Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu



SHETANI RUDISHA AKILI ZETU



MTUNZI :SINGANOJR






SEHEMU YA 89.

Ilikuwa ngumu sana kujua kama Hamza msisimko wake ulikuwa ukisababishwa na nguvu za kichawi au nishati za mbingu na ardhi , lakini kitu kimoja ambacho ni uhakika msisimko aliokuwa akitoa ulifanya watu watetemeke bila ya kujijua.

“Nishamuondoa msumbufu tayari, kama mnataka ni kheri mkijimaliza wenyewe kuliko kunisumbua maana itakuwa afadhali kwenu”aliongea Hamza akipiga hatua kumsogelea Mzee Tui.

“Muueni..”Wanajeshi wale wa kiharamia walipewa oda ya kumfayatulia Hamza risasi na ilichukua sekunde tu kukoki bunduki zao.

“Firee!!”

Kapteni Kenny alitoa ruhusa kwa jeshi lote kumshambulia na kusababisha eneo lote kujaa harufu ya milipuko, lakini sasa ilikuwa ni kama kawaida yake Hamza , walichokuwa wakilenga na bunduki zao ni udanganyifu wa macho na Hamza alikuwa ameshapotea muda mrefu sana na ile anakuja kujitokeza alikuwa nyuma ya The loner Au Mzee Tui.

“Mnamshambulia nani wakuu?”Aliongea Hamza

Kitendo cha sauti yake kugusa ngoma za masikio ya wale maharamia, waliweza kujihisi ni kama wanasikia mnong’onezo wa jini.

“Imekuwaje!!?”

Mzee Tui la nazi au The Loner alijikuta akishituka na kugeuka nyuma kwa utashi wa kutaka kujilinda kwa uwezo wake wote wa nishati za mbingu na ardhi na alimrushia ngumi nzito lakini upande wa Hamza hakuikwepa bali aliudaka mkono wake eneo la katikati na kisha aliuzungusha kwa nguvu na kilichoweza kusikika ni mifupa ya mkono kukatika.

“Arghhhhhhhhh!!!!

Yalikuwa ni maumivu yaliochanganyika na mshangao wa kutokuamini kwanini uwezo wake wa nishati za mbingu na ardhi ulikuwa dhaifu sana mbele ya Hamza ili hali adui yake alikuwa hana hata tone la nishati za mbingu na ardhi.

Hamza hakushia kumvunja mkono tu kwani palepale kwa kutumia mguu wake wa kulia alimchota mtama na kabla hajakaribia chini alikishika kichwa chake na kama anacheza mieleka alikipigiza kwenye sakafu ya meli.

Alikuwa ni kama amegongwa na gari kutokana na namna kichwa chake kilivyopasuka, kilichoonekana ni damu na uji uji mweupe.

Kitendo kile kilifanya maharamia wote kutoa macho huku wakizitafuta pumzi kwa shida, lilikuwa tukio la kutisha kweli kweli.

Hamza licha ya kufanya ukatili huo kwa binadamu mwenzake hakuonekana kuwa na hatia hata kidogo , baada ya kuusukumiza na teke mwili wa Mzee Tui alichukua bastora yake kiunoni.

Ilikuwa ni bastora ambazo zinazalishwa na kampuni ya Weiss & Smith na inabeba risasi tano pekee , lakini kwa uwezo wa kulenga shabaha aliokuwa nao risasi hizo tano zilimaanisha vifo vya watu watano.

Kitendo cha Hamza kunyanyua ile bastora na kuwalenga wale majambazi wa kundi la nafsi zinazotangatanga walingiiwa na utashi wa haraka wa kutaka kujilinda hivyo kwa mara nyingne walianza kumshambulia Hamza.

Lakini Hamza alikuwa ni kama roboti alikuwa akijua ni muda gani risasi itatoka na itapita wapi kwani aliweza kukwepa zote kwa spidi kubwa sana na wakati huo bunduki alioshikilia mkononi ilikohoa risasi tano mfuliulizo

“Bangg , bang, bang”

Baada ya milipuko ile mitano majambazi watano wa kundi la nafsi zinazotangatanga walidondoka chini wakiwa hawana uhai tena.

Baada ya kuona risasi zimemwishia alichokifanya alitumia ile bunduki kama jiwe na kumrushia ninja aliekuwa mbele yake kwa kumlenga eneo la kichwani na ninja yule hakuwa na muda wa kutosha wa kukwepa siraha ile na ilimpiga kwa nguvu kubwa eneo la kichwani na palepale alidondoka chini na kupoteza fahamu.

Hatimae walibakia watekaji wayano wa kundi la nafsi zinazotangatanga na walikuwa katika hali ya woga kiasi kwamba hawakutaka kurudisha mashambulizi na kuangalia namna ya kukimbia kwa kujitupa majini, lakini Hamza alikuwa fasta sana kwani kwa uwezo wake walikuwa ameshawafikia na alimshika wa kwanza shingo yake na kama anacheza mielekeka alimshusha na kumbabiza chini kwenye sakafu ya meli na kilichotokea ni uti wa mgono na ubongo wa nyuma kumwagika

Kilikuwa kitendo cha haraka sana Hamza alikuwa ameshamaliza maninja wote wa kundi la nafsi zinazotangatanga kwa kuwaua vifo vibaya sana na hakuna hata mmoja ambae mwili wake ulibakia katika umbo zuri , wote waliharibika aidha kichwa au mkono.

Maharamia wale walijikuta wakishangazwa na tukio lile kwa kiasi kikubwa, katika maisha yao hawakuwahi kuona mtu ambae anaweza kuua kwa kutokutumia nguvu nyingi kama Hamza.

Kwa ufupi hawakutafsiri alichokuwa kifanya Hamza kama kuua bali ni kama mtu anaekanyaga mdudu ili kumuua.

Jambo la kushangaza zaidi ni miondoko ya ki ustadi ya Hamza , alikuwa akitoka sehemu moja kwenda nyingine kwa namna ambayo ilikuwa ikifurahisha macho na kuzubaisha kwa wakati mmoja lakini ambayo haikuachii uelewa wa aina yoyote ile.

Yaani kwa lugha nyepesi ilikuwa ngumu kujifunza kile ambacho alikuwa akifanya.

Baada ya kumaliza kundi la nafsi znazontangatanga hatimae macho yake yalitua kwa Mzee Benjamini na mwanae

Mzee Benjamini muda huo macho yalikuwa mekundu huku akiwa anatetemeka kama ameona jini , James woga ulimzidia na hata kusimama alishindwa zaidi ya kupiga magoti.

“Hamza naomba usiniue , nichukulie kama uvundo, sina thamani ya kuuliwa na wewe”Aliongea James akijitahidi kupasha viganja ili aonewe huruma.

Hamza alitembea mbele yao na wakati alipokuwa akitaka kuwamaliza palepale aliweza kusikia sauti ya Kapteni Kenny kutoka nyuma.

“Unathubutu vipi kuua watu ambao wapo chini ya sisi The Shark , unadhani mimi Kapteni Kenny cheo changu nimekipata kwa kubembeleza watu?”aliongea kwa kingereza huku akiwa na hasira na muda ule ule alitoa kijikofia chake kilichochakaa kichwani na kukitupia pembeni .

Kenny licha ya kuwa kapteni wa boti hio lakini alikuwa pia ni mwanajeshi ambae aliasi , alikuwa na mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi kufikia levo ya Mzunguko kamili , hivyo matumizi yake ya siraha aina ya upanga na visu licha ya kwamba yalikuwa makali lakini yalikuwa na usahihi wa kushambulia kwa kasi kubwa , kwa lugha nyepesi ni ngumu kukwepa shambulizi lake kwani utashi wake ni zaidi ya binadamu wa kawaida.

Kitendo cha Kenny kuongea kwa hasira alikuwa tayari na upanga kwenye mkono wake na kumsogelea Hamza kwa nguvu kwa ajili ya kumfyeka , lakini Hamza alikuwa mwepesi mno kutabiria upanga ule utakapopita na alisogea pembeni na ukaenda kugonga kingo ya meli ile.

Upanga ule aina ya Kitara uliishia kuacha cheche nyingi ambazo zilisambaa na kuonekana licha ya eneo hilo kuwa na jua la machweo.

Kapteni Kenny hakuishia pale , baada ya kuona shambulizi lake la mwanzo limepita aligeuka kwa wepesi na kushambulia kwa mara nyingne akimlenga Hamza eneo la kiuno.

Lakini sasa kabla upanga ule haujamfikia Hamza alikuwa amekwisha kuruka kwenda juu na kilichotokea aliukanyaga ule upanga kwa kidole gumba na kutokana na nguvu ambayo Kenny alishikilia ule upanga na namna ambavyo Hamza alitumia nguvu kuukanyaga ule upanga , alijikuta akipiga yowe la maumivu mara baada ya kuhis mkono wake ni kama umepiwa na nyundo.

Hamza hakujali makelele yake kwani alimpiga kigoti cha taya na ilikuwa bahati tu hakutumia nguvu kubwa kumshambulia la sivyo Kenny angepoteza maisha palepale , hata hivyo kigoti kile kilimfanya kurushwa juu na kudondoka chini kama furushi akitanguliza mgongo huku damu nyingi zikimtoka puani na mdomoni.

Maharamia wote waliokuwa juu ya meli hio walishikwa na mshituko , siku zote walikuwa wakimuogopa bosi wao kwa uwezo wake mkubwa lakini kilichokuwa kikiendelea mahali hapo bosi wao alikuwa ni kama binadamu wa kawaida ambae alishambuliwa kwa stali ya pigo moja tu mpaka kuwa chini.

Hamza alichukua ule upanga wa Kitara chini na kisha akamwekea Kenny shingoni.

“For the sake of leviathan , I’ll give you a chance to live”Aliongea Hamza akimaanisha kwamba kwa ajili ya Lewiathani atampatia nafasi Kenny ya kuendelea kuishi.

Mara baada ya Hamza kumaliza kauli hio alishika ule upanga pande zote na kitengo cha kuukunja tu palepale ulikatika vipande viwili.

Kwa kenny upanga wake ulikuwa na historia kubwa sana na aliamini ndio moja ya upanga mgumu sana kuwahi kuushika katika maisha yake , lakini kwa namna ambavyo Hamza aliukata alijikuta akishangaa bila ya kuongea chcohote kwani alijihisi kuwa dhaifu mno kwa wakati huo , hata kama alikuwa na nguvu chache zilizokuwa ndani ya mwili wake bado alijihisi mdogo mbele ya Hamza kuendelea kushindana nae.

Aliishia kushukuru maamuzi yake ya kujiunga na kundi la maharamia la Sea Demons la sivyo siku hio asingekuwa hai tena.

Muda huo Afande Mwiba aliweza kusaidiwa kutoka kwenye bahari akiwa ameloa huku sura yake ikiwa imebadilika kutoka kujiammini na kuwa ya mtoto alieadhibiwa na wazazi wake na kushika adabu.

Wakati akiwa majini alikuwa na hasira kiasi kwamba alipanga akipandisha juu ya meli atazipiga tena na Hamza , lakini kile ambacho alikuwa akishuhudia kilimfanya kunywea na hakutaka hata kumkaribia Hamza.

Wanajeshi wa kitengo cha Malibu walipata kuelewa kwamba sio kosa la Afande Mwiba kumdharau Hamza , bali uwezo wa Hamza ulikuwa wa juu mno kwamba udharau au uheshimu, Hamza hawezekani.

Vile vipande viwili vya upanga alivyovunja alivirushia mbele ya mzee Benjamini na mtoto wake , kila mmoja chake.

“Nikiwaua nitakuwa najichafua tu, nawapa nafasi ya kujimaliza wenyewe”Aliongea Hamza.

Hamza aliona hao binadamu walikuwa wamepoteza kila kitu katika maisha yao na walikuwa zaidi ya binadamu wa kwaida hivyo hakutamani hata kuwaua.

Lakini hawakuwa tayari kupoteza uhai na waliendelea kusujudu mbele ya Hamza wakiomba kusamehewa.

Hamza hakuwa amekuja eneo hilo kutoa msamaha na kutokana na hilo aliwasogelea na kuwashika kola za mashati yao na kisha akawasukumia wote baharini.

James na baba yake waliishia kutapatapa kwenye maji huku wakipiga mayowe ya kuomba msaada kwani wanazama , lakini hakuna aliepiga hatua kuwasaidia kwa kumhofia Hamza.



Hamza aliona hio ndio njia pekee ya kumlipizia Edna na baba yake kisasi.

Mara baada ya kulipiza kisasi cha kwanza palepale alimkumbuka mwanamke Lamla, alikumbuka kama sio tamaa za Lamla kutaka kukwapua utajiri wa familia ya Regina , yote hayo yasingetokea , hivyo hakutaka kumuacha kirahisi.

“Kulikuwa na mwanamke wa makamo hivi , yupo wapi?”aliuliza Hamza.

“Unaongea sana kijana , unadhani kwa ulichonifanyia nitakujibu kila unachoniuliza , wewe na jeshi la Tanzania mmemuua rafiki yetu kwenye maji ya kimataifa , hili swala likifahamika unadhani tutaonekana vipi?”

“Kama heshima umeitengeneza mwenyewe na huwezi kuilinda huwezi kunilaumu mimi”Aliongea Hamza

“Hata kama mimi ni dhaifu kuliko wewe , usisahau kundi letu ni wanachama wa Sea Demons , nitamwelezea Mkuu Leviathani kila kitu kilichotokea hapa, usione hapa ndio imeisha”Aliongea Kenny.

Wanajeshi wa kitengo cha Malibu mara baada ya kusikia kauli hio walijikuta wakianza kupaniki.

Sababu kubwa ya wanajeshi hao kuhofia swala hilo ni kutokana na Serikali nyingi duniani zilikuwa zikitumia maharamia na ulimwengu wa giza kuagiza siraha na kununua teknolojia kwa siri sana ili kujitengeneza uwezo binafsi ambao hautambuliwi na maadui.

Kama Serikali ikinunua siraha zao zote kwa njia ya kawaida, inahatarisha usalama wa nchi kutokana na kwamba madili hayo yote yanaweza kugeuzwa kuwa udhaifu pale seirkali ikiingia katika vita , kwasababu kila siraha ambayo inamiliki itakuwa inafahamika uwezo wake na udhaifu wake , hivyo kwa serikali ambazo hazijitengenezei siraha zao wenyewe kama Tanzania walikuwa wakitumia makundi ya kiharamia na soko la giza kuingiza baadhi ya siraha muhimu.

Sasa Afande Barafu na Afande Mwiba walikuwa ndio viongozi wa misheni hio na chochote kikitokea wangeulizwa wao.

“Kapteni Kenny hili swala halina uhusiano wowote na jeshi la Tanzania , hivyo nakushauri kulichukulia kwa uangalifu”Aliongea Afande Caro.

Kapteni Kenny aliishia kutoa tabasamu la kejeli na alionekana kufurahia wasiwasi waliokuwa nao wanajeshi hao wa Tanzania.

“Ni jeshi lenu lililomleta huyu kichaa hapa , ni kweli hatuna uwezo wa kushindana na nyie kama nchi lakini hii haimaanishi itakuwa sawa mbele ya bosi wetu”Aliongea na muda uleule alimpa ishara kijana wake kumpatia simu ya mawasiliano ya satilaiti

Afande Mwiba na Afande Caro hawakutaka kumzuia , isitoshe hawakuwa na haki ya kufanya hivyo , kitu pekee ambacho waliona wanapaswa kufanya ni kujiandaa namna ya kwenda kujieleza kwa wakuu wakisharudi.

“Hamza ona sasa ulichofanya , wakituongelea vibaya kama jeshi kwa Sea Demons hata Mshauri mkuu hawezi kutoka katika hili”Aliongea Afande Mwiba akimbebesha lawama Hamza, lakini upande wa Hamza hakuwa na wasiwasi kabisa , alikuwa akimwangalia Kenny akifanya mawasiliano kwa utulivu.

“Ni mimi Kenny , kiongozi wa The Shark , nina swala la dharula la kuripoti kwa Mkuu Leviathani , hakikisha naongea nae moja kwa moja”Aliongea Kapteni Kenny.

&&&&&

Juu ya bahari ya bluu , meli kadhaa za kivita zenye rangi ya fedha ya kijivu zilikuwa zimejipumzisha juu ya uso wa bahari na kufanya eneo hilo lionekane kama ngome ya chuma juu ya bahari.

Juu ya meli hizo kulikuwa na bendera kubwa zilizokuwa zikipepea , zenye mistari ya rangi nyeusi na nyeupe , zikiwa na nembo kubwa ya maharamia walioshikilia mikuki na kufanya zionekane bendera ambazo hazikuashiria amani.

Kulikuwa na kila aina ya maharamia waliokuwa na rangi na miili tofauti toufauti na wakati huo baadhi yao walikuwa wakishindana kupigana , huku wengine wakijjirusha baharini na kupiga mbizi bila vifaa.

Katika deki ya boti ya kifahari mbele kabisa alionekana mwanamke wa kizungu mwenye nyele nyeupe(blonde) alievalia Bikini akiwa amekaa kihasahara hasara huku ameshikilia simu ya upepo na mara baada ya kuongea kwa sekunde kadhaa alionekana akikimbilia juu kabisa ya meli hio.

Juu kabisa ya deki alisimama mwanaume mweusi mwenye mwili mkubwa wa miraba minne huku akiwa na nywele za rasta , alikuwa ni mrefu karibia mita mbili hivi , mkononi akiwa ameshikilia glasi yenye kilevi cha Vodka kwa mkono wa kushoto na kulia kwake alikuwa amemshikilia mtoto mdogo wa kike wa umri wa miaka kama mitatu hivi.

Msichana huyo mdogo macho yake yake yote yalikuwa yakiangalia glasi alioshikilia yule mwanaume kwa macho yaliojaa matamanio na kumfanya yule mwanaume mweusi kuanza kucheka mara baada ya kuona mtoto huyo anatia huruma kwa tamaa za kutaka kuonja kila kitu.

“Leviathan , I saw it” sauti ya yule mwanamke alievalia bikini iliongea akimlenga yule mwanaume mwenye mwili mkubwa.

“Debie hebu onja kidogo , Monica mama yako hana shida”Aliongea Leviathan

“Yaani binti yako ndio kwanza anafikisha miaka mitatu unataka kumnywesha Vodka , unapanga kumfanya na yeye kuwa haramia?”Alongea Monica huku akimwangalia mume wake kwa macho makali na kumkwapua binti yake.

Msichana mdogo Debbie alionekana kutia huruma baada ya mama yake kumharibia kutokuonja utamu Vodka.

“Sioni tatizo lolote kwa mtu kuwa Haramia , nataka kumtengeneza aje kuwa mungu wa kike wa bahari kama enzi zile”Aliongea Leviathan huku akiwa na tabasamu la kizembe.

“Futa kabisa hayo mawazo yako , Debbie akishafkisha umri wa kwenda shule namrudisha nyumbani , nishaongea na bosi tayari mwakani naenda kuanza kazi na kama unataka kutuona unaweza kuja New York”Aliongea Monica.

“Darling bado tu unataka kuendelea na kazi yako ya uandishi wa habari , hivi kuna faida gani kila siku kufukuzia taarifa za hao mabepari , wakikuchokoza je?”

“Nani wakunichokoza bila sababu zaidi yako , kipindi kile nilienda kwenye usaili na matokeo yake ukanileta baharini kwa miezi yote ile , sasa mwanangu ashafikisha miaka mitatu tayari , unadhani kuendelea hapa ni bora kuliko hao mabepari unaowadharau?”

“Darling huwezi kunilaumu mimi juu ya hilo , nilikuwa bize kupambana baada ya kuzingirwa ndio maana nilikosa muda wa kukurudisha nchi kavu, halafu sidhani ni swala la kulalamika ilihali ndio kipindi kile ulianza kunipenda kwa ushujaa wangu”Aliongea huku akicheka.

“Huna aibu nani anaweza kupenda mtu kama wewe , hebu shika simu huko , nadhani kuna kitu hakipo sawa kwa yule kijana wetu mpya”Aliongea Monica akimkabidhi Leviathani ile smu ya upepo na kuweka sikioni.

“Kenny kuna shida gani , hujui sasa hivi nipo likizo?”aliongea kwa kufoka.

“Najua …Mkuu Leviathan , naomba uniwie radhi kwa kukusumbua lakini kuna swala kubwa limejitokeza”

“Kama umejamba achia ushuzi usambae , unajibana bana nini?”Aliongea huku akiwa hana ridhiko kwenye uso wake.

“Tumeshambuliwa na jeshi la Tanzania kupitia kitengo chao cha Malibu na wameua watu kumi , washirika wetu wa nafsi zinazotangatanga, wamedharau kwa asilimia mia moja nguvu yetu kama Sea Demons”Aliongea Kenny.

“Malibu!!, si upo kwenye maji ya kimataifa , kwannini Malibu wakushambulie?”

“Ndio nipo kwenye maji ya kimataifa , walitushambulia kwasababut tulikuwa na watu ambao wanawahitaji na sisi tukakataa kuwapa kutokana na kuwalinda kwasababu walishatulipa”Aliongea Kenny na bwana yule alikunja sura.

“Nimekuelewa , nnitawasiliana na mkuu wa kitengo cha Malibu kupata maelezo ya kina”

&&&&&&

Upande wa Kapteni Kenny mara baada ya kusikia maelezo hayo kutoka kwa bosi wake furaha ilimvaa palepale.

“Thank you for protecting us , Lord Leviathan , even if we were to die here today , we would be grateful to you for your boundless kindness ” Aliongea akimaanisha kwamba hata kama wakifa ndani ya eneo hilo basi wataendelea kumshukuru Bwana Leviathan kwa fadhila zake.

Mara baada ya kumsikia Kenny akitoa shukrani , kila mmoja upande wa jeshi la Malibu walijikuta wakijawa na wasiwasi mno , walijua fika ndani ya dakika chache makao makuu watapokea simu kutoka kwa Leviathan.

“Pumbavu kabisa Hamza , umetuingiza kwenye matatizo”Alilaani Afande Mwiba

Hamza aliishia kutoa tabasamu ambalo halikueleweka na alimsogelea Kenny kwa spidi kubwa kiasi kwamba hakujua hata amesogelewa vipi na kumfanya atetemeke.

“Bosi huyu Mtanzania anataka kuniua…”Kabla hata hajamaliza Hamza alishampokonya simu ile.

“Ni nani huyo kinyamkela anaethubutu kugusa vijana wangu?”Upande wa pili sauti ya Leviathani ilisikika ikifoka.

“Unafoka nini sasa wewe mjinga, ni mimi hapa..”Aliongea Hamza.

“..”

Kulkuwa na ukimya wa sekunde kadhaa upande wa pili wa simu na mara baada ya nusu dakika kupita , sauti ya Leviathan ilisikika ikiongea kwa kutetemeka na hata ule ubabe wake umeisha.

“Ndio ..Bosss!!!”Leviathani sauti yake ilisikika kwa kukatka katika kama mtu ambae ana pumua kwa shida.

“Leviathani wewe mshenzi makucha yako yamekuwa marefu sana siku hizi , yaani umefika mpaka kwenye ukanda wa Afrika mashariki , huyu mtu wako anaejiita Kenny ana kiburi na majigambo mno , ametumia zaidi ya watu mia kuninyooshea bunduki zao”Aliongea Hamza kibabe

“Ah!!.. Bosiii…..Sidhani kama unaweza kunilaumu kwa hilo , mimi ningejuaje ni wewe bosi wangu”Upande wa Leviathan alielezea kwa wasiwasi mkubwa.Ilionekana Leviathan alikuwa akimfahamu Hamza.

Kitendo cha Hamza kuongea na bosi wake kwa sauti ya utulivu kabisa , tena Hamza hata kumuita bosi wake mshenzi na mjinga Kapteni Kenny wasiwasi ulimvaa palepale mara baada ya kugundua kuna kitu hakipo sawa.

Ilionekana dhahiri Hamza hakuwa akimuogopa hata kidogo Leviathani na aliongea kwa upole pengine kwa kujali watu waliokuwa karibu yake.

Mara baada ya akili yake kufanya kazi vigoti vya miguu vilianza kulainika na kwa haraka sana aliwaashilia vijana wake kuweka siraha chini.

Upande wa Leviathani alielezea kwa uangalifu akihofia Hamza kukasirika kwa kuona yeye ndio kahusika.

“Bosi unajua mwenyewe nishaanza kuzeeka na mara chache naingia kwenye mitego ya vijana wangu , huyo bwana amekukosea sana na kama utataka kupunguza hasira zako unaweza kumuua tu na mimi Leviathani sitoongea chochote, Bosi niamini mimi natamani sana kuja Tanzania, binti yangu Debbie kashakuwa mkubwa na hajawahi kukuona .. oh tena nimekumbuka mke wangu Monica na yeye hajawahi kukuona”

Leviathani aliongea kila neno ambalo lilimkalia kwenye mdomo wake na kumfanya Hamza asijue acheke ama alie.

“Inatosha sasa Mzee , sijawahi kusikia kundi la kiharamia linaloitwa The Shark , nadhani pia ni kawaida kwao kutonifahamu kama mimi siwafahamu, hivyo nitakuacha udili nalo hili mwenyewe , huyo mkeo na binti yako nadhan siku moja nitapata nafasi ya kuonana nao , furahia maisha mdogo wangu lakini usiniibie kila kitu vinginevyo usije kunilaumu nitakachokufanya”Aliongea Hamza

“Sawa bosi wewe ndo mwenye kauli ya mwisho , nitadili na Kenny mwenyewe”

“Nadhani tumeelewena nampatia simu sasa”aliongea Hamza na kisha alimpatia simu Kenny ambae alikuwa akitetemeka tetemeka.

“Master Leviathani nini kinaendelea , Hamza ni mtu unaefahamiana nae?”Aliongea Kenny kwa kingereza.

“Sikia ninachokuelekeza , huyo mtu chochote atakachokuambia unapaswa kutii , ukipona kwenye mikono yake leo hii maana yake ni fadhila zake kwako , kuhusu yeye ni nani huna vigezo vya kumjua , hivyo usiulize maswali”Aliongea Levithiani akiwa siriasi.

“Yes Master , I understand”Aliongea Kenny haraka haraka huku akiwa na wasiwasi.

“It’s deed, serve it well and stay low from now on”Aliongea Leviathian na palepale alikata simu.

Kitendo cha Leviathian kukata simu mke wake Monica alimwangalia kwa shauku kubwa.

“Leviathan huyo uliekuwa ukiongea nae ndio mnaemwita My Prince?”Aliuliza Monica.

“Ndio , imepita zaidi ya miaka miwili tokea nisikie sauti yake mara ya mwisho”Aliongea Leviathan.

“Ni lini nitaweza kukutana nae ana kwa ana , kila siku nasikia uzushi wa kila aina ukimwelezea, wengine wanasema ana damu ya kifalme kutoka jumba la kifalme la Uingereza, wengine wanasema ni mtoto wa Muangalizi mkuu , nina maswali mengi sana juu ya kila aina ya maneno nilioyasikia kama ni ya kweli au lah… kama nikipata nafasi ya kufanya nae mahojiano nitapata umaarufu mkubwa na itanisaidia kwenye taaluma yangu”AliongeaMonica.

“Acha hizo kipenzi , kuna mambo mengi ya kuandika kuhusu bosi wangu lakini sidhani kama utaruhusiwa kuyaweka hadharani”Aliongea Leviathan.

“Huna maana wewe , kwaho kujigamba kwako kote una urafki nae kuliko mtu yoyote ilikuwa ni bure , kama unashindwa nikifanya nae mahojiano kwanini hata kukutana nae mimi na Debbie unashindwa kutusaidia?”Ailalamika Monica.

“Hatuna ujasiri wa kumsumbua , bosi hataki kabisa tukimsogelea”Aliongea huku akivuta pumzi nyingi na kuzishusha na palepale aliugeukia upande wa Tanzania na kupiga goti la utii wa kijeshi na kutamka maneno kwa nguvu.

“Selaphh!!!”

Upande wa Kenny aliongoza kundi la maharamia wenzake na walipiga magoti mbele ya Hamza kijeshi.

“Mr Hamza please forgive us , we have eyes but failed to recognise you”Aliongea akimaannisha kwamba wanaomba msamaha kwani wana macho lakini wameshindwa kumtambua.

Kitendo kile kiliwafanya Ma’Afande wa kitengo cha Malibu kuwa katika hali ya mshangao mkubwa , walishawahi kuona matukio ya kushangaza lakini hawakuwahi kuona tukio la kushangaza kama hilo na kila mmoja aliishia kujiuliza Hamza ni nani kiasi cha kumfanya Leviathan asimfanye kitu.

Afande Barafu na Afande Mwiba walishindwa kuzuia hofu yao , walijifikiria wao wenyewe na kuona haikuwa kwa bahati mbaya kwa mtu kama Hamza kufahamiana na Mshauri mkuu wa jeshi

Kitendo cha kuanza kufikiria alichokifanya tokea dakika aliokutana nae Afande Mwiba alianza kukosa utulivu , kila kitu aliona kipo nnje ya uwezo wake.

“Simameni sasa , tumepoteza muda mwingi sana na sitaki kuendelea kubaki hapa”Aliongea Hamza, alitaka kufanya haraka ili kumrudia Regina ambae alijua lazima atakuwa kwenye majonzi makubwa na ana hitaji mtu wa kuwa pembeni yake.

“Huyo Lamla yuko wapi?”Aliuliza Hamza.

“Yupo ndani pale”Aliongea Kenny kwa heshima.

“Ongoza njia , nataka kumuona”

“Yes , yes”

Kapteni Kenny hakuthubutu kukataaa na aliongoza njia kuingia kwenye Cabin sehemu ambayo Lamla aliingizwa.

Mara baada ya kuingia eneo la mapumziko, alisukuma mlango wa upande wa kulia na hatimae Lamla aliekuwa mwekundu kama nyanya kutokana na kuchezea kichappo alionekana , macho yalikuwa yamemvimba kwa kulia na muda huo hakuwa hata na fahamu.

Kwa makovu yaliokuwa kwenye mwili wake ilionyesha dhahiri alikuwa amechezewa na wanaume kibao .

“Mr Hamza huyu tuliuziwa na yule baba na mtoto wake”Aliongea Kenny

Hamza upande wake alikuwa akijua maharamia ni watu wa aina gani , hivyo hakushangaa kwa kilichomtokea Lamla.

“Muamsheni”

“Unataka kumchuukua , ngoja nimfungulie”Alionea Kenny

“Sitaki kumchukua, huyu anaweza kuendelea kubakia hapa na mtumieni mtakavyo”

Hamza mpango wake ulikuwa ni kumuua Lamla , lakini aliona itakuwa ni vizuri zaidi kuwa hai kuliko kufa bila kuteseka.

Mara baada ya kumalizana na Kenny alitoka katika meli hio na kuingia kwenye ile boti ya uvuvi kutafuta mwili wa baba mkwe wake na alifannikiwa kuupata.

Lisaa limoja baadae kwa kutumia boti le ya mwendokasi waliweza kurudi Tanzania nchi kavu giza tayari likiwa limeshaingia.

Hamza alimpigia Regina simu lakini aliepokea alikuwa ni Shangazi.

“Hamza hali ikoje?”Aliuliza Shangazi huku sauti yake ikiwa ni ya kijeshi.

“Mzee Benjamini na familia yake tushamalizana nao na kundi lote la Nafsi zinazotangatanga wamekwisha kufarki , Mwili wa marehemu nimerudi nao”Aliongea Hamza.

“Good , Good Job , hakika madam hajakosea kukuchagua , peleka mwili wa Marehemu hospitalini ukahifadhiwe na taratibu zingine zitaendelea , Regina yupo hospitalini kwasasa”

“Nini kimemtokea Regina?”

“Alipoteza fahamu baada ya kusikia taarifa za kifo cha bibi yake , sasa hivi hali yake ya akili haijakaa sawa ndio maana ameachwa akae hospitalini kwa muda”Aliongea na Hamza alielewa.

“Sawa Shangazi , nikikamilisha huku nitakuja huko mara moja”Aliongea na Hamza alikata sim.













SEHEMU YA TISINI.

Ikiwa ni saa moja na nusu kuelekea saa mbili kamili alionekana Kanali Dastani akiingia katika jengo la makazi la Dosam Homes eneo la mji wa kitajiri Dar es salaam.

Kitendo cha kuingia katika mazingira ya jengo hilo hisia zake zilikuwa nzito kutokana na taarifa za kifo cha aliekuwa mmiliki wa kampuni ya Dosam ambao ndio wamiliki wa jengo hilo la makazi namba moja Afrika mashariki na kati kwa usanifu wa hali ya ju na mvuto.

Alikuwa ndani ya eneo hilo kwa ajili ya kuonana na hawala wake Tresha Noah.

Mara baada ya kupanda Lift kwa dakika kadhaa ilienda kufunguka kwenye Penthouse ndani ya jengo hilo.

Ndani ya Tanzania nzima hakuna mwanamke ambae alikuwa akiishi maisha ya kifahari bila ya kuwa na kazi ya kueleweka kama Tresha Noah.

Kitendo cha kuishi katika floor ya mwisho ya jengo hilo la Apartment za Dosam Homes ilikuwa ni ishara tosha maisha yake hayakuwa ya kawaida likija swala zima la hela.

Penthhouse mara nyingi sio kama Apartment za kawaida , unaweza kuita nyumba juu ya ghorofa.

Sasa Tresha Noah ndio alkuwa akiishi peke yake juu ya nyumba juu ya ghorofa.

Kanali alikuwa na wasiwasi wa kuja ndani ya Apartment hizo kwasababu alikuwa akijua gharama za Tresha kuishi ndani ya hilo jengo zilikuwa zikilipwa na Mheshimiwa Eliasi Mbilu na kwa namna yoyote ile lazima ameweka watu wake wa kumfuatlia Tresha anaingiza nani ndani ya hio nyumba.

Mchana wa siku hio mara baada ya mwanamke huyo kumwambia akutane nae ndani ya jengo hilo alipinga lakini Tresha aligoma na kumwambia kama anataka kuonana nae basi anapaswa kufika ndani ya hilo eneo bila kukosa ndani ya saa moja.

Kanali mara baada ya kutoka kwenye lift hio hatimae alibonyeza kitufe maalumu na ndani ya sekunde chache alipokelewa na mwanaume alievalia sare za uhudumu na kumkaribisha.

“Karibu Mr”Aliongea yule kijana na Kanali alitingisha kichwa na kisha kuzama ndani.

Hakushangazwa na mazingira ya kifahari ya eneo hilo kwasababu haikuwa mara yake ya kwanza kufika.

“Tresha yupo wapi?”Aliuliza Kanali mara baada ya kuona eneo la sebuleni halikuwa na mtu.

“Karibu Afande”Sauti nyororo ya mwanamke ilisikika kutokea upande wa kushoto kwake na Kanali mara baada ya kugeuka aliweza kukutana na sura ya mwanamke mrembo Tresha alievalia Bathrobe na Bonnet ya rangi ya rose kichwani.

Licha ya bwana huyu kuwa na mke na watoto lakini kwa urembo wa Tresha kila anapomtia machoni mwili wake una msisimka na kusahau kabisa mpaka familia yake.

Tresha pia ni mwanamke ambae alikuwa akiwajulia sana wanaume , alikuwa ni fundi wa kucheza na akili ya mwanaume kiasi kwamba ilikuwa ngumu kutoka kwenye mtego wake, kati ya watu walioingia mazima kwenye mtego wake ni Dastani na Mheshimiwa Eliasi Mbilu.

“Hey!, Mbona umekuwa mnyonge ghafla”Aliongea na kisha kimadaha alizipiga hatua na kumsogelea Dastani na kisha alitaka kumkisi lakini Dastani alisogea nyuma kumkwepa na macho yake aliyageuzia kwa mhudumu aliekuwa akiwaangalia.

“Tresha unaniingiza kwenye mtego si ndio?”Aliongea Kanali huku akibadlika kidogo.

Tresha alitoa tabasamu na kisha alimwangalia yule mhudumu kwa macho makali na kitendo kile kilimfanya aondoke haraka ndani ya eneo hilo.

“Unamaanisha nini mtego sweatheart?”

“Umenilazmisha kuja nyumbani kwako na nilitegemea mazingira yatakuwa ni ya kikazi lakini unaanza kunitega mbele ya kijana wako, unataka kuniingiza matatizoni na hawala wako Eliasi?”Aliongea huku sauti ikipanda juu kidogo na swala lile tofauti na kumshangaza Tresha lilimchekesha.

“Niko siriasi halafu unacheka?”Aliongea.

Tresha alimsogelea Kanali Karibu kabisa na sura yake huku mkono wake wa kushoto ukiwa katika eneo la zipu ya suruali yake kana kwamba kuna kitu alichokuwa akitafuta na swala lile lilianza kumbadilisha kanali na mboni za macho kuanza kucheza cheza.

“Dastani unatakiwa kuelewa mipaka yangu kama mimi ninavyoielewa na kuiheshimu ya kwako , nikiambiwa nikuchague wewe au Eliasi nitaishia kumchagua Eliasi kwasababu licha ya umalaya wake lakini hana mke. nakuona mjinga ukianza kuonyesha wivu mbele yangu”Aliongea na kisha alipeleka mkono na kushika kidevu chake kilichojaa ndevu kana kwamba anakichunguza na kisha alimwachia mara moja na kugeuka huku akitembea kimadaha na kumpa ishara ya kumfuata.

Dastani aliishia kumwangalia mrembo huyo kwa sekunde kadhaa na kisha alimeza mate mengi na kuzipiga hatua kumfuata nyuma nyuma na walikuja kutokelezea kwenye Lounge ambayo ilikuwa ikionyesha mandhari yote ya jiji.

Tresha alijibwaga kwenye kiti cha uvivu huku akikaa kihasara hasara na kumfanya Dastani kutumia nguvu nyingi kujizuia , alikuwa akiyapenda maisha yake na kwa namna yoyote hakutaka kumsogelea Tresha kwa kuamini lazima mrembo huyo anachunguzwa na Eliasi.

“Uliondoka kimya kimya bila taarifa baada ya kuniambia swala la Amosi”Aliongea Kanali akiwa na utulivu.

“Ndio maana ukanipigia mara zote hizo?”

“Amosi alipotea kwa takribani wiki moja nzima , ulidhani ningekaa kwa amani ilihali naona viashiria vya kazi yangu kuingia dosari?”Aliongea na kumfanya mrembo huyo kutabasamu kidogo.

“Na sasa hivi unafanya nae kazi ilihali nilikuambia tumuondoe?”Aliongea huku akimwangalia kwa macho ya kejeki.

“Tena usiulize, makosa yako kila siku yanagharimu mipango yangu , nani alikuambia umteke Amos bila ya kunishirikisha?”

“Unamaanisha nini kumteka Amosi bila kukushirikisha?!”Aliuliza Tresha Noah huku akionesha mshangao.

“Unashangaa nini , ili hali kila kitu umefanya wewe? , Amosi amenitishia kuniunganisha na makosa yako ndio maana sikuwa na budi kushirikiana nae”

“Dastani unaongea ujinga , ninamteka vipi Amosi ilihali nilikuwa nje ya nchi na Mheshimiwa?”

“Kwahio unamaanisha hukumteka , Tresha acha maigizo ?, kama sio wewe hao ambao Amosi anazungumzia wamemteka ni wakina nani?”Aliuliza na swali lile lilimfanya Tresha kuonyesha kuwaza.

“Dastani nakwambia sijamteka Amosi , wala sijatoa maagizo ya yeye kutekwa , kuna mambo mawili aidha alitekwa kweli ama alikudanganya?”

“Sidhani kama alinidanganya ,Amosi hajawahi kuongea kitu ambacho hakina ukweli , niliishi nae jeshini namjua nje ndani tabia yake hana vitisho vya hewa?”

“Sijamteka mimi , ila kama alitekwa kweli basi itakuwa ni Carlos?”

“Carlos!!”

“Ndio, tokea ile siku Carlos ashindwe kumuua Amos kwenye ile hoteli hakuwahi kuridhika , ni mtu ambae hajawahi kujali matokeo kupitia maamuzi yake”Alongea na kumfanya Kanali kufikiria na kuona pengine kuna uwezekano huo maana hata yeye alikuwa akimfahamu Carlos.

“Tunapaswa kujihakikishia hili kupitia kwa Carlos kama alihusika”Aliongea na Tresha alitingisha kichwa kukubaliaa nae.

“Umefikia wapi Dastani, Madam kanipigia simu na kuniulizia maendeleo na mpaka sasa hatuna jibu la kumpatia , wewe uliharibu kuwasiliana nae kabla ya kila kitu hakijawa na uhakika”Aliongea Tresha.

“Sioni haja ya kupanikishwa na Madam , kama ameweza kuvumlia kwa miaka yote hio bila majibu kwannini ashindwe kuvumilia kwa muda huu ambao tunaelekea kupata majibu”Aliongea Kanali.

“Umempa matumaini , aliweza kuvumilia kwasababu ya matumaini kuwa madogo lakini sasaa hivi umeyapandisha”

“Nimeyapandisha kwasababu nina uhakika na alichorekodi Mchuku kina taarifa za kutosha kuhusu kifo cha Sedekia , Madam anachotaka ni kujua kwanini mtoto wake kapotea lakini sisi misheni yetu ni tofauti , tunataka kujua nini kilichompoteza Sedekia”Aliongea

“Na tunajuaje kama Rekodi bado hatujaipata?”Aliuliza Tresha.

“Tunakaribia kuipata?”

“Unamaanisha nini?”

“Mchuku kaiuza kwa mtu mwingine na akapatiwa kiasi cha pesa ambacho alitumia kumlipia mtoto wake ada ya mihula yote minne aliobakisha lakini pia kwenye akaunti yake ya benki nimegundua amebakisha kiasi cha milioni sita za Kitanzania kwa jina la mtoto wake wa kiume”

“Hela zote hizo katoa wapi? Na kama ameiuza una uhakika gani tunaweza kuipata , alieinunua pengine anaihitaji pia”

“Najua , ndio maana nilitaka kujua nani aliemuuzia na nimeweza kujua hilo kwa urahisi sana?”

“Ni nani?”Aliongea Tresha huku akionyesha hali ya msisimko.

“Hela zimehamishwa kutoka akaunti ya Dina kwenda Akaunti ya mtoto wa Mchuku kiasi cha shilingi milioni saba”Aliongea.

“Unamzungumzia Dina yupi?”

“Mkuu wa mtandao wa Chatu?”Aliongea Dastani na kauli yake ile ilimfanya Tresha kutoa macho.

“Unamaanisha Mchuku aliemuuzia ni Dina huyu huyu mwanamke katili ninaemjua mimi?”Aliongea huku akionyesha hasira kwenye macho yake.

“Acha kupaniki la sivyo hutoweza kuona maana iliojificha katika matukio yote”

“Kuna maana gani iliojificha hapo , kama Dina ndio kanunua maana yake sisi hatuwezi kuipata tena”Aliongea Tresha.

“Sio kweli , hebu fikiria vizuri , unadhani kama Dina aliitaka hio rekodi angefanya kosa la kuacha traces za muamala kama huu tuuone?”Aliuliza Kanali na kumfanya Tresha kumwangalia.

“Unamaanisha alifanya makusudi?”Aliuliza na kanali alitingisha kichwa kukubali.

“Unajua wafanyabiashara wengi wa ulimwenguwa wa Giza njia zao za malipo sio kama hizi za kwetu , malipo yao ni aidha Cash moja kwa moja ama kwa njia ya Cryptocurrency , lakini awamu hii Dina amefanya kosa la wazi na kutumia njia ya malipo ambayo inafuatiliwa na benki kuu”Aliongea Dastani na maneno yake yalioneakan kumwingia Dina.

“Maana yake aliacha nyayo za sisi kumjua ndio anaemiliki hio rekodi?”

“Asilimia mia na hapa uwezekano wa kuipata ni hamsini kwa hamsini na inaweza kuongezeka mara baada ya kujua anataka nini na kwanini aliinunua kwa Mchuku kabla yangu, kitu kingne kilichonifikirisha leo juu ya mzunguko wa hela ambao ulikuwa ndani ya akaunti ya Marehemu Mchuku , alikuwa na mzunguko mkubwa wa hela katika akaunti yake , hili limenifanya niamini kuna siri nyingi ambazo alikuwa akikusanya katika Gereza la Silo na kuna mtu ambae alikuwa akimuuzia kila alichokuwa akipata na pengine ndio mshirika wake mkubwa?”

“Unataka kusema kila alichokuwa akipata alikuwa akimuuzia Dina au?”

“Sina uhakika lakini uwezekano huo upo , leo Amosi alienda Gerezani kufanya uchunguzi wa kimaswali na inaonekana Mchuku hakuwa akifanya kazi peke yake”Aliongea na Tresha alionekana kufikiria.

“Kwa Dina tunapaswa kujiandaa, taarifa ni kwamba nguvu yake kwenye ulimwegnu wa giza hapa Tanzania imeimarika maradufu zaidi”Aliongea Dina.

“Ni kwasababu ya mahusiao yake ya karibu na Hamza”Aliongea

“Hamza!!!?”

“Ndio , huyu Hamza anafahamiana na Mshauri mkuu wa Serikali, nadhani unaelewa nguvu ya Mshauri mkuu , ndio aliepunguza nguvu ya Watu kutoka Binamu kuingilia siasa za Tanzania?, kulikuwa na uchunguzi uliokuwa ukiendelea juu ya huyu bwana anaeitwa Hamza lakini umefungwa kutokana na maagizo yake na hakuna mtu yoyote ndani ya kitengo na hata kwa Mkuu wa Majesh hajapinga”Aliongea Dastani na kauli ile ilimfanya Tresha macho yake kuchanua.

“Anaonekana sio wa kawaida , ndio maana hata Eliasi alikuwa akilitaja taja jina lake mara nyingi”Aliongea Tresha.

“Unajua kinachoshangaza zaidi?”

“Nini!?”

“Ndio mume wa bosi wa makampuni ya Dosam?”Aliongea na kauli ile ilimshangaza kwa mara nyingine Tresha.

“Ana uhusiao wa karibu na mrembo Dina na kisha ni mume wa Regina, mmiliki wa hili eneo ninalojivunia nalo, Dastani unanitia shauku ya kutaka kumjua , huna picha yake nimuone anafanana vipi?”Aliuliza Tresha huku akijiambia pengine huyo ndio mwanaume wa kumpa moyo wake kama ameweza kumpagawisha Dina na mrembo Regina.

“Picha yake ninayo hapa , ngoja nikuonyeshe”Aliongea Kanali na kisha alitoa simu yake na kwenda upande wa Picha.

“Dada..!!!”

Wakati Kanali akimkabidhi Tresha ile simu ndio muda ambao sauti ya kike nyororo iliita kutoka nyuma yao na kumfanya Tresha kugeuka.

“Anitha unafanya nini hapa usiku wote huu bila kupiga simu?”Aliongea Tresha bila kubadili muonekano huku akimwangalia msichana mrembo aliesimama nyuma yake.

“Nimetokea nyumbani kwa Chriss kwenye msiba na ni karibu na hapa , nimekumisi dada yangu”Aliongea Anitha na palepale alimsogelea na kumbusu Tresha Shavuni.

Ilkuwa sahihi kwa Hamza kumuona Anitha mrembo , msichana huyo alikuwa amefanana sana na Tresha muoenekano , alikuwa mrembo mno japo hakumzidi dada yake, pengine alikuwa amemzidi kabla ya kufanyiwa upasuaji wa kuongeza urembo.

Wakati Anitha anasimama ndio muda ambao aliweza kuona picha ya Hamza kwenye simu alioishikilia dada yake Tresha.

“Dada kwanini una hio picha , huyu si Hamza?”Aliongea Anitha huku akikwapua simu ya dada yake na kuanza kukuza ile picha na swali lake halikumshangaza Tresha tu, lilimshangaza na Kanali pia.

ITAENDELEA jumamosi- watsapp: 0687151346

END OF SEASON 3.
 
Yap! yap! Yap!
Ukioa mwanamke ambaye hana bikra huyo ni MALAYA mkubwa,isipokuwa wale waliobakwa na baadhi ya wajane(walioolewa ndoa ya kwanza wakiwa bikra)
Malaya kaliwa kuanzia primary,secondary,chuo hadi kazini halafu unamtolea mahari na kupiga goti eti "will you mary me?
PUMBAVU SIMP wewe.
 
Kuna jamaa anaitwa Elton huko kakuchukulia mashabiki comments za Arosto zimepungua sana huku Jitathimini mkuu
 
  • Thanks
Reactions: ram
SHETANI RUDISHA AKILI ZETU.



MTUNZI:SINGANOJR ,



SEHEMU YA 91.

Tresha alimwangalia mdogo wake kwa macho yaliojaa maswali na alitaka amwelezee alikuwa akimjua vipi Hamza , haikuwa kwake tu , hata kwa Kanali Dastani ilikuwa hivyo hivyo.

“Hamza kabadilika jamani , sio yule alienipigia magoti akinitaka”Aliongea Anitha huku akikuza pIcha ya Hamza kuikagua kama vile hakuwahi kumuona hapo kabla.

“Hamza amekupigia magoti kwa kukutaka, Anitha hebu kaa kwanza chini na utuambie unamjua vipi Hamza na uache uzushi wako”Aliongea Tresha.

“Tresha mdogo wako si mwanafunzi wa chuo cha FEMU?”Aliuliza Kanali Dastani kama kwamba kuna kitu ambacho alikumbuka.

“Ndio anamalizia sasa hivi mwaka wa mwisho”

“Basi nadhani ni kweli anamfahamu Hamza , na yeye ni mwanachuo pale , japo uanachuo wake una mashaka”Aliongea Kanali na kauli yake ilimfanya hata Anitha kushangaa.

“Uncle Dastani , unamaanisha nini?”Aliuliza Anitha , alikuwa akimfahamu Dastani kwa kutambulishwa na dada yake.

Licha ya Anitha kuuliza swali hilo Kanali hakuonyesha kutaka kulijibu na alimwangalia Tresha kwa ishara ya kuelewana.

“Anitha umesema huyo Hamza alikutongoza , au ni kama ulivyo na tabia ya kuzushia watu maarufu kukutongoza?”Aliuliza Tresha huku akimpokonya mdogo wake simu i.le

“Nakuambia ukweli Dada , kila mtu ndani ya darasa letu anajua na hata baadhi ya wanachuo , alifanya hivyo mbele ya watu kabisa na ndio maana nilimkataa”Aliongea huku akikaa chini kimapozi.

Upande wa Tresha na yeye alionekana kuangalia picha ile kwa umakini mkubwa kama kwamba anajaribu kuvuta kumbukumbu aliona wapi hio sura.

“Nadhan hata mimi nishawahi kumuona…”Aliongea na muda uleule alionekana kukumbuka.

“Amiri !, nilimuona na Amiri kwenye lift ndani ya hli jengo”Aliongea Tresha.

“Ni kweli Amiri ni rafiki yake?”Aliongezea Anitha.

“Amiri ndio nani?”Aliuliza Kanali.

“Amiri na Madam ni ndugu , Ni mtoto wa Mzee Khalfani maarufu kama Tajiri wa Zanzibar, mpenzi wake Mellisa anaishi hapa na ndio namuonaga mara kwa mara, siku moja nilipishana na Amiri akiwa ametangulizana na huyu kaka, ila hapa amebadilika”Aliongea huku akiikagua.

“Dada hata wewe umeona , Hamza amebadilika sana , huyu sio yule niliemkataa”Aliongea Anitha kwa kujiamini.

“Pengine alitaka umkatae”Aliongea Tresha.

“Unamaanisha nini dada?” Aliuliza lakini muda uleule Kanali alimpa ishara Tresha asiongee chochote.

“Namaanisha sio levo yako, nakushauri akikutongoza tena mkubalie, halafu hebu tuachie nafasi kwanza nina mazungumzo na Dastani”Aliongea kibabe na Anitha aliishia kusimama huku akipiga piga miguu chini kwa hasira za kuigiza na kuondoka.

“Kwanini hujataka nikimwambia kuhusu Hamza kuwa mume wa Regina?”

“Hii ni taarifa nyeti na unajua kabisa Anitha anasoma chuo kimoja na Hamza , kama akienda kuongea huko itakuwa ni habari kubwa na unaweza kumungiza mdogo wako kwenye matatizo na pengne hata Hamza kujua uwepo wetu”Aliongea Kanali kwa tahadhari na kauli ile ilionekana kumungia vizuri Tresha.

“Kwahio nini kinafuata?”

“Huu ndio muda sahihi wa kukamilisha hatua ya pili ya mipango yetu wakati wanausalama wengi macho yao yakiwa kwenye uchaguzi”Aliongea Kanali.

“Na kuhusu Amosi unamdhibiti vpi , maana kila kitu atataka kujua?”

“Amosi niachie mimi , najua namna ya kudili nae , lakini nikuhakikishie hawezi kuharibu mipango yetu, ni swala tu la sisi kuwa makini”Aliongea na Tresha alitingisha kichwa kukubali.

“Kesho nitaenda kuonana na Dina , nione anasemaje na baada ya hapo nitakupa mrejesho”Aliongea.

“Eliasi na yeye anaonekana kuhitaji kujua kinachoendelea juu ya hio rekodi , sijui nini kinaendelea lakini kuna dalili za kutosha sio taarifa nyepesi”

“Nakubaliana na wewe, ndio maana tunapaswa kuwa wa kwanza kupiga hatua kwenye hili , nina uhakika hatupo peke yetu tunaoitafuta”Aliongea na Tresha alitingisha kichwa kukubaliana nae.



******

Saa moja mbeleni wakati Hamza akiingia ndani ya maeneo ya hosptali ya Mayaya Clinic aliweza kukutana na Prisila na ilionekana alitoka kuonana na Regina.

“Hamza!!!?”

Prisila ndio aliekuwa wa kwanza kumuona Hamza hivyo mara baada ya Hamza kusikia akiitwa aligeuka.

Hamza ni kama na yeye hakutegemea kumuona Prisila ndani ya eneo hilo , tokea siku alioachana nae kwenye tukio la uzinduzi wa albamu hakuwasiliana nae tena.

“Mambo Prisila?”Alisalimia Hamza huku akiweka tabasamu kwenye uso wake.

“Niko poa , Poleni kwa msiba”

“Asante , ndio unatoka kumuona Regina?”

“Ndio , anaonekana kukusubiri wahi ukamuone”Aliongea Prisila huku akionekana kama mtu ambae aliionekana kugundua kitu baina ya Hamza na Regina , maana siku zote alikuwa akijua mahusiano ya wawili hao yalikuwa ya kikazi zaidi, lakini siku hio aligundua kitu kingne.

Hamza hata yeye alitaka kumuwahi Regina hivyo hakutaka kumpa Prisila muda mwingi na alishia kutingisha kichwa kumuaga, lakini wakati akipiga hatua kumpita, aliitwa kwa nyuma na kumfanya kusimama.

“Nilikupigia simu mara kibao , ila hukuwa ukipatikana”Aliongea Prisila na kauli ile ilimfanya Hamza kujishika pua.

“Nilikuwa sehemu ambayo haina mtandao ndio maana”Aliongea na Prisila alitingisha kichwa.

“Nilitaka kukuambia asante sana kwa zawadi ya gauni”Aliongea Prisila kwa sauti ya chini na Hamza alitoa tabasamu la kukubali.

“Sisi ni marafiki Prisila wa muda mrefu niliona ni sahih gauni lile likiwa mali yako maana ni kama umetengenezewa wewe”Aliongea Hamza huku akimpa tabasamu la maana na kauli ile ilimfanya Prisila kutabasamu na kumpa ishara ya kuendelea na safari na Hamza alitingisha kichwa na kumuacha bila kugeuka nyuma.

Lakini upande wa Prisila baada ya kupiga hatua kadhaa aligeuka nyuma na kumwangalia Hamza akitokomea.

“Nilidhani ni mahusiano ya kikazi pekee , sikudhania Edna atakubali kufunga nae ndoa”Aliwaza kwa macho ya huzuni kidogo na kisha aliendelea na safari.

Ukweli ni kwamba mtu ambae Hamza alikuwa akiongea nae kwa lugha ya kifaransa siku ile kabla ya kuelekea ukumbini eneo la tukio , Hamza alikuwa akifanya mawasiliano ya kufanikisha gauni alilovalishwa Prisila kuwa mali yake , sababu ya kufanya hivyo ni kutokana na kwamba magauni kama hayo mara nyingi sio ya kuuzwa kwani yanakuwa kama sehemu ya maonyesho na ikitokea mtu akipenda vazi hilo huweka oda maalumu na ndio hutengenezewa , inafanyika hivyo kutokana na gharama kubwa ya utengenezaji.

Sasa Prisila hakuwa mshamba , mara baada ya Meneja wa duka la gauni hilo kumpigia simu na kumwambia gauni hilo limelipiwa na asirudishe alishangaa sana , kwani kwake hata kama alikuwa na hela isingewezekana kulinunua.

Baada ya kuhoji ndio alikuja kugundua Hamza alitumia koneksheni zake na kumlazimisha mmiliki wa duka kuliuza kwa lazima . jambo hilo lilimfanya kuwa na shauku mno na kujiuliza ni koneksheni gani Hamza alikuwa nayo mpaka Mama Sedekia Bosi mwenye msimamo wa maduka hayo kukubali kuuza gauni hilo kirahisi, jambo lingine ambalo lilimshangaza ni kiasi ambacho gauni hilo lililipiwa, ilikuwa hela kubwa ambayo hajawahi kuwaza kuitumia kwa ajili ya kununua nguo moja tu.

Prisila alitamani kumuuliza Hamza kwanini kamnunulia gauni hilo la bei ghali hivyo na alitamani pia kulirudisha kwa Hamza lakini habari za msiba ndio zilimfanya kuweka swala hilo kiporo.

*****

Regna alkuwa amekwisha kuamka na alikuwa ameegamia kwenye Chago ndani ya wodi ya VIP, baada ya kumuona Hamza akiingia ndani ya wodi hio, kulikuwa na ishara ya kufarijika kwenye macho yake.

Shangazi mara baada ya kumuona Hamza akiingia hapo ndani alijiongeza haraka haraka na kuwaaga anaenda kumwandalia Regina chakula cha usiku na wote walitingisha kichwa kukubaliana nae.

Hamza alisogea taratibu na kwenda kukaa kwenye ukingo wa kitanda na kumwangalia Regina kwa macho yaliojaa huruma.

“Lile swala limeisha”aliongea Hamza

Tokea mara ya kwanza akutane na Regina hakuwahi kuuona akiwa katika hali ya namna hio ya kudhoofu.

“Nimesikia kutoka kwa Shangazi , asante kwa kuniokoa na kunisadia kwenye vitu vingi”Aliongea Regina kwa sauti hafifu.

Hamza aliishia kuangalia chini huku akicheka na alinyoosha mkono wake wa kushoto uliokuwa umevaa pete aliopewa na bibi yake Regina na kumuonyesha.

“Unachoongea ni ujinga , mimi ni mume wako ndio maana hii pete ipo kidoleni , kama unataka kunishukuru kwa nilichofanya angalau niite ‘Mume wangu’”Aliongea Hamza huku akimkonyeza.

Awamu hio Regina hakuwa na hasira zaidi kwamba alimwemwesa lipsi zake na kuangalia chini , ilionekana alikuwa akifikiria kukubaliana na ombi la Hamza.

Dakika moja ilipita na Hamza aliona ni kweli Regina alikuwa akimfikiria na alishindwa kujizuia kusubiria kuitwa jina tamu.

“Mu… Muu… hebu tuache bwana”Regina alitaka kuongea lakini aliishia kushikwa na kigugumizi.

“Unafanya nini , ongea basi”Aliongea Hamza lakini Regina alitingisha kichwa kukataa.

“Nashindwa kukuita hivyo….”

Hamza mara baada ya kusikia kauli hio alifurahi mno , kitendo cha Regina kujarbu kuongea kilikuwa na maana kubwa kwake.

Lakini kwasababu alikuwa akipitia wakati mgumu kwa muda huo hakutaka kumlazimisha zaidi.

Dakika chache baadae Shangazi alileta chakula cha usku kwa ajili ya Regina ambae hakugusa chakula kwa muda mrefu mno tokea atekwe.

Ijapokuwa Regina alikuwa kwenye hali ya msongo wa mawazo lakini alikuwa na njaa kali hivyo alikula kwa kujilazimisha.

Wakati akiendelea kula ni kama kuna kitu alikumbuka na alimwangalia Hamza na Shangazi.

“Vipi kuhusu Frank..?”Aliuliza .

Hamza ukweli hakujua Frank yupo wapi , ijapokuwa alikuwa mtoto wa nje ya ndoa lakini bado alikuwa akitambulika kama mwanafamilia , hivyo ingekuwa ngumu ghafla tu Regina kumchukulia kama mtu wa nje.

“Regina , Frank sio kaka yako tena na sio mwanafamilia”Aliongea Shangazi.

“Najua Shangazi lakini kila mtu anamjua kama mwanafamilia mwenzetu, siwezi kuvunja undugu ghafla tu”

“Regina, naelewa unachopitia kwasasa lakni unapaswa kujua hatima ya familia ipo mabegani mwako , huwezi kuyumba kwa kuwa na moyo mwepesi kwa watu waliokukosea , vinginevyo itakuwa ni kama kufuga chui”Aliongea na kumfanya Regina kumwangalia Shangazi yake kwa kiulizo..

“Shangazi , unanificha vitu vingi sana kwanini umebadilika ghafla tu”Aliongea Regina.

Katika macho yake alikuwa akimjua Shangazi Mariposa ni mwanamke ambae umri umeenda na ana ukomo wa kufanya vitu vngi tofauti na kijana , lakini muda huo alimuona mtu tofauti ambae anaweza kufanya kitu chochote ambacho kijana anaweza kufanya.

Kingine ni namna yake ya uongeaji , aliona kama Shangazi yake ni yule anaemjua basi angemuunga mkono kwenye swala la Frank, lakini muda huo aliongea kama mlinzi.

“Regina nataka kukuambia kauli ya mwisho ambayo bibi yako alitaka uisikie”Aliongea Shangazi.

“Kauli gani hio?”Aliuliza Regina kwa mshangao na shauku.

“Ukikubali kuvaa taji , ukubali na uzito wake”Aliongea.

Kauli hio ilimshangaza mno Regina, kwani hakuelewa kwanini bibi yake ameongea maneno ya aina hio kama kauli ya mwisho.

Hata Hamza hakuelewa na aliona pengne majukumu ambayo Regina ameachiwa ni makubwa ndio maana akaongea hivyo.

“Shangazi lakini sisi si wafanyabiashara tu hapa Tanzania , kwanini bibi kaongea kauli ya namna hio?”Aliuliza Regina.

“Regina unachotakiwa kukumbuka ni hayo maneno na yatakusaidia sana huko mbeleni , kuna mambo mengi yanatokea katika maisha ya mwanadamu , kama ilivyokutokea je uliwahi kuwaza kuna ulimwengu wa giza hapo Kabla na una nguvu kubwa?”Aliuliza Shangazi na Regina aliishia kukataa.

“Hiki ndio kitu ambacho siku zote watu wa kawaida wanashindwa kuona, vita halisi siku zote inapiganiwa gizani, haijalishi una utajiri kiasi gani au ushawish kiasi gani , mbele ya macho ya muuaji hakuna kiasi cha pesa ambacho kinaweza kutosha kuacha kuondoa uhai wako , mtu yoyote ambae anaitwa tajiri leo hii hajategemea uwezo wake wa nnje tu ule unaonekana lakini pia kuna nguvu nyingine iliojificha gizani. Sababu ya babu yako na bibi yako kukupa msaada wa kurithi biashara za familia ni kwasababu baba yako hakuwa na uwezo wa kutosha”Aliongea.

Ijapokuwa Regina bado hakuwa ameelewa vzuri lakini pia aliweza kugundua kitu na aliishia kuinamisha kichwa chake chini huku akila kimya kmya akionekana kuna kitu ambacho anakiwaza

Shangazi kwasababu alikuwa na maandalizi ya msiba aliondoka wa kwanza akimtaka Regina abakie hapo hospitalini mpaka siku inayofuata ili kupunguza uchomvu.

Hamza pia asingeweza kuondoka hivyo alienda kukaa zake kwenye sofa na kuanza kuchezea simu yake kwa kuperuzi mtandaoni.

Saa tatu za usiku, ikiwa ni nusu saa tu tokea Shangazi kuondoka , wafanyakazi wa ngazi ya juu wa kampuni waliweza kufika hospitalini kumtembelea Regina kasoro Prisila ambae alikuwa ameshawahi tayar kufika na kuondoka.

Taarifa za Kampuni ya Dosam kurithshwa yote kwa asilimia kubwa kwenda kwa Regina haikuwa siri tena.

Kwanzia siku hio Regina alikuwa ndio Shareholder mkuu wa kampuni katika vipengele vya sheria na hadhi ya kifamilia.

Hivyo kila mfanyakazi alitaka kujitahidi kuwa upande mzuri na Regina kama bosi wa kampuni.

Wakati taarifa zikitangazwa makampuni ya Dosam kuwa chini ya umiliki wa Regina kama mwanahisa mkuu , upande wa kampuni ya Zena ilitangazwa kufirisika rasmi baada ya Asset zao kuhitajiwa na benki kama fidia ya malimbikzo ya mikopo.

Kutokana na taarifa hio ya kampuni ya Zena kufirisika taarifa za Regina kuifanya kampuni hio kufirisika zilisambaa kwa wingi kuliko hata ile ya kuwa mrithi.

Taarifa hio ilifanya viongozi wakubwa wa makampuni mengi nchini kupatwa na wasiwasi wa ki ushindani zidi ya Regina.

Taarifa za kupotea kwa James na Mzee Benjamini zilihusishwa na Regina pia ambae alionekana kufaidika zaidi kwa kipindi cha muda mrefu kwa kuilalia kampuni ya Zena.

Hivyo kwa utashi wa watu waliamini kupotea kwa wawili hao ni Regina ambae alikuwa akihusika , huku wengi wakimbatiza jina la Black Widow yaani mwanamke hatari kama Buibui.

“Mkurugenzi…!!”

Ilikuwa ni saa nne kamili za usiku na alionekana Eliza akingia ndani ya wodi aliolazwa Regina.

Muonekano wa Eliza ni kama alitokea kazni na sio nyumbani na alionekana kuloa kiasi kutokana na mvua kuanza kunyesha muda si mrefu.

“Lizzy unafanya nin hapa , si nilikutumia meseji?”Aliuliza Hamza na namna ambavyo alimwita ilimfanya Eliza kukosa utulivu maana ni mara ya kwanza kuitwa hivyo mbele ya Regina.

“Hata kama umeniambia anaendelea vzuri , haimaanishi ni kweli kwa Mkurugenzi , nimechelewa kufika maana nilihitaji kuja wakati watu wamepungua kidogo”Aliiongea Eliza

Regina uso wake ulikuwa na ukauzu wakati wa kumwangalia Hamza lakini hakuongea kitu na alimpa ishara Eliza kukaa kwenye sofa

Eliza mara baada ya kukaa alifungua mkoba wake na kutoa nyaraka.

“Hizi ni nyaraka za mikataba ambazo Linda aliandaa leo , alihofia kuja mapema kwa kuogopa kutakuwa na watu wengi hivyo alinipatia nimsaidie kuzifikisha”Aliongea na kauli ile ilimfanya Hamza kutingisha kichwa chake kwa kutokubaliana na hali ile.

“Eliza kwanini tusiachane na maswala ya kazi kwanza , bado hajapata nguvu za kutosha huyo”Aliongea Hamza na Eliza mara baada ya kusika kauli ile haraka haraka alirudisha zile nyaraka.

“Samahani ,, nilishazoea ku…”Eliza alijikuta akishindwa kuongea neno na kigugumizi chake kilimfanya Regina midomo yake kucheza.

“Usiwe na waswasi , hebu niziangalie kwanza akili yangu haijachoka bado licha ya uchomvu”Aliongea Regina na alipokea zile nyaraka kutoka kwa Eliza na kuanza kuzipitia taratibu taratibu , hali ya chumba hicho ilikuwa nzito mno na hio yote ni kutokana na Triangle ya kimahusiano kwa wote watatu kutokuelezeka.

Hamza hakuona tatizo sana kutokana na kutokuwa na aibu , Regina hakuwa na mabadliko yoyote na alionekana kuwa siriasi kwa kile alichokuwa akifanya , Eliza ndio ambae alikuwa na wasiwas kuliko mtu yoyote hapo ndani , alikuwa ashafanya maamuzi ya kuendelea na Hamza tokea wakiwa Morogoro mara baada ya Hamza kukutana na baba yake,lakini hakuzoea hali hio hata kidogo.

Muda huo alijikuta hata akishindwa kujua mikono yake aweke wapi , alikuwa na wasiwasi mno kiasi cha kumfanya kuanza kutoka jasho na wasiwasi wake ulimfikia Regina.

“Eliza mbona unatoka jasho sana , unajisikia vbaya?”Aliuliza Regina.

“Ah! Hapana niko vizuri”Aliongea Eliza huku akijifuta jasho.

Hamza aliona ni kama Regina anamuonea Eliza , maana alikuwa akijua hali ho inasababishwa na nini lakn bado akauliza.

“Eliza Relax, tunakwenda kuwa familia kwanzia sasa , huna haja ya kuwa na wasiwasi hivyo”Aliongea Hamza huku akicheka.

“Wewe.. hebu acha kuongea…”

Eliza uso ulizidi kupata moto baada ya kuona Hamza anazidisha matatizo.

“Hebu kaa kimya , wewe ndio unamsababishia mwenzio wasiwasi , hebu kakae upande ule”Aliongea Regina kikauzu.

Hamza kwa utii aliishia kurudi nyuma na kwenda kukaa mbali ,alijiambia ili mradi Regina ukichaa haumpandi basi anapaswa kuwa mtiifu.

“Naomba karamu”Aliongea Regina.

“Ok”Aliongea Eliza huku akipatwa na ahueni na kwa haraka haraka alichukua karamu na kumpatia.

Regina alionekana kusaini nyaraka hizo kwa dakika ishirini zote mpaka kumaliza.

“Kuna kitu kingine?”Aliuliza na kumfanya Eliza kusita kidogo lakini aliongea.

“Mkurugenzi labda hujaona taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii, kuna uzushi unaoendelea kusambaa wenye athari mbaya kwa kampuni , watu wanasema umehusika na kupotea kwa James na baba yake na kupelekea kampuni ya Zena kufilisika…”

“Unaogopa hisa zetu kushuka kwasababu ya huo uzushi?”Aluliza Regina,

“Ndio Mkurugenzi , tumeanza ushirikiano wetu wa kibiashara na kampuni ya Moro Tech , lakini vilevile malengo yetu ni kujipanua zaidi katika soko la Ulaya mwaka huu, kama hisa zetu zikishuka sana itaondoa hali ya kujiamini kwa wawekezaji na wanahisa”Aliongea Eliza .

“Kitendo cha Kampuni ya Zena kufilisika imetengeneza fursa kwa baadhi ya watu, wanachokifanya sasa hivi ni kutibua kisima wakati huo wakigawana mali”Aliongea Regina

“Kwahio bos , vipi mpango wako katika hili?”Aliuliza Eliza na kumfanya Regina kufikiria kidogo kabla ya kujibu.

“Ngoja nikuulize swali , chukulia mpo kwenye boti katikati ya bahali na ghafla tu boti yenn ikapinduka na mkatumbukia majni , eneo ambalo mmetumbukia kuna Papa kibao wanaotaka kuwararua , unadhani ni mbinu ipi nzuri ya kujiokoa?”Aliuliza Regina.

“Inabidi kuogelea kwa spidi na kuwakimbia Papa kwa kadri ya uwezo wako”Alijibu Eliza lakni Regina alitngisha kichwa kukataa.

“Huwezi kumzidi Papa kwenye mbio za kuogelea , unachopaswa kufanya ni kuwazidi mbio wenzako uliozama nao na utafanikiwa”Aliongea na palepale Eliza macho yake yalichanua mara baada ya kuonekana kuelewa fumbo lile.

“Nimekuelewa Mkurugenzi , nitawasiliana na watu wa vyombo vya habari ambao tuna mahusiano mazuri nao na kuwapa kazi”Aliongea Eliza.

Hamza ambae alisikia kila kitu alishia kujiambia kwenye mbinu Eliza hakuwa vizuri kama Regina.

Kwa ambacho alielewa ni kwamba kwasababu alikuwa akiongelewa vibaya kwenye vyombo vya habari basi anapasswa kuwaongelea vibaya wengne kuwazidi na kwasababu yanayoongelewa hayana ushahdi basi ingekuwa rahisi kupindua meza na hatimae ukweli utajitokeza, yaani kwa lugha nyepesi kama kuna mtu kalipa vyombo vya habari kumchafua Regina basi anachoenda kufanya Eliza ni kulipa kiasi kikubwa zaidi ili kugeuza uzushi.

“Mkurugenzi , mimi ngoja nikuache upumzike nisiendelee kukusumbua”Aliongea Eliza akitaka kuondoka , lakini Regina alimzuia.

“Senior nina kitu nataka kukuambia kabla hujaondoka”Aliongea Regina.

Eliza alijikuta akishikwa na wasiwasi , lakini mara nyingi akisikia Regina anamwita Senior basi ni swala linalohusiana na kazi.

“Kesho nitasafiri kwenda nyumbani kumzika bibi na baba, sitoonekana kazini kwa siku kadhaa”

“Mkurugenzi ukiondoka kwa muda mrefu shughuli za kampuni….”

“Kampuni ilikuwa na wakurugenzi wasaidizi wawili , na kwasasa nafasi hizo zimebakia wazi , napanga kukuteua kuwa Mkurugenzi msaidizi na Prisila Afisa msimamizi mkuu wa kampuni Tanzu katika kikao cha bodi ya wakurugenzi kitakachofanyika mwezi ujao mapema, kwanzia wiki hii nataka uni kaimu kama CEO , nitamwamba Linda kukusaidia kadri awezavyo”Aliongea Regina.

Kitendo cha kuskia kauli hio , Eliza alijihsi kichwa chake ni kama kinapaa na muda wowote atadondoka chini na kupasuka.

“Mkurugenzi hapana , hiko cheo ni kikubwa tofauti na umri wangu..”Eliza alijikuta akijitetea, lakini baada ya maneno hayo kumtoka alijiona ni kama mjinga maana kama ni umri yeye alikuwa mkubwa kuliko Regina.

“Umri sio kigezo kwa ulimwengu wa leo , kinachoangaliwa ni uwezo wako na uelewa , nimekuchagua kwasababu unazielewa vzuri mbinu zangu za kibiashara kuliko mwandamizi yoyote ndani ya kampuni,kingine nakuamini sana ndio maana nilikupa hata kazi kubwa ya mazungumzo ya biashara na kampuni ya Moro”

Eliza alijikuta akibakia kimya , macho yake yalichanua huku akimwangalia Regina na kisha Hamza , lakini mwisho wa dakika hakuwa na sababu ya kukataa.

“Nimekuelewa Mkurugenzi nitajjitahidi kadri ya uwezo wangu”Aliongea

“Sitaki mtu ambae atajitahidi, nataka mtu ambae atafanya kazi zake vizuri, ndio sera ya Kampuni ya Dosam”Aliongea Regina.

“Nitafanya vizuri bosi”

Hamza aliishia kusikliza mazunguzo hayo bila ya kupiga kelele , moja ya kitu ambacho almkubali Regina ni uwezo wake wa kutenganisha maswala bnafsi na kazi , muda wote akikutana na Eliza maongezi yao ni ya kikazi zaidi.

Baada ya muda kidogo Eliza aliondoka na kumwacha Hamza na Regina.

“Na wewe unaweza kuondoka ukapumzike , haina haja ya kubakia hapa”Alongea Regina.

“Kwanini isiwe na haja , ni vizuri zaidi tukikaa wote hapa na kukuchangamsha la sivyo utashikwa na mawazo tu”Aliongea na muda ule ni kama Regina amekumbuka.

“Hivi ulijua Shangazi anajua mapigano?”Aliuliza na swali lile lilimfanya Hamza kushangaa kidogo maana hakudhania Regina angeingia katika hio mada, lakini Hamza hakuona haja ya kumficha.

“Mtu ambae ana mafunzo ya mapigano , mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi, uwiano wa hatua , ni watu tofauti sana, kadri unavyowaangalia unaweza kumtofautisha na mtu wa kawaida”Aliongea Hamza.

“Kwahio unasema na bibi alikuwa na mafunzo?”

“Bibi yako hakuwa na mafunzo yoyote , nadhani pia hata kwa babu yako, pengine hawakutaka kujingiza kwenye ulimwengu wa giza”Aliongea Hamza.

“Ukizungumzia ulimwengu wa Giza unamaaniisha nini?”Aliuliza Regina kwa shauku na kumfanya Hamza kukuna kichwa.

“Swali lako ni pana mno , siju hata namna ya kukujibu”Aliongea Hamza.

“Basi nielezee kwa kutumia msingi wa wale watu walioniteka”Aliongea Regina na Hamza alipata nafuu.

“Katika ulimwengu wa Giza kundi la nafsi zinazotangatanga wanachukuliwa kama kundi la daraja B , kwasababu ukubwa wa shughuli zao ni mdogo na hawajapitia majaribio mengi , kwa lugha nyepesi unaweza kusema mafanikio yao mengi yametokana na hila”

“Daraja B!, kwahio unamaanisha kuna daraja A?”

“Daraja la chini kabisa ni C na madaraja ya juu ni B, A na S , ukizungumzia daraja S , unatoka kwenye kundi na unangia kwenye umoja ama taasisi”Aliongea Hamza.

“Ni Vigezo gani vinatumika kuyapanglia hayo madaraja?”











SEHEMU YA 92

“Kigezo knachoangaliwa ni kushinda na kushindwa”Aliongea Hamza.

“Unamaanisha nini?”

“Inamaanisha kwamba kundi linaangaliwa lilipigana vita vingapi au wamekamilisha misheni ngapi na kushinda au kushindwa na ndo maksi zao hupatikana , kwa mfano chukulia kama wewe ni mtu na umeua watu kumi , maksi zako zitahesabiwa kama moja kwa kumi , ukiua mia ziitahesabiwa moja kwa mia hivyo hivyo na kuendelea , huu ni mfano tu wa baadhi ya vitu vinavyoangaliwa, kuna zaidi ya hivyo lakni msingi upo hivyo. Mfano chukulia kundi la Nafsi zinazotangatanga maana yake ni kwamba wamekamilisha misheni ambazo maksi zao zimefikia moja kwa mia , Kundi A maana yae wamejikusanyia maksi moja kwa elfu moja na kundi S maana yake wamejikusanyia maksi moja kwa elfu kumi”

“Kwahio unamaansha kwamba ili kudi lifikie daraja S lazima liue watu elfu kum?”Aliuliza Regina.

“Hapana kuua nimetolea mfano tu , ni kama nilivyosema inaweza kuwa misheni ama kuua , kwa mantiki hiio kundi S wanaweza kuwa umoja ambao umekamilisha misheni ambazo ni zaidi ya elfu kumi na hizo misheni zote zilifanikiwa ndio maana wanapewa daraja hilo, kwa Ninja ama Assassin pia wanapewa madaraja hayo hayo na hapa sasa ndio unaweza kusema kuna muuaji daraja A ambae ameua zaidi ya watu elfu moja na kuna muuaji daraja S ambae ameua watu zaidi ya elfu kumi”Aliongea na Regina macho yalimtoka.

“Kuna utofauti gani kati ya Assassin na Ninja ?”Aliuliza Regin.

“Assassn ni muuaji , kazi yake ni kuua tu na si vinginevyo ila Ninja kazi yake ni zaidi ya kuua anaweza kuwa Shushu au Jasusi ambae amepewa misheni sehemu flani na akipewa maagizo ya kuua anaua lakini wakati huo huo anaweza kutumika kukusanya intelijensia”Aliongea Hamza na kumfanya Regina kutingisha kichwa kwa kuelewa.

“Kwa mantiki hio kuna maninja wa daraja S na Assassin wa daraja S?”Aliuliza.

“Ndio , Ninja wa daraja S ana mafunzo yote ya Kikomandoo hata zaidi, lakini hamaanishi ameua watu elfu kumi mpaka kufikia daraja hilo , muda mwingne kinachoangaliwa ni nani unaemua , kama umemuua mtaalamu wa juu wa kimapigano inazidishwa mara kumi au mara mia zaidi kulingana na uwezo wake. Unaonaje ni ukichaa si ndio?”Aliulza Hamza huku akitabasamu lakini upande wa Regina alionekana kufikiria.

“Nani ambae anasimamia huu mfumo mzima wa ugawaji maksi na madaraja?”Aliuliza Regina.

“Ni taasisi za siri tofauti tofauti ambazo zinapatikana katika mataifa makubwa masalani yale yenye uchumi mkubwa , hizi taasisi zenyewe zimejiunganisha na kutengeneza umoja wa kitathimini usio funganishi ambao unaitwa SETH , au unaweza kuita Set Association.

Set
alikuwa ni mungu wa vita na machafuko wa Misri ya kale na ndio maana ili kuendana na ulimwengu wa giza ukapewa jina hilo , moja ya kazi kubwa ya huu muungano kazi yake ni kufuatilia na kutathimini ukubwa wa taasisi kulingana na mafanikio ya mapigano ama mafanikio ya misheni za siri zinazofanyika , kwa hio wakitoa maksi za juu maana yake hio taasisi au huyo muuaji amekamilisha kazi yake kwa asilimia mia moja. Vipi bado hujaelewa tu?”Aliuliza Hamza kana kwamba anajaribu kumfundisha .

“Kwanini wewe unayajua hayo mambo yote ya Giza?”Aliuliza Regina.

“Nishawahi kuwa kwenye mfumo ndio maana najua sheria zao”

Regina aliishia kuguna tu na kuacha kuendelea kuuliza maana alijua Hamza asingeongea kila anachokijua

Siku iliofuata taratbu za mazishi zilianza mara moja , lakini ajabu ni kwamba hakukuwa na habari za kuaga mwili ndani ya jiji la Dar es salaam, kwani baada ya miili kutolewa hospitalini ilisafirishwa moja kwa moja kwenda Tanga.

Hamza , Regina na Shangazi walipanda gari moja kuelekea msibani huku baadhi ya wafanyakazi wa kampuni wakienda pia.

Ulikuwa msiba wa kawaida kana kwamba aliefariki alikuwa sio mtu mashuhuri lakini kulingana na maelekezo ya Marehemu , hakutaka msiba wake uwe kama sherehe.

Tanga ndio sehemu ambayo palikuwa nyumbani kwa familia nzima ya Dosam hata bashara zao zilianzia mkoani hapo kabla ya kuhamia rasmi jijini Dar es salaam miaka mingi iliopita.

Baadhi ya ndugu , jamaa na marafiki walijumuika na Regina kumsindikiza Bi Mariaum na Mzee Wilsoni, ulikuwa msiba usiokuwa wa kawaida kutokana na kwamba baba na mama wanazikwa kwa siku moja.

Kijiji cha Malunde ndio kulikuwa na bustani maalumu ya makaburi ya familia ya Dosam kwa ajili ya kuzikia.

Hamza mara baada ya kusikia anaenda kwenye bustani hio ya kuzikia alijua kutakuwa na makaburi mengi lakini ajabu kulikuwa na makaburi machache mno na mengi yalikuwa ya zamani na moja tu la babu yake Regina ndio lilionekana kutokuwa la zamani.

Ki ufupi hayakuwa maziko makubwa sana wala madogo sana , yalikuwa ya wastani na karibia watu waliohudhuria walikuwa ni wale waliokuwa karibu na familia ya Regina.

Moja ya watu ambao Hamza alikuwa akiwafahamu , waliohudhuria maziko hayo ni baba yake Prisila , Profesa Singano na hata yeye alishangaa kumuona Hamza ndani ya eneo hilo , lakini mara baada ya kupata kuujua ukweli Hamza alikuwa na mahusiano na Regina alijikuta akishangaa na kuridhika kwa wakati mmoja.

Wakati Edna akizika wanafamilia wake , upande wa Chriss alikuwa akimzika baba yake mzazi Mzee Gabusha na ndio msiba uliokuwa mkubwa zaidi jijini Dar es salaam , pengine kufanya hata msiba wa Regina na baba yake usifahamike.

Siku mbili mbeleni muda wa jioni Hamza na Shangazi walitoka nyumbani kwenda makaburni kumsindikiza Regina ambae siku inayofuata alipanga kuondoka kurudi Dar es salaam na kuendelea na mambo mengine, hivyo kabla ya kuondoka alitaka kumuaga babu yake , bibi yake na babu yake.

Siku hio ilikuwa na mvua kubwa lakini haikumzuia Regina kutoka nyumbani kuelekea msitu wa Malunde inapopatikana bustani ya makaburi ya familia yao.

Baada ya kushuka kwenye gari, kutokana na Regina kushikilia mashada ya maua Hamza ilibidi amshikie mwamvuli huku Shangazi akiwa ameshika wa kwake akifuata nyuma nyuma.

Makaburi hayo yalikuwa juu ya mlima karibu kabisa na msitu , lilikuwa ni eneo kubwa ambalo mazingira yake yalitengenzwa na kuwa ya kuvutia.

Sasa baada ya dakika chache kutembea kutoka barabarani mpaka kwenye makaburi , wote walijikuta wakishangaa mara baada ya kumuona mwanaume akiwa amekalia juu ya kaburi la Bibi yake Regina.

Alikuwa ni mwanaume wa makamo alievalia joho la rangi nyeupe na mshipi mweusi kiunoni , alikuwa na nywele nyeupe kama mvi na alionekana wakat wa ujana wake alikuwa ni mweupe.

Si Regina wala si Hamza walionekana kumfahamu yule mwanaume , lakini upande wa shangazi mara baada ya kumwona yule mwanaume uso wake ulijawa na hali ya wasiwasi.

“Wewe ni nani?”Aliuliza Regina mara baada ya kusogea karibu kabisa huku akimwangalia yule mwanaume.

Yule mwanaume alionekana kuwa bize kuangalia kaburi hilo huku akiwa kama mtu ambae amepotelea kwenye mawazo na mara baada ya kuskia kauli ya Regina aligeuka na kuwaangalia.

“Wewe tu ndio uliebakia?”Aliuliza yule mwanaume huku akimchunguza Regina.

“Wewe ni nani?”Aliuliza Regina kwa mara ya pili akiwa siriasi na kumfanya yule mwanaume kusimama.

“Jina langu naitwa Wisu lakini sina hakika kama ushawahi kunisikia”Aliongea

‘Wisu!!”Regina aliishia kuguna na kisha alimgeukia Shangazi ili kujua kama anamfahamu huyo mwanaume lakini shangazi alitingisha kichwa kuashiria hakuwa akimjua.

“Wewe ni nani na kwanini upo kwenye makaburi ya ndugu zangu?”Aliuliza Regina na yule bwana alianza kucheka kwa sauti kama vile ameshikwa na kichaa na wale wasielewe sababu ya kucheka kwake ni nini.

“Unayaita haya ni makaburi?”Aliuliza.

“Kama sio makaburi ni nini?”Aliuliza Regina.

“Haina haja hata nikikuambia , unaweza kusema unavyojiskia ila usiniulize mimi ni nani maana itakuwa habari mbaya kwako, nipo hapa kwasababu nilikuwa nikikusubiria na unipatie ninachotaka”Aliongea yule mwanaume.

“Kitu gani unachotaka kwangu?”Aliuliza Regina huku akionekana kuchanganyikiwa , alijua pengine shangazi aliekuwa nyuma yake alikuwa akijua kitu na alikuwa akimficha.

“Ninachotaka kutoka kwako ni pete aliokuachia bibi yako”Aliongea na kauli ile ilimshangaza Regina na alimgeukia Hamza mara moja.

“Hio pete ni mali ya familia yetu na ni kama ishara , kwanini nikupatie ilihali hata sikujui?”Aliongea Regina.

“Hio pete sio mali ya familia yenu , wala sio ya kwako , kwa jinsi ulivyokuwa dhaifu hutokuwa na uwezo wa kuilinda”Aliongea

“Samahani mzee , kwa mtazamo wangu nakuona kama mwizi , na siwezi kukupatia pete ya ukoo wetu”Aliongea Regina kikauzu na kumfanya yule bwana kumgeukia Shangazi.

“Kama sikosei wewe ndio Mariposa , unadhani anachojaribu kufanya huyu msichana ni sahihi?”Aliuliza

Regina palepale aligeuza uso wake nyuma na kumwangalia Shangazi , ilikuwa ni kama alivyotegemea alikuwa akimfahamu huyo Mzee Wisu.

“Mimi ni kijakazi wa famlia, hayo maswala sio wajbu wangu”Aliongea Shangazi.

“Kweli! Bado tu mpaka sasa unajichukulia kijakazi , lakini hata hivyo sijali maana naamini Regina unamchukulia kama ndugu yako”Aliongea na palepale alibadilika na kuwa mtu mwngine kabiisa aliejaa uovu ndani yake na ghafla tu alimsogelea Shangazi kwa spidi akitaka kumkaba shingo, lakini shangazi alishtuka mapema na alirusha mwamvuli wake na kurudi nyuma kwa kufyatuka kama kwamba alikuwa amesukumwa na upepo.

“Shangazi!!!”

Regina aliita kwa nguvu akiwa haamini kama huyo mzee Wisu angeanza kumshambulia Shangazi.

Yule mzee Wisu alikuwa mwepesi mno kwenye utembeaji wake , ilikuwa ni kama vile kuna nguvu imeshikilia miguu yake na kumfanya kuwa mwepesi, yote hayo yaliwezekana kutokana na nishati za mbingu na ardhi, wote wawili Shangazi Mariposa na Mzee Wisu walikuwa na mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi kulingana na msisimko waliokuwa wakitoa.

“Mariposa , kwa uwezo wako ni aibu kuendelea kuwa kijakazi wa familia ya Dosam?”Aliongea Mzee Wisu huku akianza kufukuziana na Mariposa.

Shangazi mara baada ya kuona hawezi kumkwepa Wisu , palepale alisimama na kuanza kupambana nae ana kwa ana na wakati huo akimgeukia Regina.

“Hamza mbebe Regina ukimbie nae”Aliongea Shangazi kwa sauti iliojaa tahadhari na usiriasi ndani yake , ikiashiriia hali sio nzuri kwao.

ITAENDELEA.
 
SHETANI RUDISHA AKILI ZETU.



MTUNZI: SINGANOJR



SEHEMU YA 93.

Haikuwa rahisi kwa Regina kuondoka ndani ya eneo hilo amuache Shangazi yake , Familia yake yote ilikuwa imekwisha kutangulia mbele za haki na mtu pekee ambae alikuwa ni mwanafamilia alikuwa ni Shangazi na kama atauliwa na huyo mtu ingekuwa ngumu mno kwake kukubaliana na swala hilo.

“Naomba uache , Mzee Suwi sikujui wewe ni nani , lakni naomba uache unachokifanya tafadhali”Aliongea Regna lakini bwana alieitwa Mzee Suwi hakuwa na nia ya kuacha.

Muda huo Shangazi alikuwa ashasukumizwa kwa shambulizi na kwenda kugonga mlima na kufanya mawe kuanza kuporomoka wakati huo huo akiachia shambulizi la wimbi la upepo kumshambulia Mzee Suwi lakini bwana yule alionekana kuwa mtaalamu kwa kile alichokifanya kwani alichezesha vidole na wimbi la upepo lilimrudia Shangazi kwa nguvu.

“Bam!!”

Nguvu halisi ya nishati za mbingu na ardhi ililiripuka na kumfanya Shangazi kutoa yowe la maumivu huku kila kiungo cha mwili wake kikiwa kimekufa ganzi kutokana na maumivu makali.

“Ndio kwanza upo kwenye levo ya Wito na mimi mwishoni mwa levo ya Wito , nimekuacha hatua nne mbele , huwezi kunishinda hata kidogo”Aliongea Suwi huku akitoa tabasamu la ujivuni na kupiga hatua mbele kutaka kumkamata Shangazi.

Shangazi alichokifanya ni kusogea upande wa kushoto kwake na kisha alifyatua jiwe kwa nguvu kubwa na lilienda moja kwa moja kutua kwenye kifua cha Suwi.

“Boom!!!”

Haikueleweka kilichotokea lakini jiwe lile kabla halijamdhuru lilipasuka vipande vipande kana kwamba limepasuliwa na bomu.

“Una uwezo wa kuita Kinga ya nishati za mbingu na ardhi!?”Aliuliza Shangazi kwa mshangao.

“Kama unaijua Kinga ya nishati ya mbingu na ardhi basi jua huniwezi hata kidogo hivyo jisalimishe”Aliongea Mzee Suwi.

“Siwezi kujisalimisha kirahisi , hata kama nikiishiwa uwezo wangu wote siwezi kukuacha ufanikiwe”Aliongea Shangazi kwa ujasiri mkubwa huku akimgeukia Regina na Hamza ambao bado walikuwa wamesimama wakimwangalia.

“Hamza mbona bado umesmama hapo , ondoka na Regina haraka”

Licha ya kuongea hivyo Hamza hakuongea wala kufanya chochote,alionekana tu akifikiria kitu huku sura ikiwa imejikunja

Hata Regina hakutaka kuondoka na alimshika Hamza shati akimuomba amsaidie shangazi yake na Hamza licha ya kuombwa hivyo alisita kidogo na alimgeukia Regina na kumuuliza kama yupo tayari kuitoa pete kwenda kwa Suwi ili vita hio iishe.

Swali hilo la Hamza lilimfanya Regina kukosa jibu la moja kwa moja maana ni kama hakutegemea Hamza angemuuliza swali la namna hio.

“Kuna mawili hapa, kumsaidia Shangazi au kuondoka na wewe , lakini hata kama tukiondoka lazima watakuja tena kututafuta maana pete tunayo, labda tu uwe tayari kuwapa”Aliongea Hamza.

“Hio pete ni kitu ambacho babu yangu na bibi wamekitunza kwa hali na mahali kwa muda mrefu , haiwezekani kuikabidhi kirahisi hivyo”aliiongea Regina.

“Lakini ujue ndio mwanzo wa matatizo”

“Matatizo hayajawahi kuisha , mshindi pekee ndio anakuwa huru , simjui huyu mzee ni nani lakini ni bora nife kuliko kumpigia magoti”aliongea Regina kwa kiburi cha hali ya juu.

Hamza mara baada ya kusikia kauli hio kutoka kwa Regina macho yake yalisinyaa huku akitoa tabasamu hafifu na alinyoosha mkono wake na kumshika Regina kidevu.

“Kama nilivyotarajia , nimeoa mwanamke jasiri”Aliongea

“Wewe unanifanyia nini?”Alongea Regina mara baada ya kuona anashikwa kidevu kwa namna ambayo hapendi.

“Usiwe na wasiwasi kwasasa ninachojua mimi Shangazi hawezi kufa kirahisi”Aliongea Hamza lakini kauli yake ilimfanya Regina kuchanganyikwa, lakini dakika ileile macho yake ni kama yameshkwa na ukungu kwani Hamza alipotea mbele yake.

Upande wa Suwi alikuwa amekusanya wimbi kubwa la nishati ya mbingu na ardhi kwenye mkono wake kwa ajili ya kumshambulia nalo Shangazi.

Kutokana na Shangazi kuwa upande wa mlima ilimfanya kukosa namna ya kukwepa shambulizi hilo na kitu pekee alichofanya ni kuitutumua nguvu yake ya ndani ili kupokea pigo hilo, lakini wakati shambulizi lile linamsogelea ghafla tu kivuli cha mtu kilitokea mbele yake kama mzimu.

“Bam!”

Haikueleweka Hamza alifanya nini lakini mara baada ya kuinua mkono wake wa kulia kama anapunga upepo shambulizi la Suwi lilishindwa kumfikia yeye na Shangazi huku Suwi akikosa balansi na kudondoka chin kutokana na upepo uliotokea, mara baada ya kusimama na kuangalia upande wa Hamza alijikuta akishangazwa na jambo lile.

“Ni wewe?”

Mzee Suwi hakuweka umakini wake juu ya Hamza tokea mwanzo, kwasabbau Hamza hakuwa na msisimko wowote wa nishati ya mbingu na ardhi.

Lakini sasa sekunde hio mara baada ya Hamza kuzuia shambulizi lake na kumsukuma kiasi cha kudondoka ilimfanya kushikwa na mshituko mkubwa.

Hata Shangazi mwenyewe alijikuta akishangazwa na jambo lile , alikuwa akijua Hamza sio mwepesi tokea mwanzo lakini hakuwahi kuushuhudia uwezo wake.

“Shangaz vipi upo sawa?”Aliuliza Hamza na Shangazi alitingisha kichwa akikubali huku akihema kama mbwa.

“Wewe ondoka na Regina , niache hili swala nitadili nalo”Aliongea

Ktendo cha Shangazi kusikia kauli hio kutoka kwa Hamza alijihisi kifua kumpanda na kumshuka kutokana na presha kubwa.

Shangazi alikuwa na uzoefu mkubwa mno na alihisi kabisa uwezo wa Hamza sio wa kawaida na hauwezi kueleweka , ukweli ni kwamba tokea aanze kukaa nae alikuwa akimfuatilia mienendo yake hata kule kucheza mdundiko asubuhi asubuhi kwake hakuchukulia kama Hamza anacheza mdundiko bali aliona kitu ambachho sio cha kawaida.

Shangazi aliishia kuitikia tu huku sauti yake ikionekana ya heshima na baada ya hapo alimsogelea Regina.

“Wewe lazima utakuwa ndio mume wa Regina , kama sikosei jina lako unaitwa Hamza , si ndio?”Aliongea Mzee Suwi na Hamza aliishia kutoa tabasamu tu na muda uleule alingiza mkono wake kwenye mfuko na kutoka na ile pete.

“Unachotafuta ni hii pete sio?”Aliuliza.

Yule mzee mara baada ya kuona hio pete macho yake yalichanua huku akinyoosha mkono kuelekea kwa Hamza.

“Nipatie hio pete haraka maana sio ya kwako”

“Hii Pete ni ya kwangu na alieniachia ni Bibi Mirium”

“Acha kuongea ujinga na nipatie haraka”Aliongea yule bwana huku akiwa amekunja sura.

Upande wa Hamza hakubadili muonekano na palepale aliivaa kidoleni huku akiongea kwa kumwemwesha maneno ya kingereza.

“See-the -Truth”

Maneno yale yalimfanya Mzee Suwi kutetemeka kidogo huku uso wake ukikakamaa lakini hakuonekana kukata tamaa juu ya kupata pete ile.

“Wewe sio mwanachama wa Binamu wala huna hadhi ya damu ya watu wa Kondeni, hata uvae hio pete huwezi kuniamrisha”Aliongea.

“Kulingana na sheria za jicho la anga , haimzuii mtu ambae asie wa urithi wa damu wala asie mwanachama wa Binamu kutokuwa Mkuu wa miliki ya watu wa Kondeni, isitoshe pia umekuja peke yako hapa ikionyesha sio makubaliano ya umoja unaotokea , lakini bado nimevaa hii pete unashindwa kupiga magoti na kuonyesha heshma, kama wakuu wako wakijua hiki unachokifanya , unadhani ni kipi kitakachokutokea?”Aliongea Hamza.

“Wewe ni nani na kwanini unazijua sheria hizi za jicho la Anga kutoka Kondeni?”Aliuliza huku akiwa na mshituko na wasiwasi.

“Haha.. kama nilivyootea unaonekana umetokea Binamu bila idhini ya wakuu wako”

“Itategemea kama utakuwa hai na kusambaza taarifa zangu la sivyo sina cha kuogopa”Aliongea na palepale ulitokea mkandamizo mkubwa wa nishati ya mbingu na ardhi na ghafla tu kwenye mikono yake kulitokea tufe la hewa la rangi nyeupe na alilirusha kuelekea aliposimama Hamza na mpira ule wa nishati uligeuka na kuwa kama mshale wa moto mweupe ukitaka kumshambulia Hamza kila pande.

Hamza upande wake hakuonyesha kushitushwa na shambulizi lile na alisimama sehemu moja kama mtu ambae hakuwa na nia ya kukwepa.

Upande wa mbali , Regina na Shangazi walijikuta wakishikwa na kiwewe mara baada ya kuona Hamza amesmama tu bila ya kufanya chochote wakati anashambuliwa.

“Hamza kimbia, kimbia!”Regina alishindwa kujizuia na kumpigia Hamza makelele.

Upande wa Mzee yule mara baada ya kuona Hamza anakaribia kumezwa na moto wa nishati ya mbingu alijikuta akitoa tabasamu la ushindi.

“Bang , Bang , Bang!!!”

Ulikuwa ni mlipuko mkubwa ambao haukuwa na moto uliosikika na kusababisha upepo mkubwa kiasi cha baadhi ya miti ambayo haikuwa na mashina imara kudondoka huku sehemu aliosimama Hamza ikiwa mefunikwa na wingu kubwa kama la mvuke na kumfanya asionekane.

Sasa mara baada ya kiwingu kile kuisha wote walijikuta wakishangaa mara baada ya kutokumuona Hamza , hata kama ameyeyushwa na shambulizi hilo jambo ambalo haliwezekani mifupa ingebakia lakini haikuonekana kitu kilichomfanya Mzee Suwi kuona kuna kitu hakipo sawa na kuanza kugeuza uso wake kulia na kushoto akimtafuta Hamza.

“Unanitafuta?”Aliongea sauti ya kichokozi ilisikika nyuma yake na kumfanya Mzee huyo kutetemeka.

Kitendo cha kugeuka na kumuona Hamza akiwa nyuma yake bila kuonyesha ishara yoyote ya kuumia alijikuta macho yakimtoka.

“Nishati za mbingu na ardhi siku zote zina nguvu kubwa , hakuna ubishi wa wewe kutokea Kondeni, lakini kwa bahati mbaya hata kama shambulizi lako lina nguvu kiasi gani litaweza kumuua mtu ambae sio mjuzi pekee”Aliongea Hamza huku akicheka.

“Wewe.. umewezaje..”Mzee Huyo hakuweza kuelewa Hamza amepotea poteaje katika eneo la shabaha yake , kilichomchanganya Hamza hakuwa na ishara yoyote ya kutumia nguvu mbingu na ardhi , sasa alijiuliza ina maana Hamza ametegemea pekee uwezo wake wa kuruka ndio maana ameweza kukwepa shambulizi lake.

“Mimi sio levo yako acha kujihangaisha , hivyo kabla sijawa siriasi ni bora ukaondoka”Aliongea Hamza na kauli yake ilimfanya Suwi kushikwa na hasira mno kwani aliona ni kama kudharauliwa uwezo wake na kwa ukaribu aliokuwepo kati yake na Hamza alijiambia hawezi kumwacha aondoke hata kidogo hivyo alipanga kumshambulia , lakini Hamza alikuwa na spidi mno kwani palepale alimsogelea kwa spidi na kumshka mkono kwa nguvu.

“Narudia tena, mimi sio levo yako hivyo ondoka hapa?”Alongea Hamza kwa msisitzo na baada ya hapo alimvuta kwa nguvu kupitia ule mkono wake na kumrusha.

Mzee Suwi alijikuta akizunguka zaidi ya mara nane hewani kutokana na namna alivyorushwa na kwenda kudondokea kwenye makaburi..

Baada ya kujigonga chini alihisi maumivu makali mno , huku mkono ambao Hamza aliutumia kumrushia uliumia mno na alihisi ni kama umejitegua kutoka kwenye viungio vya bega.

Tukio lile lilimfanya Shangazi aliekuwa akiangalia kushikwa na mshituko wa hali ya juu mno , Regina ambae alikuwa na uwezo wa kibinadamu wa kawaida hakuweza kuona kilichotokea lakini Shangazi aliona kila kitu.

Kilichompagawisha zaidi ni Hamza kutotumia nishati za mbingu na ardhi maana kwa uwezo wa binadamu wa kawaida ni ngumu kumrusha mtu umbali ule bila ya nguvu za ziada.

Makisio pekee ambayo alikuja nayo ni labda Hamza anajifunza mbinu ambayo inaenda kinyume kabisa na kanuni ya nishati za mbingu na ardhi, lakini alijiuliza kam ni hivyo inawezekana vipi maana hakuwahi kusikia kitu cha namna hio.

Mzee Suwi ambae alikuwa amechafuka matope kwenye mlima kutokana na mvua aliishia kukaa chini huku akiwa haelewi , hakujua hata ni kwa namna gani alirushwa na alijishitukia tu yupo hewani.

Alijikuta akiangalia Hamza alipo na aliona kuna umbali wa mita nyingi mno na kwa mantiki hio mtu yoyote anaweza kuamini ili kumrusha mtu kwa umbali huo Hamza ametumia nguvu nyingi sana.

“Pumbavu, wewe mwanaharamu ni nani wa kunitesa kiasi hiki?”Aliongea kwa sauti kubwa na Hamza aliishia kumwangalia Suwi akiwa upande wa chini wa makabuli na alipiga hatua mbili tu alikuwa ameshafika alipo.

Mzee Suwi mara baada ya kuona Hamza anamsogelea , haraka haraka alirudi nyuma akionekana kumhofia kwani hakuwa akimjua Hamza vizuri.

“Huna haja ya kuogopa maana sina mpango wa kukupiga, nadhani unachopaswa ni kufikiria namna ya kudili na kitakacho kutokea”Aliongea Hamza na palepale alinyoosha mkono kuelekea nyuma yake.

Mzee Suwi mara baada ya kugeuza sura alijikuta mwili wake ukimtemeka.

Kulikuwa na mwanaume mtanashati mno alievalia suti , Mzungu ambae ana nywele nyeusi ndefu zilizofungwa na kibanio nyuma , hakuwa peke yake bali ametangulizana na watu waliovalia sare za majoho ya rangi kama vile ni wachungaji , sawa kabisa na namna ambavyo Mzee Suwi alikuwa amevalia.

“Suwi umeamua kukiuka sheria za jicho la Anga na kuja hapa kwa ajili ya kuipoka pete, hili swala limekwisha kuripotiwa kwa mkuu wetu na tumekuja hapa kukukamata na kukurudisha Kondeni ukapate adhabu yako inayokustahlili”Aliongea yule bwana Mzungu kwa lugha ya kingereza.

"Huge unaongea ujinga gani , nipo hapa kwa maagizo ya baba kwa ajili ya kutoa heshima zangu za mwisho kwa marehemu na sijaja kukwapua pete”Aliongea Mzee Suwi na muda ule alimgeukia Hamza.

“Pete unayozungumzia ipo kwenye mikono ya mtu wa nje ya umoja wetu ambae hana urithi wa damu”Aliongea huku akimnyooshea kidole.

Yule bwana aliefahamika kwa jina la Huge mara baada ya macho yake kutua kwa Hamza hasa kwenye kidole chake muonekano wake ulibadlika.

“Wewe ni nani?”Aliulza yule bwana Huge , lakini Hamza tofauti kujibu aliishia kutoa tabasamu.

“Mkuu kwahio kumbe unaitwa Huge?”Aliuliza.

“Vipi kama nikiitwa Huge?”

“Kwasababu Huge ni jina la ukoo , nikuulize je unamjua Mathiasi Huge?”Aliongea Hamza na swali lake lilibadilisha muonekano wa yule bwana mara moja.

“Unamfahamu vipi Master wangu?”Aliuliza kwa kingereza.

“Oh, kumbe ni mwalimu wako?” Aliongea Hamza huku akionekana kutaka kuongea kitu lakini alisita na kubadili mada.

“Nadhani mnapaswa kuondoka ndani ya hili eneo , ijapokuwa sijui ni kipi kinaendelea huko Kondeni na ndani ya kitengo chenu cha Binamu, lakini hii pete ni ya mke wangu , kama hataki kuwapatia basi hamuwezi kuichukua”Aliongea Hamza.

“Wewe ndio mume wa Regina?, kama ndio hivyo basi utakuwa unajua hio ni pete ambayo sio kila mtu anaweza kuivaa”Aliongea.

“Kwanza kabisa mim na Regina ni wanandoa hivyo huwezi kuniita mtu yoyote , pili hata kama nitake kuivaa huna cha kunifanya”Aliongea Hamza.

“Huge unamsikia , yaani anasema anaweza kufanya atakalo na hatuna la kumfanya , unadhani hii ni sawa?”Aliuliza Suwi.

“Kuhusu hili sina mamlaka nalo , nitaenda kuripoti kwa wakuu na ndio watakaofanya maamuzi , kuhusu wewe huna haki ya kuuliza chochote”Aliongea Huge na kumfanya Suwi kuishia kukunja sura kwa chuki, lakini bwana alefahamika kwa jina la Huge hakuwa na muda nae na alimwangalia Hamza kwa shauku.

“Sijawahi kumsikia Master akikuzungumzia , unafahamu vipi jina lake?”

“Simjui Master wako mimi , kwanini unauliza au unataka kushindana na mimi?”Aliuliza Hamza.

“Hio pete haiwezi kuvaliwa na mtu ambae hafahamiki”Aliongea Huge akiwa siriasi.

“Inaonekana watu wa Kondeni siku hizi mmechuja , yaani pete ipo kidoleni lakini hamuonyeshi heshima yoyote?”

“Kama sio heshima yetu , tungekuwa tushakushambulia sekunde tuliofka hapa”Aliongea na muda ule Hamza alinyamaza kimya akionekana kuwaza.

“Vipi kuhusu Selaph..”Aliongea Hamza na kauli ile ilivyomtoka Huge palepale muoenekano wake ulibadilika mara moja na wote walirudi nyuma kana kwamba wamekutana na adui mkubwa zaidi yao.

Wote walionekana kuwa na wasiwasi na mara baada ya kumwangalia Hamza na kuona hakukuwa na ishara za ukali alionyesha heshima yake.

“Since that’s the case , we’ll leave first and report this to my master”Aliongea akimaanisha kwamba kwasababau ipo hivyo basi wataondoka na kutoa ripoti kwa Master wao.

Muda ule Suwi na yeye alionyesha shara ya woga , alijua sasa kwanini Hamza alikuwa akmwambia sio levo yake , alijikuta akishukuru bado alikuwa hai.

“Mwambieni mkuu wenu kwamba , pete niliokuwa nayo ni ya mke wangu na itabakia kwangu kwa usalama kwanzia sasa na kwasababu ya amani iliokuwepo kati yetu na yeye haina haja ya kufanya mambo kuwa magumu”Aliongea Hamza

“Nitampatia taarifa hio kama ulivyoongea , Farewell”Aliongea na palepale aliawapa ishara wasaidizi wake wawli pamoja na Suwi na kisha walitoweka ndani ya hilo eneo.

Baada ya watu wale kuondoka hatmae hali ya utulivu ilirudi kwa mara nyingne na Hamza alivua ile pete na kisha alimkabidhi Regina.

“Regina unaonaje ukikaa nayo?”Aliuliza Hamza.

Regina aliishia kumwangalia Hamza na muonekano usiokuwa ukielezeka , ijapokuwa alkuwa ameshikiliwa na Shangazi kwa sababu za ki usalqama lakini aliweza kujua mambo mengi bila hata ya kuambiwa.

“Ulijua tokea mwanzo itakuletea matatizo sio?”Aliuliza Regina akikumbuka wakati ule alionekana kukataa na ni kama sasa anajua sababu iliokuwa nyuma yake.

“Ndio nilijua”Aliongea.

“Kama ni hivyo kwanini bado ukaipokea?”

“Siku zote anaekubali kupata lazima akubali kupoteza , kukubali kumuoa mwanamke mrembo kama wewe haiwezi kuwa bure”Alongea Hamza huku akicheka.

“Kwahio kwa kutaka kunioa ndio ukaamua kuhatarisha maisha yako kwa kupokea kitu cha hatari?”

“Regina babe , haina haja ya kuwa siriasi namna hio , nipo sawa”

“Lakini vpi kama ukifa?”Aliuiza Regina.

“Kama ni hivyo sitojutia kukuoa?”

“Wewe.,, wewe ni mjinga. Kichaa kabisa”Aliongea Regina huku sura ikimshuka.

“Regina tunapaswa kumshukuru Madam kwa kuona mbali , sikukosea nilivyomfikiria Hamza “Aliongea Shangazi na Regina macho yake yalianza kuwa mekundu.

“Tokea mwanzo mpaka sasa ni mimi pekee ambae sikuwa nikijua kinachoendeleam, najiona mjinga kweli”

“Kwanini unafikiria hivyo , tulifanya hivyo kwa ajili ya kukulinda , kuna vitu vngi sana kama ungejua mapema ungekuwa kwenye hatari kubwa”Aliongea Shangazi.

“Vipi kuhusu sasa , je sipaswi kujua ni kipi babu na bibi walikuwa wakinificha tokea mwanzo , kwanini hawa watu wamekuja na kuanza kuulizia hii pete , nataka kujua kila kitu”Aliongea Regina.

“Kuhusu hili..”Shangazi alionekana kusita.

“Shangazi sioni kuna haja ya kuendelea kumficha, mimi pia kuna vitu vngi sijaelewa na natarajia kuvijua kutoka kwako , ni kheri ukatuambia kila kitu ili tujue tunajilinda vipi baadae”Aliongea Hamza.

“Basi hakuna shida , nitawaeleza kila kitu maana sikutarajia kama watajitokeza mapema hivi , tukirudi nyumbani tutakaa chini na tutaongea”Aliongea Shangazi

Hamza na Regina hawakuwa na haraka , baada ya kuweka kaburi la bibi yake vizuri waliondoka na kurudi kwenye jumba lao la kifamilia na giza lilikuwa lishaingia tayari.

Kwasababu kulikuwa na baridi waliandaliwa chai ya moto na wahudumu na kisha wote walikaa kwenye masofa ili kumsikiliza Shangazi anachokwenda kusema.

Shangazi mara baada ya kuvuta pumzi kwa sekunde kadhaa , alionekana kukosa namna ya kuanza na alimwangalia Hamza kwanza.

“Hamza wewe unajua nini kwanza , hebu ongea na nitaongezea”Aliongea na Regina muda ule alimgeukia Hamza na kumwangalia kwa macho yake mazuri.

Hamza alitingisha kichwa chake kukubaliana nae na kisha alimwangalia Regina.

“Regina unakumbuka ile juzi nilivyokuwa nikikuelezea kuhusu madaraja ya taasisi na makundi ya ulimwengu wa Giza na nikaelezea kwa ufupi kuhusu taasisi ya daraja S?”Aliuliza Hamza.

“Ndio ulisema Daraja S ndiio la juu kabisa na wamefikia katika hatua hio kwa kupata maksi sawa na Ratio ya moja kwa Elfu kumi na kuendelea”Aliongea Regina na Hamza alitingisha kichwa kukubaliana nae.

“Kama ulivyosema , mpaka sasa dunia nzima kuna makundi au taasisi kuu tatu za siri ambazo zipo daraja S na kati ya taasisi hio moja wapo ni taasisi ya siri inayofahamika kwa jina la SkyEye au unaweza kuita watu wa Kondeni na wana tawi lao maarufu la kijasusi dunani lenye makao makuu yake katika ukanda wa Africa walilolipatia jina la B-I-N-A-M-U, kirefu chake ni Bureau of interdimensional Nexus and Multiversal understanding”

“Inasemakana kwamba hakuna kitu ambacho dunia iwe inafanya na kisifahamike kwao , ki ufupi ni kwamba hakua siri ambayo inaweza kufichwa mbele ya watu hawa wa Kondeni, ikitokea wakitaka kujua kitu chochote basi uwezo huo wa kujua wanao na si vnginevyo, wanajua siri nyingi sana , siri ambazo zinaweza kuiweka dunia hatarini kama wakizitoa na hata kuwafanya viongozi wakubwa kujisalimisha kwao, hakuna nchi wala kiongozi ambae anaweza kwenda kinyume zidi yao , hata kama uwezo wao wa kupigana ni mdogo lakini mfumo wa intellijensia ambao wameutengeneza miaka na miaka umeshikilia dunia nzima , hivyo ndio maana wakaamua kuitwa mfumo wao wa intellijensia Jicho la Anga , maana yake wanaona kutoka angani, moja ya lugha yao ya kutambuana ni kupitia kutamka neno la See-the- truth, maana yake ikiwa ni kwamba ukweli wa mambo yote hauwezi kuonekana isipokuwa kwa neno la pete ya Kondeni”Aliongea Hamza na maneno yale yalimshangaza mno Regina.

“Kwahio unasema kwamba babu na bibi walikuwa wanachama wa huu umoja wa siri?”Aliuliza.

“Hawawezi kumiliki pete na wasiwe wanachama , kwa kile ninachojua mwanacama ambae anamiliki pete basi cheo chake ni kikubwa mno, lakini hata hivyo ni mara yangu ya kwanza kusikia Mwafrika kumiliki pete yenye nguvu namna hii ya huu umoja na kisha akaonekana kama sio mwanachama , hiki ndio kitu ambacho kinanifanya kuwa na shauku ya kutaka kujua zaidi”Aliongea Hamza.

“Hamza mpaka hapo upo sahihi na inaonekana kweli unajua mambo mengi, ngoja niendelee sasa kwanzia hapo..”Alionea Shangazi na kuvuta pumzi.

“Nadhani Regina hujawahi kusikia ila babu yako Mzee Dosam hakuwahi kuifahamu famiilia yake kwasababu mama yake alibeba ujauzito baada ya kubakwa”Aliongea Shangazi na kauli ile ilimfanya Regina kushangaa.

“Shangazi unamaanisha Babu hakujua familia yake?”

“Sijasema hakuijua familia yake , mama yake ndio ilikuwa familia yake pekee, wakati mama yake anapitia kitendo hicho cha kusikitisha ndio alipoweza kuipata hio pete”Aliongea na kauli hio hata Hamza alimshangaza.

“Unamaanisha aliokota ama ilikuwaje?”Aluliza Hamza.

“Hapana sio kwa kuikotota , kwa maelezo yake mama yake Dosam alisema wakati akitokewa na kitendo hicho kulikuwa na mwanaume ambae alikuwa akiangalia kila kitu kilichokuwa kikiendelea na alijitahidi kuomba msaada kwa mtu huyo amsaidie asifanyiwe kitendo hiko , lakini yule mwanaume hakufanya chochote zaidi ya kuangalia tukio zima linafanyka mwanzo hadi mwisho na wale wabakaji kutoweka , anasema alichogundua juu ya yule mwanaume aliekuwa akiangala tukio lile, wale wabakaji hawakuwa wakimuona kama yeye alivyokuwa akimuona ndio maana hata baada ya kuomba msaada yule mtu hakuweza kusaidia , baada ya kupoteza fahamu alipokuja kushituka yupo eneo lilelile lakini yule mtu aliekuwa akimwangalia hakuwepo tena lakini aligundua kidoleni alikuwa amevishwa pete ambayo ndio hii sasa”Aliongea Shangazi na stori hio fupi ilimshangaza mno Hamza na Regina.

“Kwamba huyo mtu alikuwa ni kama kivuli tu na Mama yake Babu ndio mtu pekee aliekuwa akimuona?”

“Ndio hvyo kwa maelezo ya babu yako , alivyosimuliwa na mama yake”

“Baada ya hapo nini kilitoke?”

“Alibeba ujauzito ambao ndio ulimleta Dosam duniani , baada ya Dosam kufikisha umri wa miaka kumi na mbili mama yake alifariki na kabla ya mama yake kufariki alimuagiza Dosam kutafuta maana ya hio pete ni nini na kwanini mtu yule hakuonekana na wale watu , Dosam alimwamini mama yake juu ya stori yake kutokana na ushahidi wa hio pete, baada ya mwaka mmoja wa kifo cha mama yake ndipo alipokuja kukutana na Madam yaani bibi yako”

“Bibi!?”

“Ndio bibi yako na ndio kipindi ambacho Dosam alizama penzini na bibi yako na ndio huyo huyo ambae alimwambia maana ya hio pete”

“Unamaanisha Bibi Mirium alikuwa akijua maana ya hio pete?”AliulizaHamza.

“Kwasababu bibi yako asili yake ni ya watu wa Kondeni na baba yake alikuwa mwanachama mwenye cheo kikubwa ndani ya umoja huo na kwa muda mrefu umoja huo ulikuwa ukiitafuta hio pete”Aliongea.

“Kwahio baada ya hapo kipi kilimtokea Babu?”

“Kulingana na imani ya kimaandiko , Dosam alikuwa akisubiriwa na sio kutafutwa , kwani mara baada ya kuelezea namna alivyozaliwa ni kama ambavyo maandiko yalivyokuwa yametabiri , mtoto atakaezaliwa kutokana na mama yake kubakwa na kumiliki hio pete na ndio mwanzo wa damu mpya , hivyo Dosam mara baada ya kuelezea historia ya mama yake mara moja alitambulika kama mmiliki halali wa hio pete na kiongozi kulingana na sheria za umoja lakini Dosam alikataa kuwa kiongozi na kitu pekee alichohitaji ni Madam kuwa mke wake na kwasababu yeye na Mirium walikwisha kupendana tokea wakutane hakukuwa na pingamizi. Mara baada ya Ndoa Dosam alijiondoa kwenye Umoja na kutokana na Mirium kutokuwa na ndugu zake wengine , uongozi ukahama kutoka kwa baba yake ambae alifarki na kwenda kwa familia nyingne ambayo ni ya kizungu ambayo ni ya Huge, lakini licha ya kujitoa Dosam aliendelea kubakia kuwa mmiliki wa Pete na mtu mwenye ushawishi Kondeni, hivyo kujibu swali lako babu yako alikataa kujihusisha na maswala ya umoja , ila bibi yako alikuwa ni mzaliwa wa huko Kondeni”Aliongea Shangazi na maneno yote yalimshangaza mno Regina.

“Lakini kulingana na imani ya umoja na maandiko waliokuwa wakifundisha , kitendo cha Dosam kujitokeza ilikuwa ni kitu kilichosubiriwa kwa muda mrefu kwa maana iliaminika uzao wake utakuwa ni watoto wenye akili sana waliojaariwa vipaji , ambao wataweza kujifunza kuvuna nishati za mbingu na ardhi na kufikia levo ambazo hazijawah kufikiwa, hivyo hata baada ya baba yako Wilsoni kuzaliwa babu yako alifuatwa na watu wa Kondeni wakitaka kumchukua kwenda kumfunza mbinu za mapigano pamoja na nshati za mbingu na ardhi , lakini baada ya kumchunguza Wilsoni ilikuwa nje ya mategemeo kwani hakuonekana kuwa na akili nyingi.

Mzee Dosam licha ya kutokujihussha na umoja huo alihofia usalama wa familia nzima kwasababu watu ambao walikuwa na nguvu ndani ya umoja ambao alikuwa akiwategemea walianza kufariki , hata kama angesema familia yake ijilinde kwa kurudisha hio pete bado tu usalama usingekuwepo kwasababu historia ilikuwa ikimbeba’”

“Unamaanisha kwasababu alizaliwa kulingana na kile kilichotabiriwa?”Aliuliza Hamza.

“Hakika , ndio maana alichukua jukumu la kumrudisha Regina kwenye familia na mpango wake ilikuwa ni kumuingiza Regina kwenye mafunzo ya mapigano na sio kumrithisha kampuni , lakini familia ya Huge ndani ya umoja huo ilikuwa tishio na ilikuwa ikimfuatilia babu yako kwa kila hatua, hivyo kitu pekee walichofanya ili kuhakikisha amani inaendelea waliamua kuingia katika makubaliano ya kutoingilia maswala yote yanayoendelea ndani ya Umoja na pia kuishi kimya kimya”Aliongea

“Mimi nnachoona hapo Mzee Dosam na Bibi Mirium walikuwa wakijidanganya tu , kwa ninachojua huu umoja unajali sana kitu kinachoitwa urithi wa damu kuliko kitu chochote na ni muda tu haujawadia ila muda wowote watamtaka Regina kama mwanafamilia pekee aliebakia ambae ana damu ya urithi au kumuua kabisa asije kuhatarisha nafasi yao ya kimamlaka”Aliongea Hamza.

“Kwa ufupi ni kwamba licha ya kwamba upo sahihi , lakini wanachokiwinda sio urithi wa damu pekee?”

“Unamaanisha nini Shangazi?”Aliuliza Hamza kwa mshangao.









SEHEMU YA 94.

Hata Regina alishangaa mara baada ya Shangazi yake kuongea kauli hio na alitaka kujua.

Upande wa shangazi alionekana kusita kuongea na aliishia kuvuta pumzi nyingi na kuzishusha.

“Ni kuhusiana na upande wa pili wa Regina”Aliongea Shangazi na kauli hio ilimfanya Edna kushituka.

“Shangazi!!”Aliongea Regina huku akionyesha shara asiendelee kuongea kwani ni kama alishajua Shangazi anataka kuongea nini.

“Unamaanisha juu ya Regina kuwa na split personality?”Aliongea Hamza na kauli yake ilimfanya Regina kushituka na hata shangazi alishangaa.

“Ulikuwa ukijua?”Aliuliza Shangazi.

“Ndio nilikuwa nikijua”Aliongea Hamza lakini upande wa Regina aliishia kumwangalia kwa muonekano ambao haukuwa ukielezeka amekasirika Hamza kufahamu siri yake ya kuugua akili au alikuwa na hisia za kutaka kujua amefahamu vipi.

“Regina wewe ni mke wangu tayari , huna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu hili , nilikuwa nikikusubiria uniambie mwenyewe lakini kwasababu hili ni sawala linalohusu usalama wako sina haja ya kuficha kama najua”Aliongea Hamza na Shangazi alimuunga mkono Hamza.

“Alichoongea Hamza ni sahihi , unapaswa kumwambia kila kitu ili kujua namna ya kukulinda”Aliongea Shangazi lakini Regina bado hakuwa ameridhika bado , lakini kwa muda huo alilifanya swala hilo kiporo.

“Shangazi kwahio kuna uhusiano gani wa Regina kuwa na utu wa aina mbili?”Aliuliza Hamza.

“Sina uhakika wa maelezo yote , kitu pekee ambacho Madam aliniambia ni kwamba Regina sio mgonjwa wa akili na hali yake ya kubadilika ni kutokana na kuamka kwa nafsi nyingine ndani yake”

“Kuamka kwa nafsi nyingine ndani yake, unamaanisha kitu kama reincarnation au?”Aliuliza Hamza kwa mshangao.

Reincarnation ni hali ya mtu kuzaliwa upya katika mwili wa mtu mwingine.

“Shangazi huna haja ya kuupamba ugonjwa wangu , ipo hivi nikipatwa na shida ya akili nabadilika na kuwa mtu mwingine kabisa na najiita kwa jina tofauti na Regina”

“Jina gani?”

“Princess Natasha!”

“Unajiita Princess Natasha?”Aliuliza Hamza kwa mshangao huku akijiambia ni kipi kinaendelea.

“Shida yake haijawahi kujitokeza mara nyingi , lakini katika kipindi hicho anajita hivyo”Aliongea Shangazi.

“Sasa kwanini hawa watu wa Kondeni kupitia kitengo chao cha Binamu kuutaka upande wake wa pili?”

“Hilo ndio swali ambalo mpaka sasa halina majibu na pengine huko mbeleni tunaweza kujua zaidi”Aliongea Shangazi huku moyoni akijiambia sio muda wa kuongea kila kitu ambacho hana uhakika nacho.

Upande wa Hamza kuna kitu pia alihisi lakini hakuwa na uhakika nacho, ila alijiambia kadri siku zitakavyosogea ataweza kujua kila kitu.

“Shangazi tukiachana na upande wangu usio na majibu , je hii pete na maana gani kwao mpaka kuonyesha ni kitu cha thamani sana na vipi kuhusu wewe ni moja ya watu kutoka Kondeni?”Aliuliza Regina.

“Mimi sio mwanachama wa Binamu , ukizungumziia Binamu kama alivyosema Hamza ni shirika la kiitelijensia la watu wa Kondeni kupitia umoja wao wao wa SkyEye(jcho la Anga), sio kila mshirika wa Binamu ni mzaliwa wa Kondeni, mimi ni mzaliwa wa Kondeni na familia yangu ilikuwa ya daraja la chini hivyo niliangukia katika nafasi ya ukijakazi, licha ya kujua pete hio ni ya thamani kwa watu wa Kondeni lakini sina taarifa kazi yake kubwa nini ni ipi, lakini kitu nilichoweza kusikia ni kwamba pete hio ilimilikiwa na mwanzlishi wa eneo lote la Kondeni na ndio huyo huyo aliemvisha mama yake Dosam kidoleni”

Kwa namna ambavyo Regina alielewa Shangazi yake ni mtu wa Kondeni na watu wa Kondeni wana umoja wao wa siri unaitwa Jicho la Anga(Skyeye’s) na kitengo cha kiitelijensia kiitwacho Binamu.

“Kwahio Regina tulijitahidi kutokukuambia haya yote kwa muda wote kwasababu ya kukuweka salama , lakini kwAsababu sasa hivi familia ya Suwi imejitokeza inamaanisha Kiongozi mkuu anashindwa kudhibit kile kinachoendelea ndani ya Umoja, hivyo Hamza unatakiwa kuilinda hio pete kwa namna yoyote ile”Aliongea Shangazi.

Upande wa Hamza hakujua acheke ama alie maana tokea mwanzo anapokea hio pete lilikuwa wazo la Bibi Mirium kuilinda hio pete.

“Shangazi kwahio huko Kondeni ni nchi gani au ni wapi?”Aliuliza Regina

“Kondeni ni sehemu ambayo ipo ndani ya dunia lakini haionekani kwa macho ya kawaida , kuna namna ya kuingia na kutoka Kondeni , asilimia tisini ya watu wa Kondeni wanaishi kwa kuvuna nishati za mbingu na ardhi”Aliongea.

“Nakumbuka nishawahi kusikia uvumi kipindi juu ya sehemu ya siri kama hio ndani ya dunia , inasemekana mwanzilishi wa eneo hilo aliweza kufanikisha kugundua uwepo wa hilo eneo kwa kutumia kitabu kisichokuwa na maandishi”Aliongea Hamza.

“Kitabu kisichokuwa na maandishi , ni katabu cha aina gani?”Aliuliza Regina.

“Master wangu ndio alienisimulia juu ya uwepo wa hiki kitabu , ni kitabu ambacho kina kurasa hazina maandishi na inasemekana kilitupwa duniani pamoja na malaika ,sababu ya mataifa kutambua hili eneo ni kutokana na kwamba kitabu hiko baadhi yao walikiona na mara baada ya mwanzilishi huyo kufanikiwa kukisoma alipotea katika macho ya kawaida , licha ya kitabu hicho kuwa katika mikono ya bindamu mara moja lakini mpaka leo hii tofauti na mwanzilishi hakuna ambae ashawahi kujua maana yake , wanachofahamu tu ni kitabu cha malaika kisichokuwa na maandishi basi, lakini licha ya uwepo wa hii simulizi hakuna ambae aliamini na tafiti ziliishia kusema ni kitu ambacho hakiwezekani na ni hadithi tu”Aliongea Hamza.

Regina aliishia kushangaa, siku zote alikuwa ni mwanamke ambae kila alichofanya kiliendana na ushahidi wa kimantiki na hakuwahi kuamini vitu vya kufikirika hata mara moja.

Lakini Hamza aliongea kwa kujiamini mno na hakuweza kujizuia kuhisi pengne ni kweli

“Shangazi huna cha kuongezea?”

“Mimi ni kijakazi pekee , wakati Madam anakuja kuishi huku baba yake aliniambia nijifunze mbinu za mapigano na kuvuna nishati ili niwe mlinzi wake , lakini baadae Mzee Dosam aliniambia nikulinde wewe, hivyo sijui chochote , Hamza ndio mtu anaeonekana kujua vitu vngi kuliko mimi”Aliongea Shangazi na Hamza alishia kcheka.

“Regina unajua katika dunia hii kuna vitu ukiambiwa utahisi ni ngano tu za kutunga kwasababu hakuna ushahidi wa kisayansi , lakini hebu fikiria hujawahi kumuona Farao , hujawahi kumuona Yesu, wala mtume lakini maandiko na ushahidi unakufanya uamini ni watu waliowahi kuwepo , hivyo baadhi ya mambo ni hivyo hivyo , hakuna aliewahi kuona madragoni, majini wala malaika lakini kwasababu hakuna ushahidi haimaanishi kwamba hawakuwahi kuonekana au ni uongo, mpaka sasa tafiti za kisayans zinaonyesha kwamba ulimwengu ambao binadamu tunaona kwa macho ni asilimia mbili tu ya ulimwengu wote na asilimia tiisini na nane ya ulimwengu wote hatuujui na hauonekani kwetu.

“Kama Binadamu akitegemea tu ushahidi wa kisayansi na akili kwa ajili ya kufikiria uwepo ambao unapita akili zetu za kibinadamu haitokuwa tofauti na kipofu anaejaribu kugundua kitu kipya bila kuona”Aliongea Hamza.

“Kwanini unaongea hivyo , hata hivyo sitaki kufikiria chochote mlichoniambia maana kichwa kinaniuma tu , ni bora nifikirie nitakachofanya baadae na sio hili”Aliongea Regina na kisha alisimama na kupandisha ngazi kwenda floor ya juu na kujifungiia chumbani.

Hata Hamza hakumlaumu , aliona kwa mtu yoyote asingeweza kuelewa kila kitu kinachoendelea , maana vitu vingine havikuhitaji tu uelewa , vilihitaji pia uwezo wa kuhimili ukubwa wa ukweli hata kama unaonekana kuwa uongo.

Shangazi mara baada ya kuona maongezi yameisha alisimama na kisha alipiga magoti kwenye kapeti mbele ya Hamza na jambo lile lilimshitua Hamza.

“Shangazi unafanya nini?”

“Hamza kama sio wewe leo , mimi na Regina tungemalizwa na yule Wisu, kwanzia sasa Regina yupo mikononi mwako naomba usije kumkatia tamaa..”Aliongea Shangazi na Hamza hakujua acheke ama alie lakini haraka sana alimsimamisha Shangazi juu

“Shangazi usiwe na wasiwas , sijutii maamuzi yangu ya kuipokea hii pete na ili mradi nipo hai hawawezi kuichukua na kumgusa Regina”Aliongea Hamza na kauli yake ilimfanya Shangazi machozi kumtoka.

“”Nimefurahi kusikia hivyo , ngoja nikamwandalie Regina supu”Aliongea.

*****

Kutokana na tukio lililitokea siku iliofuata Regina alighaiirisha safari ya kurudi Dar na kutokana na mazngira kuwa tulivu na ya msitu Hamza aliona ni vizuri kwa Regina kupumzisha akili.

Mwanzoni Hamza alitaka kumchukua Regina na kwenda kutembea nae , lakini Regina alimwambia hajisikii vizuri , hivyo Hamza alighairisha na kubakia nyumbani kwa muda akiendelea kuangalia runinga mpaka alivyochoka na kutoka nje.

Mji huo ulikuwa ni wa kitalii na ulikuwa na maeneo mengi ya kutembelea

Wakati Hamza akiendelea kutalii kwenye mitaa mbalimbali akishangaa shangaa mazingira , simu yake ilianza kuita na mara baada ya kuangalia jina la anaepiga alikuwa ni Amiri rafikki yake na palepale alikumbuka swala la Mellisa.

*****

Saa moja kumi za jioni alionekana Kanali na Jasusi Mstaafu Amosi wakingia katika mgahawa wa kuuza chai unaomilikiwa na mrembo Dina.

Kwa Amosi hakuwa mgeni wa eneo hilo , lakini kwa Kanali ilikuwa ndio mara yake ya kwanza kufika hapo na alishangaa mara baada ya kuona kuna watu wengi tu waliokuwa wakijipatia chai na vitafunwa.

“Hujawahi kuingia ndani ya hili eneo nini?”Aliuliza Amosi.

“Nalijua hili eneo sana , lakini sikuwahi kuelewa kile kinachouzwa hapa”Aliongea.

“Hapa kunauzwa chai za kila namna ila za viwango , kwa wale ambao hawanywi pombe lakini pia wapenzi wa chai zenye faida kwa mwili hii ndio sehemu yao ya kujidai, ndio maana unaona kuna waatabu wengi hapa”Aliongea Amosi na Dastani alionekana kuelewa.

Muda huo huo mhudumu aliwasogelea na kuwakaribisha kwa ajili ya kupata huduma.

“Hatupo hapa kwa ajili ya huduma ya chai bali tumekuja kuonana na bosi wa hili eneo”Aliongea Kanali.

“Mna miadi nae?”Aliuliza yule mhudumu wa kike maana kidogo alionekana kushangazwa kauli ya watu hao.

“Hatuna miadi lakini lazima tuonane nae , ni jambo muhimu”Aliongea Amosi.

“Nadhani mnapaswa kukaa kwanza ili niongee na meneja”Aliongea yule mhudumu na Kanali alitingisha kichwa na kisha walionyeshwa sehemu ya kukaa huku yule mhudumu akiwaacha.

Ndani ya dakika chache tu , alionekana Lawrence akifika eneo walipo na alijitambulisha kama Meneja wa mgahawa huo.

“Amosi, jasusi mstaafu , unafanya nini hapa mpaka kutaka kuonana na bosi wangu”Aliongea Lawrence, alikuwa akimfahamu vyema Amosi kama mtukutu aliekuwa juu ya sheria kwa kufanya alivyokuwa akitaka kwa wadeni wake na serikali haikumchukulia hatua.

“Leo sijaja kwa shari , licha ya tofaut zetu zilizotokea wakati ule , niliweza kutii masharti yenu yote na sikumsumbua tena yule mwanamke”Aliongea Amosi akimlenga Eliza.

“Hata kama umekuja kwa shari hili ni eneo la biashara”Aliongea huku akitoa tabasamu.

“Bosi wangu hapa anatokea serikalini na ana mazungumzo na bosi wako, ni swala muhimu hivyo ni vyema kama ukitoa taarifa juu ya ujio wetu”Aliongea Amosi akiwa siriasi na Lawrence alifikiria kidogo na kisha aitingisha kichwa na kupiga simu.

“Mnaweza kunifuata madam yupo tayari kuongea na nyie”Aliongea na Amosi na Kanali waliangaliana na kisha walimfuata Lawrence mpaka ndani ya ofisi ya Dina.

Mwanamke huyo licha ya kubarikiwa uzuri , lakini vlevile alijua kukaa kimaponzi mno na kama humjui vizuri utadhani anakutega lakini ni hulka yake tu kama mwanamke.

Sio kwamba Kanali hakuwa akimjua Dina , alimfahamu sana lakini hakuwahi kukaa nae meza moja na alijikuta akijisemea ndani kwa ndani Dina alikuwa ni mzuri mno, pengine wanafikiana uzuri na hawala wake Tresha.

Dina hakuwa peke yake ndani ya ofisi hio , alionekana kuwa na mwanaume mwingine alievalia suti ambae aliwapa mgongo.

“Amosi na Dastani karibuni?”Aliongea Dina kwa sauti ya mapozi na muda uleule yule mwanaume aliewapa mgongo aligeuka na kuwaangalia huku akiwa na tabasamu usoni.

Kitendo cha Amosi na Dastani macho yao kutua kwa huyo mwanaume walijikuta wakishikwa na mshituko kama kwamba hawakutarajia kumuona ndani ya eneo hilo.

ITAENDELEA
Mnaotaka kujiunganasi watsapp nitafutnikwanamba 0687151346
 
Singano asante sana hata usipokuja hata mwezi hatukudai barikiwa sanaaaa
 
Back
Top Bottom