DO NOT SHOUT
season
Sehemu ya........09
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047
ILIPOISHIA....
"Huyu bosi sio mtu wa kawaida, tofauti kabisa na tunavyomchukulia, lakini kwa nini Yusto kaletwa huku, nini kinaendelea, au..... Hapana haiwezekani, nilishamwambia Caren huenda Yusto akawa sio mtu wa kawaida ona Sasa yeye na Madam Jane uso kwa uso hii imekaaje"
Revocatus alikua akijiuliza na kujijibu mwenyewe.
Mara ghafula alishtuka baada ya pikipiki kupita kwa kasi nyuma yake, wala hakufanikiwa kuiona.
"Ebo nini tena" Revocatus alitahamaki
SASA ENDELEA....
Revocatus alisogea eneo lenye muinuko kiasi hapo aliweza kumuona kwa mbali mtu aliyepita na pikipiki nyuma yake ambaye alikua akielekea kule iliko ngome ya madam Jane.
Mtu huyo hakuwa mwingine bali Brandina. Revocatus aliendelea kumfuatilia kupitia ile Darubini yake.
Brandina alipokaribia kufika karibu na ile ngome, alipaki pikipiki yake mahali Kisha akaanza kunyata kusogea kwenye ukuta mkubwa uliokuwa umejegwa kuzunguuka ngome hiyo.
Brandina alikua akipiga hesabu za kuingia ndani pasipo kuonekana na wale walinzi waliokuwa wametapakaa kila mahali, lengo lake likiwa ni kumtoa Yusto kwenye hatari ile akiwa salama salimini japo kwa haraka haraka ilionekana wazi haikuwa kazi rahisi hata kidogo, mbaya zaidi alikua peke yake.
"Huyu mwanamke kafuata nini huku, ni mwenzake na Yusto au, yes bila shaka nikimbana vizuri huyu atanipa majibu Yusto ni nani hasa" alisema Revocatus kisha taratibu akaanza kushuka mlima akielekea kule iliko ngome ya bosi wake madam Jane lakini yeye akiwa na misheni tofauti
[emoji294][emoji294][emoji294]
Madam Jane alifika mlangoni nje ya chumba alichofungiwa Yusto akasimama na hapo walinzi wakafungua mlango, Kisha mmoja wao akamuonyesha ishara madam Jane kuwa aingie ndani hali ilikua shwari Kama alivyotaka.
Kwa mwendo ule ule wa madaha madam Jane aliingia Kisha mlango ukafungwa.
Yusto aliekua amekalishwa kwenye kiti kisha kufungwa mikono na miguu yake kwa nyuma, alisikia vyishindo vya viatu mchuchumio vilivyolia mfano wa msumari unaokanyaga sakafu.
Aliinua uso wake taratibu huku akionekana kujeruhiwa kwenye maeneo mbalimbali ya mwili wake baada ya kupokea kipigo kizito kutoka kwa watu wa Madam Jane.
Aliinua uso wake taratibu wakatazamana na madam Jane.
Naam kwa mara ya kwanza yusto anamuona mama yake mzazi, hakuwahi kumuona katu tangu azaliwe hakuwa akiijua taswira ya mama yake, anaonekana vipi yukoje, ni mrefu au mfupi, mnene au mwembamba, Leo kwa Mara ya kwanza anamuona Janeth.
Hali ilikua hivyo kwa madam Jane (Janeth) pia anamuona Yusto kwa Mara ya kwanza tangu alipofanya jaribio la kumuuwa yeye na Zubeda ambae ndie amekuwa Kama mama mlezi wa Yusto katika kipindi chote baada ya kunusurika kifo mara kadhaa dhidi ya madam Jane aliekusudia kuwaua yeye pamoja na Yusto. Kipindi hicho Yusto alikua ni mtoto mdogo sana.
Madam Jane alifanya hivyo ili kuficha siri kwa mumewe Mark Moon ambae hakuwa anatambua kama ana mtoto.
Ni miaka mingi mno imepita Sasa mama na mtoto wanaonana tena.
Hakuna aliekua akimjua mwenzake, mama hajui kama huyu ndio mtoto wake wala mtoto hajui Kama huyu ndie mama yake mzazi.
Madam Jane alimkadilia Yusto kwanzia juu hadi chini kisha akatabasamu kwa dharau.
"Unaitwa nani kijana? Unaweza kujua kwa nini uko hapa?" aliuliza Madam Jane huku akivuta kiti na kukaa mbele ya Yusto, wakawa wanatazamana uso kwa uso.
"Unakiburi ee, mbona hujibu, nimekuuliza unaitwa nani?"
"Yusto, naitwa yusto, Yusto Abdulazack Meximo Andiwelo Fendrinado Kasim Azizi Kimaro Moon" alijibu yusto Kisha akatema mate pembeni yaliyochanganyikana na damu.
"Hahahah majina yote hayo ya nini kwani?" madam Jane alicheka na kuuliza swali
"Kila aliewahi kuwa na mchango mzuri kwenye maisha yangu kwangu mimi ni baba yangu ndio sababu nina jina refu, umeelewa Sasa au bado" Yusto alijibu kwa kujiamini,
madam Jane akamkadilia tena kwa mara nyingine akawa haelewi kijana huyo anapata wapi ujasiri wa kuongea vile halafu wala haonekani kuogopa Kama alivyotegemea.
"Anha! sawa basi nimependa jina la Yusto nitakwita Yusto kwa sababu niliwahi kuwa na mtoto mmoja mpuuzi aliitwa Yusto, kwa sasa ni marehemu alikufa hata kabla hajaota meno, kwa mara nyingine tena nakutana na mpuuzi mwenzake Yusto"
Alisema madam Jane Kisha akakata simu yake iliyokua ikiita, Kisha akaizima kabisa.
"Inamaana alikua ni mdogo sana anakuwaje akawa mpuuzi"
"Namwita mpuuzi kwa sababu yeye ndo chanzo cha haya yote, bahati nzuri alikufa, angekua hai angeleta balaa kubwa zaidi"
"Kivipi?"
"Eeh we kijana mbona unajisahau sana unaanzaje kunihoji maswali Kama hayo, hivi unajua hata uko wapi ama unanijua mimi ni nani?"
"Mimi navyojua wewe ni tajiri uliekosa muelekeo unaanzaje kuniteka mtu kama mimi? kwa lipi nakusaidia nini yani?"
"Ooh Safi sasa umekuja kwenye point, upo hapa kwa sababu ya kosa kubwa ulilolifanya, umemchoma mwanangu kisu, ani umethubutu kunyanyau mkono wako ukamdhuru mwanangu ni kosa kubwaa..."
" Haaah!, kwa hiyo wewe ndio mama yake John ha ha ha, alafu sio kisu bana ni mkasi, nimechoma na ka mkasi tena kadogo tu, nilikua na uwezo wa kumuua lakini unajua kwa nini sijafanya hivo, ee unajua?, kosa sio la John kosa ni lako wewe hapo wewe mama John umemuharibu mwanao"
Yusto aliongea kwa kujiamini.
Madam Jane alipigwa na butwaa kiasi akawa anamtazama Yusto ni Kama hamuelewi, akajikuta anavutiwa kuendelea kuongea na mateka wake huyo ambaye alionekana hajali wala nini.
Madam Jane akajikuta anazidi kupiga stori na Yusto.
"Unashangaa nini, ndiyo John kuwa vile ni kosa lako wewe"
"Mmm! kwa nini?" madam Jane aliuliza huku akiweka mikono yake yote miwili kwenye mashavu yake.
"mwanao anaamini kuwa pesa ndio kila kitu kwenye hii dunia pesa inaweza kufanya kila kitu anachotaka, ni kweli ila Ulisahau kumfundisha kuwa kuna baadhi ya vitu pesa haiwezi kununua mfano, pesa hainunui upendo, hainunui furaha, hainunui uvumilivu pesa hainunui heshima badala yake inaleta chuki kiburi dharau na majigambo hizo ndo sifa alizonazo John"
"Unaongea Kama nani Yusto, hiyo ni misemo tu mwanangu tena misemo ya wakosaji Kama wewe, ukija kwenye dunia harisi mambo hayako hivyo nakwambia, ni kitu gani kikubwa utafanya hapa duniani bila pesa, kila mtu anahangaika kuitafuta hiyo pesa ambayo wewe unaiona sio kitu kwako"
"Sikiliza usiniite mwanao, kwanza siwezi kuwa na mama Kama wewe ningejuta maisha yangu yote. Muangalie mwanao John anapesa ana kila kitu lakini hana furaha, kuna vitu kavikosa ambavyo hizo pesa zake zimeshindwa kununua mwisho wake ameingia kwenye maisha ambayo anajikuta anaanza kugombana hadi na watu tusio na pesa Kama mimi, ipo siku John atakuja kukugeuka hadi wewe kwa sababu akili yake inawaza pesa tu haijui hata upendo wa mama ukoje"
[emoji294][emoji294][emoji294]
Baada ya Caren kusuburi kwa muda mrefu hatimae uvumilivu ulimshinda, taratibu akamuacha Zubeda mama mlezi wa Yusto Kisha akaelekea kwenye chumba chake cha kubadilisha mavazi. Akavaa nguo zake za kazi, kiatu cheusi suruali nyeusi, miwani myeusi, kofia nyeusi na koti jeusi.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Brandina aliendea kuhangaika kutafuta namna ya kuingia kwenye ile ngome.
Alikua akipanda ukuta akichungulia ndani hali ni ile ile, walinzi kila kona, anahama na kupanda sehemu nyingine, lengo lake apate sehemu ambayo ataruka upande wa pili bila kuonekana.
"Mikono juu, geuka nyuma taratibu"
Mara Brandina alisikia sauti ya kiume ikiamlisha kutokea nyuma yake, akajua tayari mambo yameshaharibika.
Alinyoosha mikono yake juu na kugeuka nyuma taratibu Kama alivyoelekezwa bila ubishi wowote.
Brandina anakutana na sura ya mwanaume mmoja akiwa amemnyoshea bastola, sura hiyo haikua ngeni machoni kwa Brandina lakini hakumbuki aliwahi kumuona wapi. Alikua ni Revocatus
"Ooh my God mwanamke mrembo Kama wewe unawezaje kufanya Mambo ya hatari namna hii, hujipendi" alisema Revocatus baada ya kukutanisha macho na Brandina.
Revocatus hakuwa amekosea Brandina alikua ni mrembo na mwenye muonekano mzuri ambae anaweza kumvutia kila mwanaume atakaemuona.
"Unatafuta nini hapa?" Revocatus aliuliza kwa ukali kidogo.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Ndani mazungumzo kati ya Yusto na Madam Jane yalizidi kushika kasi.
"Sawa nimekuelewa na hizi porojo zako turudi kwenye mada kuu, kwa nini umemchoma kisu mwanangu?"
"Nimekwambia sio kisu ni mkasi"
"Haijarishi, John anaogopwa karibu na watu wote pale chuoni na hivi punde atakwenda kuwa Rais wa chuo chenu wewe ni nani hadi umfanyie hivo"
"Mimi ni mtu ambae siwezi kumuogopa mtu mwingine eti kwa sababu ya pesa zake, najua jeuri ya John najua hashindwi kuua, lakini alichokifanya amenikosea sana tena sana, nimefanya hivyo Kama kumuonya asirudie tena, unajua kwa nini hata hajataka watu wajue Kama nimechoma na mkasi, anajua amekosea nashangaa sijui imekuwaje kakwambia wewe au ndio anadeka ni last born si eti?"
" kijana unaleta jeuri unasahau kama umegusa mahali pabaya umemgusa mtu ambae hastahili hata kunyoshewa kidole, umekosea sana na lazima nikuwajibishe kwa hili"
Alisema madam Jane huku akisimama na kugeuka nyuma, alitaka kutimiza ile kauli ya ukitaka kumuua nyani usimungalie usoni kwani tayari Yusto alishaanza kumuingia na kumshinda kwa maneno akajikuta anasahau kile kilichomleta.
"Lazima nimuonye asirudie tena, lazima amuogope kwanzia leo" aliwaza Madam Jane.
"Naitwa Madam Jane mimi ndio mama wa John Kama nilivyokwambia nadhani ulisha......." Alisema madam Jane huku akigeuka nyuma taratibu lakini alishindwa kumalizia sentensi yake baada ya kuona kitu ambacho hakutarajia kukiona.
Yusto alikua amesimama nyuma yake huku akiwa amefungua zile kamba zote alizofungwa.
Yusto alikua na kisu kidogo ambacho hukificha kwa kukibana juu ya mkono wa koti lake kama siraha ya ulinzi wa dharula kwake na ndicho kilicho msaidia
Kumbe mda wote aliokua anapiga stori na madam Jane alikua akihangaika kukata zile kamba kwa nyuma bila madam Jane kugundua.
[emoji294][emoji294][emoji294]
"Unatafuta nini hapa" Revocatus aliuliza kwa ukali kidogo huku akiwa bado amemnyoshea Brandina ile bastola yake ambayo mda mfupi uliopita alikuawa ameitumia kufanya mauwaji ya Daktari wa magonjwa ya akili na saikolojia.
Brandina alibaki kimya bila kujibu chochote huku akipiga hesabu za haraka haraka ni vipi atajinasua kwenye balaa lile.
Wakati huo alindela kuvuta kumbukumbu ni wapi aliwahi kumuona mtu huyo ambae sura yake haikuwa ngeni kabisa.
Brandina aliinua uso wake na kutazama juu ukutani karibu na alipo simama Revocatus ilikuwa ni Kama vile ameona kitu cha kushtukiza.
Revo aliliona hilo haraka na yeye akaangalia juu kutazama ni kitu gani kilichomfanya Brandina atazame juu kwa haraka kiasi kile akahisi labda wameonekana na walinzi kwani yeye pia hakutakiwa kuwepo eneo lile licha ya kwamba ni eneo linalomilikiwa na bosi wake madama jane.
Kitendo cha Revo kutazama juu lilikua ni kosa kubwa kufumba na kumbua Brandina alizunguukwa kwa staili ya ajabu na kuupiga teke mkono wa Revo uliokuwa umeshikiria bastola, ingaanguka chini.
Revo alishtuka, hakua ametegemea shambulizi hilo la ghafula,
Haraka akakimbia kuiwahi bastola yake pale chini lakini Brandina hakuwa tayari kumpa hiyo nafasi, aliwahi na kumpiga kifuti maridadi kilichomrudisha Revocatus nyuma hatua kadhaa, kisha Brandina akaipiga teke bastola kwa mguu wake wa kulia ikaenda mbali zaidi.
Akasimama mbele ya Revo Kisha akajipanga tayari kukabiliana nae.
Hapo Revocatus aligundua kua mwanamke huyo hakuwa mtu wa kawaida kama alivyomchukulia, alikua mwepesi na alionekana amepitia mafunzo maalum ya upambanaji.
Naam ndivyo ilivyokuwa, Brandina alikua ni jasusi wa kujitegemea kutoka Nairobi Kenya, yupo Tanzania kwa kazi maalum chini ya bosi Mark Moon.
Revocatus alijipanga vile vile tayari kukabiliana na Brandina, akakunja ngumi na kuanza kumfuata.
Muda mfupi baadae mpambano mkali wa aina yake kati ya Revocatus na Brandina ulianza, hakukuwa na mzembe kati yao, Revo alikua mtaalum wa mambo hayo, alipata mafunzo akiwa na Caren kwa miaka 7 kambini chini ya madam Jane.
Brandina nae hakuwa haba, mpaka kuitwa Jasusi haikua kazi rahisi, aliujua vizuri mchezo.
[emoji294][emoji294][emoji294]
Wakati hayo yakiendelea nje ya ngome ya Madam Jane, ndani nako hali ilikua tete kwa upande wa madam Jane baada ya Yusto kufungua kamba alizokua amefungwa.
Madam Jane alirudi nyuma huku akitetemeka kwa hofu, alitaka kupiga kelele lakini Yusto alimuwahi na kumziba mdomo huku akiwa amembana vizuri ukutani.
"Nakupa nafasi nyingine ya kumfunza mwanao John usipofanya hivyo basi sisi walimwengu tutamfunza"
Yusto alisema kisha akamsukuma madam Jane pembeni, akaanguka chini.
Akakichukua kile kiti walichokua wamemfunga awali akakiinua juu kwa nguvu.
Madam Jane akiwa pale chini alifumba macho na kushika kichwa chake kwa woga huku akipiga kelele akahisi Yusto anampiga nacho kichwani, lakini haikua hivyo.
Yusto alikirusha kile kiti kwa nguvu hadi kwenye dirisha la kioo lililopasuka vipande vipande.
Bila kuchelewa Yusto alikimbia na kuruka pale dirishani akaangukia kwa nje.
Kelele za madam jane na kishindo cha vioo vya dirisha kuvunjwa viliwashtua walinzi waliokuwa nje, haraka wakafungua mlangona kuingia ndani kwa kasi.
Wakamkuta madam Jane amejikunyata ukutani.
"Bosi vipi uko salama"
"Salama kitu gani mfuateni hakikisheni hatoki ndani ya hii ngome nendeni harakaaaaa....."
Madam Jane aliongea kwa sauti na hapo mambo yakabadilika ndani ya ngome ya madam Jane Yusto akaanza kuandamwa.
Nje ya ngome nako mambo yalizidi kuwa moto kati ya Revocatus na Brandina.
ITAENDELEA....
Full story Tsh 1000
0756862047 -saul