Kitu Ambacho watu hawaelewi ni neno MAJESHI kama linavyotumika Kwa Mkuu wa Majeshi,
MAJESHI kama ilivyo/inavyo tumika Kwa CDF ni Vile vikosi vyote vilivyochini ya JWTZ,
Mfano Kikosi cha Anga, Maji, Nchi kavu nk ni vikosi vyenye yadhi ya kuwa jeshi kamili na inatambulika hivyo, Kwa hyo Neno MAJESHI halina Maan ya kwamba ni Majeshi mengine kama Polisi,Magereza,Uhamiaji nk isipokuwa kama nilivyoandika hapo juu, na Wakuu wa vyombo hivi haviwajibiki wa CDF isipokuwa Kwa Mamulaka za uteuzi (Rais).
Kwa Kifupi CDF ni Mkuu wa JWTZ na si vinginevyo.
Hivi vyombo vyote vya ulinzi na Usalama vinafanya kazi Kwa Kushirikiana sana,
Na Kutokana na ushirikiano huo, JWTZ kikapewa Hadhi kubwa Kwa Sababu ya Ulinzi wa Katiba na Mipaka ya Nchi na CDF kama Mkuu wa JWTZ akapewa Hadhi ya kuwa Mwenyekiti wa hivi hasa pale vinapotekeleza Majukum yake.
Na Hata ukiangalia wanavyokuwa wamekaa kama (watakutana pamoja) anaanza Mkuu wa JWTZ anafuata wa Polisi nk,
Kama Polisi wamefanya kazi ambayo inahitaji Ushirikishwaji wa JWTZ basi watafanya hivyo Hali kadhalika na vyombo vingine,
Kwa hyo Hakuna Mkubwa Kati ya Wakuu wa vyombo hivi Ila Mkubwa wao ni Rais,
Isipokuwa CDF amepewa Hadhi Kwa Sababu ya Hadhi ya chombo anachokisimamia,
Ni kama Wakuu wa Mikoa,
Hakuna Mkuu wa Mkoa Mkubwa kuliko mwenzie,
Isipokuwa muda Mwingi Mkuu wa Mkoa DSM anapewa Hadhi Kutokana na Mkoa wake lakin haina Maan kwamba ni Mkubwa kuliko Wenzie,
Kuhusu CDF kuwa chini au kwenda kujitambulisha Kwa Waziri nafikili ni Kwa sababu ya Katabia kalikozuka Awamu iliyopita Maan Viongozi wa kisiasa ilifikia hatua wakaona kama wako juu ya kila kitu.
Na Katabia haka kanaendelea Kwa Kasi Sana japo Muanzilishi wake hayupo,
Miaka ya Huko nyuma hatukuwahi kuona Maajabu kama haya ya kujitambulisha,
Ila Kutokana na Kwamba CDF ni mwanajeshi itabidi Tu akajitambulishe Kwa waziri wa Wanajeshi,
Maan Wizara ya Ulinzi ni Wizara ya Wanajeshi.