Single mother utalindaje ndoa yako kama hili likitokea kwenye mahusiano yako mapya?

Single mother utalindaje ndoa yako kama hili likitokea kwenye mahusiano yako mapya?

Utakaza na baada ya miaka mingi dogo anafanya harakati za kumtatuta Baba yake na wanatengeneza bond nzuri tu, sasa sijui utakunywa simu ufe..
Utakuta mtoto anafanya juu chini kuwaunganisha Baba na mama.
Wakati Baba yake kaoa na mama kaolewa tayari.
 
Ustawi wa jamii sijui wapoje.

Mimi niliona mdada mmoja hivi alilea mtoto pekeake mpk umri wa miaka 9.

Jamaa alikimbia mtoto tangu mimba.

Ustawi wa jamii walimpa mtoto na akatokomea nae huku mpk leo.

Sijajua wanatumia vigeo gani. Tena hawakufuata utaratibu wa kukomboa mtoto.

Nafikili rushwa ilihusika.
Elimu inahitajika kwenye hili, kulea mtoto peke yako haikupi uhalali wa kuwa unahaki zaidi ya kuwa na mtoto kuliko mzazi mwenzio,kama hatoi matunzo alipaswa kuyadai kwa kwa taratibu rasmi,na mwanaume angeshinikizwa kutoa hayo matunzo, Halafu hizo habari za kugomboa mtoto hazipo kisheria, huwezi kumnyima mtoto haki ya kumjua baba yake mzazi eti kwa sababu hajagombolewa,huo ni utumwa na ni sawa na kuuza binadamu tu.
 
S
Sjasoma kbsa lkn kun mamb hayapo sawa 1.jamaa alimpata vip ten huyo dada 2 alijuaje shule anayosoma mtoto 3. Alifanikiwa vip kubadil jina la mtoto
Story za kutunga hizi za kuwafariji single mama
 
Mtu mpaka anakubali kuingia gharama zakukulelea mtoto wako Kama wake means jamaa kashamchukulia kuwa ni sehemu ya maisha yake,na Kama mtoto ni wakike basi naamini Wana bond kubwa sana na huyo jamaa na anaumia pia

Single mother wasio na akili ndo wanasababisha wanawake wengine tutukanwe Kila uchwao
Sema huyo jamaa aliyemuoa single mother naye ni kilaza wa kutupwa,unapo oa single mother kwanza,usijiingize kwenye mtego wa kusema huyo mtoto uliyemkuta naye ni wa kwako,ukataka mpaka majina atumie ya kwako,kama unalimpia ada au kumsomesha wewe lipa bila kuweka masharti yoyote yale,ukianza kuweka masharti mwishowe unakuja kujiumiza mwenyewe kama hivyo,
Mwache mtoto atumie majina ya baba yake huyo aliyemkata,kwa maana wewe huwezi jua mtoto amekataliwa kweli au la? Maana single mother asilimia 90 hudai kuwa wametelekezwa kumbe wakati mwengine ukweli wana ujua na wao ndo sababu ya kuachwa,husema wametelekezwa kutafuta huruma ili wapate ndoa,japo wapo baadhi walio telekezwa kweli
 
Kosa la kwanza alilofanya dada yako ni kutomshirikisha mume wake kuanzia mwanzo Hilo ni kosa kubwa Sana alilofanya angemshirikisha tangu awali jamaa angejua apambane vipi kiume na Kama jamaa yupo vzr kiuchumi angempeleka hata nje ya TZ mtoto akaishi

Anyway pole yake
Vipi mtoto wangu nawe ulimpeleka kwa nani? Namtaka mwanangu.
 
Dada aliyakoroga...mwanaume akaona anamdharau...
Aliesema atamuoa single mother endapo tuu ataonyeshwa kaburi la baba wa mtoto wake alikua anataka aepushe haya...
 
Kutupa matukio yasio na kichwa wara miguu
Nimekwambia hiviii
Wanaume wengine wanasema mpk amuoe single mother ni mpka aonyeshwe kaburi la aliezaa naye ili baadae yasijeibuka mambo kama hya ya baba kuja kutaka mtoto wake...
 
Nimekwambia hiviii
Wanaume wengine wanasema mpk amuoe single mother ni mpka aonyeshwe kaburi la aliezaa naye ili baadae yasijeibuka mambo kama hya ya baba kuja kutaka mtoto wake...
Naunga mkono hoja yako mpk nione kaburi
 
Kabla ya kumuoa Single Mama hakikisha unaona Death Certificate ya baba mtoto wake. Kinyume na hapo ni sawa na kufuga Chatu. Ipo siku tu atakugeukia. Kinachonitia hasira ni kuwa single mama wengi mwanzoni huwa na nyodo na kuona hao wanaume zao kama miungu ila wakiachwa hutia huruma na kujifanya wacha Mungu. Na kamwe huwa hawaachani kwa 100% na watu waliowazalisha. Huyo dada yako alivyoanza mawasiliano ya siri na huyo baba mtoto wake kuna mengine yaliendelea ila hujataja. Ninamwonea huruma sana huyo mume wake kwa kupotezewa muda na huyo dada yako mpuuzi. SAY NO TO ALL SINGLE MOTHERS. Waolewe na waliowazalisha.
 
Back
Top Bottom