Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,743
- 25,564
- Thread starter
- #101
SEHEMU YA 46
Mara vile viatu vikageuka nyoka wa vichwa viwili.
Yule nyoka akaanza kunifata kwenye miguu yangu,
nikaogopa sana ukizingatia sikuweza kupiga makelele
kwavile mdomo ni mzito halafu ndani nilikuwa
mwenyewe kwahiyo uoga ukanijaa zaidi.
Yule nyoka akazidi kunifatilia, kwakweli nikashindwa
kustahimili na kujikuta nimeanguka chini, yule nyoka
akawa anatambaa kwenye miguu yangu. Ile hali
iknifanya nipoteze fahamu kwani nilikuwa kama mtu
aliyechanganyikiwa.
Sikujua kilichoendelea hadi kulipokucha.
Nilipozinduka nilijikuta nikiwa nimelala kwenye kochi
sebleni, nikashtuka sana ila pembeni yangu alikuwepo
mama na dada Fatuma hivyo kunifanya nisiogope
zaidi.
Mama akaanza kuongea kwa kunipa pole.
"Pole sana mwanangu"
Nikatikisa kichwa tu kama ishara ya kuipokea ile pole.
"Ila nini kimekupata mwanangu maana tumekukuta
ukiwa umelala chini tena hujitambui kabisa. Nini
Tatizo?"
Dada akadakia,
"Hawezi kueleza huyu itabidi tumpe peni na karatasi
atuambie"
Dada akanipa peni na karatasi ili niandike
kilichonisibu, nikashika peni na karatasi huku nikihofia
kubadilika kwa maneno. Mama akaniambia,
"Andika mwanangu usiogope chochote, tupo hapa
kwaajili yako"
Nikajaribu bahati yangu ya mwisho ya kueleza kuhusu
Carlos huku nikitumai kuwa wataona nilichoandika.
"Jana usiku Carlos alikuja na kujigeuza nyoka
mwenye vichwa viwili na kuanza kunitisha, sikuweza
kustahimili hadi nikazimia"
Nikamkabidhi mama ambaye alianza kukisoma kwa
sauti,
"Jana usiku....."
Kabla hajaendelea, dada Penina akakipora kile
kikaratasi na kutaka kusoma yeye, kwajinsi ambavyo
mama alisoma nilijipa moyo kuwa ni lazima itakuwa
kama nilivyoandika.
Dada Penina akaanza kukisoma sasa,
"Jana usiku sana, nilijiwa na watu wawili yani Salome
na Zuhura wakanitishia kuniroga kama sijafata
wanachosema, mara wakageuka kuwa nyoka
mwenye vichwa viwili na kuanza kunitisha. Hapohapo
nikazimia"
Mama na dada wakasikitika sana huku mama
akisema,
"Nilihisi tu kuwa hawa watu wanahusika, si unaona
Penina!"
"Naona mama yangu, sijui wanatutakia nini sisi"
"Wanataka roho zetu, yani wakishatumaliza ndio iwe
furaha yao. Hamalizwi mtu hapa nitapambana nao
hadi pumzi yangu ya mwisho"
"Au siku ile ambayo Sabrina alisema nyoka nyoka
ndio wao?"
"Ndio ni wao tu hakuna mwingine"
Nikajaribu kutingisha kichwa kama ishara ya kukataa
lakini hawakunielewa, wakaendelea kuamini
wanachoamini wao.
Niliinuka pale na kwenda kuoga kwani sikuwa na cha
kufanya, nilikuwa kama mtu mgonjwa tena ule
ugonjwa usioonekana.
Nilipomaliza kuoga, nilirudi na kukaa sebleni huku
machozi yakinitoka kwani yote yanayotokea kwangu
ni kama mazingaombwe. Sikuelewa moja wala mbili.
Mchana wa leo, nilitoka nje na kukaa mlangoni huku
nikitafakari mambo yanavyokwenda kiajabu ajabu.
Kwa mbali kidogo nikamuona wifi Joy akija huku
ameongozana na vijana wawili na mdada mwingine
mmoja, nikainuka na kuwapokea ila waliponisalimia
nilishindwa kuwajibu kwavile sikuweza kuongea,
nikaongozana nao hadi nyumbani.
Tulipofika mlangoni wifi akaanza kunieleza.
"Kama tulivyoongea kipindi kilichopita Sabrina,
nilikwambia twende kanisani ukakataa na kusema
kuwa nikuletee wachungaji hapa nyumbani. Basi leo
nimetimiza, hawa unaowaona ni wanamaombi
wamekuja leo wafanye maombi kwenye nyumba yenu
hapa. Natumai umewafurahia na wanakaribishwa."
Nikaitikia kwa kichwa kuwa wanakaribishwa,
"Ila mbona huongei Sabrina?"
Machozi yalinitoka tu ukizingatia balaa ambalo wifi
Joy atakutana nalo muda mfupi ujao toka kwa mama
na dada.
Wifi akawakaribisha wale wageni ndani, baada ya
kuingia sebleni tu wakakutana na dada Penina
ambapo akasema,
"Tena afadhari umejileta wewe mwenyewe Joy mjaa
laana usojua vibaya wewe"
Wale wageni walikuwa kimya, wifi nae alikuwa kimya.
Mara mama akatoka
chumbani na kusema,
"Umemuacha wapi mwanaharamu?"
Wifi Joy akashtuka na kuuliza,
"Mwanaharamu? Ndio nani?"
"Mwanaharamu mwanao inamaanisha hujui?"
Wifi akawa mpole sasa,
"Jamani ndugu zangu hata salamu tena mbele ya
wageni"
"Salamu kampe huyo aliyekufanya utuletee
mwanaharamu kwenye ukoo"
Wifi Joy akaona kuwa hali si shwari ukizingatia
alikuja na wageni, wifi akaamua kuwatoa nje wale
wageni. Dada Penina akamwambia,
"Unaogopa watajua siri zako eeh! Nilikuwa nakusikia
unavyomwambia Sabrina hapo nje, ooh nimekuletea
wanamaombi sijui nini na nini mbona unawatoa nje?
Waache hapa wajue uchafu wako mbwa wewe"
Kwakweli nilimuonea huruma sana wifi Joy kwani
ataniona mimi mbaya wakati nimetoa siri yake bila
kutarajia wala kutaka.
Nami nikawa namfata wifi Joy kwa nyuma, mama
akanirudisha.
"Umefungwa mdomo kwa kurogwa halafu bado
unataka kumfatilia huyo mchawi Joy na lazima
atakuwa amempa limbwata mwanangu ndiomana
limekuwa kama zezeta, kila utakachomwambia
lazima amtaje Joy"
Mama na dada waliongea sana tena bila hata nukta,
machozi yalinitiririka tu kwani sikuwa na msaada
wowote.
Wifi Joy hakurudi tena, alitokomea hukohuko na
wageni wake nadhani alijua kama akirudi basi
atakutana na varangati.
Dada na mama wakapanga kumpigia kaka simu ili aje
nyumbani wamwambie ukweli na wamuulize maswali,
nikafikiria sana jinsi kaka atakavyokuwa baada ya
kujua ukweli, sikutamani ukweli ule ujulikane ila ndio
hivyo Carlos alishafanya anayoyajua yeye na
kuharibu kila kitu.
Jioni ya leo nikiwa nyumbani nikapokea ujumbe toka
kwa wifi Joy.
"Mbona umenidhalilisha hivyo mdogo wangu?
Kwakweli sikutegemea kabisa kitu cha namna hii toka
kwako Sabrina, nilikuamini sana. Nitakuwa mgeni wa
nani mimi? Nitafanya kitu gani mimi? Sikupenda hii
kitu itokee kwangu, naumia sana. Deo akijua lazima
atanifukuza, nitaenda wapi mimi? Huyu mtoto
nitamleaje jamani, sina kazi, biashara wala chochote
ninachokitegemea zaidi ya Deo hata kama nikirudi
kwetu lazima watanifukuza kwa kosa hili, ukizingatia
ndugu zangu wengi hawanipendi sababu tu niliokoka.
Kwakweli kama ni majaribu basi jaribu hili limekuwa
kubwa sana katika maisha yangu, sina cha kufanya
wala pa kukimbilia. Nangoja hatma yangu ila Mungu
pekee ndiye anayejua"
Ujumbe wa wifi Joy ulikuwa ni mrefu sana na hakika
uliniumiza, nilimuhurumia sana ingawa kaka Deo ni
kaka yangu wa damu ila huruma ilinijaa kwa wifi Joy
ukizingatia alivyonisimulia jinsi ilivyokuwa yeye na
huyo James.
Nilimlaani James na kumuona ni mtu anayetumiwa tu
na viumbe wa ajabu kama Carlos ndiomana akafanya
ujinga aliomfanyia wifi yangu.
Nikatamani kuwaambia mama na dada kuwa
wamuhurumie wifi Joy ila naelewa wazi hata kama
ningeweza kuongea wasingekubali kunielewa kwani
ni ngumu sana kukubaliana na hili.
Mama alishawasiliana na kaka Deo kuwa aje
nyumbani siku inayofatia ili wafanye nae
mazungumzo.
Roho yangu haikuwa sawa kabisa, dada Penina
akaenda jikoni kuandaa chakula cha usiku muda
huohuo nikatumiwa ujumbe na Carlos,
"Nitakuja kula chakula cha usiku leo"
Nikainuka na simu yangu mpaka jikoni na kumpa
dada ili ausome ule ujumbe uliotumwa na Carlos.
Nikaona dada akikodolea macho ule ujumbe kwa
muda mrefu kisha akasema,
"Kumbe ni kweli"
Akanipa ile simu na kumfata mama sebleni na kuanza
kumueleza kumbe dada Penina aliuona ujumbe ule
ambao ulitumwa na wifi Joy, nilipotazama simu yangu
nikauona ule ujumbe upo juu nikaufuta haraka sana ili
kuondoa ushahidi hata kama dada ameona ila ni kwa
bahati mbaya tu.
Mama akahitaji kuusoma na yeye ule ujumbe.
Nikafungua ujumbe aliotuma Carlos na kumpa, cha
kushangaza nae mama akauona uleule ujumbe
niliotumiwa na wifi Joy. Hapo nikajua kwamba lazima
Carlos anafanya mambo yake ili yeye asionekane
kuwa mbaya.
Dada na mama wakazidi kumlaani wifi Joy na
kumuita majina ya ajabu ajabu.
"Kesho ndio mwisho wa kiburi na majivuno na huyu
changudoa Joy kwakuwa Deo anaenda kujua kila
kitu"
Kila walichoongea ilikuwa ni kumponda wifi Joy tu.
Muda wa kula ulipofika nilikuwa na mashaka sana
ukizingatia Carlos ameshasema kuwa anakuja kula
chakula cha jioni, dada na mama walikula sana leo.
Mama akaanza kusema,
"Mmh Penina umepika chakula kitamu sana leo yani
hata hatushibi"
Kwakweli huyu Carlos alikuwa mtu wa ajabu sana
hata sijui aliwezaje kula chakula chetu chote.
Ikabidi mama na dada washushie na maziwa sababu
hawakushiba kile chakula tofauti na walivyowaza wao
kuwa ni kitamu sana ila ukweli ni kwamba Carlos
alikula chote.
Muda wa kulala sikutaka kulala mwenyewe hivyo
nikamfatilia mama ambaye alinisema.
"Muda wa kulala unanifatilia tunalala wote ila usiku
sana
unarudi chumbani kwako, sijui unamatatizo gani
wewe mtoto"
Sikumjibu na kuendelea kuoatilia tu, kisha tukaenda
kulala kama kawaida.
Nilipopitiwa na usingizi mzito sikuelewa
kinachoendelea ila nilishtuka na kujikuta nikiwa
chumbani kwangu, nikakaa pale kitandani, mara
nikasikia kama mlango wangu unafunguliwa ila
nilipoutazama ulikuwa umefungwa vilevile halafu
nikaona kivuli cha mtu karibu na mlango wangu, hapo
ndipo nikaanza kuogopa halafu ule mlango
ukabamizwa kama vile mtu anaufunga nikazidi
kutetemeka maana mlango ulikuwa vilevile ila vitendo
tu ndio vilisikika.
Kile kivuli kikanifata hadi pale kitandani, nikahisi
kuguswa bega ila hakuna mtu niliyemuona kisha sauti
ikasikika.
"Kesho nakuja kukuchukua mke wangu"
Jasho jingi likanitoka, nikainuka pale kitandani ila
nikahisi mkono ukivutwa na mtu asiyeonekana tena
mikono yake ikiwa ya baridi sana, akanishika shavu
na kunibusu.
Nikausikia ule mlio wa busu ila mtu haonekani, nguvu
zikaniisha na uoga kunijaa kabisa.
Machozi yakanitiririka kwavile sikuweza kuongea,
nikahisi nikikarishwa chini huku ile sauti ikiendelea
kunisisitiza kuwa,
"Utake usitake, kesho lazima nikuchukue mke
wangu"
Nikahisi kama kuzibwa macho kwa kitambaa kwani
sikuweza kuona vya mbele tena, halafu baada ya
muda macho yangu yakafumbuliwa nikadhani nitaona
mandhari nzuri kama siku zote, ila leo nilichokiona ni
makaburi, mbele na nyuma yangu kulikuwa na
makaburi yani nilizungukwa na makaburi, nipo
katikati ya makaburi tena giza.
Uoga ulipitiliza, nikawa kama kichaa na kuanza
kukimbia hovyo, nilipolipita kaburi moja wapo
nikashikwa mguu hapohapo nikaanguka chini.
Nilipozinduka kulikuwa kumekucha, nikashangaa
kwani nilikuwa chumbani kwangu.
Wakati nashangaa pale chumbani, gafla akaingia
mama na kuniambia.
"Amka ujiandae Sabrina, amekuja kukuchukua"
Nikashtuka sana na kuanza kulia.