Sio kwa ubaya lakini wenzetu waislamu mnakera na adhana ya asubuhi

Sio kwa ubaya lakini wenzetu waislamu mnakera na adhana ya asubuhi

Nipo jirani na msikiti,
Kuanzia saa 10 alfajiri,
Kuna shehe huyo amekuwa mtangazaji wa muda,
"Sasa hivi ni saa 10 dakika 20 ewe muislamu jiandae kuamka,
Swala swala,!
Na anaendelea kutaja muda mpaka inafika saa 11 alfajiri.."

Kwakweli hebu tunaomba msaada wenu,
Ni kweli hakuna namna ya kuamshana nyie tu bila kutukera sisi?

Au nchi hii yenu pekee yenu?
Kwani hamuwezi kutegesha alarm mkaamka wenyewe mpaka mpigiwe kelele za kuamshwa kutokea mbali?

Yaani tunatafuta pesa kwa shida,
Usingizi unakuja kwa shida,
Na asubuhi asubuh ukianza kupata usingizi mtamu unaamshwa kwa lazima

Nisameheni sana lakini mnakera walah wabilah!

*****************************
Mojawapo ya comment bora ni hii number #51 kutoka kwa Etrugul bay

Nikiwa muislamu mwenye akili timamu na mawazo huru naweza sema kuna baadhi ya watoa adhana hawako sahihi kabisa

Adhana kama adhana ikitolewa kwa mara moja wala haina shida kabisa lkn shida inakuja kwa watoa adhana kuongea sana na kusahau kuna watu wengine wasio waislamu wamepumzika,,kitendo cha kila mda kusema saa ngapi kinaboa sana,,ukweli usiopingika wanao swali hata adhana moja tu inawatosha kabisa

Kuna ambao wanatoa nasaha basi bora iwe maneno machache lkn wengine wanaongea sana,,hivi kuna lipi jema unalofanya wakati jirani yako anahudhunika au kukosa raha kwa ibada yako wewe?

Tuache mihemko ya dini hapa,,kuna mahala waislamu inabidi tubadilike tufahamu kwamba kila kitu kinapendeza kikifanywa kwa kiasi,,,hata kama wengine wasio waislamu wanapiga makelele lakini haihalalishi nasi tupige kama wao

Tumesisitizwa sana kuwajali majirani,kuwajali ni pamoja na kutowakera mpaka wakatuona ni kero kwao

Narudia tena adhana ni ibada kubwa sana na itaendelea kuwepo mpaka mwisho wa dunia lakini tupunguze maongezi alfajir wakati wengine wamelala na kupumzika
Katika hili almaruhum Mohamed Said una maoni gani?
 
Muumini lazma anajua ratiba za Sara yake sio lazma aamshwe kama analazimishwa.anakuwa anaenda for show off.
Ilakama ni siku ya ibada ijumaa au mahubiri sauti kwenda mbali sioni shida.nakuja upande wa imani nyingine kuna vizehebu kupiga kelele usku na mapambio kwanini msiweke sound proof.ila j2 tunazpokea hzo kelele kiubinadamu.
 
Niliwahi kuishi Tanga Pangani, kule ndo hizi Adhana utazichukia yaani.
 
Wewe ndio unafuatilia hizo sauti , mimi hata uwashe mashine ya kusaga nalala chumba hicho hicho .
Chief nimecheka sana na umenikumbusha kuna siku nimemsindikiza mshikaji wangu dj wa kwenye madisko vumbi huwezi nililala usingizi wa maana hatua tatu kutoka kwenye spika iliyokuwa inapiga sound nzito hatari
 
Mkuu katika uislamu hamna siasa kali wewe sio muislamu, hayo maneno unayo tumia hutumika na makafiri adui wa uislamu.
Babu yangu muislam,Bibi yangu muislam,Baba & Mama waislam wewe ni nani wa kunikatalia uislam wangu ?.

Kelele za adhana hazifuti uislam wangu.
 
Babu yangu muislam,Bibi yangu muislam,Baba & Mama waislam wewe ni nani wa kunikatalia uislam wangu ?.

Kelele za adhana hazifuti uislam wangu.
Ila wewe umesha kua murtadi huwezi kupinga/ kukerwa na tabia au sunna ya mtume( saw) af ukabaki kua muislamu %100 wewe utakua murtardi tangu nizaliwe sijawahi kuona muuslamu wa kuchukia adhana ata yule muislamu mlevi hawezi kukereka na adhana, inakua je wewe? Uwe muislamu?
 
Ila wewe umesha kua murtadi huwezi kupinga/ kukerwa na tabia au sunna ya mtume( saw) af ukabaki kua muislamu %100 wewe utakua murtardi tangu nizaliwe sijawahi kuona muuslamu wa kuchukia adhana ata yule muislamu mlevi hawezi kukereka na adhana, inakua je wewe? Uwe muislamu?
Sichukii adhana.Nachukia sauti kubwa kupita kiasi.
 
Miaka gani hiyo mkuu mimi nimeishi north east LONDON kwa miaka saba adhani inaitwa tu vizuri na wazungu wanaiheshimu ni mesafiri paris mbona adhani ipo mkuu.
2015 na 2016 mkuu
 
Back
Top Bottom