Singida Big Stars tumefuzu Ligi Kuu Tanzania Bara, tupeni ushauri

Naomba kufahamu kwa nini mlibadili jina la timu kutoka DTB FC na kuwa Singida Big Stars Fc?. Na hilo jina la DTB lina uhusiano wowote na benk ya Diamond Trust?.
Nawasilisha🙏🏾
 

Ndio sababu nipo hapa kutoa ufafanuzi na kuweka mambo sawa mkuu. Asante sana.
 
Naomba kufahamu kwa nini mlibadili jina la timu kutoka DTB FC na kuwa Singida Big Stars Fc?. Na hilo jina la DTB lina uhusiano wowote na benk ya Diamond Trust?.
Nawasilisha🙏🏾

Tumeshaeleza sababu ya kubadili jina kwenye post zilizopita mkuu. Kuhusu uhusiano wa jina la DTB na Benki ya Diamond Trust Bank ni kweli.
 
Mchukueni Azizi Ki chaap atawainua sana
Haya ndio tusioyataka....yaani ligi ijae wachezaji wakigeni watupu. Huko championship dtb ilikuwa na foreign players sio chini ya saba.

Hawa wanatakiwa wajikkte kwa wazawa mbona vijana wapo ni suala la kuachana na hawa mawakala bogus na kuwa na watu wenye malengo kweli ya kujenga club. Preferably starting 11 inakuwa na wazawa nane wakigeni watatu basi
 
Ushauri:-
1. Kati ya Kulwa na Ndoto msichague mmoja wa kumkazia.

2. Muwe watu wa kufanya fitna.

3. Msiwe watu wa porojo mitandaoni, wekezeni kwenye vitendo zaidi hapo ndo mtavuna mashabiki kwa wingi.
 
Wachezaji wakigeni hata wawili tu wanatosha. Wanachangia katika kuleta ushindani baina ya wachezaji wa ndani na nje.
 
Inshu ya jezi. Jitahidini ubunifu wa jezi uwe mzuri na bei iwe rafiki. Kuna kipindi jezi ya Mbeya City ilivaliwa nchi nzima.
 
Wachezaji wa ndani viwango vyao kiukweli haviridhishi ni vya kawaida.
Acheni zenu bwana wapo wachezaji wazuri tuu sema nini....hawa mawakala na ten percent zao ndio wanafanya wakigeni wajae tuu.

Lengini ni hili unakuwa na wachezaji wakigeni kumi fanya unamlipa kila mchezaji wakigeni dollar 2000 thats $20000 kwa mwezi kama salary. Je hii ukiwekeza kwenye academy ukuze vijana baada ya kiaka mitano unapata quality players...ila hakikisha kweli wanafundishwa vizuri.

Wachezaji wanaandaliwa hiyo ndio siri. Mnasema wachezaji wa bongo hawana viwango je tumeawaandaa ipasavyo? Ni sawa na mtot wa shule ta saint kayumba ukamshindanishe na mtoto wa ist...obviously ataonekana anapwaya tuu
 
Swali zuri. Baada ya kufuzu Ligi Kuu, Benki ya DTB iliamua isiendelee na ushindani kwenye masuala ya soka, badala yake ijikite zaidi kwenye kazi zake za kibenki. Hiyo ndio sababu tukaona tubadili jina kutoka DTB na kuwa Singida Big Stars FC.
Kama DTB iliamua kujitoa je fedha za kuendesha timu Mnatoa wapi?

Kama inamilikiwa na watu je unaweza kututajia Wakurugenzi wa timu yenu?

Bajeti yenu ya msimu wa 2022/2023 ni shilingi ngapi?

Malengo ya klabu kwa miaka mi tano (5) ni yapi?
 
Mfano mzuri ni timu yetu ya taifa, wachezaji ni wakawaida kabisa yani viwango vyao ni vidogo ndiyo maana hata kutoka nje ni changamoto.

Pili wachezaji wa Kitanzania 90% hawajitambui mfano:- Ibrahim Ajib.

Angalia Morrison licha ya ujinga ujinga wake ila anawatesa vigogo wa soka hapa nchini.
 
chukueni wachezaji wanaoachwa Yanga wametoka kufundishwa na Professor Nabi anafundisha kushambulia na Kaze anafundisha kukaba!!na kombe wamebeba!

Pia imarisheni urafiki na Yanga hii wako serious na mpira.

Pia imarisheni katikati muwe na wachezaji haiba ya Aucho na Sureboy

Kipa chukueni kijana Kabwili

Mpira unataka pesa fungueni kiwanda cha mafuta ya kula na maji baridi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…