Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

Mlipita njiani laini sana....marangu! Hongera kwa kukuza jiografia yako.......
Mie nilishapanda kwa kupitia njia machame

Sent using Jamii Forums mobile app

Njia ya Machame sina hamu nayo kabisa, vyoo vibovu, mnalala kwenye mahema tu, hakuna kuoga, mnajifuta na tishu tu zile za watoto (Whipes). Mnatumia siku nyingi kuliko wanaopita Marangu.

Uzuri wa kule mambo ya jinsia hayana nafasi, tofauti kati ya mwanamke na mwanaume haipo. Mnaweza kulala hema moja na mwanamke wala usiwe na habari kabisa.
 
Kwa hio Kasie mpaka umri huo ulionao haujawahi kufika kileleni?

Sent from my GT-P5200 using Tapatalk

Wewe umewahi??

Safi sana, nikutakie kila la kheri kwenye safari ijayo. Mie sijapanga bado....
 
Hongera mrembo

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Aahahahahahahahhahaaaa looh.
Mnakuwa kama mpo bustani ya eden.
 
Ahahahaha, machame kiboko bana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi na wanangu tulifanikiwa kupanda milima mitatu ya pale Kibondo,.... Twabagondozi, Nabuhima na Nengo 😀😀. Yote hiyo Nengo Kiboko kwani umechongoka na ni hatari😡, Nawapongeza mabinti zangu kwa kufanikiwa kupanda milima yote😉😉 ingawa hatukupewa vyeti na mtu yeyote😛😛.
 

Sio kweli wanaobabuka ni kujichubua..wengi asubuh wanataka nawa maji ya moto..tatizo kule hewa inamgandamizo so boiking point kubwa ..unaweza ona maji ya baridi kumbe kama kunyonyoa kuku...kuhusu polepole..mi nlivyopanda tulipata case mzungu kufariki....ile haraka mapafu yanashindwa stahimili na ukisema ukae chini ile baridi ikiingia kwe mapafu shida especially kutoka horombo to mandara to gilmans point,.,,anayejua zaidi anaweza jazia
 
Ahahahaha, machame kiboko bana

Sent using Jamii Forums mobile app

Ukitaka ufaidi, fuata taratibu zao tu, hata kama unajisikia bado una nguvu, usiongeze mwendo, nenda taraibu kwa kasi ile ile.
Tulipofika Lava Tower ndio tumbo lilianza kuvuruga na kukumbuka kwamba chakula kikiingia kinatakiwa kitoke kwenye mwili.

Vile vile siku ya mwisho inabidi kujitahidi kupata chakula cha kutosha, hata kama haujisikii kula na mara zote hamu ya kula inakosekana kabisa. Ile ni siku ngumu kuliko zote. Mnaanza safari saa tano usiku, mtafika kileleni kwenye saa mbili asubuhi (kutokana na ukubwa wa kundi lenu). Mkifika huko mnaanza kushuka hadi pale mlipolala, mnakula na kuanza safari ya kuja kulala kituo cha chini. Unaweza kuona siku nzima ni harakati tupu.

Lakini pamoja na shida zote, asikudanganye mtu, kileleni kuzuri sana. Ukifika unasahau shida na taabu zote. Nilichukua JIWE kule juu kama kumbu kumbu, lakini lile JIWE liko tofauti na Jiwe la Dar es Salaam.
 

Tulifika sehem (Tulitumia njia ya Machame) wakasema Mlima umepumua, unatoa gesi flani inaumiza vichwa sana, watu wengi wanakua na hali mbaya kuliko maelezo. Kuna mzungu kidogo amalize mitungi yote ya oxygen. Alishushwa kwa machela hadi chini.

Ila wale wagumu hawana mapafu ya kawaida. Kule sio kwa kuishi au kufanya kazi muda mwingi.
 
Nimesema "Mfano" ili nipate kueleweka na sio sababu ya moja kwa moja inayosababisha hilo tatizo.
 
Nmepanda sana mlima kama porter kuanzia miaka ya 2005...nmepita Machame Route na Rongai ila sikuwahi kupanda na mbongo kama mtalii
Nakumbuka siku moja tukiwa school tulitoroka tukadakwa na askari, kipindi hicho kuna watu walikuwa wanaenda kuvuna asali mlimani, wakawasha moto ule moto ukawazidi wale wavunaji na asali wakakimbia moto ukawa mkubwa sana, vijana wengi walio kuwa mtaani bila kazi walikamatwa na askari tukapandishwa mlimani kwenda kuzima moto aisee, kuna raia walikuwa balaa, tulipitia njia ya rongai, sijui kama hadi sasa hvi bado wanawasha moto
 
Ukifanya kazi za milimani mda mrefu, ukifikisha miaka 55 kwenda juu ndiyo utaanza kuona madhara yake, joint za viungo vya mwili vinaanza kufail kufanya kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…