Abdallahking
JF-Expert Member
- Mar 19, 2018
- 3,985
- 10,840
- Thread starter
- #101
SEHEMU YA 74 & 75
alikuwa akilitupia macho yenye maswala ambayo yalitaka kujua kipi hasa kinachofanywa kwenye nyumba hii. Alikuwa hajapata nafasi hadi leo hii.
"Karibu sana Inspekta," sauti ya mwenyekiti ilimhimiza. Nimefurahia sana kufika kwako. Haja yangu ni kutaka ufahamu kuwa tulioko mbele yako ni raia na wazalendo wa nchi hii wenye njaa kubwa ya utajiri na kiu kali ya vyeo kiasi cha kushiriki kikamilifu katika njama za hatari ambazo hazijawahi kutokea katika historia ya ulimwengu." Wote walimsikiliza kwa mshangao. Kombora aliduwaa. Wajumbe walitetemeka.
"Labda nirudi nyuma kidogo kimaelezo. Mpango huu umeandaliwa kwa muda mrefu. Majaribio ya aina aina yamekwishafanyika. Sumu maalumu zimeandaliwa. Moja ya sumu hizo ni ile ambayo ilikusudia kumuua Joram Kiango. Iliposhindwa, msichana aliyeteuliwa kuutekeleza mpango huo, aliuawa kikatili kuliko kifo chochote cha kikatili kilichowahi kutokea. Utakumbuka Inspekta kuwa, Viungo vya msichana huyo viliokotwa chumbani kwake mfano wa nyama inayouzwa. Baada yake ndipo Joram aliuawa kwa bomu. Viungo vyake vilitapanywa ovyo hata asijulikane kabisa. Sivyo Inspekta? Na baada ya Joram, akauawa Neema Iddi yule msaidizi wake. Ni sisi hawa ambao tuko mbele yako..."
Wajumbe ambao walikuwa wakitetemeka walianza kuinuka. mmoja alipiga hatua mbili tatu kuelekea mlangoni. Lakini alirejeshwa na bastola ya Kombora ambayo ilikuwa ikimwelekea. "Yeyote atakatyeinuka atakuwa maiti. Kuanzia sasa, wote mko chini ya ulinzi."
"Usiwe na haraka Inspekta," Mwenyekiti aliendelea kwa utulivu kama awali. "Bado kuna mengi yatakayokusisimua. Kumbuka umealikwa kama msikilizaji tu. Tulioko mbele yako si tishio kubwa kwako. Yuko kiongozi wetu ambaye si mroho sana wa vyeo na utajiri, lakini anayo maradhi ya hatari zaidi. Yeye ni mtu anayependa sana mauaji. Mengi kati ya mauaji yaliyokwisha fanyika ameyafanya kwa mkono wake. Na anafurahia sana kuua. Twaweza kusema kuwa ana wazimu. Yeye ndiye kiongozi wa mpango huu na ameapa kuwa ataufanikisha. Kwa bahati mbaya hayupo hapa tena. Ametoweka..."
"Wewe ni nani?" Kombora alifoka.
"Mjumbe tu mwenye jukumu la kukupa salamu kutoka kuzimu aliko..."
"Sikia," Kombora alikatiza tena. "Huu sio wakati wa mzaha ata chembe. Kuna mtu mmoja tu mwenye sauti na tabia kama yako. Mtu ambaye alifariki kitambo na nilimzika mwenyewe. Joram Kiango. Sasa wawa ni nani? Huonekani kama mmoja wa kikundi hiki cha hatari sana. Pengine hii ni ndoto tu kesho mambo yatakuwa shwari?"
"Sio ndoto Inspekta" Mwenyekiti huyo alijibu. Labda nindoe nuru hii inayowanyimeni nafasi ya kuniona vyema." Aliupeleka mkono wake chini ya meza na kubonyeza mahala. Nuru ikatoweka. Aliyekuwa nyuma ya nuru hiyo alikuwa Joram Kiango!
Na alikuwa akitabasamu.
"Joram Kila mmoja aliropoka kwa mshangao. Akuna aliyeyaamini macho yake.
"It can' be true," Kombora alifoka kwa lugha ya kigeni. Akijisahihisha mara moja akisema, "haiwezekani. Lazima iwe ndoto ulifariki kitambo Joram. Dunia nzima inafahamu hivyo."
"Ndiyo," Joram alijibu baada ya kucheka kidogo. "Nilifariki. Na ni rafiki zangu hawa ambao walinihukumu kifo na kuhakikisha nimekufa. Lakini kuna mengi yalitokea. Nadhani Muumba alikuwa alikuwa hajaweka saini katika mkataba wa kifo changu, au ameikubali rufaa yangu. Hivyo nimerudi ili nitoe salamu zangu kwa kikao hiki. Salamu nilizozipata uko akhera," alimaliza akiachia tena tabasamu.
Lakini tabasamu la dhihaka.
Tabasamu ambalo liliwatesa sana wajumbe zaidi ya kufichulika kwa ukweli. Wote walikuwa wameamini kuwa Joram alifariki kama walivyoafikiana. Na walikuwa wamesikia hivyo katika vyombo vya habari. Na walikuwa wamehakikishiwa na "Mwenyekiti" wao ambaye hawakuwa na shaka kuwa angetimiza jukumu hilo. Vipi tena Joram awe hai! Tena mbele yao! Akiwadhihaki na kuwakebehi! Kitu gani kinatokea! La kutisha zaidi ni kufahamu kuwa Joram bado yu hai. Waliona matumaini yao yakifa mbele yao. Tazama anacheka! Tazama macho yake yanavyotoa nuru ambayo inadhihirisha kuwa siri kamili alikwisha fahamu. Siri ya kutisha ambayo inatosha kuwafanya wahukumiwe kitanzi! Yu wapi? "Mwenyekuti" huyu aliyewatumbukiza katika mkasa huu? Au tayari ametiwa mikononi?
Kombora hangeweza kustahimili, akasema "Sikia Joram. Pengine nimeanza