Sioni umuhimu wa kutafuta au kumiliki hela

Kwa sababu mahitaji yangu yote nayapata kutoka shambani na ufugaji, sasa hela ya nini?

Nikitaka kula nyama, naingia bandani nachinja kuku au naingia zizini nachinja mbuzi.

Nikitaka unga wa mahindi, nasaga mahindi niliyovuna nakula mwaka mzima.

Nikitaka mchele, nakoboa mpunga niliolima nakula mwaka mzima.

Nikitaka matunda, naingia bustanini navuna.

Sasa hela ina umuhimu gani kwangu, kama kila ninachohitaji ninapata kutoka mashambani, mabandani n.k?

Nilichogundua wale wanaotafuta hela sana, ni wavivu wakulima na kufuga.​
Huna haja ya kwenda hospitali kwa kuwa ukiumwa unakula mitishamba
ukiwa na watoto, utawafundisha mwenyewe
Huna haja ya kununua nguo, viatu nk kwani ngozi za wanyama zinatosha
Huna haja ya kumiliki nyumba ya kisasa kwani nyumba ya nyasi inatosha
Huna haja ya kumiliki simu/radio kwani taarifa za huko nje hazikuhusu
Huna haja ya kutumia usafiri kwa sababu miguu yako na punda zipo kwa ajili hiyo
Kama unaweza kuishi maisha ya karne ya 16 - hongera sana!!!
 
Kutokana na maisha hayo, nimefanikiwa kufikisha miaka 99 ya kuishi.
 
Kwa sababu mahitaji yangu yote nayapata kutoka shambani na ufugaji, sasa hela ya nini?

Nikitaka kula nyama, naingia bandani nachinja kuku au naingia zizini nachinja mbuzi.

Nikitaka unga wa mahindi, nasaga mahindi niliyovuna nakula mwaka mzima.

Nikitaka mchele, nakoboa mpunga niliolima nakula mwaka mzima.

Nikitaka matunda, naingia bustanini navuna.

Sasa hela ina umuhimu gani kwangu, kama kila ninachohitaji ninapata kutoka mashambani, mabandani n.k?

Nilichogundua wale wanaotafuta hela sana, ni wavivu wakulima na kufuga.​
Leo hii yaani hata akili ya kujua hiyo simu imetoka wapi huna?
Message zinafikaje JF hujui, kuna wenye akili hawako huko shamba ndo wamekufanye leo unabwabwaja humu mitandaoni.
Kuna tofauti ya wewe na hao ng'ombe wewe hujui tuu.
 
Back
Top Bottom