Kwa sababu mahitaji yangu yote nayapata kutoka shambani na ufugaji, sasa hela ya nini?
Nikitaka kula nyama, naingia bandani nachinja kuku au naingia zizini nachinja mbuzi.
Nikitaka unga wa mahindi, nasaga mahindi niliyovuna nakula mwaka mzima.
Nikitaka mchele, nakoboa mpunga niliolima nakula mwaka mzima.
Nikitaka matunda, naingia bustanini navuna.
Sasa hela ina umuhimu gani kwangu, kama kila ninachohitaji ninapata kutoka mashambani, mabandani n.k?
Nilichogundua wale wanaotafuta hela sana, ni wavivu wakulima na kufuga.