Sipendezwi na jinsi inavyolazimishwa sasa CDF kuwa chini ya Waziri wa Ulinzi 'Kiprotokali' wakati Waziri wa Ulinzi ndiyo anapaswa kuwa chini ya CDF

Amiri jeshi mkuu anapopokea taarifa ile asubuhi,je huwa yupo CDF tu,akimpa taarifa za vyombo vya ulinzi na usalama au huwa yupo IGP,CDF na DGI?Sikubishii,ninataka kujua ili nijue na mafunzo yao kama yanakua chini ya CDF au IGP
Mambo yanakanganya kidogo ila nitajitahidi kufafanua vile navyofahamu, amiri anapokea taarifa tofauti tofauti kutoka kwa kila jeshi kila moja kwa wakati wake. Lakini nakala za taarifa (isipokuwa zile nyeti) lazima zitue mezani kwa CDF. Yaani lazima CDF afahamu hali ya usalama wa nchi pamoja na hali za majeshi yaliyo chini yake.
 
Unaweza kutuambia kwanini wanajeshi hupiga saluti viongozi kama madc ma RC, Rais nk.
Acha kupotosha, wao jeshi hilinda nchi, na kufanikisha hilo huheshimu walioshika hatamu za nchi, kama hamtaki waliopo waheshimiwa na jeshi subirini uchaguzi mchague wa kupigiwa saluti wapya
 
Ok! naehukuru kwa kunieleza kulingana na uelewa wako.Mimi kwa experience yangu,huwa naona polisi wanaenda kwenye shughuli za amani nje ya nchi kivyao,hali kadhalika na JW kivyao,na bilashaka polisi huwajibika kwa IGP,na JW huwajibika kwa CDF,na majukumu yao yako tofauti isipokua wanaposhirikiana hasa labda wanapodhibiti uhalifu,kama ilivyotokea majuzi hapa.Polisi wao huhusika na mambo ya ndani ya nchi,JW huhusika na ulinzi hasa kwenye mipaka ya nchi.Polisi husoma sheria na haki za binadamu,upande wa JW sijui.Na nimewahi kushuhudia askari wa JW akimpigia afisa wa polisi saluti,sijajua kiundani kama mkuu wa majeshi hupigiwa salute na IGP,nadhani wote hata wakati wa utambulisho,hutambulishwa kama 'na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama mliopo hapa',ikimaanishwa IGP,CDF,DGI n.k.
 
Wanasiasa wanaogopa kutandikwa na jeshi.

Lazima waweke mtu wao juu pale ili kulinda uhai wao. [emoji1787]
 
Kitu Ambacho watu hawaelewi ni neno MAJESHI kama linavyotumika Kwa Mkuu wa Majeshi,
MAJESHI kama ilivyo/inavyo tumika Kwa CDF ni Vile vikosi vyote vilivyochini ya JWTZ,
Mfano Kikosi cha Anga, Maji, Nchi kavu nk ni vikosi vyenye yadhi ya kuwa jeshi kamili na inatambulika hivyo, Kwa hyo Neno MAJESHI halina Maan ya kwamba ni Majeshi mengine kama Polisi,Magereza,Uhamiaji nk isipokuwa kama nilivyoandika hapo juu, na Wakuu wa vyombo hivi haviwajibiki wa CDF isipokuwa Kwa Mamulaka za uteuzi (Rais).
Kwa Kifupi CDF ni Mkuu wa JWTZ na si vinginevyo.
Hivi vyombo vyote vya ulinzi na Usalama vinafanya kazi Kwa Kushirikiana sana,
Na Kutokana na ushirikiano huo, JWTZ kikapewa Hadhi kubwa Kwa Sababu ya Ulinzi wa Katiba na Mipaka ya Nchi na CDF kama Mkuu wa JWTZ akapewa Hadhi ya kuwa Mwenyekiti wa hivi hasa pale vinapotekeleza Majukum yake.
Na Hata ukiangalia wanavyokuwa wamekaa kama (watakutana pamoja) anaanza Mkuu wa JWTZ anafuata wa Polisi nk,
Kama Polisi wamefanya kazi ambayo inahitaji Ushirikishwaji wa JWTZ basi watafanya hivyo Hali kadhalika na vyombo vingine,
Kwa hyo Hakuna Mkubwa Kati ya Wakuu wa vyombo hivi Ila Mkubwa wao ni Rais,
Isipokuwa CDF amepewa Hadhi Kwa Sababu ya Hadhi ya chombo anachokisimamia,
Ni kama Wakuu wa Mikoa,
Hakuna Mkuu wa Mkoa Mkubwa kuliko mwenzie,
Isipokuwa muda Mwingi Mkuu wa Mkoa DSM anapewa Hadhi Kutokana na Mkoa wake lakin haina Maan kwamba ni Mkubwa kuliko Wenzie,
Kuhusu CDF kuwa chini au kwenda kujitambulisha Kwa Waziri nafikili ni Kwa sababu ya Katabia kalikozuka Awamu iliyopita Maan Viongozi wa kisiasa ilifikia hatua wakaona kama wako juu ya kila kitu.
Na Katabia haka kanaendelea Kwa Kasi Sana japo Muanzilishi wake hayupo,
Miaka ya Huko nyuma hatukuwahi kuona Maajabu kama haya ya kujitambulisha,
Ila Kutokana na Kwamba CDF ni mwanajeshi itabidi Tu akajitambulishe Kwa waziri wa Wanajeshi,
Maan Wizara ya Ulinzi ni Wizara ya Wanajeshi.
 
Kuna oparesheni ambazo majeshi yetu yakiwa nje yanazifanya kwa pamoja, wakifika huko polisi wanafanya kama wanavyofanya hapa na JW wanafanya kama wanavyofanya hapa. Yaani yale ya ndani kuhusu raia wanafanya polisi na ulinzi dhidi ya uvamizi wanafanya JW.

Kuhusu afisa wa polisi kupigiwa saluti na askari wa JW iko sahihi, inategemea askari wa cheo gani amekutana na askari wa cheo gani katika jeshi lipi. Kuna polisi kwa cheo chake anampigia au hampigii askari wa JW kulingana na cheo chake. Somo la saluti linachanganya sana, ndio somo linalochukua muda mrefu kwa baadhi ya majeshi.

Kuhusu kutambulishwa wanapokaa pamoja wakatambulishwa 'wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama' mara nyingi wakiwapo pamoja basi rais yupo, na ndiye mwenye majeshi yake wewe unayetambulisha vyombo unataka kumpa nani mwingine maana katika mzingira hayo mkuu wa majeshi anakuwa amiri. Sijawahi kuwaona kwa pamoja na rais asiwepo

Ni vitu fulani vinachanganya taaluma nyingi nyingi kuvifahamu zaidi
 
Nilipokuwa namjibu mdau pale nilisema ni mkuu wa majeshi kwasababu anasimamia vyombo vingine vya ulinzi na usalama nikaongezea ZIKIWEMO BRIGADE zake zote.

Nilijua kuna mtu ataibua hoja hii nisipotaja brigade. Uko sahihi, lakini ni sahihi pia tunaposema ana 'uenyekiti' wa majeshi yote
 
Nimekuelewa sana,Asante kwa ufafanuzi wako mzuri,hapa umejibu na kusaidia hata wenzangu kuelewa,nilikua sijui kuhusu (majeshi)vikosi.Asante sana
 
Waziri wa juu Sana. Hadi mkurugenzi hupigiwa saluti na cdf.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Wateule woote wa
rais Ni budi kupigiwa saluti

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Asee nashukuru kws kulielewesha Hili mkuu.
Wengi wakisikia mkuu wa majeshi wanajua Ni pamoja na Yale ambayo kwa sheria za Sasa yametajwa kuwa majeshi eg polisi, magereza,uhamiaji nk.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Kuna tatizo la afya ya akili hapa!
 
Waziri ni mwakilishi wa Rais au wa serikali . Serikali ni lazima iwe na mwakilishi popote pale ili kuratbu yanayofanyika na yatakayofanyika. CDF ni mtaalam wa Mambo ya kijeshi tu, hivyo ni lazima awe chini ya Serikali ambayo inawakilishwa na Waziri. Asante Kwa mada wengine watajazia zaidi. Ila hata ukijaona CDF anampigia saruti Jokate mwegelo usijeshangaa Kwa kuwa yeye ni mwakilishi wa Raise wilaya ya Temeke.
 
"saruti' ndiyo nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…