Sina furaha kwenye ndoa yangu, nahisi nilikurupuka

Sina furaha kwenye ndoa yangu, nahisi nilikurupuka

Usijutie chochote mueleze kitu gani hupendi ili abadili baadhi ya tabia ambazo siyo sawa, pili kuhusu u goli kipa wakati unamuoa nafikiri ulijua kabisa unaoa mwanamke asie na kazi chakufanya tafuta mtaji umfungulie biashara yoyote ndogo uone akili yake kama hiyo biashara itafanikiwa au laa

Watu hubadilika usikate tamaa mapema
 
Hukugundua wakati wa uchumba? Kosea kujenga nyumba kwani utabomoa na kujenga upya, sio kuoa. Vijana, nawaasa, kuoa ni mtihani mgumu sana.
Na hii iende kwa wazazi wote ambao wanalazimisha watoto wao kuoa, hili suala sio poa wawaache watoto wao wajitafute ili siku wakijipata na isivyo bahati wakayakanyaga basi wasilaumiwe

Ndoa ni mtihani na kupata mtu sahihi haijawahi kuwa rahisi hata punje
 
Bado kijana mdogo. Ukiwa mtu mzima utaelewa.

Hili unaloota hata uarabuni huko wanapofuga wanawake sidhani kama ni kwa kiwango hicho.
Kila mtu ashinde mechi zake usinipangie wala sijaomba ushauri
 
Wanawake wanatofautiana utashi mkuu. Huenda huyo uliyenae ukikaa nae sawa kwa kuzungumza vizuri, naamini anaweza kubadilika.
 
Ukitaka kumuacha nenda mbele zaid. Usitumie vigezo hivo. Nitafute pm nikupe skills ila ukisema hivyo utafell pakubwa sana. Unaweza usirudishe hiyo furaha yako. Ila ujue wanawake wengi mjini sio wale wa kazi siku hizo mashine zifanya kila. Kitu
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]wewe bado hujaoa hao viumbe hawaelekezeki hata upige ngumi sanasana utapata kesi tu..
Huyo mbona kaolewa tayari, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Jf jamani lol
 
Lakini b... kuna point ya msingi sana hapo hujaizingatia... hana hisia ya mapenzi tena kwa mkewe.
Katika mahusiano/ndoa, ukipoteza hisia ni point of no return. Ni ngumu sana kurudisha.

Na kupoteza huko hisia ndiko kumemfumbua macho ya kasoro hizo anazozisema juu ya mkewe.
Mapenzi upofu, eti?
Ndiyo anapaswa kusema naye b..., bila kusema naye sidhani kama ni hotua nzuri. Ndoa ni ya wawili.

Ova
 
Wakuu nakiri kabisa from heart ya kwamba hii ndoa yangu nilikurupuka sana yapata takribani mienzi minne ya ndoa yangu sina hisia ya mapenzi na nahisi kujuta sana kwenye maisha yangu na sina furaha kabisa.

Yaani sina furaha kabisa wakuu yaani najuta kuoa mwanamke wa chop money yaani yeye ni kula tu na kulala na ni mvivu sana na mbaya zaidi kinachoniuma nimetoa mahari nyingi sana lakini binti ni mvivu sana na nahisi majukumu yamenielemea kabisa.

Tafadhali naombeni ushauri wenu wakuu na nataka nimrudishe mazima kwao ili nikeep furaha yangu.

Msinipopoe wakuu
Inatokea sometimes kwa baadhi ya watu. na hata mkiongea vipi itabadilika siku moja mbili na baadaye kurudi kule kule. Najua umesema ni miezi minne tu, je mna watoto kabla ya ndoa? Au mna mtoto mtarajiwa? Kama mna watoto au mnategemea mtoto, hapo ni uvumilivu mpaka mtoto akukiwa mkubwa awe independent, then utachukua maamuzi ufanyeje. ila kama hamna watoto au hamtegemei watoto, hiyo hali ya kuyokuwa na raha itaendelea zaidi na zaidi. Chukua maamuzi sahihi. Mkeo siyo ndugu yako.
 
Back
Top Bottom