Simulizi ya kusisimua: Kaburi la Mwanamuziki

Simulizi ya kusisimua: Kaburi la Mwanamuziki

KABURI LA MWANAMUZIKI (EPISODE 09)
Mtunzi; Robert Heriel
WhatsApp 0693322300

EPISODE 09

ILIPOISHIA

‘ Gibson! Kwema ndugu yangu” Nikamsogelea
“ Kwema, vipi!” Nikasema bila uchangamfu,
“ Naona umepambana mpaka umefika level hii, ngoja tuone” Akasema,
“ Huu ndio mwanzo tuu, hakuna wa kunizuia” Nikasema,
“ Ndio maana ukaimba nyimbo ya Lusifa, hahahah! “ akacheka kwa dharau huku akimuangalia mtu aliyekuwa akimuita, nafikiri alikuwa ni dereva wake.
“ Alice anakuja wiki ijayo, lakini kabla hajaja nataka nikupe maumivu kidogo, nataka nimchukue Neema kwa hii wiki ili ujisikie vile nilivyojisikia kipindi kile ulivyonichukulia Alice wangu” Akasema, akiwa ananitazama kwa macho ya hasira iliyojificha, Nikatabasamu bila ya kumjibu kitu, nikaondoka kwenda kwenye gari walipokuwa wananisubiri Neema na Kaka yake..

ENDELEA
*****************


Nilirekodi wimbo wangu wa kwanza, kisha nikatoa na video yake, ulikuwa wimbo mzuri uliovuma nchi nzima, karibu chaneli zote za Televisheni zilionyesha video ya wimbo wangu, redioni nako ngoma yangu ilipasua anga, mitaani na kwenye Bar kote ilikuwa ndio habari ya mjini, hiyo ilikuwa hatua muhimu ya mafanikio katika maisha yangu ya muziki, nilijua jina langu limeanza kujulikana kitaifa, kila nilipopita watu walikuwa wakiniita kwa jina langu, wengine wakinisumbua nipige nao picha, mwanzoni nilijivunia walivyokuwa wanafanya hivyo lakini kadiri siku zilivyokuwa zinaenda nilianza kuona ni usumbufu,

Maisha mapya ya kuishi kama mtu mashuhuri yalianza, umashuhuri unaraha zake, ikiwemo kibiashara kwani jina langu ningelitumia kutangaza biashara yoyote ikaenda, makampuni makubwa yalikuwa yakipigana vikumbo kuja kuomba kuingia mkataba na mimi ili nitangaze bidhaa zao, mawakala na meneja wa muziki walikuwa wakiomba niwe chini yao ili kuniongoza kwenye taaluma yangu ya muziki, baada ya kutoa ngoma yangu ya kwanza ikapokelewa vizuri, ilinibidi nihame pale kwa Riadi, nilitaka kuishi kwa uhuru zaidi nikiwa najitegemea, nikaongea vizuri na Riadi, alisikitika sana, licha ya kunisihi niendelee kuishi kwake lakini niling’ang’ania kuwa nahitaji kujitegemea, basi ikawa alivyoona nimechachamaa na msimamo wangu akaniruhusu huku akinisihi nisisite kurudi kwake ikiwa mambo yataenda tofauti, akaniambia pale ni kama nyumbani, na mimi ni kama mdogo wake, basi tukaachana,

Nilikuwa nimekodi nyumba nzima, maeneo ya Mwenge, sasa nilianza maisha mapya, kwa mara ya kwanza nilianza kuyala matunda ya kipaji changu, ilikuwa nyumba kubwa ya vyumba vinne, chumba kimoja kikiwa Master, sebule mbili, jiko na stoo, ilikuwa ndani ya uzio kukiwa na vigae pamoja na bustani nzuri, niliona itafaa kwa kuanzia maisha yangu, sasa nilitamani kuishi na Mama yangu, nikamtumia mama nauli akaja mjini, mama alifurahi sana kuniona mafanikio niliyoyapata,

“ Mwanangu hii nyumba yote ni yetu?’ Mama akaniuliza,

“ Ndio mama, hii ni nyumba yako mama” Nikasema,

“ Nashukuru sana mwanangu, Uzidi kubarikiwa na kuwa mtu mkubwa” Mama akasema akiwa anaendelea kuikagua nyumba yetu. Hakuna kitu kizuri kama kumuona mama yako mzazi akiwa na furaha, moyo wangu ulikuwa umechangamka ajabu, lakini mama akaniuliza swali ambalo liliondoa uchangamfu wangu,

“ Mwanangu hii sio nyumba yako, kitu ulichokikodisha hakiwezi kuwa chako mwanangu, nakuomba usibweteke, hela unayolipa si itakuwa nyingi sana?” Mama akasema,

“ Aaah! Mama, unajua kwa sasa mimi ni Star, siwezi kuishi nyumba ya kawaida Mama, lazima nikae nyumba inayoendana na jina langu Mama” Nikasema,

“ Yote ni sawa Kijana wangu, lakini nakuomba ufanye juu chini ujenge nyumba yako mwenyewe kabla mambo hayajawa mengi, unajua kila kitu ni kirahisi kama kitafanywa kwa wakati hasa mwanzoni kabla mambo hayajakutinga” Mama akasema,

“ Usijali Mama yangu, kwanza nataka nikujengee bonge la jumba, mama kwanza kisha mimi nitafuata, nataka pale kijijini watu waliokudharau wakuheshimu, na hili nitalifanya mapema mwaka huu” Nikasema, maneno hayo yalimfanya mama atabasamu huku akiniangalia kwa macho ya upendo. Juma lilelile nilinunua gari zuri la gharama, hiyo ilikuwa ndoto yangu kumiliki usafiri wenye hadhi, nilifanya hivyo kwa sababu, nisingeweza kuendelea kupanda magari ya kukodisha kama vile Uber au Bolt, nilistahili kuwa na usafiri wangu,

Wimbo wa pili nikarekodi nikishirikiana na Neema, ulikuwa wimbo mzuri sana ambao ulizidi kuimarisha majina yetu ndani na nje ya Nchi yetu, katika tasnia ya muziki wapo wa kongwe wengi ambao tuliwakuta kwenye Game, haikuwa kazi rahisi kutukubali kama wanamuziki wenzao, wengi wao walituchukulia kama washindani na hii ilipelekea uhasama wa kila mara baina yetu, fitina na majungu kwenye muziki ni jambo la kawaida, kila kitu kizuri kinahitaji kupiganiwa, kinahitaji mtu ajitoe kisawasawa.

Nikatafuta jina la kisanii ambalo litatumika katika kazi zangu za sanaa ya muziki, kiukweli kutafuta jina sikudhani kama ni jambo gumu kiasi kile, ilinichukua wiki nzima kupata jina nililoliona litanifaa katika kazi zangu, nikajiita Gstar(tamka JISTAA) Herufi ya “G” Ikibeba jina langu Gibson, Star ikimaanisha Nyota ing’aayo. Nilikuwa nikijiona kama Nyota yenye kung’aa, nilitaka nuru yangu iwaangazie watu wa nchi yangu na dunia kwa ujumla. Nilitaka muziki ukomboe watu wangu. Jina linamchango mkubwa katika kazi za sana, pia hata katika maisha ya kawaida jina la mtu huweza kuchangia kwa sehemu kubwa mapito yake, jina zuri linaweza badilisha mtu na kuwa mtu mzuri.

Nikampigia simu Neema tuonane katika Hotel Fulani iliyokatikati ya jiji, nilikuwa nina siku kadhaa sijakutana naye kutokana na shughuli nyingi za muziki pamoja na kukaa na Mama, nilitaka mama akae na mimi mpaka hamu yake iishe, na hilo lisingetokea kwani hamu ya mama kwa mtoto wake kamwe haiwezi kuisha, ingawaje angalau niliweza kuishusha, nikakutana na Neema Hotelini, Neema naye alikuja na Gari yake, alikuwa kapendeza sana, alivalia kigauni kifupi kilichoishilizia katikati ya mapaja, chenye rangi kama ya kijani kilichopauka,

“ Nimefurahi sana kukuona Neema” Nikasema,

“ Hata mimi pia Gstaa, jina lako zuri sana, unajua kujipendelea, mimi mbona hunitungii jamani” Neema akasema, hapo tukacheka.

“ Unahitaji nikutungie jina mpenzi?’

“ Unaniuliza tena jamani, nitungie bhana, hili nililonalo alinitungia Baba yangu, nataka la usanii unitungie wewe, si unajua kwa sasa wewe ndio Baba yangu uliyebakia” Neema akaongea kwa madeko huku akiyazungusha macho yake kwa kurembua, hapo tukapeleka glass za mvinyo kinywani kisha tukaendelea.

“ OoooH! Hivi hukuwahi kuniambia habari za wazazi wako, wako wapi?” Nikamuuliza, hapo nikauona uso wa Neema ukibadilika, huzuni yenye uchungu ilizikumbatia kwa nguvu misuli ya uso wake, macho yake yakashindwa kuhimili machozi yaliyokuwa yakibisha katika miimo ya macho yake, nikamuona akilia, nilijisikia vibaya sana kumuona katika hali ile.

“ I’m sorry Neema, sikuwa lengo la kukuumiza, nisamehe sana!” Nikasema,

“ Hujawahi kuniumiza Gibson, wala hujawahi kuniudhi hata kidogo, nilikuwa nimeshakata tamaa ya kuishi duniani, furaha ilinikimbia miaka mingi iliyopita, sikuwahi kufikiri siku moja nitakuwa na furaha, lakini tangu nimekutana na wewe siku ile ya kwanza pale TGT furaha yangu ikarejea” Hapo akameza fumba la mate kisha nikachukua kitambaa nimfuta machozi,

“ Ahsante Mpenzi” Akasema huku akiniangalia kwa upendo, alinishukuru kwa kumfuta machozi,

“ Kwa vile tumekuja kuinjoi nafikiri tuachane na hiyo stori, utanisimulia siku nyingine, leo tunywe, tule tufaurahi” Nikasema, hapo nikachukua lile chupa kubwa la Wine nyekundu na kumimina kwenye Bilauri ya kioo. Tukanywa na kula, mpaka tukahisi kulewa, nikaomba mhudumu atuandalie chumba kizuri, kisha tukaelekea chumbani, ilikuwa yapata majira ya usiku wa saa mbili hivi; nikiwa chumbani na mtoto Neema, ilikuwa ni mara ya kwanza kukutana faragha, tulikuwa tumelewa lakini haikuwa sana kiasi cha kushindwa kutembea, tukabadilisha nguo na kuvaa taulo nyeupe kama makoti, kisha tukaenda bafuni, kila mmoja alikuwa na hamu na mwenzake, ulikuwa usiku mkubwa sana kwetu wa kihistoria, ndani ya bafu tulikuwepo viumbe viwili tukiwa uchi wa mnyama tukiwa tunachezea maji ya Jakuzi yaliyojaa mapovu mengi yenye marashi ya kuamsha ashki za ngono, tulichezeana kila mmoja akiufaidi mwili wa mwezake, Neema alikuwa mwanamke mzuri sana hasa mwili wake ukiwa umelowa maji, tena ukiwa na mapovu mapovu ndio ulizidi kupandisha mashetani yangu, sasa tulianza kulisakata rumba baada ya kila mmoja kumhitaji mwenzake, tulibinjuana na kuburuzana kwenye lile jakuzi huku Neema akitoa milio ya kike ya kunogewa na utamu uliomkolea, kuna saa alizungusha macho yake mazuri huku aking’ata ng’ata midomo yake kwa uhondo, nilimkunja alipokuwa kajinyoosha, nilimnyoosha pale alipokuwa amepinda, sikutaka mchezo ule uishie palepale, nilimnyanyua kwa nguvu kama mtoto na kumbeba, nikamleta chumbani na kumbwa kwenye sofa lilokuwa pale chumbani, hapo bila ya kumfuta mapovu nikambinua kisha vita vikaendelea, moyo wangu ulikuwa ukienda kasi sana, akili yangu ilikuwa haifanyi kazi sawia, nilipoteza ufahamu wa kufikiri kisawasawa, nikamnyanyua na kumtupia kitandani kisha nikawa namuangalia kama vile Jinni mla watu, yeye akawa anajiviringa viringa kama nyoka aliyejeruhiwa na kumwagiwa mafuta ya taa, ndio nilikuwa nimemjeruhi vilivyo na sasa alikuwa akinyonga nyonga akisikilizia utamu wa mapenzi yangu,

“ Come on Baby, Njoo unitese, nitese Bebe mpaka nife” Neema aliongea kisauti cha kiajabu ajabu kilichofanya Abdalakichwa wazi wangu apige guu pande kisha anyanyue kichwa juu kama Ile mijusi kafiri, kisha nikamrukia na kumsaga mpaka pale nilipoona ananing’ang’ania huku akiachia yowe kubwa ambalo lilipambana na sauti nyepesi ya muziki uliokuwa mule ndani, ukulele wake ulimaanisha kushangilia kufika mwisho wa safari ndefu, jasho lilikuwa likitutoka kama waoka mikate, sikutaka akinaiwe na ushindi wa bao moja, nikaendelea mpa mwisho alipofunga bao tatu mimi nikiwa nipo nyuma kwa bao mbili, lilikuwa ni pigano ambalo mpaka hivi leo ninalikumbuka,

Tulipumzika, Neema akiwa amelala katika kifua changu, hapoo nikamsikia akisema;

“ Wewe kweli ni mwanaume, leo umenikomba kila kitu, khaah! Sio kwa mikiki mikiki ile” Hapo nikamtazama kisha kukatokea ukimya, alafu akasema tena,

“ Furaha ya mwisho niliipata siku moja kabla wazazi wangu hawajauawa, ilikuwa miaka mingi iliyopita nikiwa mtoto, familia yetu tulikuwa mimi, mdogo wangu ambaye tumepishana mwaka mmoja hivi, ilikuwa miaka kumi na tano iliyopita ambapo familia yetu ilipatwa na tukio baya lililobadili maisha yangu, leo hata nisingekuwa hivi” Neema akasema, nikawa namtazama nikimsikiliza kwa utulivu. Akaendelea;

“ Nilikuwa nipo na Baba sebuleni, nikiwa ninamiaka kumi na nne tuu, ilikuwa likizo nikiwa nimetoka shule kwani nilikuwa kidato cha kwanza, Baba alikuwa akinipenda sana, sisemi kwamba mama hakuwa ananipenda, wote walikuwa wananipenda ila niliyekuwa karibu naye ni Baba zaidi, Mama yangu alikuwa anatumia muda mwingi na mdogo wangu wa kiume niliyemzidi mwaka mmoja” Hapo akameza mate kisha akaendelea,

“ Mama alikuwa akipenda kumsomea Mdogo wangu Bedtime Stori, hivyo alikuwa chumbani kwa mdogo wangu akimsomea stori, baada ya mdogo wangu kulala mama akarejea sebuleni akinikuta mimi na Baba tukicheza Game kwenye Tv, Mama aakawa ananisaidia tukimchangia Baba ili tumshinde” Nikaona akiachia tabasamu kwa mbali kama mtu aliyefurahishwa na kumbukumbu hiyo.

“ Wakati bado tunaendelea kucheza Ghafla mlango wetu wa sebuleni ukafunguliwa kwa nguvu kwa kuvunjwa, wakaingia wanaume wawili na wanawake wawili, wote wakiwa wameficha sura zao, wanawake wakiwa wamevaa hijabu, walikuwa wamebeba silaha, wakatuweka chini ya ulinzi” Alipofika hapo kwenye wanawake wawili waliokuwa wamevaa hijjabu nikakumbuka ile stori ya yule msela kule Jela, ni kama zilikuwa zinafanana lakini mbona yeye alisema miaka thelasini iliyopita, alafu Neema anasema miaka kumi na tano iliyopita, nikataka kumuuliza swali lakini akili yangu ikanionya na kuniambia niwe na subira.

“ Yule mwanamke akamfokea sana Mama yangu, nilikuwa najisikia vibaya sana kuona mama yangu akifanyiwa vibaya na wale majambazi, hata hivyo nilikuwa nikijiuliza sababu ya wale majambazi kutuvamia ilikuwa ni nini, kwani Baba alikuwa yupo tayari kutoa pesa zozote ili watuachie lakini hawakutaka, lakini nilimsikia mama akimwambia Baba, kuwa alimkanya Baba asiingie katika mahusiano na yule mwanamke, nikajua kuwa kumbe Baba alikuwa na mwanamke mwingine wa nje ambaye sikuwahi kumuona, yule mwanamke akanifuata mimi na kunikata kata na kisu, nilimuona Baba akijaribu kufurukuta lakini hakuweza, nikapoteza fahamu wala sikufahamu kilichokuwa kimetokea” Akameza mate, hapo nikawa nina maswali mengi sana, kisa cha Neema kilifanana kwa sehemu kubwa na kisa cha yule msela wa Jela, lakini utofauti pia upo, Dada yake yule msela alikuwa akiitwa Consolata ambaye wote walikuwa ni watoto wa Waziri, huyu anaitwa Neema, tukio la yule msela alisema Dada yake alichinjwa na kufa papo hapo, lakini Neema yeye anasema tukio lile alipoteza fahamu “ Itakuwa ni stori mbili tofauti zinazokaribiana na ukweli, kwanza Neema hajasema yeye ni mtoto wa Waziri” Nikawa nawaza, Neema akawa anaendelea,

“ Niliokolewa na Rafiki yake Baba ambaye alikuwa ni Luteni wa Jeshi, sijui ile siku alikuja kufanya nini, lakini anasema alikuwa akirudi kutoka kazini usiku ule, yeye alikuwa anakaa mtaa uliokuwa unafuata lakini barabara atakayoitumia inapita karibu na Geti letu, akiwa anakaribia kulifikia geti letu alishangaa kuona gari jeusi lenye vioo vya tinted likiwa limepaki karibu na geti letu alafu wakatoka watu wanne waliovalia kininja, wanawake wakiwa wawili na wanaume wawili, alisema, kitendo cha kuona watu wale kilimshtua akajua kuna hatari imetokea katika nyumba yetu, akapunguza mwendo wa gari wakati lile gari la wale majambazi likiondoka, akajaribu kusoma Platenumber lakini lile gari halikuwa na platenumber, akafika na kuingia katika geti letu, hapo akashtushwa na moto mkubwa uliokuwa ukiwaka katika nyumba yetu, wale majambazi waliichoma nyumba, pia alishtushwa na kuona Askari wawili wa ulinzi wakiwa wameuawa pale, hakuwa na muda wa kupoteza akaingia ndani ya Nyumba moto ukendelea kushika kasi, alipofika ndani kulikuwa na moshi mwingi huku moto mkubwa ukiunguza Masofa na mapazia, hapo alinikuta mimi nikiwa nimelala, Baba na Mama, alisema, alikuta mama na Baba akiwa amekufa, mimi nikiwa nimezimia lakini mapigo ya moyo yakiwa yanadunda kwa chini sana, akanitoa kwanza nje kisha akatako kurudi kumuangalia Mdogo wangu Paul, lakini hakuweza tena, Mdogo wangu alikufa na moto siku ile masikini” Neema akaanza kulia tena, uvumilivu ukamshinda alikuwa akitingishwa na Kwikwi kwa nguvu! Nikawa nambembeleza huku stori ile ikiwa imeniumiza sana, sasa nilihitimisha kuwa stori ya yule Msela na Neema ni stori mbili tofauti,

“ Walimchoma moto Mdogo wangu akiwa hai kalala chumbani, waliichoma miili ya wazazi wangu, Yule Baba mdogo aliniambia wakati anataka kurudi ili amuokoe Paul akashindwa kwani moto ulikuwa umechachamaa, akaondoka kinyemela akiwa kanibeba na kunipeleka nyumbani kwake ambapo kulikuwa na chumba cha matibabu, huko alikuwa akiita madaktari kwa siri hasa ambao hawanijui vizuri” Baba yangu alikufa huku uchunguzi ukipigwa danadana za kisiasa” Neema alisema machozi yakiwa yameulowanisha uso wake.

Ilikuwa simulizi yenye kusisimua sana, nilimuonea huruma sana Neema, kuna wakati nilitaka kumuuliza kuhusu kifo cha Waziri na mkewe pamoja na binti yake lakini nilipokumbuka kwenye stori ya Msela hakunielezea habari ya nyumba kuchomwa nikaona haina maana yoyote, lakini nikakumbuka kuwa Yule msela hakuwa amemalizia Stori yake, nikajikuta nataka kumuuliza Neema lakini ghafla simu ikaita, alikuwa Mama ananipigia, nikapokea, alikuwa akiniambia nipo wapi kwani usiku umeenda hivyo anawasiwasi, nikamuomba msamaha kwa kushindwa kumpa taarifa kuwa sitarudi siku ile hivyo tutakutana asubuhi.

***************************************



Kazi ya kumpeleleza Osman Midevu iliendelea, sasa nilijua yapo maficho mawili ya kuweza kumpata Bwana huyo, Ficho la kwanza ni kwake ambapo ni Mbezi Beach, Ficho la pili ni kule Tegeta walimpompeleka Kibadeni, tayari nilikuwa nimeripoti tukio la kushambuliwa kwa Kibadeni kwa Dr. Miranda wa Marekani kwa njia ya Email, nilijulishwa niendelee na kazi, suala la Kibadeni linashughulikiwa, nikaondoka mida ya saa moja hivi kuelekea Mbezi beach nikiwa na pikipiki wakati huu, sikutaka kutumia gari kwa kuhofia kukaririwa na wakazi wa eneo lile, nikavaa suruali ya jeansi, fulana nzito, na mabuti meusi, nikaiweka bastola yangu sehemu yake, kisha nikavaa miwani nyeusi usoni, kutoka Goba Mpaka mbezi shule sio mbali sana hivyo haikunichukua dakika chache kufika, giza lilikuwa limeshatawala, ungeshangaa ni kwa vipi niliendesha pikipiki kwa kasi nikiwa nimevaa miwani nyeusi usiku lakini miwani niliyokuwa nimeivaa ilikuwa ya kijasusi, hivyo ilikuwa inatumika hata kwenye giza unaona vizuri tuu. Nikaiegesha pikipiki yangu umbali wa mita thelasini nikiwa nimeipita nyumba ya Osman, nikaitoa sigara na kuipachika mdomoni, nikawa navuta huku nikitafakari jambo Fulani la zamani,

“ Taswira ta mwanamke aliyevalia nguo nyeusi zote ilikuwa ikipita kichwani mwangu, uso wake ukiwa na athari kubwa ya vipodozi, akaamka na kutoka, nami nikaamka nikaondoka pale nilipokuwa nimekaa, nikawa namfata kinyemela bila ya yeye kujua, kisha nikamuona akichukua simu yake na kubonyeza bonyeza, aalafu akairudisha simu kwenye mkoba wake, punde nikasikia kwa nyuma mtu anakuja, nikajibanza, nilishtuka kumuona Gibson akiwa anatembea kumfuata yule Mama’ Gibson anamfahamu vipi huyu Mwanamke? nikajiuliza“ Sikuamini kumuona yule mwanamke, nilifikiri nimeonana na mzimu, mara ya mwisho kumuona ilikuwa zamani kidogo kama miaka kumi hivi iliyopita” Nikawa nawaza, “ Kwa nini alimuita Gibson chobingo?” Nikawaza huku nikiwa navuta sigara yangu,

“ Mara ya mwisho kumuona yule mwanamke ilikuwa ni siku ambayo Baba yangu alinichukua tukaenda katika Hotel Fulani, alisema anaenda kukutana na mtu Fulani hivi, siku ile ilikuwa jioni ya saa kumi na moja hivi, tukafika katika Hoteli ile, tulimkuta Mwanamke mmoja wa makamo, mrefu kiasi, mweusi mwenye weusi mzuri wa kuteleza, anayejipenda, baada ya Baba kusalimiana naye, akaniambia nisogee nikakae pembeni kwenye meza ya mbali kidogo kuwapisha wazungumze, nikawapisha, nikiwa na maswali yule mwanamke ni nani, lakini kwa kazi ya Baba yangu nikaona swali langu ni lakijinga kwani Baba yangu ni kawaida kukutana na watu tofauti tofauti, nikaendelea na hamsini zangu nikishangaa bustani na miundombinu mizuri ya ile hotel, lakini kabla sijafika mbali kuufaidi uzuri wa mandhari yale nilishtushwa na maneno ya Yule Mwanamke akimuambia Baba;

“ Achana na jambo hili halitakufikisha popote, utajiingiza kwenye matatizo bure yasiyo na maana yoyote”

Baba akamjibu” Dora! Nisikilize vizuri kwa umakini. Aliyefanya jambo hili ni lazima atalipia kwa kile alichokifanya”

“ Kwa nini walikuwa wanagombana, ni jambo gani hilo ambalo Yule Mwanamke alikuwa akimzuia Baba kulifuatilia?” Nikawaza, jina la yule mwanamke ndiye Dora, sasa alikuwa anafanya nini na Gibson kule chobingo siku ile ya Tuzo za shindano la Tanzania Got Talent, “ Hapa lazima kutakuwa na jambo limejificha, itabidi nianze kumfuatilia huyu mwanamke” Nikawaza, lakini ghafla nikashtushwa na gari likitoka katika geti la nyumba ya Osman, lilikuwa gari jeusi lenye vioo vyeusi, la gharama na lenye kuvutia sana. Lile gari likaondoka nami nikalifungia Mkia kinyemela bila ya wao kujua, tukafika Bagamoyo Road tukakatisha mkono wa kushoto tukielekea Mjini, tulipofika Makumbusho lile gari likaingia kituo cha mafuta kujaza mafuta, kisha likaendelea na safari, ni mpaka tulipofika Maeneo ya Upanga, likakatisha kama linaingia barabara ya Kinondoni makaburini, kisha likakata kulia tena, hapo nikaliona likisimama kwenye Geti kubwa jeusi ambapo ndani yake kuna jumba kubwa la ghorofa, Geti likafunguka kisha lile gari likazama ndani, bila ya kupoteza muda nikaipaki Pikipiki yangu kisha nikaenda kwenye ule ukuta, nikazitengenisha nyaya za ulinzi zilizokuwa juu ya ule ukuta kwa kutumia kifaa maalumu cha kuzuia umeme usipite, kisha nikazama ndani, hapo nikapokelewa na uwanja wenye vigae maridadi na magari matatu, moja likiwa la ubalozi, la pili likiwa la binafsi na jingine ni lile nililokuwa nalifukuzia, jumba lilikuwa na giza kwa ndani isipokuwa sebuleni, nikaona Mbwa mkubwa mweusi akiranda randa kuzunguka lile jumba, Getini kulikuwa na kijumba cha mlinzi ambapo ndani yake nilimuona mwanaume mmoja aliyevalia sare ya rangi ya dark blue, nikajua alikuwa mlinzi, upande wa pembe ya kushoto wa ile nyumba kulikuwa na bustani yenye miti ya maua na ukoka, na viti kadhaa vya kupumzikia, pia kulikuwa na vyungu vikubwa vyenye maua ndani yake, nikashuka nikiteleza kama nyoka kwenye mwamba, nilipojihakikishia nipo salama nikaitoa bastola yangu mafichoni, nikawa nimeishika, nikakimbilia chungu kilichokuwa mbele yangu, nikajibanza, kisha nikapima mzunguko wa sauti na hewa eneo lile nikaona bado hali ni shwari, nikasonga kwenye chungu kilichokuwa mbele yangu nikijihami na kugundulika na yule Mlinzi na lile Jibwa kubwa aina ya Germany Sherperd. Nilikuwa nimefika kwenye Karibu na Kinoki ya ile nyumba, ambapo kulikuwa na taa ikimulika, hapo nikalisogelea dirisha nikiwa nimeinama lakini ghafla nikasikia sauti ya mbwa akija, nikageuka, alikuwa akija nilipokuwa lakini ghafla tena nikamsikia yule mlinzi akimuita kwa jina lake, akamfuata, “ Afadhali! Atakuwa hakuniona” Nikashusha pumzi nikiwa namtazama yule Mbwa mwenye mkia mnene wenye afya, nikachungulia tena dirishani, lilikuwepo pazia lililokuwa linanizuia nisione vizuri, nikawa nasikia watu wakizungumza bila ya kuwaona,

“ Imekuwa kheri mmekuja ndugu zanguni, nimepigiwa simu na mshirika wetu ambaye yupo katika ile hopsitali ya Waingereza, Kama ulivyoniambia jana Mkuu kuwa Mna mtu wenu mulimteka miezi kadhaa iliyopita, lakini mkashangaa haripotiwi kwenye vyombo vya habari tangu mlipojaribu kumuua, mkawa na hofu kuwa kama hajatangazwa basi atakuwa ameokolewa” Sauti ya kiume nyepesi ilikuwa ikizungumza, nilishtushwa na maneno hayo, tayari niliona Maisha ya Kibadeni yapo hatarini, nilijua wanamzungumzia yeye tuu wala asingekuwepo mtu mwingine.

“ Ni lazima atakuwa hai, tena ameokolewa na Yule mwehu anayeitwa Peter Mirambo, Siku ile Peter Mirambo alivyotutoroka tunahakika alienda kumuokoa Kibadeni kwa msaada wa maelekezo ya yule mlinzi wetu mwenyewe, kwa hiyo unasemaje Balozi” Sauti hiyo ilifanana kwa kiasi kikubwa na sauti ya Osman, nikajua ndiye mwenyewe, nikawa najiuliza huyo anayeitwa Balozi ni balozi jina au Balozi cheo,

“ Tayari nimefanya kama mlivyosema, nimeagiza kijana wangu niliyewapa aende akatekeleze mauaji, muda mfupi ujao” Maneno hayo yalinifanya niamke na kuondoka mbiombio bila kujali kuna mbwa au mlinzi, yule mbwa aliponiona nikikimbia akanikimbilia lakini tayari nilikuwa nimemzidi hesabu, nikauparamia ukuta na kupanda juu huku nikikoswa koswa na meno ya yule mbwa, nikatokea upande wa pili, bila kupoteza muda nikachukua pikipiki yangu na kutokomea nikimuwahi Kibadeni asije kuuawa, nusu saa nilikuwa nimesimama mbele ya Geti la Ile hospitali nikaingia ndani ya jengo kisha nikawa naifuata Lifti, wakati naikaribia Lifti nikapishana na mwanaume mmoja aliyekuwa kavaa kapero kuficha uso wake, akili yangu ikajua alikuwa ndiye muuaji aliyetoka kufanya mauaji, akawa anakuja kwa mbele yangu huku akijitahidi kuficha uso wake nisiuone, tukapishana hapo nikageuka nyuma kumtazama, naye akatembea kwa hatua kama saba hivi akageuka nyuma hapo tukatazamana alafu kwa haraka akageuka na kuanza kukaza mwendo, nikaona nimfuate, nikamfuata naye akawa anasonga zaidi, nikawa namuita, “ Oya! Wewe! Simama!” Akawa anaongeza kasi zaidi na zaidi akaifikia gari nyeusi iliyokuwa imeegeshwa akapanda nikiwa namuwahi akawasha gari akaondoka, hapo nami nikaiwahi pikipiki yangu na kupanda upesiupesi, kisha nikaitoa getini na kuanza kulifukuzia lile gari, nililkimbiza lile gari likawa linakata mitaa, yule mwanaume alikuwa anajua kuendesha gari sio utani, tutatokea Kariakoo kisha akanirejesha tena Posta, hapo akakatisha kulia kwa haraka kisha nilipokatisha nami nikakuta lile gari halipo ila kuna barabara mbili moja imekata kulia nyingine kushoto, nikafanya uamuzi wa haraka, nikakata kulia tena, hapo nikatembea na ile barabara nikiwa na pikipiki yangu, nikakata kushoto nikaikuta ile gari imepaki, nikashuka upesi nikatoa bastola yangu, nikawa naikaribia lakini kwa mbali kama hatua hamsini hivi nikaona mtu aliyevaa kofi akiwa anatembea, kisha akakatisha kushoto, nikamkimbiza kwa kasi nikiwa nimeiweka bastola yangu kuielekezea juu ikiwa mbele yangu, nikaikuta ile kona, nikamuona yule mwanaume aliyevalia kofia akiwa yule na mwanamke hivi, nilipowakaribia nikasema; “ Tulieni hivyo hivyo” Wakageuka nilishangaa kuona hakuwa yule mwanaume niliyekuwa namkimbiza niliyemuona kule hospitalini, nilibaki nimetekewa nikiwa nimechukizwa na kitendo kile cha kuzidiwa akili,

“ Mnatoka wapi usiku huu?” Nikasema, nikiwa nazuga, nikawaona wakitazamana wakiwa na hofu, ni kama mtu na mpenzi wake waliokuwa hawaelewi jambo lolote.

“ Kaka tusamehe, hatutatembea usiku tena” Yule mdada akasema akiwa anatetemeka kwa hofu, nikaona napoteza muda wangu bure, nikawaamrisha wakimbie, walitoka nduki sijawahi kuona, kidogo nicheke kwa jinsi mwanamke alivyokuwa anakimbia kwa kasi kuliko mwanaume, kwa jinsi alivyo mrembo wala usingetegemea kama anaweza kukimbia namna ile,

Nikarudi Hospitalini, baada ya kumaliza Lifti nikakuta Kibadeni akiwa ananitazama, kisha akatazama chini kama ananionyesha jambo Fulani, nikanona Dripu lililokuwa limepasuka kwa kukanyagwa, Nilifurahi kumkuta akiwa mzima, lakini kwa mazingira yale niliyoyakuta nilitamani kujua kilichokuwa kimetokea lakini Kibadeni hakuwa na uwezo wa kuongea, bado alikuwa anaumwa sana. Nikawasiliana na Dr, Miranda akaniambia ni mhamishe Wodi, alafu kuhusu walinzi haina shida atatuma usiku uleule.

“ Lakini Mkuu humu hospitali yupo Informer wao anayewapa taarifa” Nikasema,

“ Fanya nilichokuambia, mhamishe kwanza kisha mtafute huyo mtu, hakikisha umpate usiku huuhuu kabla hapajakucha” Dr, Miranda akasema, kisha simu ikakatika, tulikuwa tunawasiliana Kupitia Telegram, punde akaingia Daktari akiwa anapumua kwa woga,

“ Vipi Mkuu, imekuwaje?” Akaniuliza

“ Kama unavyoona kuna mwanaume alikuwa anajaribu kumuua Kibadeni”

“ Dr. Miranda kanipigia simu ndio kanipa taarifa, kasema nisubiri vijana wa ulinzi wakija atanipa maelekezo” Yule Dokta akasema, “ Kumbe timu ya Dokta Miranda ni kubwa kiasi hiki” Nikawaza.

“ Mimi ndio nimetoka kuongea naye sasa, hivi kasema niondoke sasa hivi”

“ Uondoke! Uende wapi?’ Dokta alikuwa akiongea kwa wasiwasi mpaka nikawa nahisi kuna jambo linamsumbua,

“ Ni lazima msaliti atafutwe, lakini sasa hivi naenda kukutana na huyo mwanaume aliyetaka kumuua Kibadeni” Nikasema,

“ Ni kweli haiwezekani watu wabaya wajue Kibadeni yupo hapa, wakati hii ni siri ya watu wachache sana, sasa utampata wapi huyo mwanaume muuaji?”? Akaniuliza,

“ Subiri utaona” Nikasema, kisha nikatoka nikimuacha anasemasema akitaka niendelee kubaki, mlangoni nikapishana na muuguzi wa kike, wala sikuongea naye jambo lolote nikaondoka,

“ Nani aliyeipasua lile Dripu” Nikawaza, nilikuwa narudi kwenye kule nilipowaacha wale vijana wawili wakike na wakiume, nilijua tuu lazima kuna mchezo walikuwa wameucheza kunizuga, nikafika mitaa ileile nilipowaona wameingia katika nyumba moja hivi baada ya kuwaamrisha wakimbie, nilikumbuka maneno ya yule dada kuwa wanaishi mtaa ule akaninyoshea kidole nyumba waliyokuwa wanaishi, nikafika palepale nikaigesha pikipiki yangu, nikabisha hodi, baada ya kugonga kwa mrefu bila kufunguliwa, nikatoa funguo maalum nikaufungua mlango na kuzama ndani, nikapokelewa na korido yenye kagiza hafifu kisha nikapokelewa na njia mbili, njia ya kwanza ilikuwa yakupanda ngazi, yapili ilikuwa inanielekeza kwenye Lifti, nikajiona mjinga nilipokumbuka nilivyokuwa napiga hodi, nilikuwa nimechanganyikiwa, unapigaje hodi kwenye nyumba ya ghorofa yenye wapangaji wengi, nikakumbuka yule mwanamke alikuwa amebeba funguo yenye kibao kilichoandikwa namba 15, nikabonyeza lifti mpaka kwenye floor ya kumi na tano, hapo nikapokelewa na mlango uliokuwa umefungwa wenye maandishi meusi yaliyosomeka Namba kumi na tano, nikatoa ile funguo nikaufungua mlango nikakutana na kelele za muziki, walikuwa wakicheza muziki, waliponiona wakapagawa, baada ya kuwaminya sana wakamtaja Dakatari ndiye aliyetoa siri ya kuwepo kwa Kibadeni hospitalini pale, walimtaja kwa jina moja Dokta Deus, nikampigia Miranda kuthibitisha jina la yule Daktari akaniambia jina lake ni Deus Zebaki, nikamuambia kuwa ndiye msaliti.

Hapo kumbukumbu zangu zilikatika nikiwa nimelewa tilalila, nilikuwa nakunywa pombe nikiwa Mbwii, zilikuwa kumbukumbu za mlevi zenye kujichanganya changanya, hata hivyo zilikuwa na ukweli kwa kiasi kikubwa, muda ule niliyekuwa nikimuwaza ni Dora, niliyemuona akiwa na Gibson siku ile ya Shindano la Tanzania Got Talent(TGT), nilikuwa nimelewa huku nikimtazama Dora aliyekuwa na Yupo na Binti mmoja aitwaye Semeni ambaye nilikuja kugundua alikuwa ni mtoto wake. Ingawaje nilikuwa nimelewa sana lakini bado akili yangu ilikuwa ikifanya kazi vizuri. Mwili pekee ndio ulikuwa hauna nguvu ya kusimama, hapo ilikuwa katika hoteli kubwa ya kitalii iliyokuwa Stonetown, Zanzibar.

*************************

ITAENDELEA, KESHO MCHANA,

Kitabu cha "Mlio wa risasi harusini" Kipo tayari
Softcopy 5,000/=
Hardcopy 15,000/=
 
KABURI LA MWANAMUZIKI (EPISODE 10)
Mtunzi, Robert Heriel
WhatsApp 0693322300

EPISODE 10
ILIPOISHIA

Hapo kumbukumbu zangu zilikatika nikiwa nimelewa tilalila, nilikuwa nakunywa pombe nikiwa Mbwii, zilikuwa kumbukumbu za mlevi zenye kujichanganya changanya, hata hivyo zilikuwa na ukweli kwa kiasi kikubwa, muda ule niliyekuwa nikimuwaza ni Dora, niliyemuona akiwa na Gibson siku ile ya Shindano la Tanzania Got Talent(TGT), nilikuwa nimelewa huku nikimtazama Dora aliyekuwa na Yupo na Binti mmoja aitwaye Semeni ambaye nilikuja kugundua alikuwa ni mtoto wake. Ingawaje nilikuwa nimelewa sana lakini bado akili yangu ilikuwa ikifanya kazi vizuri. Mwili pekee ndio ulikuwa hauna nguvu ya kusimama, hapo ilikuwa katika hoteli kubwa ya kitalii iliyokuwa Stonetown, Zanzibar.

*************************

ENDELEA

Aliyekuwa akisubiriwa kutumbuiza alikuwa ni Semeni, watu wa kutoka mataifa mbalimbali walikuwa wameujaza ukumbi mkubwa wa burudani wa hoteli ile, wengi wao walikuwa watalii kutoka nje ya nchi waliokuja kutalii Tanzania katika kisiwa cha Zanzibar, Watalii wengi hasa kutoka bara ulaya huvutiwa zaidi na vivutio ambavyo kwao havipo, Mathalani Mlima Kilimanjaro ambao ni mrefu zaidi barani Afrika ukiwa katika ukanda wa tabia ya nchi ya Kitropiki yenye hali ya joto, lakini ajabu ni kuwa licha ya kuwa katika ukanda wa joto lakini umefunikwa na barafu, uwepo wa Ngorongoro Crater, hifadhi ya Serengeti yenye wanyama wengi wa aina mbalimbali kuliko hifadhi nyingine yoyote duniani, watalii wengi hupendelea kujipumzisha katika fukwe nzuri za Zanzibar na kufurahia michezo ya majini pamoja na vyakula ainaaina vya baharini, kutokana na uzoefu wa kazi yangu ya ujasusi nilijua kabisa sio kila mtalii huja kwaajili ya kutalii bali wapo wanaoutumia utalii kama mwamvuli wa shughuli zao zingine za siri ikiwemo kufanya ujasusi wa kidola, kufanya utafiti, kusafirisha madawa ya kulevya na shughuli zingine,

Macho yangu yalikuwa sambamba na alipokuwa amekaa Dora, ingawaje tulikuwa tumekaa mbali kidogo kama hatua ishirini hivi tukitenganishwa na viti vingi na meza zilizokaliwa na watalii lakini niliweza kumuona sawia, Muziki laini wa mwambao ulikuwa ukiimbwa na kikundi cha kitamaduni mbele kwenye jukwaa, ulikuwa wimbo mzuri uliopangiliwa kwa ala nzuri za muziki, ngoma, marimba na santuri zilipigwa kwa ustadi wa hali ya juu hali iliyowafanya Watalii wa kizungu kila mara kupiga makofi huku wengine wakirekodi tukio lile kwa kutumia Simujanja zao. Kile kikundi kilipomaliza, MC alimkaribisha Semeni juu ya jukwaa, hapo nikamuona Mama yake, ndiye Dora akipiga makofi na watu wachache aliokuwa amekaa nao, nilikuja kujua watu wale walikuwa wapo pamoja na Dora,

Semeni alikuwa kava kiutamaduni, alikuwa kavaa kijsketi cha majani ya mgomba, ndani akiwa kava taiti ya kijani, chini alikuwa kava katambuga zenye urembo wa shanga, pia kiunoni alivaa shanga kama tatu hivi zilizokishika kiuno chake sawia, shanga zile zilikuwa zenye rangi yenye mpangilio wa kupendeza sana, kwenye maziwa alikuwa kavaa kivazi ambacho sikuelewa kama ni ngozi ya mnyama au ni majani, kichwani alivalia shanga zilizodizainiwa kipekee kabisa, alikuwa kapendeza sana, wakati anaimba watu wengi walimshangilia, nilimuona Dora akipagawa na uimbaji wa binti yake, furaha ya mama ni kuona mafanikio ya binti yake hiyo ilidhihirika katika uso wa Dora, Semeni akamaliza watu wakiwa hawajaridhika wakitaka aendelee lakini ratiba ilikuwa hairuhusu, kisha wakapanda watu wa tamaduni wacheza na Chatu wakicheza ngoma, wakati tukio hilo likiendelea nikamuona Dora akitoka akiwa ameiweka simu yake Sikioni, Nami nikatoka nikiwa namfuata nyuma kinyemela, akatoka mpaka nje ya ile Hoteli, akiwa anaongea na simu, akasimama kwenye ukumbi wenye nje wa ile Hotel wenye maegesho mengi ya magari, nikajibanza kwenye Ua mfano wa Mti wa mnazi, hapo nikamsikia akizungumza; “ Mbona sikuoni, gari gani?, nimeliona, si hilo linalowaka na kuzima taa, sawa!” Macho yangu yakaliona gari aina ya Benzi jeusi lenye milango sita, likiwa pembeni kabisa ya maegesho likiwaka na kuzima taa, Dora akalifuata lile gari kisha kabla hajaingia akachukua simu yake akabonyeza bonyeza alafu akaweka sikioni, kisha akaitoa sikioni nafikiri haikupokelewa, akaandika ujumbe Fulani kwenye meseji, akili yangu ikanambia alikuwa akimuaga binti yake, Semeni, alafu akaingia ndani ya ile Benzi nyeusi, wakaondoka, nikatoka mbiombio mpaka nje ya Geti kubwa la kutokea la ile Hoteli, hapo nje kulikuwa na Taksi mbili zilizokuwa zimeegeshwa, Madereva Taksi waliponiona wakanikarimu;

“ Habari Boss, Wapi twaenda?” Yule Dereva akasema kwa lafudhi ya kizenji, akiwa tayari kanifungulia mlango wa taksi niingie, nikaingia huku nikiiangalia ile Benzi nyeusi iliyokuwa inatokomea katika upeo wa macho yangu,

“ Hakikisha unaifuata hiyo Taksi bila kuipoteza, pia hakikisha wasijue unawafukuzia” Nikasema,

“ Kuna tatizo gani kwani Yakhe Boss?” Dereva akasema huku akiondoa Taksi eneo lile, giza likiwa usoni mwa nchi.

“ Unataka kujua tatizo langu au unataka pesa yangu?” Nikamuuliza kwa hasira, nikamuona akinywea, akaniomba radhi, lakini nikaona anaweza akanitilia shaka, nikasema;

“ Wanawake hawatosheki kabisa, leo ndio atanijua mimi ni nani, namhudumia karibu kwa kila kitu lakini haya ndio ameamua kunilipa” pakawa kimya kwa kitambo, nilijua Dereva taksi anafikiria asemeje, kisha akakata ukimya,

“ Unaenda kumfumania Mkeo?” Dereva akasema,

“ Ndio nimekuwa nikimfuatilia tangu tupo Dar, amekuja huku kanidanganya kaenda kwao kumsalimia Mama yake, sasa huku ndio kwao? Hana ndugu yeyote hapa Zanzibar, nimemkuta na mwanaume mmoja hivi kule Hotelini wakiangalia Tamasha la utamaduni, sasa huku sijui wanaenda wapi?” Nikasema, nikijifanya nina hasira kali kumbe nilikuwa namdanganya,

Tulifika eneo linaitwa Bwejuu hapo tukaenda kidogo, kisha nikaliona lile gari likisimama karibu na ufukwe wa bahari, mbele kidogo niliona Boti kubwa ya kisasa ikiwa imeegeshwa, hapo akashuka Dora kisha kwenye ile Boti nikaona wanaume wawili wakiwa juu yake wamesimama, moja ya wale wanaume akashuka, akakanyaga maji ya bahari mpaka alipofika ufukweni, wakasalimiana na Dora, kisha nikamuona Dora akimpungia mkono yule mtu kwenye Ile Benzi Nyeusi ambaye mpaka muda ule sikuwa nimemuona,

“ Kiasi gani Mkuu?” Nikamuuliza Dereva, akanitajia kisha nikamlipa, nikashuka,

“ Pole sana Kaka” Yule Dereva akasema, kisha akaondoka akiniacha, nikamuona Dora akibebwa mgongoni na yule mwanaume aliyekuwa ameshuka kwenye Boti, kisha ile Benzi ikakatisha na kurudi, nikajificha ikanipita, Dora akafikishwa kwenye Boti kisha yule mwanaume wa juu akampokea akamvuta juu ya Boti, sikuwa na muda wa kupoteza, nikakimbia kinyemela kuifuata ile Boti wakati yule mwanaume aliyekuwa amembeba Dora mgongoni akiwa anaishilizia kupanda ndani ya Boti, kisha alipomaliza boti ikaanza kunguruma mimi nikiwa tayari nimeyafikia maji ya bahari nikiiwahi isiniache, nikaikimbilia mpaka karibu niishike ndio ikaanza kuondoka polepole kabla haijaanza kuchanganya, nikairukia na kuikamata sehemu ya ile boti na kujidhatiti nisiiachie, hatimaye nikafanikiwa kupanda juu yake,

*****************

“Ili muziki wako ukue itakupasa uwe na kipaji kikubwa cha kuimba, lakini kipaji pekee hakitoshi kama hutokuwa na nidhamu, kwenye maisha ya namna yoyote nidhamu ni jambo kubwa kabisa ambalo mtu akiwa nalo anaweza kufanikiwa kwa yale ayatendayo, kipaji, nidhamu, bidii na juhudi zenye akili za kutambua jamii yako inahitaji nini, bidii na juhudi ni mapacha wawili watakaomsaidia mwanamuziki kuzifikia ndoto zake, lakini hawezi kuiacha haiba itakayomtambulisha katika mwonekano wa kisanii, mavazi na mitindo kwa mwanamuziki ni muhimu sana kuzingatia, lakini hayo yote yanatoka ndani ya msanii mwenyewe; Yapo yatokayo nje ya msanii ambayo ni vyombo vyombo vya habari kama vile Redio, luninga, magazeti, na media za mitandao ya kijamii kutokana na ukuaji wa sayansi na teknolojia ya dunia, mambo mengine ya nje ni kama Sera na sheria za nchi kuhusu mambo ya sanaa na haki za wasanii katika kulinda kazi zao” Mzee mmoja mkongwe akasema,

Lilikuwa tamasha kubwa la Wasanii lililoitishwa na serikali, Rais wa nchi alitaka kuzungumza nasi ikiwa umebaki mwaka mmoja wa uchaguzi, nami nilikuwa mmoja wa wasanii wa muziki niliyehuzuria katika tamasha hili, kutokana na nyimbo zangu chache nilizokuwa nimezitoa na kunifanya niwe maarufu, nilipewa nafasi muhimu katika meza za wageni wakubwa nikiwa kama msanii chipukizi ninayekuja kwa kasi katika muziiki, ingawaje zilikuwepo meza mbili ambayo moja ilikuwa jukwaani ambapo viongozi wa serikali na viongozi wa wasanii walikuwa wamekaa, mimi nilikuwa kwenye meza kuu za kwanza chini ya jukwaa, hayo kwangu yalikuwa mafanikio mengine muhimu ya kukumbukwa, nilijua vyombo vya habari karibu vyote nchini vilikuwa vikirusha tukio lile, hiyo ingeendelea kunitangaza na kujenga nafasi yangu katika muziki wa nchi yangu. Yule Mzee mkongwe katika Muziki akaendelea;

“ Muziki umeajiri watu wengi sana, yapo maelfu na maelfu ya vijana katika nchi yetu wanaendesha maisha yao na familia zao Kupitia muziki, wengine ni wasanii waimbaji, wengine ni wachukua video na picha ambazo tunaziona katika luninga na simu zetu kila siku, wengine ni wazalishaji katika studio, wengine ni wasimamizi na mameneja wa wanamuziki, wengine ni Wabunifu wa mavazi kwa wasanii, miongoni mwa fursa zingine za ajira, sijazungumzia vyombo vya habari na makampuni makumi mia yanayotumia Muziki katika kutangaza bidhaa zao, hawa wote wanategemea muziki, hii inatuambia kuwa ile dhana mbaya ya kusema muziki ni uhuni inaanza kukosa uhalali na kumezwa na hoja za muhimu kama tulivyoona” Akameza mate yake kisha akaangalia saa yake ya mkononi alafu akasema;

“ Muda hautoshi kueleza kila kitu hapa, ningewaelezea kisa kilichonitokea mimi mwenyewe miaka thelasini iliyopita, nilikosa mchumba kwa sababu ya kuwa mimi ni mwanamuziki, tena mtoto wa kiongozi mkubwa ambaye sasa ni marehemu, lakini kutokana na muda niwaachie wengine ili kukimbizana na muda kama ratiba isemavyo, Ahsanteni sana; MUZIKI!!!”

“ BURUDANI, ELIMU NA AJIRA KWA TAIFA” Wote tukaitikia, yule mzee akakaa, maneno yake yalifanya ukumbi uzue minong’ono kujadili kile alichokuwa akikisema, baada ya hapo nilishtuliwa na sauti ya Msheshereshaji alipotaja Jina langu; akasema;

“ Kabla sijamkaribisha Mhe Rais, nimeambiwa hapa nimpe nafasi GSTAR aseme walau kwa dakika mbili tuu hapa, ili kuwawakilisha wasanii chipukizi kama yeye na vijana walioko mtaani na shuleni wenye ndoto ya kuwa wanamuziki, Ndugu GSTAR karibu jukwaani, unadakika mbili tuu, tunaomba uzingatie muda” Nilihisi ubaridi ukitembea kwenye uti wa mgongo na kutapakaa mwili mzima, sijui ilikuwa ni hofu au ilikuwa ni nini, kuongea mbele ya Rais kwa mara ya kwanza awali nilifikiri ni jambo rahisi lakini kumbe sivyo, woga uliniingia na wala sikujua umetokea wapi, nikapita mbele nikiwa nimevaa suti yangu ya rangi ya kahawia, miwani kwenye uso, nikiwa nimeziweka nywele katika mtindo wa chorebwenzi, kimsingi nilikuwa nimependeza sana, ukumbi mzima ulikuwa ukinitazama nilipokuwa napanda jukwaani, hiyo haikunipa shida ila kadiri nilivyokaribia ile meza kuu jukwaani ambapo ilikuwepo Mimbari ya kutolea hotuba ndivyo mapigo yangu ya moyo yalizidi kwenda mbio, hata hivyo miwani yangu nyeusi ilinisaidia kupunguza hofu yangu kwani ilinizuia macho yangu yasionane moja kwa moja na watu.

Nikaichukua Maiki kisha nikashukuru kwa kuinama na kusalimia, alafu nikaendelea;

“ Muziki sio uhuni, muziki sio kazi ya watu wajinga, muziki ni taaluma kama zilivyotaaluma zingine, muziki ni kama vile utabibu, ualimu, uanasheria na kazi zingine, muziki sio wa kila mtu, kuufanya muziki kuwa wa kila mtu ndio umefanya wasiohusika kujiingiza na kuharibu taswira nzima na heshima ya fani hii, Kama Kauli mbiu yetu isemavyo; MUZIKI! “ BURUDANI, ELIMU NA AJIRA KWA TAIFA, muziki ni burudani ndio maana sehemu zote za starehe muziki ndio nyenzo muhimu sana maeneo hayo, muziki ni tiba ya mioyo iliyopondeka, muziki huleta faraja wote tunafahamu, jeshini muziki huleta hamasa na ari kwa wanajeshi iwe kwenye mafunzo au kwenye vita, muziki ndio njia nyepesi ya kutoa elimu kwa jamii ikaeleweka, hii ni kusema mwanamuziki ni Mwalimu wa jamii” Nikameza mate kisha nikaendelea,

“ Wasanii wenzangu, tunaowajibu wa kuondoa kasumba mbaya iliyopo kwenye jamii kuwa muziki ni uhuni, tunapaswa tufanye matendo mema ya kuigwa ndani ya jamii, mavazi yetu yawe ya heshima, mambo tunayoyaimba yalingane na maadili na utamaduni wa nchi yetu, kujiingiza katika vitendo vya kihalifu kama matumizi ya madawa ya kulevya au kuuza madawa ya kulevya au kugeuzwa punda tuyaepuke, ndugu zangu ningetaka kusema mengi lakini muda niliopewa ni mdogo, hata hivyo nisiwe mchoyo wa fadhila kwa kuwashukuru wote mlioandaa tamasha hili, MUZIKI!” Ukumbi mzima unatikia “ BURUDANI, ELIMU NA AJIRA KWA TAIFA” Kisha nikasema “ Ahsanteni” Nikainamisha kichwa changu kama ishara ya heshima, kisha nikatoka nikashikana mkono na meza kuu ambao wote walisimama, nikamfikia Rais wa nchi nikashikana naye mikono chini ya uangalizi mkali wa walinzi wake, hapo akanikumbatia alafu akanong’ona maneno Fulani sikioni mwangu, kitendo hiko kilichukua sekunde thelasini tuu, baada ya hapo nikashuka chini ya jukwaa na kurudi kukaa sehemu yangu,

Rais aliongea mambo mengi akipongeza wasanii kwa mchango wetu ndani ya nchi, kisha akamaliza mkutano wa lile tamasha ukaisha na kila mmoja akatawanyika mahali pake anapoishi.

Siku ile historia ilikuwa imeandikwa, nilikuwa na ndoto kubwa ya kuwa msanii mkubwa lakini sikudhani ingekuwa kwa haraka kiasi kile, kusimama mbele ya Rais na kukumbatiwa naye kwa haraka vile kwangu ilikuwa kama ngekewa, usijedhani kila mtu alifurahishwa na mafanikio yangu, tena kwa wasanii wenzangu baadhi yao hawakufurahia jambo lile si unajua penye riziki hapakosi Fitina, kuongea na Rais ilikuwa Promo kubwa sana kwangu lakini pia ulikuwa mtego mbaya uliofichwa katika kivuli cha mwili wangu. Hivyo ndivyo ilivyokuwa.

**************

Kuwa na jina kubwa hakukufanyi uwe na pesa nyingi, unaweza kuwa maarufu lakini usiwe na pesa nyingi, kama vile unaweza ukawa na pesa nyingi lakini usiwe maarufu, ndivyo ilivyokuwa kwangu, nilikuwa maarufu sana lakini sikuwa na pesa nyingi kama watu wa kawaida walivyokuwa wananiona na kunichukulia, wengi waliniona ni tajiri kutokana na matumizi yangu kuwa ghali, magari ya kifahari, hoteli nilizokuwa natembelea, mavazi niliyokuwa navaa yote kwa watu waliyatafsiri kama ni utajiri niliokuwa nao, kumbe haikuwa hivyo, katika umbo la ndani vitu hivyo kwa mtu mashuhuri ni vitu vidogo sana kwani makampuni na matajiri wa jijini walikuwa wakinitumia katika shughuli zao, hivyo nami kutumia vitu hivyo kwao hawakuona shida kutokana na kuwa ni vitu vidogo, Nimelisema hili kwa sababu ya Neema, tabia ya Neema ilianza kubadilika na kunipa mashaka makubwa sana, hakuwa yule Neema kabla ya shindano la TGT, aliyekuwa akinipenda na kuniheshimu, niliyekuwa nikimpigia simu anapokea kwa wakati, niliyekuwa namhitaji muda wowote anakuja, mambo yalikuwa yamebadilika.

Hofu yangu ilianza siku aliponunua jumba la kifahari lililokuwa pembezoni mwa bahari, haikuniingia akili hata kidogo, kipato cha Neema nilikuwa nakijua, Neema hakuwa ananizidi kipato kivyovyote, kazi yake ni muziki ambayo mimi ninamzidi kwa promo na matangazo kwenye makampuni mbalimbali hapa nchini, mimi mwenyewe licha ya kumzidi kimuziki na kimapato lakini nisingeweza kununua jumba kama lile, hii ingewezekanaje embu hata nawewe jaribu kufikiri, hapo nilihisi napigwa na kitu kizito muda sio mrefu.

Nikachukua simu yangu nakuipigia namba ya Neema, ilikuwa ikiita pasipo kupokelewa, nikapiga na kupiga lakini jibu lilikuwa lilelile, haipokelewi. Wivu ulianza kuung’otang’ota moyo wangu, nikaamua kwenda kwa Neema,

“ Unaenda wapi saa hizi Gibson?’ Mama akasema, nilimkuta sebuleni anaangalia tamthilia za kikorea.

“ Kuna mtu naenda kuonana naye Mama, haitachukua muda mrefu nitarudi” Nikasema,

“ Gibson mwanangu! Sipendezwi na tabia yako ya kutoka usiku usiku kila mara, fahamu kuwa usiku ni muda wa kupumzika mwanangu, huyo mtu kwa nini msionane kesho mchana, kwani kuna umuhimu kiasi hicho?” Mama akasema, nilimuona akiwa hajapendezwa na uamuzi wangu, lakini sikuwa na namna, nilimng’ang’aniza akakubali kishingo upande. Safari ikaanza ya kwenda nyumbani kwa Neema, kutokana na usiku kuwa mkubwa hapakuwa na foleni barabarani hivyo niliwahi kufika, nilisimamisha gari mbele ya geti kubwa ambalo ndani yake kulikuwa na jumba kubwa la ghorofa mbili lililokuwa linawaka mataa ungedhani ni Kasri la mfalme wa Kiarabu, nikabonyeza kengele akafungua mlinzi, alishtuka kuniona muda ule, yule Mlinzi alikuwa akinifahamu, tofauti na siku nyingine alizokuwa akinichangamkia siku ile alikuwa anawasiwasi mwingi sana usoni,

“ Vipi Boss! Mbona usiku hivi” akasema akiwa anawasiwasi,

“ Naomba unipishe niingie ndani” Nikasema

“ Subiri Mkuu! Huku huruhusiwi kupita”

“ Embu rudia kusema”

“ Boss! Huku hauruhusiwi kupita, hivyo ndivyo nilivyoambiwa” Yule mlinzi akasema,

“ Unamaana gani kusema ulivyoambiwa, nani kakuambia unizuie?” Nikasema,

“ Sikiliza Boss wangu, naomba urudi ulipotoka, tusivurugiana heshima tuliyowekeana, wala sitaki uniharibie kazi, sawa”

“ Hivi wewe unaakili sawasawa, hujui mimi ni nani kwa Neema, tafadhali nipishe nipite vinginevyo heshima yetu utaivunja wewe mwenyewe” Nikasema huku nikimsukuma kwa nguvu akapepesuka kidogo aanguke, nikazama ndani nikitembea kwa haraka, yule mlinzi akawa ananiita huku akinikimbiza kwa nyuma kunifuata, nikafika kwenye mlango wa sebule nikatoa funguo mfukoni, nikaipachika kwenye kitasa, yule mlinzi tayari alikuwa amenifikia akiwa ananivuta shati langu, nilikuwa nimefanikiwa kuufungua ule mlango lakini mlinzi akanizuia nisiingie, ikawa kukurukakara, vuta nikusukume! Mpaka nilipompiga ngumi ya uso ndipo aliponiachia, sikuwa kuwa vile, mapenzi yalikuwa yananiendesha, nikazama ndani, sebule ilikuwa imezimwa taa ingawaje mwanga wa nje ya lile jumba ulifanya mule ndani kuwe na nuru, yule mlinzi akanifuata tena tukaanza kupigana huku tukipiga makelele, Ghafla taa ikawashwa na wote tukashtuka tukiwa tumeacha kupigana, sikuweza kuamini nilipomuona Richard akiwa kava Taulo kiunoni akiwa kifua wazi, Nilibaki namtazama nikiwa kama nimepigwa na butwaa kwa kitambo huku naye akiniangalia kwa mshtuko ingawaje usio na mashaka, akashuka kwenye ngazi polepole huku akinitazama nami nikimtazama kwa chuki,

“ Boss samahani, nilijaribu kumzuia lakini alileta fujo” Yule mlinzi akasema, akiwa anajitetea, hapo nikajikuta naropoka,

“ Leo ninakuua wewe Mbweha!”

“ Hahaha! Nilikuambia nataka kukuonjesha maumivu kidogo, ujisikie vile nilivyokuwa najisikia kipindi kile ulivyomchukua Alice, nilisema nitakulipizia tuu”

“ Wewe ni mshenzi! Leo ndio mwisho wako” Nikasema nikiwa nataka kupanda kumfuata kwenye zile ngazi, lakini Mlinzi akanizuia, nikampiga kisukusuku cha usoni akaniachia, nikasonga upesiupesi kumfuata Richard nilipozikfikia zile ngazi nikiwa napanda ngazi ya kwanza, kabla sijafika ngazi ya nne ghafla kwa juu nyuma ya Richard akatokea Neema akiwa kavaa Night Dress!

“ Gibson! Unafanya nini hapa muda huu?” Neema akasema, hapo nikajikuta nimesimama kama samamu la Michelin, sijui kama nilimsikia vizuri lakini ni kama alikuwa akiniambia wewe ni nani kuniingilia katika faragha yake usiku ule.

“ Neema! Wewe ndio uniambie huyu mbwa koko anafanya nini hapa” nikasema,

“ Fungu domo lako Gibson, embu kuwa na heshima upo nyumbani kwangu, sawa, Mbwa koko ni Alice na sio huyu kipenzi change” Neema akasema, alafu akamsogelea Richard akamkumbatia kwa nyuma, kisha akapita mbele yake, alafu wakabusiana, hakika nilihisi radi ikipiga macho yangu almanusura niwe kipofu, nilihisi nipo kwenye ndoto ya kutisha, nikamgeukia yule mlinzi aliyekuwa ameshanikaribia nyuma yangu, nikamtazama kwa masikitiko makuu, nikauona uso wake ukivuja damu kwani nilikuwa nimeupasua mwamba wa pua yake na kile kisukusuku nilichompiga, nikasema;

“ Tafadhali ndugu yangu, niambie kuwa hii ni ndoto na wala sio kweli” Yule mlinzi akawa amebaki ananitazama kisha kwa nyuma ikatoka sauti ya Neema,

“ Wala sio ndoto, mfuate mpenzi wako Alice, ondoka kwangu kabla sijakuitia polisi hapa wakuchukue mzobemzobe”

“ Kaka, ondoka kistaarabu tuu, usitake kuzua makubwa zaidi” Yule mlinzi akasema, akiwa ananishika mkono wangu, wakati huu sikuleta ubishani, nguvu ningetolea wapi, nilikuwa nimeishiwa nguvu za mwili na akili, nilibaki nimemtazama Neema huku machozi yakitiririka kwenye mashavu yangu, mlinzi akinivuta kunitoa nje, nikauona uso wa Richard ukitabasamu kwa dharau,

“Neema Mpenzi wangu, huyo shetani anakudanganya Neema, usimsikilize” Nikasema, nikiwa nalia nikijizuia pale mlangoni kwa mikono nisitoke, lakini badala yake nikamuona Neema akiufuata mdomo wa Richard na kumnyonya denda, machozi ya uchungu yalibubujika zaidi na zaidi na kufunika macho yangu nikawa naona ukungu ukungu nikiwaona wakinyonyana ndimi kama mazigazi yanayoyumbayumba, sikuwa nawaona vizuri, mwishowe nikatolewa pale na kuondolewa na kutupwa nje ya Geti, nilibaki nje ya Geti nikilia huku nikiwa naligonga gonga lile geti huku nikimuita Neema, nililia mpaka machozi yakakauka, kilio cha mapenzi katika msitu wa kutisha uliojaa wasaliti, hapo nikawa naimba;

“ Yako wapi mapenzi, yale yako ya zamani,

Umeniachia simanzi, ahadi umezitupa gizani,

Bila wee siwezi, kwa mwingine haiwezekani,

Huu sasa uonezi, umeniangika msalabani,

Ona haya machozi, machungu mengi moyoni,

Ziko wapi ahadi, ulizonipa tukiwa enzini

Meruhusu Jinamizi, kukuvaa mwilini,

Lapapasa kama jizi, kuvizia vilivyosirini,

Umelipa yako enzi, ukanitupa gizani,

Lakudanganya kijambazi, hilo weka akilini,

Yako wapi mapenzi, Ahadi yako kitabuni”

Nikaimba hata sikujua ni saa ngapi nilipitiwa na usingizi ningali nimeegemea lile geti la jumba la Neema,

Mlio wa simu uliokuwa ukiita ndio uliniamsha kutoka usingizi, nilishangaa kujikuta katika kitanda nikiwa nimefunikwa na mashuka, nikavuta kumbukumbu, nikakumbuka mara ya mwisho nilikuwa kwenye geti la Neema kwa nje nikiimba,

“ Nimefikaje hapa” Nikawaza, simu bado ikiendelea kuita, sikutaka kuipokea nikawa nakikagua kile chumba kwa macho, kilikuwa chumba kikubwa kilichotosha kitanda cha ukubwa wa sita kwa sita, kulikuwepo na sofa na kimeza cha kioo, chini likiwepo zulia zuri la manyoya, pembeni kabisa lilikuwepo kabati la nguo lenye milango miwili, mlango mmoja ukiwa na kioo, mlango mwingine ukiwa umefunguka nusu, ndani yake niliweza kuona nguo za kike, juu ya kabati ilikuwepo midoli mikubwa miwili yenye kuvutia, mpaka hapo niliamini chumba kile kilikuwa cha mwanamke, macho yangu yalihama upande huo wakati yakizunguka yaliona mapazia mawili maridadi ya kisasa, yaliyofunika madirisha ambayo sikuweza kuyaona, mwisho macho yangu yalikuwa juu ya mlango ambapo kulikuwa na saa kubwa ya ukutani, na kabla sijaona ni saa ngapi mlango ukafunguliwa, nilishtuka kumuona Alice akiwa kabeba sinia lenye vikorombwezo vya kifungua kinywa, alivyoniona nimeamka akatabasamu.

ITAENDELEA KESHO MCHANA!

Kitabu cha Mlio wa Risasi Harusini kinapatikana kwa Tsh 15,000/=
Softcopy Tsh 5,000/=

Namba ya miamala
0693322300
Airtelmoney
Robert Heriel
 
Wakuu poleni kwa Arosto, na samahanini sana, mambo yaliingiliana.

Kuna kazi za vitabu zingine zimekamlika, zingine zipo hatua ya mwisho,

Nitatangaza siku ya Kuzindua Kitabu cha WAKALA WA SIRI Ambacho kimeshakamilika, wale mlioweka oda zenu mtakuwa wakwanza kupata mapema vitabu vyenu.

Riwaya; WAKALA WA SIRI
Bei; Tsh 15,000/=
Mtunzi. Robert Heriel
Mahali, Dar es salaam, Tanzania
Mawasiliano, 0693322300
 
Back
Top Bottom