Sio kwa ubaya lakini wenzetu waislamu mnakera na adhana ya asubuhi

Sawa.
 
Nani kakupa mamlaka ya kuita wabongo wote wajinga ? Umekosea Mkuu
 
Adhana wala siyo tatizo, tatizo ni kuwapigia watu kelele masaa matatu kwa ibada ambayo inakuja kufanyika saa 11 alfajiri tena kwa dakika tano tu, hili ndio tatizo na kero kubwa.
 
Dah kweli kule kipunguni nilienda kwa mshkaji wangu mmoja vyuma vikiamka tu lazima vikatize hapo juu ya paa
Kuna dege la Urusi lilikuwa linakuja zamani lina kelele hatari, sasa kwa hapo kipunguni kama ni alfajiri huwezi kulala lazima uamke.
 
Makanisani wanasema hakikisheni kelele zenu hazitoki nje.

Huku kwingine ndo hivyo tena.

Nchi ngumu.
Spika lenyewe limefungwa nje ya jengo la kanisa juu kule mnarani kengeke linaponing'inia lakini bado mnahimizana sauti isitoke nje!? Basi sawa.
 
Ndio labda waseme;hakuna kizuri kisicho na kasoro!
 
Acha uongo wewe!hiyo kitu inaswihi pale tu muhusika anapowajibika kila muda unapofika. Tunarekodi kaswida lakini sio Adhana.
Usikurupuke kuandika kitu ambacho hujakielewa, hakuna adhana za kurekodi, bali zile porojo tangu saa 9 usiku mpaka saa 11 alfajiri ni recorded na ndizo zinazolalamikiwa.

Adhana ni kitu mnachoweza kuvumilianaz lakini siyo kuleta porojo watu wamelala masaa matatu kwa ibada ya dakika tano tu.
 
Adhana wala siyo tatizo, tatizo ni kuwapigia watu kelele masaa matatu kwa ibada ambayo inakuja kufanyika saa 11 alfajiri tena kwa dakika tano tu, hili ndio tatizo na kero kubwa.
Hii ndio hoja,
Kwanini isiwe adhana pekee?
Na badala yake tuanze kuamshana saa 10 alfajiri?
 
Kila jambo mnaliweka kwenye mzani wa ukristo na uislam.
Mleta uzi anaishi karibu na msikiti na ndo huo unamkera, wewe unaeishi karibu na kanisa kama unakereka ni ruksa kusema pia.

Adhana ya mara moja haikeri ila ile mtu anaongeza maneno kibao, sauti juu halafu kila siku ni kero kubwa.

Kuna kanisa lilishurutishwa kubadili ratiba zake kwa sababu kama hizo, wao saa kumi na mojo alfajiri washaanza kuomba kwa sauti na hapo kuna muda mchungaji ana waumi wawili tu. Ila wamefunga speaker nje hizo kelele zao si mchezo.

Haijalishi ni dini gani zote ni kelele hasa nyakati za asubuhi.
 
Nyumba hiyo umepanga chumba kimoja, afadhali uhamie Kimara Temboni kwa Kuhani Musa kwenye mikesha ya usiku kucha.😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…