Simulizi ya ujasusi: Do not shout (Usipige kelele)

Simulizi ya ujasusi: Do not shout (Usipige kelele)

Wapendwa nipo kwa ajili yenu...
Naendelea kushusha vitu...
USIACHE KUSOMA KIGONGO KINGINE CHA

THE MODERN WAR-vita ya kisasa
 
DO NOT SHOUT
season
Sehemu ya........09
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA....
"Huyu bosi sio mtu wa kawaida, tofauti kabisa na tunavyomchukulia, lakini kwa nini Yusto kaletwa huku, nini kinaendelea, au..... Hapana haiwezekani, nilishamwambia Caren huenda Yusto akawa sio mtu wa kawaida ona Sasa yeye na Madam Jane uso kwa uso hii imekaaje"
Revocatus alikua akijiuliza na kujijibu mwenyewe.
Mara ghafula alishtuka baada ya pikipiki kupita kwa kasi nyuma yake, wala hakufanikiwa kuiona.
"Ebo nini tena" Revocatus alitahamaki

SASA ENDELEA....
Revocatus alisogea eneo lenye muinuko kiasi hapo aliweza kumuona kwa mbali mtu aliyepita na pikipiki nyuma yake ambaye alikua akielekea kule iliko ngome ya madam Jane.
Mtu huyo hakuwa mwingine bali Brandina. Revocatus aliendelea kumfuatilia kupitia ile Darubini yake.

Brandina alipokaribia kufika karibu na ile ngome, alipaki pikipiki yake mahali Kisha akaanza kunyata kusogea kwenye ukuta mkubwa uliokuwa umejegwa kuzunguuka ngome hiyo.
Brandina alikua akipiga hesabu za kuingia ndani pasipo kuonekana na wale walinzi waliokuwa wametapakaa kila mahali, lengo lake likiwa ni kumtoa Yusto kwenye hatari ile akiwa salama salimini japo kwa haraka haraka ilionekana wazi haikuwa kazi rahisi hata kidogo, mbaya zaidi alikua peke yake.

"Huyu mwanamke kafuata nini huku, ni mwenzake na Yusto au, yes bila shaka nikimbana vizuri huyu atanipa majibu Yusto ni nani hasa" alisema Revocatus kisha taratibu akaanza kushuka mlima akielekea kule iliko ngome ya bosi wake madam Jane lakini yeye akiwa na misheni tofauti
[emoji294][emoji294][emoji294]

Madam Jane alifika mlangoni nje ya chumba alichofungiwa Yusto akasimama na hapo walinzi wakafungua mlango, Kisha mmoja wao akamuonyesha ishara madam Jane kuwa aingie ndani hali ilikua shwari Kama alivyotaka.
Kwa mwendo ule ule wa madaha madam Jane aliingia Kisha mlango ukafungwa.
Yusto aliekua amekalishwa kwenye kiti kisha kufungwa mikono na miguu yake kwa nyuma, alisikia vyishindo vya viatu mchuchumio vilivyolia mfano wa msumari unaokanyaga sakafu.
Aliinua uso wake taratibu huku akionekana kujeruhiwa kwenye maeneo mbalimbali ya mwili wake baada ya kupokea kipigo kizito kutoka kwa watu wa Madam Jane.

Aliinua uso wake taratibu wakatazamana na madam Jane.
Naam kwa mara ya kwanza yusto anamuona mama yake mzazi, hakuwahi kumuona katu tangu azaliwe hakuwa akiijua taswira ya mama yake, anaonekana vipi yukoje, ni mrefu au mfupi, mnene au mwembamba, Leo kwa Mara ya kwanza anamuona Janeth.

Hali ilikua hivyo kwa madam Jane (Janeth) pia anamuona Yusto kwa Mara ya kwanza tangu alipofanya jaribio la kumuuwa yeye na Zubeda ambae ndie amekuwa Kama mama mlezi wa Yusto katika kipindi chote baada ya kunusurika kifo mara kadhaa dhidi ya madam Jane aliekusudia kuwaua yeye pamoja na Yusto. Kipindi hicho Yusto alikua ni mtoto mdogo sana.
Madam Jane alifanya hivyo ili kuficha siri kwa mumewe Mark Moon ambae hakuwa anatambua kama ana mtoto.
Ni miaka mingi mno imepita Sasa mama na mtoto wanaonana tena.
Hakuna aliekua akimjua mwenzake, mama hajui kama huyu ndio mtoto wake wala mtoto hajui Kama huyu ndie mama yake mzazi.

Madam Jane alimkadilia Yusto kwanzia juu hadi chini kisha akatabasamu kwa dharau.

"Unaitwa nani kijana? Unaweza kujua kwa nini uko hapa?" aliuliza Madam Jane huku akivuta kiti na kukaa mbele ya Yusto, wakawa wanatazamana uso kwa uso.

"Unakiburi ee, mbona hujibu, nimekuuliza unaitwa nani?"

"Yusto, naitwa yusto, Yusto Abdulazack Meximo Andiwelo Fendrinado Kasim Azizi Kimaro Moon" alijibu yusto Kisha akatema mate pembeni yaliyochanganyikana na damu.

"Hahahah majina yote hayo ya nini kwani?" madam Jane alicheka na kuuliza swali
"Kila aliewahi kuwa na mchango mzuri kwenye maisha yangu kwangu mimi ni baba yangu ndio sababu nina jina refu, umeelewa Sasa au bado" Yusto alijibu kwa kujiamini,
madam Jane akamkadilia tena kwa mara nyingine akawa haelewi kijana huyo anapata wapi ujasiri wa kuongea vile halafu wala haonekani kuogopa Kama alivyotegemea.

"Anha! sawa basi nimependa jina la Yusto nitakwita Yusto kwa sababu niliwahi kuwa na mtoto mmoja mpuuzi aliitwa Yusto, kwa sasa ni marehemu alikufa hata kabla hajaota meno, kwa mara nyingine tena nakutana na mpuuzi mwenzake Yusto"
Alisema madam Jane Kisha akakata simu yake iliyokua ikiita, Kisha akaizima kabisa.

"Inamaana alikua ni mdogo sana anakuwaje akawa mpuuzi"
"Namwita mpuuzi kwa sababu yeye ndo chanzo cha haya yote, bahati nzuri alikufa, angekua hai angeleta balaa kubwa zaidi"

"Kivipi?"
"Eeh we kijana mbona unajisahau sana unaanzaje kunihoji maswali Kama hayo, hivi unajua hata uko wapi ama unanijua mimi ni nani?"

"Mimi navyojua wewe ni tajiri uliekosa muelekeo unaanzaje kuniteka mtu kama mimi? kwa lipi nakusaidia nini yani?"

"Ooh Safi sasa umekuja kwenye point, upo hapa kwa sababu ya kosa kubwa ulilolifanya, umemchoma mwanangu kisu, ani umethubutu kunyanyau mkono wako ukamdhuru mwanangu ni kosa kubwaa..."

" Haaah!, kwa hiyo wewe ndio mama yake John ha ha ha, alafu sio kisu bana ni mkasi, nimechoma na ka mkasi tena kadogo tu, nilikua na uwezo wa kumuua lakini unajua kwa nini sijafanya hivo, ee unajua?, kosa sio la John kosa ni lako wewe hapo wewe mama John umemuharibu mwanao"
Yusto aliongea kwa kujiamini.

Madam Jane alipigwa na butwaa kiasi akawa anamtazama Yusto ni Kama hamuelewi, akajikuta anavutiwa kuendelea kuongea na mateka wake huyo ambaye alionekana hajali wala nini.
Madam Jane akajikuta anazidi kupiga stori na Yusto.

"Unashangaa nini, ndiyo John kuwa vile ni kosa lako wewe"

"Mmm! kwa nini?" madam Jane aliuliza huku akiweka mikono yake yote miwili kwenye mashavu yake.

"mwanao anaamini kuwa pesa ndio kila kitu kwenye hii dunia pesa inaweza kufanya kila kitu anachotaka, ni kweli ila Ulisahau kumfundisha kuwa kuna baadhi ya vitu pesa haiwezi kununua mfano, pesa hainunui upendo, hainunui furaha, hainunui uvumilivu pesa hainunui heshima badala yake inaleta chuki kiburi dharau na majigambo hizo ndo sifa alizonazo John"

"Unaongea Kama nani Yusto, hiyo ni misemo tu mwanangu tena misemo ya wakosaji Kama wewe, ukija kwenye dunia harisi mambo hayako hivyo nakwambia, ni kitu gani kikubwa utafanya hapa duniani bila pesa, kila mtu anahangaika kuitafuta hiyo pesa ambayo wewe unaiona sio kitu kwako"

"Sikiliza usiniite mwanao, kwanza siwezi kuwa na mama Kama wewe ningejuta maisha yangu yote. Muangalie mwanao John anapesa ana kila kitu lakini hana furaha, kuna vitu kavikosa ambavyo hizo pesa zake zimeshindwa kununua mwisho wake ameingia kwenye maisha ambayo anajikuta anaanza kugombana hadi na watu tusio na pesa Kama mimi, ipo siku John atakuja kukugeuka hadi wewe kwa sababu akili yake inawaza pesa tu haijui hata upendo wa mama ukoje"
[emoji294][emoji294][emoji294]

Baada ya Caren kusuburi kwa muda mrefu hatimae uvumilivu ulimshinda, taratibu akamuacha Zubeda mama mlezi wa Yusto Kisha akaelekea kwenye chumba chake cha kubadilisha mavazi. Akavaa nguo zake za kazi, kiatu cheusi suruali nyeusi, miwani myeusi, kofia nyeusi na koti jeusi.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Brandina aliendea kuhangaika kutafuta namna ya kuingia kwenye ile ngome.
Alikua akipanda ukuta akichungulia ndani hali ni ile ile, walinzi kila kona, anahama na kupanda sehemu nyingine, lengo lake apate sehemu ambayo ataruka upande wa pili bila kuonekana.

"Mikono juu, geuka nyuma taratibu"
Mara Brandina alisikia sauti ya kiume ikiamlisha kutokea nyuma yake, akajua tayari mambo yameshaharibika.
Alinyoosha mikono yake juu na kugeuka nyuma taratibu Kama alivyoelekezwa bila ubishi wowote.
Brandina anakutana na sura ya mwanaume mmoja akiwa amemnyoshea bastola, sura hiyo haikua ngeni machoni kwa Brandina lakini hakumbuki aliwahi kumuona wapi. Alikua ni Revocatus

"Ooh my God mwanamke mrembo Kama wewe unawezaje kufanya Mambo ya hatari namna hii, hujipendi" alisema Revocatus baada ya kukutanisha macho na Brandina.

Revocatus hakuwa amekosea Brandina alikua ni mrembo na mwenye muonekano mzuri ambae anaweza kumvutia kila mwanaume atakaemuona.

"Unatafuta nini hapa?" Revocatus aliuliza kwa ukali kidogo.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Ndani mazungumzo kati ya Yusto na Madam Jane yalizidi kushika kasi.

"Sawa nimekuelewa na hizi porojo zako turudi kwenye mada kuu, kwa nini umemchoma kisu mwanangu?"

"Nimekwambia sio kisu ni mkasi"

"Haijarishi, John anaogopwa karibu na watu wote pale chuoni na hivi punde atakwenda kuwa Rais wa chuo chenu wewe ni nani hadi umfanyie hivo"

"Mimi ni mtu ambae siwezi kumuogopa mtu mwingine eti kwa sababu ya pesa zake, najua jeuri ya John najua hashindwi kuua, lakini alichokifanya amenikosea sana tena sana, nimefanya hivyo Kama kumuonya asirudie tena, unajua kwa nini hata hajataka watu wajue Kama nimechoma na mkasi, anajua amekosea nashangaa sijui imekuwaje kakwambia wewe au ndio anadeka ni last born si eti?"

" kijana unaleta jeuri unasahau kama umegusa mahali pabaya umemgusa mtu ambae hastahili hata kunyoshewa kidole, umekosea sana na lazima nikuwajibishe kwa hili"
Alisema madam Jane huku akisimama na kugeuka nyuma, alitaka kutimiza ile kauli ya ukitaka kumuua nyani usimungalie usoni kwani tayari Yusto alishaanza kumuingia na kumshinda kwa maneno akajikuta anasahau kile kilichomleta.

"Lazima nimuonye asirudie tena, lazima amuogope kwanzia leo" aliwaza Madam Jane.

"Naitwa Madam Jane mimi ndio mama wa John Kama nilivyokwambia nadhani ulisha......." Alisema madam Jane huku akigeuka nyuma taratibu lakini alishindwa kumalizia sentensi yake baada ya kuona kitu ambacho hakutarajia kukiona.
Yusto alikua amesimama nyuma yake huku akiwa amefungua zile kamba zote alizofungwa.
Yusto alikua na kisu kidogo ambacho hukificha kwa kukibana juu ya mkono wa koti lake kama siraha ya ulinzi wa dharula kwake na ndicho kilicho msaidia
Kumbe mda wote aliokua anapiga stori na madam Jane alikua akihangaika kukata zile kamba kwa nyuma bila madam Jane kugundua.
[emoji294][emoji294][emoji294]

"Unatafuta nini hapa" Revocatus aliuliza kwa ukali kidogo huku akiwa bado amemnyoshea Brandina ile bastola yake ambayo mda mfupi uliopita alikuawa ameitumia kufanya mauwaji ya Daktari wa magonjwa ya akili na saikolojia.

Brandina alibaki kimya bila kujibu chochote huku akipiga hesabu za haraka haraka ni vipi atajinasua kwenye balaa lile.
Wakati huo alindela kuvuta kumbukumbu ni wapi aliwahi kumuona mtu huyo ambae sura yake haikuwa ngeni kabisa.

Brandina aliinua uso wake na kutazama juu ukutani karibu na alipo simama Revocatus ilikuwa ni Kama vile ameona kitu cha kushtukiza.
Revo aliliona hilo haraka na yeye akaangalia juu kutazama ni kitu gani kilichomfanya Brandina atazame juu kwa haraka kiasi kile akahisi labda wameonekana na walinzi kwani yeye pia hakutakiwa kuwepo eneo lile licha ya kwamba ni eneo linalomilikiwa na bosi wake madama jane.

Kitendo cha Revo kutazama juu lilikua ni kosa kubwa kufumba na kumbua Brandina alizunguukwa kwa staili ya ajabu na kuupiga teke mkono wa Revo uliokuwa umeshikiria bastola, ingaanguka chini.

Revo alishtuka, hakua ametegemea shambulizi hilo la ghafula,
Haraka akakimbia kuiwahi bastola yake pale chini lakini Brandina hakuwa tayari kumpa hiyo nafasi, aliwahi na kumpiga kifuti maridadi kilichomrudisha Revocatus nyuma hatua kadhaa, kisha Brandina akaipiga teke bastola kwa mguu wake wa kulia ikaenda mbali zaidi.

Akasimama mbele ya Revo Kisha akajipanga tayari kukabiliana nae.

Hapo Revocatus aligundua kua mwanamke huyo hakuwa mtu wa kawaida kama alivyomchukulia, alikua mwepesi na alionekana amepitia mafunzo maalum ya upambanaji.
Naam ndivyo ilivyokuwa, Brandina alikua ni jasusi wa kujitegemea kutoka Nairobi Kenya, yupo Tanzania kwa kazi maalum chini ya bosi Mark Moon.
Revocatus alijipanga vile vile tayari kukabiliana na Brandina, akakunja ngumi na kuanza kumfuata.
Muda mfupi baadae mpambano mkali wa aina yake kati ya Revocatus na Brandina ulianza, hakukuwa na mzembe kati yao, Revo alikua mtaalum wa mambo hayo, alipata mafunzo akiwa na Caren kwa miaka 7 kambini chini ya madam Jane.
Brandina nae hakuwa haba, mpaka kuitwa Jasusi haikua kazi rahisi, aliujua vizuri mchezo.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Wakati hayo yakiendelea nje ya ngome ya Madam Jane, ndani nako hali ilikua tete kwa upande wa madam Jane baada ya Yusto kufungua kamba alizokua amefungwa.

Madam Jane alirudi nyuma huku akitetemeka kwa hofu, alitaka kupiga kelele lakini Yusto alimuwahi na kumziba mdomo huku akiwa amembana vizuri ukutani.

"Nakupa nafasi nyingine ya kumfunza mwanao John usipofanya hivyo basi sisi walimwengu tutamfunza"

Yusto alisema kisha akamsukuma madam Jane pembeni, akaanguka chini.
Akakichukua kile kiti walichokua wamemfunga awali akakiinua juu kwa nguvu.

Madam Jane akiwa pale chini alifumba macho na kushika kichwa chake kwa woga huku akipiga kelele akahisi Yusto anampiga nacho kichwani, lakini haikua hivyo.
Yusto alikirusha kile kiti kwa nguvu hadi kwenye dirisha la kioo lililopasuka vipande vipande.
Bila kuchelewa Yusto alikimbia na kuruka pale dirishani akaangukia kwa nje.

Kelele za madam jane na kishindo cha vioo vya dirisha kuvunjwa viliwashtua walinzi waliokuwa nje, haraka wakafungua mlangona kuingia ndani kwa kasi.

Wakamkuta madam Jane amejikunyata ukutani.

"Bosi vipi uko salama"
"Salama kitu gani mfuateni hakikisheni hatoki ndani ya hii ngome nendeni harakaaaaa....."
Madam Jane aliongea kwa sauti na hapo mambo yakabadilika ndani ya ngome ya madam Jane Yusto akaanza kuandamwa.
Nje ya ngome nako mambo yalizidi kuwa moto kati ya Revocatus na Brandina.

ITAENDELEA....

Full story Tsh 1000
0756862047 -saul
 
DO NOT SHOUT
𝐬𝐞𝐚𝐬𝐨𝐧 2

Sehemu ya...........10

Mtunzi: Saul david
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...

"Bosi vipi uko salama"
"Salama kitu gani mfuateni hakikisheni hatoki ndani ya hii ngome nendeni harakaaaaa....."
Madam Jane aliongea kwa sauti na hapo mambo yakabadilika ndani ya ngome ya madam Jane Yusto akaanza kuandamwa.
Nje ya ngome nako mambo yalizidi kuwa moto kati ya Revocatus na Brandina.

SASA ENDELEA....
Wakati mikiki mikiki ile ikiendelea madam Jane alibaki ndani ya kile chumba akiwa amekunja sura yake kwa hasira, kitendo alichokua amekifanya Yusto kilimghadhabisha sana.
Lakini pamoja na yote hayo, kila alipokuwa akiyatafakari maongezi Kati yake yeye na Yusto alijikuta anavutiwa sana na kijana huyo licha ya kwamba alikuwa ni adui yake mkubwa wakati huo.

"Mbona hajaniua? Alikuwa na nafasi ya kufanya hivyo, kwa nini sasa kaniacha " madam jane aliwaza kisha akatoka nje ya kile chumba haraka, aliona kuna kila sababu ya kuzungumza tena na Yusto, kuna vitu vingi alitamani kuvijua kutoka kwake. Ile kauli ya damu ni nzito kuliko maji ilianza kuchukua nafasi yake kwenye moyo wa madam Jane, pasipo kujua Yusto ni mwanae wa kumzaa alijikuta anatamani kuongea naye zaidi.

"We Kindoki, wambie wenzako namuhitaji huyu kijana akiwa hai sawa, hakikisha hawamuuwi, wamlete kwangu akiwa hai"

"Sawa bosi haina tatizo"
[emoji294][emoji294][emoji294]

Yusto alionekana akikimbia huku akijaribu kuwakwepa walinzi wa ngome hiyo ambao walikuwa wametapakaa kila mahali.
Bado alikua ndani ya ngome ya Madam Jane iliyokuwa imezunguukwa na uzio mkubwa wa ukuta mpana pande zote.
Hali ilikua ni ngumu mno kwake, alichohitaji ni kutoka nje ya ngome hiyo akiwa salama lakini hadi dakika kumi zinakwisha bado hakupata mwanya huo.

"Yule pale mkamateni" alisema mmoja wa walinzi baada ya kumuona yusto akiwa amejificha nyuma ya tenki la maji.

Paaa! Paaa!
Paaa! Paaa!
Paaa! Paaa!

Milio ya risasi ilisikika zikimkosa kosa Yusto ambaye safari hii alikimbia na kuingia ndani ya jengo moja zuri lilikokua limejengwa katikati ya ngome hiyo.
Lilikuwa ni jengo lenye urefu kama ghorofa mbili hivi.
Jengo ambalo lilikua ni maalum kwa ajili ya madam Jane ambae hulitumia kupumzika ama kufanya vikao vyake muhimu vya siri.

Yusto aliona kama ndio eneo salama la kukimbilia kwani walinzi walikua wakimfuata kutoka pande zote kulia kushoto nyuma na mbele.

"Acheni, acheni nimesema, msipige risasi, madam kasema anamtaka huyu jamaa akiwa hai" alisema Kindoki

"Aiii, hivi unaelewa unachokiongea wewe huyo jamaa umeshamuona vizuri lakini, yani anakimbia kama kafungiwa mota, anaruka na kukwepa risasi kama ninja vile unafikiri tutamkamata hivi hivi" alisema mmoja wa walinzi.

"Kwa hiyo unàsemaje, unapinga agizo la bosi au?"

"hapana sina maani hiyo Kindoki, maanangu ni kwamba tusipo jiongeza wenyewe huyu jamaa atatuacha ataruka ukuta atoke nje ya hii ngome, cha kufanya ni kumgonga risasi hata ya mguu si ndio jamani"
Alisema yule bwana, walinzi wengine wakatikisa vichwa kukubaliana na maelezo yake.

"Haya sawa basi, risasi ni ya mguu sasa ole mtu afanye tofauti atakuwa na cha kujibu mbele ya mdam jane , kikosi cha Black guard ingieni ghorofa ya juu, Red guard ghorofa ya chini wengine tunaobaki tuingie floor ya chini,
haya kazi kazi masela mtu mmoja hawezi kutushinda au sio" alisema Kindoki kisha vikosi vyote vikaniminika kuingia ndani ya lile jengo aliloingia Yusto.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Amini usiamini mpambano kati ya Revocatus na Brandina hadi sasa ulikua ukiendelea kwa kasi sana huku Revocatus akionekana kuzidiwa na Brandina lakini hakutaka kukubali kirahisi namna ile, akaendelea kujikaza kiume kumkabili mdada huyo ambae alionekana kuwa ni moto ya kuotea mbali.

Milio ya Risasi zilizokuwa zikilindima kutokea ndani ya ngome ya madam Jane ndio iliyowashtua Revocatus na Brandina wakasimama kwa muda huku kila mmoja akisikilizia ni nini kilikua kinaendelea mle ndani.

"Mungu wangu Yusto" Brandina aliwaza haraka haraka akili yake ikamtuma kuwa kwa vyovyote vile Yusto alikua kwenye hatari kubwa mle ndani.
Hakutaka kuendelea kupoteza muda tena, haraka alimrukia Revo akampiga ngumi za haraka haraka zisizo na hesabu, kisha akamsindikiza na teke kali kifuani, Revo akajipigiza kwenye mti kisha akawa anaanguka chini lakini kabla hajafika chini Brandina akamuwahi akamdaka kisha akamshika mkono mmoja na kuanza kumzunguusha. Ikawa kama vile mama anacheza na mtoto wake kwa kumzunguusha.

Baada ya kufanya hivyo Brandina alimuachia Revo akaendelea kwenda na ile spidi ya kuzunguuka kutoka kulia kwenda kushoto kisha Brandina yeye akaruka teke kwa staili ya ajabu akizunguuka kutokea kushoto kwenda kulia akakutana na Revocatus katikati.
Revocatus akiwa na spidi ile ile anakutana na pigo moja takatifu kutoka kwa jasusi Brandina, lilikua ni teke kali ambalo huwa analishuhudia kwenye muvi za wahindi na wachina pekee lakini leo linamtokea yeye akiwa live nje ya ngome ya bosi wake madam Jane.

Revocatus aliona nyota kadhaa hewani kisha giza nene akaanguka chini na kutulia tuli.

Brandina alitua chini kwa ustadi mkubwa kisha akamuangalia Revocatus aliekua pale chini hoi taabani akiwa hana uwezo hata wa kujitikisa.

Brandina alikua amechachamaa hasaa, hakuwa na muda tena wa kupoteza haraka alikimbia hadi pale alipokuwa ameiacha pikipiki yake, akaiwasha na kuiungurumisha, pikipiki ikaitika.

Brandina alivaa helmet yake kisha akawa analitazama geti la kuingia ndani ya ngome ya Madam Jane, geti lilikua limefungwa.
Hakukua na nafasi kabisa ya Brandina kuingia ndani.

Paaaa!!!

Mara Brandina alisikia tena mlio mwingine wa risasi kutokea ndani ya ngome hapo akazidi kupandwa na wazimu.

"Nakuja Yusto wangu nakuja"
Alisema Brandina huku akigeuza pikipiki yake akaiendesha umbali mrefu kutoka pale ilipokuwa ngome ya madam Jane kisha akageuka tena na kuanza kuja kwa kasi, kasi kubwa mno.

Akiwa amefika karibu na geti Brandina aliinuka na kuuinua pikipiki yake kwa namna ya ajabu pikipiki ikapaa juu huku ikienda kwa kasi ile ile ikaruka geti na mwisho ikatua ndani ya ngome ya madam Jane.
Naam huyu ndiye jasusi Brandina, sasa alikua ndani ya ngome ya madam Jane tayari kutoa msaada kwa Yusto, kijana aliekua akimpenda kupita maelezo bila kujali kuwa tayari kijana huyo alikua kwenye huba zito na Caren.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Je, nini kitafuata?
ITAENDELEA...
0756862047
 
Na iendelee jioni tena aisee
 
DO NOT SHO
𝐬𝐞𝐚𝐬𝐨𝐧 2

Sehemu ya........11

𝐈LIPOISHIA...
Naam huyu ndiye jasusi Brandina, sasa alikua ndani ya ngome ya madam Jane tayari kutoa msaada kwa Yusto, kijana aliekua akimpenda kupita maelezo bila kujali kuwa tayari kijana huyo alikua kwenye huba zito na Caren.

SASA ENDELEA.....
[emoji294][emoji294][emoji294]
Yusto alizidi kukimbia akikatiza vyumba kadhaa ndani ya ile ghorofa aliyoingia.
Kwa bahati nzuri hakukuwa na mtu yeyote ndani ilikuwa ni ghorofa maalum ambayo madam Jane hupumzika au kufanya vikao vyake muhimu vya siri tu.

Yusto alipanda hadi ghorofa ya juu kabisa, akaingia ndani ya chumba kimoja ambacho ndio kilikuwa cha mwisho kabisa, ilikuwa ni chumbani kwa madam Jane.
Chumba kilikuwa tulivu, chenye mpangilio mzuri wa kitanda sofa meza kabati na vitu vingine vingi vya kifahari huku kikitoa harufu nzuri ya manukato.
Yusto alifunga mlango kwa ndani akasogea na kusimama dirishani akachungulia chini. Hapo akawaona walinzi wakimiminika kwa wingi kumfuata mle ndani.

"Wameingia wengi, kama nitatoka mapema nikawaacha humu ndani nitakuwa na nafasi ya kutoroka bila kukamatwa"
Aliwaza Yusto na hapo bila kupoteza muda alianza kukata mapazia ya mle ndani pamoja na mashuka yaliyokua yametandikwa akayaunganisha kwa pamoja ikawa kamba moja ndefu sana ambayo ingeweza kumtoa kule juu ghorofani hadi chini.
Akachagua dirisha ambalo liko upande ambao angeshuka bila kuonekana kwa urahisi.

Wakati akisogea kwenda dirishani mara Yusto alihisi ni kama ameona kitu ambacho sio cha kawaida ukutani.
Akageuka na kutazama tena, naam ni kweli, kwenye kona moja ya chumba hicho kulikuwa na picha nyingi sana zilizobandikwa ukutani.
Mwanzo picha hizo zilikuwa zimefunikwa na pazia moja wapo kati ya yale ambayo Yusto aliyakata kutengeneza kamba.

Kilichomshtua Yusto sio kuwepo kwa picha ukutani hapana bali ni picha zenyewe.
Kulikua na picha za watu mbali akiwemo mama yake mlezi ambae kwa sasa ni kichaa yaani Zubeda, kulikua na picha za bosi wake Mark moon, picha za John na picha za watu wengine wengi ambao Yusto hakuwajua.

"Mama? mama inakuwaje akapiga picha ya pamoja na huyu madam, na hii nini mbona ni picha ya harusi, kwamba madam jane aliwahi kufunga ndoa na bosi mark moon mmh mbona sielewi, Madam Jane na mama yangu wapi na wapi, mark moon je...."

Aliwaza Yusto huku zile picha zikizidi kumchanganya, hakuelewa hili wala lile, lakini taratibu akili yake ilianza kufungua.
Akahisi inawezekana kukawa na uhusiano ambao ulikuwepo kati ya mama yake mlezi na madam jane kipindi hicho kwani picha iliwaonyesha wakiwa bado ni mabinti.
Hakuwa anaijua historia ya bosi wake mark moon, lakini zile picha zilieleza moja kwa moja kuwa bosi wake aliwahi kufunga ndoa na madam Jane.
Hakuna kingine alichokijua zaidi ya hapo.
Alitazama picha nyingine zaidi akaona mama yake mlezi akiwa amepiga picha na mtoto mdogo yapata kama miezi 7 hivi, picha za Zubeda akiwa na mtoto huyo zilikua zimepigwa kipindi hicho pasipo yeye mwenyewe kujua ilionyesha wazi aliyekua akimpiga picha hizo alikua akimvizia tu.

Hilo aliligundua Yusto baada ya kutazama picha kadhaa kwa umakini.

"Kwa nini walikua wanamfuatilia mama na kumpiga picha kila alipokwenda, huyu mtoto ni nani"
Yusto alijiuliza maswali yasiyo na majibu hakuwa na picha hata moja ya utotoni hivyo ilikua ni ngumu kutambua kua yule mtoto aliyebebwa na zubeda alikua ni yeye mwenyewe.

Wakati akizidi kuzichunguza zile picha moja baada ya nyingine mara ghafula alisikia kishindo kikubwa mlangoni, tayari walinzi walishagundua kuwa Yusto alikua mle ndani, sasa walikua kwenye harakati za kutaka kuvunja mlango.

Haraka Yusto alibandua picha moja ile ambayo mama yake mlezi(Zubeda) amepiga akiwa pamoja na madam jane, akaiweka kwenye mfuko wa shati lake.

Bila kuendelea kupoteza muda Yusto alikimbia nakuruka dirishani huku akiwa ameshikilia ile kamba ambayo alikuwa tayari ameifunga vizuri, akawa anateremka chini kwa kasi sana.

Haikua kazi ngumu sana kwake kwani tayari alikuwa ni mtu mwenye mazoezi ya kutosha, aliteremka na ile kamba hadi chini.
Wakati huo tayari walinzi lishafanikiwa kuvunja mlango na kuingia ndani.
Wakatawanyika huku na huku ndani ya kile chumba lakini Yusto hakuwepo.

Mwisho mmoja wao akaiona ile kamba iliyokuwa imefungwa dirisha akasogea na kuangalia chini.

"Ooh shiiiiiiiit! yule kule kashuka chini anakimbia, huyu kiumbe sio wa kawaida, haraka tushuke chini"
Alisema yule mlinzi.

Yusto hakutaka kupoteza muda aliamini sasa ana nafasi ya kukimbia kupanda ukuta na kuruka upande wa pili asijue kuwa bado walinzi kadhaa walikua wapo kule chini na tayari walishapata taarifa.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Madam Jane akiwa nje ya kile chumba walichokuwepo awali akifanya mazungumzo na Yusto, Kwa mbali alimuona Yusto anakuja akikimbia, madam Jane akawa anamuangalia huku akijihisi mapigo yake ya moyo yakimuenda mbio, hakuelewa ni kwa nini hali hiyo inamtokea.

Wakati Yusto anaendelea kukimbia huku akiwa karibu kabisa na alipokua amesimama madam jane mara akapigwa risasi moja na walinzi.
Risasi iliyompeleka chini moja kwa moja, akapiga magoti, huku akiinua uso wake taratibu wakakutanisha macho na madam Jane mama yake.

"Yustoo....." Madam Jane alijikuta akiita kwa sauti ya chini huku roho yake ikimuuma sana.

"Kwa nini naumia hivi" alijiuliza Madam Jane.
[emoji294][emoji294][emoji294]

"Yustooo......." Zubeda mama mlezi wa Yusto alikurupuka kutoka usingizi akiwa ndani ya kile chumba chake cha matibabu.
Nae vile vile mapigo ya moyo yalikua yakimuenda mbio.

"Yusto...,mwanangu Yusto, uko wapi" alisema Zubeda hali akiangaza macho huku na huku.
Kuliwa na ukimya wa ajabu wakati huo, si Caren si Revocatus wote hawakuwepo.
[emoji294][emoji294][emoji294][emoji294]

Yusto alitanguliza mkono wake wa kulia chini kuzuia asianguke.
Alikua amepigwa risasi kwenye bega la kushoto, alipata maumivu makali lakini akajikaza kisabuni na kusimama tena huku akiwa ameshikilia eneo la jeraha kwa kujikandamiza ili damu isimtoke kwa wingi, wakati akifanya hivyo ile picha aliyoichukua kutoka ndani ya chumba cha madam Jane ikadondoka chini hakuiona, wakati huo madam Jane alikua anashuhudia kila kitu akiwa hatua kadhaa kutoka pale alipokua Yusto.

Yusto alianza tena kukimbia lakini safari hii hakuwa na kasi kama mwanzo, mbaya zaidi wale walinzi waliokua wameingia ndani ya lile ghorofa sasa walikua wametoka wote, wakawa wanakuja kwa kasi kumfuata.
Hakuna aliyethubutu tena kufyatua Risasi wakifuata agizo la madam Jane japo tayari mmoja wao alikua ameshavunja agizo hilo kwa kumpiga Yusto risasi begani.

Ghafula wote walishtushwa baada ya kuona mtu akiwa amepaa juu ya geti na pikipiki na akutua ndani kwa kishindo.

Hakuna alie amini macho yake, pikipiki ilipaa angani ikitokea nje ya ngome ya madam Jane kisha ikatua upande wa pili. ilionyesha wazi kuwa mtu aliyekua ameingia na pikipiki hiyo hakuwa wa kawaida na alikua mtaalum haswaa
Hakuanguka wala kuonyesha dalili yoyote ya kupata ajali, badala yake alikimbiza pikipiki yake na kwenda kusimama mbele ya Yusto.
Akawa katikati ya Yusto na wale walinzi.
Mtu huyo hakuwa mwingine bali jasusi Brandina.

Brandina alifunua kioo cha helmet yake akamtazama Yusto ambae alikua amejeruhiwa kwa kupigwa risasi begani.

Brandina aliuma mdomo wake kwa hasira na bila kupoteza muda alizunguuka mizunguuko kadhaa akiwa na pikipiki yake, ikatoa moshi mwingi sana kiasi cha kuwafanya wale walinzi wasione upande wa pili kwa urahisi.

"Yusto nipe mkono pandaa haraka"
Alisema Brandina huku akija kwa kasi akiwa amenyoosha mkono wake.

Yusto ambae kwa kiasi alikua amekwisha anza kukata tamaa alijikuta anapata tumaini jipya baada ya kumuona Brandina, haraka alinyoosha mkono wake na kuupokea mkono wa Brandina ambae alimshika kwa nguvu na kumvuta kisha Yusto akaruka na kudandia pikipiki kwa nyuma.

Walinzi waliokuwa bado wameshikwa na bumbuazi wasielewe kinacho endelea walishtuka usingizini baada ya kubaini kuwa mtu huyo alikuwa na lengo la kumtorosha Yusto.

"Haraka shambuliaaaa, asiondoke mtu hapaaa....." Kindoki alitoa amri na hapo zikaanza kumiminwa risasi nyingi lakini hazikua na faida yoyote tayari walikuwa wamechelewa. Baada ya ule moshi kuisha hakuonekana Brandina wala Yusto.

Hali hii iliwafanya walinzi hao kuanza kuogopa, hawakujua hatima yao dhidi ya Madam Jane ambae hakuwa mtu wa masihara kabisa, ilikua ni kosa kubwa kumruhusu mtu kuingia na kutoka ndani ya ngome hiyo ya siri.

Walinzi wote waligeuka na kumtazama Kindoki ambae ndiye alikua kama kiongozi wao, Kindoki akatoa ishara fulani akiwaamuru watoke nje kuwafuatilia Brandina na Yusto, wakafanya hivyo.

Kindoki aligeuka na kumtazama madam Jane, alishangazwa na hali aliyokuwanayo Madam Jane wakati huo, wala hakuwa anajali yale yaliyokuwa yakiendelea, akili yake ilikua mbali kabisa alionekana hayuko sawa.

Madam Jane alitembea taratibu hadi lile eneo ambalo Yusto alipigwa risasi, akatazama damu kiasi iliyokua imemwagika pale chini kisha akachuchumaa na kuikota ile picha ambayo Yusto aliidondosha.
Ilikua ni picha yake ambayo alipiga miaka mingi iliyopita akiwa pamoja na Zubeda.

Baada ya kuitazama, aligeuka na kuanza kuelekea kwenye lile ghorofa.

"Madam Madam" Kindoki aliita lakini madam Jane hakuitika wala kugeuka nyuma. ikabidi Kindoki akimbie na kumkaribia zaidi.

"Madam samahani tunaweza kutumia helkopta yako kuwafuatilia hawa watu"

"Ndio" madam Jane alijibu kwa ufupi, akaingia ndani na kufungua mlango.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Revocatus akiwa bado amelala pale chini alirejewa na fahamu zake, akainuka haraka na kukaa.
Kabla hajafanya lolote alishuhudia pikipiki ikipita juu yake kama ndege ikitokea ndani ya ngome ya madam Jane.
Ilikuwa ni tukio lililomshangaza sana,
alipotazama vizuri alimuona Brandina na Yusto wakiwa wamepakizana kwenye ile pikipiki wakatokomea msituni.

"Ee mungu wee huyu mwanamke ulimuumba wewe kweli" alisema Revocatus huku akijaribu kusimama, mwili wake ulikuwa ukimuuma kila mahali, kipigo alichokuwa amekipata kutoka kwa Brandina hakikuwa cha kawaida.

Haukupita muda akawaona walinzi wakitoka kwa kasi mle ndani baadhi wakiwa na pikipiki wengine wakiwa ndani ya gari na baadae ikafuata helkopta.

"Enhee kumekucha huko" alisema Revocatus huku akianza kukimbia kupandisha mlima akirudi kule alikokuwa amepaki gari lake.

Alihofu akionekana na wale walinzi basi angekamatwa na kupelekwa kwa bosi wake, hakuwa na chakujibu amefikaje na kwa nini yuko pale. Usalama wake pekee ulikua ni kuondoka.

Kadri alivyokua akiendelea kwenda mbele hali yake ilizidi kubadilika alijihisi kuchoka na mwili kuisha nguvu, mbaya zaidi alikua akipanda mlima.

Baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya Revocatus aliona kuna haja ya kutafuta msaada wa haraka, hapo ndipo akamkumbuka Caren.

Haraka akatoa simu yake mfukoni akaiwasha, kabla hajapiga mara simu yake ilianza kuita, mpigaji alikua ni Caren.

"Yusto yuko wapi hili ndio litakuwa swali lake la kwanza" Revocatus alijisemea Kisha akapokea na kuweka simu yake sikioni.

"Hello Caren"
"Una nini wewe mbona ukazima simu uko wapi, Yusto yuko wapi?"
Caren aliuliza maswali mfurulizo.

"Kuwa mpole Caren nahitaji msaada wako haraka njoo huku nilipo, nakutumia location sasa hivi"
Alisema Revocatus kisha akakata simu, akamtumia location alipo.
Akiwa amebakiza hatua kadhaa kulifikia gari lake Revocatus alianguka chini akiwa hoi taabani, hakuweza tena kujisogeza mbele zaidi.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Brandina alikua akikimbiza pikipiki yake kwa kasi kubwa mno akifuata barabara moja inayokatiza katikati ya msitu, Yusto alikua nyuma yake ameshikiria kwa nguvu asianguke.
Nyuma yao walikua wakifuatiliwa na vikosi vya ulinzi vya madam Jane, nao walikua wakija kwa kasi kubwa, haukupita muda mara helkopta ya madam Jane ikaonekana hewani ikija kwa kasi pia.
[emoji294][emoji294][emoji294]

Revocatus alifumbua macho taratibu baada ya kuhisi kuna mtu amemgusa.

"Caren?, Umefika"
"Revo nini kimetokea, imekuwaje upo huku, Yusto yuko wapi"
Caren aliuliza huku akimuinua Revo taratibu.

ITAENDELEA.....

𝐬𝐢𝐦𝐮𝐥𝐢𝐳 𝐡𝐢𝐢 𝐢𝐧𝐚𝐩𝐚𝐭𝐢𝐤𝐚𝐧𝐚 𝐡𝐚𝐝𝐢 𝐌𝐖𝐈𝐒𝐇𝐎 𝐤𝐰𝐚 𝐭𝐬𝐡 𝐞𝐥𝐟 𝐦𝐨𝐣𝐚 𝐭𝐮
0756862047
 
Back
Top Bottom