Simulizi ya Kijasusi: Salamu Kutoka Kuzimu

Simulizi ya Kijasusi: Salamu Kutoka Kuzimu

SEHEMU YA MWISHO

COUNT-DOWN PART 13


alipokitoa kidani hakuzungumza chochote akipeleleza juu yangu au juu ya kidani hiki?".

Nuru hakukumbuka kitu hicho. Alichokumbuka ni kwamba katika maongezi ya jana sauti ya Duncan ilikuwa ya kawaida bila dalili yoyote ya kujua mengi juu ya mkufu huo.

Mgeni aliyasoma hayo katika uso wa Nuru. Akaridhika. "Wala hakukuonya usikivae tena?", aliuliza.

"Aliniambia nikurudishie. Kwa hiyo chukua uondoke. Nataka kulala mapema", Nuru alifoka.

"Kweli", mgeni huyo aliunga mkono. Akacheka kidogo kabla ya kusema. Bi. Nuru tafadhali yasahau yote yaliyopita kati yetu. Ulikuwa mzaha tu. Nadhani utanisamehe nikikupa hii? Alitia mkono wake mfukoni na kuutoa. Ulikuwa umeshikilia kitita cha pesa. Hazikuwa chini la laki mbili. "Tafadhali pokea".

Pesa ni pesa. Zina nguvu na starehe yake. Zinashawishi. Lakini hizi zilimtisha Nuru. Kuzipokea ilikuwa kama kupokea nauli ya kuelekea kuzimu. "Mara ngapi niseme kuwa sihitaji chochote kutoka kwako?, Nuru alifoka tena. "Ondoka na pesa zako. Zinanuka".

"Zipokee. Kama hupendi ni juu yako. Lakini hizo sikupi bure. Ni malipo kwa kazi ndogo ambayo lazima utaifanya kesho mkutanoni". Akaingiza tena mkono wake mfukoni na kutoa kopo la poda ambalo lilikuwa limefungwa katika mfuko wa nailoni. Hii ni zawadi yako nyingine. Poda ya aina yake. Wewe utakuwa mtu wa pili katika nchi hii kuitumia. Hata hivyo utalazimika kuitumia kwa uangalifu sana ukifuata maelekezo yangu. Unanisikia?".

Nuru alitikisa kichwa kukubaliana na mgeni wake.

"Nisikilize kwa makini. Kesho utakwenda na poda hii kazini, ikiwa ndani ya pochi yako. Utakapowadiwa wakati wa kuwapatia wageni vinywaji ndipo utakapokwenda bafuni na kufungua poda hii. jipake ya kutosha usoni na mikononi. Kisha utarudi na kuanza kuwahudumia hao waheshimiwa. Hakikisha mikono yako inagusa karibu kila kikombe. Sawa?".
 
SEHEMU YA MWISHO

COUNT-DOWN PART 12


Hofu na mshangao vilikuwa katika macho ya Nuru. Alimtazama mgeni wake kwa hofu ingawa hakuuliza chochote. Mgeni alimtoa hofu kwa kucheka kidogo.

"Naona una wasiwasi. Usiwe na haja ya kuogopa kitu. Matokeo ya kazi hiyo yatakuwa mzaha mwingine wa kusisimua sana. Viongozi kadhaa watasinzia kwa dakika mbili tatu bila sababu. Litakuwa jambo la kuchekesha kidogo ambalo halijawahi kutokea katika historia ya dunia. Nitafurahi sana. Baada ya hapo utarudi zako kuchukua laki zako mbili uzifanye upendavyo. Halafu tutapanga mipango ya baadaye. Nitakuwa kijana sasa. Siyo mzee asiyeweza kitu. Unasemaje?".

Nuru hakuwa na jibu. Hofu zilizidi kujengeka katika fikra zake. Hofu ambayo ilimfanya azidi kumchukia mtu huyu aliyekaa mbele yake. Alitamani amfukuze tena. Lakini hakuona kama ingesaidia. Hivyo alitulia kimya akimsikiliza, na kisha kuhamishia macho yake juu ya kopo la poda na laki mbili zilizolala juu ya meza.

"Nakukumbusha tena, Utajipaka uwapo mkutanoni tu. Dakika moja kabla ya kuanza kuhudumia", alikumbusha.

"Nani aliyekwambia kuwa nitafanya kazi yako hiyo ya kishenzi?" Nuru alifoka, Ondoka na vitu vyako vyote. Nakuomba kwa mara ya mwisho. Au nitawaita polisi".

Ndipo Nuru alipoiona hasira kali katika macho ya mtu huyo. Ilikuwa hasira baridi. Hasira ya kutisha. Ilijitokeza katika sauti na tabasamu lake aliposema kwa upole. "Utaifanya. La sivyo, nitakuua hadharani. Nitakuwa pale pale mkutanoni nikikutazama. Fanya chochote kinyume cha matakwa yangu na utaona nitakavyokufanya. Utajuta kuzaliwa na kujutia kifo
chako. Kitakuwa kifo cha kinyama kuliko unavyoweza kukadiria jaribu kukiuka uone".

Shetani asingeweza kumtisha Nuru zaidi ya sauti hii: Ilikuwa sauti iliyoleta ukweli katika nafsi ya Nuru bila ya mzaha. Sauti iliyofanana na mauti yenyewe.

Ndio kwanza hofu ikautoka moyo wa Nuru. Akafumba macho na kuruhusu machozi mengi yamtoke. Alipoyafumbua mgeni wake hakuwepo. Alivyoondoka hajui. Pesa na poda vilikuwa mezani vikimsubiri. Akavuta pumzi na kuzishusha.

Sasa wakati ulikuwa umewadia. Umati mkubwa wa wananchi ulikuwa
 
SEHEMU YA MWISHO

COUNT-DOWN PART 11


umekusanyika mbele ya hoteli ya Maunt Metru kiasi cha kulifanya eneo zima liwe kama msitu wa mitu yenye uhai wa rangi mbalimbali. Wake kwa waume, wazee kwa vijana walisimama juani kwa utulivu, kando ya barabara ya Moshi- Arusha kutoka mjini kati hapa hotelini. Kila mmoja alikuwa na shauku kubwa ya kuwaona viongozi hao ambao walitarajiwa kuwasili wakati wowote.

Kila mmoja alikuwa na sababu zake zilizomfanya asitahamili ukali wa jua na kuendelea kusubiri. Wengi walikuwa wameitikia wito wa Serikali iliyowataka kujitokeza kwa wingi kuwapokea viongozi kutoka nchi mbalimbali za Afrika. Baadhi walifika eneo hilo kwa kufahamu kuwa ilikuwa fursa pakee ya kufika kuwaona ana kwa ana watu mashuhuri kama hawa ambao huwasoma kupitia magazeti na kuwasikia katika taarifa za habari za redio na televisheni. Pia walikuwepo wananchi ambao shauku yao ilikuwa kuwaona viongozi fulani tu baada ya kuzisikia sifa zake nyingi redioni. Kadhalika walikuwepo watu si haba ambao walikuwepo kwa jukumu la kuhakikisha usalama wa viongozi na wananchi hao.

Mtu mmoja tu alikuwepo kwa dhamira tofauti. Yeye alifika kwa ajili ya kushuhudia vifo vyao. Mtu huyo alipofikiria mshangao ambao utawapata wananchi baada ya kuwaona viongozi wao wakianguka mmoja baada ya mwingine, alichekelea kimoyomoyo. Kufa hadharani kama mzaha! Aliwaza kwa furaha. Kwa mara ya kwanza redio zote duniani zitangaze habari ya kusisimua. Magazeti yataripoti habari yenye moto. Televisheni zitatangaza kitu kinachostahili. Dunia itashangaa, ulimwengu utaduwaa. Litakuwa jambo ambalo halijawahi kutokea katika historia ya dunia. Kwa mkono wake, atakuwa ameusimamisha mkondo wa historia ya Afrika. Atabadili historia! Furaha iliyoje aliwaza.

Na kwanini wasife? alijiambia. Kwanini ilihali kati yao kuna walioua wenzao na kusababisha madimbwi ya damu za watu wasio na hatia katika nchi zao kabla ya kupokonywa madaraka? Kwanini wasife hata wale ambao walipewa kura na wananchi lakini wamewasaliti kwa kusahau shida za watu hao na
 
SEHEMU YA MWISHO

COUNT-DOWN PART 10
COUNT-DOWN PART 9
COUNT-DOWN PART 8
COUNT-DOWN PART 7
COUNT-DOWN PART 6
COUNT-DOWN PART 5
COUNT-DOWN PART 4
COUNT-DOWN PART 3
COUNT-DOWN PART 2
COUNT-DOWN PART 1

Yeah bado vipande 10 tumalize kigongo hiki... TUPIA UTABIRI WAKO , Nini kitatokea.

Itaendelea
 
Kama utabiri tu,
Basi duncan ambaye ni jerome ningeuchunguza ule mkufu na kuweka bugs yangu ili niweze kunasa mipango ya prosper...
Kisha baadae nije nyumbani kwa Nuru nisubiri windo langu
 
SEHEMU YA MWISHO

COUNT-DOWN PART 10


badala yeke ni wao pekee wanaonenepeana na kufura matumbo? Kwanini wasife hata wale ambao japokuwa hawatumii vyeo vyao kujaza matumbo bado wameng'ang'ania madaraka pasipo nia yoyote ya kuwaachia wengine madaraka nao watawale?. Wana haki ya kufa. Wote na kwa pamoja! Hadharani.

Wakati akiwaza hayo, Proper alikuwa katika umati wa watu waliozunguka hoteli ya Maunt Meru kama raia yeyote mwema. Macho yake yalikuwa wazi na makini kuutazama kila uso kwa makini. Nyuso nyingi alizoziona, uzoefu ulimuonyesha kuwa ni wapelelezi. Bila shaka walikuwa na silaha zao tayari, na walikuwa wakimtafuta yeye. Endapo wangemwona alijua kuwa wangemuua kwanza na kumsaili baadaye. Ndiyo alikuwa katika eneo la hatari. Hata hivyo hakuwa na hofu yoyote. Alikuwa na hakika kuwa wasingeweza kumpata. Wao walikuwa wakmtafuta Proper wanayemfahamu wakati yeye sasa alikuwa Proper mwingine ambaye hata mama yake mzazi aliyemzaa asingeweza kumfahamu. Zaidi, walikuwa wakimtafuta mtu mwenye bastola au bomu la kurushwa kwa mkono wakati yeye Proper alikuwa mikono mitupu kama raia wengine. Ama, kwa ulinzi wao wote madhubuti, watashangaa watakapoona viongozi wao wakianguka mmoja baada ya mwingine.

Hata hivyo hofu kidogo ilikuwa ikipenya katika moyo wake. Ikawa mara yake ya kwanza kuona hofu, na ikamshangaza zaidi ya ilivyomtisha. Anahofia nini? Nuru atamwangusha? Hilo halikumtia hofu. Alijuwa kuwa alikuwa amemweka Nuru katika kona ambayo asingeweza kuponyoka. Kidogo alimhukumu kwa kujuwa kuwa atakufa na viongozi hao mara baada ya kuwahudumia. Alimsikitikia zaidi Nuru kwa kujuwa kuwa kifo chake hakitapewa uzito wowote japo ni msichana mzuri mno. Itakuwa sawa na inzi aliyekufa pamoja na tembo.

Hofu iliendelea kuutekenya moyo wa Proper. Anaogopa nini? Alijiuliza tena. Kuna nini cha kuhofia ? Au amefanya makosa kuja hapa? Pengine angekaa mahala fulani akisubiri redio zimletee habari hiyo ya kusisimua? Upuuzi ulioje! Angepata wapi fursa nyingine ya kushuhudia kitendo kama hiki cha
 
SEHEMU YA MWISHO

COUNT-DOWN PART 9


kihistoria? Pindi marais zaidi ya kumi, mawaziri zaidi ya ishirini na makatibu wasio na idadi wakifa kwa kulalia meza zao, mmoja baada ya mwingine, nani atakayehangaika kumtafuta mtu wa kawaida aliyeko katika umati wa watu wa kawaida?

Zaidi ya hayo, nani atakayefaulu kumpata? Wakati wao watakapokuwa wakiwafikisha marehemu katika hospitali ya Maunt Meru yeye atakuwa Namanga akitafuta njia za mkato. Wakati habari zitakapoanza kutangazwa yeye atakuwa angani akitokea Nairobi kuelekea New York ambako atanunua gazeti la TIMES na kujua nani na nani walikufa katika mkasa huo, nani mwenye bahati ya mtende aliyeponea chupuchupu. Suala la nani atachukua madaraka baada ya nani na atafanya nini zaidi ya nani hili hakuona kama linamhuru.

Mawazo ya Proper alikatishwa na gari la kwanza ambalo liliwasili. Lilikuwa na askari wengine kadhaa wenye vyeo vya juu. Kati yao Proper alimtambua Inspekta Kombora. Alionekana kama ambaye hakuwa amepata usingizi wa kutosha kwa siku mbili tatu hivi. Proper akamhurumia kwa kujua kuwa muda si mrefu atapata mshangao mkubwa katika maisha yake, mshangao utakaomfanya apelekwe hospitali na marehemu wengine, akiwa na ugonjwa wa moyo baada ya kuzimia kufuatia uzito wa tukio hilo.

Magari yakaendelea kufika. Viongozi mbalimbali walitelemka kutoka kwenye magari hayo huku wakishangiliwa na wananchi. Waliwasalimia wananchi kwa kuwapa baadhi mikono, kisha waliingia hotelini ambamo tafrija kubwa ilikuwa imeandaliwa ikiwasubiri.

Sasa! Proper alianza kuwaza moyo ukizidi kumdunda.

Nuru alikuwa mmoja wa watu waliondaliwa kwa ajili ya kuwapokea viongozi hao na kuwaongoza katika viti vyao. Aliifanya kazi hiyo kama kawaida huku akifanya kila aliloweza kuficha hofu na wasiwasi vilivyokuwa katika roho yake kiasi cha kumfanya atetemeke kidogo. Hata hivyo shamlashamla na vigelegele vilivyokuwepo vilisaidia kuifanya hali yake isishukiwe na mtu yeyote.

Hatimaye ukawadia wakati ambao Nuru alikuwa akiuogopa kuliko nyakati zote. Wakati wa kuanza tafrija. Sasa alitetemeka bila kipingamizi. Ilimshangaza kwamba hakuna mtu yeyote aliyeonekana kumshuku hadi sasa.
 
SEHEMU YA MWISHO

COUNT-DOWN PART 8


Akayatupa macho yake nje, katika umati ya watu waliojazana mbele ya hoteli akisubiri viongozi watoke. Kama livyotegemea aliyaona macho ya yule mgeni wake wa jana akimtazama na kumkumbusha adhabu ya kifo inayomsubiri endapo hatafanya kama alivyoamriwa.

Hakuwa na la kufanya zaidi ya kwenda katika chumba chao cha maandalizi ambako pamoja na mkono wake kutetemke alitoa mfuko wake na kutoa ile poda, akaifungua karatasi ya nailoni na kuitazama kwa makini. Ilimshangaza kuona ilikuwa poda ya kawaida MALAIKA ambayo hutengenezwa na kimojawapo cha viwanda vyeti kilichomo katika mji wa Tanga. Hii kweli inaweza kufanya miujiza anayotaka ifanyike yule mwendawazumu? Nuru alijiuliza.

Ifanye, isifanye kwa hali yotote Nuru aliona kuwa alikuwa akifanya kosa kubwa sana katika maisha yake kwani kutii matakwa ya mtu yule wa ajabu. Maisha ya viongozi yana thamani kubwa. Kiongozi wa nchi ndiyo alama ya nchi yenyewe. Mamilioni ya watu yanamtegemea kiongozi. Vipi yeye Nuru, mtu asiye na lolote wala chochote ashiriki katika mzaha wa kuwafanya watu hawa wapumbazike kwa dakika kadhaa? Na vipi iwapo kuna madhara zaidi ya hayo aliyodai yule mgeni? Ni hayo yaliyomtia hofu.

Hata hivyo alijikuta hana njia zaidi ya kutii amri ile. Akaitoa poda hiyo na kujipaka kama alivyoelekezwa. Ikamshangaza kuona hata harufu ilikuwa ya kawaida, kama zilivyo poda za kawaida. Kisha akarejea ukumbini na kuanza kutoa huduma kwa viongozi. Muda si mrefu kazi ikawa imekwisha. Viongozi walitulia wakila na kunywa vinywaji vyao kama kawaida. Wawili watatu walizungumza na kutaniana. Kisha tafrija ikawa imekwisha. Wakaanza kuinuka kuyaendea magari yao, wananchi wakawashangilia.

Halikuwepo jambo lolote lisilo la kawaida lililotokea.

Ni hilo tu Nuru? alijiuliza kwa furaha. Akajidharau kwa kuhofia jambo lisilo na madhara. Bila shaka ulikuwa mzaha mwingine wa yule mtu. Kama ni mzaha, hata zile laki mbili zitakuwa mzaha pia? akajiuliza.

Haiwezekani! Proper alifoka kimoyomoyo huku akishindwa kuyaamini macho yake alipowaona viongozi hao, wote wakitoka na kuyaendea magari yao
 
SEHEMU YA MWISHO

COUNT-DOWN PART 7


ambayo yaliwapeleka katika jumba la mikutano AICC. Haiwezekani kabisa. Sumu iliyokuwemo katika poda ile ilikuwa kamili na hali ambayo ingetosha kuua kwa harufu tu. Kwanini wasidhurike? Au ni kweli kuwa wengi wao wanalindwa na miti shamba yenye nguvu? Lakini kama kweli wana uchawi mbona mara nyingi wanakufa kwa kitu kidogo kama risasi ya bastola? Kama uchawi vipi hata yule msichana mdogo Nuru asidhurike? Haiwezekani! Lilifanyika jambo. Nuru atalijutia jambo hilo alilofanya! Proper aliwaza huku akiyasaga meno yake kwa hasira.

Mtu mmoja tu katika umati huo aikuwa akiyatazama yote hayo kwa furaha, tabasamu pana likiwa usoni mwake. Akiwatazama Nuru na Proper kwa zamu, Aliyaona mawazo yao. Tabasamu lake likageuka kuwa kicheko.

Mtu huyo aliitwa au alijiita Duncan.

"Utakufa kifo cha kinyama kuliko vifo vyote vya kinyama ambavyo vimewahi kutokea na wewe kuvisikia katika historia ya dunia. Na kabla ya kifo chako utanieleza ni kitu gani ulifanya hata poda ile ikashindwa kuwaua wale mnaowaita viongozi.

Kuwaua! Ndio kwanza Nuru akafahamu jukumu gani alikuwa nalo. Kwa muda akasahamu maafa ambayo yalikuwa mbele yake, badala yake alijisikia faraja kuwa mkono wake haukuwa umefaulu kuhusika katika kitendo cha kishenzi kama kile, kama kingetokea. Angewatazamaje binadamu wengine? Angeishije katika dunia hii na doa la damu nzito ya viongozi wa nchi za Afrika.

"Ulifanya nini wewe malaya?".

Nuru akakumbuka kumtazama. Kila kitu kilikuwa wazi katika macho hayo. Yalitisha kama macho ya simba aliyejeruhiwa, yakitangaza mauaji. Hakuwa na chochote mkononi, bastola wala kisu. Lakini Nuru alijua mikono yake iliyokakamaa, ikitetemeka kwa hasira ilitosha kumuua kwa pigo moja tu. Tangu tafrija ilipokwisha Nuru alikuwa na wasiwasi. Alijua kuwa jambo moja au jingine lilikuwa limeenda kinyume cha matakwa. Alihofia sana kurejea nyumbani. Hivyo, waliporuhusiwa kuondoka yeye alipita kwa marafiki ambao alizungumza nao hadi saa tatu za usiku. Ndipo aliporudi nyumbani peke yake baada ya juhudi zake za kumshawishi mmoja wao kufuatana naye kutofanikiwa.
 
SEHEMU YA MWISHO

COUNT-DOWN PART 6



Hakushangaa kukuta zile laki mbili hazipo pale alipoziacha. Wala hakushangaa kuona ufunguo ukipenya kwenye tundu la kitasa na kufungua mlango taratibu. Kama alivyotegemea aliingia mtu yule yule akiwa katika sura na umbo la jana. Baada ya kuingia ndani aliufunga mlango kwa nyuma na kumtazama NUru kwa macho yake makali. Hakupoteza muda wake zaidi bali aliyasema yale aliyokusudia kuyasema.

Kwa mara ya kwanza Nuru akaupata ulimi wke na kujitetea kwa udhaifu, "Sikufanya chochote zaidi ya kutekeleza matakwa yako. Na kama nia yako ilikuwa kuwaua watu wale wasiokuwa na hatia basi Mungu hakutaka.

"Unajua hatia wewe?" Proper aliendelea kufoka. "Unasema ulifanya kila nilichokwambia? Ebu ilete poda hiyo niione".

Nuru alitoa poda hiyo na kumkabidhi Proper. Nae aliipokea kwa uangalifu. Mara akatokwa na ukelele wenye mchanganyiko wa hasira.

"Uliupata wapi uchafu huu?" Proper alifoka.

"Ni wewe uliyenipa", Nuru akasisitiza.

"Una wazimu", aliunguruma Proper, "Mimi nikupe takataka kama hii? Poda! iliyotengenezwa hapa hapa!" Akamkazia Nuru macho baridi. "Nakuhurumia sana bibie... Yeyote aliyekupa wazo la kunidhihaki kiasi hiki amekupa wazo la kipumbavu kuliko yote. Utakufa. Na kitakuwa kifo cha kinyama. Naapa. Lakini kabla hujafa utaniambia nani aliyekupa poda hii?"

Nuru akabaki ameduwaa. Nafasi ya hofu kwa muda ikachukuliwa na mshangao. Mtu huyu ana wazimu? Nuru alijiuliza. Ni yeye mwenyewe aliyemletea poda hiyo jana. Wala hakuwa ameigusa jana usiku bali aliiacha pale pale mezani na kulala. Na alipoamka ilikuwa pale pale pamoja na pesa zake.

"Ni wewe uliyenipa. Mimi sikuigusa wala..."

"Vizuri" Proper aliingilia maongezi ya Nuru, "Yaelekea umeamua kunidhihaki. Sasa nitakuonyesha mimi ni nani. Nadhani hujui watu wangapi wamesafiri kwenda kaburini kwa mkono huu. Utawafuata. Utakwenda kuwauliza ili wakufahamishe mimi ni nani", akasita kidogo akimtazama Nuru. "Umekuwa msichana mzuri sana. Hufai kufa kabla ya kuonjwa tuone kama uzuri huo ni wa nje tu, au hata ndani, hasa baada ya kukupa ule uongo wangu kuwa
 
Back
Top Bottom