata hivyo hali flani ilionekana katika macho yake mara moja.
“Huu ni muda wa wewe kuacha kuwa mpumbavu , najua haina maana kukuelewesha tena lakini nikuambie tu wewe ni moja kati ya maadui zangu ambae umechukua muda mrefu , ukweli sio kwamba nakuchukia kihiivyo , kabla roho yako haijauacha mwili wako nataka nikuambie kitu ,, pengine ulichosema ni kweli kwamba ni neema za Mugnu zilizonifikisha leo hii lakini unaweza kushangaa kwamba wakati wewe ukiwa mwanafunzi mzuri na kinara shuleni kwenu, unaependwa na walimu kwangu mimi sikuwa hata na uhuru wa kuitwa chokoraa .. hivi unadhani umeshindwa na mtu ambae alikuwa na kila kitu , ngoja nikuambie umeshindwa na mtu ambaye hakuwahi hata kujua alikuwa na familia wala ni wapi alizaliwa , mtu ambaye alitegemea nyama ya binadamu kuishi , mtu ambaye alikuwa ni sehemu ya majaribio ya kisayansi ambayo maumivu yake sio ya kawaida , kwasababu tu ya kupoteza ndugu na kuwa kilema ndio useme Mungu amenipendelea , ninachomshukuru Mungu leo hii kunipa nafasi ya kuendelea kuishi mpaka leo hii licha ya changaoto zote nilizopita na hii ndio tofauti yako na yangu , unaamini Mungu kanipendelea lakini mimi namshukuru kwa kunipa nafasi ya kuishi”
Machozi ndio dalili pekee ya uhai iliomtoka Lekcha na mara baada ya kuvuta pumzi ndefu palepale nywele zake zilianza kubadilika rangi na kuwa nyeupe na hatimae rangi ya kijivu na ngozi yake ikakauka na kujikunja na hatimae kukosa sifa ya ubinadamu na uhai wake ulionekana ndio unafikia mwisho taratibbu taratibu.
Katika uso wake huo ambao ulikuwa ni kama udongo hali ya furaha, huzuni na makasiriko iliweza kuonekana na alionekana kuwa wa tofauti sana kuliko mwanzo , hakuna neno ambalo liliweza kutoka katika kinywa chake kana kwamba alikuwa akisubiria wakati wake wa mwisho.
Roma aliendelea kumwangalia Lekcha jinsi alivyokuwa akibadilika rataribu kadri nishati ya ant-matter ilivyokuwa ikipotea hewani na palepale alivuta pakiti ya sigara kutoka katika hifadhi yake ya anga na kuchomoa moja.
“Vipi nikupatie moja?”Aliuliza Roma, ndio kitu pekee ambacho alikuwa na uwezo wa kumpatia Lekcha muda huo katika hatua zake za mwisho.
“Pengine hujawahi kuvuta sigara ghali kama hii maisha yako yote”Aliongea Roma na kisha alichuchumaa na kumshikisha Lekcha ile sigara na alisita kidogo na hatimae Lekcha alionekana kuishikilia japo kwa taabu na kisha akaitumbukiza katika mdomo wake, mara baada ya Roma kuiwasha Lekcha alivuta moshi kidogo tu na kushikwa na kikohozi kilichomfanya sifara kudondoka.
“Naona unanikejeli , nimepokea hii sigara kwasababu inaonekana ya thamani sana na ingesikitisha nikifa kabla ya kuonja moshi wake … usijione wewe ndio mtu pekee ambaye umepitia mengi na una uzoefu wa kuishi maisha ya kifahari”
Roma alivuta kwanza moshi na kuupuliza hewani na kisha alitoa tabasamu huku akiona kiwango cha mwisho mwisho cha nishati ya Ant-Matter kikipotea katika mwili wa Lekcha.
“Kama ningekuwa mtu mkarimu pengine ningekupatia bia ya ya thamani kubwa lakini nimekupa sigara kwani ndio kitu pekee cha thamani ndogo nilichokuwa nacho”Aliongea Roma na kumfanya Lekcha kutoa tabasamu la dhati lisilo na unafiki kwa mara ya kwanza mbele ya Roma.
Muda huo ndio aliweza kufika Aoiline kwani alijitenga mbali sana na eneo hilo na mara baada ya kutua alimwangalia Roma kwa namna ya kushangazwa nae.
Alimwangalia namna ambavyo Roma alikuwa akiwasha sigara moja baada ya nyingine huku akiangalia namna ambavyo Lekcha anavyochukuliwa na Israeli mtoa roho.
Roma baada ya kuona hakuna tumaini lolote kwa Lekcha alisimama na kisha alimsogelea Aoline na ni muda uleule aliruhusu radi kumpiga Lekcha na akageuka kuwa majivu na huo ndio ukawa mwisho wake.
“Inaonekana angalau mwishoni chuki yake zidi yako imempotea”Aliongea Aoiline.
“Labda , kumalizana nae ni kama kuagana na kipindi kingine cha maisha yangu , Ni nani ajuaye kinachonisubiri mbele”
Aliongea Roma huku akitoa tabasamu hafifu kana kwamba ashaona nini kinamngojea huko duniani.
ITAENDELEA.
 
Back
Top Bottom